2
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA TANO
وَقَضَيْنَا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا ﴿٤﴾
4. Na tukawaambiwa wana wa Israili katika kitabu, hakika mtafanya ufisadi katika ardhi mara mbili, Na hakika mtajitia uluwa, uluwa mkubwa.
فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا ﴿٥﴾
5. Basi itakapofika ahadi ya kwanza yake, tutawapelekea waja wetu wenye nguvu wakali na wakawasaka majumbani. Na ilikuwa ni ahadi iliyotimizwa.
ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ الْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ وَأَمْدَدْنَاكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَجَعَلْنَاكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا ﴿٦﴾
6. Kisha tukawarudishia nguvu dhidi yao na tukawasaidia kwa mali na watoto na tukawajaalia mkawa watu wengi zaidi.
إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيرًا ﴿٧﴾
7. Mkifanya uzuri mnajifanyia wenyewe na mkifanya ubaya mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho, ili waziharibu nyuso zenu. Na waingie msikiti kama walivyoingia mara ya kwanza na waharibu kila walichokiteka kwa uharibifu mkubwa.
عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يَرْحَمَكُمْ وَإِنْ عُدتُّمْ عُدْنَا وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ حَصِيرًا ﴿٨﴾
8. Huenda Mola wenu akawarehemu, Na mkirudia, na sisi tutarudia. Na tukaifanya jahannam ni gereza kwa ajili ya makafiri.
WAISRAILI NA UFISADI MARA MBILI
Aya 4 – 8
LUGHA
Neno Qadha lina maana nyingi; miongoni mwazo ni kuhukumu. Maana nyingine ni kuumba; kama alivyolitumia Mwenyezi Mungu aliposema: “Na akaziumba mbingu saba kwa siku mbili” (41:12). Maana nyingine ni kupitisha jambo; kama alivyolitumia Mwenyezi Mungu katika Sura hii tuliyo nayo Aya 23, aliposema: “Na Mola wako amepitisha kuwa msimwabudu yoyote ila Yeye tu na kuwatendea wema wazazi wawili.” Pia lina maana ya kutoa habari kama lilivyotumika katika Aya hii tuliyo nayo.
MAANA
Maana ya kijumla ya Aya hizi ni kuwa Mwenyezi Mungu aliwapa habari wana wa Israil kwamba wao watafanya ufisadi katika ardhi kisha Mungu atawaletea watakaowadhalilisha kwa kuuliwa kutekwa na kuporwa. Baadae Mungu atawarudishia nguvu zao, lakini watarudia ufisadi mara ya pili na Mungu atawaletea tena watakaowapa pigo mara ya pili.
Ufafanuzi wa hayo ni kama ifuatavyo:
1.Na tukawaambiwa wana wa Israili katika kitabu.
Makusudio ya neno Qadhayna hapa ni kutoa habari na kuweka wazi, sio kupitisha, kwa sababu Mwenyezi Mungu hapitishi ufisadi: “Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi machafu.” Juz,8 (7:28).
Makusudio ya Kitabu hapa ni Tawrat iliyoteremshwa kwa Nabii Musa
kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu katika Aya iliyopita: “Na tukampa Musa Kitabu.” Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwapa habari Waisraili kuwa watakaowafuatia watafanya ufisadi katika nchi mara mbili.
2.Hakika mtafanya ufisadi katika ardhi mara mbili.
Makusudio ya ufisadi hapa sio ufisadi kwa maana yake ya kiujumla ambayo yanachanganya ukafiri, uongo, kula riba, kupanga njama n.k; kwani hayo yote ndio dini yao na mazowea yao wakati wowote na katika kila kizazi chao, ambapo Mwenyezi Mungu alikwisha wasimulia pale aliposema: “Walisema Mayahudi: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba.
Mikono yao ndiyo iliyofumba, na wamelaaniwa kwa waliyoyasema… Kila mara wanapowasha moto wa vita Mwenyezi Mungu huuzima, Na wanajitahidi kuleta ufisadi katika ardhi, Na Mwenyezi Mungu hawapendi wafisadi, Juz; 6 (5: 64).
Makusudio hasa ya ufisadi hapa ni kwa maana maalum ambayo ni kutawala na kwamba utawala wao wenyewe utakuwa ni ufisadi, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwaambia Wana wa Israil:
3.Na hakika mtajitia uluwa, uluwa mkubwa.
Qur’an inalitumia neno uluwa kwa maana ya kupetuka mipaka na ufisadi. Mwenyezi Mungu anasema:
إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ ﴿٤﴾
“Hakika Fira’un alijitia uluwa katika ardhi,” (28:4).
Amesema tena:
تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾
“Hiyo nyumba ya Akhera tumewafanyia wale wasiotaka kujitia uluwa katika ardhi wala ufisadi na mwisho ni wa wenye takua.” (28:83).
Maana ni kuwa nyinyi Wana wa Israil, mtatawala mara mbili na utawala wenu mtaufanya ni nyenzo ya ufisadi mkubwa na wa hatari ambao hauna mfano wake; mtachafua sehemu takatifu, mtavunja miko ya Mwenyezi Mungu na mtadharau misimamo mizuri, maadili na kila haki ya Mungu na ya watu.
Qur’an haikueleza mahali wala wakati wa ufisadi wao huo mara mbili, lakini wanahistoria na jamaa katika wafasiri wamesema kuwa Wana wa Israil waliivamia Palestina baada ya kuhangaika, kwa uongozi wa Yusha bi Nun, (Yoshua) khalifa wa Musa bin Imran, wakaikalia kwa mabavu na wakapora mali yote baada ya kuwafyeka wenyeji wa hapo wengi ambao walikuwa ni Wakan’ani (wakanani) na waliobakia wakawafanya watumwa. Sera yao kwa Yusha ilikuwa kama ilivyokuwa kwa Musa – uasi na inadi. Hiyo ndiyo iliyokuwa mara yao ya kwanza, kama wanavyosema wafasiri na wanahistoria.
Ama mara ya pili, kuna wanaosema kuwa bado haijatokea na kwamba itatokea baadae kwa Waarabu na Waislamu katika Palestina. Wengine wanasema kuwa imekwishatokea na kuisha, Kauli hii ndiyo yenye nguvu. Kwa hali yoyote ni kwamba Qur’an inaeleza waziwazi kuwa Wana wa Israil wakitawala hufanya ufisadi katika ardhi na kupanda kiburi kikubwa.
Kwa hiyo si uzushi kwa dola ya kizayuni kupasua matumbo ya wanawake wa kipalestina wenye mimba, kuwazika wazima vijana, kuwamiminia risasi wafungwa, kuwapiga mabomu ya sumu walio majumbani, kuvunja majumba ya wenyeji na kuwaziba midomo kwa mali na kwa vikwazo. Kisha inajitia kulia kuwa eti inachokozwa na kudhulumiwa.
Tunasema hivi tukijua kuwa Qur’an haikukiashiria kikundi hiki ambacho kimejiuza kwa kila mwenye kuongoza shari, lakini imekuja ishara yake kwa sababu kina jina la Israil na kunasibika kwenye kizazi kilichogeuzwa manyani na nguruwe.
Basi itakapofika ahadi ya kwanza yake.
Yaani ya kwanza katika hizo mara mbili za kufanya ufisadi, Ahadi hapa ni kwa maana ya wakati walioahidiwa Wana wa Israil kufanya ufisadi.
Tutawapelekea waja wetu wenye nguvu wakali.
Wanaambiwa Wana wa Israil. Waja sio lazima wawe wema, kama wanavyodai wengine, wanaweza pia kuwa waovu; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:
يَا حَسْرَةً عَلَى الْعِبَادِ مَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٣٠﴾
Ni sikitiko kwa waja, hakuwafikia Mtume yeyote ila walikuwa wakimfanyia stihzai, (36:30).
Wenye nguvu na wakali, ni ukali wa vita. Hao walikuwa ni wababilon wakiongozwa na Nebuchadnezzar au baba yake Nabopolassar ambao waliwaua mayahudi, wakachoma Tawrat na wakawachukua mateka watu wengi, wake kwa waume na watoto, Hayo yalikuwa mnamo mwaka 586 kabla ya kuzaliwa Nabii Isa (586 B.C.). Imesemekana kuwa ni mwaka 596.
Na wakawasaka majumbani.
Neno kuwasaka hapa tumelifasiri kutoka neno la Kiarabu Jasu ambalo maana yake hasa ni kutafuta sana na kurudiarudia. Qur’an haikulitumia neno hili isipokuwa hapa tu.
Maana ni kuwa hao jamaa walikuwa waki- watafuta Mayahudi majumbani mwao na wakirudi tena kuwatafuta ili wawaue.
Na ilikuwa ni ahadi iliyotimizwa
bila ya kuhalifu au kuachwa Muhtasari wa Aya hizi ni kuwa Wana wa Israil walipofanya ufisadi mara ya kwanza Mwenyezi Mungu aliwapelekea watu wenye nguvu waliowaua, wakuwafurusha wanaume na kuchukua wanawake, wakapora mali zao na kuharibu majumba yao. Ufisadi huo wa kwanza na pigo lake ulikuwa kabla ya Uislamu.
Kisha tukawarudishia nguvu dhidi yao na tukawasaidia kwa mali na watoto na tukawajaalia mkawa watu wengi zaidi.
Waliorudishiwa nguvu ni Wana wa Israil dhidi ya Wababiloni; yaani Wana wa Israil walijikomboa kwa Wababilon. Inajulikana kuwa Wana wa Israil hawakupigana na Wababiloni katika miji yao wala hawakuwahi kuwashinda.
Lakini mnamo mwaka 538 Bc, mfalme wa Fursi (Iran ya sasa) aliishinda miji ya Wababiloni na akawakomboa mateka wa Kiisrail waliokuwa humo. Kwa hiyo nguvu za Wana wa Israil dhidi ya Wababiloni ni kupitia mfalme wa Fursi.
Abu Hayan Al-andalusi anasema katika Tafsir yake Albahrul-Muhit: “Mfalme alipigana vita na Wababilon. Nebuchadnezzar alikuwa ameua wana wa Israil elfu arubaini, waliobaki wakawa ndani ya Babilon wakidhalilishwa. Basi mfalme alipopigana nao na akawashinda alioa mwanamke wa Kiisrail. Huyo mke akamtaka mumewe awarudishe watu wake Baytul–Muqaddas, naye akafanya hivyo.”
Waliporejea wana wa Israil Palestina, Mwenyezi Mungu aliwasaidia kwa mali na watoto na akaifanya idadi yao zaidi ya ilivyokuwa mwanzo. Lakini mara tu iliporudi nguvu yao, walirudia uovu na kupotoka na dini kuliko mwanzo. Wakamuua Zakariya na wakaazimia kumuua Bwana Masih
.
Mkifanya uzuri mnajifanyia wenyewe, na mkifanya ubaya mnajifanyia wenyewe.
Katika maana haya ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
ل هَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ﴿٢٨٦﴾
“Faida ya yale iliyoyachuma ni yake na hasara iliyochuma ni yake.” Juz, 3 (2:286)
مَّنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ﴿٤٦﴾
“Mwenye kutenda wema basi ni kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe na mwenye kutenda uovu basi ni juu yake” (41:46).
Na ikifika ahadi ya mwisho.
Baada ya kupita ufisadi wa kwanza wa wana wa Israil na ikapita misukuosuko yake, ulikuja ufisadi wa pili na misuko suko ya pili nayo ikachukua nafasi yake, basi Mwenyezi Mungu aliwapelekea watuili waziharibu nyuso zenu.
Hapo wanaambiwa wana wa Israil. Kuharibika nyuso ni fumbo la misukosuko na kudhalilika kwao. Kwa sababu uso unadhihirisha furaha au huzuni iliyo moyoni. Ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu:
سِيئَتْ وُجُوهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ﴿٢٧﴾
“Nyuso za waliokufuru zitaharibika” (67:27).
Na waingie msikiti kama walivyoingia mara ya kwanza na waharibu kila walichokiteka kwa uharibifu mkubwa.
Makusudio ya msikiti hapa ni mji wa Quds, kwa sababu ndani yake mna hekalu la Nabii Suleiman. Limeitwa msikiti (masjid) kwa vile ni mahali pa kusujudu.
Maana ni kuwa wana wa Israil walipofanya ufisadi mara ya pili, Mwenyezi Mungu aliwapelekea watu waliowapa adhabu mbaya na hali yao ikawa kama ya kwanza – kuuliwa, kufukuzwa na kuharibiwa majumba.
Mara zote mbili za ufisadi na kuadhibiwa zilikwishapita kabla ya Uislamu.
Katika Majmau-bayan imeelezwa kuwa aliyewashambulia wana wa Israil mara ya kwanza ni Nebuchadnezzar na aliyewashambulia mara ya pil ni mfalme wa Roma, akaharibu Baytul-Muqaddas na akawateka wenyeji wake.
Haya yanaafikiana na aliyoyanukuu Al-Maraghi kutoka Tawarikhl-Yahud, akasema kuwa muda baina ya mashambulizi mawili ulikuwa miaka mia tano.
Huenda Mola wenu akawarehemu.
Kwa sharti la kutubia na kuwa na huruma. Kwa sababu asiyekuwa na huruma hahurumiwi; kama ilivyoelezwa katika Hadith tukufu.
Na mkirudia
ufisadi kujitia uluwa na kiburi,na sisi tutarudia
kuwaadhibu na kuwadhalilisha.
Walirudia na wakafanya ufisadi; wakataka kumuua Masih
na wakamkadhibisha Muhammad(s.a.w.w)
. Mwenyezi Mungu akawapelekea Waislamu, wakawaua Bani Quraydha, wakawatawala Bani Nadhir, wakaichukua Khaybar na wakafukuzwa Mayahudi Bara Arabu.
Na tukaifanya Jahannam ni gereza kwa ajili ya makafiri.
Wengine wamefasiri neno hasir kwa maana ya busati. Yaani tumeifanya Jahannam ni busati.
Vyovyote iwavyo, makusudio yake hapa ni kuwa Jahannam itawazunguka wala hakuna matarajio ya kuepukana nayo; sawa na kauli yake Mwenyezi Mungu:
أُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا ﴿١٢١﴾
“Hao makazi yao ni moto wa Jahannam wala hawatapata pa kuukimbia” Juz. 5 (4:121).
KUELEZEA MWENYEZI MUNGU NA DOLA YA ISRAIL
Mnamo mwezi Januari mwaka hu 1969, kulitokea mjadala motomoto kwenye magazeti ya Misr kuhusu Aya inayoeleza ufisadi wa wana wa Israil. Walishiriki kwenye mjadala huu wataalamu wengi wenye ghera ya haki, Uliendelea mjadala na malumbano kwa muda kiasi, Gazeti liliuchapisha kwenye matoleo mane ya kila Ijumaa ya mwezi huo tulioutaja.
Washiriki waligawanyika makundi mawili:
Kundi la kwanza linasema kuwa pigo la kwanza la wana wa Israil lilitokea kutoka kwa Umar bin Al-khttab alipoishinda Quds. Yeye na waislamu wakasaka nyumba za wapalestina. Na ufisadi wa pili wakasema kuwa ni Walivyofanya wazayuni mnamo mwaka 1967 na wanavyoendelea kufanya leo.
Kundi hili limefasiri kuwa pigo la pili la Mayahudi litatoka kwa warabu ambao watashinda hivi karibuni na warudishe ardhi zao zilizoporwa na na wakoloni hao.
Na wakasema kuwa hiyo ndio maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na waingie msikiti kama walivyoingia mara ya kwan- za.” Yaani waarabu wataukomboa Msikiti wa Aqswa kutoka kwa Waisrail kama walivyoukomboa kwanza.
Hakuna rejea ya tafsir hii isipokuwa matamanio na utabiri ambao ni wajibu kuuepusha na Qur’an. Kwa sababu hiyo ni Kitabu na nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu inayofichua kawaida na desturi ya maumbile ambayo hayageuki wala kubadilika na inaangalia kila kilichomo ulimwenguni, kuanzia chembechembe hadi vitu vikubwa; wakati huo Qur’an inambebesha kila mtu majukumu ya kufanya mambo kwa juhudi na kuchukuliwa hisabu yake mbele ya Mwenyezi Mungu, ya dhamira na ya watu wote. Kundi la pili linasema mara zote mbili za ufisadi pamoja na mapigo yake yamekwisha pita kabla ya Uislamu.
• Pigo la kwanza lilitangulia Uislamu kwa kiasi cha miaka elfu moja na lilitekelezwa na Nebuchadnezzer au baba yake, ambaye aliiharibu Quds, kuchoma Hekalu, kuua wayahudi wengi na waliobaki wakawateka nyara hadi Babiloni.
• Pigo la pili, linasema kundi hili, kuwa lilitokea mnamo mwaka wa 70.
Baada ya kuzaliwa Nabii Isa (70A.D.) lilitekelezwa na Titus (Tito) wa Roma ambaye aliuzingira mji wao na akauponda ukuta wake, akaingilia kuharibu majumba kubomoa hekalu na kuua kiasi cha watu milioni moja mbali na waliochukuliwa watumwa na kuuzwa sokoni; kama anavyosema Flavius ambaye aliishuhudia tukio lenyewe, Waliobaki wakasambaa ulimwenguni
.
Vilevile, kundi hili la pili, limesema kuwa Qur’an haishirii kwa mbali wala karibu kuhusu kikundi kilichoko katika ardhi ya Palestina kinachojiita Israil. Kwani hicho si kikundi cha kidini wala chama cha kisiasa au serikali ya kiuhakika; isipokuwa ni adui mpya wa waarabu na Waislam, nacho ni ukoloni wa kizayuni au uzayuni wa kikoloni ambacho kimevaa nguo ya Daud kikiwa kimechukua ramani ya ulafi iliyosajiliwa kwenye Tawrat ya kupangwa iliyopotolewa ‘kuanzia Nail hadi Furat’ na kunyakua mali ya taifa chini ya nembo ya uyahudi. Lengo la kwanza na lamwisho ni kuleta ukoloni mamboleo kwa waarabu na waislamu kikiongozwa na Marekani.
Kwa ufupi ni kuwa Qur’an haikuashiria kabisa Israil ya sasa na kwamba Aya zinazozungumzia Wana wa Israil zimewakusudia koo kumi na mbili katika kizazi cha Ya’qub bin Is-haq bin Ibrahim ambao walikuwa katika zama za Nabii Musa na Harun. Na hawa ambao wamenyakua ardhi yetu kwa silaha za ukoloni na mali ya kizayuni si katika kizazi cha Israil bin Is-haq wala hawako kwenye dini yake wala dini ya Musa; isipokuwa wao ni viumbe wapya wa kushangaza wasiokuwa na mfano.
Kwa sababu wamepatikana kutokana na vizazi mbali visivyokuwa na mfungamano baina yao wala kujumuika kwa mkusanyiko wa kiinchi au lugha wala hawana msingi wowote isipokuwa msingi wa kibaraka wa nguvu ya shari.
Zaidi ya hayo ni kwamba tukitafsiri kuwa Mwenyezi Mungu amek- wishaeleza kuwa tutauingia msikiti, tutabweteteka tu na kuzitupilia mbali sababu za ushindi za kawaida alizozibainisha Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake na kupitia kwa Mtume wake.
Ambapo mara anatuhimiza jihadi na mara nyingine anatuhiza kusaidiana, huku tukiwaandaa wengine, kutokata tamaa kuwa na subira na mara ningine kung’ang’ania jambo, kujitolea mali na kulifanya rahisi kila lililo ghali kwa ajili ya dini na uzal- endo; sawa na alivyofanya Muhammad, swahaba wa Muhammad(s.a.w.w)
na waliowafuatilia wao kwa wema na kama vile wanavyofanya wanaoji- tolea mhanga hivi sasa.
Baada ya yote hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu hapigani wala hatapigana na Israil na ukoloni wa kizayuni kwa niaba yetu; hata kama tukiswali na kumtarajia Yeye tu. Kwa sababu ibada bora zadi kwake ni kujitolea mhanga kwa nyenzo na nguvu zote dhidi ya dhulma, ukandamizaji, ufisadi na uchokozi.
Nasi tunamiliki uwezo wa kutosha wa kumtoa adui kwenye ardhi yetu. Tunamiliki uwezo huo kwa idadi yetu, dini yetu, turathi zetu na mali zetu. Lililobaki ni kuzitumia tu na hapana budi, lazima tuzitumie. Kwa sababu kupenda kubakia kunalazimisha hilo. Ukoloni na uzayuni umetuweka kwenye mambo mawili hakuna la tatu: Ama kufa au kuishi, Hakuna anayependa kufa kuliko kuishi au kuwa mtumwa kuliko kuwa huru au udhalili kuliko heshima.