2
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA SITA
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ بَيْنَ السَّدَّيْنِ وَجَدَ مِن دُونِهِمَا قَوْمًا لَّا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا ﴿٩٣﴾
93. Hata alipofikia baina ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu ambao takriban hawakuwa wakifahamu kauli.
قَالُوا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَىٰ أَن تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا ﴿٩٤﴾
94. Wakasema: Ewe Dhul-qar-nain! Hakika Juju na Majuju wanafanya ufisadi katika nchi. Basi je, tukulipe ujira ili utujengee baina yetu na wao ngome?
قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيْرٌ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْمًا ﴿٩٥﴾
95. Akasema: Yale Mola wangu aliyoniwezesha ni bora. Lakini nisaidieni kwa nguvu nijenge kizuizi baina yenu na wao.
آتُونِي زُبَرَ الْحَدِيدِ حَتَّىٰ إِذَا سَاوَىٰ بَيْنَ الصَّدَفَيْنِ قَالَ انفُخُوا حَتَّىٰ إِذَا جَعَلَهُ نَارًا قَالَ آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا ﴿٩٦﴾
96. Nileteeni vipande vya chuma, Hata alipojaza baina ya nafasi iliyo kati ya milima miwili, akasema: Vuvieni. Hata alipokifanya moto akasema: Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimwagie.
فَمَا اسْطَاعُوا أَن يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْبًا ﴿٩٧﴾
97. Hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa.
قَالَ هَـٰذَا رَحْمَةٌ مِّن رَّبِّي فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ رَبِّي جَعَلَهُ دَكَّاءَ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّي حَقًّا ﴿٩٨﴾
98. Akasema: Hii ni rehema itokayo kwa Mola wangu, Itakapofika ahadi ya Mola wangu atauvunja vunja. Na ahadi ya Mola wangu ni ya kweli.
وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِي بَعْضٍ وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَجَمَعْنَاهُمْ جَمْعًا ﴿٩٩﴾
99. Na siku hiyo tutawaacha wakisongana. Na parapanda itapuziwa na wote watakusanywa pamoja.
وَعَرَضْنَا جَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ لِّلْكَافِرِينَ عَرْضًا ﴿١٠٠﴾
100. Na siku hiyo tutawaonyesha wazi makafiri Jahannam waione.
JUJU NA MAJUJU
Aya 93 – 100
MAANA
Kisha akafuata sababu.
Dhul-qarnaini alirejea mji wa tatu ulioko katika Bahari nyeusi, unaokaliwa na Slaves
-kama ilivyosemekana - ambao Mwenyezi Mungu ameuashiria kwa kauli yake:
Hata alipofikia baina ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu ambao takriban hawakuwa wakifahamu kauli.
Watu aliowakuta huko walikuwa hawafahamu lugha yake wala hakufaamu lugha yao, lakini walielewana kwa ishara au kwa mkalimani; kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Wakasema: “Ewe Dhul-qar-nain! Hakika Juju na Majuju wanafanya ufisadi katika nchi. Basi je, tukulipe ujira ili utujengee baina yetu na wao ngome?
Sheikh Maraghi anasema katika Tafsir yake: “Juju ni wa Tatars, na Majuju ni wa Mongoli. Asili yao wanatokana na baba mmoja anayeitwa Turk. Miji yao inaanzia Tibet na China hadi kwenye Bahri iliyoganda. Miongoni mwao ni Changez Khan na Halako.
Kisha akanukuu Maraghi Jarida la Al-Muqtatif la mwaka 1888, kwamba jengo la ukuta wa Dhul-qarnain liko nyuma ya Amou–Daria sehemu za Balkh. Jina lake hivi sasa ni mlango wa chuma na liko karibu na mji wa Tirmidh.
Mtaalamu mmoja wa kijerumani Cyllid Burger, amelitaja katika safari zake zilizokuwa mwanzoni mwa karne ya 15. Vilevile amelitaja mwana historia wa Kihispania Clavijo katika safari zake za mwaka 1402 A.D.
Vyovyote iwavyo ni kwamba watu walimtaka Dhul-qarnain awajengee ngome itakayowakinga na Juju na Majuju waliokuwa wakiishambulia nchi yao, wakiwapa adhabu mbaya ya kuwaua, kuwateka na kupora. Wakajiwekea sharti la kumlipa katika mali zao ikiwa atawajenega ngome.
Akasema: Yale Mola wangu aliyoniwezesha
na akanipa utawala na malini bora
kuliko yale aliyowapa Mwenyezi Mungu. Nyinyi wenyewe mna haja kubwa ya mali yenu, basi itumieni kwenye masilahi yenu.
Lakini nisaidieni kwa nguvu nijenge kizuizi baina yenu na wao.
Makusudio ya nguvu hapa ni wafanyikazi na vifaa vya ujenzi.
Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipojaza baina ya nafasi iliyo kati ya milima miwili.
Yaani alipoletewa vyuma alivipanga mpaka vikajaza nafasi iliyo baina ya milima miwili, kisha wakamletea kuni akawasha moto akaweka mifuoakasema: Vuvieni. Hata alipokifanya
(chuma)moto akasema: Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimwagie.
Wakamletea, akamwagia kwenye vyuma vilivyo moto, vikashikana, ukawa mlima wa chuma.
Hawakuweza kuukwea
hao Juju na Majuju, kutokana na urefu na kutelezawala hawakuweza kuutoboa
kutokana na ugumu wake na maki yake.
Akasema: Hii ni rehema itokayo kwa Mola wangu.
Aliyesema ni Dhul-qarnain, akimshukuru Mola wake (s.w.t) kwa rehema na neema hii aliyoitimiza mikononi mwake, Hivi ndivyo anavyokuwa mumin mwenye ikhlasi. Anamnyenyekea Mwenyezi Mungu na kushukuru kila zinapokuwa neema za Mwenyezi Mungu kupitia kwake.
Kujengwa kwa ngome hii ni usadikisho wa mfano kuwa katika historia ya binadamu kulikuwa na kusaidiana baina ya mataifa makubwa na yale madogo yanayoendelea; baina ya taifa lililo na nyenzo za maendeleo na lile lisilokuwa nazo.
Nguvu za Amerika zinafanana sana na nguvu za Dhul-qarnaini, kwa vile haziwezi kukabiliwa na yoyote, lakini kuna tofauti kubwa ya matokeo na natija. Wakati nguvu zote za Dhul-qarnain zilkuwa ni utawala wa kheri ya ubinadamu na ufanisi wake, lakini nguvu za Amerika ni za kuhami uovu wa uzayuni na kutawala nyenzo zote, masoko yote kwa masilahi ya ukoloni na kuwadumaza watu kwa kila namna.
Ushahidi wa hayo hauna idadi. Kuanzia kuusaidia uzayuni dhidi ya waarabu na ubaguzi wa rangi ndani ya Amerika hadi Rhodesia,
mapinduzi ya kijeshi katika nchi za kiafrika
na kuwapiga vita wapigania ukombozi huko Kongo na kila mahali, Ama huko Vietnam ndio haisemeki. Wamekusanya majeshi na kutumia kila walicho nacho, lakini ukakamavu wa wananchi wa Vietnam umetoa somo kwa Amerika, ambalo hawatalisahau maisha.
Kwa hiyo kila ushindi wanaoupata Amerika wajue huo ni wa muda tu, utaondoka kwa upinzani wa wananchi ambao unazidi siku baada ya siku.
Itakapofika ahadi ya Mola wangu atauvunja vunja.
Yaani huo mlima atauvunja vunja, Maana ni kuwa utakapokurubia wakati wa kutokea Juju na Mjuju nyuma ya ukuta, Mwenyezi Mungu ataleta sababu za kuvunjika kwake.
Na ahadi ya Mola wangu ni kweli
haina shaka.
Shekh Maraghi anasema: “Ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ilifika kwa kutoka Changez Khan wakafanya ufisadi katika ardhi”.
Katika Tafsir Ar-Razi imeelezwa kuwa maana ya ahadi hapa ni siku ya Kiyama. Katika Tafsir At-Twabariy imeelezwa ni baada ya kuuliwa Dajjal.
Ama sisi tunapondokea kwenye kauli ya Maraghi, kwa sababu iko karibu na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Na siku hiyo tutawaacha wakisongana wao kwa wao.
Kwani tunafahamu kuwa Juju na Majuju wataenea katika ardhi baada ya kuharibika ngome na wataharibu maisha ya watu. Mwenyezi Mungu anasema:
حَتَّىٰ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ ﴿٩٦﴾
“Mpaka watakapofunguliwa Juju na Majuju wakawa wanateremka kutoka kila mlima.” (21:96).
Zaidi ya hayo ni kwamba lau ingelikuwa makusudio ya ahadi yake ni Kiyama au baada ya kufa Dajjal, ingelikuwa ngome bado ipo; na kama ipo basi ingelionekana, hasa kwa kuzingatia kuwa elimu imefanya dunia hivi sasa, pamoja na wakazi wake, ni kama familia moja inayoishi kwenye nyumba moja.
Na parapanda itapuziwa na wote watakusanywa pamoja.
Hii ndiyo siku ya mwisho kwa wale wa mwanzo na wa mwisho. Katika Tafsir Attwabariy imeelezwa kuwa Mtume(s.a.w.w)
aliulizwa kuhusu Parapanda, akasema ni pembe itakayopuziwa.
Baada ya hayo yote, tunapenda kujulisha kuwa tuliyoyaeleza au kuyanukuu kutoka kwa wengine kuhusiana na Juju na Majuju, ni kwa njia ya kuleta karibu ufahamisho sio uhakika hasa.
Kwa vile hatukupata rejea za kutegemewa; Kwa sababu hiyo basi tutuatosheka na dhahiri ya Qur’an Tukufu na kuwaachia ufafanuzi wenzetu wengine.
الَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِي غِطَاءٍ عَن ذِكْرِي وَكَانُوا لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا ﴿١٠١﴾
101. Wale ambao macho yao yalikuwa kwenye pazia ya kunitaja, Na wakawa hawawezi kusikia.
أَفَحَسِبَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن يَتَّخِذُوا عِبَادِي مِن دُونِي أَوْلِيَاءَ إِنَّا أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ نُزُلًا ﴿١٠٢﴾
102. Je, wanadhani waliokufuru kuwafanya waja wangu ndio walinzi badala yangu? Hakika sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ni mashukio ya makafiri.
قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ﴿١٠٣﴾
103. Sema: je, tuwaambie wale wenye hasara mno ya vitendo?
الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ﴿١٠٤﴾
104. Ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kuwa wanafanya kazi nzuri?
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا ﴿١٠٥﴾
105. Hao ndio ambao wamezikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye; Kwa hiyo vitendo vyao vimepomoka; nawala siku ya Kiyama hatutawapa uzito wowote.
ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَرُسُلِي هُزُوًا ﴿١٠٦﴾
106. Hiyo Jahanamu ndiyo malipo yao kwa walivyokufuru na wakazifanyia kejeli ishara zangu na Mitume wangu.
JAHANNAMU NA WALIOHASIRIKA
Aya 101 – 106
MAANA
Na siku hiyo tutawaonyesha wazi Jahannam makafiri waione.
Wenye makosa, kesho, watashuhudia kwa macho yao Jahannam kabla ya kuingizwa humo, ili wachomeke kwa aina mbili za moto: Moto wa hofu na moto wa kuungua.
Wale ambao macho yao yalikuwa kwenye pazia ya kunitaja.
Kutajwa huwa kunasikiwa na masikio. Kwa hiyo hapa maana ya pazia ya macho ni mfundo wa makafiri kwa Mtume na waumini, na kwamba wao walikuwa hawawezi kumwangalia Mtume(s.a.w.w)
wala waumini.
Na wakawa hawawezi kusikia utajo wa Mungu kutoka kwa Mtume wake Mtukufu.
Kwa maneno mengine ni kuwa wakosefu hawawezi kusikiza haki wala kuwatazama watu wa haki. Haya ndiyo tunayoyashuhudia kwa macho, ikiwa ni matokeo ya mzozo baina ya haki na batili na kheri na shari.
Je wanadhani waliokufuru kuwafanya waja wangu ndio walinzi badala yangu?
Makusudio ya waja wangu hapa ni viumbe ambao washirikina wali- wafanya ndio walinzi wao badala ya Mwenyezi Mungu. Hapa kuna maneno yanayokadiriwa kuwa: Je, wana dhani hawa kuwa tumeghafilika nao?Hapana! Hakika sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ni mashukio ya makafiri.
Mashukio ni mahali anapoandaliwa mgeni, vile vile linatumika neno hilo kwa maana ya nyumba. Maana ni kuwa tumewaandalia Jahannam kuwa ndio tosha yao. Hii ni sawa na kumwambia yule unayemdharau: unadhani mimi sikuwezi wewe nawe ni kama hiki kiatu?
THAMANI YA MTU
Sema je, tuwaambie wale wenye hasara mno ya vitendo? Ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kuwa wanafanya kazi nzuri?
Ufupi wa maana ni kuwa mwenye hasara zaidi katika watu na mwenye kuhangaika bure, ni yule mjinga sana anayeuona ujinga wake kuwa ni elimu, shari yake kuwa ni kheri na uovu wake kuwa ni wema.
Hapana mwenye shaka kuwa huyo ni mwenye hasara duniani, kwa vile yeye anaishi asivyokuwa. Vile vile huko akhera, kwa vile atakutana na Mola wake akiwa na ujinga, ghururi na matendo maovu. Aya inaashiria kuwa thamani ya mtu haiwezi kupimwa kwa kuiona yeye mwenyewe; Kwa sababu mgomvi hawezi kujihukumu. Wala pia haiwezi kupimwa kwa mtazamo wa watu.
Ispokuwa mtu hupimwa kwa kipimo cha Qur’an na misingi yake na kushikamana na mafunzo yake na hukumu zake. Hupimwa kwa ukweli na uadilifu, kuinusuru haki na watu wake na kujitolea kwa hali na mali. Qur’an imejaa aina nyingi za mafunzo haya; kama vile kauli zake Mwenyezi Mungu Mtukufu zifuatazo: “...Na kuweni pamoja na wa kweli” Juz; 11 (9:119)
قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ ﴿١٣٥﴾
“....Kuweni Imara kwa uadilifu” Juz;. 5 (4:135)
كُونُوا أَنصَارَ اللَّـهِ ﴿١٤﴾
“...Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu (61:14)
كُونُوا رَبَّانِيِّينَ ﴿٧٩﴾
“...Kuweni watumishi wa Mwenyezi Mungu”Juz.3 (3:79)
وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤١﴾
“...Na mpiganie jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu Juz.10 (9:41)
إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ﴿١٣﴾
“Hakika mtukufu wenu zaidi, kwa Mwenyezi Mungu, ni yule mwenye takua zaidi katika nyinyi” (49:13)
Unaweza kuuliza
: Mkosaji anaweza kujiona kuwa amepatia na kwamba amefanya vizuri. Je atakuwa ni miongoni mwa waliohasirika; pamoja na kujua kuwa hakuna mwenye isma (kuhifadhiwa na madhambi) isipokuwa yule mwenye isma?
Jibu
: Wenye kukosea wako aina mbili: Wa kwanza ni yule mwenye kukosea baada ya kutafiti na kuhakikisha; sawa na wanavyofanya wale wanaojitahidi, kiasi ambacho natija inayopatikana inaweza kuwa sawa na ya mtaalmu.
Hapana mwenye shaka kuwa mkoseaji huyu hawezi kuwa ni katika wale ambao juhudi zao zimepotea bure, au kuwa ni aibu ukoseaji wake; bali huyu analipwa thawabu kutokana na juhudi yake; kama ilivyoelezwa katika Hadith. Lakini kwa sharti awe na nia ya kujikosoa, yatakapofichuka makosa.
Aina ya pili, ni kukosea kulikotokana na kujiamini kwa juujuu, kulikotokana na mawazo, bila ya kufanya utafiti, kwa vile hajui misingi ya utafiti na elimu, Au anaweza kuwa anaijua, lakini asiitumie au aitumie nusunusu, aitumie kabla ya kuikamilisha. Huyu ndiye aliye miongoni mwa wale waliopata hasara katika kazi zao, hilo halina shaka. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamrisha kuwa na mazingatio na uthabiti na akakataza pupa na kusema bila ya ujuzi.
Baada ya hayo somo tunalolipata kutokana na Aya hii, ni kuwa tusijidanganye, tukajipa sifa tusizo nazo wala kujidanganya kwa maneno.
Vile vile ni wajibu tujihisabu nafsi zetu zinapokuwa na ghururi na kujitukuza, kabla hajatuhisabu Mwenyezi Mungu na watu. Pia rai zetu na kauli zetu tusizione kuwa ndio sawa mia kwa mia. Makosa yanatokea kwa yeyote.
Hao ndio ambao wamezikanusha ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye.
Mfumo wa maneno unafahamisha kuwa makusudio ya wale waliokanusha ishara za Mola wao na kukutana naye ndio wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure; ni sawa wawe wameamini ufufuo au wameukanusha. Linalozingatiwa ni imani na matendo kwa pamoja; sio imani peke yake.
Kwa hiyo vitendo vyao vimepomoka na wala siku ya kiyama hatutawapa uzito wowote.
Yaani hatutawathamini, kwa sababu hakuna heshima mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yule mwenye takua.
Hiyo Jahanamu ndiyo malipo yao kwa walivyokufuru na wakazifanyia kejeli ishara zangu na Mitume wangu.
Walimkufuru Mwenyezi Mungu na wakaifanyia masikhara haki na watu wake. Moto ndio mwisho na ukomo wa ufisadi na upotevu.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا ﴿١٠٧﴾
107. Hakika wale ambao wameamini wakatenda mema, mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi.
خَالِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا ﴿١٠٨﴾
108. watadumu humo; hawatataka kuondoka.
قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا ﴿١٠٩﴾
109. Sema: Lau bahari ingelikuwa ndio wino kwa maneno ya Mola wangu, basi bahari ingemalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu, hata tungeleta mfano wake kuongezea.
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾
110. Sema: hakika mimi ni binadamu kama nyinyi tu, nimeletewa wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu mmoja. Mwenye kutarajia kukutana na Mola wake, basi na atende matendo mema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake.
WALIOAMNI NA WAKATENDA MEMA
Aya 108 – 110
MAANA
Hakika wale ambao wameamini wakatenda mema, mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwahidi makafiri moto, sasa anatoa ahadi ya Pepo kwa waumini. Firdausi ni katika Pepo ya daraja ya juu. Mtume Mtukufu(s.a.w.w)
amesema: “Mkimuomba Mwenyezi Mungu muombeni Firdausi.”
Watadumu humo; hawatataka kuondoka.
Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawalipa wema yale ambayo hawatataka mengine, tosha kabisa! Yanatosheleza yote wanayoyataka. Aya inaashiria kuwa hakuna tamaa huko Akhera; vinginevyo ingelikuwa hakuna kutosheka. Kwani mwenye tamaa hatosheki.
Sema: Lau bahari ingelikuwa ndio wino kwa maneno ya Mola wangu, basi bahari ingemalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu, hata tungeleta mfano wake kuongezea.
Bahari ni jina la jinsi, linaenea kwenye bahari zote. Makusudio ya kabla ya kumalizika maneno, ni kuwa hayamaliziki na mfano wake ni mfano wa bahari. Maana ni kuwa lau tuchukulie kuwa bahari zote ni wino wa kuandika maneno ya Mwenyezi Mungu zisingetosha na maneno ya Mwenyezi Mungu yangelibakia bila ya kikomo.
Aya nyingine yenye maana hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na lau miti yote iliyomo ardhini ikawa ni kalamu na bahari (ikawa wino) na ikaongezewa bahari nyingine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingelimalizika.” (31:27).
Makusudio ya maneno ya Mwenyezi Mungu hapa sio matamshi yanayotokana na herufi wala si amri ya kitendo inayotokana na ibara ya ‘kuwa na kikawa,’ kwa sababu amri hii haiingii kwenye mahisabu: “Na amri haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.” (54:51).
Isipokuwa makusudio ya maneno yake hapa, ni kuweza kuvileta vitu vyote, wakati wowote atakao; ni sawa iwe ni kwa kuviambia kuwa na vikawa au aviambie muda ujao, wa karibu au mbali. Uwezo huu hauna kikomo wala mwisho, lakini bahari, miti na mifano yake ina kikomo; na kila chenye kikomo kinakwisha.
Kwa maneno mengine ni kuwa kila kitu kilichopo kitakwisha na kukoma, isipokuwa uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kukifanya hicho kitu utabakia.
Tutaifafanua zaidi fikra hii kwa mfano huu: Mtu akiwa na maarifa ya kilimo, maarifa yake haya atakuwa nayo tu wakati wote atakaokuwa hai, lakini kile atakochokilima kitaisha. Uweza wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) hauishi kwa vile hauna kikomo ni wa milele, lakini viumbe vyake vimepatikana na kila chenye kupatikana kina mwisho.
Sema: Hakika mimi ni binadamu kama nyinyi tu,
sina tofauti na nyinyi isipokuwanimeletewa wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu mmoja.
Ibn Abbas anasema: “Mwenyezi Mungu, kwa Aya hii, amemfundisha Mtume wake unyenyekevu, akamwamrisha aseme yeye mwenyewe kuwa ni binadamu kama wengine, isipokuwa Mwenyezi Mungu amemtukuza kwa wahyi.”
Nasi tunaongezea kauli ya Ibn Abbas: Na ili waislamu wasimfanye Muhammad(s.a.w.w)
kama wanaswara (wakristo) walivyomfanya Isa
.
Mwenye kutarajia kukutana na Mola wake,
kwa hisabu, thawabu na adhabu,basi na atende matendo mema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake.
Kila mwenye kufanya amali kwa ajili ya mwengine atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu kwenye ibada; ni sawa aseme waungu ni wengi au asiseme.
Tofauti ni kuwa kauli ni shirki ya waziwazi na riya ni shirki ya kificho. Kuna Hadith inayosema:
“Mwenye kuswali kwa riya amefanya shirki na mwenye kufunga kwa riya amefanya shirk”
Fananisha mengine kwenye swala na saumu.
MWISHO WA SURA YA KUMI NA NANE