7
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA NANE
إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُم مَّا اكْتَسَبَ مِنَ الْإِثْمِ وَالَّذِي تَوَلَّىٰ كِبْرَهُ مِنْهُمْ لَهُ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١﴾
11. Hakika wale walioleta uzushi ni kundi miongoni mwenu. Msiufikirie ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mmoja katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao atapata adhabu kubwa.
لَّوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَـٰذَا إِفْكٌ مُّبِينٌ ﴿١٢﴾
12. Mbona mlipousikia, waumini wanaume na waumini wanawake hawakujidhania mema na kusema huu ni uzushi dhahiri?
لَّوْلَا جَاءُوا عَلَيْهِ بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ فَإِذْ لَمْ يَأْتُوا بِالشُّهَدَاءِ فَأُولَـٰئِكَ عِندَ اللَّـهِ هُمُ الْكَاذِبُونَ ﴿١٣﴾
13. Mbona hawakuleta mashahidi wane. Na kwa kutoleta mashahidi, basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo
وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ لَمَسَّكُمْ فِي مَا أَفَضْتُمْ فِيهِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٤﴾
14. Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake katika dunia na akhera, bila shaka ingeliwapata adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyojiingiza.
إِذْ تَلَقَّوْنَهُ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَتَقُولُونَ بِأَفْوَاهِكُم مَّا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ وَتَحْسَبُونَهُ هَيِّنًا وَهُوَ عِندَ اللَّـهِ عَظِيمٌ ﴿١٥﴾
15. Mlipoyapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyoyajua, na mkifikiri ni dogo kumbe kwa Mwenyezi Mungu ni kubwa.
وَلَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُم مَّا يَكُونُ لَنَا أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَـٰذَا سُبْحَانَكَ هَـٰذَا بُهْتَانٌ عَظِيمٌ ﴿١٦﴾
16. Na mbona mliposikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya; utakatifu ni wako! Huu ni uzushi mkubwa.
يَعِظُكُمُ اللَّـهُ أَن تَعُودُوا لِمِثْلِهِ أَبَدًا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧﴾
17. Mwenyezi Mungu anawaonya msirudie kufanya kama haya kabisa ikiwa nyinyi ni waumini.
وَيُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١٨﴾
18. Na Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.
إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٩﴾
19. Hakika wale ambao wanapenda kueneza uchafu kwa waliaomini watapata adhabu chungu duniani na akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.
وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّـهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٠﴾
20. Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake na kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye kurehemu.
WALIOLETA UONGO
Aya 11 – 20
KISA CHA UZUSHI KWA UFUPI
Wameafikiana wafasri na wapokezi wa makundi yote na madhehebu ya kiislamu, isipokuwa waliotoka nje ya kundi, kwamba Aya hizi zilishuka kumuondolea tuhuma ya zina Bibi Aisha.
Sababu ya tuhuma ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.
w
)
alikuwa akitaka kusafiri, hupiga kura baina ya wake zake. Yule atakayepa- ta kura huongozana naye.
Mnamo mwaka wa tano wa Hijra, Mtume alipigana vita na Bani Mustalaq. Kura ikamwangukia Aisha, akaongozana naye. Mwenyezi Mungu akampa ushindi Mtume wake na akamuoa binti wa kiongozi wao Harith, baada ya kusilimu huyo binti. Jina lake lilikuwa Barra, Mtume akamgeuza jina na kumwita Juwayriya. Baba yake alisilimu pamoja na watu wengi wa kabila lake.
Mtume akarudi Madina pamoja na msafara wake wa ushindi, akisafiri usiku na mchana. Mpaka ilipofikia usiku wa pili akashuka na jeshi lake kupumzika kidogo.
Alipotangaza kuondoka msafara, Aisha alikwenda haja, aliporudi akapoteza mkufu wake. Akarudi kuutafuta. Aliporudi akakuta msafara wa jeshi umekwishaondoka. Akangoja palepale kuwa pengine wakimkosa kwenye msafara wanaweza kumrudia.
Swafwan bin Mua'ttwal alikuwa nyuma ya msafara, akampitia Aisha na akamjua, kwa sababu ilikuwa ni kabla ya kuteremshwa hukumu ya hijabu. Akampeleka mnyama wake naye akajitenga kidogo, mpaka alipopanda. Akamfikisha kwenye msafara au Madina.
Hapo wazushi wakapata nafasi, wakaanza kueneza uongo na kumtuhumu Aisha kufanya hiyana na Safwan. Wa kwanza aliyeuachia ulimi wake na uongo huu ni raisi wa wanfiki, Abdallah bin Ubayya, akaudakia Hassan bin Thabit, na Misatah na wanafiki wengineo. Ndipo Mwenyezi Mungu akatermsha Aya hizi kumuondolea tuhuma Aisha.
Kwa mansaba huu tunaashiria mambo mawili:
Kwanza
: kwamba Shia Imamiya wanaitakidi na kuamini kwamba wake wa mitume wote ni wasafi walio twahara na kwamba Mtume yoyote haweki maji yake ila kwenye tumbo lililo twahara.
Na mke wa Mtume anaweza kukufuru, lakini hawezi kuwa mzinifu. Kwa sababu mtume ni mtukufu zaidi kwa Mola wake, hawezi kumjaalia chini yake muasharati.
Anasema mwanachuoni, Imam Tabrasi (mshia) katika Tafsiri yake Majmau'labayan: "Hakika wake wa mitume ni lazima wawe safi na hali hii, kwa sababu ni aibu.
Mwenyezi Mungu amewatakasa Mitume wake na hilo kwa kuwapa heshima na kawaadhimisha na kuwaepusha na jambo ambalo litasababisha kukataliwa kauli zao na miito yao."
Ibn Abbas anasema: "Hakuzini mke wa Mtume kabisa. Khiyana ya mke wa Nuh ilikuwa ni kumfanya Nabii kuwa mwendawazimu na khiyana ya mke wa Lut ilikuwa ni kuwajulisha wale mahabithi kuhusu wageni wake."
Jambo la pili: Kuna baadhi wamesema kwamba Mtume(s.a.w.
w)
alimtaka shauri Imam Ali
miongoni mwa aliowataka shauri, akamshauri ampe talaka, na kwamba hilo eti ndio lilomfanya Aisha kupigana na Imam katika vita vya Jamal (ngamia). Waliosema kauli hii wameitegemeza kwenye riwaya ambayo hatuijui usahihi wake; mbali ya kuwa Mtume hahitajii ushauri wa yeyote katika maamuzi yake, kwa kuzingatia kuwa yeye ni mjuzi na mbora zaidi ya viumbe wengine wote.
Vipi Mtume anaweza kumtilia shaka mkewe na hali anajua kwamba yeye ni mtukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kujaaliwa chini yake kahaba? Lau Mtume angelimtilia shaka Aisha angelikuwa ndiye aliyekusudiwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mbona mlipousikia, wau- mini wanaume na waumini wanawake hawakujidhania mema na kusema huu ni uzushi dhahiri?"
Hapana! Muhammad(s.a.w.
w
)
hakumtilia shaka Aisha. Na mwenye kumnasibishia shaka hii atakuwa ameleta uzushi mkubwa.
Zaidi ya hayo, kuna riwaya nyingine inayosema kwamba Imam Ali
alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu:"Hakika viatu vyako havina najisi je mkeo."
Na kwamba Mtume alifurahi kwa hilo. Ismail Haqiy katika Ruuhl-bayan anasema: "Mtume alimtaka ushauri Ali kuhusu Aisha, akasema kuwa ni msafi na nimeuchukua usafi huo kutokana na tukio lililotutokea siku moja tulipokuwa tunaswali nyuma yako ukiwa na viatu vyako; kisha ukavua kiatu kimoja. Tukasema tuifanye ni sunna hiyo? Ukasema: Hapana Jibril ameniambia kuwa kiatu chako hicho kina najisi.
Basi ikiwa kiatu tu hakiwezi kuwa na najisi, vipi ahli yako? Basi Mtume akafurahi kwa hilo.
Sisi hatutaji riwaya hizi kwa kuwa tunaziamini, isipokuwa ni kuonyesha riwaya zinazopinga ushauri wa talaka.
MAANA
Hakika wale walioleta uzushi ni kundi miongoni mwenu. Msiufikirie ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu.
Wale ambao walimzulia khiyana Aisha ni kundi lililodhihirisha kuwa ni waongo na wazushi; kwamba wao wako kwenye mila ya kiislamu na kumbe hawamo kabisa.
Hilo lilimkera Nabii na maswahaba, ndio Mwenyezi Mungu Mtukufu akawambia msidhanie ni shari na madhara, hapana! Bali kuna manufaa mengi katika hili; ikiwemo kujulikana mumin aliye mwema na yule mnafiki habith ambaye anapenda kueneza uovu kwa wasiokuwa na hatia. Manufaa mengine ni majaribio ambayo yatawazidisha uongofu walioongoka na kuwazidishia wanafiki hasara.
Kila mmoja katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi.
Katika wao hapa ni wale waliozusha uongo. Maana ni kuwa kila mmoja katika hawa ana adhabu kwa kiasi alivyeeneza na kutangaza uongo na uzushi. Kwa kuwa tuhuma ya kutusi iliwathibitikia Hassan Bin Thabit, Mistah na mwanamke mmoja wa kikuraishi, Mtume aliwapa adhabu (hadd) ya viboko thamanini. Lakini Abdallah bin Ubayya alitafuta mbinu za kuhepa na kuponyoka adhabu kutokana na hadhari yake na kuwatosa wenzake. Yeye ndiye aliyekusudiwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:
Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao atapata adhabu kubwa
duniani kwa kumfedhesha kwake na kumdhihirisha vitim- bi vyake kwa watu, kiasi ambacho mmoja wa vigogo wa kabila la Khazraj alikitafuta kichwa. Vilevile kigogo wa kabila la Ausi; kama ambavyo vijana wengi wa kiansari akiwemo mwanawe walimtafuta kumuua. Ama adhabu yake katika akhera ni chungu na kubwa.
Mbona mlipousikia, waumini wanaume na waumini wanawake hawakujidhania mema na kusema huu ni uzushi dhahiri?
Mlipousikia, ni huo uzushi. Makusudio ya kujidhania ni kuwadhania wenzao wengine, kwa sababu binadamu wamejengwa kwa mshikamano mmoja; hasa waumini. Kwani imani ni ahadi na kulindana. Kuna Hadith isemayo: "Waumini ni kama nafsi moja" na Qur'an nayo inasema: "Hakika waumini wote ni ndugu" (49:10).
Matumizi haya kwenye Qur'an ni mengi; kama vile: "Wala msijiue." Juz.5 (4:29) pia katika Aya 61 ya Sura hii tuliyo nayo: 'Mjitolee salaam.'
Aya inaashiria kwamba mumin wa kweli, haijuzu kwake kunyamaza kama akisikia maneno ya uzushi na ya ubatilifu. Ama kauli mashuhuri inayosema: 'Ikiwa maneno ni fedha basi kunyamaza ni dhahabu' inakusudia kusema bila ya elimu na maneno ya upuzi na ubatilifu, kama uongo, kusengenya na fitina.
Unaweza kuuliza
: Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:"Na kusema huu ni uzushi."
inafahamisha kuwa ni wajibu kuukadhibisha na kuukana uovu na zina kwa kiasi cha kuisikia tu, bila ya kuthibitisha; jambo ambalo haliafikiani na misingi ya kiakili na kiislamu inayosema: 'Mwenye kukana kwa ulimi ni sawa na mwenye kuthibitisha, kila mmoja wao anahitaji dalili mkataa?'
Jibu
: Ndio ni kweli; hakuna shaka kabisa na msingi huu na kwamba unaenea katika kila kitu, lakini makusudio ya kukana hapa sio kuikana hiyo zina yenyewe na kuijua kwake Mwenyezi Mungu, hapana! Bali makusudio hapa ni kukana hukumu yake na matokeo yake, kama kutekeleza adhabu. Kwa hiyo inatakikana izingatiwe kama vile haikutendeka mpaka ithibitike kisharia.
Ndio maana ikawa mwenye kutuhumu anatandikwa viboko thamanini, ikiwa hakuthibitisha. Kwa maneno mengine ni kuwa kukosekana dalili ya kisharia kwenye zina ni dalili ya kukosekana hukumu na matokeo. Ushahidi mkubwa katika hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
Mbona hawakuleta mashahidi wane. Na kwa kutoleta mashahidi basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo;
yaani ni wongo katika hukumu ya Mwenyezi Mungu duniani. Ama elimu yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo inafungamana na uhakika wa mambo itabakia akhera.
Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake katika dunia na akhera, bila shaka ingeliwapata adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyojiingiza.
Mliyojiingiza ni yale ya uzushi. Rehema ya Mwenyezi Mungu kwa muasi duniani ni kule kumsitiri na kumpa muda ili aweze kutubia. Na katika akhera ni kusamehewa akitubia na kurejea.
Kisha akabainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) sababu ya kustahiki kwake adhabu kubwa duniani na akhera, kwa kusema:
Mlipoyapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyoyajua, na mkifikiri ni dogo kumbe kwa Mwenyezi Mungu ni kubwa.
Mnayazungusha maneno ya uzushi kwenye ndimi zenu na wengine wanayachukua bila ya dalili, huku mkidhani kuwa jambo hilo ni dogo, lakini mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa na lenye dhambi.
Miongoni mwa kauli za Imam Ali
ni"Ulimi ni mnyma mkali ukiachiwa unauma"
Na mbona mliposikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya kabisa,
sikwambii kuyatilia shaka tena. Bali inatakikana kuuepusha ulimi na kuizungumza zina hata kama itathibitika kisharia isipokuwa katika hali ya kukemea na kukataza. Wale wanojiburudisha kwa kuizungumzia zina na uovu ni wale wapumbavu na waovu zaidi katika watu.
Utakatifu ni wako! Huu ni uzushi mkubwa.
Ni kitu gani kikubwa zaidi kuliko kuwazulia wasiokuwa na hatia? Mumin wa kweli ni yule anayemtetea ndugu yake wala hamtuhumu kwa uovu na shari.
Mwenyezi Mungu anawaonya msirudie kufanya kama haya kabisa ikiwa nyinyi ni waumini.
Anawaonya na anawakataza. Kama haya ni haya ya uzushi. Haijuzu kufanya upuzi na kusikiliza. Kuufunga utiifu na imani ni ishara kuwa mumin akikatazwa na Mwenyezi Mungu kitu au akiamrishwa basi anafuata na kutii
Na Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.
Anawafafanulia halali na haramu katika Kitabu chake na katika ulimi wa Mtume wake, anamjua kila mmoja aliye muasi na aliye mtiifu na kuamil- iana naye kwa ujuzi wake, uadilifu wake na hekima yake.
Hakika wale ambao wanapenda kueneza uchafu kwa waliaomini watapata adhabu chungu duniani na akhera.
Uchafu ni mazugumzo machafu. Hakuna tofauti baina ya mwenye kutenda uchafu na mwenye kuutangaza. Kila mmoja ataadhibiwa ikithibitika kuwa amefanya au ametuhumu na akhera atakuwa na adhabu ya kuungua. Kila mwenye kasoro anapenda awe na wanaofanana naye. Kwa sababu mwenye kasoro huwa hawezi kuona ukamilifu kwa mwenzake.
Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.
Mumin hasemi wala hafanyi bila ya kujua, bali anayarudisha asiyoyajua kwa anayejua.
Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, ingeliwapata adhabu kubwa.
Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mpole Mwenye kurehemu waja wake akiwatakia kheri hata kama wanajitakia shari.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ وَمَن يَتَّبِعْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ فَإِنَّهُ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ مَا زَكَىٰ مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ أَبَدًا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يُزَكِّي مَن يَشَاءُ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢١﴾
21. Enyi ambao mmeamini! Msifuate nyao za shetani. Na atakayefuata nyayo za shetani, basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, asingelitakasika miongoni mwenu yoyote kabisa. Lakini humtakasa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi.
وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنكُمْ وَالسَّعَةِ أَن يُؤْتُوا أُولِي الْقُرْبَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَكُمْ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢﴾
22. Na wale katika nyinyi wenye wasaa wasiape kutowapa walio jamaa na maskini na waliohama katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe na wachilie mbali. Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
إِنَّ الَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ الْغَافِلَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ لُعِنُوا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Hakika wanaowasingizia wanawake wanaoheshimika, walioghafilika walio waumini, wamelaaniwa duniani na akhera na watapata adhabu kubwa.
يَوْمَ تَشْهَدُ عَلَيْهِمْ أَلْسِنَتُهُمْ وَأَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٤﴾
24. Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao kwa waliyokuwa wakiyatenda.
يَوْمَئِذٍ يُوَفِّيهِمُ اللَّـهُ دِينَهُمُ الْحَقَّ وَيَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ الْمُبِينُ ﴿٢٥﴾
25. Siku hiyo atawatekelezea sawa malipo yao ya haki na watajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye haki iliyo wazi.
MSIFUATE NYAYO ZA SHETANI
Aya 21 -25
MAANA
E
nyi am
b
a
o mmeamini! Msifuate nyao za shetani
kwa kutangaza uovu kwa wale ambao wameamini, wala kwa jambo linalotia wasiwasi na kuwavutia kwake.
Na atakayefuata nyayo za shetani, basi yeye huamrisha machafu na maovu.
Anayewezwa na shetani nafsini mwake, humuongoza kwenye mabaya na machafu.
Na lau si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, asingelitakasika miongoni mwenu yoyote kabisa.
Mwenyezi Mungu ametufahamisha njia ya kheri na njia ya shari, akatukataza hili na akatuamrisha lile, akatupa uwezo wa kutenda na kuacha na akaufungua mlango wa toba kwa mwenye kuasi. Hii ndiyo fadhila yake. Ama utakaso wake huwa hampi isipokuwa mwenye kusikia na akatii.
Lakini humtakasa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni Msikizi
,Mjuzi
na mwenye hekima pia. Hawatakasi isipokuwa wenye amali na nyoyo safi.
Na wale katika nyinyi wenye wasaa wasiape kutowapa walio jamaa na maskini na waliohama katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Imepokewa kuwa Aya hii ilishuka kwa ajili ya Abu Bakri alipoapa kutomsaidia Mistah Bin Athatha baada ya kushiriki pamoja na aliyeshiriki kueneza uvumi wa uovu kumhusu Ummul-mu'min (Mama wa waumin). Sifa hizi tatu zote anazo Mistah: Ni mtoto wa mama mdogo wa Abu bakr, ni maskini asiyekuwa na mali naye ni katika wahajiri na waliopigana Badri.
Na wasamehe na waachilie mbali. Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.
Hii ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kumsamehe na kumre- hemu atakayemsamehe aliyemfanyia ubaya. Imam Zaynul'abidin
alikuwa akimsamehe anayemfanyia ubaya, kisha anamwambia Mwenyezi Mungu: Ewe Mola wetu! Hakika wewe umeamrisha tumsamehe atakayetudhulumu, nasi tumesamehe, kama ulivyoamrisha, basi tusamehe; kwani hakika wewe ndiwe mbora zaidi wa hilo kuliko sisi.
Hakika wanaowasingizia wanawake wanaoheshimika, walioghafilika walio waumini, wamelaaniwa duniani na akhera na watapata adhabu kubwa.
Katika Aya ya 4 ya Sura hii Mwenyezi Mungu (s.w.t) alibainisha kwamba mwenye kumtuhumu mwanamke kwa zina na asilete mashahidi wane basi adhabu yake duniani ni kuchapwa viboko thamanini vyovyote vile atakavyokuwa na hakutaja adhabu yake akhera.
Katika Aya hii tuliyo nayo, anabainisha malipo yake huko akhera, ambayo ni adhabu kubwa, ikiwa aliyetuhumiwa ni ni msafi mwenye kujiheshimu na hayo aliyotuhumiwa. Ndio makusudio ya wenye kughafilika; yaani wenye kughafilika na zina, hawaifanyi wala hawaifikirii.
Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao kwa waliyokuwa wakiyatenda.
Duniani inahitajika ushahidi ikiwa mwanamke anadai kuwa ametuhumiwa na mdaiwa akikataa. Akishindwa kuthibitisha basi madai yake yatakataliwa. Lakini huko akhera hakuhitajiki ushahidi, kwa sababu mtendaji hana njia ya kukana. Lau tukikadiria kuwa atakana au kujaribu kukana, basi viungo vyake vitamshuhudia. Kila kiungo kitashuhudia kile kilichofanya. Ulimi wake utashuhudia ulichozungumza, mkono na ulichokishika na mguu na ulichokiendea n.k.
Siku hiyo atawatekelezea sawa malipo yao ya haki na watajua kwam- ba hakika Mwenyezi Mungu ndiye haki iliyo wazi.
Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawahisabu kesho na kuwalipa malipo ya haki na ya uadilifu. Hapo ndio watajua kwamba ufufo, hisabu na malipo walioahidiwa ni kweli, hakuna kuyakimbia.