22
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا ﴿٢١﴾
21. Hakika nyinyi mna ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – kwa mwenye kumtarajia Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi.
وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَـٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا ﴿٢٢﴾
22. Na waumini walipoyaona makundi walisema: Haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hayo hayakuwazidishia ila imani na utii.
مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا ﴿٢٣﴾
23. Miongoni mwa waumini wapo wanaume waliotimiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea; wala hawakubadilisha ahadi yao hata kidogo.
لِّيَجْزِيَ اللَّـهُ الصَّادِقِينَ بِصِدْقِهِمْ وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ إِن شَاءَ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٢٤﴾
24. Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa ukweli wao na awaadhibu wanafiki, akipenda, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ وَكَانَ اللَّـهُ قَوِيًّا عَزِيزًا ﴿٢٥﴾
25. Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha wale ambao wamekufuru na ghadhabu yao; hawakupata kheri yoyote. Na Mwenyezi Mungu amewakifia waumini, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye uwezo.
وَأَنزَلَ الَّذِينَ ظَاهَرُوهُم مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن صَيَاصِيهِمْ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ فَرِيقًا تَقْتُلُونَ وَتَأْسِرُونَ فَرِيقًا ﴿٢٦﴾
26. Na akawateremsha wale waliowasaidia katika watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao; na akatia hofu katika nyoyo zao. Badhi yao mkawa mnawaua na wengine mnawateka.
وَأَوْرَثَكُمْ أَرْضَهُمْ وَدِيَارَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ وَأَرْضًا لَّمْ تَطَئُوهَا وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا ﴿٢٧﴾
27. Na akawarithisha ardhi yao na majumba yao na mali zao na ardhi ambayo hamjaikanyaga. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.
RUWAZA NJEMA KWA MTUME
Aya 21 – 27
MAANA
Hakika nyinyi mna ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – kwa mwenye kumtarajia Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi.
Makusudio ya ruwaza hapa ni mfano wa kuigwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
, na kumtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho ni kutaraji thawabu za Mwenyezi Mungu na neema za akhera; na kumkumbuka kwa wingi ni kinaya cha kuswali Swala tano.
Maneno ‘Hakika nyinyi’ yanaelekezwa kwa wale waliomwacha Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
katika vita vya Ahzab. Makusudio ni kuwatahayariza na kuwalalumu, kwa vile walimwacha Mtume wakati mgumu; wakiwa wao wanadai ni waislamu na kuswali na pia kudai wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.
Maana ya Aya hii ni kama ile isemayo: “Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio kandoni mwao kubaki nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu; wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake.” Juz. 11 (9:120).
Aya hii iaashiria kuwa mwislamu wa kweli hasa ni yule anayemfuata na kumwiga Mtume wake bila ya kumwasi na jambo lolote.
Unaweza kuuliza
: mafakihi wameafikiana kuwa mwenye kusema: Lailaha illallah, Muhadur-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu) atatendewa wanayotendewa waislamu, awe mtiifu au mwasi, sasa itakuwaje?
Jibu
: Ndio atatendewa muamala wa kiislamu katika maisha haya ya dunia; kama vile kuozwa, urithi n.k. Lakini muamala katika maisha haya ni jambo jingine na kuzingatiwa kuwa yeye ni mwislamu mbele ya Mwenyezi Mungu ni jambo jingine.
Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa waislamu wanagawanyika mafungu mawili: Kuna mwislamu mbele za watu, lakini sio mbele ya Mwenyezi Mungu; naye ni yule aliyesema: Lailaha illallah, Muhadur-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu) na huku anamwasi Mwenyezi Mungu na Mtume. Huyu atafanyiwa muamala wa Mwislamu duniani tu.
Mwingine ni yule aliyesema Lailaha illallah, Muhadur-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu) na akamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Huyu atafanyiwa muamala wa Mwislamu duniani na akhera. Imam Ali (a.s.) anasema: “Ufukara na utajiri ni baada ya kuonekana kwa Mungu (Siku ya Kiyama).”
Na waumini walipoyaona makundi walisema: Haya ndiyo aliyotuahi- di Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hayo hayakuwazidishia ila imani na utii.
Wafsiri wa zamani wametaja kauli mbili kuhusiana na Aya hii. Ilio na nguvu zaidi ni ile isemayo kuwa Mtume alikuwa amewaahidi waislamu kupatwa na misukosuko aina kwa aina na kwamba makafiri na washirikina watajitokeza kuwapiga vita na kutaka kuwafyeka kabisa.
Ahadi hii imeelezwa katika Aya ismayo: “Au mnadhani kuwa mtaingia Peponi na hali hamjajiwa na mfano wa wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara” Juz. 2 (2:214).
Waislamu walipoona makundi ya majeshi yakiwazingira kila upande, walisema haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hali hiyo ikawazidishia imani na utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake wakazidi imani juu ya imani. Ama wanafiki na wale walio na maradhi nyoyoni mwao walisema: ‘Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakutuahidi ila udanganyifu.’
Miongoni mwa waumini wapo wanaume waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu
katika jihadi na uthabiti wakati wa kukutana na adui, mpaka wakati wa kufa.
Baadhi yao wamekwisha kufa
kabla ya vita vya Ahzab; kama mashahidi wa vita vya Badrina baadhi wanangojea
kufa shahid au ushindi;wala hawakubadilisha ahadi yao hata kidogo.
Vile vile wanafiki na wenye maradhi nyoyoni, hawakubadilika; bali walikufa na unafiki.
Wafasiri wanasema kuwa Anas bin Annadhr hakuwepo kwenye vita vya Badr; akasikitika na akasema: sikuwepo kwa mashuhudio ya kwanza alioshuhudia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
, lakini kama Mwenyezi Mungu Mtukufu bado ataniononyesha mashuhudio mengine pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
, basi ataona nitakavyofanya.
Basi akawako kwenye vita vya Uhud. Akakutana na Sa’d bin Mua’dh, aka- muliza: “Mpaka wapi ewe Abu Amru?” Akajibu: “Nakimbila harufu ya Pepo. Wallah mimi ninaisikia Uhud.” Basi akapigana mpaka akauwawa. Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwake. Kwenye kiwiliwili chake kitukufu kulipatikana majeraha ya panga, mikuki na mishale karibu thamanini.
Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa ukweli wao na awaadhibu wanafiki, akipenda, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.
Pia ni Mwadilifu na Mwenye hekima; hafanyi upuzi wala mchezo katika matakwa yake na vitendo vyake. Humpa thawabu anayestahiki; kama vile wakweli na wenye imani, ikiwa wataendelea na ukweli wao na imani yao. Na atawaadhibu makafiri na wanafiki, ikiwa watang’ang’ania ukafiri na upotevu. Ikiwa watatubia basi atawapa rehema yake na atawasamehe yaliyopita.
Kusema kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Na anawaadhibu wanafiki, akipenda,’ maana yake ni kuwa atawaadhibu ikiwa hawatatubia.
Dalili ya hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.’ Yaani wakitubia atawakubalia toba yao atawasamehe na atawapa rehema yake.
Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha wale ambao wamekufuru na ghadhabu yao.
Ni yale makundi yaliyokusanyika kumuua Mtume(s.a.w.w)
kwa kuongozwa na Abu Sufyan. Hawakupata kheri yoyote; yaani lile walilodai kuwa ni kheri; kumuua Mtume na wale walioamini pamoja naye.
Na Mwenyezi Mungu amewakifia waumini na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye uwezo.
Yaani amewatoshea kwenye vita. Abu Hayani Al-Andalusi katika Tafsir yake Al-Bahrul- muhit anasema: “Mwenyezi Mungu aliwatoshea kwenye vita kwa kupeleka upepo na majeshi ambayo ni Malaika. Na imesekana ni Ali bin Abi Twalib na wale waliokuwa pamoja naye. Walipambana, na Ali akamuua Amr.”
Kuna Hadith isemayo: “Pigo la Ali la siku ya Khandaq ni bora kuliko amali za watu na majini.” Riwaya nyingine inasema: “Kupambana Ali na Amr ni amali bora zaidi katika umma wangu hadi siku ya Kiyama.”
Wamenukuu riwaya hizi Al-Hakim katika Mustadrak. Juz. 3 uk. 32, Sayyid Muhsin Al-Amin katika A’yanushia Juz. 2 na Sheikh Al-Mudhaffar katika Dalailussidq Juz. 2.
KISA CHA BANI QURAYDHA KWA UFUPI
Na akawateremsha wale waliowasaidia katika watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao; na akatia hofu katika nyoyo zao. Badhi yao mkawa mnawaua na wengine mnawateka. Na akawarithisha ardhi yao na majumba yao na mali zao na ardhi ambayo hamjaikanyaga. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.
Yaani waliwasaidia maadui. Makusudio ya watu wa Kitabu hapa ni Bani Quraydha. Ama makusudio ya ardhi ambayo hamjaikanyaga ni bishara ya ushindi wa kiislamu.
Hapo nyuma kidogo tumeeleza kuwa Bani Quraydha walikuwa wakiishi na Mtume(s.a.w.w)
huko Madina au kwenye vitongoji vyake na kwamba walikuwa wameahidiana na Mtume kutomsaidia adui. Lakini makundi yalipouzingira mji wa Madina walivunja ahadi na wakatangaza vita; kama ilivyo desturi ya mayahudi wa zamani na wa sasa.
Aya mbili hizi tulizo nazo zinadokeza yaliyowatokea Bani Quraydha baada ya kuvunja ahadi yao na kushindwa jeshi la washirikina; kwa ufupi ni kama ifuatavyo:
Mwenyezi Mungu alipowatoshea waislamu na vita vya Ahzab, msemaji wa Mtume alipiga mbiu ya kuwa watu wawatokee Bani Quraydha. Jeshi la waislamu lilipowafikia lilizingira ngome zao. Mtume akawakaribisha kwenye Uislamu; kwamba watastahiki kama wanavyostahiki waislamu wengine; vinginevyo atawazingira mpaka wasilimu au wapigane.
Kiongozi wao Ka’b bin Asad akawashauri kusilimu na kumwamini Muhammad(s.a.w.w)
, akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu! imekwishawabainikia kuwa yeye ni Nabii aliyetumwa na kwamba yeye mnamkuta kwenye Tawrat.” Lakini walikataa na wakasema: “Hatutaiacha dini yetu.”
Vikwazo viliendelea hadi siku ya ishiri na tano, wakawa karibu waangamie kwa kuchoka na hofu. Ndipo wakamtaka Mtume - kwa hiyari yao wenyewe- wahukumiwe na Sa’d bin Mua’dh, aliyekuwa kiongozi wa Aus waliokuwa na urafiki na Bani Quraydha. Mtume akawakubalia ombi lao na akamwita Sa’d akamwambia: “Hawa wametaka kuhukumia na wewe kwa hiyari yao, basi hukumu kwa unalopenda.” Sa’d akasema: “Na hukumu yangu itatekelezwa?” Mtume(s.a.w.w)
akasema: “Ndio.”
Basi Sa’d akahukumu kwamba wanaume walioshiriki vitani wauawe. Mali yao ichukuliwe, watoto wao na wanawake wao wachukuliwe mateka na majumba yao yachukuliwe na Wahajiri sio Ansari, kwa sababu Ansar tayari wanayo majumba na Wahajiri hawana.
Basi Nabii(s.a.w.w)
akaamuru wauliwe wanaume wale walioshika silaha na wale waliowachochea Bani Quraydha kuvunja ahadi; kama Hayy bin Akhtab, kiongozi wa Bani Nadhir. Kisha mali ikagawanywa, watoto na wanawake wakawa mateka; kama alivyohukumu Sa’d, aliyechaguliwa na Bani Quraydha wenyewe. Hapa ndipo panapoashiriwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Badhi yao mkawa mnawaua na wengine mkawa mnawateka.’
Tumetangulia kuuleza kuwa mboni ya jicho la Saa’d ilidungwa na mshale wa majeshi ya Ahzab naye akaomba asife hadi aridhike kwa watakavyotiwa adabu Bani Quraydha. Basi baada ya kutekeleza hukumu yake kwao jeraha lilitutumka naye akafariki, radhi za Mungu ziwe kwake, moyo wake ukiwa umetulia kwa kufa shahidi na kukubaliwa dua yake.
JE MUHAMMAD ALIWADHULUMU BANI QURAYDHA?
Unaweza kuuliza
: Ilikuwaje Mtume(s.a.w.w)
aithibitishe hukumu ya Sa’d iliyokuwa ya nguvu na ukatili; kiasi ambacho maadui wa uislamu wamelifanya tukio hili ni nyenzo ya kuutuhumu na kuutusi Uislamu?
Jibu
: Muhammad hakuwadhulumu Bani Quraydha; isipokuwa walijidhulumu wenyewe, kwa kujichagulia wao wenyewe mwishilio huu, kwa ushahidi ufuatao:
Kwanza
: wao waliahidiana na Mtume na wakavunja ahadi katika wakati mgumu, kama ilvyo desturi ya mayahudi kuanzia zamani hadi sasa. Mwenyezi Mungu anasema: “Je, kila mara wanapofunga ahadi, kikundi katika wao huitupa? Juz. 1 (2:100).
Pili
: Mtume(s.a.w.w)
aliwaambia kuwa atawaacha bila ya kuwafanya lolote, kwa sharti waseme: Lailaha illallah, Muhadur-rasulullah (Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu). Kiongozi wao, Ka’b bin Asad aliwanasihi wamkubalie Muhammad na watamke shahada mbili, wakakataa.
Tatu
: Bani Quraydha walikataa kuhukumiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
na wakakubali hukumu ya Saa’d.
Nne, Saa’d aliwahukumu kwa sharia yao wanayohukumia watu na wanayoifuata hadi leo, inayosema: “Utakaposongea karibu ya mji kwenda kupigana juu yake, ndipo utakapowapigia ukelele wa amani.
Itakuwa watakapokujibu kwa amani, na kukufungulia, ndipo watu wote watakaoonekana humo, watafanya kazi ya shoka, na kukutumikia. Na kama hautaki kufanya amani nawe, lakini utafanya vita juu yako, ndipo uhusuru; na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga; lakini wanawake na watoto na wanyama wa mji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana, Mungu wako” (Kumbukumbu 20: 10 – 14)
.
Hii inafahamisha kuwa hukumu yao ni kali zaidi ya alivyohukumu Saa’d, kwa sababu hii inasema wazi kuwa mji ukikubli suluhu basi watu wake wote ni watumwa na ukikataa basi wanaume wote wauliwe kwa makali ya upanga, waliopigana na wale wasiopigana na kuchukua mali na kuwateka watoto na wanawake.
Kuna ibara nyingine iliyo kali zaidi ya hii, kwa sababu inaamuru wauliwe wakazi wote, mpaka wanawake na watoto, kisha mji uchomwe na vyote vilivyomo, kwa namna ambayo haitawezekana kujengwa tena; inasema:
“…Hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo na wanyama na walio humo, kwa makali ya upanga na nyara zake zote uzikusanye katikati ya njia yake; na uuteketeze kwa moto na nyara zake zote, kuwe sadaka kamili ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wako, nao utakuwa magofu milele usijengwe tena” (Kumbukumbu 13:15 – 16).
Je, baada ya yote inafaa kusemwa kuwa Muhammad amewadhulumu Bani Quraydha na kwamba Saa’d aliwaonea kwa alivyowahukumu? Ni katika hukumu ya uadilifu kumpa mtu lile alilolitaka mwenyewe na kuhukumiwa kwa mujibu wa dini na itikadi yake.
Mayahudi wanaitakidi dini yao na kuifuata kwa matendo kwa kuwachinja wanaume kupora mali kuwateka wanawake, kuvunja majumba na kuchoma vijiji na miji kwa watu wote bila ya hata kuwa na vita nao au kuwa wamevunja ahadi au kufanyiwa hata chembe ya ubaya; kama wanavyowafanyia wapalestina hivi sasa.
Je, atahisabiwa ni dhalimu aliyewahukumu kwa wanavyowafanyia watu wengine? Tena Mtume(s.a.w.
w
)
aliwaua wale waliovunja ahadi tu na wakatangaza vita. Lakini wao wanaua na wanachoma si kwa lolote ila ni kwa kuwa kuua, kuchoma na ufisadi ndio dini yao.
Hata kama wasingevunja ahadi na kutangaza vita, wakahukumiwa kuuawa, kuporwa mali na kuchukuliwa mateka, bado isingelikuwa ni dhulma, kwa sabu wamehukumiwa kwa mujibu wa dini na wanavyofanya wao.
Sharia zote za dini za Mungu na kanuni za kutungwa zimeafikiana kuwa mwenye kufuata dini atalazimiwa na hukumu zake. Hapa ndio kuna siri ya kauli ya Mtume mtukufu(s.a.w.w)
aliyomwambia Saa’d: “Umewahukumu kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu kutoka juu ya mbingu saba.”
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا ﴿٢٨﴾
28. Ewe Mtume! Waambie wake zako: Ikiwa nyinyi mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni niwape kitokanyumba na niwaache mwachano mzuri.
وَإِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٢٩﴾
29. Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia watenda mema, miongoni mwenu, malipo makubwa.
يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَن يَأْتِ مِنكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾
30. Enyi wake wa Mtume! Yeyote kati yenu atakayefanya uchafu dhahiri, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.
EWE NABII, WAAMBIE WAKE ZAKO
Aya 28 – 30
MAANA
Wake za Mtume(s.a.w.w)
walimtaradhia Mtume matumizi zaidi na mapambo, kutokana na ngawira alizompa Mwenyezi Mungu, ndipo ikashuka Aya hii:
Ewe Mtume! Waambie wake zako: Ikiwa nyinyi mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni niwape kitoka-nyumba na niwaache mwachano mzuri. Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia watenda mema, miongoni mwenu, malipo makubwa.
Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake mtukufu awahiyarishe wakeze mambo mawili: Ama awaache pamoja na kitoka-nyumba, ikiwa wanataka, wanayoyataka wanawake wengine, ya dunia.
Kitoka-nyumba ni kitu anachotoa mtaliki kumpa mtalaka wake, kwa kuangalia uwezo wa mwanamume. Tazama Juz. 2 (2:236 – 237).
Au waishi na Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kuvumilia shida [10]
1 na malipo yao mbele ya Mwenyezi Mungu huko akhera yatakuwa makubwa.
Basi wake za Mtume(s.a.w.w)
wakachagua akhera na wakaiacha dunia na mapambo yake. Aya hii inaitwa Ayatut-takhyir (Aya ya kuhiyarisha).
MTUME NA WAKE WENGI
Aya ya takhyir ni dalili mkataa ya kukadhibisha madai ya wanaokuza mambo, kuwa Mtume alikuwa na wake kwa sababu ya matamnio ya nafsi. Kwa sababu mwenye pupa ya kustarehe na wanawake – kama alivyosema Mustafa Sadiq Rafi – hawezi kuwahiyarisha baina ya kuachana nao au kuishi maisha ya tabu mpaka siku ya mwisho; bali angeliwabembeleza na kuwaambia kuwa atafanya bidii awatimizie. Kuna mithali isemayo: “Tandiko la harusi liko ghali.”
Anasema Al- aqad katika kitabu chake: Abaqriyatul-Islamiyya: “Lau ladha ya hisia kama ingelikuwa ndio kichocheo cha kuoa baada ya kufa Khadija, basi angeliridhisha hisia zake kwa kuoa wasichana tisa wanaosifika kwa urembo huko Makka na Madina na Bara Arabu kwa ujumla. Na bila shaka angewataka wangelimkubali haraka na kwa kujionea fahari, pia mawalii wao wangeliuridhia na kuuonea fahari ukwe huu ambao haushindwi na ukwe wowote.”
Kisha Al-aqad akataja wake za Mtume mmoja baada ya mmoja na akabainisha sababu zilizopelekea kuwaoa na akasema: “Hakika wanaokuza mambo wamesahahu kila hakika miongoni mwa hakika za maisha haya ya ndoa na wakasahau kuwa Muhammad aliitwa mtakatifu na mtawa wakati wa ujana wake, na kwamba yeye alikaa miaka ishirini na tano na hakuchoka katika kuitafuta halali.
Pia wamesahau kwamba alipotaka kuoa katika miaka hiyo alimuoa mwanamke wa miaka 40 aliyemchagua kwa haja ya kuzoena, wala hakuchagua uzuri uliotakiwa kwa starehe. Wamesahau kwamba mtu waliyempa sifa za hisia za starehe, siku nyingine hakuwa akishiba na mkate wa shairi. Yote haya wameyasahau, na yamethibiti katika historia. Wameyasahau kwa vile wanataka kutia kasoro na kuupotosha uhakika.”
Enyi wake wa Mtume! Yeyote kati yenu atakayefanya uchafu dhahiri, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.
Makusudio ya uchafu hapa ni maasi ya aina yoyote na dhahiri ni waziwazi. Wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wana daraja tukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na ya watu kwa kuungana kwao na Mtume mtukufu(s.a.w.w)
. Yeyote atakayefanya maasi atakuwa amehatarisha nafasi yake na kustahiki mara mbili zaidi ya anavyostahiki mwingine. Kwa sababu Mwenyezi Mungu huwahesabu watu kulingana na vyeo vyao; kama wanavyohisabiwa kadiri ya akili zao. Amewalaumu manabii kwa namna ambayo hamlaumu mwingine.
SHARTI YA KUCHAPA
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini
ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
MWISHO WA JUZUU YA ISHIRINI