2
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA
مَّا كَانَ عَلَى النَّبِيِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ اللَّـهُ لَهُ سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ قَدَرًا مَّقْدُورًا ﴿٣٨﴾
38. Hakuna ubaya kwa Nabii kufanya ambalo amefaradhiwa na Mwenyezi Mungu. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa waliopita zamani na amri ya Mwenyezi Mungu ni kadara iliyokwisha kadiriwa.
الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّـهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّـهَ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٣٩﴾
39. Ambao walifikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kumwogopa yeye, wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye anayetosha kuhisabu.
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾
40. Hakuwa Muhammad ni baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
KISA CHA ZAINAB BINT JAHSH
Aya 36 – 40
JE, MTUME ALIMTAMANI ZAINAB BINT JAHSH?
Maneno yamekuwa mengi kuhusiana na Aya hizi, kutoka kwa wanaoutetea Uislamu na pia maadui zake. Hawa waliutuhumu utakatifu wa Mtume, wakasema kuwa Mtume alimtamani Zainab bint Jahsh As-Saadiyya binti wa shangazi yake Umayma, mke wa huria
wake Zayd bin Haritha, na kwamba hilo alilificha kwa kuhofia watu, sio kumuhofia Mwenyezi Mungu. Wakitumia kauli yake Mwenyezi Mungu:“Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea.”
Watetezi wa Uislamu wakawajibu kwa kiuhakika na kimantiki, ingawaje wengine wamefuata njia inayoleta tuhuma. Lakini pamoja na hivyo sisi tutakuwa na msimamo usiopendelea, tukilazimiana na dhahiri ya tamko, hatutafanya taawili wala kutoka kwenye dalili za Aya, kisha tumwachie msomaji mwenye kuchunga haki ahukumu mwenyewe. Kabla ya kuanza kufasiri tutatanguliza yafuatayo: Zayd bin Haritha alikuwa mtumishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.
w
)
.
Siku moja akaja baba yake kwa Mtume na akamtaka ama amwache huru mwanawe au amuuzie kwa bei yoyote anayotaka. Mtume wa huruma akamwacha huru kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na akampa hiyari ya kwenda na baba yake au abakie.
Zayd akaathirika na Mtume kuliko kwenda na baba yake. Hapo baba yake, Haritha, akasema: “Enyi jamaa wa kikuraishi! Shuhudie kuwa huyu si mwanangu tena.” Mtume(s.a.w.
w
)
naye akasema:“Shuhudieni kuwa ni mwanangu.”
Watu wakadhani kuwa Mtume amemfanya Zayd kuwa ni mwanawe wa kupanga, wakawa wanamwita Zayd bin Muhammad.
Waarabu kabla ya Uislamu walikuwa na desturi ya kumfanya mtoto wa kupanga ni sawa na mtoto wa kiuhakika hata kwenye mirathi na uharamu wa nasaba. Wenye akili wote wema na waovu wanaafikiana kuwa ada inayorithiwa kutoka jadi ni kama sharia na dini, haifai kwa yoyote kuihalifu kwa hali yoyote atakayokuwa.
Hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ikataka kuiondoa ada hii, kwa vitendo sio kwa kauli tu, kwa kumuoza Zayd bin Haritha, ambaye jana alikuwa ni mtumwa asiyekuwa na uwezo wowote, mke mwenye hadhi ya kinasabu na uzuri. Hakuna anayemfikiria kumuoa isipokuwa mwinyi tu. Naye ni Zaynab bint Jahsh. Na mama yake ni Umayma bint Abdul Muttwalib, babu wa Mtume(s.a.w.
w
)
. Na kwamba Zayd amalize haja yake, ampe talaka kisha aolewe na Mtume(s.a.w.
w
)
.
Kwa sababu hilo litakuwa na nguvu na ufasaha zaidi wa kukataza desturi hiyo kwa upande mmoja. Na kwa upande mwingine mamwinyi wasione kigegezi kuwaoa waliotalikiwa na mahuria wao na walala hoi. Na zaidi ya hayo asiwe na madharau yule mwenye nasaba tukufu au walii wake kumuoza aliye chini yake kihadhi au kinasaba.
Mwenyezi Mungu akalipitisha hilo na akalikadiria, kama alivyoesema Mwenyezi Mungu (s.w.t):“Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kadara iliyokwisha kadiriwa
.”
Mwenyezi Mungu (s.w.t) akampa wahyi Mtume wake mtukufu kwa kadhaa na kadari hiyo, akamwamrisha kumuoza Zaynaba kwa Zayd.
Basi Mtume akaja kumchumbia Zaynab kwa ajili ya huria wake Zayd na akaficha moyoni mwake yale aliyompa wahyi Mwenyezi Mungu kuwa amepitisha amuoe yeye baada ya Zayd. Aliuficha Mtume wahyi huu kwa sababu ulikuwa mzito kwa watu kutokana na kuwa mbali na desturi na mila zao. Kuficha huku ndiko alikokuashiria Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: ‘Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea.’
Hata hivyo Abdallah, kaka yake Zaynab, alikataa kumuoza dada yake kwa mtu ambaye si kufu yake naye mwenyewe pia akakataa kuolewa. Ndipo ikashuka kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu ‘Haiwi kwa mumin mwananamume wala mumin mwanamke, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapoamua jambo, kuwa na hiyari katika jambo lao.’ Basi hapo Zaynab na kaka yake wakainyenyekea hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na ikafungwa ndoa.
Baada ya kupita muda uhusiano wa ndoa ukawa una matatizo. Zayd akaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akitaka kumpa talaka Zaynab; hata hivyo akamkataza na akamwamrisha awe na subira, lakini amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ipite; ikawa talaka. Baada ya kwisha eda Mtume akamuoa na nidhamu ya mtoto wa kupanga ikavunjikilia mbali.
Kwa hiyo basi suala la Mtume kumuoa Zaynab si suala la matamanio na mapenzi; bali ni suala la amri ya Mwenyezi Mungu, kadha na kadari yake kwa nukuu ya Aya zilizo wazi ambazo wazushi wamejaribu kuzipotoa na kuziletea tafsiri ile wanayoitaka wao kulingana na hawa zao.
Hizi hapa nukuu zinazosema waziwazi: ‘Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.’ ‘Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kadara iliyokwisha kadiriwa.’ ‘Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea.’
Makusdio ya amri ya Mwenyezi Mungu na yenye kukadiriwa na lile analolidhihirisha Mwenyezi Mungu ni jambo moja – Mtume kumuoa Zaynab ambako Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekutangaza waziwazi kwa kusema: ‘tulikuoza.’
Kama Mtume angelikuwa ameficha matamanio, waliyoyazusha wakuza mambo, basi Mwenyezi Mungu angeliyadhihirisha kutokana na kauli yake:‘Aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha.’
Zaidi ya hayo ni kuwa Zaynab alikuwa mikononi mwa Mtume (alikwa akimjua) na alikuwa akimtii zaidi kuliko viungo vyake. Kama angelikuwa anamtamani basi asingelingoja kwanza amuoze huria wake kisha amalize haja naye ndipo amuoe. Hasha! Bwana wa watu na majini hawezi kuwa na matamanio na hawa hizo. Yuko mbali kabisa na hayo.
Baada ya hayo ni kuwa Aya zote hizi zimekuja kwa maudhui moja, kwa hiyo zinaungana na kushikana; wala haiwezekani kwa hali yoyote kuzitenganisha na kuzigawa mafungu. Ama kuzichukua zote au kuziacha zote.
Mwenye kuchukua kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea,’ kuwa ni jumla iliyo peke yake na akaipuuza kauli yake: ‘aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha’ na ‘amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa,’ basi atakuwa ni katika wale wanaoipotosha haki kwa kuifanyia inadi na watu wake.
Kutokana na utangulizi huu, maana ya Aya yatakuwa yako wazi na pia makusudio yatakuwa yamejulikana. Kwa hiyo tutazipitia juu juu, tukiashiria mfuatano wa Aya kulingana na kisa cha ndoa ya kwanza hadi ya pili.
MAANA
Haiwi kwa mumin mwanamume wala mumin mwanamke, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapoamua jambo, kuwa na hiyari katika jambo lao. Na yeyote mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi amepotea upotevu ulio wazi.
Aya hii ilishuka pale Mtume(s.a.w.
w
)
alipomchumbia Zayanb bint Jahsh kwa ajili ya huria wake, Zayd bin Haritha. Zaynab akakataa yeye na kaka yake kwa vile Zayd sio kufu yake.
Maana ni kuwa ndoa hii ni amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na yeyote katika waumini hana hiyari mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekataa basi atakuwa katika wapotevu wa kuangamia. Basi hapo Zaynab na kaka yake wakaridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na ndoa ikakamilika.
Na pale ulipomwambia yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemsha nawe ukamneemesha.
Huyo ni Zayd bin Haritha. Mwenyezi Mungu alimneemesha kwa uislmu na usuhuba pamoja na Mtume naye Mtume akamneemessha kwa kumwacha huru.
Shikamana na mkeo na mche Mwenyezi Mungu.
Baada ya kupita muda, uhusiano wa ndoa baina ya Zaynab na Zayd ukawa sio mzuri. Akamwambia Mtume(s.a.w.
w
)
: “Nataka nimtaliki.” Mtume akamuusia kushikamana naye na amche Mwenyezi Mungu katika hali zote. Lakini Mtume alikuwa na hakika kuwa Zayd atakuja mwacha Zaynab kisha amuoe; isipokuwa hakulidhihirisha hilo kwa kuhofia lawama, ndio Mwenyezi Mungu akamwambia kwa kumwelekeza:
Ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, na ukachelea watu na hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya kumchelea.
Makusudio ya aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha, ni ndoa ya Mtume kwa Zaynab baada ya kuachwa na Zayd. Mwenyezi Mungu aliidhihirisha kwa kauli yake:
Basi Zayd alipokwisha haja naye, tulikuoza.
Haya ndiyo aliyoyaficha Muhammad(s.a.w.
w
)
na akayadhihirisha Mwenyezi Mungu. sasa yako wapi hayo matamnio aliyoyaficha Muhammad katika nafsi yake. Kwanini Mwenyezi Mungu alinyamaza baada ya kusema: ‘Aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyadhihirisha.’ Mtume alificha kujua kwake kuwa Zayd atamwacha Zaynab na amuoe yeye. Ni kuficha huku ndiko alikoambiwa na Mwenyezi Mungu kuwa mtu aliye kwenye nafasi yako hatilii umuhimu lawama za anayelaumu na kauli za wanaobobokwa.
Ili isiwe tabu kwa waumini kuoa wake wa watoto wao wa kupanga watakapokuwa wamekwisha haja nao. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.
Ndoa ya Mtume ilikuwa ni ubainifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waumini na kwa watu wote kuwa hakuna ubaya kuoa wake wa watoto wao wa kupanga ambao wamemaliza haja nao.
Hakuna ubaya kwa Nabii kufanya ambalo amefaradhiwa na Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimwamrisha Mtume wake kumuoa mtalaka wa mwanawe wa kupanga, ili kubatilisha desturi hiyo ya kijahilia. Mtume akaitikia amri ya Mwenyezi Mungu.
Kwa hiyo Mtume au mwingine hana lawama kumuoa mtalaka wa mtoto wake wa kupanga, hata kama watu watamlaumu na kumtia kasoro, madamu Mwenyezi Mungu amemuhalalishia.
Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa waliopita zamani na amri ya Mwenyezi Mungu ni kadara iliyokwisha kadiriwa. Ambao walifikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kumwogopa yeye, wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ndiye anayetosha kuhisabu.
Makusudio ya wale waliopita na wale waliofikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, ni mitume waliotangulia. Maana ni kuwa hakuna Nabii yeyote ila Mwenyezi Mungu alimtuma kulingania haki na kukataza batili, kama vile desturi na maigizo ambayo Mwenyezi Mungu hakuyateremshia dalili yoyote.
Mtume alifikisha ujumbe wa Mola wake kwa uaminifu na kwa ikhlasi, hakulegeza wala hakubabaisha na hakumwogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, alipata tabu nyingi sana katika hilo.
Wako waliofanana nawe ewe Muhammad katika mitume waliopita. Hisabu ya wakadhibishaji na wenye inadi ni kwa Mwenyezi Mungu tu peke yake.Hakuwa Muhammad
(s.a.w.
w
)
ni baba wa yeyote katika wanaume wenu
kwa nasaba wala kwa kuzaa, kuweza kumzuia kumuoa mtalaka wa Zayd bin Haritha.
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.
w
)
alizaa watoto wane wa kiume, wa tatu kutokana na Khadija; nao ni: Qasim, Twayyib, na Twahir. Imesemekana kuwa ni wawili, kwamba Twahir ndiye huyo huyo Twayyib. Na mmoja aliyetokana na Maria Qibtiya ambaye ni Ibrahim. Wote walikufa utotoni.
Ama Hasan na Husein ni watoto wa binti yake Fatima aliyewazaa na Ali
, lakini Mtume aliwazingatia kama wanawe, pale aliposema:“Wanangu hawa wawili ni maimamu wakisimama au wakikaa.”
Pia alisema:“Watoto wa binti wote wananasibiana na baba yao; isipokuwa watoto wa Fatima, mimi ni baba yao.”
Tazama Juz. 7 (6:84 – 90).
Bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu
Na Mtume si baba, ingawaje anawashughulikia sana waumini na kuwahu- rumia kuliko baba zao.
Na mwisho wa mitume,
hakuna Nabii mwingine baada ya Muhammad(s.a.w.
w
)
wala sharia nyingine baada ya sharia ya kiislamu.
Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu,
ukiwemo ujuzi wa kujua pale atakapouweka ujumbe wake na kuuishiliza kwa Muhammad(s.a.w.
w
)
.
KWA NINI UTUME ULIISHIA KWA MUHAMMAD?
Waislamu wote wameafikiana kwa kauli moja kwamba hakuna wahyi kwa yeyote baada ya Muhammad(s.a.w.
w
)
Mwenye kulipinga hilo basi si mwislamu, mwenye kudai utume baada ya Muhammad ni wajibu kuawa na mwenye kutaka dalili ya atakayedai utume huu, kwa kutaraji kumsadiki, basi ni kafiri.
Katika Tafsiri ya Isamil Haqiy, Ruhul-bayan, imeelezwa:“Lau angekuja Nabii baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.
w
) angelikuwa Ali bin Abi Twalib, kwa sababu yeye yuko kwenye daraja ya Haruna kwa Musa.”
Unaweza kuuliza
: Kwa nini utume umeishilia kwa Muhammad(s.a.w.
w
)
?
Jibu
: lengo la kwanza na la mwisho la kutumwa Nabii ni kufikisha kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake. Hakuna kitu chochote alichotaka Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwafikishia waja wake ila kimo kwenye Qur’an Tukufu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kubainisha kila kitu.”
Juz. 14 (16:89).Na akasema: “Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote.”
Juz. 7 (6: 38).
Yaani kitu chochote kinachoamabatana na wadhifa wa mitume na kuhusika kwao katika kuwaongoza viumbe na kuwaelekeza kwenye masilahi yao yanayodhamini ufanisi katika nyumba mbili (duniani na akhera).
Wala hakuna nyenzo ya kuthibitisha hakika hii ila kwa majaribio yasiyokubali shaka wala mjadala; yaani wataalamu wanatakikana waisome Qur’an kwa ukamilifu kuanzia alifu yake mpaka yee yake, kisha wailinganishe na vitabu vingine vya dini. Tuna hakika kabisa kuwa wataishia kwenye mambo mawili:
Kwanza
: kwamba Qur’an kwa ufasaha wake, itikadi yake na sharia yake ni zaidi ya vitabu vyote vya kidini.
Pili
: ndani ya Qur’an watakuta misingi na misimamo yote ambayo inaona na haja za watu, masilahi yao na maendeleo yao hadi siku ya Kiyama.
Hakuna maendelo yoyote ya kielemu au mapinduzi yoyote ya uhuru, ila Qur’an inayatolea mwito na kuyabariki. Na hakuna sharia yoyote anayoihitajia binadamu katika historia ila wataalam wanaweza kuitoa kutoka katika moja ya misingi ya Qur’an na misingi yake.
Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamemruhusu kila mwenye uwezo na maandalizi kutoa tanzu katika mizizi ya Qur’an na kutoa hukumu iliyo na heri na masilahi kwa watu kwa namna fulani. Maana yake ni kuwa hukumu ya mujtahidi mwadilifu ni hukumu ya Qur’an na ya Mtume. Ndio maana kuna Hadith isemayo kuwa kuipinga hukumu yake ni kama kuipinga hukumu ya Mwenyezi Mungu.
Vile vile hii inamanisha kuwa Mtume yuko kwa kuweko Qur’an ambayo haingiliwi na batili mbele yake wala nyuma yake. Amepatia Ibn Al-arabiy aliposema: “Mwenye kuhifadhi Qur’an ameuunganisha utume mbavuni mwake” lakini kwa sharti ya kuizingatia na kuiamini kwa imani safi.
Zaidi ya hayo, Muhammad ni mtu aliyepewa wahyi; kama Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na mitume wengineo, lakini Mwenyezi Mungu amemuhusu kwa ambayo hakumuhusu nayo yeyote katika mitume. Pamoja na kuwa Mwenyezi Mungu alimpa kila Mtume ubora wote, kwa sababu utume ni mama wa ubora wote, lakini ubora una daraja. Kuna mbora na mbora zaidi, mkamilifu na mkamilifu zaidi, mjuzi na mjuzi zaidi na mkarimu na mkarimu zaidi. Mwenyezi Mungu anasema: “Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya manabii kuliko wengine.” Juz. 15 (17:55).
Mwenyezi Mungu amemuhusu Muhammad(s.a.w.
w
)
kwa sifa na daraja ya hali ya juu; kiasi ambacho hakuna zaidi yake isipokuwa Mwenyezi Mungu na sifa za Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa sifa hizo ni kukamilishwa wahyi ulioteremshwa kwake kukamilika katika pande zote. Dalili ya hilo ni hii Qur’an ambayo ni ubainifu wa kila kitu ambacho kinaingia katika wadhifa wa mitume. Basi wapi na wapi hiyo na vitabu vingine? Haya nawalete wapinzani kimoja tu kilicho na ubainifu wa kila kitu.
Bwana wa mitume na wa mwisho wao aliashiria haya kwa kusema:“Hakika mfano wangu na mfano wa manabii walikokuwa kabla yangu, ni kama mfano wa mtu aliyejenga jengo akalijenga vizuri na akalipamba; ispokuwa sehemu ya tofali moja. Ikawa watu wanapoliona wanastaajabu huku wakisema: “Mbona huweki hili tofali? Basi mimi ndio tofali hilo na mimi ni mwisho wa mitume.”
Tutaishiliza jawabu, kwa yale tuliyoyasema kwenye kitabu Imamatu Ali wal-aql (Uimamu wa Ali na akili): Mtu akisema: “Kwa nini Muhammad(s.a.w.
w
)
akawa ndiye mwisho wa mitume?
Tutamjibu kuwa Muhammad na dini ya Muhammad ina sifa zote za ukamilifu na imefikia kikomo; sawa na jua lilivyofikia kikomo cha nuru.
Hakuna nyota yoyote wala umeme wowote unaoweza kujaza nuru ulimwenguni kote zaidi ya jua. Kadhalika hakuna Nabii atakayeleta kheri kwa watu baada ya Muhammad(s.a.w.
w
)
. Maudhui haya yanaungana na tuliyoyaandika kwa anuani ya ‘Dini na maisha’ katika Juz. 9 (8:24), Juz. 15 (17: 9) na Juz. 21 (30:30).