14
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU
Sura Ya Hamsini na Moja: Surat Adh-Dhariyat. Imeshuka Makka. Ina Aya 60.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا ﴿١﴾
1. Naapa kwa zinazotawanya sana.
فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا ﴿٢﴾
2. Na zinazobeba mizigo.
فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا ﴿٣﴾
3. Na zinazokwenda kwa wepesi.
فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا ﴿٤﴾
4. Na zinazogawanya amri.
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ ﴿٥﴾
5. Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka ni kweli.
وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ ﴿٦﴾
6. Na kwa hakika dini bila ya shaka itatokea.
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ ﴿٧﴾
7. Naapa kwa mbingu zenye umbile zuri.
إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ ﴿٨﴾
8. Hakika nyinyi bila ya shaka mko katika kauli inayokhitalifiana.
يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ ﴿٩﴾
9. Anageuzwa nayo mwenye kugeuzwa.
قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ ﴿١٠﴾
10. Wazushi wameangamizwa.
الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ ﴿١١﴾
11. Ambao wameghafilika katika ujinga.
يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٢﴾
12. Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ ﴿١٣﴾
13. Ni siku watakayojaribiwa Motoni.
ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ ﴿١٤﴾
14. Onjeni fitna yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza.
NAAPA KWA ZINAZOTAWANYA
Aya 1 – 14
MAANA
Naapa kwa zinazotawanya sana, na zinazobeba mizigo, na zinazokwenda kwa wepesi, na zinazogawanya amri.
Katika kufasiri sifa hizi nne kuna rai kadhaa: Kuna waliosema kuwa Makusudio ya zinazotawanya ni pepo, zinazobeba ni mawingu zinazokwenda kwa wepesi ni jahazi na zinazogawanya ni malaika.
Kauli yenye nguvu ni kuwa zote hizi ni sifa za pepo. Ndizo zinazotawanya kwa vile zinatawanya mchanga nk. Akitumia neno hilo, Mwenyezi Mungu Mtufu anasema:
هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ...﴿٤٥﴾
“Majani makavu yaliyokatikakatika yanayopeperushwa na upepo.” Juz. 15 (18:45).
Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameapa kwa upepo kuashiria manufaa yake, pia kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kuapa na kila anachokitaka katika viumbe vyake. Tazama Juz. 23 (37:1-10)
Sifa ya pili ni ‘Na zinazobeba mizigo,’ Makusudio yake hapa ni kuwa pepo zinabeba mzigo wa mawingu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtufu:
سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَّيِّتٍ ﴿٥٧﴾
“Tunayasukuma kwa ajili ya mji uliokufa.” Juz. 8 (7:57).
Sifa ya tatu: ‘Na zinazokwenda kwa wepesi,’ ni kuwa pepo zinakwenda kwa wepesi zikiwa zinabeba mawingu. Sifa ya nne: ‘Na zinazogawanya amri.’ Pepo zinatawanya mvua katika ardhi; kama ilivyoelezwa kwenye Juz. 8 (7:57).
Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka ni kweli, Na kwa hakika dini bila ya shaka itatokea.
Hili n jawabu la kiapo. Makusudio ya mnayoahidiwa ni uhai baada ya mauti. Na dini ni hisabu na malipo.Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu atawafufua tu walio makaburini, hilo halina shaka. Na kwamba Yeye atamlipa mtu kwa matendo yake. Yakiwa heri basi ni heri na yakiwa shari basi ni shari.
Naapa kwa mbingu zenye umbile zuri.
‘Umbile zuri’ tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu ‘Hubuk’ ambalo wafasiri wamelitolea kauli nyingi. Lakini iliyo na nguvu ni hii tuliyoifasiri; kwa maana ya kuwa katika maumbile ya mbingu kuna mpangilio, nidhamu, uzuri na kupendeza.
Hakika nyinyi bila ya shaka mko katika kauli inayokhitalifiana.
Msemo unaelekezwa kwa wale wanaomkadhibisha Mtume(s.a.w.w)
na kauli zao zote ni za mgongano, mkorogano, uwongo na njozi; kama vile kusema kuwa Mtume ni mshairi, mara mwendawazimu na mara nyingine ni mchawi. Na kuhusu Qur’an wakasema ni vigano vya watu wa kale au imetungwa na Muhammad(s.a.w.w)
n.k.
Anageuzwa nayo mwenye kugeuzwa.
Yaani anageuzwa na dini na haki yule anayeigeuka kwa hawa na ujinga; mfano wake ni sawa na kauli: “Hapofuki na hilo ila kipofu.”
Wazushi wameangamizwa.
Hao ni wale aliowabainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kusema:
Ambao wameghafilika katika ujinga.
Ujinga na upotevu umewavaa kuanzia kichwani hadi unyayoni, wakazipeleka dhana zao ovyoovyo na bila ya msingi wowote, kwenye ardhi na mbinguni na kwenye ufufuo na malipo. Wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika katika mawe na ana mabinti katika Malaika na wengine aliozaa na majini. Ama ufufuo na hisabu kwao ni upotevu.
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
Wenye dharau wanauliza, huo ufufuo utakuwa lini? Mwenyezi Mungu (s.w.t) naye anawajibu:
Ni siku watakayojaribiwa Motoni.
Ufufuo utakuwa siku watakayoonyeshwa moto na kuunguzwa humo. Husemwa kuwa kitu kimejaribiwa, ili kutoa kilichoghushiwa, kikiunguzwa motoni. Malaika wa Motoni watawaambia:
Onjeni fitna yenu! Haya ndiyo mliyokuwa mkiyahimiza.
Hii ndio adhabu mliyokuwa mkihimiza na kuifanyia dharau jana. Je, mmeionaje ladha yake?
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿١٥﴾
15. Hakika wenye takua watakuwa katika mabustani na chemchem.
آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ ﴿١٦﴾
16. Wakipokea aliyowapa Mola wao. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ ﴿١٧﴾
17. Walikuwa wakilala kidogo tu usiku,
وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Na kabla ya alfajiri wakiomba maghufira.
وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ ﴿١٩﴾
19. Na katika mali zao ipo haki ya mwenye kuomba na anayejizuia.
وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini
وَفِي أَنفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٢١﴾
21. Na katika nafsi zenu, Je, hamwoni?
وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyoahidiwa.
فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ ﴿٢٣﴾
23. Basi naapa kwa Mola wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo, kuwa nyinyi mnasema.
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ ﴿٢٤﴾
24. Je, imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanaohishimiwa?
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ ﴿٢٥﴾
25. Walipoingia kwake wakasema: Salam! Na yeye akasema: Salam! watu nisiowajua.
فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ ﴿٢٦﴾
26. Akaenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliyenona.
فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ﴿٢٧﴾
27. Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً قَالُوا لَا تَخَفْ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ ﴿٢٨﴾
28. Akahisi kuwaogopa. Wakasema: Usiwe na khofu, na wakambashiria kupata kijana
mwenye ilimu.
فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ ﴿٢٩﴾
29. Ndipo mkewe akawaelekea, na ukelele na akapiga uso wake, na kusema: kongwe tasa!
قَالُوا كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ ﴿٣٠﴾
30. Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyosema Mola wako. Hakika Yeye ni Mwenye hikima Mjuzi.
HAKI YA MWENYE KUOMBA NA ASIYEOMBA
Aya 15 – 30
MAANA
Hakika wenye takua watakuwa katika Mabustani na chemchem. Wakipokea aliyowapa Mola wao. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
Mwenyezi Mungu (s.w.t) anapokea kutoka kwa wema matendo yao; kama alivyosema:
وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ ﴿١٠٤﴾
“Na huzipokea sadaka.” Juz. 11 (9:104).
Yaani anazikubali sadaka na kuzilipa. Vilevile watu wema watapokea thawabu walizopewa kwa shangwe na furaha. Kwa maneno mengine ni:
رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١٩﴾
“Mwenyezi Mungu amewawia radhi na wao wamemwia radhi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.”
Juz. 7 (5:119).
Walikuwa wakilala kidogo tu usiku, na kabla ya alfajiri wakiomba maghufira.
Walikuwa wakilala usiku, lakini kidogo, na mara nyingi tahajudi yao inaungana na alfajiri, wakifanya tasbihi na istighifari.
Imam Ali
anasema katika wasifu wao:“Ama wakati wa usiku wanatandika miguu yao wakisoma Qur’an kwa mpangilio… wakipitia Aya yenye shauku wanakuwa na tamaa nayo …. Na wakipitia yenye hofu wanaitegea masikio ya nyoyo zao wakidhani kuwa Jahannam inachachati- ka na kuunguruma ndani ya masikio yao; basi wao wanainama kwa migongo yao wakitandika chini mapaji ya nyuso zao, na viganja vyao na ncha za nyao zao (yaani wanasujudu
) wakimtaka Mwenyezi Mungu azi
fungue shingo zao”
Na katika mali zao ipo haki ya mwenye kuomba na anayejizuia.
Mwenye kuomba ni yule anayeomba watu sadaka, na anayejizuia ni fukara ambaye anajizuia kuomba watu. Huyu amesadikishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtufu:
يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ﴿٢٧٣﴾
“Asiyewajua anawadhania kuwa ni matajiri kwa kujizuia. Utawafahamu kwa alama zao; hawaombi watu wakan’gan’gania.” Juz. 3 (2:273).
Neno ‘haki’ linafahamisha kuwa fukara ni mshirika wa tajiri katika mali yake. Hilo tumelizungumzia kwa ufafanuzi zaidi katika kifungu cha Zaka kwenye Juz. 3 2: (272-274) na katika Juz. 4 (3: 180-182) kwenye kifungu: ‘Matajiri ni mawakala sio wenyewe.’
MWENYEZI MUNGU NA MAARIFA YA HISIA
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini na katika nafsi zenu, Je, hamwoni?
Mwenye kupeleleza kwenye viumbe vyote vilivyoko na akachunguza kwa makini, hana budi kujiuliza: ni nani aliyepangilia kwa mpangilio wa uten- genezaji huu? Hatapata jawabu la kukinaisha na tafsiri sahihi isipokuwa kuweko nguvu ya hali ya juu inayoongoza. Ikiwa hatakinai na jibu hili, basi hatapata mbele yake isipokuwa sadfa na umbile pofu. Hakuna mwenye shaka kuwa hii inazidisha ujinga na upofu. Wamaada wanasema kuwa hakuna njia ya maarifa isipokuwa hisia na majaribio.
Na Mwenyezi Mungu haingii kwenye hisia wala majaribio. Kwa hiyo kumwamini hakutegemei dalili, bali ni ujinga na upotevu.
Tunajibu
:Kwanza
: hatukubaliani kuwa sababu za maarifa zinakuwa tu kwenye hisia na majaribio; bali kuna maarifa ya kiakili yanayofikiwa kwa nguvu ya dhahania. Na mwenye kuiangusha akili na mazingatio na akakana hoja inayohusiana nayo, atakuwa ameukana utu kabisa. Kwa sababu hakuna utu bila ya akili inayokata.
Zaidi ya hayo ni kuwa mwenye kukana maaarifa ya akili atakuwa ameipinga nafsi yake yeye mwenyewe; kwa kuwa atakuwa ameyakana maarifa ya akili kwa akili, na akatoa dalili ya kutokuweko kitu kwa kuweko kwake.
Pili
: Hata kama tungekubali kuwa hakuna njia ya maarifa isipokuwa hisia na majaribio, bado tunamthibitisha Mwenyezi Mungu kwa njia hiyo hiyo hasa. Kwamba yuko katika kila mashuhudio ya maumbile.
Ushuhuda huu umefikia ukomo wa uwazi na ufafanuzi na kutufikisha kwenye ilimu ya mwanzilishi, kwa kiasi cha kuangalia tu na kuchunguza bila ya kuhitajia mitambo wala ala zozote.
Lau kungekua kumjua Mwenyezi Mungu kunahitajia mitambo, basi kumwamini Mungu kungelikuwa kwa wataalamu peke yao, na isingelifaa kwa Mwenyezi Mungu kuwambia watu wote:“Enyi watu! Mcheni Mola wenu.”
Inajulikana wazi kuwa yeye, ambaye imetukuka hekima yake, amewajibisha imani kwa waja wake wote, lakini baada ya kuwawekea dalili mkataa ya kuondoa udhuru wote wa kutokuweko kwake. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amezisimamisha dalili hizi kutokana na maumbile ya kiakili na kwenye hisia vilevile kwa kutumia msingi wa kiakili unaosema: “Ushahidi ni wa mwenye kudai.”
Sisi sio tuliojitungia maneno haya wala kukosa adabu; isipokuwa Yeye, ambaye imetukuka hikima yake, ndiye aliyesema:
سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ ﴿٥٣﴾
“Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli.” Juz. 24 (41:53)
Mtu mwenyewe na vilivyo katika upeo ni katika vinavyoshudiwa na vinavyohisiwa vinavyofahamisha kuweko Mwenyezi Mungu. Na kwavyo inadhihiri haki isiyokuwa na shaka.
Mwenye kufuatilia Aya za Qur’an yenye hikima atajikuta yuko mbele ya idadi ya ishara hizi za kilimwengu zinazotoa mwito wa kumwamini Mwenyezi Mungu kwa njia ya maarifa ambayo ni matunda ya hisia na akili; miongoni mwayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtufu: “Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi na alivyoviumba Mwenyezi Mungu” Juz. 9 (7:185). Yaani vitu vinavyohisiwa na kuguswa.
Kumwamini Mwenyezi Mungu ni imani isiyoonwa na jicho wala kuguswa na mkono, lakini imani hii inalazimishwa na kuwekwa na vinavyoonwa na vinavyoguswa; sawa na anavyoamini daktari mjuzi kuwa kwenye mwili wa binadamu kuna ugonjwa fulani.
Na anaweza kugundua hivyo, kwa kiasi cha kumshika tu mgonjwa, bila ya kutumia darubini au kipimo chochote. Hakuna yeyote awe mumin au mlahidi ila atakuwa anaamini, kwa imani ya mkato, vitu vingi visivyoingia kwenye hisia.
Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyoahidiwa.
Yaani kuna sababu za riziki zenu; kama vile mvua n.k. Wakale walisema: “Lau si mbingu, watu wasingelibakia.”
Wametofautiana katika tafsiri ya “mliyoahidiwa.” Kuna aliyesema ni Pepo na Moto, mwingine akaseama ni heri na shari na wa tatu akasema ni riziki inayogawanywa.
Rai yetu ni kuwa Makusudio ya ya mliyoahidiwa ni sababu hasa za riziki, kwa dalili ya kuwa, Mwenyezi Mungu Mtufu, ameashiria kwenye Aya kwamba katika ardhi na katika nafsi zetu kuna ishara za kuhisiwa zinazoguswa, zinazomfahaisha Mwenyezi Mungu Mtufu na ukuu wake. Na kimsingi ni kuwa ishara za kuhisiwa katika mbingu zitakuwa ni mvua na sayari na wala sio Pepo, Moto nk.
Basi naapa kwa Mola wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo, kuwa nyinyi mnasema.
Razi amesema dhamiri inarudia kwenye Qur’an, kwa hiyo isemwe: ‘Hakika hiyo ni kweli;’ kama kwamba Mwenyezi Mungu amesema: Hakika Qur’an ni haki wameitamka malaika kama mnavyotamka nyinyi.
Hakuna mwenye shaka kuwa Qur’an ni haki isiyo na shaka na kwamba Jibril ameitamka pia, lakini kuanzia mwanzo wa sura hii hadi hapa tulipo bado haijatajwa Qur’an wala Malaika. Iiyotajwa ni siku ya malipo na hisabu katika Aya 12, kisha Mwenyezi Mungu akataja yaliyo katika ardhi na mbinguni kuwa ni dalili ya kuweko aliyeyaanzisha. Basi bora ni kuirudisha dhamiri kwenye yote haya.
Kwa hiyo basi Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameapa kwa utukufu wake kwamba Mwenyezi Mungu ni haki na ufufuo ni haki, wala haitakikani kutia shaka katika hayo, baada ya kusimama dalili; sawa na inavyotakikana kwa mtu kutoyatilia shaka aliyoyatamka.
Kuna riwaya inayosema kuwa bedui mmoja aliposikia Aya hii, alisema: “Nani huyo aliyemkasirisha Mwenyezi Mungu Mtufu mpaka akalazimika kuapa?” Haya si mageni kwa ambaye amekulia katika umbile alilozaliwa nalo.
Kwa manasaba wa hayo ni kua watu wa lugha wanasema: matamshi ni aina mbili: ya nje ambayo ni kutamka na ya ndani ambayo ni kufikiria na kutambua. Watu wa mantiki wakasema katika kumwelezea mtu kuwa ni mnyama anayetamka; yaani anayefikiria. Decarte naye anasema: “Mimi ninafikiria, kwa hiyo nipo.”
Misingi hii inakanusha shaka ya kuweko mwenye kufikiria, kwa sababu imetoka kwake hasa. Kwa hiyo tunaweza kufasiri kama ilivyokuwa nyinyi mnasema au kama ilivyokuwa nyinyi mnafikiria. Kwa sababu yote mawili, kutamka na kufikiria, yanakanusha shaka ya kuweko mwenye kutamka au kufikiria.
Je, imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanaohishimiwa?
Neno wageni tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu dhayf ambalo lina- tumika kwa mgeni mwanamume au mwanamke, mmoja au wengi.
Makusudio ya wageni wa Ibrahim ni malaika waliokuja kumpa bishara ya kumzaa Is-haq na kuangamizwa kaumu ya Lut. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewapa sifa ya waheshimiwa kwa kuwa ni waheshimiwa kwake na kwa waja wake waumini.
Walipoingia kwake wakasema: Salam! Na yeye akasema: Salam! watu nisiowajua.
Walimwamkia naye akawarudishia, akasema watu hawa hatuwajui.
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliyenona.
Ibrahim alifanya haraka kwenda kwa familia yake, akawaamuru wawaandalie wageni ndama aliyenona. Basi ikawa kama alivyotaka, nyama ikaiva,akawakaribisha, akasema: “Mbona hamli?
“ Lakini waliendela kutokula, kwa vile wao si watu, hawali chakula.
Akahisi kuwaogopa. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.
Walimjulisha jambo walilokuja nalo la kumpa habari njema ya kumzaa Is-haq.Ndipo mkewe
Sara aliposikia bishara ya Is-haqakawaelekea, na ukelele
wa mshangaona akapiga uso wake,
kwa furaha na mshangaona kusema
: Mimi nikikongwe tasa!
Nitazaa kweli?
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyosema Mola wako. Hakika Yeye ni Mwenye hikima Mjuzi.
Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni kikongwe tena tasa, lakini hikima yake inataka kukutunuku mtoto pamoja na uzee wako. Mwenyezi Mungu akilitaka jambo ni kuliambia ‘Kuwa na linakuwa.’
Tumefupisha tafsiri ya Aya hizi kwa vile ziko wazi na pia zimekwishatangulia katika Juz. 12 (11: 69-73) na katika Juz. 14 (15:51-56).