• Anza
  • Iliyopita
  • 7 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 9113 / Pakua: 4388
Kiwango Kiwango Kiwango
UANDISHI WA HADITHI

UANDISHI WA HADITHI

Mwandishi:
Swahili

TADWIN AL HADITH

UANDISHI WA HADITH

UCHUNGUZI WA KIHISTORIA JUU YA UKUSANYAJI NA UANDISHI WA HADITH

Kimeandikwa na:

RASUL JA'AFARIYAN

Kimetarjumiwa na

AMIRALY M. H. DATOO

(BUKOBA - TANZANIA)

UTANGULIZI

Umuhimu wa Hadith katika maadili ya mafunzo ya Kiislamu - ikiwemo Tafsir, Fiqh (Sharia), na maadili, n.k.- unakubalika katika madhehebu yote ya Kiislamu. Leo itakuwa ni vigumu kumpata mtu yeyote yule aatakayekuwa akidai kuwa Qur'an Tukufu inajitosheleza kwa Shariah ya mafunzo ya Kiislamu pamoja na maelezo bila ya msaada wa Sunnah na Hadith. Zaidi ya hayo, yapo matamko mengi ya Mtumes . a.w.w , na baadhi ya taarifa katika Qur'an yenyewe, ambazo zinaelekeza katika umuhimu wa amri na matendo ya Mtumes.a.w.w , Kwa hivyo ni dhahiri umuhimu uliopo juu ya Hadith na Sunnah za Mtumes.a.w.w , hivyo hapana shaka wala haja ya ushahidi kwa swala hili.

Madhumuni ya kitabu hiki ni kuchambua na kutazama vile mfumo wa Hadith ulivyokuja kuandikwa na kutazama muda uliotumika kukusanya matamko (kauli), matendo (fi'l) na kukubaliwa kwa ukimya (taqrir) wa Mtumes.a.w.w hadi kufikia katika sura ya ukusanyaji na uandishi. Ni dhahiri, swala hili linaweza kuwa na umuhimu wa kuchambua ushahidi wa mfumo wa Hadith.

Ama kuhusu swala la Qur'an, sisi twajua kuwa hapakuwapo na pengo la muda baina ya kufunuliwa Ayah za Qur'an na kuandikwa kwao. Vivyo hivyo, hapana shaka juu ya usahihi wa Qur'an, kwani Mtumes.a.w.w alikwishawachagua waandishi kuanzia mwanzoni mwa ufunuo na hapo walipatiwa kazi za kuzikusanya na kuzindika. Hata hivyo, utaratibu huu haukutumika katika swala la Hadith, ambavyo imekuja kupokelewa vinginevyo. Umuhimu wa hadith na daraka lake katika maswala ya kijamii na kisiasa vimesababisha baadhi ya makundi kuonyesha hali ya kiasi fulani cha kutovumilia kelekea hayo. Kutovumilia huku ndiko kuliko sababisha Hadith kucheleweshwa kusimuliwa na kuandikwa na kuenezwa. Na kwa masikitiko makubwa, kucheleweshwa huku kumeleta hali ya mtatanisho kwa ajili ya uthamini wake kwa vizazi vya baadaye.

Hata hivyo, ni lazima kutambulisha kuwa hali ya Hadith katika Shiah ilikuwa ni tosauti na ile hali ya Hadith za Ahl al-Sunnah Tofauti hii inatokana na imani ya Mashiah kuhusu Uimamu wa Shia wa Ahl al-Bayt a.s. ambapo kuwapo kwao ulikuwa ukiendelea hadi katikati ya karne ya 3 A.H. / 9 A.D. Kwa hivyo, Hadith zilizonakiliwa na Mashiah hazikukumbwa na matatizo ya kucheleweshwa kwa kuandikwa. Hapa sisi tutatazama kwa kimukhtasari sana uthibitishaji kuhusu swala hili, lakini sehemu kubwa ya uchambuzi huu utakuwa ukihusiana na historia ya uandikaji wa Hadith miongoni mwa zile za Ahl as-Sunna. Historia hii inaonyesha kuwa Hadith zilikuwa hazikuandikwa kwa kioindi fulani. Siyo hayo tu, hata kuzieneza kwao pia kulipigiwa marufuku kwa muda fulani, kwa kipindi cha miaka mia moja. Ahadith (wingi wa Hadith) zilienezwa kwa desturi ya matamshi tu. Ingawaje sehemu ya Hadith ilianza kuandikwa katika karne ya 2 A.H. / 9 A.D., sehemu yake kubwa iliandikwa tu baada ya muda wa kutosha kupita.

Hapa sisi tutatazama kwanza Maimamu( a.s ) wa Kishia wakisisitiza uandikaji wa Hadith. Na baadaye tutachukua historia ya uandikaji wa Hadith miongoni mwa Ahlal-Sunnah. Uchunguzi wa aina hii utatusaidia kama mwongozo kwa ajili ya kuthamini misingi halali ya Hadith ya Madhehebu zote za Islam na kutudhihirishia ipi iliyo na ufululizo wa uandikaji wa Hadith (bila ya kuvunjika kwa mfululizo huo) Umuhimu mkubwa wa uchunguzi huu ni utamini kwa undani wa sanad na mutun (kiini) cha Hadith, jambo ambalo linalohitaji utafiti maalum ingawaje baadhi ya kazi kama hizi zimeshaandikwa juu ya somo hili, lakini bado kunahitajika juhudi zaidi katika uchunguzi kama huu.

Kwa kifupi, kitabu hiki ni mkusanyiko wa makala yaliyokuwa yakichapishwa katika jarida la Al-Tawhid J. V, II uk. 39-55; j. V, III & IV uk. 71-84 na VI, I uk. 19-35 - Sazmaan Tablighaat Teheran Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Niliona kuwa itakuwa ni kazi yenye manufaa iwapo nitayakusanya hayo na kuyatarjumu katika lugha ya Kswahili katika sura ya kitabu.

Amiraly M.H.Datoo

P.O.Box 838

BUKOBA - TANZANIA

UANDISHI WA HADITH

1. MAIMAMU WA SHIA KATIKA UANDIKAJI NA UENEZAJI WA HADITH

Katika sehemu hii, twategemea kuzungumzia kwa mukhtasari msimamo wa Shia kuhusu uandikaji wa Hadith kutokea mwanzoni. Itaonekana kuwa ni kinyume na msimamo wa wengine kuhusu swala hili. Msimamo wa Kishia ulisisitiza mno juu ya uandikaji wa Hadith zikisaidia uhifadhi wake wakati ambapo Maulamaa mashuhuri wa Kisunni, hata kufikia mwanzoni mwa karne ya 3A.H./9 A.D. walikuwa wakipinga uandikaji wa Hadith. Ni baada ya uandikaji wa Hadith ulipokuwa dhahiri hao wanaopinga walipoanza kwenda kinyume na Hadith walizokuwa wamezitoa wakipinga uandishi na uenezaji wake na hapo wakaanza kuziandika. Alba ibn al-Ahmad ananakili kuwa mara moja Ali ibn Abi Talib a.s. wakati akitoa Hotuba juu ya mimbar, alibainisha: "Je, ni nani atakayeinunua elimu kwa Dirhamu moja?" Al-Harith ibn al-A' war alinunua karatasi yenye thamani ya Dirhamu moja na kumwijia Imam Ali ibn Abi Talib a.s. na kuandika kiasi cha kutosha cha elimu juu yake. Riwaya hii inatuonyesha vile Imam a.s. alivyokuwa akisisitiza juu ya uandikaji.

Imam Hassan ibn Ali ibn Abi Talib( a.s ) ameripotiwa akiwashauri watoto wake kama ifuatavyo:-

"Nyinyi sasa ni watoto wa Ummah ambao katika maisha ya mbeleni mtakuwa wakubwa wao. Jielimisheni Elimu; na yeyote yule miongoni mwenu atakayeweza kuhifadhi (kukariri) elimu (yaani Hadith), basi aiandike na kuiweka nyumbani mwake."

Imeripotiwa kuwa Hijr ibn Adi, mmoja wa Sahaba wa Mtumes.a.w.w na Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) , aliziandika Hadith za Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) katika kitabu na kuzirejea pale alipohitaji msaada wa mwongozo katika masuala mbalimbali Mifano hii inadhihirisha umuhimu aliokuwa ameuambatanisha Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) , watoto wake na Sahaba wake katika uandikaji wa Hadith. Mifano miwili ifuatayo itaonyesha dhahiri vile Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) alivyokuwa akisisitiza umuhimu wa Hadith na kuzihifadhi.

Umar ibn Ali anaripoti kuwa mtu mmoja alimwuliza Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) ni vipi kuwa yeye (Ali) aliweza kunakili na kusimulia Hadith nyingi za Mtumes.a.w.w kuliko Sahaba wengineo. Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) alijibu:"Hii ni kwa sababu daima nilipokuwa nikimwuliza swali Mtume s.a.w.w, alikuwa akinijibu maswali yangu. Na pale nilipokuwa nikiwa kimya, basi Mtume s.a.w.w alianzisha mazungumzo mwenyewe."

Ali ibn Hawshab anaripoti kutoka Makhul, mwanachuo kutokea Syria, kuwa Mtumes.a.w.w. aliisoma Ayah (69:12) Na hapo alimwambia Imam Ali ibn Abi Taliba.s "Mimi nimemwomba Allah swt kuwa masikio hayo yawe ni yako." Baadaye Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: "Mimi kamwe sikusahau Hadith yoyote au chochote kile kilichosikilizwa na sikio langu kikisemwa na Mtumes.a.w.w .

Umar ibn al-Harith anasema: "Wakati mmoja Alia.s aliuelekeza uso wake kuelekea mbinguni na kuurudisha chini akisema: "Mwenyezi Mungu na Mtume wakes.a.w.w. wamesema kweli." "Je, kilikuwa nini? "Kikundi cha watu kiliuliza. Imam Imam Ali ibn Abi Taliba.s alisema:"Mimi ni mpiganaji wa vita na vita vinarithishia mtu ulaghai. Vivyo hivyo, ninaweza kukubali iwapo nitaporomoka kutokea mbinguni kwa ajili ya kunaswa na ndege kuliko kumsingizia uwongo Mtume wa Allah swt. Kwa hivyo fuateni chochote kile mukisikiacho kikitoka kwangu........" Kauli juu ya uandishi wa Hadith pia zimenakiliwa kutoka Maimamu wengine.

Al-Imam al-Sadiqa.s alisema:"Andikeni na kuieneza elimu yenu miongoni mwa ndugu zenu, na iwapo mtafariki basi watoto wenu watarithi vitabu vyenu. Itafika siku ambapo patatokea machafuko na hapatakuwapo na mtu wa kumfanya rafiki na wala hapatakuwa na chochote cha kuweza kutegemewa isipokuwa ni vitabu tu.... "

Al-Imam al-Sadiqa.s pia amenakiliwa kwa kusema:"Hifadheni vitabu vyenu kwani mutakuja kuvihitaji hivyo siku moja." Vile vile ameripotiwa akisema kuwa: nguvu za moyo na kuhifadhi akilini inategemea mno juu ya maandishi.

Abu Basir anaripoti kuwa aliambiwa na Imam al-Sadiqa.s : "Baadhi ya watu waliotoka Basrah walikuwa wakija na kuniuliza kuhusu Hadith na waliziandika. Je, kwa nini nawe hauziandiki?" Na aliongezea kusema,"Elewa wazi wazi kuwa wewe kamwe hautaweza kuhifadhi Hadith bila ya kuiandika."

Idadi kubwa ya mapokezi yanaonyesha kuwa Maimamua.s walikuwa navyo vitabu na maandishi ambavyo walirithi kutoka vizazi vilivyowatangulia. Katika riwaya nyingine Imam Ali ibn Abi Taliba.s ameripotiwa akiwa amesema:"Ikamateni elimu (kwa kuiandika)," ambavyo aliirejea mara mbili.

Imeripotiwa kutoka kwa Ja'bir kuwa Abu Hanifa alikuwa akimwita al-Imam al-Sadiqa.s "Kutubi" (yaani mwenye vitabu) kwa sababu ya kutumia mno vitabu, na Imama.s alifurahishwa kwa jina kama hilo. Vile vile imeripotiwa kuwa al-Imam Muhammad ibn Ali al-Baqira.s ameziandika Hadith za Mtumes.a.w.w. ambazo zilikuwa zikinakiliwa na Jaabir ibn Abdullah Ansaari. (Ingawaje taarifa hii inaonyesha kuwa siyo ya ukweli kwani Jaabir alikuwa ameshakwisha kufariki wakati Imama.s alikuwa na umri wa miaka mitano tu, labda inawezekana kuwa Hadith ziliandikwa na mjumbe).

UANDISHI WA HADITH

2. MASHIA NA UANDISHI WA HADITH

Kwa kuwa riwaya (desturi) ya uandishi wa Hadith ilikuwapo miongoni mwa Shia tangia mwanzoni, wao walikuwa wanaongoza katika uandishi wa Hadith na Fiqh. Dr. Shawqi Dayf anaandika: "Mwelekeo na umuhimu wa Mashia katika uandishi wa Fiqh umekuja daima ni madhubuti mno. Sababu nyuma yake ilikuwa ni imani yao katika Maimamu wao ambao walikuwa ni kiongozi wao (haad) na wakiwa wameo ngozwa na Allah swt (mahdi) na fatawa zao zimekuwa zimeshikamana. Kwa hivyo, wao walipatiwa uzito na umuhimu katika misemo ya Imam Ali ibn Abi Taliba.s Na kwa sababu hiyo, mkusanyiko wa kwanza ulifanywa na Mashia, ulifanywa na Sulaym ibn Qays al-Hilali, katika zama za al-Hajjaj." Al-Allamah al-Sayyid Sharaf al-Din anaandika: "Imam Imam Ali ibn Abi Taliba.s na wafuasi wake walitilia mkazo na kufuatilia swala la uandishi kuanzia mwanzo kabisa. Jambo la kwanza kabisa lililotiliwa mkazo na kufuatiwa na Imam Ali ibn Abi Taliba.s ilikuwa ni kuiandika Quran nzima, ambayo aliifanya baada ya kifo cha Mtumes.a.w.w. kwa kuiandika kimpangilio wa ufunulio wa Aya za Qurani.Katika Qurani hiyo pia alikuwa ameonyesha ni aya zipi zilizokuwa 'amm au khass, mutlaq au muqayyad, muhkam au mutashabih. Baada ya kukamilisha hayo, aliendelea na kazi ya ukusanyaji wa kitabu kwa ajili ya Fatimah, ambacho kilikuwa kikijulikana kwa vizazi vyao kama Sahifat Fatimah. Baada ya hayo, aliandika kitabu juu ya diyat (fidia) ambacho kilijulikana kama Sahifah. Ibn Sa'id amenakili hivyo katika musnad kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Taliba.s mwishoni mwa kazi yake mashuhuri al-Jami.' Mtunzi mwingine wa Kishia ni Abu Rafi, ambaye alikusanya maandiko yakiitwa kitab al-Sunan wa al-ahkam wa al-qadhaya. "

Marehemu Sayyid Hassan al-Sadr anaandika kuwa Abu Rafi, aliyekuwa mawla wa Mtumes.a.w.w. ndiye aliyekuwa wa kwanza miongoni mwa Mashia kwa kukikusanya kitabu. al-Najashi katika Fihrist ameelezea kuwa Abu Rafi alikuwa ni mtunzi katika kizazi cha kwanza cha Mashia. Mfuasi wa Imam Ali ibn Abi Taliba.s Abu Rafi alishiriki katika vita vya Imam Ali ibn Abi Taliba.s na alikuwa ni mwangalizi wa hazina ya Serikali huko Kufah. Kitabu chake kilichokuwa kikiitwa Kitab al-Sunan wa al-ahkam wa al-qadhaya, ambacho kilikuwa kimeanza kwa sura izungumziayo Salat, kufuatiwa na sura juu ya Saumu, Hajj, Zakat, kutolewa kutoka kwa Imam Ali ibn Abi Taliba.s katika Kufah, Kitabu hiki kilinakiliwa na Zayb ibn Muhammad ibn Ja'afer ibn al-Mubarak katika nyakati za al-Najashi. Ali ibn Abi Rafi, mwana wa Abu Rafi, aliye tabi't na Mshia khalisi ameweza vile vile kukusanya kitabu kilichokuwa na sura mbali mbali juu ya mambo ya Sheria kama vile wudhuu, Salaat, n.k.

Kama ilivyoelezwa hapo awali, abu Hanifa alimwita al-Imam al-Sadiqa.s kutubi (akisema 'innahu kutubi') sifa ambayo ilimtambulisha na wengineo. Wakati Imama.s aliposikia kuhusu hayo, alicheka na kusema, "...... lakini kila alichokisema kuwa kwangu suhufi ni kweli; mimi nimesoma suhuf (vitabu) vya mababu zangu." Riwaya hii inaonyesha kwa wazi wazi kuwa Imam a.s. alikuwanavyo vitabu fulani ambavyo alipewa na mababu zake, na hiki kilikuwa ni kipindi ambacho Ahl al-Sunnah walikuwa hawakutilia mkazo katika uandishi wa Hadith. Miongoni mwa mapokezi ambayo inatuonyesha kuwa ma-Imam a.s. walikuwa navyo vitabu kama hivyo, ni mojawapo iliyoripotiwa na Muhammad ibn 'Udhafir al-Sayrafi anasema: "Mimi nilikuwa pamoja na al-Hakam ibn Utaybah na tulimtembelea al-Imam al-Baquira.s Al-Hakam alimwuliza swali Imama.s Abu Ja'afera.s alikuwa akimstahi sana. Wao walitofautiana juu ya swala fulani na hapo Abu Ja'afer alisema: "Mwanangu (mtoto wake), inuka na ukilete kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s Huyo mtoto alimletea kitabu kikubwa, ambacho Imama.s alikifungua, na kulipitishia macho hadi kulipata swala walilokuwa wakilizungumzia. Na hapo Abu Ja'afera.s alisema:"Haya ni maandish i ya Imam Ali ibn Abi Talib a.s na yaliyosemwa na Mtume s.a.w.w..........."

Katika riwaya nyingineyo ameripotiwa Imam al-Baquira.s akisema: "Katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s nimepaona ambapo Mtumes.a.w.w . akisema:'Wakati zakat itakapokuwa hailipwi, basi baraka itapotea kutoka ardhi." Vile vile ipo imeripotiwa kuwa Imam al-Sadiq a.s amesema: Baba yangu alisema: "Mimi nimesoma katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s kuwa Mtumes.a.w.w . ameandika mkataba baina ya Muhajirun na Ansar na watu wengineo wa Yathrib ambao waliungana naye, ikisemwa humo hivi:"Jirani ni sawa na mtu mwenyewe; asitendewe visivyo haki au kutendewa madhambi. Utukufu wa jirani wa mtu ni sawa na ule utukufu wa mama yake." Katika riwaya nyingine al-Imam al-Sadiq a.s amesema: Imeelezwa katika kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s "Mfano wa dunia ni sawa na mfano wa nyoka: ngozi yake nyororo mno, lakini ndani yake ni sumu kali mno. Mtu aliye mwenye busara hujiweka naye mbali, lakini jahili anafanya kila aina ya jitihada ya kutaka kuikaribia."

Kwa mujibu wa riwaya nyingineyo, habari ifuatayo imetoka katika kitab adab Amir al-Muminiin: Mtu yeyote asijaribu kurejea katika mithali katika masuala ya Din, kwani amri ya Allah swt haiwezi kutambuliwa kwa mithali. Watatokezea watu ambao watakuwa wakirejea katika mithali, na hao watakuwa na uadui pamoja na Din. Zurarah anaripoti: Nilimwuliza al-Imam al-Baquir a.s. kuhusu hisa ya babu katika urithi. Imama.s. alijibu:"Sijawahi kumwona mtu yeyote yule akilisemea swali hili bila ya kuongezea mawazo yake ya kibinafsi, isipokuwa Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s.." Mimi nilimwuliza: "Na jee alisema nini?" Imama.s alinijibu:"Njoo kesho, mimi nitakusomea kutoka kitabuni." Mimi nilisema, "Mimi niwe fidia juu yako, naomba uiseme katika mtungo wa Hadith kwani Hadith zako ni afadhali kwangu kuliko kukisoma kitabu." Imama.s alisema:"Tafadhali usikilize kile nilichokuambia. Njoo kesho na mimi nitakusomea kutoka kitabu hicho." Siku ya pili mimi nilimwendea Imama.s wakati wa adhuhuri. Jaafer ibn Muhammad mwanae Imama.s alinikaribia na Imama.s alimwambia kunisomea kitabu hicho........

Katika riwaya nyingine, Imam al-Sadiqa.s anasema: "Ipo imeelezwa katika Kitabu cha Imam Ali ibn Abi Taliba.s kuwa mtu anywaye pombe na mwenye kumsaidia aliyelewa (muskir) basi wote wanastahili kuadhibiwa, ambavyo ni sawa katika sura zote mbili." Muhammad ibn Muslim, Sahaba wa Imam al-Baquira.s asema: "Abu Jaafer alinisomea kitabu kitab al-faraidh, ambacho yalikuwemo yaliyosemwa na mtumes.a.w.w. na kuandikwa na Imam Ali ibn Abi Taliba.s : "Habari zote zilizotajwa hapo juu, ambazo ni chache sana kutokea riwaya nyingi mno kama hizo, zinatudalilisha kuwa desturi ya Mashia ya kuandika Hadith imetangulia mawaidha ya ma-Imama.s kwa sahaba wao kuhusu uandishi wa Hadith. Ilikuwa ni desturi ambayo ilianzia katika zama za Mtume Mtukufus.a.w.w . na ilikuwa imeanzishwa na Imam Ali ibn Abi Taliba.s . Zipo Hadith, nyingi katika desturi ya Mashia ambazo zimetimiza kanuni za tawatur, na vile vile yapo marejeo katika Sunni ambazo zinathibitisha na kushuhudia Hadith kama hizo.

Mambo yote hayo yanakuelekeza katika uimara na uhakikisho wa usahihi wa Hadith zilizonakiliwa na Mashia. Hii ni kwa sababu pamoja na kuendelea na maongozo ya Maimamua.s hadi kufikia katikati ya karne 3 A.H./9 A.D., Hadith za Mashia zilitoa watunzi wengi mno na ambao maandishi yao kuanzia kipindi cha al-Imam al-Sadiqa.s yamekuwa kwa hakika ni katika idadi kubwa sana. Iwapo mtu ataweza kutupia macho Rijal al-Najashi, basi huyo ataweza kuona kuwa wafuasi wa Imam a.s. wametupatia kazi kubwa ambazo zimetumika kama misingi ya Fiqh katika Ushia.

Ukweli ni kwamba, Mashia idadi yao ndogo kwa upande mmoja na maisha ya hatari waliyokuwa wakiishi kwa upande wa pili ambayo iliwazuia watu waovu na wenye kuvizia majukumu kuingia katika Ushia pamoja na umuhimu uliosisitizwa na Maimamua.s na wafuasi wao katika uandishi, ndivyo vilivyoleta matokeo ya utajiri na usahihi wa Fiqh ya Kishia. Haya ndiyo faida ambazo hazikupatikana kwa Ahl al-Sunnah kwani, kwanza, wingi wa idadi yao, pili, kwa kuwa madhehebu ya Sunni ndiyo iliyokuwa Dini ya utawala wa Dola, na tatu, kwa sababu ya ukosefu wa Hadith zilizoandikwa kwa Waislam kwa ujumla kuyafuatilia yale yanayotokana na ukweli wa misingi ya kihistoria.

UANDISHI WA HADITH

3. HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI

Kazi zote zilizopo hadi leo zinazohusu Hadith zilikuwa zimekusanywa katika kipindi cha karne 2 A.H./8 A.D. au katika karne ya 3 A.H./9 A.D. Historia inatuonyesha kuwa katika kukaribia karne ya 2 A.H. kulitokezea idadi ndogo ya Muhaddithun ambao walianza kuziandika Hadith, ingawaje hazikuwa na mpangilio. Baadaye mkusanyiko huu mdogo ulikuwa kiini cha kazi zote kubwa. Hata hivyo wingi wa Hadith zilizopo sasa kwa kukusanywa, zilienezwa kwa desturi ya kutamkwa (kusemwa), na wakati zilipokuja kuandikwa vitabuni, zilikuwa hazikuwahi kuandikwa popote kabla yake. Ucheleweshwaji katika kuandikwa kwa Hadith ni swala mojawapo muhimu katika historia ya Hadith. Umuhimu wake ni wa ukweli kwamba kucheleweshwa huu kuliathiri hasa kuhusu utunzi na idadi ya Hadith pamoja na uwepesi wao wa kuzushwa (zikaongezwa na kupunguzwa na hatimaye zikawa ni zile zilizo na uongo) na matatizo mengi mengineyo yanayohusiana.

Jambo la umuhimu huu katika swala hili linawahusu wale ambao ndio waliokuwa wamesababisha ucheleweshwaji huo wa kuandikwa kwa Hadith. Mwelekeo wao ulikuja kama ni mfano kwa ajili ya wengine katika kutoziandika Hadith. Katika sehemu yetu hii, tutaweza kuchambua makusudio yao na athari za mwenendo wao wa aina hiyo juu ya Hadith. Kila kinachoweza kukusanywa kwa shida katika Historia ni kwamba baadhi ya Makhalifa walizuia uandikaji wa Hadith kwa sababu fulani fulani. Baada yao kikundi cha Sahaba na Tabiun waliwafuata katika swala hili. Kwa mujibu wa msemo "Watu hufuata dini ya wafalme wao," wao walijiepusha na uandikaji wa Hadith kwa kukubali na kuridhia kwa kuharamishwa hivyo.

Wao walizihifadhi Hadith za Mtumes.a.w.w . kwa kuzikariri tu (kwa kuzihifadhi akilini mwao tu). Kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, wao nyakati zinginezo walijaribu kurejea katika kuziandika, ili kuyateketeza maandishi yao katika kipindi cha mwisho wa maisha yao, kama kwamba maandishi hayo yaliwasaidia wao tu katika kuhifadhi kwao. Kumbukumbu hizo za Hadith zilizokuwa zimeandikwa hazikutumiwa kwa kutaka kuzihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ni jambo la kuvutia sana kuona kuwa kupigwa marufuku wa uandikaji wa Hadith katika Sunni ulitolewa na watawala wao; na vile vile ile amri ya kuziandika Hadith pia zilitolewa na watawala wao.

Al-Zuhri anasema: "Sisi tulikuwa tukichukia mno uandishi wa elimu, hadi hapo wakuu wetu walipotulazimisha kuyaandika hayo. Hapo baadaye tulikuja kugundua kuwa hapakuwapo na yeyote miongoni mwa Waislam waliopinga. "Al-Zuhri anaendelea kusema: "Wafalme waliniambia kuandika elimu ('ilm, i.e. Hadith) kwa ajili yao. Baada ya kuwaandikia kwa muda fulani, mimi nilishikwa na aibu mbele ya Allah swt; (mimi nilijiuliza): Je, kwa nini nimejitayarisha kwa ajili ya kuwaandikia wafalme na wala si kwa ajili ya watu wengineo!?" Ni dhahiri, kama vile itakavyokuja kuonekana kwamba Hadith hazikuwa ni kweli kwa ajili ya Sahaba na Tabiun wote. Wengi wao na akiwemo Ali ibn Abi Taliba.s waliziandika Hadith na vile vile waliwaambia wengine kufanya hivyo. Wengine walianza kuziandika Hadith wakati sheria zilizowekwa na Makhalifa juu ya kutoziandika Hadith zilipobadilishwa na amri ya Kikhalifa kutoka kuziandika Hadith.

'Umar ibn Abd al-Aziz (101 A.H./719 A.D.) ndiye aliyekuwa Khalifa wa kwanza kuamrisha wanazuoni wa miji mbalimbali kuziandika Hadith na kumpelekea huyo Khalifa maandishi yote. Imeripotiwa kuwa Khalifa alimwandikia Muraah ibn Kathir akimwomba amwandikie Hadith za Mtumes.a.w.w Vile vile yeye alimwandikia Abu Bakr ibn Muhammad Hazm:"Andika Hadith yoyote ile ya mtume s.a.w.w uliyonayo na kunitumia na chochote kile kilichonakiliwa kutoka kwa Umar, kwa sababu ninayo hofu kuwa utafika wakati ambapo Hadith zitakuwa zimetoweka." Yeye pia aliwaandikia watu wa Madinah akiwataka wamwandikie chochote kile kilichobakia cha Hadith za Mtumes.a.w.w .

Ripoti hizi zinaonyesha wazi wazi kuwa uandikaji wa Hadith haukuwa jambo lenye umuhimu hadi wakati huo, hata hivyo, haimaanishi kuwa hapakuwepo na Hadith zilizokuwa zimeandikwa hadi wakati huo. Pamoja na kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz kazi hii haikufuatiliwa na Makhalifa waliofuata, na kwa mara nyingine tena uandikaji wa Hadith uliangukia katika kusahauliwa. Kukariri (kuhifadhi katika akili) ndiyo iliyokuwa njia iliyobakia. Hadith za kusemwa mdomoni tu (bila ya maandiko) ndiyo iliyokuwa njia ya uenezaji wakati ambao Sunni walirithi kutoka vizazi vyao vilivyowatangulia, ilisababisha upinzani mkubwa mno katika kuziandika Hadith. Sisi twaweza kuelewa vyema hali hii wakati tutakapokuja kujua kuwa baadhi ya Muhaddithun walichukizwa mno na uandishi wa Hadith hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. Kauli za wanahistoria kuhusiana na ukusanyaji wa Hadith hapo mwanzoni zinaelezea hayo hayo.

Abd al- Razzaq anaelezea kuwa mtu wa kwanza kuzikusanya Hadith alikuwa Abd al-Malik ibn Jurayj, aliyejulikana kama Ibn Jurayj (150 A.H./767 A.D.) Vile vile Abd al-Rahman Al-Awzai (88-157 A.H./707-773 A.D.) alikuwa ni miongoni mwa wale walioanza kuzikusanya Hadith. Al-Dhahabi anaandika kuwa, katika kipindi hiki ndipo Wanazuoni wa Kiislamu walianza kuandika Hadith, Fiqh na tafsiri katika mwaka 143 A.H./760 A.D. Wafuatao ndio waliokuwa wakiongoza katika kazi hizo nao ni Ibn Jurayj katika mji wa Makkah, Malik (179 A.H./795 A.D.) huko Madinah, al-Anzai katika Syria, Said ibn Abi Urwah (156 A.H./783 A.D.) huko Basrah, Muammar huko Yemen, Sufyan al-Thawri (156 A.H./783 A.D.) huko Kufah. Kabla ya kipindi hicho, hata hivyo, Muhaddithun waliongoza wakiripoti Hadith kutokea kukariri au kutokea kwa waliotegemewa lakini zilikuwa ni mikusanyo isiyokuwa na mipangilio.

Mahali pengine yeye ni mbainifu zaidi wakati asemapo: "Ibn Jurayj na Ibn Abi Urwah walikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith na Muammar ibn Rashid alikuwa ni wa kwanza miongoni mwao huko Yemen." Ipo habari iliyoripotiwa na Abd al-Aziz ibn Muhammad al-Darwardi kuwa mtu wa kwanza kukusanya elimu alikuwa Ibn Shihab al-Zuhri. Ibn Shihab al-Zuhr (124 A.H./742 A.D.) mwenyewe anaripotiwa akiwa amesema: "Umar ibn Abd al-Aziz alituamrisha kuzikusanya Hadith za Mtumes.a.w.w Kufuatiwa hayo sisi tuliandika katika sura ya kitabu, na kupeleka nakala ya kitabu hicho katika sehemu zote za utawala wake." Ni dhahiri, ingawaje Hadith zilikuwa zikikusanywa kwa kiasi fulani katika siku hizo, kazi ya ukusanyaji ilianza kuzorota kwa sababu ya upingamizi uliofuatia kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz, na vile anavyosema al-Dhahabi, kazi hiyo ya ukusanyaji wa Hadith uliahirishwa au kuachwa kwa kipindi cha nusu karne.

Ibn Hajar anasema: "Kazi ya ukusanyaji na upangaji (tabwib) wa Hadith ulianza katika miaka ya mwishoni mwa kipindi cha tabi'un, yaani ni kwamba; wakati ambapo Wanazuoni wa Kiislam walipokuwa wameenea katika miji. Wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith walikuwa ni Rabi ibn Subayh na Sa'id ibn Abi Urwah......hadi wakuu miongoni mwa Wanazuoni wa tabaka la tatu walipokusanya ahkam.

Al-Dhahabi pia anaelezea kitu kama hicho. Kutokana na taarifa hizo inaweza kudadisiwa kuwa ukusanyaji wa Hadith uliotokezea katika sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni mkusanyiko usio kamilifu mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. na sehemu ya pili ni ukusanyaji uangalifu katika sehemu yake ya pili. Hajji Khalifah anakubaliana na haya pale asemapo: "Wakati Islam ilipoenea katika sehemu mbalimbali, na miji ya Islam ilipopanuka, tabi'un walisambaa mote humo. Baada ya muda, mkuu wao alipofariki dunia na hivyo ndivyo ilivyokuwa imekuja kuathiri ukusanyaji wa Hadith.

Wanazuoni walianza kuhisi haja ya kuziandika Hadith na kuzihifadhi kwa njia ya kuziandika. Katika maisha yangu, lilikuwa ni jambo la maana la kuziandika Hadith, kwa sababu kukariri tu kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuja kupoteza fahamu au kuzipotoa. Baada yao, kulitokezea kipindi cha wataalamu wa Hadith kama Ibn Jurayj na Malik ibn Anas. Inasemekana kuwa mtu wa kwanza katika kukusanya Hadith alikuwa Rabi ibn Subay wa Basrah. Baada yahuyo, zoezi kama hili lilikuwa ni la kawaida.

Kutokana na taarifa hizo, tunaweza kumalizia kuwa, kotekote, kulikuwapo na vipindi vitatu katika mpitilio wa Hadith za kutamkwa. Kipindi cha kwanza kilichukua/kilidumu mwanzoni hadi mwishoni mwa karne ya 1 A.H. /7 A.D. katika kipindi hiki uandishi wa Hadith haukuwapo wala haukujaribiwa isipokuwa tu katika hali chache ambapo Sahaba walijaribu kuziandika kwa kwenda kinyume na amri ya Makhalifa. Katika kipindi cha pili, kuanzia mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. hadi kwa kufikia katikati, kulitokezea uandishi na ukusanyaji wa Hadith katika hali isiyokuwa kamilifu na pia mambo yaliyoandikwa yaliweza kukusanywa. Katika kipindi cha tatu, kilichoanzia katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., uangalifu mkubwa ulielekezwa katika ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ikiwa ni shughuli muhimu kimsingi. Vitabu vichache mno vilivyoandikwa katika kipindi hiki vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana- kama vile musannaf Ibn Abi Shaybah, musannaf ya Abd al-Razzaq na Muwatta ya Malik ibn Anas yalikuwa yameanzishwa katika sehemu ya pili ya karne ya 2 A.H./8 A.D. Kwa mujibu wa ripoti ya al-Dhahab, musnad ya kwanza ilikusanywa na Nu'aym ibn Hammad. Yahya al-Hamani huko Kufah na al-Musd huko Basrah nao ndio waliokuwa wa kwanza miongoni mwa Wanazuoni wa miji hii katika kukusanya musnad.

1

TADWIN AL HADITH

UANDISHI WA HADITH

4. SABABU ZA KUCHELEWA KUANDIKA HADITH

Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtumes.a.w.w , kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi kuhusu uandishi wa Qurani. Kimatokeo Qurani ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif). Hata hivyo, katika hali ya Hadith kwa mujibu wa imani yetu mbali na ruhusa au amri ya Mtumes.a.w.w kwa kuhusiana na uandishi wa Hadith na mbali na ukweli kwamba Hadith zilikuwa zimeandikwa katika zama za uhai wa Mtumes.a.w.w , sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu kwa kazi, pia iliweza hata kupingwa. Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni.

Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na 'udhubillah' Mtumes.a.w.w.

Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtumes.a.w.w , basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtumes.a.w.w hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao. Kwa hivyo, walimwelekezea Mtumes.a.w.w kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.

5. RIWAYA YA ABU SA'ID

Riwaya ifuatayo imenakiliwa kwa mamlaka ya Abu Sa'id al-Khudhri: "Musiandike chochote kile kutoka kwangu isipokuwa Qurani tu, na yeyote yule aliyekwisha andika chochote kile basi ni lazima ayateketeze yote." Taarifa hiyo ni wazi na yenye maana isiyofahamika. Maana inayotakiwa kuelezwa ni kwamba hakuruhusiwi kuandikwa kwa Hadith. Kwa mujibu wake, mtu yeyote aliyekuwa ameandika chochote kile basi lazima akiteketeze. Ni sawa kabisa kwa sababu ya uwazi wa ubainishi wake, vile vile pamoja na sababu zinginezo, ndiyo maana sisi hatuwezi kuikubali uhakiki wa taarifa hiyo au nyinginezo kama hizo. Sababu zetu za kutokubaliana na Hadith hiyo ya juu ni kama zifuatazo:

1.Kwanza : iwapo sisi tutaikubalia Hadith hii basi hatuwezi kuifungia kipindi cha muda. Iwapo uandishi wa Hadith ulikatazwa na haram, basi ni haram katika kila zama. Hata hivyo, sisi twaona wanaoinakili Hadith hii, wao wenyewe hawakuifuatilia na wao hatimaye waliziandika na kuzikusanya Ahadith. Uandishi huu, kama ilivyoonekana hapo juu, ulianza katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., na kukosekana kwa utiifu wa Hadith inatuonyesha kuwa hao wanainakili Hadith walikuwa hawakuichukulia kama sahihi na kweli; kwani hao walijua kuwa chochote kile kilichoharamishwa na Shariah haiwezi kubadilishwa kikawa halali. Jambo la kuvutia humu ni kwamba wao wameirekodi hata Hadith hii, ambavyo wao hawakuifuatilia, kwa kalamu zao zilizobarikiwa! Je, itawezekanaje sisi kuiamini kuwa ni sahihi na kweli?

2.Pili : waandishi hawa hawa pia wamezinakili Hadith zinginezo zinazozungumzia kuruhusiwa kuandikwa kwa Hadith, na iwapo sisi tutazichukulia Hadith zote mbili kuwa ni sawa katika maelezo na maelekezo, basi itatulazimu kuziachia mbali Hadith zote mbili hizo kwa sababu ya kupingana kwao kwenyewe. Kwa hivyo, katika hali kama hii Hadith hizi zote mbili zinapoteza ustahi wa kuaminika; navyo hata sisi, kwa kudhania tu, hatuwezi kamwe hata kutumia njia zinginezo kusadikisha Hadith ambayo ipo inakataza uandishi wa Hadith za Mtumes.a.w.w .

3.Tatu : Abu sa'id al-Khudhri, ambaye anatajwa hapo juu kwa wingi katika kuinakili taarifa hiyo, pia anatoa taarifa nyingine inayopingana na ile ya kwanza, yeye anasema:

"Katika siku hizo, sisi tulikuwa hatuandiki chochote kile isipokuwa Qurani na tashahud."

Nukta mbili zinaweza kufahamika kwa kujua sababu zake kutokana na taarifa za Abu Sa'id.

Kwanza : Abu Sa'id haelezi kuwa kutoandika kwao Hadith kulitokana na amri ya Mtumes.a.w.w kwani kama ingalikuwapo, basi angalionyesha hayo, hadi hapo isemwe kuwa maelezo kama hayo hayakuazimiwa hapa. Uwezekano huu wa pili uliotolewa, ingawaje unaweza kuchukuliwa kwetu sisi, inaonekana ya mbali mno. Na nukta ya pili ni kuongezwa kwa neno tashahhud katika taarifa hii, kitu ambacho hakipatanishi pamoja na kusudi la uharamisho wa kuandika isipokuwa Quran tu. Ni jambo la kutilia maanani kwamba Hadith nyingine kutoka kwa Ibn Mas'ud, neno istikharah limeongezwa pamoja na tashahhud.

Kwa kuhusiana na Hadith hii, inawezekana kukaulizwa, je, ni kwa nini Mtumes.a.w.w aruhusu uandishi wa tashahhud pekee yake, ambapo inatambuliwa kuwa kutapotea vile wakati uendeleavyo, hayo pia yaliweza kutokea pamoja na Hadith zinginezo, baadhi yao ambazo zilikuwa na maongozo muhimu kabisa ya Shariah za Dini. Na katika upande wa pili, iwapo kulikuwapo na madhara yoyote katika kuziandika Hadith, basi madhara hayo pia yaliweza kutokezea katika kuandika tashahhud au chochote kile. Kwa hivyo, haikubaliki kimantiki kudai kuwa Mtumes.a.w.w ndiye aliyeharamisha kuandikwa kwa Hadith.

4.Nne : kile kinachoweza kukusanywa kutokana na historia- ambacho sisi tutalisemea kwa zaidi hapo mbeleni - Abu Bakr, na hata Khalifa wa pili, walipendekeza kuandikwa kwa Hadith mwanzoni mwa Ukhalifa wao. Hata hivyo, hapo baadaye wao waliharamisha kwa kutolewa kwa sababu zao. Hao Makhalifa kamwe hawakusema kuwa kazi kama hiyo ilikuwa imeharamishwa na Mtumes.a.w.w . Zaidi ya hayo wao waliposhauriana na Sahaba wengineo kuhusu kuandika Hadith, nao pia walipendezewa na shauri hilo. Hii pia linatuthibitishia kuwa hapa kutolewa amri na Mtumes.a.w.w . ya kuharamisha kuandika kwa Hadith.

5. Katika mojawapo ya Hadith Abu Basir anaripotiwa akiwa amemwambia Abu Sa'id al-Khudhri: "Sisi twaandika chochote kile tukisomacho." Abu Sa'id alimwambia: "Je, wataka kuyakusanya ili ukitengeneze Kitabu? Mtumes.a.w.w . ametuelezea Hadith nasi pia twakuambia wewe, nawe pia kama sisi ni lazima uzikariri tu kwa mdomo bila ya kuandika." Nukta mbili hapa zinastahili kuchunguzwa.

Kwanza, Abu Sa'id hasemi kuwa Mtumes.a.w.w . ndiye aliyeharamisha uandikwaji wa Hadith. Pili, sababu aitoayo kwa kutoziandika Hadith ni sawa na zile zilizoripotiwa kutokea kwa Khalifa wa pili, ambaye naye pia hamsemi Mtumes.a.w.w . kuwa ndiye aliyeharamisha uandishi wa Hadith. Katika hali yoyote ile, ni jambo la kuyakinisha kuwa Mtumes.a.w.w . kamwe hakuharamisha uandishi wa Hadith.

6.Sita , kuna taarifa katika Hadith, moja kwa moja baada ya kutajwa hiyo ya juu, na kuwapo kwake pia kunatudalilishia kule kutothaminiwa kwake: "Simulieni (chochote kile utakacho) kutokea Waisraili. Hakuna madhara ndani yake." Kuanzia mwanzoni kabisa, kwa upande mmoja Mtumes.a.w.w anafahamika kwa kuchukizwa mno katika kusikia hadithi za Mayahudi (hujulikana kama Israiliyyat) -na kwa upande wa pili, Wanazuoni wa Kiislam wamekwisha zitambua madhara ya mawazo yanayoenezwa nayo, inaweza kusemwa kuwa Hadith hiyo nzima ni kazi ya uzushi mtupu. Hadith hii inawataka Waislam kwa upande mmoja, waziandike Hadith za Mtumes.a.w.w, na hatimaye kwamba zitaweza kusahauliwa pole pole; na upande wa pili, inawapatia leseni ya bure ya kuunganisha chochote kile wakitakacho kutoka kwa Mayahudi, Haya ndiyo maazimio maovu kabisa za Hadith kama hizi za kuzuliwa. Je, kunaweza mtu yeyote mwenye akili timamu akasema kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyetoa amri kama hiyo?

Ipo Hadith nyingineyo kutokea Abu Sa'id al-Khudhri ambayo inatuletea uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kutomruhusu Abu Sa'id kuandika Hadith kutokana na sababu maalum, ingawaje, katika mtazamo wetu, uwezekano wa kuruhusiwa katika swala hili pia ni kwamba Hadith hii vile vile ni uzushi. Abu Sa'id asema:"Mimi nilimwomba Mtume s.a.w.w. ruhusa ya kuandika Hadith, lakini yeye alikataa kunipa idhini." Je kwa sababu zipi ? Hadith hii inatuunga mkono katika uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kwa kumkatalia ruhusa ya kuandika Hadith katika swala la Abu Sa'id. Wakati inapozingatiwa katika nuru ya Hadith, ambazo sisi tutazinakili hapo mbeleni, ambapo Mtume s.a.w.w. yupo anaripotiwa kwa kutoa idhini kwa watu wengineo basi uwezekano huu utajipatia nguvu zaidi.

7. KUTOKUBALIKA KWA HADITH ZA ABU HURAYRAH

Kuhusiana na hayo, kuna Hadith kutoka kwa Abu Hurayrah ambayo pia imehusika. Abu Hurayrah asema: "Mtumes.a.w.w . alitufikia wakati tulipokuwa tunaziandika Hadith. "Je, mwaandika nini?" Aliuliza Mtumes.a.w.w mimi nilijibu: "Haya ni mambo ambayo sisi tumeyasikia kutoka kwako." Mtumes.a.w.w . alisema: "Je, munataka kuandika kitabu mbali na Kitabu cha Allah swt? Hakuna kilichopotosha mataifa isipokuwa tu pale wameandika kitabu mbali na Kitabu cha Allah (Quran)" Hadith hii pia haikubaliki kwa sababu zifuatazo:

1. Kwa sababu ya wengi waliokwisha kutoa sababu zao katika masomo yao na ambazo sisi pia tumeziona kuwa zinaweza kukubalika baada ya kuchunguzwa, hivyo usadikifu ('adalah) wa Abu Hurayrah hauwezi kukubaliwa. Vile vile inawezekana kuwa Hadith hii imezuliwa na wengine halafu wakaja kumtaja Abu Hurayrah kuwa ndiye aliyeiripoti.

2. Pili, mazungumzo yaliyomo ni sawa kabisa, kama vile yalivyokuwa yametolewa na Khalifa Umar wakati alipokuwa ameamua kuziandika Hadith na baadaye kughairi. Lakini Khalifa mwenyewe kamwe hakumsingizia Mtumes.a.w.w . Wakati ambapo Abu Hurayrah, au wale wote wengineo wakimsingizia Mtumes.a.w.w ., hawakutupatia mwanya wa kubishana nao kwa madai yao (kwani madai yao ni kuwa Mtumes.a.w.w . tu ndiye aliyeyasema, hivyo hakuna ubishi juu yakauli ya Mtume): Khalifa Umar kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, alifikia maamuzi hayo baada ya kuzingatia mambo fulani fulani.

3. Tatu, mazungumzo yaliyomo na yanayonekana katika Hadith hii ingawaje inaonekana kuwa inayo mizizi katika kauli ya Mtumes.a.w.w . ambayo itazungumzwa hapo mbeleni, inazungumzia juu ya Mtumes.a.w.w . kuharamisha vitabu vya Mayahudi na Wakristo, na wala si kuharamishwa Hadith za Mtumes.a.w.w. ambazo ni kitu kilicho kamili baada ya Quran.

4. Nne, je inawezekana kwa Mtumes.a.w.w. kuharamisha kuandikwa kwa Sunnah, ambayo ndiyo inayofuatia baada ya Quran? Au aliharamisha kuwa hivyo isibakie sambamba na Quran? Je, ni nafasi ipi iliyo ya Sunnah ya Mtumes.a.w.w. isiokuwa ubavuni mwa Quran? Je, ni ukweli unaoweza kupingwa kuwa Quran na Sunnah ndivyo kwa pamoja vinafanya Shariah za Kiislam? Ipo Hadith nyingine ivutiayo, ambayo inadhihirisha tabia ya udanganyifu wa Hadith kama hizo, nayo ni ile iliyonakiliwa na Abu Hurayrah. Baada ya kuelekezea kama taarifa tuliyonayo ipo, inaendelea kuongezea mambo mengi ambayo yanatudhihirishia upotofu katika upande wa Abu Hurayrah, au mzushi aliyezusha juu yake. Kwa mujibu wa Hadith hii, Mtumes.a.w.w. aliwasikia watu wameziandika Hadith zake. Papo hapo, alikwenda juu ya Mimbar na baada ya kumsifu Allah swt alisema: "Ni aina gani ya vitabu hivi ambavyo nimesikia mmeviandika? Kwa hakika mimi ni mwanadamu tu. Yeyote aliyeandika chochote kile, basi ni lazima aniletee mimi." Hadith hiyo kwa wazi wazi inakanusha Sunnah ya Mtumes.a.w.w. kwani Mtumes.a.w.w. yupo anakana uwezekano na uhalali wake wa utume kwa kusema kuwa yeye alikuwa ni mtu kama watu wengine wa kawaida. Hili ni jambo ambalo mtu yeyote hawezi kulikubali kwani ni uzushi mtupu. Jambo la kuvutia zaidi ni kuhusu kusema kwa Mtumes.a.w.w. hapa ('mimi ni mwanadamu') ipo imeelezwa katika Hadith nyingine kuwa hayo yalisemwa na kikundi cha watu wa Quraysh kuhusu Abd Allah ibn Amir ibn al-As, ambaye alikuwa ameandika Hadith za Mtumes.a.w.w. Hapo Mtumes.a.w.w. hatilii maanani maoni yao kwa hakika yupo anayakanusha. Anasema:"Mimi hakuna nilisemalo isipokuwa ni haki tupu."

5. Tano, ipo imeripotiwa kutoka Abu Hurayrah mwenyewe kuwa hakuna mtu yoyote yule anayemzidi katika kunakili Hadith, isipokuwa Abdallah ibn Amribn al-As, kwa sababu huyu alikuwa akiziandika wakati ambapo Abu Hurayrah hakuwa akifanya hivyo. Taarifa hii inaonyesha kutokuwapo kwa uharamisho Abdallah aliziandika Hadith zote, ambapo zipo sababu za kibinafsi zilizomfanya Abu Hurayrah asiziandike. Hivyo, inatuonyesha wazi wazi kuwa hapakuwepo na amri yoyote yenye kuharamisha kuandikwa kwa Hadith za Mtume s.a.w.w.; wote waliotaka kuziandika waliziandika, na yeyote asiyetaka kuziandika hakuziandika lakini kwa sababu zao binafsi bila ya kuzuiwa.

6. Sita, katika ripoti nyingineyo Abu Nuhayk, mwanafunzi wa Abu Hurayrah, asema: "Mimi nilikuwa nikiviazima vitabu kutoka kwa Abu Hurayrah, nilinakili, na kumchukulia (makala zangu) Abu Hurayrah na kumsomea. Kwa kila Hadith nilikuwa nikimwuliza iwapo amewahi kumsikia Mtume Mtukufus.a.w.w. akiisema, naye alikuwa akiitikia." Hadith hii pia inaonyesha uongo wa Hadith isemayo kuharamishwa uandishi wa Hadith, ambayo amesingiziwa Abu Hurayrah.

7. Imeripotiwa na Hamman ibn Munabbih, mwanafunzi wa Abu Hurayrah kuwa alikusanya mus-haf iliyokuwa na Hadith zote zilizokuwa zimenakiliwa na mwalimu wao katika uhai wake. Hayo pia yanatuonyesha kupingana na Hadith hiyo, kwani isingewezekana kwa Abu Hurayrah kunakili Hadith inayoharamisha uandishi wa Hadith wakati ambapo wanafunzi wake wameziandika Hadith mbele yake na katika uhai wake, au tuseme labda kuwa Abu Hurayrah hakutekeleza Hadith ipigayo marufuku uandishi wa Hadith kwa kunakili Hadith na kuzifundisha.

Vile vile ipo Hadith nyingineyo iliyoripotiwa na Zayd ibn Thabit kwamba siku moja alimwendea Muawiya, ambaye alimwuliza kuhusu Hadith fulani. Hapo Muawiya alimwambia mtu fulani kuiandika. Hapo Zayd alisema: "Mtume Mtukufus.a.w.w. ametuambia tusiandike Hadith ya aina yoyote ile." Sisi twaamini kwa uhakika uliowazi kuwa Hadith zilikuwa zimeandikwa na Tab'un na Tabi'in na baadhi ya wanazuoni wa Sunni, wanathibitisha kutotegemewa kwa Hadith kama hizo. Hapo mbeleni katika kulichambua swala hili, sisi tutaona uthibitisho utakaoonyesha sababu za kweli katika kuharamisha uandishi wa Hadith za Mtume Mtukufus.a.w.w. Uhakika na uthibitisho huu unaonyesha kuwa sahihi kwa kumsingizia Mtumes.a.w.w. kwa taarifa kama hizo. Pia imeripotiwa kuwa Ibn Mas'ud alielezea katika usia wake kuwa mkusanyo (sahifa) wa Hadith zilizofanywa naye, ziteketezwe. Katika sura hii, haionyeshi wazi iwapo tendo hili lilikuwa limejibu amri ya Mtume Mtukufus.a.w.w. Labda inawezekana, alikuwa akifuata amri ya Makhalifa. Pili, kama vile tutakavyozungumza hapo mbeleni, tendo hilo linaelezea kuhusu kuteketeza riwaya na mapokezi ya Mayahudi (Israilliyyat) na wala si Hadith za Mtumes.a.w.w. Vile vile imeripotiwa kuwa Abu Musa al-Ash'ari aliziteketeza Hadith zilizokuwa zimeandikwa na mtoto wake. Tukichukulia utiifu wa Abu Musa kwa Khalifa wa Pili, labda inaweza kusemwa kuwa tendo lake hili lilikuwa bila shaka chini ya ushahidi kuonyesha kuwa Abu Musa alitenda kwa kuvutiwa na uharamisho huo wa Mtumes.a.w.w. kuhusu Hadith.

Moja ya kitu kinachoonyesha kutokuwa halisi kwa mapokezi hayo yaliyozuliwa juu ya Mtumes.a.w.w. kuharamisha uandishi wa Hadith, ni kauli aliyoitoa Umar kuhusiana nalo kwa nia yake ya kutaka kukusanywa kwa Hadith za Mtumes.a.w.w. Umar anaripotiwa akiwa amesema: "Mimi nilinuia kuziandika Sunnah za Mtumes.a.w.w. Lakini lilikuja wazo akilini mwangu kuwa watu waliopita walikuwa wameandika baadhi ya vitabu na walikuwa wakivitegemea mno, hatimaye wao waliacha kukitegemea Kitabu cha Allah swt. Kwa kiapo cha Mungu, mimi sitakubaliana na chochote kile kitakachoweza kukifunika (kuachwa) Kitabu cha Allah (Quran)."

Katika riwaya ya hapo juu, inaonyesha kuwa Khalifa wa Pili alinuia kuandika Hadith hapo awali. Katika baadhi ya tafsiri ya riwaya hii inaelezea kuwa aliwashauri Sahaba wengine kuhusu swala hili nao pia walilikubalia (kuandika Sunnah za Mtumes.a.w.w; lakini hapo baadaye yeye alilibadilisha shauri lake hilo kwa sababu zake alizozitaja, na wala si kwamba Mtumes.a.w.w. ndiye anayehusika katika kuharamisha.

Jambo lingine ambalo linaloweza kuonekana kama uthibitisho wa kukanusha uhalisi wa Hadith isemayo juu ya uharamisho wa kuandika Hadith, ni maneno aliyoyasema Mtumes.a.w.w. siku ya Alhamisi ya mwisho katika maisha yake (yaani kabla ya kufariki). Siku hiyo, walikusanyika Sahaba wote katika kitanda chake Mtumes.a.w.w. na hapo Mtumes.a.w.w. aliwaambia: "Nileteeni wino na karatasi ili niweze kuwaandikieni mambo fulani fulani ambayo hapo baadaye nyie mnapashwa kujitahadharisha msitumbukie katika makosa." Hapo baadhi ya watu wakiongozwa na Umar walipinga hayo wakisema "Kitabu cha Allah kinatosheleza kwetu sisi." Riwaya hii inatuonyesha kuwa uandishi wowote mbali na Quran haukupigwa marufuku tu, bali hata ulichukuliwa na Mtumes.a.w.w. kuwa ni lazima ili kuokoa Ummah kuangukia makosa na upotofu. Wakati Mtumes.a.w.w.

alipokuwa akiulizia vifaa vya kuandikia na kikundi cha Sahaba- kikiongozwa na Khalifa wa Pili kwa mujibu wa al-Shahristani katika al-milal wa al-nihal- walimpinga Mtumes.a.w.w ., kwani Mtumes.a.w.w. alikuwa akielewa wazi maafa yatakayotokea hapo baadaye kutokea tukio au kisa hiki. Hapo mbeleni sisi tutachambua kwa undani zaidi yaliyokusanywa na kusemwa na wanazuoni wa Sunni kuhusu athari mbaya zilizotokana na kutoandikwa kwa Hadith lakini ni lazima tujiulize "Je, ni sahihi kwa kumdhania Mtumes.a.w.w. katika kuharamisha kuziandika Hadith zake, jambo ambalo limeleta maovu makubwa katika utamaduni wa Kiislamu na kusababisha Sunnah za Mtumes.a.w.w. kuchezewa na Hadith hizo za kuzuliwa? Je, ni kweli kuwa Mtumes.a.w.w. ndiye anayehusika moja kwa moja katika upotofu huu na madhara yote yaliyotokea?"

8. HADITH ZA MTUME S.A.W.W. KATIKA KURUHUSU UANDISHI WA HADITH

Hadith zimepokelewa kutoka Mtumes.a.w.w. ambamo yeye ameruhusu uandishi wa Hadith kijumla au kuruhusu kikundi fulani. Hadith hizi, zenyewe, zinatosheleza kukanusha Hadith zilizotangulia zinazozungumzia kuhusu kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith, au tuseme haikosi, kuleta vurugu la riwayaat (wingi wa riwaya) katika hali yoyote, zinashindwa kubakia na uhai wao (hujjiyyah);kwani idadi ya Hadith hizi ni kubwa mno, na kwa kutilia maanani ya makanusho yaliyonayo dhidi ya Hadith zinazozua juu ya kutoandika Hadith, basi uhalisi wa Hadith kama hizi ni zenye kusadikiwa kabisa. Hadith hizi si kwamba zinazoruhusu kuandika Hadith bali pia zinatuamrisha kuziandika Hadith za Mtumes.a.w.w.

Hadith ifuatayo imenakiliwa kupitia mfululizo wa upokezi kuwa kulikuwapo na mtu aliyemlalamikia Mtumes.a.w.w. juu ya udhaifu wake wa kuhifadhi mambo katika akili yake. Mtumes.a.w.w. alimwambia: "Chukua msaada wa mkono wa kulia (i.e. kuandika) dhidi ya udhaifu wa hifadhi ya akili yako." Mtumes.a.w.w. yupo anaripotiwa akisema: "Ikamateni (hifadheni, iandikeni) elimu kwa njia ya kuandika."

Imeripotiwa kutoka Rafi' ibn Khadij kuwa yeye alisema: "Sisi tulimwuliza Mtumes.a.w.w. ,'Je tunaweza kuandika baadhi ya mambo ambayo twayasikia kwako?' Mtumes.a.w.w. alijibu, 'Andika hayo na wala hakuna madhara ndani yake.' Imeripotiwa kwa mamlaka ya Amr ibn Shu'ayb kuwa baba yake alimwuliza Mtumes.a.w.w : "Sisi tukisikia mambo kutoka kwako ambayo hatuwezi kuhifadhi akilini mwetu kwa kipindi kirefu, je, tunaruhusiwa kuyaandika?" Hapa Mtumes.a.w.w . alijibu:Naam, muyaandike"

Imeripotiwa kupitia mifululizo ya wanaonakili, kutoka Abdallah ibn Al-As kwa kusema: "Mimi nilimwuliza Mtumes.a.w.w .: 'Je, tunaweza kuandika kile tukisikiacho kutoka kwako? Mtumes.a.w.w. alijibu, 'Naam.' Mimi niliulizia. 'Bila ya kujali wewe ukiwa umeghadhabika au mpole? Mtumes.a.w.w. alijibu,"Naam mimi sizungumzi chochote kile isipokuwa haki tupu, hata kama nikiwa nimeghadhabika au nikiwa nimefurahishwa." Katika Hadith nyingine, msimulizi anaripotiwa kwa kumwuliza Mtumes.a.w.w. "Je, twaweza 'kuikamata' elimu?" Mtumes.a.w.w. alijibu:"Naam." Huyo huyo Abd Allah ibn Amr anaripotiwa kuwa,"Nilikuwa nimezoea kuandika chochote kile nilichokisikia kutoka kwa Mtumes.a.w.w . kwa ajili ya kurekodi. Baadaye Maqureyshi walinizuia kufanya hivyo, na mimi pia niliachilia kuandika. Baadaye, mimi nilimwelezea Mtumes.a.w.w. swala hilo. Naye alisema:"kwa kiapo cha Mungu ambaye anayamiliki maisha yangu, mimi kamwe sitamki chochote kile isipokuwa haki tupu."

Imeripotiwa na Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Taliba.s kuwa Mtumes.a.w.w alisema:"Andikeni elimu (ilim) kwani mutafaidi nacho humu duniani na akhera vile vile. Eleweni kuwa elimu haikubali mmiliki wake ateketee."

Hadith nyingine mashuhuri ya Ma-Imam wa Ahl al-Bayta.s ambayo imesimuliwa na chanzo cha Sunni na Shia, inaelezea maandiko (sahifah) juu ya upanga wa Mtumes.a.w.w. Al-Imam al-Sadiqa.s anaripotiwa akiwa amesema: "Kulikuwapo na Sahifah katika mpini wa upanga wa Mtumes.a.w.w. yakisomwa:"Amelaaniwa yule anayeiba mipaka ya ardhi. Amelaaniwa yule ajifanyiaye marafiki mbali na mawali wake." Au alisema:"amelaaniwa yule ambaye anakana neema za Mola wake aliyempatia."

Abu Hurayrah anaripotiwa akisema: "Hakuna yoyote yule anayeweza kuelewa zaidi yangu kuhusu Hadith za Mtumes.a.w.w. isipokuwa Abd Allah ibn Amr, kwa sababu yeye alikuwa akiyaandika kwa mkono wake, na kuhifadhi akilini mwake, ambapo mimi nilikuwa nikiyahifadhi tu bila ya kuyaandika. Naye huyo alikuwa amepatiwa idhini na Mtumes.a.w.w. kwa ajili ya kuziandika Hadith zake." Abd Allah ibn amr anaripotiwa kwa kusema: "Mimi nataka kusimulia Hadith zako na iwapo wewe utaniruhusu mimi nitaweza kuutumikisha mkono wangu (i.e. katika kuandika) ili kuusaidia moyo wangu (i.e. kuhifadhi). Na Mtumes.a.w.w. alisema, 'iwapo ni Hadith zangu, basi lazima uchukue msaada wa mkono wako.''' Yeye pia anaripotiwa kuwa na sahifah ambayo ilijulikana vyema kama al- Sahifat al-Sadiqah, ingawaje wengine wanakana kama ilikuwa na Hadith za Mtumes.a.w.w. Al-Mughirah ibn Shu'bah anaripotiwa kwa kuthibitisha kuwa Abd Allah ibn Amr alikuwa na Sahifah iliyoitwa al-Sahifah al-Sadiqaah.

Katika Hadith nyingine, Mtumes.a.w.w. anaripotiwa akisema:"Wakati mumin anapokufa, karatasi alimoandika elimu (ilim) itabakia daima na itakuwa ni pazia baina yake na moto wa Jahannam Siku ya Qiyama."

Al-Tirmidhi ameripoti kuwa Sa'id ibn Ubadah alikuwa na sahifah ambamo alikusanya idadi kubwa ya Hadith za Mtumes.a.w.w. Mtoto wake pia alikuwa anayo mazoea ya kunukuu Hadith kutoka sahifah hiyo. Kwa mujibu wa riwayah za al-Bukhari, ilikuwa ni nakili ya sahifah ya Abdallah ibn Awfi ambaye alizoea kuandika Hadith ndani mwake kwa mikono yake mwenyewe. Samurah ibn Jundab pia alikusanya Hadith nyingi katika kitabu chake kikubwa na mtoto wake, Sulayman, aliyerithi, alizoea kunakili Hadith kutokea humo. Bila shaka yalikuwa ni maandiko haya ambayo Ibn Sirin anayasemea: "Katika risalah aliyoiacha Samurah kwa mtoto wake, humo kuna kiwango kikubwa mno cha ilimu.

Imeripotiwa na Anas akisema huku amenyooshea mkono kwa mus-haf: "Hizi ni Hadith ambazo mimi nimezisikia kutoka kwa Mtume Mtukufus.a.w.w. Mimi niliziandika na nilimpatia Mtumes.a.w.w. (kwa ajili ya uthibitisho wake)." Al-Imam Jaafer al-Sadiq a.s . anasimulia kutokea Mababu zakea.s . kwamba Mtumes.a.w.w. alisema:"Wakati unapoandika Hadith, andika pamoja na sanad yake (ufululizo wa upokezi wake). Iwapo itakuwa ni kweli, basi utagawana thawabu zake; na iwapo zitatokezea kuwa ni za uongo, basi madhambi yake yatamwia aliyesema."

Mtumes.a.w.w. pia anaripotiwa kwa kusema:"Ikamateni elimu." Na alipoulizwa ni nini alichokuwa akimaanisha, alielezea kuwa yeye alikuwa akimaanisha uandishi. Umma Salma R.A. ameripotiwa akiwa amesema: "Mtumes.a.w.w. aliulizia adim ya kondoo iliyotiwa dawa ili isioze iletwe mbele yake. Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa pamoja naye. Baadaye aliyazungumza mambo mengi mno kwa Imam Ali ibn Abi Taliba.s. hadi kukaandikwa sehemu zote mbili za ngozi hiyo na vile vile kingo zake pia zilijaa maandishi."

Hadith zote hizi zinathibitisha wazi kuwa Mtumes.a.w.w. aliruhusu uandishi wa Hadith. Wapo Wanzuonini wengi ambao wanashikilia kwamba Mtumes.a.w.w. alikuwa ameharamisha hapo mwanzoni na kuruhusu hapo baadaye. Iwapo ndiyo hali ilivyo, je, ilikuwa ni kwa misingi gani ambapo baadhi ya Makhalifa waliharamisha uandishi wake na baada ya Hadith nyingi mno kuandikwa, tukamsingizia ati kuwa ni Mtumes.a.w.w. ndiye aliyeharamisha uandishi wa Hadith? Rashid Ridha amezichambua Hadith zinazoharamisha na zenye kuruhusu kuandika Hadith.Yeye anajaribu kuthibitisha kuwa Hadith zinazopiga marufuku zinashinda zile zenye kuruhusu, hivyo Hadith zinazoelezea kuharamishwa kwa kuandika Hadith ni lazima zichukuliwe kuwa ni halisi na kweli. Yeye anaandika:

"Iwapo tutachukulia kuwapo kwa mgogoro baina ya Hadith zenye kupiga marufuku na zile zenye kuruhusu, basi mtu anaweza kusema kuwa mojawapo baina yao imetengua (batilisha) nyenzio kwa kuthibitisha kuwa Hadith zinazoharamisha zinashinda zile zenye kuruhusu, kwa sababu mbili: Kwanza, Sahaba walisimulia Hadith zinazoharamisha hata baada ya Mtume s.a.w.w. Pili, Sahaba hawa kuziandika Hadith; kwani iwapo wao wangalikuwa wameziandika, basi zingalikuwa zimetufikia sisi." Sisi hatuwezi kukubaliana na maelezo hayo kwa sababu zifuatazo: Kwanza, Sahaba ndio waliosimulia Hadith zenye kuruhusu uandikaji wa Hadith pamoja na zile zinazoharamisha, na kama vile tulivyokwisha ona hapo juu, baadhi ya Sahaba waliendelea na kuziandika hizo Hadith.

Pili, sababu ya Sahaba kutojishughulisha na ukusanyaji wa Hadith kulitokana na kutolewa kwa amri ya kuharamishwa na Makhalifa wa kwanza na pili, na wala si kuwa ni Mtumes.a.w.w. aliyeharamisha. Tatu, kwa kuwa haiwezekani sisi tukadai kuwa aina moja ya Hadith hizi zinashinda aina ya pili yake, sisi twaweza kusema kuwa ugomvi wao unazifanya zote ziwe zimebatilika na wala si kwamba mojawapo inaishinda ya pili yake. Kuhusiana na kukubali kwa Abu Hurayrah kuwa Abd Allah ibn Amr alizoea kuandika Hadith, Rashid Ridha anasema: "Hakuna sababu ya kwamba sisi tuchukulie hivyo kama uthibitisho wa ruhusa ya kuandika Hadith, kwa sababu haijaelezwa katika Hadith kuwa Abdallah aliandika Hadith kwa kuruhusiwa na Mtumes.a.w.w.

Sisi tulikwishawaonyesha hapo juu riwaya zinazoonyesha kuwa Abd Allah ibn Amr kwa hakika alikuwa amepatiwa ruhusa kama hiyo. Zipo riwayat nyingi ambazo zimeshuhudia hayo, na mojawapo hapo juu Abu Hurayrah kwa kusisitiza anasema kuwa Abd Allah ibn Amr alikuwa amepatiwa ruhusa na Mtumes.a.w.w. kama hiyo. Ama kwa upande wa upinzani, wengineo, kama Abu Zuhra, wenye mawazo ya kusema kuwa Mtumes.a.w.w. aliruhusu uandishi wa Hadith kufikia mwishoni mwa Utume wake ambapo hapakuwapo na hatari ya kuzichanganya Hadith pamoja na Aya za Quran. Iwapo sisi tutachukulia kusema kuwa matendo ya baadhi ya Sahaba, hasa yale ya Makhalifa, sisi hatuwezi kuikubalia hivyo, ama kwa upande wa pili, iwapo tutakubalia, basi itatubidi kuwalaumu baadhi ya Makhalifa kwa mienendo yao. Sisi hatujui iwapo Bwana Abu Zuhrah ataupendelea uelekeo upi.


3

4