UANDISHI WA HADITH
3. HISTORIA YA UANDISHI WA HADITH KATIKA SUNNI
Kazi zote zilizopo hadi leo zinazohusu Hadith zilikuwa zimekusanywa katika kipindi cha karne 2 A.H./8 A.D. au katika karne ya 3 A.H./9 A.D. Historia inatuonyesha kuwa katika kukaribia karne ya 2 A.H. kulitokezea idadi ndogo ya Muhaddithun ambao walianza kuziandika Hadith, ingawaje hazikuwa na mpangilio. Baadaye mkusanyiko huu mdogo ulikuwa kiini cha kazi zote kubwa. Hata hivyo wingi wa Hadith zilizopo sasa kwa kukusanywa, zilienezwa kwa desturi ya kutamkwa (kusemwa), na wakati zilipokuja kuandikwa vitabuni, zilikuwa hazikuwahi kuandikwa popote kabla yake. Ucheleweshwaji katika kuandikwa kwa Hadith ni swala mojawapo muhimu katika historia ya Hadith. Umuhimu wake ni wa ukweli kwamba kucheleweshwa huu kuliathiri hasa kuhusu utunzi na idadi ya Hadith pamoja na uwepesi wao wa kuzushwa (zikaongezwa na kupunguzwa na hatimaye zikawa ni zile zilizo na uongo) na matatizo mengi mengineyo yanayohusiana.
Jambo la umuhimu huu katika swala hili linawahusu wale ambao ndio waliokuwa wamesababisha ucheleweshwaji huo wa kuandikwa kwa Hadith. Mwelekeo wao ulikuja kama ni mfano kwa ajili ya wengine katika kutoziandika Hadith. Katika sehemu yetu hii, tutaweza kuchambua makusudio yao na athari za mwenendo wao wa aina hiyo juu ya Hadith. Kila kinachoweza kukusanywa kwa shida katika Historia ni kwamba baadhi ya Makhalifa walizuia uandikaji wa Hadith kwa sababu fulani fulani. Baada yao kikundi cha Sahaba na Tabiun waliwafuata katika swala hili. Kwa mujibu wa msemo "Watu hufuata dini ya wafalme wao," wao walijiepusha na uandikaji wa Hadith kwa kukubali na kuridhia kwa kuharamishwa hivyo.
Wao walizihifadhi Hadith za Mtumes.a.w.w
. kwa kuzikariri tu (kwa kuzihifadhi akilini mwao tu). Kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, wao nyakati zinginezo walijaribu kurejea katika kuziandika, ili kuyateketeza maandishi yao katika kipindi cha mwisho wa maisha yao, kama kwamba maandishi hayo yaliwasaidia wao tu katika kuhifadhi kwao. Kumbukumbu hizo za Hadith zilizokuwa zimeandikwa hazikutumiwa kwa kutaka kuzihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ni jambo la kuvutia sana kuona kuwa kupigwa marufuku wa uandikaji wa Hadith katika Sunni ulitolewa na watawala wao; na vile vile ile amri ya kuziandika Hadith pia zilitolewa na watawala wao.
Al-Zuhri anasema: "Sisi tulikuwa tukichukia mno uandishi wa elimu, hadi hapo wakuu wetu walipotulazimisha kuyaandika hayo. Hapo baadaye tulikuja kugundua kuwa hapakuwapo na yeyote miongoni mwa Waislam waliopinga. "Al-Zuhri anaendelea kusema: "Wafalme waliniambia kuandika elimu ('ilm, i.e. Hadith) kwa ajili yao. Baada ya kuwaandikia kwa muda fulani, mimi nilishikwa na aibu mbele ya Allah swt; (mimi nilijiuliza): Je, kwa nini nimejitayarisha kwa ajili ya kuwaandikia wafalme na wala si kwa ajili ya watu wengineo!?" Ni dhahiri, kama vile itakavyokuja kuonekana kwamba Hadith hazikuwa ni kweli kwa ajili ya Sahaba na Tabiun wote. Wengi wao na akiwemo Ali ibn Abi Talib
waliziandika Hadith na vile vile waliwaambia wengine kufanya hivyo. Wengine walianza kuziandika Hadith wakati sheria zilizowekwa na Makhalifa juu ya kutoziandika Hadith zilipobadilishwa na amri ya Kikhalifa kutoka kuziandika Hadith.
'Umar ibn Abd al-Aziz (101 A.H./719 A.D.) ndiye aliyekuwa Khalifa wa kwanza kuamrisha wanazuoni wa miji mbalimbali kuziandika Hadith na kumpelekea huyo Khalifa maandishi yote. Imeripotiwa kuwa Khalifa alimwandikia Muraah ibn Kathir akimwomba amwandikie Hadith za Mtumes.a.w.w
Vile vile yeye alimwandikia Abu Bakr ibn Muhammad Hazm:"Andika Hadith yoyote ile ya mtume s.a.w.w uliyonayo na kunitumia na chochote kile kilichonakiliwa kutoka kwa Umar, kwa sababu ninayo hofu kuwa utafika wakati ambapo Hadith zitakuwa zimetoweka."
Yeye pia aliwaandikia watu wa Madinah akiwataka wamwandikie chochote kile kilichobakia cha Hadith za Mtumes.a.w.w
.
Ripoti hizi zinaonyesha wazi wazi kuwa uandikaji wa Hadith haukuwa jambo lenye umuhimu hadi wakati huo, hata hivyo, haimaanishi kuwa hapakuwepo na Hadith zilizokuwa zimeandikwa hadi wakati huo. Pamoja na kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz kazi hii haikufuatiliwa na Makhalifa waliofuata, na kwa mara nyingine tena uandikaji wa Hadith uliangukia katika kusahauliwa. Kukariri (kuhifadhi katika akili) ndiyo iliyokuwa njia iliyobakia. Hadith za kusemwa mdomoni tu (bila ya maandiko) ndiyo iliyokuwa njia ya uenezaji wakati ambao Sunni walirithi kutoka vizazi vyao vilivyowatangulia, ilisababisha upinzani mkubwa mno katika kuziandika Hadith. Sisi twaweza kuelewa vyema hali hii wakati tutakapokuja kujua kuwa baadhi ya Muhaddithun walichukizwa mno na uandishi wa Hadith hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. Kauli za wanahistoria kuhusiana na ukusanyaji wa Hadith hapo mwanzoni zinaelezea hayo hayo.
Abd al- Razzaq anaelezea kuwa mtu wa kwanza kuzikusanya Hadith alikuwa Abd al-Malik ibn Jurayj, aliyejulikana kama Ibn Jurayj (150 A.H./767 A.D.) Vile vile Abd al-Rahman Al-Awzai (88-157 A.H./707-773 A.D.) alikuwa ni miongoni mwa wale walioanza kuzikusanya Hadith. Al-Dhahabi anaandika kuwa, katika kipindi hiki ndipo Wanazuoni wa Kiislamu walianza kuandika Hadith, Fiqh na tafsiri katika mwaka 143 A.H./760 A.D. Wafuatao ndio waliokuwa wakiongoza katika kazi hizo nao ni Ibn Jurayj katika mji wa Makkah, Malik (179 A.H./795 A.D.) huko Madinah, al-Anzai katika Syria, Said ibn Abi Urwah (156 A.H./783 A.D.) huko Basrah, Muammar huko Yemen, Sufyan al-Thawri (156 A.H./783 A.D.) huko Kufah. Kabla ya kipindi hicho, hata hivyo, Muhaddithun waliongoza wakiripoti Hadith kutokea kukariri au kutokea kwa waliotegemewa lakini zilikuwa ni mikusanyo isiyokuwa na mipangilio.
Mahali pengine yeye ni mbainifu zaidi wakati asemapo: "Ibn Jurayj na Ibn Abi Urwah walikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith na Muammar ibn Rashid alikuwa ni wa kwanza miongoni mwao huko Yemen." Ipo habari iliyoripotiwa na Abd al-Aziz ibn Muhammad al-Darwardi kuwa mtu wa kwanza kukusanya elimu alikuwa Ibn Shihab al-Zuhri. Ibn Shihab al-Zuhr (124 A.H./742 A.D.) mwenyewe anaripotiwa akiwa amesema: "Umar ibn Abd al-Aziz alituamrisha kuzikusanya Hadith za Mtumes.a.w.w
Kufuatiwa hayo sisi tuliandika katika sura ya kitabu, na kupeleka nakala ya kitabu hicho katika sehemu zote za utawala wake." Ni dhahiri, ingawaje Hadith zilikuwa zikikusanywa kwa kiasi fulani katika siku hizo, kazi ya ukusanyaji ilianza kuzorota kwa sababu ya upingamizi uliofuatia kifo cha Umar ibn Abd al-Aziz, na vile anavyosema al-Dhahabi, kazi hiyo ya ukusanyaji wa Hadith uliahirishwa au kuachwa kwa kipindi cha nusu karne.
Ibn Hajar anasema: "Kazi ya ukusanyaji na upangaji (tabwib) wa Hadith ulianza katika miaka ya mwishoni mwa kipindi cha tabi'un, yaani ni kwamba; wakati ambapo Wanazuoni wa Kiislam walipokuwa wameenea katika miji. Wa kwanza katika ukusanyaji wa Hadith walikuwa ni Rabi ibn Subayh na Sa'id ibn Abi Urwah......hadi wakuu miongoni mwa Wanazuoni wa tabaka la tatu walipokusanya ahkam.
Al-Dhahabi pia anaelezea kitu kama hicho. Kutokana na taarifa hizo inaweza kudadisiwa kuwa ukusanyaji wa Hadith uliotokezea katika sehemu mbili: Sehemu ya kwanza ni mkusanyiko usio kamilifu mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. na sehemu ya pili ni ukusanyaji uangalifu katika sehemu yake ya pili. Hajji Khalifah anakubaliana na haya pale asemapo: "Wakati Islam ilipoenea katika sehemu mbalimbali, na miji ya Islam ilipopanuka, tabi'un walisambaa mote humo. Baada ya muda, mkuu wao alipofariki dunia na hivyo ndivyo ilivyokuwa imekuja kuathiri ukusanyaji wa Hadith.
Wanazuoni walianza kuhisi haja ya kuziandika Hadith na kuzihifadhi kwa njia ya kuziandika. Katika maisha yangu, lilikuwa ni jambo la maana la kuziandika Hadith, kwa sababu kukariri tu kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuja kupoteza fahamu au kuzipotoa. Baada yao, kulitokezea kipindi cha wataalamu wa Hadith kama Ibn Jurayj na Malik ibn Anas. Inasemekana kuwa mtu wa kwanza katika kukusanya Hadith alikuwa Rabi ibn Subay wa Basrah. Baada yahuyo, zoezi kama hili lilikuwa ni la kawaida.
Kutokana na taarifa hizo, tunaweza kumalizia kuwa, kotekote, kulikuwapo na vipindi vitatu katika mpitilio wa Hadith za kutamkwa. Kipindi cha kwanza kilichukua/kilidumu mwanzoni hadi mwishoni mwa karne ya 1 A.H. /7 A.D. katika kipindi hiki uandishi wa Hadith haukuwapo wala haukujaribiwa isipokuwa tu katika hali chache ambapo Sahaba walijaribu kuziandika kwa kwenda kinyume na amri ya Makhalifa. Katika kipindi cha pili, kuanzia mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. hadi kwa kufikia katikati, kulitokezea uandishi na ukusanyaji wa Hadith katika hali isiyokuwa kamilifu na pia mambo yaliyoandikwa yaliweza kukusanywa. Katika kipindi cha tatu, kilichoanzia katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., uangalifu mkubwa ulielekezwa katika ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ikiwa ni shughuli muhimu kimsingi. Vitabu vichache mno vilivyoandikwa katika kipindi hiki vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana- kama vile musannaf Ibn Abi Shaybah, musannaf ya Abd al-Razzaq na Muwatta ya Malik ibn Anas yalikuwa yameanzishwa katika sehemu ya pili ya karne ya 2 A.H./8 A.D. Kwa mujibu wa ripoti ya al-Dhahab, musnad ya kwanza ilikusanywa na Nu'aym ibn Hammad. Yahya al-Hamani huko Kufah na al-Musd huko Basrah nao ndio waliokuwa wa kwanza miongoni mwa Wanazuoni wa miji hii katika kukusanya musnad.
1
TADWIN AL HADITH
UANDISHI WA HADITH
4. SABABU ZA KUCHELEWA KUANDIKA HADITH
Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtumes.a.w.w
, kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi kuhusu uandishi wa Qurani. Kimatokeo Qurani ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif). Hata hivyo, katika hali ya Hadith kwa mujibu wa imani yetu mbali na ruhusa au amri ya Mtumes.a.w.w
kwa kuhusiana na uandishi wa Hadith na mbali na ukweli kwamba Hadith zilikuwa zimeandikwa katika zama za uhai wa Mtumes.a.w.w
, sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu kwa kazi, pia iliweza hata kupingwa. Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni.
Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na 'udhubillah' Mtumes.a.w.w.
Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtumes.a.w.w
, basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtumes.a.w.w
hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao. Kwa hivyo, walimwelekezea Mtumes.a.w.w
kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.
5. RIWAYA YA ABU SA'ID
Riwaya ifuatayo imenakiliwa kwa mamlaka ya Abu Sa'id al-Khudhri: "Musiandike chochote kile kutoka kwangu isipokuwa Qurani tu, na yeyote yule aliyekwisha andika chochote kile basi ni lazima ayateketeze yote." Taarifa hiyo ni wazi na yenye maana isiyofahamika. Maana inayotakiwa kuelezwa ni kwamba hakuruhusiwi kuandikwa kwa Hadith. Kwa mujibu wake, mtu yeyote aliyekuwa ameandika chochote kile basi lazima akiteketeze. Ni sawa kabisa kwa sababu ya uwazi wa ubainishi wake, vile vile pamoja na sababu zinginezo, ndiyo maana sisi hatuwezi kuikubali uhakiki wa taarifa hiyo au nyinginezo kama hizo. Sababu zetu za kutokubaliana na Hadith hiyo ya juu ni kama zifuatazo:
1.Kwanza
: iwapo sisi tutaikubalia Hadith hii basi hatuwezi kuifungia kipindi cha muda. Iwapo uandishi wa Hadith ulikatazwa na haram, basi ni haram katika kila zama. Hata hivyo, sisi twaona wanaoinakili Hadith hii, wao wenyewe hawakuifuatilia na wao hatimaye waliziandika na kuzikusanya Ahadith. Uandishi huu, kama ilivyoonekana hapo juu, ulianza katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., na kukosekana kwa utiifu wa Hadith inatuonyesha kuwa hao wanainakili Hadith walikuwa hawakuichukulia kama sahihi na kweli; kwani hao walijua kuwa chochote kile kilichoharamishwa na Shariah haiwezi kubadilishwa kikawa halali. Jambo la kuvutia humu ni kwamba wao wameirekodi hata Hadith hii, ambavyo wao hawakuifuatilia, kwa kalamu zao zilizobarikiwa! Je, itawezekanaje sisi kuiamini kuwa ni sahihi na kweli?
2.Pili
: waandishi hawa hawa pia wamezinakili Hadith zinginezo zinazozungumzia kuruhusiwa kuandikwa kwa Hadith, na iwapo sisi tutazichukulia Hadith zote mbili kuwa ni sawa katika maelezo na maelekezo, basi itatulazimu kuziachia mbali Hadith zote mbili hizo kwa sababu ya kupingana kwao kwenyewe. Kwa hivyo, katika hali kama hii Hadith hizi zote mbili zinapoteza ustahi wa kuaminika; navyo hata sisi, kwa kudhania tu, hatuwezi kamwe hata kutumia njia zinginezo kusadikisha Hadith ambayo ipo inakataza uandishi wa Hadith za Mtumes.a.w.w
.
3.Tatu
: Abu sa'id al-Khudhri, ambaye anatajwa hapo juu kwa wingi katika kuinakili taarifa hiyo, pia anatoa taarifa nyingine inayopingana na ile ya kwanza, yeye anasema:
"Katika siku hizo, sisi tulikuwa hatuandiki chochote kile isipokuwa Qurani na tashahud."
Nukta mbili zinaweza kufahamika kwa kujua sababu zake kutokana na taarifa za Abu Sa'id.
Kwanza
: Abu Sa'id haelezi kuwa kutoandika kwao Hadith kulitokana na amri ya Mtumes.a.w.w
kwani kama ingalikuwapo, basi angalionyesha hayo, hadi hapo isemwe kuwa maelezo kama hayo hayakuazimiwa hapa. Uwezekano huu wa pili uliotolewa, ingawaje unaweza kuchukuliwa kwetu sisi, inaonekana ya mbali mno. Na nukta ya pili ni kuongezwa kwa neno tashahhud katika taarifa hii, kitu ambacho hakipatanishi pamoja na kusudi la uharamisho wa kuandika isipokuwa Quran tu. Ni jambo la kutilia maanani kwamba Hadith nyingine kutoka kwa Ibn Mas'ud, neno istikharah limeongezwa pamoja na tashahhud.
Kwa kuhusiana na Hadith hii, inawezekana kukaulizwa, je, ni kwa nini Mtumes.a.w.w
aruhusu uandishi wa tashahhud pekee yake, ambapo inatambuliwa kuwa kutapotea vile wakati uendeleavyo, hayo pia yaliweza kutokea pamoja na Hadith zinginezo, baadhi yao ambazo zilikuwa na maongozo muhimu kabisa ya Shariah za Dini. Na katika upande wa pili, iwapo kulikuwapo na madhara yoyote katika kuziandika Hadith, basi madhara hayo pia yaliweza kutokezea katika kuandika tashahhud au chochote kile. Kwa hivyo, haikubaliki kimantiki kudai kuwa Mtumes.a.w.w
ndiye aliyeharamisha kuandikwa kwa Hadith.
4.Nne
: kile kinachoweza kukusanywa kutokana na historia- ambacho sisi tutalisemea kwa zaidi hapo mbeleni - Abu Bakr, na hata Khalifa wa pili, walipendekeza kuandikwa kwa Hadith mwanzoni mwa Ukhalifa wao. Hata hivyo, hapo baadaye wao waliharamisha kwa kutolewa kwa sababu zao. Hao Makhalifa kamwe hawakusema kuwa kazi kama hiyo ilikuwa imeharamishwa na Mtumes.a.w.w
. Zaidi ya hayo wao waliposhauriana na Sahaba wengineo kuhusu kuandika Hadith, nao pia walipendezewa na shauri hilo. Hii pia linatuthibitishia kuwa hapa kutolewa amri na Mtumes.a.w.w
. ya kuharamisha kuandika kwa Hadith.
5. Katika mojawapo ya Hadith Abu Basir anaripotiwa akiwa amemwambia Abu Sa'id al-Khudhri: "Sisi twaandika chochote kile tukisomacho." Abu Sa'id alimwambia: "Je, wataka kuyakusanya ili ukitengeneze Kitabu? Mtumes.a.w.w
. ametuelezea Hadith nasi pia twakuambia wewe, nawe pia kama sisi ni lazima uzikariri tu kwa mdomo bila ya kuandika." Nukta mbili hapa zinastahili kuchunguzwa.
Kwanza, Abu Sa'id hasemi kuwa Mtumes.a.w.w
. ndiye aliyeharamisha uandikwaji wa Hadith. Pili, sababu aitoayo kwa kutoziandika Hadith ni sawa na zile zilizoripotiwa kutokea kwa Khalifa wa pili, ambaye naye pia hamsemi Mtumes.a.w.w
. kuwa ndiye aliyeharamisha uandishi wa Hadith. Katika hali yoyote ile, ni jambo la kuyakinisha kuwa Mtumes.a.w.w
. kamwe hakuharamisha uandishi wa Hadith.
6.Sita
, kuna taarifa katika Hadith, moja kwa moja baada ya kutajwa hiyo ya juu, na kuwapo kwake pia kunatudalilishia kule kutothaminiwa kwake: "Simulieni (chochote kile utakacho) kutokea Waisraili. Hakuna madhara ndani yake." Kuanzia mwanzoni kabisa, kwa upande mmoja Mtumes.a.w.w
anafahamika kwa kuchukizwa mno katika kusikia hadithi za Mayahudi (hujulikana kama Israiliyyat) -na kwa upande wa pili, Wanazuoni wa Kiislam wamekwisha zitambua madhara ya mawazo yanayoenezwa nayo, inaweza kusemwa kuwa Hadith hiyo nzima ni kazi ya uzushi mtupu. Hadith hii inawataka Waislam kwa upande mmoja, waziandike Hadith za Mtumes.a.w.w,
na hatimaye kwamba zitaweza kusahauliwa pole pole; na upande wa pili, inawapatia leseni ya bure ya kuunganisha chochote kile wakitakacho kutoka kwa Mayahudi, Haya ndiyo maazimio maovu kabisa za Hadith kama hizi za kuzuliwa. Je, kunaweza mtu yeyote mwenye akili timamu akasema kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyetoa amri kama hiyo?
Ipo Hadith nyingineyo kutokea Abu Sa'id al-Khudhri ambayo inatuletea uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kutomruhusu Abu Sa'id kuandika Hadith kutokana na sababu maalum, ingawaje, katika mtazamo wetu, uwezekano wa kuruhusiwa katika swala hili pia ni kwamba Hadith hii vile vile ni uzushi. Abu Sa'id asema:"Mimi nilimwomba Mtume s.a.w.w. ruhusa ya kuandika Hadith, lakini yeye alikataa kunipa idhini." Je kwa sababu zipi ? Hadith hii inatuunga mkono katika uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kwa kumkatalia ruhusa ya kuandika Hadith katika swala la Abu Sa'id. Wakati inapozingatiwa katika nuru ya Hadith, ambazo sisi tutazinakili hapo mbeleni, ambapo Mtume s.a.w.w. yupo anaripotiwa kwa kutoa idhini kwa watu wengineo basi uwezekano huu utajipatia nguvu zaidi.
7. KUTOKUBALIKA KWA HADITH ZA ABU HURAYRAH
Kuhusiana na hayo, kuna Hadith kutoka kwa Abu Hurayrah ambayo pia imehusika. Abu Hurayrah asema: "Mtumes.a.w.w
. alitufikia wakati tulipokuwa tunaziandika Hadith. "Je, mwaandika nini?" Aliuliza Mtumes.a.w.w
mimi nilijibu: "Haya ni mambo ambayo sisi tumeyasikia kutoka kwako." Mtumes.a.w.w
.
alisema: "Je, munataka kuandika kitabu mbali na Kitabu cha Allah swt? Hakuna kilichopotosha mataifa isipokuwa tu pale wameandika kitabu mbali na Kitabu cha Allah (Quran)" Hadith hii pia haikubaliki kwa sababu zifuatazo:
1. Kwa sababu ya wengi waliokwisha kutoa sababu zao katika masomo yao na ambazo sisi pia tumeziona kuwa zinaweza kukubalika baada ya kuchunguzwa, hivyo usadikifu ('adalah) wa Abu Hurayrah hauwezi kukubaliwa. Vile vile inawezekana kuwa Hadith hii imezuliwa na wengine halafu wakaja kumtaja Abu Hurayrah kuwa ndiye aliyeiripoti.
2. Pili, mazungumzo yaliyomo ni sawa kabisa, kama vile yalivyokuwa yametolewa na Khalifa Umar wakati alipokuwa ameamua kuziandika Hadith na baadaye kughairi. Lakini Khalifa mwenyewe kamwe hakumsingizia Mtumes.a.w.w
. Wakati ambapo Abu Hurayrah, au wale wote wengineo wakimsingizia Mtumes.a.w.w
., hawakutupatia mwanya wa kubishana nao kwa madai yao (kwani madai yao ni kuwa Mtumes.a.w.w
. tu ndiye aliyeyasema, hivyo hakuna ubishi juu yakauli ya Mtume): Khalifa Umar kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, alifikia maamuzi hayo baada ya kuzingatia mambo fulani fulani.
3. Tatu, mazungumzo yaliyomo na yanayonekana katika Hadith hii ingawaje inaonekana kuwa inayo mizizi katika kauli ya Mtumes.a.w.w
. ambayo itazungumzwa hapo mbeleni, inazungumzia juu ya Mtumes.a.w.w
. kuharamisha vitabu vya Mayahudi na Wakristo, na wala si kuharamishwa Hadith za Mtumes.a.w.w.
ambazo ni kitu kilicho kamili baada ya Quran.
4. Nne, je inawezekana kwa Mtumes.a.w.w.
kuharamisha kuandikwa kwa Sunnah, ambayo ndiyo inayofuatia baada ya Quran? Au aliharamisha kuwa hivyo isibakie sambamba na Quran? Je, ni nafasi ipi iliyo ya Sunnah ya Mtumes.a.w.w.
isiokuwa ubavuni mwa Quran? Je, ni ukweli unaoweza kupingwa kuwa Quran na Sunnah ndivyo kwa pamoja vinafanya Shariah za Kiislam? Ipo Hadith nyingine ivutiayo, ambayo inadhihirisha tabia ya udanganyifu wa Hadith kama hizo, nayo ni ile iliyonakiliwa na Abu Hurayrah. Baada ya kuelekezea kama taarifa tuliyonayo ipo, inaendelea kuongezea mambo mengi ambayo yanatudhihirishia upotofu katika upande wa Abu Hurayrah, au mzushi aliyezusha juu yake. Kwa mujibu wa Hadith hii, Mtumes.a.w.w.
aliwasikia watu wameziandika Hadith zake. Papo hapo, alikwenda juu ya Mimbar na baada ya kumsifu Allah swt alisema: "Ni aina gani ya vitabu hivi ambavyo nimesikia mmeviandika? Kwa hakika mimi ni mwanadamu tu. Yeyote aliyeandika chochote kile, basi ni lazima aniletee mimi." Hadith hiyo kwa wazi wazi inakanusha Sunnah ya Mtumes.a.w.w.
kwani Mtumes.a.w.w.
yupo anakana uwezekano na uhalali wake wa utume kwa kusema kuwa yeye alikuwa ni mtu kama watu wengine wa kawaida. Hili ni jambo ambalo mtu yeyote hawezi kulikubali kwani ni uzushi mtupu. Jambo la kuvutia zaidi ni kuhusu kusema kwa Mtumes.a.w.w.
hapa ('mimi ni mwanadamu') ipo imeelezwa katika Hadith nyingine kuwa hayo yalisemwa na kikundi cha watu wa Quraysh kuhusu Abd Allah ibn Amir ibn al-As, ambaye alikuwa ameandika Hadith za Mtumes.a.w.w.
Hapo Mtumes.a.w.w.
hatilii maanani maoni yao kwa hakika yupo anayakanusha. Anasema:"Mimi hakuna nilisemalo isipokuwa ni haki tupu."
5. Tano, ipo imeripotiwa kutoka Abu Hurayrah mwenyewe kuwa hakuna mtu yoyote yule anayemzidi katika kunakili Hadith, isipokuwa Abdallah ibn Amribn al-As, kwa sababu huyu alikuwa akiziandika wakati ambapo Abu Hurayrah hakuwa akifanya hivyo. Taarifa hii inaonyesha kutokuwapo kwa uharamisho Abdallah aliziandika Hadith zote, ambapo zipo sababu za kibinafsi zilizomfanya Abu Hurayrah asiziandike. Hivyo, inatuonyesha wazi wazi kuwa hapakuwepo na amri yoyote yenye kuharamisha kuandikwa kwa Hadith za Mtume s.a.w.w.; wote waliotaka kuziandika waliziandika, na yeyote asiyetaka kuziandika hakuziandika lakini kwa sababu zao binafsi bila ya kuzuiwa.
6. Sita, katika ripoti nyingineyo Abu Nuhayk, mwanafunzi wa Abu Hurayrah, asema: "Mimi nilikuwa nikiviazima vitabu kutoka kwa Abu Hurayrah, nilinakili, na kumchukulia (makala zangu) Abu Hurayrah na kumsomea. Kwa kila Hadith nilikuwa nikimwuliza iwapo amewahi kumsikia Mtume Mtukufus.a.w.w.
akiisema, naye alikuwa akiitikia." Hadith hii pia inaonyesha uongo wa Hadith isemayo kuharamishwa uandishi wa Hadith, ambayo amesingiziwa Abu Hurayrah.
7. Imeripotiwa na Hamman ibn Munabbih, mwanafunzi wa Abu Hurayrah kuwa alikusanya mus-haf iliyokuwa na Hadith zote zilizokuwa zimenakiliwa na mwalimu wao katika uhai wake. Hayo pia yanatuonyesha kupingana na Hadith hiyo, kwani isingewezekana kwa Abu Hurayrah kunakili Hadith inayoharamisha uandishi wa Hadith wakati ambapo wanafunzi wake wameziandika Hadith mbele yake na katika uhai wake, au tuseme labda kuwa Abu Hurayrah hakutekeleza Hadith ipigayo marufuku uandishi wa Hadith kwa kunakili Hadith na kuzifundisha.
Vile vile ipo Hadith nyingineyo iliyoripotiwa na Zayd ibn Thabit kwamba siku moja alimwendea Muawiya, ambaye alimwuliza kuhusu Hadith fulani. Hapo Muawiya alimwambia mtu fulani kuiandika. Hapo Zayd alisema: "Mtume Mtukufus.a.w.w.
ametuambia tusiandike Hadith ya aina yoyote ile." Sisi twaamini kwa uhakika uliowazi kuwa Hadith zilikuwa zimeandikwa na Tab'un na Tabi'in na baadhi ya wanazuoni wa Sunni, wanathibitisha kutotegemewa kwa Hadith kama hizo. Hapo mbeleni katika kulichambua swala hili, sisi tutaona uthibitisho utakaoonyesha sababu za kweli katika kuharamisha uandishi wa Hadith za Mtume Mtukufus.a.w.w.
Uhakika na uthibitisho huu unaonyesha kuwa sahihi kwa kumsingizia Mtumes.a.w.w.
kwa taarifa kama hizo. Pia imeripotiwa kuwa Ibn Mas'ud alielezea katika usia wake kuwa mkusanyo (sahifa) wa Hadith zilizofanywa naye, ziteketezwe. Katika sura hii, haionyeshi wazi iwapo tendo hili lilikuwa limejibu amri ya Mtume Mtukufus.a.w.w.
Labda inawezekana, alikuwa akifuata amri ya Makhalifa. Pili, kama vile tutakavyozungumza hapo mbeleni, tendo hilo linaelezea kuhusu kuteketeza riwaya na mapokezi ya Mayahudi (Israilliyyat) na wala si Hadith za Mtumes.a.w.w.
Vile vile imeripotiwa kuwa Abu Musa al-Ash'ari aliziteketeza Hadith zilizokuwa zimeandikwa na mtoto wake. Tukichukulia utiifu wa Abu Musa kwa Khalifa wa Pili, labda inaweza kusemwa kuwa tendo lake hili lilikuwa bila shaka chini ya ushahidi kuonyesha kuwa Abu Musa alitenda kwa kuvutiwa na uharamisho huo wa Mtumes.a.w.w.
kuhusu Hadith.
Moja ya kitu kinachoonyesha kutokuwa halisi kwa mapokezi hayo yaliyozuliwa juu ya Mtumes.a.w.w.
kuharamisha uandishi wa Hadith, ni kauli aliyoitoa Umar kuhusiana nalo kwa nia yake ya kutaka kukusanywa kwa Hadith za Mtumes.a.w.w.
Umar anaripotiwa akiwa amesema: "Mimi nilinuia kuziandika Sunnah za Mtumes.a.w.w.
Lakini lilikuja wazo akilini mwangu kuwa watu waliopita walikuwa wameandika baadhi ya vitabu na walikuwa wakivitegemea mno, hatimaye wao waliacha kukitegemea Kitabu cha Allah swt. Kwa kiapo cha Mungu, mimi sitakubaliana na chochote kile kitakachoweza kukifunika (kuachwa) Kitabu cha Allah (Quran)."
Katika riwaya ya hapo juu, inaonyesha kuwa Khalifa wa Pili alinuia kuandika Hadith hapo awali. Katika baadhi ya tafsiri ya riwaya hii inaelezea kuwa aliwashauri Sahaba wengine kuhusu swala hili nao pia walilikubalia (kuandika Sunnah za Mtumes.a.w.w;
lakini hapo baadaye yeye alilibadilisha shauri lake hilo kwa sababu zake alizozitaja, na wala si kwamba Mtumes.a.w.w.
ndiye anayehusika katika kuharamisha.
Jambo lingine ambalo linaloweza kuonekana kama uthibitisho wa kukanusha uhalisi wa Hadith isemayo juu ya uharamisho wa kuandika Hadith, ni maneno aliyoyasema Mtumes.a.w.w.
siku ya Alhamisi ya mwisho katika maisha yake (yaani kabla ya kufariki). Siku hiyo, walikusanyika Sahaba wote katika kitanda chake Mtumes.a.w.w.
na hapo Mtumes.a.w.w.
aliwaambia: "Nileteeni wino na karatasi ili niweze kuwaandikieni mambo fulani fulani ambayo hapo baadaye nyie mnapashwa kujitahadharisha msitumbukie katika makosa." Hapo baadhi ya watu wakiongozwa na Umar walipinga hayo wakisema "Kitabu cha Allah kinatosheleza kwetu sisi." Riwaya hii inatuonyesha kuwa uandishi wowote mbali na Quran haukupigwa marufuku tu, bali hata ulichukuliwa na Mtumes.a.w.w.
kuwa ni lazima ili kuokoa Ummah kuangukia makosa na upotofu. Wakati Mtumes.a.w.w.
alipokuwa akiulizia vifaa vya kuandikia na kikundi cha Sahaba- kikiongozwa na Khalifa wa Pili kwa mujibu wa al-Shahristani katika al-milal wa al-nihal- walimpinga Mtumes.a.w.w
., kwani Mtumes.a.w.w.
alikuwa akielewa wazi maafa yatakayotokea hapo baadaye kutokea tukio au kisa hiki. Hapo mbeleni sisi tutachambua kwa undani zaidi yaliyokusanywa na kusemwa na wanazuoni wa Sunni kuhusu athari mbaya zilizotokana na kutoandikwa kwa Hadith lakini ni lazima tujiulize "Je, ni sahihi kwa kumdhania Mtumes.a.w.w.
katika kuharamisha kuziandika Hadith zake, jambo ambalo limeleta maovu makubwa katika utamaduni wa Kiislamu na kusababisha Sunnah za Mtumes.a.w.w.
kuchezewa na Hadith hizo za kuzuliwa? Je, ni kweli kuwa Mtumes.a.w.w.
ndiye anayehusika moja kwa moja katika upotofu huu na madhara yote yaliyotokea?"
8. HADITH ZA MTUME S.A.W.W. KATIKA KURUHUSU UANDISHI WA HADITH
Hadith zimepokelewa kutoka Mtumes.a.w.w.
ambamo yeye ameruhusu uandishi wa Hadith kijumla au kuruhusu kikundi fulani. Hadith hizi, zenyewe, zinatosheleza kukanusha Hadith zilizotangulia zinazozungumzia kuhusu kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith, au tuseme haikosi, kuleta vurugu la riwayaat (wingi wa riwaya) katika hali yoyote, zinashindwa kubakia na uhai wao (hujjiyyah);kwani idadi ya Hadith hizi ni kubwa mno, na kwa kutilia maanani ya makanusho yaliyonayo dhidi ya Hadith zinazozua juu ya kutoandika Hadith, basi uhalisi wa Hadith kama hizi ni zenye kusadikiwa kabisa. Hadith hizi si kwamba zinazoruhusu kuandika Hadith bali pia zinatuamrisha kuziandika Hadith za Mtumes.a.w.w.
Hadith ifuatayo imenakiliwa kupitia mfululizo wa upokezi kuwa kulikuwapo na mtu aliyemlalamikia Mtumes.a.w.w.
juu ya udhaifu wake wa kuhifadhi mambo katika akili yake. Mtumes.a.w.w.
alimwambia: "Chukua msaada wa mkono wa kulia (i.e. kuandika) dhidi ya udhaifu wa hifadhi ya akili yako." Mtumes.a.w.w.
yupo anaripotiwa akisema: "Ikamateni (hifadheni, iandikeni) elimu kwa njia ya kuandika."
Imeripotiwa kutoka Rafi' ibn Khadij kuwa yeye alisema: "Sisi tulimwuliza Mtumes.a.w.w.
,'Je tunaweza kuandika baadhi ya mambo ambayo twayasikia kwako?' Mtumes.a.w.w.
alijibu, 'Andika hayo na wala hakuna madhara ndani yake.' Imeripotiwa kwa mamlaka ya Amr ibn Shu'ayb kuwa baba yake alimwuliza Mtumes.a.w.w
: "Sisi tukisikia mambo kutoka kwako ambayo hatuwezi kuhifadhi akilini mwetu kwa kipindi kirefu, je, tunaruhusiwa kuyaandika?" Hapa Mtumes.a.w.w
. alijibu:Naam, muyaandike"
Imeripotiwa kupitia mifululizo ya wanaonakili, kutoka Abdallah ibn Al-As kwa kusema: "Mimi nilimwuliza Mtumes.a.w.w
.: 'Je, tunaweza kuandika kile tukisikiacho kutoka kwako? Mtumes.a.w.w.
alijibu, 'Naam.' Mimi niliulizia. 'Bila ya kujali wewe ukiwa umeghadhabika au mpole? Mtumes.a.w.w.
alijibu,"Naam mimi sizungumzi chochote kile isipokuwa haki tupu, hata kama nikiwa nimeghadhabika au nikiwa nimefurahishwa."
Katika Hadith nyingine, msimulizi anaripotiwa kwa kumwuliza Mtumes.a.w.w.
"Je, twaweza 'kuikamata' elimu?" Mtumes.a.w.w.
alijibu:"Naam."
Huyo huyo Abd Allah ibn Amr anaripotiwa kuwa,"Nilikuwa nimezoea kuandika chochote kile nilichokisikia kutoka kwa Mtumes.a.w.w
. kwa ajili ya kurekodi. Baadaye Maqureyshi walinizuia kufanya hivyo, na mimi pia niliachilia kuandika. Baadaye, mimi nilimwelezea Mtumes.a.w.w.
swala hilo. Naye alisema:"kwa kiapo cha Mungu ambaye anayamiliki maisha yangu, mimi kamwe sitamki chochote kile isipokuwa haki tupu."
Imeripotiwa na Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib
kuwa Mtumes.a.w.w
alisema:"Andikeni elimu (ilim) kwani mutafaidi nacho humu duniani na akhera vile vile. Eleweni kuwa elimu haikubali mmiliki wake ateketee."
Hadith nyingine mashuhuri ya Ma-Imam wa Ahl al-Bayt
ambayo imesimuliwa na chanzo cha Sunni na Shia, inaelezea maandiko (sahifah) juu ya upanga wa Mtumes.a.w.w.
Al-Imam al-Sadiq
anaripotiwa akiwa amesema: "Kulikuwapo na Sahifah katika mpini wa upanga wa Mtumes.a.w.w.
yakisomwa:"Amelaaniwa yule anayeiba mipaka ya ardhi. Amelaaniwa yule ajifanyiaye marafiki mbali na mawali wake."
Au alisema:"amelaaniwa yule ambaye anakana neema za Mola wake aliyempatia."
Abu Hurayrah anaripotiwa akisema: "Hakuna yoyote yule anayeweza kuelewa zaidi yangu kuhusu Hadith za Mtumes.a.w.w.
isipokuwa Abd Allah ibn Amr, kwa sababu yeye alikuwa akiyaandika kwa mkono wake, na kuhifadhi akilini mwake, ambapo mimi nilikuwa nikiyahifadhi tu bila ya kuyaandika. Naye huyo alikuwa amepatiwa idhini na Mtumes.a.w.w.
kwa ajili ya kuziandika Hadith zake." Abd Allah ibn amr anaripotiwa kwa kusema: "Mimi nataka kusimulia Hadith zako na iwapo wewe utaniruhusu mimi nitaweza kuutumikisha mkono wangu (i.e. katika kuandika) ili kuusaidia moyo wangu (i.e. kuhifadhi). Na Mtumes.a.w.w.
alisema, 'iwapo ni Hadith zangu, basi lazima uchukue msaada wa mkono wako.''' Yeye pia anaripotiwa kuwa na sahifah ambayo ilijulikana vyema kama al- Sahifat al-Sadiqah, ingawaje wengine wanakana kama ilikuwa na Hadith za Mtumes.a.w.w.
Al-Mughirah ibn Shu'bah anaripotiwa kwa kuthibitisha kuwa Abd Allah ibn Amr alikuwa na Sahifah iliyoitwa al-Sahifah al-Sadiqaah.
Katika Hadith nyingine, Mtumes.a.w.w.
anaripotiwa akisema:"Wakati mumin anapokufa, karatasi alimoandika elimu (ilim) itabakia daima na itakuwa ni pazia baina yake na moto wa Jahannam Siku ya Qiyama."
Al-Tirmidhi ameripoti kuwa Sa'id ibn Ubadah alikuwa na sahifah ambamo alikusanya idadi kubwa ya Hadith za Mtumes.a.w.w.
Mtoto wake pia alikuwa anayo mazoea ya kunukuu Hadith kutoka sahifah hiyo. Kwa mujibu wa riwayah za al-Bukhari, ilikuwa ni nakili ya sahifah ya Abdallah ibn Awfi ambaye alizoea kuandika Hadith ndani mwake kwa mikono yake mwenyewe. Samurah ibn Jundab pia alikusanya Hadith nyingi katika kitabu chake kikubwa na mtoto wake, Sulayman, aliyerithi, alizoea kunakili Hadith kutokea humo. Bila shaka yalikuwa ni maandiko haya ambayo Ibn Sirin anayasemea: "Katika risalah aliyoiacha Samurah kwa mtoto wake, humo kuna kiwango kikubwa mno cha ilimu.
Imeripotiwa na Anas akisema huku amenyooshea mkono kwa mus-haf: "Hizi ni Hadith ambazo mimi nimezisikia kutoka kwa Mtume Mtukufus.a.w.w.
Mimi niliziandika na nilimpatia Mtumes.a.w.w.
(kwa ajili ya uthibitisho wake)." Al-Imam Jaafer al-Sadiq
. anasimulia kutokea Mababu zake
. kwamba Mtumes.a.w.w.
alisema:"Wakati unapoandika Hadith, andika pamoja na sanad yake (ufululizo wa upokezi wake). Iwapo itakuwa ni kweli, basi utagawana thawabu zake; na iwapo zitatokezea kuwa ni za uongo, basi madhambi yake yatamwia aliyesema."
Mtumes.a.w.w.
pia anaripotiwa kwa kusema:"Ikamateni elimu."
Na alipoulizwa ni nini alichokuwa akimaanisha, alielezea kuwa yeye alikuwa akimaanisha uandishi. Umma Salma R.A. ameripotiwa akiwa amesema: "Mtumes.a.w.w.
aliulizia adim ya kondoo iliyotiwa dawa ili isioze iletwe mbele yake. Imam Ali ibn Abi Talib
alikuwa pamoja naye. Baadaye aliyazungumza mambo mengi mno kwa Imam Ali ibn Abi Talib
hadi kukaandikwa sehemu zote mbili za ngozi hiyo na vile vile kingo zake pia zilijaa maandishi."
Hadith zote hizi zinathibitisha wazi kuwa Mtumes.a.w.w.
aliruhusu uandishi wa Hadith. Wapo Wanzuonini wengi ambao wanashikilia kwamba Mtumes.a.w.w.
alikuwa ameharamisha hapo mwanzoni na kuruhusu hapo baadaye. Iwapo ndiyo hali ilivyo, je, ilikuwa ni kwa misingi gani ambapo baadhi ya Makhalifa waliharamisha uandishi wake na baada ya Hadith nyingi mno kuandikwa, tukamsingizia ati kuwa ni Mtumes.a.w.w.
ndiye aliyeharamisha uandishi wa Hadith? Rashid Ridha amezichambua Hadith zinazoharamisha na zenye kuruhusu kuandika Hadith.Yeye anajaribu kuthibitisha kuwa Hadith zinazopiga marufuku zinashinda zile zenye kuruhusu, hivyo Hadith zinazoelezea kuharamishwa kwa kuandika Hadith ni lazima zichukuliwe kuwa ni halisi na kweli. Yeye anaandika:
"Iwapo tutachukulia kuwapo kwa mgogoro baina ya Hadith zenye kupiga marufuku na zile zenye kuruhusu, basi mtu anaweza kusema kuwa mojawapo baina yao imetengua (batilisha) nyenzio kwa kuthibitisha kuwa Hadith zinazoharamisha zinashinda zile zenye kuruhusu, kwa sababu mbili: Kwanza, Sahaba walisimulia Hadith zinazoharamisha hata baada ya Mtume s.a.w.w. Pili, Sahaba hawa kuziandika Hadith; kwani iwapo wao wangalikuwa wameziandika, basi zingalikuwa zimetufikia sisi." Sisi hatuwezi kukubaliana na maelezo hayo kwa sababu zifuatazo: Kwanza, Sahaba ndio waliosimulia Hadith zenye kuruhusu uandikaji wa Hadith pamoja na zile zinazoharamisha, na kama vile tulivyokwisha ona hapo juu, baadhi ya Sahaba waliendelea na kuziandika hizo Hadith.
Pili, sababu ya Sahaba kutojishughulisha na ukusanyaji wa Hadith kulitokana na kutolewa kwa amri ya kuharamishwa na Makhalifa wa kwanza na pili, na wala si kuwa ni Mtumes.a.w.w.
aliyeharamisha. Tatu, kwa kuwa haiwezekani sisi tukadai kuwa aina moja ya Hadith hizi zinashinda aina ya pili yake, sisi twaweza kusema kuwa ugomvi wao unazifanya zote ziwe zimebatilika na wala si kwamba mojawapo inaishinda ya pili yake. Kuhusiana na kukubali kwa Abu Hurayrah kuwa Abd Allah ibn Amr alizoea kuandika Hadith, Rashid Ridha anasema: "Hakuna sababu ya kwamba sisi tuchukulie hivyo kama uthibitisho wa ruhusa ya kuandika Hadith, kwa sababu haijaelezwa katika Hadith kuwa Abdallah aliandika Hadith kwa kuruhusiwa na Mtumes.a.w.w.
Sisi tulikwishawaonyesha hapo juu riwaya zinazoonyesha kuwa Abd Allah ibn Amr kwa hakika alikuwa amepatiwa ruhusa kama hiyo. Zipo riwayat nyingi ambazo zimeshuhudia hayo, na mojawapo hapo juu Abu Hurayrah kwa kusisitiza anasema kuwa Abd Allah ibn Amr alikuwa amepatiwa ruhusa na Mtumes.a.w.w.
kama hiyo. Ama kwa upande wa upinzani, wengineo, kama Abu Zuhra, wenye mawazo ya kusema kuwa Mtumes.a.w.w.
aliruhusu uandishi wa Hadith kufikia mwishoni mwa Utume wake ambapo hapakuwapo na hatari ya kuzichanganya Hadith pamoja na Aya za Quran. Iwapo sisi tutachukulia kusema kuwa matendo ya baadhi ya Sahaba, hasa yale ya Makhalifa, sisi hatuwezi kuikubalia hivyo, ama kwa upande wa pili, iwapo tutakubalia, basi itatubidi kuwalaumu baadhi ya Makhalifa kwa mienendo yao. Sisi hatujui iwapo Bwana Abu Zuhrah ataupendelea uelekeo upi.