2
TADWIN AL HADITH
UANDISHI WA HADITH
9. MAONI YA BAADHI YA SAHABA KUHUSIANA NA UANDIKAJI WA HADITH
Mbali na imani ya baadhi ya Sahaba kuwa Hadith zisiandikwe, kikundi miongoni mwao kiliendelea kufanya hivyo. Ukweli huu ni dalili yenyewe inayoelezea kuwa kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith ulitokana na Makhalifa na wala si Mtumes.a.w.w.
kama inavyodaiwa. Miongoni mwa Sahaba waliokuwa wakiamini ruhusa ya uandishi wa Hadith walikuwa Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib
na mwana wake al-Hasan
ambao si tu kwamba waliziandika Hadith, bali walitilia mkazo juu ya uandikaji wake pia.
Abdallah ibn al-Abbass, imeripotiwa kuwa alizoea kusema, "Ikamateni (kuitia mahabusi) 'ilim kwa njia ya kuiandika." Harun ibn Antarah anaripoti kutokea baba yake kuwa abd Allah ibn al-Abbass baada ya kuitamka hiyo Hadith aliyomwomba aiandike. Salami anaripoti kuwa yeye aliona vipande vya maandishi kwa Ibn abbass ambamo alikuwa ameandika matendo ya Mtumes.a.w.w.
kama vile ilivyokuwa imesimuliwa na Abu Rafi. Imeripoti kuwa Anas ibn Malik alizoea kumwambia mwanae:"Ikamateni ilim kwa kuiandika."
Al-Kattani anaripoti kuwa Ayadh alizoea kusimulia ruhusa ya kuziandika Hadith kutokea Sahaba na Tabi'un. Hata hivyo, wengi wa Sahaba, inavyoonekana, ama walikuwa hawana uhakika katika yale waliyoyaandika kuhusu kuruhusiwa kwa kuziandika Hadith au hawakuwa na ari ya kuyazingatia na kuyasisitiza hayo kimatendo; uthibitisho huo ni kule kujiepusha kwao katika ukusanyaji wa Hadith.
Zaazan anaripoti: "Mimi nilichukua baadhi ya maandishi (tasabih) kutoka Umm Ya'fur na kumwendea Imam Ali ibn Abi Talib
Naye alinifundisha hayo na baadaye aliniambia nikayarudishe kwa Umm Ya'fur."
Imenakiliwa pia kwamba Ibn Abbass alizoea kuziandika Sunan za Mtumes.a.w.w.
juu ya vibao vya kuandikia, ambazo alizichukua mwenyewe hadi pale palipokuwapo na mkusanyiko wa Wanazuoni. Pia imeanakiliwa kwa wingi (mutawatir) kuwa alipofariki aliacha vitabu vingi mno vinavyoweza kupakiwa juu ya ngamia mmoja. Kwa mujibu wa ripoti kuwa Abu Bakr aliandika baadhi ya Hadith baada ya Mtumes.a.w.w.
na baadaye alizichoma moto, nayo pia inadalilisha kuwa uandishi wa Hadith ulikuwa ni desturi iliyokuwa inakubaliwa miongoni mwa Sahaba.
Riwaya iliyonakiliwa kutoka Imam Ali ibn Abi Talib
ambamo alisema kuwa yeyote aandikaye Hadith basi aandike pamoja na sanad yake navyo pia inaungana na mawazo hayo. Vianzio vyote vyote ni dhahiri kuwa idadi ya Sahaba walikubaliana kuwa uandishi wa Hadith ulikuwa umeruhusiwa. Ripoti kuhusu Sahifah ya Ja'abir ibn Abd Allah ambayo ilikuwanayo Hadith za Mtumes.a.w.w.
pia inaunga mkono juu ya tabia na mazoea ya Sahaba katika uandishi wa Hadith zilikuwapo miongoni mwa Sahaba. Katika misingi hiyo, tunaweza kumalizia kuwa uandishi wa Hadith ulikuwa umekubaliwa na vikundi vya Sahaba na upinzani wa Mahalifa juu ya uandishi wa Hadith haukutokana na kukatazwa na Mtumes.a.w.w.
kama inavyodaiwa, bali ulitokana na uamuzi wao wenyewe.
9. AL-QURAN NA UANDISHI
Al-Khatib al-Baghdadi, ili kuunga mkono maelezo yake juu ya ruhusa ya uandikaji wa Hadith, anaelezea uthibitisho kutokea aya za Qurani.Katika misingi ya Quran inayotuamrisha kuandika vyote vile ambavyo vina hatari ya kuweza kusahaulika, yeye anaelezea kuwa Hadith, ambayo pia ipo hatarini kupotea, basi ni lazima ziandikwe. Katika uhusiano huu yeye anaelezea aya zifuatazo za Quran 2:282, 6:91 na 31:157 Al-Tahawi, pia anaelezea akitoa Aya: "Wala msipuuze kuandika, mapatano yawe ni madogo au makubwa mpaka muda wake" (2:282) kuhusu uandishi wa madeni, anasema kuwa pale Mwenyezi Mungu anapotuamrisha kuandika madeni ili kuepukana na kutokezea mashaka na mizogo, na uhakika wa elimu ambavyo pia kuuchunga kwake ni vigumu kabisa na muhimu mno kuliko kurikodi madeni basi inasimama pamoja na umuhimu mno katika kuandikwa ili kuepukana na mashaka yaliyoelezwa hapo juu. Abu Hanifa, Abu Yusuf na Muhammad ibn al-Hassan al-Shaybani pia ni watu waliokuwa na msimamo kama huo.
10. MTUME S.A.W.W. KUHARAMISHA UANDISHI WA HADITH NA SABABU ZA KWELI
Uchambuzi wetu wa hapo mwanzoni unatuonyesha kuwa lawama zozote katika ucheleweshwaji wa uandishi wa Hadith hauwezi kamwe kutupiwa Mtumes.a.w.w.
kwani riwaya zote zilizozuliwa juu yake haziwezi kamwe kukubaliwa kwa sababu mbali mbali. Katika jaribio hili, sisi tutakuwa tukitegemea mno juu ya riwaya zitegemewazo na Ahl al-Sunnah na penginepo tutatumia riwaya za Mashia. Ni mategemeo yetu kuwa msomaji ataweza kukadiria usahihi na ukweli wa uchambuzi huu kwa makini.
Aisha anaripotiwa kusema: "Baba yangu alikuwa amezikusanya Hadith mia tano za Mtumes.a.w.w.
Asubuhi moja, alinijia na kusema,''Lete Hadith zote zilizopo kwako.' Nami nilizileta mbele yake. Yeye aliziunguza zote kwa moto na kusema: 'Nisije mimi nikafa huku nimekuachia vyote hivi.''
Imeripotiwa kwa mamlaka ya al-Zuhri kuwa: Umar alikuwa akitaka kuandika Sunan ya Mtumes.a.w.w.
Yeye alikuwa akilifikiria kwa muda wa mwezi mmoja, alitarajia mwongozo kutokea kwa Allah swt katika swala hili. Siku moja asubuhi, alichukua uamuzi na kubainisha: "Mimi niliwakumbuka watu wote wale waliokwisha nitangulia, ambao waliandika na wakawa wamevutiwa mno katika yale waliyokuwa wameyaandika na ambao hatimaye walikiacha kitabu cha allah (yaani Quran)."
Abd al-'Ala ansema: "Qasim ibn Muhammad ibn Bakr alizoea kutamka Hadith mbele yangu. alisema kuwa kulikuwapo na ongezeko katika Hadith katika zama za Umar. Naye Umar aliamrisha Ahadith zote zikusanywe, na zilipokusanywa, alizichoma moto zote kwa pamoja, akibainisha: Kama muthnat ya Ahl al-Kitab 'Mathnat' kama inavyoonekana kilikuwa ni kitabu ambacho Mayahudi walikiandika wao wenyewe na ambacho kilikuwa ni tofauti na Taurati. Hapa Umar alikilinganisha kitabu hicho pamoja na Hadith za Mtumes.a.w.w.
, ambavyo alikuwa hataki ziwepo pamoja na Kitabu cha Allah (yaani Quran). Yahya ibn Ju'dah naye pia ameripoti kuwa 'Umar alidhamiriwa kuandika hadith na Sunan. Lakini alibadilisha dhamira yake na kutuma ujumbe wake katika miji yote, ikibainisha:"Yeyote yule aliyenacho chochote kutokana na hayo, ayateketeze yote."
Imeripotiwa kutoka 'Urwah ibn al-Zubayr kuwa, "Umar ibn al-Khattaab alikuwa akitaka kuandika Sunan ya Mtumes.a.w.w.
Kuhusiana na swala hili, alishauriana na Sahaba wengineo. Sahaba wote waliafikiana kuwa Hadith zote ziandikwe.Lakini Umar alikuwa akizingatia swala hilo hadi ikafika asubuhi moja alipochukua uamuzi wake wa kughairi hivyo, na akasema, 'mimi nilitaka kuandika sunan. Lakini baadaye nilijikumbusha watu walionitangulia ambao waliandika vitabu na kukiacha kitabu cha Allah (yaani Quran). Kwa kiapo cha Allah swt mimi sitakifunika Kitabu cha Allah kwa kitu chochote kile." Riwaya hii inatuonyesha kuwa Sahaba wote au angalau wale waliokuwa wameshauriwa walikubali juu ya uandishi wa Hadith. Lakini Khalifa, baada ya kufikiri kwa muda wa mwezi mmoja hivi, aliharamisha uandikaji wa Hadith katika misingi aliyoelezea yeye mwenyewe, jambo ambalo, bila shaka, halikuwepo pamoja na Sunnah za Mtumes.a.w.w.
.
10. UPINZANI WA BAADHI YA SAHABA NA TABIUN KATIKA UANDISHI WAHADITH
Baada ya Khalifa kukataza uandishi wa Hadith, kwani mienendo yao ilichukuliwa na watu kama ni Sunnah, basi kikundi cha Sahaba na Tabiun pia walijiepusha na uandishi wa Hadith na walikuwa wakitegemea mno juu ya kile kimehifadhiwa akilini mwao.Wao walieneza Hadith kwa midomo tu na walichukia wazo la kuziandika. Kwao ilikuwa sivyo sahihi katika kuziandika Hadith za Mtumes.a.w.w
. ambapo Quran na Mtumes.a.w.w
. vyote vimeweka msisitizo mkubwa juu ya uandishi kwa ujumla. Abu Burdah anaripotiwa akisema kuwa baba yake alimwambia Abu Musa al-Ash'ari amletee chochote kile alichokuwa amekiandika kutokana na riwaya za baba yake.Na yote yalipoletwa, aliyaangamiza yote na alisema, "Wewe nae pia, kama sisi, lazima ukariri tu bila ya kuandika chochote." Abd al-Rahman ibn Salamah al-Jamhi anaripoti: "Mimi nilisikia Hadith ya Mtumes.a.w.w.
kutoka kwa Abd Allah ibn Amr na niliiandika. Na baada ya kuhifadhi (kuikariri) akilini mwangu, nilikiteketeza kile nilichokiandika."
Asim alisema: "Mimi nilitaka kumwachia Ibn Sirin kitabu, lakini yeye alikataa kukiweka, akisema kuwa yeye hakutaka kuwa na kitabu chochote karibu yake." Abu Nadhrah asema: "Mimi nilimwambia Abu Sa'id awe akituandikia sisi, yeye alijibu, 'mimi sitawaandikieni na mimi siwezi kuwafanyieni chochote kama Quran kwa ajili yenu. Wewe uichukue (Hadith) kutoka sisi vile tulivyopokea kutoka Mtumes.a.w.w.
' Abu Sa'id alizoea kusema, Simulieni Hadith miongoni mwenu, kwani mmoja wenu anamkumbusha mwingine vile kujali." Imeripotiwa kuwa mamlaka ya Ibn Abi Tamin kuwa Ibn Sirin na wenzake wasingeliziandika Hadith.
Al-Harawi anaandika kuwa Sahaba na Tabiun walikuwa hawaziandiki Hadith na walikuwa wakizihifadhi akilini mwao, isipokuwa kitabu cha Sadaqa. Al-Nuwawi anaandika: "Mwelekeo wote wa Sahabah ulikuwa juu ya jihad, harakati dhidi ya matamanio ya mwili, na vile vile juu ya ibadah. Kwa hivyo wao hawakuwa na muda wa kunakili na kuandika (!).
Kwa sababu kama hizo, Tabiun pia hawakuweza kuleta chochote kile kilichoandikwa (tasnif)." Abu Kathir al-Ghubri anamnakili Abu Hurayrah akiwa amesema:"Ahadith zisifichwe wala zisiandikwe." Abd Allah ibn Muslim anaripoti kuwa Sa'id ibn Jubayr alikuwa anachukizwa na uandishi. Vivyo hivyo, Ibrahim al-Nakhai alibainisha kuwa yeye kamwe alikuwa hajawahi kuandika chochote. Wakati alipoulizwa sababu ya kutoandika, yeye alijibu, "Wakati mtu anapoandika kitu chochote, basi huja kutegemea juu ya yale aliyoyaandika."
Habib ibn Abi Thabit anaripotiwa kusema: "Mimi sina kitabu chochote ulimwenguni kote, isipokuwa kwa ajili ya Hadith ambayo ni kwa ajili ya sanda yangu."
Al-Hassan ibn Abi al-Hassan wakati wa kifo chake alimwamrisha mfanyakazi wake aliwashe tanuru na kuvitupa vitabu vyote alivyokuwa navyo isipokuwa kimoja tu. Ibn Sirin alikuwa akisema: "Iwapo mimi nitahitaji kuandika kitabu basi nitaandika kitabu juu ya barua za Mtumes.a.w.w.
"
Yahya ibn Sa'id anasema: "Mimi niliwaona Wanzuonini katika hali ambayo wanapingana juu ya kunakili na kuandika." Suleyman ibn Harb anaripoti: "Yahya ibn Sa'id alitujia na alikuwa akisema Hadith. Mwanzoni mwenzi wetu walikuwa hawaziandiki Hadith alizokuwa akizisimulia, lakini baada ya muda kupita, wao walianza kuziandika."
Qasim ibn Muhammad ibn Abi Bakr alikuwa akimwambia Abd Allah ibn 'Ala asiwe akiandika Hadith. Sufyan ameripoti kuwa, pale alipoambiwa Amr ibn Dinar kuwa yeye alikuwa akiziandika Hadith za Amr, 'Amr alisimama na kusema, "Yeyote yule anayeziandika Hadith basi atoke hapa kwangu." Sufyan anasema kuwa kuanzia hapo hakuandika chochote kile alichokisikia kutoka Amr isipokuwa alikuwa akihifadhi tu.
Imeripotiwa kutoka Ibn Tawus kuwa baba yake alisema: "mtu mmoja alimwuliza Abd Allah ibn Abbass, swali ambalo lilimfurahisha mno. Huyo mtu alimwomba Ibn Abbass amwandikie jibu lake.Lakini Ibn Abbass alisema kuwa wao kamwe hawaandiki chochote kile kilicho cha 'ilim' Riwaya hii ipo katika mzozano pamoja na riwaya zinginezo zilizotangulia za Ibn Abbass.
Malik ibn Anas anaripoti kuwa Ibn Musayyab alipofariki, hakuacha hata kitabu kimoja. Vivyo hivyo ndivyo ulivyokuwa ukweli wa Qasim ibn Muhammad, Urwah ibn al-Zubayr na Ibn Shihab al-Zuhri. Mansur ibn Mu'tamir ameripotiwa akiwa amesema: "Mimi sijaandika chochote hadi leo." Na taarifa kama hiyo hiyo ipo imeripotiwa kutokaYunus ibn Ubayd. Imeripotiwa kuhusu Ibn Abi Dhu'ayb kuwa yeye alikuwa akikariri tu Hadith. Yeye alitokana na tabaka la tano na aliishi katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D. Imesemwa kuhusu Sa'id ibn Abd al-Aziz alikuwa haandiki chochote. Ismail ibn Ayyash, aliyetokana na tabaka la sita alikuwa amehifadhi akilini mwake kiasi cha Hadith elfu kumi lakini hakuandika hata moja. Abu Hatim anaripoti kuwa yeye kamwe hakuona chochote kilichoandikwa mikononi mwa Abd al-Walid al-Tayalisi. Wote hao walikuwamo katika tabaka la saba na walichukia mno uandishi wa Hadith. Pia imesemwa kuwa al-Nufayli kamwe hakuonekana pamoja na kitabu chochote. Vile vile Sahib al-Basri inasemekana alichukia mno uandikaji.
12. KITABU KINGINECHO MBALI NA QURAN
Kama itakavyoonekana kutokana na riwayah zinazotokana na wale wote waliokuwa wakizingatia kuharamishwa kwa Hadith kuandikwa, kwamba madai yao yote ya hasa kuficha ukweli yalikuwa ni khofu ya kutokezea kwa 'kitabu kinginecho mbali na Quran', na kwamba matokeo yake yatakuwa ni kutumika vitabu vingine na kuachwa kwa Quran. Hapa sisi tutajaribu kuchambua uhakika wa khofu kama hiyo na itaonekana wazi kuwa hayo yalikuwa ni hoja za kutaka kuuficha ukweli na wala hapakuwapo na makusudio mengineyo. Al-Quran na Sunnah vinakamilishana, na kama vile Waislamu wote wanavyoelewa kuwa kimoja hakikamiliki bila ya kingine - isipokuwa tu labda wale wenye kusema kuwa:"Kitabu cha Allah kinatutosha."
Jambo ambalo linahitaji kuzingatiwa hapa ni kuwa wale mabingwa wote wa kuharamisha uandishi wa Hadith iwapo wao walikuwa ni Makhalifa au wale waliofuata katika swala hili na waliweza kutumia hivyo kwa kuhalalisha tendo lao- walikuwa wakijua kauli ya Mtumes.a.w.w
. kuhusu "Kitabu ubavuni mwa Kitabu cha Allah swt." Hata hivyo kimakosa au kimakusudi wao waliitumia visivyo hivyo kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ni kweli kuwa katika zama za uhai wa Mtumes.a.w.w.
baadhi ya Sahaba waliweza kujipatia vitabu vya Taurati na vitabu vinginevyo vya Mayahudi. Na Mtumes.a.w.w.
alipokuja kupata habari kuhusu hayo, aliwaambia wasivilinganishe sambamba na Kitabu cha Al-lah, al-Quran. Katika uhusiano huu itatubidi kuzingatia riwaya ifuatayo iliyonakiliwa na Jaabir. Jaabir anaripoti kuwa Umar al-Khattab alileta nakala moja ya Tawrati mbele ya Mtumes.a.w.w.
na kusema: "Hii ni nakala ya Tawrati ambayo mimi huwa ninaisoma." Mtumes.a.w.w.
alikaa kimya lakini rangi ya uso wake ulibadilika. Abu Bakr aliiona hali hiyo, na alimwambia Umar, "Mama yako alie katika kilio chako, je, hauoni uso wa Mtumes.a.w.w
.! Umar alipouona uso wa Mtumes.a.w.w.
akasema, "Mimi najikinga na Mungu kwa ghadhabu za Mtumes.a.w.w.
Mimi namkubalia Allah kama mmiliki wa vyote, Islam kama Dini na Muhammad kama Mtume." Juu ya hayo Mtumes.a.w.w.
alisema:"Kwa kiapo cha Mungu, iwapo Musa angalitokea hapa na wewe umfuate yeye kwa kuniacha mimi, basi ungalikuwa umepotoka njia ya haki. Iwapo Musa angalikuwa hai na kuniona mimi, angalikuwa akinifuata mimi."
Mapokezi haya yanatuonyesha Mtumes.a.w.w.
alivyokuwa amekasirishwa kwa sababu Umar alikuwa amekichukulia kitabu kingine sambamba na Quran. Katika mapokezi mengine kama haya, mtu kutoka Ansaar anachukua nafasi ya Abu Bakr. Inawezekana kuwa mapokezi hayo mawili yanatuelezea matukio mawili tofauti na kwamba tunaweza kuelewa kuwa matukio hayo mawili yametokea katika nyakati mbalimbali. Imepokelewa kutoka Abu Qalabah kuwa mara moja Umar ibn al-Khattab alipita karibu na mtu aliyekuwa akisoma kitabu. Baada ya kumsikiliza kwa muda mfupi, Umar alipendezewa na kile alichokisikia. Basi alimwomba mtu yule amwandikie kutoka kitabu hicho. Mtu huyo alikubali kumwandikia hivyo. Hapo Umar alilinunua jani na kumletea huyo mtu, ambamo mtu yule aliandika kwa kujaza sehemu zote mbili.
Baadaye Umar alifika mbele ya Mtumes.a.w.w.
na kumsomea yaliyokuwa yameandikwa. Papo hapo rangi ya Mtumes.a.w.w.
ilibadilika kwa ghadhabu. Basi hapo mtu aliyetokana na Ansaar alimwambia Umar: "Mama yako alilie kilio chako! Je, hauoni uso wa Mtumes.a.w.w.
?
"Kwa hayo Mtumes.a.w.w.
alisema: "Mimi nimetokezea kama Mtume, kama mfunguzi (fatih) na kama mfungaji (khatim), na mimi nimeleta kila kitu ambacho ilinibidi kujanacho (hivyo hakuna kilichobakia hadi nyinyi) kwenda kuvitafuta kutoka kwa watu wengineo."
Imeripotiwa kwa mamlaka ya al-Zuhri kuwa Hafsah binti yake Umar, alikileta kitabu chenye Hadith (masimulizi za Mtume Yusuf
mbele ya Mtumes.a.w.w
. Yeye alianza kukisoma huku Mtumes.a.w.w
. akiwa akisikiliza na uso wake kubadilika rangi kuwa mwekundu. Hapo ndipo Mtumes.a.w.w
. aliposema, "kwa haki ya Mungu, iwapo Yusuf mwenyewe angalikuja hapa na iwapo wewe ungalimfuata yeye na kuniacha mimi basi wewe ungalikuwa umepotoka." Riwaya hizi zote zinatuonyesha kile alichokuwa akikichukia Mtumes.a.w.w.
kilikuwa ni maandishi mapotofu ambayo athari zake zilikuwa ni kueneza imani potofu za Mayahudi ambazo zilikuwa zikiitwa Israilayyat - miongoni mwa Waislamu. Mtumes.a.w.w.
alikuwa hataki vile vitabu vya Mayahudi viwe sambamba na Quran Tukufu, maneno yote ambayo yalikuwa ni maneno ya Allah swt; katika vitabu vya Mayahudi kulikuwamo na visa na Hadithi za uwongo na zenye imani za ushirikina na kuamini uchawi, vinaweza kumfanya mtu apotoke na njia iliyo na mafundisho halisi ya Quran ambayo yameelezwa mbele yao.
Riwaya zilizoelezwa hapo juu pia zinaonyesha kuwa Khalifa na binti yake walikuwa wakipendezewa mno na usomaji wa vitabu kama hivyo na mara nyingine ilitokea kuchunguzwa na Mtumes.a.w.w.
Hata hivyo, kwa bahati mbaya, tunaona kuwa baadaye ambapo Ka'aba al-Ahbar, Myahudi aliyesilimu kidhahiri tu, alipomwijia Umar na kumwomba ruhusa ya kuisoma Tawrati, Umar alimwambia: "Iwapo wewe unajua kuwa hiyo ndiyo Tawrati aliyokuwa ameteremshiwa Musa
. huko katika Milima ya Sinai, basi uisome usiku na mchana." Na haya ndiyo yaliyokuwa majibu ya Umar baada ya Mtumes.a.w.w.
kumkataza yeye mwenyewe kutoisoma Tawrati wala mambo yoyote kama hayo.
Zipo riwaya zingine ambazo zinathibitisha fikara zetu kuwa Mtumes.a.w.w
. alichokuwa akiharamisha kuwapo kwa kitabu sambamba na Quran yalikuwa ni maandiko ya Mayahudi yaliyokuwa yakitumiwa na Waislamu. Ipo imeripotiwa kuwa Abdallah ibn Mas'ud aliposikia kuwa watu walikuwanacho kitabu ambacho walistaajabishwa na yale yaliyokuwemo,basi alikichukua na kuki teketeza, akisema:"Watu wa vitabu (Ahl al-Kitaab) waliangamia kwa sababu wao walikuwa wakitegemea mno maandiko ya Wanazuoni wao (ulamaa) na walikuwa wamepuuzia Kitabu cha Allah (yaani Tawrati)" Neno ulamaa katika Waarabu wa zama hizo ilikuwa ikimaanisha Wanazuoni wa Kiyahudi na Kikiristo na vitabu vinavyozungumzwa katika riwaya hizi ni maandishi ya Kiyahudi.
Riwaya ifuatayo inaelezea vizuri zaidi swala hili. Murrah al-Hamdani anasema: Abu Murrah al-Kindi alikileta kitabu kutoka Syria (al-Shaam) na alimpatia Ibn Mas'ud alikipitia kitabu hicho, akaleta maji na kuyaosha yale maandishi yaliyokuwa yameandikwa katika kitabu hicho. Na hapo alisema, 'Watu walioishi kabla yenu waliangamia kwa sababu ya kuvifuata vitabu kama hivi na kukiacha cha Allah (yaani Quran)" Al-Husayn anasema, "Kwa hakika asingeteketeza maandishi hayo kama yangalikuwa ni Quran na Sunnah (yaani Hadith za Mtumes.a.w.w.
Bali kilikuwa ni kitabu cha Ahl al-Kitaab."
Imam Ali ibn Abi Talib
. ameripotiwa akisema:"Yeyote yule miongoni mwenu aliyenacho kitabu (mbali na Quran na Sunnah) akiteketeze.Watu waliowatangulia nyinyi waliangamizwa kwa sababu ya kufuata masimulizi ya Wanazuoni wao huku wakikiacha Kitabu cha Allah (yaani Quran)."
Al-Imam al-Sadiq
. ameripotiwa akisema: "Baadhi ya Wanazuoni wapo wanafuatilia riwaya za Mayahudi na Wakristo, huku wakitegemea kuongeza elimu yao. Watu kama hao, nafasi yao ipo chini mno ndani mwa Jahannam. Imeripotiwa kwa mamlaka ya amr ibn Yahya ibn Ju'dah kuwa kilipokuwa kimeletwa kitabu mbele ya Mtumes.a.w.w.
alisema: "Inatosheleza kwa upumbavu na upotofu wa Ummah kwa kuyaacha yale yaliyokuwa yameletwa na Mtume wake na kuanza kuangalia yaliyokuwa yameletwa na Mitume mingine." Riwaya hii pia inatuonyesha aina ya kila kitabu kilichokuwa kimeletwa mbele ya Mtumes.a.w.w.
na pia kutupia nuru juu ya maana ya: 'Kitabu sambamba na Kitabu cha Allah (yaani Quran).'
Vile vile Ibn Abbass anasema: "Je utawaulizaje swali Ahl al-Kitaab kuhusu matatizo wakati ambapo Al-Qur'an ipo miongoni mwetu ?" Riwaya na masimulizi na mapokezi yote haya yanaonyesha kuwa Mtumes.a.w.w.
aliharamisha kutayarishwa kwa kitabu sambamba na Quran huku akitahadharisha hatari ya uingiliaji wa Israiliyyat na kamwe, vyovyote vile, hakumaanisha Sunnah yake, ambayo ipo imeshikamana (wajib al-'ita'ah), kama vile wanavyokubalia Waislamu wote. Mabishano yetu yanazidi kupata nguvu kwa uhakika kuwa Wanazuoni wa Hadith wa Islam walikuja baadaye wakaziandika na kuzikusanya Hadith. Ama kwa mfano wa wale kama 'Urwah walichoma moto Hadith walizokuwa wameziandika kwa kudai kuwa "sisi hatutaki kuwanacho kitabu sambamba na Kitabu cha allah (al-Quran),' basi ni lazima tuseme kuwa wao walitenda kwa sababu ya kutoelewa vyema mafhumu ya kauli ya Mtumes.a.w.w.
Kama itakavyokuwa imeonekana hapo awali kuwa sisi hatuwezi kusema kuwa Mtumes.a.w.w.
ndiye aliyehusika na uharamishwaji huo wa kuziandika Hadith; na msimamo kama huo unaweza kuchomoza maswali ambayo hayana majibu. Ilieleweka hapo awali kuwa baadhi ya Makhalifa walihusika moja kwa moja katika swala hili la kutoziandika Hadith na wao ndio walioharamisha uandishi wa Hadith. Hapa, baada ya kutaja sababu zilizotolewa nao kwa kuchukuwa hatua kama hiyo, sisi tutajaribu kutafuta maelezo yake. Baada ya kuthamini sababu chache zilizotolewa nao katika swala hili, sisi tutajaribu kuelezea kile tunachokiona kuwa ndiyo sababu maalum kuhusiana na uharamishwaji huo, pamoja na uthibitisho wa kutosheleza katika kuugana na maelezo yetu.
13. SABABU ZILIZOTOLEWA KWA KUHARAMISHA UANDISHI WA HADITH ZA MTUME S.A.W.W.
1. Sababu ya kwanza iliyotolewa ni khofu ya watu kushindwa kutofautisha baina ya Quran na Hadith za Mtumes.a.w.w.
ambazo zingalisababisha uharibifu (tahrif) wa maandiko ya Quran, madhambi yasiyo samehewa. Mazungumzo haya, ambayo hayawezi kukubalika, yamekanushwa na Ustadh Abu Riyyah katika maneno yafuatayo: "Mtu kama huyo anaweza kuwashawishi watu wa kawaida, lakini haiwezi kukubalika kiutafiti. Kwa sababu itakuwa ikimaanisha kuwa ufasaha wa Quran unasimama sawasawa na ufasaha wa Hadith za Mtumes.a.w.w.
Kile anachokimaanisha hapa ni muujiza wa ufasaha wa Quran unavyo tambulikana miongoni mwa watu, hatuwezi kudai kuwa wao wangalikuwa chini ya upotofu kwa kuzichanganya aya za Quran kwa Hadith za Mtumes.a.w.w,
ambazo zipo chini kwa kulinganishwa na ufasaha wa Quran. Msimamo kama huu, kwa hakika unamfanya mtu akipingana na muujiza wa Quran.
Zaidi ya hayo, kuamini katika uwezekano wa kuchanganyika kwa Aya za Quran na Hadith ni sawa na kuamini katika uwezekano wa kuja kupotea kwa maandiko ya Quran. Imani kama hiyo inakanushwa kwa sababu uhalisi wa Quran upo unathibitishwa na Allah swt katika Quran: Sura Hijr, 15:9. Tunaweza kusema zaidi ya hayo kuwa kikundi cha Sahaba walikuwa wamehifadhi moyoni mwao Quran nzima, na kwa uangalifu mkubwa na upendo wao mkubwa juu ya Quran. Hatuwezi kamwe kuwafikiria kuwa wao walikuwa na hatari ya kuchanganyikiwa baina ya Quran na Hadith. Sisi twaweza kusema kuwa labda kulikuwapo na hatari ya uwezekano tu, na uwezekano huo hauwezi kupewa uzito sawa na madhara na hatari za kutoziandika Hadith. Madhara yaliyokuwa yameshajulikana kuanzia awali kabisa Shabaha hawakukubaliana miongoni mwao katika siku za awali kuhusu baadhi ya Shariah za Kiislamu na ilikuwa ni dhahiri kuwa athari za ufarakano huo ungelikuwa na hatari kubwa iwapo Hadith za Mtumes.a.w.w.
zingalikuwa hazikuandikwa. Lakini hatari hiyo ilitokea tu. Baina ya tishio la zamani na hatari fulani, iliwabidi wao walitilie mkazo swala la uandishi wa Hadith, ingawaje, kimsingi swala la kutoruhusu uandishi wa Hadith halikuwa na uzito wowote.
2. Maelezo ya pili yatolewayo na Abu Riyyah yanasema baada ya kukubalia uharamisho wa kuandika Hadith ulitokana na Mtumes.a.w.w.
kwamba Mtumes.a.w.w.
alitaka maamrisho ya Shariah yawe katika mipaka iliyodhibitiwa na alipinga kueneza zaidi kwa maamrisho ya Shariah (adillah). Haya, kwa mujibu wake, ni sababu ambayo pia inatokana na nyakati zinginezo ambapo Mtumes.a.w.w.
alichukia kuulizwa maswali. Sababu hiyo hiyo ipo inatumika katika hali ambapo Hadith ambazo zilikuwa sahihi katika kipindi fulani na ambapo haikuruhusiwa kufuata hapo baadaye.
Sisi tunachukulia maelezo hayo kuwa ni dhaifu mno, kwani haiwezekani kamwe kudai kuwa Mtumes.a.w.w.
alipinga kwa kuenea Hadith halali kisheria zikitumika kama misingi ya kanuni halali za shariah. Je, itawezekanaje kwetu sisi kukubaliana nayo wakati Quran na Hadith kwa pamoja zinawajibika kujibu mahitaji katika sura mbalimbali ya Shariah kwa ajili ya siku ya Kiyama na siku zote kutoa maongozi kwa mwanadamu? Pamoja na hayo, sisi tutaelezea tena kwa mara ya pili kuwa sisi hatuamini ya kwamba Mtumes.a.w.w.
alitoa amri ya kuharamisha uandishi wa Hadith.
3. Al-Awzai anatoa maelezo mengineyo, anaandika: "Sayansi ya Hadith ni tukufu pale inapoenezwa kwa mdomo tu, inawafanya watu wakumbushana daima Hadith. Lakini, pale inapoandikwa, nuru yake inafifia na pia huweza kufikia mikono ya watu wasiostahili kupatiwa." Sisi tunaweza kuonyesha kuwa ingawaje kuenezwa kwa Hadith kwa mdomo kuna faida ya kukumbusha watu yaliyomo ndani mwa Hadith, utumiaji wake kama halisi, na pekee, njia za kuzirekodi hizo zipo mashakani. Kwa hakika, faida kama hizo ziliambatana na madhara makubwa mno. Hata hivyo, hii ndiyo sababu mojawapo ambayo al-Awzai ameibuni, na ipo inashukiwa iwapo ikizingatiwa na wale waliokuwa wameharamisha uandishi wa Hadith.
4. Ibn Abd al-Birr, anaandika wakati wa kutoa maelezo kama hayo: Uandishi wa Hadith uliharamishwa ili watu wasitegemee mno yale yaliyoandikwa na wao, wakiepukana na huzihifadhi. Katika hali kama hiyo, desturi ya kuhifadhi moyoni Hadith ingalikuwa imepotea. Wazo kama hilo pia haliwezi kukubalika, kwa sababu madhara yaliyotokana na kushindwa kuziandika Hadith yalikuwa ni makubwa mno kwa kulinganishwa na faida iliyotokana na kupigwa marufuku kwa uandishi wa Hadith. Ustaarabu na utamaduni wa mwanadamu umekuwa ukilindwa kwa kupitia maandishi na wala si kwa kusema tu, ingawaje kuhifadhi Hadith kwenyewe ni tabia nzuri na yenye maana.
5. Sababu nyingine imetolewa pamoja na haya ni kwamba iwapo Hadith zingalikuwa zimeandikwa basi watu wangalikuwa wameiacha Quran huku wakizipatia Hadith umuhimu wote. Mazungumzo hayo pia hayawezi kuchukuliwa kuwa ni kinga, kwani jambo kama hilo linaweza kusemwa iwapo Hadith itakayomaanishwa itakuwa ni zile zisemwazo kwa mdomo tu, na Quran kwa upande wa pili. Ni kweli kabisa kuwa kupitia umuhimu wote Hadith ni upotofu ambao wale wafanyao hivyo waonywe na wachukue umuhimu kama huo katika Quran. Lakini uharamisho wa uandishi wa Hadith, umeleta uharibifu usioweza kutegemewa katika utamaduni wa Islam, kwa njia hiyo si ya kupatikana kwa matokeo sahihi.
6. Abjad al-'ulum anaandika: "Sahaba na Tabi'un, kwa sababu ya uhalisi wa imani yao na kuwapo kwao karibu na kipindi cha Mtumes.a.w.w
., na kutokuwapo kwa mabishano na uwezekano wa kuwaelekea watu waliotegemewa, hawakuwa na hitajio la kuziandika Hadith na shariah.Lakini vile Islam ilipoanza kuenea penginepo, wao walianza kuzikusanya na kuziandika Hadith, Fiqh na tafsiri ya Quran.' Kile anachokitaka kukisema huyu mwandishi siyo sababu ya kupinga kwa baadhi ya Sahaba kwa ajili ya uandishi wa Hadith, bali ni maelezo tu- nayo pia siyo sahihi- ni kwa nini Hadith hazikuandikwa; sababu yake halisi ilikuwa ni kupingwa kwa uandishi wa Hadith, na wala si kutohitajika kama vile anavyodai mwandishi huyo. Zaidi ya hayo, ueneaji wa Islam ulitokea katika miaka ya ishirini au zaidi ya miaka hamsini baada ya kifo cha Mtumes.a.w.w.
Uandishi na ukusanyaji wa Hadith ulicheleweshwa hadi kufikia nusu ya karne ya 2 A.H./8 A.D. mbali na nukta hizo mbili inaeleweka kuwa sifa hii ya kumzulia Mtumes.a.w.w.
ilianza katika maisha yake, na hatimaye iliweza kuongezeka kwa sababu ya kutokuwepo kwa Hadith zilizoandikwa. Pia ilikuwa ni wajibu wa Sahaba, ambao walitofautiana miongoni mwao katika mambo ya Shariah, kuzuia kukua kwa upotoshi na tofauti kwa kuanza kuziandika Hadith.
8. Sababu hasa ambayo ipo nyuma ya kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith, ambayo mimi ninaamini, imeelezwa na mwanachuo mashuhuri aitwaye Sayyid Jaafar Murtadha na imethibitishwa kwa ushahidi uliopo:- Kulikuwapo na madhehebu mawili miongoni mwa Mayahudi. Dhehebu moja waliamini katika uandishi wa Hadith, ambapo dhehebu la pili halikuafiki hivyo, waliamini katika kutoandika chochote kile isipokuwa Taurati peke yake. Kundi hili la pili liliitwa Qurra (wasomaji). Haya yapo yamedokezwa na Dhadha katika kitabu chake cha fikara za Dini ya Kiyahudi. Ka'aba al-Ahbar Myahudi aliyesilimu (katika zama za Umar) alitokana na kundi hilo la pili. Mara moja Umar alimwuliza swali kuhusu mashairi ya vitu avisemavyo kuhusu Waarabu, kuwa kikundi cha kizazi cha Ismail, walikuwa wamehimili Biblia katika nyoyo zao na walizungumza kwa busara.....Labda inawezekana kuwa Khalifa alilichukua wazo hilo (la kutoandika chochote kile isipokuwa Quran tu) kutoka kwa Ka'b al-Khalifa na vile vile alikuwa akiheshimiwa kwa ushauri wake.
Zaidi ya hayo, uharamisho juu ya uandishi wa Hadith ulikuwa ukienda vyema pamoja na Siasa za tawala, kwani waliweza kuyazima malalamiko dhidi yao na kuendelea kuimarisha utawala wao. Kwa hakika hatua kama hiyo inawezekana kuwa na matokeo ya upotezi wa sehemu ya Hadith izungumziayo juu ya haki za wapinzani na ustahiki na ambayo ilifaa kuletea nguvu sehemu walizokuwa wamezidhibiti. Mtunzi huyo, kama vile taarifa yake ionyeshavyo, anadhani zipo sababu mbalimbali zilizosababisha kuharamishwa kwa Hadith, moja na muhimu kabisa ni kushawishiwa kwa mawazo ya Ahl al-Kitab juu ya Khalifa wa pili, ambaye, inavyoonekana, alipenda kusoma vitabu vyao kuanzia wakati aliposilimu. Uthibisho unaothibitisha ushawishi huu ni riwaya ya Urwah ibn al-Zubayr, isemayo kuwa Khalifa alikuwa amenuia kukusanya 'sunan' na hata pia aliwasiliana na Sahaba wengineo juu ya mpango wake huo. Wao walikubaliana nalo, lakini alibadilisha mpango wake huo kwa kusema kuwa watu wa Ahl al- Kitaab waliviacha vitabu vitukufu na kuanza kuvifuata vile walivyokuwa wameviandika na hivyo yeye hakutaka kufuata kitakachotokea juu ya Quran kama hivyo ilivyokuwa imetokea.
Ni jambo la kuweza kutokea kuwa maelezo hayo ya Khalifa yaliletwa na Ka'b al-ahbar, aliyetokana na kikundi cha Qurra, ambaye alijiepusha na kuandika chochote kile mbali na Tawrati. Ka'b alikuwa na njama mbaya dhidi ya Islam; ingawaje Khalifa alikuwa hana nia kama hizo, naye, kwa bahati mbaya, alishindwa kuona kwa kupitia ulaghai wa Ka'b. Mabishano ya Umar dhidi ya uandishi wa Hadith yalirudiwa na wengineo. Abu Burdah anaripoti kutokea baba yake aliyesema: "Banu Israil waliandika vitabu na kukiacha Kitabu cha Allah." Hakam ibn Atiyyah anaripoti kutokea Muhammad (bila shaka, Muhammad ibn Sirin) kuwa alizoea kusema: "Imenukuliwa kuwa Banu Israil walipotoshwa kwa sababu ya vitabu walivyovirithi kutokea mababu zao."
Mwanachuoni mwingine anaandika: "Moja ya ushawishi mkubwa wa Mayahudi juu ya Waislamu ulikuwa ni kuepukana na desturi ya kuandika Hadith. Imeandikwa katika Talmud, "Nyinyi hamna haki ya kuandika mambo ambayo munayazungumzia tu. "Huwezi kupinga kuwa Waislamu hawaku shawishiwa na Ka'b al-ahbar katika swala hili, ingawaje wao waliileta mbele katika sura ya Hadith ya Mtumes.a.w.w.
Ushahid wake ni amri iliyotolewa na Khalifa baada ya kuzichoma Hadith alizokuwa amezikusanya: "Mathnat (au Mishnah) kama Mathnat ya Ahl al-Kitab." Maneno haya pia yanatuonyesha vile alivyokuwa ameshikamana pamoja na desturi za Mayahudi. Abu Ubayd katika Gharib al-Hadith, anaandika: "Mimi nilimwuliza mwanachuo wa Taurati na Injili kuhusu neno 'Mathnat.' Yeye alinijibu: "Mapadre wa Kiyahudi na waalimu wa Kiyahudi waliviandika baadhi ya vitabu baada ya Musa, mbali na vitabu vitukufu, na ambavyo wao waliviita kwa jina la 'Mathnat.'
Ni dhahiri kuwa Khalifa alikuwa akiufuata mfano wa Mayahudi ambao wao walikuwa katika kambi mbali na iliyoelezwa hapa. Abu Ubayd anaendelea kusema: Baada ya kupata maelezo hayo, mimi nimeelewa maana ya riwaya hii. Na hii ndiyo iliyokuwa sababu Abd Allah ibn Amr ibn al-As alikuwa akichukia kukichukua chochote kile kutokea kwa Ahl al-Kitaab, ingawaje yeye alikuwa na baadhi ya vitabu alivyovipata wakati wa kampeni ya Yarmuk (kutokea Makanisa ya Kiyahudi).
Abu 'Ubayd anaongezea: "Ni lazima, uharamisho (wa uandishi na usambazaji) haukuhusiana na Hadith na Sunnah za Mtumes.a.w.w.
, kwa sababu itawezekanaje kuharamisha uandishi wa Hadith wakati ambapo wengi wa Sahaba wenyewe walikuwa wakinakili Ahadith. Hii inatuonyesha waziwazi kuwa Umar aliharamisha uandishi wa Hadith za Mtumes.a.w.w.
na Sunnah zake kwa sababu yeye alichukulia msimamo kama ule wa maandishi yaliyokuwa yametolewa na waalimu wa Kiyahudi. Kwa hivyo, badala ya kuangalia na kuchunga kuenea kwa imani za Isra'iliyyat, yeye alikuwa ameshawishiwa nayo, ushawishi ambao ulisababisha katika kuangamizwa kwa Sunnah za Mtumes.a.w.w.
Vile vile ni lazima iongezwe kuwa Abd Allah ibn Amr mwenyewe alikuwa mmoja wa waenezaji wa 'Isra'iliyyatambaye kamwe alikuwa si mtu aliyechukiwa mbele yao. Ilikuwa ni kwa sababu ya elimu yake ya Tawrati kwamba watu walimwambia awaeleze tabia ya Mtume mmoja.
Kile kilichotokea, katika mtizamo wetu, ni hivi: "Hadith za Mtume s.a.w.w. kwa ujumla hazikuandikwa hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 1 A.H./7 A.D., ingawaje baadhi ya Sahaba walipendelea uandikaji wake na vile vile wengineo walikuwa na vibao vilivyokuwa vimeandikwa Hadith. Uandikaji wa hapa na pale ulianza kutokea katika karne ya 2 A.H. /8. A.D. , lakini ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ulianza kwa nguvu mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D., na hasa katika karne ya 3A.H./8 9 A.D. Ingawaje inawezekana kuwa wakusanyaji walikuwa na mkusanyiko usio na utaratibu (kwani walikuwa wakikusanya chochote kile walichokipata bila ya kufanyia utafiti juu ya usahihi wake au ni nani aliyeileza), ni dhahiri kuwa wingi wa Hadith walizozikusanya zilikuwa zimetokana na kutamkwa tu. Ushahidi uliopo ni kwamba uandishi mdogo kabisa-ambao hauwezi kulinganishwa na kazi kubwa ya ukusanyaji wa Hadith-zipo dalili kidogo kabisa zenye kuonyesha kuwa kulikuwepo na uandishi wa Hadith katika karne ya 2 A.H./88 A.D. Hivyo inaweza kusemwa kuwa Hadith hazikuwa zikiandikwa kwa kipindi kirefu na zilikuwa zikisemwa kwa midomo tu bila ya kuandikwa katika kipindi hicho.