NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?
SHUBUHATI ZINAZO HUSIANA NA ITIKADI YA MASHIA JUU IMAMU MAHDI (A.F)
Zimetolewa shubuha kadhaa kuhusiana na itikadi ya imamu Mahdi (a.f), hapa tutazitaja zile za muhimu zaidi na kuzitolea majibu kwa ufupi.
SHUBUHA YA KWANZA: kuhusu urefu wa umri wa Imamu Mahdi (a.f):
Shubuha hii inatokana na kauli ya Mashia isemayo kuwa Imamu Mahdi (a.f) alizaliwa mwaka 255h, kwa kuwa si kawaida ya mwanadamu kuishi zaidi ya miaka elfu moja. Kwa sababu hiyo, ndio maana kuendelea kuitikadia kubakia kwa Imamu Mahdi (a.f) kwa kipindi chote hiki kirefu, kumekuwa ni jambo linalotumiwa kuwahujumu na kuwashambulia mashia. Hata imefikia baadhi yao kusema:
“Haujafika wakati wa pango kumzaa - huyo mnaemwita kwa ujinga wenu, haujafika wakati? Hivyo basi mmeondokewa na akili; kwa kurefusha umri wa kuishi kwake”
.
MAJIBU YA SHUBUHA HII : yanabainika kwa mambo yafuatayo:
Jambo la kwanza: kubakia kwa Imamu Mahdi (a.f) muda wote huu ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, na uwezo wake unakishamili kila kinachowezekana, na jambo hili la Imamu kubakia muda mrefu kwa Mwenyezi Mungu linawezeka. Sio tu kuwa linawezekana, bali ukweli nikuwa limekwisha wezekana kama itakavyo kubainikia hivi karibuni. Hivyo, hakuna kiziwizi kinacho uzuia uwezo wa Mwenyezi Mungu kulishamili jambo hili, bali ilipaswa iwe hivyo; kwani uimamu upo kwake na sio kwa mwingine, kama tulivyo bainisha hilo huko nyuma.
Anasema Fakhru Dini Raazi: “Baadhi ya madaktari wanadai kwamba: umri wa mwandamu, hauwezi kuzidi miaka mia na ishirini”, lakini kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
(وَ لَقَدْ أَرْسَلْنا نُوحاً إِلى قَوْمِهِ فَلَبِثَ فيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلاَّ خَمْسينَ عاماً)
“Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka khamsini”
, inaashiria na kuthibitisha kinyume cha madai yao. Na akili pia inakubaliana na aya hiyo; kwani kama isingekuwa hivyo, isingeli wezekana nabii Nuhu
akaishi muda wote huo. Ama sababu inayoweza pelekea mwaadamu kuishi na kubakia muda mrefu, inaweza ikawa ni Mwenyezi Mungu wenyewe, au kitu ambacho kinarejea kwake; kwani Mwenyezi Mungu ni mwenyekubakia milele, hivyo athari yake inaweza kubakia kwa muda autakao mwenyewe. Hivyo basi, bila shaka suala la kubakia muda mrefu na kuishi sana ni lenye kuwezekana”.
Anaendelea kusema kuwa: “Acha tuseme kwamba: hakuna mgogoro baina yetu na wao; kwani wao wanasema kuwa: “Umri wa kawaida hauzidi miaka mia na ishirini”. Na sisi tunawambia kuwa: umri wa nabii Nuhu, haukuwa wa kawaida, bali ilikuwa ni tunu na zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu. Ama kuhusiana na umri wa kawaida, kwa Imani yetu hauwezi kudumu hata sekonde chache kama Mwenyezi Mungu hakutaka, achilia mbali miaka mia moja au zaidi”
.
Nami niseme kuwa: bila shaka urefu wa umri wa Imamu Mahdi (a.j), sio kama umri wa watu wengine, bali upo inje ya ada na kawaida ya watu, isipokuwa umepatiakana kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu aliyetukuka na kutakasika, kama yalivyotokea mambo mengine mengi yaliyokuwa nje ya ada katika uhai wa manabii na mawalii wa Mwenyezi Mungu waliotangulia. Mambo ambayo waislamu wote licha ya hitilafu zao za kimadhehebu, wameafikiana kwamba yalitokea, kwa mfano: urefu wa umri wa nabii Nuhu
, kubaki kwa watu wa pangoni (as’haabul-kahaf) miaka mia tatu na tisa hali yakuwa wamelala, kuzaliwa kwa nabii Issa
bila ya baba, alivyoongea akiwa bado mtoto mchanga, kuponya kwake vipofu na wenye vibarango, kuwafufua wafu…. na mengineyo mengi ambayo hatuwezi kuyataja yote hapa.
Hivyo basi, kwakuwa uimamu na uongozi umejifunga kwa Imamu Mahdi katika zama zetu hizi kama ulivyokwishatangulia ufafanuzi wa hilo huko nyuma, na watu wetu wengi walimuona bayana, (na imamu ni lazima awepo kila zama), ndio maana tunasema kuwa umri wake mtukufu unapaswa kurefuka.
Jambo la pili: Hakika Mwenyezi Mungu aliyetukuka na kutakasika, amerefusha umri wa kundi kubwa la watu walioishi katika nyumati zilizopita kama ilivyotangulia katika aya ya surat Al-ankabut, ambayo imeonyesha kwamba nabii Nuhu
aliishi na watu wake akiwalingania kumwabudu mola wao kwa muda wa miaka elfu kasoro miaka hamsini. Vilevile nabii Adamu
aliishi miaka elfu
, watu wapangoni (as’haabul-kahaf) walibikia pangoni miaka mia tatu na tisa, kama alivyoishi Salmaani Al-faarsi miaka zaidi ya mia mbili na hamsini kwa mujibu wa kauli zote
.
Jambo la tatu: Hakika waislamu wanaamini uwepo wa watu wema tofauti na Imamu Mahadi (Amani iwe juu yake) walioibakia na kuishi kwa muda mrefu, kama vile: nabii Issa mwana wa Mariam (amani iwe juu yake) na Khidri, nabii Idirisa na Iliyasa (Amani iwe juu yao) kwa mujibu wa baadhi ya kauli, kama ambavyo wanaitakidi kubakia muda mrefu baadhi ya watu wasio wema, kama vile Dajaal.
Ama kuhusiana na nabii Issa (Amani iwe juu yake): Aya za kitabu kitukufu cha Qur’an zinaonyesha kuwa alinyanyuliwa mbinguni. Anasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا .بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٥٨ ﴾
“Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Issa, mwana wa Mariamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsulubu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima”
.
Vilevile, hadithi zilizopokelewa katika vitabu sahihi vya hadithi, zinaonyesha kwamba nabii Issa (Amani iwe juu yake) atakuja kuteremka kutoka mbinguni katika zama za mwisho. Kama ilivyo hadithi ya Muslim katika sahihi yake, kutoka kwa Abu Huraira alisema: “Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
:
(والله لينزلنّ ابن مريم عدلاً حكماً، وليكسرنّ الصليب، و ليقتلنّ الخنزير،و ليضعنّ الجزية ...)
“Ninaapa kwa jina Allah kuwa, bila shaka mwana wa Mariam atateremka kutoka mbinguni ili aje kuwa mwamuzi mwadilifu (kati ya haki na batili), na kwamba atauvunja msalaba, atauwa nguruwe na kuweka kodi (kwa makafiri) ….”. Na kutoka kwa Abu Huraira pia, alisema: “Amesema mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
:
(كيف أنتم إذا نزل ابن مريم فيكم، و إمامكم منكم؟!)
“Vipi ninyi atakapokusha kwenu mwana wa Mariam hali ya kuwa imamu wenu yupo kati yenu?
!”.
Na wasomi wakubwa wa Ahli Sunna wamema waziwazi kuwa nabii Issa (Amani iwe juu yake) yuko hai na anaishi hadi wakati huu:
Anasema Ibni Hajar Al-asqaalani: “Hakika Issa
alinyanyuliwa mbinguni, na ukweli ni kuwa yeye yuko hai”.
Ibni Kathiir anasema: “kinachokusudiwa na mlolongo wa aya hizi, ni kuonyesha kuwa nabii Issa
yupo hai mbinguni mpaka sasa, na sio kama walivyodai manasara kuwa alimsulubiwa. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake. Kisha kama zinavyo bainisha hadithi zilizopokelewa kwa wingi, atashuka duniani kabla ya siku ya Kiyama”.
Anasema katika sehemu nyingine: “Hakika Mwenyezi Mungu alimnyanyua nabii Issa
kwake, anaishi na yupo hai, na kwamba atashuka duniani kabla ya siku ya Kiyama, kama zinavyo onyesha riwaya zilizopokelewa kwa wingi”.
Bwana Qurtubi nae anasema: “Ukweli ni kuwa Mwenyezi Mungu alimnyanyua nabii Issa (a.s) mbinguni bila yakuwa amefariki wala kuwa usingizini kama alivyosema Alhasan na Ibni Zaidi. Na rai hii ndio chaguo la Tabari na ndio rai sahihi kutoka kwa Ibni Abbasi, na Dhahaku nae pia anaiunga mkono rai hii”.
AMA KUHUSIANA NA KHIDRI: Rai mashuhuri ni kuwa yupo hai mpaka leo hii.
Anasema Nawawi: “Kundi kubwa la wasomi ni kuwa Khidri yuhai na yupo kati yetu. Katika jambo hili masufi na wana maarifa wameafikiana. Hikaya zao kuhusiana na kumuona Khidri, kukusanyika nae katika vikao, kujifunza kwake, kumuuliza maswali na kupata majibu kutoka kwake, kuwepo kwake maeneo matukufu na yakheri…, ni mengi sana kiasi kuwa hayawezi kuhesabika, na nimashuhuri kiasi kuwa hayawezi kufichika”.
Sheikh Abu Amru Ibni Swalaah anasema: “Khidri yuhai kwa mtazamo wa kundi kubwa la maulamaa na watu wema, na Ahli Sunna wapo na nao katika hilo”. Anaendelea kusema: “Kwa hakika baadhi ya wasomi wa elimu ya hadithi ndio walio jitenga kwa kulipinga jambo hilo”.
Anasema Qurtubi: “Sheikh wetu Imamu Abu Muhammad Abdul-mu’utwi Ibni Mahmud Ibni Al-mu’utwi Al- Lakhmi, katika kufafanua risala ya Al-qishiiri ametaja hikaya nyingi kutoka kwa watu wema, wake kwa waume kwamba: walimuona Khidri na kukutana nae, hikaya ambazo kwa ujumla ukikusanya na waliyo yataja Naqashi na Thaalabi, zinatupa dhana kuwa Khidri yupo hai”.
Ama kuhusiana na nabii Idirisa
: baadhi ya wasomi wamesema kuwa yupo hai na anaishi.
Imepokelewa kutoka kwa Mujahidi kuhusiana kauli yake Mwenyezi Mungu:
(وَ رَفَعْناهُ مَكاناً عَلِيًّا)
“Na tulimuinua daraja ya juu”
, kwamba alisema: “Nabii Idirisa
aliinuliwa (mbinguni) kama alivyoinuliwa nabii Issa
wala hajafariki”
.
Ama kuhusiana na nabii Iliyasa
: kwa mujibu wa baadhi ya kauli, yuhai wala hajafariki.
Ibni Asaakir amepokea kutoka kwa Ka’ab (Allah awe radhi naye) kwamba alisema: “Manabii wanne mpaka leo hii wako hai: wawili wapo aridhini: Iliyasa na Khidri
, na wawili wapo mbunguni: Issa na Idirisa
”
.
Vilevile, amepokea Hakimu Nisaabouri katika kitabu chake cha Mustadrak, kutoka kwa Anasi Ibini Maaliki (Allah awe radhi naye) kwamba alisema:
(كُنَّا مَعَ رسول الله صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سفر ، فنزلنا منزلًا ، فإذا رَجُل فِي الوادي ، يَقُولُ : اللَّهُمَّ اجعلني من أمة مُحَمَّد المرحومة المغفور لَهَا المتاب عليها قَالَ : فأشرفت عَلَى الوادي ، فإذا رَجُل طوله أكثر من ثلاث مائة ذراع ، فقال لي : من أنت ؟ قلت : أَنَا أنس بْن مالك خادم رسول الله صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : فأين هُوَ ؟ قلتُ : هُوَ ذا يسمعُ كلامك قَالَ : فأته ، وأقرئه مني السلام وقل لَهُ : أخوكَ إلياس يقرئك السلام فأتيتُ النَّبِيّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فأخبرته ، فجاء حتى لقيه فعانقه وسلم عَلَيْهِ ، ثُمَّ قعدا يتحدثان ، فقال : يا رسول الله إنّما آكل فِي السنة يومًا ، وهذا يوم فطري ، فآكل أَنَا وأنت فنزلت عليهما مائدة من السماء عليها خبز وحوت وكرفس فأكلا وأطعماني ، وصليا العصر ، ثُمَّ ودعته ، ثُمَّ رأيته مر عَلَى السحاب نحو السماء).
“(Siku moja) tulikuwa safarini na mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
, tukawa tumepumzika sehemu, mara akaonekana mtu bondeni alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu, nijalie niwe katika umma wa Muhammad(s.a.w.w)
wenyekurehemewa, wenyekusamehewa madhambi na wenyekulipwa kwa mema”, akasema Anasi Ibni Malik: “Nikaelekea bondeni, mara mtu yule urefu wake ni zaidi ya dhiraa mia tatu, akaniuliza: wewe ni nani? Akasema Anasi: “nikamjibu kuwa mimi ni Anasi bn Maliki mtumishi wa mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
. Akasema: “Yeye yuko wapi?” Anasi akasema: “Nikamwambia yule pale anayasikia mazungumzo yako”. Akasema: “Nenda kwake, umfikishie salaam kutoka kwangu na umwambie: “ndugu yako Iliyasa anakusalimia”. Nikamuendea mtume(s.a.w.w)
na hivyo kumsimulia. Mtume(s.a.w.w)
akaja na kukutana nae, akamkumbatia na kumsalimia, kisha wakakaa wakiwa wanazungumza. Nabii Iliyasa akamwambia mtume: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika mimi huwa ninakula mara moja mwaka, na leo ndio siku ya kula kwangu, naomba tule pamoja. Ikawatelemkia meza ya chakula kutoka mbingini, ikiwa na mkate, samaki na figili, wakala kwa pamoja na wakanikaribisha na mimi, tukaswali swala ya Al-asri pamoja kisha nikamuaga, kisha nikamuona akipita kwenye mawingu kuelekea mbinguni”.
Ibni Asaakir amepokea kutoka Hasani (Allah awe radhi naye) kuwa alisema:
“Nabii Iliyasa ni mwakilishi wa majangwa, ama nabii Khidir ni mwakilishi wa milima. Hakika walipewa umri mrefu hapa duniani mpaka wakati wa parapanda ya kwanza na huwa wanakutana katika msimu wa hija kila mwaka”.
Amesema Abdul- Aziiz Ibni Abu Rawaad:
(إن إلياس والخضر (ع) يصومان شهر رمضان في كل عام ببيت المقدس، يوافيان الموسم في كل عام. وذكر ابن أبي الدنيا أنهما يقولان عند افتراقهما عن الموسم: ما شاء الله ما شاء الله لا يسوق الخير إلا الله ...الخ)
“Hakika nabii Iliyasa na Khidri
kuwa wanafunga mwezi wa Ramadhani kila mwaka katika Baitul- Maqdas, kama ambavyo huwa wanaudiriki msimu wa hija kila mwaka. Na Ibni Abu Dunia ameandika kwamba, wawili hao pindi wanapotaka kuachana katika kila msimu huwa wakisema: “masha Allah masha Allah, hakuna aletae kheri isipokuwa Mwenyezi Mungu… nk”
.
Amesema Ibni Hajal Al-Asqaalani kuwa: Daar Qutni ameandika katika kitabu cha Al-Afraad kupitia kwa Atwai, kutoka kwa Ibni Abbas kwamba:
(يجتمع الخضر وإلياس كل عام في الموسم، فيحلق كل واحد منهما رأس صاحبه،ويفترقان عن هؤلاء الكلمات: بسم الله ما شاء الله)
“Nabii Iliyasa na nabii Khidri hukutana kila mwaka katika msimu wa hija, kisha kila mmoja wao humnyoa mwenzake, na kuwa wanaachana kwa kusema maneno haya: bismillah, masha Allah ”. Anasema pia: “Katika mlolongo wa mapokezi ya hadithi hii kuna mtu mwenye jina la Muhamad Ibni Ahmadi bin Zaidi…, na mtu huyu ni dhaifu”. Ibni Asaakir pia amepokea mfano wa hadithi hiyo iliyotajwa hivi punde, kupitia kwa Hishaam Ibni Khalidi kutoka kwa Alhasani Ibni Yahya kutoka kwa Ibni Abu Rawaad, akaongeza kipande kifuatacho:
(ويشربان من ماء زمزم شربة تكفيهما إلى قابل)
“Huwa wanakunywa katika maji ya Zamzam kiasi kinacho watosheleza mpaka mwaka unaofuata” , katika hadithi hii watu wawili au zaidi miongoni wa wapokezi hawakutajwa. Hivyo, hadithi kama hii hujulikana kwa jina la: (Mu’udhal) katika elimu ya hadithi. Vilevile, Ahmad ameitaja hadithi hii katika kitabu cha Az-Zuhdi kwa mapokezi ya Alhasani kutoka kwa Ibni Abu Rawaad, akaongeza kipande hiki:
(أنهما يصومان رمضان ببيت المقدس)
“Hakika wawili hao (Khidri na Iliyasa) huwa wanafunga Ramahani takika Baitul-maqdas”.
Ama kuhusiana na Dajaal: riwaya za Ahli Sunna zinaonyesha kuwa nae yuko hai tangu zama bwana mtume
mpaka leo hii. Ama Dajaal huyo ni nani? Kuna kauli mbili kuhusiana na hilo. Yakwanza inasema kuwa ni Ibni Sayyaad, na kauli ya pili inasema kuwa ni mtu mwingine ambae kafungwa kwa minyororo mpaka hapo wakati wa kutoka kwake utakapofika.
Ama kuhusiana na Ibni Sayyaad, wametaja habari na sifa nyingi za kushangaza na kustajabisha kuhusiana nae.
Amesema Nawawi katika Sharhu ya Muslim mlango wa (dhikri Ibni Sayyaad): “Mtu huyu, anaitwa ‘Ibni Sayyaad au Ibni Saaid’. Ameitwa kwa majina hayo mawili katika hizi hadithi, lakini jina lake ni Swaaf.
Wamesema wanazuoni: “Kisa cha Ibni Sayyaad kina utata na jambo lake linachanganya katika kujua kuwa yeye ndie yule Masihi Dajjaal mashuhuri au ni mtu mwingine?”. Lakini jambo lisilo na shaka ni kuwa yeye ni Dajjali miongoni mwa madajjaali.
Maulamaa wamesema: “Dhahiri ya hadithi, inaonyesha kuwa bwana Mtume(s.a.w.w)
hakushushiwa wahai kuwa Ibni Sayyaad ndie Masihi Dajaal peke yake na kwamba hakuna mwengine, bali alichofunuliwa ni sifa za Dajaal, na Ibni Sayyaad alikuwa na dalili na sifa zinazo shabihiyana na sifa zile. Ndio maana bwana Mtume(s.a.w.w)
hakuwa akihukumu moja kwa moja kuwa Ibni Sayyaad ndie Dajjaali pekee na hakuna mwingine. Kwa sababu hiyo, ndio maana mtume(s.a.w.w)
alimwambia Omar (Allah awe radhi naye): “Kama Ibni Sayyaad atakuwa ndie Dajjaali, kamwe hautaweza kumuuwa”. Ama hoja ya kuwa Ibni Sayyaad ni mwislamu na Dajjaali ni kafiri, na kwamba Dajjaali hatakuwa na mtoto lakini Ibni Sayyaad ana mtoto, au kwamba Dajjaali hataingia Makka na Madina lakini Ibni Sayyaad aliwahi kuingia Madina hali yakuwa akielekea Makka, yote hayo hayana ushahidi kwa Ibni Sayyaad; kwa sababu Mtume
alielezea sifa za Dajjaali wakati atakapo dhihiri duniani na kuanzisha fitina zake.
Miongioni mwa utata wa kisa cha Ibni Sayyaad na kwamba yeye ni mmoja wa madajjaali waongo, ni kauli yake kumwambia mtume(s.a.w.w)
: "Je unashuhudia kuwa mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu?", vilevile madai yake kwamba huwa anajiwa na (malaika) mkweli na muongo, na kwamba yeye anaiona Arshi ya Mwenyezi Mungu juu ya maji, na kuwa hachukizwi wala kuona tatizo iwapo yeye ndie atakuwa Dajjaali, kama ambavyo amedai kujua mahala alipo Dajjaali katika kauli yake: "Kwa hakika mimi ninamjua Dajjaali, ninajua mahala alipozaliwa na yupo wapi", na kuvimba kwake mpaka akajaa njia nzima.
Ama kwamba alidhihirisha uislaamu, akafanya hija na kupigana jihadi, na kwamba aliachana na yote aliyokuwa nayo hapo kabla, yote hayo hayako wazi katika kuthibitisha kuwa yeye sio Dajjaali.
Anasema Alkhatwabi: "Masalafi (maswahaba) wametofautina katika suala la Ibni Sayyaad kipindi cha ukubwa wake. Imepokelewa kuhusiana na yeye kwamba: alitubia kutokana kauli yake ya kudai utume... na kwamba alifia Madina. Na pindi walipotaka kuliswalia jeneza lake, waliufunua uso wake ili watu wamuone. Wakaambiwa: "Shuhudieni".
Anaendelea kusema: "Miongini mwa yaliyopokelewa kutoka kwa Ibni Omar na Jaabir nikuwa, walikuwa wakiapa kuwa Ibni Sayyaad ndio Dajjaali, wala hawakuwa wakilishakia hilo". (Siku moja) Jaabir aliambiwa: "Hakika Ibni Sayyaad alisilimu". Jaabir akasema: "Hata kama alisilimu". Akaambiwa tena kwamba: "Hakika Ibni Sayyaad aliingia Makka na Madina". Akajibu kwa kusema: " Hata kama".
Abu Daud katika kitabu chake cha Sunan Ibni Daud, amepokea kwa mapokezi yaliyo sahihi kutoka kwa Jaabir kuwa alisema: "Tulimpoteza (alikufa) Ibni Sayyaad siku ya Hurrah". Hadithi hii inaibatilisha riwaya ya wale waliopokea kuwa Ibni Sayyaad alifia Madina na akaswaliwa huko.
Miongoni wa hadithi hizi, Muslim amepokea kwamba: Jaabir Ibni Abdallah aliapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba: Ibni Sayyaad ndie Dajjaali, na kwamba alimsikia Omar (Allah awe radhi naye) akiapa kuhusiana na jambo hilo hilo mbele ya Mtume(s.a.w.w)
, nae mtume(s.a.w.w)
hakulikanusha hilo.
Abu Daud amepokea kwa mapokezi sahihi kutoka kwa Ibni Omar kwamba alikuwa akisema: "Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa, sina shaka kwamba, Ibni Sayyaad ndie Masihi Dajjaali. Anasema Bayhaqi katika kitabu chake cha 'Alba'ath wa Nushour': "Watu wamehitafiana sana kuhusiana na suala la Ibni Sayyaad na kuwa je yeye ndie Dajjaali au la?". Anaesma: “Anaesema kuwa Dajjali ni mwingine na sio Ibni Sayyaad, alitumia hadithi aliyotajwa na Tamiimi Daari kuhusiana na kisa cha ‘Jassaasah’ kama hoja”.
Nami niseme kuwa: Ikhtilafu ya Ahli Sunna mpaka zama za hivi karibuni kuhusiana na kuwa Ibni Sayyaad ndie Dajjaali au la, inaonyesha kuwa ikiwa atakuwa ndie Dajjaali wa kweli, basi wakati huo saula la urefu wa umri wake halitakuwa na mushkeli wowote kwao.
Ama kuhusiana na hadithi ya Jassaasah, Ahli sunna wameiandika katika vitabu vyao. Hadithi hiyo inaonyesha kwamba Dajjaali alikuwa tangu wakati wa bwana mtume(s.a.w.w)
, na kwamba alikuwa amefungwa kwa minyororo akisubiri wakati wa kutoka. Ameandika Muslim katika kitabu chake kuwa, mtume(s.a.w.w)
alisema:
(إني والله ما جمعتُكم لرغبة ولا لرهبة، ولكن جمعتكم لأن تميماً الداري كان رجلاً نصرانياً، فجاء فبايع وأسلم، وحدثني حديثاً وافق الذي كنت أحدثكم عن مسيح الدجَّال، حدثني أنه ركب في سفينة بحرية مع ثلاثين رجلاً من لخم وجذام، فلعب بهم الموج شهراً في البحر، ثم أَرْفَأوا إلى جزيرة في البحر حتى مغرب الشمس، فجلسوا في أَقرُب السفينة، فدخلوا الجزيرة، فلقيتْهم دابة أهلب كثير الشعر، لا يدرون ما قُبُلُه من دُبُره من كثرة الشعر، فقالوا: ويلكِ ما أنت؟ فقالت: أنا الجسَّاسة. قالوا: وما الجسَّاسة؟ قالت: أيها القوم انطلقوا إلى هذا الرجل في الدَّيْر، فإنه إلى خبركم بالأشواق. قال: لما سمَّتْ لنا رجلاً فَرِقْنا منها أن تكون شيطانة، قال: فانطلقنا سراعاً حتى دخلنا الدَّيْر، فإذا فيه أعظم إنسان رأيناه قط خَلْقاً وأشده وِثَاقاً، مجموعةٌ يداه إلى عنقه ما بين ركبتيه إلى كعبيه بالحديد، قلنا: ويلك ما أنت؟ قال: قد قدرتم على خبري، فأخبروني ما أنتم؟ قالوا: نحن أناس من العرب، ركبنا في سفينة بحرية، فصادفنا البحر حين اغتلم، فلعب بنا الموج شهراً، ثم أرفأنا إلى جزيرتك هذه، فجلسنا في أقْرُبها فدخلنا الجزيرة... فقال: أخبروني عن نخل بَيْسان. قلنا : عن أي شأنها تستخبر؟ قال: أسألكم عن نخلها هل يثمر؟ قلنا له: نعم. قال: أما إنه يوشك أن لا تثمر. قال: أخبروني عن بحيرة الطبرية. قلنا: عن أي شأنها تستخبر؟ قال: هل فيها ماء؟ قالوا: هي كثيرة الماء. قال: أما إن ماءها يوشك أن يذهب. قال: أخبروني عن عين زُغَر. قالوا: عن أي شأنها تستخبر؟ قال: هل في العين ماء؟ وهل يزرع أهلها بماء العين؟ قلنا له : نعم هي كثيرة الماء، وأهلها يزرعون من مائها. قال: أخبروني عن نبي الأميين، ما فعل ؟ قالوا: قد خرج من مكة ونزل يثرب. قال: أَقاتَله العرب؟ قلنا: نعم. قال: كيف صنع بهم؟ فأخبرناه أنه قد ظهر على من يليه من العرب وأطاعوه. قال لهم: قد كان ذلك؟ قلنا: نعم. قال: أما إن ذاك خير لهم أن يطيعوه، وإني مخبركم عني، إني أنا المسيح، وإني أوشك أن يؤذَن لي في الخروج فأخرج، فأسير في الأرض، فلا أدع قرية إلا هبطتها في أربعين ليلة، غير مكة وطَيْبة، فهما محرَّمتان عليَّ كلتاهما، كلما أردتُ أن أدخل واحدة أو واحداً منهما استقبلني مَلَك بيده السيف صَلْتاً يصدّني عنها، وإن على كل نَقْب منها ملائكة يحرسونها
قالت: قال رسول الله ( ص ) وطعن بمخصرته في المنبر: هذه طَيْبَةُ، هذه طَيْبَةُ، هذه طَيْبَةُ ـ يعني المدينة ـ ألا هل كنت حدَّثتكم ذلك؟ فقال الناس: نعم. فإنه أعجبني حديث تميم أنه وافق الذي كنت أحدِّثكم عنه وعن المدينة ومكة، ألا إنه في بحر الشام أو بحر اليمن، لا بل من قِبَل المشرق ما هو، من قبل المشرق ما هو، من قبل المشرق ما هو. وأومأ بيده إلى المشرق)
“Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba, Mimi sijakukusanyeni hapa ili nikuhimizeni wala nikuhofisheni juu jambo, isipokuwa nimekuiteni nikusimulieni kwamba: Hakika Tamiimi Daari aliekuwa mnaswara, amekuja kwangu na ametoa kiapo cha utii na hatimae akalisilimu. Na amenihadithia kisa kinachoafikiana na niliyokuwa nikikuelezeni kuhusiana na Masihi Dajjaali. Amesema kuwa: Yeye pamoja na watu thelathini wa makabila ya Lakhm na Judhaam walipanda merikebu, mawimbi yakawazungusha baharini kwa muda wa mwezi mzima, mpaka walipofikia kisiwa wakati wa magharibi, wakakaa ukingoni mwa merikebu (au juu ya ngalawa ya kushushia watu). Hatiame wakaingia kisiwani, mara wakamkuta kiumbe mwenye nywele nyingi sana, kutokana na wingi wa nywele hakujulika wapi ni mbele na wapi ni nyuma. Wakasema: "Ole wako! wewe ni nani?". Akasema: "Mimi ni Jassaasah". Wakauliza: "Jassaasah ndio nini?". Akasema: "Enyi watu, nendeni kwa huyu mtu kijijini Dairi, hakika ana shauku kubwa ya kujua habari zenu". Akasema: "Kiumbe yule alipotutajia jina lake tukahofia asije kuwa shetani". Anaendelea kusema: "Tukaondoka haraka mpaka tulipowasili kijijini Dairi, na hapo tukamuona mtu mkubwa hatukupata kuona mfano wake kimaumbile. Mikono yake imefungwa shingoni pake, na amefungwa kwa vyuma kuanzia magotini mpaka visigino vya miguu yake."
Tukamuambia: "Ole wako, wewe ni nani?"
Akasema: "Mumekwishazijua habari zangu, niambieni ninyi ni akina nani?". Wakasema : "Sisi ni watu katika waarabu, tulisafiri kwa merikebu na ikasadifu bahari kuchafuka. Mawimbi yakatuzungusha kwa muda wa mwezi kisha tukateremka katika kisiwa chako hiki. Akasema "Nipeni habari za mitende ya Bisaan". Tukamuuliza : "Nini unataka tukuelezee kuhusu mitende hiyo? Akajibu kwa kusema : "Ninakuulizeni kuhusu mitende ya eneo hilo kuwa je bado inatoa matunda?" Tukamwambia: "Ndio". Akasema : "Muda sio mrefu haitatoa matunda". Akasema: "Nielezeni kuhusu ziwa la Genesareti au bahari ya Galilaya". Tukamuuliza: "Unauliza nini kuhusiana na ziwa hilo? Akasema: "Je lina maji?" Wakasema: "Ndio, maji mengi". Akasema: "hakika hivi karibuni maji yake yatatoweka". Akasema: "Nielezeni kuhusu chemchemi za Zughar". Tukamuuliza: "Ni nini waulizia kuhusu chemchemi hizo?" Akasema: "Je chemchemi bado zina maji? na Je watu wa eneo hilo wanayatumia kwa kilimo?". Tukamjibu: "Ndio, zina maji mengi, na watu wake wanalima kwa kutumia maji yake". Akasema: “Nipeni habari kuhusiana na nabii wa wasiojua kusoma wala kuandika (warabu), amefanya nini? Wakasema: "Kahama kutoka Makka amefikia Madina". Akuuliza: "Je warabu walimpiga vita?" Tukasema: "Ndio". Akahoji tena kuwa: "Amewafanya nini?" Tukamjulisha kuwa: "Amehamia kwa warabu mengine wanao muunga mkono na kumtii". Akasema: "Na nikweli wamefanya hivyo?". Tukasema: "Ndio". Akasema: "Hakika ni bora kumti. Na sasa ninakupeni habari zangu. Mimi ndie Masihi (Dajjaali), na hivi karibuni nitapewa idhini ya kutoka na nitatoka na kutembea aridhini, na wala sitoacha kijiji ila lazima nikipitie ndani ya muda wa siku arubaini, isipokuwa Makka na Twiibah (Madina), hakika miji hii miwili ni haramu kwangu kuingia ndani yake. Kila nitakapotaka kuingia katika mojawapo wa miji hiyo, atanikabili malaika mikononi mwake akiwa na upanga ulionolewa akinizuwia. Hakika katika kila upande yupo malaika mwenye kulinda miji hiyo”.
Akasema Fatimah Binti Qaysi: "Akasema mjumbe wa Mwenyezi Mungu huku akigonga kwa fimbo yake katika mimbari: "Hii ndio Twiibah, Hii ndio Twiibah, Hii ndio Twiibah (akimanisha Madina)". Mtume(s.a.w.w)
akasema: "Je sikuwa nikikuelezeni haya?". Hapo watu wakasema: "Ndio". Akasema(s.a.w.w)
: "Kwa hakika nimenifurahishwa na kisa cha Tamiim kwa kuwa kimeafikiana na niliyokuwa nikiwaambieni juu ya Makka na Madina. Alaa! Kwa hakika Dajjaali atatokea katika bahari ya Syiria au bahari ya Yemeni, hapana, bali atatokea upande wa Mashariki. Hakika niupande wa Mashariki. Hakika ni upande wa Mashariki”. Akaashiria kwa mkono wake upande wa Mashariki"
Amesema Qurtubi baada ya kutaja hadithi iliyopokelewa kutoka kwa mtume(s.a.w.w)
kuwa, alisema(s.a.w.w)
:
(أُقسم بالله ما على الأرض من نَفْس منفوسة تأتي عليها مائة سنة).
"Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa, hakutakuwa na nafsi inayopumua juu ya mgongo wa Ardhi itakayoishi miaka mia moja": Maulamaa wetu wanasema kuwa: tija inayotolewa na hadithi ni kuwa, bwana mtume(s.aw.w)
kabla ya mwezi mmoja kufariki alitoa bishara kuwa, mwanadamu yeyote atakaekuwepo kipindi hicho (cha kudhihiri kwa Dajjaali), umri wake hauatazidi miaka mia moja, kwa sababu kauli ya mtume(s.a.w.w)
inasema: “hakuna nafsi yenyekupumua”. Kwa upande mwingine ibara hii haiwahusu malaika wala majini; kwani haijathibiti kuwa wao wana sifa hiyo. Vilevile ibara hiyo, haimshamili kiumbe alisiekuwa na akili; kwa kuwa kauli aliyoitaja mtume(s.a.w.w)
: "wala yeyote miongoni mwa ambao wapo katika mgongo wa Ardhi", kwa kawaida huambiwa ambae ana akili. Hivyo basi, inabainika kuwa anaekusudiwa ni mwandamu, bali hata Ibni Omar nae aliibanisha maana hii pale aliposema: "Anachokilenga kwa kusema vile, ni kuwa karne hiyo itakwisha".
Vilevile, mwenyekushikilia hadithi ili kubatilisha kauli ya anaesema kuwa: "Khidri yuhai" hana hoja; kwani kauli ya mtume: "hakuna nafsi yenye kupumua", ina maana pana. Na zaidi ya hapo, upana huu hata kama unatilia mkazo kuvishamili vitu vyote, lakini haina maana kuwa kila kitu lazima kiingie ndani yake, bali kuna uwezekano wa kuuhadidi na kuufanya kuwa unavihusu baadhi ya vitu na vyote.
Vilevile maneno ya mtume, hayamshamili nabii Issa
, kwani yeye kwa mujibu wa aya ya Qur'an, hajafariki wala hajauwawa, kama ambavyo hayamuhusu Dajjaali, licha ya kuwa yupo hai kwa ushahidi wa hadithi ya Jassaasah. Vilevile, maneno hayo hayamshamili Khidri
hata kama haonwi na watu, hashirikiani nao wala hata hawamuwazii katika mazungumzo yao. Hivyo, mfano wa upana huu nae pia haumshamili
.
Ikiwa hayo yameeleweka, tunasema: kama ambavyo dalili madhubuti imeonyesha kubakia hai kwa nabii Issa na Khidri
, na ikaonyesha kubakia hai Dajjaali kwa muda mrefu zaidi ya umri wa kawaida, hivyo hivyo, ndivyo dalili madhubuti ambazo ufafanuzi wake ulishatangulia hapo kabla, zinavyo onyesha uwepo wa Imamu Mahdi (a.f), na kwamba yuko hai mpaka leo hii. Hivyo, habana budi kuukubali uwepo wake na kukiri kwa hilo.
Kubakia hai Imamu Mahdi (a.f) kwa umri mrefu, hakuna maana ya kuzitupilia mbali dalili sahihi zinazothibitisha uwepo wake, uhai wake na uimamu wake, kama ambavyo hazikutupiliwa mbali dalili zinazothibitisha kubakia hai nabii Issa na Khidri
kwa sababu ya umri wao kuwa mrefu.
SHUBUHA YA PILI
Je kuna faida gani kuwa na Imamu alie ughaibuni na aliefichikana machoni mwa watu? Imamu ambae hawanufaiki wala kufaidika nae waislaam na waumini, licha ya kuwa na haja nae sana, na hasa pale wanapo kumbwa na matatizo au wanapopatwa na majanga?!
MAJIBU YA SHUBUHA
1. Haya ni majibu aliyoyatoa Sayyidi Murtadhaa (Allah aliinue daraja lake) kuwa, ikwa tumetambua kuwa Mahdi (a.f) ndie Imamu za zama hizi na simwingine, na sasa ameingia ughaibuni hatumuoni kwa macho, tunajua kuwa bila shaka kwakuwa yeye ni maasumu na amehifadhika na mathabi, hawezi kuingia ughaibuni isipokuwa kwa sababu iliyomlazimu kufanya hivyo, na kwa masilahi au madhara yaliyompelekea kufanya hivyo, hata kama sisi tunaweza kushishindwa kujua ufafanuzi wa hilo kwa mapana, bali hatuna ulazima wa kujua ufafanuzi wa hayo. Na kwa njia hii, mazungumzo yetu kuhusiana na ghaiba yake yatakuwa mfano wa kuzungumzia masilahi yaliyopo katika kutupa mawe huko Minaa na kufanya twawafu na mfano wa hayo; kwani ikiwa tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu alietakasika ni mwenye hekima, bila shaka hakutakosa sababu nzuri katika yote hayo, hata kama sisi hatutaijua. Kwa majibu haya, tunakuwa tumefunga mlango wa maswali ya wapinzani wetu, isipokuwa tunabaki tunajitolea kutoa majibu ya baadhi ya maswali ili kuonyesha uwezo
.
2. Nasi tunawarejeshea mfano wa shubuha waliyoileta, nayo nikuhusiana na Issa mwana wa Mariam
, kwani nae yupo ughaibuni mbinguni, bali tunaweza kusema kuwa, kunufaika na Imamu Mahdi
ambae yuko ughaibuni ardhini kunafikirika zaidi kuliko kwa nabii Issa
ambae yuko ughaibuni mbinguni.
Na hata kama tutasalimu amri kwamba Imamu Mahdi katika ughaibu wake hatuna faida nae, bado hilo halina tatizo; kwakuwa manufaa yake yaliyohifadhiwa ambayo ni kuijaza ardhi usawa na uadilifu, yana uhakika. Kama ambavyo hakuna tatizo kutonufaika na nabii Issa
kwa sasa; kwakuwa manufaa yake yana uhakika katika zama za mwisho.
3. Hakika watu wananufaika na Imamu
hata kama yuko ughaibuni. Ughaibu wake hauziwii kuwa na manufaa muhimu, maadamu hayafungamani na kubainisha hukumu za kisheria, kwa mfano: kuwalinda na kuwakinga watu na adhabu (kuwaondolea watu adhabu); kwa sababu Imamu
ni katika ahlul-baiti wa bwana mtume(s.a.w.w)
ambao ni amani (kinga/ngao) ya adhabu kwa watu wa ardhini kama ilivyopokelewa katika hadithi ya Jaabir Al-answaari (Allah awe radhi nae) kutoka kwa mtume(s.a.w.w)
alisema:
(النجوم أمان لأهل السماء، فإذا ذهبتْ أتاها ما يوعدون، وأنا أمان لأصحابي ما كنتُ، فإذا ذهبتُ أتاهم ما يوعدون، وأهل بيتي أمان لأمتي، فإذا ذهب أهل بيتي أتاهم ما يوعدون).
"Nyota ni kinga na ngao kwa waishio mbingini, zinapotoweka huwafika waliyokuwa wakiahidiwa, na mimi ni kinga kwa maswahaba wangu maadamu nipo, nitakapotoweka yatawafika waliyoahidiwa, na watu wa nyumba yangu (ahalul-baiti zangu) ni kinga kwa umma wangu, watakapotoweka yatawafika waliyo ahidiwa"
.
Pamoja na kuwa nyadhifa za Imamu katika kipindi cha ughaibu hatuzijui wala kuzielewa zote, lakini mashia wengi waliopata majanga, matatizo na mabalaa Imamu alikutana nao na aliwaokoa kutokana na matatizo yao akawasaidia katika shida zako.
Mimi nashindwa kuelewa kuwa, wapinzani wamepata wapi uhakika huu kuwa, hakuna mwislamu anaeweza kuonana na Imamu
au eti hakuna muumini anaeweza kunufaika nae? wakati jambo hili hawana elimu nalo, wala hawana njia ya kuwa na uhakika nalo? na hasa ukizingatia kuwa, Imamu
aliwahofia wao hao hao na akajiziwia nao, akaingia ughaibuni na kuchificha kwa sababu yao? Ni jambo lisiloingia alikini kwamba Imamu awadhihirikie au akutane nao wamjue au wazijue sifa zake.
4.Imamu
hakuingia mafichoni, bali sisi ndio hatuijui khashsia yake wala hatuwezi kumtofautisha na wengine. Imepokelewa kutoka kwa Abdallah Ibni Mas'uud (Allah awe radhi nae) katika habari za kudhihiri kwa Imamu
kwamba, makabila baadhi yatawavamia wenzao, watapigana na mahujaji wataporwa mizigo yao, damu zitachirizika mpaka kwenye Jamratul-Aqabah. Watajitokeza watu saba wasomi kutokea maeneo mbalimbali bila yakuwa wameahidiana kukutana. Kila mmoja miongoni mwao atakuwa ameshachukua kiapo cha utii kwa watu mia tatu kumi na kidogo. Watakusanyika ndani ya Makka. Baadhi yao watawauliza wenzao: Nini kumekuleteni hapa? Watasema: Tumekuja kumtafuta huyu mtu ambae fitina itakwisha kupitia kwake, na mji wa Constantinopla (ambao ulikuwa ni mji mkuu wa Roma) utafunguliwa kupitia kwake, tulimjua kwa jina lake, kwa jina la baba yake na kwa jina la mama yake. ...Wote saba wataafikiana kufanya hivyo, kisha watamtafuta ndani ya Makka, watamwambia: Je wewe ndio fulani Ibni fulani? Atawajibu: Hapana, bali mimi ni mtu miongoni mwa maaswaari. Mara atawatoka. Kisha watatoa wasifu wake kwa wenyekumjua na kumtambua. Atasema: Huyo ndie mtu wenu mnaemtafuta, hakika ameelekea Madina. Watamtafuta Madina, kisha yeye atarudi zake Makka... Hali itaendelea hivyo hivyo mpaka mara tatu... Kwa mara ya tatu, ndio wale watu saba watakuja kumpata ndani ya Makka akiwa kwenye Rukuni, watamwambia: “Madhabi yatakuwa juu yako na damu zetu ziko juu yako kama hautaunyosha mkono wako tukakupa kiapo cha utii... Imamu akakaa kati ya Rukni na Maqamu, akaunyosha mkono wake na kuanza kuchua kiapo cha utii
.
Kwa hakika kauli yake: "Kisha watatoa wasifu wake kwa wenye kumjua na kumtambua", inaonyesha uwepo wa watu wanaomjua vizuri kabisa, hata kama wanaweza wasiwe wanajua kuwa ndie Mahdi anaesubiriwa.
Vilevile kauli yao: "Huyo ndie mtu wenu mnaemtafuta", inaonyesha hao watu saba walimkuta akisifika na sifa njema na za juu ambazo zinamfanya astahiki kuwa ndie Mahdi na mkombozi wa umma huu, ambae ataujaza ulimwengu usawa na uadilifu baada ya kujaa dhuluma na uovu. Na hakuna shaka kwamba, maarifa na utambuzi wa aina hii hauwezi kupatikana bila ya kuishi na kuchanganyikana nae kwa muda mrefu.
SHUBUHA YA TATU: NI KUHUSIANA NA UIMAMU NA UONGOZI WA MTOTO NA MAZAZI YAKE
Miongoni wa mambo yanayoenda sambamba na kauli ya kuwa Muhammad Ibni Alhasani Al-Al-Askari Almahdi
ni Imamu, ni kudai kwamba alipata uimamu na uongozi wa waislamu hali ya kuwa ana umri wa miaka mitano, wakati hairuhusiwi mtoto mdogo kubeba uongozi wa waislamu; kwa sababu hana pawa ya kulibeba jukumu hilo nzito, ukiongezea kuwa mtoto ni mwenye kutawaliwa, sasa inakuwaje awe na mamlaka juu wengine?!
MAJIBU YA SHUBUHA
Nikwamba sharti la imamu na kiongozi wa waislamu anatakiwa awe ni mwenye uwezo wa kuongoza, awe na sifa zinazomfanya aweze kusimamia majukumu ya uongozi, kama vile: uwelewa wa mambo, wepesi wa kujua njia za utatuzi wa mambo, akili timamu, uchamungu, awe ni mjuzi wa hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu... na mengineyo.
Ama kwamba ni lazima awe na umri mkubwa na awe ameishi sana, yote hayo siyenye kutiliwa manani, maadamu mtoto atakuwa na uwezo wa kusimamia majukumu ipasavyo.
Na kwa sababu kama hii, ndio maana utaona kwamba cheo hiki hakupewa mtu ambae ni mkubwa zaidi kiumri baada ya kufariki mtume(s.a.w.w)
. Hivyo, hakuna kiziwizi cha kijana kuwa imamu na kiongozi, kama ambavyo hakuna tatizo Mwenyezi Mungu alietakasika akawanemesha manabii na mawalii wake kwa neema za siri na dhahiri, neema ambazo huwafanya wastahiki wa cheo cha utume au uimamu, sawa sawa wawe wadogo au wakubwa. Bali Mwenyezi Mungu mtukfu ameyaelezea haya ndani ya kitabu chake madhubuti kwamba: alimpatia nabii Yahya
akiwa ni kijana mdogo, pale aliposema:
( يا يَحْيى خُذِ الْكِتابَ بِقُوَّةٍ وَ آتَيْناهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا )
"Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto"
.
Shaukaani amesema: "Makusudio ya neno ( الْحُكْمَ ) lililoko kwenye aya tukufu ni hekima, ambayo maana yake ni kukifahamu kitabu alicho amrishwa kukishika, na kuzifahamu hukumu na sheria za dini. Vilevile, imesemwa kuwa maana ya hekima ni: "Elimu, kuihifadhi na kuifanyia kazi". au " Unabii" au " Akili". Bali hakuna kiziwizi kuwa neno ( الْحُكْمَ ) linaweza kubeba maana zote zilizotajwa
.
Fakhru Raazi anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu alietukuka aliimarisha akili yake -yaani: nabii Yahya- katika udogo wake na akamfunulia (akampa wahai), na hii nikwakuwa Mwenyezi Mugu aliwapa utume nabii Yahya na Issa
wakiwa ni watoto, tofauti na alivyo wapa unabii na utume Mussa na Muhammad
"
.
Si hivyo tu, bali Mwenyezi Mungu ameelezea kuwa alimpatia kitabu nabii Issa na akamfanya kuwa nabii hali yakuwa ni mtoto mdogo akingali mbelekoni mwa mama yake, bado hata haujapita muda tangu kuzaliwa kwake isipokuwa kidogo. Amesema Mweyezi Mungu mtukufu:
فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّـهِ آتَانِي َ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا .وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا ﴿٣٢﴾
"Akawaashiria mtoto. Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu"
Fakhru Raazi Anasema: "Kwa hakika kauli yake: "Amenipa Kitabu", inaonyesha kuwa alikuwa ni nabii wakati ule akiyasema hayo"
.
Ameendelea kusema: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu amemjalia nabii Issa
-licha ya udogo wa mwili wake-, kuwa ni mwenye maumbile yenye nguvu na aliekamilika kiakili, kiasi cha kuweza kutekeleza swala na zaka. Mwenyezi Mungu akamuelekezea amri ya swala na zaka kwa kusema: "Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai"
, jambo ambalo linaonyesha kuwa nabii Issa
alikuwa kashawajibikiwa na sheria tangu mwanzo wa maisha yake
.
Kwa maelezo hayo, inabainika wazi kuwa hakuna kiziwizi kwa Imamu Mahdi (a.f) kuwa kiongozi wa waislamu akiwa mdogo mwenye umri wa miaka mitano au sita. Si hivyo tu, bali kumkubali ni bora zaidi; kwani ikiwa kwao unabii wa mtoto mchanga ni sahihi, basi uimamu wa kijana nao ni sahihi tena kwa ubora zaidi.
Nasi hapo kabla tumethibitisha kwa hoja kuwa, kumfanya mtu nabii au Imamu ni jukumu la Mwenyezi Mungu mtukufu, wala sio jambo la ikhitayari ya watu. Vilevile, tumethibitisha kwa dalili kuwa, Imamu Mahdi (a.f) kachaguliwa na Mwenyezi Mungu mtukufu, na yeye ndie aliemjalia na kumfanya kuwa Imamu hali yakuwa ni kijana kwa kutimiza kwake vigezo vya uimamu na uongozi, na kuwa udogo wa umri wake sio kikwazo na tatizo, kama alivyo mfanya Issa
nabii hali yakuwa ni mtoto mchanga kwa kutimiza kwake vigezo vya masharti ya unabii kipindi kile.
Ama kuhusiana na suala la Mwenyezi Mungu kumpa hekima Imamu Muhammad Ibni Alhasani Al-askari Almahdi
akiwa ni kijana, wamelikubali baadhi ya wasomi wa Ahli Sunna. Hakika Ibni Hajari Alhaitami amesema:
(مات [الحسن العسكري] بسر من رأى، ودُفن عند أبيه، وعمره ثمانية وعشرون سنة... ولم يخلّف غير ولده أبي القاسم محمد الحجّة، وعمره عند وفاة أبيه خمس سنين، لكن آتاه الله فيها الحكمة، ويُسمَّى القائم المنتظر)
"(Alhasani Al-askari) alifia Samaraa na kuzikwa karibu na baba yake akiwa na umri wa miaka ishirini na nane... Hakuna aliemuacha zaidi ya mwanae Abul-Qaasim Muhammad Alhujja akiwa na umri wa miaka mitano wakati alipo fariki baba yake. Lakini Mwenyezi Mungu alimpa hekima katika umri huo, na kijana huyo anaitwa Al-Qaaim Almntadhar
.
Baada ya haya yote, kunabaki hakuna pingamizi la yeye kuwa kiongozi na Imamu wa waislamu licha ya udogo wa umri wake. Na kwa njia hii kwa neema ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, shubuha inakuwa imetoweka.
SHUBUHA YA NNE: KUHUSIANA NA KUWA JINA LAKE (IMAMU MAHDI) NI MUHAMMAD IBNI ABDALLAH
Wameandika Abu Daud katika Sunani yake, Ibni Habbaan katika sahihi yake, Haakim katika Mustadraku yake na wengineo kwa kupokea kutoka kwa Ibni Mahdi kutoka kwa Sufiyan kutoka kwa Zarri Ibni Abdallah Ibni Masu'ud (Allah awe radhi nae) kwamba alisema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
:
(لو لم يبقَ من الدنيا إلا يوم لطوَّل الله ذلك اليوم، حتى يبعث فيه رجلاً مني، أو من أهل بيتي، يواطئ اسمه اسمي، واسم أبيه اسم أبي، يملأ الأرض قسطاً وعدلاً كما مُلئتْ ظلماً وجوراً)
"Kama isingelibakia isipokuwa siku moja ili dunia kuisha, basi Mwenyezi Mungu angeliirefusha siku hiyo ili amlete mtu anaetokana nami, au katika watu wa nyumba yangu, ambae jina lake ni sawa na jina langu, na jina la baba yake ni sawa na jina la baba yangu, atakaeijaza dunia usawa na uadilifua baada ya kujazwa dhuluma na uovu"
. Kufanana kwa jina la Mahdi na jina la mtume(s.a.w.w)
, vile vile, jina la baba wa Mahdi na jina la baba wa mtume(s.a.w.w)
, kunamaanisha kuwa jina la Mahdi (a.f) litakuwa ni: Muhammad Ibni Abdallah, na sio Muhammad Ibni Alhasani kama wanavyodai mashia.
MAJIBU YA SHUBUHA YA NNE
1.Hadithi hii imepokelewa kwa matamshi tofauti tofauti kama itakavyokuja, lakini pia imepokelewa kwa njia tofauti na zakwetu. Hivyo haiwezi kuwa ni hoja dhidi yetu, hali yakuwa kwetu haujathibiti usahihi wake. Ukiachilia mbali hayo, hadithi yenyewe haijafikia kiwango cha usahihi, bali wanachokisema zaidi kuhusiana na hadithi hiyo ni kuwa ni ( حسن ) yaani: nzuri. Hivyo basi, kwa hadithi hiyo hatuwezi kuzibatilisha hoja na dali zote za kiakili na zile za kinukuu (aya na hadithi) ambazo zimeonyesha na kuthibitisha kuwa Mahdi ndie Imamu Muhammad Ibni Alhasani Al-askari
, kama ambavyo hatuwezi kuzipuuza ishkali zote zilizotolewa ili kupinga na kukanusha umahdi wake.
2.Hakika hadithi ambayo kipengele cha "na jina la baba yake ni sawa na jina la baba yangu" kimetajwa, njia zake zote za mapokezi zinaishia kwa A'asimu Ibni Abi Anujuud ambae ni mmjoa kati ya watu wa visomo mashuhuri vya Qur'an. Bwana huyu kwa wasomi wa Ahli Sunna anajulikana kuwa hifdhi yake ni mbaya. Yafuatayo ni waliyoyasema kumhusu bwana huyo:
- Anasema Adhahabi: "(A'asimu) ni madhubuti katika kisomo cha Qur'an, na simadhubuti katika hadithi, ni mkweli kwao".
- Na Yahya Alqatwan anasema: "Sijakuta mtu ambae jina lake ni A'asimu isipokuwa nimemkuta ni mbaya wa kuhifadhi".
- Annasaai anasema: "(A'asimu) simwenye kuhifadhi".
- Na Addaar-qutni amesema: "Katika hifdhi ya A'asimu kuna kitu (tatizo)".
- Vilevile amesema Ibni Kharaash: "Katika hadithi yake kuna tatizo".
- Shu'ubah nae anasema: "Ametusimulia A'asimu Ibni Abi Annujuud, na ndani ya nafsi (yangu) kuna kitu".
- Ibni Sa'adi anasema: "Ni mwaminifu isipokuwa ni mwingi wa kukosea katika kusimulia kwake ( في حديثه )".
- Anasema Abu Hatam: "Si mahala pake kumwita mwaminifu".
- Yakubu Ibni Sufiyan nae anasema: "Katika kusimulia kwake kuna shaka, na yeye ni mwaminifu".
- Ibni Aliyah kamzungumzia kwa kusema: "Kila ambae jina lake ni A'asimu alikuwa ni mbaya wa kuhifadhi".
- Al-Uqaili amesema: "Hakuwa na chochote isipokuwa hifdhi mbaya".
Nami niseme kuwa: ikiwa hali ya huyu bwana ndio hii, inawezekanaje kuitegemea hadithi yake, tena katika suala muhimu kama hili, wakati ambao dalili zinazo thibitisha kuwa Mahdi Almuntadhar (a.f) ndie imamu Muhammad Ibni Alhasani
?!
3. Hakika hadithi hii iliyopokelewa kutoka kwa Aa'simu imehitilafiana kwa upande huu, kwamba wapo walioipokea kutoka kwake bila kutaja kipengele "na jina la baba yake ni sawa na jina la baba yangu", na wapo waliopokea kutoka kwake ikiwa na kipengele hicho.
Tirmidhi Ameandika kwa mapokezi kutoka kwa Sufiyan Ibni A'iinah kutoka kwa A'asimu kutoka kwa Zarri kutoka kwa Abdallah kutoka kwa Mtume(s.a.w.w)
kuwa alisema: "Atafuatia mtu katika watu wa nyumba yangu, ambae jina lake linafanana na jina langu". Vilevile amepokea kwa upokezi kutoka kwa Sufiyan Athouri kutoka kwa Badlah kutoka kwa Zarri kutoka kwa Abdallah kwamba alisema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
:
(لا تذهب الدنيا حتى يملك العرب رجل من أهل بيتي، يواطئ اسمه اسمي).
"Dunia haitaisha mpaka atakapo wamiliki warabu mtu katika watu wa nyumba yangu, ambae jina lakeni sawa na jina langu"
.
Kuna watu wengi walioipokea hadithi hii kutoka kwa A'asimu bila yakuwa na kipeangele: "na jina la baba yake ni sawa na jina baba yangu", miongoni mwao ni:
1. Muhammad Ibni Ibrahim Abu Shihabu katika kitabu cha: Sahih Ibni Habbaan, Juz: 13, uk: 284, na: Mawaaridu Dwam'an, Juz: 2, uk: 839.
2. Othiman Ibni Shabrmah, katika kitabu cha: Sahihi Ibni Habbaan, Juz: 15, Uk: 238, na: Mawaaridu Dwam'an, Juz: 2, Uk: 839.
3. Hamiid Ibni Abi Ghunyah katika kitabu: Al-Mu'jamu Al-ausat Cha Tabraani, Juz: 5, Uk: 135.
4. Abu Al-Ahwadh Salaam Ibni Saliimu katika kitabu: Almu'jamu Aswaghiiru Cha Tabraanim Jz: 2, Uk:148, Na: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 136.
5. Amru Ibni Marrah, katika kitabu: Almu'jamu Aswaghiiru Cha Tabraanim Juz:10, Uk:148, Na: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 131.
6. Al-A'mash, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 133.
7. Abu Is'haaq Ashaibaani, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 133.
8. Abdallah Ibni Hakiim Ibni Jubair, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.
9. Shu'bah, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.
10. Sufiani Athuur, katika kitabu: Sunan Abi Daud, Juz: 4, Uk: 108, Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.
11. Sufiani Ibni Aiinahm katika kitabu: Musnad Ahmad, Juz:1, Uk: 376, Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.
12. Abdul Maliki Ibni Abi Ghunyah, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.
13.Omar Ibni Obeid Atwanaafisim katika kitabu: Musnad Ahmad, Juz:1, Uk: 376, Na: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 135.
14.Waasitu Ibni Alhaarthi, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 135.
15. Abu kabari Ibni ayaash, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 135.
16. Ma'adhu Ibni Hishaamu kutoka kwa baba yake, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 133.
17. Amru Ibni Qaisi, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 137.
18. Abdallah Ibni Shabrmah, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 137.
Baadhi ya wapokezi waliopokea hadithi hii ikiwa na ziada ya kipengele "na jina baba yake linafanana na jina baba yangu", wapeipokea pia bila kuwa na kipengele hicho, miongoni mwao:
1. Omar Ibni ubaid, ameipokea hadithi hii ikiwa na ziada katika kitabu: sunan abi daudm jz:4, uk:106, wakati ameipokea bila ziada kama ilivyotangulia kwenye namba 13.
2.abu bakari Ibni a'yaashi, ameipokea ikiwa na ziada katika kitabu: sunan abi daudm jz:4, uk:106, wakati ameipokea bila ziada kama ilivyotangulia kwenye namba 15.
3. Sufiani, kaipokea ikiwa na ziada katika kitabu: sunan abi daud, jz:4, uk: 106, na katika kitabu: sahihi Ibni hayaani, jz:15, uk:236, na ameipokea bila ziada kwenye namba:10, 11.
4. Amru Ibni abi qaisi, ameipokea ikiwa na ziada katika: almuujamu alkabiir cha tabraani, jz:10, uk:135, na bila ziada kama ilivyo kwenye namba: 17.
Ikiwa hali ndio hii ya mashaka katika hii hadithi, inawezekanaje kuitegemea katika kuthibitisha jina la mzazi wa Imamu Mahdi almuntadhar (a.f).
4. Hakika hadithi hii pia imepokelewa kwa mapokezi ambayo A'asimu Ibni abu najoud hakutajwa na bila kuwa na ziada ya kipengele cha "na jina la baba yake ni sawa na jina baba yangu".
Albazaar katika kitabu chake Almusnad ametaja kwa mapokezi kutoka kwa muawiya Ibni Qurrah kutoka kwa baba yake (allah awe radhi nae) amesema: alisema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
:
(لتملأن الأرض جوراً وظلماً، فإذا مُلئتْ جوراً وظلماً بعث الله رجلاً مني، اسمه اسمي أو اسمه اسم أبي ، يملؤها عدلاً وقسطاً كما مُلئتْ جوراً وظلماً...).
“Kwa hakika ardhi itajaa uovu na dhuluma, itakapojaa uovu na dhuluma, Mwenyezi Mungu atamleta mtu anetokana na mimi, jina lake ni sawa na jina langu au jina lake ni sawa na jina la baba yangu,
ataijaza ardhi uadilfu na usawa kama itakavyokuwa imejaa uovu na uadilifu…”
.
Na Alhauthami ameindika pia katika kitabu chake (Zawaaid) kwa mapokezi kutoka kwa Muawiya Ibni Qurrah kutoka kwa baba yake (allah awe radhi nae) amesema: alisema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
:
(لتملأن الأرض جوراً وظلماً، فإذا مُلئتْ جوراً وظلماً بعث الله عزَّ وجل رجلاً مني، اسمه اسمي أو اسم نبي، يملؤها قسطاً وعدلاً كما مُلئتْ جوراً...)
“Kwa hakika ardhi itajaa uovu na dhuluma, itakapojaa uovu na dhuluma, Mwenyezi Mungu alietukuka na kutasika atamleta mtu anetokana na mimi, jina lake ni sawa na jina langu au jina lake ni sawa na jina la nabii, ataijaza ardhi uadilfu na usawa kama itakavyokuwa imejaa uovu na uadilifu…”
.
5. Hata kama tukisalimu amri kuwa hadithi hii ni sahihi, tunaweza kusema kuwa: makudio ya jina ni kuniya; kwani huwenda jina likatumiwa huku ikikusudiwa kuniya.
Bukhari kaandika katika kitabu chake Sahihi Bukhari kwa mapokezi kutoka kwa Sahalu Ibni Sa'adi alisema:
(ما كان لعلي اسم أحب إليه من أبي تراب، وإنْ كان ليفرح به إذا دُعي بها).
“Ali hakuwa na jina analo lipenda zaidi kuliko jina la Abu Turaab, hakika alikuwa akifurahi anapoitwa kwa jina hilo”
.
Vilevile, Sahalu amesema katika sahihi muslim: “Ali hakuwa na jina analolipenda zaidi kuliko jina la Abu Turaab, na likuwa akifurahi sana akiitwa kwa jina hilo, akamwambia: tusimulie kisa chake ni kwanini aliitwa Abu Turaab? akasema: "(Siku moja) mtume wa Mwenyezi Mungu
alikuja nyumbani kwa Fatwimah akawa hakumkuta Ali nyumbani mpaka akasema: "Kisha mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
akamkuta Ali
hali ya kuwa amelala, shuka lake upande mmoja likiwa limeanguka chini na kupatwa na udongo, mtume(s.a.w.w)
akawa anaupangusa ule udongo kwenye shuka lile huku akisema: "Amka ewe Abu Turaab, Amka ewe Abu Turaab"
.
Ni jambo lililokowazi kuwa ‘Abu Turaab’ ni kuniya, kwakuwa kuniya ni kila jina lililoanza na neno: ‘Abu au Umu’ yaani: baba au mama. Kwa sababu hiyo, ndio maana Ibni Hajari katika kitabu cha 'Fat'hul Baari' katika kauli yake: "(Babu Aliqaailat Fil Masjidi) kaitaja hadithi ya Ali ambayo inaelezea sababu ya kuitwa kwake Abu Turaab"
. Hivyo basi, makusudio ya hadithi hiyo yenye kipengele “Jina lake ni sawa na jina langu na jina la baba yake linaendana na jina baba yangu” ni kwamba kuniya ya mzazi wa Mahdi ni sawa na kuniya ya mzazi wa mtume(s.a.w.w)
, kwani wote wawili kuniya zao ni Abu Muhammad.
Vilevile, iko wazi kuwa kauli yake: "Jina lake linaendana/ ni sawa na jina langu na jina la baba yake linaendana/ ni sawa na jina baba yangu", ni ibara ndefu na ambayo haiashirii moja kwa moja kwamba kinacholengwa ni jina. Hivyo, kuna uwezekano wa kuifupisha kwa ibara ambayo ipo kibalagha na wazi zaidi kwa kusema: "Jina lake ni Muhammad Ibni Abdallah, au Muhammad Ibni Alhasani", lakini kwakuwa malengo ya mtume(s.a.w.w)
yahakuwa kulitaja wazi jina la Mahdi (a.f); kwakuwahofia watawala waovu na viongozi wapotovu, ndio maana akatumia ibara ambayo inabeba maana zaidi ya moja, ili kila mmoja afikirie atakavyo; na ili isiwe rahisi kwa wanaomtafuta wamuuwe au wamtie mbaroni kumjua na kumtofautisha na wengine.
SHUBUHA YA TANO: KWAMBA MAHDI (A.F) NI KATIKA KIZAZI CHA IMAMU HASANI ALMUJTABA
Ametaja Abu Daud kwa upokezi kutoka kwa Abu Is'haaqa alisema: Amesema Ali (Allah awe radhi nae), akimtazama mwanae Hasani:
(إن ابني هذا سيِّد كما سمَّاه النبي ( ص )، وسيخرج من صلبه رجل يُسمَّى باسم نبيكم، يشبهه في الخُلُق، ولا يشبهه في الخَلْق)
“Katika kizazi chake atatokea mtu atakaeitwa jina la mtume wenu, atafanana nae katika tabia wala hatafafa nae katika maumbile”. Kisha akataja kisa cha (Ataijaza Ardhi uadilifu)
.
MAJIBU YA SHUBUHA
1. Hakika hadithi hii kwa upande wa sanadi na upokezi ni dahaifu; kwakwa Abu Daud hajaipokea kutoka kwa Haruna Ibni Almughiira mwenyewe, bali kaipokea kutoka kwa alieisimulia kutoka Haruna Ibni Almughiira. Hivyo hadithi hii ni mursala.
Vilevile, Haruna Ibni Almughiira hata kama Ibni Habbaan kamtaja katika orodha ya waaminifu, isipokuwa amesema kuwa: "Huwenda alikosea"
.
Kama ambavyo katika upokezi na sanadi ya hadithi hii yupo Amru Ibni Abi Qaisi. Abu Daud anasema yafuatayo kuhusiana na Amru Ibni Abi Qaisi: “Hana tatizo, (lakini) katika kusimulia kwake ( في حديثه خطأ ) kuna makosa”. Na Adhahabi nae anasema: "Nimkweli, (lakini) ana makosa ( صدوق له أوهام )"
. Ama Othumani Ibni Abu Shaibah, amesema: “Hana tatizo, alikuwa akikosea kidogo katika hadithi au kusimulia”
. Ama Is'haaqa Asubaiy, imesemekana kuwa: "Hakuwahi kupokea kutoka kwa Amiirul Muunminina Ali
, bali alimuona mara moja". Ibni Almundhiri nae anasema: "Hadithi hii imekatika katika sanadi na mapokezi yake (munqatwiu)”, kwani Abu As'haaqa Asubai'y alimuona Ali
mara moja
. Hali kadhalika, Albani katika kusherehesha kitabu cha 'Mishkaatu Almisbah' alisema: "Sanadi na upokezi wa hadithi hii ni dhaifu
.
2. Zaidi ya hadithi hii hatujawakuta na dalili nyingine inayo onyesha kuwa Mahdi (a.f) ni katika kizazi cha Imamu Hasani
, isipokuwa baadi ya dhana na Istihisani ambazo hazina mashiko katika uwanja wa elimu.
Anasema Almulaa Ali Alqaari katika kitabu cha 'Mirqaatu Almafaatiih': "Wamehitilafiana kuhusina na Mahdi (a.f), kuwa anatokana na kizazi cha Hasani au kizazi cha Huseini
, na kuna uwezekano akawa amekusanya nasaba zote mbili za Hasani na Huseini
, ingawaje kilicho dhahiri zaidi ukilinanganisha na kilichotokea kwa watoto wa nabii Ibrahimu Ismaili na Is'haaqa
, ni kuwa yeye kwa upande wa baba anatokana na Imamu Hasani, wakati kwa upande wa mama anatokana na Imamu Huseini; kwani manabii wote wa wana wa Israeli walitokana na kizazi cha nabii Is'haaq
, wakati mtume wetu(s.a.w.w)
alitokana na kizazi cha nabii Ismaili
, akachukua nafasi ya manabii wote, -hakika ilikuwa ni badala nzuri!- akawa ndio wamwisho wa mitume. Vilevile, kwakuwa maimamu wengi na wakubwa wa umma huu wametokana na kizazi cha Huseini
, ni mahala pake Hasani nae apewe badala bora ya mtoto atakaekuwa wa mwisho wa mawalii, atakaechukua nafasi ya wateule na mawasii wengine,“kwakuwa hata imesemekana kwamba: Imamu Hasani
alipojivua ukhalifa na uongozi kidhahili kama zilivyo pokelewa sifa zake katika kibatu cha 'Al-ahaadithu Anabawiyah'-, alipewa cheo cha utawala wa Alqutbiyah (liwau wilayatul martabat alqutbiyah), hivyo ikawa ni pahala pake kupewa nasaba ya Imamu Mahdi
inayo fanana na nasaba ya nabii Issa
, pamoja na kukubaliana kuliinua neno la utume… Na yatakuja yanayoashiria maana hii kwa uwazi kabisa katika hadithi ya Abu Is'haaqa kutoka kwa Ali (Allah awe radhi nae), Mwenyezi Mungu ndie mjuzi zaidi
.
JAWABU KUHUSU HADITHI HII:
· Hakika nasaba ya Imamu Mahdi (a.f) haiwezi kuthibitishwa na istihisani za namna hii, bali inabidi ithibitishwe na hadithi sahihi. Hivyo, maneno yake hayana thamani yoyote ile kielimu; kwani yamejengeka juu ya dhana ambazo hazina mashiko katika kuthibitisha nasaba.
· Ama kuhusiana na kauli yake kuwa: "kuna uwezekano wa kuwa amekusanya nasaba zote mbili za Hasani na Huseini
", majibu yake ni kama ifuatavyo:
Hakika sisi haturumbani nae juu ya uwezekano wa jambo hilo, bali marumbano yetu nae ni kuhusiana na kuwa Imamu Mahdi (a.f) anatokana na Imamu Hasani
kwa upande wa baba. Ama kauli yake kuwa: "ingawaje kilichodhahiri zaidi ukilinanganisha na kilichotokea kwa watoto wa nabii Ibrahimu Ismaili na Is'haaqa
, ni kuwa yeye kwa upande wa baba anatokana na Imamu Hasani, wakati ambao anatokana na Imamu Huseini kwa upande wa mama ", inajibiwa kwakusema kuwa: nasaba kuwa hazithibitishwi kwa kulinganisha mambo wala kwa istihisani ambazo hazina dalili.
Vilevile, hatuwezi kusema kuwa, maadamu baadhi ya hadithi zinaonyesha kuwa Imamu Mahdi (a.f) anatokana na kizazi cha Imamu Hasani
na zingine zinaonyesha kuwa anatokana na kizazi cha Imamu Huseini
, hivyo ili kukusanya kauli zote mbili inabidi tukubaliane na kuwa, Imamu Alimahdi (a.f) kwa upande wa baba anatokana na kizazi cha Imamu Hasani, na kwa upande wa mama anatokana kizazi cha Imamu Huseini
, la hasha, kwani kinyume chake pia kinawezekana. Kwa maana kuwa, anaweza akatokana na Imamu Huseini kwa upande wa baba na Imamu Hasani kwa upande wa mama. Yote haya, ikiwa tukijalia kuwa hadithi zinazosema kuwa anatokana na kizazi cha Imamu Hasani kwa upande wa baba ni sahihi, lakini imeshatangulia kuwa hadithi hizo sio sahihi.
Ama kuhusiana na kauli yake: "kwani manabii wote wa wana wa Israeli walitokana na kizazi cha Is'haaqa, wakati mtume wetu (s.a.w.w) alitokana na kizazi cha Ismaili, akachukua nafasi ya manabii waote, -hakika ilikuwa ni badala nzuri! - akawa ndio wamwisho wa mitume. Vilevile, kwakuwa maimamu wengi na wakubwa wa umma huu ni katika watoto wa Huseini, ni mahala pake Hasani nae apewe badala bora ya mtoto atakaekuwa wa mwisho wa mawalii, atakaechukua nafasi ya wateule na mawasii wengine", majibu tunasema kwamba:
Bila shaka huku ni kulinganisha mambo kusikokuwa sahihi; kwa sababu mtume wetu alikuwa ni wamwisho wa manabii na mbora wao, lakini Imamu Mahdi (a.f) hata kama ni wamwisho wa maimamu, isipokuwa haijathibiti kuwa yeye ni mbora kuliko maimamu wengine.
Na zaidi ya hayo, ni kwamba: kuwateuwa mitume au maimamu hakufanyiki kwa minasaba ya namna hii, bali hufanyika kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kujua kuwa nabii au imamu ni mstahiki wa cheo hicho, kama alivyosema katika kitabu chake:
(اللَّهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسالَتَهُ)
"Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake"
.
Ama kauli yake: “kwakuwa hata imesemekana kwamba: Imamu Hasani
alipojivua ukhalifa na uongozi kidhahili kama zilivyo pokelewa sifa zake katika kibatu cha 'Al-ahaadithu Anabawiyah'-, alipewa cheo cha utawala wa Alqutbiyah (liwau wilayatul martabat alqutbiyah), hivyo ikawa ni pahala kupewa nasaba ya Imamu Mahdi
inayo fanana na nasaba ya nabii Issa
, pamoja na kukubaliana kuliinua neno la utume”, majibu yake ni kuwa mazigira haya yanayodaiwa sisi hatuyakubali, wala nasaba haiwezi kuthibitishwa kwayo kama ilivyotangulia.
Na tunashindwa kuelewa kuwa ni nini anakusudia kwa kusema: “cheo cha utawala wa Alqutbiyah!”. Kwani ikiwa makusudio yake ni cheo cha uongozi na waislamu, bila shaka Imamu Hasani
alikuwa na uongozi mkubwa tu kabla ya kujivua uongozi ule kidhahiri na baada yake. Na akiwa anakusudia kwa maneno hayo kwamba Imamu alipata cheo kingine kinyume na uongozi na uimamu kwa sababu ya kujivua uongozi, hili linahitajia ufafanuzi na uthibitisho kutoka kwake; ili itubainikie kuwa: je ni kweli ilikuwa ni mahala pake nasaba ya Imamu Mahdi
iwe ni sehemu ya cheo hicho au la?
Ama aliposema kuwa: "Yatakuja yanayoashiria maana hii kwa uwazi kabisa katika hadithi ya Abu Is'haaqa kutoka kwa Ali
" , jawabu lake nikuwa, tumekwisha bainisha udhaifu wa sanadi na upokezi wa hadithi hii hapo kabla, na kwamba haifai kuwa ni dalili na hoja hapa.
3. Hakika baadhi ya hadithi zao zinaonyesha kuwa Mahdi (a.f) ni katika kizazi cha Imamu Huseini
. Ameandika Abu Nua'imu Al-Asfahani katika kitabu chake 'Swifatul Mahdi' kwa mapokezi yake kutoka kwa Hudhaifa (Allah awe radhi nae) kuwa alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alituhutubia, akatukumbusha kuwa yeye ni nani, kisha akasema:
(لو لم يبقَ من الدنيا إلا يوم واحد لَطوَّلَ الله عزَّ وجل ذلك اليوم، حتى يبعث فيه رجلاً من ولدي اسمه اسمي). فقام سلمان الفارسي ( رض ) فقال: يا رسول الله، من أي ولدك ؟ قال: (هو من ولدي هذا)، وضرب بيده على الحسين (ع).
"Kama haitakuwa imebakia isipokuwa siku moja tu ili Dunia iishe, basi Mwenyezi Mungu aliyetukuka na kutakasika, atairefusha siku hiyo; ili amlete ndani ya siku hiyo mtu anaetokana na mwanangu, ambae jina lake ni sawa na jina langu". Salmani Alfarisi (Allaha awe radhi nae) akasimama na kusema: "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anaetokana na mwanao yupi?". Akajubu kwa kusema: "Yeye ni kutokana na mwanangu huyu", akaupiga mkono wake kwa Imamu Huseini"
.
Na Nua'imu Ibni Hammaad ameandika katika kitabu cha 'Al-fitanu' kwa mapokezi kutoka kwa Aballah Ibni Amru, alisema:
(يخرج رجل من ولد الحسين من قبل المشرق، ولو استقبلتْه الجبال لهدمها واتخذ فيها طُرُقاً).
"Atatokea mtu katika kizazi cha Huseini upande wa Mashariki, (ambae) hata kama milima ingelimuelekea na kumkabili angeivunja na kupasua njia ndani yake"
.
Vilevile, hadithi mfano wa hii imepokelewa kutoka kwa Abu Qabiili, amesma:
(يخرج رجل من ولد الحسين لو استقبلتْه الجبال الرواسي لهدَّها واتخذ فيها طُرُقاً).
"Atatokea mtu katika kizazi cha Huseni upande wa Mashariki, (ambae) hata kama ingelimuelekea na kumkabili milima iliyo inuka angeivunja na akapasua njia ndani yake"
.
4. Hadithi sahihi zilizopo kelewa kutoka wa maimamu wa nyumba ya mtume
, zimeonyesha kwamba Imamamu Mahdi (a.f) ni katika kizazi cha Imamu Huseni
. Miongoni mwa hadithi hizo:
· Ni hadithi sahihi ya Swaduuq, iliyotangulia kutoka kwa Salmani Alfaarisi (Allah awe radhi nae), kwa hakika alisema: " (Siku moja) niliingia kwa mtume(s.a.w.w)
, mara Huseini akawa amekaa juu ya mapaja ya mtume(s.a.w.w)
, huku mtume akiyabusu macho na midomo yake akisema:
(أنت سيِّد ابن سيِّد، أنت إمام ابن إمام أبو الأئمة، أنت حجة ابن حجة أبو حُجَج تسعة من صلبك، تاسعهم قائمهم).
"Wewe ni bwana mtoto wa bwana, wewe ni Imamu mtoto wa Imamu na baba wa maimamu, wewe ni hojjah mtoto wa hojjah na baba wa mahojjah tisa watokanao na kizazi chako, watisa wao ndie Qaaimu wao"
.
· Hadithi hasani ya Abu Hishaam Alja'afari, alisema: "Nilimsikia Abul Hasani Al-askari
akisema:
(الخلف من بعدي الحسن ابني، فكيف لكم بالخلف من بعد الخلف؟! قلت: ولِـمَ جعلني الله فداك؟ فقال: لأنكم لا ترون شخصه، ولا يحل لكم ذكره باسمه. قلت: فكيف نذكره؟ فقال: قولوا: الحجة من آل محمد صلوات الله وسلامه عليه).
"Mrithi baada yangu ni mwanangu Alhasani. Basi ninyi ni vipi mtakuwa kwa mrithi atakaekuwa baada ya mrithi huyo?! Nikasema: "Mwenyezi Mungu anifanye kuwa fidia yako, kwa nini?". Akasema: "Kwa sababu ninyi hamtamuona, wala hamtaruhusiwa kulitaja jina lake". Nikasema: "Ni vipi tutamtaja?" Akajibu kwakusema: " Semeni: Alhujjah katika ahli wa Muhammad rehema za Mwenyezi Mungu na amani yake iwe juu yake"
.
Hizi ndio shubuha muhizo zilizotolewa katika suala hili, na zipo shubuha zingine dhaifu tumeziacha ili kufupisha, mwenyekuzitaka akazitafute mahala pake.
(وَ كَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَ هُوَ الْحَقُّ قُلْ لَسْتُ عَلَيْكُمْ بِوَكيلٍ).
"Na watu wako wameikanusha, nayo ni Haki. Sema: Mimi sikuwakilishwa juu yenu"
.