NI NANI KHALIFA WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI

NI NANI KHALIFA WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI0%

NI NANI KHALIFA WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI Mwandishi:
: D.RAIHANI YASINI
Kundi: Misingi mikuu ya Dini
Kurasa: 10

NI NANI KHALIFA WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI

Mwandishi: ALY AALI MUHSINI
: D.RAIHANI YASINI
Kundi:

Kurasa: 10
Matembeleo: 37758
Pakua: 2470

Maelezo zaidi:

NI NANI KHALIFA WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 10 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 37758 / Pakua: 2470
Kiwango Kiwango Kiwango
NI NANI KHALIFA WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI

NI NANI KHALIFA WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI

Mwandishi:
Swahili

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

MTUNZI: SHEKH ALY AALI MUHSINI

MTARJUMI: SHEKH REHANI YASINI

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UTANGULIZI

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na sala na salamu zimwendee Nabii wetu Muhammadi na Aali zake watoharifu.

Hakika swala la ukhalifa, na ninani aliyepaswa kuwa khalifa, ni katika mambo yaliyo kithiri ndani yake majadiliano, na ikhtilafu baina ya makundi ya kiislamu, hususani baina ya Shia na Sunni.

Ikhtilafu hizo zilianza punde tu baada ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu kufariki dunia, hivyo kutokea marumbano na mabishano baina ya maswahaba katika mgahawa (saqifa) wa bani Saaidah, kuhusu nani anaye paswa kuwa kiongozo na khalifa baada ya mtume(s.a.w.w) , ikiwa ni katiaka jaribio lao la kwanza la kumteua kiongozo.

Hali hiyo haukuishia hapo, bali iliendelea katika kipindi chote cha mtiriko wa uongo (ukhalifa) wa waislamu, kuanzia za maswahaba mpaka leo hii. Hivyo kutokea makunduzi, na vita mbali mbali, viliyo pelekea kumwagika damu za waislamu bila hatia yoyote.

Kutokana na mazingira hayo, masunni waliwakubali viongozi waliokuwa wakitawala kwa mabavu, na kutoa kiapo cha utii kwa viongozi hao, pia kuhukumu kuwa: ukhalifa wa viongozi hao ni wakisheria, hivyo haipaswi kuupinga na kusimama dhidi yake.

Ingawaje baada ya utala wa Amamu Ali Ibni Abi Twalibi(a.s) , ukhalifa ulibadilika na kuwa ufalme, unaorithiwa na watoto kutoka kwa baba zao, pasipo na mashauriono baina ya waislamu, Isipokuwa tu ili kuuhalalisha ufalme huo ulibakia na jina la uislamu.

Baada ya kudhoofika hali ya kidini na yakisiyasa ya waislamu na kuzidi kuwa mbaya, miji ya kiislamu iligawika na kuwa vinchi vidogo vidogo, vyenye kugombewa na wafalme mbali mbali, wasio na sifa za kuwa viongozi wa waislamu, kama ilivyokuwa katika utawa wa bani Umayyah na bani Abbasi.

Hali hiyo iliendelea katika mfomo huo mpaka leo hii.

Kwa minajili hiyo, yalianza mazingira mapya katika miji ya kiislamu, yanayo pingana na maamuzi ya wanazuoni wa kisunni, ambayo ni: ulazima wa kutoa kiapo cha utii kwa kiongozi mmoja wa waislamu katika kila zama, na kuto kubali mfumo wa viongozi wengi, kama tutakavyo kuja kufafanuwa huko mbeleni.

Baada ya mazingira hayo, usahihi wa ishkali ya Mashia juu ya itikadi ya Masunni kuhusu ukhalifa na Makhalifa kwa ujumla, ulibainika zaidi.

Itikadi ya Mashia kuhusu ukhalifa ni kwamba: khalifa nilazima awe maasum na awe amaeteuliwa na Mwenyezi Mungu kupitia mtume wake, lakini pia awe ni katika kizani toharifu cha Mtume. Kwa sababu kama hiyo hawakukubali ukhalifa wa watu wasiokuwa na sifa hizo, kwani ukhalifa si haki ya yeyote yule, bali ni uteuzi utokao kwa Mwenyezi Mungu.

Ingawaje mgogoro mkubwa ulikithiri juu ya itikadi ya Mashia kuhusu Imamu Mahdi, Muhamadi Ibni Hasani Alaskari(a.s) , aliye zaliwa mnamo mwaka 255 hijiriya, na kwamba bado yupo hai mpaka sasa. Kwani Ahlisunnah wana amini kuwa itikadi hiyo, ni dalili tosha ya ufahamu dhaifu, kwani haiwezekani kumsadiki kiongozi aliyezaliwa kabla ya miaka mia moja tisini na sita, na kisha kudai kuwa bado yupo hai mpaka sasa. Madai hayo yalitokana na kuamini kuwa umri wa mtu wa kawaida, hauwezi kufikia miaka yote hiyo kwa vyovyote iwavyo.

Ahlisunnah waliwashambulia Mashia kwa madai hayo, bila kutoa majibu kuhusu nani kiongozi wa waislamu katika zama hizi. Wao waliinyamazia Haki, pamoja na umuhimu wake, na wala hawakutaka kulizungumzia swala hilo, kiasi ambacho hakuna Msunni yoyote mwenye majibu sahihi juu ya swala hilo.

Ninatarajia; kutokana na Utafiti huu, niwe nimetoa ufafanuzi kuhusiana na swala hili, na kuyafichua yaliyofichika.

Ninamuomba Mwenyzi Mungu mtukufu, aifanye kazi hii iwe kwaajili ya kutaka radhi zake, na aipokee kutoka kwangu kwa mapokezi mazuri, hakika yeye ni msikivu na mwenye kujibu maombi, na Sala na Salamu zimwendee Muhammadi na Aali zake watoharifu.

Tarehe 20 mwezi ramadhani 1424 hijiriya.

ALY AALI MUHSINI.

1

ULAZIMA WA KUTEULIWA KIONGOZI KWA MUJIBU WA MADHEHEBU YA AHLI SUNNAH

Wamekubaliana wanazuoni wa Ahlu sannah kuwa: ni wajibu kwa waislamu wote kumteua kiongozi wao wa kila zama, pia wakasema kuwa: ulazima huo ni katika wajibu za kidini ambazo hazipaswi kuachwa au kuzichelea.

Amesema Al-ijey katika kitabu cha mawaqifu kuwa: kwa mujibu wa madhehebu yetua, ni wajibu kwetu kumteua kiongozi

Pia akasema: walikubaliana waislamu wa zama za kwanza, baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) kuwa: haipaswi kupita zama, bila kuwa na kiongiozi. Maneno haya pia aliyasema Abubakari, (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) katika hotuba yake aliyo itoa baada ya kufariki Mtume kwa kusema: (Hakika Muhammadi kasha fariki, na nilazima kwa dini hii iwe na msimamizi). Hivyo waislamu wote wakamteua, huku wakiwa wameacha swala la muhimu zaidi, ambalo ni kumzika Mtume(s.a.w.w) .

Swala hilo la kumteua kiongozi katika kila zama, liliendea mpaka leo hii....[1] .

Pia akasema Al-maawardi kuwa: swala la kuteuliwa kiongozi atakaye simamia mambo ya umma, ni wajibu kwa mujibu wa ijmau[2] .

Na akasema Annawawi kuwa: wamekubaliana wanazuoni wote kuwa: ni wajibu kwa waislamu wote kumteua kiongozi, na uwajibu huo ni wakisheria na sio wakiakili... ama hoja ya kubakia umma bila kiongozi kwa kipindi cha mashauriano katika saqifah, na pia baada ya kufariki Omari(radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), ni kwa sababu hawakuwa wameacha kumteua kiongozi, bali walikuwa wakifanya juhudi za kuangalia ni nani anaefaa kuteuliwa[3] .

Pia akasema Albayhaqi kuwa: Baadhi ya wanazuoni wetu (akikusudia Ahmadi Ibni Hambali) walitaja kuwa; ushahidi wa ulazima wa kuteliwa kiongozi kisheria ni: ijmau ya maswahaba, pale walipo kubaliana, kumteua kiongozi, punde tu baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) [4] .

Na akasema Taftazani kuwa: kuteuliwa kiongozi, ni wajibu kwa mujibu wa madhehebu yetu, na muutazilah wote[5] .

Pia akasema Ibun hajari alhaytami: tambua kuwa; Maswahaba wote (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao), walikubaliana juu ya uwajibu wa kumteua kiongozi, baada ya kumalizika muda wa utume. Bali waliufanya uwajibu huo kuwa ni katika wajibu muhimu, kiasi kwamba walishughulishwa nao, hata kabla ya kumzika mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ikhtilafu zao katika kumteua kingozi, haziathiri ijmau hiyo iliyo tajwa[6] .

Naweza kusema kuwa: ulazima wa kuteuliwa kiongozi kwa waislamu wote, si makhsusi kwa zama za maswahaba tu, na tabiina na walio kuja baada yao, bali ni wajibu kwa waislamu wote katika kila zama, kama ilivyo wazi katika maneno ya wanazuoni, yaliyo tajwa hapo juu.

ULAZIMA WA KUHARAKIA KUMTUEA KIONGOZI WA WAISLAMU

Hakika hadithi sahihi za Ahlisunnah, zimetaja ulazima wa kumteua kiongozi wa waislamu katika kila zama.

Muslimu katika sahihi yake, na Baihaqi, katika sunanilkubra, na Haitami, katika Majmau azzawaidi, na wengineo, wamepokea hadithi kutoka kwa Mtume kuwa;

( من مات وليس في عنقة بيعة مات ميتة جاهلية )

Yeyote atakaye kufa bila kuwa na kiapo cha utii (bayia), Shingo Mwake, Atakufa kifo cha kijahili [7] .

Pia Ahmadi, katika Musnadi yake, Na Alhaytami, katika Majmau Alzzawaaidi, Na Abu Daaudi Attwayaalisi, katika musnadi yake, Na Ibuni Habbaani, katika sahihi yake, Na Abu Naimi, katika Hilyatul-auliyaa, pia wengineo, wamepokea kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuwa alisema:

( من مات بغير إمام مات ميتة جاهلية)

Atakaye kufa bila kuwa na Imamu (kiongozi), Atakufa kifo cha kijahili [8] .

Pia amepokea Haithami na Ibuni Abi Aswimu, kuwa mtume(s.a.w .w ) alisema:

( من مات وليس عليه إمام مات ميتة جاهلية )

Yeyote atakaye kufa bila kuwa na Imamu (kiongozi), atakufa kifo cha kijahili [9] .

Katika riwaya nyingine:

(من مات وليس عليه طاعة مات ميتة جاهلية)

Atakaye kufa bila kuwa na twa’a, atakufa kifo cha kijahili [10] .

Al-haakimu katika Mustadraki, Amepokea pia, kutoka kwa Mtume kuwa;

(من مات وليس عليه إمام جماعة فإنّ موتته موتة جاهلية)

Yeyote atakaye kufa bila kuwa na Imamu wa jamaa (kiongozi wa pamoja), basi bila shaka atakufa kifo cha kijahili [11] .

Twabarani, katika Alkabir na Al-ausatwu, Abu Yaali, na Ibun Abi Aswimu, pia wamepokea kutoka kwa mtume(s.a.w .w ) kuwa alisema;

(من مات وليس عليه إمام فميتته جاهلية)

Yeyote atakaye kufa bila Imamu (kiongozi), basi kifo chake ni cha kijahili [12] .

UCHAMBUZI KATIKA HADITHI

Mtumne(s.a.w .w ) aliposema: atakaye kufa; anatujulisha ulazima wa kuharakia kutoa kiapo cha utii kwa kiongozi (Imamu) wa waislamu, na kutochelea katika swala hilo, kwa kuhofia kufa bila kuwa na Imamu.

Ama maneno ya Mtume kuwa; bila kuwa na baiyah shingoni mwake, maana yake ni; kuto kuwa na baiyah ya lazima shingoni mwake, kama ilivyo katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa:

وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ ﴿١٣﴾

Na kila mtu tumemfungia a'mali yake shingoni mwake [13] .

Hivyo haipaswi kuivunja baiyah hiyo kwa Imamu wa haki. Na ili maneno hayo yawe na maana ya ulazima, Mtume hakusema;

(من مات ولم يبايع إماماً)

Atakaye kufa bila kum-bayi imamu .

Neno; (البيعة) Albayi’ah, linamaana ya kufunga Ahadi ya usikivu na utii. Neno hili huenda likawa limenyambuliwa katika neno; (البيع) , Albayi, hivyo mwenye kutoa kiapo cha utii kwa Imamu, ni kama kamuuzia nafsi yake, na kumpa twa’a, usikivu na kumnusuru.

Kwa minajili hiyo, kiapo hicho hakiwi kwa Imamu aliye kufa, bali kina kuwa kwa Imamu aliye hayi, kwa sababu maiti huwezi kufunga nayo mkataba. Na ama kuwaamini Maimamu walio tangulia, hakuna maana ya kutoa kiapo cha utii.

Ama maneno yake; atakufa kifo cha kijani, mana yake: atakufa kama kifo cha watu wakijahili.

Alisema Nawawi: yaani atakufa kifo kinacho fanana na kifo cha wajinga, kutokana na kwamba kifo chao hakikuwa na Imamu[14] .

Pia akasema Ibuni Hajari: makusudio ya kifo cha kijahili, ni kufa katika mazingira ya watu wa zama za kijahili, ambao walikufa katika upotevu, bila kuwa na Imamu anaye tiiwa, kutokana na kuwa wao hawakuwa wanalitambua hilo. Na haina maana kuwa atakufa akiwa kafiri, bali atakufa akiwa ni mwenye kuasi[15] .

Naweza kusema kuwa: kinacho kusuduwa, katika kufananisha kifo cha aliyeacha kutoa kiapo cha utii kwa Imamu wa zama, na kifo cha kijahili, ni kwakuwa; kuacha kufanya hivyo, maana yake ni kuacha kutoa baiyah kwa Imamu wa haki, jambo ambalo litamfanya mtu awafuate viongozi wa ovu, hivyo kusababisha kuingia katika upotevu, hatimaye kuwa sawa na watu wa kijahili waliokufa katika upotovu.

Kwa sababu hiyo, walikubaliana wanazuoni wote wa kisunni kuwa; niwajibu kwa umma kumbayi kiongozi wa waislamu katika kila zama, na hairuhusiwi kumkhalifu kwa hali yoyote ile.

Alisema Qurtubi: iwapo uongozi utakuwa kwa makubaliano ya wanasheria na wanaitikadi, au ukawa kwa mmoja, basi ni wajibu kwa watu wote kutoa baiyah ya kumtii na kumsikiliza, pia kukisimamisha kitabu cha Mwenyezi Mungu na sinnah za mjumbe wake(s.a.w.w) . Na atakaye acha kutoa baiyah kwa udhuru, atasamehewa, ama atakaye acha kutoa baiyah bila udhuru, atalazimishwa kwa nguvu, ili umma usije ukafarakiyana[16] .

Na akasema Ibuni Hazmu: Hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alisisitizia ulazima wa uimamu, na kwamba hairuhusiwi kubakia hata usiku mmoja bila kutoa baiyah[17] .

Akasema: hairuhusiwi kwa mwislamu, kubakia siku mbili bila kuwa na baiyah shingoni mwake[18] .

Pamoja na yote hayo, tunakuta kuwa; baada ya zama za Makhalifa, Ahlisunna wote waliacha wajibu huu, na kuacha kulizungumzia swala hili, na kujiepusha nalo. Bali hakuna juhudi zozote zinazo onekana upande wao za kulifanyia uchunguzi swala hili, pamoja na umuhimu wake, kiasi ambacho wameacha hata kuzifanyia uchambuzi hadithi hizo.

Mfano wa hilo ni Al-imamu Nawawi, ambaye kasherehesha Swahihi Muslimu, hakika yeye hakuongeza chochote juu ya hadithi isemayo; atakaye kufa bila kuwa na kiapo cha utii (buiyah) shingoni mwake, atakufa kifo cha kijahili.

Khususani ukizingatia kuwa, Annawawi alifariki mwaka 676 hiriya, baada ya kuanguka utawa wa Bani Abbasi, na kugawika miji ya kiislamu katika viAmiji vyenye ukhalifa wa kujitegemea[19] .

Inawezekana sababu ya hilo, ikawa ni uoga wa chuki ya wafalme juu ya wanazuoni wa kisuni, kama wata wakosesha vigezo vya kuwa viongozi wa waislamu, lakini pia kuogopa kuwakosoa Masuni wote katika kuliacha jambo muhimu na lawajibu, ambalo haipaswi kulichelea au kulizembea.

2

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

BAADHI YA SIFA ZA KIONGOZI WA WAISLAMU

Nilazima kwa anaye taka kuwa kiongozi wa waislamu, awe na vigezo vitakavyo muwezezsha kuwa kiongozi wa wengine, hivyo wanazuoni wa kisuni wametaja baadhi ya vigezo hivyo, ambavyo anatakiwa kuwa navyo kiongizi wa waislamu, vigezo hivyo ni vifuatavyo:

1- Awe mkurayshi

Hautasihi uongozi wa yeyote asiye kuwa mkurayshi, hiyo imetokana na maneno ya Mtume(s.a.w.w) kuwa:

(الأئمة من قريش)

Viongozi (Maimamu) watatoka katika ukoo wa Kuraishi [20] .

Alisema Annawawi: jamuhuri ya wanazuoni waliifanyia kazi hadithi hii, hivyo waka weka sharti kwamba; kiongozi ni lazima awe katika makuraishi.

Pia akasema: hadithi hii ndio iliyo kuwa hoja ya mashekhe wa wili (Abubakari na Omari) siku ya saqifah, na ikakubalika kwa Maswahaba wote bila kipingamizi[21] .

Na alisema Ibuni Hajari, akinukuu kutoka kwa Ayyadhi kuwa: wanazuoni wote, wamekubaliana kuwa; kiongozi ni katika makuraishi, wala haikuwahi nukuliwa pingamizi, kutoka kwa yeyote katika hilo, pia akasema: kauli ya Makhawariji na walio waafiki katika muutazila, hazita zinagatiwa, kutokana na kwamba zina pinzana na jamuhuri ya waislamu[22] .

Na akasema Almaawardi kuwa: kiongozi kuwa katika ukoo wa makuraishi, imetokana na hadithi ya Mtume, pia ijmau, hivyo hauta zingatiwa ukeukaji wa Bin Amru, palea alipo ruhusu uongozi kwa watu wote, kwa sababu hoja ya Abubakari siku ya saqifa kwa Answari, ya kukataa uteuzi wao kwa Saadi Bin Ubadah, ilisimamia maneno ya Mtume(s.a.w.w) yasemayo: Viongozi(Maimamu) ni katika kuraishi, hivyo hayata zingatiwa maneno ya yeyote atakaye pinga[23] .

Ibun Hazmi pia alisema: hauta sihi uongozi wa asiye toka katika kizazi cha kuraishi, hivyo utakuwa batili uongozi wa yeyote asiye kuwa katika ukoo huo, wala hata kuwa na amri yoyote, bali atakuwa fasiki na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu mtukufu, yeye na kila mwenye kumsaidia, au kuridhia uongozi wake, kwa sababu watakuwa wamevuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w) [24] .

Abdulqaahir Albaghdadi, katika (Alfarqu baina Alfiraqu)[25] . Na Ibun Hazmu, katika: (Alfaswilu Filmilali wal Ahawaa wa Annihali). Na Taftazani, katika: (Sharhilmaqaswidi)[26] . Na Alghazali, katika: (Qawaidul-aqaidi)[27] . Na Alqurtubi, katika: Tafsiri yake[28] . Na wengineo, walilitaja sharti hili, la kuwa kiongozi ni katika makuraish.

2- Awe mwenye elimu na mujitahidi

Alisema Al-ijey: Jamuhuri ya wanazuoni ina amini kuwa; kiongozi inabidi awe na uwezo wa kuifahamu itikadi na sheria, ili aweze kuisimamia dini ipaswavyo[29] .

Na akasema Abdulqahir Albaghdadi: wanazuoni wa kisuni, wali wajibisha kuwa kiwango cha Elimu, anacho paswa kuwa nacho kiongozi, kiwe kimefikia ijitihadi katika sheria[30] .

Akasema pia Alqurtubi: kiongozi anatakiwa awe ni katika wasomi waliofikia kiwango cha kuwa kadhi, mwenye ijitihadi, asiye wahitajie wengine katika kutoa hukumu (fat’wa) ya matukio, na hili lime kubaliwa na wote[31] .

Sharti hili la kuwa kiongozi wa waislamu, ni lazima awe mujitahidi, pia lime tajwa na: Almaawardi, katika: (Al-ahkamu Asultwaniyah)[32] . Na Tafatazani, katika: (Sharhi Almaqaswidi)[33] . Na Baaqilani, katika: (Altamuhidi)[34] . Na wengineo.

3- Awe muadilifu, asiwe fasiki

Alisema Albaghdadi, baada ya kuwa ametaja sharti la uadilifu: wanazuoni wa kisuni wali wajibisha kwa kiongizi, awe muadifu, katika dini yake, mwenye kujihifadhi katika mali na hali yake, asiwe mwenye kufanya madhambi makubwa, wala kuendelea kufanya madhambi madogo[35] .

Na akasema Al-ijey: Nilazima kiongozi awe muadilifu, asiye fanya maovu. Akaongeza kuwa: sharti hili lime kubaliwa na wote[36] .

Qurtubi pia akasema: Kiongozi anatakiwa awe muadilifu, kwa sababu hakuna tofauti baina ya wanazuoni kuwa; hairuhusiwi kumpa uongozi fasiki.

Kisha Jmamuhuri ya wanazuoni, ikasema: hakika utabatilika uongozi wa kiongozi yeyote atakae fanya maovu dhahiri, au kujulikana, kwa sababu imethibiti kuwa; uongozi uliwekwa kwa ajili ya kusimia sheria, kurejesha haki za wanyonge, kuhifadhi mali za mayatima, na mengineyo yaliyo tajwa huko nyuma, hivyo kama tutamruhusi fasiki kuwa kiongozi, itakuwa ni kinyume na malengo ya uongozi huo[37] .

Sharti hili la kuwa kiongozi wa waislamu, ni lazima awe muadilifu, pia lime tajwa na: Almaawardi, katika: (Al-ahkamu Asultwaniyah)[38] . Na Alghazali katika: (Qawaidul-aqaidi)[39] . Na Tafatazani, katika: (Sharhi Almaqaswidi)[40] . Na wengineo.

Na sifa zingine mfano wa hizo, ambazo hawakuwa nazo viongozi wao wengi, kwani uongozi baada ya kubadilika na kuwa ufalme, unaothiriwa na watoto kutoka kwa baba zao, masharti hayo hayakuzingatiwa, hivyo waislamu wakatawaliwa na mafasiki, ambao hawakuwa na maarifa ya hukumu za dini, ukiachia mbali kuwa hawakuwa na Elimu yoyote.

Yote hayo yalifanywa mbele ya wanazuoni wa kisuni, ambao wali usahihisha uongo wa viongozi hao, na wakahukumu kuwa ni uongozi wa kisheria, na kwamba ni lazima kutoa kiapo cha utii kwa uongozi huo, na kuwa hairuhusiwi kusimama dhidi yake.

HAWAWI VIONGOZI WA WILI WAKATI MMOJA

Wanazuoni wa kisuni, wameeleza kuwa; hairuhusiwi kutoa kiapo cha utii kwa viongozi wa wili, wakati mmoja, hata kama watakuwa katika maeneo tofauti.

Alisema Annawawi: Wame kubaliana wanazuoni kuwa; hairuhusiwi kutoa kiapo cha utii, kwa viongozi wa wili katika wakati mmoja, hata kama miji ya kiislamu itakuwa mingi.

Kisha akanukuu maneno ya Imamu wa Makkah na Madini kuwa: kuna uwezekano ikaruhusiwa, kama miji ya kiislamu ita panuka. Akasema kujibu kauli hiyo kuwa; ni kauli fasidi, inayo pingana na kauli ya wanazuoni, pia dhahiri ya hadithi[41] .

Akasema pia Ibun Kathiri, katika tafsiri yake: Ama kuwateua viongozi wa wili, au zadi ya wawili katika wakati mmoja, hairuhusiwi, hiyo inatokana na maneno ya Mtume(s.a.w.w) pale aliposema: yeyote atakaye kujieni na ilihali mna uongozi mmoja, na akataka kukufarakisheni, basi muuweni. Na hii ndio kauli ya jamuhuri. Na imenukuliwa na wengi, ijmau juu ya hilo, miongoni mwao ni Imamu wa Makka na Madina[42] .

Na akasema Ibun Hazmi, katika kitabu chake; Almuhalaa: Hairuhusiwi katika Dunia kuwa na kiongozi zaidi ya mmoja, bali uongozi utakuwa ni wa mwanzo kupewa baiyah[43] .

Akasema pia Qirtubi: Hairuhusiwi kuteuliwa viongizi wawili au watatu wakati mmoja. Alisema Imamu Abulmaali: wamekataa wanazuoni wetu kuteuliwa viongozi wawili wakati mmoja. Kisha akasema: kama itatokea kuteuliwa viongozi wawili wakati mmoja, basi itakuwa ni sawa na mawali wawili kumuozea binti mmoja kwa wanamume wawili, bila ya mmoja wao kujua kuwa kasha ozeshwa na mwengine[44] .

Kuna hadithi nyingi zilizo zungumzia hali itakayo wakumba waislamu, ya kukithiri wanao dai uimamu, na watakao pora ukhalifa, na kwamba watakuwa wengi, katika wakati mmoja.

Amepokea Bokhari na Muslimu, katika sahihi zao, na wengineo, kutoka kwa Abu Huraira kuwa; alipokea kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuwa alisema:

(كانت بنو إسرائيل تسوسهم الأنبياء، كلما هلك نبي خلفه نبي، وإنّه لانبي بعدي، وسيكون خلفاء فيكثرون. قالوا: فما تأمرنا؟ قال: فوا ببيعة الأوّل فالأوّل، أعطوهم حقّهم فإنّ الله سائلهم عمّا استرعاهم.)

Wana wa israeli walikuwa wakiongozwa na Manabii, ilikuwa kila anapo kufa Nabii, hufuatia Nabii mwengine, lakini baada yangu hakuta kuwa na Nabii, hivyo wata kithiri Makhalifa. Wakasema maswahaba: katika mazingira hayo, ni upi wadhifa wetu? Akawajibu; Toeni baiyah kwa mmoja baada ya mwengine, wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawasaili juu ya walicho simamia[45] .

Na hadithi zingine zikaeleza wadhifa wa wajibu juu ya hali hiyo, kwa kusema kuwa: wajibu wa waislamu juu ya hali hiyo, ni kushikamana na na khalifa wa kwanza, na kuuliwa khalifa mwengine, kama hata kubali.

Amepokea Muslimu katika Swahihi yake, kutoka kwa Abi Saidi Alkhidri kuwa; Mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , alisema kuwa:

(إذا بويع لخليفتين فاقتلوا الآخر منهما)

Iwapo watachaguliwa viongozi wa wili, basi muuweni mmoja wao [46] .

Alisema Annawawi, katika Sharhi ya Swahihi Muslimu: Maana ya hadithi hii ni kwamba: atakapo chaguliwa Khalifa baada ya kuchaguliwa mwengine, basi uchaguzi wa kwanza utakuwa Sahihi, na inatakiwa utiiwe, na uchaguzi wa pili utakuwa batili, na hairuhusiwi kuutii, sawa sawa awe amechaguliwa bila kujua kuwa kuna mwengine kasha chaguliwa au la, na sawa sawa iwe katika nchi moja au nchi mbili, hii ndiyo inayo kubaliwa na jamuhuri ya wanazuoni[47] .

Na akasema Qurtubi, katika tafsiri yake: watakapo chaguliwa Makhalifa wa wili, basi ukhalifa utakuwa ni wamwanzo, na mwengine atauliwa, lakini wanazuoni walikhtilafiana kuhusu kinacho kusudiwa katika kumuuwa, je inakusudiwa kumuenguwa katika uongozi, au kumuuwa? Lakini maana ya kwanza ndio yenye mashiko zaidi; Alisema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) : Watakapo chaguliwa viongozi wa wili, basi auliwe mmoja wao. Hadithi hii imepokelewa na Muslimu kutoka kwa: Abu Saidi Alkhidri.

Hiyo ndio dalili kubwa inayo kataza kuwepo viongozi wa wili, kwa sababu kuwepo viongozi wa wili kutazidisha unafiki, mifarakano, fitina na kutoweka Nema[48] .

Na akasema Sharbini: Wala hairuhusiwi kuteliwa viongozi wa wili, au zadi, hata kama itakuwa katika mataifa tofauti yaliyopo mbali mbali, kutokana na kwamba swala hilo lina sababisha kutofautiana rai, na kufarikiana, hivyo kama watateuliwa viongozi wa wili kwa wakati mmoja, uongozi huo uta batilika, na kama mmoja wao ata tangulia, basi yeye ndiye atakuwa kiongozi, kama ilivyo katika ndoa, na wapili ata adhibiwa, yeye na walio muunga mkono, kwa sababu wame fanya haramu.

Inasemekana kuwa: imepokewa katika Muslimu: watakapo chaguliwa makhalifa wa wili, basi muuweni mmoja wao, hivyo inakuwaje aadhibiwe tu? Jibu lake ni kwamba, maana ya Hadithi hiyo ni kwamba: Msimtii, hivyo basi kuwa sawa na aliye uliwa[49] .

MAZINGIRA YA AHLI SUNNAH KATIKA ZAMA HIZI

Tunapo angalia uhalisia wa Ahlu sunnah, katika zama hizi, na kabla yake, tunawakuta kuwa walizikhalifu Hadithi zilizo sahihi kwao, ambazo tumezinukuu baadhi yake hapo kabla, lakini pia wakayaacha maneno ya wanazuoni wao, kama tulivyo nukuu maneno yao.

Hakika wao hawa kumteua kiongozi mmoja, pamoja na kuwa ni wajibu kwao kufanya hivo, hivyo waka ridhia kutawaliwa na wafalme tofauti tofauti ambao si makhalifa, bali ni wafalme, maraisi na maamiri.

Kama Ahlu sunnah wanaamini kuwa wafalme hao na wengineo, si viongozi wa kisheria, basi ni wajibu kwao kuwaenguwa madarakani, na kumteua kiongozi mmoja wa waislamu, kinyume na hivyo, watakuwa wanafanya takiya ambayo wao hawaiamini.

Na kama watakuwa wana amini kuwa wao ni viongozi wa kisheria, basi watakuwa wamekhalifu makubaliano ya maswahaba na wanazuoni wao, ambao walisema kuwa: hairuhusuwi kuteua viongozi wa wili wakati mmoja. Na hawa kuzifanyia kazi hadithi sahihi zinazo eleza ulaziama wa kumpa baiyah kiongozi mmoja, na kumuua kiongozi mwengine.

Ukiongezea kuwa hawakuzingatia sharti la kwamba; kiongzi anatakiwa awe mkuraishi, na kwamba natakiwa awe muadilifu na mwenye Elimu.

Hivyo Uongozi ukawa ni wakila mwenye kuwashinda wengine kwa nguvu.

Mjumuisha wa hayo ni kwamba: Ahlu sunnah wote, wametumbukia katika madhambi, sawa sawa wawe wametoa baiyah ya utii kwa wafalme hao au la, hiyo ni kwa sababu hawakumteua awe ni kiongozi wa waislamu wote, kwa minajili hiyo, wanakuwa wameacha wajibu na wadhifa wao wa kisheria.

JUHUDI ZA KUJIBU ISHKALI HIYO NA MAJIBU YAKE

Wanaweza kusema kuwa: kila kikundi cha Ahlu sunnah, katika kila taifa, kilimteua kiongozi wake wa kisheria, hivyo kutekeleza wadhifa wao wa kisheria walio faradhishiwa na Mwenyezi Mungu, wa kumbayei kiongozi wao wa zama hizi.

JAWABU :

1- Hatakama tutakubaliana na hilo, ukweli ni kwamba; kila kikundi cha Ahlu sunnah, kitakuwa kimemteua kiongozi wake tu, na wala hakitakuwa kimewateua vingozi wa mataifa mengine.

Na hapa twaweza kusema kuwa: uteuzi huo, ima utakuwa sahihi, hivyo basi kulazimika wengine kuwafuta katika hilo, kiasi kwamba ikiwa wataacha kufanya hivio, watakuwa wameacha wajibu. Au uteuzi huo usiwe sahihi, hivyo kuto kuwa na thamani (mazingatio) yoyote.

2- Uteuzi wao kwa viongozi wao unapingana na uteuzi wa wengine katika miji mingine ya kiislamu, na hairuhusiwi kuwateua viongozi wa wili katika wakati mmoja, hivyo uchaguzi wowote utakao fanyika utakuwa batili, kwa minajili hiyo, ishkali itabakia kwa Ahlusunnah walio wengi.

3- Watu hao waliotoa baiya, walitoa baiyah hiyo kwa kiongozi wao ili awe kiongozi wa taifa lao, na si awe kiongozi wa waislamu wote, kwasababu hiyo, ndio mana hatujawahi sikia kuwa kunakiongozi yeyote katika zama hizi, aliye dai uongozi kwa waislamu wote, na uongozi unaokuwa wa wajibu, ni huu wapili na sio ule wa mwanzo.

4- Ukhalifa wa haki, kwa mujibu wa Ahlusunnah, hauwi isipokuwa kwa Amri ya Mwenyezi Mungu, au ya mjumbe wake, au kwa kuteuliwa na kiongozi wa kabla yake, au kwa mashauriano (shura) baina waislamu wote, au kwa kufanya mapinduzi katika miji mingine ya kiislamu. Na tunapowaangalia viongozi wa sasa, hakuna yeyote aliyeteuliwa kwa kutuliwa kwa kutumia njia hizo.

Lakini pia kwa mujibu wao, uongozi unaweza kuwa, kwa kuteuliwa na wanazuoni, hivyo basi kama waliotoa baiyah, watakuwa ni katika wanazuoni, basi uteuzi wao utakuwa sahihi, na kama haitakuwa hivyo, basi uteuzi wao hauta kuwa sahihi.

Na hakuna kikundi cha kisunni katika zama hizi, chenye sifa hizo, kwa minajili hiyo, uteuzi wa watu hao hautakuwa sahihi, na wala uteuzi huo hautawalazimu wengine, bali uteuzi huo utakuwa chini ya maneno ya Omari Ibunl-khatwabi ya kuwa:

(فمن بايع رجلاً على غيرمشورة من المسلمين فلايتابع هو ولا الّذي بايعه تعِزَّة() [50] ) أن يقتلا)

Atakaye mpa baiyah mtu, bila ya mashauriano (shura) baina ya waislamu, basi hatofuatwa yeye na aliyemachagua, kwa kuhofia kuuliwa[51] .

Pia kwa mujibu wao, uteuzi hauwi sahihi isipukuwa kiongozi anapokuwa ni katika ukoo wa Quraishi, muadilifu na mwenye elimu, kama ilivyo tajwa huko nyuma, lakini viongozi wao wote hana sifa hizo, hivyo uteuzi wao utakuwaje lazima kwa waislamu wote?!.

JUHUDI NYINGINE NA MAJIBU YAKE

Inawezekana wakasema kuwa: Hakika kila mmoja katika Ahlusunnah, anamfuata kiongozi (Imamu) katika viongozi wa waislamu, na kama ilivyo wazi kuwa Ahlusunnah wana maimamu wanne; miongoni mwao kuna wanaomfuata Abuhanifa Annuumani, na kuna wengine wanaomfuata Maliki Ibun Anasi, na wengine humfuata Ahmadi bin Hambali, kama ambavyo kuna wengine kati yao humfuata Muhammadi Ibun Idrisa Alshafi’i, hivyo basi kila mmoja kati yao anapo kufa, hufa akiwa na baiyah shingoni mwake ya mmoja kati ya maimamu hawa, na hivyo kuto kuwa na ishkali.

JIBU LAKE

1 – Mazungumzo yetu ni kuhusu kutoa baiyah kwa kiongozi atakaye wasimamia waislamu, na kuwa na utawala wa muda kwa watu wote, hii ndio baiyah waliyoiwajibisha Ahlusunah katika ibara zao zilizo tangulia, na pia hadithi zilizo tangulia. Na wala mazungumzo yetu si kuhusu Imamu wa wanazuoni ambao watu hufuata fat’wa zao, na kuzifanyia kazi, kwani hao si wajibu kuwabayi’i kwa itifaki ya wanazuoni wote, bali ni wajibu kuwauliza ilikujua hukumu ya kisheria, kama alivyo sema Mwenyezi Mungu mtukufu kuwa:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٧﴾

Basi waulizeni wenye elimu ikiwa nyinyi hamjui [52] .

2 – hakuna yeyote kati ya maimamu wanne, aliyewahi kutoa fat’wa juu ya uwajibu wa kuwapa baiyah wao au wanazuoni wengine, kama ambavyo haijanukuliwa kutoka kwa yeyote katika wanazuoni wa kisunni, kuwa waliwahi kupewa baiyah, si katika zama zao au katika zama za baada yao, hivyo kama kuwapa baiyah ingekuwa ni wajibu wangewaambia watu, na kuwasisitiza juu ya kutoa baiyah hiyo.

3 – tulisema huko nyuma kuwa: kutoa baiyah, maana yake ni kuahidi, na ahadi hiyo haiwezi kuthibiti isipokuwa kwa imamu aliye hai, kwa minajili hiyo haiwezekani kumpa baiyah yeyote kati ya maimamu tulio wataja hapo nyuma, kutokana na kwamba walisha kufa, hilo lipo wazi na halihitaji ufafanuzi zaidi.

JUHUDI YA TATU NA MAJIBU YAKE:

Wanaweza kusema: hakika imam wa waislamu ni mmoja kati ya wanazuoni wa waislamu wasasa, nasisi wadhifa wetu ni kuwafuata katika fat’wa zao.

JIBU LAKE:

1 - Tuliyo yasema hapo nyuma, hapa pia yanakuja, kwani tulisema kuwa; maongezi yetu ni kuhusu kumteua kiongozi atakaye simamia mambo ya waislamu, na kuwa kiongozi wao, na si kuhusu maimamu wa wanazuioni, hakika maimamu wa wanazuoni, si wajibu kuwapa Baiyah kwa mujibu wa Ahlusunnah.

2 - Tulisema hapo mwanzo kuwa: ni sharti kwa kiongozi awe mujtahidi, na kwakuwa mlango wa ijtihadi ulifungwa, na ukabakia kwa maimamu wanne tu, hivyo basi wanazuoni wa ahlusunnah wasasa watabakia kuwa wamuasi tu, na yeyote miongoni mwao atakae dai ijitihadi, hato kubaliwa, na hivyo yeyote kati yao kukosa sifa ya kuwa kiongozi.

3 – Hata kama tutakubaliana kuwa katika wanazuoni hao wasasa kuna mwenye sifa ya kuwa kiongozi, hawezi kuwa kiongozi kwa kupata sifa tu, bali ili awe kiongozi anabidi achaguliwe, na awe na nguvu katika miji yote ya kiislamu, kama ilivyo itifaki ya Ahlisunnah, kwa sababu hiyo, walimuhesabu Muawiya kuwa ni katika maimamu kumi na mbili.

JUHUDI YA NNE NA MAJIBU YAKE:

Pia wanaweza kusema kuwa: tukubaliane kuwa Ahlusunnah waliacha faradhi hii ya kumteua kiongozi wao, sawa sawa katika zama hizi, au zama zilizo fuatia zama za makhalifa, lakini hilo, hali maanishi kuwa wao walifanya maasi, hivyo kufa kifo cha kijahili, kwa sababu hilo linge walazimu kama wangeacha kwa makusudi na si kwadharura[53] .

JIBU LAKE:

1 - Sisi hatukubali kuwa: Ahlusunna wameshindwa kumteua kingozi wao katika zama hizi, kwa sababu baiyah, niagano la kuusilikiliza na kuutii uongozi, na hili linawezekana, kwani wanazuono wao wanaweza kutoa muongozo kwa wafuasi wao watoe baiyah kwa kiongozi mmoja wanaomuona kuwa anasifa ya kuwa kiongozi.

Ama kuhusu kuogopa hasira za wafalme wao katika miji yao, si sababu ya kuwafanya waache faradhi hii muhimu, na kuacha wadhifa adhimu kama huu, kwa sababu wao hawaamini kufanya taqiyah kwa wafame wao, kwa minajili hiyo, ilikuwa katika ubora wa Maliki bin Anasi, na Ahmadi bin Hambali, pia wengineo ni kuwa kwao wa wazi katika itikadi zao, pamoja na wafalme wa zama zao kuto kuwa radhi nao, Hivyo kuingia matatizoni.

Hayo ni mbali na kwamba; kunasehemu za kimataifa zinazo wawezesha kuongea, na kutangaza itikadi yako bila wasi wasi, hivyo hilo nijambo linalo wezekana kwa wote, au wengi wao, lakini pamoja na yote hayo kati yao aliyeongea juu ya hilo.

2 – Tukubaliane kwamba Ahlusunnah walishindwa kumteua kiongozi wao, kwa sababu ya dharura, jambo ambalo linawatoa katika madhambi, kutokana na kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu hawakalifishi watu kwa lile wasiloliweza.

Ama kuhusu kuto kufa kifo cha kijahili, kwa sababu ya udharura huo, hatuwezi kukubalina nao, kwa sababu hata wale walioishi zama za kijahili, ambao hawakuwa wanajua chochote kuhusu dini au maisha zaidi ya chakula, na wakaashi maisha ya kudhoofishwa katika ardhi, wao twaweza kusema hawata adhibiwa kwamijubu wa maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu, pale aliposema:

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا ﴿١٥﴾

Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume. [54]

Lakini pamoja na hayo watabakia kuwa katika wapotovu, kwa sababu kila mwenye kuiacha haki, atakuwa mpotevu, hatakama atakuwa na udhuru.

Nasi pia tunalolizungumzia ni mafano wa hilo, kwa sababu hadithi ya Muslimu ilisema kuwa; yeyote hatakuwa na baiyah shingoni mwake, basi atakufa kifo cha kijahili, hivyo hadithi hii inamshamili hata aliye na udhuru au kushindwa.

Kutokana na yaliyo tangulia, tunaweza kusema kuwa: hakika masunni, katika miji yote ya kiislamu, ima watakuwa na mtu mwenye vigezo vya kuwa kiongozi wa waislamu, hivyo kupaswa kumpa baiyah ili awe kiongozi wao.

Au hawatakuwa na mtu mwenye vigezo hivyo, na kutakiwa kutoa baiyah kwa kiongozi mmoja wa waislamu wote, mwenye vigezo vilivyo tajwa, na hairuhusiwi kuwaacha waislamu bila kuwa na kiongozi, kama ilivyothibiti katika hadithi na maneno ya wanazuoni.

Ahlusunah katika miji yote, hawakumteua kiongozi wao, hivyo wao wapo kinyume na fat’wa za wanazuoni wao, na wamezipuuza hadithi sahihi za mtume(s.a.wa.w) , hivyo kifo chao kitakuwa cha kijahili, kwa mujibu wa hadithi iliyo pokewa na Muslimu.

3

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

KIONGOZI (KHALIFA) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI NI IMAMULMAHDI(A.S)

Baada ya kuwa tumefahamu kuwa ahlisunnah, hawakutekeleza wadhifa wao wa wajibu, wa kumteua kiongozi wao wa zama hizi, na kwamba watakufa bila kuwa na baiyah shingoni mwao, tunaweza kusema kuwa:

Hakika Mashia wanao amini maimamu kumi na mbili, wanaamini kuwa kiongozi wa zama hizi ni Imamu Muhammadi bin Hasani Al-askari(a.s) .

Na kwakuwa swala hili, lilizua mjadala mkubwa ndani yake, hivyo tutalitolea ufafanuzi na maelezo katika pande tofauti:

SEHEMU YA KWANZA: TUTAMZUNGUMZIA IMAMU HUYO:

Imamu huyo ni; Muhammadi bin Hasani, bin Ali, bin Muhammadi, bin Ali Riza, bin Musa, bin Jaafar Swadiq, bin Muhamadi, bin Ali Zainul-abidina, bin Husaini, bin Ali, bin Abi Twalibi, sala na salamu za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote.

Alizaliwa tarehe 15 mwezi Shaabani, mwaka; 255 hijiriya, katika mji wa Samarraa.

Na kupata uongozi tarehe: 8/3/260 hijiriya, akiwa na umri wa miaka mitano punde tu baada ya kufariki baba yake. Alitoweka katika macho ya watu mpaka mwaka 329 hiriya, ambako kulifahamika kwa Ghaibutu sughra, ambapo alikuwa akionekana kwa baadhi ya Mashia wake, na baada ya kufariki balozi wake wanne, alitoweka na kutooneka kwa watu mpaka leo hii, ambako kunajulikana kwa Ghaibutu kubra. Ataendelea kubakia hivo mpaka hapo Mwenyezi Mungu atakapo taka adhihiri, kwaajili ya kueneza uadilifu na usawa duniani, baada ya kujaa uovu na uonevu.

SEHEMU YA PILI: KUTHIBITISHA KUZALIWA KWAKE:

Baadhi ya Ahlusunnah, walikanusha kuzaliwa kwake, wakidai kuwa baba yake (Imamu Hsani Al-askari, a.s.) alifariki bila kuwa na mtoto.

Alisema ibun Hajari Alhaitami: wanazuoni wengi wanasema kuwa Hasani Al-askari hakuwa na mtoto, kwa sababu kaka yake, ambaye ni Jaafari, alidai urithi wake, hivyo kama angekuwa na mtoto, asingerithiwa na kaka yake[55] .

Shamsu Alddini Adhahabi nae pia alisema: alisema ibun Hajari, na ibun Qanii, na wengineo kuwa: Hasani bin Ali Al-askari hakuwa na mtoto[56] .

Lakini baada ya kusimama dalili sahihi zenye kuthibitisha kuzaliwa kwake, hayata kuwa na thamani maneno ya wenye kukanusha kuzaliwa kwake.

Hivyo tuta taja dalili za kiakili na hadithi zenye kuthibitisha kuzaliwa kwake.

MIONGONI MWA DALI ZA KIAKILI NI:

1 – Ikiwa hatuta kubali kuzaliwa kwa Imamu Almahdi(a.s) na kuendelea kuwa hai, basi hatuna budi kukubali kuwa; katika zama hizi hatuna Imamu atokanae na kizazi kitukufu cha Mtume, kama alivyo tueleza kuwa:

(إنّي تاركٌ فيكم الثقلين: كتاب الله وعترتي أهل بيتي، ما إن تمسّكتم بهما فلن تضلّوا من بعدي أبداً، وإنّهما لن يفترقا حتّى يَرِدَ عليّ الخوض، فانظروا كيف تخلفوني فيهما).

Hakika mimi nimekuachieni vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha nyumba yangu, kamwe hamta potea, madamu mta shikamana navyo, na hakika vizito hivyo kamwe havita tengana, mpaka vitanirejea katika hauzi, tazameni ni vipi mtashikana navyo baada yangu[57] .

Hivyo ni kwa sababu kwamba; kama hatakuwepo, hakutakuwa na Imamu mwengine atokanae na kizazi kitukufu cha mtume, anayefaa kushikwa, na hadithi hii haitakuwa na maana yeyete katika zama hizi, na hivyo kuwa batili. Na hilo halikubaliki kwa sababu hadithi hiyo imeeleza kwa uwazi kuwa; wapo wenye vigezo vya kuwa Mamamu (viongozi) wa kila zama, mpaka sijku ya kiyama, kinyume na hivyo tungeona utengano kati ya vizito hivyo viliwi, jambo ambalo limekataliwa na hadithi hiyo.

2 – ikiwa hatuta kabali kuzaliwa kwa Imamu Almahdi(a.s) , na kuwepo kwake, na si Imamu wazama, hatunabudi kukubali kuwa; waislamu wote wa zama hizi na zama zilizo pita, wanakufa kifo cha kijahili, kwamujibu wa maneno ya mtume(s.a.w.w) kuwa:

( من مات وليس في عنقة بيعة مات ميتة جاهلية )

yeyote atakaye kufa bila kuwa na kiapo cha utii (bayia), shingoni mwaake, atakufa kifo cha kijahili [58] .

Kwa sababu waislamu wote hawatakuwa na Imamu (kiongozi), na hilo si sahihi kwa ijmau ya wote.

3 – Ikiwa hatuta kubali kuzaliwa kwa Imamu Almahdi(a.s) , na badala yake tukasema kuwa; Imamu Mahdi atazaliwa baadae, kama wanavyo itikadia Masunni, hilo litasababishia matatizo mengi, ambayo tutayataja mwishoni mwa kitabu.

4 – kwamba wanazuoni wengi wa Ahlusunnah, walikuri kuzaliwa kwake, tutakuja kuwa taja hivi punde panapo majaaliwa.

Hivyo ni upuuzi mkubwa, kukanusha kwazaliwa kwa mtu ambaye wamekiri kuzaliwa kweke, wanazuoni wengi, ambao hawatuhumiwi kufanya jama na watu wenye kuitikadia kuzaliwa kwake!!

NA MIONGONI MWA DALILI ZA HADITHI NI:

(ما رواه الكليني في كتاب الكافي بسند صحيح، عن محمد بن يحيى، عن أحمد بن إسحاق، عن أبي هاشم الجعفري قال: قلت لأبي محمد×: جلالتك تمنعني من مسألتك، أتأذن لي أن أسألك؟ فقال: سل. قلت: يا سيّدي هل لك ولد؟ فقال: نعم. فقلت: فإن حدَثَ بِكَ حدَثٌ فأين أسأل عنه؟ فقال: بالمدينة).

1 – Alipokea Kulaini, (Mungu amrehemu), katika kitabu cha Alkafi, kwa Sanadi sahihi, kutoka kwa Muhammadi bin Yahya, kutoka kwa Ahmadi bin Is’haqa, kutoka kwa Abi Hashimu Aljaafari kuwa alisema: nili mwambia Abi Muhammadi(a.s) : utukufu wako unanifanya nishindwe kukuuliza, je unaniruhusu ni kuulize? Akasema: uliza. Nika muuliza: bwana wangu, je unamtoto? Akanijibu: ndio. Nikamuuliza: je kama litakukuta la kukuta, nitamtafutia wapi? Akajibu: mtafute mjini[59] .

Watu wote wanapo taka kuthibitisha mazazi ya mtoto, hurejea kwa baba wa mtoto, hivyo kama atawathibitishia kuzaliwa kwake, kwa riwaya moja sahhihi, kuwa amethibisha kuwa anamtoto, hatunabudi kumsadiki na kukiri, na tunaangalia katika hadithi hapo juu, tunakuta kuwa; Imamu Al-askari, kakiri kuwa anamtoto.

Pia tutataja hapo mbele, hadidhi zingine, zinazo thibitisha kuzaliwa kwake.

2 – Wanazuoni wengi, pia waumini, na watu wema, walimuona Imamu Amahdi(a.s) , katika matukio mengi na maeneo tofauti, mpaka Mirza Nuri Altwabarasi (utukuke utajo wake) katika kitabu chake cha: (Jannatulmaawa fi dhikraa man faaza bi liqaailhujjah), alitaja visa nyingi vilivyo tajwa na watu walio muona Imamu Almahdi(a.s) .

Na kitabu hiki kimechapwa mwishoni mwa juzuu ya khamsini na tatu ya Biharul-anwari.

Hata baadhi ya wanazuoni wa Ahlusunnah, walikiri kuwa walimuona Imamu Almahdi(a.s) , miongoni mwao ni: Asshekhe Hasani Al-iraqi, kama alisema Abdulwahhabu Asshaarani, katika kibu chake cha: (Alyawaqiti wa Aljawahiri), pale alipo sema: mpaka itakapo kuwa dini ngeni kama ilivyo anza... hapo ndipo utangojwa ujio wa Almahdi(a.s) , ambaye ni katika watoto wa Imamu Hasani Al-askari(a.s) , na mazazi yake yalikuwa ni katika mwezi Shaabani tarehe 15, mwaka; 255 hijiria, nae ataendelea kuwa hai mpaka na kutana na Nabii Issa bin Maryamu(a.s) , hivyo umri wake mpaka sasa utakuwa miaka mia saba na sita. Hivi ndivyo alivyo niambia Asshekhe Hasani Al-iraqi, aliyezikwa katika baadhi ya miji inayo lindwa na Imamu Almahdi, pale alipo kutana nae, na pia bwana wangu Ali Alkhawasi [60] .

SEHEMU YA TATU; DALILI YA UIMAMU WAKE:

Dalili ya kwanza: Imamu (Kiongozi) wa waislamu nilazima awe Maasumu.

Na ushahidi juu ya hilo ni mambo ya fuatayo:

1 – Asiye kuwa Maasumu, maneno yake hayaaminiki, na nivigumu kutekeleza amri yake au hukumu yake, kwa sababu inawezekana akawa amekosea au kusahau, au kughafilika, au kusema uongo na kuto kuwa na maarifa. Hivyo hawezi kuwa chini ya maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ﴿٥٩ ﴾

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi [61] .

Kwani Mwenyezi Mungu mtukufu, ameiweka twa’a yake sawa na twa’a ya wenye madaraka, amabao ni Maimamu, kwa sababu ya kuto kuwa na makosa.

2 – Asiye kuwa Maasumu, anaidhulumu nafsi yake, kwa kufanya maasi, kwani kila mwenye kufanya maasi, anaidhulumu nafsi yake, kwaminajili hiyo hafai kuwa Imamu (kiongozi), kwa mujibu wa maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu, pale aliposema:

قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾

Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu[62] .

Aya ilipotaja, kujidhulumu, inakusudia kujidhulumu mwenyewe, au kumdhulumu mwengine, na mana ya Ahadi, ni uimamu, kwa ushahidi wa maneno yaliyo tangulia katika Aya tajwa.

3 – Uimamu (uongozi) ambao dini au kunyoka mambo ya waislamu, vya tegemea Uimamu huo, hauwezi kupewa mtu ambaye, hukosea au kupatia, kwa sababu kufanya hivo, kutasababisha kubadilika sheria za dini, kwa kadiri watakavyo kuwa wakibadilika Maimamu. Kwa sababu hiyo, ndio mana Mwenyezi Mungu, aliwafanya mitume kuwa Maasumina, na kuwa epusha na makosa, kwa kuwa wao ndio wafikishaji wa Dini na sheria, na ili Dini ihifadhike na kubaki daima.

Baada ya kufahamika yote hayo, tunasema: Hakika Uimamu (uongozi), upo kwa Imamu Almahdi(a.s) , kwa sababu yeye ameepushwa na madhambi ya kila aina, kwa mujibu wa maneno ya mtukufu mtume(s.a.w.w) , pale aliposema:

(يملؤها قسطاً و عدلاً بعد ما ملئت ظلماً وجوراً)

Ataeneza uadilifu na usawa duniani, baada ya kujaa uovu na uonevu[63] .

Alisema Barzanji: Ama kuhusu isma ya Mahdi, ipo katika hukumu yake.

Kisha akasema: Imamu Mahadi, anahukumu kwa kile anacho funuliwa na malaika kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Malaika ambaye alitumwa kumuongoza, na hiyo ndiyo sharia ongofu ya mtume Muahammadi, sheria ambayo, hata yeye angekuwa hai asinge hukumu kinyume na sheria hiyo... hayo aliyasema mtukufu mtume akimsifia kuwa:

(يقفو أثري لايخطئ)

Atafuata nyayo zangu bila kukosea. Hivyo tukafahamu kuwa; yeye ni mfuasi, na si mwenye kuongeza sheria, na kwamba ni Maasumu. Na haina maana awe maasumu katika hukumu, bila kuwa Maasumu katika makosa. Kwani hukumu ya Mtume, hainasibishwi na makosa, kwa sababu yeye hatamki kwa matamanio, bali ni ufunuo ulio funuliwa[64] .

Kwaminajili hiyo, ndio maana tukasema kuwa; Al’imamu Almahdi ni Maasumu, na kwamba yupo katika zama hizi, kama ambavyo uwepo wake unabaibisha uimamu wake, kwa sababu umma unakubali kuwa hakuna mwengine, mwenye sifa ya kuwa Maasumu katika zama hizi, ghairi yake, na maasumu hutangulizwa juu ya asiye kuwa maasumu, vinginevyo, tutakosa Imamu katika zama hizi, jambo amalo halikubaki.

Dalili ya pili: Imamu wa waislamu (kiongozi), ni lazima awe ameteuliwa kwa aya na hadithi;

Ushahidi juu ya hilo ni:

1 - Imethibiti kuwa; ni sharti Imamu awe maasumu, na isma ni swala la kinafsi, hawezi kulifahamu kila mtu, hivyo basi ni lazima ateuliwe na ambaye anayajua yaliyofichika vifuani na nyoni, ambaye ni Mwenyezi Mungu mtukufu.

2 – Kuacha kumteua kiongozi (Imamu), kuta fungua mlango wa Mifarakano na marumabano, kama ilivyo tokea katika Saqifah bani Saidah, (kwa madai kuwa mtukufu Mtume hakuteua kiongozi). Marumbano hayo haya kuishia hapo, bali yaliendelea mpaka leo hi, ambapo ni kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu katika Qur’ani pale alipo tutaka kuwa pamoja, na kushikamana, kwa kusema:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ﴿١٠٣ ﴾

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane [65] .

Pia akasema: { لا تَنازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَ تَذْهَبَ ريحُكُمْ} Wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu[66] .

Hivyo hafai kwa Mwenyezi Mungu kuwafungulia waislamu mlango wa mizozano na mifarakano, kwa kuwaacha waislamu wajichagulie kiongozi.

3 – Kuteua Kiongozi kinyume na uteuzi wa Mwenyezi Mungu, kutapelekea kumteua Kiongozi asiyefaa, kwa sababu maranyingi huteuliwa kwa kuangalia maslahi binafsi, kufuata matamanio ya nafsi, au ubaguzi.

Hivyo kumuacha aliye bora, kama atakuwa mkali katika haki, au kuto kuwa na mali, Wasaidizi, na ukoo.

Hayo yote ni kama watu watamjua ni nani mbora, lakini, kuna wakati wanashindwa kujua ni nani bora, hususani kama atakuwa ya tukio la kumteua kiongozi huyo.

Kwaminajili hiyo, haifai kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, awaachie watu swala muhimu la kumteua kiongozi, ambao wengi wao amewataja katika Qur’ani kwa sifa mbaya kwa kusema:

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ﴿١١٦﴾

Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu [67] .

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾

Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi [68] .

وَأَكْثَرُهُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ ﴿٧٠﴾

Na wengi wao wanaichukia Haki [69] .

Hivyo hakuna njia zaidi ya kumuainisha kiongozi, kwani Mwenyei Mungu mtukufu, ndiye anaye jua maslahi ya viumbe wake, na nani anayefaa kuwa kiongozi, na kuwaongoza.

4 – Uimamu (Uongozi), ni khilafa ya Mwenyezi Mungu na mtume wake, hivyo basi, uongozi huo hauwezi kupatikana isipokuwa kwa uteuzi wao. Na ama uteuzi utakao fanyika kinyume na uteuzi wao, utakuwa kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

5 – Qur’ani tukufu imebainisha kwa uwazi kuwa; Mwenyezi Mungu ndiye anayemteua nabii, imamu, waziri au khalifa, wala hatujaona aya hata moja katika Qur’ani, inayosema kuwa; uteuzi huo umeachwa kwa watu.

Ama ushahidi wa kuteuliwa manabi katika Qur’ani, ni pale aliposema Mwenyezi Mungu mtukufu katika aya zifuatazo:

اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنبِيَاءَ ﴿٢٠﴾

Kumbukeni Neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu, alipo wateuwa Manabii kati yenu [70] .

وَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَكُلًّا جَعَلْنَا نَبِيًّا ﴿٤٩﴾

Tulimpa Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja tukamfanya Nabii [71] .

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا وَإِبْرَاهِيمَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِمَا النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ ﴿٢٦ ﴾

Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu [72] .

اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ﴿١٢٤﴾

Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake [73] .

إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧﴾

Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume [74] .

Ama dalili kuhusu kumteua khalifa, au waziri, zinapatikana katika aya zifuatazo:

يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ ...﴿٢٦﴾

Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi [75] .

وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ﴿٣٠﴾

Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi) [76] .

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾

Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amri yetu. Na tukawafunulia watende kheri, na washike Sala, na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu Sisi tu [77] .

قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي قَالَ لَا يَنَالُ عَهْد ِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾

Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu[78] .

وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ ﴿٢٤﴾

Na tukawafanya miongoni mwao waongozi wanao ongoa watu kwa amri yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na Ishara zetu [79] .

Baada ya kufahamika hayo, tunasema kuwa; Hakika imamu Almahdi(a.s) kama atakuwa ndiye Imamu mteuliwa katika zama hizi, basi itathibiti kinacho kusudiwa. Na kama tutasema kuwa; hajazaliwa, na kwamba hayupo, ukiachia mbali kuteuliwa, basi inabidi tukubali kuwa zama hizi hazina kiongozi, kwa sababu ghairi ya imamu Mahdi, hakuna mwenye sifa ya kuwa kiongozi wa zama hizi. Na kubaki zama bila kuwa na kiongozi, ni kinyume na itifaki ya waislamu wote.

DALILI YA TATU: Ni hadithi ya vizito viwili; ambayo ime pokewa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuwa:

(إنّي تركت فيكم الثقلين، ما إن أخذتم به لن تضلّوا بعدي: أحدهما أكبر من الآخر، كتاب الله حبل الله ممدود من السماء إلى الأرض، وعترتي أَهل بيتي، ألا وإنّهما لن يفترقا حتى يرد عليّ الحوض).

Hakika mimi nimekuachieni vizito viwili, kimoja ni kikubwa kuliko chengine, kitabu cha Mwenyezi Mungu, kamba iliyo nyoka kutoka mbingini mpaka ardhini, na kizazi cha nyumba yangu, kamwe hamta potea, madamu mta shikamana navyo, na hakika vizito hivyo kamwe havita tengana, mpaka vitanirejea katika hauzi[80] .

Hadithi hii inatuonyesha wazi, ulazima wa kushikamana na Imamu (kiongozi) Mwema, atokanae na nyumba ya Mtume(s.a.w.w) , na kwamba hata tofautiana na kitabu cha Mwenyezi Mungu, katika maneno yake na matendo yake, na yeye ndiye mwenye kuyafahamu maana za dhahiri na batini, za kitabu kitukufu.

Hivyo tunapo sema kuwa Imamu Mahdi yupo, maana yake, yeye ndiye kiongozi wa umma kwa zama hizi, vinginevyo hakuna mwengine anaye faa kushikwa, kutoka katika nyumba ya bwana Mtume katika zama hizi. Kwani umma umekubaliana kuwa; asiye kuwa yeye, anatofautiana na Qur’ani katika matendo yake na maneno yake, kutokana na kuwa si Maasumu.

DALILI YA NNE: wanazuoni wa kisunni, walitaja vigezo, ambavyo anatakiwa kuwa navyo khalifa wa waislamu, vigezo ambavyo anavyo Imamu Mahdi, kwa sababu yeye, ni katika makuraishi, kutokana na kwamba yeye ni katika kizazi cha Mtume(s.a.w.w) , Pia ni muadilifu, kwa mujibu wa maneno ya Mtume(s.a.w.w) pale aliposema: ( يملؤها قسطاً و عدلاً ), Ataeneza uadilifu na usawa duniani. Na kwamba yeye ni mjuzi wa wajuzi, kwa sababu atahukumu, kwa hukumu ya Mtume(s.a.w.w) , na wengine hawana sifa hizo, kama tulivyo taja huko nyuma.

Hivyo kama watasalimu kuwa yeye ndiye kiongozi mteule, basi itathibiti hoja yetu, na kama hawata salimu, basi ulimwengu utabakia bila Imamu, kwa sababu Ahlusunnah, hawana khalifa mwenye sifa za kuwa kiongozi, lakini pia Mashia, zaidi ya kuamini kuwa, imamu mahdi ndiye mwenye sifa hizo. Na kubakia zama bila kuwa na kiongozi, nikinyume na itifaki ya waislamu wote duniani.

DALILI YA TANO: kama Imamu Mahdi, hata kuwa Imamu wa zama, basi vifo vya waislamu wote, vitakuwa vya kijahili, hivyo umma mzima kuwa katika makosa, kitu ambacho ni batili, na hakikubaliki kwa wote, kwa sababu imesihi kwa wo te hadithi isemayo: ( لاتجتمع أمتي على ضلالة أو خطأ) , umma wangu hawezi kukosanyika katika upotevu au makosa.

Shubhat na jibu lake:

Waweza kusema kuwa: Imamu Almahdi, hajazaliwa, na wala hayupo, bali atazaliwa mwishoni mwa zama (akheri zamani), na si Muhammadi bin Hasani Al-askari, kama wanavyo dai Mashia.

JIBU LAKE:

1 – Tulithibisha huko nyuma, kuzaliwa kwake, na kuwepo kwake, na kwamba yeye ndie kiongozi wa zama hizi, vingine itatulazimu kuyakubali yote tuliyo yakanusha huko nyuma.

2 – Wanazuoni wengi wa kisunni, wamekiri kuwa; Almahdi anaye kusudiwa, ni Muhammadi Ibni Hasani Al-askari(a.s) , na kwamba bado yupo mpaka sasa. Itikadi hiyo, pamoja na kuwa inapingana , na itikadi ya wanazuoni wengi wa kisunni, hawakuacha kuitaja katika vitabu vyao, kwa kuwa ndiyo itikadi sahihi isipo.

Na miongoni mwa wanazuoni hao ni:

1 – Muhammdi bin Twalha Alsshafi’i: (582 – 652 hijiriya): katika kitabu chake (Matwalibu Assauli), malango wa kumi nambili, Alisema; Muhammadi bin Hasani Al-askari(a.s) , huitwa; Almahdi Alhujjah Alkhalafu Asswalehe.

Kisha akasema: Ama kuhusu mazazi yake; ilikuwa; tarehe ishirini na tatu, mwaka 258, hijiriya.. kisha akanukuu baadhi ya hadithi zinazo husu kuzaliwa kwake, kisha akataja baadhi ya shubuhati na kuzijibu.

2 – Muammadi bin Yusufu bin Muammadi Alkanji Asshafi’i( [81] ) (alifariki;658 hijiriya): katika mlango wa mwisho wa kitabu chake cha: (Albayani fi Akhbari Swaahibu Alzzamani): alitaja ushadi juu ya bakia hai Al-imamu Almahdi, tangu alipo toweka (ghaibah).

3 – Ali Ibni Muhammadi, afahamikae kwa; ibu Alswabbaghu Almaaliki( [82] ) (784 – 855): katika mlango wa kumi na mbili wa kitabu chake cha (Alfusulu Almuhimmah), Alisema kuwa: Abu Muhammadi Alhasani Al-askari, aliacha mtoto mmoja, ambaye ni; Alhujjah Alqaaimu, anayegojwa kusimamisha dola ya haki. Na alikuwa ameficha kuzaliwa kwake, kutokana na ugumu wa mazingira ya wakati ule, na kuhofia asiuliwe na wafalme wa zama zile[83] .

4 – Sibtwi Ibuni Aljauzi: katika; Tadhkiratul-khawaasu, malngo maalumu wa Imamu Almahdi, Alisema kuwa ni: Muhammadi Ibni Alhasani, Ibni Ali, bin Muhammadi, bin Ali, bin Musa Alriza, Ibni Jaafar, bin Muhammadi, Ibni Ali, Ibni Alhusaini, Ibni Ali, Ibni Abi Twalibi(a.s) , na kuniya yake, ni: Abulqaasimu, ambaye ni Alkhalafu Alhujjah, Swaahibu Alzzamani, Alqaaimu, Almuntazari, naye ndiye mwisho wa maimamu. Hivyio ndivyo alivyo tueleza Abdul-azizi Ibni Mahmudu Albazzazi, kutoka kwa ibun Amru, kutoka kwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuwa alisema:

(يخرج في آخر الزمان رجل من ولدي، اسمه كاسميو، وكنيته ككنيتي، يملأ الأرض عدلاً كما ملئت جوراً)

Katika zama za mwisho, atatokea mtu atokanae na kizazi changu, jina lake ni kama jina langu, na kuniya yake ni kama ya kwangu, Ataeneza uadilifu na usawa duniani, baada ya kujaa uovu na uonevu, huyo ndiye Mahdi.

Hadithi hii ni mashuhuri... mpaka mwisho wa maneno yake[84] .

5 – Abdulwahhabu Assha’arani[85] (892 – 973hijiriya): Aliyataja hayo katika mlango wa sitini na tano, wa kitabu chake cha (Alyawaakiti wa Aljawahir fi Aqaaidi Al-akabir).

6 – Muhyi Alddini ibun Arabi (560 – 638 h): katika kitabu chake cha (Alfutuhati Almakkiyah), mlango wa mia tatu na sitini nasaba, alisema kuwa: tambueni kuwa; Almahdi(a.s) , ni lazima atatokea... nae ni katika kizazi cha mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , katika wana wa Fatwima (radhi za mola ziwe juu yake). Babu yake ni Huseini Ibni Ali, Ibni Abi Twalibi (radhi za mola ziwe juu yao). Na baba yake ni Hasani Al-askari, Ibni Imamu Ali Alnnaqiyu, Ibni Imamu Muhammadi Altaqiyu, Ibni Imamu Ali Alriza, Ibni Imamu Musa alkadhwimu[86] .

7 – Alhafidhu Khawaja Barsaa: katika kitabu chake cha (Faswilu Alkitwabu) Alisema kuwa: miongoni mwa maimamu wa Ahlulbayti wa toharifu, ni; Abu Muhammadi Alhasani Al-askari. Alizaliwa siku ya jumaa,tarehe; sita, mwezi wa; tatu, mwaka mia mbili thelathini na moja. Alizikwa pembeni ya baba yake... Aliacha mtoto mmoja ambae ni; Abalqaasimu, Muhammadi, Almuntadhwir. Ambae huitwa pia; Alqaaimu, Alhujjah, Almahadi, Swahibu alzzamani. Na ndie Mwisho wa maimamu kumi na mbili, kwa Mashia. Imamu huyo, alizaliwa tarehe; kumi na tano, mwezi; Shaabani, Mwaka; mia mbili khamsini na tano. Baba yake alifariki, akiwa na miaka mitano. Na Mama yake anaitwa; Narges, amabae alifahamika kwa; Ummu waladi. Abu Muhammadi; Alhasani Al-askari, na mwanae Muhammadi Almuntadhwir Almahdi (radhi za mola ziwe juu yao), ni maarufu kwa watu wa zama zile[87] .

8 – Swalahu Alddini Alsswafadi (797 – 764 hijiriya): Kunduzi katika kitabu chake cha; Yanaabiu Alisema kuwa: Alsshekh Alkabir Alkamil, mjuzi wa siri za herufi, Swalahu Alddini Alsswafadi katika kitabu cha; Sharhu Alddairah Alisema kuwa: Hakika Mahdi mtarajiwa, ni Imamu wa kumi na mbili, katika maimamu kumi na wa wili, ambapo wa kwanza kati yao ni, Bwana wetu Ali, na wa mwisho wao ni; Almahdi, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na kutunufaishe nao[88] .

9 – Muhammadi Ibni Ali Twuluni (880 – 953 hijiriya): katika kitabu chake cha (Al-aimatu Al-ithna Asharah), Alielezea kuhusu uwepo wa Imamu Almahdi, kwa Mashairi, ambayo ni:

عليك بالأئمة الاثنى عشَر من آل بيت المصطفى خير البشر

أبو ترابٍ، حسنٌ، حسينُ وبغضُ زينِ العابدين شين

محمدُ الباقر كم علمٍ درى والصّادق ادعُ جعفراً بين الورى

موسى هو الكاظم وابنه علي لقِّبه بالرضا وقدره علي

محمد التفيُّ قلبه معمور عليُّ النقيُّ دُرُّه المنثور

والعسكريُّ الحسن المطهَّر محمد المهديُّ سوف يظهر

Shikamana na Maimamu kumi na mbili watokanao na nyumba ya Mtume mbora wa vimbe.

Abu Turabu (Ali bin Abi Twalibi), Hasani, Huseini Na kumchukia Zainul-abidina ni vibaya.

Muhammadi Albaaqir, ni kiasi gani alikuwa na elimu Na Alsswadiq, aliyefahamika kwa viumbe Jaafar.

Musa Alkadhwimu na Mwanae Ali Ambae aliitwa Alrrizaa, na kadari yake ni Ali.

Muhammadi Altaqiy, Ali Annaqiy.

Na Al-askari Alhasani Almutwahharu Muhammadi Almahdi, ambae atadhihiri[89] .

10 – Sulaymani Alqunduzi Alhanafi: Hakika yeye katika kitabu chake cha; ( Yanaabiu Almawaddah) alijitahidi kuthibitisha kuwa Almahdi, mtarajiwa, ndie Muhamaadi Ibni Hasani Al-askari(a.s) . Na aliweka milango mbali mbali kwaajili ya kuthibitisha hilo, miongoni mwa milango hiyo ni; Mlango unaotaja mazazi ya Almahdi. Pi Mlango wa karama zilizo zidhihirika kwa watu, na kwamba baba yake Al-imamu Al-askari, aliwaonyesha baadhi ya Mashia wake mwanae Almahdi, na kuwajulisha kuwa yeye ndie atakuwa Imamu baada yake. Na mlango mwengine, ni kuhusu waliomuona Almahdi baada ya kutoweka. Na mlango wa mwisha, alitaja Maneno ya wanazuoni, yanayothibisha kuwa; Almahdi mtarajiwa ni mwana wa Al-imamu Alhasani Al-askari(a.s)[90] .

Almirza Huseini Annuri, katika kitabu chake cha (Kashfu Al-astaari), alitaja majina arobaini ya wanazuoni wa kisunni, ambao aliuta katika vitabu vyao kuwa; Al-imamu Muhammadi Ibni Alhasani Al-askari(a.s) , ndie Almahdi Almuntadhwar[91] .

3 – Hakika baadhi ya Masunni, walikiri kumuona Al-imamu Almahdi, na kuonana nae. Miongoni mwao ni; Asshekh Hasani Al-iraqey, kama tulivyo taja huko nyuma, kutoka kwa Abdulwahhabu Alssha’araani, katika kitabu chake cha: ( Alyawakitu wa Aljawahir).

TIJA: Ni kwamba; Al-imamu Almahdi, Muhammadi Ibni Alhasani Al-askari(a.s) , ndie Imamu (kiongozi) wa zama hizi, kwa mujibu wa dalili Sahihi tulizo zitaja huko nyuma. Ama wengine, hatuna ushahidi wa kuthibitisha uongozi wao.

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

USAHIHI WA HADITHI SAHIHI JUU YA KUZALIWA AL-IMAMU ALMAHDI

Kuna bwana mmoja, aliye jiita ( Ahmadi Alkatibu), alidai katika baaadhi ya vituo habari kuwa: hakukuta dalili hata moja ya kihistoria, inayothibisha kuzaliwa kwa Al-imamu Almahdi, Muhammadi Ibni Hasani Al-askari(a.s) . Na anacho kikusudia kunako dalili ya kihistiria, ni; hadithi sahihi zinazo thibisha kuzaliwa kwake, hatakama zitakuwa za kishia. Huku akiwa amejitia kuto zifahamu dalili za kiakili, zinazo thibitisha kuzaliwa kwake na kuwepo kwake. Lakini alidai kuwa aliwaomba wanazuoni wa kishia wamthibitishie hilo, lakini hakuma yeyote aliye jitokeza.

Ingawaje madai yake ni ya uongo, kwani yeye hana Maarifa yoyote juu ya hadithi sahihi. Nasi tutamthibishia uongo wake, ili wasije wakadanganyika baadhi ya watu na uongo wake; kwakusema:

1 - katika kuthibisha kuzaliwa kwa Imamu Almahdi, inabidi tuchukuwe hadithi sahihi, na wala hatupaswi kutosheka na dalili za kihistoria tu, kwa sababu kila dalili sahihi tunapaswa kuikubali, wala hatuna sababu ya kuzitangulizaa dalili za kihistoria juu ya zingine. Na mazazi ya Swahibu Alzzamani, yamethibiti kwa dalili mbali mbali sahihi. Ambazo za tosha kwa mwenye moyo salama, na kuwa tayari kuzipokea.

2 – Dalili zingine, zaweza kuwa za kiakili tu, au zilizo changanyika kati ya dalili za kiakili na za kihadithi, dalili hizo, ndizo zenye kutangulizwa kuliko dalili za kihistoria, kwa sababu baada ya kuthibiti dalili za kiakili, hakuna haja ya dalili za kihistoria zisizo za uhakika.

3 – Mazazi ya mtu hayathibiti kwa historia tu, kwani kama ingekuwa hivo, tusinge kubali mazazi ya watu wengi maarufu katika historia, kwani mazazi yao hajathibiti katika historia thabiti, na mutawatir.

4 – Watu wote wanapo taka kuthibitisha mazazi ya mtoto, hurejea kwa baba wa mtoto, hivyo kama atawathibitishia kuzaliwa kwake, hata kwa riwaya moja sahhihi, kuwa anamtoto, hatunabudi kumsadiki na kukiri. Na tutakuja kuthibisha huko mbeleni kuwa; Al-imamu Al-askari, alikiri kuwa anamtoto.

5 – Maneno ya wanazuoni na waumini wema,ya kuwa walimuona katika matukio mbali mbali, yatosha kuwa ushahidi wa kuzaaliwa kwake. Na tulitaja huko nyuma, kuwa; Almirza Alnnuri katika kitabu chake cha (Jannatu Alma’awa fi dhikri Man fazaa bi Liqaai Alhujjah), alikusanya majina khamsini na tisa, ya watu waliomuona Al-imamu Almahdi(a.s) .

Lakini pia tulitaja kutoka kwa; Asshekh Abdulwahhab Alssha’arani, katika kitabu chake cha; (Alyawaqitu wa Aljawahir), wanazuoni wengi wa kisunni, waliokiri kumuona Al-imamu Almahdi.

Je baada ya yote hayo, inafaa kwa mwenye busara, kuyakathibisha yote hayo, ukizingitia kwamba miongoni mwa wazuoni hao, ni masunni.

6 – Dalili za kihadithi, ambazo Ahamadi Alkatibu, alizitaja kuwa ni zakihistoria, ili kukadhibisha kuzaliwa kwa Al-imamu Al-mahdi, zinathibisha kuzaliwa kwa Imamu huyo, nazo twaweza kuzigawa katika makundi tofauti:

KUNDI LA KWANZA: hadithi zinazo thibisha kuwa Almahdi ni mtoto wa tisa wa Imamu Huseini(a.s) .

Amepokea Swaduqi, katika kitabu cha: Alkhiswalu wa kamalu Alddini, kwa sanadi sahihi, kutoka kwa baba yake, alisema: Alituahadithia Sa’adu Ibni Abdallah, kutoka kwa Yaaqubu Ibni Yazidi, kutoka kwa Hammaadi Ibni Isa, kutoka kwa Abdallah Ibni Maskaani, kutoka kwa Abaani Ibni Taghlibu, kutoka kwa Sulaymu Ibni Qaisi Alhilali, kutoka kwa Salmani Ibni Farisi kuwa alisema: " Siku moja niliingia kwa mtume(s.a.w.w) , mara Huseini akawa amekaa juu ya mapaja ya mtume (s.a.w.w), huku mtume akiyabusu macho na midomo yake akisema:

أنت سيِّد ابن سيِّد، أنت إمام ابن إمام أبو الأئمة، أنت حجة ابن حجة أبو حُجَج تسعة من صلبك، تاسعهم قائمهم)

"Wewe ni bwana mtoto wa bwana, wewe ni Imamu mtoto wa Imamu na baba wa maimamu, wewe ni hojjah mtoto wa hojjah na baba wa mahojjah tisa watokanao na kizazi chako, watisa wao ndie Qaaimu wao"[92] .

Pia Kulayni katika kitabu Alkafi, amepokea hadithi sahihi, kutoka kwa Ali Ibni Ibrahimu, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Umairi, kutoka kwa Saidi Ibni Ghazawani, kutoka kwa Abu Baswiri, kutoka kwa Abu Jaafari(a.s) kuwa alisema:

(يكون تسعة أئمة بعد الحسين بن علي، تاسعهم قائمهم)

"Baada ya Huseini Ibni Ali(a.s) , wata kuwa maimamu ( viongozi) tisa, watisa wao ni Al-imamu al-mahdi".

Shekhe Swaduq kati Akhiswali, amepokea hadithi yenye sanadi na matini kama hiyo hiyo, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ali ibni Ibrahimu[93] .

NATIJA: Nikwamba Sanadi za hadithi hizi ni sahihi, nazo zinathibisha kwa uwazi kabisa kuwa; Almahdi ni mtoto wa tisa wa Imamu Huseini(a.s) , na Imamu Huseini hana mtoto wa tisa anaefaa kuwa Imamu, zaidi ya Imamu Almahdi, Muhammadi Ibni Hasani Al-askari(a.s) .

KUNDI LA PILI: hadithi zinazo thibisha kuzaliwa kwa Imamu Almahdi, Muhamadi Ibni Hsani Al-askari(a.s) .

Amepokea Kulaini, katika Alkafi, kutoka kwa Huseini Ibni Muhammadi Al-ash’ari, kutoka kwa Muala Ibni Muhammadi, kutoka kwa Ahmadi Ibni Abdallah kuwa; Alisema: alitoka kwa Abu Muhamadi(a.s) , pindi alipo uliwa Zubair ( laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) huku akisema; haya ndio malipo ya aliemfanyia ujasiri Mwenyezi Mungu kwa mawalii wake, aliekuwa akidai kuwa ataniua, na kwamba sina mtoto, Mwenyezi Mungu kamuonyesha uwezo wake. Akapata mtoto mwaka wa mia mbili khamsini na sita, aka mwita Muhammadi[94] .

Pia Kulaini alipokea katika Alkafi, kutoka kwa Ali Ibni Muhammadi, kutoka kwa Muhammadi Ibni Ali Ibni Bilali, kuwa Alisema: siku moja Abu Muhammadi alinijulisha kuhusu atakae kuwa baada yake, kabla ya kumalizika miaka miwili. Kisha kabla ya kupita siku tatu, akanijulisha pia atakae kuwa baada yake.

(و روى أيضاً في الكافي بسند صحيح، عن محمد بن يحيى، عن أحمد بن إسحاق، عن أبي هاشم الجعفري قال: قلت لأبي محمد×: جلالتك تمنعني من مسألتك، أتأذن لي أن أسألك؟ فقال: سل. قلت: يا سيّدي هل لك ولد؟ فقال: نعم. فقلت: فإن حدَثَ بِكَ حدَثٌ فأين أسأل عنه؟ فقال: بالمدينة).

" Pia Kulaini (Mungu amrehemu) katika kitabu chake cha Alkaafi, Alipokea kwa Sanadi sahihi, kutoka kwa Muhammadi ibni Yahya, kutoka kwa Ahmadi Ibni Is’haqa, kutoka kwa Abi Hashimu Aljaafari kuwa alisema: nili mwambia Abu Muhammadi(a.s) : utukufu wako unanifanya nishindwe kukuuliza, je unaniruhusu ni kuulize? Akasema: uliza. Nika muuliza: bwana wangu, je unamtoto? Akanijibu: ndio. Nikamuuliza: je kama litakukuta la kukuta, nitamtafutia wapi? Akajibu: mtafute mjini" [95] .

KUNDI LA TATU: hadithi zinazo thibisha kuwa baadhi ya watu walimuona:

Hadithi hizo ni nyingi mno, na sanadi zake ni sahihi. Miongoni mwa hadithi hizo, ni ile iliyo pokewa na Kulaini katika Alkaafi, kutoka kwa Muhammadi Ibni Abdallah na Muhammadi Ibni Yahya, kutoka kwa Abdallah Ibni Jaafar Alhimyari, kuwa alisema:

"Siku moja, nilikuwa na Alshekh Abu Amru (Mungu amrehemu) kwa Ahmadi Ibni Is’haqa, akaniashiria kuwa; ni muulize Abu Amru kunako Almahdi, nami nikamuuliza: ewe Abu Amru, hakika mimi nina taka nikuulize kitu, ambacho sina mashaka nacho, kwani imani yangu ni kuwa; Ardhi haikosi Hojja, mpaka zibakie siku arobaini kabla ya kiyama, hapo ndipo Mwenyezi Mungu ata muondosha na kufunga mlango wa toba, hivyo haito faa imani ya mtu, ambaye hakuwa ame amini kabla ya hapo. Hao ndio viumbe washari zaidi, na hao ndio watakao pata adhabu kali mno. Lakini mimi nilipenda nizidi imani, kwani hata Ibrahimu, alimuomba Mwenyezi Mungu mtukufu, Amuonyeshe vipi anavyo wa fufua wafu. Mwenyezi Mungu aksema: kwani huamini? Akasema: Hasha, lakini ili moyo wangu utue. Hakika aliniambia Abu Ali Ahamadi Ibni Is’haq, kutoka kwa Abu Alhasani(a.s) kuwa alimuuliza: kwa nani nichukue hadithi, na nani ni amiliane nae, na kukubali maneno yake? Akamjibu: Al-amri, ni mkweli kwetu, hivyo atakacho kwambieni kutoka kwangu, basi kimetoka kwangu, msikilize na umtii, kwa hakika yeye ni mkweli muaminifu. Pia aliniambia Abu Ali kuwa; alimuuliza Abu Muhammadi(a.s) swali kama hilo, akamjibu: Al-amru na mwanae ni wakweli, hivyo watakacho kufikishia kimetoka kwangu, na watakacho kwambia, kimetoka kwangu, wasikilize na uwatii, kwa hakika wao ni wakweli waaminifu. Haya ni maneno ya maimamu wa wili. Muulizaji akasema: Abu Amru baada ya kusikia maneno hayo, alisujudu na kulia, kisha akasema: uliza. Nikamuuliza: Je uliwahi kumuona Imamu Almahdi, kiongozi baada ya Abu Muhammadi(a.s) ? akajibu: ndio. Nikamwambia: limebaki swali moja. Akaniambia: uliza. Nikamuuliza: ni lipi jina lake? Akaniambi: mmekatazwa kuuliza jina lake, haya siyasemi kutoka kwangu, kwani mimi sina haki ya kuharamisha au kuhalalisha, bali nayasema haya kutoka kwake(a.s) , kwa sababu mfalme anadai kuwa Abu muhammadi Alifariki bila mtoto... hivyo kama jina lake litatajwa, wataanza kumtafuta, hivyo muogopeni Mwenyezi Mungu, na acheni kuuliza juu hya hilo" [96] .

Vile vile amepokea kuleyni katika Alkaafi, kwa Sanadi sahihi kutoka kwa Ali Ibni Muhammadi, kutoka kwa Muhammadi Ibni Ali Ibni Ibrahimu, kutoka kwa Abu Adallah Ibni Swaaleh kuwa: hakika yeye alimuona Almahdi(a.s) Mkkah, watu wakitufu katika hali ya kusukumana, nae asema: hivyo sivyo walivyo amrishwa[97] .

KUNDI LA NNE: hadithi zisemazo kuwa atatoweka, hivyo watu kushakia kuzaliwa kwake:

Amepokea kulayni katika Usulu Alkaafi, kwa Sanadi sahihi, kutoka kwa Ali Ibni Ibrahimu, kutoka kwa Alhasani Ibni Musa Alkhasshaab, kutoka kwa Abdallah Ibni Musa, kutoka kwa Abdallah Ibni Bukayri, kutoka kwa Zurara kuwa alisema: nili msikia Abu Abdallah akisema: hakika Almahdi atatoweka kabla ya kudhihiri. Akasema: nikamuuliza: kwa nini? Akanijibu: kwahofia kuuliwa. Kisha akasema: ewe zurara, huyo ndie Almuntadhwar, ambaye yatashukiwa mazazi yake. Kuna ambao watasema: baba yake alifariki bila kuacha mtoto. Na kuna wengine watasema: baba yake alifariki kabla ya kuzaliwa. Na miongoni mwao kuna ambao watasema: alizaliwa miaka miwili kabla ya kufariki baba yake. Yeye ndie Almuntadhwar, isipo kuwa Mwenyezi Mungu atawatahini Mashia, hapo ndipo watajulikana wakweli...[98] .

Pia katika Usulu Alkaafi, kwa sanadi sahihi, kutoka kwa Ibni Yahya, kuto kwa Muhammadi Ibni Huseini, kutoka kwa Ibni Mahbub, kuto kwa Is’haaq Ibni Ammar, alisema kuwa: alisema Abu Abdallah(a.s) : Alqaaimu atatoweka mara mbili: mara ya kwanza; atachukua muda mfupi, na mara nyingine; atachukua muda mrefu. Kutoweka kwa kwanza, hawata fahamu isipo kuwa Mshia wake maalumu. Na kutoweka kwa pili, hawata fahamu sehemu yake isipo kuwa wafuasi wake maalumu[99] .

Kundi la sita: hadithi zinazo thibitisha kuwa; Almahdi ndiye Alhujjah Ibni Alhasani Al-askari.

Amepokea Swaduuq katika (Kamaalu Alddini), kwa Sanadi Sahihi, kutoka kwa Ibni Alhasani (Mungu amrehem), kuwa alisema: alituambia Saadi Ibni Abdallah, alisema kuwa: alituambia Abu Jaafar Ibni Ahmadi A-alwi, kutoka kwa Abu Hashimu Daudi Ibni Alqaasimu Aljaafar, Alisema kuwa: Nilimsikia Abu Alhasani Swahibu Al-askari(a.s) akisema:

"kiongozi baada yangu ni mwanangu Alhasani... hamta muona, na hamruhusiwi kumuita kwa jina lake. Nika muuliza: tumwite je? Akanijubu: mwiteni: Alhujjah min Aali Muhammadi (s.a.w.w) " [100] .

Kutokana na yote yaliyo tangulia, tunaona kuwa: hakuna njia zaidi ya kuhukumu kuwa; Al-imamu Muhammadi Ibni Alhasani Al-askari, alisha zaliwa. Hayo ni kwa mujibu wa hadithi Sahihi tulizo zitaja baadhi yake. Ambazo zime pokewa katika vitabu vya hadithi, ambavyo ni maarufu kwa mashia, kama vile Alkafi, Alttahadhibu, Al-istibswari, na Man La Yahbwuruhu Alfaqihi.

Hayo yote ni kwa mwenye kuzi amini hadithi za Ahlul Bayti(a.s) . Lakini pia akatumia njia sahihi katika kusahihisha hadithi, kama alivyo dai Ahmadi Alkatibu. Na kuzikanusha hadithi hizo, ni ubishi wa bili ushahidi.

4

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

SHUBUHATI ZINAZO HUSIANA NA ITIKADI YA MASHIA JUU IMAMU MAHDI (A.F)

Zimetolewa shubuha kadhaa kuhusiana na itikadi ya imamu Mahdi (a.f), hapa tutazitaja zile za muhimu zaidi na kuzitolea majibu kwa ufupi.

SHUBUHA YA KWANZA: kuhusu urefu wa umri wa Imamu Mahdi (a.f):

Shubuha hii inatokana na kauli ya Mashia isemayo kuwa Imamu Mahdi (a.f) alizaliwa mwaka 255h, kwa kuwa si kawaida ya mwanadamu kuishi zaidi ya miaka elfu moja. Kwa sababu hiyo, ndio maana kuendelea kuitikadia kubakia kwa Imamu Mahdi (a.f) kwa kipindi chote hiki kirefu, kumekuwa ni jambo linalotumiwa kuwahujumu na kuwashambulia mashia. Hata imefikia baadhi yao kusema:

“Haujafika wakati wa pango kumzaa - huyo mnaemwita kwa ujinga wenu, haujafika wakati? Hivyo basi mmeondokewa na akili; kwa kurefusha umri wa kuishi kwake”[101] .

MAJIBU YA SHUBUHA HII : yanabainika kwa mambo yafuatayo:

Jambo la kwanza: kubakia kwa Imamu Mahdi (a.f) muda wote huu ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, na uwezo wake unakishamili kila kinachowezekana, na jambo hili la Imamu kubakia muda mrefu kwa Mwenyezi Mungu linawezeka. Sio tu kuwa linawezekana, bali ukweli nikuwa limekwisha wezekana kama itakavyo kubainikia hivi karibuni. Hivyo, hakuna kiziwizi kinacho uzuia uwezo wa Mwenyezi Mungu kulishamili jambo hili, bali ilipaswa iwe hivyo; kwani uimamu upo kwake na sio kwa mwingine, kama tulivyo bainisha hilo huko nyuma.

Anasema Fakhru Dini Raazi: “Baadhi ya madaktari wanadai kwamba: umri wa mwandamu, hauwezi kuzidi miaka mia na ishirini”, lakini kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

(وَ لَقَدْ أَرْسَلْنا نُوحاً إِلى‏ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلاَّ خَمْسينَ عاماً)

“Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka khamsini”[102] , inaashiria na kuthibitisha kinyume cha madai yao. Na akili pia inakubaliana na aya hiyo; kwani kama isingekuwa hivyo, isingeli wezekana nabii Nuhu(a.s) akaishi muda wote huo. Ama sababu inayoweza pelekea mwaadamu kuishi na kubakia muda mrefu, inaweza ikawa ni Mwenyezi Mungu wenyewe, au kitu ambacho kinarejea kwake; kwani Mwenyezi Mungu ni mwenyekubakia milele, hivyo athari yake inaweza kubakia kwa muda autakao mwenyewe. Hivyo basi, bila shaka suala la kubakia muda mrefu na kuishi sana ni lenye kuwezekana”.

Anaendelea kusema kuwa: “Acha tuseme kwamba: hakuna mgogoro baina yetu na wao; kwani wao wanasema kuwa: “Umri wa kawaida hauzidi miaka mia na ishirini”. Na sisi tunawambia kuwa: umri wa nabii Nuhu, haukuwa wa kawaida, bali ilikuwa ni tunu na zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu. Ama kuhusiana na umri wa kawaida, kwa Imani yetu hauwezi kudumu hata sekonde chache kama Mwenyezi Mungu hakutaka, achilia mbali miaka mia moja au zaidi”[103] .

Nami niseme kuwa: bila shaka urefu wa umri wa Imamu Mahdi (a.j), sio kama umri wa watu wengine, bali upo inje ya ada na kawaida ya watu, isipokuwa umepatiakana kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu aliyetukuka na kutakasika, kama yalivyotokea mambo mengine mengi yaliyokuwa nje ya ada katika uhai wa manabii na mawalii wa Mwenyezi Mungu waliotangulia. Mambo ambayo waislamu wote licha ya hitilafu zao za kimadhehebu, wameafikiana kwamba yalitokea, kwa mfano: urefu wa umri wa nabii Nuhu(a.s) , kubaki kwa watu wa pangoni (as’haabul-kahaf) miaka mia tatu na tisa hali yakuwa wamelala, kuzaliwa kwa nabii Issa(a.s) bila ya baba, alivyoongea akiwa bado mtoto mchanga, kuponya kwake vipofu na wenye vibarango, kuwafufua wafu…. na mengineyo mengi ambayo hatuwezi kuyataja yote hapa.

Hivyo basi, kwakuwa uimamu na uongozi umejifunga kwa Imamu Mahdi katika zama zetu hizi kama ulivyokwishatangulia ufafanuzi wa hilo huko nyuma, na watu wetu wengi walimuona bayana, (na imamu ni lazima awepo kila zama), ndio maana tunasema kuwa umri wake mtukufu unapaswa kurefuka.

Jambo la pili: Hakika Mwenyezi Mungu aliyetukuka na kutakasika, amerefusha umri wa kundi kubwa la watu walioishi katika nyumati zilizopita kama ilivyotangulia katika aya ya surat Al-ankabut, ambayo imeonyesha kwamba nabii Nuhu(a.s) aliishi na watu wake akiwalingania kumwabudu mola wao kwa muda wa miaka elfu kasoro miaka hamsini. Vilevile nabii Adamu(a.s) aliishi miaka elfu[104] , watu wapangoni (as’haabul-kahaf) walibikia pangoni miaka mia tatu na tisa, kama alivyoishi Salmaani Al-faarsi miaka zaidi ya mia mbili na hamsini kwa mujibu wa kauli zote[105] .

Jambo la tatu: Hakika waislamu wanaamini uwepo wa watu wema tofauti na Imamu Mahadi (Amani iwe juu yake) walioibakia na kuishi kwa muda mrefu, kama vile: nabii Issa mwana wa Mariam (amani iwe juu yake) na Khidri, nabii Idirisa na Iliyasa (Amani iwe juu yao) kwa mujibu wa baadhi ya kauli, kama ambavyo wanaitakidi kubakia muda mrefu baadhi ya watu wasio wema, kama vile Dajaal.

Ama kuhusiana na nabii Issa (Amani iwe juu yake): Aya za kitabu kitukufu cha Qur’an zinaonyesha kuwa alinyanyuliwa mbinguni. Anasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا .بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٥٨ ﴾

“Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Issa, mwana wa Mariamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsulubu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima”[106] .

Vilevile, hadithi zilizopokelewa katika vitabu sahihi vya hadithi, zinaonyesha kwamba nabii Issa (Amani iwe juu yake) atakuja kuteremka kutoka mbinguni katika zama za mwisho. Kama ilivyo hadithi ya Muslim katika sahihi yake, kutoka kwa Abu Huraira alisema: “Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(والله لينزلنّ ابن مريم عدلاً حكماً، وليكسرنّ الصليب، و ليقتلنّ الخنزير،و ليضعنّ الجزية ...)

“Ninaapa kwa jina Allah kuwa, bila shaka mwana wa Mariam atateremka kutoka mbinguni ili aje kuwa mwamuzi mwadilifu (kati ya haki na batili), na kwamba atauvunja msalaba, atauwa nguruwe na kuweka kodi (kwa makafiri) ….”. Na kutoka kwa Abu Huraira pia, alisema: “Amesema mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(كيف أنتم إذا نزل ابن مريم فيكم، و إمامكم منكم؟!)

Vipi ninyi atakapokusha kwenu mwana wa Mariam hali ya kuwa imamu wenu yupo kati yenu? !”.[107]

Na wasomi wakubwa wa Ahli Sunna wamema waziwazi kuwa nabii Issa (Amani iwe juu yake) yuko hai na anaishi hadi wakati huu:

Anasema Ibni Hajar Al-asqaalani: “Hakika Issa(a.s) alinyanyuliwa mbinguni, na ukweli ni kuwa yeye yuko hai”.[108]

Ibni Kathiir anasema: “kinachokusudiwa na mlolongo wa aya hizi, ni kuonyesha kuwa nabii Issa(a.s) yupo hai mbinguni mpaka sasa, na sio kama walivyodai manasara kuwa alimsulubiwa. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake. Kisha kama zinavyo bainisha hadithi zilizopokelewa kwa wingi, atashuka duniani kabla ya siku ya Kiyama”.[109]

Anasema katika sehemu nyingine: “Hakika Mwenyezi Mungu alimnyanyua nabii Issa(a.s) kwake, anaishi na yupo hai, na kwamba atashuka duniani kabla ya siku ya Kiyama, kama zinavyo onyesha riwaya zilizopokelewa kwa wingi”.[110]

Bwana Qurtubi nae anasema: “Ukweli ni kuwa Mwenyezi Mungu alimnyanyua nabii Issa (a.s) mbinguni bila yakuwa amefariki wala kuwa usingizini kama alivyosema Alhasan na Ibni Zaidi. Na rai hii ndio chaguo la Tabari na ndio rai sahihi kutoka kwa Ibni Abbasi, na Dhahaku nae pia anaiunga mkono rai hii”.[111]

AMA KUHUSIANA NA KHIDRI: Rai mashuhuri ni kuwa yupo hai mpaka leo hii.

Anasema Nawawi: “Kundi kubwa la wasomi ni kuwa Khidri yuhai na yupo kati yetu. Katika jambo hili masufi na wana maarifa wameafikiana. Hikaya zao kuhusiana na kumuona Khidri, kukusanyika nae katika vikao, kujifunza kwake, kumuuliza maswali na kupata majibu kutoka kwake, kuwepo kwake maeneo matukufu na yakheri…, ni mengi sana kiasi kuwa hayawezi kuhesabika, na nimashuhuri kiasi kuwa hayawezi kufichika”.[112]

Sheikh Abu Amru Ibni Swalaah anasema: “Khidri yuhai kwa mtazamo wa kundi kubwa la maulamaa na watu wema, na Ahli Sunna wapo na nao katika hilo”. Anaendelea kusema: “Kwa hakika baadhi ya wasomi wa elimu ya hadithi ndio walio jitenga kwa kulipinga jambo hilo”.[113]

Anasema Qurtubi: “Sheikh wetu Imamu Abu Muhammad Abdul-mu’utwi Ibni Mahmud Ibni Al-mu’utwi Al- Lakhmi, katika kufafanua risala ya Al-qishiiri ametaja hikaya nyingi kutoka kwa watu wema, wake kwa waume kwamba: walimuona Khidri na kukutana nae, hikaya ambazo kwa ujumla ukikusanya na waliyo yataja Naqashi na Thaalabi, zinatupa dhana kuwa Khidri yupo hai”.[114]

Ama kuhusiana na nabii Idirisa(a.s) : baadhi ya wasomi wamesema kuwa yupo hai na anaishi.

Imepokelewa kutoka kwa Mujahidi kuhusiana kauli yake Mwenyezi Mungu:

(وَ رَفَعْناهُ مَكاناً عَلِيًّا)

“Na tulimuinua daraja ya juu”[115] , kwamba alisema: “Nabii Idirisa(a.s) aliinuliwa (mbinguni) kama alivyoinuliwa nabii Issa(a.s) wala hajafariki”[116] .

Ama kuhusiana na nabii Iliyasa(a.s) : kwa mujibu wa baadhi ya kauli, yuhai wala hajafariki.

Ibni Asaakir amepokea kutoka kwa Ka’ab (Allah awe radhi naye) kwamba alisema: “Manabii wanne mpaka leo hii wako hai: wawili wapo aridhini: Iliyasa na Khidri(a.s) , na wawili wapo mbunguni: Issa na Idirisa(a.s)[117] .

Vilevile, amepokea Hakimu Nisaabouri katika kitabu chake cha Mustadrak, kutoka kwa Anasi Ibini Maaliki (Allah awe radhi naye) kwamba alisema:

(كُنَّا مَعَ رسول الله صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سفر ، فنزلنا منزلًا ، فإذا رَجُل فِي الوادي ، يَقُولُ : اللَّهُمَّ اجعلني من أمة مُحَمَّد المرحومة المغفور لَهَا المتاب عليها قَالَ : فأشرفت عَلَى الوادي ، فإذا رَجُل طوله أكثر من ثلاث مائة ذراع ، فقال لي : من أنت ؟ قلت : أَنَا أنس بْن مالك خادم رسول الله صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : فأين هُوَ ؟ قلتُ : هُوَ ذا يسمعُ كلامك قَالَ : فأته ، وأقرئه مني السلام وقل لَهُ : أخوكَ إلياس يقرئك السلام فأتيتُ النَّبِيّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فأخبرته ، فجاء حتى لقيه فعانقه وسلم عَلَيْهِ ، ثُمَّ قعدا يتحدثان ، فقال : يا رسول الله إنّما آكل فِي السنة يومًا ، وهذا يوم فطري ، فآكل أَنَا وأنت فنزلت عليهما مائدة من السماء عليها خبز وحوت وكرفس فأكلا وأطعماني ، وصليا العصر ، ثُمَّ ودعته ، ثُمَّ رأيته مر عَلَى السحاب نحو السماء).

“(Siku moja) tulikuwa safarini na mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , tukawa tumepumzika sehemu, mara akaonekana mtu bondeni alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu, nijalie niwe katika umma wa Muhammad(s.a.w.w) wenyekurehemewa, wenyekusamehewa madhambi na wenyekulipwa kwa mema”, akasema Anasi Ibni Malik: “Nikaelekea bondeni, mara mtu yule urefu wake ni zaidi ya dhiraa mia tatu, akaniuliza: wewe ni nani? Akasema Anasi: “nikamjibu kuwa mimi ni Anasi bn Maliki mtumishi wa mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Akasema: “Yeye yuko wapi?” Anasi akasema: “Nikamwambia yule pale anayasikia mazungumzo yako”. Akasema: “Nenda kwake, umfikishie salaam kutoka kwangu na umwambie: “ndugu yako Iliyasa anakusalimia”. Nikamuendea mtume(s.a.w.w) na hivyo kumsimulia. Mtume(s.a.w.w) akaja na kukutana nae, akamkumbatia na kumsalimia, kisha wakakaa wakiwa wanazungumza. Nabii Iliyasa akamwambia mtume: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika mimi huwa ninakula mara moja mwaka, na leo ndio siku ya kula kwangu, naomba tule pamoja. Ikawatelemkia meza ya chakula kutoka mbingini, ikiwa na mkate, samaki na figili, wakala kwa pamoja na wakanikaribisha na mimi, tukaswali swala ya Al-asri pamoja kisha nikamuaga, kisha nikamuona akipita kwenye mawingu kuelekea mbinguni”.[118]

Ibni Asaakir amepokea kutoka Hasani (Allah awe radhi naye) kuwa alisema:

“Nabii Iliyasa ni mwakilishi wa majangwa, ama nabii Khidir ni mwakilishi wa milima. Hakika walipewa umri mrefu hapa duniani mpaka wakati wa parapanda ya kwanza na huwa wanakutana katika msimu wa hija kila mwaka”.[119]

Amesema Abdul- Aziiz Ibni Abu Rawaad:

(إن إلياس والخضر (ع) يصومان شهر رمضان في كل عام ببيت المقدس، يوافيان الموسم في كل عام. وذكر ابن أبي الدنيا أنهما يقولان عند افتراقهما عن الموسم: ما شاء الله ما شاء الله لا يسوق الخير إلا الله ...الخ)

“Hakika nabii Iliyasa na Khidri(a.s) kuwa wanafunga mwezi wa Ramadhani kila mwaka katika Baitul- Maqdas, kama ambavyo huwa wanaudiriki msimu wa hija kila mwaka. Na Ibni Abu Dunia ameandika kwamba, wawili hao pindi wanapotaka kuachana katika kila msimu huwa wakisema: “masha Allah masha Allah, hakuna aletae kheri isipokuwa Mwenyezi Mungu… nk”[120] .

Amesema Ibni Hajal Al-Asqaalani kuwa: Daar Qutni ameandika katika kitabu cha Al-Afraad kupitia kwa Atwai, kutoka kwa Ibni Abbas kwamba:

(يجتمع الخضر وإلياس كل عام في الموسم، فيحلق كل واحد منهما رأس صاحبه،ويفترقان عن هؤلاء الكلمات: بسم الله ما شاء الله)

“Nabii Iliyasa na nabii Khidri hukutana kila mwaka katika msimu wa hija, kisha kila mmoja wao humnyoa mwenzake, na kuwa wanaachana kwa kusema maneno haya: bismillah, masha Allah ”. Anasema pia: “Katika mlolongo wa mapokezi ya hadithi hii kuna mtu mwenye jina la Muhamad Ibni Ahmadi bin Zaidi…, na mtu huyu ni dhaifu”. Ibni Asaakir pia amepokea mfano wa hadithi hiyo iliyotajwa hivi punde, kupitia kwa Hishaam Ibni Khalidi kutoka kwa Alhasani Ibni Yahya kutoka kwa Ibni Abu Rawaad, akaongeza kipande kifuatacho:

(ويشربان من ماء زمزم شربة تكفيهما إلى قابل)

“Huwa wanakunywa katika maji ya Zamzam kiasi kinacho watosheleza mpaka mwaka unaofuata” , katika hadithi hii watu wawili au zaidi miongoni wa wapokezi hawakutajwa. Hivyo, hadithi kama hii hujulikana kwa jina la: (Mu’udhal) katika elimu ya hadithi. Vilevile, Ahmad ameitaja hadithi hii katika kitabu cha Az-Zuhdi kwa mapokezi ya Alhasani kutoka kwa Ibni Abu Rawaad, akaongeza kipande hiki:

(أنهما يصومان رمضان ببيت المقدس)

“Hakika wawili hao (Khidri na Iliyasa) huwa wanafunga Ramahani takika Baitul-maqdas”.[121]

Ama kuhusiana na Dajaal: riwaya za Ahli Sunna zinaonyesha kuwa nae yuko hai tangu zama bwana mtume(a.s) mpaka leo hii. Ama Dajaal huyo ni nani? Kuna kauli mbili kuhusiana na hilo. Yakwanza inasema kuwa ni Ibni Sayyaad, na kauli ya pili inasema kuwa ni mtu mwingine ambae kafungwa kwa minyororo mpaka hapo wakati wa kutoka kwake utakapofika.

Ama kuhusiana na Ibni Sayyaad, wametaja habari na sifa nyingi za kushangaza na kustajabisha kuhusiana nae.

Amesema Nawawi katika Sharhu ya Muslim mlango wa (dhikri Ibni Sayyaad): “Mtu huyu, anaitwa ‘Ibni Sayyaad au Ibni Saaid’. Ameitwa kwa majina hayo mawili katika hizi hadithi, lakini jina lake ni Swaaf.

Wamesema wanazuoni: “Kisa cha Ibni Sayyaad kina utata na jambo lake linachanganya katika kujua kuwa yeye ndie yule Masihi Dajjaal mashuhuri au ni mtu mwingine?”. Lakini jambo lisilo na shaka ni kuwa yeye ni Dajjali miongoni mwa madajjaali.

Maulamaa wamesema: “Dhahiri ya hadithi, inaonyesha kuwa bwana Mtume(s.a.w.w) hakushushiwa wahai kuwa Ibni Sayyaad ndie Masihi Dajaal peke yake na kwamba hakuna mwengine, bali alichofunuliwa ni sifa za Dajaal, na Ibni Sayyaad alikuwa na dalili na sifa zinazo shabihiyana na sifa zile. Ndio maana bwana Mtume(s.a.w.w) hakuwa akihukumu moja kwa moja kuwa Ibni Sayyaad ndie Dajjaali pekee na hakuna mwingine. Kwa sababu hiyo, ndio maana mtume(s.a.w.w) alimwambia Omar (Allah awe radhi naye): “Kama Ibni Sayyaad atakuwa ndie Dajjaali, kamwe hautaweza kumuuwa”. Ama hoja ya kuwa Ibni Sayyaad ni mwislamu na Dajjaali ni kafiri, na kwamba Dajjaali hatakuwa na mtoto lakini Ibni Sayyaad ana mtoto, au kwamba Dajjaali hataingia Makka na Madina lakini Ibni Sayyaad aliwahi kuingia Madina hali yakuwa akielekea Makka, yote hayo hayana ushahidi kwa Ibni Sayyaad; kwa sababu Mtume(s.a) alielezea sifa za Dajjaali wakati atakapo dhihiri duniani na kuanzisha fitina zake.

Miongioni mwa utata wa kisa cha Ibni Sayyaad na kwamba yeye ni mmoja wa madajjaali waongo, ni kauli yake kumwambia mtume(s.a.w.w) : "Je unashuhudia kuwa mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu?", vilevile madai yake kwamba huwa anajiwa na (malaika) mkweli na muongo, na kwamba yeye anaiona Arshi ya Mwenyezi Mungu juu ya maji, na kuwa hachukizwi wala kuona tatizo iwapo yeye ndie atakuwa Dajjaali, kama ambavyo amedai kujua mahala alipo Dajjaali katika kauli yake: "Kwa hakika mimi ninamjua Dajjaali, ninajua mahala alipozaliwa na yupo wapi", na kuvimba kwake mpaka akajaa njia nzima.

Ama kwamba alidhihirisha uislaamu, akafanya hija na kupigana jihadi, na kwamba aliachana na yote aliyokuwa nayo hapo kabla, yote hayo hayako wazi katika kuthibitisha kuwa yeye sio Dajjaali.

Anasema Alkhatwabi: "Masalafi (maswahaba) wametofautina katika suala la Ibni Sayyaad kipindi cha ukubwa wake. Imepokelewa kuhusiana na yeye kwamba: alitubia kutokana kauli yake ya kudai utume... na kwamba alifia Madina. Na pindi walipotaka kuliswalia jeneza lake, waliufunua uso wake ili watu wamuone. Wakaambiwa: "Shuhudieni".

Anaendelea kusema: "Miongini mwa yaliyopokelewa kutoka kwa Ibni Omar na Jaabir nikuwa, walikuwa wakiapa kuwa Ibni Sayyaad ndio Dajjaali, wala hawakuwa wakilishakia hilo". (Siku moja) Jaabir aliambiwa: "Hakika Ibni Sayyaad alisilimu". Jaabir akasema: "Hata kama alisilimu". Akaambiwa tena kwamba: "Hakika Ibni Sayyaad aliingia Makka na Madina". Akajibu kwa kusema: " Hata kama".

Abu Daud katika kitabu chake cha Sunan Ibni Daud, amepokea kwa mapokezi yaliyo sahihi kutoka kwa Jaabir kuwa alisema: "Tulimpoteza (alikufa) Ibni Sayyaad siku ya Hurrah". Hadithi hii inaibatilisha riwaya ya wale waliopokea kuwa Ibni Sayyaad alifia Madina na akaswaliwa huko.

Miongoni wa hadithi hizi, Muslim amepokea kwamba: Jaabir Ibni Abdallah aliapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba: Ibni Sayyaad ndie Dajjaali, na kwamba alimsikia Omar (Allah awe radhi naye) akiapa kuhusiana na jambo hilo hilo mbele ya Mtume(s.a.w.w) , nae mtume(s.a.w.w) hakulikanusha hilo.

Abu Daud amepokea kwa mapokezi sahihi kutoka kwa Ibni Omar kwamba alikuwa akisema: "Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa, sina shaka kwamba, Ibni Sayyaad ndie Masihi Dajjaali. Anasema Bayhaqi katika kitabu chake cha 'Alba'ath wa Nushour': "Watu wamehitafiana sana kuhusiana na suala la Ibni Sayyaad na kuwa je yeye ndie Dajjaali au la?". Anaesma: “Anaesema kuwa Dajjali ni mwingine na sio Ibni Sayyaad, alitumia hadithi aliyotajwa na Tamiimi Daari kuhusiana na kisa cha ‘Jassaasah’ kama hoja”.[122]

Nami niseme kuwa: Ikhtilafu ya Ahli Sunna mpaka zama za hivi karibuni kuhusiana na kuwa Ibni Sayyaad ndie Dajjaali au la, inaonyesha kuwa ikiwa atakuwa ndie Dajjaali wa kweli, basi wakati huo saula la urefu wa umri wake halitakuwa na mushkeli wowote kwao.

Ama kuhusiana na hadithi ya Jassaasah, Ahli sunna wameiandika katika vitabu vyao. Hadithi hiyo inaonyesha kwamba Dajjaali alikuwa tangu wakati wa bwana mtume(s.a.w.w) , na kwamba alikuwa amefungwa kwa minyororo akisubiri wakati wa kutoka. Ameandika Muslim katika kitabu chake kuwa, mtume(s.a.w.w) alisema:

(إني والله ما جمعتُكم لرغبة ولا لرهبة، ولكن جمعتكم لأن تميماً الداري كان رجلاً نصرانياً، فجاء فبايع وأسلم، وحدثني حديثاً وافق الذي كنت أحدثكم عن مسيح الدجَّال، حدثني أنه ركب في سفينة بحرية مع ثلاثين رجلاً من لخم وجذام، فلعب بهم الموج شهراً في البحر، ثم أَرْفَأوا إلى جزيرة في البحر حتى مغرب الشمس، فجلسوا في أَقرُب السفينة، فدخلوا الجزيرة، فلقيتْهم دابة أهلب كثير الشعر، لا يدرون ما قُبُلُه من دُبُره من كثرة الشعر، فقالوا: ويلكِ ما أنت؟ فقالت: أنا الجسَّاسة. قالوا: وما الجسَّاسة؟ قالت: أيها القوم انطلقوا إلى هذا الرجل في الدَّيْر، فإنه إلى خبركم بالأشواق. قال: لما سمَّتْ لنا رجلاً فَرِقْنا منها أن تكون شيطانة، قال: فانطلقنا سراعاً حتى دخلنا الدَّيْر، فإذا فيه أعظم إنسان رأيناه قط خَلْقاً وأشده وِثَاقاً، مجموعةٌ يداه إلى عنقه ما بين ركبتيه إلى كعبيه بالحديد، قلنا: ويلك ما أنت؟ قال: قد قدرتم على خبري، فأخبروني ما أنتم؟ قالوا: نحن أناس من العرب، ركبنا في سفينة بحرية، فصادفنا البحر حين اغتلم، فلعب بنا الموج شهراً، ثم أرفأنا إلى جزيرتك هذه، فجلسنا في أقْرُبها فدخلنا الجزيرة... فقال: أخبروني عن نخل بَيْسان. قلنا : عن أي شأنها تستخبر؟ قال: أسألكم عن نخلها هل يثمر؟ قلنا له: نعم. قال: أما إنه يوشك أن لا تثمر. قال: أخبروني عن بحيرة الطبرية. قلنا: عن أي شأنها تستخبر؟ قال: هل فيها ماء؟ قالوا: هي كثيرة الماء. قال: أما إن ماءها يوشك أن يذهب. قال: أخبروني عن عين زُغَر. قالوا: عن أي شأنها تستخبر؟ قال: هل في العين ماء؟ وهل يزرع أهلها بماء العين؟ قلنا له : نعم هي كثيرة الماء، وأهلها يزرعون من مائها. قال: أخبروني عن نبي الأميين، ما فعل ؟ قالوا: قد خرج من مكة ونزل يثرب. قال: أَقاتَله العرب؟ قلنا: نعم. قال: كيف صنع بهم؟ فأخبرناه أنه قد ظهر على من يليه من العرب وأطاعوه. قال لهم: قد كان ذلك؟ قلنا: نعم. قال: أما إن ذاك خير لهم أن يطيعوه، وإني مخبركم عني، إني أنا المسيح، وإني أوشك أن يؤذَن لي في الخروج فأخرج، فأسير في الأرض، فلا أدع قرية إلا هبطتها في أربعين ليلة، غير مكة وطَيْبة، فهما محرَّمتان عليَّ كلتاهما، كلما أردتُ أن أدخل واحدة أو واحداً منهما استقبلني مَلَك بيده السيف صَلْتاً يصدّني عنها، وإن على كل نَقْب منها ملائكة يحرسونها

قالت: قال رسول الله ( ص ) وطعن بمخصرته في المنبر: هذه طَيْبَةُ، هذه طَيْبَةُ، هذه طَيْبَةُ ـ يعني المدينة ـ ألا هل كنت حدَّثتكم ذلك؟ فقال الناس: نعم. فإنه أعجبني حديث تميم أنه وافق الذي كنت أحدِّثكم عنه وعن المدينة ومكة، ألا إنه في بحر الشام أو بحر اليمن، لا بل من قِبَل المشرق ما هو، من قبل المشرق ما هو، من قبل المشرق ما هو. وأومأ بيده إلى المشرق)

“Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba, Mimi sijakukusanyeni hapa ili nikuhimizeni wala nikuhofisheni juu jambo, isipokuwa nimekuiteni nikusimulieni kwamba: Hakika Tamiimi Daari aliekuwa mnaswara, amekuja kwangu na ametoa kiapo cha utii na hatimae akalisilimu. Na amenihadithia kisa kinachoafikiana na niliyokuwa nikikuelezeni kuhusiana na Masihi Dajjaali. Amesema kuwa: Yeye pamoja na watu thelathini wa makabila ya Lakhm na Judhaam walipanda merikebu, mawimbi yakawazungusha baharini kwa muda wa mwezi mzima, mpaka walipofikia kisiwa wakati wa magharibi, wakakaa ukingoni mwa merikebu (au juu ya ngalawa ya kushushia watu). Hatiame wakaingia kisiwani, mara wakamkuta kiumbe mwenye nywele nyingi sana, kutokana na wingi wa nywele hakujulika wapi ni mbele na wapi ni nyuma. Wakasema: "Ole wako! wewe ni nani?". Akasema: "Mimi ni Jassaasah". Wakauliza: "Jassaasah ndio nini?". Akasema: "Enyi watu, nendeni kwa huyu mtu kijijini Dairi, hakika ana shauku kubwa ya kujua habari zenu". Akasema: "Kiumbe yule alipotutajia jina lake tukahofia asije kuwa shetani". Anaendelea kusema: "Tukaondoka haraka mpaka tulipowasili kijijini Dairi, na hapo tukamuona mtu mkubwa hatukupata kuona mfano wake kimaumbile. Mikono yake imefungwa shingoni pake, na amefungwa kwa vyuma kuanzia magotini mpaka visigino vya miguu yake."

Tukamuambia: "Ole wako, wewe ni nani?"

Akasema: "Mumekwishazijua habari zangu, niambieni ninyi ni akina nani?". Wakasema : "Sisi ni watu katika waarabu, tulisafiri kwa merikebu na ikasadifu bahari kuchafuka. Mawimbi yakatuzungusha kwa muda wa mwezi kisha tukateremka katika kisiwa chako hiki. Akasema "Nipeni habari za mitende ya Bisaan". Tukamuuliza : "Nini unataka tukuelezee kuhusu mitende hiyo? Akajibu kwa kusema : "Ninakuulizeni kuhusu mitende ya eneo hilo kuwa je bado inatoa matunda?" Tukamwambia: "Ndio". Akasema : "Muda sio mrefu haitatoa matunda". Akasema: "Nielezeni kuhusu ziwa la Genesareti au bahari ya Galilaya". Tukamuuliza: "Unauliza nini kuhusiana na ziwa hilo? Akasema: "Je lina maji?" Wakasema: "Ndio, maji mengi". Akasema: "hakika hivi karibuni maji yake yatatoweka". Akasema: "Nielezeni kuhusu chemchemi za Zughar". Tukamuuliza: "Ni nini waulizia kuhusu chemchemi hizo?" Akasema: "Je chemchemi bado zina maji? na Je watu wa eneo hilo wanayatumia kwa kilimo?". Tukamjibu: "Ndio, zina maji mengi, na watu wake wanalima kwa kutumia maji yake". Akasema: “Nipeni habari kuhusiana na nabii wa wasiojua kusoma wala kuandika (warabu), amefanya nini? Wakasema: "Kahama kutoka Makka amefikia Madina". Akuuliza: "Je warabu walimpiga vita?" Tukasema: "Ndio". Akahoji tena kuwa: "Amewafanya nini?" Tukamjulisha kuwa: "Amehamia kwa warabu mengine wanao muunga mkono na kumtii". Akasema: "Na nikweli wamefanya hivyo?". Tukasema: "Ndio". Akasema: "Hakika ni bora kumti. Na sasa ninakupeni habari zangu. Mimi ndie Masihi (Dajjaali), na hivi karibuni nitapewa idhini ya kutoka na nitatoka na kutembea aridhini, na wala sitoacha kijiji ila lazima nikipitie ndani ya muda wa siku arubaini, isipokuwa Makka na Twiibah (Madina), hakika miji hii miwili ni haramu kwangu kuingia ndani yake. Kila nitakapotaka kuingia katika mojawapo wa miji hiyo, atanikabili malaika mikononi mwake akiwa na upanga ulionolewa akinizuwia. Hakika katika kila upande yupo malaika mwenye kulinda miji hiyo”.

Akasema Fatimah Binti Qaysi: "Akasema mjumbe wa Mwenyezi Mungu huku akigonga kwa fimbo yake katika mimbari: "Hii ndio Twiibah, Hii ndio Twiibah, Hii ndio Twiibah (akimanisha Madina)". Mtume(s.a.w.w) akasema: "Je sikuwa nikikuelezeni haya?". Hapo watu wakasema: "Ndio". Akasema(s.a.w.w) : "Kwa hakika nimenifurahishwa na kisa cha Tamiim kwa kuwa kimeafikiana na niliyokuwa nikiwaambieni juu ya Makka na Madina. Alaa! Kwa hakika Dajjaali atatokea katika bahari ya Syiria au bahari ya Yemeni, hapana, bali atatokea upande wa Mashariki. Hakika niupande wa Mashariki. Hakika ni upande wa Mashariki”. Akaashiria kwa mkono wake upande wa Mashariki" [123]

Amesema Qurtubi baada ya kutaja hadithi iliyopokelewa kutoka kwa mtume(s.a.w.w) kuwa, alisema(s.a.w.w) :

(أُقسم بالله ما على الأرض من نَفْس منفوسة تأتي عليها مائة سنة).

"Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa, hakutakuwa na nafsi inayopumua juu ya mgongo wa Ardhi itakayoishi miaka mia moja": Maulamaa wetu wanasema kuwa: tija inayotolewa na hadithi ni kuwa, bwana mtume(s.aw.w) kabla ya mwezi mmoja kufariki alitoa bishara kuwa, mwanadamu yeyote atakaekuwepo kipindi hicho (cha kudhihiri kwa Dajjaali), umri wake hauatazidi miaka mia moja, kwa sababu kauli ya mtume(s.a.w.w) inasema: “hakuna nafsi yenyekupumua”. Kwa upande mwingine ibara hii haiwahusu malaika wala majini; kwani haijathibiti kuwa wao wana sifa hiyo. Vilevile ibara hiyo, haimshamili kiumbe alisiekuwa na akili; kwa kuwa kauli aliyoitaja mtume(s.a.w.w) : "wala yeyote miongoni mwa ambao wapo katika mgongo wa Ardhi", kwa kawaida huambiwa ambae ana akili. Hivyo basi, inabainika kuwa anaekusudiwa ni mwandamu, bali hata Ibni Omar nae aliibanisha maana hii pale aliposema: "Anachokilenga kwa kusema vile, ni kuwa karne hiyo itakwisha".

Vilevile, mwenyekushikilia hadithi ili kubatilisha kauli ya anaesema kuwa: "Khidri yuhai" hana hoja; kwani kauli ya mtume: "hakuna nafsi yenye kupumua", ina maana pana. Na zaidi ya hapo, upana huu hata kama unatilia mkazo kuvishamili vitu vyote, lakini haina maana kuwa kila kitu lazima kiingie ndani yake, bali kuna uwezekano wa kuuhadidi na kuufanya kuwa unavihusu baadhi ya vitu na vyote.

Vilevile maneno ya mtume, hayamshamili nabii Issa(a.s) , kwani yeye kwa mujibu wa aya ya Qur'an, hajafariki wala hajauwawa, kama ambavyo hayamuhusu Dajjaali, licha ya kuwa yupo hai kwa ushahidi wa hadithi ya Jassaasah. Vilevile, maneno hayo hayamshamili Khidri(a.s) hata kama haonwi na watu, hashirikiani nao wala hata hawamuwazii katika mazungumzo yao. Hivyo, mfano wa upana huu nae pia haumshamili[124] .

Ikiwa hayo yameeleweka, tunasema: kama ambavyo dalili madhubuti imeonyesha kubakia hai kwa nabii Issa na Khidri(a.s) , na ikaonyesha kubakia hai Dajjaali kwa muda mrefu zaidi ya umri wa kawaida, hivyo hivyo, ndivyo dalili madhubuti ambazo ufafanuzi wake ulishatangulia hapo kabla, zinavyo onyesha uwepo wa Imamu Mahdi (a.f), na kwamba yuko hai mpaka leo hii. Hivyo, habana budi kuukubali uwepo wake na kukiri kwa hilo.

Kubakia hai Imamu Mahdi (a.f) kwa umri mrefu, hakuna maana ya kuzitupilia mbali dalili sahihi zinazothibitisha uwepo wake, uhai wake na uimamu wake, kama ambavyo hazikutupiliwa mbali dalili zinazothibitisha kubakia hai nabii Issa na Khidri(a.s) kwa sababu ya umri wao kuwa mrefu.

SHUBUHA YA PILI

Je kuna faida gani kuwa na Imamu alie ughaibuni na aliefichikana machoni mwa watu? Imamu ambae hawanufaiki wala kufaidika nae waislaam na waumini, licha ya kuwa na haja nae sana, na hasa pale wanapo kumbwa na matatizo au wanapopatwa na majanga?!

MAJIBU YA SHUBUHA

1. Haya ni majibu aliyoyatoa Sayyidi Murtadhaa (Allah aliinue daraja lake) kuwa, ikwa tumetambua kuwa Mahdi (a.f) ndie Imamu za zama hizi na simwingine, na sasa ameingia ughaibuni hatumuoni kwa macho, tunajua kuwa bila shaka kwakuwa yeye ni maasumu na amehifadhika na mathabi, hawezi kuingia ughaibuni isipokuwa kwa sababu iliyomlazimu kufanya hivyo, na kwa masilahi au madhara yaliyompelekea kufanya hivyo, hata kama sisi tunaweza kushishindwa kujua ufafanuzi wa hilo kwa mapana, bali hatuna ulazima wa kujua ufafanuzi wa hayo. Na kwa njia hii, mazungumzo yetu kuhusiana na ghaiba yake yatakuwa mfano wa kuzungumzia masilahi yaliyopo katika kutupa mawe huko Minaa na kufanya twawafu na mfano wa hayo; kwani ikiwa tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu alietakasika ni mwenye hekima, bila shaka hakutakosa sababu nzuri katika yote hayo, hata kama sisi hatutaijua. Kwa majibu haya, tunakuwa tumefunga mlango wa maswali ya wapinzani wetu, isipokuwa tunabaki tunajitolea kutoa majibu ya baadhi ya maswali ili kuonyesha uwezo[125] .

2. Nasi tunawarejeshea mfano wa shubuha waliyoileta, nayo nikuhusiana na Issa mwana wa Mariam(a.s) , kwani nae yupo ughaibuni mbinguni, bali tunaweza kusema kuwa, kunufaika na Imamu Mahdi(a.s) ambae yuko ughaibuni ardhini kunafikirika zaidi kuliko kwa nabii Issa(a.s) ambae yuko ughaibuni mbinguni.

Na hata kama tutasalimu amri kwamba Imamu Mahdi katika ughaibu wake hatuna faida nae, bado hilo halina tatizo; kwakuwa manufaa yake yaliyohifadhiwa ambayo ni kuijaza ardhi usawa na uadilifu, yana uhakika. Kama ambavyo hakuna tatizo kutonufaika na nabii Issa(a.s) kwa sasa; kwakuwa manufaa yake yana uhakika katika zama za mwisho.

3. Hakika watu wananufaika na Imamu(a.s) hata kama yuko ughaibuni. Ughaibu wake hauziwii kuwa na manufaa muhimu, maadamu hayafungamani na kubainisha hukumu za kisheria, kwa mfano: kuwalinda na kuwakinga watu na adhabu (kuwaondolea watu adhabu); kwa sababu Imamu(a.s) ni katika ahlul-baiti wa bwana mtume(s.a.w.w) ambao ni amani (kinga/ngao) ya adhabu kwa watu wa ardhini kama ilivyopokelewa katika hadithi ya Jaabir Al-answaari (Allah awe radhi nae) kutoka kwa mtume(s.a.w.w) alisema:

(النجوم أمان لأهل السماء، فإذا ذهبتْ أتاها ما يوعدون، وأنا أمان لأصحابي ما كنتُ، فإذا ذهبتُ أتاهم ما يوعدون، وأهل بيتي أمان لأمتي، فإذا ذهب أهل بيتي أتاهم ما يوعدون).

"Nyota ni kinga na ngao kwa waishio mbingini, zinapotoweka huwafika waliyokuwa wakiahidiwa, na mimi ni kinga kwa maswahaba wangu maadamu nipo, nitakapotoweka yatawafika waliyoahidiwa, na watu wa nyumba yangu (ahalul-baiti zangu) ni kinga kwa umma wangu, watakapotoweka yatawafika waliyo ahidiwa"[126] .

Pamoja na kuwa nyadhifa za Imamu katika kipindi cha ughaibu hatuzijui wala kuzielewa zote, lakini mashia wengi waliopata majanga, matatizo na mabalaa Imamu alikutana nao na aliwaokoa kutokana na matatizo yao akawasaidia katika shida zako.

Mimi nashindwa kuelewa kuwa, wapinzani wamepata wapi uhakika huu kuwa, hakuna mwislamu anaeweza kuonana na Imamu(a.s) au eti hakuna muumini anaeweza kunufaika nae? wakati jambo hili hawana elimu nalo, wala hawana njia ya kuwa na uhakika nalo? na hasa ukizingatia kuwa, Imamu(a.s) aliwahofia wao hao hao na akajiziwia nao, akaingia ughaibuni na kuchificha kwa sababu yao? Ni jambo lisiloingia alikini kwamba Imamu awadhihirikie au akutane nao wamjue au wazijue sifa zake.

4.Imamu(a.s) hakuingia mafichoni, bali sisi ndio hatuijui khashsia yake wala hatuwezi kumtofautisha na wengine. Imepokelewa kutoka kwa Abdallah Ibni Mas'uud (Allah awe radhi nae) katika habari za kudhihiri kwa Imamu(a.s) kwamba, makabila baadhi yatawavamia wenzao, watapigana na mahujaji wataporwa mizigo yao, damu zitachirizika mpaka kwenye Jamratul-Aqabah. Watajitokeza watu saba wasomi kutokea maeneo mbalimbali bila yakuwa wameahidiana kukutana. Kila mmoja miongoni mwao atakuwa ameshachukua kiapo cha utii kwa watu mia tatu kumi na kidogo. Watakusanyika ndani ya Makka. Baadhi yao watawauliza wenzao: Nini kumekuleteni hapa? Watasema: Tumekuja kumtafuta huyu mtu ambae fitina itakwisha kupitia kwake, na mji wa Constantinopla (ambao ulikuwa ni mji mkuu wa Roma) utafunguliwa kupitia kwake, tulimjua kwa jina lake, kwa jina la baba yake na kwa jina la mama yake. ...Wote saba wataafikiana kufanya hivyo, kisha watamtafuta ndani ya Makka, watamwambia: Je wewe ndio fulani Ibni fulani? Atawajibu: Hapana, bali mimi ni mtu miongoni mwa maaswaari. Mara atawatoka. Kisha watatoa wasifu wake kwa wenyekumjua na kumtambua. Atasema: Huyo ndie mtu wenu mnaemtafuta, hakika ameelekea Madina. Watamtafuta Madina, kisha yeye atarudi zake Makka... Hali itaendelea hivyo hivyo mpaka mara tatu... Kwa mara ya tatu, ndio wale watu saba watakuja kumpata ndani ya Makka akiwa kwenye Rukuni, watamwambia: “Madhabi yatakuwa juu yako na damu zetu ziko juu yako kama hautaunyosha mkono wako tukakupa kiapo cha utii... Imamu akakaa kati ya Rukni na Maqamu, akaunyosha mkono wake na kuanza kuchua kiapo cha utii[127] .

Kwa hakika kauli yake: "Kisha watatoa wasifu wake kwa wenye kumjua na kumtambua", inaonyesha uwepo wa watu wanaomjua vizuri kabisa, hata kama wanaweza wasiwe wanajua kuwa ndie Mahdi anaesubiriwa.

Vilevile kauli yao: "Huyo ndie mtu wenu mnaemtafuta", inaonyesha hao watu saba walimkuta akisifika na sifa njema na za juu ambazo zinamfanya astahiki kuwa ndie Mahdi na mkombozi wa umma huu, ambae ataujaza ulimwengu usawa na uadilifu baada ya kujaa dhuluma na uovu. Na hakuna shaka kwamba, maarifa na utambuzi wa aina hii hauwezi kupatikana bila ya kuishi na kuchanganyikana nae kwa muda mrefu.

SHUBUHA YA TATU: NI KUHUSIANA NA UIMAMU NA UONGOZI WA MTOTO NA MAZAZI YAKE

Miongoni wa mambo yanayoenda sambamba na kauli ya kuwa Muhammad Ibni Alhasani Al-Al-Askari Almahdi(a.s) ni Imamu, ni kudai kwamba alipata uimamu na uongozi wa waislamu hali ya kuwa ana umri wa miaka mitano, wakati hairuhusiwi mtoto mdogo kubeba uongozi wa waislamu; kwa sababu hana pawa ya kulibeba jukumu hilo nzito, ukiongezea kuwa mtoto ni mwenye kutawaliwa, sasa inakuwaje awe na mamlaka juu wengine?!

MAJIBU YA SHUBUHA

Nikwamba sharti la imamu na kiongozi wa waislamu anatakiwa awe ni mwenye uwezo wa kuongoza, awe na sifa zinazomfanya aweze kusimamia majukumu ya uongozi, kama vile: uwelewa wa mambo, wepesi wa kujua njia za utatuzi wa mambo, akili timamu, uchamungu, awe ni mjuzi wa hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu... na mengineyo.

Ama kwamba ni lazima awe na umri mkubwa na awe ameishi sana, yote hayo siyenye kutiliwa manani, maadamu mtoto atakuwa na uwezo wa kusimamia majukumu ipasavyo.

Na kwa sababu kama hii, ndio maana utaona kwamba cheo hiki hakupewa mtu ambae ni mkubwa zaidi kiumri baada ya kufariki mtume(s.a.w.w) . Hivyo, hakuna kiziwizi cha kijana kuwa imamu na kiongozi, kama ambavyo hakuna tatizo Mwenyezi Mungu alietakasika akawanemesha manabii na mawalii wake kwa neema za siri na dhahiri, neema ambazo huwafanya wastahiki wa cheo cha utume au uimamu, sawa sawa wawe wadogo au wakubwa. Bali Mwenyezi Mungu mtukfu ameyaelezea haya ndani ya kitabu chake madhubuti kwamba: alimpatia nabii Yahya(a.s) akiwa ni kijana mdogo, pale aliposema:

( يا يَحْيى‏ خُذِ الْكِتابَ بِقُوَّةٍ وَ آتَيْناهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا )

"Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto" [128] .

Shaukaani amesema: "Makusudio ya neno ( الْحُكْمَ ) lililoko kwenye aya tukufu ni hekima, ambayo maana yake ni kukifahamu kitabu alicho amrishwa kukishika, na kuzifahamu hukumu na sheria za dini. Vilevile, imesemwa kuwa maana ya hekima ni: "Elimu, kuihifadhi na kuifanyia kazi". au " Unabii" au " Akili". Bali hakuna kiziwizi kuwa neno ( الْحُكْمَ ) linaweza kubeba maana zote zilizotajwa[129] .

Fakhru Raazi anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu alietukuka aliimarisha akili yake -yaani: nabii Yahya- katika udogo wake na akamfunulia (akampa wahai), na hii nikwakuwa Mwenyezi Mugu aliwapa utume nabii Yahya na Issa(a.s) wakiwa ni watoto, tofauti na alivyo wapa unabii na utume Mussa na Muhammad(a.s) "[130] .

Si hivyo tu, bali Mwenyezi Mungu ameelezea kuwa alimpatia kitabu nabii Issa na akamfanya kuwa nabii hali yakuwa ni mtoto mdogo akingali mbelekoni mwa mama yake, bado hata haujapita muda tangu kuzaliwa kwake isipokuwa kidogo. Amesema Mweyezi Mungu mtukufu:

فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّـهِ آتَانِي َ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا .وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا ﴿٣٢﴾

"Akawaashiria mtoto. Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu" [131]

Fakhru Raazi Anasema: "Kwa hakika kauli yake: "Amenipa Kitabu", inaonyesha kuwa alikuwa ni nabii wakati ule akiyasema hayo"[132] .

Ameendelea kusema: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu amemjalia nabii Issa(a.s) -licha ya udogo wa mwili wake-, kuwa ni mwenye maumbile yenye nguvu na aliekamilika kiakili, kiasi cha kuweza kutekeleza swala na zaka. Mwenyezi Mungu akamuelekezea amri ya swala na zaka kwa kusema: "Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai"[133] , jambo ambalo linaonyesha kuwa nabii Issa(a.s) alikuwa kashawajibikiwa na sheria tangu mwanzo wa maisha yake[134] .

Kwa maelezo hayo, inabainika wazi kuwa hakuna kiziwizi kwa Imamu Mahdi (a.f) kuwa kiongozi wa waislamu akiwa mdogo mwenye umri wa miaka mitano au sita. Si hivyo tu, bali kumkubali ni bora zaidi; kwani ikiwa kwao unabii wa mtoto mchanga ni sahihi, basi uimamu wa kijana nao ni sahihi tena kwa ubora zaidi.

Nasi hapo kabla tumethibitisha kwa hoja kuwa, kumfanya mtu nabii au Imamu ni jukumu la Mwenyezi Mungu mtukufu, wala sio jambo la ikhitayari ya watu. Vilevile, tumethibitisha kwa dalili kuwa, Imamu Mahdi (a.f) kachaguliwa na Mwenyezi Mungu mtukufu, na yeye ndie aliemjalia na kumfanya kuwa Imamu hali yakuwa ni kijana kwa kutimiza kwake vigezo vya uimamu na uongozi, na kuwa udogo wa umri wake sio kikwazo na tatizo, kama alivyo mfanya Issa(a.s) nabii hali yakuwa ni mtoto mchanga kwa kutimiza kwake vigezo vya masharti ya unabii kipindi kile.

Ama kuhusiana na suala la Mwenyezi Mungu kumpa hekima Imamu Muhammad Ibni Alhasani Al-askari Almahdi(a.s) akiwa ni kijana, wamelikubali baadhi ya wasomi wa Ahli Sunna. Hakika Ibni Hajari Alhaitami amesema:

(مات [الحسن العسكري] بسر من رأى، ودُفن عند أبيه، وعمره ثمانية وعشرون سنة... ولم يخلّف غير ولده أبي القاسم محمد الحجّة، وعمره عند وفاة أبيه خمس سنين، لكن آتاه الله فيها الحكمة، ويُسمَّى القائم المنتظر)

"(Alhasani Al-askari) alifia Samaraa na kuzikwa karibu na baba yake akiwa na umri wa miaka ishirini na nane... Hakuna aliemuacha zaidi ya mwanae Abul-Qaasim Muhammad Alhujja akiwa na umri wa miaka mitano wakati alipo fariki baba yake. Lakini Mwenyezi Mungu alimpa hekima katika umri huo, na kijana huyo anaitwa Al-Qaaim Almntadhar[135] .

Baada ya haya yote, kunabaki hakuna pingamizi la yeye kuwa kiongozi na Imamu wa waislamu licha ya udogo wa umri wake. Na kwa njia hii kwa neema ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, shubuha inakuwa imetoweka.

SHUBUHA YA NNE: KUHUSIANA NA KUWA JINA LAKE (IMAMU MAHDI) NI MUHAMMAD IBNI ABDALLAH

Wameandika Abu Daud katika Sunani yake, Ibni Habbaan katika sahihi yake, Haakim katika Mustadraku yake na wengineo kwa kupokea kutoka kwa Ibni Mahdi kutoka kwa Sufiyan kutoka kwa Zarri Ibni Abdallah Ibni Masu'ud (Allah awe radhi nae) kwamba alisema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(لو لم يبقَ من الدنيا إلا يوم لطوَّل الله ذلك اليوم، حتى يبعث فيه رجلاً مني، أو من أهل بيتي، يواطئ اسمه اسمي، واسم أبيه اسم أبي، يملأ الأرض قسطاً وعدلاً كما مُلئتْ ظلماً وجوراً)

"Kama isingelibakia isipokuwa siku moja ili dunia kuisha, basi Mwenyezi Mungu angeliirefusha siku hiyo ili amlete mtu anaetokana nami, au katika watu wa nyumba yangu, ambae jina lake ni sawa na jina langu, na jina la baba yake ni sawa na jina la baba yangu, atakaeijaza dunia usawa na uadilifua baada ya kujazwa dhuluma na uovu"[136] . Kufanana kwa jina la Mahdi na jina la mtume(s.a.w.w) , vile vile, jina la baba wa Mahdi na jina la baba wa mtume(s.a.w.w) , kunamaanisha kuwa jina la Mahdi (a.f) litakuwa ni: Muhammad Ibni Abdallah, na sio Muhammad Ibni Alhasani kama wanavyodai mashia.

MAJIBU YA SHUBUHA YA NNE

1.Hadithi hii imepokelewa kwa matamshi tofauti tofauti kama itakavyokuja, lakini pia imepokelewa kwa njia tofauti na zakwetu. Hivyo haiwezi kuwa ni hoja dhidi yetu, hali yakuwa kwetu haujathibiti usahihi wake. Ukiachilia mbali hayo, hadithi yenyewe haijafikia kiwango cha usahihi, bali wanachokisema zaidi kuhusiana na hadithi hiyo ni kuwa ni ( حسن ) yaani: nzuri. Hivyo basi, kwa hadithi hiyo hatuwezi kuzibatilisha hoja na dali zote za kiakili na zile za kinukuu (aya na hadithi) ambazo zimeonyesha na kuthibitisha kuwa Mahdi ndie Imamu Muhammad Ibni Alhasani Al-askari(a.s) , kama ambavyo hatuwezi kuzipuuza ishkali zote zilizotolewa ili kupinga na kukanusha umahdi wake.

2.Hakika hadithi ambayo kipengele cha "na jina la baba yake ni sawa na jina la baba yangu" kimetajwa, njia zake zote za mapokezi zinaishia kwa A'asimu Ibni Abi Anujuud ambae ni mmjoa kati ya watu wa visomo mashuhuri vya Qur'an. Bwana huyu kwa wasomi wa Ahli Sunna anajulikana kuwa hifdhi yake ni mbaya. Yafuatayo ni waliyoyasema kumhusu bwana huyo:

  • Anasema Adhahabi: "(A'asimu) ni madhubuti katika kisomo cha Qur'an, na simadhubuti katika hadithi, ni mkweli kwao".
  • Na Yahya Alqatwan anasema: "Sijakuta mtu ambae jina lake ni A'asimu isipokuwa nimemkuta ni mbaya wa kuhifadhi".
  • Annasaai anasema: "(A'asimu) simwenye kuhifadhi".
  • Na Addaar-qutni amesema: "Katika hifdhi ya A'asimu kuna kitu (tatizo)".
  • Vilevile amesema Ibni Kharaash: "Katika hadithi yake kuna tatizo".
  • Shu'ubah nae anasema: "Ametusimulia A'asimu Ibni Abi Annujuud, na ndani ya nafsi (yangu) kuna kitu".
  • Ibni Sa'adi anasema: "Ni mwaminifu isipokuwa ni mwingi wa kukosea katika kusimulia kwake ( في حديثه )".
  • Anasema Abu Hatam: "Si mahala pake kumwita mwaminifu".[137]
  • Yakubu Ibni Sufiyan nae anasema: "Katika kusimulia kwake kuna shaka, na yeye ni mwaminifu".
  • Ibni Aliyah kamzungumzia kwa kusema: "Kila ambae jina lake ni A'asimu alikuwa ni mbaya wa kuhifadhi".
  • Al-Uqaili amesema: "Hakuwa na chochote isipokuwa hifdhi mbaya".[138]

Nami niseme kuwa: ikiwa hali ya huyu bwana ndio hii, inawezekanaje kuitegemea hadithi yake, tena katika suala muhimu kama hili, wakati ambao dalili zinazo thibitisha kuwa Mahdi Almuntadhar (a.f) ndie imamu Muhammad Ibni Alhasani(a.s) ?!

3. Hakika hadithi hii iliyopokelewa kutoka kwa Aa'simu imehitilafiana kwa upande huu, kwamba wapo walioipokea kutoka kwake bila kutaja kipengele "na jina la baba yake ni sawa na jina la baba yangu", na wapo waliopokea kutoka kwake ikiwa na kipengele hicho.

Tirmidhi Ameandika kwa mapokezi kutoka kwa Sufiyan Ibni A'iinah kutoka kwa A'asimu kutoka kwa Zarri kutoka kwa Abdallah kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuwa alisema: "Atafuatia mtu katika watu wa nyumba yangu, ambae jina lake linafanana na jina langu". Vilevile amepokea kwa upokezi kutoka kwa Sufiyan Athouri kutoka kwa Badlah kutoka kwa Zarri kutoka kwa Abdallah kwamba alisema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(لا تذهب الدنيا حتى يملك العرب رجل من أهل بيتي، يواطئ اسمه اسمي).

"Dunia haitaisha mpaka atakapo wamiliki warabu mtu katika watu wa nyumba yangu, ambae jina lakeni sawa na jina langu"[139] .

Kuna watu wengi walioipokea hadithi hii kutoka kwa A'asimu bila yakuwa na kipeangele: "na jina la baba yake ni sawa na jina baba yangu", miongoni mwao ni:

1. Muhammad Ibni Ibrahim Abu Shihabu katika kitabu cha: Sahih Ibni Habbaan, Juz: 13, uk: 284, na: Mawaaridu Dwam'an, Juz: 2, uk: 839.

2. Othiman Ibni Shabrmah, katika kitabu cha: Sahihi Ibni Habbaan, Juz: 15, Uk: 238, na: Mawaaridu Dwam'an, Juz: 2, Uk: 839.

3. Hamiid Ibni Abi Ghunyah katika kitabu: Al-Mu'jamu Al-ausat Cha Tabraani, Juz: 5, Uk: 135.

4. Abu Al-Ahwadh Salaam Ibni Saliimu katika kitabu: Almu'jamu Aswaghiiru Cha Tabraanim Jz: 2, Uk:148, Na: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 136.

5. Amru Ibni Marrah, katika kitabu: Almu'jamu Aswaghiiru Cha Tabraanim Juz:10, Uk:148, Na: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 131.

6. Al-A'mash, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 133.

7. Abu Is'haaq Ashaibaani, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 133.

8. Abdallah Ibni Hakiim Ibni Jubair, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.

9. Shu'bah, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.

10. Sufiani Athuur, katika kitabu: Sunan Abi Daud, Juz: 4, Uk: 108, Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.

11. Sufiani Ibni Aiinahm katika kitabu: Musnad Ahmad, Juz:1, Uk: 376, Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.

12. Abdul Maliki Ibni Abi Ghunyah, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 134.

13.Omar Ibni Obeid Atwanaafisim katika kitabu: Musnad Ahmad, Juz:1, Uk: 376, Na: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 135.

14.Waasitu Ibni Alhaarthi, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 135.

15. Abu kabari Ibni ayaash, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 135.

16. Ma'adhu Ibni Hishaamu kutoka kwa baba yake, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 133.

17. Amru Ibni Qaisi, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 137.

18. Abdallah Ibni Shabrmah, katika kitabu: Almu'jamu Alkabiiru, Juz:10, Uk: 137.

Baadhi ya wapokezi waliopokea hadithi hii ikiwa na ziada ya kipengele "na jina baba yake linafanana na jina baba yangu", wapeipokea pia bila kuwa na kipengele hicho, miongoni mwao:

1. Omar Ibni ubaid, ameipokea hadithi hii ikiwa na ziada katika kitabu: sunan abi daudm jz:4, uk:106, wakati ameipokea bila ziada kama ilivyotangulia kwenye namba 13.

2.abu bakari Ibni a'yaashi, ameipokea ikiwa na ziada katika kitabu: sunan abi daudm jz:4, uk:106, wakati ameipokea bila ziada kama ilivyotangulia kwenye namba 15.

3. Sufiani, kaipokea ikiwa na ziada katika kitabu: sunan abi daud, jz:4, uk: 106, na katika kitabu: sahihi Ibni hayaani, jz:15, uk:236, na ameipokea bila ziada kwenye namba:10, 11.

4. Amru Ibni abi qaisi, ameipokea ikiwa na ziada katika: almuujamu alkabiir cha tabraani, jz:10, uk:135, na bila ziada kama ilivyo kwenye namba: 17.

Ikiwa hali ndio hii ya mashaka katika hii hadithi, inawezekanaje kuitegemea katika kuthibitisha jina la mzazi wa Imamu Mahdi almuntadhar (a.f).

4. Hakika hadithi hii pia imepokelewa kwa mapokezi ambayo A'asimu Ibni abu najoud hakutajwa na bila kuwa na ziada ya kipengele cha "na jina la baba yake ni sawa na jina baba yangu".

Albazaar katika kitabu chake Almusnad ametaja kwa mapokezi kutoka kwa muawiya Ibni Qurrah kutoka kwa baba yake (allah awe radhi nae) amesema: alisema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(لتملأن الأرض جوراً وظلماً، فإذا مُلئتْ جوراً وظلماً بعث الله رجلاً مني، اسمه اسمي أو اسمه اسم أبي ، يملؤها عدلاً وقسطاً كما مُلئتْ جوراً وظلماً...).

“Kwa hakika ardhi itajaa uovu na dhuluma, itakapojaa uovu na dhuluma, Mwenyezi Mungu atamleta mtu anetokana na mimi, jina lake ni sawa na jina langu au jina lake ni sawa na jina la baba yangu,[140] ataijaza ardhi uadilfu na usawa kama itakavyokuwa imejaa uovu na uadilifu…”[141] .

Na Alhauthami ameindika pia katika kitabu chake (Zawaaid) kwa mapokezi kutoka kwa Muawiya Ibni Qurrah kutoka kwa baba yake (allah awe radhi nae) amesema: alisema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(لتملأن الأرض جوراً وظلماً، فإذا مُلئتْ جوراً وظلماً بعث الله عزَّ وجل رجلاً مني، اسمه اسمي أو اسم نبي، يملؤها قسطاً وعدلاً كما مُلئتْ جوراً...)

“Kwa hakika ardhi itajaa uovu na dhuluma, itakapojaa uovu na dhuluma, Mwenyezi Mungu alietukuka na kutasika atamleta mtu anetokana na mimi, jina lake ni sawa na jina langu au jina lake ni sawa na jina la nabii, ataijaza ardhi uadilfu na usawa kama itakavyokuwa imejaa uovu na uadilifu…”[142] .

5. Hata kama tukisalimu amri kuwa hadithi hii ni sahihi, tunaweza kusema kuwa: makudio ya jina ni kuniya; kwani huwenda jina likatumiwa huku ikikusudiwa kuniya.

Bukhari kaandika katika kitabu chake Sahihi Bukhari kwa mapokezi kutoka kwa Sahalu Ibni Sa'adi alisema:

(ما كان لعلي اسم أحب إليه من أبي تراب، وإنْ كان ليفرح به إذا دُعي بها).

“Ali hakuwa na jina analo lipenda zaidi kuliko jina la Abu Turaab, hakika alikuwa akifurahi anapoitwa kwa jina hilo”[143] .

Vilevile, Sahalu amesema katika sahihi muslim: “Ali hakuwa na jina analolipenda zaidi kuliko jina la Abu Turaab, na likuwa akifurahi sana akiitwa kwa jina hilo, akamwambia: tusimulie kisa chake ni kwanini aliitwa Abu Turaab? akasema: "(Siku moja) mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a) alikuja nyumbani kwa Fatwimah akawa hakumkuta Ali nyumbani mpaka akasema: "Kisha mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akamkuta Ali(a.s) hali ya kuwa amelala, shuka lake upande mmoja likiwa limeanguka chini na kupatwa na udongo, mtume(s.a.w.w) akawa anaupangusa ule udongo kwenye shuka lile huku akisema: "Amka ewe Abu Turaab, Amka ewe Abu Turaab"[144] .

Ni jambo lililokowazi kuwa ‘Abu Turaab’ ni kuniya, kwakuwa kuniya ni kila jina lililoanza na neno: ‘Abu au Umu’ yaani: baba au mama. Kwa sababu hiyo, ndio maana Ibni Hajari katika kitabu cha 'Fat'hul Baari' katika kauli yake: "(Babu Aliqaailat Fil Masjidi) kaitaja hadithi ya Ali ambayo inaelezea sababu ya kuitwa kwake Abu Turaab"[145] . Hivyo basi, makusudio ya hadithi hiyo yenye kipengele “Jina lake ni sawa na jina langu na jina la baba yake linaendana na jina baba yangu” ni kwamba kuniya ya mzazi wa Mahdi ni sawa na kuniya ya mzazi wa mtume(s.a.w.w) , kwani wote wawili kuniya zao ni Abu Muhammad.

Vilevile, iko wazi kuwa kauli yake: "Jina lake linaendana/ ni sawa na jina langu na jina la baba yake linaendana/ ni sawa na jina baba yangu", ni ibara ndefu na ambayo haiashirii moja kwa moja kwamba kinacholengwa ni jina. Hivyo, kuna uwezekano wa kuifupisha kwa ibara ambayo ipo kibalagha na wazi zaidi kwa kusema: "Jina lake ni Muhammad Ibni Abdallah, au Muhammad Ibni Alhasani", lakini kwakuwa malengo ya mtume(s.a.w.w) yahakuwa kulitaja wazi jina la Mahdi (a.f); kwakuwahofia watawala waovu na viongozi wapotovu, ndio maana akatumia ibara ambayo inabeba maana zaidi ya moja, ili kila mmoja afikirie atakavyo; na ili isiwe rahisi kwa wanaomtafuta wamuuwe au wamtie mbaroni kumjua na kumtofautisha na wengine.

SHUBUHA YA TANO: KWAMBA MAHDI (A.F) NI KATIKA KIZAZI CHA IMAMU HASANI ALMUJTABA(A.S)

Ametaja Abu Daud kwa upokezi kutoka kwa Abu Is'haaqa alisema: Amesema Ali (Allah awe radhi nae), akimtazama mwanae Hasani:

(إن ابني هذا سيِّد كما سمَّاه النبي ( ص )، وسيخرج من صلبه رجل يُسمَّى باسم نبيكم، يشبهه في الخُلُق، ولا يشبهه في الخَلْق)

“Katika kizazi chake atatokea mtu atakaeitwa jina la mtume wenu, atafanana nae katika tabia wala hatafafa nae katika maumbile”. Kisha akataja kisa cha (Ataijaza Ardhi uadilifu)[146] .

MAJIBU YA SHUBUHA

1. Hakika hadithi hii kwa upande wa sanadi na upokezi ni dahaifu; kwakwa Abu Daud hajaipokea kutoka kwa Haruna Ibni Almughiira mwenyewe, bali kaipokea kutoka kwa alieisimulia kutoka Haruna Ibni Almughiira. Hivyo hadithi hii ni mursala.

Vilevile, Haruna Ibni Almughiira hata kama Ibni Habbaan kamtaja katika orodha ya waaminifu, isipokuwa amesema kuwa: "Huwenda alikosea"[147] .

Kama ambavyo katika upokezi na sanadi ya hadithi hii yupo Amru Ibni Abi Qaisi. Abu Daud anasema yafuatayo kuhusiana na Amru Ibni Abi Qaisi: “Hana tatizo, (lakini) katika kusimulia kwake ( في حديثه خطأ ) kuna makosa”. Na Adhahabi nae anasema: "Nimkweli, (lakini) ana makosa ( صدوق له أوهام )"[148] . Ama Othumani Ibni Abu Shaibah, amesema: “Hana tatizo, alikuwa akikosea kidogo katika hadithi au kusimulia”[149] . Ama Is'haaqa Asubaiy, imesemekana kuwa: "Hakuwahi kupokea kutoka kwa Amiirul Muunminina Ali(a.s) , bali alimuona mara moja". Ibni Almundhiri nae anasema: "Hadithi hii imekatika katika sanadi na mapokezi yake (munqatwiu)”, kwani Abu As'haaqa Asubai'y alimuona Ali(a.s) mara moja[150] . Hali kadhalika, Albani katika kusherehesha kitabu cha 'Mishkaatu Almisbah' alisema: "Sanadi na upokezi wa hadithi hii ni dhaifu[151] .

2. Zaidi ya hadithi hii hatujawakuta na dalili nyingine inayo onyesha kuwa Mahdi (a.f) ni katika kizazi cha Imamu Hasani(a.s) , isipokuwa baadi ya dhana na Istihisani ambazo hazina mashiko katika uwanja wa elimu.

Anasema Almulaa Ali Alqaari katika kitabu cha 'Mirqaatu Almafaatiih': "Wamehitilafiana kuhusina na Mahdi (a.f), kuwa anatokana na kizazi cha Hasani au kizazi cha Huseini(a.s) , na kuna uwezekano akawa amekusanya nasaba zote mbili za Hasani na Huseini(a.s) , ingawaje kilicho dhahiri zaidi ukilinanganisha na kilichotokea kwa watoto wa nabii Ibrahimu Ismaili na Is'haaqa(a.s) , ni kuwa yeye kwa upande wa baba anatokana na Imamu Hasani, wakati kwa upande wa mama anatokana na Imamu Huseini; kwani manabii wote wa wana wa Israeli walitokana na kizazi cha nabii Is'haaq(a.s) , wakati mtume wetu(s.a.w.w) alitokana na kizazi cha nabii Ismaili(a.s) , akachukua nafasi ya manabii wote, -hakika ilikuwa ni badala nzuri!- akawa ndio wamwisho wa mitume. Vilevile, kwakuwa maimamu wengi na wakubwa wa umma huu wametokana na kizazi cha Huseini(a.s) , ni mahala pake Hasani nae apewe badala bora ya mtoto atakaekuwa wa mwisho wa mawalii, atakaechukua nafasi ya wateule na mawasii wengine,“kwakuwa hata imesemekana kwamba: Imamu Hasani(a.s) alipojivua ukhalifa na uongozi kidhahili kama zilivyo pokelewa sifa zake katika kibatu cha 'Al-ahaadithu Anabawiyah'-, alipewa cheo cha utawala wa Alqutbiyah (liwau wilayatul martabat alqutbiyah), hivyo ikawa ni pahala pake kupewa nasaba ya Imamu Mahdi(a.s) inayo fanana na nasaba ya nabii Issa(a.s) , pamoja na kukubaliana kuliinua neno la utume… Na yatakuja yanayoashiria maana hii kwa uwazi kabisa katika hadithi ya Abu Is'haaqa kutoka kwa Ali (Allah awe radhi nae), Mwenyezi Mungu ndie mjuzi zaidi[152] .

JAWABU KUHUSU HADITHI HII:

· Hakika nasaba ya Imamu Mahdi (a.f) haiwezi kuthibitishwa na istihisani za namna hii, bali inabidi ithibitishwe na hadithi sahihi. Hivyo, maneno yake hayana thamani yoyote ile kielimu; kwani yamejengeka juu ya dhana ambazo hazina mashiko katika kuthibitisha nasaba.

· Ama kuhusiana na kauli yake kuwa: "kuna uwezekano wa kuwa amekusanya nasaba zote mbili za Hasani na Huseini(a.s) ", majibu yake ni kama ifuatavyo:

Hakika sisi haturumbani nae juu ya uwezekano wa jambo hilo, bali marumbano yetu nae ni kuhusiana na kuwa Imamu Mahdi (a.f) anatokana na Imamu Hasani(a.s) kwa upande wa baba. Ama kauli yake kuwa: "ingawaje kilichodhahiri zaidi ukilinanganisha na kilichotokea kwa watoto wa nabii Ibrahimu Ismaili na Is'haaqa(a.s) , ni kuwa yeye kwa upande wa baba anatokana na Imamu Hasani, wakati ambao anatokana na Imamu Huseini kwa upande wa mama ", inajibiwa kwakusema kuwa: nasaba kuwa hazithibitishwi kwa kulinganisha mambo wala kwa istihisani ambazo hazina dalili.

Vilevile, hatuwezi kusema kuwa, maadamu baadhi ya hadithi zinaonyesha kuwa Imamu Mahdi (a.f) anatokana na kizazi cha Imamu Hasani(a.s) na zingine zinaonyesha kuwa anatokana na kizazi cha Imamu Huseini(a.s) , hivyo ili kukusanya kauli zote mbili inabidi tukubaliane na kuwa, Imamu Alimahdi (a.f) kwa upande wa baba anatokana na kizazi cha Imamu Hasani, na kwa upande wa mama anatokana kizazi cha Imamu Huseini(a.s) , la hasha, kwani kinyume chake pia kinawezekana. Kwa maana kuwa, anaweza akatokana na Imamu Huseini kwa upande wa baba na Imamu Hasani kwa upande wa mama. Yote haya, ikiwa tukijalia kuwa hadithi zinazosema kuwa anatokana na kizazi cha Imamu Hasani kwa upande wa baba ni sahihi, lakini imeshatangulia kuwa hadithi hizo sio sahihi.

Ama kuhusiana na kauli yake: "kwani manabii wote wa wana wa Israeli walitokana na kizazi cha Is'haaqa, wakati mtume wetu (s.a.w.w) alitokana na kizazi cha Ismaili, akachukua nafasi ya manabii waote, -hakika ilikuwa ni badala nzuri! - akawa ndio wamwisho wa mitume. Vilevile, kwakuwa maimamu wengi na wakubwa wa umma huu ni katika watoto wa Huseini, ni mahala pake Hasani nae apewe badala bora ya mtoto atakaekuwa wa mwisho wa mawalii, atakaechukua nafasi ya wateule na mawasii wengine", majibu tunasema kwamba:

Bila shaka huku ni kulinganisha mambo kusikokuwa sahihi; kwa sababu mtume wetu alikuwa ni wamwisho wa manabii na mbora wao, lakini Imamu Mahdi (a.f) hata kama ni wamwisho wa maimamu, isipokuwa haijathibiti kuwa yeye ni mbora kuliko maimamu wengine.

Na zaidi ya hayo, ni kwamba: kuwateuwa mitume au maimamu hakufanyiki kwa minasaba ya namna hii, bali hufanyika kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kujua kuwa nabii au imamu ni mstahiki wa cheo hicho, kama alivyosema katika kitabu chake:

(اللَّهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسالَتَهُ)

"Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake"[153] .

Ama kauli yake: “kwakuwa hata imesemekana kwamba: Imamu Hasani(a.s) alipojivua ukhalifa na uongozi kidhahili kama zilivyo pokelewa sifa zake katika kibatu cha 'Al-ahaadithu Anabawiyah'-, alipewa cheo cha utawala wa Alqutbiyah (liwau wilayatul martabat alqutbiyah), hivyo ikawa ni pahala kupewa nasaba ya Imamu Mahdi(a.s) inayo fanana na nasaba ya nabii Issa(a.s) , pamoja na kukubaliana kuliinua neno la utume”, majibu yake ni kuwa mazigira haya yanayodaiwa sisi hatuyakubali, wala nasaba haiwezi kuthibitishwa kwayo kama ilivyotangulia.

Na tunashindwa kuelewa kuwa ni nini anakusudia kwa kusema: “cheo cha utawala wa Alqutbiyah!”. Kwani ikiwa makusudio yake ni cheo cha uongozi na waislamu, bila shaka Imamu Hasani(a.s) alikuwa na uongozi mkubwa tu kabla ya kujivua uongozi ule kidhahiri na baada yake. Na akiwa anakusudia kwa maneno hayo kwamba Imamu alipata cheo kingine kinyume na uongozi na uimamu kwa sababu ya kujivua uongozi, hili linahitajia ufafanuzi na uthibitisho kutoka kwake; ili itubainikie kuwa: je ni kweli ilikuwa ni mahala pake nasaba ya Imamu Mahdi(a.s) iwe ni sehemu ya cheo hicho au la?

Ama aliposema kuwa: "Yatakuja yanayoashiria maana hii kwa uwazi kabisa katika hadithi ya Abu Is'haaqa kutoka kwa Ali(a.s) " , jawabu lake nikuwa, tumekwisha bainisha udhaifu wa sanadi na upokezi wa hadithi hii hapo kabla, na kwamba haifai kuwa ni dalili na hoja hapa.

3. Hakika baadhi ya hadithi zao zinaonyesha kuwa Mahdi (a.f) ni katika kizazi cha Imamu Huseini(a.s) . Ameandika Abu Nua'imu Al-Asfahani katika kitabu chake 'Swifatul Mahdi' kwa mapokezi yake kutoka kwa Hudhaifa (Allah awe radhi nae) kuwa alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alituhutubia, akatukumbusha kuwa yeye ni nani, kisha akasema:

(لو لم يبقَ من الدنيا إلا يوم واحد لَطوَّلَ الله عزَّ وجل ذلك اليوم، حتى يبعث فيه رجلاً من ولدي اسمه اسمي). فقام سلمان الفارسي ( رض ) فقال: يا رسول الله، من أي ولدك ؟ قال: (هو من ولدي هذا)، وضرب بيده على الحسين (ع).

"Kama haitakuwa imebakia isipokuwa siku moja tu ili Dunia iishe, basi Mwenyezi Mungu aliyetukuka na kutakasika, atairefusha siku hiyo; ili amlete ndani ya siku hiyo mtu anaetokana na mwanangu, ambae jina lake ni sawa na jina langu". Salmani Alfarisi (Allaha awe radhi nae) akasimama na kusema: "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anaetokana na mwanao yupi?". Akajubu kwa kusema: "Yeye ni kutokana na mwanangu huyu", akaupiga mkono wake kwa Imamu Huseini"[154] .

Na Nua'imu Ibni Hammaad ameandika katika kitabu cha 'Al-fitanu' kwa mapokezi kutoka kwa Aballah Ibni Amru, alisema:

(يخرج رجل من ولد الحسين من قبل المشرق، ولو استقبلتْه الجبال لهدمها واتخذ فيها طُرُقاً).

"Atatokea mtu katika kizazi cha Huseini upande wa Mashariki, (ambae) hata kama milima ingelimuelekea na kumkabili angeivunja na kupasua njia ndani yake"[155] .

Vilevile, hadithi mfano wa hii imepokelewa kutoka kwa Abu Qabiili, amesma:

(يخرج رجل من ولد الحسين لو استقبلتْه الجبال الرواسي لهدَّها واتخذ فيها طُرُقاً).

"Atatokea mtu katika kizazi cha Huseni upande wa Mashariki, (ambae) hata kama ingelimuelekea na kumkabili milima iliyo inuka angeivunja na akapasua njia ndani yake"[156] .

4. Hadithi sahihi zilizopo kelewa kutoka wa maimamu wa nyumba ya mtume(a.s) , zimeonyesha kwamba Imamamu Mahdi (a.f) ni katika kizazi cha Imamu Huseni(a.s) . Miongoni mwa hadithi hizo:

· Ni hadithi sahihi ya Swaduuq, iliyotangulia kutoka kwa Salmani Alfaarisi (Allah awe radhi nae), kwa hakika alisema: " (Siku moja) niliingia kwa mtume(s.a.w.w) , mara Huseini akawa amekaa juu ya mapaja ya mtume(s.a.w.w) , huku mtume akiyabusu macho na midomo yake akisema:

(أنت سيِّد ابن سيِّد، أنت إمام ابن إمام أبو الأئمة، أنت حجة ابن حجة أبو حُجَج تسعة من صلبك، تاسعهم قائمهم).

"Wewe ni bwana mtoto wa bwana, wewe ni Imamu mtoto wa Imamu na baba wa maimamu, wewe ni hojjah mtoto wa hojjah na baba wa mahojjah tisa watokanao na kizazi chako, watisa wao ndie Qaaimu wao"[157] .

· Hadithi hasani ya Abu Hishaam Alja'afari, alisema: "Nilimsikia Abul Hasani Al-askari(a.s) akisema:

(الخلف من بعدي الحسن ابني، فكيف لكم بالخلف من بعد الخلف؟! قلت: ولِـمَ جعلني الله فداك؟ فقال: لأنكم لا ترون شخصه، ولا يحل لكم ذكره باسمه. قلت: فكيف نذكره؟ فقال: قولوا: الحجة من آل محمد صلوات الله وسلامه عليه).

"Mrithi baada yangu ni mwanangu Alhasani. Basi ninyi ni vipi mtakuwa kwa mrithi atakaekuwa baada ya mrithi huyo?! Nikasema: "Mwenyezi Mungu anifanye kuwa fidia yako, kwa nini?". Akasema: "Kwa sababu ninyi hamtamuona, wala hamtaruhusiwa kulitaja jina lake". Nikasema: "Ni vipi tutamtaja?" Akajibu kwakusema: " Semeni: Alhujjah katika ahli wa Muhammad rehema za Mwenyezi Mungu na amani yake iwe juu yake"[158] .

Hizi ndio shubuha muhizo zilizotolewa katika suala hili, na zipo shubuha zingine dhaifu tumeziacha ili kufupisha, mwenyekuzitaka akazitafute mahala pake.

(وَ كَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَ هُوَ الْحَقُّ قُلْ لَسْتُ عَلَيْكُمْ بِوَكيلٍ).

"Na watu wako wameikanusha, nayo ni Haki. Sema: Mimi sikuwakilishwa juu yenu"[159] .

5

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

ISHKALI KUBWA KATIKA ITIKADI YA AHLI SUNNA KUHUSIANA NA IMAMU MAHDI (A.F

Ahli Sunna wanaseama kuwa Imamu Mahdi (a.f) ni mtu atakaezaliwa katika zama za mwisho, Jina lake ni Muhammad, na kwamba anatotokana na kizazi cha bibi Fatwimah(a.s) , kama atakavyoijaza Ardhi usawa na uadilifu kipindi ambacho itakuwa imejaa dhuluma na uovu.

Anasema Alhaafidhu Abul Huseini, Muhammad Ibni Alhuseini Al-Abiri Asajazi, mtunzi wa kitabu cha 'Manaqibu Ashaafi'i', aliefariki mwaka: 363H: " Hakika zimekithiri na kupokelewa kwa wingi hadithi kutoka kwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) zinazomtaja Mahdi (a.f), na kuwa yeye ni katika ahlil-baiti wake, atatawala kwa muda wa miaka saba, na kwamba ataijaza Ardhi uadilifu, na kuwa nabii Issa(a.s) atatoe na kuja kumsaidia kupambana na Dajjaali, atauongoza umma huu, na nabii Issa ataswali nyuma yake"[160] .

Wakati huo huo, Ahli Sunna hawaitakidi kuwa Imamu Mahdi (a.f) ni maasumu na aliehifadhika na kutenda madambi, wala hawaamini kuwa aliteuliwa na Mwenyezi Mungu kwa dalili, kama ambavyo hawakubali kuwa atakuwa anapokea amri kutoka mbinguni, kupitia njia ya malaika au njia nyingine. Bali wanaona kuwa yeye hatatofautiana na makhalifa wengine waliomtangulia, isipokuwa tu Mwenyezi Mungu atampa taufiki na hatimae ataijaza Ardhi usawa na uadilifu.

Anasema dokta Abdul-Aliim Albastawi katika kitabu cha 'Almahdi Almuntadhar': "Hivyo basi, Mahdi sio miongoni mwa mambo ya ajabu Duniani, kuna ajabu gani nikisema kuwa: "Katika zama za mwisho, mtu katika kizazi cha Mtume(s.a.w.w) atasimamia mambo ya waislamu, jina lake litakuwa ni Muhammad bin Abdallah, atahukumu kwa uadilifu na Mwenyezi Mungu atambariki katika utawala wake, umma wa kiislamu katika zama zake utaishi katika neema na raha" Ama yaliyothibiti kuwa Issa atashuka na kwamba Mahdi atamuuwa Dajjaali, ni matukio maalumu kwa ajili ya zama hizo[161] .

Ikiwa hiyo ndio itikadi yao, tunawaambia kuwa: Hakika itikadi hii inakabiliwa na mishkeli kadhaa mikubwa ambayo haina majibu, uchambuzi wa mishkeli hiyo ni kama ifuatavyo:

ISHKALI YA KWANZA: NI KWAMBA IMAMU MAHDI MWENYEWE HATAJIJUA!

Kwa hakika Imamu Mahdi (a.f) ikiwa hapokei amri kutoka mbinguni, bila shaka hataweza kujijua kuwa yeye ndie Mahdi Almuntar; kwa sababu hatakuwa na alama zinazomtofautisha na wengine. Kwani Ahli Sunna hawajataja alama zake maalumu isipokuwa kuwa jina lake ni Muhammad, labda wakaongeza kuwa jina la baba yake ni Abdallah, na kuwa atatokana na kizazi cha bibi Fatwimah(a.s) , au kwamba atakuwa na paji la uso pana na pua ndefu.

Alama hizi hazitoshelezi kumjua na kumtofautisha na watu wengine, ili mwenyewe apate uhakika na matumaini ya kuwa yeye ndie Mahdi alieahidiwa. Kwa sababu hiyo, ndio maana waliodai kuwa ni akina Mahdi katika Ahli Sunna ni wengi. Huwenda baadhi ya watu hao walilifahamu pengo hili kubwa liliopo katika itikadi ya yao, wakalitumia kuwa ndio nafasi ya kujitangazia umahdi, au yawezekana hata walidhani kweli wao ndio akina Mahdi, kwa sababu ya kutokuwa kwao na sifa za Mahdi zilizowazi.

Amesema Al-ustadhi Ahmadi Amiini Almisiri katika kitabu chake 'Dhuhal Islaam': "Miongoni mwa athari zake - yaani, fikra ya Mahdi- ni kutokea mapinduzi yaliyofatana katika historia ya waislaamu. Katika kila zama alijitokeza mtu au watu, kila mmoja akidai kuwa yeye ndie Mahdi Almuntadhar, na kundi la watu likawa likimkusanyikia na kumuunga mkono... Kama ambavyo tukijaribu kuorodhesha watu waliojitokeza katika historia ya kiislaam wakidai umahdi, na tukasherehesha mapindizi waliyoyafanya, na matatizo waliyoisababishia dola ya kiislamu, kama vile: kuleta mpasuko katika dola, kuigawa na kuipotezea muda, mazungumzo juu mambo yao yatakuwa marefu mno"[162] .

Vilevile, amesema Dokta Muhammad Ahmadi Ismaili Almuqaddam katika kitabu chake cha 'Almahdi wa fiqhu ashraatwi asa’a' "Hakika fikra ya Mahdi imewashughulisha watu wengi, hata baadhi yao wakadai kuwa wao ndio akina Mahdi. Na sababu yake, ima ni baadhi yao kuwa na alama za Mahdi, au kwakuwa walijilazimisha kusifika na alama hizo... Miongoni mwao, wapo ambao hawakudai umahdi hata kidogo, lakini walikuwa na sifa njema zilizowafanya wapenzi na wafuasi wao kudai kuwa wao ndio akina Mahdi Almuntadhar"[163] .

Nami niseme kuwa: bila shaka dhana hii ya kudai umahahdi imetokana na kuwepo upenyo na pengo kubwa katika itikadi yao, Pengo lililotoa njia na nafasi ya madai yote haya batili katika kipindi chote cha historia. Wakati hauwezi kukuta mfano wa pengo hilo katika itikadi ya mashie. Ndio maana hatujawahi kumwona shia aliedai kuwa yeye ndie Imamu Mahdi, kwakuwa madai ya namna hii kwao, bila shaka hatima yake ni kupingwa na kutupiliwa mbali. Na sababu yake ni kwamba, Imamu Mahdi kwa Mashia shakhsia yake inakujikana, nasaba yake na sifa zake kamili, ambazo hakuna anaeweza kusifika zao katika hao wanaodai umahdi. Na jambo hili, linatosha kabisa kufunga mlango wa kudai umahdi kwao.

Wala sio mahala pake kabisa, ikasemwa kuwa: Sio lazima Mahdi ajijue kwamba yeye ndie Mahdi, bali inatosha akajua kuwa yeye ni mtu anaetaka kuleta uadilifu katika Ardhi na kuijaza usawa na uadilifu. Kwa sababu tutamjibu mwenyekusema hayo kwa kusema: Nilazima Mahdi ajijue; kwa sababu atadai kuwa yeye ndie Mahdi aliyeahidiwa, na watu watamsifu hivyo hivyo, na yeye itabidi awakubalie[164] . Na yeye kudai hivyo na watu kumridhia bila kujijua na kuwa na uhakika haiwezekani.

ISHKALI YA PILI: ITAMLAZIMU IMAMU MAHDI ATOE KIAPO CHA UTII KWA MMOJA WA WATAWALA WA ZAMA ZAKE

Kwani kama hatatoa kiapo cha utii kwa mmoja wao atakuwa ameacha wajubu muhimu miongoni mwa wajibu za dini, kwakuwa haruhusiwa kulala hata usiku mmoja bila kutoa kiapo cha utii kwa kiongozi, kutoka na kauli ya mtume(s.a.w.w) iliyotangilia kuwa:

(مَنْ مات وليس في عنقه بيعة مات ميتة جاهلية).

"Ataekufa hali yakuwa hajatoa kiapo cha utii, atakuwa kafa kifo cha kijahili"[165] . Vilevile, kauli yake bwana mtume(s.a.w.w) :

(مَنْ مات ليس عليه إمام فميتته جاهلية).

"Yeyote akaekufa bila kuwa na kiongozi, kifo chake ni chakijahili"[166] .

Na ikiwa Imamu Mahdi (a.f) atatoa kiapo cha utii kwa mmoja wa hao watawala, hataruhusiwa kufanya mapinduzi dhidi yake, kwani kumtolea kwake kiapo cha utii kunamanisha kuwa utawala wake ni wakisheria kama ambavyo kunamanisha kuwa ni lazima amtii.

Lakini ishkali hii hauna nafasi katika madhehebu ya Shia, kwa sababu Imamu Mahdi (a.f) ndie imamu na kiongozi wa zama ambae waislamu wote wanalazimika kumtii, kumnusuru na kumtawalisha, wala yeye hatalazimika kumtii yeyote katika raia wake.

ISHKALI YA TATU: UHARAMU WA KUSIMAMA IMAMU MAHDI DHIDI YA WATAWALA WA ZAMA ZAKE

Kwani ikiwa watawala wa zama zake watakuwa wanahukumu kwa uadilfu, hataruhusiwa kusimama dhidi yao. Vilevie, ikiwa watakuwa ni madhalimu; Kwa sababu kwa Ahli Sunna ni wajibu kufanya subira, kusikiliza na kutii, pia hataruhusiwa kusimama dhidi yao.

Imekuja katika Sahihi Muslim kutoka kwa mtume(s.a.w.w) kwamba alisema:

(يكون بعدي أئمة لا يهتدون بهداي ولا يستنُّون بسنَّتي،وسيقوم فيهم رجال قلوبهم قلوب الشياطين في جثمان إنس قال: قلت: كيف أصنع يا رسول الله إن أدركت ذلك؟ قال: تسمع وتطيع للأمير وإن ضرب ظهرك وأخذ مالك فاسمع وأطِعْ).

"Baada yangu watakuja viongozi ambao hawatafuata uongofu wala hawatatenda kwa mujibu wa suna yangu, na miongoni mwao watasimama watu ambao nyoyo zao ni nyoyo za mashetani katika viwiliwili vya kibinadamu". Akasema: Nikamuuliza: "Nitafanyaje ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ikiwa nitazidiriki zama hizo?". Akasema: "Usikilize na utii hata utapigwa mgongo wako na ikachukuliwa mali yako wewe sikiliza na utii"[167] .

Na kutoka kwa Ibni Abbasi amesema: alisema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(مَنْ كَرِهَ من أميره شيئاً فليصبر عليه، فإنه ليس أحد من الناس خرج من السلطان شبراً فمات عليه إلا مات ميتةً جاهلية).

"Yeyote atakaechukizwa na kitu kutoka kwa kiongozi wake, basi amvumilie, kwakuwa hakuna mtu yeyote atakaetoka dhidi ya kiongozi shibiri moja kisha akafa katika hali hiyo, isipokuwa atakuwa amekufa kifo cha kijahili"[168] .

Ndio maana kwa sababu ya kufuata maagizo ya hadithi hizo, mwenendo wa maulamaa wa Ahli Sunna katika kipindi chote ulikuwa hivyo, bali itifaki yao ilijengeka juu ya hilo na maneno yao kuhusina na jambo hilo ni mengi. Kwa hakika wao hawakusimama dhidi ya watawala wa dola la Bani Umaya na lile la Bani Abbasi, hawakumruhusu mtu kuvunja kiapo na kuacha kuwatii watawala hao, bali walijisalimisha kwao licha ya kufanya kwao dhuluma kubwa na kudhihirisha maasi na kutojali.

Anasema Qurtubi: "Jambo ambalo wamelishikilia wasomi wengi nikuwa, kuvumilia na kufanya subira katika kumtii kiongozi muovu ni bola kuliko kutoka dhidi yake, kwa sababu kugogora nae na kutoka dhidi yake kunaondoa amani na kuleta hofu, kunasababisha umwagaji damu, wajinga kutayamani wasiyoendana nayo, kushambuliwa waislamu na kuleta ufisadi Ardhini"[169] .

Na Abu Twayibu Alqunuji katika kitabu chake alichokiita 'Al-ibrah mimaa ja'a fil ghazwi wa shahadah wal hijrah' amesema: "Zimepokelewa hadithi nyingi zikikataza kutoka dhidi ya viongozi maadamu hawajadhihirisha ukafiri waziwazi au wakaacha swala. Ikiwa moja ya mambo haya mawili halijadhihiri kwa kiongozi wa kwanza hairuhiwi kutoka dhidi yake, hata kama atafanya dhuluma kwa kiwango kikubwa, isipokuwa ni lazima kumwamrisha mema na kumkataza maovu kwa kadiri itakavyo wezekana"[170] .

Amesema Ibni Battaal: "Kwa hakika wanazuoni wameafikiana juu yakumtii kiongozi muovu na kushirikiana nae katika Jihadi, kwani kumtii ni bora kuliko kutoka dhidi yake; kwa sababu katika hilo kuna kuziwia umwagaji damu na utulivu wa raia Isipokuwa kiongozi huyo atakapo dhihirisha ukafiri uliowazi, wakati huo haitaruhusiwa kumtii, bali kwa mwenye uwezo itakuwa ni lazima kupambana nae".

Vilevile, Nawawi anasema: "Ama kutoka dhidi yao na kupambana nao ni haramu kwa mujibu wa itifaki ya waislamu, hata kama watakuwa ni waovu na madhalimu. Kwa hakika zimepokelewa kwa wingi hadithi zinazotoa maana hii niliyoitaja Wanasema maulamaa: “Sababu ya kutoruhusiwa kumuondoa kiongozi muovu na kuharamisha kutoka dhidi yake, ni fitina, umwagaji damu na kutoweka umoja na mshikamano vitakavyo sababishwa na kufanya hivyo”. Hivyo, madhara ya kumuondoa madarakani ni makubwa zaidi kuliko kuendelea kubakia". Akaendelea kusema: "Kundi kubwa la maulamaa wa Ahli Sunna katika sheria, hadithi na elimu ya kalamu wanasema: “Kiongozi muovu haondoki madarakani kwa sababu ya uovu, dhuluma wala kutokutenda haki. Haifai kumuondoa na kutoka dhidi yake kwa sababu ya mambo hayo, bali kwa mujibu wa hadhithi zilizopo kwelewa kuhusiana na hilo, ni lazima awaidhiwe na ahofishwe"[171] .

Mwenye kuzitazama kwa umakini hadithi zao, atazikuta nyingi zikionyesha ulazima wa kuwa pamoja, na kwamba siruhusa kufanya mapinduzi hata kama waislamu hawatakuwa na kiongozi. Bukhari na Muslim katika sahihi zao wameandika kutoka kwa mtume(s.a.w.w) kwamba alimwambia Hudhaifa:

(تلزم جماعة المسلمين وإمامهم. فقلت: فإن لم تكن لهم جماعة ولا إمام ؟ قال: فاعتزل تلك الفِرَق كلها، ولو أن تعض على أصل شجرة حتى يدركك الموت وأنت على ذلك).

"Shikamana na umoja wa waislamu na kiongozi wao". Nikasema: "Je kama hawatakuwa na umoja wala kiongozi?". Akasema: "Basi jitenge na hayo makundi yote, hata kama utalazimika kuling'ata shina la mti mpaka yakufike mauti nawe ukiwa katika hali hiyo"[172] .

Baada ya kueleweka hayo, inabainika kuwa kwa Ahli Sunna hakuna kitakacho sahihisha mapinduzi ya Imamu Mahdi (a.f) dhidi ya watawala wa zama zake kwa mujibu wa zinavyo onyesha hadithi sahihi. Ama kwa mashia, mfano wa ishkali hii haina nafasi katika madhehebu yao, kwa sababu Imamu Mahdi (a.f) kwao ni maasumu na amehifadhika na makosa, na anacho kifanya ni haki, sawa sawa asimame dhidi ya watawala hao waovu au asisimame dhidi yao.

ISHKALI YA NNE: HAKIKA WATU HAWATAWEZA KUMTOFAUTISHA IMAMU MAHDI ALMUNTADHAR NA WATU WENGINE

Na sababu yake ni kuwa, Imamu Mahdi (a.f) kwa Ahli Sunna hana alama zinazomtofautisha na wengine, wala hakuna karama atakazokuwa nazo zinazomtenganisha na watu wengine wanaodai umahdi. Na hili ni jambo ambalo liliwakanganya wengi kiasi cha baadhi yao kuwasadikisha wenyekudai umahdi au wengine kuwadhania baadhi ya watu kuwa ndio akinamahdi.

Ama kwa upande wa mashia jambo ni rahisi kwao, kwakuwa wao hawaukubali umahdi wa mtu ambae hatakuwa na karama zinazoonyesha kuwa ni mkweli katika madai yake. Kila atakaeshindwa kudhihirisha karama inayothibitisha kuwa yeye ndie Mahdi, basi huyo kwao atakuwa ni muongo na mzushi.

Wala sio mahala pake kabisa, ikasemwa kuwa: Sio lazima watu wajue kuwa yeye ndie Mahdi Almuntadhar, bali inatosha wakajua kuwa yeye ni mtu anaetaka kusimamisha uadilifu, hivyo wakamfuata kwa hilo. Kwa sababu tutajibu kwakumsema kuwa: Nilazima watu wamjue kuwa yeye ndie Mahdi Almuntadhar; ili wamnusu katika harakati yake ya amani ikiwa kweli wanaamini kuwa ni wajibu wao kumnusuru dhidi ya adui yake. Lakini pia nilazima wamjue ili wasije kumpiga vita na kuwanusuru watawala waovu dhidi yake ikiwa wanaamini kuwa ni wajibu wao kusimama nae.

ISHKALI YA TANO: NI WAJIBU KUPAMBANA NA IMAMU MAHDI NA KUMZIWIA KUFANYA MAPINDUZI

Na sababu ya hilo, nikuwa yeye atakuwa amechupa mipaka ya utii na amefarakanisha umoja.

Ametaja Muslim katika Sahihi yake kwa mapokezi kutoka kwa Arfajah, alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akisema:

( إنه ستكون هَنَاتٌ وهنات، فمن أراد أن يفرِّق أمر هذه الأمة وهي جميع فاضربوه بالسيف كائناً من كان).

"Kwa hakika itatokea shari na ufisadi, yeyote atakaetaka kulifarakanisha jambo la umma huu hali yakuwa umeshikamana, mpigeni kwa upanga hata kama ni nani"[173] . Na kutoka kwa Arfajah, alisemema: nilimsikia mtume wa Mweyezi Mungu(s.a.w.w) akisema:

(مِنْ أتاكم وأمركم جميع على رجل واحد يريد أن يشق عصاكم أو يفرِّق جماعتكم فاقتلوه).

"Yeyote atakaekujieni hali yakuwa jambo lenu wote liko kwa mtu mmoja (mmempa kiapo cha utii), akitaka kuivunja fimbo yenu au kuusambaratisha umoja wenu, basi pambaneni nae"[174] .

Amesema Qurtubi katika tafsiri yake: "Ikiwa Khaarijii[175] atatoka dhidi ya kiongozi anaejulikana kwa uadilifu, itakuwa ni wajibu wa watu kupambana nae, na ikiwa kiongozi ni muovu na kharijiyu ni mwenye kudhihirisha uadilifu, haipaswi kwa watu kuharakia kumnusuru Kharijiyu mpaka jambo lake kuhusina na uadilifu anaoudhihirisha libainike, au watu waafikiane kumng'oa madarakani kiongozi wa mwanzo"[176] .

Nasema kuwa: Hadithi na maneno yao vinaonyesha ulazima wa kupambana na kila mwenyekutoka dhidi ya kiongozi, na kwakuwa Imamu Mahdi (a.f) hana sifa maalumu katika huu upande, hivyo hizi hadithi zinamshamili na yeye, na zinajibisha kupambana nae na kumziwia kufanya mapinduzi.

Ni jambo lililowazi kuwa ishkali hii haina nafasi katika madhehebu ya Shia, kwa sababu ya kuamini kwao kwamba Imamu Mahdi (a.f) ni kiongozi ambae niwajibu atiiwe na anusuriwe.

ISHKALI WA SITA: UWAJIBU WA KUWATII WATAWALA WAOVU PINDI ATAKAPO SIMAMA IMAMU ALMHDI (A.F) DHIDI YAO

Hakika Ahli Sunna ikiwa watakuwa wamekwishatoa kiapo cha utii kwa viongozi na watawala wa zama zao kuwa watatii na kusikia, kwa mujibu wa hadithi aliyoitoa Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Abdallah Ibni Omar kutoka kwa mtume(s.a.w.w) alisema:

( مَنْ خلع يداً من طاعة لقي الله يوم القيامة لا حُجَّة له).

"Atakae ishi bila kiongozi, atakutana na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama akiwa hana hoja"[177] , hawataruhusiwa kuvunja baia yao ya kusikia na kutii. Na hadithi nyingine kutoka kwa mtume(s.a.w.w) alisema:

(وإذا رأيتم مِنْ ولاتكم شيئاً تكرهونه، فاكرهوا عمله، ولا تنزعوا يداً من طاعة).

"Na mtakapoona kitu kinachokuchukizeni kwa viongozi wenu, basi kichukieni kitendo chake, wala msitoe mkono kwenye kiapo"[178] . Vilevile, kutoka kwake(s.a.w.w) alisema:

(اسمعوا وأطيعوا، فإنما عليهم ما حُمِّلوا، وعليكم ما حُمِّلتم).

"Sikilizeni na mtii, kwa hakika ni jukumu la viongozi kutekeleza waliyobebeshwa, na ninyi ni jukumu lenu kutekeleza mliyobebeshwa"[179] .

Na kama hawatakuwa wamewatolea kiapo cha utii hao watawala kuwa watasikia na kutii, basi watakuwa wameaacha jambo lililowawajibikia la ulazima wa kuharakia kutoa kiapo cha utii kwa kiaongozi wa waislamu kama zilivyoonyesha hadithi zao na kauli za maulamaa wao zilizotajwa huko nyuma.

Na wakati huo itabidi tujiulize: Ni upi msimamo wao kuhusiana na Imamu Mahdi (a.f)? Je watamtolea kiapo cha utii na watamnusuru wakati walishatoa kiapo kwa mtu mweingine? au watashakamana na kiapo chao kwa awali walichokitoa kwa watawala zama zao na hivyo wawanusuru wao dhidi ya Imamu (a.f), na hawatambaii Imamu isipokuwa baada ya kushinda?!

Lakini Shia kwakuwa hawaoni ulazima wa kumtolea kiapo cha utii asiekuwa Imamu maasumu na aliehifadhika na kutenda madhambi, ishkali kimsingi haina nafasi kwao.

ISHKALI YA SABA: UTAWALA WA IMAMU MAHDI (A.F) HAUTAKUWA HALALI NA WAKISHERIA!

Na sababu yake ni kuwa uhalali wa utawala na uongozi ima uwe kwa njia ya dalili ya aya na hadithi au kwa njia baia na kutoa kiapo cha utii.

Ama dalili za aya na hadithi zinazoonyesha kuwa Imamu Mahdi (a.f) ni Imamu na kiongozi hawana, kwa sababu hawakubali kuwa kuna yeyote aliyeteuliwa kwa aya au hadithi, na hadithi za Mahdi kwao hazijamtaja mtu makhsusi, isipokuwa zimetaja baadhi ya sifa zake kidogo.

Ama kuhusiana na kiapo cha utii, ikiwa baadhi ya waislamu ndio watakaompa kiapo cha utii, kiapo chao hakitakua na manufaa kwa mjibu wa hadidhi iliyopokelewa kutoka kwa Omari Ibni Khatwab, alisema:

( مَنْ بايَعَ رجلاً عن غير مشورة من المسلمين فلا يُتابَع هو ولا الذي بايعه تغرَّة أن يُقتلا).

"Yeyote atakaetoa kiapo cha utii kwa mtu bila ya mashauriano ya waislamu, atakuwa kaiweka nafsi yake na nafsi ya aliyempa kiapo hicho katika hatari ya kuuwawa"[180] .

Na ikiwa watakaompa kiapo cha utii ni wale wanaodai kuwa wao ni Ahlil- Hilli Wal - Iqdi, vilevile kiapo chao hakitakuwa na maana yoyote, kwakuwa baada ya zama za maswahaba hakuna kundi la watu linalofahamika kwa sifa hiyo kama ilIvyotangulia.

Na ikiwa waislamu wote ndio watakaompa kiapo cha utii, bila shaka kiapo cha namna hii hakiwezi kutokea labda mpaka imamu (a.f) atakapoyatwala maeneo yote ya kiislamu, na hii inamanisha kuwa uongozi wake kabla ya kupewa kiapo cha utii hautakuwa halali wala waisheria kwa hali yoyote, jambo ambalo athari yake nikuwa hairuhusiwi kumnusuru katika harakati yake ya amani, na kwamba kila atakaekuwa alimnusuru atakuwa kafanya madhambi.

Kwa sababu hii alisema Hafsu Ibni Gayaath: Nilimwambia Sufiani Athouri:

(يا أبا عبد الله، إن الناس قد أكثروا في المهدي فما تقول فيه؟ قال: إنْ مَرَّ على بابك فلا تكن معه في شيء حتى يجتمع الناس عليه).

"Ewe Abu Abdallah, hakika watu wamekithirisha maneno kuhusiana na Mahdi (a.f), wewe unasemaje kuhusiana nae? akasema: "Ikiwa atapita mlangoni kwako basi usishirikiane nae katika chochote mpaka watu wamkusanyikie "[181] .

ISHKALI YA NANE

Ni kwanini tendo la kuijaza ardhi usawa na uadilifu halikutimia kupitia kwa baadhi ya manabii na mitume au watu wengine wanaofadhilishwa na Ahli Sunna juu ya Imamu Mahdi (a.f), na badala yake litimie kupitia kwa mtu ambae fadhila na ubora wake ni mdogo ukimlinganisha na watu wema wengi waliokuwa katika umma huu?

Kwa hakika Ahli Sunna hawawalinganishi Ahli baiti(a.s) na wengi miongoni mwa makhalifa wao, wanazuoni wao na watu wao wema, achilia mbali kuwalinganisha na baadhi ya manabii waliotangulia, ndio maana wakaupinga kila ubora wa Ahli Baiti (a.f) ambao haujathibiti kwa mtu mwengine wa umma huu, kama vile: kuponya ukoma na vibarango, na kumhuisha mfu na mfano wake.

ISHKALI YA TISA

Kupingana kwa hadithi zinazowajibisha kuwatii watawala waovu na kutotoka dhidi yao pindi atakasimama Imamu Mahdi (a.f) dhidi yao.

Hii ni kwa sababu hadithi zilizojaa ndani vitabu vyo vya sahihi, haziruhusu kutoka dhidi ya watawala waouvu, bali zinawalazimisha waislamu kuwatii kama ilivyotangulia kwa ufafanuzi, lakini pia ndani ya hadithi hizo hakuna kilichoruhusu kusimama kwa Imamu Mahdi kama jambo maalumu.

Kwa minajili hiyo, tubakia na moja ya khiyari mbili, ima tuhukumu kuwa hadithi zote zinazokataza kisimama dhidi ya viongozi waovu ni batili na sio sahihi hata kama wamezitaja katika vitabu vyao vya sahihi, au tuhukumu kuwa kusimama kwa Imamu Almhdi (a.f) dhidi ya watawala hao sio sahihi, kwa sababu kunapingana hadithi sahihi.

Ifahamike kuwa, mfano wa ishkali hii haina nafasi kwa mashia, kwakuwa hawana hadithi zinazokataza kusimama dhidi ya watawala waovu, ambazo zinamshamili na imamu maasumu.

ISHKALI YA KUMI: KWAMBA IMAMU MAHDI (A.F) NI MBORA KULIKO ISSA IBNI MARIAM(A.S)

Na hii ni kwakua Ahli sunna wameafikiana -kama ilivyotangulia katika maneno ya Al-Abri Asajzi- kwamba nabii Issa(a.s) ataswali nyuma ya Imamu Mahdi, na haya yamepokelewa katika hadithi zao. Ametaja muslim katika sahihi yake kutoka kwa jaabir kwamba alisema: nilimsikia mtume(s.a.w.w) akisema:

(لا تزال طائفة من أمتي يقاتلون على الحق ظاهرين إلى يوم القيامة. قال: فينزل عيسى بن مريم ( ع ) فيقول أميرهم: تعال صلِّ لنا. فيقول: لا، إنَّ بعضكم على بعض أُمَراء تكرمةَ الله هذه الأمَّة).

"Kundi katika umma wangu halitaacha kupigania haki mpaka siku ya Kiyama” Akasema: "Kisha atashuka Issa Ibni mariam(a.s) ” Kiongozi wao atasema: “Njoo utuswalishe”. Nabii Issa(a.s) atasema: “Hapana, hakika baadhi yenu ni viongozi wa wengine, hii ni heshima ya mwenyezi mungu kwa uma huu”[182] .

Na kutoka kwa Abu Hurairah, amesema: Alisema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(كيف أنتم إذا نزل ابن مريم فيكم، وإمامكم منكم).

"Je hali yenu itakuwaje atakapo teremka Ibni Mariam kwenu, na imamu wenu akiwa yuko kati yenu?”[183] .

Sehemu ya ishkali ni hapa : ni vipi Issa Ibni Mariam(a.s) amfuate Imamu Almhdi (a.f) ambae ni mmoja kati yawatu wema wa uma huu, hali ya kuwa yeye ni nabii, bali ni katika manabii ulil- azm?

Ikiwa inasemwa kuwa: hilo litafanyika kwa amri ya Issa(a.s) . Nasi tutasema kuwa: hakika mbora hapaswi kumfuata asiekuwa mbora, na nabii hapaswi kumfuata alie chini yake. Hivyo, kukataa kupita mbele kuwaswalisha watu ni dalili kuwa Mahdi ni bora kuliko yeye.

Jambo lingine linalothibitisha hilo, waislamu wameafikiana kwamba atakaeshika uongozi wa umma huu ni imamu Mahdi na sio Issa(a.s) kwani yeye atakuwa ni miongoni mwa raia wa Imamu(a.s) . Na ishkali hii haina utatuzi zaidi ya kusema kuwa Mahdi (a.f) ni mbora zaidi nabii Issa(a.s) .

Baadhi yao wamesema kwa nabii Issa(a.s) ataswali nyuma ya Imamu Mahdi (a.f) mara moja tu, na baada ya hapo nabii Issa(a.s) ndie atakeendelea kuwaswalisha waislamu mpaka atakapofariki. Isipokuwa kauli hii haina ushahidi, bali inapingwa na hadithi sahihi zinazo onyesha kuwa Imamu Mahdi (a.f) baada ya kudhihiri kwake hakutakuwa na wakumtangulia, na kwamba yeye ndie atakuwa kiongozi na khalifa wa waislamu, atakaeijaza ardhi usawa na uadilifu licha ya nabii Issa(a.s) kushuka katika zama zake.

Na zaidi ya hayo, hadithi ya Muslim imeeleza wazi sababu ya uimamu na uongozi wa Mahdi (a.f) kuwa ni takrima kutoka kwa Mwenyezi Mungu alietakasika kwa umma huu, kumfanya kiongozi na imamu atokane na umma huu na sio mwingine, jambo linaloafikiana na kuendelea uongozi kama isivyofichika.

6

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

MAMBO YALIYO INJE YA ADA KATIKA KADHIA YA IMAMU MAHDI (A.F)

Mara nyingi baadhi ya wasiojua wamekuwa wakisema kuwa, itikadi ya Shia kuhusiana na Imamu Mahdi (a.f) ni itikadi isiyokubalika; kwa sababu imesimama juu ya misingi ya mambo ya kubuni na siyokuwa na uhakika, kwa sababu haingii akilini kwamba Mahdi awe ameishi miaka zaidi ya elfu moja, kama ambavyo ni jamo lisilokubalika Mahdi awe ni kiongozi na Imamu wa waislamu akiwa na umri wa miaka mitano!

Ama itikadi ya Ahli Sunna, ni itikadi ambayo imetokana na hadithi sahihi zisizopingana na akili na uhalisia wa mambo; kwani zimeepukana na yaliyo inje ya ada na yasiyokubalika. Ahli Sunna wanaamini kuwa Mahdi ni mtu atakaezaliwa katika zama za mwisho, ambae Mwenyezi Mungu atamwafikisha kuijaza ardhi usawa na uadilifu baada ya kujaa dhuluma na uovu, sio chini ya hayo wala zaidi.

Lakini ukweli ni kuwa maneno haya hayana uadifu hata kidogo; kwani Imani ya Ahli Sunna nayo juu Imamu Mahdi (a.f) imekusanya mambo yaliyo nje na ada. Mambo hayo ni mengi, miongoni mwayo ni:

IMAMU MAHDI(A.F) KUZITAWALA PANDE ZOTE ZA DUNIA

Kwa hakika atakalolifanya Imamu Mahdi (a.f) -yaani kutawala pande zote za Ardhi na kuijaza usawa na uadilifu- ni jambo lililo nje ya ada na kawaida; kwani jambo hilo halijafanywa na yeyote kati ya manabii, makhalifa na watu wema wengine, bali hakuna mtu mwenye uwezo wakulifanya hata kama atakuwa kapewa pawa na wasaidizi kiasi gani, kama matukio yanayojiri katika zama zote yanavyoshudilia hilo.

MWENYEZI MUNGU ATAMUANDALIA IMAMU MAHDI(A.F) MAZINGIRA YA USHINDI NDANI YA USIKU MMOJA

Ahmad Ibni Hanbal, Ibni Maajah, Abu Nuaim na Ibni Abu Shaibah wameandika kutoka kwa Ali(a.s) kuwa alisema: Alisema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

( المهدي مِنَّا أهل البيت ، يصلحه الله في ليلة).

"Mahdi ni katika sisi Ahli Baiti, Mwenyezi Mungu atamuandaa ndani ya usiku mmoja"[184] . Yaani, Mwenyezi Mungu atamtengenezea jambo lake ndani ya usiku mmoja[185] , kwa kumwandalia sababu na mazingira ya ushindi.

Mshereheshaji wa Sunan Ibni Maajah Amedai kuwa, makusudio ya hadithi hiyo ni kumwandaa Imamu kwa ajili ya uongozi ndani ya usiku mmoja[186] . Haifichiki kuwa, sawa sawa kuandaa huko kuwe ni maana hii au ile, yote bado ni mambo ambayo yako nje ya ada.

HAKIKA MAHDI HATADHIHIRI MPAKA JUA LITAKAPO CHOMOZA NA ALAMA

Ameandika Abdurazaki katika kitabu cha 'Almuswannafu' kwa mapokezi sahihi kutoka kwa Ali Ibni Abdallah Ibni Abbaasi, alisema:

(لا يخرج المهدي حتى تطلع مع الشمس آية).

"Hatadhihiri Mahdi mpaka jua lichomoze na alama"[187] . Abdurazaki kaipokea kutoka kwa Muammar kutoka kwa Inbi Twawuusi kutoka kwa Ali Ibni Abdallah Ibni Abbaasi, na upokezi huu ni sahihi, na wapokezi wa hadithi hiyo ni waaminifu kwao.

Vilevile, Daaru Qutni ameandika katika Sunan yake kutoka kwa Jaabir kutoka kwa Muhammad Ibni Ali, alisema:

(إن لمهديِّنا آيتين لم تكونا منذ خلق السماوات والأرض، ينكسف القمر لأول ليلة من رمضان، وتنكسف الشمس في النصف منه، ولم تكونا منذ خلق الله السماوات والأرض).

"Kwa hakika Mahdi wetu ana alama mbili abazo hazijawahi kutokea tangu Mbingu na Ardhi vinaumbwa. Mwezi utapatwa usiku wa Ramadhani mosi, na Jua litapatwa katikati yake, na mambo haya hayajatokea tangu kuumbwa mbingu na Ardhi”[188] .

NABII ISSA(A.S) KUSHUKA ZAMA ZA ALMAHDI(A.F) NA KUSWALI AKIWA NYUMA YAKE

Ufafanuzi wa jambo hili umekwisha tangulia hapo kabla.

JESHI LITAKALOTOKA LIKIKUSUDIA KUMUUWA IMAMU ALMHDI(A.F) LITAANGAMIZIWA KATIKA ARDHI YA ALBAIDAU

Amesema Ibni Habbaan katika sahihi yake: "Katika kusimulia hadithi yenyekueleza wazi kuwa watu watakao angamizwa, hakika wao ni wenyekutoka wakimkusudia Mahdi kwa lengo la kumnyanganya utawala". Vilevile kanukuu kutoka kwa Ummu Salamah, kwamba alisema: Alisema mjume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(يكون اختلاف عند موت خليفة، فيخرج رجل من قريش من أهل المدينة إلى مكة، فيأتيه ناس من أهل مكة فيُخرجونه وهو كاره، فيبايعونه بين الركن والمقام، فيبعثون إليه جيشاً من أهل الشام، فإذا كانوا بالبيداء خُسف بهم، فإذا بلغ الناس ذلك أتاه أبدال أهل الشام وعصابة أهل العراق فيبايعونه... فيقسم بين الناس فَيْأَهم، ويعمل فيهم بسُنَّة نبيِّهم (ص)، ويلقي الإسلام بجرانه إلى الأرض، يمكث سبع سنين )

"Kutakuwa na ikhtilafu wakati wa kifo cha kiongozi, basi mtu mmoja katika Makuraishi atatoka Madina kuelekea Makka, watu watamfuata kisha watamtoa akiwa simwenyekupenda, na watampa kiapo cha utii akiwa kati ya Rukuni na Maqaam. Watamtumia jeshi katika watu wa Shaam (ili kwenda kumuuwa), watakapokuwa katika ardhi ya tambarare (kati ya Makka na Madina) wataangaminzwa. Taarifa hiyo itakapowafikia watu, watamjia watu wema miongoni mwa watu wa Shaam na kundi katika watu wa Iraq, kisha watampa kiapo cha utii... Atazigawanya ngawira kwa watu, na atawatendea kwa mujibu wa Sunna ya mtume wao (s.a.w.w), atauimarisha Uislamu Ardhini, na atabakia kwa muda wa miaka saba"[189] .

Suala la kuangamizwa jeshi katika ardhi ya tambarare limetajwa katika hadithi nyingi sana walizozitaja wahifadhi wengi wa hadithi, kama vile: Muslim katika kitabu chake cha Sahihi, Alhaakem katika Mustadrak, Ahmad Ibn Hanbali katika Musnadi na wengineo[190] .

MAAJABU YALIYOTAJWA KUHUSIANA NA VITA VYAKE

Ametaja Muslim katika kitabu chake cha Sahihi kwa mapokezi yake kutoka kwa Abu Hurairah kwamba mtume(s.a.w.w) alisema:

(سمعتم بمدينة جانبٌ منها في البر وجانبٌ منها في البحر؟ قالوا: نعم يا رسول الله قال: لا تقوم الساعة حتى يغزوها سبعون ألفاً من بني إسحاق، فإذا جاؤوها نزلوا، فلم يقاتلوا بسلاح، ولم يرموا بسهم، قالوا: ( لا إله إلا الله والله أكبر ) فيسقط أحد جانبيها. قال ثور: لا أعلمه إلا قال: الذي في البحر، ثم يقولوا الثانية: (لا إله إلا الله والله أكبر) فيسقط جانبها الآخر ، ثم يقولوا الثالثة : ( لا إله إلا الله والله أكبر ) فيفرج لهم، فيدخلوها فيغنموا، فبينما هم يقتسمون المغانم إذ جاءهم الصريخ فقال: ( إن الدجال قد خرج ) فيتركون كل شيء ويرجعون)

"Je mmesikia mji ambao upande wake mmoja ni nchi kavu na mwingine ni bahari? wakasema: "Ndio, ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu". Akasema: "Hakitasimama Kiyama mpaka watakapo ufavamia mji huo watu sabini wanaotokana na kizazi cha nabii Is'haaka(a.s) . Watakapoufikia mji huo watapumzika, na hawatapigana kwa silaha wala hawatatupa mshale, bali watasema: "Laa ilaha ilallah wallahu akbaru", kisha upande wake mmoja utaanguka. Thouri Akasema: “Siujui upande huo, isipokuwa alisema: ni upande ambao upo baharini”. Kisha watasema kwa mara ya pili: "Laa ilaha ilallah wallahu akbaru" upande wake wa pili nao utaanguka, kisha watasema kwa mara ya tatu: "Laa ilaha ilallah wallahu akbaru", watapewa ushindi. Hapo wataungia mji huo na watapata ngawaira. Katika kipindi ambacho wao watakuwa wakigawana ngawira hizo, mara atawajia mtoa mnada na kusema: "Kwa hakika Dajjal ametoka", wataacha kila kitu na kurejea"[191] .

Ninasema kuwa: Kauli yake: "Kwa hakika Dajjal ametoka", ni dalili kuwa watu hawa waliofungua mji huo ni wafuasi na jeshi la Imamu Mahdi (a.f), kwani Dajjal atatoka baada ya kudhihiri kwa Imamu (a.f).

Qurtubi baada ya kuitaja hadithi hii katika kitabu chake cha ‘Akhbaarul Mahdi’ Alisema: "Huwenda ushindi wa Mahdi ukawa wa namna mbili: mara kwa kupingana na mara nyingine kwa takbira, yaani kwa kusema: " Laa ilaha ilallah wallahu akbaru"[192] .

KWAMBA MBINGU ITATEREMSHA MVUA YAKE NA ARDHI ITATOA BARAKA ZAKE

Alhaakem katika kitabu cha Mustadrak ametaja kutoka kwa Abu Saidi Alkhidri kwamba mtume alisema:

(فيبعث الله عزَّ وجل رجلاً من عترتي، فيملأ الأرض قسطاً وعدلاً كما مُلئت ظلماً وجوراً، يرضى عنه ساكن السماء وساكن الأرض، لا تدَّخر الأرض من بذرها شيئاً إلا أخرجتْه، ولا السماء من قطرها شيئاً إلا صبَّه الله عليهم مدراراً).

"Kisha Mwenyezi Mungu atamtuma mtu katika kizazi changu, ataijaza Ardhi asawa na uadilifu baaya kujazwa dhuluma na uovu, waishio mbinguni na ardhini watamridhia, Ardhi haitabakisha mbegu yoyote isipokuwa itaitoa, na mbingu haitabakisha mvua yake isipokuwa Mwenyezi Mungu ataimimina juu yao"[193] .

UMMA UTANEMEKA KWA NEEMA AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA HAPO KABLA

Ibni Maajah, Alhaakem, Twabraani na wengineo wametaja katika misnadi zao kutoka kwa Abu Said Alkhidri kwamba Mtume(s.a.w.w) alisema:

(يكون في أمتي المهدي، إن قُصِرَ فَسَبْع وإلا فتِسْع، فتنعم فيه أمتي نعمة لم ينعموا مثلها قط، تؤتَى أُكُلها، ولا تدَّخر منهم شيئاً، والمال يومئذ كُدُوس، فيقوم الرجل فيقول: يا مهدي أعطني. فيقول: خذ).

"Mahdi atakuwa ni katika umma wangu, ikiwa atakukumu kwa muda mfupi basi itakuwa ni miaka saba, kama sihivyo basi ni miaka tisa. Umma wangu utanemeka kwa neema ambazo wahajapata kunemeka nazo kamwe, Ardhi itatoa mazao yake wala haitabakisha kitu, mali kipindi hicho zitakuwa rundo, hata itafikia hatua mtu kusema: "Ewe Mahdi, naomba (mali)". Imamu atamwambia: "Chukua"[194] .

CHUKI NA WIVU VITATOWEKA KATI YA WATU

Muslim na Ibni Habbaan katika sahihi zao wamepokea kutoka kwa Abu Hurairah kwamba alisema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(والله ثم لينزلنَّ ابن مريم حكماً عادلاً، فليكسرنَّ الصليب، وليقتلنَّ الخنزير، وليضعنَّ الجزية،ولتُتركنَّ القِلاص فلا يُسعَى عليها، ولتذهبنَّ الشحناء والتباغض والتحاسد، وليَدْعُوَنَّ (وليُدعَوُنَّ) إلى المال فلا يقبله أحد)

"Ninaapa kwa jina Allah, kisha bila shaka atateremka mwana wa Mariam awe ni hakimu mwadilifu, kisha kwa yakini atauvunja masalaba, atauwa nguruwe, ataweka kodi (kwa makafiri), ndama wa ngamia wataachwa na hakuna ataeshughilika nao, chuki na wivu vitatoweka kwa watu, watu wataitwa kuchukua mali hakuna atakubali kuchukua"[195] .

MBWA MWITU ATASHIRIKIANA NA MBUZI NA KONDOO KATIKA MALISHO, NA SIMBA NA NGAMIA WATACHANGIA MALISHO, NA WATOTO WATACHEZEA NYOKA

Ameandika Haakim Nishabouri katika Mustadrak, Ibni Habbaan katika Sahihi na Ahmad katika Musnadi kutoka kwa Abu Hurairah (Allah awe radhi nae), kwamba alisema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :

(إن روح الله عيسى بن مريم نازل فيكم... فيدق الصليب، ويقتل الخنزير، ويضع الجزية، ويدعو الناس إلى الإسلام، فيهلك الله في زمانه المسيح الدجال، وتقع الأمنة على أهل الأرض حتى ترعى الأسود مع الإبل والنمور مع البقر والذئاب مع الغنم، ويلعب الصبيان مع الحيَّات لا تضرُّهم )

"Hakika Ruhullah Issa mwana wa Mariam(a.s) ni atateremka kwenu... kisha atauvunja msalaba, na atauwa nguruwe, atawawekea kodi makafiri, na ataawalingania watu kwenye Uislamu, kisha Mwenyezi Mungu atamuangamiza Masihi Dajjal katika zama zake, na amani itaenea kwa watu ardhini kiasi cha simba na ngamia kulisha kwa pamoja, chui na ng'ombe, mbwa mwitu na mbuzi na kondoo nao watalisaha kwa pamoja, watoto watacheza na nyoka na hazitawadhuru..."[196] .

MASWAHABA WA MAHDI (A.F) MWENYEZI MUNGU NDIE ATAKAE WAKUSANYA NA KUZIUNGANISHA NYOYO ZAO

Ametaja Alhaakim Nishaaburi katika Mustadrak, na Thahabi akasahihisha na kuiafiki, kutoka kwa Ali(a.s) kwamba alisema:

(ذاك يخرج في آخر الزمان إذا قال الرجل: ( الله الله ) قُتل ، فيجمع الله تعالى له قوماً قزع كقزع السحاب، يؤلِّف الله بين قلوبهم، لا يستوحشون إلى أحد، ولا يفرحون بأحد، يدخل فيهم على عدة أصحاب بدر، لم يسبقهم الأولون ولا يدركهم الآخرون، وعلى عدد أصحاب طالوت الذين جاوزوا معه النهر)

"Huyo atatokea katika zama za mwisho, wakati mtu atakapokuwa akisema: "Allah Allah" anauwawa, wakati huo Mwenyezi Mungu atamkusanyia watu ambao watakaokuwa wamesambaa mfano wa mawingu ya msimu wa vuli yaliyosambaratika yanavyokusanyika, Mwenyezi Mungu ataziunganisha nyoyo zao, kiasi kuwa hawatamuogopa mtu yeyote, wala mtu kujiunga nao hakutawafanya wafurahie, ididi yao ni sawa na idadi ya watu wa Badri, hakuna aliewahi kufikia mfano wa daraja yao miongoni mwa waliotangulia, wala hakuna watakaolifikia, vilevile idadi yao ni sawa na idadi ya wafuasi wa Twalout waliovuka nae mto"[197] .

MAMBO MENGI YANAYOHUSIANA NA DAJJALI YAKO NJE YA ADA

MIONGONI MWA MAMBO YAHO: kwamba atakuwa na mito miwili, mmoja wa maji na mwingine wa moto.

Ameandika Muslim na Ibni Habbaani katika Sahih zao na wasiokuwa hao pia wameandika hadithi hii kutoka kwa Rab'ii Ibni Haraash, alisema: " Siku moja Hudhaifah na Abu Maso'ud walikusanyika, Hudhaifah akasema: Mimi ni mjuzi zaidi wa mambo atakayokuwa nayo Dajjali, kwa hakika atakuwa ana mto wa maji na mto wa moto, ule mtakao ona ni moto yatakuwa ni maji, na ule mtakao ona ni maji utakuwa ni moto, hivyo yeyote miongoni mwenu atakaekuwa kipindi hicho akataka kunywa maji, basi anjwe katika ule mto anaodhania kuwa ni moto; kwani atakuta ni maji"[198] .

MAMBO MENGINE : kwamba milima ya mikte na mito ya maji itakuwa ikitembea na Dajjali.

Kwa hakika Ahmad Ibni Hambali ameandika katika Musnadi wake, na wengine pia wameandika kwamba mjumbe Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(أنذرتُكم المسيح، وهو ممسوح العين، قال: أحسبه قال اليسرى، يسير معه جبال الخبز وأنهار الماء).

"Ninakuhadharisheni na Masihi Dajjali, na yeye ni kipofu, kasema: nadhani alisema jicho la kushoto, milima ya mkate na mito ya maji vitatembea nae "[199] .

Jambo lingine: kwamba kati ya macho yake kuna maandishi ambao wataweza kuyasoma wasiojua kusoma na wanaojua.

Muslim ameandika katika Sahihi yake kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(وإن الدجال ممسوح العين، عليها ظفرة غليظة، مكتوب بين عينيه: (كافر) يقرؤه كل مؤمن كاتب وغير كاتب).

"Hakika Dajjali ni kipofu, juu ya jicho lake kutakuwa ngozi[200] nzito, kati ya macho kutakuwa kumeandikwa neon: “kafiri” atakalolisoma kila muumini mwenye kujua kuandika na asiejua"[201] .

Jambo lingine: kwamba Dajjali atakapomuona nabii Issa(a.s) , atayeyuka kama inavyoyeyuka chumvi.

Hakika Muslim, Ibni Habbaan, na wengineo wameandika kutoka kwa Abu Hurairah katika hadithi kwamba alisema:

(فإذا جاؤوا ـ أي المؤمنون ـ الشام خرج، فبينما هم يُعِدُّون للقتال يُسوُّون الصفوف إذ أُقيمت الصلاة، فينزل عيسى بن مريم ( ع ) فأمَّهم، فإذا رآه عدو الله ذاب كما يذوب الملح في الماء، فلو تركه لانذاب حتى يهلك، ولكن يقتله الله بيده، فيُريهم دمه في حربته)

"(Waumini) watakapokuja Shamu atatoka, wakati wao wakijiandaa kwa ajili ya vita wanapanga mistari, mara itakimiwa Swala, hapo atateremka Issa mwana Mariam(a.s) kisha atawaswalisha, pindi adui wa Mungu atakapomuona tu, atayeyuka mfano wa chumvi iyeyukavyo katika maji, lau angalimuacha angaliyeyuka mpaka akaangamia, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuuwa kwa mkono wa nabii Issa, kisha nabii Issa atawaonyesha damu yake ikiwa kwenye ncha ya kali"[202] .

Jambo lingine : kwamba Dajjali atawajia watu kisha atawataka waungane nae watamwamini na kuukubali wito wake, ataiamuru mbingu iteremshe mvua na mvua itanyesha, na ataiamuru Ardhi itatoa mimea... kisha atawatajia watu wengine na kuwataka waungane nae hawataukubali wito wake, Dajjaali atawaacha na kuondoka zake. Watapatwa na ukame, hawatabaki na kitu chochote wanachokimiliki miongoni mwa mali zao. Kisha atapita kwenye magofu ya zamani, atayaambia: "Toa hazina zako", hazina za eneo hilo zitamfuata mfano makundi ya nyuki yanavyomfuata malikia wao, kisha atamwita mtu kijana, atamkata kwa upanga vipande viwili. Kisha atamwita tena kijana yule (baada kurudi kuwa hai) atakuja hali yakuwa uso wake ukionyesha tabasamu na kucheka"[203] .

Jambo lingine: kwamba Dajjali ataponya ukoma na vibarango na atawafufu wafu.

Ameandika Ahmad katika kitabu chake cha Musnad, kutoka kwa Samrah Ibni Jundub kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(إن الدجَّال خارج، وهو أعور عين الشمال، عليها ظفرة غليظة، وإنه يُبرئ الأكمه والأبرص ويحيي الموتى).

"Hakika Dajjaal atatokea, yeye ni kipofu jicho lake la kushoto, juu ya jicho hilo kuna ngozi nzito, na kwa hakika yeye anaponya magonjwa ya ukoma na vibarango na atawafufua wafu"[204] .

Jambo lingine: ni yaliyopokelewa kuhusiana na sifa za punda wa Dajjali.

Ahmad Ibni Hambal na Haakim wameandika katika vitabu vyao Musnad na Mustadrak, kutoka kwa Jaabir kutokakwa Mtume(s.a.w.w) kwamba alisema kuhusiana na sifa za punda Dajjaali:

(وله حمار يركبه، عَرْض ما بين أذنيه أربعون ذراعاً).

"Dajjali atakuwa na punda anaempanda, upana uliopo katika masikio yake ni dhiraa arobaini"[205] .

MATUKIO MENGINE YAKUSTAJABISHA KUHUSU MAUDHUI HAYA

Miongoni mwa matukio hayo: kwamba Ibni Sayyaad alichukia, kisha akavimba hata akajaa njia nzima.

Ameandika Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa Naafi'i kuwa alisema: "Ibni Omar alikutana na Ibni Sayyaad katika baadhi ya njia za Madina, akamwambia kauli iliyomchukiza, basi Ibni Sayyaad akawa amevimba kiasi cha kujaa njia nzima. Ibni Omar akawa ameingia kwa Hafsa hali yakuwa taarifa hiyo ilishamfikia, Hafsa akamwambia Ibni Omar: Allah akurehemu, ulitaka nini kutoka kwa Ibni Sayyaad? Je haukujua kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(إنما يخرج من غضبة يغضبها).

"Hakika yeye (Ibni Sayyaad) huwa anatoka katika hali yake ya kawaida anapo ghadhibishwa "[206] .

Niseme kuwa mimi binafsi nashindwa kuelewa kwamba wanaamini vipi kuwa mtu anaweza kuchukia kisha akavimba kiasi cha kujaa pande zote mbili za njia, kisha akarudi katika hali yake ya mwanzo?!

Jambo lingine: kwamba ndenge watambeba nabii Issa na wafuasi wake, na mambo mengine ya ajabu yanayo husiana na vyakula na vinywaji.

Ameandika Muslim na wengineo kutoka kwa Nawaasi Ibni Sam'aan katika hadithi ndefu, imekuja katika hadithi hiyo kuwa: "Na Mwenyezi Mungu atawatuma Yaajuju na Maajuju, nao watateremka kwa kasi katika kila mlima, wakwanza wao watapita juu ya bahari ya Galilaya kisha watakunywa kile kilichomo ndani yake, kisha wengine watapita nakusema: (awamu hii yatakuwa ni maji kweli). Nabii wa Mwenyezi Mungu Issa(a.s) na wafuasi wake watazingirwa vikali, hata itafikia hatua mmoja wao kuwa na kichwa cha ng'ombe ni bora kwake kuliko kuwa na Dinari mia moja siku hiyo. Kisha nabii Issa na wafuasi wake watamwomba Mwenyezi Mungu na kumkabidhi mambo yao yeye. Hapo ndipo Mwenyezi Mungu atakapo watuma wadudu wanaokuwa mapuani mwa ngamia, mbuzi na kondoo, wajulikanao kwa jina la: ( النَّغَف ), kwenye mashingo ya maaduwi, wote wataangamia kwa mpigo mfano wa kifo cha mtu mmoja. Kisha nabii Issa na wafuasi wake watafika nchi kavu. Hawatakuta katika Ardhi hiyo sehemu ya ukubwa wa shibri hata moja isipokuwa watakuta mafuta na harufu mbaya za maadui. Kisha nabii Issa(a.s) na wafuasi wake watamwomba Mwenyezi Mungu na kumkabidhi mambo yao yeye tu. Mwenyezi Mungu atawatumia ndenge mfano wa ngamia wa Khurasani, watawabeba na hatimae kuwashusha mahala atakapopataka Mwenyezi Mungu. Kisha Mwenyezi Mungu ataiteremsha mvua ambayo hakuna nyumba yoyote ya udogo wala ya manyoa itakayoweza kuizuwia. Mvua hiyo itaisafisha Ardhi na kuiacha kama kioo. Hapo ndipo Ardhi itakapo ambiwa: "Otesha mimea na matunda yako na rejesha kheri na baraka zako". Wakati huo kundi kubwa la watu litashiba kwa kula komamanga moja, na ganda lake wataweza kulifanya kuwa kivuli na nahala pakujinga na jua. Maziwa ya wanyama yataongezeka, hata kufikia kiasi maziwa ya ndama wa ngamia yatatosheleza kundi kubwa la watu, na maziwa ya ndama wa ng'ombe yatalitosheleza kabila nzima, na maziwa ya mtoto wa kondoo au mbuzi yataitosheleza familia kubwa"[207] .

Niseme kuwa bado nashindwa kuelewa kwamba Ahli Sunna, wanawezaje kivikubali visa hivi vya visivyo na uhalisia na vyakupuni ambavyo kiakili havikubaliki, na je inaingia akilini kwamba nabii moingoni manabii wakubwa (ulul-azm) akabebwa na ndege?! Je inewezekana komamanga likakuwa kiasi cha nganda lake kutumiwa na kundi kubwa la watu kama kivuli?! Na ikiwa maziwa ya ndama yanaweza kulitosheleza kundi kubwa la watu, basi ukubwa wa ndama huyo utakuwa ni kiasi gani?! Bila shaka atakapokuwa atakuwa ni sawa mlima wenye kilele kirefu!!

Jambo lingine: kwamba mawe na miti vitaongea katika vita na Mayahudi.

Wameandika Bukhari, Muslim -maneno ya hidhithi hii ni ya Muslim- na wengineo kutoka kwa Ibni Omar kutoka kwa bwana mtume(s.a.w.w) kuwa alisema:

(لتُقاتِلُنَّ اليهود فلتقتُلُنَّهم، حتى يقول الحجر: يا مسلم هذا يهودي، فتعال فاقتله)

"Bila shaka mtambana na Mayahudi, na bila shaka mtawauwa, hata jiwe litakuwa likisema: Ewe mwislamu, huyu ni yahudi njoo umuuwe"[208] .

Na kutoka kwa Abu Hurairah, kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema:

(لا تقوم الساعة حتى يقاتل المسلمون اليهود، فيقتلهم المسلمون، حتى يختبئ اليهودي من وراء الحجَر والشجر، فيقول الحجر أو الشجر: ( يا مسلم يا عبد الله هذا يهودي خلفي، فتعال فاقتله )، إلا الغَرْقَد فإنه من شجر اليهو).

"Kiyama hakitasimama mpaka waislamu wapigane na Mayahudi, kisha waislamu watawauwa Mayahudi, mpaka myahudi atakuwa akijificha nyuma ya jiwe na mti, kisha jiwe au mti utasema: "Ewe mwislamu, ewe mja wa Mwenyezi Mungu, huyu hapa myahudi kajificha nyuma yangu, hivyo njoo umuuwe", isipokuwa mti wa nitraria ( الغرقد ), hakika mti huo ni wa mayahudi"[209] .

Qurtubi amesema: "Mwawiji[210] unapokuwa huitwa nitraria, na katika hadithi: kwamba mti huo ni miongoni mwa miti ya mayahudi. Hivyo, atakapo teremka nabii Issa(a.s) na akawauwa mayahudi watakao kuwa na Dajjaal, hakuna yeyote miongoni mwao atakaejificha nyuma ya mti isipokuwa utatamka na kusema:" Ewe mwislamu, huyu hapa muyahudi nyuma yangu, njoo umuuwe". Isipokuwa mti wa Nitraria, kwani ni miongoni mwa miti ya mayahudi, hivyo hautatamka. Muslim kaisahihisha hadithi hii"[211] .

Jambo lingine: kuwa chakula cha watu katika zama za Dajjaal kitakuwa ni Takbiir, Tahlil na Tasbiih.

Wameandika Ahmad Ibni Hambal, Abu Ya'alaa na wengineo kutoka kwa Aisha, kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alitaja uwezo atakaokuwa nao Dajjaal, wakasema: Ni mali gani itakuwa ni bora kipindi hicho? Akasema:

(أيُّ المال خير يومئذ؟ قال: غلام شديد يسقي أهله الماء، وأما الطعام فليس قالوا: فما طعام المؤمنين يومئذ ؟ قال: التسبيح والتكبير والتهليل. قالت عائشة: فأين العرب يومئذ ؟! قال: العرب يومئذ قليل).

"Kijana mwenye nguvu ataweza kuwapa maji watu wake, na sio chakula". Wakamuuliza: Hivyo basi, nini kitakuwa ni chakula cha waumini kipindi hicho? Akajibu kwa kusema: "Tasbiih (kusema: Sub'haanallah), Takbiir (kusema: Allahu Akbar) na Tahlil (kuesma: Laa ilaaha illa llah)". Bibi Aisha akasema: "Wakati huo warabu watakuwa wapi?". Akasema: "Warabu watakuwa wachache wakati huo"[212] .

Vilevile, Hakim Nisaaburi ameandika katika kitabu chake cha Mustarak kwa mapokezi kutoka kwa Ibni Omar kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) aliulizwa kuhusiana na chakula cha waumini katika zama za Dajjaal, akasema: "Chakula cha malaika". Wakasema: "Chakula cha malaika ni kipi?". Akawajibu kwakusema: "Chakula chao ni kufanya Tasbiih na Taqdiis (kumtakasa Mwenyezi Mungu) , hivyo yeyote ambae matamshi yake kipindi hicho yatakuwa ni Tasbiih na Taqdiis, Mwenyezi Mungu atamuondolea njaa, na hataokopa njaa"[213] .

Na jambo lingine: kwamba masiku katika zama za Dajjaal yatatofautiana na masiku mengine.

Wametaja Muslim katika Sahihi yake, Abu Daud katika Sunan yake na wengieo katika hadithi ndefu, kwamba mtume(s.a.w.w) aliulizwa kuhusu Dajjaal, akaambiwa:

(يا رسول الله وما لبثه في الأرض ؟ قال: أربعون يوماً، يوم كسنة، ويوم كشهر، ويوم كجمعة، وسائر أيامه كأيامكم. قلنا: يا رسول الله، فذلك اليوم الذي كسنة أتكفينا فيه صلاة يوم ؟ قال: لا، اقدروا له قدره).

Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, atabakia ardhini kwa muda gani? Akasema: "Miaka arobaini, siku moja itakuwa ni sawa na mwaka, na siku nyingine itakuwa ni sawa na mwezi, na siku inayofuata itakuwa ni sawa na wiki moja, masiku yaliyosalia yakuwa kama masiku yenu". Tukasema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, je siku hiyo itakayokuwa sawa na mwaka, sala ya siku moja itatutosha ndani ya siku hiyo? Akasema: Hapana, mtaikadiria kwa kiwango chake"[214] .

Vilevile Haakim amaeandika na Dhahabi akaisahihisha na kuikubali, kutoka kwa Kaahuli kutoka kwa mtume(s.a.w.w) kwamba alisema -katika hadithi ndefu ambayo ndani yake ametaja mambo yatakayo kuwa zama za Dajjaal: "... Hakika masiku ya Dajjaal yatakuwa arobaini, siku moja itakuwa sawa na mwaka mmoja, na siku nyingine itakuwa sawa na mwezi, na siku inayofuatia itakuwa ni sawa na wiki moja, masiku mengine yatakuwa sawa na masiku ya kawaida, ama siku ya mwisho itakuwa kama sarabi, mtu atakuwa akiamkia kwenye mlango wa Madina, mpaka jioni inaingia kabla hajaufikia mlango wake mwingine". Maswahaba wakamuuliza: "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, katika masiku hayo mafupi tutakuwa tukiswali vipi?". Akasema: "Mtakuwa mkikadiria katika masiku yaho, kisha mtaswali kama mnavyokadiria katika masiku marefu"[215] .

ANGALIZO

Haifichiki kuwa nasi hatuyakanushi mengi ya mabo haya yaliyo nje ya ada, bali ukweli ni kwamba waislamu katika baadhi ya mambo hayo wameafikiana, kama vile: Imamu Mahdi (a.f) kutawala pande zote za Dunia, kuijaza Ardhi usawa na uadilifu baada yakuwa imejaa dhuluma na uovu, kuteremka nabii Issa mwana wa Bi Mariam(a.s) na mfano wa hayo yanayojulikana na yaliyomashuhuri, isipokuwa nilichotaka kumbainshia msomaji mpendwa ni kuwa, sauala la Imamu Mahdi (a.f) limezungukwa na mambo mengi ya ghaibu na yaliyo nje ya ada na kawaida ya mwanadamu, na kwamba kuingia kwake ughaibuni kwa muda mrefu na umri wake mtukufu kuwa mrefu - hata kama ni mambo ya kawaida- ni sawa na mambo mengine yaliyothibiti kwa dalili na hoja sahihi, wala sio busara kuyapinga na kuyakanusha au kuyatumia kama kigezo cha kuhujumu na kuchafua jina la Ushia na Mashia.

7

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI?

MATOKEO NA TIJA YA UTAFITI HUU

Baada ya yote yaliyotangulia, ni matumaini yangu kuwa, mambo kadhaa muhimu yatakuwa yamembainikia msomaji mpendwa:

1. kwamba maulamaa wa Ahli Sunna wamewawajibishia wailamu wote wa katika kila zama na kila mahala kujichagulia kiongozi na khalifa mmoja kwa ajili ya waislimu wote, na wakafanya kuwa ni lazima kuharikia kufanya hivyo bila kuchelewa wala kufanya uzembe.

2. Vilevile, wamewajibisha kumtolea kiapo cha utii kiongozi wa waislamu katika kila zama, na kwamba hairuhusiwa kwa mwislamu kulala hata usiku mmoja bila ya kuwa kutoa kiapo cha utii, na kwamba atakaekufa bila kutoa kiapo cha utii, kifo chake kitakuwa ni chakijahili.

3. Maulamaa hao wakisuni wamewekamasharti kwamba kiongozi na khalifa wa waislamu lazima awe ni mkuaraishi, mjuzi wa sheria za dini, mujtahidi, mwadilifu na asiwe fasiki, wakahitilafiana katika kumng'oa madarakani kiongozi fasiki, baadhi yao wamewajibisha kumng'oa madarakani, na wengi wao wanakataza kufanya hivyo.

4. Jambo lingine ni kuwa, wailamu wameafikiana kwa ujumla kwamba, hairuhusiwi kuwateuwa viongozi wawili katika zama moja, bali nilazima waislamu wawe na kiongozi mmoja kwa ajili maeneo yote ya kiislamu hata kama yatakuwa mbalimbali. Bali zimepokelewa hadithi zinazowalazimisha waislamu kumpa kiapo cha utii kiongozi wa kwanza na kumuuwa kiongozi wa pili ikiwa atatoa kudai uongozi.

5. Ahli Sunna katika zama hizi wamepatwa na mkanyiko mkubwa, kiasi cha kushindwa kutekeleza kile kilichoashiriwa na hadithi sahihi, bali wameshindwa kuzifanyia kazi kauli za maulamaa juu ya jambo hili, na hivyo kushindwa la kufanya. Kwani wameshindwa kumchagua kiongozi wao licha kuwa ni wajubu na lazima, matokeo yake miji yao imegawanyika na kutawaliwa na watawala tofauti tofauti, wasio na sifa na vigezo walivyovifanya kuwa ni lazima awenavyo kiongozi wa wailamu.

6. Kwamba hoja na dalili sahihi zimeonyesha kuwa, koingozi wa waislamu katika zama hizi ni Imamu Mahdi, Muhammad Ibni Hasani Al-askari(a.s) ; na hii kwakuwa kuukanusha uongozi wake kuna viziwizi vingi ambavyo hawezi kuepukana navyo.

7. Shubuha na Ishkali zilizozitolewa na Ahli Sunna kuhusiana itikadi ya Mashia juu Imamu Mahdi (a.f) zote zinajibika, kama ambavyo ishkali zao hazo hazina thamani yoyote baada ya hoja sahihi kuthibitisha kuwa Imamu Mahdi yupo hai na nikiongozi.

8. Itikadi ya Ahli Sunna kuhusiana Imamu Mahdi (a.f) sio sahihi; kwakuwa inakabiliwa shubuha na ishkali nyingi na nzito zisizojibika.

Na kwa mnasaba huu, napenda niitumie fursa hii kuzielekeza nasaha zangu kwa ndungu zangu Ahli Sunna kuwa, wafanye haraka kusahihisha itikadi zao katika suala hili na katika masuala mengineyo ambayo wamehitilafiana na wafuasi wa Ahli baiti(a.s), kabla ya kupatwa na umauti, na hivyo mlango wa matendo kufungwa na hatimaye malango wa hesabu kufunguliwa.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu aliyetukuka na kutakasika, aijalie kazi yangu hii kuwa nimeifanya kwa ajili yake, na awanufaishe nayo ndugu zangu waumini, na aninufaishe nayo siku yangu ya haja na ufakiri.

Kama ninavyo muomba Allah alietukuka, awawafikishe waislamu wote kutenda yale anayo yapenda na kuyaridhia, na awajumuishe katika kumtii yeye na kumuomba; kwani yeye ni msikivu mwenyekuitikia maombi ya anaemuomba, na rehema za Mwenyezi Mungu zimwendee mbora wa viumbe wake Muhammad(s.a.w.w) na Ahli zake wema watwaharifu.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

8

YALIYOMO

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI? 1

MTUNZI: SHEKH ALY AALI MUHSINI 1

MTARJUMI: SHEKH REHANI YASINI 1

UTANGULIZI 1

ULAZIMA WA KUTEULIWA KIONGOZI KWA MUJIBU WA MADHEHEBU YA AHLI SUNNAH 3

ULAZIMA WA KUHARAKIA KUMTUEA KIONGOZI WA WAISLAMU 4

UCHAMBUZI KATIKA HADITHI 5

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI? 7

BAADHI YA SIFA ZA KIONGOZI WA WAISLAMU 7

HAWAWI VIONGOZI WA WILI WAKATI MMOJA 9

MAZINGIRA YA AHLI SUNNAH KATIKA ZAMA HIZI 11

JUHUDI ZA KUJIBU ISHKALI HIYO NA MAJIBU YAKE 11

JAWABU : 11

JUHUDI NYINGINE NA MAJIBU YAKE 12

JIBU LAKE 12

JUHUDI YA TATU NA MAJIBU YAKE: 13

JIBU LAKE: 13

JUHUDI YA NNE NA MAJIBU YAKE: 13

JIBU LAKE: 13

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI? 15

KIONGOZI (KHALIFA) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI NI IMAMULMAHDI(A.S) 15

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI? 24

USAHIHI WA HADITHI SAHIHI JUU YA KUZALIWA AL-IMAMU ALMAHDI 24

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI? 29

SHUBUHATI ZINAZO HUSIANA NA ITIKADI YA MASHIA JUU IMAMU MAHDI (A.F) 29

SHUBUHA YA PILI 38

MAJIBU YA SHUBUHA 38

SHUBUHA YA TATU: NI KUHUSIANA NA UIMAMU NA UONGOZI WA MTOTO NA MAZAZI YAKE 39

MAJIBU YA SHUBUHA 40

SHUBUHA YA NNE: KUHUSIANA NA KUWA JINA LAKE (IMAMU MAHDI) NI MUHAMMAD IBNI ABDALLAH 41

MAJIBU YA SHUBUHA YA NNE 42

SHUBUHA YA TANO: KWAMBA MAHDI (A.F) NI KATIKA KIZAZI CHA IMAMU HASANI ALMUJTABA(A.S) 45

MAJIBU YA SHUBUHA 46

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI? 50

ISHKALI KUBWA KATIKA ITIKADI YA AHLI SUNNA KUHUSIANA NA IMAMU MAHDI (A.F 50

ISHKALI YA KWANZA: NI KWAMBA IMAMU MAHDI MWENYEWE HATAJIJUA! 50

ISHKALI YA PILI: ITAMLAZIMU IMAMU MAHDI ATOE KIAPO CHA UTII KWA MMOJA WA WATAWALA WA ZAMA ZAKE 52

ISHKALI YA TATU: UHARAMU WA KUSIMAMA IMAMU MAHDI DHIDI YA WATAWALA WA ZAMA ZAKE 52

ISHKALI YA NNE: HAKIKA WATU HAWATAWEZA KUMTOFAUTISHA IMAMU MAHDI ALMUNTADHAR NA WATU WENGINE 54

ISHKALI YA TANO: NI WAJIBU KUPAMBANA NA IMAMU MAHDI NA KUMZIWIA KUFANYA MAPINDUZI 54

ISHKALI WA SITA: UWAJIBU WA KUWATII WATAWALA WAOVU PINDI ATAKAPO SIMAMA IMAMU ALMHDI (A.F) DHIDI YAO 55

ISHKALI YA SABA: UTAWALA WA IMAMU MAHDI (A.F) HAUTAKUWA HALALI NA WAKISHERIA! 56

ISHKALI YA NANE 56

ISHKALI YA TISA 57

ISHKALI YA KUMI: KWAMBA IMAMU MAHDI (A.F) NI MBORA KULIKO ISSA IBNI MARIAM(A.S) 57

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI? 59

MAMBO YALIYO INJE YA ADA KATIKA KADHIA YA IMAMU MAHDI (A.F) 59

IMAMU MAHDI(A.F) KUZITAWALA PANDE ZOTE ZA DUNIA 59

MWENYEZI MUNGU ATAMUANDALIA IMAMU MAHDI(A.F) MAZINGIRA YA USHINDI NDANI YA USIKU MMOJA 59

HAKIKA MAHDI HATADHIHIRI MPAKA JUA LITAKAPO CHOMOZA NA ALAMA 60

NABII ISSA(A.S) KUSHUKA ZAMA ZA ALMAHDI(A.F) NA KUSWALI AKIWA NYUMA YAKE 60

JESHI LITAKALOTOKA LIKIKUSUDIA KUMUUWA IMAMU ALMHDI(A.F) LITAANGAMIZIWA KATIKA ARDHI YA ALBAIDAU 60

MAAJABU YALIYOTAJWA KUHUSIANA NA VITA VYAKE 61

KWAMBA MBINGU ITATEREMSHA MVUA YAKE NA ARDHI ITATOA BARAKA ZAKE 61

UMMA UTANEMEKA KWA NEEMA AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA HAPO KABLA 62

CHUKI NA WIVU VITATOWEKA KATI YA WATU 62

MBWA MWITU ATASHIRIKIANA NA MBUZI NA KONDOO KATIKA MALISHO, NA SIMBA NA NGAMIA WATACHANGIA MALISHO, NA WATOTO WATACHEZEA NYOKA 62

MASWAHABA WA MAHDI (A.F) MWENYEZI MUNGU NDIE ATAKAE WAKUSANYA NA KUZIUNGANISHA NYOYO ZAO 63

MAMBO MENGI YANAYOHUSIANA NA DAJJALI YAKO NJE YA ADA 63

MATUKIO MENGINE YAKUSTAJABISHA KUHUSU MAUDHUI HAYA 65

ANGALIZO 68

NINANI KHALIFA ( KIONGOZI ) WA WAISLAMU KATIKA ZAMA HIZI? 69

MATOKEO NA TIJA YA UTAFITI HUU 69

SHARTI YA KUCHAPA 70

MWISHO WA KITABU 70

YALIYOMO 71

9

[1] . Al-mawaqifu, uk:395. Mwanazuoni huyo (Al-ijey), aliishi kuanzia mwaka 700-756 hijiriya.

[2] . Al-ahkamu assultwaniyyah, uk:29.

[3] . Sharhi Swahihi Muslim linnawawi, 12/205. Ibara hii pia imenukuliwa na: Ibun hajari, katika: fat-hil-bari 13/176. Pia Almubarikafuri, katika: tuhfatil-ahudhi 6/397. Pia kainukuu: Al-adhimuabadi, katika: Aunil-maabudi 7/112. Pia Asshaukani, katika: Nailul-autwari 6/166.

[4] . Shuabul-imani/6/6.

[5] . Sharhulmaqaswid 5/235.

[6] . Asswawaiqulmuhriqah, uk:30.

[7] . Swahih muslim, 3/1478. Assunanulkubra, 8/156. Majmauzzawaidi, 5/218. Mishkatulmaswaabihi, 2/96. Silsilatul-ahadithu asswahiha, 2/715.

[8] . Musnadi ahmadi, 4/96. Majmau azzawaidi, 5/218. Musnadu attwayalisi, uk: 259. Al-ihsani bitartibi swahihi ibun habani, 7/49. Hilyatul-auliyaa, 3/224.

[9] . Majmau azzawaidi, 5/224 – 225. Kitabu asunnah, 2/489. Amesema Albani: Sanadi yake ni hasan, na wapokezi wake ni thikqah.

[10] . Musnadi Ahmadi, 3/446. Kanzul-ummali, 6/65. Kitabu asunnah, 2/490. Almatwalibul-Aaliya, 2/228.

[11] . Almustadraki Alaswahihayni, 1/150. Alisema Alhaakimu; Hadithi hii ni sahii kwa masharti ya mashekhe wa wili (Muslimu na Bokhari). Na imeafikiwa na Addhabey, 1/204.

[12] . Amuujamul-kabir, litwabarani 10/289. Almuujamul-ausatwu, 2/317. Musanadi Abi Yaali, 6/215. Kitabu Asunnah, Iiibun Abi Aswimu, 2/489. Alisema Albani; sanadi yake ni hasani, na wapokezi wake ni thiqah, ingawa kuna uthaifu kidogo, juu ya Aaswimu, ambaye ni Ibun Abi annujudi, wa Abi Bakari bun Ayashi. Majmau Azzawaidi,224 – 225.

[13] . Suratul-israa, Aya ya: 13.

[14] . Sharhu Swahihi Muslimu, 12/238.

[15] . Fathul-baari, 13/5.

[16] . Aljaamiu Liahkamulqur’ani, 1/272.

[17] . Alfaswilu filmilali wal-ahwaa wa annihali, 4/179.

[18] . Almuhalaa, 8/420.

[19] . Rejea: Swahihi Muslimu bisharhi Annawawi,12/240.

[20] . Hadithi hii, imepokewa na: Ahmadi bin Hambali, katika musnadi yake,3/129, 183, 4/421. Twayalisi, katika musnadi yake,uk:125, na 284. Alhaakimu, katika mustadraki yake,4/501. Na ika sahihiswa na Alddhahabi. Pia ikapokewa na: Suyuutwi, katika Aljaamii alswaghiru,1/480. Abunaemu, katika Hilyatul-auliyaa,1/171, na 5/7, 7/242, 8/123. Alhaythami, katika Majmau alzzawaidi,5/192. Albayhaqi, katika sunanilkubra,3/534. Akasema naemu katika hilyatu,3/171 kuwa: hadithi hii ni mashuhuri,iliyo thibiti, na katika hadithi za Anasi. Na akasema Bayhaqi katika sunani,3/121 kuwa: ni mashuhuri, na nikatika hadithi za Anasi. Na Suyutwi katika kitabu cha Katwiful-azhaarilmutanathira,248. Na katinani katika Nadhimulmutanathira,uk:179. Na Ibun hazmi, katika Alfaswilu fil milali wal Ahwaa wa annihali,4/152. Na wengineo, waliioroshesha hadithi hii, katika hadithi mutawatiri.

[21] . Faidhul-qadeer,3/189.

[22] . Fatihulbaari,13/102.

[23] . Al-ahkamu alsultwaniyah, uk:32.

[24] . Almuhalaa,8/420 – 421.

[25] . Alfarqu baina Alfiraqu, uk:349.

[26] . Sharhilmaqaswidi, 5/243.

[27] . Qawaaidul-aqaidi, uk: 230.

[28] . Aljaamiu li ahkamil-qur’ani, 1/270.

[29] . Almawaqifu, uk: 398.

[30] . Alfarqu baina alfiraqu,uk: 349.

[31] . Aljamiu li ahkamulqur’ani, 1/270.

[32] . Al-ahkamu asultwaniyah, uk: 31.

[33] . Sharhi almaqaswdi, 5/233.

[34] . Altamheedi, uk: 181.

[35] . Alfiraqu baina alfarqu, uk: 349.

[36] . Almawaqif, uk: 389.

[37] . Aljamiu li Ahkamilqur’ani, 1/270.

[38] . Al-ahkamu asultwaniyah, uk: 31.

[39] . Qawaidul-aqaidu, uk: 230.

[40] . Sharhi almaqaswdi, 5/233.

[41] . Sharhu Annawawi li Swahihi Muslimu, 12/232.

[42] . Tafsirulqur’anil-adhim, 1/72.

[43] . Almuhalaa, 9/360.

[44] . Aljamiu li Ahkamilqur’ani, 1/273.

[45] . Swahihi bokhari, 2/1074. Swahii muslimu, 3/1471. Musnadi Ahmadi, 2/297. Sunani Ibun Maajah, 2/958. Assunnanilkubraa lilbaihaqi, 8/36.

[46] . Swahihi Muslimu, 3/1480. Assunanulkubra lilbaihaqi, 8/411. Almuujamil-ausatwi, 2/124. Majmau azzawaidi, 5/198. Alisema Haithami: hadithi hii imepokewa na Twabarani katika Alkabeer na Al-ausatwu, Na wapokezi wake ni thiqah. Shuabul-eimani, 6/10.

[47] . Swahihi Muslimu bi sharhi annawawi, 12/231.

[48] . Mughunilmihtaaji, 4/171.

[49] . Mughunilmihtaaji, 4/171.

[50] . kana kwamba aliyefanya hivyo ni sawa na kujiadhibu yeye na mwenzie, na hivyo kujitia katika umauti.

[51] . Swahihulbukhari, 9/100, kitabul-ahkamu, babul-istikhilafu.

[52] . Suratul-ambiyaa, aya ya:7.

1. jibu hili ni la; Saadu addini Taftazani (712 – 793 hiriya) katika kitabu chake cha: Sharhul-maqaswidu, 2/239.

[54] . Suratul-israa, Aya: 15.

1. Aswawaaiqul-muhriqah, uk: 482.

2. Almultaqa Min Minhajil-itidali, uk: 172.

3. Sunanu tirimidhi, 5/622, 663, na alisema tirmidhi: hadithi hii ni Hasani, lakini ni ngeni kwa upande huu. Mustadraki Ala swahihaini, 3/109 – 110, 148. Alisema hakimu: hadithi hii ni sahihi kwa sharti ya mashekhe wa wili. Na kaiafiki Adhahabi. Albidayatu wa Nihaya, 5/184, na alisrma Ibun Kathiri: alisema shekhe wetu Abu Abdallah Addhahabi: hadithi hii ni Sahihi. Majmau Zawaidi, 9/162, alisema Alhaitami: hadithi hii ilipokewa na Ahmadi, na sanadi yake ni nzuri. 2/170, na alisema: hadithi hii aliipokea pia twabarani katika kabir, na wapokezi wake ni thiqah. Aljamiu Swaghir, 1/402, na suyutwi alisema ni sahihi. Almatwalibul-aliyah,4/65, na alisema Ibun Hajari: hii sanadi yake ni sahihi. Makhtaswari it’hafu saadatulmahri,9/194, na alisema Albuswairi: hadithi hii aliipokea Ishaqah kwa sanadi sahihi.8/461, na alisema: hadithi hii ilipokewa na Abubakari bin Abi Shaibah na Abdu bin Hamidi, na wapokezi wake ni thiqah. Na imesahihishwa na Albaani katika mrorongo wa hadithi sahihi,4/356, na Swahihuljamiu swaghir,1/482.

[58] . Swahih muslim, 3/1478. Assunanulkubra, 8/156. Majmauzzawaidi, 5/218. Mishkatulmaswaabihi, 2/96. Silsilatul-ahadithu asswahiha, 2/715.

1. Alkafi,1/328.

[60] . Alyawaqiti wajawahiri,2/562, na ameyanukuu maneno haya kutoka kwake Asshekhe Muhammadi Ali Swaabbani, katika; Is’afu Alrraaghibina, uk;154. Na alitaja Shekh Alnabahany, katika kitabu chake cha; Jamiu karamatil-auliyaa,1/400, kisa cha kukutana Shekhe Hsani al-iraqi, na Al-imamu Almahdi (a.s).

[61] . Surat Annisaa:59.

[62] . Surat Albaqarah:124.

[63] . Hadithi hi, imepokewa na; Abu Daudi, katika; Sunani yake,4/106,107 75. Na imesahihishwa na; Albani katika Swahihu Sunani Abi Daudi,3/807,808. Musnadi Ahmadi bin Hambali,3/27,28,36. Al-ahdithu Almukhtarah,2/172. Mishkatu Almaswabihu,3/1501. Aljaamiu Alswaghiru,2/438. Swahihu Aljaamiu Alswaghiru,2/938. Almuswannafu Libni Abi Shaibah,7/513.

[64] . Al-isha’atu Li Ash’ratwu Alssa’a, uk;108.

[65] . Surat Ali Imraani:103.

[66] . Surat Al-anfaal:46.

[67] . Surat Al-aniamu:116.

[68] . Surat Yusuf: 103.

[69] . Surat Almuuminina:70.

[70] . Surat Almaaidah:20.

[71] . Surat Maryam:49.

[72] . Surat Alhadid:26.

[73] . Surat Al-aniamu:124.

[74] . Surat Alqaswasi:7.

[75] . Surat Swadi:26.

[76] . Surat Albaqarh:30.

[77] . Surat Al-ambiayaa:73.

[78] . Surat Albaqarah:124.

[79] . Surat Asajdah:24.

[80] . Tulitaja huko nyuma vyanzo vya hadithi hii, katika uk:28.

1. Rejea historia yake katika kitabu cha: Alwaafi bil wafiyati,5/254. Na Muujamulmualifina,12/134. Na Al-a’lamu,7/150.

2. Rejea histori yake katika kitabu cha: Al-aalamu li Zarkali,5/8. Na Muujamulmualifina,7/178.

[83] . Alfusulilmuhimmah, uk:286,287.

[84] . Tadhkiratul-khawasu,uk:325.

[85] . Rejea historia yake katika: Shadharatu Addhahabi,8/372. Muujamul-muallifina,6/218. Jaamiu Karaamati Al-auliyaa,2/134.

[86] . kutoka katika: Is-a’afu Alrraghibina,uk:154.

[87] . kutoka katika: Yanaabiu Almawaddah,uk:451.

[88] . kutoka katika: Yanaabiu Almawaddah,uk:471.

1. Muujamu Almualifina,11/51.

2. Yanaabiu Almawaddah, uk:249 – 471, Mlango wa;79 na baada yake.

3. Kashfu Al-astaar, uk:89.

[92] . Alkhiswaal, Juz: 2, uk: 475. Kamaalu ddiini wa Itmaamu nniimah, jz: 1, uk: 262.

[93] . Kitabu Alkhiswali, juzu:1, uk:480.

[94] . Kitabu Alkaafi, juzu:1, uk: 328.

[95] . Akaafi,1/328.

1. Kitabu Alkaafi, juzu:1, uk:329.

2. Chanzo kilicho pita, juzu1,uk:331.

[98] . Alkaafi, Juz,1. uk:331.

[99] . Chanzo cha hapo juu, Juz,1. uk:337.

[100] . Kamaalu alddini wa Tamamu Anni’mah, Juz,2. uk:381.

[101] . As-Swaiq al-muhriqah, uk:198. Na Al-manar almuniif fii swahih wa dhaiif, uk:152.

[102] . Surat Al-ankabut,14.

[103] . At-Tafsiir Al-Kabiir, jz:25, uk:42. Kwa maelezo yetu.

[104] . Qisas Al-anbiyaa, jz:1, uk: 57.

[105] . Ibni Hajar katika kitabu cha Al-iswaabah, jz:2, uk: 62, anasema: “Amesema Ad-Dhahabi: “Nimezikuta kauli zote sinazohusiana na umri wake, zikionyesha kwamba ulizidi miaka mia mbili na hamsini, hitilafu ipo kwenye kiwango kilichozidia hapo…” Anaendelea kusema: “Ikiwa walichokisema kitathibiti, basi jambo hilo, litakuwa ni mojawapo ya mambo yaliyoko nje ya ada katika haki yake, na ni kipi kinachoziwia hilo kutokea?! Hakika Abu sheikh katika kitabu cha Tabaqaat Al-isfahaniyyiin amepokea kupitia njia ya Al-Abbas ibun Yazid kwamba, alisema: “Watu wa elimu (wasomi) wanasema: Salmaan aliishi miaka mia tatu na hamsini, ama kuhusiana na (kuishi) miaka mia mbili na hamsini, hata hawalitii shaka hilo”.

[106] . Surat An-Nisaai, 157-158.

[107] . Sahihi Muslim, Juz:1, uk: 136.

[108] . Fathul-Baari, Juz:6, uk:290.

[109] . An-Nihayah fil-fitan wal-malaahim, uk: 93.

[110] . Tafsiir Al-qur’an Al-adhiim, Juz:1, uk: 577.

[111] . Al-Jaamiu liahkaam Alqur’an, Juz:4 uk: 100.

[112] . Sharhu Sahihi Muslim, Juz: 15, uk: 135. Tahdhiib Al-asmaai wal- Lughaat, jz: 1, uk: 177.

[113] . Sharhu Sahihi Muslim, Juz: 15, uk: 135. Alhadharu fii Amril-Khidri, uk:76. Tahdhiib Al-asmaai wal- Lughaat, Juz: 1,

[114] Al-Jaamiu liahkaam Alqur’an, jz:11 uk: 43.

[115] . Surat Mariam, 57.

[116] . Ad-Durru Al-Manthuur, Juz:5, uk: 519. Tafsiir Al-qur’an Al-adhiim, Juz:3, uk: 126.

[117] . Ad-Durru Al-Manthuur, Juz:7, uk: 117.

[118] . Almustadrak, Juz:2, uk: 674. Amesema Hakimu: “Hadithi nii mapokezi ni sahihi (kwa mujibu wa masharti ya kupokea hadithi kwa Bukhar na Muslim), lakini wahakuitaja katika sahihi zao”. Al-Jaamiu liahkaam Alqur’an, Juz:15, uk: 116. Tafsiir At-Tabari, Aludhmah, Juz:5, uk:1531.

[119] . Ad-Durru Al-Manthuur, Juz:7, uk: 117.

[120] . Al-Jaamiu liahkaam Alqur’an, Juz:15 uk: 116.

[121] . Fathul Baari, Juz: 6, uk: 337.

[122] . Sahihi Muslim bisharhi AnNawawi, jz:18, uk:46.

[123] . Sahihi Muslim, Juz:4, uk: 2262. Hadithi Jassaasah imepokelewa kwa maneno tofauti tofauti, rejea: Sahihi Muslim, Juz:4, uk:22647Sahihi Ibni Habaan, Juz: 15, uk:194, 195,198. Sunanu AtTirmidhi, Juz:4, uk:521, Amesema Attirmudhi: Hadithi hiini hasani na sahihi. Sunanu Abi Daud, jz:4, uk:118=120. Sunanu Ibni Maajah, jz:2, uk:1354. Asunanulkubrah cha Annasaai, Juz:2, uk:281. Majmau Zawaaid, Juz:2, uk:346. Musnad Ahmad, Juz:6, uk:373, 412, 417. Almuswanaf cha Ibni Abi Shaibah, Juz:7, uk:497, 510. Almu'ujamu Alausat cha Twabaraani, Juz:1, uk:625. Almu'ujamu Alkabiir, Juz:2, uk:54, Juz:24, uk:371, 372, 385 -403. Musnad Alhumaidi, Juz:1, uk:77. Musnad Atwayaalis, uk:227. Musnad Abi Ya'alaa, Juz:2, uk:324, 327,334.

[124] . Al-Jaamiu liahkaamil Qur'an, Juz:11, uk: 42.

[125] . Rasaailu Ashariifu Arradhiy, Juz: 2, uk: 295.

[126] . Almustadraku alaa swahihaini, Juz:2, uk:486 na Juz:3, uk: 517. Alhaakimu anasema: "Mapokezi ya hadithi hii ni sahihi, lakini Bukhaari na Muslimu hawakuitaja". Almu'ujamu Al-ausatu, Juz: 5, uk: 319.

[127] . Alfitanu cha Nu'aim Ibni Hammaad, uk: 241. Lawaamiu Alnwaari Albahiyyah, Juz:2, uk: 81. Al-urful Wardi, kilichochapwa katika Alhaawi lilfataawaa, Juz:2, uk: 72. Al-isha'ah liashraati Sa'ah, uk:94.

[128] . Suratu Mariam: 12.

[129] . Fathul-Qadiir), jz: 3, uk: 320. Rejea Tafsiiru Alqurtubi, jz: 11, uk: 87. Alkashaafu, jz: 2, uk: 407. Tafsiirul-Qur'an Al-a'dhiim, jz: 3, uk: 113. Tafsiir Atwabari, jz: 16, uk: 42. Atafsiiru Alkabiir, jz: 21, uk: 191.

[130] . Atafsiiru Alkabiir, Juz: 21, uk: 191.

[131] . Suratu Mariam: 29-32.

[132] . Attafsiiru Alkabiir, jz: 21, uk: 214. Ninasema kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu: "na amenifanya Nabii", ina dalili ya wazi zaidi kuwa wakati ule alikuwa nabii kuliko hiyo aliyoitaja Fakhru Raazi, bali kwa mujibu wa wakati uliopita wa kitenzi "amenifanya", hata kabla ya wakati huo akiyasema hayo, alikuwa kashakuwa nabii.

[133] . Suratu Mariam:31

[134] . Attafsiiru Alkabiir, jz:21, uk: 215.

[135] . Aswaiqul Muhriqah, uk: 240.

[136] . Sunanu Abi Daud, Juz: 4, uk: 106-107.

[137] . Rejea kauli hizi katika kitabu: Mizaanul I'tidaali, Juz: 4, uk: 13-15.

[138] . Tahdhiib Attahdhiib, Juz: 5, uk: 35-36.

[139] . Sunanu Attirmidhi, Juz: 4, uk: 505. Tirmidhi amesema: "Hadithi hii ni hasan sahihi. Vilevie ameitaja hadithi hii katika mlango huo huo kutoka kwa Ali, Abu Said, Ummu Salamah na Abu Huraura.

( [140] ) Haya ni mashaka ya mpokezi, itakuja katika hadithi ijayo kwamba: "jina lake ni sawa na jina la jina langu, au jina lake ni sawa na jina la nabii".

( [141] ) Musnad Al-bazaar, jz: 8, uk: 258.

[142] . Musnad cha Al-haarith (Zawaidul Haithami), Juz:8, uk: 258. It'haaf al-kiyaratul muhrah: Juz:10, uk: 281.

[143] . Sahihi Bukhari, Juz: 4, uk: 1874.

[144] . Sahihi Muslim, jz: 4, uk: 1874.

[145] . Fat'hul Baari, jz:11, uk: 57.

[146] . Sunan Abi Daud, Juz:4, uk: 108.

[147] . Kitabu Athuqaat cha Ibni Habbaan, Juz: 9, uk: 238

[148] . Mizaanul Iit'daal, Juz: 5, uk: 341.

[149] . Tah'dhiibu Atahdhiib, Juz: 8, uk: 82.

[150] . Tuhfatul Ahwadhi, Juz: 6, uk: 403.

[151] . Mishkaatu Almisbah, Juz: 3, uk: 26.

[152] . Mirqaatul Mafaatiih, Juz: 9, uk: 349.

[153] . Surat An-a'am: 124.

[154] . Kitabu Swifatul Mahdi, cha Abu Nua'imu (kutoka kwenye U'qadu Adurari, uk: 24.

[155] . Al-fitanu cha Nua'imu Ibni Hamadi, uk: 262.

[156] . Al-fitanu cha Nua'imu Ibni Hamadi, uk: 264.

[157] . Alkhiswaal, jz: 2, uk: 475. Kamaalu ddiini wa Itmaamu nniimah, jz: 1, uk: 262.

[158] . Ilalu Asharai'u, jz: 1, uk: 245.

[159] . Suratu Al-an'aam:66.

[160] . Walioinukuu kwake ibara hii bila ya kuitilia dosari ni: Ibni Qayyimu Aljauzia katika kitabu 'Almanaaru Almuniifu, uk: 142', na Ibni Hajari Al-asqalaani katika kitabu 'Tahdhiibu Atahdhiib, Juz: 9, uk: 126, katika tarjuma ya Muhammad Ibni Khalidi Aljundi,' na Suyutwi katika kitabu ''Al-urful Wardi' kilichochapishwa ndani ya kitabu kingine kwa jina la 'Alhaawi' cha fatuwa, Juz: 2, uk: 58' na Ibni Hajari Almaithami katika kitabu 'Aswawaaiqu Almuhriqah, uk: 197', vilevile katika kitabu' Alqaulu Almukhtaswaru fii A'alamaati Almahdi Almuntadhar, uk: 23' na Alqurtubi katika kitabu 'Atadhkiratu fii Ahwaali Almautaa wa Umuuri Al-akhirah, uk: 701', na Asafaariini katika kitabu 'Lawaamiul Anwaaril Bahiyyah, Juz: 2, uk: 86' na Albazanji katika kitabu 'Al-isha'a liashraatwi Sa'a, uk: 87, 112' na Alkataani katika kitabu 'Nadhmul Mutanathir, uk: 239' na wengio.

[161] . Almahdi Almuntadhar, Juz: 1, uk: 379.

[162] . Dhuhal Islaam, Juz:3, uk: 244.

[163] . Almahdi wa ashraatwu asaa, uk: 365.

[164] . Tirmidhi katika kitabu chake ' Sunanu Atirmidhi, Juz: 4, uk: 506', ametaja kuwa: Mtu atakuwa akimjia Almahdi na kumwambia: Ewe Mahdi nipe, nipe. Akasema: Hivyo Imamu hummiminia muombaji yule katika nguo yake kiasi anachoweza kubeba. Tirmidhi anasema: Hadithi hii ni hasani. Pia hadithi inayokaribina na hii ipo katika kitabu 'Sunanu Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 1367, na Albaani katika vitabu 'Sahihi Sunani Atirmidhi, Juz: 2, uk: 387,489. Na katika kitabu 'Musnadu Ahmad, Juz: 3, uk: 37, imekuja kwamba: Almahdi atamwambia yule aliemuomba mali: Nenda mhazina umwambie: Hakika Almahdi, anakuamuru unipe mali. Mtunza hazima atamwambia: Kinga (chombo). Atakapo weka pajani mwake, atapatwa na majuto kisha atasema: Katika umma wa Muhammadi mimi ndio nimekuwa mtu wa pupa.... akasema: kisha atairudisha mali ile kwa muhazina lakini hatakubaliwa, ataambiwa: Sisi huwa hatupokei kili tulichokwishakitoa.

Alhaithami amesema katika kitabu cha 'Majmau Azawaid, Juz: 7, uk: 314': Hadithi hii amepokea Ahmadi kwa mapokezi mengi, na Ab Ya'alaa kaipokea kimuhktasari sana, na wapokezi wao ni waaminifu.

[165] . Rejea zake zimeshatangulia uk: 13.

[166] . Rejea zake zimeshatangulia uk: 14.

[167] . Sahihi Muslim, Juz: 3, uk: 1476.

[168] . Sahihi Muslim, Juz: 3, uk: 1478.

[169] . Aljaamiu liahkamil Qur'an, jz: 2, uk: 109.

[170] . Kutoka katika kitabu cha Nadhmul Mutanaathir, uk: 171.

[171] . Sharhu Sahihi Muslim, Juz: 12, uk: 229.

[172] . Sahihi Bukhari, Juz: 3, uk: 1112. na Sahihi Muslim, Juz: 3, uk: 1476.

[173] . Sahihi Muslim, Juz: 3, uk: 1479.

[174] . Sahihi Muslim, Juz: 3, uk: 1480.

[175] . Kharijiyu ni mtu anae toka dhidi ya mtawala na kiongozi, ima kwa sababu ya kuamini kuwa kiongozi huyo ni muovu nk...

[176] . Aljaamiu liahkamil Qur'an, Juz: 1, uk: 273.

[177] . Sahihi Muslim, Juz: 3, uk: 1478. na Sahihi Ibni Habbaani, Juz: 10, uk: 439.

[178] . Sahihi Muslim, Juz: 3, uk: 148.

[179] . Sahihi Muslim, Juz: 3, uk: 1475.

[180] . Sahihi Bukhari, Juz: 9, uk: 100, kitabul ahkam, mlango wa al-istikhlaaf, chapa namba: 4/2132.

[181] . Hulyatul Auliyaa, JUz: 7, Uk: 31.

( [182] ) Sahihi Muslim, Jz: 1, Uk: 137.

( [183] ) . Sahihi Bukhari, jz:2, uk: 136. Na Sahihi Ibni Habbaan, jz: 15, uk: 213.

[184] . Musnad Ahmad, Juz: 1, uk: 84. Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 1367. Albaani kasema kusema kuwa hadithi hii ni hasani katika kitabu cha: Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 389, na katika kitabu cha: Silsilatul Ahaadithi Aswahihah, Juz:5, uk: 486. Hulyatul Auliyaa, Juz: 3, uk: 177. Almuswannafu cha Abu Shaibah, Juz: 7, uk: 153.

[185] . Kamaalu d-dini wa Itmaamu n-niimah, Juz:1, uk:152.

[186] . Sharhu Ibni Maajah, Juz:1, uk: 300.

[187] . Almuswannafu cha Abdurazaki, Juz: 10, uk: 317.

[188] . Sunan d-daarqutni, Juz: 2, uk: 65. At-tadhkirah fii Ahwaalil-Almautaa wa umuuril Akhirah, uk: 703.

[189] . Sahihi Ibni Habbani, Juz:15, uk: 158. Almu'jamul Ausatwu, Juz: 1, uk:321 na Juz: 6, uk: 476. Mustadrakul Haakem, Juz: 4, uk: 478.

[190] . Rejea: Sahihi Muslim, Juz:4, uk:2210. Musnad Ahmad, Juz:6, uk: 285, 287. Mustadrak, Juz:4, uk: 476, 565. Tafsiirul Qurtubi, Juz: 7, uk: 392. Majmau Zawaaid, Juz: 7, uk: 314, 316. Mawaarid Dham'an, Juz: 2, uk: 840.

[191] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2238. Almustarak, Juz:4, uk: 523.

[192] . Atadhkiratu fii ahwaalil mautaa wa umouril akhirah, uk:707.

[193] . Almustadrak, Juz: 4, uk: 512. Musnad Ahmad, Juz: 3, uk: 21.

[194] . Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 1366. Albani kasema kuwa: “Hadithi hii ni hasan”, katika kitabu cha Sahihi fii Sunan Ibni Maajah, Juz:2, uk: 389. Muswannaf cha Abu Shaibah, Juz: 7, uk: 512. Mustadrak, Juz: 4, uk: 701. Mujmau Zawaaid, Juz: 7, uk: 317. Amesema Haithami: "Hadithi hii haipokea Tabraani katika kitabu cha Al-ausatwu, na wapokezi wake ni waaminifu. Mu'jamu Al-ausatwu, Juz:4, uk: 116.

[195] . Sahihi Muslim, Juz: 1, uk: 136. Sahihi Ibn Maajah, Juz: 15, uk: 227.

[196] . Mustadrak, Juz:2, uk: 601. Sahihi Ibni Haban, Juz:15, uk: 227, 233. Musnadi Ahmad, Juz:2, uk: 416, 437.

[197] . Mustadrak, Juz: 2, uk: 596.

[198] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2250. Sahihi Ibni Habbaan, Juz: 15, uk: 209. Sunan Abu Daud, Juz: 4, uk: 115. Sahihi Sunan Abu Daud, Juz: 3, uk: 813.

[199] . Musnadi Ahmad Ibni Hambal, Juz: 5, uk: 364. Mujmau Zawaaid, Juz: 7, uk: 343. Alhaithami amesema: "Hadithi hii kaipokea Ahmad na wapokezi wake ni waminifu”.

[200] . Nawawi katika kitabu kijulikanacho kwa jina la Sharhu Sahihi Muslim, Juz: 18, uk: 61, amesema: "Dhafrah, ni ngozi inayofunika mboni ya jicho". Na Asma'i nae amesema kuwa: "Ni kinyama kinachoota kwenye incha jicho upande unaokaribiana na pua".

[201] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2249. Sahihi Ibni Habbaan, jz: 15, uk: 184. Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 1360. Musnadi Ahmad Ibni Hambali, Juz: 5, uk: 38,386,404 na Juz: 3, uk: 228-229. Majmau Zawaaid, Juz: 7, uk: 337. Alhaithami amesema: "Hadithi hii kaipokea Ahmad na wapokezi wake ni waminifu”.

[202] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2221. Sahihi Ibni Habbaan, Juz: 15. uk: 224.

[203] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2252. Mustadrak, Juz: 4, uk: 538. Sunan Tirmithi, Juz: 4, uk: 511. Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 1356. Musnad Ahmad, Juz: 4, uk: 181. Tafsiir Ibni Kathiir, Juz: 3, uk: 195.

[204] . Musnad Ahmad Ibni Hambal, Juz: 5, uk: 13. Majmau Zawaaid, Juz: 7, uk: 336. Alhaithami amesema: "Hadithi hii kaipokea Tabraani na Ahmad na wapokezi wake ni waaminifu”.

[205] . Mustadrak, Juz: 4, uk: 575, na Dhahabi hadithi hii kaisahihisha na kuikubali. Musnad Ahmad, Juz: 3, uk: 367. Majmau Zawaaid, Juz:7, uk: 344, Alhaithami amesema kuwa: "Ahmad kaipokea hadithi hii kwa mapokezi ya aina mbili, wapokezi wa moja ya mapokezi hayo ni waaminifu”.

[206] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2246.

[207] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2254. Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 1358. Musnad Ahmad, Juz: 4, uk: 181. Tafsiir Ibni Kathiir, Juz: 3, uk: 195. Hadithi hii kaisahihisha Albaani katika kitabu cha Sahihi Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 387.

[208] . Sahihi Bukhari, Juz: 2, uk: 901, na Juz: 3, uk: 1109. Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2238-2239.

[209] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2239.

[210] . Aina ya mmea wenye miba na matunda yake ni yaduwara.

[211] . Aljaamiu liahkamul qur'an, Juz: 13, uk: 282.

[212] . Musnad Ahmad Ibni Hambal, Juz: 6, uk: 75, 125. Musnad Abu Ya'alaa, Juz: 4, uk: 152. Majmau Zawaaid, Juz: 7, uk: 335, Alhaithami amesema kuwa: Hadithi hii kaipokea Ahmad na Abu Ya'alaa, na wapokezi wake ni waaminifu.

[213] . Mustarak, Juz: 4, uk: 557. Haakim amesema: “Hadithi hii upokezi wake ni sahihi kwa mujibu wa masharti ya Muslim na Bukhar, lakini hawakuiandika”.

[214] . Sahihi Muslim, Juz: 4, uk: 2252. Sunan Abu Daud, Juz:4, uk: 117. Sunan Tirmidhi, Juz: 4, uk: 511. Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 1356. Mustadrak, Juz: 4, uk: 534. Musnad Ahmad Ibni Hambal, Juz: 4, uk: 181. Tafsiir Alqur'an Al-adhiim, Juz: 1, uk: 580.

[215] . Sunan Ibni Maajah, Juz: 2, uk: 1362. Mustadrak, Juz: 4, uk: 580.

10