MOTO NA PEPO
PEPONI NA MOTONI
SEHENU YA 1
1. MAELEZO JUU YA PEPONI
Pepo ni mahala ambapo kunatofautiana hali ya starehe, pema na furaha za kila aina. Si kama Jahannam ambapo ni shimo refu mno la moto mkali, Pepo ni eneo (tambarare au imeinuka kidogo), kiasi kwamba hata mito yake haivunji kuta zake bali inabubujika vyema. Kuna Pepo au Bustani zaidi ya moja. Ayah ya Qur'an ya Surah Al-Rahman (Sura 55) inatujulisha neno moja Mudhamutan ambayo inaelezea Bustani mbili zilizo za rangi zilizoiva za kijani, ambapo Ayah ya 62 ya Sura hiyo hiyo inatuambia "mbali na Bustani hizi mbili zipo Bustani zingine mbili," zikijumlisha kuwapo kwa Bustani nne kwa ujumla katika Akhera. Bora ya Pepo ni Bustani ya Eden, orjanat 'adan. Katika kitabu Lisan al-'Arab, j.13, Uk. 99, sisi twaambiwa kuwa Pepo inamaanisha: Bustani ya miche ya matunda mbalimbali.
Katika ukurasa wa 279, juzuu 13 ya kitabu Lisan al-'Arab, twaambiwa kuwa Pepo 'Adan inamaanisha kuwa "Mahala pa milele", Bustani ya Kati (al-awsat)." Kitabu hichohicho kinatutambulisha katika uk.427, juzuu ya 7 kuwa al-awsat inaweza kumaanisha kuwa: iliyo Bora. Hakuna shaka kuwa tutaweza kuona na kupata maelezo na mafafanuzi zaidi juu ya Pepo 'adan kuliko kusema tu al-firdows, Pepo au Peponi, katika Qur'an Tukufu. Hali hii inatuacha sisi kwa kudadisi kuwa mahala bora kabisa, na iliyokuu, inayolengwa katika Pepo zote ni Pepo 'Adan.
Peponi, au al-Firdows kama vile inavyoitwa katika Kiarabu, ni neno la kuazimwa. Waarabu aliowatokezea Mtume Muhammad(s.a.w.w)
walikuwa hawana itikadi ya maisha baada ya kufa, na Pepo na Jahannam. Na kwa hakika swala hili lilikua gumu kwake Mtume(s.a.w.w)
alipoanza kuhubiri. Sura-i-Yasin,36, Ayah ya 78 inatuelezea
'Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake - akasema: "Nani atakaihuisha mifupa na hali imesagika ?"
Vile vile Qur'an inatuambia katika, Sura Ya-Sin, 36; Ayah 79:
قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ ﴿٧٩﴾
Sema: "Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya) kuumba"
Hata mwandishi wa kazi nzuri kabisa za Kiarabu, Lisan Al-'Arab, hanauhakika iwapo neno hili la Firdaws limeazimwa kutoka Kilatini au Kiajemi, au ni al-Majlisi, kama mwandishi huyo anavyokubali katika uk. 91, Juzuu ya 8 kati ya Juzuu 110 ya Encyclopedia - bila ya kuihesabu Juzuu ya Sifuri - ijulikanayo kwa jina la Bihar al-Anwar. Wazo la tatu, ambalo linaweza kuwa sahihi zaidi ni kwamba inawezekana uasili wake ukawa Babilonia. Neno lingine lililotumika katika Qur'an Tukufu ni Pepo au Bustani. Lakini kwetu sisi Pepo inamaanisha sana kuliko kutaja Bustani au shamba la miti ya matunda. Waarabu kamwe hawakuwa na tabia ya kuishi katika mshamba yao ya miti ya matunda.
Majumba yao yaliyokuwa yamejengwa kwa udongo uliochomwa au uliokaushwa kwa jua, walikuwa wakiishi kwa kujumuika katika mashamba yao kama ilivyo katika swala la Pepo. Kuwapo kwa Mayahudi wengi katika mji wa madinah (walikuwa wengi zaidi kwa kutokana na hali ya hewa) na wakazi wa Makkah waliwakubalia Mayahudi kuchangia katika baadhi ya maneno kama hayo. Jahannam linatokana na neno la Kihibrew Gehinnom (kwa mujibu wa Oxford English Dictionary (GED), jina lake kwa kikamilifu katika Kihibrew ni ge hen Hinnom, Bonde la mto wa L - Linnom, ikielezea mahala karibu na Jerusalem ambapo kwa mujibu wa Jeremiah 19 : 5, watoto walichomwa moto kwa kutolewa mhanga kwa Baal, mungu mwenye uwezo wa kuzalisha wa makafiri wa Canaaniti au kwa Molech (Moloch). Kwa habari zaidi unaweza kurejea II Wafalme 23:10 na Jeremiah 32:35 katika Biblia) (Kilatini Zehenna), Jahannam, ni lingine.
Swala hili linaweza kujitosheleza kuandika kitabu kikubwa sana ambapo si makusudio yetu hapa, hivyo kwa mukhtasari sana tuangalie milango yake ya kuingilia kama ilivyoonwa na Mtume Muhammad(s.a.w.w)
ambaye ananakiliwa katika Bihar al-Anwar j. 8, uk. 144, akielezea kama ilivyofikishwa na Abdullah ibn Mas'ud kama ifuatavyo:
"Wakati Allah swt aliponiruhusu kwenda Pepo, Jibrail
aliniambia, "Mimi nimeamrishwa kukutembeza na kukuonyesha yote yaliyomo ndani mwa Pepo na Jahannam." Hivyo mimi niliiona Pepo na baraka na mema yote yaliyokuwamo na vile vile nimeiona Jahannam pamoja na mateso yote yaliyomo. Pepo inayo milango minane, kila mlango inayo misemo minne, ambayo kila mojawapo ni bora kuliko ulimwengu mzima na kile ambacho kipo ndani mwake ni kwa ajili ya wale wanaotafakari na kufuatilia kwa kutenda kimatendo. Na Jahannam inayo milango saba, na kila mlango inayo misemo mitatu, ambapo kila msemo ni afadhali kuliko dunia yetu hii na kilichomo ndani mwa kila msemo ni kwa ajili ya kutafakari na kuyatendea kazi. Malaika Jibraili
aliniambia, "Ewe Muhammad! Soma yaliyoandikwa katika milango hizi! "Na hivyo mimi niliyasoma yote.
MILANGO YA PEPO
Katika mlango wa kwanza wa Pepo kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na njia za kujipatia riziki ni nnne : kutosheleka, kutumia katika njia sahihi, kukana kisasi na kufanya uhusiano pamoja na watu waliookoka yaani katika njia nyoofu.
Katika mlango wa pili wa Pepo kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na na njia za kujipatia furaha katika maisha ya Aakhera ni nnne : Kuonyesha huruma kwa mayatima, kuwawia wema wajane, kuwasaidia wacha-mungu katika kufanikisha malengo yao na kuwaangalia na na kuwasaidia masikini na wasiojiweza.
Katika mlango wa tatu wa Pepo kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi; zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na na njia za kujipatia siha njema katika maisha haya mafupi ni nne: Kuongea kwa uchache, kulala kidogo, kutembea kidogo na kula kidogo.
Katika mlango wa nne wa Pepo kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi; Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wageni wake; Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa jirani zake; Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wazazi wake; Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe ni mwenye kusema mema au anyamaze kimya.
Katika mlango wa tano wa Pepo kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi; Yeyote yule ambaye hataki kunyanyaswa siku ya Qiyamah, basi naye asimnyanyase mtu yeyote; Yeyote yule ambaye hataki kusengenywa siku ya Qiyamah, basi naye asimsengenye mtu yeyote; Yeyote yule ambaye hataki kudhalilishwa siku ya Qiyamah, basi naye asimdhalilishe mtu yeyote; Mtu yeyote yule ambaye anataka kujishikiza kwa umadhubuti katika maisha haya mafupi na yale ya Aakhera, basi lazima atoe shahada kuwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi.
Katika mlango wa sita wa Pepo kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi; Yeyote yule anayetaka kaburi lake liwe pana na lenye nafasi ya kutosha (kutombana) basi ajenge Misikiti; Yeyote yule anayetaka wadudu na minyoo ya ardhini wasimle, aifanye Misikiti iwe nyumba yake (yaani awe akiizuru kwa mara nyingi kama kwamba anaishi humo); Yeyote yule anayetaka kubakia freshi, (yaani asipate shida na taabu za kiu katika maisha haya na ya Aakhera ambapo kila mtu atakuwa akitafuta hata tone moja la maji) basi awe akifagia Misikiti; na yeyote yule amabye anataka kuiona nafasi yake hapo Pepo basi atengeneze sakafu na kuweka mazulia au mikeka katika Misikiti.
Katika mlango wa saba wa Pepo kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi. Moyo halisi unapatikana kwa mema manne: Kuwatembelea wagonjwa, kutembea nyuma ya jeneza, kununua sanda kwa ajili ya maiti na kulipa madeni.
Katika mlango wa nane wa Pepo kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
ni mja (Walii) Wake halisi; Yeyote yule anayetaka kuingia katika milango hii basi lazima awe na sifa nne zifuatazo: Ukarimu, adabu njema, moyo wa kujitolea na kujiepusha katika kuwadhuru waja wa mungu.
Al-Majlisi, katika uk. 131, j. 8, ya kitabu chake kiitwacho Bihar al-Anwar, ananakili uk. 39, j. 2, ya AI-Kaisal,ambapo Ubayy anamnakili Sa'd anayemnakili al-Barqi akimnakili babake akimnakili na kuthibitisha kuwa ibn al-Nasr akimnakili 'Amr ibn Shemr akimnakili Jabir ibn Abdullah al-Ansari akimnakili Imam Ja"fer al-Sadiq
akisema, "Fikirieni kuhusu Allah swt kwa bora ya mawazo yenu, na mjue kuwa Pepo inayo milango nane na upana wa kila mlango ni upana wa miaka arobaini.
Katika hotuba mbalimbali katika Nahjul Balagha, Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
anazielezea kwa undani na mapana sana kuhusu Pepo na Jahannam; hapa ninawadondosheeni machache vile anavyoelezea Pepo:
"Kipeo cha furaha na mustarehe na pongezi au hongera inatofautiana sana baina ya mtu mmoja na mwingine au mahala moja na nyingine; starehe zake kamwe haziishi; wale waliobahatika kuingia na kuishi humo kamwe hawafukuzwi au kuhamishwa, na kamwe hawapatwi na uzee, na kamwe hakuna anayeambukizwa ugonjwa wa ubakhili (Hotuba nambari 85). Wao hawajivuni wala kujigamba wala kamwe hawazaliani watoto. (Hotuba nambari 161).
Hakuna anayeingia Pepo isipokuwa wale ambao wanaouelewano mwema (na kufuata nyayo zao) pamoja na Ma-Imamu
kutokea kizazi cha Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
na ambao ndio waliothibitishwa ndivyo katika Siku ya Qiyamah (Hotuba nambari 152).
Iwapo utaingiwa na imani kwa kile utakachoelezewa kuhusu Pepo, basi nafsi yako itajitoa mbali na mavutio ya macho na mapotoshi ya duniani humu (ambayo yanafurahisha macho tu) utashangazwa kuona vile miti ilivyopangwa katika mistari na mizizi yao ikiwaimefukiwa katika marundo ya maski (mishki) katika mwambao wake. Matunda yao yanaweza kuchumwa kwa urahisi. Wakazi wake wanakarimiwa kila wakati kwa vinywaji vya asali halisi na mivinyo mbalimbali, ambayo haileweshi ulevi, wakazi wa humo watakuwa wakistarehe katika majumba yao ya fakhari. Itakuwa imeezekwa kwa 'Arsh-i-Ilahi (mbingu ya Allah swt); starehe zake ndizo nuru, na wakazi ndani ya Pepo huwa mara kwa mara wakitembelewa na Malaika wa Allah swt.
Raha na furaha kubwa kwa ajili ya wakazi wa Pepo itakuwa ni kule kuwa karibu na Allah swt na watakuwa na mawasiliano naye kwa ukaribu zaidi. Allah swt atakuwa akiongea nao kama vile mwenyeji anapokuwa akizungumza na wageni wake.
Katika uk. 114, j. 8, ya kitabu chake Sahib, al-Bukhari anamnakili Ma'ath ibn Asad akimnakili Abdullah akimnakili Malik ibn Anas akimnakili Zayd ibn Aslam akimnakili 'Ata ibn Yasar akimnakili Abu Sa'eed al-Khudri, Allah swt awe radhi nae, akimnakili Mtume wa Allah swt akisema kuwa Allah swt atawahutubia wakazi wa Pepo kwa kusema: "Enyi watu wa Pepo! nao watamjibu Allah swt kwa kusema, "Labbayk Mola wetu! Kwa furaha Yako!"
Na hapo ndipo atakapowauliza, "Je mmetosheka na kuridhika?" Nao watamjibu, "Je kweli itawezekanaje sisi tusitosheke na kuridhika wakati ambapo ulichotupatia sisi haujawapatia viumbe vyako vingine ?" Hapo atasema, "Mimi nitawapatieni mema zaidi ya hayo," nao watasema, "Ewe Mola wetu! Je ni jambo gani lililobora zaidi ya hayo ?" Allah swt atasema, "Mimi nitawateremshieni rehema na baraka zangu ziwe juu yenu, na kamwe sitawaghadhabikieni.
"
Mwandishi huyu huyu, katika Sura juu ya Tawhid, anamnakili Muhammad ibn Sinan akimnakili Fulayh akimnakili Hilal akimnakili 'Ata ibn Yasar akisema kuwa siku moja Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alikuwa akisema hadith na katika kikao icho alikuwapo bedui mmoja alikuwapo hapo. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alisema kuwa Bedui mmoja miongoni mwa wakazi a Pepo alimwomba ruhusa Allah swt kwa ajili ya kutaka kulima ardhi, ambapo Allah swt alimwuliza, "je haukupata chochote kile ulichokihitaji (kutokea miti na mimea ya humu Pepo?)"
Mbedui huyo alijibu, "Naam (nimepata kila kitu nilichokuwa nimekihitaji, lakini bado ninapendelea kulima ardhi." Kwa hayo allah swt alimruhusu kufanya hivyo; basi alipanda mbegu ardhini na katika sekundi chache tu zikaota katika miti na kukomaa na kutoa matunda mengi mno kama milima. Kwa hayo ndipo Allah swt alipomwambia, "Chukua, Ewe mwana wa Adam, kwani hakuna kinachoweza kukuridhisha wewe!" Kwa kusikia hayo, yule Mbedui aliyekuwa ameketi anayasikia hayo, akainuka na kusema, "Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
! Mtu huyo bila shaka alikuwa akitoka Quraish au kutokea Ansar, kwani wao ndio wakulima ambapo sisi Mabedui si wakulima." Kwa kuyasikia hayo, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alionyesha tabasamu.
Tabia na shauku ya kukusanya na kulimbikiza ipo katika mishipa ya wanadamu, al-Tirmithi, katika uk. 89-90, J. 2, ya kitabu chake Jami', anainakili hadith ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ambapo anawajulisha Ma-Sahaba kuwa wakazi wa Pepo watakuwa wakijumuika kila mara humo katika karamu mbalimbali kama ukumbusho wao walivyokuwa wakizipitisha Ijumaa wakati wakiwa humu duniani, nao watakuwa wakienda bazaar (masoko au gulio) ambapo watakuwa wakijichagulia nguo, vito vya thamani au chochote kile watakachokuwa wakikitaka na kuvichukua katika makazi yao.
"Bustani ya Eden," yaani Pepo 'Adan, imetajwa katika Qur'an katika mahala pengi zaidi ya moja. Kwa mujibu wa Ibn Mas'ud, ni sehemu ambayo iliyopo katikati ya Pepo. Kwa mujibu wa al-Dhahhak, ni mji uliopo ndani ya mji, ambamo wakazi wake ni Mitume
, Mashahidi, na ma-Imamu
watakuwa wakiishi huku wamezungukwa na wengine. Majengo yake yamejengwa kwa jawhari, Lulu, na vito vyenye thamani, dhahabu, almasi,fedha na kuvikwa kwa muski, na, kwa mujibu wa Muqatil na al-Kalbi, hewa nzuri na baridi itakuwa ikipepea kutokea 'Arsh ikiitumbukiza katika (kama ukungu wa) mushk nyeupe. Hata Ibilisi, shaytani, aliwaonea wivu wanaadamu kwa sababu ya Bustani ya 'Eden.
Katika ukurasa wa 115 wa kitabu Al-Mahasin, Muhammad ibn Qays anamnakili Imam Abu Ja'fer al-Baqir
akisema kuwa, "Siku moja Shaitani alimwona Mtume Nuh
akisali, basi Shaitani alimwonea wivu Mtume Nuh
na hakuweza kujizuia, akasema. "Ewe Nuh! Allah swt aliyetukuka, Mkuu, amejenga mwenyewe Bustani ya Eden , akapanda miti na kutiririsha mito ndani mwake. Na kisha akaangalia mandhari hayo na kusema, "Kwa hakika waumini na waongofu ndio washindi! La, Kwa Utukufu wangu! Mtu mwenye utovu wa adabu (mwenye madhambi) kamwe hataingia kuishi humu.
"
Aina za vyakula na vinywaji vinazungumziwa na kutajwa katika Qur'an na Sunnah, na vile vile hur al-'ayn wanawake wenye macho makubwa ndio watakaokuwa wake wa wale waliobahatika, lakini hapa mtu anaweza kujiuliza swala bila ya kujizuia : Je ni kitu gani kile kitakachowafurahisha mno wakazi wa Pepo? Je yatakuwa ni vinywaji, vyakula, sauti kama za muziki zitokanazo na matawi na majani ya miti ya Pepo , au nyimbo zitakazokuwa zikiimbwa na hawa hur al-'Ayn ama mmoja mmoja au kimakundi, zitakazokuwa zikimsifu Allah swt na kumtukuza? Katika Tafsiri ya Tafsir, al-'Ayyashi, kama ilivyoandikwa katika uk. 139, J. 8, ya Bihar al-Anwar, anamnakili Abu Baseer akimnakili Abu Abdullah Imam Ja'fer al-Sadiq
akisema: 'Wakazi wa Pepo watastarehe vyakula na vinywaji zaidi kuliko masuala ya kujamiiana.
"
Katika ukurasa wa 438-439 ya kitabu cha Ali ibn Ibrahim Tafsir, kama ilivyonakiliwa katika uk. 120-121, J. 8, ya al-Majlisi Bihar al-Anwar, imeelezwa kuwa Ibn Abu 'Umayr anamnakili Abu Busayr kuwa yeye alimwuliza mara moja Abu Abdullah Imam Ja'fer al-Sadiq
kuchochea hisia zake za matamanio kuhusu Pepo , Imam
alimjibu, "Ewe Abu Muhammad! Je kunaweza kuhisiwa manukato mazuri kabisa ya Pepo hata kutokea mwendo wa maelfu ya miaka, na makazi patakatifu katika Pepo ni yale ambapo Majini na wanadamu watakwenda; humo watahudumiwa vyakula na vinywaji vya kila aina bila ya kupungua au kuisha kwa kitu chochote kile. Bora miongoni mwa wakazi za Pepo ni yule ambaye, atakapoingia katika mabustani yake, ataona mabustani matatu (na wala si bustani moja) iliyojaa wanawake, wajakazi, mito na matunda ya kila aina ambayo yatafurahisha macho na moyo wake kwa furaha isiyoelezeka. Mtu huyo atakapokamilisha kumshukuru na kumtukuza Allah swt, yeye ataambiwa kukiinua kichwa chake kwa ajili ya kuiangalia Bustani ya pili, kwani kutakuwamo yale yasiyokuwamo katika Bustani ya kwanza. Kwayo, atamsifu na kumtukuza Allah swt na kumwomba, "Ewe Mola wangu! Ninakuomba unipe Bustani hii (badala ya ile ya kwanza)! Kwa hayo Allah swt atamwambia, Iwapo nitakupa Bustani hii, basi wewe utaanza kunitaka nikupatie nyingine badala ya hii! Basi huyo mtu atasema, "Kwa hakika hii tu ndiyo ninayoihitaji, Ewe Mola wangu!" Na wakati atakapoingia humo ndani, furaha zake zitaongezeka zisizo na kifani, na atamshukuru na kumsifu na kumtukuza Allah swt, na hapo ndipo milango itakapoamrishwa kufunguliwa na ataambiwa kuinua kichwa chake.
Pale Bustani ya milele itakapokuwa wazi mbele yake, yeye ataangalia mara kwa mara kama alivyokuwa ametaza hapo awali. Wakati furaha zake zitakapokuwa zimezidi kifani, atasema, "Usifiwe Ewe Mola wangu ! Kwa hakika sifa hazina kiwango cha kukusifu kwa yale yote uliyonijaalia : Bustani na kuniepusha na Jahannam (Motoni)." Hapo, Abu Busayr hakuweza kujizuia kwa kuangua kilio, na alijikaza na akamwomba Imam
amwelezee zaidi. a l-Imam Muhammad al-Baqir
akaendelea kumwambia: "Ewe Abu Muhammad! Katika kingo za mito ya Pepo kuna wanawake wanaowasubiri waume zao kama vile zilvyo miti iliyoota katika mstari. Pale atakapomchukua mmoja, basi mwingine atakuwa ameshawekwa kuziba pengo hilo
."
Abu Busayr akasema: "Niwe fidia kwako! Tafadhali sana naomba uniambie zaidi
!"
Al-Imam Muhammad al-Baqir
aliendelea kumwambia: "Mumin ataozeshwa kwa bikira mia nane, elfu nne tayyibs (ni wanawake waliokua ama hawakuolewa ambao ni wajane wacha-mungu wema au waliochiwa na waume zao) na hur al-'Ayn wawili." "Bikira mia nane ?!" Abu Busayr alimwuliza Al-Imam Muhammad al-Baqir
kwa mshangao mkubwa sana. "Naam. Yeye atawaona hivyo hivyo pale atakapojamiiana nao." "Maisha yangu yaweyametolewa kwa ajili yasko," alisema Abu Busayr, "Je hur al-'Ayn wameumbwa kwa kitu gani?" Al-Imam Muhammad al-Baqir
alimjibu kuwa: wameumbwa kwa mada ya Pepo iliyoumbwa, na kuongezea, "Miguu yao itakuwa ikionekana hata kama kutavishwa mavazi sabini.
"
Abu Busayr alimwuliza Al-Imam Muhammad al-Baqir
, "Maisha yangu yawe fidia kwako, je wanazungumza chochote huko?" Al-Imam Muhammad al-Baqir
alimjibu, "Wao wanazungumza yale ambayo hakuna mwanadamu aliyewahi kuyasikia." Abu busayr aliuliza, "Je ni nini hayo ?" Al-Imam Muhammad al-Baqir
alimjibu, " Sisi tutaishi milele na kamwe hatutakufa! Sisi ni wale waliobarikiwa, hivyo kamwe hatutahangaika na kutaabika! Sisi ni wale tuishio na kamwe hatutatengana! Sisi ni wale wenye furaha na kutosheka, hivyo kamwe hatuna mashitaka! Habari njema kwa wale waliokuwa wameumbwa kwa ajili yetu, na habari njema kwa ajili ya wale tuliokuwa tumeumbiwa! Sisi ni wale ambao kama tungening'inia angani, basi nuru yetu ingeling'arisha kila sehemu ."
Ibn Qawlawayh, na vile vile al-Majlisi ambaye katika uk. 143, J. 8, ya kazi yake Bihar al-Anwar, anamnakili Sa'd akimnakili Ibn 'Eisa akimnakili Sa' eed ibn Janah akimnakili Abdullah ibn Muhammad akimnakili Jabir ibn Yazid akimnakili Imam Abu Ja'fer al-Baqir
akiwanakili Mababu zake
(yaani ma-Imamu
wakisema kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alisema, "Mitume yote imekatazwa kuingia Pepo kabla yangu, na mataifa yote yamekatazwa kuingia humo kabla ya waumini watufuatao sisi, sisi Ahlul Bayt
, kuingia ndani mwake." Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
amenakiliwa akisema, uk.139, J.8 ya Bihar al-Anwar, akisema, "Pepo inayo milango sabini na moja ya kuingilia: Ahlul Bayt
yangu na wafuasi wao wataingilia milango sabini, wakati ambapo watu wengine wataingilia mlango uliobakia."
Furaha nyingine ya Pepo ni kwamba kule hakuna kuzeeka kwa wakazi wa Pepo, na kamwe hawatapatwa na maumivu ya aina yoyote yale, na kamwe hawatataka kujisaidia kwa choo ndogo au kubwa; na badala yake kile wakilacho kitatoka mwilini kama jasho lenye manukato mazuri mno. Hawatakuwa na ukiritimba wa aina yoyote ile na kamwe hawatanyimwa kitu chochote kile. Matamanio yao yatatimizwa, na furaha zao kamwe hazitaisha na kamwe hawatajisikia wanyonge wasio na raha. Tunamwomba Alah swt atuingize Pepo bila ya kujali mema kiasi gani tufanyayo, kwani Yeye ndiye pekee wakutuhurumia na kutufanyia hisani. Yeye ndiye anayetujaalia moyoni mwetu moyo wa kufanya mema: Ni yeye pekee anayetuwezesha sisi kufanya mema, na ni Yeye pekee ambaye anakubalia mema yetu na kutulipa thawabu zake, kwani ni dhahiri kuwa sisi tusingaliweza kujifanyia mema kwa uwezo wetu wenyewe. Allah swt ndiye pekee chanzo cha wema na ndiye wema pekee.
Mwishoni, kila mtu anajawa na shauku ya kujiuliza vile Pepo itakavyokuwa kwa ujumla. Kwa mujibu wa habari tulizozisoma hapo juu, kuhusu Pepo 'Adnan inaelezwa kuwa itakuwa ni mzunguko na Bustani ya Eden itakuwa katikati ikizungukwa na Bustani zinginezo za wale waliokuwa wafuasi na wapenzi wa ahlul Bayt
ya wananyumba ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
na kuyafuata matendo yake,wakizungukwa na wale waliokuwa waaminifu kwao kwa maneno na vitendo, n.k. Iwapo utaendelea kutoka hoja hiyo, iwapo upeo wa matendo na malipo yako yatakavyokuwa kidogo, ndivyo atakapokuwa katika Pepo na furaha zake. Ukiwa na daraja la juu basi utafaidika zaidi, na ikiwa daraja lako ni chini kidogo basi, na starehe za huko pia zitakuwa zimepungua kidogo. Uduara unamaanisha kudumu kwa milele. Bustani hiyo inadhaniwa kuwa ni duara, lakini Allah swt ndiye ajuaye zaidi.
SABABU ZIMFANYAZO MTU KUINGIA PEPONI
1. IMANI NA MATENDO MEMA
Kwa hakika Imani na matendo mema ndiyo masuala bora kabisa na ambayo yanamletea furaha mtu na inasadikiwa kuwa ndiyo ufunguo wa Pepo na baada yake sababu zote zitakazoendelea kuelezwa basi mutaona kuwa zote hizo ni matawi ya hoja hili na Allah swt pia anasema kuhusu Imani na Matendo mema kuwa mtu yeyote atakayetekeleza hayo humu duniani basi Allah swt lazima atamjaalia Pepo. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Baqarah ,2 , Ayah 82
Na wale walioamini na wakatenda mema, hao ndio watu wapeponi, humo watadumu
.
2. TAQWA
Taqwa inamaanisha kujiepusha yaani yale yote yaliyosemwa na Ahlul Bayt
ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
kuwa ni halali basi ndiyo halali na yale yote yaliyosemwa ni haramu basi yawe ni haramu. Allah swt ametoa ahadi kuwa atakayeishi kwa Taqwa basi mahala pake patakuwa ni Pepo. Na hivyo ndivyo maana anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Maryam ,19 , Ayah 63:
Hiyo ndiyo Pepo tutayowarithisha katika waja wetu walio kuwa wachamungu
Vile vile twaambiwa katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Hujurat ,49, Ayah 13:
Enyi watu! Hakika Sisitumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa na mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Allah swt ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi
.
3. IHSANI NA MATENDO MEMA
Yaani kuwafanyia watu mambo mema na matendo yetu yawe mema kwa ujumla na kwa hakika haya ndiyo mambo mema na bora kabisa na ndiyo sababu za kuingia Pepo. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al-Maidah,5, Ayah 85:
Basi Allah swt atawalipa, kwa yale waliyoyasema, Bustani zipitazo mito katika yake; humo watadumu. Na haya ndiyo malipo ya wafanyao wema.
4. JIHADI NA KUWA SHAHIDI
Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al- Tawbah, 9:111:
Hakika Allah swt amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Allah swt - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'an. Na nani atimizae ahadi kuliko Allah swt ? Basi furahini kwa biashara yenu mliy fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.
5. KUTOKUFUATA NAFSI YAKE
Yaani mtu hafuati matamanio ya nafsi yake na badala yake anaikhilafu. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Naziat, 79: 40 - 41:
Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt Mlezi, na akijizuilia nafsi yake na matamanio,Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake
!.
6. KUSHINDANIA KATIKA KULETA IMANI
Allah swt atuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al- Waqia, 56: 10 - 13:
Na wa mbele watakuwa mbele. Hao ndio watakao karibishwa Katika Bustani zenye neema
.
7. HIJRAH NA JIHAD
Tumeshaona kuwa Jihadi imeshatajwa hapo mwanzoni (Jihadi na kuwa Shahidi, namba. 4) hapa Jihadi imekuja lakini pamoja na Hijrah. Yaani Hijra ni Jihadi mojawapo kwa ajili ya Mumin. Tumeona kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
aliiacha Makkah na kwenda Madina, hii ilikuwa ndiyo Jihadi mojawapo ambayo ndiyo kwa ajili ya Allah (s.w.t) na Dini.
Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al- Tawbah, 9: 20-22:
Wale walioamini na wakahama, na wakapigana Jihadi katika njia ya Allah swt kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Allah swt. Na hao ndio wenye kufuz. Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu. Watadumu humo milele. Hakika kwa Allah swt yapo malipo makubwa
.
8. SUBIRA NA USTAHIMILIVU WAKATI WA SHIDA
Kufanya Subira na Ustahimilivu wakati mtu anapopatwa na shida na matatizo mbalimbali ama yakupoteza mali, kufiwa, kuugua n.k Katika vitabu tunapata habari kuwa Mitume(s.a.w.w)
na Maimamu
pia wamepitia shida kali kali ambazo wao wamezifanyia subira na ustahimilivu kwa ajili ya furaha ya Allah swt. Qur'ani Tukufu, Sura al-Dahar, 76, Ayah 12:
Na atawajaza Bustani za Pepo na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri
.
Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Ra'd, 13, Ayah 24:
Hao ndio watu wa Pepo, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. (Wakiwaambia) Assalamu 'Alaikum! amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera
.
9. KUWA IMARA KATIKA DINI
Inambidi mtu awe madhubuti katika Dini kama ukuta wa Shaba yaani awe na uwezo wa kukabiliana na kila sura itakayojitokeza mbele yake kiasi kwamba kamwe hataweza kulega lega katika dini na kamwe hataweza kurudi nyuma katika msimamo wake wa Dini. Allah swt anasema katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Ahqaf, 46, Ayah 13 - 14:
Hakika waliosema:Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu; kisha wakatengenea,hawatajuwa na khofu, wala hawatahuzunika
.
10. Kumtii Allah swt na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Inatubidi sisi kumtii Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ili kuwa mustahiki wa Pepo. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4, Ayah 13:
Na anayemtii Allah swt na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa
.
11. IKHLAS (UHALISI)
Iwapo kama hakutakuwapo na uhalisi katika kila jambo basi hakutakuwa na usahihi wa kitu au jambo hilo. Uhalisi lazima uwepo katika Imani, matendo na akili na fahamu zetu na kwa hakika huu ndio ufunguo wa kuingia Pepo na ndivyo maana Allah swt ameweka sharti hili la kumwezesha mtu kuingia Pepo na Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Safaat, 37, Ayah 39 - 43:
Wala hamlipwi ila hayo hayo mliyokuwa mkiyafanya. Isipokuwa waja wa Allah swt walio khitariwa. Haom ndio watakaopata riziki maalumu, Matunda, nao watahishimiwa
.
12. UKWELI
Kwa hakika sharti hili ni la umuhimu wa aina yake kwani kila jambo tulifanyalo linahitaji ukweli na kama hakuna ukweli basi kila kitu kitaharibikiwa. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al-Maidah,5: 119: Allah swt atasema:
Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Allah swt amewawia radhi, nao awe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa
.
13. KUJITAKASISHA MWENYEWE
Inambidi kila mtu atulie na kujitakasisha nafsi yake mwenyewe kwa kila jambo na hivyo alete mapinduzi ndani mwake. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura Ta-Ha, 20: 75- 76:
Na atakayemjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu
.Bustani za milele zipitazo mito kati yake,wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa
.
14. KUTOA KATIKA NJIA YA ALLAH SWT NA KUOMBA TAWBA
Allah swt anatutaka sisi tule na tuwalishe wengine pia tuwe wakarimu na kamwe tusiwe mabakhili na tuombe Tawba kwa ajili ya madhambi yetu. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura Ali Imran, 3, Ayah 133-136:
Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyowekwa tayari kwa wachamungu,
Ambao hutoa wanapokuwa na wasaa na wanapokuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Allah swt huwapenda wafanyao wema; Na ambao pindiwafanyapo uchafu au wakjidhulumu nafsi zao humkumbuka Allah swt na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nai anayefuta dhambi isipokuwa Allah swt? - na wla hawapendelei na waliyo yafanya na hali wanajua. Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mto kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao.
15. HOFU YA ALLAH SWT
Kuna msemo kwamba Mwogopeni yule mtu ambaye hamwogopi Allah swt! Na wala musimwogope yule mtu ambaye anamwogopa Allah swt! Kwa sababu yule mtu ambaye anamwogopa Allah swt kamwe hatakudhuru nyuma yako na atakuwa akijua kuwa Allah swt hatafurahishwa na hatua yoyote ile ya kukuletea madhara. Ndiyo maana tunaambiwa kuwa tusiwaogope Waumini, tuongee nao waziwazi bila ya kuwa na hofu ya aina yoyote, lakini bila ya kuwatuhumu. Lakini yule asiye na hofu ya Allah swt atatafuta kila hila na mbinu za kukudhuru wewe kwa sababu hana hofu ya Allah swt. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al-Rahman, 55, Ayah 46:
Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt atapata Pepo (Bustani) mbili
Vile vile nitapenda kuwaleteeni Hadith ya Al-Imam Ja'afar as-Sadiq
amesema katika Majma'ul Bayan:
"Mtu yeyote ambaye anajua na kutambua wazi kuwa mimi nifanyapo jema au baya, basi Allah swt yupo anashuhudia matendo yangu haya, basi mtu kama huyu daima atakachokuwa akikifanya basi atakuwa mwangalifu mno katika matendo yake na atajiambia kuwa lau nitafanya kazi hii njema basi Allah s.w.t atalipa mema kadha na kadha na lau nitafanya maasi na madhambi, basi Allah swt ataniandikia adhabu kadha wa kadha. Kwa hivyo watu kama hawa wamewekewa Bustani mbili katika Pepo
."
16. TAWALLA NA TABARRA
Ama kuhusu mtu atakaye fuata masuala haya mawili basi Allah swt atamjaalia Pepo na uthibitisho wake ni kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, Sura al-Mujadilah, 58, Ayah 21:
Allah swt ameandika:Hapana shaka Mimi na Mtume wang tutashinda. Hakika Allah swt ni Mwenye nguvu, mwenye kushinda
.
Tawalla maana yake ni kuwa rafiki wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
na Ahl al-Bayt
na Tabarra inamaana ya kujiepusha na kujiweka mbali na kutokuwa na uhusiano wowote pamoja na wale maadui wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
pamoja Ahl al-Bayt
.
17. KUDUMISHA SALA
Katika maana yake ni kwamba inambidi kila Mwislamu awe akisali sala zote zilizofaradhishwa juu yake kwa kuzingatia umuhimu na nyakati zake. Zipo Sala nyingi ambazo tumefaradhishiwa katika Islam kwa mfano Sala tano za siku, Sala za matukio kama mitetemeko, kupatwa kwa jua au mwezi, n.k. (rejea vitabu vya fiq-hi). Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al-Ma'arij, 70, Ayah 22 -34:
Isipokuwa wanaosali,Ambao wanadumisha Sala zao,Na ambaokatika mali yao iko haki maalumu Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba; Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. Na ambao anahifadhi tupu zao.Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - Lakini wanaotaka kinyume ya haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka. Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, Na ambao wanazihifadhi sala zao. Hao ndio watakao hishimiwa Peponi.