UKWELI WA SHIA ITHNA ASHARIYA
SEHEMU YA PILI
UADILIFU WA MASAHABA
Maneno yamekuwa mengi kuhusu uadilifu wa Masahaba, na watu katika hilo wamekhitalafiana Ikhtilaf kubwa. Ahl as-Sunnah wanaona kuwa Masahaba wote ni waadilifu hawatuhumiwi wala haijuzu kwa yeyote kuwakosoa, au kushuku katika mapokezi yao katika Hadith za Mtume wa Allah
. Na anayefanya hivyo wanatoa Fatwa juu ya ufasiki wake na wanazingatia kuwa ni zandiki, na wao kwa hilo wanajilazimisha kwa kila alicho kipokea Sahaba, kwa mfano inatosha kwao kukubali Hadith iliyopokelewa kwa Sahaba yeyote yule, na Sahaba kwao ni kama alivyoeleza Al-Bukhari: “Ni ambaye alifuatana na Mtume Muhammad Mustafa
au aliye mwona miongoni mwa Waislamu.”
Na wala sioni katika hukumu yao hiyo katika ufasiki wa kila anaye mkosoa yeyote miongoni mwa Masahaba, isipokuwa ni israf katika kuamini na ni kupinga Kitabu cha Allah (s.w.t), Sunnah za Nabii wake na tabia ya binadamu kama tutakavyo thibitisha hayo katika kurasa zinazofuata.
Hakika wanayo singiziwa Shi’a kwamba wao wanakufurisha Masahaba wote, kwa kuongeza kuwatukana kwao na kuwalaani, hayo si kingine isipokuwa ni uongo ulio wazi na wala hauna usahihi wowote. Shi’a hawawakufurishi Masahaba lakini wanaona kuwa wao wanaweza kukosolewa na kurekebishwa na kwamba wote hawakuwa katika daraja moja ya uadilifu, na kumkosoa kwao Sahaba huyu au yule haina maana ya kuwakufurisha, kama wanavyoeneza baadhi ya wapumbavu, na kama ukosoaji wao umesimama juu ya dalili, sasa hasira ni ya nini? Na kelele yote hii ni ya nini?
Katika Masahaba kuna waumini walio wema, Allah (s.w.t) amewasifu katika Qur’an tukufu kwa kauli yake:
لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا ﴿١٨﴾
Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu
. (Al-Fath 48:18)
Hivyo Allah (s.w.t) amewasifu tu waumini mahsusi, kati ya waliohudhuria tukio la Bay’atus-Shajarah na hakuwahusisha wanafiki ambao walihudhuria mfano ‘Abdallah bin ‘Ubay na Aus bin Khauli. Na hakuna dalili katika Ayah juu ya Allah (s.w.t) kuridhia Masahaba wote waliobay’i - pamoja na kuwa wao wanawahesabia kuwa ni katika Masahaba kwa madai ya Bukhari na mfano wake - bali haionyeshi juu ya mwisho mwema kwa waumini wote walio bay’i.
Ayah haionyeshi zaidi ya kwamba Allah (s.w.t) ameridhia Bai’a yao hii - yaani ameikubali kutoka kwao - na amewapa thawabu, ridhaa ya Allah (s.w.t) juu ya watu wa Bai’a hii hailazimu ridhaa yake hii kuwa ni daima, na dalili katika hilo ni kauli ya Allah (s.w.t) katika jambo lao
إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّـهَ يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّـهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٠ ﴾
Hakika wale wanaokubay’i wanambay’i Allah (s.w.t) mkono wa Allah (s.w.t) uko juu ya mikono yao na atakaye tengua (Bai’a yake) basi hakika anatengua kwa ajili ya nafsi yake, na atakaye tekeleza aliyomwahidi Allah (s.w.t) basi atampa malipo makubwa”. (Al-Fath 48:10).
Na miongoni mwa Masahaba kuna ambaye Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w
)
ameeleza kuritadi kwake baada ya kufa kwake na kisha kuangamia kwao siku ya Qiyamah kama yanavyo dhihirika wazi hayo katika Hadith mbili zifuatazo chini:-
Sa’ad amesema nimemsikia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w
)
amesema: “Mimi nitawatangulia katika Hawdh atakaye nifikia atakunywa kwayo na atakaye kunywa hata pata kiu kamwe baada yake, watanijia watu na wajua na wananijua kisha kutawekwa kizuizi baina yangu na wao.”
Akasema nilimsikia akiongezea: Akasema: “Hakika wao ni katika watu wangu, itasemwa: Hakika wewe hujui waliyo yabadilisha baada yako, basi nitasema, awe mbali aliye badilisha baada yangu
.”
Amesema ‘Abdillah kwamba amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w
)
: “Mimi nitawatangulia katika Hawdh, hakika wataletwa wanaume mionngoni mwenu mpaka nitakapo karibia ili niwapatie (maji) watazuiwa dhidhi yangu, basi nitasema: Ewe Allah (s.w.t), Masahaba wangu.’ Atasema: ‘Hujui waliyoyazua baado yako
.
Na mkazo wa Hadith mbili zilizo tangulia ambazo zinaonyesha kuzua na kubadilisha – yaani kuritaddi - hakika Hadith ifuatayo inawalinganisha na ‘Ummah za Kiyahudi na Kinasara ambao walipotosha maneno katika makusudio yake. (Kutoka kwa Nabii amesema: “Hakika mtafuata nyendo za waliokuwa kabla yenu shibr kwa shibr, dhiraa kwa dhiraa hata kama wataingia katika shimo la kenge mtawafuata.” Nikasema: “Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
: “MAyahudi na Manasara?” Akasema: “Ni nani basi?”
Katika Masahaba kuna miongoni mwa aliowaelezea Allah (s.w.t.) katika Kitabu chake kitukufu:
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ وَاللّ َـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١﴾
“Na wanapoona biashara au upuuzi wanakimbilia huko na wanakuacha umesimama
…”(Al-Juma’a 62:11).
Ayah hii imeteremka kwa Masahaba walioondoka msikitini wakati Mtume(s.a.w.w
)
amesimama anawahutubia siku ya Ijumaa ulipowasili msafara kutoka Sham na hawakubaki pamoja na Mtume(s.a.
w.w
)
isipokuwa wanaume kumi na mbili kama inavyodhihirika katika Hadith mbili hapa chini.
Amesema Jaabir ibn Abdillahi: Uliwasili msafara wa ngamia siku ya Ijumaa na sisi tuko pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w
)
basi watu walitoka isipokuwa wanaume kumi na mbili, basi Allah (s.w.t) akateremsha Ayah; “Na wanapoona biashara au upuuzi wanaenda huko”
Amesema:”Tulipokuwa tunasali pamoja na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w
)
basi ukawasili msafara wa ngamia umebeba chakula wakauendea na hawakubaki pamoja na Nabii isipokuwa wanaume kumi na wawili basi ikateremka Ayah hii (Na wanapoona biashara au upuuzi wanauendea na wanakuacha umesimama)
.
Idadi hiyo hiyo - katika mamia yote hayo miongoni mwa Masahaba - walibaki pamoja na Mtume wakati walipokimbia katika vita vya Uhud kiasi kwamba Mtume(s.a.w.w
)
alijiweka mbali nao kutokana na kitendo chao.
Amesema: Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w
)
alimpanga ‘Abdallah bin Jubayr katika wapiganaji wanao kwenda kwa miguu siku ya Uhud na wakakimbia waliposhindwa, hivyo Mtume akawa anawaita kwenye Akhera yao, na hawakubaki pamoja na Nabii isipokuwa wanaume kumi na wawili)
.
(Kutoka kwa Anas (r.a) amesema: Alitoweka ami yangu Anasi bin Nadhir katika vita vya Badr akasema: Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w)
: Nilighibu katika vita vya mwanzo ulivyowapiga washirikina, naapa kama Allah (s.w.t) atanijaalia kupigana vita na washirikina basi Allah (s.w.t) ataona nitakavyofanya.
Siku ya Uhud ilipofika na Waislamu wakashindwa na kukimbia, akasema: “Ewe Allah mimi naomba samahani kwako kwa waliofanya hawa watu, yaani Masahaba wake
.”
Na siku ya Hunain kukimbia kwao kulikuwa ni jambo la kushangaza wakati ambapo walikuwa maelfu.
وَيَوْمَ حُنَيْنٍ إِذْ أَعْجَبَتْكُم ْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ ﴿٢٥﴾
“Na siku ya Hunain ulipowashangaza wingi wenu na haukuwasaidia kitu chochote na ardhi ikawa finyu kwenu kutokana na mlivyoshambuliwa kisha mkakimbia kurejea nyuma, halafu Allah akateremsha utulivu wake kwa Mtume wake na waumini.
”(At-Taubah 9:25-26).
Na katika masahaba kuna ambao wameteremkiwa na Ayah:
مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْ آخِرَةَ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٦٧﴾ لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٦٨ ﴾
“Haikuwa kwa Nabii awe na mateka hadi apate dhiki katika ardhi, mnataka utajiri wa kidunia na Allah anataka akhera. Allah ni Mtukufu na ni Mwenye nguvu. Kama si Kitabu kitokacho kwa Allah basi ingekufikieni adhabu kubwa kwa yale mliyoyafanya
.(Al-Anfaal 8:67-68).
Ayah hii imeteremka siku ya Badr, au baada yake katika kundi miongoni mwa masahaba. Nabii alikuwa amewataka ushauri ili kuona upeo wa kuwa kwao tayari kwa ajili ya vita-basi maoni yao yakawa ni kuteka ngamia na kilichobebwa na msafara wa Abu Sufian na wala wasipigane kama yanavyo dhihirika hayo katika Hadith ifuatayo ambapo inadhihiri ta’assub yao ya kikabila-na wao ni katika masahaba…hata mbele ya Mtume?
‘Amru amesema: “Nilimsikia Jaabir bin ‘Abdillah (r.a) akisema: ‘Tulikuwa katika vita, Sufian akasema (maneno fulani) katika jeshi, basi mtu mmoja katika Muhajirin akampiga mtu (mwengine) miongoni mwa Ansar, yule mu-Ansar akasema: Enyi Ansar (wenzangu) na (yule mwengine katika) Muhajirin akasema: Enyi Muhajirin (wenzangu), Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
akasikia hayo akasema: Huu mwito wa kijahili ni wa nini
.”
Sa’ad bin Ma’adh akasimama na kusema: “Ewe Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
nakuomba msamaha kwa hayo kama ni katika Aus tutamkata shingo lake na kama ni katika ndugu zetu wa Khazraj utatuamuru amri yako.” Akasimama Sa’ad bin ‘Ubadah naye ni bwana wa Khazraji na kabla ya hapo alikuwa ni mtu mwema, na alikuwa ameshikwa na ta’assub akasema: “Uongo hutamwua wala hilo huliwezi, akasimama Usiad bin Hadhiri akasema: “Umesema uongo Wallahi tutamuuwa, hakika wewe ni mnafiki unajadili juu ya wanafiki.
Basi ikazuka fujo kati ya Aus na Khazraj mpaka wakataka kupigana na Mtume yuko juu ya mimbar, alishuka akawatuliza hadi wakanyamaza naye akanyamaza
.
Na katika Masahaba kuna baadhi yao walikuwa wanamchukia Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib
, ambaye kumchukia ni alama ya unafiki kama ilivyoelezwa:
Kutoka kwa Buraydah amesema: Nabii alimtuma ‘Ali kwa Khalidi kuchukua Khums, na nilikuwa namchukia ‘Ali na alikuwa ameshaoga, nikamwambia Khalid, je humwoni huyu? Tulipofika kwa Nabii nikamweleza akasema: “Ewe Buraydah unamchukia ‘Ali?” Nikasema: “Ndiyo,” akasema usimchukie hakika yeye katika Khums ana zaidi ya hayo
.
Na miongoni mwao kuna walio mkosoa Mtume katika kumpa uongozi Usama bin Zaid juu yao: - Kutoka kwa ‘Abdillah bin ‘Umar amesema Mtume alituma kikosi na akampa Usama bin Zaid uongozi baadhi ya watu wakakosoa katika kumpa uongozi, Nabii akasema kama mnakosoa katika uongozi wake basi mlikwishakosoa katika uongozi wa baba yake kabla yake
.
Na katika Masahaba kuna aliowatoa Nabii katika majilisi yake walipomtuhumu kwa neno baya, naye yuko katika maradhi yake ya mwisho kabla ya kuyaaga maisha ya dunia. Sa’id bin Jubayr alimsikia Ibn ‘Abbas anasema siku ya Alhamisi, ni ipi siku ya Alhamisi, kisha akalia mpaka machozi yake yakaloanisha changarawe nikasema:
“Ewe Ibn ‘‘Abbas ni ipi siku ya Alhamisi?” Akasema: “Mtume alizidiwa na maradhi yake akasema: ‘Nileteeni karatasi niwaandikie maandiko hamtapotea kamwe baada yake’, basi wakazozana na haifai kuzozana mbele ya Mtume, wakasema, ‘ana nini, anaweweseka? Muulizeni’, akasema: ‘Niacheni kwani niliyo nayo ni bora kuliko hayo mnayo niitia
.”
Na katika Masahaba kuna waliogombania uongozi baada ya kufariki Mtume mpaka ikafikia kutaka kuchaguliwe viongozi wawili mmoja wa Muhajirin na mwingine wa Ansar.
Kisha akasema; ‘amma ba’ad, sisi ni Ansar wa Allah (s.w.t) na kikosi cha Kiislamu na nyinyi Muhajirin ni kundi na limenyemelea kundi katika kaumu yenu basi wakawa wanataka kututoa katika msingi wetu na kutupokonya uongozi
.
Msemaji wa Ansar akasema: Mimi ni shina lake lenye nguvu na tawi lake lenye matunda akasema: Mimi ni shina lake lenye nguvu na tawi lake lenye matunda kwetu kuwe na kiongozi na kwenu kuwe na kiongozi, enyi Maquraish. Basi ugomvi ukawa mkubwa na makelele yakawa mengi mpaka nikatoka na kuacha ikhtilafu
.”
Na katika Masahaba kuna Abu Huraira - ambaye tumetenga nafasi yake maalumu katika sehemu ya nne - vile vile kuna Mu’awiyah bin Abi Sufian hivyo rejea tuliyoyataja kuhusiana naye katika sehemu ya kwanza kwa kuongezea hadith nne zifuatazo:-
Kutoka kwa baba yake amesema: Nabii alimtuma Khalid bin Al-Walid kwenda kwa Bani Jadhima akawalinganie Uislamu, basi hawakuweza kusema kwa ufasaha: “Aslamna (tumesilimu) wakawa wanasema: “Sabaana Sabaana” Khalidi akawa anawaua baadhi yao na kuwateka, na kutupa kila mmoja wetu mateka ilipopita siku Khalidi akaturuhusu kila mtu auwe mateka wake: “Nikasema Wallahi sitouwa mateka wangu na wala hatouwa mtu katika wafuasi wangu mateka wake, mpaka tukafika kwa Mtume Muhammad Mustafa
tukamweleza Nabii
akanyanyua mikono yake akasema: Ewe Allah, mimi najikinga kwako na aliyoyafanya Khalidi mara mbili
.”
Tumeona katika siku ya Hudaibiyyah yaani suluhu ambayo ilikuwa baina ya Nabii na washirikina, na kama tungeona vita basi tungepigana, akaja ‘Umar akasema, je hatuko katika haki? Na wao wako katika batili? Je, watu wetu si wataingia Jannat na watu wao wataingia Jahannam? Akasema: “Ndiyo”, akasema kwa nini tuwe wanyonge katika dini yetu na tunarudi, na Allah bado haja hukumu baina yetu?” Akasema: “Ewe mtoto wa Khattab! Mimi ni Mtume wa Allah (s.w.t) na Allah (s.w.t) hawezi kunipoteza kamwe.”
Akarejea akiwa na hasira, hakusubiri akamwendea Abubakr akasema: “Ewe Abubakr je, hatuko katika haki na wao wako katika batil?” Akasema: “Ewe mtoto wa Khattab, hakika yeye ni Mtume wa Allah, na allah hatampoteza kamwe
.”
Hivyo ‘Umar bin Al-Khattab hakuridhika na kupata tumaini kwa majibu ya Mtume akaenda kwa Abubakr na akaeleza upinzani wake pamoja na kwamba haijuzu Nabii kupingwa na yeyote katu.
Kutoka kwa ‘Urwah kutoka kwa ‘Aisha (r.a) amesema Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
aliingia kwangu nikiwa na wasichana wawili wakiimba wimbo wa jeshi, akajilaza kitandani na akageuza uso wake, akaingia Abubakr akanikemea na akasema zumari za Shetani mbele ya Mtume wa Allah
, Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
akamjia akamwambia waache, alipolala nikawafanyia ishara, wakatoka
.”
Habari hii haisihi kwa hali yeyote, kwa sababu Mtume haiwezekani akasikiliza zumari na muziki ukiachilia mbali hayo kutendeka ndani ya nyumba yake, wakati ambapo Abubakr anajizuia kutokana na hayo na kuyaita zumari za Shetani. Je Abubakr ni mchamungu zaidi ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w
)
? Na habari hii imepokewa kutoka kwa Sahaba; namna gani tutaafiki uadilifu wao na ukweli wao? Kutoka kwa Mulaikah amesema: “Ilikaribia Wema wawili kuangamia: Abubakr na Umar walinyanyua sauti zao mbele ya Nabii ulipowasili msafara wa Bani Tamim”
.
Hakika kuwa rafiki wa Nabii sio sifa kubwa kuliko utukufu wa kuoa kwa Nabii. Amesema Allah (s.w.t) kuhusu wanawake:
يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَن يَأْتِ مِنكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ و َكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾
“Enyi wake wa Nabii atakayefanya miongoni mwenu uovu ulio wazi basi ataongezewa adhabu mara mbili
.” (Al-Azhaab 33:30).
ن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ ﴿٤﴾
Tubuni kwa Mwenyezi mungu kwani nyoyo zenu zimeasi na kama mtasaidiana dhidi yake basi Allah (s.w.t) ni mlinzi wake.” (At-Tahriim 66:04)
ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ ﴿١٠﴾
Hadi kauli yake “Allah (s.w.t) amepiga mfano kwa wale walio kufuru, mke wa Mtume Nuh
na mke wa Mtume Lut
walikuwa chini ya waja wawili miongoni mwa waja wetu wema, basi wakafanya hiyana hivyo haikuwasaidia chochote mbele ya Allah (s.w.t) na ikasemwa ingieni motoni pamoja na wenye kuingia.” (At-Tahriim 66:10).
Tazama Hadith zifuatazo zinazoweka wazi baadhi ya maana ya Ayah zilizotangulia: Kutoka kwa ‘Ubaid bin Hunain kutoka kwa Ibn ‘Abbas amesema: “Nilikaa mwaka na mimi nataka kumwuliza ‘Umar juu ya wanawake wawili ambao wamemuasi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w
)
basi nikawa namwogopa siku moja aliteremka sehemu akaingia katika mti wa miiba alipotoka nikamwuliza, akasema:
‘Aisha na Hafsa, kisha akasema tulikuwa katika ujahili hatuwahesabu wanawake kuwa ni chochote, ulipokuja Uislamu na Allah (s.w.t) akawataja tukaona kuwa wana haki kwetu bila ya kuwaingiza kwa chochote katika mambo yetu na kulikuwa na maneno baina yangu na mke wangu akanikasirikia, nikamwambia: hakika wewe uko huko, akasema unaniambia mimi hayo ilihali binti yako anamwudhi Mtume wa Allah (s.a.w.w.)? Basi nikamwendea Hafsa nikamwambia na kumtahadharisha juu ya kumuasi Allah (s.w.t) na Mtume wake
.
Kutoka kwa ‘Aisha amesema: Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
alikuwa anakunywa asali kwa Zainab binti Jahshi na kukaa kwake nikaafikiana mimi na Hafsa yeyote kati yetu akiingia kwake basi amwambie, umekula maghaafiir hakika mimi nanusa kutoka kwako harufu ya maghafir, akasema hapana isipokua nilikuwa na kunywa asali kwa Zainab binti Jahshi basi sitokunywa, nimeapa na usimwambie hayo yeyote
.
Kutoka kwa ‘Aisha (r.a): hakika wake wa Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
walikuwa makundi mawili kundi ambalo yumo ‘Aisha, Hafswa, Swafiyyah na Sauda na kundi jingine yumo Umm Salamah na wake wengine wa Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
.
Kutoka kwa ‘Aisha (r.a) amesema: “nilikuwa nawaonea gherah wake ambao wametoa nafsi zao hiba kwa Mtume(s.a.w.w)
na nasema: ‘Mwanamke ametoa nafsi yake?’ Basi Allah (s.w.t) alipoteremsha Ayah isemayo (umuahirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze umtakae.
Na kama ukimtaka yule uliyemtenga basi si vibaya kwako) nikasema naona Mola wako anafanya haraka katika matamanio yako
. “
Kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Sikumwonea gherah mwanamke yeyote kama nilivyomfanyia gherah Khadija, na alikwishakufa kabla ya kunioa mimi kwa miaka mitatu, kwa yale niliyokuwa namsikia akimtaja na Mola wake alikwisha mwamuru ambashirie nyumba ya marumaru Jannat na alikuwa anachinja mbuzi kisha anatoa zawadi kwa marafiki zake
.
Kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Halah binti Khuwailid dada wa Khadija alitaka idhini kwa Mtume wa Allah
basi akajua kubisha hodi kwa Khadija akafanya haraka kwa hilo. Akasema (Mtume): “Ee Allah! Ni Halah huyo.” Akasema (‘Aisha): “Nikaona gherah na kusema: “Nini unamtaja kikongwe katika vikongwe wa Kiquraish mwekundu wa mashavu ameshakufa na Allah (s.w.t) amekubadilishia aliye bora kuliko yeye?”
Kutoka kwa Hisham kutoka kwa Baba yake kutoka kwa ‘Aisha amesema: “Sikufanya gherah kwa yeyote kati ya wake wa Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.) kama nilivyofanya gherah kwa Khadija na wala sikumwona, lakini Nabii alikuwa akimtaja kwa wingi na huenda alichinja mbuzi kisha anawagawa na kuwapelekea rafiki zake Khadija, na huenda nilimwambia: “Kana kwamba hapakuwa na mwanamke duniani isipokuwa Khadija.” Akasema: “Hakika alikuwa; na nimepata watoto kutoka kwake
.”
Amesema: “Nabii alisimama alihutubia akaashiria upande wa makazi ya ‘Aisha akasema: ‘Hapa kuna fitina mara tatu, ambapo utatokea upembe wa Shetani
.”
Hakika Hadith ya mwisho ya juu inaashiria fitina ambayo ameelekezewa ‘Aisha kwa kutoka kwake kuongoza jeshi ili kumpiga vita Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib
Khalifa wa Waislamu katika vita vya Jamal - rejea maelezo zaidi katika sehemu ya kwanza.
Na ambacho wanakitegemea wanaoitakidi uadilifu wa Masahaba wote ni madai yao kuwa Mtume wa Allah(s.a.w.w
)
amesema: “Masahaba wangu ni kama nyota yeyote mtakaye mfuata mtaongoka” na katika Hadith nyingine: “Kwa yeyote utakayechukua kauli yake...”.
Tukiachilia kuwa Hadith hii ni sahihi, na kwa kuchukulia Hadith zilizotangulia hiyo itamaanisha kuwa atakayemfuata aliyeondoka msikitini kwa ajili ya maslahi ya kidunia yenye kupita na Mtume(s.a.w.w
)
amesimama akihutubia, basi atakuwa ameongoka na kwamba atakayewafuata walioacha sehemu zao ambazo Mtume aliwaamuru wasiziache kwa ajili ya kuchukua baadhi ya ngawira atakuwa ameongoka!
Na kwamba anayemfuata anaye tuhumu uongozi aliouweka Mtume
kwa Usamah basi atakuwa ameongoka! Na kwamba anayemfuata anayepinga na kumuasi Nabii(s.a.w.w
)
atakuwa ameongoka!
Hakuna shaka kwamba katika hilo kuna mgongano unao kataliwa na tabia ya kibinadamu na fitra sahihi, tukiachilia mbali kwamba kuitakidi kwetu usahihi wa Hadith hiyo ina maana ya Uma’asum wa Masahaba vile vile, kwa sababu kauli yao hiyo ni dhamana ya amri kutoka kwa Mtume
kwa Waislamu kufuata Masahaba wote bila ya sharti au pingamizi kulingana na mafhum ya Hadith. Lakini haiwezekani Mtume kuamuru kufuatwa ambaye anaweza kufanya maasi, na kwa sababu hiyo Hadith hizo hazikubaliwi kwa yale yaliyo julikana na ni dhahiri kwamba sahaba sio ma’asum.
Hakika Hadith hizo zimezuliwa ili ziwe badala ya Hadith tukufu za Nabii
ambazo amezitoa Al-Hakim katika Mustadark As-Sahihain kwa Sanad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbas: “Amesema Mtume wa Allah
nyota ni tumaini kwa watu wa ardhini kutokana na kughariki na Ahlul-Bayt (a.s.) ni tumaini kwa ‘Ummah wangu kutokana na ikhtilafu, basi kama kabila (lolote) la Kiarabu litawakhalifu, watakhitalifiana na kuwa makundi ya Ibilisi
.”
Na miongoni mwa athari mbaya ambazo ni matokeo ya kuitakidi uadilifu wa Masahaba wote ni kupatikana idadi kubwa ya Hadith hizo potovu katika vitabu vya Hadith kama vile Israiliyyaat, Masihiyyaat *na nyinginezo katika upotovu ambazo ndiyo mianya ya tuhuma katika dini ya Kiislamu, hiyo ni kwa sababu Hadith zimechukuliwa na kuaminiwa kwa kuwa tu zimepokewa kutoka kwa Sahaba pamoja na kuwa kuna uwezekano wa kufanya ambayo tumeyabainisha katika Hadith zilizotangulia.