MAMBO YANAYO MUHUSU MAITI
NAMNA YA KUMWOSHA MAITI
Baada ya kusafishwa mwili wote wa yule maiti hapo (yule mwoshaji) atanuia kuwa, namwosha (huyu maiti) ghusli ya kwanza kwa maji yaliyochanganyishwa na majani ya mkunazi kama tulivyoeleza huko nyuma.
(a) Kwanza ataanzia kwa kummwagia maji kichwani (maji yafike hadi utosini kwenye ngozi) masikio, pua, mdomo, macho na shingo pia aoshe. Ahakikishe kilmara anapomwosha, maji yafike sehemu zote za mwili wake.
(b) Tena upande wa mbele wa kulia kutoka begani chini ya shingo na pote kulia hadi kwenye nyayo tena baadaye amlaze ubavu amwoshe sehemu ya nyuma kama alivyomwosha sehemu ya mbele ya kulia.
(c) Baadaye atamwosha upande wa mbele wa kushoto na baadaye upande wa nyuma kama alivyomwosha upande wa kulia.
(d) Utupu wa maiti lazima uoshwe anapokoshwa kila upande (maana yake kwa kila mwosho (ghusli) ataosha utupu mara mbili). Ni haramu kuangalia utupu wa maiti na mwoshaji akiangalia ametenda dhambi, lakini ile ghusli haibatiliki.
(e) Mwoshaji wakati anapoosha utupu wa maiti Iazima aviringe kitambaa au avae mfuko wa kitambaa mkononi, ni haramu kupeleka mkono upekee.
Hii ndio namna ya kumwosha maiti ambayo utaratib huo kwa kisheria unaitwa "ALGHUSL AT-TAR-TIBI" na inambidi kwa kila mwenye Janaba pia akitaka kuondo (kuoga) Janaba au mwanamke mwenye hedhi au nifasi au kuoga ghusli za sunna lazima waoge vivyo hivyo kama tulivyoeleza katika kitabu chetu cha Sala (mlango wa ukurasa wa 33).
Kwa kuoshwa ghusli tatu hizo, tena haina haja kumwogesha, ghusli ya janaba au hedhi au nifas ikiwa maiti alikuwa katika hali ile.
Ikiwa SIDRI (majani ya mkunazi) au KAA-FUR (Kafuri maiti) zote mbili au mojawapo haipatikani, basi maiti ataoshwa kwa maji haya ya kawaida kwa nia ya badala ya Sidri au Kafuri mradi lazima maiti aoshwe Ghusli tatu tu (mara tatu).
(a) Ikiwa maji hayapatikani au maiti ameungua au alikuwa na maradhi fulani na akitiwa maji nyama au ngozi itatoka, basi badala ya maji atafanyiwa Tayamamu mara tatu kwa Ghusli tatu.
(b) Tayamamu ni lazima ifanywe na yule hai, na kumpaka maiti, na kama inamkinika kutayamamu kwa mikono ya maiti pia ifanywe - (Namna ya Tayamamu angalia kitabu chetu cha 'Sala' ukurasa wa 44 Mlango wa 8).
Mambo Ya Faradhi Baada Ya Kuogeshwa Maiti Hadi Kuzikwa Kwake
Haifai wakati anapooshwa maiti kuweko moto au kiteso cha kufukiza wala wakati wa mazishi hadi mwisho.
AL-HUNUUT: Kupakwa maiti kafuri mahali maalum ni faradhi kwa Waislamu baada ya kumwosha na kupanguswa (afutwe vizuri kwa nguo kavu) maiti kabla ya kusaliwa na kuzikwa apakwe 'Kafuri' laini sehemu saba (viongo vya kusujudia) navyo ni kipaji, viganja viwili, magoti mawili, ncha za vidole gumba viwili. Na sunna kupakwa kwenye pua, vile vile sunna kuwekwa pamba kwenye utupu wa maiti na kila penye tundu. Wakati wa kupaka HUNUUT ni baada ya kuogeshwa na kupanguswa na kabla ya kuvikwa sanda au wakati wa kuvikwa sanda.
Ikiwa Kafuuri haikupatikana hatakumwoshea maiti, basi hapo faradhi ya HUNUUT inaondoka, na kama amekogeshwa na Kafuuri lakini haikuzidi kwa ajili ya HUNUUT basi si kitu.
AL-HUNUUT: Kupakwa maiti Kafuri ni faradhi kwa kila maiti mdogo, mkubwa mwanamke, mwanamume, huru au mtumwa isipokuwa maiti yule aliyekufa hali yuko katika Ihramu ni haramu kumpaka Kafuri. Kafuri lazima iwe mpya si kukuu yenye kupotea harufu yake, na pia lazima iwe laini iliosagwa.
Sanda Ya Maiti Iliyo Wajibu
Ni faradhi kuvishwa maiti mwanamume au mwanamke mkubwa au mdogo vipande vitabu vya nguo:
(1) Kanzu (2) Shuka (3) Shuka
(1) Kanzu: Bila kuishona, itobolewe sehemu ya shingo tu halafu kitumbukizwe kichwa. Kuanzia begani hadi nusu ya miguu kupita goti.
(2) Shuka: Kama anavyovaa mwanamume kutoka kitovuni
hadi magotini, na ni bora si wajibu kuanzia kifuani hadi chini ya magoti.
(3) Shuka: Kitambaa kikubwa cha kumfunika mwiIi wake wote mzima mbele na nyuma kwa urefu hata uweze kufunga pande zote mbili (upande wa kichwa na upande wa miguu) na kwa upana, ncha moja iweze kuja juu ya ncha va pili
SUNNA
Si wajibu bali ni sunna:
(a) Kuvishwa mwanamume kiIemba, mwanamke sidiria na ushungi
(b) Nguo nyeupe isiyokuwa na rangi yoyote
(c) Nguo iwe ya pamba
(d) Ni bora kama aliwahi kuhiji basi 'IHRAMU' itumiwe au nguo za kusalia ambazo akisali nazo.
SANDA: Kwa kiasi kilichofaradhi lazima gharama yake na gharama ya vitu vya kumwoshea maiti, maji, Sidri, Kafuri, ardhi pa kuzikiwa na gharama zake zote haya hutoka katika asili ya mali ya maiti kabIa ya kulipwa deni au kufuatwa wasia wake. Na yako mambo ya sunna katika sanda ikiwa ameusia sanda itolewe katika theluthi (1/3) ya mali yake, au ameusia theluthi ya mali atumiliwe yeye basi sanda itatolewa humo, na kama hakuusia theluthi (1/3) basi kiasi kilichowajibu kitatolewa katika asili mali.
Sanda ya mke juu ya mumewe hata ikiwa mke anayo mali ya kutosha, na vivyo hivyo yule mke aliyeachwa kwa mara ya kwanza au ya pili na bado yupo katika eda, mume lazima atoe sanda. Ikiwa mtu mwingine yoyote ametoa sanda ya yule maiti (mwanamke) basi faradhi humuondokea mume.
Ni sunna kwa kila mwislamu kutayarisha SANDA yake na kuiweka nyumbani, pia ni sunna kuiangalia hiyo sanda kila mara. Mtukufu ,Mtume(s.a.w.
w
)
amesema, "Mwenye kutayarisha sanda yake, huwa kila siku zipitazo kila huandikwa thawabu kila apoiangalia, na kwa kufanya hivyo hatahesabiwa miongoni mwa waliomsahau Mwenyezi Mungu.
Namna Ya Kumkafini (Kumvisha Sanda Maiti)
Baada ya kukatwa mapande hayo, kwanza utatandika ile shuka kubwa ya Namba 3: Na ndio ya kwanza, baadaye utatandika Kanzu Kanzu kwa kuikunjua upande mmoja, (na hii ni ya pili), baadaye utaliweka shuka kwa upana kwa kukunjua. Ukisha tandika yote hayo vipande vitatu vya vitambaa vilivyo wajibu, basi sasa atalazwa maiti juu ya mapande yote ya sanda.
Kwanza utamfunga shuka na kuondoa kile kitambaa ulichotumia wakati wa kumwoshea kuficha utupu wake.
Utaurejesha ule upande wa kanzu ulioukunjua kwa kupitisha kichwa cha maiti kwenye shingo.
Ikiwa umeshafanya mambo ya 'AL-HUNUUT' basi utaikunja hiyo shuka kubwa kwa kuiweka ncha moja juu ya pili, na kama bado hujampaka AL-HUNUUT na mambo yake basi fanya, ndipo umalize kumfunika.
Kumsalia Maiti
Sala Ya Maiti: Lazima iwe baada ya kuvishwa sanda na kutia HUNUUT (KUPAKA KAFURI kwenye VIUNGO VYA KUSUJUDIA). Kuanzia maiti mwenye umri wa miaka sita (6) huwa faradhi kusaliwa sala ya maiti.
Sala ya maiti haina Adhana wala Kukimu na pia hakuna rukuu wala sijda, lakini inakusimama tu, na ina Takbira tano tu (badala ya sala tano za faradhi za kila siku). Hakuna shuruti ya kuwa na wudhuu lakini ni sunna kuwa nao. Ni sunna pia wakati wakutoa kila Takbira, anyanyuwe mikono hadi masikioni mwake yule mwenye kuswali.
Namna Ya Kumsalia Maiti
Mwenye kumsalia lazima asimame nyuma ya jeneza (jeneza liwe mbele yake) asiwe mbali nae, aelekee Qibla, kichwa cha maiti kiwe upande wa kulia wa mwenye kumsalia, na miguu upande wa kushotona awe amesimama. Akiwa maiti mwanamume basi ni sunna kusimama kati-kati na akiwa maiti mwanamke, asimame sawa na kifua cha maiti. Huwezi kumsalia maiti asiyekuwa mbele yako ijapokuwa akiwa mjini humo.
Namna ya Kumsalia Maiti kwa Njia ndefu
(1) Baada ya kupata ruhusa kwa wafiwa ndipo kwanza atatia nia ya kumsalia huyo maiti aliyoko mbele yake. Nia ni moyoni tu, kutamka si lazima katika ibada zote za faradhi (isipokuwa katika mambo ya Hijani sunna kutamka).
(2) Baada ya Takbira ya kwanza atasema hivi:
ASH-HADU AN LAA ILAA-HA IL-LAL LAA-HU WAH-DAHU LAA SHA-RIY-KA LAH, WA ASH-HADU AN-NA MUHAM-MADAN AB-DUHU-WARA-SUU-LUH, AR-SALA-HU BIL-HAK-KI BASHIY-RAN WANA-ZIY-RAN BAY-NA YADA-YIS-SAA-AH.
(3) Baada ya Takbira pili atasema:
AL-LAA-HUMMA SAL-LI ALAA MUHAM-MADIN WA AALI MUHAM-MAD, WAR-HAM MUHAM-MADAN WA AALA MUHAM-MAD, KA-AFDHALI MAA SAL-LAY-TA, WABAA-RAK-TA, WATA-RAH-HAMTA, ALAA IB-RAA-HIMA, WA AALI IB-RAA-HIM- IN-NAKA-HAMIY DUN MAJIYD, WA SAL-LI ALAA JAMIY-IL AN-BIYAA-I WAL MUR-SALIYN".
(4) Baada ya Takbira ya tatu atasema:
"AL-LAA-HUM-MAGH-FIR LIL MU'U-MINIY-NA WAL MU'U-MINAAT WAL MUS-LIMINA WAL MUS-LIMAAT, AL-AHYAA-I, MIN-HUM WAL-AMWAATI, TAA- BIU,BAY-NANAA- WA BAY -NAHUM BIL-KHAY-RAATI, IN-NAKA MUJIY-BUD DA'AWAAT IN-NAKA ALAA KUL-LI SHAY-IN-QA-DEER".
(5) Baada ya Takbira ya nne atasema hivi:
AL-LAA-HUM-MA IN-NA HAA-DHAA, AB-DUKA WAB-NU AB-DIKA,WAB-NU AMA-TIKA, NAZALA BIKA WA-ANTA, KHAY -RU MAN-ZUU-LIN BIH, AL-LAA-HUM-MA, IN-NAA, LAA, NA'ALAMU MIN-HU, IL-LAA KHAY-RAA, WA AN-TA, A'ALAMU, BI-HI MIN-NAA, ALLAA-HUM-MA IN- KAA-NA, MUH-SINAN, FAZID FlY IH-SAA-NIH, WA-IN -KAA-NA, MUSIY-AN, FATA-JAA-WAZ AN-HU-WAGH-FlR LAH, AL-LAA-HUM-MA, AJ-ALHU IN-DAKA FIY, A' ALAA IL-YEEN, WAKH-LUF ALAA AH-LIHI, FIL GHAA-BIRIYN, WARHAM-HU, BIRAH-MATIKA YAA AR-HAMAR-RAA-HIMIYN.
Akiwa Maiti ni Mwanamke baada ya Takbira ya nne atasema hivi :
AL-LAA-HUM-MA IN-NA HAA-DHIHI, AMATUKA WAB-NATU AB-DIKA,WAB-NATU AMA-TIKA, NAZALAT BIKA WA-ANTA, KHAY -RU MAN-ZUU-LIN BIH, AL-LAA-HUM-MA, IN-NAA, LAA, NA'ALAMU MIN-HA, IL-LAA KHAY-RAA, WA AN-TA, A'ALAMU, BI-HA MIN-NAA, ALLAA-HUM-MA IN- KAA-NAT, MUH-SINATA, FAZID FlY IH-SAA-NIHA, WA-IN -KAA-NAT, MUSIY-ATAN, FATA-JAA-WAZ AN-HA WAGH-FlR LAHA, AL-LAA-HUM-MA, AJ-ALHA IN-DAKA FIY, A' ALAA IL-YEEN, WAKH-LUF ALAA AH-LIHA, FIL GHAA-BIRIYN, WARHAM-HA, BIRAH-MATIKA YAA AR-HAMAR-RAA-HIMIYN.
(6) Utatoa Takbira ya tano ni kama salamu ya hiyo Sala.
Pia kuna njia fupi ya kumsalia Maiti huyo, nayo ni na ifuatayo:
(1) Baada ya Takbira ya kwanza atasema "ASH-HADU LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH WA ASH-HADU ANA-MUHAM-MADAR RASUU-LUL-LAAH."
(2) Baada ya Takbira ya pili atasema: AL-LAA-HUMA SAL-LI ALAA-MUHAMMADIN WA AA-LI MUHAMMAD.
(3) Baada ya Takbira ya tatu:
AL-LAA-HUM-MAGH- FIR LIL MU'U-MINIY-NA WAL MU' MINAA-TI.
(4) Baada ya Takbira ya nne atasema hivi:
AL-LAA-HUM-MAGH-FIR LI-HAA-DHAL, MAY-YIT
(5) Akiwa maiti ni mwanamke baada Takbira ya nne sema hivi:
AL-LAA-HUM-MAGH-FIR LI HAA DHIHIL, MAY-YIT.
(6) Utatoa Takbira ya tano ni kama salamu ya hiyo na, hakuna faradhi ya kusoma kitu baada ya hiyo Takbira tano, ni sunna kusema, "RAB-BANAA AATINAA, FIDUN-YAA, HASA-NA- TAN, WAFIL AA-KHIRATI; HASANATAN, WA QINAA ADHAA-BAN NAAR."
Ukisali namna hiyo pia yatosha.
Ikiwa baada ya kusaliwa maiti, ikajulikana kwamba maiti alipinduka kifudifudi, basi lazima awekwe chali na asaliwe tena. Na kama kwa kusahaulika maiti hakusaliwa hadi akazikwa ni wajibu asaliwe juu ya kaburi, na vivyo hivyo ikiwa baada ya kuzikwa ikajulikana kuwa sala aliyosaliwa si sahihi.