UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA

UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA0%

UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA Mwandishi:
: Sheikh Haruna Pingili
Kundi: Akida

UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: Sheikh Haruna Pingili
Kundi:

Matembeleo: 7259
Pakua: 2440

Maelezo zaidi:

UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 4 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 7259 / Pakua: 2440
Kiwango Kiwango Kiwango
UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA

UDHUU KWA MTAZAMO WA QURANI NA SUNNA

Mwandishi:
Swahili

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA

MWANDHISHI: SHEIKH JA'FAR AL-SUBHANI

MTARJUMU: SHEIKH HARUN PINGILI

Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: kilichoandikwa na Sheikh Ja'far al-Subhani. Sisi tumekiita: "Udhuu kwa mtazamo wa Qur'ani na Sunnah"

Kitabu hiki kinahusu Udhuu. Udhuu ni tendo la kunawa (kutawadha) kisheria kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Swala. Swala ni nguzo kubwa ya dini haikamiliki mpaka mtu awe na Udhuu: "Enyi! ambao mmeamini mnapokusudia kuswali osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye viwiko, na pakeni sehemu za vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyu mbili…"(al-Maidah; 5: 6).

Aya hii ni mojawapo ya Aya za hukumu ambazo humo huchukuliwa hukumu za kisharia kiutekelezaji inayorejea kwenye kunadhimu matendo ya wanaopasa kutenda katika ambayo yanaambatana na shughuli za maisha yao ya kidini na ya kidunia.

Bahati mbaya kuna tofauti ya jinsi ya kutawadha kati ya Shi'a na Sunni kiasi kwamba kila mmoja anamshangaa mwenzake, hususani mwiongoni mwa wafuasi. Wengi wa wanachoni wa Kisunni wamejuzisha kukosha miguu, ambapo wanachuoni wa Kishi'a wamejuzisha kupaka miguu.

Imekuwa in kawaida ya watu kukubali kila jambo linalofanywa na watu katika jamii wanayo ishi bila ya kuhoji ubaya au uzuri wa jambo hilo. laki- ni hii yote ni kwa sababu ya kutojuana na kutotaka kujuana.

Mwandishi wa kitabu hiki ameshughulikia suala hili kwa kutumia Qur'ani na Sunnah, vyanzo viwili ambavyo ndio chimbuko la sheria na hukumu zote za dini kwa madhehebu zote za Kiislamu, na akahitimisha kwa mujibu wa vyanzo hivyo viwili.

Kwa ajili hii tumeona tukitoe kwa lugha ya Kiswahili kwa wasomaji wetu wa Kiswahili ili wapate kunufaika na maudhui hii. Tunataraji kwamba wote watanufaika na somo hili na kutekeleza ibada zao kwa mujibu wa sheria.

Tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Harun Pingili kwa kubali jukumu hili la kutarjum kitabu hiki. Halikadhalika tunawashukuru wale wote walioshiri- ki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji:

Al-Itrah Foundation

S. L. P. 19701

Dar-es-Salaam, Tanzania.