1
JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA
SEHEMU YA PILI
SABABU ZINAZOPELEKEA USTAWI WA VIJANA
1- MAARIFA
KUJIELIMISHA
Mwenyezi Mungu amesema: "Sema: Je wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.
" (Surat Zumar: 9).
Amesema tena: "Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu, na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda.
" (Surat Mujadalah: 11).
Akasema tena: "Wala usifuate usiyo na elimu nayo, hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa
." (Surat Al-Israi: 36).
Imam Ali
amesema: "Hakuna harakati yoyote ila unahitajika uwe na maarifa nayo
."
Imam Ali
amesema: "Enyi kundi la vijana! Jengeni ngome ya heshi- ma yenu kwa adabu, na dini yenu kwa elimu.
"
Imam Ali
amesema: "Mambo ya kwanza wanayopasa vijana kujifun- za ni yale ambayo pindi watakapokuwa watu wazima watayahitajia.
"
Imam Ali
amesema: "Msiwalazimishe wanenu juu ya adabu zenu, kwani hakika wao wameumbwa kwa ajili ya zama zisizokuwa zama zenu
."
KUJITAMBUA
Mwenyezi Mungu amesema: "Na hakika tumewatukuza wanadamu na tumewabeba nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku katika vitu vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi wa wale tuliowaumba, kwa utukufu mkubwa
." (Surat Al-Israi: 70).
Imam Ali (a.s) amesema: "Hekima bora kabisa ni mwanadamu kuitambua nafsi yake.
"
Imam Ali
amesema: "Atakayeitambua nafsi yake bila shaka amefikia kilele cha kila maarifa na elimu.
"
Imam Ali
amesema: "Ujinga mkubwa ni mwanadamu kutojitambua yeye mwenyewe
."
Imam Ali
amesema: "Asiyeitambua nafsi yake basi kajitenga mbali na njia ya uokovu, na kaangukia ndani ya upotovu na ujahili.
"
Imam Ali
amesema: "Namshangaa mtu anayetambulisha na kuk- itafuta alichokipoteza, ilihali keshaipoteza nafsi yake na wala haitafuti
."
Imam Ali
amesema: "Anayeitambua nafsi yake huipiga vita, na asiyeitambua huipuuza.
"
Imam Ali
amesema: "Atakayeitambua thamani ya nafsi yake hatoid- harau kwa vitu vya kupita (vya kutoweka).
"
Imam Ali (a.s.) amesema: "Atakayeitambua nafsi yake atamtambua Mola wake Mlezi.
"
Imam Ali
amesema: "Namshangaa asiyeijua nafsi yake vipi atam- tambua Mola wake Mlezi.
"
Imam Ali
amesema: "Mwanadamu ameumbwa akiwa na nafsi itamkayo, akiitakasa kwa elimu na vitendo basi hufanana na johari za mwanzo wa kiini chake
"
Abdalluh bin Sinan alimuuliza Imam Jafar As-Sadiq
: "Je kati ya Malaika na mwanadamu n i nani bora?" Akasema: Jemedari wa waumini Ali bin Abu Talib amesema: 'Hakika Mwenyezi Mungu alimwekea Malaika akili bila matamanio, na akamwekea mnyama matamanio bila akili, na akamwekea mwanadamu vyote viwili, hivyo yule ambaye akili zake zitayashinda matamanio yake yeye ni bora kuliko Malaika. Na yule ambaye matamanio yake yataishinda akili zake yeye ni duni kuliko mnya- ma." [73]
KUIJUA QUR'ANI TUKUFU
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
amesema: "Atakayejifunza Qur'ani ujanani mwake basi itajichanganya na nyama yake na damu yake.
"
Imam Ali
amesema ndani ya barua yake kwa mwanae Hasan
: "Na nikakuanza kwa kukufunza kitabu cha Mwenyezi Mungu na taawili yake, sheria za Uislamu na kanuni zake.
"
Imam Jafar As-Sadiq
amesema: "Atakayesoma Qur'ani angali kijana muumini basi Qur'ani itajichanganya na nyama yake na damu yake, na Mwenyezi Mungu atamweka pamoja na waandishi watukufu wachamungu, na Qur'ani itakuwa kinga yake siku ya Kiyama.
"
KUJIFUNZA DINI
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
amesema: "Kila kitu kina nguzo, na nguzo ya dini hii ni elimu ya sharia (Fiqhi)
."
Imam Al-Baqir na As-Sadiq
wamesema: "Lau kama nikiletewa kijana yeyote miongoni mwa vijana wa Kishi'a asiyejifunza sharia basi nitamwadabisha.
"
Imam Al-Baqir
alikuwa akisema: "Jifunzeni sharia, la sivyo ninyi ni mabedui.
"
Imam Al-Baqir
amesema: "Lau kama nikiletewa kijana miongoni mwa vijana wa Kishi'a hajifunzi sharia ya dini basi nitamtia machungu.
"
Imam As-Sadiq
amesema: "Lau kama nikiletewa kijana miongoni mwa vijana wa Kishi'a hajifunzi sharia basi nitairekebisha adabu yake.
"
Imam As-Sadiq
amesema: "Harakisheni kuwafunza vijana wenu Hadith kabla Murjia hawajawatangulia kwao.
"
Imam As-Sadiq
amesema: "Sipendi kumwona kijana miongoni mwenu ila akiwa amezama katika hali mbili: Ima msomi au mwenye kujie- limisha, na kama hatofanya hivyo basi kavuka mipaka, na akivuka mipaka kapoteza, na akipoteza katenda dhambi, na akitenda dhambi kaishi motoni. Naapa kwa yule aliyempa unabii Muhammad (s.a.w.w) kwa haki.
"
Kutambua kwamba elimu na imani ni mapacha: Mwenyezi Mungu amesema: "Mwenyezi Mungu na Malaika na wenye elimu, wameshuhudia kuwa hakuna aabudiwaye ila Yeye tu, ni Mwenye kusimamia uadilifu. Hakuna aabudiwaye isipokuwa Yeye tu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
" (Surat Imraan: 18).
Akasema tena: "Na waliopewa elimu wanafahamu ya kuwa yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako ndiyo haki, nayo huongoza kwenye njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.
" (Surat Sabai: 6). Akasema: "Na ili wajue wale waliopewa elimu ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wako na waiamini, na zinyenyekee Kwake nyoyo zao. Na kwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye awaongozaye wale walioamini kwenye njia iliyonyooka.
" (Surat Al-Hajji: 54).
Imam Ali
amesema: "Asili ya imani ni elimu.
"
Imam Ali
amesema: "Imani na elimu ni mapacha na marafaki wawili wasiotengana.
"
Imam Ali
amesema: "Matunda ya elimu ni kumtambua Mwenyezi Mungu.
"
Imam Kadhim
alimwambia Hisham bin Al-Hakam: "Ewe Hisham! Mwenyezi Mungu hakupeleka mitume Wake na Manabii Wake kwa waja Wake ila ni ili wawaelimishe kuhusu Mwenyezi Mungu, hivyo wenye kuwakubali vizuri ni wale wenye maarifa mazuri
."
UMUHIMU WA UDADISI
Mwenyezi Mungu anasema: "Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.
" (Surat Annahli: 43).
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
amesema: "Elimu ni hazina na ufunguo wake ni udadisi, basi ulizeni Mwenyezi Mungu atawarehemu. Kwa hakika hulipwa watu wa namna nne: Muulizaji, mzungumzaji, msikilizaji na mwenye kuwapenda.
"
Imam Ali
amesema: "Atakayeuliza udogoni mwake atajibu ukubwani mwake
."
Imam As-Sadiq
amesema alipoulizwa na Humran bin Aayan: "Hakika watu huangamia kwa kuwa hawaulizi
."
Imepokewa kutoka kwa Imam As-Sadiq
kuwa: "Mtume(s.a.w.w)
aliambiwa kuwa kuna mtu alipatwa na janaba akiwa na jeraha, akaamrishwa kuoga ndipo akakaukia na hatimaye akafariki." Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
akasema: "Wallahi wamemuuwa, Mwenyezi Mungu awauwe. Hakika dawa ya kushindwa ilikuwa ni kuuliza
."
Imepokewa ndani ya kitabu Musnad Ahmad bin Hanbal kutoka kwa Abu Umamah amesema: "Kuna kijana alimjia Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
na kumwambia: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Naomba unipe idhini ya kuzini.' Hapo watu wakamvamia na kumfokea na kumwambia: 'Nyamaza, nyamaza.' Mtume akasema: 'Msogezeni.' Basi akasogezwa karibu yake kisha akaketi. Mtume akamwambia: 'Unalipenda hilo kwa mama yako?' Kijana akasema: 'La wallahi, Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako!' Akasema: 'Na watu hawalipendi kwa mama zao.' Akasema: "Unalipenda hilo kwa binti yako?' Kijana akasema: "La wallahi, Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.'
Akasema: 'Na watu hawalipendi kwa mabinti zao.' Akasema: 'Unalipenda hilo kwa shangazi yako?' Kijana akasema: 'La wallahi, Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako!' Akasema: 'Na watu hawalipendi kwa shangazi zao.' Akasema: 'Unalipenda hilo kwa mama zako wadogo?' Kijana akasema: 'La wallahi, Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako!' Akasema: "Na watu hawalipendi kwa mama zao wadogo.' Mtume akaweka mkono juu ya bega lake na kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu! Msamehe dhambi yake, safisha moyo wake, na uhifadhi utupu wake." Basi baada ya hapo kijana hakuwa tena akifikiria hilo."
2 - AZMA
Imam Ali
amesema: "Lakini Mwenyezi Mungu amewapa Mitume Wake nguvu katika azma zao, na udhaifu katika kile kinachoonwa na macho yao katika hali zao
."
Imam Ali
amesema: "Pambaneni na ulegevu kwa azma
."
Imam Ali
amesema: "Azma na walima havikai pamoja, hakuna kiondoacho usingizi kama azma za siku, na kifutacho giza kama kukumbuka hima
."
Imam Al-Kadhim
amesema katika moja ya dua zake za mwezi wa Rajab: "Na nimejua kuwa matumizi bora ya msafiri ajaye Kwako ni azma ya utashi unaokuchagua Wewe
."
KUJITUMA
Mwenyezi Mungu asema: "Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya. Na kwamba amali yake itaonekana
." (Surat Najmu: 39 - 40).
Na akasema tena: "Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu, lazima tutawaongoza kwenye njia zetu.
" (Surat Ankabut: 69).
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
amesema: "Atakayedumu kugonga mlango ataingia
."
Imam Ali
amesema: "Atakayedumu kugonga mlango na kukazana ataingia
."
Imam Ali
amesema: "Atakayetoa juhudi za nguvu zake atafikia asili ya muradi wake."
Imam Ali
amesema: "Atakayekitafuta kitu kwa juhudi atakipata chote au sehemu yake.
"
Imam Ali
amesema: "Kamwe haiwezekani kupata ufanisi kwa kujib- wetesha na urahisi.
"
Imam Ali
amesema: "Ukikumbana na jambo liingie, kwani hakika ugumu wa kujiepusha nalo ni mkubwa kuliko yale unayokhofia toka humo.
"
Imam Ali
amesema: "Ukiogopa ugumu wa jambo basi jitume kwalo litakuwa jepesi kwako. Na udanganye wakati kuhusu matukio yake basi yatakuwa mapesi kwako
."
Imam Ali
amesema: "Zamani nilikuwa na ndugu katika dini ya Mwenyezi Mungu.alikuwa dhaifu aliyedhoofishwa, lakini juhudi zinapokuja huwa simba dume na nyoka swila
."
MALENGO YA JUU
Imam Ali
amesema: "Ambaye malengo yake yatakuwa ya juu basi thamani yake itaongezeka
."
Imam Ali
amesema: "Kuwa mwenye malengo ya mbali pindi utafutapo
."
Imam Ali
amesema: "Atakayelikeshesha jicho la fikira zake basi atafikia asili ya lengo lake
."
Imam Ali
amesema: "Hakuna kitu kimwinuacho mtu kama lengo lake, na hakuna kimbwagacho kama matamanio yake
."
Imam Ali (a.s) amesema: "Apandaye daraja za malengo basi mataifa humkweza
."
Imam As-Sadiq
amesema: "Matatu humzuia mtu kutafuta yaliyo juu: Ufupi wa lengo, uchache wa mbinu na udhaifu wa mawazo
."
KUJIHESHIMU
Imam Ali
amesema: "Ijengee nafsi yako heshima kwa kujiepusha na mambo duni, hata kama yatakusukuma kwenye raghba, kwani hakuna sehemu yoyote ya dini yako na heshima yako uitowayo yenye mbadala wa thamani, hata iwaje
."
Imam Ali
amesema: "Ijengee nafsi yako heshima kwa kujiepusha na mambo duni, hata kama yatakusukuma kwenye raghba, kwani hakuna sehemu yoyote ya nafsi yako uitowayo yenye mbadala wa heshima
."
Imam Ali
amesema: "Bora kifo kuliko udhalili, bora ufakiri kuliko ombaomba
."
Imam Ali
amesema: "Bora ufakiri kuliko udhalili
."
Imam As-Sadiq
amesema: "Atakaye heshima bila jamaa, utajiri bila mali na haiba bila utawala, basi atoke kwenye udhalili wa kumwasi Mwenyezi Mungu mpaka kwenye heshima ya kumtii
."
Kujitosheleza: Imepokewa ndani ya kitabu Al-Khiswal kutoka kwa Sahlu bin Saad amesema: "Jibril alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na kumwambia: 'Jua hakika sharafu ya mtu ni kusimama usiku, na heshima yake ni kutokuwahitajia watu
."
Imam Ali
amesema: "Atakayejua thamani ya nafsi yake basi vitu vya kupita havitomdhalilisha
."
Imam Ali
amesema: "Utajiri mkubwa ni kutojali yaliyomo mikononi mwa watu..
"
Imam Ali
amesema: "Udhalili ni kuwaomba watu
."
Imam Zaynul-Abidina
amesema: "Kheri yote nimeiona imekusanyi- ka kwenye kuacha za tamaa dhidi ya yale yaliyomo mikononi mwa watu
."
MSIMAMO
Imam Ali
amesema: "Atakayeshikamana na msimamo basi usalama utashikamana naye
."
Imam Ali
amesema: "Jueni kuwa Mwenyezi Mungu huwachukia waja wake wasio na msimamo, hivyo msiteleze nje ya haki na wilaya ya Ahlul-Baiti, kwani kwa hakika atakaeleta mbadala dhidi yetu basi kaangamia
."
Imam Ali
amesema: "Shikamana na mfumo wa msimamo, kwani wenyewe utakuletea heshima na kukulinda dhidi ya lawama
."
KUMTAWAKALI MWENYEZI MUNGU
Mwenyezi Mungu amesema: "Utakapoazimia basi mtegemee Mwenyezi Mungu
" (Surat Ali Imran: 159).
Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
amesema: "Atakayemtawakali Mwenyezi Mungu basi atamtosheleza matumizi yake na kumruzuku kwa namna asiyotarajia
."
Imam Ali
amesema: "Yeye ndiye Ambaye atakayemtawakali hum- tosheleza na atakaemuomba humpa
."
Imam Jawad
amesema: "Kumtegemea Mwenyezi Mungu ni thamani ya kila ghali na ngazi ya kuelekea heshima ya juu
."
Imepokewa ndani ya kitabu Kanzul Fawaid kuwa: "Miongoni mwa hekima na usia wa Luqman (a.s) kwa mwanae ni: 'Ewe mwanangu mpendwa! Mtegemee Mwenyezi Mungu, kisha waulize watu: Je, kuna yeyote kamtegemea Mwenyezi Mungu kisha hajamwokoa?! Ewe mwanangu mpendwa! Mtawakali Mwenyezi Mungu, kisha waulize watu: Ni nani aliyemtawakali Mwenyezi Mungu kisha hajamtosheleza?
!"