JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA0%

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA Mwandishi:
: HEMEDI LUBUMBA SELEMANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

Mwandishi: Muhammad Reyshahri
: HEMEDI LUBUMBA SELEMANI
Kundi:

Matembeleo: 15355
Pakua: 3585

Maelezo zaidi:

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 15355 / Pakua: 3585
Kiwango Kiwango Kiwango
JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

Mwandishi:
Swahili

3

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

UDONDOZI KUTOKA KITABU: JAWAAHIRU AL-HIKMAH LI 'SH-SHABAAB

3 - HIJABU

Mwenyezi Mungu asema: "Ewe Nabii, waambie wake zako, na mabinti zako na wake wa wau- mini: Wateremshe juu yao shungi zao. Hivyo inaelekea zaidi waju- likane na wasiudhiwe, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu ." (Surat Ahzab: 59).

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Kijana mmoja wa kianswari alimgeukia mwanamke huko Madina na wanawake walikuwa wamevaa skafu zao nyuma ya masikio yao, basi akamtazama ilihali mwanamke yule akiwa mkabala naye, alipovuka mwanamke yule basi kijana akaingia mtaa uliokuwa ukiitwa Bani Fulani, akawa akimtazama kwa nyuma na hatimaye akaugonga uso wake kwenye ukuta na uso wake ukapasuka. Mwanamke alipotoweka akajitazama na kukuta damu zikishururuzika juu ya kifua chake na nguo yake, akasema: Wallahi ni lazima nimwendee Mtume wa Mwenyezi Mungu nikampe habari hii, basi akamwendea. Mtume wa Mwenyezi Mungu alipomuona akamwambia umefanya nini? Ndipo akampa habari ilivyokuwa, na ndipo Jibril akatelemka na Aya hii: "Waambie waumini wanaume wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao, bila shaka Mwenyezi Mungu anazo habari za yale wanayoyafanya ." (Surat Nur: 30)."[284]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mwenyezi Mungu amewalaani wanaume wenye kujishabihisha na wanawake. Na Mwenyezi Mungu amewalaani wanawake wenye kujishabihisha na wanaume ." [285]

Imam Ali(a.s) amesema: "Nilikuwa nimeketi pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu huko Baqii siku yenye mvua na upepo, basi ghafla mwanamke akapita na punda na ghafla mkono wa punda ukaingia ndani ya shimo na hatimaye mwanamke akaanguka, basi Mtume akageuza uso. Wakamwambia: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika yeye amevaa suruwali.' Akasema: 'Ewe Mwenyezi Mungu wasamehe wanawake wenye kuvaa suruwali (Mara tatu). Enyi watu tengenezeni suruwali hakika zenyewe ni miongoni mwa nguo zenu zenye sitara mno, na wahifadhini wake zenu kwazo pindi watokapo ."[286]

Imam Ali(a.s) amesema: "Zama za mwisho, na karibu na Kiyama kutadhihiri wanawake wenye kujiacha wazi uchi, wenye kujitoa katika dini, wenye kuingia katika fitina, wenye kuelemea kwenye matamanio, wenye kuharakishia starehe, wenye kuhalalisha haramu basi hao watadumu motoni ."[287]

NDOA

A: MKAZO WA KUOA UJANANI

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Hakuna kijana anayeoa ujanani ila ni lazima shetani wake alie: 'Ole wangu, ole wangu! Amenizuilia theluthi ya dini yake.' Basi mja amche Mwenyezi Mungu kwenye theluthi mbili zilizobaki ." [288]

Imam Ali(a.s) amesema: "Enyi kundi la vijana! Ni juu yenu kuoa, na kama hamuwezi basi ni juu yenu kufunga, kwani kwenyewe ni kinga ."[289]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ewe kijana oa na jiepushe na zinaa, kwani yenyewe huondoa imani moyoni mwako ."[290]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Kijana wa kianswari alimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumlalamikia haja yake, basi akamshauri aowe. Kijana akasema: 'Mimi naona haya kurudi tena kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Basi akakutana na mtu kati ya maasnwari, akamwambia: 'Mimi nina binti mzuri, na hatimaye akamuoza. Basi Mwenyezi Mungu akam- panulia riziki, na kijana akamwendea Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumpa habari. Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: 'Enyi kundi la vijana! Ni juu yenu kuoa ."[291]

B: MUME MARIDHAWA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakapowajieni mnayemridhia dini yake na tabia yake basi muozesheni na kama hamtofanya hivyo basi itakuwa ni uharibifu na ufisadi mkubwa aridhini ." [292]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Nilimuoza Mikdad na Zayd ili iwe mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mwenye tabia njema kati yenu ." [293]

Alipoulizwa Imam Al-Baqir(a.s) kuhusu ndoa, alisema: "Atakayeleta posa kwenu na mkaridhia dini yake na uaminifu wake basi muozeni, na kama hamtofanya basi itakuwa ni uharibifu na ufisadi mkubwa aridhini ."[294]

Alikuja mtu mmoja kwa Husein(a.s) akimtaka ushauri juu ya kumuoza binti yake. Akasema: "Muoze kwa mwanamume mchamungu, kwani hakika yeye kama atampenda basi atamkirimu, na kama atamchukia basi hatomdhulumu. "[295]

C: MKE MARIDHAWA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Oeni mabinti vijana kwani hakika wao ndio wenye tabia njema. " [296]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mwanamke huolewa kwa sifa nne: Kwa mali yake, dini yake, uzuri wake na kwa nasaba yake na familia yake, basi ni juu yako kwa mwenye dini ." [297]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakayemuoa mwanamke kwa ajili ya uzuri wake basi hatopata kwake anachokipenda. Na atakaemuoa kwa ajili ya mali basi Mwenyezi Mungu atamtegemeza kwake. Basi ni juu yenu kwa mwenye dini ." [298]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakayemuoa mwanamke kwa mali ya halali lakini akataka fahari na kujionyesha basi Mwenyzei Mungu hatomzidishia chochote ila udhalili na fedheha. " [299]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Oeni kwenye matum- bo mema, kwani hakika damu hurithisha. " [300]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Zichagulieni mbegu zenu sehemu yenye kheri, kwani hakika wanawake huzaa shabihi wa ndugu zao wa kiume na ndugu zao wa kike ." [301]

D: KUOA AKRABA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Tafuteni wageni na wala msisababishe kuzaa wembamba ." [302]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msioe akraba (ndugu wa karibu), kwani hakika mtoto huumbwa mwembamba." [303]

HAYA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Katika methali za Manabii haijabaki ila kauli ya watu: Ukiwa hauna haya basi fanya utakalo ." [304]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Kuwa na haya ndio kheri yote ." [305]

Imam Ali(a.s) amesema: "Haya ni sababu ya kuelekea kwenye kila jamali. "[306]

Imam Ali(a.s) amesema: "Haya ni tabia njema. "[307]

Imam Ali(a.s) amesema: "Haya ni ufunguo wa kila kheri ."[308]

Imam Ali(a.s) amesema: "Haya huzuia kutenda tendo baya ."[309]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Haya ina sehemu kumi: Tisa kwa wanawake na moja kwa wanaume. "[310]

HAYA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Haya ina namna mbili: Haya ya akili na haya ya ubaradhuli. Haya ya akili ni elimu na haya ya ubaradhuli ni ujinga ." [311]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mambo matatu hayaonewi haya: Mtu kumhudumia mgeni wake. Kumsimamia baba yake na mwalimu wake toka alipokaa. Na kuitafuta haki hata kama ni ndogo ."[312]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayeona haya kusema haki basi huyo ni baradhuli ."[313]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Haya zina wajihi mbili: Moja ni udhaifu na nyingine ni uimara nayo ndio Uislamu na imani ."[314]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mwenye haya elimu yake ina manu- faa ."[315]

UNYENYEKEVU

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Aliye bora kati ya vijana wenu ni mwenye kujipamba kwa pambo la vikongwe wenu. Na aliye mbaya kati ya vikongwe wenu ni yule mwenye kujipamba kwa pambo la vijana wenu ." [316]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mwenyezi Mungu anampenda mtoto wa miaka ishirini anaposhabihiana na mtu wa miaka the- manini. Na anamchukia mtu wa miaka sitini anaposhabihiana na mtoto wa miaka ishirini ." [317]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mwenyezi Mungu huvutiwa na kijana asiyekuwa na kiburi . " [318]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Aliye bora kati ya vijana wenu ni mwenye kujishabihisha na vikongwe wenu. Na aliye mbaya kati ya vikongwe wenu ni yule mwenye kujishabihisha na vijana wenu ."[319]

MTAZAMO WA MBALI

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mtu mmoja alimjia Mtume(s.a.w.w) na kumwambia: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niusie.' Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia:'Je utafuata usia iwapo mimi nitakuusia?' akamuuliza hivyo mara tatu naye akijibu ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia:'Hakika mimi nakuusia utakapoazimia jambo chunguza matokeo yake, ikiwa kuna mafanikio basi litekeleze na kama kuna kufeli basi liache ." [320]

Imam Ali(a.s) amesema: "Kufikiri kabla ya kutenda kunakusalimisha na majuto ."[321]

Imam Ali(a.s) amesema: "Fikiri kabla ya kutenda ili usiaibike kwa uliyotenda ."[322]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenye akili sana kati ya watu ni yule mwenye kuchunguza sana matokeo ya baadaye ."[323]

Imam Hasan(a.s) alipoulizwa kuwa ufanisi ni nini? Alisema: "Ni kusubiria fursa yako na kuharakisha yale uwezayo ."[324]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Simama kwenye kila jambo mpaka utakapojua mwanzo wake na mwisho wake, kabla hujaliingia ukaja kujuta ."[325]

Kuwataka ushauri wenye rai: Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu aliambiwa: Ufanisi ni nini? Akasema: 'Ni kuwataka ushauri wenye rai na kuwafuata ."[326]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hakuna ushindi imara kama kuomba ushau- ri ."[327]

Imam Al-Kadhim(a.s) amesema: "Atakayeomba ushauri hatokosa kusifiwa iwapo atapatia, na hatokosa udhuru iwapo atakosea ."[328]

UHURU

Imam Ali(a.s) amesema: "Usiwe mtumwa wa mwenzako ilihali bila shaka Mwenyezi Mungu amekufanya huru ."[329]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayejiepusha na matamanio basi atakuwa huru ."[330]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hakika kuwa na haya na utawa ni miongoni mwa maumbile ya imani, nazo ni tabia za mtu huru na pambo la watu wema ."[331]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Sifa tano asiyekuwa nayo moja basi si mwenye kustarehe sana: Ya kwanza: ni utekelezaji wa ahadi. Pili: ni kupanga mipango. Tatu ni haya. Nne ni tabia njema. Tano ni uhuru, nayo ndiyo yenye kukusanya sifa zote hizi ."[332]

KUKUBALI UDHURU

Imam Ali(a.s) amesema: "Kubali msamaha wa ndugu yako, kama hana udhuru basi muombee udhuru ."[333]

Imam Ali(a.s) alipokuwa akimuusia mwanae Muhammad bin Al- Hanafiyah alisema: "Usimlazimishe ndugu yako kwa kufuata shaka, na wala usijitenge naye bila kumuomba akuelezee, kwani huenda ana udhuru nawe wamlaumu bure ."[334]

Imam Al-Kadhim(a.s) amesema: "Baba yangu alinishika mkono kisha akasema: 'Ewe mwanangu mpendwa! Hakika baba yangu Muhammad bin Ali alinishika mkono kama nilivyokushika na akaniambia: Hakika baba yangu mpendwa Ali bin Husain(a.s) alinishika mkono kama nilivyokushika na akaniambia:Ewe mwanangu mpendwa! Mfanyie kheri kila aliyeitafuta kutoka kwako, ikiwa ni anayestahiki basi utakuwa umepatia sehemu yake, na ikiwa si anayestahiki basi wewe utakuwa ni unayestahiki. Hata kama mtu atakushutumu kuliani mwako kisha akageuka kushotoni mwako na akakuomba msamaha basi kubali msamaha wake ."[335]