JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA0%

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA Mwandishi:
: HEMEDI LUBUMBA SELEMANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

Mwandishi: Muhammad Reyshahri
: HEMEDI LUBUMBA SELEMANI
Kundi:

Matembeleo: 15357
Pakua: 3585

Maelezo zaidi:

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 15357 / Pakua: 3585
Kiwango Kiwango Kiwango
JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

Mwandishi:
Swahili

5

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

MADHARA YA KIELIMU NA KISIASA

WAJIBU WA KUJIKINGA DHIDI YA MADHARA YA KIELIMU

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Wahadharisheni watoto wenu na maghu- lati ili wasiwaharibu, kwani hakika maghulati ni viumbe wabaya mno kati ya viunbe vya Mwenyezi Mungu. Wanadharau utukufu wa Mwenyezi Mungu na wanadai uungu kwa waja wa Mwenyezi Mungu ."[411]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Harakisheni kuwafunza wanenu hadithi kabla murjiina hawajawatangulia kwao ."[412]

Tahadhari dhidi ya kuwafuata mbumbumbu: Mwenyezi Mungu amesema: "Wala usifuate usiyo na elimu nayo, hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa ." (Surat Banii Israil: 36).

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msiwe mabubusa, mnasema: 'Watu wakifanya wema nasi tunafanya, wakidhulumu nasi tunadhulumu. Lakini zipeni mamlaka nafsi zenu, watu wakifanya wema nanyi fanyeni wema, wakifanya ubaya basi nyinyi msidhulumu ." [413]

Kumayl bin Ziyad amesema: "Jemedari wa waumini Ali bin Abu Talib alinishika mkono akanitoa hadi jangwani, basi alipoligusa tu jangwa alivuta pumzi kidogo na kisha akasema:'Ewe Kumayl bin Ziyad! Hizi nyoyo ni vyombo na kilicho bora zaidi ni kile chenye kuzingatia. Basi hifadhi kutoka kwangu yale nikwambiayo: Watu ni wa aina tatu: Yupo alimu mtiifu kwa Mola, mwenye kujifunza katika njia ya uokovu. Na mawimbi wafuata upepo wenye kumfuata kila mpiga kelele, wanafuata kila upepo, hawajaangaziwa kwa nuru ya elimu na wala hawajakimbilia kwenye nguzo imara. "[414]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Msiwe mabubusa, mnasema: Mimi niko pamoja na watu nami ni kama mmoja kati ya watu ."[415]

Abu Hamza Thumali amesema: Abu Abdillah(a.s) aliniambia: 'Jiepushe na uraisi na jiepushe usiwe mfuata nyayo za watu." Nikamwambia: 'Mimi ni fidia kwako. Ama urais tunaujua, ama kufuata nyayo za watu ni kuwa theluthi ya niliyonayo ni kutokana na kufuata nyayo za watu.' Akaniambia:'Si kama unavyodhani, ni kuwa jiepushe kumpa mtu utawala bila kuwa na hoja, ukaja kumsadikisha kwa kila alisemalo ."[416]

Imam Al-Kadhim(a.s) alimwambia Fadhlu bin Yunus: "Fikisha kheri na sema kheri na wala usiwe bubusa." Nikamwambia: 'Bubusa ni nani?' akasema: 'Usiseme: Mimi ni kama mmoja miongoni mwa watu, kwani hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: 'Enyi watu! Hakika njia ni mbili: Njia ya kheri na njia ya shari. Hivyo njia ya shari isiwe ipendwayo kwenu kuliko njia ya kheri ." [417]

WAJIBU WA KUWAKHALIFU VIONGOZI WAOVU

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Enyi kundi la vijana mcheni Mwenyezi Mungu na wala msiwafuate viongozi, waacheni mpaka wawe wafuasi. Msiwafanye watu marafiki wa moyo mkamwacha [418] Mwenyezi Mungu. Hakika sisi wallahi ni bora kwenu kuliko wao.' Kisha akapiga mkono wake juu ya kifua chake ."[419]

MAAFA YA KITABIA NA KIMATENDO

KUTOTIMIZA HAKI ZA WAZAZI WAWILI

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Lau kama Mwenyezi Mungu angefahamu kilicho chini zaidi ya (kusema kumwambia mzazi) Akh! katika kutotimiza haki za wazazi wawili basi angekiharamisha. Mwenye kushindwa kutimiza haki za wazazi afanye afanyavyo hatoingia Peponi ." [420]

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Baba yangu alimwona mwanaume akiwa na mwanaye akitembea kwa miguu huku mtoto akiwa kaegemea kwenye dhiraa ya baba. Akasema: Basi baba yangu hakumsemesha kwa ajili ya kuchukizwa naye mpaka anaiacha dunia ."[421]

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Baba mbaya ni yule ambaye wema unam- peleka kwenye uvukaji mipaka. Na mtoto mbaya ni yule ambaye kupuuzia humpelekea kutotimiza haki za wazazi ."[422]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Kiwango cha chini kabisa cha kutotimiza haki za wazazi ni neno Akh. Na lau kama Mwenyezi Mungu angejua kitu chepesi zaidi ya hilo basi angekikataza ."[423]

Imam Al-Askar(a.s) amesema: "Ujasiri wa mtoto dhidi ya baba yake utotoni mwake hupelekea kumnyima haki zake ukubwani mwake ."[424]

TABIA MBAYA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Tabia mbaya ni dham- bi isiyoghufiriwa ." [425]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alipoambiwa: "Fulani anafunga mchana na kuswali usiku lakini yeye ana tabia mbaya anamuudhi jirani yake kwa ulimi wake.'Akasema: 'Hana kheri, naye ni miongoni mwa watu wa motoni ." [426]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye tabia zake zitakuwa mbaya basi riziki yake itabana ."[427]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye tabia yake itakuwa mbaya atatengwa na rafiki ."[428]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Ambaye tabia yake itakuwa mbaya basi ameiadhibu nafsi yake ."[429]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Luqman(a.s) alisema:'Ewe mwanangu mpendwa! Jiepushe na ghadhabu, tabia mbaya na uchache wa subira, haku- na mtu anayekuwa sawa juu ya sifa hizi. Ilazimishe nafsi yako ridhaa kati- ka mambo yako, na ivumilishe nafsi yako katika matumizi ya jamaa na wafanyie watu wote tabia njema ."[430]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Ambaye ulimi wake utaogopwa na watu basi huyo ni mtu wa motoni ."[431]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Maafa ya uzuri ni mawazo hewa (yatokanayo na kiburi) ." [432]

KUJIONA/ KUJIKWEZA

Imam Ali(a.s) amesema: "Lililo baya mno kati ya mambo ni mtu kujikweza mwenyewe ."[433]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayejiona adhimu ndani ya nafsi yake basi mbele ya Mwenyezi Mungu atakuwa duni ."[434]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mcheni Mwenyezi Mungu wala msihusudiane nyinyi kwa nyinyi, hakika miongoni mwa sheria za Isa bin Maryam ilikuwa ni kutembea mjini, ndipo siku moja akatoka katika

matembezi yake akiwa na mwanaume mbilikimo miongoni mwa sahaba zake, naye alikuwa ni mwandama mno wa Isa bin Maryam(a.s) .

Isa(a.s) alipofika baharini alisema: 'Bismillahi' kwa usahihi akiwa na yakini nayo, akatembea juu ya maji. Basi mtu yule mbilikimo alipomtazama Isa(a.s) alimuiga kwa usahihi akiwa na yakini nayo, naye akapita juu ya maji na kuungana na Isa(a.s) . Hilo likamfanya ajikweze, akasema: 'Huyu Isa(a.s) Ruhullah anatembea juu ya maji nami pia natembea juu ya maji, basi ana ubora gani juu yangu.' Hapo hapo akazamishwa ndani ya maji na ndipo akaanza kuomba msaada toka kwa Isa(a.s) , akamshika mkono na kumwopoa toka ndani ya maji, kisha akamwambia: 'Ulisema nini ewe mbilikimo?' Akasema: 'Nilisema: Anatembea juu ya maji nami natembea juu ya maji, basi hilo likanifanya nijione.' Isa(a.s) akamwambia: 'Umeiweka nafsi yako sehemu isiyokuwa ile aliyokuweka Mwenyezi Mungu, ndipo Mwenyezi Mungu akakuchukia kwa uliyosema, hivyo tubu kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uliyose- ma.' Basi mbilikimo yule akatubu na akarejea kwenye daraja lake ambalo Mwenyezi Mungu alimweka. Mcheni Mwenyezi Mungu msihusudiane nyinyi kwa nyinyi."[435]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Jiepusheni na kiburi, kwani hakika kiburi huwa kwa mtu hata kama ana joho ." [436]

PUPA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Hakika mwanaadamu ni mwenye pupa juu ya yale aliyonyimwa ." [437]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenye pupa ni fakiri hata kama ataimiliki dunia kwa mikono yake ."[438]

HUSUDA

Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda ni matokeo ya kuchoka ."[439]

Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda huzuia raha ."[440]

Imam Ali(a.s) amesema: "Husuda haileti ila madhara na hasira. Hudhoofisha moyo wako na kuuguza mwili wako. Na shari ambayo inayohisiwa na moyo wa mtu ni husuda ."[441]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi milele ni mgonjwa (alilu) ."[442]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi daima ni mgonjwa hata kama ni mwenye mwili wenye siha ."[443]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi hafanikiwi ."[444]

Imam Ali(a.s) amesema: "La ajabu ni mghafiliko wa mahasidi kunako usalama wa miili ."[445]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasidi hudhihirisha mapenzi yake kwenye kauli zake na huficha chuki yake kwenye vitendo vyake. Ana jina la rafiki na sifa ya adui ."[446]

Imam Ali(a.s) amesema: "Matunda ya husuda ni mahangaiko ya dunia na akhera. "[447]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Luqman(a.s) alimwambia mwanae:'Hasidi ana alama tatu: Anasengenya anapokuwa hayupo. Huonesha mapenzi ya uongo anaposhuhudia na hufurahia msiba ."[448]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Hasidi ni mwenye kujidhuru yeye mwenyewe kabla hajamdhuru mhusudiwa, kama ambavyo Ibilisi kwa husuda yake alirithisha laana ndani ya nafsi yake, na akarithisha kwa Adam (a.s) kujielekeza (kwa Mola wake) ."[449]

CHUKI YA NDANI (HIKDI)

Imam Ali(a.s) amesema: "Hikdi huumiza nafsi na huongeza maumivu ya moyo ."[450]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayetoa chuki basi moyo wake na akili yake hustarehe .''[451]

HASIRA

Imam Ali(a.s) amesema: "Hasira ni sehemu ya uwendawazimu kwa sababu mwenye nayo hujuta, na ikiwa hajuti basi uwendawazimu wake huendelea ."[452]

UBISHI

Imam Ali(a.s) amesema: "Ubishi hunyakua rai ."[453]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ubishi huharibu rai ."[454]

Imam Ali(a.s) amesema: "Matunda ya ubishi ni kuangamia ."[455]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mbishi hukumbana na balaa. "[456]

Imam Zainul-Abidiin(a.s) amesema: "Ubishi huambatana na ujinga, na ushabiki huletwa na msiba, na sababu ya heshima ni unyenyekevu. "[457]

UVIVU

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alimwambia Ali(a.s) : "Jiepushe na sifa mbili: Hasira na uvivu, kwani hakika wewe ukikasirika hutosubiri juu ya haki, na ukifanya uvivu hutotekeleza haki ."[458]

Imam Al-Baqir(a.s) amesema: "Hakika mimi nachukia sana mtu kufanya uvivu kunako jambo la dunia yake. Na atakayefanya uvivu juu ya jambo la dunia yake basi ni mvivu kunako jambo la akhera yake ."[459]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hakika mambo yalipochanganyikana, uvivu na kushindwa vilijichanganya pamoja na hatimaye vikazaa ufakiri ."[460]

Imam Ali(a.s) amesema katika sifa za muumini: "Utamuona uvivu wake uko mbali; na uchangamfu wake ni wa daima ."[461]

Imam Zainul-Abidiin(a.s) amesema katika dua zake: "Ewe Mola wetu Mlezi tupe neema ya uchangamfu na utukinge na kufeli na uvivu ."[462]

KUVUKA MIPAKA KATIKA IBADA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Jiepusheni kuifanya nzito dini, kwani hakika Mwenyezi Mungu ameifanya nyepesi, ichukueni kadri muwezavyo, kwani hakika Mwenyezi Mungu hupenda maadamu tu ni katika amali njema hata kama ni ndogo. " [463]

Imam Ali(a.s) amesema: "Atakayeifanya nzito dini basi hatafika kwenye haki ."[464]

Imam Ali(a.s) amesema: "Hutomuona mjinga ila ni mwenye kupuuza au mwenye kupituka ."[465]

KUJIPAMBA KULIKOKEMEWA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Si miongoni mwetu wale wanawake wenye kujishabihisha na wanaume. Na wala wanaume wenye kujishabihisha na wanawake ." [466]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Makundi ya aina mbili ni ya motoni na sitoyaona: Kaumu wenye mijeledi kama mikia ya ng'ombe wanaitumia kuwapiga watu. Na wanawake wenye kujiachia wenye kubaki uchi, wenye kushawishi wenye kuringa.hawatoingia peponi na wala hawatoipata harufu yake ."[467]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenye kushabihiana na kaumu hukaribia kuwa miongoni mwao ."[468]

KUENDEKEZA KUFIKIRIA STAREHE

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye fikara zake zitazama kwenye starehe basi zitamshinda ."[469]

Imam Ali(a.s) amesema: "Ambaye fikara zake zitazama kwenye maasi yatamwita ayaendee ."[470]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Wanafunzi wa Isa(a.s) walijikusanya kwake na kumwambia: 'Ewe mwalimu wa kheri tuongoze.' Akawaambia: 'Hakika Musa Kalimullah aliwaamuru msiape kwa Mwenyezi Mungu ilihali ni waongo. Na mimi nawaamuru kuwa msiape kwa Mwenyezi Mungu ilihali ni waongo na si wakweli.' Wakasema: 'Ewe Ruhullah tuzidishie.' Akasema:'Musa Nabii wa Mwenyezi Mungu aliwaamuru msizini nami nawaamuru msizisimulie nafsi zenu zinaa achia mbali kuitekeleza. Kwani hakika mwenye kuisimulia nafsi yake zinaa anakuwa kama mtu aliyewasha moto ndani ya nyumba iliyorembwa, na hatimaye moshi ukaharibu marembo hata kama nyumba haikuungua ."[471]

KUNYWA POMBE

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Pombe ni mama wa maovu na maasi ." [472]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Pombe ni mama wa mabaya. " [473]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Shari yote imekusany- wa ndani ya nyumba, na kunywa pombe kukafanywa ndio ufunguo wake ." [474]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Atakaelala amelewa basi huwa amelala akiwa biharusi wa shetani ." [475]

Imam Ali(a.s) amesema: "Mwenyezi Mungu alifaradhisha kuacha pombe ili kuilinda akili ."[476]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Hakika maasi akiyatenda mja kwa siri hayamdhuru ila mtendaji wake. Na akiyatenda waziwazi bila kukemewa hudhuru jamii nzima ." [477]

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA

SEHEMU YA NNE

HAKI ZA VIJANA

HAKI ZA VIJANA JUU YA WAZAZI WAO

UMUHIMU WA HAKI ZA MTOTO

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mzazi hupatwa kutokana na haki za mtoto wake yale ambayo humpata mtoto kutokana na haki za mzazi wake ." [478]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Wazazi hupatwa kutokana na kutomtimizia haki mtoto wao yale ambayo humpata mtoto wao kutokana na kutowatimizia haki zao ." [479]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Wazazi hupatwa kutokana na kutomtimizia haki mtoto wao iwapo ni mwema yale ambayo humpata mtoto ." [480]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mtoto ni bwana miaka saba, ni mtumwa miaka saba na ni waziri miaka saba ." [481]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mwache mwanao acheze miaka saba, na huadabishwa miaka saba na mfuatilie miaka saba ."[482]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Ambaye mwanae atafikia umri wa kuoa na akawa ana mali anayoweza kumuozesha lakini hakumuozesha kisha (mtoto) akizua la kuzua madhambi ni juu yake (mzazi) ." [483]

UADILIFU

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Fanyeni uadilifu baina ya wanenu. Fanyeni uadilifu baina ya wanenu ." [484]

Nu'man Bin Bashir amesema: "Baba yangu alinipa kipawa basi Amrat bint Rawaha akasema: 'Siridhii mpaka umshuhudishe Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Akamjia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na kumwambia: 'Hakika mimi nimempa mwanangu toka kwa Amrat binti Rawaha kipawa, akaniamuru (Amrat) nikushuhudishe wewe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Akamuuliza: 'Je umewapa wanao wengine kama hivyo?' akasema 'La.' Akamwambia: 'Mcheni Mwenyezi Mungu na fanyeni uadilifu baina ya wanenu.' Anasema: Basi akarejea na kumnyang'anya kipawa kile."[485]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Uadilifu ni mtamu kuliko maji ayanywayo mwenye kiu. Ni upana ulioje wa uadilifu pindi mtu akifanyiwa hata kama ni mdogo ."[486]

DUA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Dua njema ya mzazi kwa mwanae ni sawa na dua njema ya Nabii kwa umma wake ." [487]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Dua njema ya mzazi kwa mwanae ni sawa na maji kwenye mmea kwa manufaa yake ." [488]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Mwenyezi Mungu humrehemu anayemsaidia mwanae kumfanyia mema, nako ni kumsamehe makosa yake na kumuombea mema katika yale yaliyopo kati yake na Mwenyezi Mungu ." [489]

KUACHA KUMUOMBEA MABAYA

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msiwaombee mabaya wanenu ikaja kuwa mwafaka kwa jibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ." [490]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msijiombee mabaya na wala msiwaombee mabaya wanenu, wala msiiombee mabaya mali yenu, msifanye iwe mwafaka na saa ambayo humo huombwa kipawa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hatimaye akawajibu ." [491]

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Msitamani kuhiliki kwa vijana wenu hata kama wana madhara, kwani hakika wao pamoja na hivyo walivyo bado wana vipindi (vya manufaa): Ima watubu na Mwenyezi Mungu awakubalie toba yao, na ima madhara yawapate. Na ima adui aje wamuue, ima janga la moto walizime, na ima maji wayazuie ." [492]

Imam As-Sadiq(a.s) amesema: "Mtu yeyote atakayemuombea mwanae mabaya basi Mwenyezi Mungu humrithisha ufakiri (mtu huyo) ."[493]

Alama ya kuvuka mipaka katika kumlaumu: Imam Ali(a.s) amesema: "Utakapomkemea kijana basi mwachie nafasi katika kosa lake ili kumkemea kusimpelekee kuwa na jeuri ."[494]

Imam Ali(a.s) amesema: "Kuzidisha kukemea huwasha moto wa ubishi (upinzani) ."[495]

Imam Ali(a.s) amesema: "Unapokemea kemea kwa wastani ."[496]

HAKI ZA KIJANA KIJAMII

KUWAKIRIMU

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Wapeni nafasi vijana katika mabaraza, waelewesheni hadithi, kwani hakika wao ni warithi na watu wa hadithi ." [497]

Sahlu bin Sa'ad amesema: "Mtume(s.a.w.w) aliletewa bilauri akanywa kilichomo, kuliani mwake kulikuwa na kijana mdogo kuliko wote waliokuwepo, na kushotoni mwake(s.a.w.w) kulikuwa na wazee, basi akamwambia: 'Ewe kijana unaniridhia niwape wazee kilichomo?' akasema:'Siwezi kumrithisha yeyote fadhila yangu kutoka kwako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Basi akawa amempa ." [498]

Kuwaomba ushauri

Imam Ali(a.s) amesema: "Ukihitaji ushauri wa jambo lililokutokea basi lidhihirishe kwa kuwaanza vijana kwani hakika wao ni moja ya akili na wepesi wa kutafakari, kisha baada ya hapo lirejeshe kwenye rai ya wazee na vikongwe ili walipitie tena, na wafanye uteuzi wa maamuzi mazuri, kwani hakika uzoefu wao ni mwingi ."[499]

Kutilia umuhimu mahitaji yao maalumu

Ima Al-Baqir(a.s) amesema: "Hakika Ali(a.s) aliwaendea mabazazi na kumwambia aliye mtu mzima: 'Niuzie nguo mbili.' Mwanaume yule akasema: 'Ewe Jemedari wa waumini, kwangu kuna haja yako.' Alipojua kusudio lake akamwacha na akaenda kwa kijana, akachukua nguo mbili, moja kwa dirhamu tatu na nyingine kwa dirhamu mbili, akasema: 'Ewe Qanbar chukua ya dirhamu tatu.' Akasema:'Wewe ndiye aula kwayo kwani unapanda mimbari na kuhutubia watu.' Akamjibu: 'Nawe ni kijana na bado una mvuto wa ujana, nami naona haya mbele ya Mola wangu Mlezi kuwa mbora juu yako ."[500]

Na mwisho wa dua yetu ni kumshukuru Allah Bwana Mlezi wa walimwengu.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

YALIYOMO

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 1

UDONDOZI KUTOKA KITABU: JAWAAHIRU AL-HIKMAH LI 'SH-SHABAAB 1

KIMEANDIKWA NA: MUHAMMAD REYSHAHRI 1

KIMETARJUMIWA: HEMEDI LUBUMBA SELEMANI 1

NENO LA MCHAPISHAJI 1

DIBAJI 2

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 4

SEHEMU YA KWANZA 4

NAFASI YA KIPINDI CHA UJANA KATIKA USTAWI 4

1- KIPINDI CHA USTAWI WA MAISHA 4

KUNUFAIKA NA FURSA YA UJANA 4

HAZINA YA SIKU 6

JUHUDI ZA DHATI KATIKA NJIA YA MAENDELEO 6

2- USTAWI KATIKA KUJIJENGA 7

NAFASI YA VIJANA KATIKA KUJIELIMISHA 8

MAFUNZO YA KIROHO 9

MANABII(A.S) WALITUMWA WAKIWA VIJANA 9

3 - NAFASI YA VIJANA KATIKA SERIKALI YA 10

BALOZI WA KWANZA WA MTUME (s.a.w.w) NI KIJANA 10

GAVANA WA KWANZA WA MAKKA NI KIJANA WA MIAKA ISHIRINI NA MOJA 11

NAFASI YA VIJANA KATIKA SERIKALI YA IMAM WA ZAMA ZETU 12

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 13

SEHEMU YA PILI 13

SABABU ZINAZOPELEKEA USTAWI WA VIJANA 13

1- MAARIFA 13

KUJIELIMISHA 13

KUJITAMBUA 13

KUIJUA QUR'ANI TUKUFU 14

KUJIFUNZA DINI 15

UMUHIMU WA UDADISI 16

2 - AZMA 17

KUJITUMA 17

MALENGO YA JUU 18

KUJIHESHIMU 18

MSIMAMO 19

KUMTAWAKALI MWENYEZI MUNGU 19

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 20

3 - UHUSIANO NA MWENYEZI MUNGU 20

THAMANI YA IBADA KATIKA KIPINDI CHA UJANA 20

BARAKA ZA IBADA YA UJANANI 21

MAANA YA IBADA 21

WASTANI KATIKA IBADA 22

4 - RAFIKI MWEMA 22

NAFASI YA RAFIKI MAISHANI 22

KUMJARIBU RAFIKI 22

AINA ZA MARAFIKI 23

MARAFIKI BORA 23

HAKI YA MWENZI WAKO 25

5 - MAHITAJI YA HALALI NA NGUVU ZA MWILI 25

NGUVU ZA MWILI ZASIFIWA 25

SABABU ZA MVUTO 26

BURUDANI 26

MATEMBEZI 27

MIZAHA 27

KUOGELEA NA KUTUPA MSHALE 28

MIELEKA 29

MASHINDANO 29

6 - THAMANI YA TABIA NJEMA NA MATENDO MEMA 30

KUACHA MAASI 30

TOBA 31

NIDHAMU 34

KUHESHIMU HAKI ZA WAZAZI WAWILI 34

KAZI 35

KUWAHUDUMIA WATU 36

UAMINIFU 37

KUJIPAMBA 38

MAADILI MEMA 39

UTAWA 40

KUANGUSHA MACHO 41

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 43

UDONDOZI KUTOKA KITABU: JAWAAHIRU AL-HIKMAH LI 'SH-SHABAAB 43

3 - HIJABU 43

NDOA 44

A: MKAZO WA KUOA UJANANI 44

B: MUME MARIDHAWA 44

C: MKE MARIDHAWA 44

D: KUOA AKRABA 45

HAYA 45

HAYA 46

UNYENYEKEVU 46

MTAZAMO WA MBALI 46

UHURU 47

KUKUBALI UDHURU 47

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 49

3 - SEHEMU YA TATU 49

VIZUIZI VINAVYOZUWIA USTAWI WA VIJANA 49

KUTOKUJISHUGHULISHA KWAKEMEWA 49

MADHARA YA KUTOJISHUGHULISHA 50

ULEVI 50

KILA KILEVI KIMEHARAMISHWA 50

TAHADHARI DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA 51

RAFIKI MBAYA 51

MADHARA YA RAFIKI MBAYA 51

ULEVI WA UJANA 53

MATAMANIO YA KIJINSIA 53

MTEGO WA SHETANI 53

MALIPO YA UTAWA WA JINSIA 56

MALIPO YA MWENYE ASHKI ALIYE MTAWA 57

MITEGO YA SHETANI 57

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 59

MADHARA YA KIELIMU NA KISIASA 59

WAJIBU WA KUJIKINGA DHIDI YA MADHARA YA KIELIMU 59

WAJIBU WA KUWAKHALIFU VIONGOZI WAOVU 60

MAAFA YA KITABIA NA KIMATENDO 60

KUTOTIMIZA HAKI ZA WAZAZI WAWILI 60

TABIA MBAYA 60

KUJIONA/ KUJIKWEZA 61

PUPA 62

HUSUDA 62

CHUKI YA NDANI (HIKDI) 63

HASIRA 63

UBISHI 63

UVIVU 63

KUVUKA MIPAKA KATIKA IBADA 64

KUJIPAMBA KULIKOKEMEWA 64

KUENDEKEZA KUFIKIRIA STAREHE 64

KUNYWA POMBE 65

JOHARI ZA HEKIMA KWA VIJANA 66

SEHEMU YA NNE 66

HAKI ZA VIJANA 66

UMUHIMU WA HAKI ZA MTOTO 66

UADILIFU 66

DUA 67

KUACHA KUMUOMBEA MABAYA 67

HAKI ZA KIJANA KIJAMII 68

KUWAKIRIMU 68

SHARTI YA KUCHAPA 68

MWISHO WA KITABU 68

YALIYOMO 69