1
USUULID DIIN
UIMAMU
IMAMU WA PILI
HASSAN BIN ALI
Alie maarufu kwa lakabu (jina na umashuhuri) ya "Azzakiyu"na "Al-mujtaba". Alizaliwa Madina katikati ya mwezi wa Ramadhani mwaka wa 3 H.
Amekulia kwenye malezi ya Utume na uwanda wa Qur'ani na kwenye nyumba iliyo kuwa ukishuka wahyi ndani yake. Alikuwa ni mmoja wa "Maimamu wawili wa uongofu"
na mmoja kati ya "mabwana wawili wa vijana wa peponi"
, na mmoja wapo kati ya watu wawili ambao kizazi chote cha mtume kimetokana nao, nae ni mmoja wapo kati ya watu wanne ambao Mtume aliwachukua kwa ajili ya maapizano na manasara (wakristo) wa Najran, na ni mmoja wapo kati ya watu watano ambao Mwenyezi Mungu aliwatakasa na kuwaondolea uchafu kiukamilifu.
Aliishi miaka saba pamoja na babu yake Mtume(s.a.w.w)
kisha alikuwepo kwenye matukio yote ambayo baba yake alikumbana nayo na kutaabika kwa machungu yake na kuyavumilia maumivu na machungu yake, ukhalifa ulimfikia kutokana na kufariki kwa baba yake
na ulimwengu wote wa kiislamu ukampa baia (kiapo cha utii) isipokuwa Mu'awiya na watu wa miji ya Sham na akalazimika, ili kutekeleza wajibu wa kuihifadhi hii amana ya dini, kulipeleka jeshi lake ili kupambana na Muawiya na jeshi lake. Kisha utokaji ule ulimalizika kwa kufanya suluhu ambayo ni maarufu. Imamu huyu alikuwa kama babu yake alivyo sema kumuhusu: "Hakika mwanangu huyu ni Sayyid, Mwenyezi Mungu atafanya suluhu kupitia kwake kati ya makundi mawili makubwa.
Utafiti kuhusu suluhu yake pamoja na Muawiya kwa kuangalia utangulizi na mazingira yake, na sababu zilizo mfanya Imamu kufanya suluhu hiyo na siri ya msimamo alio uchukua kwenye suluhu hiyo na vifungu vya mkataba wake, na masharti yake, pia ahadi zake. Kisha kuangalia ni kwa kiasi gani Muawiya alitekeleza masharti yale, ni bah'thi ambayo nafasi haituruhusu kuweza kuyaelezea, na ni juu ya mwenye kutaka ufafanuzi zaidi asome kitabu "Sulhul-Hassan". Muandishi amekusanya na kuhifadhi na akafanya utafiti mzuri, na kitabu hicho kimechapi-shwa zaidi ya mara moja.
Hakika wapigaji kelele walipandikiza na kumzulia mambo Imamu
na kudai kuwa alikuwa ni mwingi wa kuoa na kuacha, hadi mmoja wapo kati yao alidai kuwa idadi ya wakeze ilikuwa kati ya miatatu na mia tisa,
Lakini uchunguzi wa kihistoria haukuthibitisha kuwa na wake walio maarufu zaidi ya saba au wanane.
Kama ambavyo utafiti wa kihistoria haukuthi-bitisha matukio ya talaka kwa imamu zaidi ya tatu.
Na Dr.Ahmad Mahmood Sub'hi amesema akifafanua suala la Imamu kuwa na wake wengi: "Huenda kuwa na wake wengi alikuwa akikusudia kuwa na wake wengi kwenye makabila ya waarabu, kwa sababu mtawala, kama maelezo ya Ibnu Khaldun yasemavyo, hutegemea katika utawala wake ukabila. Na kutoka-na na kuwa bani Umaya hawakushinda na kujimakinisha kwenye ardhi isipokuwa kutokana na asabiya (hisia ya ukabila) waliyo kuwa nayo. Hassan alielewa mambo yatakayo kuja kuwatokea watu wake wa karibu na kizazi chake kama vile kubanwa na kuuliwa ambako hakutakifanya kizazi cha Mtume kibakie na kiwe ni chenye kuhifadhiwa isipokuwa kwa kuoa kwake wake wengi na kuwa na kizazi kingi.
Alifariki kwa sumu ya Muawia, kwenye mji wa Madina kwenye mwezi wa Safar, mwaka wa (50) Hijiria.
Na akazikwa kwenye ardhi ya Baqii' iliyotwahara.
IMAMU WA TATU
HUSSEN BIN ALY
.
Alie maarufu kwa lakabu ya "Seyyidu shuhadaa" (bwana wa mashahidi).
Amezaliwa katika mji wa Madina, tarehe tano mwezi wa shaaban mwaka 4.H.Alikuwa kwenye kivuli cha utume na sehemu iliyo shushwa ujumbe wa Mwenyezi Mungu, na sehemu ambayo Malaika walikuwa wakipishana, na kwenye chimbuko la elimu.
Alishirikiana pamoja na kaka yake Hassan katika sifa zote za msingi:Yeye kama nduguye, ni mmoja kati ya "maimamu wawili wa uongofu", na mmoja wapo kati ya mabwana wawili wa vijana wa peponi" na ni mmoja kati ya watu wawili ambao kizazi chote cha mtume kinatokana nao, na ni mmoja kati ya wanne ambao Mtume aliwachukua kwa ajili ya maapizano na wakiristo na ni mmoja kati ya watu watano walio takaswa kutokana na uchafu na walio twahirishwa kiukamilifu.
Aliishi miaka sita kwenye malezi ya babu yake(s.a.w.w)
na akawepo kwenye matukio yote yaliyo wasibu watu wa nyumba ya Mtume tangu alipofariki babu yake hadi kuuliwa kwa kaka yake kwa sumu, na kupitiwa na mambo yaliyo msibu mama yake na yaliyo mtaabisha baba yake, na yaliyomkumba kaka yake.
Na wakati alipokufa Muawiya na yazidi kurithi ukhalifa, waumini walimtaka akubali suala la uongozi na kufanya mapinduzi dhidi ya khalifa mpya, akaitika wito au maombi yao na akatangaza kupinga kwake kutoa baia (kiapo cha utii) kwa kijana huyo mwenye pupa. Na tunaweza kuzieleza kwa ufupi sababu zilizo mfanya afanye mapinduzi katika sababu tatu za msingi:
1- Yazidi kuto stahiki na kutofaa kuwa khalifa.
2- Kumalizika kazi ya mkataba uliofungwa kati ya kaka yake Hassan na Muawiya, nao ni mkataba ambao ulielezea kwenye madda au kifungu chake cha pili kwamba "Utawala uwe kwa Hassan baada ya Muawiya na ikiwa Hassan atapatwa na tukio lolote (kifo) utawala utakuwa kwa nduguye Hussen, na haimpasi Muawiya kumpa ukhalifa huo mtu yeyote"
. Na maana ya mane-no haya ni kuwa Hussen baada ya Muawiya kufariki, amekuwa mwenye haki rasmi ya kuwa khalifa kwa kukubali kwa Muawiya (kukiri), pale alipo tia sahihi yake kwenye mkataba huo.
3- Mazingira yote kwa ujumla ambayo yalikuwa yakimla-zimisha kutekeleza wajibu huo. Hussen alikuwa ameshaelezea hali na mazingira pindi alipo taja sababu zilizo msukuma kufanya mapinduzi kwenye hadithi yake alipo sema: "Hakika mimi sikutoka kwa ujeuri na kiburi wala kwa kutaka shari wala nikiwa mharibifu wala sikutoka nikiwa dhalimu. Hakika nimetoka kutafuta suluhu kwenye umma wa babu yangu Muhammad(s.a.w.w)
ninataka kuamrisha mema na kukataza maovu".
Na amesema akiashiria kwenye mazingira hayo katika barua alizo zituma kwa baadhi ya mashia wake (wafuasi wake): "Ninaapa kwa umri wangu, si imamu isipokuwa mwenye kuhukumu kwa Kitabu, mwenye kusimamia uadilifu, mwenye kufuata dini ya kweli, mwenye kuifunga nafsi yake juu ya dhati ya Mwenyezi Mungu".
Na sababu hizi zinapokuwa wazi na bayana na kudhihiri sababu za kiislamu zitiazo msukumo mkubwa wa mapinduzi hayo hapo huonekana ukubwa wa makosa aliyo fanya Abubakari Bin Araby na mfano wake pale walipo sema kuwa Hussen alifanya makosa kwenye mapinduzi yake, na wakaona kuwa ilikuwa ni bora kwake kutoa baia (kiapo cha utii) na kunyamaza.
Na vipi itakuwa bora kwake kunyamaza wakati ambapo wajibu wake wa dini unamlazimisha afanye mapinduzi, na yaliyoandikwa kwenye mkataba ambao Muawiya alitia sahihi yake yanampa haki ya kutotoa baia na kutonyamaza.
Na hivi ndivyo Hussen alivyo kuwa mshindi na mwana mapinduzi mkubwa katika historia, hata kama alipata hasara kwenye mapigano ya kijeshi yaliyo fanyika kwa wakati maalumu katika uwanja wa karbalaa, nao walio muuwa wakawa ni wenye kulaaniwa na vizazi vyote kwa muda wa historia ya wanadamu, hata kama walipata ushindi kwenye mapigano yao, huo ni ushindi wa wakati mfupi tu, bali "historia haijaweza kuwajua watu fulani walio fanya harakati fulani na kupata ushindi, kisha wakawa wakijiuma vidole kwa kujuta (alama za majuto) kama wale ambao walishinda kwenye uwanja wa Karbalaa".
Alikufa shahidi tarehe kumi ya mwezi wa Muharram baada ya adhuhuri, mwaka 61H,
na kuzikwa pale pale alipo fia akiwa shahidi kwenye ardhi ya Karbalaa.
IMAMU WA NNE
ALI BIN HUSSEN
Ajulikanae kwa lakabu mbili maarufu "Assajjad" na "Zainul-Abidiina" (yaani mwingi wa kusujudu) na (pambo la wafanya ibada).
Alizaliwa kwenye mji wa Madina mwaka 37 H. Na alikuwepo kwenye zama za tukio la kuuliwa Amirul Muuminiin, akiwa ni mdogo na pia alikuwepo kwenye zama za baba yake mkubwa au ami yake Hassan alipo patwa na mitihani iliyo mpata na ambayo ilimfanya afanye suluhu pamoja na Muawiya (na tumeelezea kuhusiana na mtihani huo).
Kisha akaishi, akiwa kijana kwenye matukio ya huzunishayo na ya kikatili ya Karbalaa na kuyaona machungu yake na jinsi yanavyo sikitisha na kuhuzunisha. Na akachukuliwa hadi Sham akiwa miongoni mwa mateka.Yeye pamoja na Shangazi yake walikuwa na dauru kubwa katika kuifanya mikakati ya bani umayya ishindwe.
Mikakati yenye kutisha iliyo kusudiwa kufuta uovu wa kuuliwa kwa Hussen
na kuyafanya yaliyo tokea kuwa ni tukio la kijeshi la kuwaadabisha watu walio asi na kutoka kinyume cha dini na serikali (utawala).
Kisha akaendelea kuishi hadi mwaka wa pili, tangu kuuliwa baba yake, na kushuhudia tukio la "Harra" na maovu yake yote, na fedheha waliyo ifanya. Na pale wana mapinduzi walipo amua kuwafukuza bani Umayya wengine kutoka kwenye mji wa Madina, Mar'wan binilhakam hakupata makimbilio ya kumuha-kikishia usalama wake na familia yake isipokuwa nyumba ya Imamu Assajad na kuiacha familia yake kwa Imamu.
Na Imamu kuwakubali na kuwapokea wakimbizi hao lilikuwa ni somo kubwa lililo dhihirisha mbele ya watu na historia maana ya uimamu kwa mafhumu yake ya mbinguni yaliyo takasika na matukufu.
Imamu alichukua msimamo wa upinzani dhidi ya serikali ile, na msimamo huu wa upinzani ulionekana na kudhihiri kwenye mfumo au umbile la dua na nyuradi walizo kuwa watu wakijifunza kutoka kwake na kuzitawanya kati yao. Hakika Imamu aliweza kueleza kwenye dua na nyuradi hizo mambo yenye kuhitaji kufanyiwa mazingatio na kuangaliwa kwa makini kabisa, Kwani yalikuwa yakielezea uhakika wa serikali ilivyo dhalimu na ukubwa wa dhuluma yake na jeuri kubwa waifa-nyayo, na pia alikuwa akiziamsha akili na mabongo ya watu juu ya mambo yaliyo fanywa na watawala wale ya kuyafisha mafundisho ya dini na kuitumia nafasi ya wateule na waaminifu wa Mwenyezi Mungu kuyapotosha mambo ya faradhi ya dini na kukiacha kitabu na kuziacha sunna.
Na wakati huo huo akijaribu kulitibu lile tatizo la kitabia ambalo lilikuwa ni kali na ambalo lilikuwa likiitaabisha jamii kutokana na athari zake mbaya kwa wakati huo.
Na dua hizo zilikusanywa kwenye kitabu kiitwaho "Swahifatu-Sajjadiya". Dua hizo zimekuwa ni mfano kwetu sisi na vizazi vyetu vyote vijavyo na sehemu muhimu ya urithi wa Imamu, na kitabu hiki kimechapishwa mara nyingi sana.
Kama ambavyo miongoni mwa urithi wenye kubakia milele wa Imamu, ni ujumbe wake au kijitabu chake kihusianacho na "Haki" na alikusudia kwenye kijitabu hicho kuweka wazi au kubainisha haki makhsusi kwa watu makhsusi na haki za watu wote kwa jumla ambazo ndizo ziwekazo nidhamu ya mahusiano na mwenendo kati ya mtu na Mola wake, au mtu na viungo vyake, au mtu na watu wengine katika jamii yake, na kijitabu hiki kimechapishwa zaidi ya mara moja.
Alifariki (Rehma na Amani ziwe juu yake) kwenye mji wa Madina, mwaka 95H,
na kuzikwa kwenye makaburi ya Baqi'i tukufu.
IMAMU WA TANO
MUHAMMAD BIN ALI
Alie maarufu kwa lakabu ya "Al-baaqir"aliyopewa na babu yake Mtume(s.a.w.w)
. Alizaliwa Madina, mwaka 57.H.
Aliyashuhudia, akiwa bado ni mtoto, matukio ya kuhuzuni-sha ya Karbalaa na akaishi kwenye ujana wake, katika matatizo hayo na mitihani hiyo na machungu yake, matukio ambayo baba yake Sajjad aliyo yapata na watu wengine wa familiya yake. Ali pindi uimamu ulipomfikia, baada ya kufariki baba yake, aliamua kuwa na msimamo wa upinzani dhidi ya serikali iliyo kuwa ikiwatawala kwa Uhuru wote na kutoshiriki kwa aina yoyote ile kwenye matukio ya zama zake, bali aliamua kuutumia wakati wake wote kwenye juhudi za kufundisha dini na kuufafanua Uislamu Sahihi na wa kweli na kuondoa athari za kutu na mawingu yaliyo tanda juu ya sheria, fiqhi na hadithi katika zama za bani umaya wa mwanzo.
Pamoja na kukatika mawasiliano kati yake na watawala wa zama zake, wao walikuwa wakimkimbilia kwenye baadhi ya matatizo yote ya ujumla wakimtaka ushauri na nasaha, na Imam alikuwa hafanyi ubakhili wa kuwapa nasaha na kuwaelekeza ili kulinda na kuhifadhi jengo la Uislamu yaani mujtamaa na maslahi yake ya juu.
Kama mfano juu ya ushauri alio kuwa akiutoa ni kuwa baadhi ya wanahistoria wamesimulia kwamba Khalifa Abdul Maliki bin Mar'waan alizuwia kuenea kwa aina fulani ya vyombo na nguo zilizo kuwa zikitengenezwa na baadhi ya wakristo kwenye nchi ya misri na juu yake wakivipamba na kuweka juu yake nembo au alama ya baba, mwana, na roho mtakatifu kwa Lugha ya kisiriyaniya na kukafanyika mazungumzo kati ya khalifa na mfalme wa Roma kuhusu suala hilo, na Khalifa alikuwa akikataa na kupinga na kutokubali maombi au matakwa ya mfalme huyo wa Roma ya kuendelea kuuza bidhaa zile, na mwishowe mfalme akatishia, ikiwa Khalifa hata kubali maombi yake, kuwa ataweka sentensi za kumtusi Mtume wa Uislamu juu ya dirhamu na dinari (aina za pesa za wakati huo) zitumikazo kati ya waislamu na hadi wakati huo pesa zilikuwa zikitengenezwa kwenye nchi ya Roma.
Na pindi Abdul-Malik alipo tatizika kuhusu suala hilo, hapakuwa na budi isipokuwa ni kumtaka Imam Baaqir, ushauri kuhusiana na suala hilo, na akamuita hadi Sham kwa lengo hilo. Imamu akaitika wito wake na kwenda Sham, na baada ya kufika tu akakutana na Abdul-Malik. Khalifa yule akamueleza tatizo lenyewe. Alicho kifanya Imamu ni kumuamuru kuwaleta wahunzi. Khalifa akawaleta, Imam akawafahamisha jinsi na namna ya kutengeneza dirham na dinar na kuunda umbo au muundo wake na kupima kiwango chake.
Na kwa ushauri huu akaweza kulishinda tatizo lile na kuvunja mbinu na mikakati iliyo kuwa imewekwa na kupangwa na mfalme wa Roma, ya kuwafanya waislamu wafuate na kuvinyenyekea vitisho vyake visivyo na haya.
Wanafunzi wa Imamu ni wengi sana na hatuna nafasi ya kuwaorodhesha. Na urithi wake uliohifadhiwa ni wenye thamani na mzuri, na riwaya zake zimo kwenye vitabu vya tafsiri na fiqhi na hadithi, pia kwenye vitabu vya akida na historia. Alifariki kwenye mji wa Madina mwezi wa dhul hijja, mwaka 114H na kuzikwa kwenye makaburi ya "Baqi'i"tukufu.
IMAM WA SITA
JAAFAR BIN MUHAMMAD
Alie maarufu kwa lakabu ya "Aswaadiq". Amezaliwa kwenye mji wa Madina mwaka 83 H. Alikuwepo kwenye zama ambazo dola la bani umaya lilidhoofu na kuanguka, na mwanzoni mwa dola la bani Abbas, na jinsi walivyo kuwa wakijishughulisha na uwekaji wa nguzo za utawala mpya. Mazingira haya yalimsaidia sana kuwafaidisha watu na kuwafundisha, pia kuwapatia elimu na malezi wanafunzi wengi na wanazuwoni ambao walikuwa na athari kubwa katika kuzipa msukumo harakati za kielimu na kuzifanya zisonge mbele na kupanuka (kwa kuzama kwenye elimu kadha) kwenye ulimwengu wa kiislamu.
Na kutokana na wingi wa wanafunzi wake na riwaya zake kuwa nyingi, ushia katika matumizi ya watu uliitwa kwa jina la "Madhehebu ya Jaafariya" kwa kuyanasibisha na Imam Jaafar Aswadiq
wakati ambapo ushia ni mfumo wa Ahlul baiti wote bila kuhusika na Imamu fulani au kuyafungamanisha nae pekee.
Na inatosha kufahamu nafasi ya Imamu huyu katika kazi na ujuzi aliokuwa nao kwa kuyasoma yaliyo andikwa na mmoja wapo kati ya wanahistoria kwa kuorodhesha idadi ya wapokezi wa hadithi kutoka kwa Imamu waliofikia watu elfu nne.
Na pia kwa kusoma maneno yaliyo wazi ya Abul-Hassan Al-washau, pale alipo sema kwenye moja wapo kati ya mazungumzo yake kuhusu hadithi zake:
"Niliwaona kwenye msikiti huu (akikusudia msikiti wa kufa) mashekhe mia tisa na wote wakisema: Amenieleza Jaafar bin Muhammad".
Kisha inatutosha kuelewa urithi wa Imamu wa kielimu aliotuachia tangu siku hizo kwa kuelewa kiasi tu, ili tuone ukubwa na utukufu wenye kudhihiri kwa Imamu huyu mtukufu.
Hakika zimepokelewa kutoka kwa Imamu hadithi nyingi katika kuitafsiri Qur'ani na katika elimu ya fiq'hi na sheria, pia katika falsafa na akida, na mambo mengine mengi, lau kama yangekusanywa yange weza kuunda au kufikia kitabu kikubwa sana na kisicho na mfano.
Kisha miongoni mwa urithi ulio patikana kwake ni zile kanuni za tiba na vyanzo vya msingi katika masuala ya afya kwa ujumla, urithi ulio kusanywa kwenye vitabu viwili kama vifuatavyo
"Tawhidul-mufadhal" na "Al-ihliilijah".Vitabu hivi vimekusanya maudhui mbali mbali, kati ya maudhui zilizomo kwenye vitabu hivyo ni kuelezea wazi kwa ufafanuzi wenye kutosheleza kuhusu mas'ala ya "ugonjwa wa kuambukiza" ambao hupelekea kuvifahamu "vijidudu vya magonjwa" (mikrobu) ambavyo nafasi yake kwenye elimu ya magonjwa inafahamika. Kama ambavyo vimeelezea pia jinsi Imamu
alivyo tangulia kugundua siri ya mzunguko wa damu kabla hajaweza kuugunduwa na kuuelewa Dr.Harfi kwa karne nyingi.
Na mwisho, ikiwa si mwishoni, kuna mambo katika urithi wa Imamu ambayo alimueleza mwanafunzi wake ayaandike ambae ni Jaabir bin Hayani, zikiwemo kanuni za kikemia na misingi yuke, na kwa kufanya hivyo alikuwa ametoa elimu ya kemia kidhati kama Dr Muhammad Yahya Al-hashimy alivyo muita
.
Naye mwalimu Donald Son anazungumzia njia ya Imamu katika ufundishaji na anasema: "Hakika njia yake ilikuwa kama Sokrati, yeye alikuwa akiwaanzia wanafunzi wake kwa mazungu-mzo na majibizano na akienda hatua kwa hatua kwenye maudhui madogo na mepesi hadi kufikia kwenye maudhui magumu na yaliyo fungika na siri zisizo fahamika"
.
Amefariki Imamu (Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kwenye mji wa Madina katika mwezi wa mfungo mosi (Shawwal) mwaka 148.H
na kuzikwa kwenye uwanja wa "Baqi'i"ulio mtukufu.
IMAM WA SABA
MUSSA BIN JAAFAR
Alie mashuhuri kwa lakabu mbili za "Al-kaadhim" na "babul-hawaaij".
Alizaliwa kwenye sehemu iitwayo Ab'waa, karibu na mji wa Madina, mwaka 128.H. Aliyamaliza masiku ya maisha yake akiwa ni mwenye kuadhibiwa na kufukuzwa na watoto wa ami yake Banu Abbas. Akapambana na vikwazo vyao, nae akiwa huru, pia kupambana na maudhi yao, akiwa jela mambo ambayo hayawezi kuelezeka. Siku za mtawala Rashiid zilikuwa ni zama mbaya sana kwa Imamu.
Na baadhi ya wanahistoria wanasimulia sababu ya kuwepo hali hiyo ni kuwa: Rashiid wakati alipo kwenda Madina na kuingia kwenye msikiti wa Mtume, akizungukwa na viongozi mbali mbali na maraisi alilielekea kaburi tukufu la Mtume, akamsemesha mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)
kwa kusema:
"Amani iwe juu yako ewe Mwana wa ami yangu". Alijaribu kwa kusema vile kuwahadaa watu kuwa anahaki ya ukhalifa kwa sababu ya ukaribu uliopo kati yake na Mtume. Imamu hakuna alilo lifanya isipokuwa ni kuweka wazi udhaifu wa hadaa hiyo, pale nae alipo msemesha Mtume(s.a.w.w)
kwa kusema:"Amani iwe juu yako ewe baba". Uso wa Rashiidi ukageuka na kudhihiri alama za hikidi (chuki) na uovu (shari).
Na kulifanyika mazungumzo mengi kati ya Imamu na Rashiid kuhusiana na maudhui haya, na mazungumzo yalihu-siana na kumbainisha na kumfahamu alie karibu zaidi na Mtume kati yao na mambo muhimu aliyokuwa akiyasema Rashiid katika mazungumzo hayo ni kukataa kwake na kupinga watoto watoka-nao na binti kuhesabiwa kuwa ni katika "kizazi" (dhuria) na kuhesabika kuwa ni "watoto" wa babu yao kwa sababu maneno haya mawili "dhuria" na "abnaau" (watoto) yanakusudia kizazi au watoto watokanao na waendelezao kizazi kwa upande wa baba na si upande wa mama.
Na muhtasari wa majibu ya Imamu yalikuwa kama ifuatavyo:
1- Lau kama Mtume(s.a.w.w)
angekuwa hai au angefufuka, anaweza kumchumbia binti yake Rashiid na kumuoa. Lakini asingeweza kumchumbia na kumuoa binti wa Imamu.
2- Kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo "Yeyote mwenye kukutolea hoja kuhusiana nao (Uislamu) baada ya kukujia elimu sema"Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu ". Na waislamu wote wali fahamu kuwa watoto waliotoka na Mtume kwa ajili ya maap izano walikuwa ni Hassan na Hussen watoto wa Fatuma
na Qur'an imewaita watoto "abnaau"
3- Kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo kutoka kwa Ibrahim Alkhalil (Rafiki wa Mwenyezi Mungu) "Na katika kizazi chake ni Daudi na Sulaiman na Ayyub na Yusufu na Mussa na Harun na hivyo ndivyo tuwalipavyo watu wema. Na zakaria na Yahya na Issa..". Issa nae hana baba, na Qur'ani imemuhesabu kwenye kizazi cha Ibrahim kwa sababu ya mama yake. Na yote hayo yana maana kuwa mwenye ukaribu kupitia kwa mama ni katika "Ukoo au kizazi" (dhuria) vile vile kama Qur'ani ilivyo elezea wazi.
Pamoja na matatizo aliyo kumbana nayo Imamu na jela mbali mbali alizo kuwa akihamishiwa, hakika alikuwa haiachi nafasi yoyote ipite bila kuwafundisha watu na kuwafaidisha, na kutokana na baraka za muda mchache alio kuwa huru aliweza kutuachia urithi mkubwa ambao umo kwenye vitabu vikubwa vya kiislamu.
Alifariki (Rehema na amani ziwe juu yake) tarehe sita mwezi wa Rajabu mwaka 183 h,
na kuzikwa kwenye makaburi ya makuraishi yafahamikayo hivi leo kwa jina la "Kaadhimiya" ikinasibishwa sehemu hiyo na Imamu mwenyewe.
IMAMU WA NANE
ALI BIN MUSSA
Ni maarufu kwa lakabu ya "Ar-ridhwa". Alizaliwa Madina mwaka 148.H. Alikulia kwenye zama za mtawala wa kwanza wa bani Abbas. Na akaishi kwenye machungu na maumivu yote yaliyo msibu baba yake kwenye jela na kuwekwa mahabusu. Na ukhalifa ulipo mfikia Maamun nchi zote za kiislamu kwa ujumla zilikuwa na matatizo mengi ya kimsingi yaliyo kuwa ni muhimu zaidi, kati ya hayo ni: Kudhoofu heshima ya dola baada ya mapigano ya Amini na Maamun, (Wana wa Harun Rashid) na bani Abbas pamoja na wafuasi wao kuchukizwa sana na kitendo cha Maamun kuhamishiwa mji mkuu wa ukhalifa au utawala na kupelekwa Iran na kujikurubisha kwake (Maamun) sana kwa wafursi. Kisha harakati za mapinduzi zilizo kuwa zikiongozwa na Alawiyyiin (kizazi cha Imam Ali) katika mji mtukufu wa Makka Yemen, Al-kufa, Basra na Khurasaan.
Maamun alifikiria sana jinsi ya kutatua tatizo hilo, na hakuwa na budi isipokuwa ni kumwita Imam Ridhwa kwenda sehemu iitwayo Mar'wo, na akamfikishia fikra ya kujitoa na kujiweka kando na ukhalifa kwa ajili yake pindi tu alipo kutana nae, kisha akakazania na kumsisitiza Imam kwa usisitizaji ambao hauna jinsi ya kulikimbia au kulihepa jambo hilo kuwa akubali cheo cha wilayatul ahdi (Mrithi wa ukhalifa) baada ya kukikataa cheo cha ukhalifa Lau kama Maamun angelegeza msimamo wake.
Na sababu zilizo mfanya khalifa kufanya vile ni kujiokoa kutokana na hali ya hatari iliyokuwa imefikia kwa wakati huo, na hasa mapinduzi yaliyokuwa yakifanywa au kufanyika pande zote za ulimwengu wa kiislamu, kiasi kwamba aliona kuwa kushiriki kwa Imamu Ridhwa kwenye utawala wake itakuwa ni Sababu ya mapinduzi yale kupoteza moto na kasi yake na kupunguza utetezi wa watu walio wengi kuendelea, ambao ni kuwapenda kizazi cha Ali na kuwaita watu kumuelekea Imamu Ridhwa ambae ni katika kizazi cha Muhammad.
Na sababu iliyo mfanya Imamu kukataa ni kufahamu kwake kuwa Maamun ameamua kusisitiza suala hilo kutokana na maslahi ya kisiasa yaliyokuwepo kwa wakati huo, na huenda siku za mbele akawa ni kiongozi wa harakati za kisiasa zilizo dhidi yake, au atawaweka baadhi ya Alawiyyin (watu wa kizazi cha Ali) wafanye maelewano nae na kuwasukuma kuuza dhamiri pamoja nae, na kuwa kiongozi wa mbele wa harakati zile zilizo dhidi yake.
Lakini Imamu, pamoja na kuyajua yote hayo, alikuwa akihisi taabu kuhusiana na suala hilo alilo ambiwa, kwa sababu kukataa moja kwa moja itamaanisha kuwa anakubali na kukiri kuwa hana haki ya suala lile, na kuwa hana uwezo wa kustahmili mikiki yake, kwa maana hiyo akakubaliana na fikra ya wilayatul ahdi (mrithi wa ukhalifa) ili kiwe ni kipimo cha majaribio na mtihani kwa Maamun. Basi Imamu akawa mrithi wa ukhalifa rasmi wa serikali.
Na mambo ya fitina na kuzuwa mambo ya kuwachanganya watu yakaanza kusukwa na kutengenezwa hapa na pale, kisha Imamu akafariki kwenye mazingira yenye kutatanisha yasiyo epukana na shaka na tuhuma, mambo ambayo nafasi yetu haitu-ruhusu kuyaelezea.
Ama urithi wa kielimu wa Imamu ni riwaya nyingi zinazo-patikana kwa mwenye kufanya utafiti kwenye vyanzo (vitabu) vikubwa vya kiislamu. Na kati ya urithi huo ni kitabu chake cha tiba kiitwacho "Adhahabiya" alicho kiandika kwa jina lake "Twibu Arridhwa", na Dr Swahib Zayni alikifafanua na kukishe-rehesha kwa kulinganisha kati ya madhumuni yake na mambo mengine yaliyo gunduliwa na kufahamika kwenye tiba ya kisasa na asili ya kitabu hicho ilichapishwa pamoja na sherehe yake huko Baghadad kabla ya miaka kadhaa iliyo pita.
Alifariki (rehema na amani ziwe juu yake) sehemu iitwayo Tuusi katika mwezi wa Safar mwaka 303 H
, na kuzikwa huko na hivi sasa sehemu aliyozikwa huitwa "Mash'had" kwenye mkoa wa Khorasani, huko Iran.