14
MAISHA YA ABU DHARR
Hapana shaka kwamba Abu Dharr alipata daraja la juu zaidi la imani. Alizingatia hadi dakika za mwisho za uhai wake kwamba aliapa kwa Mtume kusema kweli na bila kujali shutuma yoyote kwa ajili ya ukweli. Shah Walyullah Dehlavi ameandika kwamba katika utekelezaji kwa Mtume(s.a.w.w)
ni kwamba alichukua viapo vya uaminifu vya aina mbali mbali kutoka kwa watu mbali mbali yaani kwenda Jihad, kukataa bidaa, kuanzisha sheria za Kiislamu, na kusema kweli. (Shifau alil).
Kiapo alichochukua kutoka kwa Abu Dharr ni kusema kweli. Abu Dharr alifanya kwa mujibu wa kiapo cha uaminifu baada ya kutambua vema maana yake na kwamba asingefanya hivyo, ambapo alikwisha sadiki sana hali ambayo iliondoa shaka kwake, kwamba chochote alichofanya kililingana na Ridhaa ya Mwenyezi Mungu na nia ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
.
Kuhusiana na hilo, kamwe hakujali nguvu za serikali wala kuogopa kupata matatizo. Alistahamili kila aina ya ukandamizaji na alibeba kila aina ya usumbufu lakini hakuacha kusema kweli, hadi akafukuzwa na kupelekwa uhamishoni mara mbili. Uhamisho wa Abu Dharr wa mara ya mwisho hauna mfano wake.
Alijitolea mhanga kwa kuzuiliwa kwenye jangwa ambalo ni pweke. Bila kuzungumzia habari za nyumba ya kuishi, alifanya kivuli cha mti kuwa makazi yake. Hakuwa na mpango wowote wa chakula na makazi ambapo angepumzika au kulala. Lakini kwa ujasiri wake wa hali ya juu na azima aliokuwa nayo, Abu Dharr aliyachukua matatizo yote kwa uchangamfu kwa sababu ya kumridhisha Mwenyezi Mungu. Mke na mtoto wake wa kiume walipokufa sasa muda ulikaribia ambapo alikuwa anangojea kifo chake mwenye we akiwa kwenye sehemu pweke kama hiyo akiwa na mtoto wake wa kike tu.
Loo! Siku ya mwisho ya uhai wa Abu Dharr kwenye sehemu hiyo pweke ilikaribia. Alikuwa anasali mara nyingi na binti yake alikuwa na wasi wasi na shauku kuhusu hali ya baba yake na mwisho wake uliokuwa unakaribia. Hapakuwepo na mtu. Hapakuwepo na hata mnyama. Muda wa kuwasili malaika wa kifo ulikaribia. Muda ambao binadamu hulia na mtoto wa kike kunyang'anywa mapenzi ya baba yake.
Si tu kwamba alikuwa anaangalia kwa makini kwa kutokuwa na msaada kwa baba yake ambaye mapenzi yake yalisababisha mshtuko mara kwa mara7
7. Waandishi wengi wa historia wamehusisha tukio la kifo cha Abu Dharr kwa mke wake Umm Dhar, lakini haioneshi kuwa sahihi kwa sababu waandishi wa historia kama vile Masudi na Yaqubi, wameandika kwamba mke na binti yake Abu Dharr walikwisha fika huko Rabzah. Majilisi ametoa maelezo ya kifo cha mke wake huko Rabza kama alivyoeleza bint yake. Tabari amesema kwamba mtoto wa kike alipelekwa Madina baada ya kifo cha Abu Dharr. Bin Athir pia amekiri kuwepo kwa mtoto wa kike [135]
na hakuna hata mwandishi yeyote wa historia mwenye kuaminika ambaye ametamka kuhusu kuwasili kwa mke wa Abu Dharr Madina.
Hapa tunatoa maelezo ya historia ya hatari ya kifo cha Abu Dharr kama ilivyosimuliwa na binti yake kama ilivyoandikwa na Majlisi. Binti huyu anasema; "Siku zetu zilipita katika mateso yasiyo elezeka kwenye upweke. "Siku moja ilitokea kwamba hatukuweza kupata chochote chakula. Tulijitahidi kutafuta lakini hatukufanikiwa. Baba yangu aliyekuwa taabani akaniambia, "Binti yangu kwa nini una wasi wasi sana leo?" Nikasema, "Baba, mimi nina njaa sana na wewe unazidi kudhoofika pia kwa sababu ya njaa. Nimejaribu kujitahidi kila nilivyoweza kupata chakula ili niweze kuhisi ninaheshimika kwako lakini sikufanikiwa." Abu Dharr akasema, "Usiwe na wasi wasi.
Mwenyezi Mungu ndiye mpangaji mkuu wa mambo yetu." Mimi nikasema, "Baba! Ni sawa lakini hakuna kitu chochote sasa ambacho kinaweza kukidhi mahitaji yetu."
Akasema; "Binti yangu! Nishike bega langu na unipeleke hapa na pale. Labda tunaweza tukapata chochote huko." Nilimshika mkono wake na tukaanza kwenda kuelekea upande alikonielekeza. Wakati tupo njiani baba yangu aliniambia nimkalishe chini. Nikamketisha kwenye mchanga wenye joto. Akakusanya mchanga na akalaza kichwa chake juu ya mchanga huo.
Mara tu alipolala chini, macho yakaanza kuzunguka na akahisi uchungu wa kifo. Nilipoona hivi nikaanza kulia kwa sauti kubwa sana. Akajikaza kidogo na akasema, "Kwa nini unalia, binti yangu?" Nikasema, "Nitafanya nini baba yangu? Hapa ni jangwa na hakuna mtu yeyote. Sina sanda ya kukuvesha na pia hakuna mtu wa kuchimba kaburi hapa. Nitafanya nini mauti yakikufika hapa kwenye sehemu hii pweke."
Akalia baada ya kuona jinsi nilivyokuwa sina jinsi ya kuwa na msaada wowote na akasema, "Binti yangu! Usiwe na wasi wasi. Huyo rafiki yangu ambaye kwa ajili ya kumpenda yeye na watoto wake ninavumilia matatizo yote haya, aliniambia kuhusu tukio hili mapema, Sikiliza, Ewe bint yangu mpendwa Alisema mbele ya kundi la masahaba wake wakati wa Vita ya Tabuk kwamba mmojawao angekufa lakini jangwani na kundi la masahaba wangekwenda kwenye maziko na mazishi yake. Sasa hakuna hata mmoja wao aliyehai isipokuwa mimi. Wote wamekufa wakiwa kwenye sehemu zenye watu. Ni mimi tu niliye baki na pia nipo kwenye upweke wa pekee. Kamwe sijapata kuona jangwa la aina hii ambapo nimelala sasa na mwenye uchungu wa kifo. Binti yangu mpendwa! Nikifa nifunike joho langu na ukae kwenye njia inayoelekea Iraq. Kundi la watu waumini watapita hapo. Waambie kwamba Abu Dharr sahaba wa Mtume(s.a.w.w)
amekufa. Kwa hiyo tafadhalini tayarisheni mazishi yake."
Alikuwa anazungumza na mimi wakati malaika wa kifo alipofika na kumtazama uso wake. Baba yangu alipomtazama uso wake ukawa mwekundu na akasema, "Ewe Malaika wa Kifo! Umekuwa wapi hadi sasa? Nimekuwa ninakungojea wewe. Ewe rafiki yangu! Umekuja wakati ambapo mimi ninakuhitaji sana. Ewe Malaika wa kifo! Na asiokolewe mtu asiyefurahi kuonana na wewe. Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nichukue haraka sana na unipeleke kwa Mwenyezi Mungu mwenye Huruma sana ili niweze kupumzika na matatizo ya dunia hii."
Baada ya hapo alimwambia Mwenyezi Mungu, "Ee Msitawishaji wangu! Ninaapa Kwako Wewe, na Unajua kwamba ninasema kweli kwamba kamwe sikuchukia kifo na kila mara nilitamani kukutana na wewe."
Baada ya hapo jasho la kifo likatoka kwenye uso wa baba yangu na aliponitazama, aligeuza uso wake na kuiaga dunia daima milele. Sisi tunatoka kwa Mwenyezi Mungu na Kwake tutarejea."8
Binti yake Abu Dharr aliendelea, "Baba yangu alipokufa nilianza kulia huku ninakimbia kuelekea kwenye njia inayoelekea Iraq. Nilikuwa nimeketi pale nikangojea kundi la watu linalokuja. Ghafla nilikumbuka kwamba maiti ya baba yangu ilikuwa haina mtu wa kuiangalia. Kwa hiyo, nilikimbia hadi ilipokuwa maiti. Tena nikarudi kwenye njia isije kundi likapita bila kulitaarifu. Kwa hiyo, ikawa ninakwenda kwenye maiti na kurudi njiani, mara kadhaa.
Sasa, ghafla nikawaona watu wanakuja wakiwa wamepanda ngamia. Walipokaribia, nikawaendea huku nikilia na kutokwa na machozi na nikawaambia; "Enyi masahaba wa Mtume! Sahaba wa Mtume amekufa." Wakaniuliza sahaba huyo ni nani?" Nikajibu; "Baba yangu, Abu Dharr Ghifari."
Mara waliposikia waliteremka kutoka kwenye ngamia na wakafuatana na mimi huku wakilia. Walipofika hapo wakalia sana kuhusu kifo chake cha kuhuzunisha na wakashughulikia ibada ya mazishi yake.
Mwandishi wa historia Atham Kufi, amesema kwamba kundi la watu waliokuwa wanakwenda Iraq, alikuwepo; Ahnaf bin Qays, Tamimi,
8. Imetamkwa kwenye masimulizi ya kwamba Abu Dharr hakuhisi uchungu wowote wa kifo, na uhalali wake ulithibitika kwa sababu uchungu wa kifo anauhisi yule tu ambaye matendo yake yalikuwa ya kuchukiza au ambaye amefanya kitu ambacho kumbukumbu yake katika maisha husababisha kizuizi kwa roho kutoka. Mathalani Aishah alipohisi mateso makubwa alipokuwa kwenye uchungu wa kukata roho na alianza kupumua kwa nguvu sana watu wakamuuliza, Ewe Mama wa Waumini! Kwa nini imekuwa hivi? Nini kinachokusumbua" Akajibu, Vita vya Ngamia vinasonga roho (Rauzatul Akhyar anasimulia kutoka kwenye Rabiul Abrar).
Sasaah bin Sauhan al-Abdi, Kharijah bin Salat Tamimi, Abdulah bin Muslimah Tamimi, Halal bin Malik Nazle, Jarir bin Abdullah bajali, Malik bin Ashtar bin Harith na wengineo. Watu hawa walimkosha Abu Dharr na wakafanya mpango wa kumvisha sanda. Baada ya mazishi Malik bin Ashtar alisimama pembeni mwa kaburi na akatoa hutuba ambapo ilirejea mambo ya Abu Dharr na kumwombea yeye. Baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu Mweza wa yote akasema"
"Ee Mwenyezi Mungu! Abu Dharr alikuwa sahaba wa Mtume Wako na muumini wa Vitabu Vyako na Mitume Wako. Alipigana kishujaa sana katika njia Yako, alikuwa, mfuasi imara wa sheria Zako za Kiislamu na kamwe hakubadilisha au kugeuza amri yoyote miongoni mwa amri Zako.
Ee Mola wangu Mlezi! Alipoona ukinzani unafanywa dhidi ya Kitabu na Sunna akapiga kelele na kuwa tahadharisha wahusika kwa umma ili wajirekebishe, matokeo yake wakamtesa, wakamhamisha kutoka sehemu moja hadi nyingine, wakamfedhehesha, wakamhamisha kutoka katika nchi ya Mtume Wako mpendwa na kumweka kwenye matatizo makubwa sana. hatimaye amekufa akiwa katika hali ya upweke kabisa sehemu ambayo hawaishi watu.
Ee Mwenyezi Mungu! Mpe Abu Dharr sehemu kubwa ya hizo neema za mbinguni ambazo Umewaahidi waaminio na umlipe kisasi yule ambaye amemfukuza kutoka Madina na umpe adhabu kamili anayostahiki."
9. Upo uwezekano kwamba matokeo ya laana hiyo Uthman aliuawa baadaye kwa mfano wake. Historia inasema kwamba mwili wake ulilala juu ya lundo la kinyesi kwa muda wa siku tatu na mbwa walikula mguu wake mmoja. (Tarikh Atham Kufi).
Baada ya mazishi ya Abu Dharr watu waliondoka Rabzah lakini mwanae wa kike aliendelea kukaa hapo kufuatana na wasia wake. Baada ya siku kadhaa, khalifa Uthman alimwita na akampeleka kwao.
Malik Ashtar alimwombea Abu Dharr kwenye hotuba yake na wote wale ambao walikuwepo hapo na akasema, "Amini" (Na iwe hiyo). Hata hivyo, walipokamilisha ibada ya mazishi ilikuwa jioni na wakawa hapo hadi asubuhi. Wakaondoka asubuhi siku iliyofuata."
Hata hivyo bint yake Abu Dharr ambaye aliendelea kukaa hapo Rabzah kwa muda wa siku chache zaidi. Siku moja usiku alimuona Abu Dharr kwenye ndoto ameketi na anakariri Qurani Tukufu. Akasema, Baba! Nini kimekutokea na umerehemewa kwa kiwango gani na Mwenyezi Mungu ambaye ni Mwingi wa Rehma? Akasema, Ewe binti yangu! Mwenyezi Mungu amenizawadia upendeleo usio na mipaka, amenipa starehe zote na amenipa kila kitu. Ninafurahia sana ukarimu Wake. Ni wajibu wako kujishughulisha na kumuabudu Mwenyezi Mungu kama kawaida na usiruhusu aina yoyote ya maringo na kiburi kuja kwako."
Wasomi na waandishi wa historia wanakubaliana kwamba Abu Dharr alikufa tarehe 8, Zilhajjah, 32 A.H, Rabzah. Alikuwa na umri wa miaka 85.
SURA YA ISHIRINI NA MOJA
Baada ya kupata mateso ya kugandamizwa na matatizo mfululizo na mfuatano wa kuhamishwa kutoka kwa watu wenye fikra za kidunia, Abu Dharr aliiacha dunia hii ya muda mfupi akiwa Rabzah. Lakini hadith ya mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu bado inaendelea kuishi hadi daima milele. Historia imejaa mifano, ukweli na hotuba zake zilizowazi na kuaminika zitaendelea kusikika kwenye nyoyo za waumini. Abu Dharr bado yu hai kupitia kwa tabia yake hata baada ya kifo chake; na ataendelea kuwa hai kupitia kwa kanuni alizozishikilia sana.
Dunia inatambua kwamba Abu Dharr alikufa katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Aliteseka kwa matatizo na dhiki kwa ajili ya kutetea ukweli na kuanzisha na kutangaza kanuni za Uislamu katika Nchi za Kiislamu. Lakini inasikitisha kuona kwamba dhalimu hataki kutubu kwa udhalimu wake. Tunatoa maelezo ya tukio hili hapa kwa maneno ya mfasiri wa 'Hitoria' yaliyoandikwa na Muhammad bin Ali bin Atham Kufi, mwandishi wa historia wa karne ya 3 Hijiriya. Ameandika;
Habari za kifo cha Abu Dharr zilipomfikia Uthman, Ammar bin Yasir alikuwepo hapo. Ammar akasema; "Mwenyezi Mungu amhurumie Abu Dharr. Mwenyezi Mungu! Uwe shahidi kwamba tunaomba kwa nyoyo na roho zetu umhurumie yeye. Ee Mwenyezi Mungu umsamehe."
Mara tu khalifa aliposikia akakasirika na akasema, "Ewe mpumbavu! Na wee utakutana na hatima ya aina hii hii. Nisikilize! Sioni aibu kwa sababu ya kumhamisha Abu Dharr na kifo chake cha upwekeni." Ammar akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, hii haitakuwa sababu ya mwisho wangu."
Khalifa aliposikia hivi akaagiza wafanya kazi wake wa baraza, "Msukumeni nje, mhamisheni hapa Madina na mpelekeni sehemu hiyo hiyo ambako Abu Dharr alipelekwa Yeye pia aendeshe maisha ya aina ile ile na msimruhusu arudi Madina almradi bado nipo hai."
Ammar akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Napenda zaidi kuwa jirani na mbwa mwitu na mbwa kuliko kuwa karibu na wewe." Baada ya kusema hivyo alinyanyuka na kuondoka hapo na akaenda kwake.
Khalifa alipoamua kumpeleka Ammar huko Rabzah na taarifa ikalifikia kabila lake la Bani Makhzum, wakakasirika. Wakasemezana wao kwa wao kwamba Uthman alikwisha chupa mipaka ya uadilifu. Baada ya hapo walikaa kikao cha baraza na wakafikiria kwamba ingekuwa bora endapo kabla ya kuchukua hatua yoyote jambo hili lisuluhishwe kwa maelewano. Wakiwa na lengo hili katika maoni yao, walikwenda kumuona Ali. Ali akawauliza, kwa nini nyinyi wote mmenijia wakati kama huu? Wakasema, "Lipo tatizo kubwa linatukabili, khalifa ameamua kumfukuza Ammar kutoka Madina kwenda Rabzah. Uwe mwema kiasi cha kutosha, uende kwa khalifa na umsihi kwa maneno yenye busara amwache Ammar kama alivyo na asimfukuze kutoka jijini, vinginevyo ghasia ya aina hiyo inaweza kuanzisha vurugu ambayo itakuwa si rahisi kuizima."
Imamu Ali aliwasikiliza, akawaliwaza na akawaomba wasifanye haraka. Akawaambia, "Nitakwenda nijaribu kusuluhisha jambo hili. Ninao uhakika litasuluhishwa kwa makubaliano. Ninatambua vema hali hii. Nitamfikisha pale kwenye fikra yenu."
Baada ya mazungumzo haya, Ali alikwenda kwa khalifa Uthman na akasema, " Ewe Uthman! Kuna mambo mengine unayafanya haraka na unadharau ushauri wa marafiki na washauri. Wakati fulani ulimfukuza Abu Dharr Madina. Alikuwa Muislamu Muadilifu sana, sahaba mashuhuri wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na muhajirina bora sana. ulimpeleka Rabzah ambako alifariki katika hali ya upweke. Kwa sababu ya tukio hili, Waislamu sasa tayari wamekugeuka, hawako na wewe. Sasa ninasikia kwamba umeamua kumfukuza Ammar kutoka Madina. Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu usiwape usumbufu wa aina hii masahaba wa Mtume(s.a.w.w)
na waache waishi kwa amani." Uthman aliposikia hivi akamjibu Ali kwa hasira; "Wewe ndiye unayetakiwa kufukuzwa kwanza kutoka hapa jijini kwa sababu ni wewe ndiye unayemharibu Ammar na wengine."
Ali aliposikia maneno haya yasiyofaa, akassema; "Ewe Uthman! Unawezaje kudiriki kunifikiria mimi namna hii? Hutaweza kufanya jambo hili hata kama unatamani kulifanya na kama unatilia mashaka maneno yangu, jaribu kufanya hivyo. Hapo ndipo utakapotambua hali halisi ya mambo na ndipo utakapotambua ni nani hasa unaokabiliana nao. Na sasa unasema kwamba mimi ninamharibu Ammar na wengine. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, vurugu hii inatoka upande wako. Sioni kama watu hawa wana dosari yoyote. Unafanya matendo ambayo ni kinyume cha dini na maadili mema. Watu hawatayavumilia, na sasa wanaanza kukupa kisogo, na wewe huwezi kuvumilia mambo haya. Unahisi unakosewa na kila mtu na halafu unawasababishia matatizo. MsImamuo huu upo mbali sana na vile walivyofanya wazee wetu." Baada ya maneno haya akanyanyuka na kuondoka hapo.
Watu wa Bani Makhzum walipokwenda kwa Ali kutaka kujua khalifa alimwambia nini kuhusu suala lao, Ali aliwaambia, "Mwambieni Ammar asitoke nje ya nyumba yake.
Mwenyezi Mungu atamkomboa kutoka kwenye mbinu za hila." Khalifa pia alipata taarifa ya mazungumzo haya kupitia kwa mtu mwingine na akaacha kumfukuza Ammar. Zayd bin Thabit akamwambia Uthman, "Endapo khalifa anataka hivyo tunaweza kwenda kwa Ali na kubadilishana mawazo naye kwa lengo la kuondoa hali ya kutoelewana ambayo imejitokeza na uelewano uendelee kama kawaida." Khalifa akasema; "mnao uhuru wa kufanya hivyo."
Zayd bin Thabit na Mughyrah bin Ahnas Thaqafi walikwenda kwa Ali, wakamsalimia na wakaketi. halafu Zayd bin Thabit alianza kumsifu Ali na akasema, "Hapana mtu yeyote hapa duniani ambaye anao ukaribu huo, undugu, daraja na heshima kwa Mtukufu Mtume
kama wewe ulivyo. Hapana mtu yeyote anaweza kulingana na wewe katika kuunga mkono Uislamu na kuwa mtu wa kwanza kuwa Muislamu. Wewe ni chemchem ya uadilifu na chanzo cha ukarimu."
Baada ya wasifu huu Zayd bin Thabit akasema lengo lake hasa lililompeleka kwake na akasema; "Ewe Ali bin Abi Talib! Tulikwenda kwa khalifa Uthman. Ametoa aina fulani ya malalamiko dhidi yako, na amesema kwamba wakati mwingine unapinga matendo yake na unaingilia mambo anayotaka kuyafanya. Kwa hiyo, ili maudhi na kero zilizopo kati yenu ziondolewe kwani hiyo itakuwa ni furaha na shangwe kwa Waislamu wote."
Ali akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa kadiri nilivyoweza. Sikupinga kitu chochote wala sikuingilia jambo lolote. Lakini, sasa, mambo yamekuja kwenye kiwango ambacho haiwezekani kuonesha uvumilivu au kunyamaza. Nilimwambia ukweli kuhusu Ammar jambo ambalo lilimaanisha ustawi wake Uthman, uswalama na manufaa yake mwenyewe. Nilifanya kazi yangu na sasa shauri yake kufanya apendavyo."
Aliposikia hivi Mughyrah bin Ahmad akasema; "Ewe Ali! Unatakiwa kukubaliana na hayo anayoyasema au anayoyataka kufanya Khalifa hata kama unasadiki moyoni mwako au hapana. Unatakiwa kufikiria kwamba utiifu kwa amri zake ni muhimu kwa sababu yeye anaoudhabiti juu yako na wewe huna udhibiti juu yake. Ametutuma kwako kwa sababu anataka tu tushuhudie yale unayoyasema na baada ya hapo, anaweza akasema lolote kuwa kosa."
Aliposikia maneno ya Mughyrah, Ali alikasirika na akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, yule nnaye muunga mkono, kamwe hataheshimiwa na yule ambaye mna mfukuza kamwe hatapumzika. Ondoka nenda zako."
Mughyrah alipatwa na bumbuwazi kwa yale aliyoyasema Ali na hakuweza kusema, "Ewe Ali! Mughyrah amesema upuuzi. Amesema mambo haya kufuatana na anavyotaka mwenyewe. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, hatukuja kwako kwa ajili ya kushuhudia wala si nia yetu kukukosoa wewe au kupinga yale unayoyasema. Tulitaka tufungue mlango wa maelewano na mapatano na kwamba hiyo ndio sababu iliyotuleta hapa. Tunakuomba ufikirie jambo hili." Ali akaonesha ridhaa yake na Zayd bin Thabit akarudi.
Imesimuliwa hapo juu jinsi Ali alivyopinga mwenendo wa Uthman. Bila shaka kuchupa mipaka kwa Uthman, iliwafanya masahaba wa Mtume(s.a.w.w)
kuwa na wasi wasi na kusumbuka sana. Tayari walikwisha mkasirikia Uthman waliposikia mateso ya Abu Dharr. Mkasa huu ulisababisha hasira kubwa miongoni mwa Waislamu wa matabaka yote. Kwa hiyo, watu walianza kumkosoa Khalifa kibinafsi na kwa makundi.
Kuhusu suala hili, Zubayr bin al-Awam, sahaba wa Mtume alikwenda kwake na akasema, "Hivi Umar alichukua ahadi kwako kwamba hungewapachika watoto wa Abi Muit kwa watu?" Khalifa akasema, "Ndio, alichukua ahadi hiyo kutoka kwangu." Zubayr akasema, "Kwa nini ulimteua Walid bin Uqbah Gavana wa Kufah?" Khalifa akasema, "Nimefanya hivyo kama Umar alivyompa Ugavana wa Kufah Mughayrah bin Shubah. Kama mambo yalivyo, nilikwisha mteua kuwa gavana wa kufah lakini tabia yake ilipogeuka na kuwa kinyume na Uislamu, yaani akaanza kunywa mvinyo na kuzini, nilimwondoa na kumweka mtu mwingine kushika nafasi yake." Halafu Zubayr akasema, kwa nini ulimteua Muawiyah kuwa Gavana wa Syria kwa mujibu wa maoni ya Umar bin Khatab kwa sababu kabla yangu ni yeye ndiye aliyemteua Muawiyah kuwa Gavana wa Syria." Tena akauliza, "Kwa nini uliwakemea masahaba wa Mtume, ingawa wewe si bora kuliko wao kwa namna yoyote ile?" Uthman akasema,
Sikukusema wewe kwa ubaya. Kwani unajali nini ikiwa niliwakaripia wengine?"
Halafu akauliza, Kwa nini ulisema kwamba kukariri nakala ya Quran Tukufu ya Abdullah bin Masud ni vibaya, ambavyo alijifunza kukariri Qurani Tuklufu kutoka kwa Mtume Zaidi ya hayo, kwa nini ulimgandamiza? Ukaagiza apigwe hadi akapoteza fahamu." Khalifa akasema, "Alikuwa na desturi ya kusema maneno ambayo hayangevumiliwa." Akauliza tena, "Kwa nini ulimpiga mateke Ammar bin Yasir na kwa agizo lako akapigwa sana hadi akapata maradhi ya henia?" Uthman akasema, "Kwa sababu alikuwa na desturi ya kuwachochea watu waniasi mimi."
Zubayr akamuuliza tena, kwa nini ulimhamisha Abu Dharr na ukamtupa mahali ambapo penye upweke na hakuna hata mti. Mtu alikufa katika hali ya kukata tamaa kwa kutokuwa na msaada. Ewe Uthman! Hukuwa unatambua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimfanya kuwa rafiki yake mkubwa, na akasema kwamba hapana mtu aliye mkweli zaidi ya Abu Dharr kati ya mbingu na dunia? Hukuwa unajua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuwa anastahamili kuwa mbali naye na wakati wowote walipokuwa hamuoni alitoka kwenda kumtafuta Abu Dharr?" Uthman bin Affan akajibu, "Alikuwa anawachochea watu wa Syria waniasi, alikuwa ananikashifu na alikuwa anafichua mapungufu yangu kwa watu." Halafu Zubayr akauliza, "Kwa nini ulimfukuza Malik Ashtar na masahaba wake kutoka Kufah na kwa nini uliwatenganisha na familia zao?" Uthman akasema, "Walikuwa wanasababisha vuruga Kufah na hawakumtii Gavana wangu Said bin Aas." Zubayr bin Awam akasema, Ewe Uthman matendo yako si halali. Hukuwa unafikiri na kujua ni nani hao uliokuwa unawachukulia hatua kama hizo. Mambo uliyoyataja hayakuwa sababu ya kuwafanyia mateso kama hayo masahaba wa Mtume walio heshimiwa sana.
Ewe Uthman! Endapo utaniruhusu, nitakutajia matendo yako yaliyokiuka mafundisho ya imani. Ninasisitiza kwamba umuogope Mwenyezi Mungu na usijitenge kwa sababu ya serikali ya Kiislamu ambayo wewe ni kiongozi, vinginevyo siku utakapopata malipo ya matendo yako hapa duniani, wala haipo mbali. Adhabu hii itakuwa nyongeza ya adhabu utakayopata Akhera."