9
MAISHA YA ABU DHARR
Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbab, wakati wa kifo chake, Mtume alimwambia mwanawe Fatimah Zahra awaite wanawe wa kiume. Aliwapeleka mbele yake. Wajukuuu hao wawili, waliketi karibu na babu yao baada ya kumpa heshima yake na walipomwona yupo katika maumivu makubwa ya ugonjwa, walilia sana hivyo kwamba watu waliowaona nao pia wakaanza kulia. Hasan aliweka uso wake kwenye uso wa Mtume na Husein aliweka kichwa chake kwenye kifua chake. Mtume alifungua macho na akawatazama kwa huba, akawapapasa kwa mahaba, na akaonesha utashi wake kwa watu kwamba wanastahili kuheshimiwa na kunyenyekewa. Pia ipo Hadith kwamba baada ya kumsikia Husain analia, wote wale waliokuwa hapo walianza kulia na alipowasikia Mtume pia alianza kulia. Halafu akaagiza ndugu yake mpendwa, Ali aende kwake, Ali alikwenda na akaketi kuelekea kichwa cha Mtume. Aliponyanyua kichwa chake, Ali alikuwa anasogea karibu naye, alikiweka kichwa cha Mtume kwenye mkono wake. Mtume akasema, "Ali! Nimekopa kiasi hiki cha deni kutoka kwa Myahudi fulani kwa ajili ya vifaa vya jeshi la Usamah. Mlipe kiasi hicho cha fedha. Ewe Ali! Utakuwa mtu wa kwanza kuja kwangu kwenye Haudhi ya Neema na utapata matatizo makubwa baada yangu. Yakabili matatizo hayo kwa uvumilivu na utakapoona kwamba watu wamechagua dunia, wewe shughulikia mambo ya akhera."
Pia imeandikwa kwenye Madarijun Nubuwah kwamba Fatimah Zahra lipata mshituko mkubwa kwa sababu ya kifo cha Mtume na alilia sana kwa uchungu. Muhadithi Dehlavi ameandika kwenye kitabu 'Ma thabatabis Sunnah" kwamba matukio mengi ya hatari yalitokea baada ya kifo cha Mtume. Ameyataja kwenye shairi akisema kwamba endapo matatizo ambayo yalimpata, yangeipata mchana ungegeuka kuwa usiku wa giza. Mwandishi wa Rauzatul Ahbah anasema kwamba baada ya kifo cha Mtume hakuna mtu aliyemwona anacheka.
Tabaqatcha bin Sad ameandika kwamba kichwa cha Mtume kilikuwa kwenye paja la Ali wakati wa mwisho wa uhai wake. Hakim anasema kwenye Mustadirak kwamba Mtume kabla hajakata roho alipitisha siri kwa Ali na alitatua matatizo yake ya kimuujiza.
Abdul Barr kwenye kitabu chake, Istiab amemnukuu Abdullah bin Abbas akisema, "Ali anazo sifa nne za aina hiyo na hakuna miongoni mwenu aliye nazo. Kwanza, Alikuwa mtu wa kwanza kupata heshima ya kuswali na Mtukufu Mtume. Pili, alikuwa ndiye mshika bendera pekee wa Mtume katika kila vita. Tatu, ambapo wakati wa vita vitakatifu wakati mwingine watu walikuwa wanakimbia kutoka kwenye uwanja wa vita na kumwacha Mtume nyuma, Ali alikuwa imara kuwa pamoja na Mtume. Nne, Ali ni mtu aliyeiosha maiti ya Mtume na kuizika kaburini."
Kwa mujibu wa imani ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, Mtukufu Mtume alifariki siku ya Jumatatu terehe 28 ya mwenzi wa Safar (machi), 11A.H. (Muwaddatul Qurba), uk. 49 kimechapishwa
Bombay, 1310 A.H). Baada ya kifo chake palikuwepo na masikitiko na kilio miongoni mwa watu wa nyumba yake na masahaba walioheshimiwa. Abu Dharr, Salman, Miqdad, Ammar na masahaba wengine waaminifu walikuwa wanalia sana. Kwa ufupi alikuwa kama rafiki mpenzi aliyekuwa na masikitiko kando yake. Historia inaonyesha kwamba Abu Dharr Ghifari alikuwa na maono ya kudumu kuhusu msiba huu. Manazir Aksan Gilan ameandika, "Kwenye maelezo mengi ya maisha ya Abu Dharr japokuwa dalili za wazi zinaonekana za maumivu hayo ambayo bila ya kuwepo muumini anakuwa si muumini, hata hivyo yapo matukio kadhaa ya kutia moyo ambayo yanadhihirisha taswira nzuri ya uhusiano wa wote wawili yaani anayependa na anayependwa katika macho ya akili zetu."
Wakati Mtukufu Mtume anakata roho, Abu Bakr alikuwa nyumbani kwake, Sakh, umbali wa maili moja kutoka Madina. Umar alizuia taarifa ya kifo isienee na Abu Bakr alipofika wote wawili walikwenda Saqifah Banni Saidah iliyopo maili tatu kutoka Madina, na pamoja nao pia alikuwa Abu Ubaydah bin Jarrah ambaye kazi yake ilikuwa mwosha. Vyovyote vile, masahaba wakuu wa Mtume walikwenda kuungana na kugombea Ukhalifa na kuacha maiti yake, na Ali alifanya mpango na akamudu mambo ya kuosha maiti ya Mtume na maziko. Ali aliosha maiti, Fazal bin Abas alinyanyua kaptura yake, Abbas na Qathm walimgeuza na Usamah na Shaqran walimwagia maiti maji. Baada ya maiti ya Mtume kuoshwa, ilivishwa sanda. Abu Talhah alichimba kaburi. Ali, aliongoza Swala ya kumsalia maiti na yeye ndiye aliyeingia kaburini na kuilaza maiti inavyo stahili mahali pake. Baadda ya hayo, alifukia kaburi kwa masikitiko makubwa. Abu Bakr na Umar na wengineo hawakushiriki matayarisho ya maziko yaani kuosha maiti, kuvesha sanda kusalia hadi kushusha maiti ndani ya kaburi, na kufukia kaburi la Mtukufu Mtume. Kwa sababu waliporudi kutoka Saqifah, Mtume alikwisha zikwa.
Mtukufu Mtume alikuwa na umri wa miaka 63 alipotawafu.
SURA YA KUMI
Baada ya kifo cha Mtume, wale masahaba ambao hawakuridhika kwa kitendo chake cha Ghadir Khum ambao walimpinga Ali, haraka sana walikusanyika Saqifah Bani Sadah mahali ambapo palitayarishwa maalumu kwa mashauriano yasiyofaa (Ghayathul Lughaat) na watu wachache wapatao 200 ambao walikuwemo Muhajirina na Ansar waliokubali na wasikubali walikuwemo, walianzisha msingi wa serikali ya mtu binafsi. Aliporudi Madina kutoka Saqifa, baada ya maziko ya Mtume, walianza kudai kiapo cha utii kutoka kwa watu kwa lengo la kupatia serikali hiyo ya kibinafsi sura ya pamoja na aina ya kidemokrasia. Ili kukamilisha lengo hili walionesha tabia ambayo katika ubinadamu wa kawaida inatetemesha si tu kwa masahaba wa kuheshimiwa lakini pia kwa Ahlul-Bait.
Kiini hasa cha hadithi hiii inayoumiza ya kipindi hiki ni kwamba, Ali alilazimishwa kutoa kiapo cha utii (Rauzatul Ahbab) na alipokataa, jeshi la Khalifa lilimpeleka mahakamani, huku shingo yake ikiwa imefungwa kwa kwamba (Bin Abil Hadid Motazali). Nyumba ya Fatimah ilichomwa moto (Tarikh Tabari, Tarikh al-Imamuah wa as-Siyasah Miratul Uqul) Mlango wa nyumba ulimwangukia Fatimah na kusababisha kuharibika kwa mimba ya mtoto wake wa kiume.(al-Milal wan Nahl of Shahristani). Allamah Mukkah Muin Kashifi ameandika kwamba Fatimah aliugua kwa sababu ya mshtuko wa tukio hili, na hatimaye alifariki.
Halafu wale watu ambao walikataa kula kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr walilazimishwa kwa ukali, na wengine walipigwa sana. Salman Farsi ambaye Mtume alikwisha mjumuisha kwenye Ahlul Bait wake, pia alikuwa mmoja wapo wa majeruhi wa udikteta wao. Alipigwa sana hivyo kwamba shingo yake ilitenguka na hali hiyo ilidumu hadi kifo chake.
Majina ya wale waliokuwepo Madina na ambao walikataa kula kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr yameorodheshwa chini: Imamu Ali, Abu Dharr, Salman Farsi, Ammar bin Yasir, Miqdadi bin al-Aswad Khalid bin Said, Burayda Aslami, Ubay bin Kab, Huzayma bin Thabit, Suhayl bin Harrif, Uthman bin Hanif, Abu Ayyub Al-Ansari, Hudhayfa bin al-Yamani, Sad bin Ubaydah, Qays bin Sad Abdullah bin Abbas, Abbas bin Abdul Muttalib, Abdul Haytham bin Tayhan, Jabir bin Abdullah, Abdullah bin Thamit, Ubaydah bin Thamit, Abu Said Khidri. [31]
Imeandikwa kwenye ukurasa wa 43 wa kitabu hicho hicho (Tabsaratul Awam) kwamba baada ya siku chache Sad bin Ubaydah alipigwa mshale na akafa kwa sababu ya kukataa kwake kutoa kiapo cha utii.
Vyovyote vile uhuni huu wa kisiasa uliendelea baada ya kifo cha Mtukufu Mtume. Waandishi wa historia wameandika kwamba kiunga cha Fadak, rasilimali ya Ahlul bait kilinyang'anywa kwa sababu tu ya kukataa kutoa kiapo cha utii. Watu hawa walisema kwamba Ukhalifa ni haki isioondolewa kwa Ali na lazima apate. Maelezo marefu ya madai haya bado yapo kwenye hotuba ya Ali ya Shiqthiyyah iliyopo kwenye Nahjul Balaghah. Ali amesema wazi kwamba Ukhalifa ilikuwa haki yake ambayo iliporwa kutoka
kwake. Pia amesema jaribio lake la kuanzisha madai yake kama inavyoonekana kwenye ukurasa wa 231 katika kitabu cha an-Nihayah cha bin Athir. Sasa tunanukulu kutoka kwenye Tarikhi Ahmadi kuhusu msiba wa tukio hili la maangamizi ambalo liliwatokea Ahlul-Bait na masahaba waaminifu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume, hivyo kwamba msomaji aweze kujua nini kilitokea baada ya yote kwa uzao wa Mtume na masahaba wake waaminifu majuma mawili tu baada ya kifo cha Mtume na Abu Dharr aliwajibika vipi kwa hali mambo yalivyokuwa.
Kwa mujibu wa Tarikh bin Jasir, Umar alikuwepo wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume lakini Abu Bakr hakuwepo. Alikuwa kwenye kijiji kiitwacho Sakh. Mtume alipokufa, Umar alisema, "Kufuatana na dhana ya wanafiki, Mtume ametawafu, lakini ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba yu hai."
Kwa mujibu wa al-Milal wan Nihal cha Shahristani, Umar alitishia kumuua kwa upanga wake endapo mtu anasema Mtume ametawafu. Tukio hili pia limeandikwa kwenye vitabu vingine.
Kwa mujibu wa Rauzatul Alhbab watu walianza kuwa na shaka kuhusu kifo cha Mtume waliposikia tishio hili la Umar. Wakati huo, Abu bakr alikuwa nyumbani kwake Sakh. Alipopewa taarifa ya kifo cha Mtume haraka sana alikwenda Madina na alipofika kwenye msikiti wa an-Nabi aliona kwamba watu walikuwa katika ghasia nyingi.
Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Abu Bakr alipoona hali hii ya watu, akakariri Aya ifuatayo: "Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma?
(Qurani 3:144).
Waliposikia hivi watu wakasadiki kuhusu kifo cha Mtukufu Mtume. Baada ya hapo watu wote waliondoka kwenda Saqifah Bani Sadah.
Kwa mujibu wa Tarikh Bin Khaldun, baada ya kufika Saqifah Abu Bakr alisema, "Sisi ni sahaba na ndugu wa Mtume na kwa hiyo tunastahili zaidi kudai Ukhalifa wa Mtume kuliko mtu mwingine yeyote."
Kwa mujibu wa Tarikh Tabari cha Bin Jarir, Umar alimwambia Abu Bakr; "Nyoosha mkono wako ili niweze kutoa kiapo cha uaminifu kwako" Abu Bakr alisema, "Hapana; wewe ndiye unyooshe mkono kwa sababu katika kila hali wewe ni mwenye uwezo zaidi kuliko mimi." Pambano hili liliendelea kwa kipindi fulani. Hatimaye Umar aliunyoosha mkono wa Abu Bakr na akatoa kiapo cha uaminifu kwake na pia alisema, "Pia uelewe kwamba nguvu zangu zimeunganishwa."
Kwa mujibu wa Tarikh Kamil cha Bin Athir, Umar na watu wengine waliapa kuwa waaminifu kwa Abu Bakr, lakini Ansar wote au baadhi miongoni mwao walisema, "Hatutatoa kiapo cha uaminifu kwa yeyote isipokuwa Ali."
Kufuatana na Tarikg Khamis, wakati Abu Bakr alipomaliza kazi ya kupokea viapo, aliondoka Saqifa na kwenda Msikiti wa Nabi na akaketi kwenye mimbari. Hapa, pia, aliendelea kupokea viapo hadi mwisho wa siku na watu walishindwa kuhudhuria mazishi ya Mtukufu Mtume. Ilikuwa siku ya Jumanne usiku.
Kwa mujibu wa Kanzul Ummal imesimuliwa na Urwa kwamba Abu Bakr na Umar hawakuwepo kwenye mazishi ya Mtukufu Mtume, lakini walikuwepo kwenye kundi la Ansari (huko Saqifa bani Sadah) na Mtume alizikwa kabla ya kurudi kutoka huko.
Kwa mujibu wa Nihayah cha Bin Athir Jazari, Majma al-Bidar cha Mulla Tahir Qutni na al- Milal wa Nihal cha Shahristani, baadaye Umar alisema kwamba kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr ni jambo lililotegemewa lakini Mwenyezi Mungu alitunusuru kutoka kwenye uovu wake.
Kufuatana na Tarikh Abu Fida kundi la Bani Hashim na pia Zubayr bin al-Awam, Miqdadi bin Amr, Salman Farsi, Abu Dharr, Ammar al-Yasir, Bara bin Azib na wengine waliokuwa upande wa Ali, walikaa pembeni wakati wa kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr.
Imeandikwa kwenye Istiab cha Abdul Barr kwamba wakati kiapo cha uaminifu kilikuwa kinatolewa kwa Abu Bakr, Ali hakuapa uaminifu kwake na alikaa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa Muruj uz-Zahab cha Masudi, ambapo mnamo siku ya Saqifah kiapo cha uaminifu kilitolewa kwa Abu Bakr, Ali alimwambia Abu Bakr; "Umeharibu mambo yetu, ulituona kwa ushauri na hukufikiria haki yetu." Abu Bakr akasdma, "Lalamiko lako ni halali lakini nimefanya hivyo kwa kuhofia maasi."
Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbab, Abu Bakr alipomaliza kazi ya kutafuta kiapo cha uaminifu kwake, alimwita Ali kupitia kwa Wahajirina na Ansari kadhaa. Ali alikwenda na akauliza kwa nini nimeitwa? Umar akasema, "Umeitwa ili kutoa kiapo cha uaminifu kama ambavyo wengine wamekwisha fanya". Ali akasema, "Ninaiweka mbele yako hoja ile ile, ambayo umewaambia Ansari kupata Ukhalifa. Niambie kwa uaminifu mtu ambaye yu karibu zaidi na Mtume."
Umar alisema, "Hatutakuachia hadi hapo utakapotoa kiapo cha uaminifu." Ali alisema, "Jibu swali langu kwanza halafu niambie suala la kutoa kiapo cha uaminifu." Abu Ubaydah bin Jarrah akasema, "Ewe Abul Hasan! Ni wewe tu ndiye unayestahili Ukhalifa na utawala kwa sababu ya kutangulia katika Uislamu na ukaribu wako kwa Mtume, lakini kwa kuwa masahaba wamemkubali Abu Bakr, ni vema wewe pia uungane nao," Ali akasema Abu Ubaydah! Unataka kuhamisha neema kubwa ambayo Mwenyezi Mungu ameipatia familia ya Mtume na kupeleka kwingineko. Tazama! Sisi ni mahali palipoteremshwa Wahyi, mahali ambapo ziliwasili amri na makatazo, chanzo cha uadilifu na maarifa, na mgodi wa akili na ustahamilivu.
"Aliposikia hivi, Bashir bin Said akasema, "Ewe Abu Hasan! Tulidhania kwamba kukaa kwako nyumbani ulikuwa tayari kujitoa katika kinyang'anyiro cha Ukhalifa." Ali akasema, "Hivi nyinyi watu mnaona ni sawa kuacha maiti ya Mtume bila kukafiniwa, kuvishwa sanda na kuzikwa, na kwa hiyo ningejiingiza kwenye kugombania na kukirimu watu kwa kutafuta Ukhalifa?"
Imeandikwa kwenye Usudul ul-Ghibah kwamba Ali alimnukuu Mtukufu Mtume akisema, "Ewe Ali! Wewe ni kama Ka'abah ambapo
kila mtu huenda kuzulu, ambapo yenyewe haiendi kuzulu mtu yeyote. Kwa hiyo, endapo watu wa kundi lako wanakuja kwako kutoa kiapo cha uaminifu kwako kubali. Usiende kwao hadi wao waje kwako."
Kwa mujibu wa Rauzatul Ahbah, Abu Bakr aliposikia mambo haya na kuona kwamba kila sababu na hoja ya Ali, Ilikuwa haipingiki, thabiti na dhahiri kama hoja elfu moja, alisema kwa upole, "Ewe Abul Hasan! Nilidhani kwamba hungekataa kutoa kiapo cha uaminifu kwangu. Kama ningejua kwamba ungekataa, nisingekubali kuwa Khalifa. Sasa, kwa kuwa watu wametoa kiapo cha utii kwangu, nafikiri ni vema uungane nao, kama utapenda. Lakini, kama unasita kwa sababu hii, sitakulaumu." Baada ya Ali kusikia haya alinyanyuka na kwenda nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa Iqdul Farid, cha Shahabuddin bin Abd Rabbihi Undlusi, watu waliokataa kutoa kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr walikuwa; Ali, Abu Dharr, Zubayr na Sad bin Ubadah. Miongoni mwao, Ali Abbas na Zubayr walikaa nyumbani kwa Bibi Fatimah hadi Abu Bakr alipomtuma Umar aende kuwatoa nje watu hao na kutumia upanga endapo wangekataa. Kwa hiyo, Umar alifika hapo akiwa na moto kwa lengo la kuchoma nyumba hiyo. Fatimah alipotambua nini kinachoendelea, alisema; "Ewe mwana wa Khattab! Umekuja kuchoma moto nyumba yangu!?" Umar alisema, Bila shaka nimekuja kwa nia ya hiyo, au vinginevyo, watu waliomo ndani ya nyumba hii watoke na watoe kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr."
Kwa mujibu wa Tarikh Abul Fida, Umar alikwenda na moto kwa nia ya kuchoma moto nyumba ya Fatimah. Fatimah alipotambua, alisema, "Ewe mwana wa Khatab! Umekuja kuchoma moto nyumba
yangu!?" Umar akajibu, "Ndio, vinginevyo watu waliopo ndani watoe kiapo cha uaminifu kwa Abu Bakr."
Kufuatana na Tarikhut Tabari cha bin Jarir, Umar alikwenda nyumbani kwa Murtaza (Imamu Ali) ambamo walikuwemo Talha, Zubayr na muhajirina kadhaa na akasema, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Nitachoma moto nyumba hii vinginevyo mtoke nje kwa ajili ya kutoa kiapo cha uaminifu."
Imeandikwa kwenye Al-Imamah wa as-Siyasah cha bin Qutaybah Dinuri kwamba Abu Bakr alipogundua kwamba wale waliokuwa na Ali hawakuwepo wakati kiapo cha auaminifu kilipokuwa kinatolewa, alimtuma Umar awaite. Watu hao walikuwa ndani ya nyumba ya Ali. Walikataa kutoka nje. Umar aliagiza apewe kitita cha kuni zilizowashwa moto na akasema, "Tokeni nje au vinginevyo kwa jina la Mwenyezi Mungu nitawachoma watu waliomo ndani kwa moto!" Watu wakasema, "Fatimah, binti yake Mtukufu Mtume na yeye pia yupo ndani ya nyumba hii."
Umar akajibu, "Haidhuru kitu," Waliposikia hivi watu wote waliokuwa ndani ya nyumba walitoka nje isipokuwa Ali aliyekuwa anawapa maelezo watu ambao walitumwa wamwite, akasema; "Enyi kundi la Muhajirina! Ninayo haki zaidi ya kuchukua Ukhalifa kuliko nyinyi katika hali zote.
Sitatoa kiapo cha uaminifu kwenu. Kwa usahihi zaidi, nyinyi mnatakiwa kutoa kiapo cha uaminifu kwangu.
Tazama! Mmepata Ukhalifa kwa hoja mliyowapa Ansari kwamba nyinyi ni ndugu wa Mtume na jambo la kushangaza ni kwamba sasa mnajaribu kuchukua isivyo halali Ukhalifa kutoka kwa Ahlul-Bait wa Mtume.
Hamweki madai yenu katika msingi kwamba nyinyi ni bora zaidi kuzidi Ansari kwa kisingizio kwamba Mtume alikuwa wa kabila lenu? Sasa nakupeni hoja hiyo hiyo ambayo mliwapa Ansari kwamba, uhusiano wetu na Mtume ni mkubwa na karibu zaidi kuliko wenu wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake.
Sasa mnatakiwa kutenda haki bila upendeleo endapo nyinyi mnamwanini Mwenyezi Mungu na kumwogopa Yeye.
Kuhusu kundi la wahajirina! Mkumbukeni Mwenyezi Mungu na msichukue uongozi wa Mtume kutoka kwenye nyumba yake na kupeleka nyumbani kwenu." Baadhi ya hapo, Fatimah alisema akiwa kwenye ngazi za mlango wake, "Enyi watu! Mlituachia maiti ya Mtume, mkatatua jambo la Ukhalifa kwa kujipendelea nyinyi na hamkuzingatia haki yetu."
Kwa mujibu wa Tarikh bin Qataybah Umar alipokwenda kwa Abu Bakr alisema, kwa nini hutoi amri ya kukamatwa Ali ambapo anapinga kutoa kiapo cha utii kwako?
Kwa mara nyingine Abu Bakr alimtuma mtumwa wake Qanfaz amwite Ali. Qanfaz alimwambia Ali, "Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu anakuita wewe." Ali akasema, 'Mmemkashifu Mtume haraka kiasi hicho nyie watu."
Qanfaz alirudi kwa Abu Bakr na akarudia maneno aliyoambiwa na Ali. Baada ya kusikia Abu Bakr aliendelea kulia kwa kipindi fulani. Umar akamwambia Abu Bakr kwa mara ya pili, "Usimpe muda Ali ambaye hataki kutoa kiapo cha utii kwako." Abubakr akamuagiza tena Qunfaz kwenda kwa Ali na kusema, Amiri wa Waumini anakuita ili utoe kiapo cha uaminifu. Qanfaz aliwasilisha ujumbe wa Abubakr kwa Ali. Ali akasema kwa sauti kubwa "Mwenyezi Mungu na
asifiwe! Bwana wako amedai uhusiano huo ambao hana uwiano nao." Qafaz akaenda kwa Abu Bakr na kurudia maneno ya Ali. baada ya kusikia hivi, Abu Bakr alianza kulia tena. Halafu Umar akasimama na akifuatana na kundi la watu, alikwenda nyumbani kwa Fatimah na akagonga mlango. Aliposikia kelele za watu, Fatimah alianza kulia kwa sauti kubwa, "Ewe Baba! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni tatizo gani hili lenye uzito mkubwa ambao limeletwa kwetu na mwana wa Khattab na Abu Quhafah!" Watu waliposikia kilio cha Fatimah, wengi wao walirudi huku wanalia na wachache tu ndio waliobaki nyuma na Umar. Halafu Ali akatoka nje ya nyumba na akaenda nao kwa Abu Bakr. Ali aliambiwa atoe kiapo cha uaminifu kwa Abu bakr. Alisema, "Endapo sitatoa kiapo cha utii itakuwaje?" Akasema, "Endapo hutatoa kiapo cha uaminifu, kwa jina la Mwenyezi Mungu tutakuua."