• Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 20100 / Pakua: 3440
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA ABU DHARR

MAISHA YA ABU DHARR

Mwandishi:
Swahili

9

MAISHA YA ABU DHARR

Abu Dharr alikwisha choshwa na kuchukizwa na mwenendo wa Uthman uliokiuka mafundisho ya Kiislamu, lakini alipofikia Syria na kuona tabia ya Muawiyah ambayo ilikuwa inaharibu Uislamu, alishangaa sana na akajisemea peke yake kwamba mfumo wote wa utawala ulikuwa mbovu. Alilazimika kufikiria kuhusu mtindo wa maisha ya Muawiyah kwamba Uislamu kama ulivyo dhihirishwa na Mtume si tu ulikuwa unadhoofu lakini ulikuwa unazimwa. Kufuatana na hali hii, hisia zake za kawaida zilisisimuka.

Alilazimika kuanzisha tena kilio cha ukweli kufuatana na sifa zake za uaminifu na kusema kweli. Kwa kuwa alikuwa jasiri sana, hakusikia kusema kweli kwa hivyo, bila kufikiria kwamba Muawiyah alikuwa ndiye mtawala wakati huo, alianza kufanya kazi zake za Kiislamu na akaanza kusema kwa lengo la kumzuia Muawiyah asifanye matendo yaliyo kinyume cha Uislamu. Alimwambia wazi kwamba alikuwa anaendesha utawala kinyume na Uislamu kama ule wa Uthman bin Affan. Alamah Subaiti ameandika kwamba Uthman alipochukua hatua ya kumhamisha Abu Dharr na kumpeleka Syria ni uthibitisho wa uhakika wa kweli kwamba alikuwa anakwepesha msimamo wa ukosoaji wa Abu Dharr kutoka kwake kwenda kwa Muawiyah (Abu Dharr al-Ghifari).

Mwandishi wa historia Balazari Allamah majlis, Allamah Subaiti na Allamah Amyni wameandika kwamba Abu Dharr alipofika Syria Muawiyah alikuwa anajenga Ikulu yake 'al-Khizra.' Maelfu ya vibarua walikuwa wanafanya kazi hapo.

Siku moja Muawiyah alikuwa anaiangalia Ikulu hiyo kwa majivuno. Abu Dharr akamuona, akamkaribia, na akasema, "Ewe Muawiyah! Endapo Ikulu hii inajengwa kwa kutumia hazina ya Taifa ni uvunjaji wa uaminifu na endapo inajengwa kwa fedha yako binafsi ni ubadhirifu."

Aliposikia hivi Muawiyah alinyamaza kimya, aligeuza uso wake na kutazama upande mwingine na hakujibu. Abu Dharr aliondoka na kafika msikitini. Alitafuta nafasi akaketi. Baadhi ya watu walilalamika kwa Abu Dharr kuhusu Muawiyah kwa kusema kwamba hawajapata chochote katika zawadi ambazo hutolewa na sasa mwaka umepita. Abu Dharr aliinamisha kichwa chake kuelekea mbele halafu akasImamua. Watu walimwangalia. Akasema; "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, bidaa za namna hii zinaenea siku hizi kwani hazipo kwenye Quran Tukufu au Hadith za Mtume. Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, nimeona kwamba ukweli unadumazwa na uwongo unazidi kuwa na nguvu. Watu wakweli wanasingiziwa kuwa waongo na waovu wanapewa upendeleo kuzidi waadilifu.

Enyi watu wakuu! Ewe Muawuyah na magavana wake! Wasikitikie masikini. Wale wanaokusanya dhahabu na fedha na hawatumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wanajua kwamba nyuso zao, pande zote na migongo yao itapigwa chapa ya mo to. Enyi mnaohodhi utajiri! Hamjui kwamba mtu anapokufa kila kitu hufarakana naye. Vitu vitatu tu hubaki naye; sadaka ya kudumu, elimu yenye manufaa, na mtoto mwema, ambaye humwombea yeye."

Watu walisikia mhadhara wake wanao gandamizwa na masikini walikusanyika kumzunguka yeye na matajiri wakaanza kumuogopa. Habith bin Muslim Fahri alipoona kundi la watu karibu na Abu Dharr alisema, 'Hali ni kero kubwa!" alikwenda kwa Muawiyah haraka na akamwambia; "Ewe Muawiyah! Abu Dharr atavuruga kabisa utawala wa Syria. Endapo unawahitaji watu wa Syria, lazima uzuie usumbufu huu kabla haujakomaa.Muawiyah alitafakari jambo hili peke yake.

"Nimshughulikie kwa ukali au kwa upole? Nikitumia ukali moto utawaka na kuenea. Je, Ni lazima nilalamike kwa Uthman? Lakini, Uthman atasema nini? "Atasema kwamba sikuweza kumfanya atengamae hata mtu mmoja miongoni mwa raia wangu. Kwa hiyo ni vizuri zaid kumwondoa Syria."

Imekuwa ni mazoea ya kawaida kukandamiza kwa ukali maneno ya kweli ya watu wa kimungu kwa sababu ya uchungu wao. Ingewezekana watu wapenda mambo ya kidunia wanyamaze baada ya kusikia hotuba za Abu Dharr zenye hamasa ya kidini imekuwa jambo la kawaida kwake, na halafu inawezekanaje mtu ampende Muawiyah, ambaye alifikiria mtu mkubwa kabisa aliyeko chini yake katika majisifu yake ya uwezo na hila, afuate ushauri wa Abu Dharr na angewezaje kuvumilia maneno yake makali?

Abu Dharr akitumia sauti ya kunasihi alikuwa na desturi ya kukariri Aya ya Qurani:

"Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii kwa njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie habari ya adhabu iliyo chungu ." (Quran 9:34).

Na alikuwa na kawaida yake kwamba alikariri aya hii dhidi ya Muawiyah mwenye mitaa mingi zaidi na barabara za Syria. Kila alipokiariri Aya hii, masikini na wenywe kuhitaji wakimzunguka yeye na mara nyingi walimlalamikia kuhusu magavana wanaotafuta anasa za utajiri na umasikini wao. Muawiyah alikuwa na kawaida ya kupata taarifa ya mahubiri yake mara kwa mara. Hatimaye alimwekea mipaka mnikali na kumtesa kwa kila njia. Ilipoonekana kwamba hata hatua hii haikufaa, alimtishia Abu Dharr kwa kifo.

Abu Dharr aliposikia tishio hilo la kifo alisema, "Ufalme wa Muawiyah unanitishia mimi kwa umasikini na kifo. Ninapenda

kuwaambia kwamba umasikini ni wa kutamanika zaidi kwangu kuliko utajiri, na ninapenda kuwa chini ya ardhi kuliko kuwa juu yake. Wala siogopeshwi kwa tukio la kifo, ama kifo chenyewe."

Allamah Majlisi ameandika kupitia kwa mamlaka ya Shaykh Mufid watu wa Syria walisema nini kuhusu hotuba nzito za Abu Dharr; "Uthman alipomhamisha Abu Dharr kutoka Madina kwenda Syiria, aliishi miongoni mwetu, na akaanza kuhutubia mlolongo wa hotuba ambazo zilitusisimua sana. Alikuwa na mazoea ya kuanza hotuba yake kwa kumsifu Mwenyezi Mungu na Mtume na halafu alisema; "Kuwapenda uzao wa Mtume(s.a.w.w) ni wajibu wa kila mtu. Yule asiye wapenda hawa hatanusa hata ile harufu ya Pepo." Halafu aliongeza; "Enyi watu! Nisikilizeni. Nilikuwa na kawaida ya kuheshimu maagano yangu kabla sijakubali Uislamu, wakati wa ujahiliya kabla ya wahyi wa Quran na kabla ya kuteuliwa kwa Mtume. Alisema kweli, niliwafanyia wema majirani zangu, niliona kwamba ukarimu ni wajibu wangu, nilikuwa nawakirimu masikini, na niligawia utajiri wangu. Baadaye, Mwenyezi Mungu alipoleta ufunuo wa Kitabu chake na akamteua Mtume wake, niliulizia kuhusu mambo haya nikatambua kwamba ni namna na desturi zile zile tulizokuwa tunazitumia sisi, pia zilikuwepo kwenye nasaba za Mtume. Enyi watu! Inafaa zaidi Waislamu kuwa waadilifu. Ni kweli kwamba Waislamu walifuata mwenendo kufuatana na mafundisho ya Uislamu, lakini rafiki zangu! Tabia ya Waislamu ilikuwa njema kwa kipindi kifupi. Halafu ilitokea kwamba madhalimu walionesha matendo maovu ambayo tulikuwa hatujayaona kabla yake. Watu hawakuharibu Sunna za Mtume, walianzisha bidaa, walimpinga mtu aliyesema kweli, wakaungana na kundi lka watu waovu na kuwaacha wale waliokuwa wacha Mungu na wanaofaa.

"Ewe Mwenyezi Mungu! Ichukue roho yangu endapo unayo mambo mazuri kwa ajili yangu unayo kulijko haya yaliomo katika dunia hii, kabla sijapotosha imani Yako au kubadili Suna za Mtume Wako."

Aliendelea kwa kusema, 'Enyi watu! Shikamaneni na ibada ya Mwenyezi Mungu na mjiepushe na dhambi." Halafu akaelezea sifa za Ahlul Bait ambazo alizisikia kutoka kwa Mtume na akawashauri watu waambatane na Ahlul Bait.

Watu wa Syria wanasema kwamba walisikiliza hotuba zake kwa umasikini sana na kundi kubwa la watu lilikusanyika kumzunguka yeye alipokuwa anahutubia, hadi Muawiyah akamtaarifu Uthman kuhusu matukio haya, kwa hiyo, alimwita Abu Dharr aende Madina.

Kwa kuwa Abu Dharr alimuudhi sana Muawiyah kwa mihadhara yake ya kidini, yeye, katika jitihada ya kumnyamazisha kwa vyovyote vile alifanya ujasiri wa kumpelekea mfuko wa fedha kwa sababu hakuweza kufikiria njia nyingine yoyote ya kufanya.

Wasomi na waandishi wa historia wanasema kwamba Muawiyah alimpelekea Abu Dharr mfuko wa dinari za dhahabu mia tatu zilizopelekwa na mjumbe ili kumnyamazisha. Alipoona hivi alisema, "Mwambie Muawiyah kwamba sihitaji fedha yoyote kutoka kwake," na akarudisha mfuko huo.[40]

Abu Dharr aliona kwa macho yake baada ya kutawafu Mtume matukio yote hayo ya hatari ambayo Ale Muhammad (Uzao wa Mtume) walilazimishwa kupambana nayo. Alisema wazi dhidi ya kuhodhi utajiri, kwani alikwisha elewa kwa ukamilifu, lengo la Hazina ya taifa na madhumuni ya Qurani Tukufu, aliona namna ya utendaji wa Mtume na alikuwa anachunguza mwenendo wa maisha ya uzao wa Muhammad. Alipoona tabia na namna ya maisha ya wale wenye madaraka ya Ukhalifa ni kinyume kabisa na Suna hizi, alihisi wasi wasi sana kwa sbabu ya imani yake kuwa imara. Kamwe alikuwa hajafikiria yale aliyo yaona kwa macho yake. Mara tu baaada ya Uthman kushika hatamu ya serikali na Ukhalifa, alilazimisha hisia zake kutoka kwanye moyo wake na kuzipeleka mdomoni mwake na alilazimika kifichua kile alichokificha moyoni mwake kwa muda mrefu. Aliona kwamba utajiri uliongezekla kuliko alivyo fikiria, upendeleo na fadhila kwa ndugu ni mambo ambayo yalifika upeo wa juu sana, utajiri wa Hazina ya Taifa ulikuwa inagawiwa kwa ndugu, marafiki na wanaomunga mkono badala ya watu wanao stahili, bila hata kufikiria, na kwa sababu ya utajiri huu bida zilizokuwa zinztikisa misingi ya Uislamu, zilikuwa zinzongezeka bila ya kuzuiz. Kwa hiyo, kufuatana na mkataba wa uaminifu aliofanya na Mtume, alianza kukataa na kuwakosoa wale wenye kuwajibika, ambayo matokeo yake alihamishwa Madina na kupelekwa Syria. Huko aliona bidaa nyingi za kutafuta starehe ambazo zilikuwa zinapingana na Uislamu na ambazo zilizidi hata njia za maisha ya anasa za Kaisari na Khussoe. Kwa kuwa alilazimishwa na amri ya Mtume, na ahadi iliyofanywa kwake, na ahadi iliyofanywa kwake, na pia kwa uimara wake, wa kidini alianza pia kuhubiri huko. Alianza kuhadhiri huko Syria chini ya mwongozo wa Aya ile ile ya Quran ambayo ilikuwa kiini cha hotuba zake Madina. Katika uhusiano huu, alihutubia hotuba nyingi, baadhi ya hizo zimetajwa kwenye kurasa za nyuma.

Maelezo ya hotuba yake ya kushutumu kuhodhi utajiri ilikuwa Aya ifuatayo:

"Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie habari ya adhabu iliyochungu. Siku zitapotiwa moto katika Moto wa Jahanamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa; Haya ndio mliyojilimbikizia nafsi zenu, basi onjeni mliyokuwa mkilimbikiza. " (Qurani 9:34).

Wasomi na waandishi wa historia wanasimulia kwamba: alipokuwa anahutubia kundi huko Syria, alisema; "Kwa jina la Mwenyezi Mungu! Ninaamini kwamba kweli inaangamia, udanganyifu unahusishwa, watu wa kweli wanawekewa pingamizi na watu wanaendekeza uchoyo badala ya uchaji Mungu."[41]

Aliendelea kusema; "Dhahabu na fedha zitageuka kuwa miale ya moto na zitawazunguka kuwa miale ya moto na zitawazunguka wale wanaoziweka kwa kuzifungia hadi wazitumie katika njia ya Mwenyezi Mungu." Akisisitiza jambo hili alisema; "Vipande vilivyochomwa moto wa Jahanamu vitawekwa kwenye vifua vya wale wanaokusanya dhahabu na fedha, hadi vitoboe mbavu zao na mifupa ya mabega yao." (Sahih Bukhari-Kitab az-Zakat).

Abdul Hamid, mwandishi wa Misri ameandika kwamba badaye Abu Dharr alipowasili kwenye msikiti watu walikusanyika na kumzunguka na akawaambia; "Tumieni chochote ambacho Mwenyezi Mungu amewapeni. Tahadharini sana hivyo kwamba maisha ya dunia yasiwadanganye. Weka fungu la rasilimali yako liwe haki ya wasio nacho. Mtume amesema kwamba tama ya wingi wa rasilimali imefanya mzame kwenye kusahau."

Mwanadamu anasema; "Mali yangu! Mali yanngu! Lakini mali yako ni ile ambayo umekula imeksisha au umetoa sadaka; kwa maana kwamba umeweka kwa lengo la kuhifadhi. Mwenyezi Mungu amezuia kuhodhi mali. Mtume amesema; "inasikitisha, inasikitisha dhahabu na fedha," Ngawira ni haki ya Waislamu, lakini Muawiyah amehifadhi na kuitumia kwa watumishi na walinzi wake na kwa ufahari na maonesho yake. Muawiyah amesahau kwamba ni majoho mawili tu yanaruhusiwa kwake kutika kwenye hazina ya Taifa, maja kwa alili ya majira baridi na lingine kwa ajili ya majira ya joto. Zaidi ya hayo, anaweza kuchukua matumizi ya Hijja na familia yake tu kama ambavyo familia ya tabaka la kati ya Quraishii inaweza kuchukua.

Ngawira lazima igawanywe kwa miongoni mwa Waislamu wote walio masikini. Lakini, sasa ardhi inatwaliwa, na nyumba zinajengwa, na maelfu ya dinari yanatumika katika kuziremba nyumba hizi na Waislamu walio masikini wanatelekezwa."

Mtu alimnong'oneza sikioni mwake, "Tafadhali! Unasema nini kuhusu Muawiyah? Humuogopi?"

Abu Dharr alimjibu na kumwambia; "Rafiki yangu alinishauri niseme kweli, hata kama inaumiza, na bila kujali shutuma za anayeshutumu, ambapo nipo kwenye njia iliyonyoka. Ninamuomba Mwenyezi Mungu anilinde nisiwe na uoga, ubakhili na ujinga." Halafu akaongeza, "Watu wameanza kupika vyakula vya aina tofauti, na wanatumia dawa ili visagwe. Mtume wetu hakula chakula cha aina mbili kwa wakati mmoja hata siku moja hadi mwisho wa uhai wake. Kama alikula tende hakula mkate. Wazao wa Mtukufu Mtume kamwe hawakula mkate wa shayiri hadi kushiba kwa siku tatu mfululizo hadi mwisho wa uhai wao. Nyumbani kwa Mtume(s.a.w.w) , mara nyingine ilitokea kwamba wala moto haukukokwa, ama mkate, ama chakula cha aina nyingine kilipikwa mfululizo kwa mwezi moja."

Mtu mmoja aliuliza, "Aliwezaje kuwa hai Abu Dharr akajibu; "Mtukufu Mtume alikula tende na kunywa maji. Alisema kwamba hakuna mtu aliyeona chombo kibaya sana kuliko tumbo lake.

Vipande vichache tu vinamtosha mtu kuwa hai. Endapo ni muhimu kula, theluthi moja ya tumbo liwe wazi kwa ajili ya chakula, theluthi moja kwa ajili ya maji na iliyobaki iwe kwa kwa ajili ya chakula, theluthi moja kwa ajili ya maji na iliyobaki iwe kwa ajili ya hewa. Mtume ametushauri kwamba tusile chakula kupita kiasi kwa sababu hutengeneza ulegevu, huharibu mwili na kumhusisha mtu na magonjwa. Uwe na ulinganifu unaostahili katika mlo kwa sababu utaepukana na israfu, mwili utakuwa na nguvu na husaidia katika ibada. Mtume kamwe hakukusanya au kuhodhi kitu chochote. Kinyume chake, alikuwa akitoa sadaka chochote alichopata, hivyo kwamba hakuna kilichobaki kwa ajili ya mlo wake. Bila kuhusisha Hazina ya taifa Mtume alikuwa anatoa hata mgao wake kama sadaka."

Makabaila walimsihi Muawiyah na wakalalamika kuhusu propaganda ya Abu Dharr. Muawiyah alimwita na akamwambia kuhusu azimio imara la kuondosha tishio hili ambalo lilitikisa misingi ya serikali yake na kuvunja matumaini yake.

Abu Dharr aliingia kwenye baraza la Muawiyah akiwa na mwili mwembamba na mkondefu. Dalili za ushupavu na uimara zilionekana kwenye uso wake wa mviringo alisimama kumkaribisha na akamwonesha mahali pa kuketi karibu na yeye. Halafu akawaita watumishi na akawagiza walete chakula. Nguo ya chakula ilitandikwa na vyakula vya aina nyingi mbali mbali ambavyo vilizidisha ladha, vilitayarishwa.

Muawiyah akamwambia Abu Dharr, "Ndio, tafadhali." Abu Dharr alikataa na akasema, "Mimi ninakula kilo mbili za ngano kwa juma moja. Haya yamekua mazoea yangu tangu uhai wa Mtume. Kwa jina la Mwenyezi Mungu sitafanya chochote kuzidi hapo hadi nitakapoungana naye." Halafu akamgeukia Muawiyah akamwambia,

"Umebadili mwenendo wako chakula kinachotayarishwa kwa ajili yako sasa, sio kama kile cha zamani. Unakula mkate uliopikwa unga mzuri, unakuwa na vyakula vya aina kadhaa kwenye mlo moja na unavaa nguo tofauti na ile ya jioni. Wewe hukuwa na tabia hii wakati wa uhai wa Mtume. Hali yako haikuwa tofauti na ile ya mtu masikini." (Sahih Muslim, Sunan Nisai na Sunan Baihaqi).

Muawiyah; "Maafisa wangu wanalalamika kuhusu wewe. Wanasema kwamba unawachochea masikini wawachukie wao."

Abu Dharr; "Ninawazuia wasihodhi."Muawiyah; "Kwa nini unafanya hivyo?"

Abu Dharr: "Ninafanya hivi kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema; "Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu,wabashirie bahari ya adhabu iliyochungu. " (Qurani 9:34).

Abu Dharr; Ewe Muawiyah! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitaacha hadi hapo utajiri utakapogawiwa kwa masikini."

Vyovyote vile, matatizo yalimzunguka Abu Dharr pande zote. Mateso makubwa yalimpata kutoka kwa Bani Umayyah. Aligandamizwa sana. Lakini hakuonesha udhaifu wowote na hakuacha kuhubiri. Sasa alianza mashambulizi makali zaidi.

Abdullah Subaiti, Abdul Hamid Misri na Manazir Ahsan Gilani wanasema kwamba; Abu Dharr aliendelea kufanya kazi ya kuhubiri mara kwa mara na akiwaonya kuhusu adhabu kali kwa wanaohodhi. Hatimaye Muawiyah akaanza kufikiria mipango ya kujinasua kutoka kwenye michomo ya maneno yake na kuzuia utekelezaji wa malengo yake. Hata hivyo, aliamua kwamba pangeweza kuwepo fursa ya kuwa huru kutokana na mashambulizi endapo tabia ya kuhodhi mali inaweza kuthibitishwa na wale wanao ishambulia. Kwa hiyo, alipata mpango, na aliridhika kwamba mpango huo ungefanya kazi iliyokusudiwa.

Bin Athir baada ya kutaja Aya za Qurani, ameandika kwamba ilipoonekana si rahisi kumnyamazisha Abu Dharr kwa namna yoyote ile, Muawiyah alimtuma mtu na dinari elfu moja kwenda kwake wakati wa usiku. Abu Dharr alizichukua fedha hizo na akazigawa kwa masikini kabla ya alfajiri na hakubakisha hata sarafu moja kwa ajili ya matumizi yake.

Muawiyah, alimwita mtu aliyepeleka sarafu za dhahabu kwa Abu Dharr, baada ya Swala ya alfajiri, akamuamuru aende kwa Abu Dharr na amwambie kwa kujifanya anao wasi wasi, "Ewe Abu Dharr! Niokoe kutokana na mateso ya Muawiyah. Muawiyah aliniamuru nipeleke hizo sarafu za dhahabu kwa mtu mwingine lakini mimi nimekuletea wewe kwa makosa."

Mjumbe wa Muawiyah alikwenda kwa Abu Dharr na kumwambia kama alivyoagizwa na Muawiyah. Abu Dharr akasema, "Ewe mwana! Mwambie Muawiyah kwamba fedha alizoniletea nilizigawa kwa watu wanaozihitaji kabla alfajiri leo. Sina hata sarafu moja sasa hivi na kama anataka fedha hizo zirudi kwake, atalazimika kunipa siku tatu, ambapo nitazipata fedha hizo kutoka mahali pengine ili nimrudishie."

Mtu huyo alirudia taarifa hiyo kwa Muawiyah kama alivyoisikia kutoka kwa Abu Dharr, ambaye alisema, Bila shaka Abu Dharr hufanya yale ambayo huwaambia wengine wafanye."[42]

Abdullah Subaiti, baada ya kunukuu tukio hili ameandika katika maelezo ya kifalsafa kwamba Abu Dharr alikuwa mtu mwenye tabia ya hali ya juu sana. Bani Umayyah walionesha kutokuwa na uwezo wa kuona mbali kiakili katika kumweleza yeye. Ndio sababu waliona umuhimu wa kufanya utapeli wa kisiasa. Abdul Hamid Misri ameandika baada ya tukio hili. Muawiyah alielewa kwamba Abu Dharr alikuwa mkweli kwa maneno yake. Alitumia dinari zote ka usiku moja Muawiyah alishindwa kutimiza lengo lake. Alionesha huruma kwa Abu Dharr lakini haikufaa kitu. Halafu akatumia nguvu dhidi ya Abu Dharr lakini hakuathirika. Hatimaye akataka amnunue kwa dinari mia tatu, lakini hakufaulu.[43]

Kwa mujibu wa wasomi na waandishi wa historia, Abu Dharr alikuwa bado yupo Syria Muawiyah alipotuma jeshi kwa ruhusa ya Uthman kwa vita vya majini (Tarikh Abul Fida).

Abu Dharr alikuwa anashughulika na kazi yake. Baada ya vita hiyo kwisha, Muawiyah akamwagiza Abul Darda, Umar bin al-Aas, Ubadah bin Samit na Umme Hizam, ambao walikuwa masahaba wa Mtukufu Mtume waende kwake.

Walipofika, Muawiyah aliwaambia; "Nimechoka kumwonya Abu Dharr lakini hataki kunisikia. Inanisumbua. Nyinyi pia mmepewa heshimna ya kuwa masahaba wa Mtume kama Abu Dharr alivyo. Nendeni kwake na mwambieni aache shughuli zake na aishi maisha ya kimya na utulivu. Nimechoshwa sana na mtu huyu na pia watu matajiri wa nchi hii."

Watu hawa walikubali haraka sana kwamba wangekwenda kwa Abu Dharr na wangemwomba afanye kama ilivyoagizwa na Muawiyah. Kwa hiyo, walikubaliana kwa pamoja kuhusu mpango fulani na wakamtembelea. Wakamwambia Abu Dharr; "Tumekuja kwa niaba ya Muawiyah. Ametutuma tuje kwako na ombi kwamba uache mahubiri yako na uendeshe maisha yako kwa amani."

Aliposikia hivi, Abu Dharr alikasirika. Alifikiria kwamba watu hao waliyaona mahubiri yake ni halali kabisa na walijua kwamba lolote alilokuwa anafanya liliendana na Radhi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na bado walikwenda kwake kwa amri ya Muawiyah.

Kwanza kabisa alimwambia Ubadah bin Samit; "Ewe Abul Walid Ubadah! Hapana shaka kwamba unanitangulia mimi kwa kila namna na unanizidi kwa ubora katika kila njia. Wewe ni mkubwa kwa umri na umekuwa pamoja na Mtume kwa kipindi kirefu zaidi. unazo busara, akili, unajua sana mambo ya dini na utu wako ni bora. Lakini ninasikitika kusema kwamba licha ya kujua kila kitu sawa, umekuja kunishauriu mimi ka ombi la Muawiyah.

"Ewe Ubadah! Kwani sielewi mambo? Hivi nimepoteza akili ya kuhoji. Hutambui hali ya mambo? Haya ninayo si sahihi? Nasaha zangu haziendani na nia ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake? Ewe Ubadah! Iliniuma sana kwamba wewe ni mtu mwenye akili, unajua kila kitu sana, unakuja kwangu kunishauri mimi. Sikiliza! Ninayo chuki kubwa kwa ujumla huu wote kwa sababu mtu mwenye kuelewa mambo kama wewe umejumuika kwenye ujumbe huu."