10
MAISHA YA ABU DHARR
Halafu akamgeukia Abu Darda na akasema; "Ewe Abu Darda! Umepewa neema ya kumpenda Mtume angalau kidogo. Ilikuwa wazi kwako kwamba endapo hungekubali haraka, hungepewa heshima ya usahaba kwa sababu ya kifo cha Mtume. Lakini uliikubali imani, ukapewa heshima ya usahaba, na ukafikiriwa kuwa sahaba mzuri. Lakini sikiliza! Wewe hukufaidika na usahaba wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
kama nilivyuofaidika mimi. Wewe huwezi kuelewa malengo yake kwa kiasi ninachoelewa mimi. Ninayaelewa malengo ya Mtume na ninafanya kufuatana na utashi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kwa hiyo, huna haki ya kunishauri mimi."
Halafu akaanza kuzungumza na Umar bin Aas kwa kumwambia kwa sauti ya ukali; 'Ewe Umara bin Aas! Ninakutambua wewe vizuri sana. Umefanya nini zaidi ya kushiriki kwenye vita? Kama hali ilivyo, ulipewa heshima ya usahaba wa Mtukufu Mtume lakini kwamwe hukupata nafasi ya kuishi na yeye. Kila mara ulikuwa mbali na Mtume(s.a.w.w)
kwa sababu ya vita. Wala huwezi kuelewa nia yake ama kuwa na uwezo wa kutosha kuunda maoni sahihi kuhusu matendo na tabia yangu. Ninajua kwamba wewe upo kwenye mvuto wa Muawiyah wakati huu ndio maana umekuja kuniona mimi bila kufikiria kwanza."
Halafu akamgeukia Ummu Hizam na kusema; "Nikwambie nini wewe? Wewe ni mwanamke. Lakini bado wewe ni mwanamke, kwa kiwango chochote kile, na unazo akili za kike." Halafu akasema; "Nendeni mwambieni Muawiyah aone akili zake, aendeshe mambo kufuatana na ushauri wangu na asipoteze imani kwa ajili ya dunia."
Waliposikia mambo yote haya, wote walinyamaza kimya. Baada ya muda mfupi waliondoka kwa Abu Dharr na kurudi kwa Muawiyah. Walimwambia kwamba walifikisha ujumbe kwa Abu Dharr. Aliwauliza walichosema na majibu waliyopewa na Abu Dharr. Ubadah bin Samit alirudia tukio lote na mwishowe akasema, "Kamwe sijawahi kukaa mahali ambapo shutuma kali kama hizo zinatolewa kwa wazi sana." (Musnad bin Hanbal, Masanid Abu Dharr).
Abu Dharr alikuwa anashughulika na mahubiri huko Syria wakati wa Hija ulipofika. Aliomba ruhusa kutoka kwa Uthman na kusema alitaka kutoka nje ya Syria aende kuhiji na akae kwenye kaburi la Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
kwa muda wa siku chache. Uthman akampelekea barua ya ruhusa kutoka Madina na Abu Dharr akaenda Hija. alifanya ibada ya Hija na akaenda Madina. Alikaa karibu na kaburi la Mtume kwa siku chache na halafu akarudi Syria. Balazari pia amesimulia tukio hili kwa sentenso chache.
Aliporudi kutoka Hija akaanza tena shughuli yake ya kuhubiri. Kwa upande moja alikuwa anatumia nguvu zake zote katika kutoa nasaha na kwa upande mwingine maombi mengi sana yalikuwa ya watu matajiri yalikuwa yanamfikia Muawiyah kwamba akomeshe kelele za Abu Dharr. Kiini cha maombi haya ni kwamba watu walikuwa wanakariri mitaani na barabarani Aya ya Qurani ambayo inawaonya watu wenye fedha ambao wanapigwa chapa kwa dhahabu na fedha iliyochomwa moto, kwa hiyo inakuwa vigumu wao kupita kwenda Syria. Na matokeo yake ni kwamba Muawiyah alitangaza kwamba hakuna mtu yeyote kuwasiliana kwa namna yoyote na Abu Dharr
.
Abu Dharr alipopata taarifa ya kususiwa kijamii, yeye mwenyewe alianza kuwaambia watu wasiende kwake au kuketi naye. Hii ni kwa sababu alidhani kwamba endapo mtu alikwenda kwake angeteswa na serikali. Lakini kwa kuwa yeye ilimwia vigumu kuacha kuhubiri, yeye mwenyewe alikwenda kwenye mikusanyiko ya watu na akaanza kufanya kazi yake.
Kwa mujibu wa bin Khaldun, kundi la watu lilipokwenda kumuona baada ya amri ya kumsusa, Abu Dharr aliwaambia watu hao waondoke na yeye abaki peke yake.
.
Inaonyesha kutoka kwenye taarifa ya Balazari kwamba watu hao waliofanya mawasiliano na Abu Dharr na kusikiliza hotuba zake, walishughulikiwa kwa ukali zaidi kuliko hata Abu Dharr mwenyewe.
.
Abu Dharr alikuwa jasiri kiwango gani! Hakuvumilia ukatili wowote kwa wale waliokuwa wanamwendea, na hakutaka watu hao wapate usumbufu wowote. Lakini almuradi hisia zake za moyoni zilimpa msukumo, alisisitiza kuendelea kuzisoma kwa watu kwa imani na hamasa kamili.
Yeye hakujali kuhusu mafanikio au hasara yoyote katika njia ya Mwenyezi Mungu.
SURA YA KUMI NA NNE
Abu Dharr alikuwa mtu mkweli. Alikuwa anawaonya watu wengine wafanye matendo mema. Muawiyah alikuwa mtu aliyependa mambo ya dunia. Kila mara Abu Dharr alikuwa anamwelekeza kufanya matendo mazuri hadi watu wa Syria walianza kuona aibu. Siku moja Muawiyah alimwambia Abu Dharr, "Wewe si muadilifu kiasi cha kunielekeza mimi kufanya matendo mema mbele ya umma." Aliposikia hivi Abu Dharr akasema, "Nyamaza! Huoni hata aibu!"
Kwa ufupi, Muawiyah alipoona kwamba hangeweza kujirekebisha na hangemnyamazisha Abu Dharr, aliamua kumhamisha Syria. Kwa hiyo, aliamua kumpeleka Jabal al-Amul. Subaiti anasema kwamba Abu Dharr alipowaita watu wa huko kuwaelekea Ahlul-Bait, walikubali wito huo haraka sana! Kwa kuwa sehemu hiyo ilikuwa pana sana, wito wake haukubakia kwenye mipaka ya ndani ya Jabal al-Amul lakini ilifika hata kwenye sehemu za karibu. Ni dhahiri kwamba Muawiyah alimpeleka Abu Dharr Jabal al-Amul kutoka Syria kwa sababu tu alidhani kwamba shughuli zake za kuhubiri miongoni mwa watu hao wageni zingesimama, lakini aliposikia kwamba Abu Dharr na hotuba zake kali aliwafanya watu wa Jabal al-Amul waelekee ukweli, alimwita arudi Syria haraka.
Vita hii ilitwa Zaat al-Ruqa (vita ya viraka vya nguo) kwa sababu njia ilikuwa na mawe mengi sana na mashimo, kwa sababu hiyo, mibuu ya watu ilipasuka na kuifunga kwa vipande vya nguo. Zainul Ma'ad.
Abu Dharr alianza tena kazi yake alipofika Syria. Alikuwa na tabia ya kukaa mahali paitwapo bab Damishq (lango la Dameski), baada ya Swala ya alfajiri na kila anapoona msururu wa ngamia uliobeba mali ya serikali aliita kwa sauti kubwa; "Watu! Msururu huu wa ngamia ambao unakuja haukubeba mali ile umebeba moto. Wamelaaniwa watu wanao walekeza wenzao kufanya wema lakini wao hawafanyi hivyo, na iwaangukie laana watu wanaowakataza wengine wasifanye uovu lakini wao hufanya uovu."
Halafu Abu Dharr aliondoka mahali hapo na kwenda kwenye lango la Ikulu ya Muawiyah na akatoa ho tuba hiyo. Hili ilikwisha kuwa kawaida yake na alifanya hivyo mara kwa mara. Hatimaye Muayiyah alimkamata.
Abu Dharr aliizingatia hadith ambayo imenukuliwa na Khatib al-Baghdad na Almad bin Hanbal. Kufuatana na maelezo ya hadith hii Mtukufu Mtume aliwaambia masahaba wake; "Enyi masahaba wangu! Sikilizeni kwa makini.
Baada yangu watawala wa umma wangu watakuwa kama makabila. Wao hawatatofautisha haki na dhuluma na kweli na uwongo. Lakini, yeyote atakayekwenda upande wao na kuthibitisha uwongo wao na kuwa unga mkono katika udhalimu wao, hatakuwa na uhusiano na mimi, na hatakutana na mimi kwenye Haudhi ya Neema. Mtu ambaye hatakuwa na uhusiano nao, hatahalalisha uwongo wao, na hatawaunga mkono katika udhalimu wao, huyo atakuwa ametoka kwangu na mimi nitakuwa nimetoka kwake na atanikuta kwenye Haudhi ya Neema.
.
Mtu yeyote mwenye akili ataelewa kwamba katika hali hiyo Abu Dharr hangejali mamlaka yoyote. Tabia ya Abu Dharr, zaidi ya
kuwa mtu wa kawaida na wa hulka, kuwa matokeo ya mafundisho ya Mtukufu Mtume. Hakuna hata mfano moja uliotajwa kwenye historia za kuaminika kuonesha kwamba katika uhai wake Abu Dharr alisita kusema kweli.
Jalam bin Jandal Ghifari, Gavana wa Qiusarin anasema; "Wakati mmoja, wakati wa ukhalifa wa Uthman nilipokuwa Gavana wa Qiusarin nilikwenda kwa Muawiyah, Gavana wa Syria kwa shughuli za kikazi. Ghafla nilisikia mtu anasema kwa sauti kubwa kwenye lango la ikulu. Msururu wa ngamia unaokuja kwako umebeba Moto wa Jahanamu. Mwenyezi Mungu na awalaani wale wanao waambia wenzao kufanya matendo mema, lakini wao wenyewe hawafanyi hivyo. Mwenyezi Mungu na awalani wale wanaowakataza wenzao kufanya matendo maovu ambapo wao hufanya maovu.
"Wakati huo niliona kwamba uso wa Muawiyah ulibadilika rangi kwa sababu ya hasira. Aliniuliza kama nilikuwa humtambua mtu huyo, ambaye alikuwa analia. Nilimjibu hapana. Halafu Muawiyah akasema, 'Huyu ni Jandab bin Janedah Ghifari. Huja kwenye lango la Ikulu yetu kila siku na kurudia maneno yale yale ambayo uliyasikia muda mfupi uliopita. Halafu akaamuru auawe. "Ghafla nikamuona Yaqudunah anamleta Abu Dharr akimburuza na akamsimamisha mbele. Muawiyah akamwambia, ewe adui yake Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kila siku unakuja kwetu na kurudia rudia maneno hayo. Hakika ningekwisha kukuua kama ningeweza kumuua sahaba wa Mtume bila ruhusa ya Uthman. Sasa nitaomba ruhusa kuhusu wewe." Nikataka kumuona Abu Dharr kwa sababu anatoka kwenye kabila letu. Nilipomtazama, nilimuona alikuwa amesinyaa, mwembamba na mrefu. Ndevu zake hazikuwa nyingi, na mgongo wake ulikunjika kwa sababu ya kuzeeka.
Abu Dharr alimjibu Muawiyah; "Mimi si adui yake Mwenyezi Mungu na Mtume Wake lakini wewe ndiye adui yake Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na baba yako pia alikuwa adui yake Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Nyinyi watu mlitangaza Uislamu kwa maslahi ya kibinafsi lakini katika nyoyo zenu mlikuwa makafiri. Mtume wa Uislamu alikulaani mara mbili na alikuapiza hivyo kwamba ule bila kushiba. Nimesikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba Umma wake utadhani fitina ya mtu mwenye macho makubwa na koo pana, ambaye hatosheki chakula ingawa hula sana, pale atakapokuwa mtawala wa umma huu.
Aliposikia hivi Muawiyah akasema; "Mimi si yule Mjumbe wa Mwenyezi Mungu," alisema; Abu Dharr akasema; 'Ewe Muawiyah! Haina maana kukanusha kwa hakika wewe ni mtu yule yule na sikiliza! Mtume ameniambia kwamba mtu huyo alimaanisha wewe na wewe peke yako. Ewe Muawiyah! Siku moja ulipokuwa unapita mbele ya Mtume, nilimsikia akisema; Ee Mwenyezi Mungu! Mlaani huyo na ulijaze tumbo lake vumbi. Ewe Muawiyah! Nimemsikia Mtume akisema pia kwamba upande mmoja wa Muawiyah upo kwenye Moto wa Jahanamu. Aliposikia hivi, Muawiyah alicheka kicheko cha aibu, akaamuru Abu Dharr akamatwe, akapelekwa jela na akamwandikia barua Uthman kuhusu jambo hili.
Baada ya kumpeleka Abu Dharr jela Muawiyah katika barua aliyo mwandikia Uthman alilalamika kuhusu Abu Dharr kwa maana kwamba angeondolewa Syria na kurudishwa Madina. Kufuatana na Barua hiyo Uthman alimrudisha Abu Dharr Madina. Kwa mujibu wa tafsiri ya Tarikh Atham Kufi Shafii
Maudhui yake ni kama yafuatayo:
"Baada ya heshima ipasayo kwako Muawiyah bin Sakhr kwa unyenyekevu kwa kusema kwamba Abu Dharr amewachochea watu wa Syria waasi dhidi yako. Anawahamasisha watu wakuchukie wewe. Anawakumbuka Umar na Abu Bakr kila wakati na anakumbusha kuhusu mwenendo na uadilifu wao mzuri. Hukutaja wewe kwa kutumia maneno mabaya na husema maneno yako na matendo yako ni maovu na yenye makosa. Haifai kumruhusu aishi Syria, Misri na Iraq kwa sababu watu wa nchi hizi ni wapenda fitina na huungana na watu wachochezi haraka na kusababisha ghasia. Nimekutaarifu kuhusu yaliyo jitokeza. Sasa vyovyote khalifa atakavyo amua ni bora. Wasalam."
Mpanda ngamia aliondoka na barua ya Muawiyah na kuiwasilisha kwa Uthman huko Madina. Mara baada ya Uthman kupokea barua hiyo alirudisha majibu kwa Muawiyah mara moja. "Ninayo barua yako; nimekwisha elewa ulichoandika kuhusu Abu Dharr. Mara upatapo barua hii msafirishe Abu Dharr aje Madina kwa kutumia ngamia wa mwendo wa haraka ambaye ataendeshwa na mtu mwenye moyo mgumu ambaye atamkimbiza ngamia mchana na usiku ili Abu Dharr achoke na alale ili asahau kusema mambo yako na yangu."
Baada ya kupokea barua hii, Muawiyah alimwita Abu Dharr na akamsafirisha kwenda Madina kwa kupanda ngamia asiye na tandiko la kukalia na ambaye ni mtundu na mwendeshaji mbaya. Muawiyah alimwagiza mwendesha ngamia kumfanya ngamia akimbie usiku na mchana bila kupumzika hadi Madina. Abu Dharr alikuwa mrefu na mwembamba na wakati huo tayari alikuwa mzee sana hivyo kwamba nywele na ndevu zake zilikuwa kijivu. Zaidi ya haya alidhoofu sana. hapakutandikwa
nguo au tandiko la kukalia kwenye mgongo wa ngamia huyo. Mshika hatamu wa ngamia hakuwa na huruma naye. Kwa sababu ya matatizo yote haya na majeraha, mapaja ya Abu Dharr yalipata majeraha na alihisi maumivu makali na kuchoka.
Waandishi wa historia wanakubaliana kwamba Abu Dharr alipelekwa Madina peke yake. Familia yake haikuwa naye. Labda inaezekana hakuruhusiwa kwenda nyumbani kwake kuchukua familia yake. Lazima aliitwa kutoka jela na kusafirishwa kwenda Madina moja kwa moja.
Kwa mujibu wa Allamah Majlis na Allamah Subaiti Abu Dharr alipokaribia kuondoka kwenda Madina, taarifa iliwafikia Waislamu ambao walikwenda kumuona na kumuuliza alikuwa anakwenda wapi. Abu Dharr akajibu; "Uthman ameniita Madina. Ninakwenda kuitika wito wake. Enyi Waislamu! Uthman alipohisi nimekosea, alinileta hapa kwenu. Sasa ninaitwa tena Madina. Ninatambua kwamba safari hii nimeitwa ili niteswe. Lakini ni muhimu mimi, kwenda, kwa vyovyote vile. Sikilizeni! Uhusiano wangu na Uthman utabakia hivi. Msisikitike na msiwe na wasi wasi kuhusu suala hili."
SURA YA KUMI NA TANO
Abu Dharr alipokuwa anaondoka, watu walimsindikiza kumuaga hadi walifika dair Maran sehemu iliopo nje ya jiji. Hapo aliswali Swala ya jamaa. Halafu akahutubia watu na tafsiri yake ni kama ilivyotolewa na Hayatul Qulub.
"Enyi watu! Ninawaachieni wasia wa kitu ambacho kitakuwa na manufaa kwenu." Baada ya hapo aliwaambia wamshukuru Mwenyezi Mungu. Wote wakasema, "Sifa zote zinastahiki kwake Mwenyezi Mungu." Halafu Abu Dharr akashahidilia Upweke wa Mwenyezi Mungu na Utume wa Muhammad na wote wakasema kama alivyosema. halafu akasema; "Ninakiri kuwepo kwa Ufufuo na Siku ya Hukum na kuwepo kwa Pepo na Jahanamu. Ninaamini yale ambayo Mtume alileta kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ninawatakeni mshuhudie hii imani yangu." Wote wakasema, "Tunashahidilia yale ambayo umeyasema. "Baada ya hapo akasema, "Yeyote miongoni mwenu atakaye kufa akiwa kwenye imani hii atapata habari njema za huruma na wema wa Mwenyezi Mungu almuradi yeye si msaidizi wa watenda dhambi anayeunga mkono matendo ya wagandamizaji, mshirika wa madhalimu. Enyi kundi la watu! Ghadhabu na msononeko iwe pia sehemu ya Swala zenu na kufunga Swaumu, mnapowaona watu wanafanya dhambi kinyume na matashi ya Mwenyezi Mungu. Msiwafurahishe viongozi wenu kwa vitu ambavyo ni sababu ya hasira ya Mwenyezi Mungu. Endapo watu hao wanaingiza vitu katika imani ya Mungu ambavyo ukweli wake hamjui, waacheni na mfichue makosa yao hadharani, hata kama watawatesa na kuwaondoeni kwenye makundi yao, hata kama watawanyang'anya zawadi zao, na kuwahamisheni kutoka kwenye miji, ili Mwenyezi Mungu apate kufurahishwa na nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ametukuka mno na yuko Juu sana. Haistahili kumkasirisha Yeye kwa sababu ya kuwafurahisha viumbe Vyake Mwenyezi Mungu na waghufirie nyinyi na mimi. Sasa ninawaacheni kwa Mwenyezi Mungu na ninawatakia amani na huruma za Mwenyezi Mungu."
Wote wakajibu; "Ewe Abu Dharr! ewe sahaba wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na akuweke salama na akuridhie neema Zake! Hungependa tukuchukue tena tukurudishe jijini kwetu na tukuunge mkono mbele ya maadui." Abu Dharr akasema; "Mwenyezi Mungu na akupeni rehema! Sasa mnaweza kurudi. Hakika mimi ni msitahimilivu zaidi kwenye mabalaa kuliko nyinyi. Kamwe msifarakane na msiwe na wasiwasi na msitofautiane miongoni mwenu."
Waandishi wa historia wanasema kwamba Abu Dharr alipofika Madina akiwa ameiacha familia yake Syria, akiwa amenyong'onyea na kuchoka sana alipelekwa mbele ya mfalme wa wakati huo, Khalifa Uthman. Wakati huo watu wengi walikuwepo kwenye baraza. Mara Khalifa Uthman alipomuona Abu Dharr, alianza kumshutumu bila kujali heshima yake mbele ya Mtukufu Mtume. Inaonekana kwenye wasomi wa histoira kama vile Uthman alisema chochote kilichokuwa akilini mwake akiwa kwenye hasira na ghadhabu. Hata alisema, "Ni wewe ndiye ambaye amefanya matendo yasiyostahili." Abu Dharr akasema, "Mimi sikufanya lolote isipokuwa nilikupa ushauri na ukauwelewa vibaya ushauri wangu na ukanihamisha na kunipeleka mbali na wewe. Halafu nika,shauri Muawiyah. Na yeye pia hakupenda ushauri wangu na amenihamisha na kunipeleka mbali na yeye ." Uthman akasema; "Wewe ni mwongo. Wewe unaendekeza uhaini akilini mwako. Unataka kuichochea Syria iniasi mimi." Abu Dharr akasema; "Ewe Uthman! Fuata nyayo za Abu Bakr na Umar tu na hakuna mtu atakayesema lolote dhidi yako." Uthman akasema, "Kuna umuhimu gani mimi kufuata nyayo zao au nisifuate nyayo zao. Mama yako na afe!" Abu Dharr akasema; "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, huwezi kunishutumu mimi kwa lolote isipokuwa mimi ninawaelekeza watu wafanye matendo mema na kuwakataza wasifanye matendo mabaya.
Aliposikia maneno haya Uthman alijaa hasira na akasema, "Enyi wazee wa baraza! Nipeni ushauri nimfanye nini huyu mzee mwongo. Nimpe adhabu ya kumtandika viboko, nimfunge jela, auawe, au nimpeleke uhamishoni. Amesababisha wasiwasi katika jamii ya Waislamu." Baada ya kusikia hivi, Ali ambaye alikuwepo hapo, alisema; "Ewe Uthman! Nina kushauri wewe kama muumini wa taifa la Firauni umwache mtu huyo alivyo. Endapo yeye ni mwongo basi atapata malipo yake na kama yeye ni mkweli hakika wewe ndiye utakaye umia. Mwenyezi Mungu hamwongozi yule ambaye ni mbadhirifu na mwongo." Hapa palitokea mabishano makali kati ya Uthman na Ali ambayo sitaki kuyaeleza hapa.
Muhammad bin Ali bin Atham Kufi, Ameandika kuhusu mzozo huo:
11
MAISHA YA ABU DHARR
Ali alimwambia khalifa Uthman, "Usimsumbue Abu Dharr. Endapo yeye ni mwongo atateseka kufuatana na matokeo ya matendo yake, na kama ni mkweli, yale anayoyasema yatatokeza dhahiri." Uthman hakukubaliana na usemi huu wa Ali. Alimwambia Ali kwa hasira, "Usiingilie jambo lisilokuhusu! Ali pia alirudia maneno hayo hayo. Halafu Ali akasema; "Ewe Uthman! Unafanya nini sasa? Ni dhuluma iliyoje unaifanya sasa! Haistahili wewe kutamka maneno kama hayo kuhusu Abu Dharr ambaye ni rafiki yake Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya mambo yasiyojulikana ambayo Muawiyah ameyasema. Hivi huna habari kwamba upo upinzani, ugandamizaji, maasi na uovu wa Muawiyah? Aliposikia hivi Khalifa Uthman alinyamaza."
Sayed Nurullah Shustari ameandika kwamba mara tu Abu Dharr alipomuona Khalifa Uthman mbele yake alikuwa na desturi ya kukarir Aya ya Qurani; "Iogope siku ambapo Moto wa Jahanamu utaunguza nyuso zao na zitapigwa chapa." Akimaanisha kusema kwamba, 'Ewe Uthman! Ni kosa kwako unapoacha kuwapa masikini utajiri unao hodhi lakini unapotoa, huwapa ndugu zako. Siku hiyo ipo karibu ambapo pande zako na uso wako utapigwa chapa huko Jahanamu."
Kwa mujibu wa Tabari ilitokea Ali alimwambia Uthman; "Umeacha kufuata nyayo za wale waliokutangulia na sasa kwa urahisi tu unazidisha kuwapa mali uzao wa Umayyah na ndugu zako. Umewasahau masikini kabisa unavyofanya si sawa hata kidogo. Umepata wapi haki ya kugawa rasilimali ya Waislamu kwa njia ya
dhuluma?" Uthman akakasirika aliposikia maneno haya ya Ali na akajibu, "Wale walio tangulia waliwakosea ndugu zao. Mimi sitaki kufanya hivyo. Nitawapa ndugu zangu masikini kile nitakachoweza." Ali akasema; "Ndio hao tu watu wenye haki ya kuwapa maelfu ya dinari kutoka kwenye Hazina ya Taifa ya waislamu? Hakuna masikini mwingine?"
Waandishi wa historia kama Abul Hassan Ali bin Husein bin Ali al-Masudi (alifariki maka 346 A.H) Ahmad bin Abi Yaqubi na Ishaq bin Jafar bin Wahhab bin Wazeh Yaqubi (alifariki mwaka wa 278 A.H), na Muhammad bin Sad al-Zahri al-Basri, Katib al-Abbasi al-Waqidi (alifariki mwaka 230 A.H) wamesimulia tukio hili hivi: Abu Dharr alipofikishwa kwenye baraza la Uthman alimwambia Abu Dharr; "Nimeambiwa kwamba umewaambia watu hadithi ya Mtume kwamba wakati idadi ya wanaume wa Bani Umaah thelathini kamili, wataifikiria miji yote ya Mwenyezi Mungu kuwa ngawira yao na waja wa Mwenyezi Mungu watumishi wao wa kiume na wakike na wataifanya dini ya Mwenyezi Mungu kama udanganyifu." Abu Dharr akasema, "Ndoto, nimemsikia Mtume anasema hivyo." Uthman akawauliza wasikilizaji wa baraza, "Mlimsikia Mtume anasema hivyo?" Wakasema, "hapana!" Halafu akamwita Ali na akasema, "Ewe Abul Hassan! Unathibitisha hadith hii?" Ali akasema; "Ndio." Uthman akasema; "Nini uthibitisho wa ukweli wa hadithi hii?" Ali akajibu, Usemi wa Mtukufu Mtume kwamba hakuna msemaji chini ya mbingu na juu ya ardhi, ambaye ni mkweli kuzidi Abu Dharr."
Abu Dharr alikaa Madina kwa siku chache tu baada ya tukio hili ambapo Uthman alimpelekea ujumbe kwamba, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, hakika utahamishwa kutoka Madina."
Allamah Majlis ameandika kwamba baada ya kurudi kutoka Syria, Abu Dharr aliugua. Siku moja aliingia barazani akiwa na mkongojo. Alikuwa ndio amefika hapo ambapo maofisa wa serikali waliingia hapo wakiwa na dinari 100,00, ambazo walikusanya kutoka sehemu mbali mbali za nchi. Mara tu Abu Dharr alipoziona akasema, "Ewe Uthman! Rasilimali hiyo ni ya nani?" Akajibu, "Rasilimali ya Waislamu." Akauliza, "Itakuwa kwenye hazina hadi lini kabla haijawafikia Waislamu?" Khalifa akasema, "Fedha hii nitakuwa nayo hadi zitakapopatikana dinari zingine 100,000, kwa sababu wameniletea mimi utajiri huu. Kwa hiyo, ninangojea zingine zaidi, ili niweze kumgawia yeyote ninayemtaka, na kuzitumia ninapoona pana stahili." Abu Dharr akasema, "Zipi nyingi, dinari nne au 100,000?" Uthman akasema; "100,000 ndizo nyingi." Aliposikia hivi Abu Dharr akasema:
Ewe Uthman! Hukumbuki ya kwamba siku moja wewe na mimi tulikwenda kwa Mtume usiku sana na tulipomuona amehuzunika tukamuuliza sababu ya huzuni yake, hata hakusema na sisi kwa sababu ya uzito wa majonzi yake. Halafu tuliokwenda kumuona tena asubuhi tulimkuta anafurahi na anacheka, tukamuuliza kwa nini usiku wa jana yake alisema na huzuni sana na kwa nini alifurahi sana asubuhi hiyo, Usiku wa jana, baada ya asubuhi hiyo, Usiku wa jana, baada ya kugawa rasilimali ya Waislamu zilibaki dinari nne tu, kwa hiyo nilifadhaika sana. Lakini nimempa mtu aliye na haki ya kuzipata. Kwa hiyo, sasa ninafurahi."
SURA YA KUMI NA SITA
Tumeonesha kwa ufupi kuhusu Uthman kwenye kurasa za nyuma, na tumesema , kwamba kwa kugawa fedha ya Waislamu miongoni mwa ndugu zake tu alikuwa anawanyima haki watu masikini. Abu Dharr, kwa ajili ya ushupavu wake wa kidini katika kufuatilia mafundisho
matukufu ya Mtume, alilazimika kupiga kelele kukemea maovu hayo. Matokeo yake alipelekwa Syria. Halafu aliitwa kutoka Syria na kurudi Madina kwa namna ya kuadhibiwa. Akawekwa katika taabu nyingi. Kwa kuwa Abu Dharr alikuwa mtu mwenye msimamo na alikuwa makini katika kutimiza ahadi yake ya kuwa mkweli ambayo alimwahidi Mtukufu Mtume, aliendelea na kazi yake bila kujali mamlaka yoyote au shutuma kutoka popote pale. kamwe hakujali ama alikuwa anazungumza kwa mfalme au kwa mtu wa kawaida. Hakujali kama pale alipokuwa anasema ni mtaani, sokoni, msikitini au baraza. Mzigo na aina ya kilio chake cha ukweli ulikuwa ni ule ule.
Sasa tunataka kuandika kwa kina kwa taarifa yako jinsi Uthman alivyofungua mlango wa Hazina ya Taifa kwa ajili ya washirika wake na jinsi ndugu wa wafuasi wake walivyo tajirika kupindukia. Hapa tunaorodhesha majina ya watu kuhusu na jambo hili ambapo itakuwa rahisi wewe msomaji kuamua jinsi wale waliofuata nyayo za Mtume(s.a.w.w)
yaani Ali, Abu Dharr, Salman, Miqdadi, Ammar, na masahaba wengineo wa Mtume, walivyoweza kuwa kimya. Hata hivyo, wao pia walikuwa na wajibu wao kwa Uislamu. Ndio sababu watu hawa waolifanya upinzani dhidi ya utendaji wa aina hiyo.
Sasa tunataka kunukuu mifano michache ya ubadhirifu na upendeleo wa Uthman. Lakini, kabla ya hapo tunataka kuelezea jinsi fikra ya kuionesha upendeleo kwa uzao wa Umayyah ilivyo anza akilini mwake na jinsi alivyo vuka mipaka ya mwenendo mwema. Bin Asakir, mwandishi wa historia na mtoa maoni wa labda karne ya pili ya A.H ameandika:
Kwa mujibu wa simulizi za Anas bin Malik, siku moja Abu Sufyani bin Harb, ambaye alikwishapofuka, alikwenda kwa Uthman na akauliza kama palikuwepo na mtu mwingine pale. Masahaba wake wakasema, 'hapana." halafu akasema, "Ewe Uthman! Ifanye serikali hii ya Kiislamu iwe ya kabla ya Uislamu; iache inchi iwe kama ile
iliyonyakuliwa kutoka kwa mtu na uitunze iwe ya kudumu kwa ajili ya uzao wa Umayyah."
Waheshimiwa wasomaji! Ni Abu Sufyani yule yule aliyemfanyia Mtukufu Mtume karaha zisizo na mfano kabla ya Uislamu. halafu akaingia kwenye Uislamu bila kupenda. Hakuheshimu Uislamu katika yakini ya moyo wake.
Uthman alikubali ushauri wake akawaunga mkono kwa ukamilifu Bani Umayyah, akawafanya kuwa matajiri na kufanya serikali kuwa nchi iliyonyakuliwa kutoka kwa mtu, akaanza kuwatendea matendo mabaya na kuwadharau wenyewe wa mwanzo. Ni dhahiri kwamba haki ya kumiliki utawala ulitakiwa uende kwa Ali na uzao wake. Kwa hiyo, Uthman kuwatendea uonevu kama alivyoshauriwa na Abu Sufyani haiendani na utaratibu uliowekwa.
Inathibitika kutoka kwenye maelezo ya kihistoria kwamba usiku huo alipofariki Umm Kulthum, Uthman alifanya tendo la ndoa na mwanamke mwingine bila kumjali yule anayeugua kwa sababu ya kwamba alikuwa na uhusiano wa kindugu na Mtume.
Maelezo kuhusu sababu ya watu kuwa wapinzani wa Uthman waandishi wa historia wameandika kwamba Uthman alimpa Marwani bin Hakam, Fadak (Kiunga kilichoporwa kutoka kwa Fatimah wakati wa utawala wa Abu Bakr -khalifa wa Kwanza).
Fadak ni rasilimali iliyobakia kwenye miliki ya Marwani na wazao wake hadi hapo Umar bin Abdul Aziz aliichukua kutoka kwake na akawarudishia kutoka Ahlul Bait ambao ndio walikua na haki ya kumiliki.
Uthman hakumpa Marwan bin Hakam alikuwa binamu yake na mume wa bint yake, Umme Aban, umilikaji wa Fadak tu lakini alimpa pia sehemu yatano (1/5) ya ngawira iliyopokelewa kutoka Afrika yaani dinari laki tano ambazo Abdul Rahman bin Hanbal al-Jamai al-Kindi wakati anazungumza na Khalifa alikariri aya za kejeli. Kwenye mojawapo ya Aya hizi anasema;
"Ewe Khalifa! Ulimleta Marwan aliyelaaniwa karibu sana na wewe kinyume na walivyofanya wale waliokutangulia na ukamfanya kuwa mkwe wako, na halafu ukampa moja ya tano ya ngawira ya Afrika ukawadhulumu masikini."
Waandishi wa historia bin Kathir na Waqidi wanasimulia kwamba jumla ya thamani ya ngawira ya Afrika aliyopewa Marwan ilikuwa sarafu za dhahabu elfu ishirini.
Tabari anasema kwamba ilikuwa dinari laki tano, sarafu aza dhahabu elfu ishirini
Zaidi ya haya pia alipewa moja ya tano ya ngawira kutoka Misri. [62]
.
Bin Abil Hadid ameandika, khalafu alipomuoza mwanae kwa Marwan pia alimpa dinari laki moja kutoka kwenye Hazina ya Taifa. Kwa kitendo hiki, Zayd bin Arqam alimtupia Uthman funguo za hazina na akasema kwamba Marwan hakustahili kupewa hata dinari mia moja
.
Waandishi wa historia wote, watoa maoni, wahadithi na wasimulizi miongoni mwao, dinari Aishah anashika nafasi ya kutambulikana.
wanasema wazi kwamba wote wawili Marwan na baba yake Hakam na pia uzao wao alilaaniwa na walichukiwa na Mtume. Aishah anasema kwamba Marwan alizaliwa kutokana na mbegu ya kiume iliyolaaniwa na Mtume hakuvumilia kuishi kwao hapa duniani. Mwenyezi Mungu aliwatangaza wao, wahenga wao na wazao wao mti wa nasaba iliyolaaniwa na Mtume wa Mwenyezi Mumngu alimhamisha Hakam kutoka Madina. Abu Bakr na Umar pia hawakuwaruhusu kurudi. Lakini Uthman aliwarudisha, akawapa zawadi na akamwoza binti yake Umm Aban kwa Marwan.
.
Marwan bin Hakam aliporudi kwa kuitwa na Uthman alivaa matambaa na alipotoka ndani ya baraza lake alivaa nguo za hariri na josho. Khalifa alimpa laki tatu kutoka kwenye sadak ya Yemen.
Ni mtu ambaye alihamishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu na Abu Bakr na Umar pia hawakumruhusu kuingia Madina. Lakini Uthman alimwita akampa zawadi ya dinari laki moja
.
Harith bin Hakim alikuwa ndugu yake Marwan na mume wa Ayesha bint yake Uthman. Uthman alimpa dinari laki tatu kutoka kwenye rasilimali ya Waislamu. Pia kama sadaka
. Uthman pia alimpa soko "Mahzuni, ambalo liliasisiwa na Mtume hapo Madina.
Zaidi ya hii, sehemu ya kumi (1/10) ya pato lililopokelewa kutoka kwenye masoko ya Madina pia ikitengwa kwa ajili ya Harith.
Uthman alimpa Said bin Aas bin Umayyah dinari laki moja. (Abu Makhnaf na Waqidi) Aas baba yake na Said alikuwa mtu aliyekuwa na tabia ya kumtesa sana Mtume Ali alimua kwenye vita ya Badr
. Said mtu ambaye wakati moja alimwita Hashim bin Utabah mtu mwenye jicho moja kwa dharau wakati wa kuangalia mwezi. Mtu huyu alipoteza jicho moja katika vita ya Siffin. Matokeo ya kejeli ya Said masahaba waheshimiwa wa Mtume wakampiga na kuichoma nyumba yake. (Tabaqat bin Sad). Inaeleweka kwamba Ali, Talha, Zubayr na Abdul Rabman bin Auf alipinga kitendo cha Uthman kumpa Said dinari laki moja, lakini khalifa hakujali
.
Uthman alimpa kaka yake wa kambo Walid bin Uqbah bin Abi Muit bin Abi Umar bin Umayyah mkopo wa dinari laki moja kutoka kwa Abdullah bin Masud, mweka hazina wa Kufah. Baadaye, bin Masud alimwambia arudishe fedha hizo za Hazina ya taifa, alimwandikia barua Khalifa kwamba bin Masud alimwambia arudishe deni la fedha za Hazina ya taifa ambazo yeye Uthman alimpa. Tukio hili lilimfanya Khalifa Uthman aandike barua kwa Abdullah bin Masud, "Wewe ni mweka hazina wangu. Ninakuamuru usimwambie Walid kurudisha deni ambalo amekopa kutoka Hazina ya taifa, wala usikatae kutekeleza amri hii."
Alipoona hali hii, Abdullah bin Masud alikwenda kwenye msikiti wa Kufah siku ya Ijumaa na akawaambia watu tukio hili la Walid na Uthman bila kuficha. Walid akamtaarifu Uthman kuhusu jambo hili ambapo matokeo yake Abdullah bin Masud alifukuzwa kazi
.
Huyu Walid ni mtu ambaye baba yake, Uqbah alikuwa adui mbaya sana wa Mtukufu Mtume. Kwa mujibu wa simulizi ya Aishah, Mtukufu Mtume mara nyingi alikuwa akisema; "Nimechoshwa na majirani zangu wawili. Mmojawapo ni Abu Lahab na mwingine ni Uqbah bin Abi Muit. Wote wawili, zaidi ya fitina zingine, huacha lundo la uchafu na takataka, mlangoni mwangu."
.
Waandishi wa historia wametengeneza orodha ya watu kama hawa ambamo majina ya Abu Lahab, Uqbah Abu Jahl, Hakam bin Abil, Aas bin Umayyah ni maarufu.
Watoa maoni na waandishi wa historia wanayomaoni kwamba Uqbah ni mtu aliye laaniwa ambaye alikwenda asi baada ya kuingia kwenye Uislamu. Aya hii iliteremshwa kwa ajili yake;
"Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake
." (Surah al-Furqan, 25:27).
Kwa ufupi, yapo maandishi mengi sana kwenye vitabu vya historia na hadith kuhusu tabia mbaya ya Walid na baba yake kwamba kitabu
cha pekee yake kinaweza kuandika kuhusu watu hawa. Kwa ufupi ni kwamba Walid alikuwa asherati, mzinifu, fisadi, na mlevi ambaye alinajisi imani. hapa chini tunaorodhesha baadhi ya matukio muhimu ambayo yana dhihirisha tabia yake:
Kwenye Msikiti wa Kufah, Walid asali Swala ya rakaa nne wakati wa Swala ya alfajiri badala ya rakaa mbili kwa sababu alilewa.
Kwa amri ya Imamu Ali, Abdullah bin Jafar alimwadhibu Walid kwa kumchapa viboko thelathini kwa sababu ya kunywa mvinyo.
Walid bin Aas aliposhikanafasi ya Ugavana wa Kufah baada yake, alihakikisha mimbari ilisafishwa na alisema, "Ondoeni uchafu wa Walid kutoka humo." Na zaidi ya hayo.
Khalifa Uthman alimpa Abdullah bin Khalid bin Usayd bin Aas bin Umayah dinari laki tatu na dinari elfu moja kwa kila mtu wa kabila lake. [77]
Yaqubi ameandika kwamba Uthman alimuoza binti yake kwa Abdullah bin Khalid na Usayd na akaamuru apewe dinari laki sita na kuhusu jambo hili alimwandikia Abdullah bin Aamir kwamba kiasi hicho cha fedha kichotwe kutoka kwenye Hazina ya Taifa ya Basrah
.
Kila mtu anajua tabia ya Abu Sufyani bin Harb, Uthman pia alimpa mtu huyu dinari laki mbili kutoka kwenye Hazina ya taifa fedha hii ilitolewa siku moja alipopewa Marwan bin Hakam dinari laki moja
.
Khalifa Uthman alimpa Abdullah bin Sad bin Abi Sarah kaka yake wa kuchangia ziwa sehemu ya tano ya ngawira kutoka Afrika. Kwa mujibu wa Abul Fida thamani ya ngawira hiyo ilikuwa dinari laki moja
.
Bin Abil Hadid ameandika kwamba Uthman alimpa Abdullah bin Sad ngawira yote iliyopokewa kutoka Afrika ya Magharibi bila kupunguza hata sehemu ndogo kumpa Muislamu yeyote
.
Sad bin Abi Sarah ndiye mtu aliyeingia kwenye Uislamu kabla Makkah haijatekwa. Halafu akahamia Madina na akaasi imani ya Uislamu. Baada ya uasi wake, Mtume wa Mwenyezi Mungu akatangaza kwamba Sad bin Abi Sarah lazima auawe popote pale atakapoonekana hata kama alikuwa chini ya kifumiko cha Ka'abah takatifu. Katika kuangalia mambo haya, Uthman alimficha na akamwombea msamaha akasamehewa
.
Uthman alimpa Talha bin Abdullah dinari laki mbili
na alimpa mifuko kadhaa ya dhahabu na fedha.
Mifano iliyotajwa hapo ju imeonesha upendeleo wa Uthman na jinsi alivyo watengeneza Bani Umayyah wanagalagala kwenye utajiri wa Waislamu. Sasa tunataka kueleza jinsi watu wengine ambao si masahaba walivyoanza kutafuta dunia baada ya kifo cha Mtume na sasa dunia imewashinda. Lakini kabla ya hapo tunataka kuonesha kwamba msukumo waliopewa bani Umayyah na Uthman ilikuwa kinyume na radhi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Mwenyezi Mungu amewaita 'mti uliolaaniwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu amewaita watu walioapizwa na umma. Wasomi wanakubaliana kwa pamoja kwamba Bani Umayyah walikuwa na chuki dhidi ya Mtume.
Ali anasema kwamba kila umma ulikuwa na shida za nambna moja au nyingine Balaa la uma huu ni Bani umayyah.
Kwa mujibu wa maoni yaliyothibitishwa ya Mtume na uzao wake, Bani Ummayah walikuwa balaa la uma lakini msimamo wa Uthman kwao ni kwamba alijivunia kitendo cha kufungua hazina ya Taifa kwa ajili yao. Khalifa Uthman alikuwa akisema; "Hazina ya Taifa ni yetu. Tutatumia kama tupendavyo na hatuta kubali ushauri wa mtu yeyote."
.
Sasa tutatoa maelezo kuhusu urithi kwa baba wa masahaba. Itahakikishwa kutoka kwao utajiri kiasi gani wa Waislamu ulifujwa na Uthman na jinsi alivyo watajirisha ndugu zake.
Zubayr bin Awam alikuwa mkwe wa khalifa wa kwanza.
Alichoacha baada ya kifo chake ni;
Nyumba kumi na moja -Madina
Nyumba mbili -Basrah
Nyumba moja- Kufah.
Nyumba moja Misri.
Alioa wanwake wanne.
Baada ya kutoa theluthi moja (1/3) ya utajiri wake, kila mke alipata robo (1/4) ya thamani ya utajiri wa rasilimali yake yote ilikuwa dinari laki nane.
Muhammad bin Sad al-Dhahri al-Basri, Kitab al-Abbasi al-Qaqidi (Alifariki mwaka 230 A.H), ameandika kwamba alikuwa na mashamba huko Alexandria, Misri na Kufah na nyumba kadhaa Basrah. Alipokea magunia mengi sana ya nafaka kutoka Madina.
Abul Has Ali bin Husain bin Ali Masud alikufa mwaka 346 A.H) ameandika kwamba zaidi ya vitu hivi aliacha farasi elfu moja, watumishi elfu moja, watumishi wa kike elfu moja na sehemu kubwa ya ardhi.
Talha bin Ubaydullah Tamim pia alikuwa mkwe wa Khalifa wa kwanza. Alikuwa na nyumba Kufah iliyojulikana kwa jina la Kanaas. Pato lake la kila siku kutokana na mauzo ya nafaka ilikuwa dinari elfu moja. Alikuwa na nyumba za kulala wageni kadhaa ambazo zilikuwa kati ya Tahama na Taif. Alimiliki ikulu ya hali ya juu sana Madina. Alikuwa na rasilimali Iraq ambayo ilikuwa inazalisha pato la dinari 10,000 kila mwezi Musa bin Talha anasema kwamba aliacha dinari laki mbili fedha taslim. Pia aliacha ardhi ya kilimo. Zaidi ya hayo, aliacha magunia ya ngozi mia tatu yaliyojaa dhahabu na fedha. Bin Jauzi anasema magunia hayo yalitengenezwa kwa ngozi ya ngamia na yalikuwa makubwa sana.