12
MAISHA YA ABU DHARR
Abdur Rahman bin Auf alikuwa shemeji yake Uthman na ni mtu huyu ndiye wakati Umar alimfanya Uthman kuwa Khalifa badala ya Ali, kama ambavyo imekwisha simuliwa. Aliacha ngamia elfu moja, mbuzi elfu themanini na farasi mia moja na aliacha dhahabu nyingi sana hivyo kwamba ilibidi ikatwe kwa shoka ili igawanyike. Alikuwa na wanawake wanne wa ndoa. Kila mmojawao alikuwa na dinari 83,000. Alimtaliki mke mmoja wakati anaugua na alimpa dinari 83,000. Aliacha kondoo 10,000, wenye thamani ya dinari 84,000.
Sasa kutokana na uritha iliooacha sababu iliyomfanya amweke Uthman kwenye Ukhalifa badala ya Ali bin Abi Talib.
Sad bibn Abi Waqqas aliacha dinari 250,000 na nyumba iliyojengwa mahali paitwapo Aqiq. Nyumba hii ilikuwa nzuri, kubwa yenye nafasi ndefu kwenda juu.
wa Tafsir ya kitabu cha Abdul Hamid Jaudatus Sahar kwamba Sad bin Abi Waqqas alikuwa amenakshi sehemu ya ndani ya ikulu yake kwa mawe magumu.
Yala bin Ummayah ambaye alikuwa gavana wa Yemen aliacha dinari 500,000, wadeni wake wengi na ardhi kubwa. Zaidi yake, aliacha rasilimali yenye thamani ya Dinari 100,000.
Zaid bin Thabit ni mtu aliye msaidia Uthman kwa kila njia na alikuwa mnyenyekevu kwake. Alipokufa, aliacha dhahabu na fedha katika hali ambayo haingegawika isipokuwa kuikata kwa shoka na kishoka. Zaidi ya hayo, aliacha mali nyingine iliyokuwa na thamani ya dinari laki moja.
Huu ulikuwa ukarimu, upendeleo na fadhila za Uthman, Khalifa wa tatu kwa watu wake waliokuwa wanamtakia mema. Hakuna mfuasi wa Mtume ambaye angevumilia namna yake ya kugawa utajiri wa
Waislamu miongoni mwa watu wake. Ndio sababu Ali, Salman, Abu Dharr, Miqdadi na Ammar walikuwa wanampinga wakati wote kuhusu tabia yake.
Inawezekana watu wakasema kwamba lolote alilofanya Uthman ilikuwa kwa ajili ya ndugu zake kama alivyo sema yeye mwenyewe kwamba aliwafikiria kwamba walistahili na hakufanya lolote kwa maslahi yake. Jibu la maoni ya Uthman linaweza kuwa mtu asiye zingatia sharia ya dini katika masuala yahusuyo ndugu zake, kwa hakikahatakuwa muangalifu hata kwa mambo yanayo mhusu yeye mwenyewe. Uthman alikuwa na meno kadhaa yaliyotengenezwa kwa dhahabu. Kivazi chake kilikuwa joho la hariri na manyoya ambalo thamani yake ilikuwa dinari mia moja. vazi la mkewe Nailah pia liligharimu dinari mia moja.
Palikuwepo kasha kwenye Hazina ya Taifa huko Madina ambalo lilijaa dhahabu na fedha. Alitengenezesha urembo kwa ajili ya familia yake kutokana na madini hayo. Watu walimpinga sana kuhusu suala hilo, na alizozana na Ali pia, lakini hakujali lolote.
Alijenga ikulu Madina; jingo hilo liliimarishwa kwa mawe na nmara na milango yake ilitengenezwa kwa mbao za mvule zenye ubapa unaoteleza. Alihodhi utajiri mwingi nsana. Alimiliki chemchem kadhaa Madina. Waandishi wa historia wanasema kwamba baada ya kuuawa, aliacha dinari laki hamsini. Miongoni mwa mali zake na vitu vingine vilivyokuwa kwenye miliki yake, vile vilivyokuwa kwenye bonde la Qura na Hunayn peke yake thamani yake ilifika dinari laki moja. Zaidi ya hayo aliacha farasi na ngamia wengi. Kwa mujibu wa bin Sad thamani urith wa bonde la Qura na Khaybar ulikuwa dinari laki mbili.
Na kwa mujibu wa Jovji Zaydan urith huo ulikuwa dinari laki 10.
Zaid yake, aliacha watumishi elfu moja.
Umar khalifa wa pili pia hakuweza kuepuka ladha ya ukabaila. Alikuwa na bustani Hijaz iliyokuwa inaingiza pato la dinari elfu 40 kwa mwaka ambalo alitumia yeye binafsi na familia yake Bani Adi.
kwa mujibu wa hadith ilioko sahih Bukhari, Umar aliuliza kiasi cha deni lake alilotakiwa kulipa Hazina ya Taifa. Watu walifanya hesabu na wakamwambia deni lake lilikuwa dinari elfu themanini na sita. Akawaamuru walipe deni hilo kutoka kwenye fedha ya ndugu zake mwenyewe. Ni kwamba, aliwaambia walipe deni hilo kutoka kwenye rasilimali yake.
Naafe mtumishi wa bin Umar, amekanusha kwamba Umar ahakuwa na deni na amesema ingewezekanaje Umar kwua na deni ambapo mmojawapo wa warithi wake aliuza mgawo wa rasilimali kwa dinari laki moja. (Kitab Madina Umar bin Shaybah).
Akitoa maoni kuhusu usemi wa Naafe bin Hajaz alisema kwamba wakati mwingine hutokea kwamba mtu anakuwa na deni licha ya utajiri wake.
Ndugu alimuomba Umar fedha. Mara ya kwanza alimdharau lakini baadaye alimpelekea dinari elfu kumi.
Yakiwepo mambo kama haya tunapoangalia uzao wa Mtume na jinsi walivyoteseka, tunawasikitikia na tunashtuka sana tunapoona kwamba watu hawa waliwanyang'anya Ahlul-Bait hata ile haki yao yak humus.
SURA YA SABA
Ni ukweli ulio thabiti kwamba Abu Dharr alikuwa karibu sana na Mtukufu Mtume na Ahlul Bait wake na aliendelea kuwa msiri wao mkubwa. Aliona kwa uangalifu sana kila kipengele cha maisha yao, na alijifunza mengi kutokana nao. Ameona kwa macho yake si mara moja lakini mara nyingi kwamba Mtukufu Mtume alikuwa anajilaza msikitini akiwa na njaa na watoto wake nyumbani walikuwa na njaa.
Abu Dharr pia alimuona Ali bin Abi Talib akifanya kazi ya kupokea ujira akiwa amevaa nguo kukwaruza. Aliona majani ya mtende kwenye joho la bint yake Mtume. Pia aliusikia Ali akimnasihi mtumishi wake wa kike Kiafrika Fizzah; "Ewe Fizah! Sisi Ahlul Bait hatukuumbwa kwa ajili ya dunia au kutafuta faida ya kidunia. Badala yake tumeumbwa kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu na kutangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu, Uislamu. Ni kazi yetu kuongoza thamani ya uadilifu wa mtu, kuwasha mwanga wa Upweke wa Mwenyezi Mungu kwenye mioyo ya watu na kuwapa njia na namna ya kuendesha na kustawisha maisha yao.
Abu Dharr pia aliona kwamba Ali alikuwa na kawaida ya kula mkate mkavu wa shayiri na alizika mifuko unga wa Shayiri yake kwa ustadi mkubwa hivyo kwamba haingewezekana mtu kuweka samli.
Pia alimuona Ali kwamba alikuwa na desturi ya kubeba mfuko ya unga yeye mwenyewe kuwapelekea wajane masikini na mayatima. Pia alimuona Ali akiiambia dunia, "Ewe Dunia! Nenda ukawadanganye wengine. Nimetengana na wewe." Pia alishuhudia kwa macho yake kwamba wazawa wa Muhammad walikuwa na tabia ya kula chakula pamoja na watumishi na watumwa wao. Alikumbuka vizuri kwamba
wakati fulani ambapo zilibaki dinari nne zilibaki baada ya Mtume kugawa fedha aliyokuwa nayo na kiasi hiki hakingemfikia mtu anayestahili, alisikitika sana. Alikuwa bado anakumbuka maneno haya ya Mtume aliyomwambia yeye, Ewe Abu Dharr! Hata kama nina miliki dhahabu yenye ukubwa sawa na Mlima Uhud sipendi ibakiea kwangu hata chembe."
Katika hali kama hii, ingewezekanaje Abu Dharr anyamaze wakati Uislamu ulikuwa unageuzwa na mafundisho ya viongozi wa Uislamu yalikuwa yanadharauliwa? Mara tu Mtukufu Mtume alipotawafu kila kitu kilibadilishwa. Dhuluma na udikteta ni hali iliyoshamiri, watu walilazimishwa kutoa kiapo cha uaminifu, nyumba ya Ahlul Bait ilichomwa moto, na mlango ulivunjwa na kumwangusha Fatimah, bint yake Mtukufu Mtume.
Ali alifungwa kwamba shingoni na masahaba mashuhuri waliishi maisha ya upweke majumbani mwao. Katika kulazimishwa na hali halisi Abu Dharr alistahamili kwa kipindi fulani. Hatimaye akaondoka Madina na kwenda Syria na akakaa huko. Baada ya muda alipokwenda tena Madina aliona kwamba viongozi walifika kwenye kilele cha kuendelea mambo ya dunia.
Fahari na maonesho ya kifalme yalishika nafasi ya bustani aliyoishi Mtukufu Mtume. Fadhila na upendeleo ni tabia ambazo zilishamiri, na uaminifu na uchaji Mungu vilionekana kuwa vitu vya zamani. Utajiri wa Hazina ya Taifa ulikuwa unafujwa. Utajiri wa Waislamu ulikuwa unatumiwa kwa maslahi ya binafsi. Kila ndugu na anayemtakia mema khalifa alipata umilionea. Ukabaila ulipanuka. Palikuwepo na utajiri mwingi sana. hakuna mtu aliyejali Zakai. Hakuna Mtu aliyejali mayatima na wajane.
Alipoona mambo mengi yasiyo na idadi kama haya, Abu Dharr alijaribu kumwonya Khalifa Uthman kwa ajili ya kuulinda umma wa Kiislamu na serikali ya Kiislamu na akamshauri kadiri alivyoweza, lakini Khatifa hakutilia maanani ushauri wake. Hatimaye kwa kuzingatia ahadi aliyoahidi kwa Mtukufu Mtume na ule uzio wa imani ambao Mwenyezi Mungu alihifadhi moyoni mwake, alijitokeza uwanjani na akaanza kutangaza dosari za Uthman. kuunganisha na hayo, pia alikemea tabia ya kuhodhi utajiri na ukabaila na alianza hotuba yake na zile aya za Qurani zinazokosoa kuhodhi utajiri.
Kwa kuwa Abu Dharr hakuvumilia kuona utajiri wa rasilimali ya taifa inatumika kwa kuwagawia ndugu zake khalifa tu na mayatima na wajane wanakufa kwa njaa, aliongeza kazi ya mahubiri yake, na kwa hiyo alikwenda sehemu nyingi mbali mbali. Alihamishwa kutoka Madina na kupelekwa Syria na wakati mwingine alilazimishwa kuishi kwenye sehemu iliyokuwa tupu kama Rabzah.
Ni dhahiri kwamba kugawa utajiri miongoni mwa fukara ni muhinu, lakini pia ni muhimu kufikiria utajiri huo ugawiwe kwa kanuni gani kwa masikini na watu wengine wanaostahili. Ilikuwa ni kanuni ya Mtume kwamba aligawa utajiri bila upendeleo. Kuhusu ngawira ya kivita, alisema kwamba moja ya tano (1/5) ilikuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na sehemu nne ya tano (4/5) kwa ajili ya jeshi la Uislamu ambamo mashujaa wote wanapata mgawo sawa. Hakuna anayestahili kupata zaid ya mwingine (Sunan Baihaqi). Inajulikana kutoka kwenye vitabu vya hadithi kwamba alikuwa na kawaida ya kugawa pato la ushuru miongoni mwa Waislamu siku hiyo hiyo ya kupokea pato hilo. Watu waliooa aliwapa mgawo mara mbili na mgawo moja kwa mseja.
Utaratibu huo huo ulifuatwa na Imamu Ali. Hafidh Baihaqi anasema kwamba wakati fulani alipata fedha na rasilimali kutoka Isfaham. Aligawa fedha na rasilimali hiyo katika sehemu saba za mgawo zilizo sawa. mkate wa boflo moja ulibaki lakini aliugawa pia katika vipande saba vilivyo sawa na kuweka kipande kimoja kwenye kila mgawo katika hiyo migawo saba. Aliandika majina na alimpa mtu mgawo ambaye jina lake lilitokea kwenye kura.
Wakati fulani wanawake wawili walimwombea.
Mmojawao alikuwa huru na mwingine alikuwa na asili ya utumwa. Alimpa kila mmoja ngano kidogo na dinari arobaini. Mwanamke mwenye asili ya utumwa alikwenda na mgawo wake lakini yule mwanamke huru akasema, "Umenipa mgawo sawa na ule wa mtumwa, ingawa mimi ni mwanamke huru wa Kiarabu ambapo mwenzangu ni mtumwa na si Mwarabu." Amiri wa Waumini akasema, Nemepelekua kwa uangalifu wa mkubwa Kitabu cha Mungu lakini sikuona sababu yoyote ya ubora wako."
Muhammad Razi Zangipuri ameandika kwamba wakati wa utawala wa Ali ambapo utaratibu wa Mtume alifuatwa na fedha iligawanywa katika misingi ya usawa, hali ya kutokuridhika chuki na kero ilionea miongoni mwa masahaba wa Mtume walio mashuhuri wakipinga mbinu hiyo. Ali akasema kuhusu kuonesha kwao chuki na kero; "Mtakuwa mnaniamuru mimi kwamba nitafute msaada wenu na kuniunga mkono kwa kufanya udhalimu kwa watu ambao kuwa ajili yao mimi nimewafanywa mtawala? Ni kwamba, niwapunje stahili yao ili
nyingi niwazidishe mgawo na kwa hiyo kuwafanyeni nyinyi kuwa watu wanao niunga mkono? Kwa jina la Mwenyezi Mungu hadi hapo ambapo hadithi za usiku zinaendelea kusimuliwa na nyota inafuata nyingine yaani nyota zinakuwa kwenye mwendo, sitakaribia utaratibu kama huo. Hata kama ingekuwa rasilimali yangu binafsi, ningeigawa sawa kwa sawa miongoni mwa watu, lakini sasa inapokuwa hii ni mali ya Mwenyezi Mungu, kwa nini nisizingatie usawa. Lazima mtambue kwamba kugawa fedha na wema bila kuzingatia usawa ni ubadhilifu na ufujaji ambao unamnyanyua mgawaji juu hapa duniani na kumremsha chini na kumfedhehesha huko akhera."
Ni wazi kwamba kutokana na kanuni iliyotajwa kwenye kurasa za nyuma ya kugawa utajiri kwamba rasilimali zitagawanywa bila upendeleo miongoni mwa masikini, wasiojiweza na aina zote za watu wanaostahili. Mara tu Ali alipokalia kiti cha Ukhalifa alitangaza, "Nyingi ni waja wake Mwenyezi Mungu. Utajiri utagawanywa sawa sawa miongoni mwenu bila ubaguzi au kutofautisha.
"
Endapo Waislamu wanafuata njia za Kiislamu, maisha ya umasikini hayatakuwa mzigo kwao.
SURA YA KUMI NA NANE
Baada ya Abu Dharr kurudi Madina kutoka Syria, alijishughulisha na mahubiri yake ambapo tukio lingine la kupasua moyo lilitokea kwa mara nyingine na hilo lilikuwa ni kuchomwa kwa Qurani.
Tayari alikwisha huzunika kuona Serikali ya Kiislamu ilikuwa inaharibiwa. Utajiri wa Waislamu ulikuwa unatumika kuwapa ndugu na jamaa wa Khalifa. Mlango wa Hazina ya Taifa ulifungwa kabisa kwa wanaohitaji, masikini, mayatima na wajane, lakini ulikuwa umefunguliwa wazi sana kwa uzao wa Umayyah. Watu masikini walikuwa wanateseka kwa njaa ambapo ndugu wa khalifa walikuwa wananunua nyumba, mabustani na ardhi. Ghafla akapata taarifa kwamba khalifa alikuiwa na nakala tofauti za Qurani ambazo zilikusanywa kutoka sehemu mbali mbali na akazichoma moto. Kwa hiyo, tukio hili muhimu likawa lenye mahubiri yake.Mwandishi wa historia Abul Fida ameandika kwamba tukio hili lililotokea mwaka wa 30 A.H.
Mwandishi wa historia Yaqubi
ameandika kwenye kitabu chake kwamba Uthman alikusanya Qurani na akazipanga kwa namna ambayo aliziweka sara ndefu pamoja na sura fupi pamoja mbali mbali, na akaagiza nakala kutoka kila sehemu, zikaoshwa kwa maji ya moto na siki na akazichoma moto. Matokeo yake ni kwamba hakuna nakala ya Qurani iliyobakia isipokuwa nakala iliyomilikiwa na Bin Masud ambayo alikuwa nayo Kufah. Abdullah bin Amir, gavana wa Kufah alipomuuliza bin Masud amwoneshe nakala yake akakataa. Uthman alipopata taarifa hii alimwandikia barua Amir amkamate bin Masud na ampeleke kwake Madina. Bin Masud alipoingia msikitini, Uthman alikuwa anatoa hotuba.
Alipomuona Bin Masud akasema; "Mnyama mbaya na katili amekuja." Bin Masud naye alitoa jibu kali. Uthman aliposikia, akaamuru watu wampige. Kwa hiyo, watu wakampiga na kumburuza kwa namna ambayo kwamba mbavu zake mbili zilivunjika.
Imeandikwa kwenye tarjumi ya Kiajemi ya Tarikh Atham Kufi
kwamba Uthman alipasua Quran na ikachomwa mo to. Ni maelezo ya aina haya haya yapo kwenye kitabu 'Successors of Muhammad'
Kwa mujibu wa Majatul Mumin usemi wa Mulla Mohsin Kashmiri, Uthman akavunja mbavu za bin Masud na akamnyang'anya Quran na akaichoma mo to.
Uthman aliamuru Qurani yangu lazima ipewe nafasi ya kuenea kwenye utawala wangu na nakala zingine zichomwe mo to.
Uthman alipeleka taarifa kwa Hafsah, mke wa Mtukufu Mtume, ili ampelekee Maandishi ili aweze kunakili na halafu amrudishie. Hafsah alimpekea nakala alizokuwa nazo na Uthman akamteua Zayd bin Thabit, Abdullah bin Zubayr, Said bin As, Abdul Rahman bin Harith kukusanya na kunakili maandiko hayo, na aliwataka watu hao wote watatu wa Quraishii kuandika Qurani kwa kutumia mazungumzo ya Quraishi endapo pangetokea tofauti fulani katika mambo kadhaa, kwa sababu Qurani iliteremshwa katika lugha yao. Watu hao watatu walifanya kufuatana na walivyoagizwa hadi mwisho na Uthman akayarudisha Maandiko hayo kwa Hafsah kama alivyoahidi na akampelekea nakala iliyotayarishwa upya. Sasa, nakala ya Qurani iliyobakia ni hiyo tu iliyotayarishwa na Uthman iliendelea kuwepo na nakala zingine zote zilichomwa mo to.
Kwa mujibu wa Fathul Bari, usemi wa bin Hajar Asqalani Juz. 4, uk 226, Uthman alirudisha Qurani ya Hafsah lakini Marwan alichukua kwa nguvu na akaichoma mo to. Kwa mujibu wa Tarikh Khamis uk. 270, Istiab uk. 373 na Sawaiq Muhrizah uk. 68 Uthman alihakikisha nakala zote za Qurni zimechomwa moto isipokuwa ya kwake na aliamuru Abdullah bin Masud apigwe sana hivyo kwamba alipata maradhi ya henia
(ngiri). Halafu akamfunga jela na akafia huko. Kwa mujibu wa Tuhfah Ithna Ashariyah, usemi wa Abdul Aziz, Ubayy bin Kab alimpa Uthman Qurani yake na hakupigwa. Qurani hiyo pia ilichomwa mo to.
Kwa hali yoyote ile imeandikwa kwenye vitabu vingi sana kwamba Uthman alichoma maandiko matakatifu. Hizi ni nakala za Qurani zilizokusanywa wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr. Aishah Ummul Muminin alipopata habari ya Qurani kuchomwa moto alikuwa na wasi wasi. Akasema, "Enyi Waislamu! Muueni mtu huyu ambaye anachoma Qurani! Amefanya udhalimu mkubwa sana."
Aishah hakuridhika na jambo hili alifululiza kudhihirisha kero dhidi ya Uthman. Alisema tena na tena; "Muueni Yahudi huyu, Na'thal. Mwenyezi Mungu na amuue. Amekuwa asi."
Kwa mujibu wa Tazkirab Khawasul Ummah uk. 38, 40, 41 bin Athir Jazari alikwua akisema, "Muueni Na'thal huyu. Mwenyezi Mungu na amuue." Kwa matamshi haya alikuwa anamaanisha khalifa Uthman. halafu bin Athir anaeleza kwa nini Aishah alimuita Uthman Na'thal. Sababu ni kwamba Na'thal alikuwa yahudi wa Misri na ndevu zake zilifanana na zile za Uthman. Halafu tena anasema kwamba kufuatana na matamshi ya Shaykh ilimaanisha mpumbavu. Anaendelea kusema kwamba baadae Aishah alikwenda Makkah (Nihayah bin Athir).
Mwandishi wa historia Ibn Taqtaqi ameandika kwamba Uthman aliuawa kwa matokeo ya amri ya Aishah, 'muueni Na'thal huyu." Siku hiyo hiyo nyumba yake ilipozingirwa, Aishah alikwenda Makkah.
Inaeleweka wazi kwamba Aishah akiwa mwanamke alishtushwa na tukio hili, kwa nini Ali asingeshtushwa na tukio hili la kutisha? Imejulikana kutokana na maandishi ya wasomi wa kuaminika kwamba Ali alishtushwa sana na tukio hili la kuchomwa Qurani. Kwa hiyo, aliona umuhimu wa kutaka ushauri wa Abu Dharr kuhusu suala hili. Allamah Majlis ameandika kwamba baada ya tukio hili Ali alimuomba Abdul Malik, mtoto wa Abu Dharr ampeleke baba yake kwake. Alipofika, alibadilishana mawazo naye kuhusu tukio hili, alionesha kuhuzunika kwake na akasema jambo hili limenyoshwa na kupasuliwa vipande vidogo. Inawezekana Mwenyezi Mungu atalipa kisasi kwake kwa jinsi ile ile. Abu Dharr akasema , "Ewe Ali! Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema kwamba wafalme dhalimu watawaua watu wa nyumba yake." Ali akasema, "Ewe Abu Dharr! Unataka kunikumbusha kuhusu kuuawa kwangu?" Abu Dharr akasema, "Hapana shaka, hilo litatokea na wewe utakuwa mtu wa kwanza miongoni mwa uzawa wa Mtume kuuawa."
Kwa ufupi, inaonesha wazi kwamba Abu Dharr aliathirika sana na tukio hili la kuogofya. Pia aliongeza maudhui moja zaidi kwenye ho tuba zake na kuliita tukio hili njia isiyo ya Kiislamu. Na itambulike kwamba kwa kuwa kitendo cha kuchoma Qurani kinatia jeraha moyo wa Kiislamu kwa baadhi ya waandishi wa siku hizi, wamebadilisha neno kuchoma pale ambapo maelezo ya kuchomwa Qurani yanatolewa. Shah Walyullah Dehlavi, kwenye matukio
katika maisha ya Uthman ameandika......Aliyaondoa maandiko
mengine ambayo yalifikiriwa kusababisha migongano.
SURA YA KUMI NA TISA
Waandishi wa historia wanasema kwamba Abu Dharr alitoa hotuba zake kuhusu mada maalum. Msikitini, nje ya msikiti, kwenye baza, kwenye viwanja vya maonyesho ya michezo, mitaani na mahali popote alipopata fursa ya kufanya hivyo. Hakuogopa kuuawa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu alikwisha mwambia kwamba hakuna mtu ambaye angeweza kumua au kumfanya aache imani yake wala hakuogopa shutuma kwa sababu aliapa mbele ya Mtukufu Mtume kuhusu suala hili. Alikuwa na uhakika kabisa kwamba lolote alilofanya ilikuwa linakubaliana na utashi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Ndio sababu alikuwa anashughulika wakati wote katika kutekeleza kazi yake kwa ujasiri na hamasa kubwa.
Kwa upande moja mahubiri ya Abu Dharr yalizidi kupamba moto na kwa upande mwingine Uthman alikuwa anaendelea na zoezi la kuipima dhamiri yake kwenye kioo cha tabia yake mwenyewe. Alitaka ushauri kutoka kwa Marwan ili aweze kujua Abu Dharr angenyamazishwa kwa njia gani na shutuma zake kuhusu tabia ya Uthman na upinzani wake kuhusu kuhodhi utajiri ungesitishwa.
Marwan akasema, "Ipo njia moja tu ya kuweza kufanikiwa ni kwamba, kiasi fulani cha fedha kipelekwe kwa Abu Dharr. Labda anaweza akakubali na kunyamaza." Uthman alisikia jibu hili la Marwan na akanyhamaza. Sababu ya kimya chake ni kwamba alikuwa anatambua tabia ya Abu Dharr. Alijua kwamba Abu Dharr alikuwa hana tama ya fedha. Marwan aliwaita watu wawili, akawapa mfuko wenye dinari mia mbili na akasema, "Mpelekeeni Abu Dharr na mwambieni kwamba Uthman anamtakia kila la kheri na amemwomba akubali kuchukua mfuko huo wa fedha na atumie apendavyo."