HUKUMU ZA KUSISIMUA ZILIZOTOLEWA NA IMAM ALI
KIMEKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA: AMIRALY M H DATOO
KIMETOLEWA WAVUNI NA TIMU YA: AHLUL BAYT DIGITAL ISLAMIC LIBRARY PROJECT
(1). MWANAMKE KUMKATAA MTOTO WAKE
Al-Kulaini na Sheikh Muhyid-Din ibn 'Arabi wameelezea kwa mamlaka ya Aasim bin Hamza Al-Saluli,ambaye anasema kuwa yeye alimwona kijana mmoja akilia katika mtaa mmoja mjini Madina: "Ewe Allah swt! Amua kesi baina yangu na mama yangu." Umar al-Khattab,ambaye alikuwa akipita hapo,alimkanya kijana huyo: "Usilitaje jina la mama yako!" Kijana huyo alisema: "Ewe Amiral-muminiin! Mama yangu alinizaa na kuninyonyesha maziwa kwa miaka miwili, lakini sasa nilipokua,ananikataa kata kata kuwa mimi si mtoto wake.Yeye pia anakana kuolewa na baba yangu,ambaye alishafariki,na anataka kujichukulia milki yote huku akidai kuwa alikuwa ni ndugu yake tu,na hivyo kuninyima sehemu yangu ya urithi."
Kwa kuyasikia hayo, Umar alimwita yule mwanamke ambaye alikuja na mashahidi arobaini wa upande wake. Hao wote walitoa ushahidi kumpendelea yeye. Kwa hayo, Umar alitoa hukumu ya kijana yule kufungwa kwa kosa la 'iftara (kusingizia).
Wakati yule kijana alipokuwa akichukuliwa kifungoni, alikutana njiani na Imam Ali
Kijana yule alimlilia Imam Ali
kumsaidia na akamwelezea kisa chote. Hapo Imam Ali
aliwaamrisha wasindikizaji wake kumpeleka tena kwa Umar. Walipofika Umar aliwauliza sababu ya kumrudisha, nao walijibu kuwa Imam Ali
ndiye aliyewaambia hivyo kuwa wamrudishe. Na wakati huo Imam Ali
alifika hapo na kumwambia Umar kutaka kwake kutoa uamuzi. Kwa hiyo, Umar alisema: "Vyovyote iwe vile, je ni kipi kitakachokuwa afadhali kuliko haya? Mimi nimemsikia Mtume (s.a.w.w) akisema kuwa ilimu yako ni bora kuliko sisi sote
."
Imam Ali
alimwita yule mwanamke pamoja na mashahidi wake wote. Wao wote mmoja baada ya mwingine walisema vile vile walivyokuwa wamesema mbele ya Umar. Baada ya kuyasikiliza hayo, Imam Ali
aliwaambia jamaa zake mwanamke iwapo wataridhika kuolewa kwa mwanamke huyo, nao wote walikubali.
Hapo ndipo Imam Ali
alipomwambia mtumwa wake Qambar alete Dirham 400, na alimwambia yule mwanamke: "Mimi nakuoza wewe kwa huyu kijana kwa mahari ya Dirham 400." Wakati Dirham zilipoletwa alimkabidhi kijana huyo na alimwambia aende na mwanamke huyo na ampatie mahari yake.
Wakati yule kijana alipotaka kuondoka, Imam Ali
alisema: "Njoo kwangu tena, kwa sharti la kupitisha usiku mmoja kama bibi na bwana!
"
Kwa kuyasikia hayo, yule mwanamke akapiga kelele: "Loh! Ewe nduguye Mtume (s.a.w.w) wewe unanioza mtoto wangu?
"
Mwanamke akaomba msamaha na kwa kushika mkono wa mtoto wake, wote waliondoka kwa furaha.
Baada ya hao wote kuondoka Bwana Umar alisema: "Lau asingalikuwapo Ali, Umar angalikuwa ameangamia
.
Tukio hilo pia limeelezwa na Sahab Fazail ibn Shaazan kutokea Waqadi, kutokea Jabir na kutokea Salman kwa wakati, pamoja na tofauti kidogo.
(2). MTUMWA ADAI BWANA WA BWANA
Imeelezwa na Kulaini na Sheikh kwa mamlaka ya Imam Ja'afar as-Sadiq
kuwa katika kipindi cha Ukhalifa wa Imam Ali
watu wawili, mtumwa na bwana, walikuwa wakielekea kufa baada ya Hijja.
Mtumwa alifanya kosa na bwana wake alimpiga kwa kosa hilo. Hapo kwa maajabu, yule mtumwa alimwambia bwana wake. "Loh! Wewe u mtumwa wangu na wanipigia bure tu!" Ama kwa kusikia hayo, watu waliokuwa katika msafara huo walistaajabishwa na hawakuweza kuamua baina yao, na huyo mtumwa alirudia kila mara, hadi wakaingia mjini kufa.
Bwana alimwambia mtumwa: "Twende kwa Amir ul Muminiin ili tuamuliwe, "Kwa hayo Mtumwa alikubali na hivyo walitokea mbele ya Imam Ali
, na wakati walipokuwa wakitoa maelezo na hoja zao, wote walidai kuwa bwana. Yule mtu aliyekuwa bwana wa kweli alielezea akililia: "Baba yangu alinipeleka Hijja na wakati tulipokuwa tukirudi mtumwa huyu alifanya makosa ambayo nilimpiga. Hivyo hizi ndizo, mbinu zake za kutaka kunidhulumu mali yangu yote
."
Na mtumwa pia alielezea vivyo hivyo huku akila kila aina ya viapo. Baada ya kuwasikiliza wote wawili, aliwaambia: "Nendeni na mrudi kwangu hapo kesho.
"
Imam Ali
aliamrisha kutobolewa matundu mawili katika ukuta kiasi cha kupitisha kichwa cha mtu mmoja hadi mabega. Siku ya pili, wote wawili walifika mbele ya Imam Ali
, na waliamrishwa kuweka vichwa vyao katika yale matundu, kila mmoja. Baada ya hapo, Imam Ali
alimwamwa ni wake, hadi kuchukuliwa kwa Umar ambaye pia aliona ugumu kufikia hukumu. Hivyo nae pia aliielekeza kesi hiyo kwa Imam Ali
ili ipatiwe ufumbuzi ipasavyo.
Imam Ali
aliwaita wanawake wote wawili na kujaribu kuwatishia. Lakini wote wawili hawakuogopa wala kushtushwa kwa hayo na walibakia katika mabishano yao, ukaidi wao!.
Imam Ali
alitamka "Nileteeni msumeno mkali!"
"Je wataka kuufanyia nini?" Wote wawili waliuliza.
"Nitamkata mtoto katika sehemu mbili zilizo sawa, na nitawapatieni kipande kimoja kimoja kila mtu
."
Mmoja wao alibakia kimya wakati mwingine alisema: "E Mungu wangu! Abul Hasan, iwapo hapana ufumbuzi mwingine, basi mwachie huyo mwenzangu amchukue huyo mtoto, ninamwachia." huku machozi yakimtiririka.
Imam Ali
alisema: "Allah akbar! Huyu ndiye mtoto wako na wala si wa mwenzako. Iwapo angalikuwa mtoto wake, basi naye pia angalihangaika na kutapatapa
."
Kwa hayo huyo mwanamke mwenye madai ya uongo alikiri kuwa yu mwongo.
Hivyo Bwana Umar alisaidiwa na alimshukuru Amir al Muminiin
kwa kumwokoa katika maamuzi yake.
(3). WANAUME NA AMANA
Imeripotiwa na kulaini na Sheikh kwa mamlaka ya Zazaan kuwa wanaume wawili waliweka amana yao kwa mwanamke mmoja kwa masharti kuwa asiwarudishie amana hiyo hadi wao wote wawili waje kwa pamoja.
Baada ya muda kupita, mmoja wao alimwendea yule mwanamke na kumwambia: "Nipe ile amana yetu tuliyokuachia kwani mwenzangu amefariki. "Yule mwanamke alimpa amana hiyo kwa kuyaamini ayasemayo. Baada ya muda kupita, akaja yule mtu wa pili akielezea vile alivyokuwa ameelezea mtu wa kwanza.
Mtu huyo alipoelezwa yaliyotokea, alimshtaki mwanamke kwa Bwana Umar, ambaye alishindwa kutoa hukumu, hiyo alielekeza mbele ya Imam Ali
kwa kupatiwa hukumu.
Imam Ali
aliwaita wote na akamwambia yule mwanamme: "Hiyo amana ipo kwangu, na mimi sitaweza kuitoa kwa yeyote yule hadi muje wote wawili kwa pamoja,kwa mujibu wa masharti yenu wenyewe!"
Kwa hivyo,aliendelea Imam
: "Nenda ukamlete mwenzako ili niwarudishie amana yenu.
"
Mtu huyo aliaibika na akaondoka zake.(Inaonekana kuwa hao walikula njama ya kutaka kumtapeli mwanamke huyo).
(4). MTUMWA NA TUHUMA
Imeelezwa na kulaini na Sheikh Sadduq vile vile katika sahihi Bukhari, kwa mamlaka ya Imam Jaafar as-Sadiq
kuwa kijakazi aliletwa mbele ya Bwana Umar kwa mashtaka ya kwenda kinyume na bwana wake.
Kisa chenyewe kilikuwa hivi:
Mtu mmoja alimtunza binti mmoja yatima. Kwa kuwa alikuwa akienda safari za kikazi kila mara, hivyo alimkabidhi mke wake ili amlee.
Hali hii iliendelea kwa miaka kadhaa na binti yule alikua na kupendeza. Yule mwanamke, akitafuta mbinu za kumzuia mume wake asimwoe kijakazi huyo, alimlewesha, kwa mbinu zake na kwa msaada wa wanawake wenzake na vile vile alithubutu hata kuuharibu ubikira wake.
Bwana yule aliporudi kutoka safari, alimkuta yule kijakazi hayupo na hivyo alimwuliza mke wake kuhusu huyo.
Mwanamke huyo alijibu: "Huyu ametoroka pamoja na kijana wa majirani.
"
Bwana huyo kwa hasira, alitoka kumtafuta huyo kijakazi, na alipompata, alimburuta hadi mbele ya Umar, allipokuwa Khalifa.
Bwana Umar alipoisikiliza kesi hiyo, aliiona ngumu kuihukumu na hivyo aliielekeza kwa Imam Ali
kwani alikwisha shughulikia kesi kama hizo.
Imam Ali
aliwaagiza Bwana, Bibi, kijakazi na mashahidi wote kuhudhuria mbele yake katika kesi hiyo. Bwana na Bibi walisimulia kisa vile vile walivyofanya mbele ya bwana Umar, na waliwaleta wanawake wanne kwa upande wao wa ushahidi kama vile alivyotaja yule mke wake, dhidi ya mshitakiwa.
Imam Ali
allimwita mwanamke wa kwanza wa upande wa mashtaka na aliuweka upanga baina yake na ya yule, na akasema: "Je wajua, kuwa mimi ni Ali ibn Abi Talib? Na hivyo nakutaka uniambie ukweli na ukweli mtupu na kwamba si chochote kile ila ukweli mtupu.
"
Kwa kuwa mwanamke huyo alikuwa mjanja, hivyo alielezea uongo vile vile kama alivyokuwa ameelezea mbele ya Umar, na alisisitizia pia.
Imam Ali
alipoyaona hayo, alisema kuwa huyo atengwe na mashahidi wengine. Baada ya hapo, Ali
alimwita shahidi mwingine, kumwambia: "Je unauona upanga huu? Iwapo hautaniambia ukweli basi nitakukata kichwa chako kwa upanga huu huu. Vile vile kumbuka kuwa huyo mwanamke aliyekutangulia katika kutoa ushahidi, amenielezea yote kwa ukweli na wazi wazi, kwa sababu hiyo, nimemsamehe. "Kwa kusikia hayo na kwa kuhofia maisha yake, alielezea yote kwa ukweli, bila ubishi au uzushi wowote.
Baada ya kusikiliza hayo yaliyo ya ukweli, Imam Ali
alisema: "Baada ya Mtume Daniel, mimi ni mtu wa kwanza katika kulazimisha mshahidi wa tofauti katika mashahidi wawili.
"
Alitoa hukumu ya adhabu kwa mke wa yule. Na alimwamrisha yule mtu kumpa talaqa mkewe na kumwoa yule kijakazi. Baada ya kutekelezwa kwa hukumu zake, alilipa mahari kutoka mfukoni mwake. Vile vile aliwatoza adhabu ya Dirham mia moja kila mmoja wa mashahidi katika kesi hiyo, na alimpa yule kijakazi Dirham zote hizo.
Baada ya kumalizika kwa maamuzi yaliyo sahihi, Bwana Umar alimshukuru mno Imam Ali
kwa yote hayo na vile vile alimwomba amsimulie masimulizi ya Mtume Daniel
Imam Ali
kwa ombi hilo, alianza:
"Mtume Daniel alikuwa ni yatima, ambaye alifiwa na wazazi wake wote wawili. Wakati huo kulikuwa na mtawala kutoka Bani Israili, ambaye alikuwa na Qadhi wawili katika Baraza lake. Qadhi wote wawili, walikuwa wakimtembelea mtawala huyo wakiwa pamoja na mcha Mungu mno mmoja katika siku zao.
Siku moja mtawala ikamtokea kazi ya dharura na muhimu kabisa nje ya dola yake, hivyo aliwaomba wale Qadhi wamtafutie mtu mwaminifu mno katika raia wake.
Qadhi wale walimshauri amtume yule yule mcha Mungu ambaye huwa wanakwenda wote kila leo.
Mtawala alimkabidhi kazi hiyo yule mcha mcha Mungu pamoja na maelekezo yote.
Yule mcha Mungu alikuwa na mke mrembo mno na mwenye kupendeza pia, vile vile alikuwa mcha Mungu kama bwana wake. Sasa yule bwana alipokuwa akienda safari hiyo aliyotumwa, aliwaomba Qadhi wale wawili wamtunze mke wake kwa uwema na vyema na kumsaidia iwapo angalihitaji msaada wao. Ndipo alipoondoka.
Siku moja Qadhi hao walifikia nyumbani mwa huyo mcha Mungu, na waliweza kumwona mke wake na vile alivyo. Kwa kumwona huyo mwanamke, wote wawili walighadhalibiwa na shaitani na hivyo walimwashiki.
Wao walimwelezea mwanamke huyo tamaa yao na mwanamke yule mwema, alikataa kata kata. Kwa hayo wao walimtishia kwa kumstaki kwa Mfalme kwa kuzini hivyo angaliuawa kwa kupigwa na mawe.
Katika majibu yake, aliwaambia: "semeni chochote kile mukitakacho, lakini mimi kamwe sitakubali uovu huo.
"
Baada ya hapo, wale Qadhi walimwambia mfalme kuwa mke wa yule mcha Mungu amezini. Kwa hayo, Mfalme alishangaa mno kwa taarifa hiyo kwani alijua kuwa mwanamke yule alikuwa mcha Mungu. Alikiinamisha kichwa chake chini, na alipokiinua, aliwaambia:
"Mimi naamini ushahidi wenu lakini nawaombeni munipatie siku tatu kabla sijatoa amri yoyote katika swala hili.
"
Hapo Mfalme alishauriana na Waziri wake, akimwambia "Mimi sidhani kuwa yeye amezini, je wasemaje?"
Kwa kuyasikia hayo, Waziri pia alistajaabishwa na alimwambia Mfalme: "Mimi pia nimestaajabishwa kwa hayo!"
Siku ya tatu, Waziri huyo alipita mahala ambapo walikuwa wakicheza watoto wadogo, na Mtume Daniel
alikuwa mmoja wa watoto hao.
Kwa kumwona Waziri huyo akipita, Mtume Daniel
alimwambia mmoja wa watoto wenzake: "Njooni sisi tucheze mchezo wa kuigiza - Mchezo wa Qadhi wawili na mke wa mcha Mungu. Wewe utakuwa mke wa mcha Mungu na nyie mutakuwa Qadhi.
Wakati huo Mfalme alikuwa ameshapiga mbiu ya mgambo, kwa kuwaita watu wote kuja kushuhudia kutolewa hukumu ya mwanamke wa Mcha Mungu kunyongwa kwa kuzini kwa mujibu na desturi zao kwani Qadhi wawili waliripoti hivyo.
Mtume Daniel alimwita kijana mmoja ambaye alikuwa akiigiza kama Qadhi, na kumwuliza:- "Je wewe unasemaje kuhusu swala hili?" Yeye pia aliuelekeza upanga wa ubao ulioviringwa katika nguo, "iwapo utasema uongo basi nitakukata kichwa chako kwa upanga huu
."
Kijana huyo, kama Qadhi, alimjibu: "Ewe Mfalme! mke wa mcha Mungu huyo amezini, na mimi ninatoa ushahidi wangu kwa hayo
."
Hapo Mtume Daniel
alimwuliza: "Wapi na lini na siku gani na wakati gani?"
Kijana huyo aliyejibu maswali yote aliyokuwa ameulizwa na Mtume Daniel
Baadaye, Mtume Daniel
alimwita kijana wa pili, kama Qadhi wa pili, na alimwuliza maswali hayo hayo, lakini majibu yake yalikuwa ni tofauti kabisa.
Baada ya kuyasikia yote hayo, Mtume Daniel
alisema: "Allah Akbar! Nyie mmetoa ushahidi wa uongo na kumsingizia mwanamke mcha Mungu katika kesi hii.
"
Baada ya hapo alimwachilia yule mwanamke kwa heshima zote na kuwahukumu kifo wale vijana waliocheza kama Qadhi wawili.
Yule Waziri aliutazama kwa makini mno ule mchezo wa watoto wale na uamuzi ulivyotolewa na Mtume Daniel
katika mchezo huo, na aliripoti vyote kwa Mfalme ambaye pia alifuata vile vile ile kesi na akatoa hukumu yake vivyo hivyo."
(5). MTOTO MWENYE RANGI TOFAUTI
Mnigro mmoja alimwijia Bwana Umar. Mke wake alikuwa mweusi. Yeye alimwambia Umar kuwa yeye pamoja na mke wake ni mweusi, lakini amezaa mtoto mwenye rangi ya kunde kinyume na rangi yao. Yeye pia alisema kuwa haina shaka kuwa mke wake amezini na mtu mwingine ambaye ana rangi ya mtoto huyo.
Bwana Umar hakuwa na majibu ya swala hilo hivyo alielekeza kesi hiyo kwa Imam Ali
ili kupatiwa ufumbuzi wake.
Imam Ali
alimwuliza Mnigro huyo: "Je iwapo nitakuuliza swali, utanijibu kwa usahihi?
Mnigro huyo alimjibu: "Ndiyo Bwana! Kwa uwezo wangu wote na kwa usahihi."
Imam Ali
alimwuliza huyo Mnigro: "Je ulimwendea mke wako yaani ulimwingilia yeye akiwa katika vipindi vyake vya mwezini?"
Mnigro alijibu: "Ndiyo Bwana, nafikiri nilifanya hivyo."
Kwa majibu hayo, Imam Ali
alimwambia: "Rangi ya mtoto ni matokeo ya tendo lako hilo. Kwa hivyo, wewe ndiwe mwenye hatia na wala si mke wako." Mnigro aliaibika na akajiondokea.
(6). MTU MLEVI
Kesi hii ya kwanza kutolewa hukumu baada ya kifo cha Mtume(s.a.w.w)
na ni ya aina yake.
Bwana Kulaini ameripoti kwa mamlaka ya Imam Ja'afar as-Sadiq
kuwa: "Katika zama za Abubakar mlevi mmoja aliletwa ili ahukumiwe kisharia.
Hata hivyo, mtu alisema: "Mimi ingawaje ni Mwislamu, lakini naishi miongoni mwa watu ambao hawajui kuwa pombe ni haramu katika Islam na wala mimi sikuwahi kusikia hivyo."
Kwa hayo, Abubakar alishangazwa na hali hiyo na akaona vigumu kutoa hukumu. Wengine waliokuwa pamoja nae walimwambia, mwulizie Imam Ali
kwani ni yeye pekee atakayeweza kujibu swala hili.
Imam Ali
aliwatuma Waislamu wawili waaminifu katika makazi ya Muhajirin na Ansar na kuwaambia "Wawaulize iwapo yeyote miongoni mwao amemsomea (huyu mtu) Aya ya Quran zinazoharamisha pombe au iwapo alishawahi kuwambia Hadith za Mtume(s.a.w.w)
Iwapo yeyote miongoni mwao atatoa ushahidi basi atatolewa huku na iwapo hatapatikana mtu basi ataambiwa aombe msamaha na kutubu, hivyo ataachiwa huru."
Hao watu wawili walirejea kwa majibu ya kutoambiwa kwa mtu huyo chochote kile kihusianacho na kuharamishwa kwa pombe.
Kwa matokeo hayo, Imam Ali
alimkanya vikali mtu kulewa kwake tena na alitubu huyo mtu. Aliachwa huru.
(7). MTOTO AITWA 'DINI IMEKUFA
Imeripotiwa kuwa Siku moja Imam Ali
aliingia msikitini kufa, akamwona kijana mmoja akilia mno huku akiwa amezungukwa na watu waliokuwa wakimhurumia. Imam Ali
aliwauliza hoja ya kilio hicho.
Kijana huyo alisema: "ya Amir Ul-Muminiin, Shurayh, Qadhi wetu amenihukumu kesi dhidi yangu na kuninyima haki yangu."
Imam Ali
alimwuliza: "Je kesi yako inahusiana na jambo gani?"
"Watu hawa" alisema kwa kuwaelekeza watu waliokuwapo, "walimchukua baba yangu katika safari pamoja nao. Wao wamerejea lakini yeye hakurejea. Mimi niliwauliza kuhusu baba yangu, nao walinijibu kuwa amefariki safarini. Nami niliwauliza kuhusu mali aliyokuwanayo, nao waliniambia: 'Sisi hatujui lolote lile kuhusu mali yake hiyo! Hapo ndipo Qadhi Shurayh alipowaambia wale viapo kwa maelezo yao, nao walikula viapo, hapo ndipo aliponiambia kuwa nisiwabughudhi hao watu au kuwaingilia katika mambo yao.
Imam Ali
alimwambia Qambar: "Waite na wakusanye watu na shurtat al-Khamis
.
Aliketi na kuwaita wale watu (waje mbele yake) pamoja na yule kijana. Alimwambia yule kijana aelezee, naye alielezea vile vile kama awali huku akilia, kwa kusema: "Kwa kiapo cha Mwenyezi mungu, mimi ninawashtaki hawa watu kwa kumwua baba yangu. Ewe Amiral-Muminiin. Wao walimdanganya na kumchukua pamoja nao ili wao waweze kunyang'anya mali yake."
Imam Ali aliwageukia hao watu kwa kuwauliza nao walimjibu vile vile kama vile walivyokuwa wamemjibu Qadhi Shurayh: "Huyo bwana alikufa tu na wala hatujui kuhusu mali yake.
"
Baada ya hapo, aliwatazama usoni mwao na kuwaambia: "Je mnafikiriaje? Je mnadhani kuwa mimi sijui lolote lile mulilomfanyia huyo baba wa kijana huyu? Basi itamaanisha kuwa mimi nitakuwa na ilimu kidogo kabisa.
"
Alitoa amri ya kutenganishwa, nao walitenanishwa humo msikitini. Kila mmoja alisimamishwa kwenye kizingiti. Alimwamrisha Ubayd Allah. Abi Rafi, mwandishi wake wakati huo, aketi karibu hapo. Na hapo alimwita mmoja wao, na alimwambia: "Niambie ni siku gani mulipotoka nyumbani kwa ajili ya safari pamoja na babake huyu kijana? Na uyaseme hayo bila ya kuipaza sauti yako
."
"Siku fulani na fulani "yeye alijibu.
"Yaandike hayo," alimwambia Ubayd Allah.
"Ulikuwa mwezi gani" aliuliza Imam Ali
"Ulikuwa mwezi fulani fulani " alijibiwa.
"Yaandike hayo pia," alisema.
"Ulikuwa mwaka gani?" "Ulikuwa mwaka fulani."
"Yaandike,
Ubayd Allah alikuwa akiyaandika yote hayo.
"Kwa magonjwa gani alifariki? aliuliza
"Kwa ugonjwa fulani fulani" alijibiwa.
"Mahala gani alifariki?"
"Mahala fulani fulani"
"Nani aliyemwosha na kumvisha sanda?"
"Fulani fulani,"
"Mulimvisha sanda ya nini?"
"Kwa kitu fulani fulani,"
"Nani aliyesalisha sala ya maiti?"
"Fulani fulani."
"Ni nani, aliyemteremsha kaburini?"
"Fulani fulani.
Ubayd Allah alikuwa akiyaandika yote hayo yaliyokuwa yakiulizwa na kujibiwa. Walipofikia swali la kaburi, Imam Ali
alitoa Takbiri kwa nguvu kiasi kwamba kila mtu aliyekuwapo hapo Msikitini alisikia. Hapo akaamrisha yule mtu arejeshwe mahala pake.
Baada ya huyo, alimwita mtu wa pili akae karibu naye. Imam Ali
alimwuliza maswali hayo hayo aliyomwuliza mtu wa kwanza, majibu yake yote kwa pamoja yalikuwa kinyume kabisa na ya yule wa kwanza. Hayo yote pia yalikuwa yakiandikwa na ubayad Allah. Alipomaliza mtu huyo kutoa majibu yake, Imam Ali
alitoa Takbir kwa sauti kiasi kwamba wote walisikia. Aliamrisha wote wawili wafungwe kifungo lakini wasubiri kwenye mlango wa Msikiti.
Imam Ali
alimwita mtu wa tatu na kumwuliza vile vile alivyowauliza waliotangulia. Naye pia alijibu kinyume na wenzake wawili. Imam Ali
aliamrisha achukuliwe kwa wenzake wawili.
Hapo alimwita mtu wa nne. Maneno yake yalitatanisha na kubabaisha. Imam Ali
alimwonya na kumtishia. Mtu huyo alikiri kwa wenzake walimwua yule bwana na kuchukua mali na kwamba alizikwa mahala fulani fulani karibu na mji wa Kufa. Imam Ali
alitoa Takbir, na kuamrisha achukuliwe mahabusu.
Kwa mara nyingine tena, Imam Ali
alimwita mmoja wa wale waliokwisha kuulizwa, na kumwambia: "Wewe ulidai kuwa mtu huyo alikufa akiwa kitandani. Ambapo nyie mumemwua. Niambie ukweli kabisa kuhusu hali halisi, ama sivyo nitakuadhibu vikali kiasi kwamba utakuwa ni fundisho kwa wengine kwamba niwe nikiambiwa ukweli mtupu
." Mtu yule alikiri kumwua yule bwana kama vile alivyokuwa ameelezea mwenzake.
Hapo aliwaita wote waje mbele yake, nao wote walikiri kumwua yule bwana. Imam Ali
aliwaamrisha baadhi ya watu wake waondoke na hao hadi pale walipokuwa wameizika mali ya bwana, hivyo kumpa mtoto wake marehemu.
Imam Ali
alimwuliza yule kijana: "Je umetaka kufanyiwa nini hawa watu kwani umekwishajua kile walichomtendea baba yako.
"
"Mimi nataka Mungu atuamue siku ya Qiyama na hivyo ninawaachilia humu duniani." alijibu kijana.
Kwa hivyo, Imam Ali
hakuwaadhibu kwa mujibu wa adhabu za kuuwa bali aliwaadhibu vikali kwa madhambi yao.
Qadhi Shuryh alistaajabishwa kwa uamuzi huo wa Imam Ali
na hakuweza kujizuia kwa kumwuliza Imam Ali
"Ewe Amir ul-Muuminiin! Je umewezaje kufikia uamuzi huu?"
Imam Ali
alimjibu: "Mtume Daudi
aliwapita baadhi ya watoto waliokuwa wakicheza na aliitwa mmoja wao, 'Dini imekufa'. Hapo alikuwa akiwajibu. Mtume Daudi
aliwaendea, na kumwuliza mmoja, "Ewe, kijana, je unaitwa nani?" 'Jina langu ni Dini imekufa,' alijibu.
'Je ni nani aliyekupatia jina hilo?" aliuliza Mtume Daud
Alijibu, "Mama yangu, aliye nyumbani. 'Ndipo Mtume Daud
alipomwambia, twende utupeleke nyumbani kwenu. "Hivyo walikwenda hadi nyumbani kwao na kumwita nje mama yake, 'Ewe mama je, mtoto wako anaitwa nani?' Jina lake ni Dini imekufa.' alijibu huyo mama. Mtume Daudi
aliendelea kumwulizia,'Je ni nani aliyempatia, jina hilo? Huyo mama alijibu, "Baba yake mzazi
."
Imam Ali
alimwuliza, "Je ni kwa sababu zipi alimpatia jina hilo?" Huyo mwanamke alijibu: nilipokuwa mja mzito, baba yake alikwenda safari pamoja na baadhi ya watu. Wale watu wote walirejea salama lakini yeye hakurejea. Mimi nilijaribu sana kuwauliza kuhusu bwana wangu lakini wao walijibu kuwa alifariki safarini. Vile vile niliwaulizia kuhusu mali aliyokuwa nayo, lakini wao walisema kuwa hakuwa na chochote na hivyo wao hawakujua chochote kile! Vile vile niliwauliza iwapo alisema chochote katika usia wake. Nao walisema kuwa aliwaambia mtoto atakayezaliwa aitwe Dini imekufa, na hivyo ndivyo nilivyomwita hivyo kwani sikutaka kwenda kinyume na usia wake.'
Hapo Mtume Daudi alipomwuliza yule mwanamke, "Je unawajua watu hao?" Mwanamke alijibu 'Naam!' Wale wote waliochukuliwa nesi hiyo ilipokuja mbele ya Imam Ali
alitoa hukumu ya mtu wa kwanza mwenye amana ya Dinar mbili alipwe Dinar moja na wagawane sawasawa na mtu wa pili ile Dinar ya pili.
(8). KUZALIWA KWA MTOTO WA MIEZI SITA
Mwanajeshi mmoja aliporejea nyumbani kwake alikuta mke wake amezaa mtoto wa kiume ambapo yeye anadai kuwa aliishi nao kwa miezi sita tu. Mwanajeshi huyo alimkatalia huyo mtoto,na kupeleka kesi yake mbele ya Umar,ambaye alitoa hukumu ya kupigwa mawe huyo mwanamke (mama mtoto).
Kwa bahati Imam Ali
pia alikuwapo hapo, alisema: "Iwapo utapingana na kitabu cha Allah s.w.t basi tutaikhatalafiana. Allah s.w.t. amesema katika Quran tukufu: "Nabeba mimba yake hata kumwachisha ziwa (uchache wake) ni miezi thelathini
. (46:5).
Vile vile Allah s.w.t amesema katika Quran Tukufu: "Wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili
.......'(2:233). Wakati mwanamke alipotimiza kunyonyesha kwa miezi thelathini.... Kwa sasa (yeye ametimiza tu) wajibu (wa kumnyonyesha) kwa miezi sita (na hivyo hawezikuuawa)."
Umar alimwachilia huru yule mwanamke na alikubaliana na uamuzi huo. Ma-Sahaba walifuata hilo na vile vile al-tabi'un pia wameitumia hadi leo.
(9). MAMA MZAZI AADHIBIWA
Kisa kama kile cha Na. 10 kilitokea katika zama za Bwana Uthman ambapo aliamrisha yule mwanamke auawe kwa kupigwa mawe.
Imam Ali
alipoingilia kati, Uthmani alimpeleka mtu kwenda kuzuia utekelezaji wa adhabu aliyoitoa, mwanamke akawa ameshauwa.
(10). KESI YA MKATE
Al-Hassan b. Mahbub ameripoti: Abd al-Rahman b. al-Hajjaaj aliniambia: Nimemsikia Ibn Abi Layla akisema: Amir ul-Muminiin
ameamua kesi ambayo haikuweza kuamuliwa na mtu mwingine kabla yake.
Watu wawili waliondoka kwenda safari, wakakaa kula chakula kwa pamoja. Mmoja wao alitoa vipande vitano vya mkate na mwenzake vitatu. Alitokezea mtu mmoja akapita aliwasalimia. Nao walimkaribisha ale nao. Naye alipomaliza kula nao, aliwapa Dirham nane akisema: "Hii ni malipo ya chakula nilichokula
."
Hao watu wawili walianza kuzozana juu ya Dirham hizo nane. Yule aliyekuwa na vipande vitatu alidai kuwa "Tugawane sote sawa sawa yaani Dirham nne wewe na Dirham nne mimi.
"
Mwenzake alisema: "Mimi lazima nipate tano na wewe tatu."
Kwa kuwa hawakuweza kuafikiana hivyo, walifikia kwa Imam Ali
kuweza kupatiwa ufumbuzi. Hivyo, walimwelezea mambo yote. Imam
aliwajibu."
Hili ni jambo dogo, halihitaji mzozo wala ngumi kwani suluhisho ndilo jambo bora.
"Mimi nitaridhishwa tu pale utakapotoa uamuzi wako Ewe Amir ul-Muminiin! alisema mwenye vipande vitatu vya mkate.
"Kwa kuwa wewe utaridhishwa na hukumu yangu" alisema Imam Ali
"wewe utapata Dirham moja tu ambapo rafiki yako atapata Dirham saba. " alimalizia Imam
"Mungu asifiwe, " alinena, "Je itawezekanaje swala hili kuwa hivi?"
"Nilikuambia siyo?" alisema "Si ulikuwa na vipande vitatu tu vya mkate?"
"Naam! Alijibu "Yaani ni ishirini na nne (inapozidishwa) kwa tatu, alisema Imam
"Kwa hiyo wewe ulikula nane, mwenzako nane,na mgeni wenu nane (kwani alitoa saba ya nane ya chakula cha mgeni wenu) na moja kwako wewe (kwani wewe ulitoa moja ya nane ya chakula cha mgeni)." Wote wawili waliondoka kwa furaha.