1
MAISHA YA IMAM HASANI
AL ASKARI (A.S)
UMAARUFU WAKE WA KIELIMU
Ingawa aliishi miaka ishirini na nane tu, aliiua kiu ya kisomo ya wanachuoni wengi wa wakati ule na pia aliweza kupambana vya kutosha na mafalsafa wa wakati huo ambao walikuwa wakieneza mambo yaliyokuwa kinyume cha mafundisho ya dini.
Mtu mmoja aliyeitwa Ishaq Kindi alikuwa akiandika kitabu juu ya migongano ya aya za Qur'ani. Habari hizi zilipomfikia Imamu
alianza kutafuta nafasi. Siku moja wanafunzi kadhaa wa Ishaq aliwauliza, "Hakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye akili za kutosha kumshauri mwalimu aache upuuzi aufanyao juu ya Qur'ani? Walisema, "Tutafanya nini na sisi ni wafunzi wake tu"? "Imamu alisema, "Vizuri, je, mnaweza angalau kumwambia yale ninayowaambieni? Wakasema, "ndiyo tunaweza kufanya".
Ndipo Imamu alipowaonyesha baadhi ya zile aya za Qur'ani zinazozungumziwa na akawaambia waende wamuulize mwalimu wao kama maneno ambayo alikuwa anayatumia katika hoja zake yana maana hizo tu alizoyachukulia tu au kama kwa kutazama matumizi ya maneno ya Waarabu, maana nyingine za maneno hayo zilipatikana, ambazo kama yakifikiriwa maneno hayo kwa maana hizo yanaondoa suala lolote lile Ia kupingana kwa aya hizi. Kama zipo maana nyingine, basi alikuwa na haki gani ya kung'ang'ania kuyachukua maneno hayo kwa maana hizo alizozichukulia yeye? Kisha Imamu
aliwaeleza wale wanafunzi maana halisi yaa aya hizo. Nao wakaenda na wakafanya kama walivyoagizwa. Ishaq alipozisikia zile hoja walizozitoa aliwauliza wamweleze walipojifunza yote hayo. Kwanza, walitaka kuficha lakini aliposisitiza kuwa hayo siyo mawazo yao, walikubali kuwa walijifunza kutoka kwa Abu Muhammad, yaani Imamu
. Ishaq alisema "Hakuna mwingine ambaye angelifanya hivyo, isipokuwa mtu wa ukoo wa Mtume". Kisha akachoma yale yote aliyokwisha kuandika.
Huu ni mfano mmoja tu wa yale aliyokuwa akiyafanya Imamu kila siku, akielewa kuwa hiyo ni kazi yake akiwa mrithi wa kweli wa Mtukufu Mtume. Na serikali ikidai kuwa ni ya Kiislamu, ilikuwa inafanya mambo ya zinaa na ulevi, na wakati watawala rahisi waliposhika madaraka ilikuwa ni kuongeza vizuizi tu kwa lmamu. Lakini alikuwa mfano halisi wa subira na uvumilivu na hivyo aliendelea katika njia yake ya kazi hii tukufu.
Katika kukusanya Hadithi za Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
"wakusanya hadithi" wamechukua hadithi toka kwake. Moja ya hadithi muhimu sana ni ile isemayo, "Mlevi ni sawa na mwenye kuabudu sanamu". Hadithi hii imekaririwa na Bwana Ibn Al-Jauzi katika kitabu chake kiitwacho 'Tabrim-ul-Khamr' (Uharamu wa Kulewa Mvinyo). Na Bwana Abu Na'im Fazl bin Wakin alisema kuwa hadithi hii ni ya kuaminika sana na imechukuliwa kutoka kwenye ukoo wa Mtukufu Mtume na pia imepokewa na kundi Ia masahaba wa Mtukufu Mtume.
Bwana Sam'ani katika kitabu chake kiitwacho 'Kitab-Al-Ansab' ameandika, "Abu Muhammad Ahmad bin Ibrahim bin Hashim Tusi Baladhuri Hafiz Wa'iz alisikia hadithi ya Mtukufu Mtume huko Maka kutoka kwa Imamu atokanaye na dhuria wa Mtume, Hasan bin Ali bin Muhammad bin Ali bin Musa Al-Ridha na akazikusanya".
Zaidi ya bwana huyu, majina ya wanafunzi wengine mashuhuri wa Imamu yanaorodheshwa hapa chini:
1. Bwana Abu Hashim Dawud bin Qasim Ja'fari aliyekuwa Mwanachuoni mzee ambaye aliwaona Maimamu wanne kutoka lmamu Ali Ridha
hadi Imamu Hasan Askari
na alisoma kwao wote. Vile vile alikuwa mjumbe wa Imamu Hasan Askari
.
2. Bwana Dawud bin Abi-Zaid Nishapuri aliwaona Imamu Hasan Askari
na baba yake lmamu Ali Naqi
.
3. Bwana Abu Tahir Muhammad bin Ali bin Hilal.
4. Bwana Abul Abbas Abdullah bin Ja'far Himyari Qummi alikuwa mwanachuoni mashuhuri sana na mwandishi wa vitabu vingi ambavyo miongoni mwao Qurb-al-Asnad bado kipo mpaka leo na ndiyo chanzo cha kitabu kiitwacho Kafi na vitabu vingine.
5. Bwana Muhammad bin Ahmad bin Ja'far Qummi alikuwa mmoja wa wajumbe mashuhuri wa Imamu.
6. Bwana Ja'far bin Suhail Saiqal pia alikuwa mjumbe mashuhuri wa Imamu.
7. Bwana Muhammad bin Hasan Jaffar Qummi alikuwa mwanachuoni mashuhuri na mwandishi wa vitabu kadhaa kati ya hivyo, Basa'irul Darajat kinajulikana. Pia alihifadhi barua walizokuwa wakiandikiana na Imamu Hasan Askari kuhusu sheria za kidini.
8. Bwana Abu Ja'far Humani Barmaki aliandika kitabu cha majibu ya Imamu kuhusu maswali ya sheria za kidini ambayo mwandishi aliandika kumwuliza Imamu
.
9. Bwana lbrahimu bin Abi Hafs Abu Ashaq Katib, Bwana huyu alikuwa miongoni mwa wafuasi wa Imamu na aliandika kitabu.
10. Bwana Ibrahim bin Mehryar, alikuwa mwandishi wa kitabu kiitwacho 'Kitabul Basharat'.
11. Bwana Ahmad bin Ibrahim bin Isma'il bin Dawud Hamdan Al-Katib Al-Nadim, alikuwa na elimu kubwa ya uandishi wa vitabu na lugha. Aliandika vitabu vingi na alijiambatanisha sana na Imamu.
12. Bwana Ahmad bin Ashaq Al-Ashari Abu Ali Al-Qummi, alikuwa mwanachuoni mwenye elimu ya kutosha. Aliandika vitabu vichache miongoni mwao kikiwemo kitabu kiitwacho "Ilal-Al-Saum", (Falsafa ya Funga).
Haya ni majina machache tu. Patahitajika kitabu kizima kuweza kuyataja majina yote.
Bwana Abu Ali Hasan Khalidi bin Muhammad bin Ali Barqi aliandika Tafsir (kitabu juu ya ufafanuzi wa Qur'ani Tukufu) kwa njia ya imla aliyosomewa na Imamu. Wanachuoni wa kidini wanasema kuwa kitabu hiki kiligawanywa katika juzuu 120.
Kwa bahati mbaya maandishi haya muhimu sana hayapatikani siku hizi. Hata hivyo katika Tafsiri kadhaa kuna kumbukumbu za Imamu ambazo zinaweza zikawa zinatokana na kitabu hiki. Kitabu kingine juu ya somo hilo kilichopo na kinachosemekana kuwa kimetokana na Imamu hakiaminiki. Waraka mrefu wa Imamu, aliomwandikia Bwana Ishaq bin Isma'il Ash'ari na mkusanyo mkubwa wa hadithi za kuaminika, mafundisho na hotuba vimehifadhiwa katika kitabu Kiitwacho 'Tuhaful-Uqul'.
Yote hii ni kazi ya maisha ya muda wa miaka 28, muda ambao miaka sita tu ndiyo aliyokuwa Imamu baada ya kifo cha baba yake Imamu Ali Naqi
na hiyo pia aliitumia katika hali ya majaribio magumu kama ilivyokwisha elezwa awali.
KUFARIKI KWAKE
Baada ya maisha yenye shughuli namna hiyo kuna uwezekano wa kupatikana wakati wo wote ule kwa ajili ya fitina za kisiasa au lo lote lile lifananalo na hilo? Lakini kuongezeka kwa mvuto wake kwa watu katika mambo ya Kiroho na kuwa kwake chanzo cha Elimu ya Kidini vilikua ndiyo sababu kubwa ya watawala kutaka kuyaondoa maisha yake. Kwa maana dola ya Bani Abbas ingeliweza kusimama iwapo tu, Uislamu wa kweli usingelifahamika; au kwa ujumla hakukuwepo nafasi kwa wafalme wa ukoo huo, na matendo yao yote hayawezi kupata kibali cho chote kile cha raia isipokuwa tu, kama raia hao wakiwekwa gizani kuhusu kuwepo kwa Falsafia yo yote ile ya maisha yaliyo mazuri kuliko yale yanayofuatwa na serikali. Maimamu wa ukoo wa Mtukufu Mtume(s.a.w.w)
walikuwa ni mifano halisi ya mafundisho ya Mtume(s.a.w.w)
ambayo yalipinga kabisa desturi za Waarabu, zilizothibitika au yo yote kati ya madhehebu zilizoamini aina yo yote ile ubora wa taifa au yo yote kati ya zana nyingi za kimataifa ambazo hubadilika kila siku kulingana na matakwa ya watawala.
Hivyo, kutaka kuyaondoa maisha ya Imamu lilikuwa jambo muhimu sana kwa kuendeleza maisha ya serikali kama ilivyokuwa kabla hivyo mwishowe walifikiria hivyo.
Imamu alifariki (kwa kupewa sumu na Mu'tamad) mnamo tarehe 8 Rabi-ul-Awwal (Mfunguo Sita) mwaka 260 Hijiriya. Alizikwa huko Samarrah (Iraq) karibu na kaburi la baba yake, ambako, licha ya hali mbaya msikiti wa kaburi hilo bado umesimame, ambao ni moja ya sehemu kadhaa zilizo takatifu kwa watu wote.
NYONGEZA
Mifano ya Maandishi na Hadithi za Imamu
1. Jiepushe na kuwa pamoja na mjinga hata kama yu akutakiaye kila Ia kheri na usijiepushe na mtu mwenye hekima hata kama ni adui yako. Kwani mjinga atakuumiza uhitajipo msaada ambapo utu wa mtu mwenye hekima utamzuia kufanya jambo lililo chanzo cha uadui.
2. Waraka wake kwa watu wa Qum, Iran: Mwenyezi Mungu aliudhihirisha wema wake kwa viumbe wake kwa kumleta Mtume wake Muhammad(s.a.w.w)
na ahadi zake na maonyo yake na kakubarikini kwa Rehema zake kwa kukuwezesheni mkubali dini yake ya kweli na kukutukuzeni kwa kukuangazeni na akapanda mbegu ya imani katika mioyo ya wahenga wenu na kuwabariki wale watu miongoni mwenu ambao wanaishi maisha marefu na kawabariki kwa kuwepo kwa Dhuria wa Mtume wake
kuwa ndiyo viongozi wao.
Hivyo, wale waifuatao njia ya Haki watafaulu na kufaidi yale matunda waliyochuma kabla.Tunastarehe kwa sababu ya maarifa yenu mazuri na uhusiano wetu ni wa kuaminika. Shikaneni na amri zile ambazo wahenga wetu waliwapa vijana wenu na muwe na uhakika na zile ambazo vijana wetu waliwaahidi baba zenu. Mwenyezi Mungu awabarikini nyote.
3. Barua yake kwa Bwana Ibn Babawaihi Qummi: Ewe Hasan bin Ali bin Husain bin Babawaihi Al-Qummi, kuwa mvumilivu ili kungojea nyakati nzuri. Marafiki zetu wataendelea kuwepo kila wakati katika hali hii ya hatari mpaka aje mwanangu ambaye Mtukufu Mtume wa Mungu(s.a.w.w)
alimbashiri kuwa ataijaza dunia kwa haki na usawa kama vile ambavyo ingelijaa mateso na dhuluma.
Hivyo, Ewe Sheikh, muwe wavumilivu wewe mwenyewe na wale marafiki zetu wote. Mwenyezi Mungu humpa hii dunia yake ye yote yule amuonaye kuwa anafaa katika viumbe wake. Na hakika mwishilizo mwema utakuwa na wale wamchao Mwenyezi Mungu. Amani ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake na ziwe juu yako na juu ya marafiki zetu. Neema Zake na ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad(s.a.w.w)
na Dhuria wake
.
SHARTI YA KUCHAPA
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini
ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
MWISHO WA KITABU