1
MAISHA YA IMAM HADI
UKWELI KATIKA MINYORORO (IMAMU ALI NAQI
TABIA ZAKE NJEMA
Imamu Ali An-Naqi
alikuwa na tabia njema kama zile za kila mmoja, wa watu wa ukoo wa Mtukufu Mtume[s.a.w.w]
. Akiwa nje au ndani ya jela, tabia ya maisha ya Imamu Ali Naqi
iliyojulikana sana ilikuwa ni sala, ibada na huruma kwa viumbe vya Mungu.
Popote pale alipoishi alipokuwa jela alitayarisha kaburi na mahaIi alipokuwa akisalia. Alipoulizwa maana yake, alijibu kuwa alitaka kila mara kuliweka wazo la kifo mbele akilini mwake. Hakika hilo liIikuwa jibu la kufaa kwa matakwa ya watawala dhaIimu kwa lmamu
kuwa aache kuitangazia Imani ya kweli na kuitii serikali ya kiupotovu isiyokuwa na msimamo. Alikuwa akisema kuwa mtu aliye tayari kufa wakati wowote hawezi kutishwa mpaka akatiishwa.
Ingawa milki ya ukoo wa Bani Abbas ilikuwa imezorota sana, lmamu
hakufikiria kuiangusha na serikali haikuweza kupata kisingizio cha kuyahalalishia mateso waliyompa.
Chuki aliyoionyesha Muntasir na mtumwa wake wa Kirumi aitwaye Baghir aliyempenda kwa baba yake Mutawakkil, kugawanyika kwa utawala na maangamizi ya watu wenye vyeo vya juu srikalini na mwishowe uamuzi wa wanawe Mutawakkil wa kumwondoIea baba yao kiti cha enzi, na wakati wa utawala wa Musta'in kuondoka kwa Yahya bin Ami Alawi, kuanzishwa serikali ya kujitegemea huko Tabaristan na Hasan bin Zaid, maasi ya watumwa wa Kituruki katika mji mkuu wa nchi, kukimbia kwa Musta'in kutoka katika mji huo mkuu na kwenda Baghdad, na mwishowe kulazimishwa kujiuzulu na baadaye kuuawa na Mu'ttaza; na vitendo vya uchochezi vya watumwa wa Kirumi katika zama za Mu'ttazz, Mu'ttazz kutokuwaamini ndugu zake na mwisho wa maisha ya Bani Mu'awiyyah na kufungwa kwa Muwaffaq huko mjini Basrah, matukio yote haya yalimtoa Imamu
katika hali ya kudhaniwa kuwa anahusika na kitendo chochote cha kisiasa. Je, hii haionyeshi uwezo wa hali ya juu na usio na kifani wa Imamu
katika kujali zaidi ujumbe wake licha ya majaribu hayo yote ambayo kwa kweli yangeweza kabisa kumwambukiza mtu wa kawaida?
Ustahimilifu uIioonyeshwa na Imamu kwa serikali ambayo alijua kuwa ni ya kidhalimu na haribifu kwa sheria ya Islamu na kwamba imemuwekea taabu nyingi mno, inaonyesha kuwa ni tabia bora mno ya kiakili (inayotokana na Mwenyezi Mungu) ambayo ingeweza kuufanya Mwenge wa Mwanga Mtukufu kuendelea kuwaka.
NYONGEZA YA KWANZA
Mwanahistoria Bwana Mas'ud ananakili tukio ambalo habari zake amezichukua kutoka katika kitabu kiitwacho 'Al-Mubarrad' na ambalo mwanahistoria mwingine Bwana Ibn Khallikan ameliweka katika maelezo (katika Juzuu ya Pili, uk. 214 wa tafsiri ya Kifaransa ya "Tarikh" ya Bwana Ibn Khallikan iliyofanywa na Bwana de Slane) ya Imamu Ali Naqi (Abul Hasan Askari
lisemalo kuwa, "Habari ya siri ilipelekewa Al-Mutawakkil kuwa lmamu alikuwa na zana na vita, vitabu na vitu vingine ambavyo ilikuwa vitumiwe na wafuasi wake waliyojificha nyumbani mwake, na kushawishiwa kwa taarifa mbaya ili waamini kuwa alikuwa akijitahidi kuipata dola ile. Usiku mmoja Muttawakil alipeleka askari wa Kituruki kuingia nyumbani humo wakati asiotegemea hivyo. Walimkuta akiwa peke yake na akajifungia chumbani mwake akiwa amevaa shati la manyoya na kichwani kwake akiwa amejitanda shuka ya sufu na akielekeza uso wake mjini Makka, akisoma aya za Qur'ani zenye kuonyesha ahadi na vitisho vya Mwenyezi Mungu akiwa hana hata zulia lolote ila kokoto na mchanga tu.
Alichukuliwa hivyo hivyo na kutolewa nje gizani mpaka kwa Al-Mutawakkil ambaye wakati huo alikuwa anakunywa mvinyo. Alipomwona Imamu
alimpokea kwa heshima na alipoambiwa kuwa hakuna kilichoonekana nyumbani mwa Imamu
kiwezacho kuthibitisha yale mambo yaliyodhaniwa, alimwambia aketi karibu naye na akampa kikombe cha mvinyo alichokuwa nacho mikononi mwake. Abul Hasan (Imamu
akasema, "Ewe Amirul-Muuminin", kufuatana na imani ya wanahistoria waandishi wala sio kwa mujibu wa aaminivyo Imamu
; pombe kama hii haijachanganywa na mwili na damu yangu, hivyo nisamehe nisiinywe." Mfalme alimkubalia ombi lake lakini alimwomba Imamu
amsomee beti fulani fulani za Mashairi ambazo zingelimfurahisha. Imamu Abul Hasan
alimjibu kuwa alikuwa amekariri mashairi machache sana lakini Al-Mutawakkil aliposisitiza kuwa aimbe, aliimba mashairi haya yafuatayo:
"Usiku kucha walikesha katika vilele vya milima,
Wakilindwa na askari shujaa, Lakini hata hivyo maficho yao hayakufaa kitu. Baada ya fahari na madaraka yote waliyonayo,Iliwalazimu wateremke kutoka kwenye ngome zao, ndefu na kuingia mwenye kifungo cha kaburi,O! Mabadiliko hayo ni yenye kuogofya kiasi gani?
Makaburi yao yalikwisha wapokea wakati sauti iliposikika ikisema: Ziko wapi falme zenu na mataji na kanzu zenu za heshima? Sasa ziko wapi nyuso za hao wazuri, zilizofunikwa na maovu na kulindwa na mapazia ya kumbi za wasikilizaji? Kwa ombi hili kaburi lilitoa jibu kamili.
Likasema, sasa mafunza wanazifurahia nyuso hizi (kwa kuzila).
Watu hawa walikuwa wakila na kunywa kwa muda mrefu lakini sasa badala yake wanaliwa.
Kila mtu aliyekuwepo pale alihofia usalama wa Abul Hasan [a]. Waliogopa kuwa Mutawakkil katika hasira yake ya kwanza tu angeweza kuimalizia hasira yake kwake. Lakini badala yake walimwona Mfalme huyo akilia kwa uchungu mwingi sana, machozi yakatiririka kutoka ndevuni mwake hivyo wote waliokuwa pale walianza kulia nao. AI-Mutawakkil aliamuru mvinyo huo utolewe na badala ya hayo alisema: "Niambie Abul Hasan una deni lolote udaiwalo. "Ndiyo", alijibu Imamu
"Nilikopa dinari mia nne. Mfalme aliagiza Imamu
apewe fedha hiyo na apalekwe kwake kwa heshima zote."
NYONGEZA YA PILl
Siku moja Mutawakkil alimwomba Bwana Ibn Sukait (Soma maandishi ya kitabu hicho jina hili limeandikwa kitabuni humo lbn-Al-Sakit) kumwuliza Imamu
maswali magumu sana ambayo yangemshinda kuyajibu. Hivyo alimwuliza maswali yafuatayo:
Ibn Sukait: Mungu alimpa Musa Muujiza wa fimbo na Isa alipewa Muujiza wa kuwaponya wakoma na kuwafufua wafu na Muhammad Mtume wetu alipewa Qur'ani na upanga: Kwa nini hakuwapa mitume hawa wote muujiza wa aina moja?
Imamu
: Kila muujiza unafaa kwa wakati wake ulipotolewa. Wakati wa Musa wachawi walikuwa mashuhuri sana, hivyo alipewa muujiza huo wa Fimbo na Taa ya mkono. Wakati wa Isa, sayansi ya utabibu ilikuwa imefikia kilele chake, hivyo alipewa muujiza wa kuponya magonjwa na kufufua wafu Na wakati wa Mtakatifu Mtume, ufasaha wa kusema, elimu ya usemaji na ushujaa vilikuwa na sifa zaidi, hivyo alipewa Kitabu (Qur'ani) na Upanga, ili kupambana navyo.
lbn Sukait: Sasa siku hizi wakati ambapo hakuna mwenye muujiza, nini "Hujjah" (Kipomo cha tabia ya watu)?
Imamu
"Ni akili yao ya kuweza kujua mema na mabaya.
Ibn Sukait: Lakini akili ilikuwepo katika miili tangu awali?
Imamu: Lakini milango ya kupambanua ilikuwa bado haijafunguliwa. Milango hiyo imefunguliwa na Mitume.
Ibn Sukait:Ni nani huyu anayetajwa katika Qur'ani, kwani "... yule aliyekuwa na elimu ya Kitabu...
" (Qur'ani, 27:40).
Imamu
: Asif bin Barkhiya.
Ibn Sukait: Lakini wakati Mtume Suleiman alipowauliza wafuasi wake ni nani kati yao awezaye kumleta Malkia Bilqis (wa Sheba) pamoja na kiti chake cha enzi, haujua kwamba Asif anaweza kufanya hivyo?
Imamu
: AIijua, lakini alitaka kuhakikisha ubora wa Asif kwao na kuwaambia kuwa atakuwa Mrithi (Khalifa) wake.
Ibn Sukait: Kwa nini Yaaqub alimsujudia Yusufu? Je, ni haki baba kumsujudia mwanawe? Je, mwanadamu anaweza kufanya hivyo kwa mwanadamu mwenzie?
Imamu
: Kusujudu kule kulikuwa ni utii kwa Mwenyezi Mungu na kumtakia heri Yusuf. Kusujudu huku kulikuwa sawa na kule malaika walikokufanya kwa Adamu. Kusujudu kwa Yaaqub na wanawe kulikuwa ni shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwamba aliwakutanisha tena wakawa pamoja tena baada ya kutengana kwa muda mrefu.
Ibn Sukait: Ni mti gani ule Adamu alioamriwa asiukaribie wala kula matunda yake?
Imamu
: Ulikuwa ni mti wa Wivu. Mwenyezi Mungu alitaka kawaokoa wana wa Adamu kutokana na wivu.
SHARTI YA KUCHAPA
Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein
Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini
ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.
MWISHO WA KITABU
YALIYOMO
MAISHA YA IMAM HADI (A.S) 1
UKWELI KATIKA MINYORORO (IMAMU ALI NAQI AL HADI (A.S) 1
KIMEANDIKWA NA: MAULANA SAYYID ALI NAQI SAHEB 1
KIMETAFSIRIWA NA: MAALIM DHIKIRI OMARI KIONDO 1
IMAMU KATIKA QUR'AN NA HADITHI 1
UTANGULUZI 1
JINA NA NASABA YAKE 1
KUZALIWA NA KULELEWA KWAKE 1
MABADILIKO YA KISIASA 2
SHIDA NA MATESO 2
KUFARIKI KWAKE 5
MAISHA YA IMAM HADI(a.s) 6
UKWELI KATIKA MINYORORO (IMAMU ALI NAQI[a.s] 6
TABIA ZAKE NJEMA 6
NYONGEZA YA KWANZA 6
NYONGEZA YA PILl 7
SHARTI YA KUCHAPA 8
MWISHO WA KITABU 8
YALIYOMO 9