NENO LA WACHAPAJI
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.
Allah (s.w.t) ameumba uhai na umauti kwa makusudio maalum Amelielezea hilo kwa njia ya vitabu vinavyobainisha wazi wazi kati ya matendo mema na maovu. Maelezo fasaha na yenye mtiririko mzuri yanatuthibitishia kuwa kila mmoja wetu na wa kila rika na jamii tofauti anaweza kukielewa kitabu hiki kwa urahisi. Imani ya Dini imemuweka mwanadamu katika upeo wa juu ambao haulinganishwi na zama za Kijahiliyya. Kwa kuujua uwezo wa Allah (s.w.t) huwapelekea watu kuwa na matumaini na furaha katika maisha ya hapa Ulimwenguni na Akhera. Katika mada hii Quran tukufu inasema: "Ambao ni wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia" Al-Raad:28. Hapana yeyote mwenye kuujua udhaifu wa mwanadamu na mapenzi ya Allah (s.w.t); atashindwa kubadilika kwa mafunzo yaliyomo katika Sahifa. Ndani yake tunapata mafunzo ya kiroho ya Kiislam au mafundisho ya kina na mapana ya Dini ya Kiislamu yanayohusu matendo na ukweli katika maisha na mahusiano kati ya mwanadamu na Allah (s.w.t) ambayo yameandikwa katika lugha za Kimataifa kwa kuweka misingi imara ya kiroho kwa ukamilifu. Kwa Niaba yetu sote tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Mtukufu Allah (s.w.t) na kwa mwandishi wa kitabu hiki kitukufu kilichotuwezesha kuandika tafsiri ya pili na tunaungana na kufurahia kazi ngumu ya tafsiri yake ya Kiswahili pamoja na Mzee wetu Ayatullah Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi wa Bilal Mission of Tanzania. Tunamuomba Allah (s.w.t) ambariki na amlipe kwa kazi yake kubwa aliyoifanya katika nyanja hii; pamoja na wale waliotoa mchango wao wa hali na mali Mission na Mwandishi pia wanatoa shukurani zao za dhati kwa wale wote waliotoa mchango wao katika kazi hii. Tunaweka kalamu yetu chini kwa kumalizia na methali ya Kiswahili isemayo, "Fuata nyuki ule asali."
DIBAJI KUHUSIANA NA USHUHUDA - THABITI WA SAHIFA
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema - Mwenye Kurehemu
Mtukufu Sayyed Najmu Deen Bahausharafu Abul-Hasan Muhammad bin Ahmad bin Ali bin Muhammad bin Umar bin Yahya Al-Alawi Al-Husayn - Mungu amrehemu - alituhadithia Alisema: Alitupa khabari Shaikh heri zimfikiye Abu Abdilahi Muhammad bin Ahmad bin Shahriyar muweka hazina wa hazina ya Amiyrul Muuminen Maulana Aliy bin Abiy Taalib alayhis-salaam katika mwezi wa Rabi-u-Awal (mwezi wa tatu A.H.) mwaka wa 516 mwezi May - June wakati Sahifa ilikuwa inasomwa mbele yake nami nasikia.
Alisema nimeisikia kutoka kwa Shaikh ikisomwa mbele yake Shaikh Swaduqu Abiy Mansoor Muhammad bin Muhammad ibun Ahmad bin Abdil-Aziz Al-Ukbari mwadilifu Mungu amreheu kutoka kwa Abil-Mufazzali Muhammad bin Abdilahi ibnil-Mutalib Ashaybaanee. Alisema: Sharifu Abu Abdilahi Jaafar bin Muhammad ibun Jaafar ibunil Hasani ibin Jaafar ibunil Hasan Ibunil Hasan ibun Ameril-muumineena Aliy ibn Abiy Taalib amani juu yake ametuhadithia. Amesema: Ametuhadithia Abdulahi ibin Umar ibin Khataab Azaya mwaka wa mia mbili sitini na tano 265 (878-9) Amesema: Ametuhadithia mjomba wangu Ali bin Anuumani Al-Aalamu. Amesema: Ametuhadithia Umairi bin Mutawakili Athaqafiyu Al-Balakhiyu naye... kutoka kwa baba yake Mutawakili bin Haroon. Alisema nimekutana na Yahya bin zaid bin Aliy Alayhi-salaam naye akiwa yu aelekea khurasani baada ya kuuliwa baba yake nilimsalimia. Aliniuliza umetoka wapi? Nikasema kutoka Hajji. Aliniuliza kuhusu Ahli wake na watoto wa ami yake huko Madina na alisisitiza swali kuhusu Jaafar bin Muhammad amani iwe juu yake.Nilimuelezea khabari zake na khabari zao na huzuni walionayo kuhusu baba yao Zaid bin Aliy amani iwe juu yake. Aliniambia: Ami yangu Muhammad bin Aliy amani iwe juu yake alimshauri baba yangu asitoke na alimjulisha kuwa endapo atatoka na kuiacha Madina mambo yatavyomuwia. Je ulipata kukutana na mtoto wa ami yangu Jaafar bin Muhammad amani iwe juu yake? Nikamwambia ndio. Akasema je ulipata kumsikia anasema chochote kunihusu? Nikasema ndio.
Akasema: Alisema nini kunihusu? Nikasema nimejitoa muhanga kwako sipendi nikukabili kwa yale niliyoyasikia kutoka kwake. Akasema wanitishia umauti? Lete ulichosikia. Nikasema nimemsikia akisema kwa hakika kabisa kuwa utauliwa na utasulubiwa kama alivyouliwa baba yako na alisulubiwa. Basi uso wake ulibadilika na akasema: (Mungu huyafuta apendayo na huyathibitisha na kwake ipo asli ya kitabu). Ewe! Mutawakilu hakika Mwenyezi Mungu mwenye enzi na ametukuka ameliunga mkono jambo hili kupitia kwetu na ametupa sisi elimu na upanga. Haya mawili yameunganishwa na sisi na wamepewa wana wa ami yetu khususan elimu tu peke yake. Nikasema nimejitoa kwako muhanga mimi naona watu wanaelemea sana kwa mwana wa ami yako Jaafar amani iwe juu yake kuliko kwako na kwa baba yake. Akasema: kwa hakika ami yangu Muhammad na mwanawe Jaafar amani iwe juu yao wamewaita watu kwenye uhai na sisi tumewaita kwenye umauti. Nikasema ewe mwana wa mjumbe wa Mungu je wao wanaelimu zaidi au ninyi? Aliinama punde kisha akainuwa kichwa chake na akasema: Sote tunaelimu isipokuwa wao wanayajua yoote tuyajuwayo nasi hatujuwi yote wayajuwayo. Kisha aliniambia: Je umeandika chochote kutoka kwa mwana wa ami yangu? Nikasema naam. Akasema nionyeshe, nikamtolea aina kadhaa za elimu na nikamtolea duwa nilizoandika kutoka kwake Abiy Abdilahi amani iwe juu yake. Na alinihadithia kuwa baba yake Muhammad bin Aliy amani iwafikie alimwandikia kwa imla na akampa khabari kuwa ni miongoni mwa DU'A za baba yake Aliy bin Husain amani ziwe juu yao ni miongoni mwa DU'A za Sahifa al-Kamila. Yahya aliiangalia mpaka mwisho wake na aliniambia: Je waniruhusu niinakili? Nikasema Ewe mwana wa mjumbe wa Mungu waomba ruhusa kile ambacho ni kutoka kwenu? Akasema hakika nitakutolea Sahifa ya DU'A kamili zile alizozihifadhi baba yangu kutoka kwa baba yake na kwa hakika baba yangu ameniusia kuilinda na kutompa asiyestahiki. Umairu alisema: Alisema baba yangu: Basi nilisimama na kumwendea nikabusu kichwa chake. Na nikamwambia naapa ewe mwana wa mjumbe wa Mungu hakika mimi nitafanya dini ya Mungu kupitia upendo wenu na kuwatii ninyi, nami nataraji anipe Mungu maisha ya faraja na umauti mwema kwa wilaya yenu (kuwa penda). Basi alitupa zile kurasa zangu nilizompa kwa mtoto alikuwa pamoja naye na akasema andika DU'A hii kwa hati bayana nzuri kisha nipe huenda nikaihifadhi kwani nilikuwa naiomba kutoka kwa Jafari Mungu amhifadhi naye alikuwa akiniziwiya nayo. Mutawakilu alisema: Nilijutia nililofanya sikujuwa la kufanya na Abu Abdilahi amani imfikiye hakuniambia kuwa nisimpe yeyote! Baadaye aliagiza kisanduku ambacho humo alitowa sahifa iliyofungwa na kupigwa muhuri akauangalia ule muhuri na akaubusu akalia akavunja na kufunguwa kufuli. Kisha aliikunjuwa ile sahifa na akaiweka kwenye macho yake na kuipitisha usoni kwake na akasema walahi ewe! Mutawakilu lau kama kwa ajili ya yale uliyoyasema miongoni mwa usemi wa mwana wa Amiy yangu yakuwa mimi nitauwawa na kusulubiwa nisingekupa hii sahifa ningeifanyia ubakhili. Lakini natambua kuwa usemi wake ni wa haki ameuchukua kutoka kwa baba zake na itatimia hivyo basi nimeogopa elimu kama hii iwafikie baniy Umayya wataificha katika kabati zao kwa ajili yao tu. Ichukue ihifadhi kwa niaba yangu na ungoje ukiwa nayo Mungu atapopitisha jambo langu na jambo la hawa watu na atapitisha.
Basi hiyo ni amana yangu kwako mpaka uifikishe kwa wana wawili wa Amiy yangu Muhammad na Ibrahim wana wawili wa Abdilahi bin Hassan bin Hassan amani iwafikie. Kwa sababu wao ndio watakaoshika jambo hili baada yangu.Mutawakilu akasema: Niliipokea sahifa. Na alipouliwa Yahya bin Zaid nilikwenda Madina nikakutana na Aba Abdilah, amani imfikie. Nilimsimulia zile khabari kumuhusu Yahya alilia sana na huzuni kumuhusu ilikithiri na akasema: Mungu mrehemu mwana wa Amiy yangu na amkutanishe na baba zake na babu zake. Wallahi ewe Mutawakilu halikunizuwia kumpa ile DU'A yeye isipokuwa lile alilolihofia kuhusu sahifa ya baba yake, basi iwapi sahifa? Nikasema: Ni hii.Aliifungua na akasema: Wallahi hizi ni hati za Amiy yangu Zaid na ni DU'A ya babu yangu Aliy bin Hussain amani iwafikie. Kisha alimwambia mwanawe: Simama ewe Ismael niletee ile DU'A ambayo nilikuamuru uihifadhi kwa moyo na kuilinda Ismael alisimama na aliitowa ile sahifa kama ile aliyo mkabidhi Yahya bin Zaid Abu Abdilahi aliibusu na aliiweka machoni kwake na akasema huu ni mwandiko wa baba yangu na aliiandika kwa imla aliyoifanya babu yangu amani iwe juu yao mimi nikiwa naona. Nikasema ewee mwana wa Mtume wa Mungu waonaje nikiilinganisha na sahifa ya Zaidi na Yahya? Aliniruhusu kufanya hivyo na alisema: Nakuona wafaa kwa hilo.Nikazichunguza naona kuwa zi kitu kimoja sikuipata hata herufi moja inatofautiana na zilizo kwenye sahifa nyingine. Kisha nilimwomba ruhusa Aba Abdilah amani iwe juu yake ili niwape sahifa watoto wawili wa Abdilahi bin Husain. Akasema (hakika Mungu anakuamrisheni kuzifikisha amana kwa wenyewe) ndio wape hao wawili.Nilipoinuka ili kukutana nao aliniambia: bakia mahali pako. Kisha alituma waitwe Mohammad na Ibraheem, na akasema huu ni urithi wa mwana wa Amiy yenu Yahya kutoka kwa baba yake amempeni ninyi khususan na kuwaacha ndugu zake. Nasi tunakuwekeeni sharti. Wakasema sema kwani kauli yako yakubalika. Akasema musitoke nayo sahifa hii nje ya Madina.Wakasema: Kwanini iwe hivyo? Akasema: Kwa hakika mwana wa Amiy yenu aliihofia jambo nami nalihofia kwenu. Wakasema kwa hakika aliihofia alipojua kuwa atauwawa. Akasema Abu Abdilah amani imwendee; na ninyi musijiaminishe, kwa kweli najua kuwa ninyi mutapinga kama alivyopinga na mutauwawa kama alivyouwawa. Walisimama huku wakisema hapana hila wala nguvu ila kwa kuwezeshwa na Mungu aliye na enzi ya juu mno mtukufu.Walipokwisha toka akaniambia Abuu Abdilahi amani imfikiye: Ewe Mutawilu: vipi Yahya alikwambia kuwa hakika Amiy yangu Mohammad bin Aliy na mwanawe Jaafar wanawaita watu kwenye uhai nasi tunawaita kwenye umauti? Nikasema ndio Mungu akuweke katika islahi aliniambia hivyo mwana wa ami yako Yahya. Akasema Mungu amrehemu Yahya, hakika baba yangu alinihadithia naye alihadithiwa na baba yake naye toka kwa babu yake toka kwa Aliy amani juu yake kuwa mjumbe wa Mungu(s.a.w.w)
alisinzia kidogo akiwa juu ya membari yake akaona akiwa katika usingizi wake kuwa watu wanaruka ruka juu ya membari yake kama ngedere na kuwafanya watu warudi kinyume nyume.Mtume wa Mungu alikaa sawasawa(s.a.w.w)
hali ikiwa huzuni imetanda usoni kwake. Jibrilu
alimjia na aya hii: (Hatukuifanya njozi tuliyokuonyesha isipokuwa ni mtihani kwa watu na mti ulio laaniwa katika Qur'an na tunawahofisha lakini haiwazidishii ila kuvuka mipaka kukubwa) Awakusudia Baniy Umayya kwa tamko la mti uliolaaniwa katika Qur'an.
Akasema ewe Jibril watakuwa katika muda wangu na katika wakati wangu? Akasema la hapana lakini kinu cha Uislamu kitazunguka toka kuhama kwako na kubaki miaka kumi baada ya hapo kinu cha Uislam kitazunguka mpaka miaka thelathini na tano toka kuhama kwako. Baada ya hapo kitabaki miaka mitano kisha hapana budi kutakuwa na maongozi potovu ya kuwa katika muhimili wake kisha kutakuwa na ufalme wa mafirauni. Akasema na Mungu mtukufu aliteresha aya ya Qur'an kuhusiana na hayo: (Kwa hakika tumeiteremsha usiku wa maazimio kitu gani kitakujulisha usiku wa maazimio nini usiku wa maazimio ni bora kuliko miezi elfu). Watamiliki Baniy Umayya wakati ambao hautakuwa na usiku wa maazimio. Akas.ema Mwenyezi Mungu mtukufu alimjulisha Nabiy wake(s.a.w.w)
utawala wa umaa huu na mamlaka yao muda wote huu. Hata lau milima ingerefuka kupita kiasi wangejirefusha na wao hata kushinda mirima mpaka Mungu mtukufu aidhinishe kutoweka ufalme wao na wao katika wakati huo wote wamepandisha bendera ya chuki na bughudha dhidi yetu sisi Ahla Bayt. Mungu alimpasha khabari Nabiy wake yale watakayopambana nayo Ahli Bayt wa Muhammad na wapenzi wao na Shia wao toka kwao (Baniy Umayya) katika siku za ufalme wao. Akasema: Mungu ameteremsha kuhusu hawa watu: (huwaoni ambao wameibadilisha neema ya Mungu kwa kukufuru na kuwafanya watu wao kubaki katika maangamizi wataunguwa katika jahannam na ni makazi mabaya mno.) Na neema ya Mungu ni Muhammad na Ahli Bayt wake kuwapenda wao ni iymani yaingiza peponi na kuwachukia ni ukafiri na unafiki uingizao motoni.Mtume wa Mungu aliiweka siri hiyo kwa Aliy na kwa Ahli Bayt wake. Akasema: Kisha Abu Abdilahi amani iwe juu yake alisema: Hajatokea wala hatotokea kati yetu Ahli Bayt yeyote mpaka siku ya kusimama na kujitokeza kwa qaim wetu Imamu Mehdi ili aziwiye dhulma au kuifanya haki itekelezeke ila atagongana na balaa na itakuwa kujitokeza kwake ndio sababu ya kuzidisha uadui na msiba juu yetu na Shia wetu. Mutawakilu bin Haroon alisema: kisha Abu Abdilahi aliniandikia DU'A kwa njia ya imla nazo zikiwa katika milango 75 imenipotea kutokana nazo milango kumi na moja na nimehifadhi miongoni mwa DU'A hizo milango sitini na kitu. Ametuhadithia Abul-Fazzal amesema: Na amenihadithia Muhammad bin Al-Hassan Ibun Ruzbih Abu Bakr Al-madaini mwandishi ni mkazi wa Arrah'ba alitusimulia akiwa nyumbani mwake. Amesema: Amenihadithia Mohammad bin Ahmad bin Muslim Al-Mutaharyu, amesema: amenihadithia baba yangu kuutoka kwa Umairi bin Mutawakili Al-Balkhiyi toka kwa baba yake Al-Mutawakilu bin Haroon. Alisema: Nilikutana na Yahya bin Zain bin Aliy amani iwe juu yao na aliitaja hadithi kikamilifu mpaka ile njozi ya Nabiy(s.a.w.w)
ambayo Jaafar bin Muhammad aliitaja toka kwa baba zake amani iwafikie. Na katika riwaya ya Almutahari imetajwa milango nayo ni:
1. Kumuhimidi Mungu mwenye enzi na ametukuka.
2. Sala kwa Muhammad na Ali wake.
3. Sala kwa wabeba arshi (kitanda.)
4. Sala kwa wanomsadiki Mtume.
5. DU'A kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wamuhusuo.
6. DU'A ya kila asubuhi na jioni.
7. DU'A yake kwa ajili ya mambo yanayotisha na muhimu.
8. DU'A yake kwa ajili ya kujikinga.
9. DU'A yake kwa ajili ya ayapendayo.
10. DU'A yake kwa kutaka Mungu awe ndio kimbilio lake.
11. DU'A yake kwa ajili ya mwisho mwema.
12. DU'A yake kwa ajili ya kukiri.
13. DU'A yake kwa ajili ya mahitaji.
14. DU'A yake kwa ajili ya matendo ya dhuluma.
15. DU'A yake wakati wa ugonjwa.
16. DU'A yake kutaka ufumbuzi.
17. DU'A yake dhidi ya shetani.
18. DU'A kwa kujihadhari na hatari.
19. DU'A yake kuomba maji.
20. DU'A yake kwa ajili ya kuwa na tabia njema.
21. DU'A yake akihuzunishwa na jambo.
22. DU'A yake wakati wa shida.
23. DU'A yake kwa ajili ya afya njema.
24. DU'A yake kwa ajili ya wazazi wake wawili.
25. DU'A zake kwa ajili ya watoto wake.
26. DU'A yake kwa ajili ya majirani zake na rafiki zake.
27. DU'A yake kwa ajili ya walinda mipaka.
28. DU'A yake katika mfadhaiko.
29. DU'A yake inapokuwa haba riziki.
30. DU'A zake ili kupata msaada wa kulipa deni.
31. DU'A yake kwa ajili ya toba.
32. DU'A yake katika sala za usiku.
33. DU'A yake katika kumwomba Mungu amchagulie lililobora (istikhara)
34. DU'A yake apatwapo na balaa au aona balaa ya nyemelea
kumfedhehesha kwa dhambi.
35. DU'A yake kuonyesha ridha kwenye maamuzi ya Mola.
36. DU'A yake asikiapo radu.
37. DU'A yake katika kuonyesha shukurani.
38. DU'A yake kuomba udhuru.
39. DU'A yake kuomba msamaha.
40. DU'A yake akumbukapo umauti.
41. DU'A yake kuomba kusitiriwa na hifadhi.
42. DU'A yake wakati wa kuhitimisha Qur'an.
43. DU'A yake anapouona mwezi mwandamo.
44. DU'A yake uingiapo mwezi wa Ramadhani.
45. DU'A yake kuuaga mwezi wa Ramadhani.
46. DU'A yake kwa ajili ya Iddi ya Fitri na Ijumaa.
47. DU'A yake siku ya Arafat.
48. DU'A yake siku ya uzhiya (kuchinja) na siku ya Ijumaa.
49. DU'A yake kujikinga na vitimbi vya maadui.
50. DU'A yake wakati wa hofu.
51. DU'A yake katika kumwomba Mungu sana na unyenyekevu.
52. DU'A yake katika kuomba kwa bidii.
53. DU'A yake katika kujidhalilisha (mbele ya Mungu).
54. DU'A yake ili kuondoa maudhi.
Ama milango iliobaki ni kwa matamko ya Abiy Abdilahi Al-Hasaniy rehma za Mungu zimfikie.
Ametuhadithia Abu Abdilah Jaafar bin Mohammad Al-Hasaniy, amesema: Ametuhadithia Abdulahi bin Umairi bin Khataab Azzayatu. Amesema: Amenihadithia mjomba wangu Aliy bin Annuumani Al-Halam.
Amesema: Amenihadithia umairu bin Mutawakilu Athaqafiyu Al-Balakhiyu kutoka kwa baba yake Mutawakilu bin Haroon. amesema amenifanyia imlaa bwana wangu Aswadiqu Abu Abdilahi Jaafar bin Muhammad.
Amesema: Babu yangu Aliy bin Husain alimfanyia imla mbele ya macho yangu baba yangu Muhammad bin Aliy, juu ya wote amani ya Mungu iwafikie.