• Anza
  • Iliyopita
  • 8 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 3307 / Pakua: 3137
Kiwango Kiwango Kiwango
MASOMO YA KI-ISLAMU 1

MASOMO YA KI-ISLAMU 1

Mwandishi:
Swahili

MASOMO YA KI-ISLAMU

KITABU CHA KWANZA

DIBAJI

Je, wajua nani Mwislamu? Mwislamu ni ambaye anaamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na Muhammad ni Mtume wake wa mwisho. Kama ukiamini haya, basi wewe ni Mwislamu.

Lakini haitoshi kusematu kuwa mimi ni Mwislamu; bali ni wajibu juu yako kutenda kwa mujibu wa kanuni za Ki-islamu, ili uwe Mwislamu wa ukweli, na uishi duniani katika raha, na upate utukufu Akhera[1] kwa kuingia peponi na kupata ridhaa za Mwenyezi Mungu.

Basi ni lazima juu yako kujitahidi kufanya hayo.

Na Uislamu una sehemu tatu:

(1) Asili (Mizizi) ya Dini

(2)Matawi ya Dini

(3) Tabia (Mwenendo) ya Dini

Basi anayekubali kwa ukweli Asili ya Dini, na kutumia Matawi ya dini. na akiishajipamba na tabia ya dini, basi yeye ni mbora duniani na akhera (Kiyama)[2] .

Kitabu hiki Kimefasiriwa na Sheikh Muhammed Ali Ngongabure, na kimesahihishwa na kimepangwa na Ayatullah Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Muasisi na Muhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania.

Wabillahi Tawfiq.

MASOMO YA KIISLAMU

SOMO LA KWANZA

MIZIZI YA DINI

Mizizi ya Dini ni mitano (5):

(1) Kumpwekesha Mungu (Umoja wa Mungu)

(2) Uadilifu wa Mungu

(3)Utume

(4) Uimamu (Makhalifa)

(5) Marudio (Kiyama)

KUMPWEKESHA MWENYWZI MUNGU

Kumpwekesha Mungu, maana yake ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu. Nako ni kujua kuwa hakika vilivyoko vimeumbwa na Mungu, vimekuwepo baada ya kuwa havikuwepo; na mikononi mwake kimo kila kitu. Kuumba, kuruzuku, kutoa, kuzuia, kufisha, kuhuisha, uzima na ugonjwa, yote haya yapo chini ya irada yake na kutaka kwake.

" إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾ "

Hakika atakapopitisha amri yake kwa cho chote hukiambia kuwa kikawa.

Na dalili (uthibitisho) ya kuwepo kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ambavyo tunavyoviona miongoni mwa mbingu na vilivyomo, kama Jua lenye anga na Mwezi wenye nuru, na Nyota zenye kung' aa, na Mawingu na Upepo na Mvua; na ambavyo vimo katika ardhi na vilivyomo kama Bahari na Mito na Matunda na Miti, na Madini mbali mbali yenye thamani kama dhahabu na fedha na zumaridi, na vinginevyo kama Wanyama wenye kuruka hewani. na wenye kuogelea majini na wanaochungwa ardhini kwa umbo mbali mbali. na sauti zenye kubainika, na kirimbo zenye kufanana na zisizofanana; na mti wa kiajabu: masikio na ulimi (lugha), na mwenye ugonjwa na afya na furaha na ghadhauu na huzuni na vinginevyo.

Vyote hivi ni dalili ya kuwepo MOLA Mwenye Hekima na Uj uzi.

Kwa hivyo tunaamini kwaye na kumwabudu, natunamtaka msaada na kumtegemea Mwenyezi Mangu Huyo Mtakatifu

Na Yeye jina lake ni ALLAH.

Mungu Mtakatifu Anazo sifa nyingi sana. Kwa mfano:

(l)Ujuzi (Elimu)

Yeye anajua kila kitu, kikiwa kikubwa au kidogo; na anajua vilivyomo nyoyoni. Hapana chochote cha siri kwake.

(2) Uwezo (Qudra)

Mwenyezi Mungu anao uwezo juu ya kila kitu na kila jambo: kama kuumba, kutoa riziki, na kufisha na kuhuisha na mengineyo.

(3)Uhai Yeye ni hai-hafi.

(4) Irada (Kutaka)

Mungu yupo mwenye Irada (kutaka). Hutaka kitu ndani yake umo utengeneo; wala hataki kuwemo ndani yake uharibifu. Na vitendo vy'ake vyote hutenda kwa hiari yake mwenyewe; hana anayemlazimisha.

(5) Idraaku:

Yeye yuna udiriko (utambuo). Kwa hivyo huona kila kitu. ijapokuwa hana macho; na husikia kila sauti - ijapokuvva mnong'ono ndani ya sikio hata kama hanamasikio.

(6) Utangu

Mwenyezi Mungu hana mwanzo wala mwisho. Yeye ni watangu kabla ya kila kitu, kisha kaumba vitu, na atasalia baada ya vitu hivyo milele kwa milele.

(7) Kusema

Yeye ni msemi na huwasemeza waja wake awatakao ambao ni watakatifu, na wajumbe wake, na malaika wake. Na yeye anaweza kukisemesha chochote, kama alivyotia msemo katika mti na akazungumza naNabii Musa(a.s) , na alivyoumba sauti katika Nuru na akazungumza na Nabii wetu Muhammad(s.a.w.w)

(8)Ukweli

Mungu ni mkweli na husadikika ambayo anayosema, wala hageuzi waadi wake, na ahadi zake.

Na kadhalika Mungu Mtakatifu ni Muumba, Mtoa riziki, Muhuishaji, Mtoaji, Mzuiaji, Mpole, Msameheji, Mtukufu, Mkarimu.

Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutakasika kunako upungufu. Kwa mfano:

Hana mwili wala hana sehemu zenye kupandana katika mafungu mbali mbali.

Yeye hawezekani kuonekana popote, si duniani wala akhera (Kiyama).

Mwenyezi Mungu hashukiwi na vizuko, kama kuumwa wala kuwa na njaa, wala kuwamkongwe.

Mwenyezi Mungu hana mshiriki kamwe, ni mmoja (Ahad).

Sifa zake ni dhati (nafsi) yake, yeye Mjuzi, Mweza, tangu Azali Wala hakuwa kama mfano wetu, ambao tulikuwa wajinga, kisha tumekuwa wajuzi, na tulikuwa waelevu, kisha tumekuwa wawezaji.

Yeye Mwenyezi Mungu ni mkwasi ambaye hahitaji chochote. Hahitaji mashauri na yeyote wala msaidizi au waziri au askari na namna yoyote inavyopelekea hivyo. Yeye hategemei juu ya yoyote.

Mwenyezi Mungu Amesema:

Sema! Yeye Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Mwenyezi Mungu asiyehitaji. Ambaye wote wanahitaji kwake; Hakuzaa wala hakuzaliwa; Wala Hana anayefanana naye hata mmoja. (Qur an).

MASOMO YA KIISLAMU

SOMO LA PILI

UADILIFU WA MWENYEZI MUNGU

Maana yake hakika Mwenyezi Mungu ni Mwadilifu, hamdhulumu yeyote wala hatendi yanayo kanusha hekima.

Na kila umbo, na riziki, na utoaji. na kuziwia yote yanayotokana kwake. Nayo kwa maslaha, ijapo hatujui maslaha (hekima na manufaa) hayo.

Kwa mfano, mganga anapomfanyia dawa moja wapo, tunajua ndani yake imo maslahi, ij apokuwa hatuj ui namna ya kuponesha dawa hiyo. Kwa hivyo. tunapoona Mwenyezi Mungu kamtajirisha mtu, na kamfakirisha mwingine, au mmoja kampa utukufu na kamnyima mwingine, au kampa mmoja afya na mwingine ugonjwa (na mifano mingine) basi ni lazima tukubali kwa ukweli (tuamini) hakika yote haya yanafanyika kwa maslaha na hekima, ijapokuwa hatujui hekima zake.

HADITHI

Nabii Mussa(a.s) kamwomba Mwenyezi Mungu kuwa amjulishe sehemu tu ya Uadilifu wake katika yanayomtabisha kujua hekima zake uonekanavyo. Hapo Mwenyezi Mungu akamwamuru aende katika chemchem ya maji jangwani, ili atazame nini kinachotendeka huko.

Wakati alipofika Nabii Mussa(a.s) kamwona mpanda farasi akateremka katika chem chem akafanya haja zake. Basi mapesa aliyokuwa nayo yakadondoka hapo hapo. Kisha akaja mtoto baada ya muda akaokota mfuko wa mapesa na akaondoka nao. Baadaye akaja kipofu ili atawadhe katika chem chem hiyo. Punde akarudi yule mpanda farasi; akadhani kuwa pesa zake kachukua yule kipofu. Yakawa mabishano, mpaka akamuua yule kipofu kwa kumtuhumu kuwa ni mwizi wake.

Alipoondoka mpanda farasi, Mungu akapeleka habari kwa Nabii Mussa(a.s) kwamba yule mpanda farasi alikuwa ameiba mali ya baba yake yule mtoto; kwa hiyo tumeirudisha mali ile kwa warithi na yule mtoto ndie mrithi. Na yule kipofu ndie alie muua baba wa mpanda farasi, basi naye kachukua kisasi chake.

Tazama, ewe, ndugu yangu!

Hii ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na usawa wake, ijapokuwa katika fikra zetu ni jambo lililo mbali na kawaida zetu.

Imesemekana, Mfalme wa Iran, Kisra, aliulizwa, "Kwa nini umejifunza Uadilifa?"

Akajibu, "Mimi ninajua hakika kila analotenda mtu, jambo zuri au baya, hapana shaka atalipwa malipo yake."

Akaulizwa, "Nilikuwa siku moja nikitoka kwenda porini kuwinda.

Nikamuona paa, nikamtumia mbwa akamkamata kwa desturi, akamuuma mguu wake yule paa na akauvunja.

Baadaye hapakupita muda yule mbwa alikwenda mbele ya farasi, akapigwa teke na farsi, mguu wake yule mbwa ukavunjika.

Kwa hiyo, nikatambua kuwa mtu atapofanya usawa atapata usawa wake, na akifanya udhalimu atakuta malipo ya udhalimu wake. Kwa hiyo ninatenda usawa.

Ewe, ndugu yangu, baada ya maelezo haya unatamani tena kufanya ubaya? Laa, hasha, jiepushe nao.

MASOMO YA KIISLAMU

SOMO LA TATU

UTUME

Mtume (Nabii) ni mtu (mwanaume) ambaye kapelekewa wahyi[3] na Mungu, kwa kuokoa watu kunako giza la dhulma, ubatilifu na uj inga na kuwaita katika nuru ya haki, ukweli na elimu.

Mitume wanagawika sehemu mbili:

(1) Mtume Mursali:ni Mtume ambaye kapewa sharia mpya kuwafikishia watu.

(2) Mtume asiyekuwa Mursali: ambaye hakupewa sharia mpya, bali akafuata sharia ya Mtume Mursali.

Na hesabu ya Mitume ni laki moja na ishirini na nne elfu (124,000). Mtume wa kwanza ni Adamu(a.s) na wa mwisho wao ni Muhammad(s.a.w.w) .

ULUL-AZM NI WATANO

1.Nabii Nuhu(a.s.)[4]

2.Nabii Ibrahim(a.s)

3.Nabii Mussa(a.s)

4.Nabii Issa(a.s)

5.Nabii Muhammad(s.a.w.w.) [5]

Mayahudi ni katika wafuasi wa Nabii Mussa(a.s) na Wakristo ni katika wafuasi wa Nabii Issa(a.s) , na Waislamu ni wafuasi wa Nabii Muhammad (s.a.w.w.) Maana yake: "Rehma na Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe juu yake na kizazi vyake."

Na Uislamu umefuta dini zilizo tangulia (kama Uyahudi na Ukristo), wala haifai kubakia katika dini hizo, ispokuwa inalazimu kwa watu wote kufuata dini ya ki-Islamu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

"Atayefuata dini isiyokuwa Uislamu hatakubaliwa kwake, na yeye siku ya Kiyama atakuwa ni mwenye hasara".

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

Basi dini za Kiyahudi na kinaswara zimebatilika kabisa, na Uislamu unabaki sharia yake Mwenyezi Mungu mpaka Kiyama, haifutwi milele.

Hakika umejua kwamaba Mtume Muhammad(s.a.w.w) ni wamwisho wa Mitume wote, na dini yake yaani Uislamu umefuta dini zote, na sheria yake itasalia mpaka siku ya Kiyama.

BAADHI YA HALI ZAKE TUKUFU

Yeye ni Muhammad(s.a.w.w) , mwana wa Abdullah, na mama yake ni Bibi Amina binti Wahabi. Kazaliwa siku ya Ijumaa, mwezi kumi na saba, mwezi wa mfungo sita, baada ya kuchomoza alfajiri, mwaka wa ndovu, mji wa Makka Mtukufu, zama za mfalme Naushirwan (wa Iran).

Alishukiwa na Jibril(a.s) (naye ni malaika mtukufu) na Mtume(s.a.w.w) wakati huo yuko katika pango la Jabal Hiraa lililoko nje ya Makka.

Akamletea Jibril sura ya Qur'an nayo:

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾

(Soma kwa jina la Mola wako ambaye kaumba, kamuumba mwanadamu kwa tone la damu iliyoganda. Soma, na Mola wako ni mkarimu sana, ambaye alifundisha na kalamu, alimfundisha mwanadamu asiyo yajua.)

Akasimama Mtume(s.a.w.w) kwa kufikisha ujumbe wa Mola wake. Akawa anapitapita njiani na katika uchochoro, na anasema: "Enyi watu, semeni 'Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah Mungu ni mmoja tu mtaokoka.)

(Ayyuha Nnasu, Quuluu Lailahailla Llahu, Tuflihuu) .

Kwa sababu watu wa Maka walikuwa wanaabudu masanamu wakawa wanamfanyia mizaha na kumcheka na kumfanyia mambo ya maudhi, mpaka Mtume(s.a.w.w) akasema: "Hakuudhiwa Mtume yeyote mfano (kama) nilivyo udhiwa mimi."

Wala hawakuamini ispokuwa kundi dogo. Na mwanzoni wao ni mkewe Khadija(a.s) , baadae Imam Amiirul Muuminiin Ali bin Abi Talib (juu yao rehma na amani), kisha watu wengine.

Ilipozidi fujo ya mushirikina[6] kwake, akahama kwenda Madina, na uhamiaji huo ndio mwanzo wa tarehe ya kiislamu. Nahuko walizidi Waislamu, na ikaendelea Dola ya kiislamu kuzidi nguvu na idadi mpaka ikazidi utamaduni wote ulimwenguni na dini na mila zote.

Na Mtume zama alipokuwa Madina ikambidi kujikengea kwa kupigana vita na mashambulizi. Vita hivyo vilikuwa kwa sababu ya mashambulizi ya mushirikina na Wayahudi na Wanaswara kwa Waislamu. Akawa

Mtume(s.a.w.w) kwa vitendo vyote hivyo akipelekea upande wa usalama na rehema na upole. Na kwa huruma kama hivyo haikufikia idadi ya walio uliwa katika vita vyote hivyo (ambavyo vimefikia zaidi ya thamanini) zaidi ya elfu na mia nne kwa pande mbili zote (Waislamu na maadui), kama ilivyoandikwa katika vitabu vya tarekhe.

Na tangu alipopewa Mtume(s.a.w.w) ujumbe mpaka akafa, ilikuwa Qur'ani ni hakiim[7] inamshukia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kiasi kwa kasi, katika matokeo mbali mbali, mpaka kikakamilika kitabu hiki kitukufu kwa muda wa miaka ishirini na tatu.

Akawa Mtume(s.a. w.w) anaistawisha dini ya Waislamu na dunia yao, na anawafunza Qur ani na hekima zake, na kuwakunjulia kanuni za ibada na mambo ya kutendeana na mikusanyiko na siasa na mengineyo.

Na baada ya kukamilika dini likashuka neno la Mola Mtumkufu:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣﴾

(Leo hii nimekukamilishieni dini yenu, na nimetimiza juu yenu neema zangu na nimekuwa radhi kwenu kuwa Uislamu ndio Dini.) Swadaka llahul adhwiim[8] .

Mtume(s.a.w.w) akapatwa na ugonjwa khafifu, lakini ukazidi mpaka ukapeleka kukutana na Mola wake siku ya ishirini na nane mwezi wa mfungo tano, mwaka wa kumi na moja wa Hijra. Akasimamia kwa kumkosha na kumkafini na kumsalia na kumzika Amirul Muuminiin[9] Ali bin Abi Talib(a.s) . Na kazikwa mji wa Madina Munawwara (Mji wenye nuru) palipo kaburi lake sasa.

Hakika Mtume(s.aw.w) alikuwa katika hali zake zote ni mfano bora kabisa wa uaminifu na ikhlaswi[10] na ukweli na uzuri wa tabia yake na elimu na upole na ubora na uhifaziko na uadilifu na unyenyekevu na ujihadi.

Na kilikuwa kiwiliwili chake Mtukufu kizuri mno katika ulingamanifu na munasaba[11] bora, na uso wake ulikuwa mng'avu kama mwezi usiku wa utulivu.

Na kwa hakika alikuwa Mtume(s.a.w.w) mkusanyiko ya utukufu. na ndio mafungamano ya utukufu na ukarimu, na ni mji wa elimu na usawa na fadhila, na asili ya dini na dunia. Wala hakutokea mfano wake kwa waliopita wala hatakuja baada yake milele kwa milele.

Basi huyo ni Mtume wa Uislamu na mkunjuwaji waUislamu. Dini yake ni bora kuliko dini zote, na kitabu chake ni bora kuliko vitabu vyote, hakiingiliwi na ubatilifu mbele yake wala nyuma yake, ni ushuko utokao kwa Mwenyezi Mungu Mwenye hekima na kuhimidia.

Kaacha Mtume(s.a.w.w) kwa umati wake vitu viwili navyo vikubwa: Kitabu cha Mungu (Qur'an) na Ahlul bayt (vizazi) vyake vitoharif. Akasema Mtume(s.a.w.w) : "Mimi nina kuachieni kwenu vitu vizito viwili namkishikamana navyo hamtapotea baada yangu milele, navyo ni Kitabu cha Mungu na kizazi changu Ahlul bayt. Hakika hivyo havitawachana mpaka vifike kwangu kwenye hodhi. Tazameni vipi mtafanya na viwili hivyo baada yangu."

Nilazima juu yetu sisi Waislamu, kama tukipenda uongofu na utukufu duniani na ubora na pepo akhera, kushikamana na hivi vitu viwili vizito: kwa kuwafuata na kuwapenda Maimamu watoharifu na kumchukia ambaye anawachukia, na kuchukua maneno yao kwa kila sharia na Qur'ani alhakim kwa kuisoma vizuri na kuifahamu na kuifuata Qur'ani katika mambo yetu yote.

Lau Waislamu wakishikamana kwa hivi vitu viwili vikubwa wangalitukuka duniani kwa uadilifu na ustawi na ingalitukuka dunia nao kama ilivyotukuka na wazazi wao.

MASOMO YA KIISLAMU

SOMO LA NNE

UIMAMU

Tunajua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Ambaye Aliagiza Mitume wake. Basi vilevile Mwenyezi Mungu ndiye ambaye anayo Madaraka (Uwezo) wa kuteua mawasii[12] (Makhalifa) wa Mitume.

Mungu kamtajia Mtume wetu Muhammad(s.a.w.w) mawasii na makhalifa wake kumi na wawili. Na hao maimamu[13] kumi na wawili mashuhuri kwa Waislmu wote.

Nao ni:

(1) Imam Amirul Muuminiin Ali bin Abi Talib. Naye ni mtoto wa baba yake mkubwa Mtume(s.a.w.w) , tena kamwoza Mtume binti yake Fatima(a.s.)

(2) Imam Hassan bin Ali(a.s) na mama yake ni Fatima binti Muhammad(s.a.w.w) .

(3)Imam Hussein bin Ali (Shahid), na mama yake ni Fatima binti Muhammad(s.a.w.w) .

(4) Imam Zainul Abidiin(a.s) [14] Ali bin Hussein(a.s).

(5) Imam Al-Baquir[15] Muhammad bin Ali(a.s) .

(6) Imama As-Sadiq[16] Jafar bin Muhammad(s.a.w.w) .

(7) Imam Al-Kadhim[17] Mussa bin Jaffer(a.s) .

(8) Imam Al-Ridha[18] Ali bin Mussa(a.s) .

(9) Imam Al-Jawad[19] Muhammad(a.s) .

(10) Imam Al-Had[20] Ali bin Muhammad(a.s) .

(11) Imama Al-Askari[21] Hassan bin Ali (a.s.).

(12) Imam Al-Mahdi [22] ([22]) Muhammad bin Hassan Al- Qaim Al- Muntazar (a.s.).

Hawa Maimamu ni hoja za Mungu juu ya viumbe, nao wamekuwa wote katika nuru ya Mtume wa Mungu (s.a.w.w), wamekuwa kama Mtume katika elimu na upole na utukufu na uadilifu na uhifadhiko na tabia nzuri na sifa njema nyingine. Je! isiweje hivyo, nao ni makhalifa wake Mtume na mawasii wake na maimamu na viongozi wa viumbe, na hoja za Mungu kwa viumbe wake wote.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w) Amesema:-

Mfano wa Ahlul Bayt wangu (kizazi changu) ni mfano wajahazi ya Mtume Nuhu (ilipokuja gharika waliopanda jahazi hilo wakavuka na wasiopanda wakazama na kuangamia) basi mwenye kushikamana na kuwapenda Ahlul Bayt ndio kaongoka na kufuzu na mwenye kuwatenga hawa ataangamia katika upotovu na ujinga.

MASOMO YA KIISLAMU

SOMO LA TANO

AL-MAAD - MAREJEO YA QIYAMA

Na maana yake ni kuwa Mungu Mtukufu atahuisha wana damu baada ya kufa. ili alipwe mwenye kupata mema, na mabaya kupata mabaya.

Aliyeamini nakutenda mema, akasali, akafunga, akatoa zaka, kwa utakasiflu, akawahifadhi mayatima, akawalisha masikini na mengineyo - basi ataingia peponi, pepo ambayo hupita chini mito katika vivuli vifunikavyo na rehema kunjufu, na majumba mazuri, na neema zinginezo za Mwenyezi Mungu.

Na anayekufuru na kufanya mabaya, na kukanusha, na kuhini na kuua na kuiba, na kunywa ulevi, na mengineyo, basi atalipwa adabu ya Jahannam, umejaa moto na adhabu, na chakula chake ni Zakkumi, na kinywaji chake ni maji ya moto, atakuwa ndani ya huzuni daima, na adhabu ya milele.

Na huko. kabla ya pepo na moto yapo mambo mawili:

(l) Kaburi- Kilammoja huulizwa kaburini mwake kwa yale aliyoyafanya, hulipwa kwa matendo mazuri na matendo mabaya. Kwa hivyo, akasema Mtume(s.a.w.w) kuwa:- "Kaburi huwa shimo la moto au Bustani ya Pepo."

Humshukia mtu kaburini mifano kama inavyo mshukia mwenye kulala, ambaye huona ndoto nzuri anafurahi nayo. au ndoto mbaya ikimwadhibisha, lakini yule ambaye yuko karibu naye hajui kuwa yumo ndani ya raha au adhabu.

Hivi hivi, walio hai hawaoni hali ya mtu aliyekufa ispokuwa mwili uliovunjika, lakini yeye yumo adhabuni au neemani, huwa hawahisi.

(2) Kiyama - Nacho baada ya kuhuishwa wote makaburini, watakusanywa wote katika uwanja mkubwa. Na huko itasimamishwa mahakama kubwa: itawekwa mizani na watahudhuria mahakimu (nao ni Mitume ya Mungu na ma-Imamu), na kugawiwa vitabu vya vitendo, na watakuja mashahidi, watatukuka waliyofanya vitendo vyema duniani, na watadhalilika wabaya walio fanya mabaya duniani.

Ni juu ya mtu kujitahidi kiasi cha uwezo wake kutenda vitendo vyema ili asipate hasara ambayo hamna makimbilio.

SHARTI YA KUCHAPA

Sharti ya kuchapa au kusambaza ni kutaja rejeo hili. haki zote zimehifadhiwa na Taasisi ya Al-Hasanain Taasisi ya Imamu Husein(a.s)

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini(a.s) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini.

MWISHO WA KITABU

YALIYOMO

MASOMO YA KI-ISLAMU 1

KITABU CHA KWANZA 1

DIBAJI 1

MASOMO YA KIISLAMU 2

SOMO LA KWANZA 2

MIZIZI YA DINI 2

KUMPWEKESHA MWENYWZI MUNGU 2

MASOMO YA KIISLAMU 4

SOMO LA PILI 4

UADILIFU WA MWENYEZI MUNGU 4

HADITHI 4

MASOMO YA KIISLAMU 6

SOMO LA TATU 6

UTUME 6

ULUL-AZM NI WATANO 6

BAADHI YA HALI ZAKE TUKUFU 6

MASOMO YA KIISLAMU 9

SOMO LA NNE 9

UIMAMU 9

MASOMO YA KIISLAMU 11

SOMO LA TANO 11

AL-MAAD - MAREJEO YA QIYAMA 11

SHARTI YA KUCHAPA 11

MWISHO WA KITABU 11

YALIYOMO 12


[1] . Akhera: Ufufuo

[2] . Kiyama - Siku ya kufufuliwa.

[3] . Wahyu: Ufunuo, khabari kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

[4] . (a.s): Hii ni muhtasar wa" Alaihis-Salaam." Maanayake: "Iwe Juu yake Amani ya Mwenyezi Mungu."

[5] . (s.a.w.w): Hii ni muhtasari wa "Swalallahu Alayhi wa Aalihi wa Sallam."

[6] . Mushrikina: Hu ni wingi wa 'Mushrik'', Mushrik: Ambaye anaabudu sanamu au vitu vinginevyo.

[7] . Al-Hakiim: Chenye Hekima.

[8] . Swadakallahu :-Mwenyezi Mungu kasema kweli.

[9] . Amirul Muuminiin:-Kiongozi wa Walioamini.

[10] . Ikhlaswi: Moyo safi.

[11] . Munasaba: Usawa, ukamilifu wa umbo.

[12] . Mawasii (wa Mitiime): Hii ni uwingi wa "Wasii" Wasii: Mshika makamu wa mtume.

[13] . Maimamu: Hii ni uwingi wa Imamu, Imam: Kiongozi vva dini.

[14] . Zainul Abidiin: Pambo la wacha Mungu.

[15] . Al-Baquir: Mchimbua Elimu.

[16] . As-Sadiq: Msemakweli.

[17] . Al-Kadhim: Mvunja ghadhabu.

[18] . Al-Ridha: Mwenye kupenda anayoyapenda Mungu.

[19] . Al-Jawad: Mkarimu.

[20] . Al-Hadi: Mwongozi.

[21] . Al-Askari: Mwenyekukaa mahala pa majeshi.

[22] . Al-Mahd: Mwenye uongozi bora.