MASOMO YA KIISLAMU
SOMO LA TATU
UTUME
Mtume (Nabii) ni mtu (mwanaume) ambaye kapelekewa wahyi
na Mungu, kwa kuokoa watu kunako giza la dhulma, ubatilifu na uj inga na kuwaita katika nuru ya haki, ukweli na elimu.
Mitume wanagawika sehemu mbili:
(1) Mtume Mursali:ni Mtume ambaye kapewa sharia mpya kuwafikishia watu.
(2) Mtume asiyekuwa Mursali: ambaye hakupewa sharia mpya, bali akafuata sharia ya Mtume Mursali.
Na hesabu ya Mitume ni laki moja na ishirini na nne elfu (124,000). Mtume wa kwanza ni Adamu
na wa mwisho wao ni Muhammad(s.a.w.w)
.
ULUL-AZM NI WATANO
1.Nabii Nuhu
2.Nabii Ibrahim
3.Nabii Mussa
4.Nabii Issa
5.Nabii Muhammad(s.a.w.w.)
Mayahudi ni katika wafuasi wa Nabii Mussa
na Wakristo ni katika wafuasi wa Nabii Issa
, na Waislamu ni wafuasi wa Nabii Muhammad (s.a.w.w.) Maana yake: "Rehma na Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe juu yake na kizazi vyake."
Na Uislamu umefuta dini zilizo tangulia (kama Uyahudi na Ukristo), wala haifai kubakia katika dini hizo, ispokuwa inalazimu kwa watu wote kufuata dini ya ki-Islamu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:
"Atayefuata dini isiyokuwa Uislamu hatakubaliwa kwake, na yeye siku ya Kiyama atakuwa ni mwenye hasara".
وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾
Basi dini za Kiyahudi na kinaswara zimebatilika kabisa, na Uislamu unabaki sharia yake Mwenyezi Mungu mpaka Kiyama, haifutwi milele.
Hakika umejua kwamaba Mtume Muhammad(s.a.w.w)
ni wamwisho wa Mitume wote, na dini yake yaani Uislamu umefuta dini zote, na sheria yake itasalia mpaka siku ya Kiyama.
BAADHI YA HALI ZAKE TUKUFU
Yeye ni Muhammad(s.a.w.w)
, mwana wa Abdullah, na mama yake ni Bibi Amina binti Wahabi. Kazaliwa siku ya Ijumaa, mwezi kumi na saba, mwezi wa mfungo sita, baada ya kuchomoza alfajiri, mwaka wa ndovu, mji wa Makka Mtukufu, zama za mfalme Naushirwan (wa Iran).
Alishukiwa na Jibril
(naye ni malaika mtukufu) na Mtume(s.a.w.w)
wakati huo yuko katika pango la Jabal Hiraa lililoko nje ya Makka.
Akamletea Jibril sura ya Qur'an nayo:
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾
(Soma kwa jina la Mola wako ambaye kaumba, kamuumba mwanadamu kwa tone la damu iliyoganda. Soma, na Mola wako ni mkarimu sana, ambaye alifundisha na kalamu, alimfundisha mwanadamu asiyo yajua.)
Akasimama Mtume(s.a.w.w)
kwa kufikisha ujumbe wa Mola wake. Akawa anapitapita njiani na katika uchochoro, na anasema: "Enyi watu, semeni 'Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah Mungu ni mmoja tu mtaokoka.)
(Ayyuha Nnasu, Quuluu Lailahailla Llahu, Tuflihuu)
.
Kwa sababu watu wa Maka walikuwa wanaabudu masanamu wakawa wanamfanyia mizaha na kumcheka na kumfanyia mambo ya maudhi, mpaka Mtume(s.a.w.w)
akasema: "Hakuudhiwa Mtume yeyote mfano (kama) nilivyo udhiwa mimi."
Wala hawakuamini ispokuwa kundi dogo. Na mwanzoni wao ni mkewe Khadija
, baadae Imam Amiirul Muuminiin Ali bin Abi Talib (juu yao rehma na amani), kisha watu wengine.
Ilipozidi fujo ya mushirikina
kwake, akahama kwenda Madina, na uhamiaji huo ndio mwanzo wa tarehe ya kiislamu. Nahuko walizidi Waislamu, na ikaendelea Dola ya kiislamu kuzidi nguvu na idadi mpaka ikazidi utamaduni wote ulimwenguni na dini na mila zote.
Na Mtume zama alipokuwa Madina ikambidi kujikengea kwa kupigana vita na mashambulizi. Vita hivyo vilikuwa kwa sababu ya mashambulizi ya mushirikina na Wayahudi na Wanaswara kwa Waislamu. Akawa
Mtume(s.a.w.w)
kwa vitendo vyote hivyo akipelekea upande wa usalama na rehema na upole. Na kwa huruma kama hivyo haikufikia idadi ya walio uliwa katika vita vyote hivyo (ambavyo vimefikia zaidi ya thamanini) zaidi ya elfu na mia nne kwa pande mbili zote (Waislamu na maadui), kama ilivyoandikwa katika vitabu vya tarekhe.
Na tangu alipopewa Mtume(s.a.w.w)
ujumbe mpaka akafa, ilikuwa Qur'ani ni hakiim
inamshukia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kiasi kwa kasi, katika matokeo mbali mbali, mpaka kikakamilika kitabu hiki kitukufu kwa muda wa miaka ishirini na tatu.
Akawa Mtume(s.a. w.w)
anaistawisha dini ya Waislamu na dunia yao, na anawafunza Qur ani na hekima zake, na kuwakunjulia kanuni za ibada na mambo ya kutendeana na mikusanyiko na siasa na mengineyo.
Na baada ya kukamilika dini likashuka neno la Mola Mtumkufu:
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣﴾
(Leo hii nimekukamilishieni dini yenu, na nimetimiza juu yenu neema zangu na nimekuwa radhi kwenu kuwa Uislamu ndio Dini.) Swadaka llahul adhwiim
.
Mtume(s.a.w.w)
akapatwa na ugonjwa khafifu, lakini ukazidi mpaka ukapeleka kukutana na Mola wake siku ya ishirini na nane mwezi wa mfungo tano, mwaka wa kumi na moja wa Hijra. Akasimamia kwa kumkosha na kumkafini na kumsalia na kumzika Amirul Muuminiin
Ali bin Abi Talib
. Na kazikwa mji wa Madina Munawwara (Mji wenye nuru) palipo kaburi lake sasa.
Hakika Mtume(s.aw.w)
alikuwa katika hali zake zote ni mfano bora kabisa wa uaminifu na ikhlaswi
na ukweli na uzuri wa tabia yake na elimu na upole na ubora na uhifaziko na uadilifu na unyenyekevu na ujihadi.
Na kilikuwa kiwiliwili chake Mtukufu kizuri mno katika ulingamanifu na munasaba
bora, na uso wake ulikuwa mng'avu kama mwezi usiku wa utulivu.
Na kwa hakika alikuwa Mtume(s.a.w.w)
mkusanyiko ya utukufu. na ndio mafungamano ya utukufu na ukarimu, na ni mji wa elimu na usawa na fadhila, na asili ya dini na dunia. Wala hakutokea mfano wake kwa waliopita wala hatakuja baada yake milele kwa milele.
Basi huyo ni Mtume wa Uislamu na mkunjuwaji waUislamu. Dini yake ni bora kuliko dini zote, na kitabu chake ni bora kuliko vitabu vyote, hakiingiliwi na ubatilifu mbele yake wala nyuma yake, ni ushuko utokao kwa Mwenyezi Mungu Mwenye hekima na kuhimidia.
Kaacha Mtume(s.a.w.w)
kwa umati wake vitu viwili navyo vikubwa: Kitabu cha Mungu (Qur'an) na Ahlul bayt (vizazi) vyake vitoharif. Akasema Mtume(s.a.w.w)
: "Mimi nina kuachieni kwenu vitu vizito viwili namkishikamana navyo hamtapotea baada yangu milele, navyo ni Kitabu cha Mungu na kizazi changu Ahlul bayt. Hakika hivyo havitawachana mpaka vifike kwangu kwenye hodhi. Tazameni vipi mtafanya na viwili hivyo baada yangu."
Nilazima juu yetu sisi Waislamu, kama tukipenda uongofu na utukufu duniani na ubora na pepo akhera, kushikamana na hivi vitu viwili vizito: kwa kuwafuata na kuwapenda Maimamu watoharifu na kumchukia ambaye anawachukia, na kuchukua maneno yao kwa kila sharia na Qur'ani alhakim kwa kuisoma vizuri na kuifahamu na kuifuata Qur'ani katika mambo yetu yote.
Lau Waislamu wakishikamana kwa hivi vitu viwili vikubwa wangalitukuka duniani kwa uadilifu na ustawi na ingalitukuka dunia nao kama ilivyotukuka na wazazi wao.