6
HADITH HADITH ZA MTUME (s.a.w.w)NA MA-IMAMU (a.s)
UJAHILI
155. Hakuna maumivu ya kupita zaidi ya ujahili.
156. Watu ni adui kwa kile walichobakianacho jahili.
157. Fadhila za jahili ni sawa na bustani juu ya chungu cha kinyesi.
158. Wasi-wasi ni matokeo ya ujinga.
159. Nia kuu ya busara ni kule mtu kukubali na kukiri ujinga wake (iwapo anao).
160. Ni mtu mpumbavu kabisa iwapo atapuuzia umuhimu wake (atajidharau, kujidhalilisha)
161. Mjinga ni mwenye hasara hata kama akiwa katika hali gani ile.
162. Ujinga uliodhalilishwa (wa ujinga) ni kule kumtii mwanamke.
UTUKUFU NA UMUHIMU WA WANAZUONI
162. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Yapo makundi mawili ya Ummah wangu kwamba wanapokuwa wachaAllah swt, Ummah wangu utakuwa sahihi na wakati watakapokuwa wameingiliwa na ufisadi, basi Ummah wangu utageuka kuwa waovu
."
Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
aliulizwa kuhusu waliokuwa wakimaanishwa. Alijibu: "Wanazuoni wa Din na watawala
."
163. Amesema Imam Muhammad al-Baqir
: "Utakapokuwa umekutana na Mwanazuoni basi uwe mwenye kutaka kujua mengi kuliko kujifanya msemaji zaidi, na ujifunze namna ya kusikiliza na namna ya kuzungumza vyema, na wala usimkatize kauli yake yoyote atakayokuwa akizungumza."
164. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Ewe 'Ali ibn Abi Talib! Malaika Jibraili alitaka alitamani kuwa mwanadamu kwa sababu saba zifuatazo:
1. Sala za Jama'a
2. Uhusiano pamoja na wanazuoni
3. Kudumisha amani miongoni mwa watu wawili
4. Kuwahurumia na kuwahishimu mayatima
5. Kuwatembelea na kuwajua hali wagonjwa,
6. Kuhudhuria na kushiriki katika mazishi
7. Kuwagawia maji mahujjaji
Kwa hivyo nyinyi pia muwe watu wa kuzipenda na kuvitekeleza vitu hivyo."
165. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. Amesema katika: "Iwapo matamshi ya watu wenye busara yatakuwa katika malengo yao, basi huwa kama matibabu, lakini yanapokuwa siyo sahihi basi ni sawa na ugonjwa
."
.
166. Amesema al-Imam Hassan al 'Askari
. katika: "Maulamaa wa Kishia'h ni walinzi wa mishikamano ya Islam. Kwa hivyo, yeyote yule katika wafuasi wetu anayechukua jukumu hili basi ni bora kuliko kupigana vita dhidi ya Waroma (kwa sababu huyu analinda mishikamano ya imani zetu).
167. Amesema al-Imam 'Ali ar-Ridha
: "Jihadharini kuwa hakimu wa kidini wa kweli ambaye anapatia watu mema na huruma, na kuwahifadhi dhidi ya maadui wao, kuwazidishia neema za Peponi na kuwapatia ridhaa za Allah swt kwa ajili yao (kwa kupitia hidaya)
."
168. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s).Amesema katika: "Malipo kwa Mwanazuoni ni zaidi kuliko malipo ya mtu afungaye saumu nyakati za mchana na kusali nyakati za usiku na akipigana vita vya jihadi kwa ajili ya Allah swt. Na, wakati mwanazuoni anapokufa, basi kutatokezea pengo katika Islam ambalo haliwezi kuzibwa illa kwa aina yake tu
."
169. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema: "Ewe Kumayil! Wale wanaojilimbikizia utajiri na mali ni watu waliokwisha kufa hata kama watakuwa bado hai, wakati maulamaa (wanazuoni) wenye elimu watabakia hadi hapo dunia itakapokuwa ikibakia. Hata kama watakuwa lakini mafunzo na mifano yao itabakia mioyoni mwa watu
."
170. Amesema al-Imam Husayn
: "Kwa hakika, njia ya masuala ya Waislamu na hukumu za Shariah zipo katika mikono ya Wanazuoni wakiAllah swt ambao ndio wenye amana za Allah swt katika mambo ayatakayo na yale asiyoyataka
"
.
KUWA MAKINI KUHUSU AKHERA
171. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
, "Wafuasi wa Mtume Isa (a.s). walimwuliza ni watu gani wawafanye marafiki wao, naye (a.s). aliwajibu: "Pamoja na wale ambao wanapokuwa nanyi humkumbusha Allah swt, mazungumzo yao hukuzidishieni ilimu na matendo yao huwavutieni ninyi kutenda matendo mema kwa ajili ya Aakhera
."
172. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
.Amesema katika: "Kusiwepo na shughuli ya aina yoyote ile ambayo itakuzuia kutenda matendo kwa ajili ya Aakhira, kwa hivyo, muda wa kufanya hivyo upo mdogo sana
."
173. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema katika: "Yeyote yule atakayeiuza Aakhera yake kwa maisha ya humu duniani, basi kwa hakika amepoteza yote kwa pamoja
."
.
174. Al-Imam 'Ali ibn Muhammad al-Hadi
. Amesema: "Kumbuka pale utakapokuwa kitandani ambapo mauti imekukalia kichwani na huku umezungukwa na ndugu na maJama'a zako, na hapo hakuna mganga anayeweza kukuepusha na kifo hicho wala hakuna rafiki anayeweza kukusaidia
."
JANNAT
175. Al Imam Ja'afer as-Sadiq
. amesema, "Kila mtu katika Jannat atahudumiwa kwa vitu vizuri vya Jannat kiasi kwamba hata atakapopata wageni kwa malaki na malaki lakini hakutapungua chochote neema nyingi tele
"
176. Al Imam Ja'afer as-Sadiq
. alijibu: "Allah swt ni mwadilifu. Iwapo matendo mema ya mwanamme yatakuwa zaidi ya mwanamke, basi mwanamme atapewa fursa kwanza kufanya chaguo na uamuzi iwapo anapendelea kuishi na mke wake au hapana. Na vivyo hivyo iwapo matendo mema ya mwanamke yatakuwa zaidi basi naye atapewa chaguo kama hili yaani iwapo atapenda kuishi na mume wake au hapana. Iwapo mwanamke huyo hatamchagua bwanake awe mume wake hapo Jannat, basi huyo mwanamme aliyekuwa mume wake humu duniani hatakuwa mume wake huko Jannat ."
177. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alisema kuwa Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu Sura-i-Yasin,36, Ayah ya 78 'Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake - akasema: "Nani atakaihuisha mifupa na hali imesagika?"
178. Katika Milango yote 8 ya Jannat kumeandikwa: Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. ni mja (Walii) Wake halisi,
179. Mlango wa kwanza Katika mlango wa kwanza wa Jannat kumeandikwa: Zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na njia za kujipatia riziki ni nnne: "kutosheka, "kutumia katika njia sahihi, "kukana kisasi na "kufanya uhusiano pamoja na watu waliookoka yaani katika njia nyoofu.
180. Mlango wa pili Zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na njia za kujipatia furaha katika maisha ya Aakhera ni nne : " Kuonyesha huruma kwa mayatima, " kuwawia wema wajane, " kuwasaidia wacha-mungu katika kufanikisha malengo yao na " kuwaangalia na na kuwasaidia masikini na wasiojiweza.
181. Mlango wa tatu Zipo njia mbalimbali za kujipatia kila kitu, na na njia za kujipatia siha njema katika maisha haya mafupi ni nne: " Kuongea kwa uchache, " kulala kidogo, " kutembea kidogo na " kula kidogo.
182. Mlango wa nne " Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wageni wake; "Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa jirani zake; "Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe mkarimu kwa wazazi wake; "Yeyote yule amwaminiaye Allah swt na siku ya Qiyamah basi lazime awe ni mwenye kusema mema au anyamaze kimya.
183. Mlango wa tano " Yeyote yule ambaye hataki kunyanyaswa siku ya Qiyamah, basi naye asimnyanyase mtu yeyote; " Yeyote yule ambaye hataki kusengenywa siku ya Qiyamah, basi naye asimsengenye mtu yeyote; " Yeyote yule ambaye hataki kudhalilishwa siku ya Qiyamah, basi naye asimdhalilishe mtu yeyote; " Mtu yeyote yule ambaye anataka kujishikiza kwa umadhubuti katika maisha haya mafupi na yale ya Aakhera, basi lazima atoe shahada kuwa : Hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu; Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume Wake; Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. ni mja (Walii) Wake halisi.
184. Mlango wa sita " Yeyote yule anayetaka kaburi lake liwe pana na lenye nafasi ya kutosha (kutombana) basi ajenge Misikiti; " Yeyote yule anayetaka asiliwe na wadudu au minyoo ya ardhini, aifanye Misikiti iwe nyumba yake (yaani awe akiizuru kwa mara nyingi kama kwamba anaishi humo); " Yeyote yule anayetaka kubakia freshi, (yaani asipate shida na taabu za kiu katika maisha haya na yale ya Aakhera ambapo kila mtu atakuwa akitafuta hata tone moja la maji) basi awe akifagia Misikiti; " Na yeyote yule ambaye anataka kuiona nafasi yake hapo Jannat basi atengeneze sakafu na kuweka mazulia au mikeka katika Misikiti.
185. Mlango wa saba " Moyo halisi unapatikana kwa mema manne: " Kuwatembelea wagonjwa, " kutembea nyuma ya jeneza, " kununua sanda kwa ajili ya maiti na " kulipa madeni.
186. Mlango wa nane " Yeyote yule anayetaka kuingia katika milango hii basi lazima awe na sifa nne zifuatazo: " Ukarimu, " adabu njema, " moyo wa kujitolea na " kujiepusha katika kuwadhuru waja wa mungu.
187. Al Imam Muhammad al-Baqir
. ananakiliwa riwaya na Muhammad ibn Qays katika ukurasa wa 115 wa kitabu Al-Mahasin: "Siku moja Shaitani alimwona Mtume Nuh
. akisali, basi Shaitani alimwonea wivu Mtume Nuh
. na hakuweza kujizuia, akasema. "Ewe Nuh! Allah swt aliyetukuka, Mkuu, amejenga mwenyewe Bustani ya Eden , akapanda miti na kutiririsha mito ndani mwake. Na kisha akaangalia mandhari hayo na kusema, "Kwa hakika waumini na waongofu ndio washindi! La, Kwa Utukufu wangu! Mtu mwenye utovu wa adabu (mwenye madhambi) kamwe hataingia kuishi humu."
188. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alisema, "Mitume yote imekatazwa kuingia Jannat kabla yangu, na mataifa yote yamekatazwa kuingia humo kabla ya waumini watufuatao sisi, sisi Ahlul Bayt
., kuingia ndani mwake."
189. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amenakiliwa akisema:, akisema, "Jannat inayo milango sabini na moja ya kuingilia: Ahlul Bayt
. yangu na wafuasi wao wataingilia milango sabini, wakati ambapo watu wengine wataingilia mlango uliobakia."
TAQWA
227. Qur'ani Tukufu , Sura al-Maryam ,19 , Ayah 63: Hiyo ndiyo Jannat tutayowarithisha katika waja wetu walio kuwa wachamungu.
190. Vile vile twaambiwa katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Hujurat , 49, Ayah 13 : Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa na mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Allah swt ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi
191. Allah swt anatuambia:
فَأَثَابَهُمُ اللَّـهُ بِمَا قَالُوا جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٥﴾
Basi Allah swt atawalipa, kwa yale waliyoyasema, Bustani zipitazo mito katika yake; humo watadumu. Na haya ndiyo malipo ya wafanyao wema
. (Qur'ani, 5: 85).
192. Allah swt anasema:Hakika Allah swt amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Jannat. Wanapigana katika Njia ya Allah swt - wanauwa na wanauawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'an. Na nani atimizae ahadi kuliko Allah swt? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.(
Qur'ani, 9: 111).
193. Allah swt anasema:Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt Mlezi, na akijizuilia nafsi yake na matamanio, Basi huyo, Jannat itakuwa ndiyo makaazi yake
! (Qur'ani,79: 40 – 41).
194. Allah swt atuambia:Na wa mbele watakuwa mbele. Hao ndio watakao karibishwa Katika Bustani zenye neema
. (Qur'ani,56: 10-13).
195. Qur'ani Tukufu , Sura al-Dahar, 76, Ayah 12:Na atawajaza Bustani za Jannat na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri
.
196. Allah swt anatuambia: Hao ndio watu wa Jannat, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.(Wakiwaambia) Assalamu 'Alaikum! amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.( Qur'ani, 13: 24)
197. Allah swt anatuambia: Na anayemtii Allah swt na Mtume wake, Yeye atamtia katika Jannat zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.( Qur'ani, 4:13).
198. Allah swt anatuambia: Wala hamlipwi ila hayo hayo mliyokuwa mkiyafanya. Isipokuwa waja wa Allah swt walio khitariwa. Hao ndio watakaopata riziki maalumu, Matunda, nao watahishimiwa. ( Qur'ani, 3, 39 – 43).
199. Allah swt anatuambia: Allah swt atasema:Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Allah swt amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa
. (Qur'ani, 5: 119).
200. Allah swt anatuambia:Na atakayemjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya juu. Bustani za milele zipitazo mito kati yake,wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa
. (Qur'ani, 20: 75- 76).
201. Allah swt anatuambia:Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Jannat ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyowekwa tayari kwa wachamungu, Ambao hutoa wanapokuwa na wasaa na wanapokuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Allah swt huwapenda wafanyao wema; Na ambao pindiwafanyapo uchafu au wakijidhulumu nafsi zao humkumbuka Allah swt na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anayefuta dhambi isipokuwa Allah swt ? - na wala hawapendelei na waliyo yafanya na hali wanajua. Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao
.( Qur'ani, 3: 133-136).
202. Allah swt anatuambia:Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Allah swt atapata Jannat (Bustani) mbili
. (Qur'ani, 55: 46).
203. Al-Imam Ja'afar as-Sadiq
. amesema katika Majma'ul Bayan: "Mtu yeyote ambaye anajua na kutambua wazi kuwa mimi nifanyapo jema au baya, basi Allah swt yupo anashuhudia matendo yangu haya, basi mtu kama huyu daima atakachokuwa akikifanya basi atakuwa mwangalifu mno katika matendo yake na atajiambia kuwa lau nitafanya kazi hii njema basi Allah swt atalipa mema kadha na kadha na lau nitafanya maasi na madhambi, basi Allah swt ataniandikia adhabu kadha wa kadha. Kwa hivyo watu kama hawa wamewekewa Bustani mbili katika Jannat."
204. Qur'ani Tukufu , Sura al-Mujadilah, 58, Ayah 21: Allah swt ameandika : Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Allah swt ni Mwenye nguvu, mwenye kushinda. Tawallah maana yake ni kuwa rafiki wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
na Ahl al-Bayt
. na Tabarrah inamaana ya kujiepusha na kujiweka mbali na kutokuwa na uhusiano wowote pamoja na wale maadui wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
pamoja Ahl al-Bayt
.
205. Allah swt anatuambia: Isipokuwa wanaosali, Ambao wanadumisha Sala zao, Na ambao katika mali yao iko haki maalumu Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba; Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo Na ambao anahifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - Lakini wanaotaka kinyume ya haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka. Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, Na ambao wanazihifadhi sala zao. Hao ndio watakao hishimiwa Jannat. (Qur'ani, 70: 22 -34).
206. Al Imam Ja'afer as-Sadiq
. amesema, katika Al-Kafi: "Katika mlango wa Jannat kumeandikwa 'Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaka na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni." Sifa nne za watu wa Jannat 207. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Yeyote yule atakayekuwa na sifa nne basi Allah swt ataliandika jina lake miongoni mwa watu wa Jannat : " Mtu ambaye mwepesi kwa kutoa shahada kuwa hakuna mungu mwingine isipokuwa Allah swt tu na Mimi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ni Mtume wa Allah swt. " Mtu ambaye anasema: Alhamdu lillaah pale apatapo neema " Mtu yule asemayeAstaghfirullah pale atendapo dhambi " Na yule asemaye Inna lillaahi wa inna ilayhi rajiun pale apatapo msiba.
208. Al Imam Ja'afer as-Sadiq
. amesema: "Mumin masikini na mafukara ndio watakaokuwa wa kwanza kuingia Jannat kwa miaka arobaini kabla ya Mumin matajiri kuingia Jannat. (Nitawapeni mfano. Ni sawa na meli mbili zinazopita katika vituo vya ukaguzi wa maofisa wa forodha. Naye baada ya ukaguzi anaona kuwa meli moja haina chochote, ipo tupu, hivyo ataiachilia ipite na kuendelea na safari yake. Na pale anapoikagua meli ya pili, anakuta kuwa imejaa shehena na hivyo huisimamisha na kuanza uchambuzi na ukaguzi.)
208. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
aliulizwa kuhusu Ayah ya Qur'an Tukufu: Surah al-Waqiah, 56, Ayah ya 10, 11, 12 Na wa mbele watakuwa mbele Hao ndio watakao karibishwa Katika Bustani zenye neema
209. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
akasema: "Jibrail
. kaniambia: 'Inamaanisha Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. na Mashi'ah. Wao ndio watakao kuwa wa kwanza kabisa kukaribia Jannat, wakiwa wamemkurubia Allah swt, Aliye Mkuu, kwa heshima mahususi waliyojaaliwa."
210. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amesema: "Je itakuwaje pale ambapo wewe utakuwa umesimama mbele ya Jahannam, na Daraja (Siraat) litakapowekwa, na watu watakapoambiwa: 'Vukeni Daraja ( Siraat ) hili.'
Na wewe utauambia moto wa Jahannam ' Huyu ni kwa ajili yangu, na huyu ni ka ajili yako !' Hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. alijibu: "Ewe Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
, je ni nani hao watakaokuwa pamoja nami ?" Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
akamjibu: "Hao ni Mashi'ah wako, watakuwa pamoja nawe popote pale uwapo." Amepokewa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
akisema: "Haki ipo pamoja na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. yupo pamoja na haki."