7
HADITH ZA MTUME (s.a.w.w)NA MA-IMAMU (a.s)
JAHANNAM
211. Al Imam Ja'afer as-Sadiq
. kuhusu adhabu katika daraja la tatu la Jahannam (iitwayo Saqar) ni kama ifuatavyo: "Humo yako Mateso makali mno, inapopumua wakazi wake huungua kuwa majivu kwa kutokana na joto lake, lakini hawatakufa. Nyama yao itaunganikana tena Humo pia kuna kisima kiitwacho Saqar ambayo ni kwa ajili ya wale wajivunao, wakandamizaji na wadhalimu, na walioasi na ambapo mateso yatakuwa makubwa zaidi. Iwapo hii ndiyo itakuwa hali ya daraja la nne la Jahannam sasa hebu fikiria hali itakayokuwa katika daraja la tano, sita na saba. Tumwombe Allah swt atuepushe na Jahannam! Amin
.
212. Al Imam Musa al-Kadhim
. amesema: "Muelewe waziwazi kuwa hakuna atakayeishi katika Jahannam kwa milele isipokuwa kafiri, Munafiki na watendao madhambi na uasi. Ama kwa watu wataomaliza kutimiza kipindi cha adhabu zao, watatolewa huru kutoka Jahannam
."
213. Qur'an Tukufu Surah ya Al-Balad, 90, Ayah ya 19-20 zisemazo:Lakini waliokanusha Aya Zetu, hao ndio watu wa upande wa shari. Moto uliofungiwa (kila upande) utakuwa juu yao
.
214. Qur'ani Tukufu Surah al-Humazah, 104, Ayah 5 - 9:Hasha! Bila shaka atavurumizwa katika (Moto unaoitwa) Hutama. Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini ( Huo Moto unaoitwa ) Hutama? Ni Moto wa Allah swt uliowashwa (kwa ukali barabara). Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo (Moto) watafungiwa (wewemo ndani yake ). Kwa magogo marefu marefu.
215. Qur'ani Tukufu Surah al-Mursalat, 77: Ayah ya 32: "Hakika (Moto huo) hutoa macheche yaliyo kama majumba
."
MILANGO YA JAHANNAM
216. Mlango wa kwanza "Yeyote yule atakayekuwa na matumaini katika Allah swt basi daima atakuwa mtu mwenye furaha na mafanikio; "Yeyote anayekuwa na khofu ya Allah swt basi anajaaliwa usalama; " mtu mwovu na aliyepotoka na mstahiki wa adhabu za Allah swt ni yule ambaye hana matumaini yoyote kwa Allah swt na wala hana khofu ya aina yoyote ile ya Allah swt.
217. Mlango wa pili "Yeyote yule asiyetaka kufanywa uchi Siku ya Qiyama, basi awavalishe nguo wale walio uchi humu duniani, " Yeyote yule asiyetaka kupatwa na kiu Siku ya Qiyamah, basi awanywishe wale wenye kiu humu duniani, "Yeyote yule asiyetaka kupatwa na njaa Siku ya Qiyamah, basi awalishe wale wenye njaa humu duniani
.
218. Mlango wa tatu "Allah swt huwalaani wale wasemao uongo" Allah swt huwalaani wale walio mabakhili, "Allah swt huwalaani wale wanaowanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge.
219. Mlango wa nne " Allah swt humdhalilisha yule ambaye anaidharau Dini ya Islam, " Allah swt humdhalilisha yule anayewakashifu Ahl ul-Bayt
. ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
"Allah swt humdhalilisha yule ambaye anawasaidia wadhalimu katika kuwadhulumu watu.
220. Mlango wa tano "Msiendekeze matamanio yenu, kwani matamanio yanapingana na tendo la kusadikisha; "Musiyaongelee zaidi yale yasiyowahusu kwani mtaondoka katika Baraka za Allah swt; "Na kamwe msiwe wasaidizi wa madhalimu.
221. Mlango wa sita " Mimi nimeharamishiwa kukubalia Mujtahid (hawa ni wale ambao wamefikia upeo wa Ijtihad, uwezo wa kutoa fatwa. Rejea vitabu vya Fiqh ndipo utakapoweza kupata ilimu zaidi katika somo hili). " Mimi nimeharamishiwa kukubalia wale wanaofunga saumu.
222. Mlango wa saba "Ujihisabie mwenyewe matendo yako kabla hujafanyiwa hisabu ya matendo yako; "Uikaripie nafsi yako kabla wewe hujakaripiwa; "Na mwabudu, Allah swt aliye Mkuu na aliyetukuka, kabla ya wewe hujafika mbele yake na ambapo hautaweza tena kumwabudu na kumtukuza.
223. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amenakiliwa katika uk.145, J.1 ya al-Zamakhshari's Rabee' al-Abrar akiwa amemwuliza Malaika Jibrail
., "Je ni kwa nini mimi kamwe sijamwona Malaika Mikaili
. akicheka au kutabasamu?" Malaika Jibraili
. alimjibu: "Mikaili kamwe hakucheka wala kutabasamu kuanzia pale Jahannam ilipoumbwa."
224. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amesema: "Katika safari yangu ya usiku wa ('Israa), mimi nilisikia sauti kubwa mno, hivyo nilimwuliza Malaika Jibrail
., 'Je sauti hii kubwa ni ya nini, Ewe Jibraili ?' Naye alinijibu, 'Ni jiwe lililotupwa kutokea juu kuangukia ndani mwa Jahannam , na imekuwa ikianguka kwa muda wa vipindi sabini vya baridi, na sasa ndipo ilipofika chini."
225. Abu 'Asim 'Ubayd ibn 'Umayr ibn Qatadah al-Laythi, Hakimu wa Makkah (aliyeariki 68 A.H.), amesema, "Jahannam hupumua mara moja kwa sababu yake Malaika na Mitume
. yote hutetemeka, kiasi kwamba hata Mtume Ibrahim
. hupiga magoti na kusema, "Ewe Mola wangu! Nakuomba uniokoe!
"
226. Abu Sa'eed al-Khudri amenakiliwa akisema, "Iwapo milima itapigwa kwa rungu mara moja inayotumiwa na Malaika wa Jahannam , basi itavunjika vipande vipande na kuwa vumbi
."
227. Tawoos ibn Keesan al-Khawlani amenakiliwa akisema, "Wakati Jahannam ilipoumbwa, Malaika walishtushwa mno, na wakati nyie wanaadamu mulipoumbwa, basi walitulia
."
228. Al-Hasan ibn Yasar al-Basir amesema, "Kwa kiapo cha Allah swt! Hakuna hata mja mmoja wa Allah swt anayeweza kustahimili joto la Jahannam! Tumeambiwa iwapo mtu atasimama Mashariki na Jahannam ikawa upande wa magharibi na ikafunuliwa kidogo tu, basi bongo ya mtu huyo aliye Mashariki itachemka. Iwapo kama kiasi cha ndoo moja ya usaha wa Jahannam ukimwagwa juu ya ardhi hii ya dunia, basi hakuna hata kiumbe kimoja kingalibakia hai."
229. Abu Zar al-Ghaffari, Allah swt amwie radhi, alikuwa akisema, "Waambieni wale ambao hupenda kulimbikiza utajiri wao kuwa watachomwa nayo juu ya paji la uso wao, pembeni mwao, na migongoni mwao hadi watakapokuwa wamejaa kwa mioto
."
230. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amesema, kama vile tuambiwavyo, "Hakuna Mja wa Allah swt mwenye utajiri au mali na hataki kulipa Zaka isipokuwa kwamba atachomwa kwa vipande hivyo vya mapesa vitakavyokuwa vimepashwa moto katika moto wa Jahannam na kwamba watatumbukizwa katika adhabu hizo kuanzia juu ya vipaji vyao vya nyuso zao na migongo yao hadi pale Allah swt atakapokuwa amemaliza kupokea mahisabu na adhabu za waja wake Siku ya Qiyamah, muda ambao ni wa maelfu ya miaka kwa mujibu wa mahisabu yetu. Hapo ndipo watakapotumwa ama kuingia Jannat au Jahannam
."
231. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amesema : "Italetwa mbele yake, naye atachukizwa nayo; na itakapoletwa karibu yake, itauchoma uso wake na kifuvu kitadondoka. Iwapo ataweza kunywa hata kidogo kutokamo, basi matumbo yake yatakatika vipandevipande na kutokezea sehemu za nyuma ya kutokezea haja kubwa."
271. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
ameripotiwa akisema, "Sala za mtu anayekunywa pombe hazikubaliwi kwa siku arobaini; na iwapo atakufa huku pombe ikiwamo tumboni mwake, basi Allah swt atamlazimisha anywe sadiid, maji yatokayo kwenye sehemu za uchi wa malaya ambayo yatakusanywa katika birika huko Jahannam na kupewa watu hawa, na kwayo matumbo na ngozi zao zitachomwa
."
232. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. anavyotupatia picha ya Jahannam, tumwombe Allah swt asitutumbukize humo:'Janga kubwa kwa mtu ni kule kutumbukia katika Jahannam; yeye atajihisi kuwa anachemshwa mzimamzima, na ataona mateso yake yasiyona mwisho, na kiumbe fulani kinakoroma na kupumua, viumbe vyote vilivyo humo hukosa raha na kamwe hawapati fursa ya kupumzika, na kamwe hawatapata kupumzika kutokana na adhabu zake au mauti ya uhakika. Yeye hasinzii hata kidogo wala hakutakuwa na mapumziko katiko mateso yake: Kutakuwa na maumivu yakudumu kiasi ambacho tunamwomba Allah swt atunusuru na kutusaidia
.' (Hotuba 83).
233. 'Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa kuliko sehemu yoyote ile, mahala ambapo mikono ya wakazi wake yanakuwa yamefungwa shingoni mwao, na vichwa vyao vimefungwa na miguu yao kwa minyororo na mavazi yao yametengenezwa kwa lami. Mashati yao yametengenezwa kwa moto wakati ambapo adhabu zao za moto usiozimika kamwe hazitakwisha kamwe mahala ambapo mlango wake utakuwa umejazwa watu, katika moto mkali kabisa kiasi kwamba sauti zao zinasikitisha na kutisha, na miale ya moto ikipaa na kufikia kila sehemu na wala hakuna kujitoa kutoka humo na wala hakuna muda utakaokwisha,na wala haina mwisho wake kwa wale wanaoteketezwa na kuchomwa humo.' ( Hotuba 109 ).
234. 'Joto lake ni kali mno, kufikia chini kwake ni mbali mno, sakafu yake ni chuma, vinywaji vyake ni usaha.' (Hotuba 120 ).
235. 'Siku ya Qiyamah, madhalimu wote wataletwa bila ya kuwapo na mtu yoyote wa kuwasaidia au kuwatetea, na hivyo watatumbukizwa katika moto wa Jahannam na humo atasagwasagwa kama vile machine za kusaga zifanyavyo, hadi hapo atakapojigonga kichwa katika sakafu ya chini kabisa.' ( Hotuba 164 )
236. 'Iwapo Malik (msimamizi wa Jahannam) atakuwa mkali, husababisha sehemu yake moja kuminyana na sehemu zingine, anapogombeza, milango yake huruka juu na chini (hutema kama volkeno). (Hotuba 183 )
237. Ayah 23 ya Surah al-Fajr, 89 na katika Ayah zinginezo pia:Basi Siku hiyo italetwa Jahannam. Siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini
?
238. Qur'ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4, Ayah 140: Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnaposikia Aya za Allah swt zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano wao hao. Hakika Allah swt atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.
239. Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Surah al-Nisaa,4, Ayah 145:Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Jahannam, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru
.
240. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al-Nisaa, 4, Ayah 55 : Basi wapo miongoni mwao walioamini, na wapo walioyakataa. Na Jahannam yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza.
241. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Jinn, 72, Ayah 23:Na wenye kumuasi Allah swt na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannam wadumu humo milele
.
242. Allah swt antuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Nisaa, 4 , Ayah 115 : Na anayempinga Mtume baada ya kudhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyokuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamwingiza katika Jahannam. Na hayo ni marejeo maovu.
243. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-Kahaf, 18, Ayah 106: Hiyo Jahannam ni malipo yao kwa walivyokufuru na wakafanyia kejeli Ishara zangu na Mitume wangu.
244. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu,Sura al-'A'raf, 7, Ayah 179: Na tumeiumbia Jahannam majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika.
245. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-'A'raf, 7, Ayah 18: Akasema : Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.
246. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura az-Zumar, 39, Ayah 32:Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemsingizia uwongo Allah swt na kuikanusha kweli imfikiapo? Je! Siyo katika Jahannam makazi ya hao makafiri?
247. Na vile vile Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Sura al-A'raf,7, Ayah 36:Na wale watakaokanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hao ni watu wa Motoni; humo watadumu.
248. Allah swt anatuambia katika:
وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ ﴿١١٣﴾
Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Allah swt, wala tena hamtasaidiwa. (Qur'ani, 11: 113).
249. Allah swt anatuambia:Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui
. (Qur'ani,5: 2).
250. Allah swt anatuambia: Na walisema:
وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٢٤﴾
Hapana ila huu uhai wetu a duniani - twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipokuwa dahar. Laini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu. (Qur'ani, 45:24)
251. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. anasema:Safari ndefu lakini matayarisho ya safari ni madogo. Tukiwa watumwa wa dunia basi tutatumbukia Jahannam
.
252. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
amesema katika Mizanul Hikmah kuwa: "Mapenzi ya dunia ndiyo chanzo chote cha kila aina ya madhambi
."
253. Allah swt anatuambia:
مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا ﴿١٨﴾
Anayetaka yapitayo upesiupesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayoyataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannam; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa. (Qur'ani, 17:18).
254. Allah swt anatuambia katika:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٣٤﴾ يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ ﴿٣٥﴾
Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia Njia za Allah swt. Na wanaokusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Allah swt. Wabashirie khabari ya adhabu iliyochungu. Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahannam , na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, "Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya ) yale mliyokuwa mkikusanya." (Qur'ani, 9: 34 – 35).
(Imeelezwa katika riwaya kuwa neno lililotumika katika Ayah hii kanz inamaanisha mali yoyote ile ambamo zaka haijatolewa).
255. Allah swt anatuambia:Enyi Mlioamini! Mkikutana na waliokufuru vitani msiwageuzie mgongo. Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo - isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Allah swt Na pahala pake ni Jahannam, na huo ni mwisho muovu
. (Qur'ani, 8: 15 – 16)
256. Allah swt anatuambia:Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika wakiwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi
. (Qur'ani, 5: 32).
257. Allah swt anatuambia:Na mwenye kumuuwa Mumiin kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam humo atadumu, na Allah swt amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa
. (Qur'ani,4:93).
258. Qur'ani Tukufu, Sura al-Ali Imran, 3, Ayah 21 : Hakika wanaozikataa Ishara za Allah swt , na wakawauwa Manabii pasipo haki, na wakawauwa watu waamrishao Haki wabashirie adhabu kali.
259. Watu wa Jannat watawauliza watu wa Jahannam kile kilichowaingiza Jahannam. Nao watawajibu kuwa wao hawakuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Sura al-Muddathir,
إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ ﴿٣٩﴾ فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٤٠﴾ عَنِ الْمُجْرِمِينَ ﴿٤١﴾ مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ ﴿٤٢﴾ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ ﴿٤٣﴾ وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ ﴿٤٤﴾ وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ ﴿٤٥﴾ وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿٤٦﴾
Isipokuwa watu wa kuliani. Hao watakuwa katika mabustani, wawe wanaulizana Khabari za wakosefu: Ni nini kilichokupelekeni Motoni (Saqar)? Waseme: Hatukuwa miongoni waliokuwa wakisali. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini. Na tulikuwa tukizama pamoja na waliozama katika maovu. Na tulikuwa tukiikanusha Siku ya malipo. (Qur'ani: 74: 39 – 46).
260. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu,Surah al-Fussilat,41, Ayah 7:Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa akhera
.
301. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:
إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ﴿١٠﴾
Hakika wanaokula mali ya mayatima kwa dhuluma, hapana shaka yoyote wanakula matumoni mwao moto, na watingia Motoni. (Qur'ani, 4: 10).
302. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:
الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾
Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu. (Qur'ani, 2:275).
Allah swt huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka.
303. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ ﴿٢٨﴾ جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا وَبِئْسَ الْقَرَارُ ﴿٢٩﴾
Hebu hukuwaona wale walio badilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamizo?!. (Qur'ani, 14: 28-29).
304. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu , Surah al-Mutaffifiin,:
وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ ﴿١﴾ الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ ﴿٢﴾ وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ ﴿٣﴾ أَلَا يَظُنُّ أُولَـٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ ﴿٤﴾ لِيَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥﴾ يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾ كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ ﴿٧﴾ وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ ﴿٨﴾ كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٩﴾ وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٠﴾
Ole wao hao wapunjao! Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe. Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa Katika Siku iliyo kuu, Siku watapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. Unajua nini Sijjin? Kitabu kilichoandikwa. Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! (Qur'ani, 83: 1 – 10).
305. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:
وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾ الَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُ ﴿٢﴾ يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ أَخْلَدَهُ ﴿٣﴾ كَلَّا لَيُنبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ ﴿٤﴾ وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحُطَمَةُ ﴿٥﴾
Ole wake kila safihi, msengenyaji! Aliyekusanya mali na kuyahisabu. Anadhanim kuwa mali yake yatambakisha milele! Hasha! Atavurumishwa katika Hutama Na nani atakujuvya ni nini Hutama? Moto wa Allah swt uliowashwa. Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo utafungiwa nao Kwenye nguzo zilionyooshwa. (Qur'ani, 104: 1 – 5).
306. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu, Surah al-Mumin, 23, Ayah 43:Hapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza
.
307. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:
إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِرَبِّهِ كَفُورًا ﴿٢٧﴾
Kwa hakika wabadhirifu ni ndugu wa Masheitani. Na Shaitani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi. (Qur'ani, 17: 27).
308. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:
إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿٧٤﴾ لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ ﴿٧٥﴾
Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannam Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa. (Qur'ani, 43: 74 – 75).
309. Allah swt anatuambia katika Qur'ani Tukufu:
وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٤﴾
Na anayemuasi Allah swt na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Allah swt) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha. (Qur'ani, 4: 14).
310. Allah swt amewaamrisha Malaika kuwa: Mtu anaponuia kutenda jambo jema wamwamdikie thawabu. Na anapoanza kutembea katika kulifanya tendo jema basi hapo pia anaongezewa thawabu nyingi na pale anapolianza kutenda tendo jema basi huongezewa zaidi ya hayo na anapomaliza kulitenda tendo jema basi hapo analipwa thawabu nyingi mno zisizo na hisabu. Lakini mtu anaponuia kutenda dhambi basi hapo haandikiwi adhabu, na anajitoa kwenda kutenda dhambi napo pia haandikiwi kwa sababu inawezekana akarudia njiani na anapolianza tendo ovu pia kuna uwezekano wa kutolikamilisha na kwa masikitiko makubwa, anapolikamilisha basi kwa huruma zake Allah swt, huandikiwa dhambi moja tu.
TAWBA
311. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
katika, Al-Mahajjat-ul-Baydha: "Majonzi makubwa ya watu wa Jahannam ni kuahirisha kwao Tawba
"
312. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir
: "Yeyote yule anayefanya Tawba ni sawa na yule mtu ambaye hana mzigo wowote wa madhambi ya aina yoyote ile
."
313. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema: "Wapo waahirishaji ambao huahirisha kufanya Tawba hadi hapo mauti inapowafikia
."
314. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
alimwambia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
: "Ewe 'Ali! Amebarikiwa yule ambaye anatazwa na Allah swt wakati pale anapolia kwa ajili ya kutaka msamaha wa madhambi ambayo hakuna mwingine ajuaye illa Allah swt tu
."
.
(Baadhi ya Ahadith zinasisitiza kuwa haimpasi mtu kuwaambia watu wengine juu ya madhambi yake mwenyewe. Hivyo inambidi aungame madhambi yake kwa Allah swt tu na wala si kwa mtu mwingine.)
315. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Katika kila sehemu ya tatu ya usiku na usiku wa kuamkia Ijumaa kuanzia usiku uingiapo( hadi alfajiri) Allah swt huwauma Malaika mbinguni ili kuita: 'Je yupo mwenye kuomba ili nimtimizie ombi lake?' Je yupo yeyote mwenye kufanya tawba ili nimrejee? Je yupo aombaye msamaha ili nimsamehe
?"
.
Tanbihi
: Katika utamaduni wa Kiislamu, tunafundishwa kuwa kulala katika usiku wa kuamkia Ijumaa kunaitwa usingizi wa masikitiko; kwa sababu Siku ya Qiyama watu watakuwa wakisikitika mno kwa kulala usiku hizo.
316. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq
: "Fungeni milango ya madhambi kwa kumwomba Allah swt, na mufungue milango ya utiifuu kwa kusema: Bismillah Rahmaan Rahiim
."
KULINDA HESHIMA YA WAUMINI
317. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir
: "Ni faradhi kwa kila Mwislamu kusitiri na kuzificha aibu sabini (70) za Mwislamu mwenzake (ili kulinda heshima yake)
."
(Makosa na kasoro zake zote zishughulikiwe kibinafsi na wala zisienezwe na kutangazwa kwa watu wengine).
318. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema: "Kubali msamaha akuombao Nduguyo Mwislamu na kama hakufanya hivyo, jaribu kumvumbulia hivyo
."
319. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema: "Hali mbaya kabisa ya uhaini ni kutoboa habari zilizo siri
."
.
320. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema: "Kumuonya kwako aliyetenda makosa miongoni mwa au mbele ya watu ni kumdhalilisha
." (Inakubidi uongee naye katika faragha)."
321. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq
: "Katika matendo yote aypendayo Allah swt, ni kule kumletea furaha Mwislamu kwa mfano: kumshibisha, kumwondolea majonzi yake, au kumlipia madeni yake
."
MATENDO MEMA
322. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Kwa kufanya usuluhisho na amani miongoni mwa watu wawili (kwa kulinganisha) ni borai kuliko ibada za sala na saumu zake mwenyewe
."
323. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema: "Iwapo mtu atakufikia wewe kwa mema, basi inakubidi uhakikishe kuwa fikira zake zinabakia kweli
."
.
324. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Yeyote yule awaongozaye watu kwa taqwa (atalipwa) sawa na yale ayatendayo (aliyeongozwa) hayo matendo mema.
."
325. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq
: "Yapo matendo sita ambayo Mwislamu Momiin anaweza kufaidika nayo hata baada ya kufariki kwake: " Kumwacha nyuma mtoto atakaye mwombea maghfira, " Kuacha Mus.-hafu sharifu ambao watu watakuwa wakisoma, " Kuchimba kisima cha maji kitakachokuwa kikiwafaidisha watu, "Mti alioupanda yeye, "Sadaka aliiyoitoa katika kusababisha maji yakatirika vyema, "Ahadith na Sunnah nzuri atakazokuwa ameacha nyuma yake na zikifuatwa na watu.
326. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Iwapo isingalikuwa vigumu kwa Ummah wangu basi ningalikuwa nimewaamrisha kupiga miswaki kwa kila Sala
."
DHULUMA NA UONEVU
327. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Siku ya Qiyama, mwitaji ataita:' Je wako wapi wadhalimu na wasaidizi wao na wale wote waliowatengenezea wino au waliowatengenezea na kuwakazia mifuko yao au waliowapatia wino kwa ajili ya kalamu zao? Kwa hivyo, wakusanye watu wote hawa pamoja nao!
"
.
328. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema: "Kwa kiapo cha Allah swt, Iwapo nitapewa umiliki wa nchi sana pamoja na yale yote yaliyomo chini ya mbingu zilizo waz ili nimuasi Allah swt kwa kiasi cha mimi kunyofoa punje moja ya shairi kutoka kwa sisimizi, basi mimi kamwe sitafanya hivyo
."
329. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baqir
: "Zipo aina tatu za dhuluma: moja, ni ile ambayo Allah swt anasamehe, pili, ile ambayo Allah swt haisamehe, na tatu ni ile ambayo Allah swt haipuuzii. Hivyo, dhuluma ambayo Allah swt haisamehe ni ukafiri dhidi ya Allah swt. Na dhambi ambalo Allah swt anaisamehe ni kile mtu anachojifanyia dhidi yake mwenyewe na Allah swt. Lakini dhambi ambalo Allah swt haipuuzii ni ile ambayo inavunja haki za watu
."
Ufafanuzi
: Aina ya tatu ya dhuluma ni ile ambayo mtu hukiuka na kuvunja haki za watu. Njia saheli ya kutaka kusamehewa ni kwanza kumridhisha yule ambaye haki zake zimekiukwa na kuvunjwa. Iwapo mtu huyo atamsamehe yule aliyemvunjia haki zake, basi hapo dhuluma hiyo itageuka kuwa dhuluma dhidi yake binafsi. Na hapo ndipo ataweza kuwa mstahiki wa kuomba msamaha wa Allah swt.
330. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. Amesema: "Dhuluma husababisha miguu kupotoka, inaondoa baraka na kuangamiza umma au taifa
."
331. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. Amesema: "Hakuna kitu kinachovutia na kuharakisha kuondolewa kwa neema za Allah swt spokuwa kuendekea kwa dhuluma, kwa sababu Allah swt anazisikiliza dua za madhulumu na huwa yuko tahadhari pamoja na madhalimu."
HAKI ZA WAISLAMU WENZAKO
332. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Yeyote yule anayemhuzunisha Mwislamu mwenzake basi kamwe hawezi kumfidia hata kama atamlipa dunia nzima kwani haitatosha (ispokuwa iwapo atatubu na kumfurahisha Mwislamu huyo)
."
333. Al-Imam Musa al-Kadhim
. Amesema: "Moja ya faradhi miongoni mwenu kuelekea Mwislamu mwenzenu ni kutokumficha kitu chochote ambacho kinaweza kumfaidisha humu duniani au Aakhera
."
334. Al-Imam Al-Hassan Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. Amesema: "Watendee watu vile utakavyopenda wewe kutendewa
."
335. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
.Amesema: "Alla swt humrehemu mtu ambaye anahuisha yaliyo haki na kuangamiza na kuteketeza yale yaliyo batili, au hukanusha dhuluma na kuimarisha uadilifu
."
336. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq
: "Tabia hizi nne ni kutokea tabia za Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w): haki, ukarimu, subira na kuvumilia katika shida, na kusimamia haki ya Mumiin
."
.
337. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
Amesema: "Kwa hakika ni watu wa kawaida ndio walio nguzo za Din, nguvu ya Waislamu na hifadhi dhidi ya maadui. Hivyo mwelekeo wako daima uwe kuelekea wao na uwanynyekee
."
.
338. Amesema Al-Imam Ja'afar as-Sadiq
: "Allah swt haabudiwi zaidi ya thamani kuliko kutimiza haki ya Mumiin
."
339. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Yeyote yule anayemuudhi Mumiin, basi ameniudhi mimi
."
340. Amesema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) katika,: "Yeyote yule atakayemdhulumu Muumin mali yak pasi na hakie, basi Allah swt ataendelea kumghadhibikia na wala hatazikubalia matendo yake mema atakayokuwa akiyatenda; na hakuna hata mema moja itakayoandikwa katika hisabu zake nzuri hadi hapo yeye atakapofanya tawba na kuirudisha hiyo mali kwa mwenyewe
."
SALAAM -- KUSALIMIANA
341. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Pale munapokutana miongoni mwenu basi muwe wa kwanza kwa kutoa salaam na kukumbatiana; na munapoachana, muagane kwa kuombeana maghfirah
."
342. Al-Imam Hussein ibn Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. Amesema: "Thawabu sabini (70) ni kwa ajili ya yule ambaye anaanza kutoa salaam na thawabu moja ni kwa ajili ya yule anayeijibu hiyo salaam
."
(Wakati watu wawili wanapoonana, mtanguliaji katika kutoa salaam hupata thawabu zaidi).
343. Al Imam Ja'afer as-Sadiq
. Amesema: "Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) aliwakusanya watoto wa 'Abdul Muttalib na kuwaambia: Enyi watoto wa Abdul Muttalib! muwe waanzilishi wa salaamu, mujali Jama'a zenu, musali sala za usiku wakati watu wengine wanapokuwa wamelala, walisheni vyakula watu, na muongee maneno mazuri na hayo kwa hakika mutaingia Peponi kwa amani
."
344. Al Imam Ja'afer as-Sadiq
. Amesema: "Yeyote yule anayekuwa ni muanzilishi wa kutoa salaamu basi atakuwa ni mpenzi sana wa Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w)"
.
KUTENDA MEMA NA KUKATAZA MABAYA
345. Allah swt anatuambia katika Qur'an:
وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٤﴾
Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.(Qur’an, 3:104).
346. Amesema Mtume Mtukufu(s.a.w.w)
. "Itakapofika wakati katika umma wangu ambapo Waislam watakuwa wakitekenya wengine wafuate mema na wajizuie na mabaya, basi kwa hakika watakuwa wametangaza vita dhidi ya Allah swt
."
347. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema: "Yeyote yule anayeacha kukataza wengine wasifanye maovu kwa maneno na kwa matendo (ni tofauti na kuona maovu yakitendeka) basi huyo ni maiti inayotembea miongoni mwa walio hai
."
348. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Kumzuia Muislam asitende matendo maovu ni sawa na Allah swt kumlipa thawabu za Hija 70 zilizokubaliwa
"
349. Alisema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
: "Ambizeni miongoni mwenu kutenda mamea; basi mtakuwa miongoni mwa watendao mame. Muwazuie wengine wasitende maovu kwa maneno yenu, na mujiepushe, na uwezo wenu wote, na yeyote yule anayetenda hivyo. Mumtumikie Allah swt kama ni wajibu wenu; na angalieni kusiwepo na mulaumiaji au lawama yoyote itakayoweza kuwazuia nyie katika kutekeleza maswala ya Allah swt. Jitupeni jitumbukizeni katika hatari kwa ajili ya kunusuru ukweli popote pale itakapo hitajika
."
.
350. Al Imam Muhammad al-Baquir
. Amesema: "Kwa hakika kuwaambia watu yaliyoyakweli na kuwazuia kwa yale yaliyo potofu ndiyo sirah ya Mitume (a.s). na waja wema. Kwa hakika ni jambo moja kubwa (wajib) kutokana na hiyo mambo mengine mengi yaliyo faradhishwa yanaweza kubakia, Ummah zingigine zinawea kunusurika, maelewano ni halali, dhuluma imekatazwa, na hakikaamani itajaa juu ya ardhi hii
"
351. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
: "Uimara wa dini ni kule kuamrisha yaliyo mema na kukatza yale yaliyo maovu, na kubakia katika mipaka ya Allah swt
."
352. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
"Yeyote anayeona maovu au mabaya yanatendeka basi ayazuie kwa matendo yake, kama ana uwezo huo, bila shaka; kama hawezi kufanya hivyo, basi azuie kwa ulimi wake, na kama hawezi kufanya hivyo pia basi anaweza kulaani kimomoyo
."
.
353. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Yeyote yule katika 'Umma wangu anayechukua jukumu nakumamrisha mema na kukataza maovu na anaye jihusisha katika ucha-Allah swt,wataishi kwa raha na mustarehe na watakapo acha kufanya hivyo, basi baraka na neema za Allah swt zitaondolewa kwao
."
354. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
: "Akiwambia Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib (a.s). na Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib (a.s). wakati Ibn Muljam (Laana za Allah swt zile juu yake) alipompiga dharuba kali katika Masjid Kufa"Muogopeni Allah swt (Na akasema tena)Muogopeni Allah swt katika mambo ya Jihad, (Jitihada za vita vitakatifu), kwa misaada ya mali, maisha na mazungumzo yenu katika njia ya Allah swt
"
.
Msiache kuamrisha mema na kukataza maovu isije hawa waovuwakachukua nafasi juu yenu, na baadaye(Katika hali hiyo)mtakapo Sali basi salah zenu hazita kubaliwa
355. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
: "Kuamrisha mambo memani jambo mmoja jema kabisamiongoni mwa watu
."
356. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
: "Matendo mema yote kwa ujumla, ikiwemu Jitihada za vita vitakatifu vya Jihad katika njia ya Allah swt, kwa kulinganisha na kuamrisha mema na kukataza maubaya, ni sawa na kyasi kidogo cha mate ya kilinganishwa na bahari yenye kina kirefu
."
357. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir
: "Allah swt alimteremshia Wahyi Mtume Shua'ib
"Mimi nitawaadhibu watu wako kiasi cha laki moja na kati yao arobaini elfu ni waovu na elfu sitini ni katika watendao wema." Mtume Shua'ib
aliulizia hawa waovu wanastahili adhaabu lakini hawa watendao wema je akasema kwa hayo Allah swt alimterenshia wahi tena" Wao (walio wema)wamehusiana na watendao dhambi na hawa kuwa wakali hawa kughadhabishwa kwasabasbuadhabu na khofu zangu.
358. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
: "Wambieni wenzenu wa tende wemana wajizui na ubaya kwani hamutambui kuwa kwakuamrisha mema kamwe haikaribishi mauti wala kukatisha riziki
.
359. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq
: "Ole wale watu ambao hawaisaidi Dini ya Allah swt kwa kuamrisha mema na kwa kutaza maovu
.