8
HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU (a.s)
ULIMI NA MAOVU YAKE
360. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Matokeo yatokanayo na ulimi ni mabaya kabisa (yaliyo sabasishwa nayo) kuliko dharuba ya upanga mkali
.
361. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Miongoni mwa mambo yote, ulimi unastahilikuwekwa katika mahabusukwakipindi kirefu zaidi kuliko kitu kinginechochote
. (Kwasababu madhambi yetu mengi yana tokana nayo, kama vile kuwasuta watu, kusema uongo, kuzua mambo, kuwadhihaki wengine, na vile vile kuwa tuhumu watu wengi, n.k)
.
362. Amesema Al Imam Amiril Momineen
: "Fikirieni na mupime kabla hamja ongea ili kwamba muweze kujizuia dhidi ya (kutenda) makosa
."
363. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Maangamizo ya mtu yako katika mambo matatu "Tumbo lake, matamaniyo yake, na ulimi yake
."
.
364. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir
: "Hakuna mtu yeyote aliye salimika kutokana na ulimi wake hadi hapo yeye atakapo udhibiti ulimi wake
."
.
KUSENGENYA NA KUTAFUTA KOSA
365. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Uzushi unafanya kazi dhidi ya Imani ya Mwislamu, Mumim kwa haraka zaidi kuliko ugonjwa wa Ukoma unavyo enea mwilini
."
366. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
: "Msikilizaji wa kile kinacho sengenywa ni sawa na yeye ndiomsengenyaji
."
367. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
: "Kuacha tabia ya kusengenya ina thamani kubwa sana mbele ya Allah swt kuliko kusali sala yenye raka'h elfu kumi zilizo sunnah
.
368. Amesema 'Abdul Mu'min-il-Ansari: "Kuwa wakati moja yeye alikuwa mbele ya Imam Abil HassanMusa Ibn Jaffer
ambapo Abdillahi Jaffer alikuwa akitokezea na Abdul Mu'min alitoa tabasamu mbele yake. Na hapo Imam
alimuuliza Abdul Mu'min iwapo alimpenda Abdillahi Jaffer na alipomjibu Imam kuwa yeye hakumpenda ('Abdillah ) isipokuwa yeye alikuwa ni Imam wa saba. Hapo Imam
alimwambia yeye ni ndugu yako, ni Mu'min na Mu'min moja ni ndugu wa Mu'min mwingine hata kama wazazi wake ni watu tofauti. Hivyo amelaaniwa yule anayemtuhumu ndugu yake wakiislamu, analaaniwa yule anayemgeuka ndugu yake Mwislamu, analaaniwa yule asiyempa muongozo mwema ndugu yake Mwislamu, na analaaniwa yule ambaye anamsengenya Mwislamu mwenzake."
369. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib
. Amesema: "Mwovu miongoni mwa watu ni yule ambaye anatafuta kasoro za watu wengine wakati akiziacha kasoro zake
."
370. Al Imam Musa al-Kadhim
. Amesema: "Amelaaniwa mtu yule ambaye anawasengenya ndugu zake wengine (Waislamu wenzake)
."
UHARAMISHO WA KUSEMA UWONGO
371. Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah An-Nahl,16, Ayah ya 105,Wanaozua uwongo hawana imani
372. Vile vile Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema: "Mtu mwovu kabisa ni yule ambaye ni msema uwongo
."
373. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema: "Allah swt humlaani mwongo hata kama atasema ukweli
"
374. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema: "Jitahadharisheni, Mimi ninawaambieni dhambi Kuu kabisa katika Madhambi Makuu: " Kumshirikisha Allah pamoja na mtu mwingine "Wazazi kukufanya Aaq" Na kusema uwongo
375. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema: "Ugonjwa wa kusema uwongo ndio ugonjwa mbaya kabisa."
376. Vile vile Imam Hasan al-'Askari amesema katika Mustadrad al-Wasa'il,Kitabu Hajj, mlango wa 12: "Maovu yote yamefungwa katika chumba kimoja kwa kufuli, na uwongo ndio ufunguo wake."
377. Amesema al-Imam Musa ibn Ja'afar
: "Mtu mwenye busara kamwe hawezi kusema uwongo hata kwa matamanio yake mwenyewe."
378. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema: "Itakuwa vyema kwa Waislamu iwapo hawatafanya urafiki na udugu pamoja na Mwongo."
379. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir
. katika Al-Kafi, j.2: "Uwongo unateketeza misingi ya Imani
.".
380. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail : "Mumin anaposema uwongo bila ya shida yoyote,basi Malaika elfu sabini humlaani!" "Na hutoka harufu mbaya kabisa kutokea moyoni mwake, harufu hiyo hufika hadi 'arsh" "Na Allah swt humwandikia kwa dhambi hilo moja, madhambi sabini ya zinaa na zinaa zenyewe si zinaa za kawaida bali zinaa pamoja na mama yake ."
381. Riwaya moja inasema: 'Uwongo ni mbaya zaidi kuliko ulevi.'
382. Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah An-Nahl,16, Ayah ya 105, Wanaozua uwongo hawana imani.
383. Vile vile Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Az-Zumar ,39, Ayah ya 3, ..Bila shaka Allah hamuwongozi aliye mwongo, aliye kafiri.
384. Kwa mujibu wa Ayah za Qur'an Tukufu tunaambiwa kuwa mwongo ni mstahiki wa adhabu za Allah swt na Allah swt huwa daima ameghadhabikia. Kama vile tuonavyo katika Ayah zifuatazo : Surah Aali-Imran, 3, Ayah ya 61 '.. Tutake laana ya Allah swt iwashukie waongo.'
385. Surah An-Nuur ,24 , Ayah ya 7: ' Laana ya Allah iwe juu yake iwapo ni miongoni mwa waongo.'
386. Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Baqarah, 2, Ayah ya 197, kuwa : 'Na katika Hajj hairuhusiwi maneno machafu wala ufusuka.' Katika Ayah hii takatifu neno 'fisq' inamaanisha uwongo kwa mfano katika Qur'an Tukufu, Surah Al-Hujurat , 49, Ayah ya 6, tunaona kuwa uwongo unaitwa kuwa ni 'ufasiki'. Ayah yenyewe inasema: Enyi mlioamini! Iwapo mtaijiwa na mwongo na habari yoyote basi msikubalie tu bali mufanye upelelezi
387. Tumepewa hukumu ya kujiepusha na kuabudu masanamu na kutosema uwongo na inasemwa kuwa: 'Basi mjiepusheni na uchafu (wa mfano wa masanamu) na jiepusheni na maneno ya uwongo.' Qur'an Tukufu, Surah Al-Haj, 22, Ayah 30, Hapa qauli dhur au laghwu inamaanisha uwongo.
388. Katika riwaya dhambi linaitwa Ithm au Dhamb kwa Mfano amesema al-Imam Muhammad al-Baqir
: Uwongo yote kwa yote ni ithm na dhamb.
389. Mwongo huwa ni mustahiki wa laana na ghadhabu za Allah swt na mfano wa kauli isemwayo katika Qur'an Tukufu Surah An-Nuur, 24 , Ayah 7, isemayo: Laana ya Allah iwe juu yake iwapo ni miongoni mwa waongo.
390. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema katika Mustadrak al-Wasail kuwa "Jiepusheni na uwongo kwani uwongo huufanya uso wenu kuwa mweusi."
391. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir
. katika Usuli Kafi, Kitabul Iman wal-Kufr, mlango wa uwongo: "Bila shaka Allah swt ametengenezea kufuli kila dhambi na ufungua wa kufuli hizo ni ulevi ambapo uwongo ni mbaya hata kuliko ulevi
."
392. Iwapo ulevi unaangamiza akili na fahamu lakini uwongo si kwamba unaangamiza akili na fahamu lakini unamfanya mtu akose adabu na heshima kiasi kwamba yeye huwa tayari kwa jambo lolote la kishetani. Iwapo mlevi atakapokuwa amelewa, huwa hana uwezo wa kuiharibu jamii kwani anakuwa hana fahamu wala habari zake mwenyewe lakini mwongo akiwa katika fahamu zake timamu huweza kuiharibu na kuiteketeza jamii nzima kwa hila na uwongo wake. Na hivyo kuleta hasara kubwa sana kwa jamii nzima.
393. Zipo riwaya zisemazo kuwa Siku ya Qiyama midomo ya wasema uwongo itakuwa ikinuka harufu mbaya kabisa!.
394. Harufu mbaya iliyozungumzwa hapo juu, itakuwa mbaya kabisa kiasi kwamba hata Malaika Siku ya Qiyama watachukizwa kumkaribia huyo mwongo anayenuka harufu mbaya. Lakini si Siku ya Qiyama tu, bali hata humu duniani pia wanaisikia harufu mbaya ikitoka vinywani mwa wasema uwongo. Ipo Hadith ya Mtume Muhammad(s.a.w.w)
isemayo : "Wakati mja wa Allah swt anaposema uwongo, basi hutokwa na harufu mbaya kabisa kutoka mdomo wake kiasi kwamba hata Malaika pia wanajiweka naye mbali." (Mustadrak al-Wasail.).
395. Allah swt humlaani msema uwongo kama vile Aya ya Mubahila inavyoelezea Qur'an Tukufu, Surah An-Nuur, 24, Ayah ya 7 kama ilivyokwishaelezwa kuwa inadhihirisha waziwazi. ' Laana ya Allah iwe juu yake iwapo ni miongoni mwa waongo.'
396. Imepokelewa riwaya kuwa harufu mbaya inayotoka midomo ya mwongo huifikia mbingu.
397. Imepokelewa riwaya kuwa Malaika walio karibu ya Allah swt pia humlaani msema uwongo.
398. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir
. katika Al-Kafi: "Uwongo ni kiangamizacho Imani."
399. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Al-Kafi: "Mtu yeyote hataweza kuionja imani hadi hapo atakapoiacha uwongo, ama uwongo huo uwe wa kikweli au kimzaha." ndivyo inavyopatikana kwa mujibu wa riwaya. 400. Ipo katika Hadith moja ya Mtume Muhammad(s.a.w.w)
isemayo: "Kwa mtazamo wa heshima na kiadabu, mtu aliye chini kabisa ni yule msema uwongo
."
401. Imeripotiwa kuwa uwongo ni ufunguo wa kufuli ambayo imepigwa katika nyumba iliyofungwiwa maovu yote.
402. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema katika Mustadrak al-Wasail kuwa : "Jiepusheni na uwongo kwani hiyo ni mojawapo ya aina za ufiski, na vyote hivi viwili ni vitu vya Jahannam
."
403. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail kuwa: "Zipo alama tatu za mnafiki : kusema uwongo, kufanya khiana na kugeuka ahadi alizozitoa
."
404. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail: "Ushauri wa mwongo hauna umuhimu wowote
."
405. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail: "Na ugonjwa wa uwongo, ni ugonjwa mbaya kabisa wa kiroho
."
406. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema: "Bila shaka Ibilisi hujipaka wanja, huvaa uchawi vidoleni na hutumia vyombo vya kuvutia hewa puani. Ama wanja wake kufanya ni visingizio na uvivu, ama uchawi wake vidoleni ni uwongo na chombo cha kuvutia puani ni takabari na ghururi
!"
407. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail: "Mapato maovu kabisa ya mwanadamu, ni uwongo
."
408. Imeripotiwa katika Al-Mustadrak al-Wasail kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w)
alijiwa na mtu mmoja aliyeuliza: "Ewe Mtume Muhammad (s.a.w.w) Je ni matendo yapi hasa yanawafanya watu waingine Motoni (Jahannam)
?"
409. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
alimjibu: "Uwongo! Iwapo mtu atasema uwongo, basi atakuwa amejiingiza katika dhambi la uasherati, na hivyo amekufuru, na anayekufuru ataingia Motoni (Jahannam)."
410. Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique
. katika Wasa'il al-Shiah: "Kwa hakika mtu ambaye anapindukia kusema uwongo huadhibiwa adhabu ya kumuasi Allah swt ambavyo mojawapo ni ugonjwa wa usahaulivu!" Na hivyo ndivyo ilivyo kuwa mtu husema uwongo na mara husahau kama yeye alikuwa amesema uwongo na hatimaye uwongo wake hukamatwa na hivyo kudhalilika, na katika kujaribu kujitetea na kujihifadhi inambidi azungumze uwongo mmoja baada ya mwingine na hivyo huingia katika machachari ya kutaka kuilinda uwongo wa kwanza. Lakini hatambui kuwa kila asemavyo uwongo mmoja baada ya mwingine, anaendelea kujidhalilisha tu."
B Yaani mara nyingi tunajaribu kuinusuru uwongo mmoja kwa uwongo hata mia, bila hata ya kuona aibu, na hii ndiyo laana ya Allah swt kwa msema uwongo. Hapa roho na akili yake vinamkataza, lakini wasiwasi wa Shaitani unamburuta tu katika kusema uwongo baada ya uwongo kwani yeye anakuwa yu mfungwa wa Shaitani.
411. Msema uwongo huadhibiwa kwa adhabu mahususi. Mheshimiwa Rawandi katika kitabu chake Da'awat anaandika Hadith moja ndefu ya Mtume Muhammad(s.a.w.w)
katika maudhui haya ambayo inazungumzia vile alivyokuwa akisimulia Mtume Muhammad(s.a.w.w)
kile alichokiona katika Me'raj, kuwa: "Nilimkuta mtu mmoja amelazwa juu ya tumbo lake na yupo mtu mwingine ambaye amesimama juu ya kichwa chake na ambaye anayo nyundo ya misumariambayo anakaa akimpiga yule mtu aliyelazwa na kumjeruhi. Uso wake unajeruhiwa kiasi cha kubomokabomoka kabisa katika vipande vipande! Nyundo inapoinuliwa juu mtu huyo huwa salama na punde inapoteremka chini hujeruhiwa hivyo hivyo na hivyo ilivyo adhabu zake." Kwa hayo Mtume Muhammad(s.a.w.w)
anasema kuwa: "Mimi niliuliza ni sababu gani ya kuadhibiwa hivi?" Alijibiwa: "Huyu ni yule mtu ambaye alipokuwa akitoka nyumbani kwake, alikuwa akisema uwongo kiasi kwamba watu wa duniani walikuwa wakipata hasara kubwa kutoka na uwongo wake. Basi adhabu hii atabakia nayo hadi Qiyama."
412. Mwongo hukosa sala za usiku wa manane (salatul Layl) na baraka zote zipatikanazo kwa sala hii huzikosa na baraka mojawapo ya sala hii ni kupatikana na kuongezeka kwa riziki. Bwana Sharif, anamnakili Al-Imam Ja'afar as- Sadique
. akiwa amesema, katika Bihar al- Anwar: "Mtu anaposema uwongo hukosa baraka ya kusali sala za usiku wa manane na kama atakosa baraka za sala hiyo basi na baraka za riziki pia hukosekana!"
413. Allah swt Anasema:Bila shaka Allah hamuwongozi aliye mwongo, aliye kafiri
. (Qur'an, 39: 3).
414. Mtume 'Isa ibn Maryam
. amesema, katika Al-Kafi: "Mtu ambaye anakithiri kwa uwongo basi ubanadamu wake humwondokea. Na kwa hayo huwa ana uhusiano na watu kwani na watu wenyewe huwa hawana moyo nae
."
415. Uwongo ni ukhabithi na uchafu mkubwa.
416. Uwongo upo mbali na imani bali tuseme kuwa ni kinyume ya imani.
417. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema, katika Al-Mustadrak al-Wasail: "Kila kutakavyozidi kusemwa kwa uwongo, basi ndivyo vivyo hivyo imani ya mtu itakwenda ikipungua
!"
418. Mwongo ndiye mwenye madhambi mengi kuliko wote.
419. Katika Al-Mustadrak al-Wasail ipo Hadith ya Mtume Muhammad(s.a.w.w)
inayosema: "Mojawapo ya dhambi kuu niya mtu mwenye mazungumzo na uwongo wa mtu kupindukia kiasi
."
420. Mwongo hujiteketeza kwa uwongo wake
421. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail "Jiepusheni na uwongo hata kama mtaona ufanisi ndani yake, lakini kwa hakika huo si ufanisi bali ni maangamizo ndani yake
."
422. Mwongo hastahiki kuwa ndugu na rafiki wa watu
423. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Wasa'il al-Shiah:
"Inambidi kila Mwislamu asiufanye uhusiano na kiudugu na urafiki pamoja na msema uwongo aliyekithiri
!"
424. Akaendelea Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. kusema: "Kwani rafiki wake mwongo pia huchukuliwa kuwa ni mwongo! Kiasi kwamba hata kama atasema ukweli wowote, ukweli huo hautasadikiwa kuwa ni ukweli
."
425. Allah swt hawaongozi wafujaji na waongo
426. Allah swt anatuambia kuwa:'Kwa hakika Allah hamwongozi yule ambaye amepindukia mipaka na mwongo
.' (Qur'an, 40:28).
Hivyo inamaanisha kuwa msema uwongo na mfujaji huwa wako mbali na haki na uhakika.
427. Mwongo huonekana kuwa ni binadamu, lakini sivyo
428. Ipo riwaya katika kitabu kiitwacho 'Uyunil Akhbar ar-Ridhaa
: "Kwa hakika mwongo huonekana kuwa ni binadamu lakini katika hali ya Barzakh hana uso wa kibinadamu. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema akiwa anamwelezea Bi.Fatimah az-Zahra
. tukio la Mi'raj,: "Usiku wa Mi'raj mimi nilimwona mwanamke mmoja ambaye kichwa chake kilikuwa kikifanana na kichwa cha nguruwe na mwili mzima uliobakia ulikuwa kama wa punda. Sababu ya hayo ni kuwa yeye alikuwa na tabia ya fitina na alikuwa akisema uwongo."
429. Allah swt anatuambia:Na msiseme kwa sababu ya uwongo usemao midomo yenu, hili ni halali na hili ni haramu ili msije mkamzulia uwongo Allah. Hakika wale wanaomzulia uwongo Allah , hawatafanikiwa
. (Qur'an,16: 116 na 117).
430. '(Duniani) Kuna faida kidogo tu lakini (Aakhera) watapata adhabu kali ziumizazo.'
431. Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique
. katika Al-Kafi: "Msituzulie hata uwongo mmoja kwani kama hivi uwongo utakutoweni nje ya Dini bora kama ya Islam." Yaani kwa kuwazulia Maimamu
. uwongo hata moja kunatokomeza Nuru ya Imani kutoka moyoni mwa waongo. Iwapo uwongo kama huu utazuliwa kwa Maimamu
. katika hali ya saumu, basi saumu inabatilika papo hapo.
432. Ni jambo la kawaida kwetu sisi kusema: "Allah swt yupo shahidi kuwa kile nikisemacho ni sahihi au Allah swt anajua kuwa kile nikisemacho ni kweli mtupu."
433. Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique
. katika Al-Kafi: " 'Mtu yeyote atakayesema kuwa Allah swt anajua' wakati Allah swt anajua asili (yaani kinyume na achojidai huyo mtu kwa kutenda kinyume) basi 'arsh-i-Ilahi inatetemeka kwa kuona Ukuu wa Allah swt."
434. Vile vile Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique
. katika Wasa'il al-Shiah ,Kitabul Iman, mlango na.5: "Iwapo mtu atasema kuwa 'Allah swt anajua wakati kwamba ni mwongo' basi Allah swt anamwambia 'je ewe haukumpata mwingine wa kumdanganya isipokuwa mimi tu? Ambaye unamzulia uwongo ?"
435. Kwa mujibu wa riwaya zinginezo, inasema kuwa wakati mtu anapomfanya shahidi Allah swt katika uwongo anaouzua, basi Allah swt humwambia: "Je haujampata mdhaifu mwingine yeyote kuwa shahidi wako katika uwongo na uzushi wako huo isipokuwa umenipata mimi tu ?"
436. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir
. katika Kashaful Hujjat: "Kamwe musinakili Ahadith kutoka mtu ambaye hategemewi kuwa sahihi amasivyo wewe utakuwa umesema uwongo mkubwa kabisa.na mwongo ni mtu aliyedhalilika mbele ya Allah swt na viumbe vyake."
437. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Nahjul- Balagha, alimpa nasiha Harith Hamdani kwa barua aliyokuwa amemwandikia: "Usiwe ukiwaambia watu yale yote uliyoyasikia, kwani kunatosheleza katika kusema uwongo."
438. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema, katika Wasa'il al-Shiah: "Mtu yeyote atakachoninasabia kile ambacho sijakisema, basi makao yake yatakuwa ni Jahannam (Motoni) tu
."
438. Bwana Nuuri katika kitabu chake Darus-Salaam anaandika kuwa bwana mmoja aliyeelimika na mwenye matendo, kwa ajili ya kukisanifu kitabu maqame' alimwendea Bwana Muhammad 'Ali huko Karmanshah na kusema : "Mimi nimeota usingizini kuwa ninaiparua nyama ya al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib
., sasa je nini utabiri wa ndoto hii ?"
439. Bwana Muhammad 'Ali aliinamisha kichwa chake na kufikiria, baada ya punde akasema: "Bila shaka wewe ni khatibu wa kusoma Majlis na kusoma masaibu." Huyo Bwana akajibu: "Naam!" Akamwambia: "Ama shughuli hii uiache au usome kwa kutoa maudhui yako kutokea vitabu vinavyoaminiwa na kutegemewa kwa usahihi." Imeandikwa katika kitabu Shifaus-Suduur kuwa siku moja Shekhe mmoja alikuwa akisoma waadhi mbele ya Ayatullah al-Haj Muhammad Ibrahim Kalbasi. Sheikh huyo alikuwa akionyesha kuwa al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib
. alisema "Ya Zainab! Ya Zainab!" kwa kuyasikia hayo Ayatullah Kalbasi akasema kwa sauti ya kupaaza: "Allah swt auvunje uso wako! Al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib
. hakusema mara mbili, badala yake alisema mara moja tu!"
440. Daraja moja lingine la uwongo ni kule kula kiapo cha uwongo, kutoa ushahidi wa kiuwongo au kuficha ushahidi katika Mahakama ya Shariah. Hakuna shaka kuwa haya ndiyo uwongo ambazo zimo katika Madhambi Makuu. Insha Allah yote hayo yatazungumzwa kiundani ili kueleweka vyema.
441. Amesema al-Imam Zayn-al-'Aabediin
. katika Al-Kafi: "Jiepusheni na uwongo, ama iwe ndogo au kubwa, au iwe katika hali ya masikitiko au huzuni au katika mzaha."
442. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Al-Kafi : "Mtu yeyote hawezi kamwe kuionja Imani yake hadi hapo ajiepushe na uwongo, haidhuru kama itakuwa katika huzuni au mzaha."
443. Imeripotiwa kutoka Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Wasa'il al-Shiah: "Hakuna wema katika uwongo hata kama itakuwa katika hali ya huzuni au furaha. Wala hautakiwi kutoa ahadi za uwongo kwa watoto wako, ahadi ambazo hauna nia ya kuzitimiza. Kwa hakika uwongo unampotosha mtu kutenda madhambi makubwa makubwa ambayo hatimayake humtumbukiza mtu katika Moto wa Jahannam."
444. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
alipokuwa akimwusia Abu Dhar al-Ghaffari,alimwambia: "Ewe Abu Dhar! Mtu yeyote atakayejihifadhi dhidi ya uharamisho sehemu zake za siri na ulimi wake, basi ataingia Peponi. Mtu yeyote atakayetamka uwongo katika mzaha basi uwongo huo katika mzaha utampeleka hadi Jahannam!" "Ewe Aba Dhar! Ole wake yule mtu ambaye anapozungumza huzungumza kwa uwongo ili aweze kuwachekesha watu. Vile vile ole wake! Ole Wake! Ewe Abu Dhar! Yule ambaye atakayekaa kimya ataongoka. Hivyo kukaa kimya kwako ni faradhi kuliko kunasibisha uwongo na kusitoke kamwe uwongo hata kiasi kidogo kutoka kinywani mwako."
445. Bwana Abu Dhar anasema: "Je tawba ya mwenye kusema uwongo kwa kujua hivyo, itakuwaje ?"
446. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
alisema katika Wasa'il al-Shiah :: "Kufanya Isteghfar na kusali sala tano kwa kutimiza masharti yake ndiyo yanayoweza kuyaosha madhambi hayo."
447. Vile vile Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema katika Jihad : "Laana ya Allah swt inamwia msema uwongo hata kama atasema katika mzaha"
448. Vile vile Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema, katika Al-Khisal : "Mimi ninachukua dhamana ya kumpatia nyumba katika daraja iliyo ya juu kabisa katika Jannat kwa ajili ya mtu yeyote ambaye anajiepusha na ugomvi na vita halafu hata kama yeye atakuwa katika haki. Na nitampatia nyumba mtu yeyote yule katika daraja iliyo ya kati ambaye anajiepusha kusema uwongo hata kama atakuwa katika mzaha. Na vile vile nitampatia nyumba katika bustani za Jannat kwa mtu yeyote yule mwenye tabia njema."
449. Imepokelewa riwaya: kuwa Asma' binti 'Umays anasema: "Usiku wa kwanza wa 'Aisha, Mtume Muhammad(s.a.w.w)
alinipa chombo kimoja cha mazima akisema 'wape wanawake wanywe'
450. Wanawake wakasema: "Sisi hatuna njaa' Mtume Muhammad(s.a.w.w)
kwa kuyasikia hayo alisema: 'Njaa pamoja na Uwongo musivichanganye kwa pamoja!"
451. Asma' akauliza: "Iwapo sisi tutakuwa tukitamani au tukitaka kitu na tukasema kuwa hatukitaki au hatukitamani, basi jee huo ni uwongo ?"
452. Basi Mtume Muhammad(s.a.w.w)
alimjibu: "Naam! Bila shaka kila aina ya uwongo unaandikwa kiasi kwamba hata uwongo mdogo mdogo pia huitwa uwongo
."
453. Ipo riwaya moja isemayo: ipo riwaya ifuatayo: Siku moja al-Imam Ja'afar as- Sadique
. alikuwa ameketi pamoja na mwanae Isma'il, na akaja mfuasi wake mmoja akatoa salaam na akaketi pamoja nao. Wakati Imam
. alipoondoka kuelekea nyumbani m wake, basi na yule mtu pia akaondoka kumfuata Imam
. hadi kizingitini mwa nyumba ya Imam
. Imam
. hapo hapo aliagana nae na kuingia nyumbani mwake, mwana wa Imam
., Isma'il alimwuliza babake ni kwa nini hakumkaribisha mtu huyo kuingia nyumbani mwao kama desturi njema? Imam Ja'afar as- Sadique
. alimwambia kuwa haikuwa munasibu kwa mtu yule kuingia ndani, kwani mimi binafsi sikuwa nataka huyo mtu aje ndani na wala sikutaka Allah swt anihesabu miongoni mwa watu ambao wanasema nini mdomoni na wanavyo nini moyoni mwao!"
454. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema kuwa uwongo Mkuu upo katika makundi matatu: "Kumwita mtu kwa jina mbali na jina la mzazi wa kweli. "Kusema ndoto za uwongo ambazo hakuziota, "Au aseme kile ambacho mimi (Mtume Muhammad(s.a.w.w)
sikusema..
455. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema kuwa: "Uwongo ulio ovu kabisa ni kunakili kwa riwaya zilizo za uwongo."
456. Siku moja al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib
. alikuwapo katika baraza la Mua'wiyah na hapo mtu mmoja akaanza kutamka maneno yenye kashfa dhidi ya al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib
..
457. Al-Imam Husayn ibn 'Ali ibn Abi Talib
. alimjibu: "Ewe 'Umar ibn 'Uthman! Tabia yako ina upumbavu ambao wewe hauwezi kuuelewa. Mfano wako ni kama ule wa mbu ambaye akijiona mkubwa aliukalia mtende na wakati wa kutaka kuruka, aliuambia mtende: 'jizatiti kwa umadhubuti, kwani niko naruka kwa ajili ya kuteremka!' Kwa hayo mti ukamjibu: 'Mimi wala sijui ni kutoka wakati gani umenikalia juu, sasa hebu niambie kuondoka kwako kutaniangusha ?!"
458. Tuelewapo kuwa jambo lililopo ni uwongo basi na kulisikiliza pia ni haram. Kama vile kuandika na kusomwa kwa uwongo umeharamishwa basi na kunakili uwongo pia umeharamishwa. Kwa hakika Qur'an Tukufu imekuwa ikiwalaumu Mayahudi na Makafiri kwa kupeleka habari za uwongo za huku kupeleka huko na za huko kuleta huku. Qur'an Tukufu inatuambia: ' Enyi wasikilizaji wa maneno ya uwongo .'
459. As-Shayk Sadduq (a.r) ameinakili riwaya ifuatayo kutoka kwa al-Imam Ja'afar as- Sadique
. kuwa al-Imam
. aliulizwa: "Je inaruhusiwa kusikiliza uwongo wa waongo kwa makini?
"
460. Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique
. katika kumjibu (Kitab-i-'itiqadat): "Hapana! Iwapo mtu anamsikiliza kwa hamu na basi huwa anafanya ibada kwa mujibu wake. Iwapo msemaji anamwamini Allah swt basi msikilizaji atafanya ibada ya Allah swt. Na iwapo msemaji anafuata maneno ya Shaitani basi msikilizaji atafanya ibada ya Shaitani."
461. Allah swt anatuambia katika: "Mjiepusheni na maneno ya upuuzi
" (Qur'an, 22: 30).
462. Allah swt anatuambia: 'Na wale ambao hawashuhudii shahada za uwongo'
( Qur'an, 25: 72).
463. Popote pale ambapo kutakuwa na hatari ya maisha, mali au heshima ya mtu na kama kwa kusema uwongo kutamwondolea hatari hizo basi kunaruhusiwa kusema uwongo katika sura hizo. Hatari hizo ama ziwe kwa ajili yake mwenyewe au kwa ajili ya mtu mwingine. Hata hivyo imeruhusiwa kula kiapo cha uwongo kwa ajili ya kunusuru hayo. Katika baadhi ya nyakati, ni faradhi kusema na kula kiapo cha uwongo katika kuyanusuru maisha ya mtu, mfano, iwapo dhalimu atataka kumwua Mwislamu, ataka kumpiga na kumdhuru Mwislamu, au anataka kumdhalilisha na kumkashifu, anataka kumdhulumu na kumnyang'anya mali yake au anataka kumfunga mahabusu. Sasa iwapo huyo mdhalimu akikuomba anwani ya Mwislamu huyo, basi ni faradhi kwako kutompatia anwani yake, halafu hata kama itakubidi useme uwongo na ule kiapo cha kiuwongo kuwa wewe haujui chochote.
464. Sheikh Ansari anawanakili Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. na al-Imam Ja'afar as- Sadique
. katika Makasib kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema: "Mnaweza kula kiapo cha uwongo lakini mumnusuru ndugu yenu Mwislamu asiuawe kibure!"
465. Ismail Ibn Sa'ad ambaye Hadith yake ni sahihi anasema: "Mimi nilimwuliza Al-Imam 'Ali ar-Ridha
. kuhusu mtu ambaye amekula kiapo cha uwongo mbele ya mfalme kwa ajili ya kutaka kuinusuru mali yake."
466. Al-Imam 'Ali ar-Ridha
. alimjibu: "Hakuna shida yoyote
."
467. Mwandishi anasema kuwa yeye alimwuliza tena Al-Imam 'Ali ar-Ridha
: "Je inaruhusiwa kwa mtu kula kiapo cha uwongo kwa ajili ya kunusuru mali ya Mwislamu mwenzake kama vile alivyokula kiapo cha uwongo kwa ajili ya mali yake mwenyewe?"
468. Al-Imam 'Ali ar-Ridha
. alimjibu: "Naam! Inaruhusiwa."
469. Al-Imam Ja'afar as- Sadique
. anasema katika Faqiyyah: "Iwapo itambidi Mwislamu kula kiapo cha uwongo kwa ajili ya kumnusuru Mwislamu mwenzake pamoja na mali yake isichukuliwe na mdhalimu au mwizi, basi hakuna shida ndani ya kula kiapo cha uwongo na si hayo tu, bali hatatakiwa kulipa kaffara ya kula kiapo cha uwongo na badala yake atapewa malipo mema kabisa pamoja na thawabu nyingi mno kutoka kwa Allah swt."
470. Vile vile iwapo ataweza kuvumilia hasara basi ni Sunnah kuvumilia na hivyo asiseme uwongo. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Nahjul-Balagha, kuwa: "Ni alama ya Imani kuwa mtu aseme ukweli tu hata katika wakati wa kupatwa hasara na asiseme uwongo kwa ajili ya kupata faida
."
471. Al-Imam Ja'afar as- Sadique
. amesema katika Wasa'il al-Shiah, Kitabu Al-Hajji: "Mazungumzo yapo aina tatu: "Ukweli "Uwongo" Kuwasuluhisha watu
472. Kuna mtu aliuliza :"Mimi niwe fidia kwako! Je kuwasuluhisha watu ni kitu gani?
473. Al-Imam Ja'afar as- Sadique
. alimjibu: "Wewe umsikie mtu mmoja akimzungumza mtu mwingine na ukamwambia mtu mwingine kuwa fulani bin fulani alikuwa akikuzungumza vyema kabisa (ambapo kwa hakika ni kinyume chake kabisa) "
474. Vile vile iwapo bibi na bwana wamekwisha tengana na umefika wakati wa talaqa basi inambidi mtu azungumze hata uwongo ilimradi aweze kuwasuluhisha, na kwa hakika hili ndilo litakuwa jambo jema kabisa.
475. Mtu anaweza kumwendea mume na kumwambia kuwa "Loh ! Mke wako kwa kweli anasikitika mno kwa kuachana kwani anakupenda kupita kiasi na hivyo hataweza kuvumilia kuachana kwenu na anaweza kuugua."
476. Na vivyo hivyo amwendee bibi na kumtengenezea mambo kama hayo ya uwongo ili kusafishwe mazingira na kuleta usuluhisho na muungano baina ya bibi na bwana.
477. Imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad(s.a.w.w)
akiwa amesema: "Hakuna tendo lililo bora kabisa baada ya kutimiza yaliyo faradhishwa kama vile kuwasuluhisha watu! Hii ni kheri ambayo inayoeneza kheri duniani kote."
478. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w)
alisema wakati wa usia, katika: "Ewe Ali! Bila shaka Allah swt anapendelea uwongo katika kusuluhisha na hapendezewi ukweli katika kuzua ufisadi na magomvi !"
479. Vile vile Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema: "Kusuluhisha miongoni mwa watu, kufikiria usulihisho na kuepusha magomvi ni bora kuliko sala na saumu."
480. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
amesema: "Hakuna uwongo kwa mtu anayesuluhisha."
481. Amesema al-Imam Ja'afar as- Sadique
: " "Uwongo ni mwovu na haikubaliki isipokuwa katika sura mbili: "Katika kuuondoa shari ya mdhalimu "Kuwapatanisha watu
".
482. Mtume Muhammad(s.a.w.w)
anasema: "Zipo nafasi tatu ambapo uwongo unapendeza: kudanganya katika vita, ahadi aitoayo mume kwa mke wake na kuwapatanisha watu."
483. Ama kuhusiana na ahadi ya mume kwa mke wake, Islam inapendelea kuwaona wakiishi kwa raha na mustarehe na waishi kwa kupendana. Hivyo kumwambia mke wako uwongo wa kumtimizia jambo fulani, kama unao uwezo basi vyema kabisa, lakini kama hana uwezo, basi anaweza kumpa ahadi ya uwongo ili kuepukana na ugomvi na kumuudhi mke wake.
Kwa mfano, wewe hauna uwezo wa kumtimizia ombi fulani la mke wako, kama kwa mfano anataka nyumba, lakini wewe kwa kutokuwa na uwezo huo, utamdanganya kuwa nitakujengea au kukununulia ili kumridhisha mke wako. Sote tunajua kuwa ukaidi wa mwanamke ni ukaidi mkubwa kabisa na vile vile Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema kuwa "mwanamke ni kama mfupa wa ubavu, upo umepinda, hivyo usijaribu kuunyosha, utavunjika" hivyo tutumie mbinu kama hizi kwa nia njema ili kutuliza mambo nyumbani.
484. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Al-Kafi (ikizungumzia thawabu za Allah swt na juu ya adhabu na matumaini ya kusamehewa): "Jiepusheni na kusema uwongo! Pale mtu anapotarajia kupata kitu basi anataka akipate tu hicho kitu (basi huwa tayari kufanya kazi yoyote ili aipate) na vile vile mtu anapokiogopa kitu chochote kile, basi hujiweka mbali nacho."
485. Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. amesema katika Nahjul-Balagha: "Mtu yeyote anayefikiria kuwa yeye anamtegemea Allah swt lakini matendo yake hayaonyeshi hivyo basi kwa kiapo cha Allah swt aliye Mkuu, mtu huyo ni mwongo. Ingawaje mtu anapokitegemea kitu basi mwenendo wake hudhihirisha hivyo. Lakini itawezekanaje yeye amtegemee Allah swt ambapo matendo yake hayadhihiri hivyo? (mtu kama huyu kwa hakika si miongoni mwa wale wamtegemeao Allah swt basi anajidanganya mwenyewe). Vile vile mtu anapokiogopa kitu chochote basi matendo yake yatadhihirisha hali hiyo yaani ataamua kukikimbia kitu hicho. Lakini mtu anapodai kuwa anamwogopa Allah swt na kwa nini sasa hakimbii mbali na madhambi?"
486. Al-Imam Ja'afar as- Sadique
. amesema katika Misbah As-Shari'ah : "Wakati musemapo Allahu Akbar basi muelewe kile kilicho baina ya mbingu za juu na ardhi, vyote ni vidogo mbele ya Allah swt na kwa undani wa moyoni mwenu muelewe kwa sababu Allah swt anapoona kuwa kuna mja wake ambaye hasemi Allahu Akbar kutokea undani mwa moyo wake, basi Allah swt (humwambia) 'Ewe mwongo! Wewe unataka kunidanganya basi kwa kiapo cha heshima na Utukufu Wangu basi mimi nitakuepusha na dhikr yangu !'"
487. Mtu anaposema kuwa: "Mimi ninayo furaha kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w)
ni Mtume wangu na Qur'an Tukufu ni kitabu Kitakatifu na kuwa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib
. ni Imamu wangu. Na vyote hivyo vipo kwa ajili ya kuniongoza."
Ingawaje anatamka kwa mdomo lakini kimatendo utaona kuwa Shaitani na matamanio yake ya nafsi ndio viongozi wake! Na huvifuata hivyo! Utaona kuwa yeye havitilii maanani mafunzo na hidaya ya Qur'an Tukufu Na vile vile hatilii maanani maamrisho na mafunzo yaliyotolewa na Maimamu
. Kwa hivyo mtu kama huyu ni mwongo.
488. Wakati mtu anapofanya dua na akasema "(Ewe Mola wangu!) Mimi ninapoziangalia madhambi yangu basi hulia na ninapoangalia ukarimu wako ninajawa na matumaini kuwa Wewe utanisamehea." Kwa hakika utaona kuwa tunatamka hivyo lakini hatujali madhambi na hata anapotambua kuwa jambo fulani ni dhambi, basi hulitenda bila ya woga wowote ule! Uso wake haushtuki hata punje kidogo wakati wa kutenda dhambi! Basi hujitoa katika ukarimu na rehema za Allah swt! Je mtu kama huyu anapoyatamka maneno kama hayo yalivyo katika dua, anasema ukweli? Je uwongo wake si upo wazi !?
489. Vile vile mtu anapotamka "Mimi ninalia kwa kutokwa nafsi yangu na ninalilia maswala ya kaburini na ninalilia khofu ya Qiyama" ingawaje ni dhahiri kuwa hakuna anachokililia kitu kama hicho Huo ni uwongo wake kwani matendo yake hayaonyeshi kama kweli anayo khofu kama hiyo moyoni mwake. Al-Imam Zaynul 'Aabediin
. amesema katika Dua-i-Abu Hamza Thumali: "Ewe Allah swt! Labda Wewe umenipata katika ngazi za waongo na kwa hivyo (umeniondolea mtazamo wako wa kirehema) na umeniacha katika hali niliyonayo." Yaani mimi nimekuwa nikiyatimiza matamanio ya nafsi yangu na wala sijui nitaangukia katika maangamizo yapi.
490. Mfano wa kuwaambia uwongo Maimamu
. ni kama vile tunavyosema katika Ziyarat: "Enyi Aimma Ma'asumiin
.! Mimi nimezikubali kauli zenu na ninayafuata hukumu (na maamrisho) zenu na mimi ni mwenye kuwatiini." Sasa iwapo mtu atazisikia kauli na maamrisho ya Maimamu
. na asizifuate na badala yake akazifuata matamanio na maamrisho ya nfsi yake basi bila shaka mtu kama huyu ni Shaitani ! Basi inadhihirika waziwazi kuwa huyo ni mwongo kwa Maimamu
.!
491. Vile vile mfano mwingine wa kusema uwongo upo unapatikana katika Ziyarat, wakati tusemapo: "Enyi Aimma watoharifu! Mtu yeyote aliye na amani pamoja nanyi basi mimi pia nitakuwa na amani pamoja naye na yeyote yule atakayepigana vita pamoja nanyi au kuwapinga basi nami nitakuwa na vita naye na nitampinga vile vile!"
492. Kwa hakika hivyo ndivyo tunavyodai, lakini matendo yetu ni kwamba tunao urafiki mzuri wa kidugu pamoja na maadui wa Islam! Na badala yake sisi tunafanya uadui pamoja na wapenzi na wafuasi wa Aimma
.. Wakati anaposema "Enyi Maasumiin
.! Mimi ninawaacha wale wanaokukhilafu nyinyi." Lakini kwa hakika haya haytekelezwi kimatendo Sasa jee mtu kama huyu si mwongo mbele ya Maimamu
.?
493. Hivyo sisi tunaweza kusema kuwa muumin hawasemi uwongo mfano kuwa kila Mumiin anakuwa na khofu ya Allah swt kama vile tunavyoambiwa katika Qur'an Tukufu: 'Kama nyinyi ni mumiin wa kweli basi muwe mukiniogopa Mimi tu' (Surah Aali-Imran, 3, Ayah ya 175). Na vivyo hivyo Mumiin wote ndio wanaomtegemea Allah swt tu na bila shaka wote wanakuwa na khofu ya Allah swt na matumaini yao pia yanakuwa na ngazi mbalimbali na kamwe haiwezekani zinalingana na za Aimma
.
494. Dua-i Abu Hamza Thumali : "Ewe Allah swt! Mimi madhambi niliyoyatenda si kwamba nikukupinga wewe na wala sikutenda madhambi hayo kuwa nikichukulia hukumu zako ati ni za kawaida na wala sikutenda madhambi kwa kufikiria kuwa adhabu zako ni ndogo bali nimetenda kwa kutokana na kasoro zangu za kinafsi na ujeuri wangu.."
495. Du'a: "Ewe Allah swt ! Nakuomba unipatie yakini ya kweli kwayo ambayo mimi niweze kutii amri zako kikamilifu."
496. Inapatikana katika riwaya kuwa "Mtu anapokitaka kitu basi kwa kufanya jitihada, anakipata tu."
497. Qur'an Tukufu katika Surah at-Tawbah, 9, Ayah ya 119: 'Muwe pamoja na Wasemao ukweli
.' Katika Ayah hii Allah swt anatuambia kuhusu 'Sadiqiin' ambao ndio Ahlul Bait
. ya Mtume Muhammad(s.a.w.w)
'.