• Anza
  • Iliyopita
  • 4 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 4256 / Pakua: 3445
Kiwango Kiwango Kiwango
UWAHHABI Asili na kuenea kwake

UWAHHABI Asili na kuenea kwake

Mwandishi:
Swahili

UWAHHABI ASILI NA KUENEA KWAKE

(Uchambuzi wa kihistoria)

KIMEKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA:AMIRALY M. H. DATOO

MANENO MACHACHE

KWA JINA LA ALLAH MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

Natoa shukurani zangu kwa Allah swt, Mtume Muhammad(s.a.w.w) pamoja na Ahli Bayt tukufu ya nyumba yake(a.s) kwa kunijaalia uwezo wa kukikusanya na kukitarjumu kitabu hiki. Allah swt amewatuma Mitume(a.s) kuja kutuongoza na kutuletea maamrusgo Yake ili tusihangaike kwa kutapa huku na huko tukitafuta kipi ni kweli na sahihi. Lakini wapo watu wenye uchu wa kujitakia dunia kwa hali yoyote ile, hivyo wanawasahau Mitume(a.s) na ujumbe waliokuwa wametuletea katika miaka yote hiyo. Kwa tamaa na uroho wao wanachafua dunia na desturi za amani.Wanawatesa na kuwateketeza watu bila ya kujali kuwa wao wafanyavyo si haki. Mtume(s.a.w.w) alisema kuwa, "Ummah wangu utagawanyika katika makundi sabini na tatu, ni kundi moja tu litakaloingia Peponi." Hivyo makundi sabini na mbili , kama zilivyobainishwa, zitaingia Motoni kwa sababu za itikadi zao potofu, na kwa hakika hayo yamshakwisha tokea. Makundi haya sabini na mawili si makundi ya makafiri kwa kutojua ilimu sahihi ya Qur'an na Hadith, lakini wataingizwa Motoni kwa sababu wao wamediriki kuubadilisha Uislamu.Na hao wanaitwa ahlul-bid'a au -dalala, wakaidi. Wakaidi, kwa sababu wao ni Waislamu, na hapo mbeleni watatolewa kutoka Jahannam na kupelekwa Peponi. Mbali na hao, wapo wale ambao ni Waislamu lakini wanakuwa katika jitihada za kuubadilisha kwa ilimu yao potofu na kipeo chao kidogo, hivyo wanatoka nje ya Uislam. Kwa hakika hao watabakia Motoni kwa milele. Nao ni Zindiq na wachafuzi. Leo, watu waitwao la-madhhabi wanatumia mamilioni ya madola kwa kueneza imani zao potofu katika kila nchi humu duniani. Ni jambo lakusikitisha mno kuona kuwa hawa waroho wa mapesa wamekuwa wakivutiwa mno katika imani zao potofu na za kufitini, huku nyuma wakiachia hazina kubwa waliyoachiwa na Ahlu al-Bayt(a.s) ya Nyumba ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) na Maulamaa wa Ahlu as-Sunna. Hao Mawahhabi wamejaribu kwa jitihada zao zote kuwadanganya Waislamu kuwa vitabu vya Maulamaa wao vinawapotosha. Wao wametayarisha vitabu na propaganda zao dhidi ya Islam halisi iliyokuja kwetu kutokea Mtume Muhammad(s.a.w.w) , kwa maandiko ya Mawahhabi yaliyojaa upotofu na vitisho na ulghai.

hakika Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab na kizazi chake wamekuwa wakitoa imani zao potofu kwa kuchapa vitabu ambavyo vimekuwa vikiwapotosha Waislamu kwani walikuwa wakizitumia Ayah za Qur'an tukufu dhidi ya Waislamu wenyewe. Wao hata walithubutu kuwaita Wailsamu kuwa ni Makafiri kwa kuelezea kiuongo Ayah na Hadith. Na jambo hili ndilo limenifanya mimi nijiandae kukitoa kitabu hiki ambacho kitafichua uasili wao. Kijitabu hiki kilicho mikononi mwenu ni sehemu moja ya kitabu kamili juu ya Mawahhabi. Sehemu hii inazungumzia vile Mawahhabi walivyotokezea, vile walivyo enea vile majahili na makatili waliojiingiza katika Uwahhabi ili kujipatia mali na cheo wamewateketeza na kuwaua Waislamu na kuzipora mali zao. Vile vile ninakitayarisha kitabu kingine ambacho kitazungumzia imani za Mawahhabi na kuzichambua moja baada ya pili ili Waislamu wajue waziwazi kuwa wao wanadanganywa juu juu tu. Vitabu vingi vimeandikwa juu ya Mawahhabi, lakini kuna haja ya kutoboa mambo yao ili uasili wao ujulikane. Hivi karibuni rafiki yangu mmoja Msunni, ambaye alikuwa akitoa mihadhara dhidi ya wauaji wa Imam Hussain(a.s) huko Karbala, Iraq, nimesikia amejiunga na Mawahhabi hawa. Hivyo natumai atakapoisoma habari zilizoandikwa humu, labda atajifikiria. Jambo la pili, nimebishana na rafiki yangu mmoja ambaye ni shabiki mkubwa wa mpira. Mimi nilimwambia kuwa katika siku atakazokuwa yeye akiangali mechi za footbal za Kombe la dunia 1998,Ufaransa,mimi nitakitayarisha kitabu kimoja. Hivyo tuone yule anayeupoteza muda na yule anayeutumia muda kwa ajili ya manufaa ya wengine. Tunamwomba Allah swt awasaidie Waislamu wasiteleze kutumbukia katika mitego ya Mawahhabi.

Amiraly M. H. Datoo

P.O.Box 838

BUKOBA

9 June 1998

SEHEMU YA KWANZA (1) UWAHHABI: ASILI NA KUENEA KWAKE

Katika zama za utawala wa Uthmaniyyah (Ottoman Empire), tawala zote ambazo zilikuwapo katika bara la Uarabu, kila jimbo lilikuwa na maofisa waliokuwa wameteuliwa kutoka serikali kuu. Baadaye, kila mkoa isipokuwa Hijaz ilikuwa mikononi mwa wale walioweza kuzinyakua na kuwa tawala za Kifalme. Imani za Mawahhabi zilizoenezwa na Muhammad ibn 'Abdul-Wahhab zilikuwa zimeshabadilika kuwa katika sura za kisiasa katika kipindi kifupi katika mwaka 1150 A.H.(1737) na zilienea Bara zima la Arabia. Baadaye, kwa amri za Khalifa wa Istanbul, Muhammad 'Ali Pasha, Gavana wa Misri, aliikomboa Arabia kwa msaada wa majeshi ya Misri. 'Abd u al-'Azizi ibn Muhammad, aliyewaamini Mawahhabi, alitangaza vita kwa mara ya kwanza katika 1205 A.H. (1791) dhidi ya amir wa Makkah, Sharif Ghalib Effendi. Wao walikuwa wamekwisha eneza Uwahhabi kisirisiri hadi hapo. Wao waliwaua na kuwatesa Waislamu wengi mno, kuwachukua wanawake na watoto wao mateka na kuzipora mali zao zote.

Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab alitokana na kabila la Bani Tamim. Alizaliwa katika kijiji cha Uyaina karibu na mji wa Huraimila huko katika jangwa la Najd, mwaka 1111 A.H.(1699) na kufa 1206 A.H.(1792). Hapo awali alikuwa na nia ya kufanya biashara, hivyo alisafiri hadi Basra, Baghdad, Iran, India na Damascus, ambako kote huko alijipatia sifa la jina kama Sheikh wa Najdi kwa sababu za ujanja na tabia yake.Yeye aliona na kujifunza mambo mengi katika sehemu hizi na hivyo akawa na hamu ya kuwa kiongozi mkubwa. Hivyo ili kutaka kutimiza hamu yake hiyo ilimbidi abuni njia moja iliyokuwa tofauti na njia zinginezo ili aweza kutimiza malengo yake, na kwa kujitayarisha kwa hayo, alianza kuhudhuria mihadhara ya maulamaa wa Kihanbali waliokuwapo katika Mji Mtukufu wa Madinah na baadaye huko Damascus kwa kipindi fulani. Wakati aliporejea Najd, alianza kuandika makala juu ya maudhui ya dini kwa ajili ya wanakijiji wake.Katika kuandika makala hayo,yeye alikuwa akiongezea fikara zake alizokuwa amezipata kutoka makundi ya bid'a ya Mu'tazila na wengineo. Wanakijiji wengi waliokuwa masikini majahili, hususan wakazi wa Dar'iyya na chifu wao jahili, Muhammad ibn Sa'ud, walikuwa wakimfuata Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab. Waarabu walikuwa wakiheshimu mno ukabila na kwa kuwa Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab alikuwa si kutoka kabila maarufu, basi alimtumia Muhammad ibn Sa'ud kama chombo kwa kuutangaza fitna yake mpya aliyokuwa ameiita Uwahhabi. Yeye alijitambulisha kama Qadhi (mkuu wa mambo ya dini) na Muhammad ibn Sa'ud kama Hakim (mtawala). Kwa hila zake alikwishafanya mabadiliko katika katiba yao kuwa wao hawatarithiwa na mtu yeyote yule isipokuwa watoto wao tu.

Katika mwaka 1306 (1888) wakati ambapo kitabu kiitwacho Mir'atu al-Haramain kilipoandikwa, kiongozi wa Najd alikuwa 'Abdullah ibn Faysal, kutokea kizazi cha Muhammad ibn Sa'ud, na Qadhi pia alikuwa ametokana na kizazi cha Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab. Baba yake mzazi wa Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab, 'Abdu al-Wahhab, ambaye alikuwa ni mcha Mungu, 'alim halisi katika Madina, ndugu yake Sulaiman ibn 'Abdu al-Wahhab na waalimu wake walikuwa wamekwisha tambua kutoka maneno, matendo, ishara na mawazo yake, ambayo mara kwa mara alikuwa akidhihirisha katika sura ya maswali alipokuwa mwanafunzi huko Madina, kuwa atakuwa mpotofu ambaye ataidhuru mno Islam kwa undani katika kipindi kifupi kijacho. Wao wote kwa pamoja walimuasa na kumnasihi aache mawazo yke hayo ya upotoshi na vile vile walikuwa wakiwashauri Waislamu wote kwa ujumla wasimfuate na wajiepushe na Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab. Lakini katika muda mfupi tu walikumbana na jambo walilokuwa nalo khofu, na yeye alianza kueneza uzushi wake huo kidhahiri kwa jina la Uwahhabi. Kwa ajili ya kuwapotosha majahili na wapumbavu, yey alijitokeza kwa mawazo ya kurekebisha na kuzua mambo ambayo hayakubaliani na vitabu vya maulamaa wa Islam. Yeye alithubutu kwa kishindo kuwatuhumu Waislamu wa Ahlu as-Sunnah wal Jama'a kuwa ni makafiri. Yeye alikuwa akiamini kuwa ni shirk kumwomba Allah swt kwa kupitia Mtume Muhammad(s.a.w.w) au Mitume mingine(a.s) au ma-Awliya'' na kuzuru makaburi.

Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab alikuwa akimwona mtu yeyote yule anayesali na kuomba karibu na kaburi kuwa ni Mushrik. Yeye alisisitiza kuwa Waislamu wasemao kuwa mtu fulani au kitu fulani mbali na Allah swt kimefanya hivi au vile,kwa mfano, kwa kusema kuwa dawa fulani na fulani zimeponyesha au mimi nimeweza kupata kile nilichokuwa nikihitaji kwa kupitia Wasila wa Mtume Muhammad(s.a.w.w) au au mawali fulani fulani basi hao wote ni Mushrik. Ingawaje waraka wa Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab hazikuwa chochote isipokuwa ni uongo na fitina tu, lakini majahili hawakuweza kutofautisha baina ya ukweli na uongo, wale wasiokuwa na kazi, wazururaji, majahili, wenye kuvizia bahati na wenye nyoyo ngumu walizipokea mawazo yake na kujiweka bega kwa bega pamoja naye na kuamini wale Waislamu waliokuwa katika njia sahihi kuwa wote kwa pamoj ni makafiri.

Wakati Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alipowaomba ruhusa watawala wa Dar'iyya kutaka kueneza imani zake za uzushi kwa kupitia utawala wao, wao walimpokea kwa mikono miwili kwa matumaini ya kupanua eneo la utawala na kuzidi kwa nguvu zao. Wao walijitolea kwa hali na mali kueneza imani hizo kila mahala. Wao hata walithubutu kutangaza vita dhidi ya wale wote waliokuwa wakimkataa na kumpinga. Watu Mahayawani na wateka nyara wa jangwani walikuwa wakishindana katika kujiunga na jeshi la Muhammad ibn Sa'ud wakati pale iliposemwa kuwa ni halali kumwua na kupora mali za Waislamu. Katika mwaka 1143 (1730), Muhammad ibn Sa'ud pamoja na Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab wakishirikiana kwa pamoja walifikia maafikiano kuwa wale wote ambao hawata kubalia Uwahhabi, basi watakuwa ni makafiri na Mushrik, na hivyo ilikuwa ni halali kwao kuwaua na kutaifisha mali yao yote, na walitangaza rasmi amri hiyo miaka saba iliyofuatia. Hapo ndipo Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab alipoanza kutunga uzushi wa ijtihad pale alipokuwa na umri wa miaka thelathini na miwili na aliitangaza kidhahiri pale alipokuwa na umri wa miaka arobaini. As-Sayyid Ahmad ibn Zaini Dahlan, Mufti wa Makkah, akielezea katika somo la Al-fitnat al-Wahhabiyya (kitabu cha Al-Futuhat al-Islamiyya) kuhusu imani za Uwahhabi na dhuluma na maafa zinazowapata Waislamu kutoka kwa Mawahhabi. Yeye anaandika: "Ili kutaka kuwadanganya ma'ulamaa wa Ahlu as-Sunnah katika miji ya Makkah na Madinah, wao waliwatuma watu wao katika miji hizo, lakini watu wao walishindwa kujibu maswali ya Maulamaa wa Kiislamu. Imekuwa dhahiri kuwa wao kwa hakika walikuwa ni wazushi majahili. Kulipitishwa sharia ikiwasema kuwa ni makafiri na kuenezwa kila mahala. Shariff Mas'ud ibn Sai'd, Amir wa Makkah, aliamrisha kuwa Mawahhabi watiwe mahabusu. Baadhi ya Mawahhabi walikimbilia Dar'iyya na kuelezea yale yaliyowapata." Maulamaa wa Hijaz, wanaotokana na Madhehebu yote manne, akiwemo Sulaiman ndugu yake Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab na waalimu wake waliokuwa wamemfundisha, walivisoma vitabu vya Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab na wakatayarisha katika sura ya vitabu majibu ya maandiko yake, yenye kuleta utenganishi na kuidhuru Islam, kwa ajili ya kuwatanabahisha Waislamu, wajitahadhari na kujitenga na upotoshi wa Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab.

Kwa hakika vitabu hivi havikuweza kusaidia zaidi na badala yake ziliongeza hasira na chuki za Mawahhabi dhidi ya Waislamu na kumzuzua zaidi Muhammad ibn Sa'ud awashambulie Waislamu na kusababisha umwagikaji mwingi wa damu. Yeye alitokana na kabila la Bani Hanifa, kabila ambalo alitokamo mzushi wa Utume Musailamat al-Kadh-dhab. Muhammad ibn Sa'ud alikufa katika mwaka 1178 (1765), na hivyo kwa mujibu wa katiba waliyokuwa wametunga, mwanake 'Abdu al-'Aziz alimrithi. 'Abdu al-'Aziz aliuawa kwa kupigwa kisu tumboni, katika msikiti wa Dar'iyya katika mwaka 1217 (1803). Na hapo mtoto wake Sa'ud ibn 'Abdu al-'Aziz ndiye aliyekuwa chifu wa Mawahhabi. Hawa wote watatu walijitolea kimabavu kama kwamba walikuwa wakishindana, katika kumwaga damu ya Waislamu ili waweze kuwadanganya na kuwapotosha Waarabu na kueneza Uwahhabi. Mawahhabi wanadai kuwa Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab alikuwa akihubiri mawazo yake kwa ajili ya kujipatia utukufu katika imani yake katika upweke wa Allah swt na kuwakomboa Waislamu wasitumbukie katika Shirk. Wao wanadai kuwa Waislamu wamekuwa wakitenda dhambi la Shirk kwa karne sita mfululizo na hivyo yeye alikuja kuirejesha upya dini ya Waislamu. Yeye anazitoa Ayah za Qur'an Tukufu nambari 5 ya Surah al-Ahqaf, Ayah 106 surah Yunus, Ayah 14 sura al-Ra'd ili kwamba Waislamu wote wakubaliane na mawazo yake. Hata hivyo, zipo Ayah nyingi kama hizo, na Maulamaa wanasema kuwa hizo Ayah zimekuwa zikiwazungumzia makafiri waliokuwa wakiabudu miungu na masanamu au waliokuwa washirikina. Kwa mujibu wa Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab, Mwislamu anakuwa Mushrik pale anapoomba kwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) , au kwa Mtume(a.s) mwingine, au wali au mcha Mungu karibu na kaburi au mbali kutoka hapo, yaani, iwapo anapomwomba msaada wa kutokana na shida aliyonayo, au anapoomba kutetewa mbele ya Allah swt kwa kutaja jina lake au anapotaka kuzuru kaburi lake. Allah swt anatuambia kuhusu makafiri wanaoabudu miungu na masanamu katika Ayah ya tatu ya surah al-Zumar, lakini Mawahhabi wanaonyesha Ayah hii kama ndio waraka wa kuhalalisha utumiaji wao wa neno la Mushrik kwa ajili ya Waislamu waombao kwa kuwaweka Mitume(a.s) au Mawalii kama ndio watu walio baina yao na Allah swt. Wao wanasema kuwa hata Mushrik waliokuwa wakiabudu miungu pia awaikuwa wakijua kuwa vyote vilikuwa vimeumbwa na Allah swt. Wao wanasema kuwa Allah swt amebainisha: Na kama ukiwauliza, Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akalitiisha jua na mwezi?" Bila shaka watasema, Allah (Surah Ankabut, ayah ya 61na Sura Zukhruf, Aya ya 87). Wao wanadai kuwa hao Mushrik walikuwa hivyo makafiri Mushrik si kwa sababu walikuwa wakiamini hivyo bali wao walizungumza kama ilivyosemwa katika Ayah ya 3 ya Surah az-Zumar: Wale wanaofanya marafiki na wale mbali na Allah wanasema, "Wao wanatusaidia kutufikisha karibu (ya Allah swt) kwa kututetea mbele Allah'" Wao wanadai kuwa Waislamu wanaoomba katika makaburi ya Mitume, ma-Awliya' kwa utetezi na misaada basi wanakuwa Mushrik kwa kusema hivyo.

Ni jambo la kipumbavu kabisa kwa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab kuwasema Waislamu wanakuwa makafiri na Mushrik kwa Ayah hiyo. Kwa sababu, makafiri wanawaambudu masanamu ili kwamba ni masanamu hayo tu ndiyo yatakayowasaidia kuwatetea wao; wao wanamwacha Allah swt na badala yake wanakluwa na imani moja tu ya kuwaomba miungu na masanamu hiyo kuwa watetezi wao. Lakini ni uhakika uliyo bayana kuwa Waislamu kamwe hawawabudu Mitume(a.s) au Ma-Awliya' lakini wanayo imani kuwa kila kitu kinatoka kwa Allah swt. Sisi tunapenda kuwa hao ma-Awliya' wawe ni Wasila wetu. Makafiri wanaamini kuwa miungu na masanamu yao inawaombea chochote kile wakitakacho na kumfanya Allah swt kuwatimizia chochote kile wakitakacho. Wakati ambapo, Waislamu wanaomba msaada wa Awliya' ambao wanawajua kuwa hao ndio watumwa wapenzi wa Allah swt, kwa sababu Allah swt ameahidi katika Qur'an tukufu kuwa Yeye atawaruhusu waja wake wapenzi kuwatetea na atakubali utetezi wao na Sala na kwa sababu Waislamu wanaamini ubashiri mzuri katika Qur'an. Kamwe huwezi kulinganisha baina ya kafiri anayeabudu miungu na masanamu na Waislamu wakiomba msaada wa Awliya'. Waislamu na Makafiri wote ni binadamu kwa miili, na wanafanana kwa kuonekana, lakini Waislamu ni marafiki wa Allah swt na watakuwa Peponi kwa milele wakati ambapo Makafiri ni maadui wakubwa wa Allah swt na watakuwapo kwa milele katika Motoni. Kujionesha kwao hakumaanishi kuwa watabakia vivyo hivyo daima. Wale wanaowaabudu masanamu na miungu ambao ndio maadui wakubwa wa Allah swt, yatawafikisha hadi kuingia Jahannam. Lakini wale wanaowafanya marafiki wa Allah swt kuwa marafiki wao, basi Allah swt atawabariki na kuwarehemu. Ipo Hadith isemayo: Rehema za Allah swt zinateremka pale waja wake wapenzi wanapotajwa, nayo pia inatuonyesha kuwa Allah swt ataonyesha rehema zake na misamaha yake pale Mitume(a.s) na Awliya' wanapoombwa.

Waislamu wote kwa pamoja wanatambua waziwazi kuwa Mitume(a.s) na Awliya' si watu wa kuabudiwa na wala si washiriki wa Allah swt. Waislamu wanatambua vile vile kuwa wapo waja wa Allah swt ambao hawastahili kuombwa na papo hapo wapo waja wengineo ambao maombi yao hukubaliwa Kwake. Katika surah Maidah, Ayah ya 35 tunaambiwa: "Tafuteni Wasila wa kunifikia Mimi" Allah swt anamaanisha kuwa Yeye atakubalia ibada za waja wake halisi na kuwapatia kile wakiombacho. Tunapata Hadith sharif iliyonakiliwa na al-Bukhari, Muslim na katika Kunuzi ad-daqaiq, isemayo: "Kwa hakika, wapo wacha Mungu halisi wa Allah swt ambapo Yeye anawaumbia kile walacho kiapo; kamwe hawasingizii." Waislamu wanawachukulia Awliya' kama Wasila na kutegemea maombi na msaada wao kwa sababu wao wanaamini Ayah na hadith za hapo juu. Ingawaje wapo baadhi ya makafiri wanaowaabudu masanamu wakidai kuwa ingawaje masanamu wao si waumbaji lakini Allah swt tu ndiye muumba, hivyo wao wanaamini kuwa masanamu wao wanastahili kuabudiwa kwa sababu masanamu hao wananao uwezo wa kumfanya allah swt awatimizie kile wakiombacho. Wao wanawashirikisha masanamu wao pamoja na Allah swt. Iwapo mtu yeyote atakayemwomba yeyote yule ambaye ameshirikishwa na Allah swt kwa ajili ya maombi yake basi huyo mtu atakuwa kafiri. Lakini yule asemaye kuwa: "Kwa hakika maombi yangu hayatakubaliwa kwa amri yake. Yeye ni sababu tu. Allah swt anawapenda wale ambao wanaojiimarisha katika njia Yake. Ni yeye anaumba kwa matokeo ya sababu. Mimi namwomba msaada huyu mtu kwa sababu ya kuwa imara katika njia ya Allah swt, lakini nategemea maombi yangu kukubaliwa na Allah swt. Mtume Muhammad(s.a.w.w) alikuwa ni mja wake mpenzi na mimi ninazifuata Sunnah zake katika utiifu Wake," basi atapata thawabu. Iwapo maombi yake yatakubaliwa basi atamshukuru Allah swt; na kama sivyo, basi itabidi aridhike kwa amri ya Allah swt. Kuabudu masanamu na miungu kwa Makafiri si sawa na vile Waislamu wawaombavyo Awliya' kwa maombi, utetezi na misaada. Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye atasema kuwa makundi mawili haya yako sawa bali atasema kuwa makundi haya mawili yapo tofauti kabisa. Hakuna muumba isipokuwa Allah swt pekee.

Mushrik na Makafiri, hata hivyo, huwachukulia masanamu wao kuwa ni ilah (miungu) au ma'bud (anayestahili kuabudiwa) na huwa wanawaabudu ingawaje wao wanatambua waziwazi kuwa masanamu kamwe hawawezi kuwaumbia chochote. Baadhi yao wanakuwa mushrik kwa kuwachukulia masanamu wao kuwa ni ilah ambapo wengine kwa kuwaabudu au kuwachukulia kama ma'abud. Watu hao sio Mushrik kwa sababu wanasema kuwa masanamu yao itawatetea na kuwafanya karibu zaidi ya Allah swt, bali wao ni Mushrik kwa sababu wao wanawachukulia kama ma'bud na kwa sababu wanawaabudu. Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema, "Utafika wakati ambapo Ayah zilizoteremshwa kuhusu Makafiri zitatumika dhidi ya Waislamu." na "Ninayo khofu sana kuwa watu watakuja kuzitumia Ayah za Qur'an kwa matumizi ambayo Allah swt hazikubalii." Hadith hizi mbili zinadalilisha kuwa watu wasio na dini watatokezea na kuzibandika Waislamu Ayah zile zilizoteremshiwa Makafiri na hivyo kuichezea Qur'an. Waislamu wanazuru makaburi ya wale, wanaowaamini kuwa wanapendwa na Allah swt. Wao wanamwomba Allah swt kwa kuwapitia waja wake wanaopendwa naye. Mtume Muhammad(s.a.w.w) pamoja na ma-Sahaba watukufu pia walifanya hivyo na sisi pia tumeambiwa kufanya hivyo. Mtume Muhammad(s.a.w.w) baada ya kumlaza kaburini mama yake na Imam Ali(a.s) Fatimah bint Asad na aliomba: "Ewe Mola wangu! Mrehemu Mama Fatima bint Asad! Mrehemu mno kwa mapenzi ya Mtume Wako na Mitume waliyokuwa wamenitangulia mimi! "

Mtu mmoja kipofu alimwomba Mtume Muhammad(s.a.w.w) amwombee duaa ili apone upofu wake. Mtume Muhammad(s.a.w.w) alimwambia aombe hivi: "Ewe Mola wangu! Kwa hakika mimi ninakuomba na ninaelekea kwako kupitia kwa Mtume wako Mtume wa Rehma, Ewe Muhammad! Kwa hakika mimi naelekea kwa Mola wangu kupitia kwako katika haja yangu ili ikubaliwe, ewe Mola wangu! Mfanye Muhammad kuwa muombezi wangu." Mtume Adam (a.s) aliomba: "Ewe Mola wangu! Naomba nisamehe kwa mapenzi ya mwanangu Mohammad(s.a.w.w) !" wakati alipoteremka katika kisiwa cha Serandib (Ceylon) baada ya kula tunda la mti alilokuwa amepigiwa marufuku na Allah swt. Na Allah swt alibainisha: "Ewe Adam! Mimi ningalikuwa nimekubali utetezi wako iwapo ungekuwa umeomba msamaha kupitia Muhammad kwa ajili ya viumbe vyote vilivyopo duniani na mbinguni." Umar alimchukua 'Abbas (r.a) kwa ajili ya kuomba mvua kwa nia ya kumchukua kama Wasila, na maombi yake yalikubaliwa. Katika historia kuna matukio na habari nyingi zielezeazo ruhusa kuzuru makaburi na kuhusu kuwataja watu waliokwisha kufa kuwafanya Wasila katika kuomba duaa. Muhammad ibn Sulaiman Effendi anadondoa kuwa Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab alikuwa mwovu na aliyepotoka na kwamba alikuwa na tabia ya kutumia Ayah za Qur'an na Hadith visivyotakiwa. Yeye ameandika:"Ewe Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab! Usiwatukane Waislamu! Mimi ninakushauri kwa kiapo cha Allah swt. Mwambie ukweli yeyote yule asemaye kuwa kuna muumba mwingine mbali na Allah swt! Msahihishe huyo kwa kumtolea uthibitisho ulio sahihi! Wasilamu kamwe hawawezi kuitwa Makafiri! Wewe pia u Mwislamu pia. Inawezekana ukamwita mtu mmoja kuwa ni Kafiri kuliko kuwaita mamilioni. Kwa hakika ni dhahiri kuwa yeyote yule ajitoaye nje ya jumuiya yake basi anaangukia hatarini. Katika surah an-Nisa, Ayah ya 115 tunaambiwa:

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿١١٥﴾

"Na atakayemwasi Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na akafuata njia isiyokuwa ya Waislamu, tutamgeuza alikogeukia mwenyewe na tutamwingiza katika Jahannam; napo ni pahali pabaya kabisa pa mtu kurudia."

Kwa hakika Ayah hii inawasema wale waliojitoa katika madhehebu ya Kiislamu.

Zipo Hadith nyingi mno zinazoelezea kuwa imeruhusiwa kuzuru makaburi. Masahaba walikuwa wakiizuru kaburi ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) kwa mara nyingi mno kwa ajili ya kutaka kupata baraka, na kumeandikwa makala na vitabu vingi mno juu ya baraka za kuzuru hapo. Kamwe haidhuru kuomba kwa kupitia Mawali' (Wasila), kuomba kwa kutaja majina yao. Ni imani potofu kuamini kuwa mtu atajwaye atakuwa akimwathiri mwombaji na atamfanyia chochote kile atakacho na atakuwa akijua mambo asiyoyajua.Waislamu kamwe wasituhumiwe kwa mambo kama hayo kwani wao hawaamini hivyo. Waislamu wanaomba kwa kupitia waja wake wapenzi wa Allah swt wawe kama watetezi wao, wawaombee wao. Sifa ya kuumba kile kiombaccchwo ni kwa ajili ya Allah swt tu peke yake na wala hakuna mwingine. Allah swt anawataka waja wake wamwombe Yeye kama vile alivyoamrisha katika Surah al-Maidah, Ayah 27: Allah huwakubalia (ibada,duaa n.k.) wale awapendao. Watu waliokufa hawatakiwi kutimiza kile walichoombwa bali wanakuwa ni watu wa kati kwa Allah swt kuwatimizia kile walichomuomba Allah swt kutimiziwa. Hairuhusiwi kuwaomba wafu kitu chochote na Waislamu hawafanyi hivyo. Inaruhusiwa kuwataka wawe watu wa kati katika kutimiziwa maombi yao. maneno Istighatha, Istishfa' na tawassul vyote hivyo vinamaanisha kuomba kwa Wasila Allah swt ndiye pekee muumbaji na ni desturi Yake kumfanya mja wake kuwa Wasila au sababu ya kuumbwa kwa kitu kingine. Yeyote yule atakaye Allah swt aumbe jambo basi achukue Wasila ambacho ndiccho kitakachokuwa Wasila wa kuumbwa kitu hicho. Mitume yote imekuwa ikitumia Wasila katika masuala yao.

Allah swt anasifia mno matendo ya kutawassuli na vile vile Mitume(a.s) pia wametuamrisha hivyo. Matukio ya kila siku pia yandalilisha umuhimu wake na inambidi mtu ang'angie ili aweze kufanikiwa katika kutimiziwa haja zake. Ni muhimu kutambua kuwa Allah swt tu ndiye afanyaye hizo sababu kuwa sababu za vitu, na huziumba baada ya mtu kuzishikilia kwa madhubuti sababu. Mtu yule anayeamini anaweza kusema: "Nimejipatia kitu hiki kwa kutokana na sababu hiyo." Sentenso hii haimaanishi kuwa hiyo sababu ndiyo iliyoumba kitu hicho, bali inamaanisha kuwa Allah swt amekiumba kitu hicho kwa kupitia sababu. Kwa mfano, sentenso, "dawa nilizozitumia zimeniponya"; "Mgoonjwa wangu amepona baada ya mimi kuchukua nadhiri ya Sayyidat Fatimah"; "Supu imenikinaisha," na "maji yametuliza kiu changu," vyote hapo vinamaanisha sababu hizo kuwa ni Wasila. Ni muhimu kutambua kuwa Mwislamu asemaye kauli kama hizi huwa anaamini hivyo. Wale wanaoamini hivyo kamwe hawawezi kuitwa Makafiri. Mawahhabi nao pia wanasema kuwa inaruhusiwa kuoma kitu kutoka wale walio karibu na hai. Wao wanaomba mmoja kwa mwinginw na hata kuwaomba maofisa wa serikali kwa mambo mengi.; hata kuthubutu kusema kuwa wanawaomba kuwatimizia maombi yao. Kwao ni shirk kuwaomba waliolkufa au waliombali, bali si shirk kuwaomba walio hai. Hata hivyi iwe wazi kuwa Maulamaa wa Dini hii wanasema kuwa si shirk kwa sababu wa pili hayupo na hakuna tofauti baina yao. Kila Mwislamu anaamini kuwa kile kilicho faradhi ni faradhi na kile kilicho haraamu ni haraamu tu. Na vile vile ni imani yetu ya msingi kuwa Allah swt ndiye muumba pekee na afanyake kwa kudura zake na wala hakuna mwingine anayeumba wala mwenye uwezo kama Allah swt. Iwapo Mwislamu atasema, "Mimi sitasali," basi itaeleweka kuwa yeye hatasali wakati huo au katika mahala hapo, au kwa sababu amekwisha kusali.Si haki kwa mtu yeyote kumtuhumu kuwa yeye hatasali kamwe.Kwa sababu, kuwa kwake Mwislamu itawazuia wengine wasimwite kafir au Mushrik. Hakuna mtu yeyeote mwenye haki kumwita Mwislamu ati ni kafiri au Mushrik kwa sababu amezuru makaburi, awaombaye waliokufa kwa msaada na utetezi au asemaye "Maombi yangu kadhaa wa kadhaa yakubaliwe," au "Ewe Rasulullah! Tafadhali naomba unitetetee mimi! "Kuwapo kwake Mwislamu kunadalilisha kuwa maneno na matendo yake yote yapo kwa mujibu wa imani iliyokubaliwa, halali na nia.

Imani potofu na maandiko ya Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab yatavunjika na kukanushwa katika misingi yake kwa nguvu za ufahamu na uamuzi kwa kutokana na maelezo yafuatayo. Katika kuongezea, kwa hakika kumeandikwa vitabu vingi mno kwa kuthibitisha kuwa Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab alikuwa ni mtu aliyepotoka, amewatukana Waislamu na amefanya njama zake zote za kuungamiza Uislamu undani mwake. Sayyid 'Abd ar-Rahma (r.a), Mufti wa Zabid, Yemen, ameandika kuwa itatosheleza kabisa kuandika Hadith ifuatayo ili kumthibitishia yeye kuwa alikuwa amepotoka: "Baadhi ya watu watatokezea Mashariki mwa bara la Arabia. Wao watasooma Qur'an tukufu. Lakini Qur'an tukufu haitawashuka kooni mwao. Wao wataiacha Islam kama vile mshale unavyouacha upinde. Wao wananyoa nyuso zao."Nyuso zao kunyolewa inamaanisha waziwazi kuwa ni wale watu ambao wanasemwa kupotoka ni wafuasi wao. Hakuna haja ya kupekua vitabu vingine baada ya kuisoma Hadith hii. Imeamriwa katika kitabu cha Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab kuwa wafuasi wake wanyoe ngozi ya kichwa pamoja na nywele na pembeni za uso. Amri kama hii haipatikani katika madhehebu zote sabili na mbili za Kiislamu.

MWANAMKE AMNYAMAZISHA IBN 'ABDU AL-WAHHABU

Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab vile vile aliwatolea wanawake amri ya kunyoa nywele zao zote. Alitokezea mwanamke mmoja, kwa ujasiri akamwambia: "Nywele ni pambo muhimu kwa mwanamke kama vile ilivyo ndevu kwa ajili ya mwanamme. Je amri hii inataka kuwafanya wanaadamu wajinyime opambo walilojaaliwa na Allah swt?" Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab hakuweza kumjibu mwanamke huyo. Ingawaje kuwa mambo maovu mengi katika imani potofu za Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab, zipo imani tatu kuu:

1. Yeye amefundisha kuwa matendo yanafanya sehemu ya imani na yeyote yule anayepuuzia faradhi (kwa mfano, hajatimiza sala mara moja kwa sababu ya uvivu au hajatoa Zaka kwa muda wa mwaka mmoja kwa sababu ya ubahili, ilhali anajua kuwa sala na zaka vyote hivyo ni faradhi) basi atageuka kuwa kafiri, na lazima auawe na mali yake yote igawiwe miongoni mwa Mawahhabi.

2. Wao wanaamini kuwa ni tendo la shirk kuwafanya Wasila Mitume(a.s) na Awliya'' na kuomba kwa kupitia wao kwa ajili ya kutimizika haja yake au kuwa katika hali ya amani dhidi ya khofu. Wao wanasema kuwa ni haramu kabisa kukisoma kitabu cha sala kiitwacho Dala'il al-Khairat.

3. Wao wanasema kuwa ni ushirikina kwa kujenga misikiti karibu na makaburi ya watu wema, kuwasha taa au vibatari katika misikiti hiyo kwa ajili ya wale wafanyao ibada au kwa kutoa misaada kutoa nadhiri ya kuchinja mnyama kwa ajili ya watu waliokufa. Kwao kila mojawapo la tendo hilo ni katika sura ya 'ibada ya mtu sambamba na Allah swt.

Makaburi yote ya Ahlu al-Bayt(a.s) ,Masahaba wote, ma Awliya'' na Mashahidi yaliteketezwa isipokuwa lile la Mtume Muhammad(s.a.w.w) wakati Sa'us ibn 'Abdu al-Aziz alipoishambulia Makkah na Madinah.Makburi hayakuweza kutambuliwa. Ingawaje wao wamejaribu hila zao za kutaka kuteketeza kaburi la Mtume Muhammad(s.a.w.w) , kwani wale waliokuwa wameinua mapanga na mashoka, waligeuka kuwa wehu au walipooza miili yao, na hivyo hawakuthubutu kutenda maovu yao hayo. Wao walipoishika Madinah,Ibn Sa'ud aliwakusanya Waislamu na akiwa tuhumu alisema: "Dini yenu kwa sasa imekamilshwa na Mawahhabi na Allah swt ameridhika nanyi. Wazazi wenu walikuwa makafiri na mushrik. Kamwe musiifuate dini yao! Waambieni watu wote kuwa wao walikuwa ni makafiri. Imeharamishwa kusiomama mbele ya kaburi la Mtume Muhammad(s.a.w.w) na kuomba. Nyie munaweza kusema: "As-salaamu 'ala Muhammad" wakati mpitapo katika msikiti. Hamuruhusiwi kuomba utetezi wake mbele ya Allah swt."

(2) MISHENI YA KWANZA YA MAWAHHABI

Abd al- Aziz ibn Muhammad , ambaye amewaua kikatili Wailsamu wengi kupita kiasi kwa kuueneza Uwahhabi, aliwatuma Mawahhabi watatu kwenda Makkah katika mwaka 1210 A.H. (1795). Maulamaa wa Ahl as-Sunna walikabiliana nao kwa kuwatolea Ayah za Qur'an Tukufu na Hadith sharifu kiasi kwamba Mawahhabi hao wawakilishi hawakuweza kujibu vyovyote vile. Wao hawakuwa na lolote lile la kuzungumzia isipokuwa kukubaliana na ukweli mtupu uliojitokeza mbele yao. Hao wawakilishi wa ki-Wahhabi waliandika ilani ndefu mno na kuzitia sahihi zao kuwa Ahl as-Sunna wapo katika njia ya haki na kweli na kwamba wao watatu walikuwa katika njia iliyopotoka, njia ya wendawazimu. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba kiongozi wao 'Abdu al-Aziz hakukuyatia maneno ya viongozi wake wa kidini yenye nasiha kwake masikioni mwake kwani yeye alichokuwa akikitaka ni matakwa yake ya kisiasa na alikuwa amekwishaufanya roho yake kwa ajili ya uchifu. Yeye aliongezea kuwatesa Waislamu siku baada ya siku nyuma ya pazia la kidini. Kwa hakika Waislamu waliangamizwa na kuteketezwa kwa uwezo wake wote. Mawahhabi hao watatu waliweka hoja ishirini za kuwashawishi Waislamu wakazi wa Makkah. Hoja zao hizo ishirini zimegawanyika katika makundi hayo matatu tuliyoyazungumzia. Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab alisema kuwa ni Ijtihad ya Imam Ahmad ibn Hanbal, kuwa ibada ni sehemu ya imani. Hatahivyo, Ijtehad zote za Imam Ahmad ibn Hanbal zilikuwa zimerekodiwa katika vitabu na Maulamaa wa Makkah walikuwa wakizijua zote, hivyo wao waliweza kwa urahisi mno kuwashawishi Mawahhabi hao watatu kuwa shutuma za Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab zilikuwa za uongo na potofu.

Mawahhabi hao watatu walikuwa na uhakika kuwa imani ya Maulamaa wa Ahlu as-Sunna yalikuwa ni sahihi nao hata walithubutu kusema: "Waislamu wa Makkah wanazuru makaburi ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) , 'Abdullah ibn Abbas na Mahjub (Mahjub Sayyid 'Abd ar-Rahman, alikuwa ni 'Alim mashuhuri katika zama zake, alifariki katika mwaka 1204 A.H. (1790) na alizikwa katika makaburi ya Mu'alla (makaburi ya Maqureishi) ) na huwa wakisema: 'Ewe Rasul - Allah!' au 'Ewe Ibn 'Abbas!' au 'Ewe Mahjub!' Hatahivyo, kwa mujibu wa ijtihad ya Imam wetu Muhammad ibn 'Abdu al-Wahhab, wale wasemao 'La ilaha Illallah Muhammadun Rasulullah,' lakini wanawaomba watu wengine hugeuka kuwa makafiri. Hivyo ni halali kuwaua na kuzichukua mali zao zote." Maulamaa wa Ahlu as-Sunna waliwajibu: "Kuzuru makaburi ya waja wapenzi wa Allah swt kwa ajili ya kuwafanya tawassul au kuwaomba watuombee, haimaanishi kuwa wao wanaabudiwa. Wao wanapowazuru, hapakuwi na nia ya kuwaabudu bali ni kwa madhumuni ya kumwomba Allah swt wawe wasila, yaani, kuwapitia na kuwafanya watetezi." Na wao walitoa hoja zao kwa vithibitisho kuwa imeruhusiwa na vile vile ni muhimu kuwachukua hao kama ndio sababu.

Zipo dalili na uthibitisho mwingi wa uhalali wa kuzuru makaburi ya Awliya' kwa ajili ya kuwafanya wasila au kuwaomba wawe wasila wakati wa kumwomba Allah swt hoja zetu: Ayah ya 35 ya Surah al-Maidah inasema, "Enyi Waumini! Mwogopeni Allah natafuteni Wasila wa kunifikia Mimi!" Vitabu vyote vya tafsiri vinaandika chochote au yeyote apendwaye au akubaliwaye na Allah swt huwa wasila. Ayah ya 80 ya Sura an-Nisa' inasema: "Yeyote amtiiaye Rasul basi amemtii Allah." Hii ni sababu kwa nini wasila katika Ayah iliyotangulia ni Rasulullah kwa mujibu wa maulamaa' wengi wa Kiislam. Kwa hivyo, inaruhusiwa kufanya wasila wa Mitume(a.s) na warithi wao - Awliya' na waja halisi Waislamu - na kujaribu kumkaribia Allah swt kwa kuwapitia hao. Iwapo ingalikuwa ni ukafiri au ushirikina kwa kuwataja au kuwaomba, wale ambao husali basi wote kwa pamoja watakuwa makafiri; basi Mawahhabi pia watakuwa makafiri kwa mujibu wa taarifa ya hapo juu - kama ilivyonakiliwa fatwa ya Muhammad ibn Sulaiman, kwani kila Mwislamu anatuma salaam juu ya Rasulullah na dua kwa ajili ya mtukufu Mtume(s.a.w.w) katika kila sala kwa kusoma"As-salaamu 'alaika ayyuhan Nabiyyu wa rahmat-Allah."

Zipo faida nyingi mno kwa kuzuru makaburi na kumwomba Allah swt kwa kuwafanya Awliya' kama wasila. Kwa sababu Hadith iliyotolewa na Ibn 'Askari na kunakiliwa katika Kunuz ad-daqaiq inasema, "Mwislamu ni kioo cha Mwislamu ndugu yake."Tunaelewa kutokana na Hadith hiyo kuwa roho ya Mwislamu mmoja ni kioo cha Mwislamu mwingine. Hivyo zinaonekana ndani mwao. Uwema unatoka kutoka roho ya walii kuingia katika moyo wa yule mtu ambaye anayemfikiria na kuwa wasila wake wakati wa kulizuru kaburi la wali huyo. Roho iliyo dhaifu inapata nguvu. Huu ni mfano wa vyombo viliwi vinavyounganishwa kwa bomba. Roho iliyo na nguvu au cheo cha juu ndiyo inayopungukiwa. Iwapo roho ya yule aliye kaburini itakuwa dhaifu basi roho ya aliyemzuru itakuwa imeudhika. Na hii ndiyo sababu kuu ya kuharamishwa kuzuru makaburi hapo katika kipindi cha mwanzoni cha Islam, kwa sababu makaburi hayo yalikuwa ni ya watu wale waliotoka katika kipindi cha ujahili wakati huo. Baada ya muda ilitolewa ruhusa kuzuru makaburi kwa sababu palikuwa pamezikwa Waislamu. Mtu atakuwa akifikiria Mtume Muhammad(s.a.w.w) au wali atakapokuwa akizuru kaburi lake. Ipo Hadith sharifu isemayo: "Allah swt huonyesha rehema wakati waja Wake watukufu wanapofikiriwa." Hivyo imeeleweka kutokana na Hadith hii vile vile kuwa Allah swt humpelekea rehema mtu anayezuru makaburi, na Yeye huzikubalia sala za waja Wake wale ambao huteremshiwa rehema Zake.Hivyo kusema kidhahiri kuwa: "Makaburi yasitembelewe. Awliya' hawawezi kuchukuliwa kama wasila," ni maoni yanayotakiwa kupuuzwa. Ipo Hadith tukufu isemayo: "Yeyote yule anayezuru kaburi langu baada ya kutimiza faradhi za Hijja basi atakuwa kama ametembelea mimi pale nilipokuwa hai," inakanusha imani hii katika misingi yake na hivyo kuonyesha umuhimu wa kuzuru makaburi. Hadith hii imetolewa kutoka Kunuz ad-daqa'iq.

Mawahhabi nao wanaleta mbele Hadith: "Wanalaaniwa wale wanawake ambao huzuru makaburi na wale wafanyao sala makaburini na wale ambao huwasha mishumaa juu ya makaburi," kama kisingizio cha kubomoa makaburi ya shakhsiyyah watukufu. Wao vile vile wandai kuwa mambo kama hayo hayakuwapo katika zama za Mtume Muhammad(s.a.w.w) na wanatoa Hadith ifuatayo, "Mambo ambayo hayapo katika zama zetu lakini yataletwa mbeleni na wala musiyanasabishe kwetu." Wawakilishi wa Mawahhabi walikubaliana na Maulamaa wa Ahlu as-Sunna kwa sababu majibu ya dai lao la pili yalikanusha madai yao.

(3) WAISLAMU WA TA'IF WAPORWA NA KUUAWA

Wakati Maulamaa wa Ahlu as-Sunna walipowanyamazisha Mawahhabi katika mwaka 1210 A.H. (1796), Maulamaa wa Makkah walitayarisha waraka na kutia sahihi zao ambamo waliandika Ayah za Qur'an Tukufu pamoja na Hadith sharif kwa kuthibitisha kuwa Uwahhabi ni njia iliyo tofauti na mbali na Islam, mtego wa hila na njama zilizotengenezwa na maadui wa Islam kwa ajili ya kuuteketeza Uislam undani mwake. Mawahhabi wale watatu waliokuwa wametubu kwa upotofu wao, walihakikisha na kuthibitisha waraka huo. Nakala za azimio hilo zilitumwa katika nchi zote za Kiislamu. Baadhi ya Mawahhabi wa Makkah walimwendea 'Abdu al-'Azizi, mtawala huko Darr'iyya, na kumwelezea kuwa wawakilishi wao hawakuweza kuwakabili Maulamaa wa Makkah na kwamba waraka wa azimio lao kuwa Uwahhabi ulikuwa ni upotofu na njama dhidi ya Islam, zimepelekwa kila nchi ya Kiislam. 'Abdu al-'Azizi ibn Muhammad ibn Sa'ud na wafuasi wake, waliingiwa na hasira kali kabisa dhidi ya Ahlu as-Sunna, waliishambulia Makkah katika mwaka 1215. Amir wa Makkah, Sharif Ghalib ibn Musa'id ibn Sa'id Effendi, aliwakabili vikali. Damu nyingi ilimwagika pande zote mbili. Sharif Ghalib Effendi hakuwaruhusu hao kuingia Makka, lakini makabila ya Waarabu kuzunguka Makkah walikubali Uwahhabi. Baina ya Idi mbili za mwaka huo huo, Sa'ud alituma jeshi katika mji wa Ta'if. Huko wao waliwatesa na kuwachinja ovyo Waislamu wanawake na watoto wa Ta'if.

Mateso na mauaji ya Ta'if wakiwemo wanawake na watoto yalifanyika kwa amri ya adui mkubwa wa Islam, brigadia mwovu kabisa aliyekuwa akiitwa 'Uthman al-Mudayiqi. Mtu huyu na Muhsin walikuwa wametumwa na Sharif Effendi kwenda Dar'iyya ambapo walitakiwa kuzungumzia mapatano ya awali ya kuwazuia Mawahhabi wasiizingire Madina na kutowatesa Waislamu. Lakini mnafiki huyu alikuwa ni jasusi kwa Sharif Effendi.Yeye alimhadaa mwenzake Muhsin, wakati wanaelekea Dar'iyya kuwa angeliweza kumpatia mafanikio mengi. Hao wawili walitoboa siri zao kwa Sa'ud ibn 'Abd al-'Aziz huko Dar'iyya. Sa'ud, alipowatambua kuwa wao walikuwa watumwa wake watiifu, aliwaweka waporaji chini ya ukamanda wao. Wao walikwenda hadi mahala paitwapo Abila karibu na Ta'if na huko wakampelekea Sharif Ghalib Effendi barua kuwa Sa'ud na wao, wasaliti hao wawili, walikuwa hawatambui uhalali wa maptano ya hapo awali na kwamba Sa'ud alikuwa akijitayarisha kuuzingira mji wa Makka. Sharif Ghalib Effendi aliwajibu katika lugha laini akiwashauri, lakini 'Uthman mkatili, alikuwa kwa hakika adui mkubwa wa Islam, alizichana barua. Yeye aliwashambulia Waislamu waliokuwa wametumwa na Amir na kuwaghalibu.. Ilimbidi Sharif Ghalib Effendi alirudi hadi ngome ya Ta'if na kuchukua hatua za kujihami. Huyu Mwahhabi katili aliweka kambi za majeshi yake huko Malis karibu na Ta'if mwishoni mwa mwezi wa Shawwal katika mwaka 1217 A.H. (1802). Yeye vile vile alioomba msaada kutoka mkatili Amir wa Bisha, Salim ibn Shakban, ambaye alikuwa na roho katili kuliko jiwe lililojaa uadui dhidi ya Uislamu. Kulikuwapo na tawala za kifalme takriban ishirini katika majangwa na kila falme alikuwa na kikosi cha Mawahhabi mia tano zaidi ya kikosi cha Salim mwenyewe kipatacho elfu moja.

Wakazi wa Ta'if wakiongozwa na Sharif Ghalib Effendi, waliwashambulia majeshi ya Mawahhabi huko Malis. Alifanikiwa kuwaua waporaji elfu moja na mia tano wa Salim ibn Shabkan. Salim pamoja na wafuasi wake walitoroka Malis. Lakini walikusanyika na wengine na kurejea kuishambulia Malis na waliupora mji mzima. Sharif Ghalib Effendi alikwenda Jeddah kutafuta msaada wa kijeshi. Wakazi wengi wa Ta'if walikuwa wamejaa kwa khofu na walitoroka kwa kisiri siri pamoja na vitu vyao vya majumbani. Ingawaje wale wakazi wa Ta'if waliokuwa wamejisitiri katika ngome, waliweza kuwashinda majeshi madogo madogo ya Mawahhabi waliokuwa wakijaribu kuwashambulia, wao walipeperusha bendera nyeupe ya kutaka usitihwaji wa vita baina yao kwani Mawahhabi walikuwa wakimiminika majeshi mengi. Wao walikubali kujisalimisha kwa masharti kwamba maisha na heshima zao hazitadhuriwa. Ingawaje maadui pia walikuwa wamekwisha nguvu na kudhoofika kwani nao pia walipata pigo kubwa la kuuawa na wengi walitoroka kutoka majeshi yao na walidhoofika pia, akatokea mwakilishi wa wakazi wa Ta'if, ambaye alikuwa mwovu na msaliti mkubwa, ingawaje alikuwa akiwaona Mawahhabi wanatoroka kwa kukimbia hapo, aliwapigia sauti kubwa kwa kuwaambia, "Sharif Ghalib ametukimbia kwa kuogopa! Na hivyo wana-Ta'if hawana nguvu ya kukabiliana nanyi! Wao wamenituma kuwaleteeni habarri kuwa wao wapo tayari kujisalimisha na kuisalimisha ngome nzima mikononi mwenu na wanawaombeni muwasamehe.

Mimi ninawapenda Mawahhabi. tafadhalini rudini! Nyinyi mumemwaga damu nyingi kupita kiasi na haitakuwa jambo la busra kwenu nyinyi kurudi bila ya kuikamata Ta'if. Ninaapa kuwa wana-Ta'if watajisalimisha wao na ngome hiyo. Wao watakubalia chochote kile mutakacho nyinyi." Kwa hakika lilikuwa ni kosa la Sharif Ghalib Effendi katika kuipoteza Ta'if bila maana. Iwapo angalikuwa amebakia Ta'if pamoja na Waislamu, basi isingalifika maafa hayoo. Kwa sababu waporaji ni waoga, Mawahhabi hakudhani kuwa wana-Ta'if watajisalimisha vile kirahisi. Lakini walipoona bendera ya kutaka amani juu ya ngome, walimtuma jasusi kuja kujua hali halisi iliyokuwapo ndani mwa ngome. Wana-Ta'if walimvuta ndani kwa kamba huyo mjumbe. Mjumbe huyo aliwaambia: "Kusanyeni mali zenu zote hapa na mujisalimishe kama munataka kuishi hai." Mali zao zote zilikusanywa na kurundikwa mahala pamoja kwa msaada wa Mwislamu mmoja aliyekuwa akiitwa Ibrahim. Mjumbe huyo alisema: "kwa hakika hii haitoshi." Aliendelea kuseam kuwa "Sisi kamwe hatuwezi kuwasameheni kwa haya tu, lazima mulete zaidi na zaidi!" Yeye aliwapa daftari na kuwaambia "orodhesheni majina ya wale wanaokataa kutoa mali zao! Wanaume wapo huru kwenda popote pale watakapo isipokuwa wanawake na watoto watafungwa kwa minyororo." Kwa hakika wote kwa pamoja walimwomba awe mlaini mwenye huruma kidogo, basi yeye aliongeza udhalimu na uovu wake. Ibrahim, alishindwa kuvumilia zaidi ya hapo na hivyo alimpiga kifuani kwa jine na kumwua. Wakati malumbano haya yanaendelea, Mawahhabi waliishambulia na ngome hiyo na hivyo waliweza kukwepa kulengwa mizinga na risasi. Wao walibomoa milango na kufanikiwa katika kuingia ndani ya ngome. Mawahhabi waliwaua wanawake, wanaume na watoto wote waliowaona na hata kuthubutu kuwaua watoto wachanga waliokuwa katika masusu yao. Mitaa ya mji ilijaa kwa mito ya damu. Wao walishambulia kila nyumba na kupora vyote vilivyokuwamo na popte pale walichokipata, wakawa wakishambulia kama vichaa na kikatili hadi usiku ulipoingia.

Wao hawakuweza kuzichukua nyumba za mawe upande wa mashariki wa ngone, hivyo walizishambulia nyumba hizo kwa risasi. Mlaghai moja wa Kiwahhabi alipiga kelele: "Sisi tunawasameheni! Munaweza kwenda popote pale mupendapo pamoja na wake na watoto wenu," lakini wao waliyapuuzia bila kujali. Wakati huo Mawahhabi waliwakusanya watu, ambao walikuwa wakijitayarisha kuondoka na kuhama, juu ya mlima na kuzizunguka zile familia halisi wa Waislamu, ambao wamekua katika mapenzi na udugu na wengi wao walikuwa ni wanawake na watoto, na kuwaweka wakafa kwa njaa na kiu kwa muda wa siku saba, na kuwatesa mno kwa visingizio, kupiga mawe na vitisho vya aina mbalimbali. Mawahhabi walimwita mmoja baada ya mwingine na kuwapiga na kuwauliza:

"Tuambieni pale mulipoficha mali zenu!" na walipiga makelele, "Siku yenu ya kufa inawadia!" kwa wale walioomba msamaha. Ibn Shakban, baada ya kuyakamdamiza majumba hayo ya mawe kwa muda wa siku kumi na mbili bila ya kufanikiwa kuyabonyeza, aliahidi kuwa wale wote watakaotoka nje ya nyumba zao na kujisalimisha pamoja na silaha zao, basi watasamehewa. Kwa hayo, Waislamu walimwamini na kutoka nje, lakini, wakiwa wamefungwa mikono yao migongoni mwao, wao waliburutwa na Ibn Shakban hadi juu ya mlima pale ambapo walikuwapo Waislamu wengine waliokuwa wameshikiliwa. Waislamu mia tatu na sitini na saba, wakiwemo wanaume, wanawake na watoto (Allah swt awarehemu) wote kwa pamoja walichinjwa chinjwa mlimani hapo. Mawahhabi waliwaachia wanyama wao wawakanyage Waislamu hao na hatimaye kuwaacha hapo bila ya kuwazika ili waliwe na ndege wa kuwinda kwa muda wa siku kumi na sita. Wao walifanya hujuma kubwa ya kupora mali za Waislamu katika kila nyumba, na waliweza kukusanya mali nyingi mno mpaka kukutokea kama mlima mbele ya lango la ngome hiyo na walimtumia Sa'ud asilimia ishirini ya yale yaliyoporwa na iliyobakia waligawana miongoni mwao. Wadhalimu na nvua za masika zilizoa mapesa na vito vya thamani mno na hapo kulibakia kiasi cha rial za dhahabu elfu arobaini tu, katika mikono ya Ahlu as-Sunna; kiasi cha rial elfu kumi ziligawiwa miongoni mwa wanawake na watoto, na vitu viliuzwa kwa bei ndogo kabisa.

Mawahhabi walizichana nakala za Qur'an tukufu na vitabu vya tafsir, Hadith na vitabu mbalimbali vya Kiislamu walivyovichukua kutoka maktaba, misikiti na majumbani mwa watu, na kuvitupa huku na huko. Wao walithubutu hata kutengenezea viatu kwa ajili miguu yao michafu vya majalada ya dhahabu ya Qur'an na vitabu vinginevyo. Kwa hakika zilikuwapo zimeandikwa Ayah tukufu za Qur'an juu ya majalada hayo. Majani (makurasa) ya Qur'an tukufu zilikuwa zimetupwa ovyo mitaani mwa mji wa Ta'if kiasi kwamba kulikuwa hakuna hata nafasi ya kuuweka mguu juu ya ardhi ya mji wa Ta'if. Ingawaje inasemekana kuwa Ibn Shakban alikuwa ametoa amri ya kutokuzichana nakala za Qur'an Tukufu, lakini hao Mawahhabi waporaji wa majangwani hawakujua Qur'an ni nini, na hivyo walizichana chana nakala zote walizozipata na kuzikanyaga kanyaga ovyo. Inajulikana kuwa ni nakala tatu tu za Qur'an Tukufu na nakala moja tu ya Sahih al-Bukhari ndizo zilizo salimika kutokana na hujuma na uporaji wa Mawahhabi katika mji mkubwa wa Ta'if.