HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 20%

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2 Mwandishi:
Kundi: VITABU VYA HADITHI

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 21309
Pakua: 4201

Maelezo zaidi:

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 21309 / Pakua: 4201
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.NA MA-IMAMU a.s.V0L 2

Mwandishi:
Swahili

2

HADITH ZA MTUME (s.a.w.w) NA MA-IMAMU(a.s)

SEHEMU YA PILI

HARAKISHENI KUOA

825. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Kwa hakika bikira ni kama matunda ya mtini; matunda hayo yanapokomaa na kama hayakuchumwa, basi mwanga wa jua una waharibu na upepo unawatawanya. Hivyo bikira wapo katika hali hiyo hiyo. Na pale wanapo tambua kile anachohisi mwanamke, basi hakuna dawa yao yoyote isipokuwa kuolewa na bwana. Iwapo wao hawataozwa, basi hawataweza kuepukana na uchafuzi, kwa sababu wao ni binaadamu, vile vile. (kwa sababu wao pia wanahisia na matakwa kama binaadamu wengineo) ." [42]

826. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Kijana yeyote anayeoa mwanzoni mwa ujana wake, Shaytani wake analia na kujuta kabisa kuwa yeye ameikomboa sehemu mbili ya tatu ya imani yake kutoka kwa Shaytani ." [43]

827. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Ewe kijana! Iwapo kuna yeyote miongoni mwenu anayeweza kuoa, basi afanye hivyo, kwa sababu ni vizuri kwa macho yenu (msiwachungulie wanawake wengine) na inahifadhi sehemu zenu za siri (ili muendelee kubakia wacha Allah swt) ." [44]

828. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Allah swt ameharamisha hali ya kutokuoa, na amewaharamishia wanawake kutokujitenga bila kuolewa (hivyo lazima na wanawake pamoja na kuwa wacha Allah swt lazima waolewe) ." [45]

KUWASAIDIA NA KUINGILIA KATI KATIKA NDOA ZILIZO HALALI

829. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Yeyote yule anayefanya jitihada za kuwaunganisha Waislam wawili katika ndoa iliyo halali ili waweze kuoana kwa sheria takatifu za Allah swt, basi Allah swt atamjaalia kwa ndoa hiyo Hur ul-'Ain mwenye macho meusi katika Jannat, na atamjaalia thawabu za ibada za mwaka mmoja kwa kila hatua atakayochukua au neno atakalolizungumza ." [46]

830. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Ibada bora kabisa ni kule wewe kuingilia kati ya watu wawili kwa ajili kuoana ki halali kwa mujibu wa amri za Allah swt ."[47]

831. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) : "Katika siku ya Qiyamah, ambapo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha rehema za Allah swt, basi kutakuwa na aina tatu ya watu ambao watapewa kivuli hicho cha 'Arish ya Allah swt: Mtu yule aliye sababisha kusaidia kufunga ndoa ya Mwislamu mwenzake, au yule ambaye amemhudumia, au yule ambaye amemfichia siri zake kwa ajili ya suala lake hilo ."[48]

832. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Yeyote yule anayewaunganisha wasioolewa katika ndoa basi wao watakuwa miongoni mwa wale watu ambao Allah swt atawatazama kwa rehema Zake siku ya Qiyamah ."[49]

833. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) : "Katika siku ya Qiyamah, kutakuwa na kivuli maalum cha Allah swt ambamo hakutakuwapo na wengine isipokuwa Mitume (a.s) au vizazi vyao, au Muumin anayemfanya huru mtumwa, au Muumin anayelipa deni la muumin mwingine, au Muumin ambaye anawaunganisha waumini ambao katika ndoa (waumini ambao hawajaoana )."[50]

834. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Yeyote yule anayejaribu kuwaunganisha Waislam wawili katika ndoa kwa mujibu wa sheria za Allah swt, basi Allah swt atampatia Hur ul-'Ain elfu moja (wahudumu wanaokaa Jannat wakiwa na macho meusi makubwa) katika ndoa na ambapo kila mmoja wao atakuwa katika ngome ya Malulu na Almas na Rub i." [51]

MWANAMKE NA MAHARI.

835. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Ubashiri mbaya wa mwanamke ni kuwa mahari yake ya juu kabisa na ghadhabu zake ." [52]

836. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) Amesema: "Waizi huwa wa makundi matatu: La kwanza wale wanaozuia kutoa sadaka; pili wale wanao jiwekea mahari ya mwanamke na kujihalalishia kwa ajili yao wenyewe; tatu wale wanaochukua mikopo na hawajaamua kurudisha mikopo hiyo kwa ajili ya kulipa madeni yao ."

837. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Kwa hakika moja ya baraka za Allah swt kwa mwanamke ni mahari yake kutokuwa juu, na moja ya maovu ya mwanamke ni kuwa na mahari kubwa ."[53]

838. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Msifanye mahari ya wanawake ikawa nzito, kwa sababu hiyo inaleta uhasama na uadui ."[54]

839. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Kuna madhambi maovu kabisa ya aina tatu: Kuwatesa wanyama wakati wa kuwachinja, Kuchelewesha na kutokulipa mahari ya mwanamka, na Kutokulipa mishahara ya wafanyakazi ."[55]

AFADHALI MAHARI NDOGO.

840. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Ndoa ile imebarikiwa ambayo ina gharama ndogo ." [56]

841. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Wanawake bora kabisa katika umma wangu ni wale ambao nyuso zao ni zenye urembo na mahari yao huwa ni ndogo ." [57]

842. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Oeni hata kama mtakuwa na pete ya chuma (kama mahari) . [58]

843. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule anayetoa hata kiasi cha tonge moja ya nafaka au tende kama mahari (kwa kukubaliwa na mwenzake), basi kwa hakika ndoa yake ni halali na sahihi kabisa ." [59]

844. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). alitoa mahari ya Zirah moja yenye thamani ya Dirham thelathini katika ndoa ya binti yake Fatimah az- Zahra (a.s). akiwaolewa na Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) ."[60]

NDOA KWA KUJALI IMANI NA UAMINIFU

845. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . bila kujali daraja la kizazi cha mtu, amesisitiza na kusema: "Mtu yeyote anapokuletea habari za kutaka kukuoa na wewe kwa kuridhika unakubalia, kwa adabu zake na dini yake, basi ungana naye kwa ndoa. Na iwapo hutafanya hivyo, basi wewe utakuwa umesababisha fitina na ufisadi mkubwa kabisa juu ya ardhi ." [61]

846. Imam Jawad(a.s) . ameandika katika barua: "Mtu yeyote akutakaye wewe katika ndoa anayetaka kukuoa na wewe unakuwa umeridhika na dini na uadilifu wake, basi ungana naye kwa ndoa ."[62]

847. Siku moja mtu mmoja alimwambia Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa: "Yeye alikuwa na binti wake na alimwuliza Imam(a.s) . kuwa yeye amwoze binti wake kwa nani, kwa hayo Imam(a.s) . alimjibu: Muoze binti wako kwa yule ambaye ana imani na ni mcha Allah swt: Kwa sababu atampenda na kumheshimu huyo binti wako, na iwapo yeye atakuwa mkali juu ya binti yako, basi hatamdhuru."[63]

848. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Yeyote yule atakaye muoza binti wake kwa mtu ambaye si mcha Allah swt basi kwa hakika amevunja uhusiano wake pamoja naye ." [64]

AZMA YA MWANAMME KATIKA NDOA

849. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa urembo wake tu (bila ya kujali imani yake), basi yeye hataambulia kile alichokitaka; na yeyote anayeoa mwanamke kwa ajili ya mali na utajiri wake (basi Allah swt atampa hiyo mali na utajiri tu peke yake.) Kwa hivyo ni juu yenu nyie kutafuta mwanamke aliye katika dini na mcha Allah swt ." [65]

850. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa matarajio ya utajiri, basi Allah swt anampa utajiri na mali peke yake ."[66]

851. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Yeyote anayeoa mwanamka kwa utajiri wake, Allah swt humwachia hayo tu; na yeyote anayeoa mwanamke kwa ajili ya urembo wake na uzuri wake, basi yeye atayaona yale ndani ya mwanamke yale asiyoyapenda; lakini yule anayeoa mwanamke kwa misingi ya imani na dini yake, basi Allah swt atamjazia kila aina ya sifa ya mambo hayo kwa ajili yake ." [67]

852. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa ajili ya urembo wake tu, basi Allah swt atamjaalia uzuri wake na uzuri wa mwanamke huyo utamdhuru na kumletea matatizo huyo mwanamme ." [68]

853. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) : "Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt, na kuungana naye kwa wema basi Allah swt atamjaalia taji la heshima na ufanisi ."[69]

854. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Msioe wanawake kwa ajili ya urembo wao tu kwa sababu urembo wao unaweza kusababisha wale wasiwe wacha Allah swt wala si kwa ajili ya mali yao kwa sababu mali yao inaweza ikawasababisha wakawa wasiwe watiifu; lakini muwaoe kwa misingi ya imani ya dini yao ." [70]

KUTAFUTA RIZIKI

855. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Amelaaniwa, amelaaniwa yule ambaye hawajali wale anaotakiwa kuwalisha ambao wanamtegemea, kwa hakika amelaaniwa kwa mara nyingi ." [71] .

856. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Mwanamme yule ambaye anafanya subira kwa hasira mbaya za mke wake, na anatafuta ile subira kwa Allah swt, basi Allah swt anamjaalia thawabu na ujira mkubwa sana kwa wale wenye kushukuru ." [72]

857. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Yeyote yule anayevumilia taabu za kutafuta pesa kwa ajili ya kumtimizia haja ya mke wake, ni sawa na yule anayepigana vita vya Jihadi katika njia ya Allah swt ."[73]

858. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Ni dhambi moja kubwa kabisa inamtosheleza mtu yule ambaye anawapuuzia wale wanaomtegemea yeye kwa kuwapatia riziki. (Dhambi hili kubwa linaweza kumteketeza huyo mtu) ."[74]

859. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Mtu mwenye furaha ni yule ambaye anasimamia na kuratibu maswala ya mke na watoto wake ."[75]

WAKE KUWAWIA WEMA WAUME ZAO

860. Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura Ar-Rum, 30, Ayah ya 21. Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.

861. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alipopata habari kutoka kwa Ummi Salama kuhusu Uthman ibn Mazu'un, basi aliondoka kuelekea wafuasi wake na huku akiwaambia kuwa: "Je nyie mnajitenga na wake zenu? Kwa hakika, mimi mwenyewe huwaendea wanawake, huwa ninakula chakula nao mchana, na kulala nao usiku. Kwa hakika yeyote yule anayejitenga na maisha ninavyoishi mimi basi hatakuwa miongoni mwangu yaani atakayeipa mgongo ." [76]

862. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Yeyote yule anayeikataa ndoa na kuipuuzia kwa hofu ya gharama itakayo mfikia, basi anaondoa imani yake juu ya Allah swt kwani inamaanisha kuwa yeye hamwamini Allah swt ."[77]

863. Imeripotiwa kutoka kwa Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . kuwa: "Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . kwa kumjibu wa mwanamke ambaye alikuwa hataki aolewe ili abaki bila kuolewa, kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . alimjibu " usifanye hivyo, kwa sababu iwapo ndivyo ingekuwa ni kutukuka huko, basi Bi Fatimah az-Zahara(a.s) . angekuwa ni mwanamke wa kwanza kutokuolewa kuliko wewe (kwa sababu yeye alikuwa na wadhifa mmoja mkubwa sana akiwa ni binti wake Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na kwa hakika hakuna mwanamke yeyote duniani ambaye anaweza kuwa na utukufu zaidi ya Bi Fatimah az-Zahara(a.s) ."[78]

864. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . ameripotiwa kusema kuwa: "Wanawake watatu walimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . na kusema kuwa waume zao wamekataa kula nyama au kutumia manukato au kuwakaribia wake zao. Na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . (Akikaripia matendo yao) alikwenda haraka juu ya Mimbar na baada ya Kumhimidi Allah swt alisema: Je wamekuwaje baadhi ya watu kuwa hawataki kula nyama, na wala hawataki kutumia manukato, na wameacha kuwakaribia wake zao?." [79]

865. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . Amesema: "Kuwa wakati mke wa Uthman ibn Mazu'un, alipomwelezea Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . kuwa bwana wake daima amekuwa akifunga saumu siku za mchana na kusali wakati wa usiku alikuwa hajali maisha yake na wala alikuwa hamjali mke wake pia, kwa kusikia hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . aliondoka akaenda moja kwa moja nyumbani kwake na akamkuta yuko anasali. Wakati Uthman alipomaliza sala zake, Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . alimwambia: "Ewe Uthman, Allah swt hakunituma mimi kuwa Ruhbani (Kuwa kama Mapadre kwa kikirsto) bali amenituma mimi kwa ajili ya dini iliyo rahisi ambayo inalinda haki za mwili na roho. Mimi hufunga saumu, huwa nikidumisha sala, na huwa nikichanganyikana na kujumuika pamoja na familia yangu kwa ukamilifu. Na yeyote yule anayependa Sunnah yangu na mwenendo wangu basi lazima afuate mwenendo wa maisha yangu, na Sunnah yangu; Na kwa hakika ndoa ikiwa ni mojawapo ya Sunnah zangu ." [80]

KUWAHESHIMU WAKE ZENU

866. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . amenakili kutoka kwa baba yake hadi kufikia kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Amelaaniwa mwanamke yule ambaye anamfanya mme wake akasirike, na mwanamke mwenye furaha ni yule ambaye humridhisha bwana wake kwa furaha ." [81]

867. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Yeyote yule aliye na wanawake wawili na kama hawawii kwa haki kwa nafsi na mali yake miongoni mwao, basi siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa amefungwa kwa minyororo na nusu ya mwili wake hautakuwa wima hadi kule atakapo tumbukizwa Jahannam. " [82]

868. Imam Muhammad al-Baqir(a.s) . Amesema: "Yeyote yule anayeoa mwanamke lazima amheshimu kwa heshima zote, kwa sababu mwanamke kwa mtu yeyote anamaanisha raha na mustarehe, kwa hiyo yeyote anayemwoa mwanamke asimharibu wala kumdhalilisha yeye (Kwa kutojali haki zake zinazostahili) ."[83]

869. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Kwa hali yoyote ile na katika sura yoyote ile lazima mpatane na wake zenu, na muongee nao vyema kwa kutumia maneno mema mazuri, na hivyo matendo yao yatakuwa mema na watabadilika kuwa wake wema na wazuri kwa ajili yenu ."[84]

870. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) . kwa kumnakili baba(a.s) . yake ambao wamemnakili Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . akisema: "Kiasi chochote cha imani cha mtu kitakachoongezeka basi na kumjali kwa mke wake pia kutaongezeka ." [85]

871. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . kuwa: "Kutokana na vitu vya duniani, mimi huwajali wanawake na manukato zaidi, lakini ibada ni nuru ya macho yangu, (mapenzi na ibada ya Allah swt) ." [86]

MWANAMKE KUMRIDHISHA MUME WAKE

872. Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) . amesema: "Siku ya Qiyamah mwanamke hataokolewa na hatapata uokovu wowote kutoka kwa Allah swt bila ya idhini ya bwana wake ."[87]

873. Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) . ameripoti kutoka kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) . ambaye amesema: "Bora wa wanawake miongoni mwenu ni yule ambaye ana sifa tano Mwanamke asiye na matatizo, Mtiifu, Mnyenyekevu, Mwenye matumizi madogo Mvumilivu wakati bwana wake anapokasirika Mshiriki mwema na msaidizi wakati wa shida, Mpaji wa hima kwa bwanake anapokuwa amezongwa na mawazo na shida Mtunzaji wa mhifadhi wa nyumba ya bwana wake anapokuwa hayupo. Kwa hivyo mwanamke kama huyo ni wakala wa mawakala wa Allah swt na kwa hivyo mawakala wa Allah swt hawatakuwa wenye hasara (yeye anapata matumaini sahihi).[88]

874. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . amesema: "Mwanamke yeyote yule anayepitisha usiku ambapo mume wake amemkasirikia na kumghadhibikia, ibada zake hazikubali hadi pale huyo mwanamke atakuwa amemridhisha bwana wake ."[89]

875. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . amesema: "Haki za bwana kwa mke wake ni kuziwasha taa, kutayarisha na kupika chakula na kumpokea mume wake anapokuja mlangoni kwa maneno mazuri na kamwe asimkatalie mume wake anapomhitaji yeye binafsi (kujamiiana) isipokuwa anapokuwa sababu zake . " [90]

876. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Mwanamke kamwe hatatekeleza haki za Allah swt hadi yeye ametekeleza haki za mume wake ." [91]

877. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Siku moja mwanamke mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). na kumwambia: 'Ewe Mtume wa Allah swt ! Je bwana haki gani kwa mke wake ?' Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). alimjibu: Mwanamke amtii mume wake na wala asimuasi ."[92] .

TALAKA NA ATHARI ZAKE

878. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Amesema: "Kwa hakika Allah swt hapendi kabisa au humlaani mwanamme au mwanamke yeyote ambaye anakuwa na nia ya talaka au anaoa kwa ajili ya kustarehe tu ." [93]

Na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . ameirejea kauli hii mara tatu kusisitiza kuwa mwanamme yeyote yule anayempa mke wake talaka kwa ajili ya kuoa mwanamke mwingine na kutaka kustarehe starehe za ndoa mwanmke mpya na vile vile mwanamke yeyote yule anayeomba talaka kwa sababu kama hizo hizo na kuolewa na mwanamme mwingine, basi wote hawa wanajitumbukiza katika laana za Allah swt.

879. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Wanawake katika umma wangu ambao wanafuata sunnah nne (mambo mema manne) basi wataingizwa Jannat: Iwapo yeye atalinda utukufu wake, Anamtii mme wake, Anatimiza sala zake tano, na Anafunga saumu katika mwezi wa Ramadhani ." [94]

KUPELEKA MACHO CHINI NA KULINDA HESHIMA

880. Allah swt anatwambia katika Qur'an Tukufu, Sura An Nuur, 24, ayah ya 30. Waambieni waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Allah swt anazo khabari za wanayo yafanya.

881. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . anatuambia: "Kutazama kiharamu kwa wale walio haramishwa kwetu ni sawa na mshale kutoka upinde wa Shaytani ambayo imejaa sumu. Yeyote anayejiepusha naye kwa ajili ya Allah swt, na wala si kwa sababu zinginezo, basi Allah swt atampa imani ambamo yeye ataipata furaha ndani mwake ."[95]

882. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Zinaa ya macho ni kuangalia yale yaliyo haramishwa, kwa mtazamo wa matamanio, Zinaa ya midomo ni kuwabusu wale walio haramishwa (wasio maharimu), na Zinaa ya mikono ni kuwagusa (mikono na sehemu zingine za wale walio haramishwa Wasio-maharimu) bila kujali iwapo atakuwa na hamu au hatakuwa na hamu ya kujamiiana ."[96]

883. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). amemlaani yule mtu ambaye anaangalia sehemu za siri za mwanamke ambaye si halali kwake, na vile vile ememlaani yule mtu ambaye anafanya khiyana pamoja na mke wa ndugu yake, na vile vile yule mtu ambaye anachukua rushwa kwa watu kwa msaada wanaohitaji kutoka kwake ."[97]

MWANAMKE NA KUJIPAMBA

884. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Neno asemalo mwanamme kumwambia mke wake: 'Nakupenda basi kamwe halitatoka moyoni mwa mke wake '." [98]

885. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) : "Haijali chochote au vyovyote vile mwanamke ajirembavyo kwa ajili ya bwana wake ."[99]

886. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) : "Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w). ameharamisha kujiremba kwa mwanamke kwa ajili ya mwanamme mwingine mbali na mume wake mwenyewe na akasema: 'Na kama atafanya hivyo, basi ni haki ya Allah swt kumchoma moto katika Jahannam. (Hadi hapo atakapofanya Tawba )"[100]

887. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Yeyote yule anayezidisha mapenzi yetu (Ahlul Bayt (a.s).) basi na atazidisha mapenzi yake kwa mke wake vile vile ."[101]

888. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Bora katika wake zenu ni yule ambaye ni mcha Allah swt na mtiifu kwa mume wake katika mapenzi na kujirembesha (lakini sio kuwavutia wanaume wengine) ." [102]

ZINAA NA ATHARI ZAKE MBAYA

889. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Imeandika katika Tawrat: Mimi ni Allah swt, muuaji wa wauaji na muadhibu wa wazinifu ." [103]

890. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) : "Ziko athari sita za zinaa, tatu ambazo zinapatikana humu duniani na tatu zitapatikana huko akhera. Zile zitakazoonekana duniani: Itaondao heshima ya mtu na kumdhalilisha; Itamfanya mtu awe maskini; na Itafupisha umri wa maisha yake (yaani atakufa haraka). Na zile zitakazo patikana Akhera ni: Adhabu za Allah swt, Hali ngumu kabisa katika utoaji wa hesabu, na Kutumbukizwa katika Jahannam kwa ajili ya milele ."[104]

891. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) . Kutokea Tawrat: "Kuwa enyi watu msizini kwa sababu mkifanya hivyo wake zenu pia watafanya vivyo hivyo. Kile mkipandacho ndicho mtakacho kivuna. (kila ufanyavyo na wewe utafanyiwa hivyo) ." [105]

892. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "yeyote yule amkumbatiaye mwanamke, ambaye ameharamishiwa kwake, basi atafungwa kwa minyororo ya mioto pamoja na Shaytani na wote kwa pamoja watatupwa katika Jahannam ." [106]

893. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) . wakati mmoja aliulizwa na 'Amar ibn Mussa kuhusu kufanya tendo la kujamiiana pamoja na wanyama au kujitoa manii kwa mkono au kwa kutumia sehemu zinginezo za mtu mwenyewe, na Imam(a.s) . alimjibu: "Hali yoyote katika hizi na vyovyote vile ambavyo mwanamme humwaga maji yake, inachukuliwa kuwa ni zinaa (na imeharamishwa) ."[107]

894. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) : "Amelaaniwa! Amelaaniwa yule mtu ambaye anafanya tendo la kuwaingilia wanyama ." [108]

895. Amesema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w); "(Zinaa miongoni mwa jamii moja) mwanamme kwa mwanamme au mwanamke kwa mwanamke (ni zinaa) ."[109]