• Anza
  • Iliyopita
  • 6 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 17144 / Pakua: 3473
Kiwango Kiwango Kiwango
UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

Mwandishi:
Swahili

4

UTUMWA KATIKA MTIZAMO WA KIISLAMU NA KIMAGHARIBI

BIASHARA YA WATUMWA YA AFRIKA YA MASHARIKI

Kama ilivyokuwa Afrika ya Magharibi, biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki ilikuwa mashuhuri na ilianzishwa kikamilifu na kutokana na maendeleo na jitiha-da za nchi za Kikristo za Ulaya. Bwana E. A. Alpers anaandika kwenye "African Slave-Trade (Biashara ya Utumwa ya Afrika): 118. Boswell, J, Life of Johnson (N.Y. Modern Library Edition, 1965) Uk. 365 "Ushahidi zaidi kwamba biashara ya watumwa kwa vyovy-ote vile ilikuwa mashuhuri katika Afrika ya Mashariki kabla ya karne ya kumi na nane, imeletwa na Wareno. Hakika Wareno, wakiwa ndiyo waasisi (waanzilishi) wa Atlantic Slave-Trade, wangejaribu kuendeleza biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki kama wangeikuta tayari ipo na imekwisha shamiri. Lakini maandiko ya mwanzo ya Wareno yanataja tu biashara ya watumwa kwa kupitia tu. Lililokuwa muhimu zaidi ni wale wafanyabiashara za dhahabu na pembe za ndovu walizipeleka Arabuni na India. Wavamizi wa Kireno walielekeza juhudi zao kwenye bidhaa hizo wakati wa karne ya kumi na sita na kumi na saba, sio tu kwenye pwani ya Kenya na Tanzania, bali pia katika Msumbiji na Zimbabwe. Hata nta na ambari zinaonyesha zilikuwa bidhaa muhimu zaidi kuzidi watumwa wakati mrefu sana wa kipindi hiki. Kwani tofauti na wakoloni katika nchi ya Amerika, Wareno kamwe hawakuanzisha uchumi wowote wa kilimo huko India. Biashara ya watumwa ya Wareno kutoka Msumbiji kwenda India kwa nadra sana ili-fika idadi ya watu elfu moja katika kipindi cha mwaka mmoja wowote ule, na kwa kawaida ilikuwa chini ya nusu ya idadi hiyo. Huko Brazil ilikuwa haramu kufanya biashara ya watumwa hadi mwaka 1645, na kamwe haikuli-tiliwa maanani hadi mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa. Hadi mwaka wa 1753, wakati misingi ya biashara mpya ya watumwa ilikuwa inawekwa Afrika ya Mashariki, palikuwe-po na jumla ya watumwa 4399 tu wa Kiafrika katika India yote yaWareno.

"Misingi hii ni ipi? Licha ya mahusiano ya muda mrefu baina ya Waarabu na Afrika ya Mashariki, biashara ya watumwa haikutiliwa matumaini na Wafaransa. Kwa mujibu wa tarakimu rasimi, zaidi ya watumwa 1,000 walikuwa wanasafirishwa kila mwaka. Wafaransa, waki-fanya magendo kwa ajili ya kukwepa kodi ambazo zilitozwa Msumbiji, labda waliongeza idadi na kufika angalau 1,500. Inawezekana ni idadi ile ile ilichukuliwa kutoka Ibo wakati wa muongo huu. Kwa hiyo Wareno kule Msumbiji na Ibo (na baadaye Quelimane, karibu na mdomo wa mto Zambezi - unapoingilia baharini) walijishughulisha na sera ya biashara ya watumwa na hawakurudi nyuma, wakaendelea nayo hadi kukomeshwa kwake. Biashara ya watumwa ilizidi kupamba moto mnamo miaka ya themanini, hasa zaidi baada ya kumalizika vita ya uhuru wan chi ya Amerika. Katika miaka ya sabini, wafanya biashara ya utumwa wachache wa Kifaransa walichukua mizigo kutoka Msumbiji kwenda visiwa vya West-Indies, kwa sababu waliiona hasara ilikuwa inaongezeka katika wakati wa kutafuta bidhaa zao zinazohamashika kwenye pwani ya Guinea. Sasa, wakati wa amani, kwa mashindano makubwa zaidi ya kutafuta watumwa katika Afrika ya Magharibi, ilifunguliwa njia kwa ajili ya upanuzi mkubwa wa biashara ya watumwa ya Waamerika kutoka Afrika ya Mashariki. Wakati huo huo meli za Wareno pia zilianza sehemu ya kufaa (ingawa ilikuwa bado ni ya kufuata) katika biashara ya watumwa kwenda kisiwa cha Mascarene. Tarakimu rasimi kutoka Msumbiji peke yake zinaonyesha kwamba tangu 1781 hadi 1794 jumla ya watumwa 46,461 walipakiwa kwenye meli za Kireno na za kigeni, ambazo karibu zote zilikuwa za Wafaransa. Ikijumlishwa na idadi ndogo ya magendo, angalau watumwa 4,000 lazima walikuwa wanaondoka Msumbiji wakati wa kipindi hiki kila mwaka." 119. 119. Alpers, op. cit., uk. 5-6.

Ilikuwa katika hali hii ambayo Waarabu walipanua msaada wao kuwasaidia hawa wafanyabiashara ya utumwa wa Kikristo. Mwandishi huyo huyo anasema: "Baada ya Waarabu wa Oman kuitika wito wa baadhi ya watawala wa Kiswahili wa miji ya pwani na kwa msaada wao waliwatoa Wareno kutoka Mombasa mnamo 1698 na sehemu zingine muhimu za mbali, wao wenyewe walikuwa wanyonge sana kushughulika na jambo lingine zaidi ya kuwasumbua na kuwaibia watu hao hao waliowaomba msaada wao; lakini baada ya familia ya Busaid ilipowapindua Yarubi na kuanzisha utawala wao katika Oman mnamo 1744, wali-weza kuanza unyonyaji wa kiuchumi wenye faida kutoka kwa watu wa Afrika ya Mashariki. Kama walivyofanya wafanya biashara wote wa zamani sehemu ya pwani, lengo lao kubwa na la msingi ni kupata pembe za ndovu, lakini kuanzia hapo pia tunaweza kuona ongezeko katika biashara ya watumwa. "Hata hivyo, hakuna takwimu sahihi zozote zile zenye kuonyesha kuhusu ukubwa wa biashara ya utumwa iliy-ofanywa na Waarabu katika karne ya kumi na nane. Dalili ya kwanza iliopo inatoka kwa mfanya biashara ya watumwa wa Kifaransa aitwaye Jean Vincent Morice, ambaye alifanya biashara Zanzibar na Kilwa, ambayo ilikuwa bandari muhimu ya watumwa katika pwani, mnamo miaka ya 1770. Mnamo tarehe 14, September, 1776, Morice alifanya mkata-ba na Sultani wa Kilwa kwa ununuzi wa angalau watumwa 1,000 kwa mwaka. Katika misafara mitatu kabla ya kuutia sahihi mkataba huu, Morice alikwisha nunua watumwa 2325 kwa ajili ya kuwasafirisha nje. Morice hatuambii Waarabu walikuwa wakiwachukua watumwa wangapi kutoka pwani kila mwaka, lakini kwa wazi aliona kuwa ilikuwa biashara kubwa kwa viwango vya Kifaransa. Inaonekana ni sawa kusema kwamba angalau watumwa 2000 walikuwa wanachukuliwa kwa mwaka katika kipindi hicho. Kwa hiyo, licha ya kwamba Wafaransa hawakutawala biashara ya watumwa hapa kama walivyofanya Msumbiji, walikuwa kichocheo kwa mahitaji ya soko la watumwa katika kipindi ambacho biashara ya Waarabu ilikuwa bado ndiyo inakua katika uchanga wake.

Juhudi za Ufaransa ziliendelea hadi miaka ya 1780, lakini mnamo mwishoni mwa karne hiyo, juhudi hizi zilionyesha zilikwisha pungua sana umuhimu wake kuliko biashara ya Waarabu. Mambo kadhaa mapya yalisababisha kuongezeka mahitaji ya watumwa kutoka Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya kumi na tisa. Katika eneo la mamlaka la pwani ya Ureno, palikuwepo na ongezeko la juu sana katika biashara ya utumwa kwenda Brazil. Hii ilisababishwa na kuondolewa kwa familia ya kifalme ya Kireno kutoka Lisbon kupelekwa Brazil wakati wa Vita za Napoleon. Ruhusa maalum zili-tolewa kwa Wabrazil na mara biashara inayoshamiri katika watumwa ikawa inaendeshwa kupitia Rasi ya Tumaini Jema huko Afrika ya kusini. 1 "Sasa ni ukweli unaokubalika miongoni mwa wataalam wa historia makini wa Afrika ya Mashariki kwamba njia ndefu za biashara kati ya bara na pwani zilianzishwa hasa zaidi kwa kutumia ujasiri na moyo wa kujituma wa Waafrika. Kwa maneno mengine njia za biashara zilibuniwa na Waafrika kutoka bara kwenda pwani, wala si Waarabu, au Waswahili, ambao walisafiri kutoka pwani kwenda bara kupitia sehemu zisizojulikana. 120. Ibid uk. 7-8. Wafanya biashara wa Kiswahili walianza tu kutelekeza usalama wa pwani mnamo nusu ya pili ya karne ya kumi na nane, na walisafiri kufuata njia safi ambazo ziliendelezwa kwa miongo mingi kabla yake. Ni baada tu kuanza karne ya kumi na tisa ndipo wafanya biashara wa Kiarabu wali-jasiri kufuata njia hiyo." 121. Wayao ambao walikuja kuwa wafanya biashara makini sana wa Kiafrika wa biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki, hivyo walikuwa na desturi ya muda mrefu ya kubeba pembe za ndovu na bidhaa zingine halali kwenda pwani miongo mingi kabla ya mahitaji ya pamoja ya Wafaransa na Waarabu kutaka watumwa yalipoelewe-ka."122.

"Katika Afrika Magharibi njia hizi ziliendeshwa kwenda bara kutoka pwani na Waafrika ambao kazi yao hasa ilikuwa kutafuta watumwa. Watumwa walitawala biashara ya Afrika ya Magharibi tangu mwanzo. Katika Afrika ya Mashariki wala hapakuwepo na hali zilizolingana na hiyo. Biashara ya watumwa lazima ionekane kuwepo katika mazingira ya mapema zaidi, iliyokwishajengeka kwa umakini, na biashara yenye faida ya masafa marefu ambayo chimbuko lake ilikuwa ubebaji wa pembe za ndovu. Hii ni muhimu kukumbuka hasa kwa mikoa ya kusini ambalo kila mara ilikuwa hazina kuu ya "Biashara ya Utumwa katika Afrika mashariki." 123. Bwana Alpers anahitimisha, "lazima iwe wazi sasa kwamba fikira ya zamani inayotamkwa kiholela kwamba wengi wa watumwa walikamatwa na wafanya biashara wanyang'anyi 121. Ibid, uk. 13.

122. Bid, uk. 14.

123. Ibid uk. 15.

wa Kiarabu na Kiswahili ni moja wapo ya mambo ya kubuniwa na ngano tu ambazo zimekuzwa kuhusu biashara ya watumwa ya Afrika mashariki. Lakini lazima tuwe waangalifu tusifanye kosa la kutoa tathmini potofu kuhusu mchango waliotoa watu hawa kwenye biashara hii." 124. Kwa mara nyingine, lazima nisisitize kwamba lengo langu si kudhihaki juhudi za kundi dogo la waadilifu ambao walikuwa wanashughulika na propaganda dhidi ya utumwa. Ninachotaka kuonyesha ni kwamba juhudi zao hazikufaulu (na hazingefaulu) hadi pale shinikizo la kiuchumi lilipoilaz-imisha kwanza Uingereza ilipolazimika kufuatana na mata-tizo ya kiuchumi kuanza kuzuia utumwa, biashara ya utumwa na halafu kukomesha utumwa.

Kwa kweli, Uingereza ilipojitokeza kwa ajili ya kutaka kukomesha utumwa haikusimama kwenye mapaa ya nyum-ba na kutangaza kwamba ilikuwa inakomesha utumwa kushindana dhidi ya wenye viwanda wa Kifaransa. Uingereza ililigeuza jambo hili kuwa suala la kimaadili na kiunyofu kabla haijatumainia kushinikiza serikali zingine kufuata mpango wake. Na ilifanya hivyo. Tunatambua jinsi Uingereza ilivyoanzisha vita si kwa lengo la kulinda maslahi ya himaya yake kiuchumi na kisiasa, lakini ilifanya hivyo ili "kulinda Uhuru wa Watu." Ndivyo ilivyokuwa kuhusu vita yake dhidi ya utumwa. Murua na maadili mema lilikuwa suala la waadilifu wachache tu ambao hawakuwa na uwezo. Suala halisi, kama serikali mbali mbali na walowezi na wakoloni walivyohusika, lilikuwa kuhusu uchumi. 124. Ibid uk. 24.

MATESO YA WATUMWA

Tumekwisha ona Uislam ulichofanikiwa katika kupunguza ukali wa maumivu ya taabu ya watumwa na jinsi gani, kwa mara ya kwanza na mara ya mwisho katika historia, watumwa walivyopewa hadhi ya ubinadamu wakiwa na haki juu ya wamiliki wao. Sasa hebu tuangalie jinsi Wakristo walivyo watendea watumwa wao. Kabla ya kutoa maelezo, lazima niweke jambo moja wazi. Maelezo haya ni ya kuhusu taabu za watumwa katika kipindi cha karne tano zilizopita ambapo, kama ilivyoelezwa mapema, Wakristo walianza biashara ya watumwa ya huko nyuma katika kiwango kisichoeleweka. Kama nilivyoonyesha kwenye sura iliyo pita, Waarabu pia waliwapa Wakristo msaada katika jambo hili kwa hiyari yao katika kipindi cha robo ya mwisho ya karne ya kumi na nane. Kwa kuwa maelezo mengi mno ya nchi za Ulaya kuhusu biashara ya utumwa katika bara la Afrika, huanza kwenye kipindi hiki, kwa hiyo yapo maelezo mengi yaliyo wazi kabisa kuhusu yale yaliyoonekana na watu huko. Hivyo, Wakristo lazima wabebe uzito wa kuhusika na machukizo haya kwa kiwango kikubwa. Wakristo walikuwa wanawapa mateso haya kwa kipindi cha karne nne ikilinganishwa na karne moja ambayo ndicho kipindi ambacho Waarabu wali-ungana nao katika kuwashawishi ingawaje walihiyari kufanya hivyo. Waathirika hao walikuwa Waafrika masikini wasiokuwa na ulinzi, watu wewusi (manegro) wa pwani ya magharibi na Mashariki ya Afrika na pia waliotoka katikati ya bara hilo. Waafrika walifanywa kama mali inayohamishika tu na vitendea kazi au viliyo vibaya zaidiya hapo. Ilibidi wafanye kazi, au pengine walilazimishwa kufanyakazi katika masharti yaliyo magumu sana kwenye mashamba mapya yaliyomilikiwa na mabwana zao, mataifa yenye nguvu yaliyo ya Kikristo ya nchi za Magharibi, ambao walichukua na kuvimiliki visiwa vyote kuvuka bahari ya Atlantic na katika ulimwengu mpya na vile vile hata nyumbani nchini Ureno na Hispania na nchi za Ulaya ya kati ya Ufalme Mtakatifu wa Kirumi chini ya miliki ya mapapa wa Kanisa Katoliki.

Mateso ya biashara ya utumwa yalijitokeza zaidi wakati wa robo ya mwisho ya karne ya kumi na tisa. Popote pale uvamizi ulipofanyika kijijini, vifo na uharibifu vilifuatia (vilitokea). Watu wengi zaidi walikufa wakilinda nyumba na familia zao, au kutokana na matokeo ya njaa na magonjwa ambayo kwa kawaida yalitokea baada ya vurugu kama hizo kuzidi, basi watu wengi waliofanywa kuwa watumwa, achilia mbali na wale waliouzwa huko pwani. Mtu anaweza kutetemeka anapofikiria njia mbaya sana na za kikatili mno zilizotumika kuwakamata wazalendo masikini wa Afrika, walitenganishwa na ndugu zao, walichukuliwa na kutendewa vibaya zaidi kuliko hayawani. Sasa tutatoa maelezo mafupi kutoka kwenye vitabu vyao wenyewe, vya waandishi wa nchi za magharibi ili tuonyesha jinsi gani watumwa walivyoteswa na mbinu zipi za kikatili zilizotu-miwa na wawindaji wa watumwa. Mbinu zao wakati fulani zilitekelezwa kiholela, na ziliingiza hasara, kwa sababu walikuwa wezi, si wapiganaji."Utendaji wao ulikuwa kuzunguuka vijiji kadhaa ambavyo waliviteua kuvivamia, walinyemelea kimya kimya wakati wa usiku. Kwa kawaida kijiji kilikuwa kimejengeka kwa vibanda vilivyojengwa kwa tope ya kawaida na kuezekwa kwa mianzi na majani ya mchikichi, vyote hivi vikiwa vinashika moto na kuungua kwa urahisi sana, kwa hiyo, wavamizi walichoma moto vibanda hivyo bila aibu wala haya, na mara nyingi wali-fanya hivyo wakati wa alfajiri. Wakazi wa vibanda hivyo walipoamka kutokana na mngurumo wa moto unaowaka kwa ukali walijikuta hawana la kufanya isipokuwa kukim-bilia nje, ambako huko walizingirwa na kukamatwa. Yeyote miongoni mwao aliyejaribu kuleta upinzani, aliuawa, kwani wawindaji wa watumwa hawakuwa na huruma. Wazee na wasiojiweza na watoto wachanga waliuawa hapo papo kwani hawakuwa na shida nao, na ni wale tu wanaume na wanawake wenye nguvu, na wavulana na wasichana, wali-achwa hai, ili wapelekwe utumwani, huku nyuma wakiacha maiti tu na majivu ya nyumba zilizoungua, mahali ambapo hapo mwanzo palikuwepo familia zenye furaha na makazi yaliyokuwa yanashamiri. Hasara ilikuwa kubwa mno kuzi-di hiyo zawadi. Lakini uharibifu, mkubwa mno ilikuwa kama alama ya utumwa wa watu weusi, tangu nyakati zake za mwanzo, hadi mwisho. Popote pale utumwa ulipotokeza hali iliyofuata, ni vifo, magonjwa na maangamizi.

Watu waliokamatwa kutoka katikati ya mikoa ya bara walikuwa na bahati mbaya kidogo, walilazimika kutembea kwa miguu yao hadi pwani - mwendo mrefu wa kuchosha na kutia huzuni wa maili nyingi na msitu mnene na jangwa baya. Walitembea bila kuwa na nguo za kutosha, bila ya kinga yoyote dhidi ya miba mikaliu na mawe yenye ncha chonge na yenye kukeketa. Ili kuwazuia watumwa wasitoroke, walivishwa kongwa shingoni, wale waliokuwa wasumbufu, mikono yao iliingizwa kwenye ubao unao kwaruza wenye matundu, visigino vya miguu yao ilifungwa kwa minyororo. Misitari mirefu iliyojulikana kwa jina la watumwa, iliunganishwa kwa kamba, walisafiri mwendo mrefu kwa taabu kuelekea kwenye hatima yao ya kutisha, kwani Waafrika wote walikuwa wakielewa kwamba wazun-gu walikuwa wanakula nyama ya watu weusi ambao wali-wanunua kutoka kwenye boma. Wamiliki wao waliwaswa-ga mbele kwa mateso makali na bila kupumzika, bila kujali majeraha na mikwaruzo ya ngozi, waliishiwa na nguvu kwa sababu ya kuchapwa mijeledi mingi. Kama kuna yeyote aliyeelemewa na mateso hayo na akashindwa kabisa kuen-delea mbele, alitupwa pembeni mwa njia, na kama kuna mmoja wao alizidiwa na maradhi, aliachwa afe au kwa kuhurumiwa zaidi aligongwa kichwa ili afe haraka." 125. "...Kwenye hali ya hewa nzuri au mbaya, pamoja na magonjwa na vifo, na kwa maasi yote na kujiua wenyewe, kila mwaka meli zilileta maelfu ya watumwa Marekani na katika visiwa vya West Indies. Walikuja kwa meli za mataifa mengi: Ufaransa, Udachi, Ureno, na Danmark -lakini zaidi ya nusu waliletwa na meli za Kiingereza ambazo zilisafiri kutoka Bristol, London, au Liver pool. Kila mwaka, walifikishwa pwani katika hali ya kuugua au wazima wa afya, wakiwa wamekubali matokeo ya maisha au kukata tamaa na daima milele hawakurudi tena walikozali-wa... Matumizi ya watumwa, kama ilivyo matumizi yake mabaya, kamwe hayabadiliki; yalifanana kote duniani na kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Huko Marekani na katika visiwa vya West-Indies, kama ilivyokuwa wakati wa Rumi ya kale, au Ugiriki au mwanzo wa historia isiyo dhahiri, utumwa uligawanywa kwenye aina mbili pana -utumwa wa kutumika ndani ya nyumba na utumwa wa kutu-mika mashambani." 12 125. Sherrad, B. A., Freedom from Fear (London, 1959) uk. 61-62. 126. Ibid. uk. 67f.

Sasa ngoja tuoneshe nukuu zingine zaidi kutoka kwenye kitabu hicho hicho "Freedom from Fear or the Slave and his Emancipation" kilicho andikwa na O.A. Sherrard, kuonye-sha jinsi gani na kwa kiwango gani mataifa ya mwanzo kabisa ya Kikristo kutoka Magharibi yalivyowatesa kinya-ma mno bila ya huruma watu Weusi ambao hawakuwa na namna yoyte ya kujilinda. Pia msomaji ataona imani na fiki-ra zao duni kuhusu binadamu ambao walitofautiana nao kwa rangi na taifa. "Tukiangalia historia kwa mapana yake, walipita katika hatua mbili: katika hatua ya kwanza uvumilivu mabegani mwao, kama Atlas mstahamilivu, utukufu wa mamlaka nyingi zilizostaarabika zilizokufa zamani; na hatua ya pili yenye kudhalilisha zaidi kuliko ya kwanza, walipoteza hata ile heshima ya uwakilishi, na kuanguka kwenye hali ya uny-onge ambamo mchango wao ulikuwa kutumikia uroho wa watu binafsi. Hali yao, hasa zaidi katika hatua ya pili, wangeweza kuiogopesha dhamiri mbaya ya dunia ya Kikristo kwa jina, lakini jambo la kushangaza ni kwamba waliiacha hivi hivi bila yenyewe kusisimka. Wazo la utumwa lilikolea sana hivyo kwamba hakuna mtu aliye hoji usahihi wake. Mataifa yote ama yalifumbia macho au yali-furahia jambo hilo." 127. Watumwa wengi waliofanya kazi kwenye mashamba, kazi yao ilikuwa ngumu sana, kazi aliyopewa, kwa mawazo yake ilikuwa kazi ya kifundi; alitakiwa kulima zao ambalo lilikuwa geni kwake - kwa sehemu kubwa miwa katika visiwa vya West Indies, pamba na tumbaku huko Marekani 127. Ibid uk. 11. - na kwamba kazi yake ilikuwa mpya alistahamili mzigo mzito zaidi kuliko mwenzake huko Ugiriki au Rumi au miongoni mwa watwa na wajakazi wa Ulaya... Kila kitu kilikuwa kipya na kigeni kwake; kwa hiyo, alivunjwa vun-jwa moyo humo; alitakiwa afundishwe kazi zake mpya; ali-zoneshwa kama usemi ulivyokuwa. 'Kuzoesha' ilikuwa neno lililotumika badala ya nidhamu kali, ambayo ilifikiri-wa na wapinzani wa utumwa kubeba si chini ya asilimia ishirini ya wale waliopitia humo.

Inawezekana hiyo inazidi kiwango halisi, lakini hata hivyo lazima ikubalike kwamba idadi kubwa walikufa. Nidhamu ilikuwa chungu, hapakuwe-po na nafasi ya kurekebisha kwa kuifanya kuwa nzuri zaidi na asili mia sabini hawakufika mwisho. 1 Watumwa walipita kwenye hatua ngumu za mateso ya kuo-gofya na kutisha hasa. Limbikizo la athari za mateso yote zilikuwa msiba mkubwa. Tunamnukuu Sherrard tena, "hii ilikuwa kweli zaidi kwenye mpito wa 'nidhamu', kwani bila shaka yoyote sehemu kubwa ya watumwa waliokufa kwenye nidhamu yake wangekufa katika tukio lolote kutokana na athari za mpito wa kati. Uzoefu ulionyesha kwamba idadi kubwa zaidi ya watumwa waliokuwa dhaifu au kukonda wakati walipowasili, walikufa muda mfupi baa-daye kutokana na jambo lolote walilofanya. Mamlaka za tiba zilitoa taarifa kwamba hali hiyo ilisababishwa na kufungiwa kwenye nyumba za watumwa kwa muda mrefu kabla ya kupanda meli, haja ya usafi na hewa wakati wapo ndani ya meli, kubadilisha nguo, chakula na tabia, na hasa zaidi mabadiliko ya hewa (Buxton, uk. 188). 128. Ibid. uk. 69.

Lakini walikubali kwamba palikuwepo na jambo lingine zaidi ya hilo - hujuma ya kisaikolojia au kiroho, ambayo waliielezea, labla kwa namna ya ajabu, kama 'masikitiko ya kukumbuka ndugu na urafiki, uvunjaji sheria wa kifidhuli wa yale yote yaliyokuwa yanaheshimiwa sana na mapenzi ya kijamii ya nchi na undugu, na matumaini yasiyo na mwisho ya kushushwa daraja ya utumwa kamili.' Hili liki-jumlishwa kwenye mateso ya kimwili pia lilivunja utashi wa kuishi na mtumwa alifanya hivyo haraka sana pindi alipopa-ta nafasi ya kwanza, au kwa urahisi zaidi, alijibana na kufa." Kwa uchache, walikuwepo wamiliki wa aina tano na sura tano za utumwa wa watu weusi - Kihispania, Kifaransa, Kidachi, Kidenishi na Kiingereza bila kuhesabu Marekani, ambayo mwanzoni ilikuwa Kiingereza. Waamerika ndani ya U.S.A., hadi sasa, karne hii ya ishirini, wanavunja sheria zao wenyewe na mtu mweusi bado hajafuzu kupata haki kamili za uraia, na yapo matatizo kwa Mtu Mweusi (Mnegro) nchini kwake mwenyewe kama dunia ijuavyo fika (vema). Hatima ya kuogofya ya mtumwa wa shamba ni mbaya -jinsi alivyopigwa chapa kwa chuma chenye moto, alivy-olazimishwa kushughulikia minyororo mizito, mgongo wake ulichanika na kuwekwa alama za kuchapwa kwa kiboko, jinsi alivyofungiwa jela wakati wa usiku, makazi na malazi yake, mara nyingi yamejengwa chini ya ardhi na ni machafu." Wareno walijenga msululu wa ngome, katika pwani ya Guinea, ambamo Waafrika wanyonge waliwekwa baada ya kukamatwa hadi idadi ilipotimia kustahili kusafirishwa kwenda Hispania, kwenye utumwa na baadaye Marekani na Ulimwengu Mpya... roho zao zilihukumiwa kwenye mateso ya milele; miili yao ilikuwa mali ya taifa la Kikristo ambao wangekalia nchi yao." 129. Mwandishi anaelezea jinsi utumwa ulivyoanzishwa kwenye makoloni ya Uingereza ndani ya Marekani: "Meli ya Kidachi ilikuwa inaingia kwenye Mto Jame huko Virginia na kupakuwa watumwa weusi ishirini wa kuuzwa. Wakoloni waliwanunua haraka sana na hivyo utumwa wa Mtu Mweusi ukaanzishwa huko kwenye makoloni ya Uingereza yaliyokuwa Marekani." Kwa kipindi kifupi," Uingereza ili-pata nafasi ya kwanza ya shehena za siri za watumwa, nafasi ambayo ilishikilia kwa kipindi cha zaidi ya miaka tisini."

Watumwa waliuzwa kwenye minada, walinunuliwa wakiwa uchi wa mnyama, wanaume kwa wanawake wote namna moja, na mtumwa alikalishwa kwenye kiti, ambapo wanunuzi (wazabuni) walimkagua na kushika shika misuli yake na kukagua meno na kumfanya aruke na kunyoosha mikono, ili kuthibitisha kwamba hawakununua mtumwa mgonjwa au asiye jiweza. Kwa kuwa watumwa walinunuliwa mmoja mmoja, kilichofuata ni kwamba mume na mke, watoto na wazazi walikwenda kwa wamiliki tofauti; na hasara ya ndugu na jamaa na yote yale ambayo watumwa walikuwa wanayapenda yalijumlishwa kwenye hasara ya kukosa uhuru, kwa hiyo mtumwa aliondoka kwenye chum-ba cha mnada, akiwa amenyang'anywa kila kitu, kuanza maisha mapya yalio duni, ya kukata tamaa na utumwa wa kuangamiza." ^O 129. Ibid. uk. 26. 130. Ibid uk. 67

MAKANISA YASHIRIKI BIASHARA YA WATUMWA

Kanisa la Kikristo lilikuwa na msimamo gani kuhusu biashara ya utumwa wa mtu Mweusi? Tangu mwanzo wake, Ukristo ulifumbia macho hali mbaya ya watumwa. Kama ambavyo imeelezwa huko mwanzoni, ni katika rejea moja tu kuhusu utumwa ndipo inapatikana kwenye waraka wa Mt. Paulo, akimrudisha mtumwa kwa Filimoni kwa mmiliki wake. Basi, ni hiyo tu basi. Ameer Ali anafafanua kwa usahihi kwamba: "Ukristo ulikuta utumwa ni taasisi inay-otambuliwa na ufalme; ulikubali mpango huo bila kujaribu kupunguza ukali wa tabia yake ya uovu; au kuendeleza kuukomesha pole pole, au kunyanyua hadhi ya watumwa." *^ I li kutambua nini Makanisa ya Kikristo yal-ifanya kwenye biashara ya watumwa ni vema mtu asome tena maneno ya Bwana Alpers ambaye anaandika, pamoja na mambo mengineyo, kwamba: "Wakristo walitambua kwamba kuuza binadamu wenzao hakungehalalishwa na kuthibitishwa kimaadili. Hata hivyo, kanisa la Kikristo lili-jitokeza na visingizio kuhusu biashara ya watumwa. Wachungaji wenyewe wengi walifanya biashara ya watumwa, hasa zaidi katika nchi ya Angola, na wengine wengi walimiliki watumwa huko Amerika ya Kusini na Kaskazini. Sababu moja tu ambayo ilitolewa na Kanisa Katoliki kuhusu kuwepo kwake kwenye biashara ya watumwa ni kwamba lilikuwa linajaribu kukomboa roho za Waafrika kwa kuwabatiza watumwa. Waprotestanti walikuwa ndiyo wabaya zaidi, kwani wao hawakukubali hata angalao kusema wazi kwamba wanakubali kwamba Waafrika wana roho. 131. Ameer Ali, Spirit of Islam (London: University Paperbacks, 1965) uk. 260.

Badala yake waliunga mkono wazo kwamba mtumwa wa Kiafrika alikuwa sehemu ya rasilimali kama fenicha au mnyama wa kufugwa. Hakuna sehemu ya historia ya kanisa la Kikristo ambayo ilikuwa ya kufedhehesha zaidi kuliko kujihusisha kwake na "Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki." 132. Hoja za James Boswell zimekwisha nukuliwa ambamo ame-sisitiza kwamba utumwa ni taasisi ambayo iliruhusiwa na Mungu katika vipindi vyote na kwamba kuikomesha ingekuwa sawa na kufunga lango kuu la huruma kwa wanadmau! Sasa ninanukuu kutoka kwenye "Capitalism and Slavery" maandishi ya Dk. Eric Williams, ambaye alikuwa mtaalam wa historia aliyetambuliwa na pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago. Anaadika: "Pia Kanisa liliun-ga mkono biashara ya watumwa. Wahispania waliona fursa ya kuwageuza imani wapagani ndani ya biashara hiyo, na (madhehebu ya Kikristo ya) "the Jesuits", "Dominicans" na "Franciscans" walijihusisha mno na kilimo cha miwa, ambacho kilisababisha umilikaji wa watumwa muhimu. Hadithi imesimuliwa kuhusu mzee wa Kanisa huko Newport ambaye kila wakati, Jumapili iliyofuata baada ya kuwasili watumwa kutoka pwani, alikuwa anamshukuru Mungu kwamba mzigo mwingine wa viumbe washenzi uliletwa mahali ambapo wangeweza kupata manufaa ya neno la Injili.' Lakini kwa ujumla wakulima wa Kiingereza walipinga Ukristo (kufundishwa) kwa watumwa wao.

Ukristo uli-wafanya watumwa kuwa wapotovu zaidi, kutokuwa watiifu 132. Alpers, op. cit., uk 22. na kwa hiyo wanakuwa hawana thamani. Pia ilikuwa na maana pia kutoa maelekezo kwa lugha ya Kiingereza, jambo ambalo liliruhusu makabila mbali mbali kukutana pamoja na kupanga njama za uasi... Gavana wa Barbados mnamo mwaka wa 1695 alilihusisha hilo na wakulima kukataa kuwapa watumwa mapumziko siku ya Jumapili na sikukuu, na mwishoni mwa 1832 maoni ya umma wa Uingereza (Britsh public opinion) yalishtushwa na wakulima walipokataa pendekezo la kuwapa Watu Weusi siku moja ya kupumzika ili kuruhusu kukomesha soko la Jumapili la Watu Weusi. Kanisa lilitii. "Society for the Propagation of the Gospel" (chama cha kuitangaza Injili) kilikataza mafundisho ya Kikristo kwa watumwa wake huko Barbados, na kuwapiga chapa ya 'Society' (chama) watumwa wake wapya kuwatofautisha na wale waliomiliki-wa na watu wa kawaida; watumwa wa mwanzo walikuwa urithi wa Christoper Codrington. Sherlock, baadaye akawa Bishop wa London, aliwahakikishia wakulima kwamba 'Ukristo na kuikumbali Injili hakuleti hata cheme ya tofauti kuhusu mali za raia.' Wala haukuwekwa vikwazo katika shughuli za kikanisa. Kwa kazi zake kuhusu Asiento ambazo zilisaidia kumfanya kama muwakilishi (Balozi) mwenye mamlaka kamili wa Uingereza huko Utrecht, Bishop Robinson wa Bristol alipandishwa cheo na kuwa Askofu wa dayosisi ya London. Kengele za makanisa ya Bristol zililia kushangilia kuhusu taarifa ya kukataliwa na Bunge muswada wa Wilberforce uliotaka kukomeshwa kwa biashara ya watumwa. Mfanyabiashara wa biashara ya watumwa, John Newton, aliyashukuru makanisa ya Liver-Pool kwa ushindi wa jaribio hili la mwisho kabla hajabadi-lika na akaomba baraka za Mungu zimjie yeye. Alianzisha ibada ya hadhara mara mbili kwa siku kwa uchu wake, aki-hubiri yeye mwenyewe, na alitenga siku moja ya kufunga saumu na kusali, si kwa ajili ya watumwa bali kwa ajili ya wafanyakazi wa meli. 'Sikujua,' aliungama, 'utamu au saa zaidi za sakramenti takatifu ziwe mara nyingi zaidi kuliko kwenye safari mbili za baharini za kwenda Guinea.'

Kadinali Manning maarufu wa karne ya kumi na tisa alikuwa mtoto wa mfanya biashara tajiri wa visiwa vya West Indies aliye kuwa anashughulika na bidhaa zilizo limwa na watumwa. Wamisionari wengi waliona ni faida kubwa kumfukuza Beelzebub kwa Beelzebub (yaani, kumfukuza shetani kwa kumtumia shetani). Kwa mujibu wa mwandishi wa siku hizi za karibuni sana wa Uingereza kuhusu biashara ya watumwa, walifikiri kwamba njia nzuri zaidi ya kureke-bisha matumizi mabaya ya watumwa Weusi ilikuwa kum-fanya mwenye shamba kuwa mfano mzuri kwa kuwatunza watumwa na mashamba wao weneywe, ili kutimiza katika utekelezaji wa aina hii ukombozi wa wamiliki wa mashamba na kuendeleza misingi yao.' Wamisionari wa Kanisa la Moravian kisiwani hapo walimiliki watumwa bila kusita; Wamissionari wa Kanisa la, mwandishi mmoja wa historia anaandika kwa mtiririko wa mvuto kwamba Baptists (yaani, Wakristo wa madhehebu ya Baptst) hawakuruhusu wamisionari wao wa mwanzo kupinga kumiliki watumwa. Hadi mwisho kabisa, Askofu wa Exeter aliendelea kuwa na watumwa wake 655, na mnamo mwaka wa 1833 alilipwa pauni za Kiingereza 12,700 kama fidia ya watumwa hao. Wataalam wa historia wa Kanisa waliomba msamaha wa kufedhehesha, kwamba dhamiri ilizinduka polepole sana kutathmini uovu ulioletwa na utumwa na kwamba utetezi wa utumwa uliofanywa na watu wa kanisa 'ulitokana na utashi wa uzuri wa utambuzi wa maadili.' Hakuna haja ya kuomba msamaha wa aina hii. Msimamo wa watu wa kanisa ulikuwa ndio msimamo wa mtu wa kawaida. Karne ya kumi na nane kama nyingine yoyote, haingeweza kuvuka mipaka ya uchumi wake. Kama alivyo hoji Whitefield alipokuwa anatetea kusomwa tena kila kipengele cha mkataba wa Georgia uliositisha utumwa, 'Ni rahisi kuonyesha kwamba nchi za joto haziwezi kulimwa bila Watu Weusi.'

Quaker (kundi la Wakirsto ambalo halipendelei mikutano rasmi na halipendelei ghasia au vita) - wasiofuata kanuni, hawakukubali kuacha biashsra ya watumwa. Mwaka wa 1756 walikuwepo Quaker themanini na nne waliorodhesh-wa kama wanachama wa kampuni ifanyayo biashara kwen-da Afrika, miongoni mwao ni "the Barclay": na "Baring families." Shughuli ya watumwa ilikuwa moja wapo ya uwekezaji wenye faida kubwa wa Quaker wa Uingereza halikadhalika na wale wa Marekani na jina la mfanya biashara ya watumwa, The Willing Quaker, aliarifu kutoka Boston - Siera Leone mwaka wa 1793, inaashiria uthibitisho ambao ulisababisha biashara ya watumwa kuheshimiwa katika jamii ya Quaker. Jamii ya Quaker ili-fanya upinzani dhidi ya biashara ya watumwa kwanza kutoka Marekani na kutoka kwenye vijiji vya jamii ndogo vya kaskazini, ambavyo havikujihusisha na nguvu kazi ya watumwa. 'Ni vigumu', anaandika Dk. Gray, 'kukwepa dhana kwamba upinzani huo dhidi ya mpango wa watumwa kwanza uliwekewa mipaka kwa kundi ambalo halikupata manufaa ya moja kwa moja kutoka kwenye biashara hiyo, kwa hiyo walikuwa wapinzani.'

Utumwa ulikuwepo wakati wa Mwingereza wa karne ya kumi na nane. Na sarafu ya Kiingereza, guinea, ingawaje ilipatikana kwa nadra, chanzo chake ilikuwa biashara ya Africa. Mhunzi wa dhahabu wa Westminster alitengeneza kufuli kwa ajili ya Watu Weusi na mbwa. Sanamu za watu weusi na tembo, ishara ya biashara ya watumwa zilipamba ukumbi wa Liverpool Town Hall. Alama za cheo na vifaa vya wafanya biashara ya watumwa vilionyeshwa wazi ili vinunuliwe kwenye maduka na kutangazwa kwenye maga-zeti. Watumwa waliuzwa kwenye minada ya wazi. Watumwa wakiwa rasilimali isiyo na thamani, na wanao-tambulikana kidogo sana kisheria, posta masta alikuwa wakala aliyetumiwa mara nyingi kuwakamata watumwa wanaokimbia na matangazo yalichapishwa kwenye vyombo vya habari vya kiserikali. Watumishi Weusi walionekana sehemu mbalimbali. Wavulana weusi wadogo walikuwa wasaidizi wa makapteni wa watumwa, wanawake wa mitin-do au wanawake waadilifu. Mashujaa wanawake wa Hograrth, 'The Harlots Progress' kinahudumiwa na mvulana Mweusi, na Orabella Burmester ya Mar'guerito steen anaonyesha maoni yake ya kupenda mvulana mweusi mdogo ambaye angempenda kama mtoto wake wa paka mwenye manyoya marefu. Watumwa Weusi walioachwa huru walionekana miongoni mwa ombaomba wa London na walijulikana kama ndege weusi wa Mtakatifu Giles. Walikuwa wengi mno hivyo kwamba iliundwa kamati ya bunge mwaka 1786 kwa lengo la kuwasaidia masikini weusi.

Mshairi Cowper aliandika: "Watumwa hawawezi kupumua Uingereza.' Hii ilikuwa leseni ya mashairi. Mwaka 1677 iliaminika kwamba 'Watu Weusi kwa kuwa ni kawaida kwamba hununuliwa na kuuzwa miongoni mwa wafanyabi-ashara, kwa hiyo wao ni bidhaa, na pia kwa kuwa kwao makafiri, inaweza kuwepo mali kwao. Mwaka 1726 Mwana sheria Mkuu alitangaza kwamba ubatizo haukumpa mtumwa uhuru au kufanya mabadiliko yoyote katika hali ya mpito ya mtumwa; juu ya hayo mtumwa hakuwa huru kwa kuletwa Uingereza, na mara afikapo Uingereza mmiliki wake angeweza kulazimishwa kisheria mtumwa husika kurudi mashambani. Hiyo mamlaka adhimu kama Sir William Blackstone aliamini kwamba kuhusu haki yoyote mmiliki wa mtumwa anaweza kupata uhalali kamili kwa ajili ya utumishi wa kuendelea wa John na Thomas (yaani watumwa waliobatizwa), watabaki katika hali ileile ya kutawaliwa maisha yote; hapa Uingereza au penginepo popote." 133.

Wakati meli zilizobeba watumwa kutoka nchi za Kikristo kwenda katika nchi za magharibi za Amerika ya Kaskazini na Kusini, wachungaji, wa Kikristo walikuwa na desturi ya kuzibariki meli hizo kwa jina la Mweza Mwenye nguvu zote na kuwaonya watumwa wawe watiifu. Kamwe haikupata kuingia akilini mwao hao wachungaji kuwaonya wamiliki wa watumwa kuwa na huruma kwa watumwa. Ni vigumu kuamini lakini inaonyesha kwamba Kanisa Katoliki linafikiri ni sahihi kabisa na inaafikiana na mafundisho ya kanisa lao kununua watumwa hata katika kipindi hiki cha miaka ya 1970. Mwezi Augosti, 1970 dunia ilishtushwa kusikia kwamba Kanisa Katoliki lilimnunua, kwa bei ya kuanzia pauni za Kiingereza 250 hadi 300 kila mmoja, kiasi cha wasichana wa Kihindi 1500 na kuwafun-gia kwenye mabweni ya kidini kwa sababu wasichana wa Kizungu hawataki kuishi maisha ya usista. 1 133. Williams, op. cit., uk. 42-5 134 Sunday Times (London,) kama ilivyonukuliwa katika East African Standard (Nairobi) Augast, 1970. Palitokea kilio kikubwa hapa duniani hivyo kwamba Vatican ililazimika kuunda tume ya kuchunguza jambo hili. Lakini hata kabla ya tume kuanza kazi yake ya uchunguzi, msema-ji wa Vatican alikubali kuwepo kwa "ukweli" kwenye taari-fa hiyo, ingawaje katika kutimiza wajibu wa kazi yake alilaumu gazeti la Sunday Times kwa uchuuzaji wake wa hisia za watu.