WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU0%

WAULIZE WANAOFAHAMU Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi: Muhammad Tijani As-samawi At-Tunisi
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 51505
Pakua: 5470

Maelezo zaidi:

WAULIZE WANAOFAHAMU
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 26 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 51505 / Pakua: 5470
Kiwango Kiwango Kiwango
WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi:
Swahili

5

WAULIZE WANAOFAHAMU

Kama uonavyo ewe msomaji kwamba, madai yote hayana ushahidi wowote na wala akili na ukweli ulivyo havikubaliani. Sisi tutaleta ushahidi ili kuyatengua (madai hayo). Kama Mtume(s.a.w.w) alikuwa akimpenda kwa kuwa yeye ni mzuri na kuwa yeye ni bikra pekee aliyepata kumuoa, basi ni jambo gani lililomzuwia Mtume kuowa wanawake bikra na wazuri ambao walikuwa bora kwa wema na uzuri na walikuwa wakipigiwa mfano (kwa uzuri) katika makabila ya Kiarabu wakati yeye Mtume alikuwa akiwafahamu' Na juu ya hayo wanahistoria wanautaja wivu wa Aisha kwa Zainab binti Jah-shi na Safiyyah binti Huyayi na Mariyah Al-Qibtiyyah kwa sababu wao walikuwa wazuri zaidi kuliko yeye. Ibn Saad ndani ya Tabaqat yake Juzuu ya 8 uk.148 na Ibn Kathir katika tarekh yake wameleta riwaya kwamba, Mtume(s.a.w.w) alimuoa Mulaikah binti Ka'b, na bibi huyu alikuwa akifahamika kwa ubora na uzuri, basi Aisha akamwendea bibi huyu (nyumbani kwake) kisha akamwambia: "Hivi huoni haya kuolewa na mtu ambaye amemuua baba yako?" (Kutokana na ushawishi huu) bibi yule akamwambia Mtume: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana nawe." (Neno hilo likamchukiza) Mtume(s.a.w.w) akamtaliki bibi huyo, kisha jamaa zake wakaja kwa Mtume(s.a.w.w) wakamwambia "Huyu ni mtoto mdogo naye hana hiyari, kwa hakika amehadaiwa mrejee" Mtume(s.a.w.w) akakataa, na baba wa binti huyu aliuawa siku ya Fat-hi Maka, aliuawa na Khalid ibn Walid mahala paitwapo Khindimah.

Riwaya hii inatujulisha wazi kwamba makusudio ya Mtume wa Mwenyezi Mungu haikuwa kuoa mabinti wadogo tena wazuri, vinginevyo (kama malengo yake yangekuwa ni kuoa watoto wadogo tena wazuri) asingeachika Mulaikah binti Ka'b hali yakuwa ni msichana mdogo na bora tena mzuri kama ambavyo riwaya hii na nyinginezo zinavyotuonesha njia alizozitumia Aisha kuwahadaa wanawake waumini wasio na kosa lolote na (kusababisha) wasiolewe na Mtume wa Mwenyezi Mungu? Na (huyu bi Mulaikah) alitanguliwa na kuachika kwa As-ma binti Nuuman pale Aisha alipomuonea wivu akamwambia kuwa: "Mtume humfurahia sana mwanamke pindi akiingia kwake akamwambia, najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana nawe." (Bibi Aisha pia) anamchochea huyu bi Mulaikah hisia za mauaji ya baba yake na kwamba aliyemua ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na anamwambia, "Huoni haya kuolewa na mtu aliyemuua Baba yako?" Maskini binti huyu hakuwa na jawabu lolote isipokuwa ni kumchukia Mtume wa Mwenyezi Mungu, unadhani angejibu nini binti huyo wakati ambapo watu walikuwa bado wapo kwenye zama za ujinga na wakichukua kisasi na kumcheka asiyechukua kisasi kwa ajili ya baba yake? Kilichobaki tujiulize na tunayo haki ya kujiuliza, Ni kwa nini Mtume(s.a.w.w) aliwaacha wanawake hawa wawili bila kosa lolote na ambao walikuwa muhanga wa vitimbi na hadaa za Aisha?

Kabla ya kufanya kitu cho chote, hatuna budi tufahamu katika akili zetu kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ni Maasum (hafanyi dhambi) na wala hamdhulumu yeyote wala hafanyi ila ni haki, basi (kama ni hivyo) hapana budi kwa kuwataliki (kina mama hao) kuna hekima ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanaoifahamu kama ambavyo Mtume hakumtaliki Aisha pamoja na matendo yake, vile vile kuna hekima yake. Pengine huenda tunaweza kuwa na msimamo wa jambo fulani katika hekima hiyo katika uchambuzi ufuatao. Ama kwa upande wa yule mwanamke wa kwanza ambaye ni Asma binti Nuuman, bila shaka kutotumia kwake busara kunadhihirika pale hila za Aisha zilipomchemsha, basi neno lake la kwanza alilomkabili nalo Mtume wa Mwenyezi Mungu wakati alipomnyooshea mkono wake likawa "Ninajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana nawe". Pamoja na uzuri wake na ubora wake Mtume hakumbakisha kutokana na ujinga wake (wa kutofikiri). Ibn Saad na wengineo anasema ndani ya Tabaqat yake Juz.8 uk.145.

Imepokewa kutoka kwa ibn Abbas amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuoa Asma binti Nu'uman na (bibi huyu) alikuwa mzuri mno miongoni mwa wanawake wa zama zake na alikuwa ametimia." Basi huenda Mtume(s.a.w.w) alitaka kutufundisha kwamba akili pevu ni bora kuliko uzuri, kwani ni mara ngapi mwanamke mzuri ujinga wake umempelekea kufanya uchafu?.

Ama kwa upande wa yule mwanamke wa pili ambaye ni Mulaikah bint Ka'ab aliyebeuliwa na Aisha kwa kuambiwa kuwa mumewe ndiye aliyemuua baba yake, Mtume hakutaka mwanamke huyu maskini (ambaye alikuwa na umri mdogo asiye na uamuzi kama walivyoshuhudia hayo jamaa zake aishi pamoja na) Aisha mwenye vitisho na mawazo yaliyo komaa mambo ambayo huenda yangesababisha matatizo makubwa hasa hasa kutokana na Aisha ambaye asingempa nafasi ya kufurahi na Mtume(s.a.w.w) . Na hapana shaka kwamba zipo sababu nyingine ambazo Mtume wa Mwenyezi Mungu anazijuwa na kwetu zimefichikana. Jambo la muhimu ni kufahamu kwamba, Mtume(s.a.w.w) alikuwa havutiki kwa uzuri na matamanio ya mwili na kijinsiya kama walivyodhania baadhi ya watu wajinga na baadhi ya Mustashrikina[58] ambao wanasema eti lengo la Muhammad lilikuwa ni kujipatia wanawake wazuri. Kwa hakika tumeona jinsi gani Mtume wa Mwenyezi Mungu alivyowataliki wanawake hawa wawili bila kujali udogo wao na uzuri wao, kwani walikuwa wazuri mno katika zama zao kama ilivyoandikwa katika vitabu vya historia na vitabu vya hadithi. Kwa hiyo kauli ya anayedai kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akimpenda Aisha kwa umri wake mdogo na uzuri wake inapingwa na haikubaliki. Ama wale wasemao kwamba Mtume alimpenda Aisha kwa sababu ni binti ya Abubakr, jambo hili siyo sahihi, lakini tunaweza tu kusema kwamba Mtume alimuoa Aisha kwa sababu ya Abubakr, kwa kuwa Mtume aliwaoa wanawake kutoka katika makabila mbali mbali kwa sababu za kisiasa ili kuziunganisha nyoyo (za watu hao) na kuyaelekeza mapenzi na huruma kwa makabila hayo badala ya (kueneza) ugomvi na chuki. Hapana shaka kwamba Mtume alimuoa dada yake Muawiyah, Ummu Habibah binti Abi Sufiyan, wakati ambapo huyu Abu Sufiyan alikuwa ni adui namba moja wa Mtume(s.a.w.w) na alifanya hivyo kwa kuwa yeye (Mtume) siyo mtu mwenye chuki pia yeye ndiye rehma kwa walimwengu. Huruma na upole wa (Mtumes.a.w.w ) vilivuka kutoka kwenye makabila ya Kiarabu mpaka akafikia hadi ya kuwaolea Mayahudi na Wakristo na hata Waqibt (wa Misri) ili awaunganishe watu wa dini wao kwa wao.

Jambo muhimu linalotupasa sisi kulifahamu kupitia maarifa tuyasomayo ndani ya vitabu vya Sira ni kwamba Abubakr ndiye aliyemtaka Mtume(s.a.w.w) amuoe binti yake Aisha, kama ambavyo Umar naye alimtaka Mtume(s.a.w.w) amuowe binti yake Hafsah, Mtume(s.a.w.w) alikubali kwani moyo wake uko wazi kuwaenea walimwengu wote. Mwenyezi Mungu anasema:

وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ﴿١٥٩﴾

"Na lau ungekuwa (wewe Muhammad) ni mkali na mwenye moyo mgumu bila shaka wangekukimbia." (Qur'an, 3:159).

Tukizirejea riwaya ambazo amezitaja Aisha na akasema katika riwaya hizo kwamba, "Mtume(s.a.w.w) hakukaa muda mrefu ila alidhani kuwa nimepitiwa na usingizi, akachukua nguo yake taratibu na akafungua mlango akatoka kisha akaufunga." Basi tunafahamu uongo wa madai ya kwamba Mtume alikuwa hawezi kuvumilia kwa kumkosa Aisha.

Matokeo ya utafiti huu siyo natija ya kubahatisha iliyoundwa kimawazo tu (bila ushahidi) sivyo kabisa, bali inao ushahidi ndani ya vitabu vya Kisunni. Muslim ameandika riwaya ndani ya Sahih yake, na wengineo ndani ya Sihah zao za Kisunni kwamba, Umar ibn Khatab amesema, "Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipojitenga mbali na wakeze, niliingia msikitini nikawakuta watu wakiwa wanawaza na wanasema, Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amewataliki wakeze, na tukio hili lilitokea kabla hawajaamriwa kuwa na hijab, basi Umar akasema, hapana budi nilitambue jambo hilo leo. Akasema, nikaingia kwa Aisha nikamwambia, Ewe binti Abubakr hivi hadhi yako imefikia kiasi cha kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) "?

Aisha akasema, "Ewe Mwana wa Khatab kuna uhusiano gani kati yangu na wewe kamuulize binti yako" Omar akasema: "Nikaingia nyumbani kwa Hafsah binti Umar nikamwambia, Ewe Hafsah hivi hadhi yako imefikia kiasi cha kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, Wallahi bila shaka wewe unajua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakupendi na lau siyo mimi Mtume wa Mwenyezi Mungu angekwisha kukuacha, Hafsah akalia sana" Bila shaka riwaya hii inatujulisha wazi kwamba hapana shaka kuwa Mtume(s.a.w.w) alimuoa Hafsah binti Umar si kwa sababu ya kumpenda, lakini ni kwa maslahi ya kisiasa ambayo hali halisi ilipelekea iwe hivyo. Miongoni mwa mambo yanayotuongezea uhakika wa kukubalika kwa mtazamo tulionao katika kuyapata matokeo mazuri ya uchambuzi huu ni kwamba, Umar ibn Khatab anamuapa Mwenyezi Mungu kuwa Mtume(s.a.w.w) hampendi Hafsah, na Umar anatuongezea uhakika tena kwamba binti yake Hafsah yeye pia anafahamu ukweli huu wenye uchungu, pale alipomwambia, "Wallahi hakika wewe unafahamu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakupendi." Basi baada ya hayo hakuna shaka yoyote inayobakia kwetu sisi kwamba kuolewa kwa Hafsah kulikuwa ni kwa ajili ya maslahi ya kisiasa (hasa) pale Umar aliposema: "Lau si mimi Mtume wa Mwenyezi Mungu angekwisha kukuacha."

Kwa hiyo riwaya hii inatufanya tuifikirie vile vile sababu iliyomfanya Mtume kumuoa Aisha binti Abubakr na kuonesha kwamba Mtume alisubiri na akavumilia maudhi yote ya Aisha kwa ajili ya Abubakr, vinginevyo kwa Hafsah itakuwa ni afadhali zaidi Mtume ampende yeye kwani hapakuwa na mambo mengi yaliyotokana naye aliyoyafanya kumuudhi Mtume, tena kwa kiwango kikubwa kuliko mambo aliyoyatenda Aisha binti Abubakr. Na tukiuchunguza ukweli halisi na tukazipuuza riwaya zilizozushwa ambazo Banu Umayyah wamezitengeneza kuhusu ubora wa Aisha, bila shaka tutakuta kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu mara nyingi alikuwa akikerwa na Aisha na mara nyingi alikuwa akimgombeza. Hapa tunanakili riwaya moja aliyoiandika Bukhari na wanachuoni wengi wa hadithi wa Kisunni inayoeleza kiwango cha kero ambayo alikuwa akiionesha Ummul-Muuminina Aisha mbele ya mumewe (ambaye ni) Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) . Bukhari amethibitisha ndani ya Sahih yake katika juzuu ya saba katika mlango wa "Kauli ya mgonjwa, hakika ninaumwa, au Eeh kichwa changu. " Amesema: Nilimsikia Qasim ibn Muhammad amesema: "Aisha alisema, Eeh, kichwa changu!" Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, "Lau hali hiyo ingekupata nami nikawa ni hai basi ningekutakia msamaha na kukuombea dua" Aisha akasema,"Ole wangu, Wallahi hakika nikuonavyo wewe (naona) unapenda nife, na lau nitakufa bila shaka jioni (usingejali bali) ungeendelea kufurahi na baadhi ya wake zako." Je, riwaya hii inakujulisha juu ya Mtume kumpenda Aisha?

Mwisho tunafupisha (kwa kusema) kwamba, hakika Banu Umayyah wakiongozwa na Muawiya ibn Abi Sufiyan wanamchukia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , na tangu pale Ukhalifa ulipowazungukia walifanya (kila njia) kuubadilisha ukweli kinyumenyume, wakawapandisha (kwa ubora) watu fulani fulani mpaka wakawafikisha kwenye daraja la kusifiwa na kutukuzwa, wakati ambapo (watu hao) katika zama za uhai wa Mtume(s.a.w.w) walikuwa ni watu wa kawaida tu wala hawakuwa na lolote la maana. Na wakati huo huo Banu Umayyah waliwanyanyasa watu wengine ambao walikuwa katika daraja tukufu na yenye heshima katika siku za uhai wa Mtume(s.a.w.w) . Mimi naamini kwamba, kipimo chao pekee katika kuwapandisha daraja baadhi ya watu na kuwanyanyasa wengine hakuna isipokuwa ni ule uadui wao mkali na chuki yao isiyo na kipimo dhidi ya Mtume Muhammad na watu wa nyumba yake (ambao ni) Ali, Fatmah, Hasan na Husein (a.s) . Na kwa hali hiyo kila mtu ambaye alikuwa mpinzani wa Mtume(s.a.w.w) na watu wa nyumba yake ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na amewatakasa sana sana, Banu Umayyah walimpandisha daraja na kumtengenezea riwaya na ubora kemkem, walimkumbatia na kumpa vyeo na zawadi nyingi na hatimaye akawa mwenye hadhi kwa kutukuzwa na watu na kuheshimiwa.

Ama kila yule aliyekuwa akimpenda Mtume(s.a.w.w) na akimtetea, wao walifanya kila juhudi kumuangusha na kumzushia maovu ya uongo na kumtengnezea riwaya ambazo zinakanusha heshima yake na ubora wake. Kwa hakika hali kama hii ndiyo iliyomfanya Umar ibn Khatab akawa ndiyo kiongozi mkuu wa Uislamu katika zama za utawala wa Banu Umayyah, Umar ambaye alikuwa akimpinga Mtume(s.a.w.w) katika kila maamrisho yake mpaka akamtuhumu Mtume(s.a.w.w) kwamba anaweweseka wakati wa mwisho wa uhai wake Mtume(s.a.w.w) .

Ama Ali ibn Abi Talib ambaye kwa Mtume(s.a.w.w) alikuwa na cheo kama kile cha Nabii Harun kwa Nabii Musa, na ambaye alikuwa akimpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wakimpenda (Ali) ambaye ni mtawala wa kila muumini, zilipofika zama za utawala wa Banu Umayyah akawa analaaniwa kwenye Minbar za Waislamu kwa muda wa miaka themanini. Hali kama hii (katika dola ya Banu Umayyah) Aisha ambaye alimsonga koo Mtume(s.a.w.w) na akaasi amri zake nyingi kama ambavyo (kwa kumuasi Mtume) alimuasi Mola wake na akampiga vita wasii wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na kwa fitina yake hiyo kubwa ambayo Waislamu waliifahamu, alisababisha mauaji ya maelfu ya Waislamu. basi mwanamke huyu akawa ndiyo mwanamke mashuhuri katika Uislamu na eti watu wajifunze kwake hukumu za dini. Ama bibi Fatmah Zahra mwanamke bora ulimwenguni, ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu hukasirika pindi Fatmah anapokasirika na huwa radhi Mwenyezi Mungu pindi Fatmah anapokuwa radhi, huyu akawa ni mtu aliyesahauliwa kabisa, kiasi kwamba alipofariki alizikwa usiku tena kwa siri. Na kabla ya hapo alitishiwa kuchomwa moto, na walimkamua tumbo lake kwa kumbana na mlango mpaka ujauzito ukampromoka, na kutokana na mazingira haya hakuna hata Muislamu mmoja katika Masunni anayefahamu japo riwaya moja aliyoipokea Fatmah kutoka kwa baba yake.

Hali ni hiyo hiyo (kwa shinikizo la Banu Umayyah) Yazid ibn Muawiyah na Ziyad mwana wa baba yake na mwana wa Mar-wan na Haj-Jaj na mwana Al'as na wengineo miongoni mwa waovu waliolaaniwa kwa mujibu wa Qur'an kupitia ulimi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, wote hawa wakawa ndiyo viongozi wa waumini na watawala wa mambo yao. Ama Hassan na Husein ambao ni mabwana wa vijana wa peponi na ni kiliwazo cha Mtume katika umma huu na ambao ni Maimamu wanaotokana na kizazi cha Mtume(s.a.w.w) ambao ndiyo ngome ya umma huu, wao wakawa ni wenye kufukuzwa, kutiwa magerezani na kuuawa kwa kutiliwa sumu. Mazingira ni yale yale, yule mnafiki Abu Sufiyan ambaye hapana vita yoyote iliyotokea dhidi ya Mtume isipokuwa yeye alikuwa ni kiongozi wa vita hiyo, huyu akawa mwenye kusifiwa na kushukuriwa mpaka ikasemwa eti Mtume kasema: "Yeyote atakayeingia ndani ya nyumba ya Abu Sufiyan atakuwa katika amani."

Kinyume chake Bwana Abu Talib ambaye ni mlezi wa Mtume(s.a.w.w) na alimlinda Mtume kwa uwezo wake wote, na yeye ndiye aliyetumia uhai wake akiwapinga jamaa zake na watu wake kwa ajili ya kufanikisha mwito wa mtoto wa nduguye kiasi kwamba aliishi miaka mitatu ndani vikwazo vya kiuchumi pamoja na Mtume kwenye viunga vya mji wa Maka, na aliificha imani yake kwa ajili ya maslahi ya Uislamu, ili tu zipatikane njia za yeye kuwa pamoja na Maquraish wasiwaudhi Waislamu kwa namna wanavyotaka, na hilo ni kama ilivyokuwa kwa yule Muumini wa jamaa ya Firaun aliyeficha imani yake, Abu Talib huyu malipo yake yakawa eti yumo ndani ya moto wenye joto hafifu na akiweka humo mguu wake mafuta yaliyoko katikati ya mifupa yake yatachemka. Kadhalika hali ni hiyo hiyo kwa Muawiya ibn Abi Sufiyan, ambaye ni muachwa huru mwana wa muachwa huru na ni mwenye kulaaniwa mwana wa aliyelaaniwa, mtu ambaye lizichezea hukumu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wala hakuzipa uzito unaostahiki, ambaye aliwauwa watu wema wasio na kosa lolote ili tu apate kuyatimiza malengo yake maovu, mtu ambaye alimtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu mbele ya macho na masikio ya Waislamu, mtu huyu akawa anaitwa ndiye mwandishi wa wahyi, na wanasema eti kwamba Mwenyezi Mungu amewaamini juu ya wahyi wake Jibril, Muhammad na Muawiyah, huyu akawa husifiwa kuwa yeye ni mwenye hekima, siasa na mnadhimu bora. Watu kama Abu Dharri Al-ghifari ambaye hapakuwepo mkweli kuliko yeye, huyu akaonekana kuwa ndiyo mwenye fitina. akapigwa na kufukuzwa na kuondolewa mjini Madina akapelekwa "Rabdhah."

Nao Salmaan Al-Farisi, Miqdad, Ammar, Hudhaifah na Masahaba wote wema ambao walimtawalisha Ali na wakamfuata, kwa hakika walipambana na mateso na walitawanywa ovyo na kuuawa. Kutokana na mazingira haya basi, wafuasi wa Makhalifa, wafuasi wa Muawiyah na wafuasi wa madhehebu ambayo yaliundwa na tawala za kidhalimu, wao ndiyo waitwao "Ahl-lus-sunnah Wal-jamaa" ambao (kwa mtazamo wao)wanajiona kuwa ni wao pekee ndiyo wanaoutekeleza Uislamu ipasavyo na yeyote anayewapinga wanamuona kuwa yu miongoni mwa makafiri, hata kama atakuwa ni mfuasi wa Maimamu wema wa nyumba ya Mtume waliotakasika. Ama wafuasi wa Maimamu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w) , ambao wamemfuata (Ali) ambaye ni mlango wa elimu na mtu wa kwanza kusilimu, ambaye haki huzunguka pamoja naye popote alipo, na wakawafuata watu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w) ambao ni Maimamu Maasum, basi hawa wakawa ndiyo (huitwa) watu wa bid'a na upotofu, na yeyote mwenye kuwapinga na kuwapiga vita huyo ndiyo Mwislamu sawa sawa. "Lahaula wala quwwata illa billahil-aliyyil-adhim. " Amesema kweli Mwenyezi Mungu pale aliposema:"Na wanapoambiwa, msifanye uharibifu ulimwenguni wao husema, Sisi ni watenda mema, Hakika wao ni waharibifu lakini hawatambui. Na wanapoambiwa aminini kama walivyoamini watu, husema, Oh hivi sisi tuamini kama walivyoamini wapumbavu". Hakika wao ndiyo wapumbavu lakini hawatambui" (Qur'an 2:11-13).

6

WAULIZE WANAOFAHAMU

Na tukirejea kwenye maudhui ya Mtume(s.a.w.w) kumpenda Aisha kwa kuwa eti alihifadhi kutoka kwa Mtume nusu ya dini, na yeye Mtume alikuwa akisema, "Chukuweni nusu ya dini yenu kutoka kwa kijanajike hiki chekundu". Hadithi hii haifai wala haina msingi wowote wa kusihi kwake, wala haiwezi kulingana na hadithi ambazo zimepokewa kutoka kwa yeye Aisha (akielezea) miongoni mwa hukumu zinazochekesha na kuhuzunisha, hadithi ambazo (ukweli ulivyo) Mtume wa Mwenyezi Mungu kamwe hakuzisema. Basi hebu na tutosheke na mfano mmoja juu ya hayo unaohusu suala la kumnyonyesha mtu mzima, hadithi ambayo Aisha alikuwa akiieleza kuwa imetoka kwa Mtume(s.a.w.w) na ni hadithi ambayo Muslim ameithibitisha ndani ya Sahihi yake, na Maliki naye ndani ya Muwatta yake na ni hadithi ambayo tumetosheleza juu ya uchunguzi wetu kuhusiana nayo ndani ya kitabu chetu "Liakuna Maas-Sadiqin" basi atakaye ufafanuzi na uthibitisho wa uwazi wa mambo na akirejee kitabu hicho. Na itoshe tu kuhusu riwaya hii mbaya ya kwamba wakeze Mtume wote waliyapinga matumizi yake na wakaikanusha mno kiasi kwamba hata huyo aliyeipokea alibakia kwa mwaka zima anaogopa kuitaja kutokana na ubaya wake na kutokuwa na haya. Na tutakapoirejea Sahihi Bukhari katika mlango usemao, "Sala hupungnzwa mtu akitoka nyumbani mwake " amesema: Kutoka kwa Az-zuhri, naye kutoka kwa Ur-wah, amepokea toka kwa Aisha (r.a) amesema: "Hapo mwanzo Sala ilifaradhishwa rakaa mbili, Sala ya safari ikabakishwa (kuwa rakaa mbili) na Sala isiyo ya safari ikakamilishwa (kuwa rakaa nne). Az-Zuhri akasema nikamwambia Ur-Wah, mbona Aisha anakamilisha (rakaa nne katika safari)? Akasema, Anabadilisha kama alivyobadilisha Uthman" Riwaya hii ameithibitisha Muslim ndani ya Sahihi yake katika mlango wa Sala ya wenye safari na kuipunguza.

Kwa maelezo yaliyowazi zaidi ni kama ilivyo ndani ya Bukhari amesema: "Imepokewa kutoka kwa Az-zuhri, naye kutoka kwa Ur-wah naye kutoka kwa Aisha kwamba, hapo mwanzo Sala ilifaradhishwa rakaa mbili, basi Sala ya safari ikabakishwa kuwa rakaa mbili na Sala isiyo ya safari ikakamilishwa (kwa rakaa nne) Az-zuhri akasema, nikamuuliza Ur-wah mbona Aisha anakamilisha (rakaa nne) katika safari? akasema: "Amebadilisha kama alivyobadilisha Uthman." Bila shaka ni kupingana kuliko dhahiri, yeye mwenyewe bibi Aisha ndiye aliyepokea kwamba Sala ya msafiri ilifaradhishwa rakaa mbili, lakini ni yeye huyo huyo anafanya kinyume cha vile alivyofaradhisha Mwenyezi Mungu na alivyofanya Mtume wake, na anabadilisha na kuzigeuza hukumu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili aimarishe sunna ya Uthman, na kwa sababu hizi basi tunakuta ndani ya Sihah za Ahlis-Sunnah wal-jamaa mna hukumu nyingi lakini hawazitumii kwa kuwa wao mara nyingi wanatumia (hukumu) zilizoanzishwa na Abubakr na zile zilizoanzishwa na Ummar, Uthman, Aisha na zile alizoanzisha Muawiyah ibn Abi Sufiyan na Masahaba wengineo. Sasa basi iwapo kijanajike hiki chekundu ambacho kwake inapatikana nusu ya dini kinafanya mabadiliko katika hukumu za Mwenyezi Mungu vile kinavyopenda, mimi siamini kwamba mumewe ambaye ni Mtume wa mwenyezi Mungu(s.a.w.w) anakiridhia, na katika hali hiyo awaamuru watu wakifuate. Wakati huo huo kumekuja riwaya ndani ya Sahihi Bukhari na Sihah nyigine za Masunni zikiashiria kwamba, kukifuata (kijanajike chekundu hicho) ndani yake kuna maasi dhidi ya Mwenyezi Mungu, na tutakutosheleza kwa hilo utapofika wakati wake apendapo Mwenyezi Mungu.

Ama wale wasemao kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alikuwa akimpenda bibi Aisha kwa sababu Jibril alimjia Mtume akiwa na picha ya bibi Aisha kabla hata hajamuoa, na kwamba Jibril alikuwa haingii kwa Mtume ila awapo nyumbani kwa bibi Aisha, riwaya hizi zinawachekesha hata wenda wazimu, kwa sababu mimi binafsi sifahamu iwapo picha hiyo aliyokuja nayo Jibril ilikuwa ni ya Photograph au ya kuchora, wakati ambapo Ahlus-sunna wanazo riwaya kwamba, Abubakr ndiye alimtuma Aisha aende kwa Mtume akiwa na chombo kilichotiwa tende ili tu Mtume amuangalie Aisha, na Abubakr yeye ndiye aliyemtaka Mtume(s.a.w.w) amuoe Binti yake huyo, basi je, kulikuwa na haja gani kwa Jibril kushuka na picha yake wakati Mwanaisha anaishi umbali wa mita chache tu kutoka nyumbani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ? Mimi naamini kwamba bibi Mariyah Al-qibtiyyah aliyekuwa akiishi Misri akiwa mbali na Mtume(s.a.w.w) na hapana yeyote aliyekuwa akitazamia kuja kwake, yeye ndiye aliyestahiki kuwa Jibril ashuke na picha yake na ambashirie Mtume(s.a.w.w) kwamba Mwenyezi Mungu atamruzuku kutokana naye Ibrahim.

Lakini riwaya hizi ni miongoni mwa uzushi wa Aisha ambaye alikuwa hapati kitu cha kujifaharisha kwa wake wenzi isipokuwa visa ambavyo mawazo yake huvizusha, au riwaya hizo ni katika uzushi wa Banu Umayyah kwa kupitia ulimi wa bibi Aisha ili wapate kuyatukuza mambo yake mbele ya watu wenye akili finyu. Ama kusema kwamba Jibril alikuwa haingii nyumbani kwa Mtume akiwa kalala isipokuwa nyumbani kwa Aisha riwaya hii ni mbaya kuliko ile ya kwanza, kwani kinachofahamika katika Qur'an ni kuwa, Mwenyezi Mungu alimkemea bibi Aisha pale alipokula njama dhidi ya Mtume wake, akamkemea kwa kumjulisha kwamba, ''Jibril na Waumini wema na Malaika baada ya msaada wake (Mwenyezi Mungu) watamsaidia (Mjumbe wa Mwenyezi Mungu). Basi kauli za Masheikhe wetu si chochote isipokuwa ni dhana na mawazo yao tu, na kwa hakika dhana haitoshelezi cho chote mbele ya haki, basi waambie je mnayo elimu yoyote ile muitoe kwetu sisi, (hamna) bali hakuna mnachokifuata isipokuwa ni dhana na hamna chochote ila mnazua tu. Aisha baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) Ama tunapoyasoma maisha ya Ummul-Muminina Aisha binti Abubakr baada ya mumewe kufariki (roho yangu iwe fidia yake) na baada ya mambo kumkalia vizuri na baba yake kuwa ndiyo Khalifa na kiongozi juu ya umma wa Kiislamu, hapo ndipo bibi Aisha akawa yeye ndiye mwanamke bora katika dola ya Kiislamu kwa kuwa mumewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na baba yake ni Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Kwa kuwa yeye anaamini au anadhani kuwa ndiye mbora miongoni mwa wakeze Mtume(s.a.w.w) , si kwa chochote bali kwa kuwa Mtume alimuoa akiwa bikra, na Mtume hakupata kuoa mwanamke bikra ila yeye, kisha Mtume(s.a.w.w) alifishwa na yeye bibi Aisha akiwa katika umri wa ujana, kwani umri wake ulikuwa miaka kumi na minane siku Mtume alipofishwa kwa mujibu wa makadirio ya juu na riwaya zilizo mashuhuri. Na wala hakuishi pamoja na Mtume isipokuwa miaka sita au minane kwa tofauti za riwaya, kwani miaka ile ya mwanzo aliimaliza akicheza michezo ya kitoto hali yakuwa ni mke wa Mtume(s.a.w.w) na katika hali hiyo kama alivyomueleza Burairah mjakazi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) aliposema kuhusu Aisha: "Hakika yeye ni msichana mdogo akilala na kuuacha unga uliokandwa na matokeo yake huja mnyama miongoni mwa wanyama wafugwao na kula ule unga uliokandwa." Naam miaka kumi na minane kwa msichana aliyefikia umri wa kuvunja ungo kama isemwavyo hivi leo, na aliyetumia nusu ya umri wake akiwa pamoja na Mtume na akiwa miongoni mwa wakewenza wanaofikia kumi au tisa, na (siyo wakeze Mtume tu alioishi nao bibi Aisha nyumbani kwa Mtume) bali kuna mwanamke mwingine ambaye tumeghafilika kumtaja aliyekuwepo katika zama za maisha ya bibi Aisha. Mwanamke huyo alikuwa ni tishio kwa Aisha kuliko mkemwenziwe yeyote, kwani upendo wa Mtume(s.a.w.w) kwake ulikuwa hauna mfano naye si mwingine bali ni Fatmah ambaye ni binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) aliyemzaa kwa bibi Khadija, na Khadija huyu Mkuu ni nani? Huyo ni Khadija ambaye Jibril alimtolea salam na kumbashiria nyumba peponi isiyokuwa na fujo wala makelele Khadija ambaye ilikuwa haiwezekani kupita tukio lolote isipokuwa Mtume(s.a.w.w) humtaja Khadija, na hapo ndipo Aisha maini humkata na moyo kumuwaka kwa wivu, kwa hasira zake hufura na kupoteza muruwa wake, akawa hutukana kwa lile aonalo linafaa na bila kujali heshima na uhusiano uliopo kati yake na mumewe.

Hebu na tumsikilize yeye mwenyewe bibi Aisha anasimulia juu ya Khadija kama alivyopokea Bukhari, Ahmad, Tirmidhi na Ibn Majah: Amesema bibi Aisha, "Sikumuonea wivu mke yeyote wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kama nilivyomuonea wivu Khadija na hii ni kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akimtaja mara nyingi na kumsifu, basi nilimwambia (Mtume) ni kwa jambo gani unamtaja ajuza huyu miongoni mwa maajuza wa Kiquraish mwenye kona za midomo myekundu, na amekwisha kufa zamani, hapana Mwenyezi Mungu amekubadilishia mbora kuliko yeye." Bibi Aisha anasema, (ghafla) uso wa Mtume ulibadilika sana na nilikuwa siuoni kubadilika hivyo ila unaposhuka Wahyi na akasema (Mtume): "Wallahi Mwenyezi Mungu hajanibadilishia mke bora kuliko yeye (Khadija), kwa hakika aliniamini wakati watu waliponipinga na alinisadiki wakati watu waliponikatalia na aliniruhusu nitumie mali yake wakati watu waliponinyima na Mwenyezi Mungu aliniruzuku watoto kwake wakati alininyima watoto kwa wanawake wengine." Hapana shaka kwamba jibu la Mtume(s.a.w.w) kwa Aisha linabatilisha madai ya wale wasemao kwamba Aisha alikuwa bora mno na akipendwa mno miongoni mwa wake wa Mtume(s.a.w.w). Na ubaya zaidi ni kwamba, Aisha aliongeza wivu na chuki kwa Khadija pale Mtume wa Mwenyezi Mungu alipomkemea kwa kemeo hili na akamjulisha kwamba Mola wake hajambadilisha mke bora kuliko Khadija. Ni kwa mara nyingine tena Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) anatufahamisha kwamba yeye hafuati matamanio na wala hapendi (kwa sababu ya) uzuri na bikra, kwani Khadija (a.s) kabla ya Mtume(s.a.w.w) alikuwa kisha olewa mara mbili na alikuwa mkubwa zaidi ya Mtume kwa miaka kumi na mitano, lakini pamoja na hayo Mtume alimpenda mno wala hakuacha kumtaja, na kwa hali hii naapa kuwa hii ndiyo tabia ya Mtume(s.a.w.w) ambaye hupenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na huchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo basi kuna tofauti kubwa kati ya riwaya hii ya kweli na zile riwaya zilizoundwa ambazo zinadai kwamba Mtume(s.a.w.w) alikuwa akimpenda mno Aisha mpaka wakeze wanamtumia ujumbe kumtaka awe muadilifu kuhusu Binti ya Abu Quhafah. Na hebu tumuulize Ummul-Muminina Aisha ambaye hakupata kumuona Bibi Khadija japo mara moja katika uhai wake wala hakukutana naye, ni vipi anamsema kuwa ni kikongwe mwenye kona za midomo myekundu? Na je, hii ndiyo tabia ya mwanamke Muumini wa kawaida ambaye inaharamishwa kwake kumteta mwenzake awapo hai, basi vipi itakuwa hali kwa yule aliyekwisha kufa na kufika mbele ya Mola wake? Basi hali itakuwaje ikiwa mke wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ndiye atetwaye, mke ambaye Jibril alikuwa akishuka nyumbani mwake na kumbashiria kupata nyumba yenye utulivu peponi? Na kwa kutilia mkazo ni kwamba, chuki na wivu uliokuwa ukifukuta ndani ya moyo wa Aisha kwa sababu ya Khadija ilikuwa ni lazima ufure na upate mahali pa kupumulia, vinginevyo bibi Aisha angepasuka!! Kwa hiyo basi Aisha hakupata (mahali pa kushushia pumzi zake) isipokuwa hapo mbele yake alikuweko Fatmah binti ya Khadija ambaye ni mtoto wa kambo wa bibi Aisha na ambaye alikuwa katika umri unaolingana naye au anamzidi kidogo kwa (mujibu wa) tofauti ya riwaya. Bila shaka vile vile kwamba lile pendo la kweli la Mtume(s.a.w.w) kwa Khadija lilitengenezeka na kuimarika kwa binti yake wa pekee Fatmah, kwani ndiye yeye peke yake aliyeishi pamoja na baba yake akiwa amebeba sifa njema kutoka kwa Khadija ambazo Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akizipenda, Mtume akawa humwita (Fatmah) mama wa baba yake.

Bibi Aisha alizidi wivu kumuona Mtume wa Mwenyezi Mungu anamtukuza na kumwita kuwa yeye ni mwanamke bora kuliko wanawake wote ulimwenguni na ni mwanamke bora kati ya wanawake wa peponi. Kisha Mwenyezi Mungu akamruzuku Mtume kutokana na Binti yake huyu mabwana wa vijana wa peponi Hasan na Husein, na ndiyo maana Aisha akawa humuona Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) anakwenda kwa Fatmah na kukesha huko kwa ajili ya kuwalea wajukuu zake na anasema: "Wanangu hawa wawili ni viliwazo vyangu katika umma huu." Ikawa huwabeba mabegani kwake, na yote hayo humuongezea Aisha wivu kwa kuwa yeye ni mgumba. Kisha Aisha alizidi wivu mpaka akamuingiza katika wivu huo mume wa Fatmah baba wa Hasan na Husein, si kwa lolote bali ni kwa sababu ya Mtume akimpenda mno mume wa Fatmah na kumtanguliza mbele kuliko baba yake Aisha kwa kila hali, basi hapana shaka kwamba, bibi Aisha alikuwa akiishi katika mazingira haya. Hatimaye anamuona mwana wa Abu-Talib (Ali) anafuzu kila mara dhidi ya baba yake (Aisha) na anakuwa mbele kwa kupendwa na Mtume(s.a.w.w) na kumtanguliza juu ya wengine.

Aisha hakika alikuwa akifahamu kwamba baba yake alirudi akiwa ameshindwa katika vita ya Khaibar yeye pamoja na aliokuwa nao katika jeshi, na kwamba Mtume(s.a.w.w) alihuzunishwa na jambo hilo na akasema: "Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda mtu huyo, ni shujaa wala si mwoga." Na mtu huyo alikuwa ni Ali ibn Abu Talib mume wa Fatmah, kisha Ali alirudi baada ya kushinda vita ya Khaibar akiwa na Safiyyah binti Huyayi ambaye Mtume(s.a.w.w) alimuoa na kwa hilo moyo wa Aisha ukawa kama umepigwa na radi. Kadhalika Aisha alifahamu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alimtuma baba yake akiwa na Suratul-Baraah ili akaifikishe (awasomee) Mahujaji, lakini baadaye Mtume alimtuma Ali ibn Abi Talib amfuate na akaichukue kutoka kwa Abubakr, na huyo baba yake Aisha akarudi huku analia na kumuuliza Mtume sababu (ya kumrudisha). Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akamjibu, "Hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru asifikishe Surah hiyo isipokuwa mimi au mmoja katika watu wa nyumba yangu."

Bila shaka vile vile bibi Aisha alikuwa akifahamu kwamba Mtume(s.a.w.w) alimtawaza mwana wa ammi yake Ali(a.s) awe ni Khalifa kwa Waislamu baada yake, na akawaamuru Masahaba na wake zao wampongeze kwa kupata uongozi kwa waumini, na baba yake Aisha alikuja akiwa miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo huku akisema: "Pongezi pongezi ewe Mwana wa Abu Talib, leo umekuwa kiongozi wa kila Muumini mwanaume na Muumini wa kike." Bila shaka Bibi Aisha alikuwa akifahamu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimpa uamiri jeshi kijana mdogo mwenye umri wa miaka kumi na saba juu ya baba yake, na Mtume akamuamuru baba yake Aisha aende akiwa chini ya uongozi wa kijana na huyu na aswali nyuma yake. Hapana shaka kwamba Ummul-Muuminina Aisha alijihusisha kikamilifu katika matukio haya, kwani (yaonekana) alikuwa amekamia makusudio ya baba yake ya kugombea Ukhalifa na njama hizo zilikuwa zikipikwa na viongozi wa makabila katika Maquraish. Kwa hiyo basi alikuwa akizidisha chuki na ubaya dhidi ya Ali na Fatmah, na akijaribu kwa kila juhudi kuingilia kati ili kubadilisha msimamo kwa ajili ya maslahi ya baba yake kwa njia mbali mbali na kwa gharama yoyote ile.

Bila shaka tumekwisha muona ni jinsi gani alivyomwita baba yake eti kwa niyaba ya Mtume na akamuamuru aswalishe watu, baada ya yeye Bibi Aisha kugundua kwamba Mtume(s.a.w.w) amemwita Ali ili amkabidhi jukumu hilo, na Mtume alipoifahamu njama hiyo alilazimika kutoka (kwenda msikitini) na hapo ndipo Abubakr alipompisha Mtume(s.a.w.w) akawasalisha watu hali ya kuwa amekaa, na akamkemea kwa kumwambia. "Hakika ninyi ndiyo wale wanawake waliomfanyia vitimbi Yusuf' akiwa na maana kwamba, Vitimbi vya Aisha ni vikubwa. Na mtu yeyote mwenye kufanya uchambuzi ndani ya tukio hili ambalo bibi Aisha mwenyewe amelisimulia kwa njia ya riwaya zenye kutofautiana na kupingana, atakuta kuna mgongano ulio wazi kwani ilivyo ndivyo ni kwamba Mtume(s.a.w.w) alikuwa kisha muandaa baba yake Aisha na kumuamuru atoke katika jeshi chini ya uongozi wa Usamah ibn Zaidi kabla ya kuswaliwa kwa Sala hiyo siku tatu kabla. Inavyofahamika moja kwa moja ni kwamba, kiongozi wa jeshi ndiye Imamu katika Sala, kwa hiyo Usamah alikuwa ni Imam wa Abubakr ndani ya msafara wa jeshi hilo.

Bibi Aisha alipokwishafahamu jambo hilo aliona kuwa ni udhalili kwa baba yake na aliyajua makusudio ya Mtume(s.a.w.w) , na hasa alipogundua kwamba Mtume hakumchagua Ali ibn Abi Talib kuwemo ndani ya jeshi hilo ambalo alikuwa ameliandaa ili ndani ya jeshi hilo wawemo vigogo wa Muhajirina na Ansar ambao kwa Maquraish walikuwa ni watu watukufu na wenye daraja kubwa.

Isitoshe mama Aisha alikwisha fahamu kama ambavyo wengi wa masahaba walikwisha fahamu kuwa siku za kuishi Mtume(s.a.w.w) zimebakia za kuhesabu, na huenda bibi Aisha aliungana na maoni ya Umar ibn Khattab kwamba sasa Mtume anaweweseka hajui alifanyalo. Kwa sababu hiyo wivu wake mkali ukamlazimisha kufanya vile aonavyo ili mradi tu akinyanyue cheo cha baba yake dhidi ya Ali Bin Abi Talib ambaye ni mgomvi wake.

Kutokana na yote haya ndiyo maana bibi Aisha alikanusha kuwa Mtume aliusia kuwa Ali ni Khalifa, na kwa sababu hiyo alitaka kuwakinaisha watu wenye mawazo finyu kwamba Mtume(s.a.w.w) alikufa akiwa amempakata na ameegemea kifuani kwake, na pia ndiyo maana akasimulia kwa kusema kwamba, "Mtume alipokuwa mgonjwa alimwambia (bibi Aisha) niitie baba yako na nduguyo ili niwaandikie maandiko kwani huenda akadai mwenye kudai, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini hawamkubali yeyote isipokuwa Abubakr." Basi Je, kuna mwenye kumuuliza bibi Aisha, "Ni jambo gani lililomzuwia asiwaite?".