WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU0%

WAULIZE WANAOFAHAMU Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi: Muhammad Tijani As-samawi At-Tunisi
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 51495
Pakua: 5470

Maelezo zaidi:

WAULIZE WANAOFAHAMU
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 26 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 51495 / Pakua: 5470
Kiwango Kiwango Kiwango
WAULIZE WANAOFAHAMU

WAULIZE WANAOFAHAMU

Mwandishi:
Swahili

7

WAULIZE WANAOFAHAMU

MSIMAMO WA AISHA DHIDI YA AMIRUL-MUUMININA ALI (A.S.)

Kwa mtafiti yeyote juu ya msimamo wa bibi Aisha dhidi ya Abul-Hasan Ali(a.s) , atakuta mambo ya ajabu na ya kushangaza na hataweza kupata tafsiri yoyote kwa mambo hayo isipokuwa ni wivu na uadui dhidi ya watu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.w) . Historia imezisajili chuki na bughdha za bibi Aisha kwa Imam Ali, chuki ambazo hazina mfano, na zilifikia kiasi cha bibi Aisha kushindwa hata kulitamka jina la Imam Ali(a.s) na wala hataki hata kumuona, na aliposikia kuwa watu wamempa baia Imamu Ali kuwa Khalifa baada ya kuuawa Uthman akasema: 'Natamani lau mbingu ingeifunika ardhi kabla hajaukalia Ukhalifa mwana wa Abutalib." Hapo ndipo bibi Aisha alipofanya kila njia kumuangamiza Imam Ali na akaongoza jeshi kubwa ili kumpiga Ali(a.s) na hatimaye zilipomfikia habari kwamba Imamu Ali amefariki alisujudu sijda ya kumshukuru Mwenyezi Mungu. Je, kwa nini hamuwashangai pamoja nami Masunni ambao wanasimulia ndani ya vitabu vyao kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: "Ewe Ali hatakupenda isipokuwa Muumini na hatakuchukia isipokuwa mnafiki" Kisha wanasimulia ndani ya Sihah zao na Musnad zao na vitabu vyao vya historia kwamba bibi Aisha akimchukia Imam Ali kiasi cha kushindwa hata kulitamka jina lake. Basi je, huo si ushahidi unaotoka kwao juu ya hali halisi ya mwanamke (huyu)? Kama ambavyo Bukhari anavyosimulia ndani ya Sahihi yake kwamba, Mtume(s.a.w.w) amesema: "Fatmah ni sehemu itokanayo nami, yeyote mwenye kumkasirisha (atakuwa) kanikasirisha mimi, na mwenye kunikasirisha mimi basi hakika kamkasirisha Mwenyezi Mungu ."

Kisha Bukhari huyo huyo anasimulia kwamba, Fatmah alikufa hali ya kuwa amemkasirikia Abubakr na mpaka amefariki hakumsemesha. Je, huo sio ushahidi utokanao na wao (Ahlul-Sunnah) kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamemkasirikia Abubakr? Ukweli unafahamika kwa kila mwenye akili. Ndiyo maana Mimi siku zote nasema kwamba, ukweli hapana budi uonekane japokuwa watu waovu watauficha na kwa namna yoyote (ukweli utadhihiri) japokuwa watetezi wa Banu Umayyah watajaribu kuuvuruga, kwani hoja ya Mwenyezi Mungu imesimama juu ya waja wake tangu siku Qur'an iliposhuka mpaka siku ya Qiyama "Kila sifa njema anastahiki kusifiwa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu. " Imam Ahmad ibn Hambal amesimulia kwamba, "Siku moja Abubakr alikuja na kubisha hodi kwa Mtume(s.a.w.w) , na kabla hajaingia aliisikia sauti ya Aisha imeparama juu anamwambia Mtume(s.a.w.w) , Wallahi mimi nafahamu kwamba, Ali unampenda mno kuliko mimi na baba yangu." Alikariri maneno hayo mara mbili au tatu.... Mambo ya Aisha na chuki yake dhidi ya Imam Ali yalifikia kiasi kwamba siku zote Aisha alikuwa akijaribu kumtenganisha Ali na Mtume(s.a.w.w) kwa njia zozote anazoziweza.

Na amesimulia Ibn Abil-hadid kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) siku moja alimsindikiza Imam Ali, basi mazungumzo yao yakawa marefu, na bibi Aisha alikuwa akija nyuma yao mpaka akaingia katikati yao na akawaambia mnazungumza nini nyie mbona mmerefusha (mazungumzo)? Mtume alikasirika kutokana na (tendo) hilo. Vile vile amesimulia kwamba bibi Aisha wakati fulani alimwendea Mtume(s.a.w.w) hali yakuwa anazungumza na Ali, akapiga kelele na akasema, "Kuna nini baina yangu mimi na wewe ewe mwana wa Abutalib? Hakika mimi ninayo siku moja tu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu." Mtume(s.a.w.w) alichukia. Ni mara nyingi bibi Aisha amemchukiza Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kwa matendo yake yanayotokana na wivu mkali, tabia yake ngumu na maneno yake yanayoudhi. Je, hivi ni kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu anamridhia Muumini mwanaume au Muumini wa kike ambaye moyo wake umejaa chuki na bughudha dhidi ya mwana wa ammi yake na Bwana wa kizazi chake ambaye Mtume amesema kumuhusu yeye kuwa, "Anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda."

Na akasema Mtume juu ya Ali(a.s) . "Yeyote mwenye kumpenda Ali basi bila shaka kanipenda mimi, na yeyote mwenye kumchukia Ali basi bila shaka kanichukia mimi" Tulieni majumbani mwenu wala msioneshe mapambo yenu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamuru wakeze Mtume(s.a.w.w) watulie majumbani mwao na wala wasitoke hali wamedhihirisha mapambo yao, na akawaamuru wasome Qur'an, wadumishe Sala, watoe Zaka na wamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w) . Wakeze Mtume(s.a.w.w) wote waliitumia na kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume wake ambaye naye aliwakataza wakeze kabla ya kufa kwake na kuwahadharisha aliposema; "Ni nani kati yenu atakayepanda ngamia na watambwekea mbwa wa Hauab?" Wakeze Mtume wote (walifuata amri) isipokuwa Aisha ambaye alivunja amri zote na kupuuza maonyo (ya Mtume(s.a.w.w) . Wanahistoria wanaeleza kwamba Hafsah binti Umar alitaka kutoka pamoja na Aisha, lakini nduguye Hafsah Bwana Abdallah alimhadharisha na akamsomea aya (inayohusu katazo la kutoka) basi akavunja azma yake ya kutoka, Amma Aisha yeye alipanda ngamia na wakambwekea mbwa wa Hauab. Twaha Husein ndani ya kitabu chake kiitwacho, "Al-fitnatul-kubra anasema: "Aisha alipita mahala penye maji, mara mbwa wa mahala hapo wakambwekea na akauliza kuwa maji haya ni ya mahali gani? Akaambiwa kuwa hapo ni Hauab ."

Alitishika sana na akasema; "Nirudisheni, nirudisheni hakika nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema na mbele yake walikuwepo wakeze (akatuambia) Ni nani kati yenu atakayebwekewa na mbwa na Hauab? Abdallah ibn Zubair akaja akamtuliza bibi Aisha na akamletea watu hamsini katika Baniamir wakamuapia viapo vya uongo kwamba maji haya siyo maji ya Hauab. Mimi naamini kwamba riwaya hii iliwekwa katika zama za utawala wa Bani Umayyah ili kumpunguzia Ummul-Muuminina uzito wa maasi yake, hali yakuwa wakitegemea kwamba Ummul-Muuminina (Aisha) atasameheka baada ya mtoto wa dada yake Bwana Abdallah ibn Zubair kumhadaa na kumletea watu hamsini wakamuapia kwa Mwenyezi Mungu na kumpa ushahidi wa uongo kwamba maji yale siyo maji ya Hauab. Kwa hakika ni upuuzi mtupu, wanataka (hao Banu Umayyah) kuzipamba riwaya kama hizi kwa watu wenye akili finyu ili wawakinaishe kwamba Aisha alihadaiwa alipopita kwenye maji hayo na kusikia sauti za mbwa, na hatimaye akaulizia kuhusu mahali hapa na akaambiwa kuwa ni Hauab kisha akatishika na kusema nirudisheni nirudisheni.

Lakini je, watu hawa wapumbavu ambao waliweka riwaya hii wanaweza kumtakia msamaha Aisha katika maasi yake dhidi ya amri ya Mwenyezi Mungu iliyoshuka ndani ya Qur'ani juu ya wajibu wa yeye Aisha kutulia nyumbani mwake au wanaweza kumpa udhuru kwa kukiuka amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu iliyomtaka akae nyumbani mwake na asipande ngamia, kabla ya kufika mahali penye mibweko ya mbwa katika maji ya Hauab? Je, hivi (watu hawa) wanamuona Ummul-Muumina Aisha atasameheka baada ya kupinga nasaha ya Ummul-Muuminina Ummu-Salamah ambaye wanahistoria wanamtaja kuwa alimwambia bibi Aisha (alipoazimia kutoka): "Je, (Aisha) unakumbuka siku Mtume alipofika kwenye maji upande wa kaskazini nasi tukiwa pamoja naye kisha akakaa feragha na Ali akawa anazungumza naye kwa kipindi kirefu, mara wewe ukataka kuwavamia (kwenye mazungumzo yao), mimi nikakukataza ukanipinga na ukawavamia, lakini punde si punde ulirudi huku unalia, mimi nikakuuliza una nini? Ukasema, nimewaendea wakiwa wanazungumza nikamwambia Ali, miye kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu sina isipokuwa siku moja katika siku tisa, basi huniachii siku yangu ewe mwana wa Abu Talib? Mtume amenitazama hali ya kuwa uso wake ni mwekundu amekasirika, kisha akaniambia rudi ulikotoka, Wallahi yeyote hambughudhi (huyu Ali) ila huwa ametoka nje ya imani basi nimerudi hali yakuwa nina juta." Bibi Aisha akasema, "Jambo hilo nalikumbuka." Ummu-Salamah akasema; ninakukumbusha vile vile, tulikuwa mimi na wewe pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akatuambia: "Nani kati yenu atakayepanda ngamia, na atabwekewa na mbwa wa Hauab? Huyo atakuwa ameacha njia ya sawa." Sote tukasema, Twajilinda kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kutokana na hilo, kisha Mtume akakupiga mgongoni kwako na akasema, Ole wako ewe kijanajike chekundu, usije kuwa wewe." Aisha akasema "Hilo nalikumbuka.

"Ummu Salama akasema: "Je, unakumbuka siku alipokuja baba yako akiwa pamoja na Umar, nasi tukasimama tukaingia ndani, nao wakapita wakawa wanazungumza na Mtume kuhusu mambo yao mpaka ikafikia wakasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bila shaka sisi hatufahamu muda utakaoishi pamoja nasi, basi lau utatujulisha ni nani utakayetuachia baada yako kusudi awe ndiyo mategemeo yetu." Mtume akawaambia: "Amma mimi namuona mahala pake, lau nitafanya (kama mtakavyo) mtatofautiana juu ya mtu huyo kama walivyotofautiana wana wa Israil juu ya Haruna." Baba yako na Umar wakanyamaza na kisha wakaondoka, na walipoondoka sisi tukatoka mpaka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha wewe ukamwambia nawe ulikuwa shupavu mno kwake kuliko sisi (ukasema); "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani basi utakayewaachia?" Mtume akasema, "Ni yule anayeshona viatu." Tukatoka nje tukamuona Ali. wewe ukasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu simuoni isipokuwa Ali." Mtume akasema "Huyo ndiye . " Aisha akasema: "Ndiyo nakumbuka jambo hilo.'" Ummu Salamah akamwambia Aisha: "Basi baada ya yote haya ni utokaji gani utokao ewe Aisha"? Aisha akasema: "Sitoki kwa jingine lolote isipokuwa kwa ajili ya kuleta mapatano baina ya watu ".

Ummu Salamah akamkataza Aisha asitoke na akamkemea sana, akamwambia, "Bila shaka nguzo ya Uislamu ikipinda hainyooshwi na wanawake na ikivunjika haitengenezwi na wao, ukomo wa sifa za wanawake ni kuinamisha macho na kulinda heshima zao, utasema nini ewe Aisha lau kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu atakuona umepanda ngamia wako unakwenda kutoka kituo hadi kituo kingine, Wallahi lau ningekwenda kwa mwendo wako (huu) kisha nikaambiwa ingia ndani ya pepo ya Fir-daus, hakika ningeona haya kukutana na Muhammad hali yakuwa nimevua hijabu aliyonivalisha. kama ambavyo Aisha Ummul-Muumina hakukubali kusikia nasaha ya masahaba wengi wenye nia njema (pia nasaha ya ummu Salama hakuikubali). Tabari anasimulia ndani ya Tariikh yake kwamba, Jariyah ibn Qud-damah As-suudi alimwambia bibi Aisha, "Ewe Ummul Muuminina, Wallahi kuuawa Uthman ibn Af-fanni ni jambo jepesi kuliko kutoka kwako nyumbani mwako kwenda kupigana hali ya kuwa umepanda ngamia huyu aliyelaaniwa, kwa hakika wewe ulikuwa na sitara kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na umeivua sitara yako na heshima yako umeifedhehesha, kwa hakika anayeona hivi unavyopigana vita basi bila shaka anaona kukuuwa wewe ni sawa tu, basi iwapo umekuja kwetu kwa hiyari yako mwenyewe, basi rudi nyumbani kwako, na ikiwa uumekuja kwa kulazimishwa. basi waombe msaada watu hawa vvakusaidie. Ummul-muuminina Aisha (awa) kiongozi mkuu.

Wanahistoria wanaeleza kuwa, bibi Aisha alikuwa ndiyo kiongozi mkuu, yeye ndiye aliyekuwa akitawalisha (viongozi katika jeshi lake hilo) na kuwauzulu pia kutoa amri zote, mpaka kuna wakati Tal-ha na Zubair walipohitilafiana kuhusu uongozi wa Sala na kila mmoja wao akitaka awasalishe watu, bibi Aisha aliingilia kati na kuwauzulu wote wawili kisha akampa uongozi mtoto wa dada yake (Bibi Aisha) bwana Abdallah ibn Zubair awasalishe watu. Ni yeye bibi Aisha aliyekuwa akituma wajumbe wapeleke barua zake alizokuwa akizisambaza katika miji mingi kuomba msaada dhidi ya Imam Ali ibn Abi Talib na pia akichochea (ndani ya barua hizo) chuki na upinzani wa zama za ujinga. Ilifikia kiwango ambacho alifanikiwa kuandaa jeshi la watu elfu ishirini au zaidi linalotokana na watu wasiofikiri miongoni mwa Waarabu na watu wenye tamaa, (wote hawa) ni kwa ajili ya kumpiga vita na kumuangamiza jemedari wa waumini (Ali ibn Abi Talib). bali alichochea fitina mbaya ambayo ilisababisha watu wengi wauawe kwa kisingizio cha kumtetea Ummul-Muuminina na kumsaidia.

Wanahistoria wanasema kwamba, watu wa Aisha walipomfanyia khiyana Uthman ibn Hunaif aliyekuwa mtawala wa Basra na hatimaye wakamteka yeye na watu wake sabini waliokuwa wakilinda nyumba ya hazina (Baitul-Mali), kisha waliwaleta mpaka kwa Aisha akaamuru wauawe. watu hao walichinjwa kama achinjwavyo mbuzi. Na inasemekana watu hao walikuwa mia nne, na pia inasemwa kuwa ndiyo watu wa kwanza miongoni mwa Waislamu kukatwa shingo zao katika mazingira hayo. As-sha'abi amesimulia kutoka kwa Muslim ibn Abi Bakrah nave toka kwa baba yake amesema: "Wakati Twal-ha na Zubair walipofika Basra mimi nilibeba upanga wangu nikitaka kuwasaidia, nikaenda kwa Aisha nikamkuta anatoa amri na kukemea, si hivyo tu kumbe mambo yote yalikuwa chini ya mammlaka yake, hapo hapo nikaikumbuka hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) niliyomsikia akisema: Kamwe hawawezi kufanikiwa watu ambao mambo yao yanaendeshwa na mwanamke, pale pale nikaondoka na nikawaacha." Kama ambavyo Bukhari ameandika kutoka kwa Abi Bakrah kauli yake isemayo: "Hakika Mwenyezi Mungu amenipa manufaa ya neno siku ya (vita vya) Jamal, Mtume alipopata habari kwamba Wafursi wamemtawalisha binti ya Kisra akasema: Kamwe hawawezi kufanikiwa watu ambao wamempa mwanamke mammlaka ya mambo yao."

Miongoni mwa mambo yanayochekesha na kumfanya mtu alie kwa wakati mmoja ni kwamba, Aisha Ummul-Muuminina alitoka nyumbani mwake hali ya kuwa anamuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yeye huyo huyo aliwaamuru Masahaba watulizane majumbani mwao, kwa kweli ni jambo la kushangaza!! Basi yalikuwaje yote haya ewe bwana, je unayajua? Amepokea Ibn Abil-hadid Al-muutazili ndani ya Shar-h Nahjul-balagha na pia wanahistoria wengine wanasema kwamba, Aisha alipokuwa Basra aliandika barua kumuandikia Zaid ibn Sauhan Al-abadi akasema ndani ya barua hiyo: "Kutoka kwa Aisha Ummul-Muuminina binti Abi-bakris-sidiq, mke wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwenda kwa mwanawe mpendwa Zaid ibn Sauhan, amma ba'ad. Bakia nyumbani mwako na uwatenganishe watu (wasihusiane) na mwana wa Abu Talib, na (nataka) zinifikie habari nizipendazo kutoka kwako, kwani mimi nakutumainia mno miongoni mwa watu wangu, Was-Salaam." Mtu huyu mwema (Zaid ibn Sauhan) akamjibu mama Aisha kama ifuatavyo: (Barua) kutoka kwa Zaid ibn Sauhan kwenda kwa Aisha binti Abubakr ama ba'ad, bila shaka Mwenyezi Mungu amekuamuru jambo (linalokuhusu) nasi akatuamuru jambo(linalotuhusu) amekuamuru utulizane nyumbani mwako na ametuamuru sisi (tupigane) jihad, kwa hakika barua yako imenifikia ukiniamuru nifanye kinyume cha vile alivyoniamrisha Mwenyezi Mungu, na nitakuwa nimefanya yale Mwenyezi Mungu aliyokuamrisha wewe (kama nitatii amri yako) na wewe umekwisha fanya yale aliyoniamrisha mimi, kwa hiyo mimi siwezi kutii amri yako na barua yako haina jawabu."

Tukio hili linatubainishia kwamba Aisha hakutosheka na uongozi wa jeshi la ngamia peke yake. bali aliazimia kuwa amirijeshi wa waumini wote duniani, na kwa yote haya yeye ndiye aliyekuwa akiwahukumu Talha na Zubair ambao Umar ibn Khatab alikuwa amewapendekeza kwa ajili ya Ukhalifa. sasa basi, bibi Aisha kwa kuutaka uongozi (mkuu) alijihalalishia mwenyewe kuwasiliana na viongozi wa makabila na watawala, akawataka msaada na kuwapa matumaini ya mambo mbali mbali. Kutokana na yote hayo bibi Aisha alifikia daraja hiyo na umashuhuri huo mbele ya Banu Umayyah, akawa yeye ndiye anayetazamwa na kutukuzwa mbele ya wote na pia nguvu zake na upinzani wake vikawa vinaogopewa. Kwa hiyo ikiwa mashujaa na watu mashuhuri miongoni mwa mashujaa wanakimbia na kukwepa safu (ya mapambano) mbele ya Imam Ali ibn Abi Talib na wala hawawezi kusimama mbele yake, cha kushangaza Aisha alisimama kidete akachochea (vita) na kupiga makelele na akatamba. Kutokana na sababu hii basi akili (za watu) zilichanganyikiwa na wanahistoria walioufahamu msimamo wa bibi Aisha katika vita ndogo ya Jamal walishangazwa kabla ya kufika kwa Imam Ali, na pia katika vita kubwa ya Jamal baada ya kufika kwa Imam Ali na kumtaka mama Aisha arudi kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu (wafanye sulhu), lakini bibi Aisha alikataa na akang'ang'ania vita vipiganwe tena kwa ukaidi ambao hauna tafsiri isipokuwa kama tutaufahamu wivu mkali na chuki ambayo Ummul-Muuminina ameibeba dhidi ya wanawe (Waumini) waliojitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w) .

Onyo la Mtume(s.a.w.w) kwa Aisha na fitina yake.

Bila shaka Mtume(s.a.w.w) alikuwa akifahamu kwa undani mipango na njama zilizokuwa zikimzunguka kila upande, na hapana shaka kwamba alifahamu athari na fitina waliyonayo wanawake dhidi ya wanaume, kama ambavyo Mtume(s.a.w.w) alifahamu kwamba vitimbi vya wanawake ni vikubwa vinakaribia kung'oa milima. Na hasa alifahamu kuwa mkewe Aisha yeye ndiye muhusika mkuu katika njama hizi za hatari kutokana na wivu na chuki aliyonayo katika nafsi yake dhidi ya Khalifa wake na wasii wake kwa upande mmoja na watu wa nyumbani mwake Mtume kwa upande wa pili. Basi kwa nini Mtume asifahamu hali yakuwa yeye binafsi aliishi katika mazingira (yanayomuonesha wazi) msimamo wa bibi Aisha na uadui wake dhidi yao, kiasi kwamba wakati fulani Mtume alikuwa akikasirika na wakati mwingine uso wake ulikuwa ukimbadilika, na akijaribu mara nyingi kumtosheleza (kumkinaisha) bibi Aisha kwamba ampendaye Ali ni mpenzi wa Mwenyezi Mungu na yule amchukiaye Ali ni mnafiki, na Mwenyezi Mungu anamchukia mtu huyo. Lakini wapi hadithi hizo za Mtume hazikuweza kupenya ndani ya nafsi hizo ambazo hazikuitambua haki kuwa ni haki isipokuwa kwa manufaa yake, na hazikutambua ukweli kuwa ni ukweli isipokuwa ukitokana nazo. Ndiyo maana basi, Mtume(s.a.w.w) aliweka msimamo kutokana na kufahamu kwake kwamba (bibi Aisha) yeye ndiyo ile fitina aliyoiweka Mwenyezi Mungu katika umma huu ili aupe mtihani (umma huu) kwa fitina hiyo kama zilivyotahiniwa nyumati zilizotangulia. Mwenyezi Mungu anasema:

الم ﴿١﴾ أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾

"Alif Lam Mim, Je watu wanadhani wataachwa (wasitiwe msukosuko) kwa kuwa wanasema tumeamini, basi ndiyo wasijaribiwe. (Qur'an, 29:1-2).

Kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu aliutahadharisha umma wake kutokana na bibi Aisha mara nyingi mpaka siku moja alisimama na akaielekea nyumba ya bibi Aisha akasema: "Hapa ndipo itakapoanzia fitina, hapa ndipo itakapoanzia fitina pale pembe la Shetani litakapochomoza." Bukhari katika Sahih yake ndani ya mlango uliokuja kuzungumzia nyumba za wakeze Mtume amesema: "Imepokewa toka kwa Nafii naye kutoka kwa Abdallah (r.a) amesema: Mtume(s.a.w.w) alisimama kuhutubia akaiashiria nyumba ya Aisha akasema: "Hapa ndipo itakapoanzia fitina (mara tatu) wakati pembe la Shetani litakapochomoza."

Kama ambavyo Muslim ndani ya Sahihi yake ameandika mapokezi kutoka kwa Ikrimah ibn Ammar kutoka kwa Salim naye kutoka kwa Ibn Umar amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alitoka katika nyumba ya Aisha akasema: "Chanzo cha kufru kitaanzia hapa wakati pembe la Shetani litakapochomoza ". Hakuna mazingatio yoyote kwa nyongeza waliyoiongeza waliposema, "Yaani eti Mtume alikusudia upande wa mashariki" kwani ni wazi kabisa kwamba tamko hilo limewekwa ili kumpunguzia (mzigo) Ummul-Muuminina na kumuepusha na tuhuma hii. Na imekuja ndani ya Sahihi Bukhari vile vile, amesema: "Wakati Talha, Zubair na Aisha walipokwenda Basra, Imam Ali alimtuma Ammar ibn Yasir na Hasan ibn Ali kisha wakapanda juu ya mimbari, Hasan ibn Ali akapanda juu zaidi kwenye mimbar na Ammar akawa chini ya Hasan, basi sisi tukakusanyika kisha nikamsikia Ammar anasema, Bila shaka Aisha amekwenda Basra na Wallahi yeye ni mke wa Mtume wenu duniani na akhera. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu amekupeni mtihani ili ajue je, mtamtii Mwenyezi Mungu au Aisha?" Allahu Akbar!! Habari hii vile vile inajulisha kwamba katika kumtii Aisha ni kumuasi Mwenyezi Mungu na kumuasi Aisha na kusimama dhidi yake ni kumtii Mwenyezi Mungu.

Vile vile tunaona ndani ya hadithi hii kwamba wasimuliaji miongoni mwa Banu Umayyah wameongeza neno jingine katika, "Hakika yeye (Aisha) ni mke wa Mtume wenu duniani na akhera", ili tu wawapotoshe watu wa kawaida kwamba eti Mwenyezi Mungu amemsamehe (Aisha) madhambi yake yote aliyoyatenda na amemuingiza katika pepo yake na kumuozesha kipenzi chake Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) kama sivyo, basi Ammar amefahamu kutoka wapi kwamba Aisha ni mke wa Mtume huko Akhera? Hizi ndizo hila za mwisho walizotumia wazushi miongoni mwa wazushi wa riwaya katika zama za Banu Umayya, kwani kila walipoikuta hadithi inayotajwa sana na watu ambayo hakuna uwezekano wa kuikanusha au kuipinga walikuwa wakifanya makusudi kabisa kuongezea sentensi au neno kwenye hadithi hiyo, au kugeuza baadhi ya matamko yake ili kuipunguza makali au kupoteza maana inayohusika kwenye hadithi hiyo, kama walivyofanya hayo kwenye hadithi isemayo, "Mimi ndiyo mji wa elimu na Ali ndiyo mlango wake na Abubakr ndiyo msingi wake, na Umar ndiyo kuta zake na Uthman ndiyo paa lake." Nyongeza iliyopo kwenye hadithi hiyo haifichikani kwa watu wachunguzi wenye uadilifu, kwani waadilifu na watu wanaochunguza wanaweza kuzitengua nyongeza hizo ambazo sehemu kubwa zinajulisha juu ya ubovu wa akili za wazushi hao na kutokuwa kwao na hekima na mwangaza wa hadithi za Mtume(s.a.w.w) .

Hapana shaka kwamba wataiona kauli isemay'o kuwa Abubakr ni msingi wa mji huo, maana yake ni kuwa elimu yote ya Mtume wa Mwenyezi Mungu imetokana na elimu ya Abubakr na hii ni kufru, kama ambavyo kusema Umar ni kuta za mji huo, maana yake ni kwamba Umar yuko pale kuzuia watu kuingia kwenye mji huo, yaani anawazuia kuifikia elimu, na kusema kwamba Uthman ni paa la mji huo, moja kwa moja (kauli) hiyo ni batili, kwani hakuna mji wenye paa na haiwezekani. Kama ambavyo wachunguzi wataona kwamba Ammar anamuapa Mwenyezi Mungu kwamba Aisha ni mke wa Mtume(s.a.w.w) duniani na akhera, hii ni kusema mambo wasiyoyajua, basi iweje Ammar aapie kitu asichokijua? Je, anayo aya katika kitabu cha Mwenyezi Mungu inayomjulisha hilo au yeye ndiye aliyeachiwa jukumu hilo na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) ?

Bila shaka usahihi wa hadithi unabakia kuwa Aisha alikwenda Basra, na kwamba yeye ni mke wa Mtume wenu, lakini Mwenyezi Mungu amekupeni mtihani ili apate kubaini iwapo mtamtii yeye Mwenyezi Mungu au Aisha. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia akili, na kwa akili hizo tukaweza kupambanua haki kutokana na batili, na akatubainishia njia kisha akatutahini kwa mambo mbali mbali ili iwe ni hoja dhidi yetu siku ya malipo.