• Anza
  • Iliyopita
  • 5 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 6019 / Pakua: 4102
Kiwango Kiwango Kiwango
WAJIBU WA VIJANA

WAJIBU WA VIJANA

Mwandishi:
Swahili

WAJIBU WA VIJANA

MTUNGAJI: SHEYKH HASAN SAFFAR

MFASIRI: ABU AHMAD HUSSEIN

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Jaribio la Kumfahamu Kabla ya kufikia umri wa miaka kumi na mitano kwa kipindi kidogo, mwanadamu hukabiliana na kipindi muhimu na cha hatari katika uhai wake, nacho ni kipindi cha ujana (ubarobaro) ambacho huendelea nacho hadi kufikia umri wa miaka ishirini au ishirini na tano hivi. Hiki ndicho kipindi cha ubarobaro (ushababi), nacho ni kipindi muhimu na cha hatari.

Hebu tujiulize kwa nini kuwa ni muhimu na hatari?

Ni muhimu kwa kuwa huihukumu hali ya baadaye ya umma na mwisho wake. Vijana hawa wanaokua hivi leo bila shaka wao ndio umma wa kesho. Umma huu ulioko hivi sasa utaondoka na pahali pao na vyeo vyao vitachukuliwa na hawa vijana. Naam, utawaachia pahali pake umma unaokuja, umma mpya. Nao huo umma mpya ni hawa vijana wa leo na mabarobaro wa sasa.

Kwa hakika ni kweli kabisa kwamba mwanachuoni wa leo wa kidini hatakuwa ndiye mwanachuoni wa kesho, bali hapana shaka yoyote kwamba pahali pake na cheo chake ataviacha kisha atakuja mtu mwingine miongoni mwa hawa vijana mabarobaro iIi achukue pahali pake. Mkuu wa mkoa au wilaya wa leo hatakuwa ndiye mkuu wa mkoa au wilaya wa siku zijazo, bali hapana budi nafasi yake itafikia kikomo, atakufa na pahali pake patachukuliwa na mtu mwingine.

Vivyo hivyo, rais wa nchi wa leo, hakimu, amiri, waziri, kiongozi, n.k. watakufa na pahali pao patachukuliwa na vilana wa leo. Hii ndiyo tabia ya uhai na tabia ya maumbile. Huu ndio mwenendo wake kwamba kizazi kimoja kinapoondoka badala yake huja kizazi kingine. Je, hao watu wengine watakaochukua nafasi ya jamii ya sasa katika siku zijazo ni akina nani? Hakika wao ni hawa vijana wa leo, kwani wao ndio watakaounda jamil ya kesho. Siku moja Imam Hasan bin Ali(a.s) aliwakusanya watoto wake na kuwaambia: "Nyinyi leo ni watu wadogo, mnatarajiwa kuwa watu wazima kwa wengine. "

Vijana wetu wa leo ikiwa watalelewa vyema hadi wawe wema na wanyofu, tunaweza kubashiri kuwa umma wetu na jamii zetu bali na vizazi vyetu vijavyo vitakuwa na mustakbali mwema; lakini wasipokuwa wema au wasipofuata njia nyofu basi itamaanisha kuwa huenda mustakbali wao ukawa mwovu, mweusi na wenye giza.

Kipindi cha ushababu ni muhimu sana kwa sababu ndicho upeo wa mustakbali wa umma na mustakbali wa wananchi, na kutokana na sababu hii ndio mafundisho bayana ya dini yanatilia mkazo sana kukizangatia kipindi hiki kutokana na umuhimu wake. Kwa mfano kauli ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) aliposema: "Hakika nyayo za mja hazitaweza kunyanyuka katika siku ya Kiyama hadi aulizwe ameumaliza umri wake katika njia gani na ameutumia ujana wake katika nini. "

Wakati kama huu ni hatari kwa kijana kwa kuwa huishi katika hali maalum inayoathirika kimwili, kifikra na kijamii. Katika hali hii ya pekee anayoishi kijana katika kipindi cha ujana, inatakikana ama ajiimarishe katika mazingira yaliyo mema na maongozi yaliyo salama ili aweze kuvuka kipindi hiki akiwa ni kijana mwenye juhudi sana ambaye ataweza kuunufaisha umma kutokana na kuwepo kwake na harakati zake; au aondokee kuwa ni kijana aliyeharibika katika mazingira ya ufisadi na matokeo yake iwe ni kuibomoa nafsi yake na kuibomoa jamii yake.

Vipambanuzi vya Kipindi cha Ujana Kipindi cha ubarobaro kinajipambanua kwa wingi wa sifa na vipawa. Sifa hizi na vipawa hivi hupatikana kwa wingi katika shakhsia ya barobaro katika pande zote za maisha yake.

Upande wa Kimwili: Katika kipindi cha uvulana na ubarobaro, mwili wa mwanadamu hutangaza kuwasili kwake kwenye kilele cha kukomaa na kukamilika, kwani huchukua umbile lake halisi na nguvu zake hukamilika na kimo chake humuongezea urembo wa kitabia. Qur'ani Tukufu yaelezea kuwa wakati wa uvulana ndio wakati wa nguvu. Mwenyezi Mungu amesema:

اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْقَدِيرُ ﴿٥٤﴾

"Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza." (30:54).

Mwanadamu huja kwenye uhai akiwa yu mtoto mdogo dhaifu, hawezi hata kumwondoa nzi aliyetua usoni mwake, kisha hukipita kipindi hicho cha udhaifu (utoto) huenda katika kipindi cha uvulana, kipindi chenye nguvu na nishati; kisha unyonge humjia tena na kumtawala mara nyingine kwa jinsi ambayo huingia katika zama za uzee na ukongwe. Vilevile katika wakati wa ujana, hisia za mwanadamu hulipuka na hisia za jinsia hazimpi nafasi. Kijana huishi katika hali ya zahama, dhiki na vurugu za kijinsia (shahawa) na huendelea katika hali hii. Hisia hizi huwa zinahitaji kushibishwa na kuondoshewa kiu yake.

Upande wa Kijamii: Baada ya kukipita kipindi cha utoto alipokuwa mdogo akinyenyekea amri za wakubwa, akiwa hana rai wala hamiliki jambo lolote, sasa huona kuwa ni barobaro. Nafsini mwake anajihisi kuwa ana nguvu, na kifuani mwake amejawa na hisia ya kujamini dhati yake. Wakati huo hutafuta jukumu Ia kutekeleza katika jamii. Sasa yeye si mtoto tena, bali hujihisi kuwa ni mtu mzima (mme) aliyekamilika uume (utu), na ni wajibu wake kufanya yale yanayofanywa na wakubwa. Umekwisha ule wakati aliokuwa akitendewa kama mtoto mdogo, wakati alipokuwa akitii amri za wakubwa na kunyenyekea matakwa yao. Hivi sasa yeye amekuwa mkubwa si mdogo tena. Anayo rai anataka aitekeleze na anatafuta jukumu katika jamii alitekeleze ili aijaze hi faragha ya kinafsi aliyokuwa nayo muda mrefu.

Upande wa Kinafsi: Katika kipindi hiki cha ubarobaro, ndani mwa nafsi ya ubarobaro huwemo matakwa ya kutaka kukataa kila jambo na roho ya kutaka kuasi, kama kulipizia kisasi kwa aliyofanyiwa alipokuwa mdogo, wakati alipokuwa akitii matakwa ya wazazi wake na vilevile kuzinyenyekea ada za jamii yake bila ya kuweza kupinga au kuhalifu na kujitenga. Kijana anapokuwa mkubwa na mwenye nguvu hupendelea naye atekeleze haki yake katika kupinga au kukubali na kuwa na rai huru. Huu ndio wakati ambao hukua nafsini mwake roho ya kutaka kupinga na kuasi. Tena hapa kuna sifa nyingine anayosifiwa barobaro kuwa nayo katika wakati huu wa uvulana na ujana, nayo ni ule upendo wake wa kujitolea na kuwa tayari kwake kujitoa mhanga. Tabia ya binadamu na umbile lake kila anapoishi muda mrefu hapa duniani, tamaa na pupa lake Ia kutaka kubakia zaidi hapa duniani huzidi kuambatana naye.

Ama tunapomzingatia barobaro kwa kuwa ni chipukizi anayeanza kukua katika hii dunia, yeye hawi mwingi wa tamaa na pupa Ia kutaka kubakia hapa duniani kama anavyokuwa mzee mwenye umri mkubwa. Mwenye kuyachunguza kwa makini matendo ya barobaro atagundua kuwa ana tabia ya kujiingiza kwenye hatari au kushikilia lilelile analolitaka, kupambana bila ya kujali kufa hasa anapojawa na hamasa. Ama mtu mkubwa wa umri, yeye hujihifadhi, tena huwa mwenye utulivu na husara katika matendo yake na shughuli zake. Kule kuwa kwake na majaribio humpa aina fulani ya kuwa na mizani na kujihifadhi, tena pupa lake Ia kubakia duniani halimkubalii kuwa na upendo wa kujiigiza katika mambo bila ya kuzingatia.

Hapa kuna mfano mwepesi kuhusu hakika hii. Hebu mpeleleze barobaro anapoendesha gari, kisha mpeleleze mtu wa makamo uendeshaji wake uko namna gani. Imerekodiwa kwamba katika zama za khallfa wa Kiabbasi Harun Rashid, aliambiwa kuwa yuko mtu aliyeishi na Mtume Mtukufu na akasikia hadithi zake. Yeye ni sahaba aliyekuwa na umri mrefu ambaye aliishi tokea zama za Mtume Mtukufu hadi zama za Harun Rashid. Umri wake ulikaribia miaka mia moja na thelathini (130) Kwa vile sahaba huyu ana heshima kuu, Harun Rashid alipendelea kukutana naye. Harun Rashid akaamuru aletwe na akaletwa kwake huku amebebwa. Harun Rashid akamwuliza: "Je, wewe umekutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu?"

Mzee akainamisha kichwa chake kama kuonyesha alama ya kujibu ndio.

"Je, umewahi kuyasikia mazungumzo (hadithi) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu?"

"Ndio."

"Je, unakumbuka mazungumzo yoyote miongoni mwa mazungumzo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu?"

"Ndio"

"Hebu nizungumzie iIe hadithi unayoikumbuka uliyoipokea kwa Mtume Mtukufu." Mzee akasema kwa sauti dhaifu sana: "Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu siku moja akisema: 'Mwanadamu huzeeka na hubakia ndani mwake sifa mbili -tamaa na matumaini." Mzee akayakata mazungumzo huku akiwa hana uwezo wa kuendelea nayo. Harun Rashid akaamuru apewe zawadi, nayo ilikuwa ni kiwango fulani cha mali, na iliwekwa juu ya kitanda chake. Kisha wakambeba ili kumrudisha nyumbani kwake.

Harun Rashid akahisi kwamba mdomo wa sahaba mzee ulikuwa ukichezacheza kana kwamba alikuwa akisema kitu. Akaamuru arejeshwe. Watumishi wakaja naye hadi ubavuni karibu na Harun Rashid. Akamwuliza: "Nimeuona mdomo wako ukichezacheza wakati ulipokuwa ukirudishwa kana kwamba ulikuwa ukisema kitu." Mzee akasema: "Ndio, nilikuwa nikiwauliza waliokuwa wakinibeba: 'Je, huyu Harun Rashid ataifanya zawadi hii iwe ni ya kila mwaka, awe akinipa mfano wake ili niweze kumzuru mwanzo wa kila mwaka?'" Harun Rashid akacheka, kisha akasema: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema kweli kabisa katika ile hadithi uliyoisema hivi sasa kwamba: 'Mwanadamu huzeeka na hubakia ndani mwake sifa mbili - tamaa na matumaini.'" Hivi ndivyo ilivyo.

Tamaa ya mwanadamu na matumaini yake ya kutaka kuishi duniani huzidi kukua nafsini mwake kila umri wake unapozidi. Hubakia ana busara na hujihifadhi katika matendo yake na mambo yake yote, ambapo barobaro huwa yuko tayari kujitoa sadaka na kujiingiza katika mambo ya hatari bila ya kujali hatari zilizoko mbele yake.

Upande wa Kinafsi: Aghlabu vijana na barobaro katika kipindi hiki cha ujana huwa na faragha na udhaifu wa kiakili katika kufungamana kwao na watu. Katika kipindi hiki cha ubarobaro akili ya binadamu hufumka na vipawa vyake hufunguka. Huanza kuyafikiria mambo kwa undani. Akilini mwake huchoreka maswali mengi kuhusu maisha yake na maisha ya jamii. Maswali ambayo hayana budi kujibiwa wazi. Vilevile hujiona kwamba halazimiki tena kuzikubali fikra za watu wake na mazingira yao, madamu ameamini nafsini mwake kuiamini dhati yake, na kupendelea kufuata mtindo wa kukataa na kupinga kila jambo na kupondokea zaldi upande wa kubeba majukumu mazito mazito na ya hatari. Kwa ajili hiyo, barobaro huwa yuko tayari kuipokea na kuifuata fikra yoyote mpya japo iwe ya hatari namna gani.

Ama mtu mkubwa yeye ana ukinaifu, imani na fikra anazoziamini na kuzitukuza miaka mingi. Yeye hana faragha ya kiakili wala hahisi kuwa na haja ya kuwa na itikadi nyingine mpya, bali yeye hayuko tayari kuiacha fikra aliyoiamini muda mrefu na kuitukuza miaka mingi. Kwa ajili hiyo utaona kwamba kila ujumbe na mafunzo kutoka mbinguni yalisimama na kupata nguvu kutokana na mabarobaro (vijana) wale ambao kwamba wao huwa wepesi kuziamini hizo fikra mpya na huwa tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya kuzitetea. Tuchukue mfano mmoja:

Nabi Ibrahim(a.s) alipowapelekea watu wake ujumbe wa kumpwekesha na kutomshirikisha Mwenyezi Mungu, ni nani aliyemwamini na kuukubali wito wake? Watu wake hawakuukubali ujumbe wake, isitoshe wakamtuhumu kwa kuwa aliaminiwa na kikundi cha vijana maskini, kama Qur'ani Tukufu inavyosema:

وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ الرَّأْيِ ﴿٢٧﴾

"Na hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale wanyonge katika sisi wenye fikra ya mwanzo." (11:27).

Naye Nabii wetu Muhammad(s.a.w.w) pia. Wale waliofanya upesi kumwamini na kuufuata ujumbe wake walikuwa ni kikundi cha mabarobaro, wadogo kwa umri, kama Ali bin Abu Talib(a.s) , Bilal Mhabeshi na Ammar bin Yaasir, n.k.

Jambo hili liliwafanya wazee na viongozi wa Makureshi kumtuhumu Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba yeye amewaharibu vijana wao na wakayasema hayo hayo katika mashitaka yao waliyoyapeleka kwa ami yake Abu Talib. Wakasema: "Hakika mwana wa nduguyo amewatusi miungu wetu, na amezipuuza ndoto zetu na amewaharibu mabarobaro wetu ." lli kuitilia nguvu hakika hii, Mtume Mtukufu amesema: "Nawausia kuwafanyia wema mabarobaro, kwani wao wana mioyo laini zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu amenituma mimi (niwe) mbashiri na mhofishaji, mabarobaro wakaapa kushikamana nami na wazee wakanihalifu... Na muda wao (wa kuishi duniani) ukawa mrefu na nyoyo zao zikasusuwaa (zikawa ngumu) ."

Amirul Mu'miniyn Ali bin Abu Talib amesema: "Hakika moyo wa kijana ni kama ardhi isiyokuwa na kitu (isiyolimwa) chochote kinachoingizwa (kinacholimwa) ndani yake hukikubali. "

1

WAJIBU WA VIJANA

VIPI TUFAIDIKE KATIKA KIPINDI CHA UBAROBARO

Hayo yote yaliyotangulia ndiyo mambo muhimu na sifa muhimu zinazompambanua barobaro zikiwemo sifa za machimbuko yaliyo hatari pia. Kwa hivyo, imetubainikia kwamba ni kwa miongozo mema na taratibu zilizo salama tu, ndipo itamkinika kufaidika na hivi vipawa na kuvipatiliza katika kuujenga utu wa Kiislamu unaotakikana ili vijana wetu wawe ni mfano halisi wenye kufanana na maisha ya vijana wa Kiislamu waliopigana jihadi kama Ammar bin Yaasir, Mus'ab bin Umayr, Malik Ashtar na Al bin Husayn al-Akbar. Ikiwa tutawapuuza vijana wetu na kutowajali katika wakati huu ulio hatari au tukawatendea vibaya katika sifa zao na vipawa vyao vya kifikra, huenda tukaonjwa kwa kupata umma mpya uliopotoka na kuharibika. Umma huu mpya utapotosha njia na lengo, na vilevile utaubomoa mustakbali wake mwema.

Swali Ietu hivi sasa ni hili: Ni kwa njia gani tutafaidika na wakati huu wa ubarobaro (uvulana)?

Vipi tutavikuza vipawa vyake na kumpangia nyadhifa kwa ajili ya maslahi yake na kuujenga utu wake, ili aweze kuubeba wajibu wa ujumbe huu wa Kiislamu? Haya ni miongoni mwa yale yatakayomfanya kijana awe ni msingi mwema wenye utendaji katika maendeleo ya kijamii na kuuendeleza mbele ujumbe huu wa Kiislamu.

Hapa napendelea kuelezea kwa kirefu kila kipawa cha kipindi hiki cha uvulana, na kuyaelezea mambo yenye kumpangia wadhifa na kumwongoza kwa ajili ya kujenga viongozi miongoni mwa vijana na umma wa Kiislamu unaokuja. Hapo tutaona vipi tutaweza kufaidika na kila kipawa chake, miongoni mwa hizi sifa tulizozitaja wakati atalelewa na kukua katika maongozi sahihi.

Vikwazo vya Matamanio ni Fursa Nzuri ya Kuimarisha Matakwa Ikiwa vijana wa umma wanamiliki irada (matakwa) na nguvu ya nafsi iliyo thabiti ambayo inashinda matamanio ya nafsi, nia na Irada thabiti yenye kupambana na ghururi, hakika umma utakuwa umetukuka na kupata heshima kuu. Tena umma kama huu utakuwa una uwezo wa kukabiliana na maadui na kupambana na wakoloni. Hautaweza kurukuu na kuyaitikia matakwa ya wakoloni, na hautamnyenyekea dhalimu au kuridhia kuwa watumwa wa wadhalimu na wakoloni. Umma ni muundo wa mkusanyiko wa watu. Ikiwa watu wanaounda umma ni watu waliopondokea kwenye uharibifu na maovu, na ni wenye tabia ya ghururi na shahawa, basi msimamo wa umma na muamala wao kwa maadui zao utakuwa ni baridi na wenye kukubaliana na maovu hayo na dhuluma hiyo. Ama ikiwa watu wanamiliki irada (nia thabiti), nguvu ya nafsi na uwezo wa kupambana na vikwazo, hakika umma ukishikana na vijana wake unaweza kukabiliana, kupinga na kusimama kwa ushujaa dhidi ya tamaa za maadui na njama za madhalimu na wakoloni. Wakati huu wa uvulana ni fursa nzuri yenye thamani ya kuikuza irada (matakwa) ya mtu katika umma. Sababu ni kwamba irada ya binadamu haipati nguvu mara moja kwa kuipa mawaidha au kuipa miongozo, bali hupata nguvu kwa kupitia ukinzani na kwa kupambana na ghururi na vikwazo vya kila aina.

Kwa mfano, mtu ambaye ataikuta nafsi yake imezingirwa na mambo yenye udanganyifu na hadaa zenye nguvu, tena ikawa nafsi imebanwa katika vikwazo vyenye shahawa kali, yamkinika kwake kuilelea nafsi yake kwa matendo, kwa kuwa mgumu wa kutoyatii matamanio yake, aikuze kwa kuiviza irada yake kwa majaribio ya kimatendo. Mtu kama huyu anaweza kupata ushindi, hasa pale atakapoitukuza nafsi yake na kuzidharau zile ghururi na shahawa na aikanye nafsi yake kuvinyenyekea vikwazo vya matamanio. Vivyo hivyo, kipindi hiki cha ujana kwa vijana ni kipindi cha kuipa mazoezi irada na kuifanyia majaribio nafsi yake. Kijana akipata miongozo iliyo salama na kupata mafunzo (elimu) sahihi yaliyojaa ubinadamu katika malezi yaliyo mema, ataweza kuyapita majaribio haya kwa ushindi mkubwa, na baada ya mtihani huu atakuwa mwenye irada yenye nguvu na ushujaa. Hakika mara nyingi mabarobaro husumbuliwa na hisia kali za matamanio nafsini mwao, vilevile hupambana na ghururi (hadazi) za aina mbalimbali zenye nguvu, lakini huweza kupata ushindi upesi hasa anapoweza kuitawala nafsi yake, kuuhifadhi utu wake na heshima yake, akaweza kupambana na hadazi zote na akaweza kujiepusha na vitimbi vikubwa vya matamanio yenye kiwi, hasa katika hizi jamii zetu kunakopatikana kwa wingi upondokeaji kwenye uharibifu na ufisadi. Barobaro akiweza kuyashinda hayo yote, yamaanisha kwamba ameimiliki irada yake iliyo thabiti na amemiliki nafsi yenye kutoteteleka. Wakati ambapo umma utamiliki watu pamoja na vijana wa namna hi basi hapo utaweza kuwa na matumaini ya kuwa na mustakbali mwema. Riwaya na hadithi tukufu zilizopokewa katika mafunzo matukufu ya Qur'ani zimeelezea kwamba barobaro anayo sifa tukufu ya kuyapa nyongo mambo yenye ghururi na ya haramu kwa kutubu, kwani toba inadhihirisha kujihifadhi kwake na kulingana kwake.

Mtume Mtukufu amesema: "Toba ni nzuri, na kwa barobaro ni nzuri zaidi. "

Pia imepokewa kwake kuwa amesema: "Hakuna kitu kizuri kinachopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kumwona barobaro mwenye kutubu. " Ni kwa nini kitendo hiki kinamfurahisha Mwenyezi Mungu? Sababu ni kwamba barobaro anapojiondoa kwenye maasi na kuyadhibiti matamanio yake huwa amefanya ukinzani mkubwa dhidi ya nafsi yake, vilevile huwa anailelea nafsi yake juu ya misingi ya kupania, kukakamia na kushikamana na imani yake. Tunapoidurusu historia ya viongozi wakubwa wa historia ya binadamu, tunakuta kwamba aghlabu yao walikuwa na jitihada ya hali ya juu sana wakati wa ujana wao katika kuzijenga nafsi zao na kuzielekeza kwenye maongozi matukufu yenye utu na ukamilifu. Na sababu ni kwamba wao walishikamana na mkondo wa matukufu na kulazimiana nayo, na wakakataa kupomoka kwenye lindi Ia matamanio na upotevu wenye kutenganisha na haki, pamoja na kwamba kulikuweko hali zenye kusaidia kuwavuta kwenye matamanio na kuzama zaidi kwenye mambo ya ufisadi. Hebu tujionee baadhi ya kumbukumbu za maisha ya baadhi ya viongozi wakuu ambao wamefaidika kwa kuziviza irada zao katika wakati wa ujana wao, wakazipa nguvu nafsi zao kwa kukakamia kujiepusha na shahawa za nafsi. Kutokana na kufuata njia hii, walizipa nafsi zao nafasi ya kwanza ya kuyavaa matukufu na kuvikwea vilele vya matukufu na ukamilifu.

1. Hebu tuitazame historia ya Nabii wa Mwenyezi Mungu, Yusuf bin Yaakub AS akiwa ameyakosa malezi ya wazazi wake pamoja na huruma yao tokea udogoni mwake baada ya kumpoteza mama yake, ndugu zake walimlia njama na kumtupa kisimani, kisha akanunuliwa na mmoja wa misafara ya Misri kwa thamani ya chini ya dirhamu chache.

Tazama ndugu msomaji, majaaliwa yalitaka aishi katika zama zake za ubarobaro ndani mwa nyumba ya Mfalme wa Misri pamoja na mkewe Zulaikha ambaye alivutwa vilivyo na uzuri wa Nabii Yusuf AS uliojulikana na uliokuwa ukipigiwa mfano. Ashiki ya kumpenda Yusuf ikavama moyoni mwa Zulaikha, na nyumba walimokuwa wakiishi haikuwa na yeyote mwenye kutia zahama, na hali haikuwa na pingamizi yoyote ya kuzuia kutekeleza hila za kishetani. Hebu sawirisha ewe kijana uliye barobaro, kuwa wewe umeingia kwenye mtego wa Nabli Yusuf AS. Pia chukulia kuwa uko katika mazingira yanayosaidia kupotoka, Je, ungefanya nini? Na wajibu wako ungekuwa ni nini katika hali kama hii? Naam, ukweli ni kwamba wengi wa barobaro wetu wa sasa, mara nyingi wanatatizwa na ghururi zilezile ambazo zilimtatiza huyu barobaro mtukufu Yusuf, vilevile wanaishi katika mazingara sampuli ileile aliyoishi.

Kwa hivyo, ni juu ya vijana wetu kumfanya Nabii Yusuf AS kuwa ni kiongozi wao na kugizo chao, wamwige katika kupambana kwake na ghururi kama zile katika kukabiliana kwake na hali kama zile. Hebu tutazame msimamo wake ulikuwa namna gani? Qur'ani Tukufu yatusimulia kwa ufasaha mkubwa ikitumia njia yake ya kimbinguni. Yatutolea baadhi ya visa vinavyoelezea baadhi ya ile mikasa hatari aliyoipata Nabii Yusuf(a.s) katika nyumba ya Mfalme wa Misri, pamoja na tukio Ia kurukiwa na Zulaikha. Mwenyezi Mungu asema: "Na akasema yule aliyemnunua huko Misri kumwambia mkewe: 'Mweke pahali pazuri huenda akatufaa au tukamfanya mwana. 'Na hivi ndivyo tulivyommakinisha Yusuf katika ardhi (nchi,) ili tumfundishe taawili (ufafanuzi) za hadithi na Mwenyezi Mungu ni Mshindi juu ya jambo Lake lakini watu wengi hawajui. Na alipofikia ukamilifu wake tukampa hukumu na elimu na vivi hivi huwalipa wonaofanya wema. Na akamtaka [Yusuf kutenda haramu] yule [Zulaikha] ambaye yeye yuko nyumbani kwake nafsi yake, na akafunga milango [ili asikimbie] na akasema: 'Ni toyari njoo [nimejitayarisho kwa ajili yako].' Akasema [Yusuf]: 'Namwogopa Mwenyezi Mungu, Yeye ni Mlezi wangu, ameyafanya mazuri makao yangu. Hakika madhalimu hawafuzu.' " (12:21-23) Qur'ani inaendelea kuyafafanua baadhi ya maelezo ya kisa chenyewe kutokana na umuhimu wake hadi pale ilipomdondoa Zulaikha akisema: Hakika nilimtaka nafsi yake akajizuia (akakataa) na ikiwa hatafanya ninayomwamuru, atafungwa na atakuwa katika wanyonge.' Akasema [Yusuf]: 'Mola wangu, jela ni boro zaidi kwangu kuliko yale wonayoniita kuyafanya, na ikiwa hutaniepusha na vitimbi vyao, nitapondokea kwao na nitakuwa miongoni mwa wajinga.' Basi Mola wake akamjibu, akamwepushia vitimbi vyao; hakika Yeye ni Mwenye kusikia na ni Mjuzi." (12:32-34)

Vivi hivi Yusuf alimwomba Mwenyezi Mungu amsaidie katika kupambana na ghururi za matamanio na hali za upotofu. Naye Mwenyezi Mungu akayajibu maombi yake, na Nabii Yusuf akazishinda zile hali zote za uharibifu na ufisadi ingawa alistahamilia maovu na kwa muda mrefu alibaki jela kwa azma, nia thabiti na nafsi yenye ushujaa. Na hivi ndivyo inavyotakikana kijana mwema awe.

2. Kuna kisa kingine chenye kuvutia na kustaajabisha kama kinachoelezwa katika historia. Kisa chenyewe kinamhusu Sayyid Mir Damad, aliyekuwa mwanachuoni mashuhuri sana nchini Iran. Yaelezewa kwamba Sayyid huyu alifikiwa na kisa hiki wakati akiwa kijana mbichi mwanzo wa kubalehe kwake, naye alikuwa ni mwanafunzi katika madrasa moja ya kidini katika jiji Ia Tehran. Katika usiku mmoja wakati binti wa Shah wa Iran katika zama hizo alipokuwa akitembea mitaani pamoja na vijakazi na watumishi wake, kwa ghafla kukanyesha mvua kubwa na kukavuma upepo mkali na kila mmoja miongoni mwa watumishi wa binti wa Shah akakimbia kutafuta mahali pa kujificha kibinafsi. Binti wa Shah akabakia peke yake mitaani katika lile janga Ienye kutisha na kuhofisha, ikawa naye hana budi kutafuta pahali pa kujificha. Katika kutazamatazama kwake huku na huko iIi angaa naye apate pahali pa kujificha na kujistiri, akauona mlango wa madrasa uko wazi, akaingia madrasani. Kwa bahati akagonga mlango wa chumba cha huyu Sayyid kijana na akamkuta yuko kando ya moto akijiota ili ajiondoshee baridi aliyokuwa nayo.

Binti huyu akamwelezea huyu Sayyid kijana kisa chake, kwamba yeye ni msichana aliyepotea njia na anachohitaji ni msaada, pahali pa kulala na kujistiri usiku ule, hadi hali ya anga iwe tulivu na ipambazuke. Sayyid aliona hana budi kulijibu ombi lile Ia msichana, hivyo akamkaribisha chumbani mwake, yeye akakaa katika kipembe kimoja na msichana naye akakaa katika kipembe kingine. Baada ya kupita muda katika usiku huo, shetani akaanza kucheza mchezo wake mwovu katika hali kama hii, kama ilivyopokewa katika hadithi ikisema: "Mwanamume hakai faragha na mwanamke ila shetani anakuwa wa tatu wao." Shetani akawa anamshawishi Sayyid huyo kijana namna ya kuipatiliza hii fursa na kutenda haramu kwamba mambo yote yako sawa kwa kila njia, mlango umefungwa, wala msichana hana njia yoyote na kujikinga au kujitetea.

Lakini vipi itakuwa? Kwani Sayyid huyo alikuwa ni kijana mwema na mwongofu, anayetambua hila na vitimbi vya Shetani. Akawa anafikiria njia ya kujiepusha kutokana na makucha haya ya shahawa na mtego huu wa Shetani. Mwishowe akafikia kwenye uamuzi mgumu. Akaamua kuitumia njia hii kwa ajili ya kupambana na shahawa zake na kuutatua wasiwasi wa shetani. Uamuzi wenyewe ukawa ni kuweka kidole chake juu ya kaa Ia moto, hadi ashughulishwe na uchungu wa kuchomeka ili asifikirie mambo ya haramu. Naam, aliendelea kujichoma hivihivi usiku kucha, huku akistahmilia uchungu na maumivu na huku akiihutubia nafsi yake: "Onja moto wa dunia ili uuogope moto wa Akhera!"

3. Je, ndugu! Vijana wamewahi kukisikia kisa cha lbn Siriin ambaye alikuwa mwanachuoni mkubwa wa elimu ya nafsi na aliyejulikana kwa kufasiri ndoto? Katika wakati wa ubarobaro wake Ibn Siriin alikuwa mwenye umbo jema, kiwiliwili kizuri, mwenye uso mwangavu na uzuri wa kitabia wenye kuvutia. Alikuwa akifanya kazi kwa mfanya biashara mmoja wa nguo. Siku moja alifika mwanamke dukani kununua vitambaa, alipomaliza kununua mahitaji yake, akamtaka yule mfanya biashara amtume mfanyakazi wake Ibn Siriin ili ambebee mizigo yake aliyonunua hadi nyumbani kwake, kisha ampe ujira. Ibn Siriin akabeba mizigo na kuandamana naye hadi nyumbani, walipoingia nyumbani mwanamke huyo akafunga milango, kisha akamtaka afanye naye kitendo cha haramu, lakini yeye akakataa. Mwanamke alipoona amekataliwa akazidi kutumia hila za kumlazimisha zaidi. Mwisho Ibn Siriin alijiona kuwa ametumbukia mtegoni, na hapana budi kufikiria njia ya kujisalimisha kutokana na mtego huo Alipoigundua hila yenyewe alimwomba huyo mwanamke amruhusu aende chooni kujisaidia. Mwanamke akamruhusu kufanya hivyo, naye alipoingia chooni tu alijipaka mavi mwili mzima, kisha akamtokea mwanamke yule akiwa katika hali kama hii ya kunuka. Mwanamke alipomwona katika hali kama ile, akamkimbia na kumfukuza nyumbani. Na kutokana na hila kama hii lbn Siriin alijiokoa kutoka mtego huu wa matamanio yaliyo na ghururi.

Wajibu wa Vijana katika Jamii Vipawa vingi vya binadamu huchimbuka katika wakati huu wa ujana. Huwa na ukunjufu wa wakati na nafsi. Vilevile huwa anamiliki nguvu, uwezo na nishati. Hivi vyote vinampa nafasi nzuri na kumshajiisha kuwa na wadhifa maalum katika jamii. Hapo mbeleni tuliwahi kuelezea juu ya matakwa ya kijana yenye kiwi ya kutaka kutekelezwa, na kupenda kwake kushiriki katika nyadhifa mbalimbali ili ahisi kwamba yuko huru na awathibitishie wengine uwezo wake na uume wake baada ya kuwa alikuwa mdogo akiishi katika hali ya kuwanyenyekea wengine na kupondokea kwenye matakwa yao. Baada ya kuwa alikuwa akitendewa kama mtoto mdogo, sasa ataka atendewe na jamii kama mtu mkubwa, mwenye heshima yake kamili na mwenye matakwa na irada.

Lau twampa nafasi kijana na kumuacha kutekeleza nyadhifa na wajibu anazoziweza katika jamii, na tukamwelekeza kufanya mambo mema Yenye faida na kumsaidia kuujenga utu wake na kuvikuza vipawa vyake, hakika tutakuwa tumefanya wema kwa kuyajua na kuya pambanua yale yanayoweza kumdanganya katika wakati wa ubarobaro. Na ikiwa hatutashughulika na masiala haya na ikawa hatutampa nafasi barobaro kutoa maoni yake na kutekeleza matakwa yake katika nyadhifa za kijamii kupitia maongozi mema, basi natija itakuwa moja kati ya mambo mawili: Ima vipawa vya barobaro vitafifia, na vitazimika au vitakufa na matumaini yake yatazikika, au atajiingiza katika kutekeleza mambo yaliyopotoka na kufanya mambo maovu ya ufisadi. Na huu ndio mushkili unaoutatiza umma wetu wa Kiislamu. Jamli nyingi hazijajua vipi zishirikiane na vijana wao katika upande huu. Wazee wengi pamoja na viongozi wale wanaoyatawalia mambo ya wananchi na kushikilia hatamu za uongozi, aghlabu yao hawako tayari kuwapa vijana wao fursa ya kutumia ujuzi wao na vipawa vyao, hawawapi nafasi yoyote ya kusimamia jambo lolote la kijamii, na hawawaamini, bali huwazingatia kuwa ni watoto wasiojua kitu na walio dhaifu. Kutokana na sababu hii vijana wetu hukua huku wakiwa na juhudi chache sana na maarifa yao huwa ni ya daraja Ia chini. Hivyo, hupotoka na kuiacha njia ya utukufu yenye utengevu, hasa wanapochukuliwa na makundi mengine ya upotevu na kupewa nyanja za kuziamini nafsi zao na kupewa nyadhifa za kujishughulisha na mambo muhimu yaliyo hatari.

Kitabia, utamwona kijana akivutika kwa urahisi na kujiingiza katika lile kundi ambalo linashughulikia vyema na kumthamini kama mtu mwenye nguvu. Na utamwona mara moja anawaacha wale watu ambao wanaoshughulikiana naye kama mtoto mdogo au kijana dhaifu. Tunasikitishwa sana kuona ya kwamba jamii yetu hadi sasa haijaacha kuwapima watu na kuwapa kima (hadhi na heshima) kupitia kipimo cha umri. Imekuwa kwamba kabla kijana hajakata masafa marefu ya umri, basi jamii ya watu wakubwa hawamwangalii kwa jicho Ia uaminifu na heshima, wala hawampi nafasi ya kutaharaki au kuwa na nishati yoyote.

Mtukufu Mtume ameitangaza wazi rai ya dini ya Kiislamu na akaelezea waziwazi juu ya kukataa kwake kipimo cha umri na miaka, na akafafanua kwamba kipimo cha pekee kilicho sahihi ni kipimo cha ujuzi na matendo, na kwamba kijana mwenye ujuzi na matendo anayestahili na ni bora zaidi na anayo haki ya kutangulizwa kuliko mwingine yeyote. Mtume Mtukufu alimtawalisha Ittaab bin Usaid mjini Makka, juu ya kuwa umri wake wakati huo ulikuwa ni miaka Ishirini na moja. Akamwamuru kusalisha sala ya jamaa na kusimamia shughuli nyinginezo kwa niaba ya Mtume Mtukufu. Kijana huyo alikuwa ni amiri wa kwanza kusalisha jamaa mjini Makka baada ya kukombolewa mji huo. Mtume Mtukufu alimwambia: "Ewe Ittaab! Unajua nimekutanguliza kwa watu gani? Nimekutanguliza na kukufanya mwakilishi wangu kwa watu (waja) wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na lau ningekuwa namjua aliye mbora zaidi kukushinda wewe ningemteua." Baadhi ya wakaazi wa Makka walipopinga uteuzi huo, Mtume Mtukufu alisema: "Mtu asihoji kwa hoja ya udogo wa umri wake, kwani ukubwa si ubora, bali ubora ndio ukubwa." (Jawaan, Sheikh Muhammad Taqi Falsafi; uk. 30).

Vilevile taaluma za Kiislamu zinashajiisha kuvikunjulia vipawa hivi vya vijana chipukizl ili vivie na kuendelea. Kwa mfano, utaona katika vitabu vya fiqihi kuna masiala ambayo yanaruhusu vijana wasiobalighi bado kuwaongoza vijana wenzao katika sala ya jamaa; na hii ni kwa sababu ya kumpa kijana moyo na kumshajiisha ili akulie na hisia ya kuiamini nafsi yake, kwani vijana wanapoona kuwa wana sala yao ya jamaa, watatambua kwamba wamethaminiwa na kwamba wao pia wanaweza kuwa viongozi kama walivyo watu wazima. Wakati tunaposoma sera za viongozi wa Kiislamu na historia ya maisha yao, tunaona wazi kwamba wao wanaamiliana na vijana muamala wa kuwashajiisha na kuwaheshimu. Vilevile huwapa heshima kubwa wale vijana walio na ujuzi, na mara nyingine huwatwisha majukumu mazito zaidi na ya hatari. Angalia jinsi Mtume wetu Muhammad(s.a.w.w) alivyomchagua Musa'b bin Umair, yule kijana mwenye imani na mpiganaji jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, awe balozi wake mjini Madina, ili auongoze umma wa huko katika njia ya Uislamu, autayarishe mji wa Yathrib kuwa makao ya machimbuko ya Uislamu na makao makuu ya serikali yake changa. Mus'ab alifika mjini Madina akiikuta katika hali nzito kutokana na tofauti iliyokuwepo baina ya makabila ya Aws na Khazraj. Akiwa amebeba ule wajibu mkubwa kuiongoza Madina, Mwenyezi Mungu amemwafikia kufaulu katika kutekeleza wajibu huo kutokana na imani yake ya kweli, ikhlasi aliyovama moyoni na jihadi yake thabiti.

Katika tukio jingine lenye kuthibitisha hakika kama hii katika uhai wake wa mwisho, Mtume Mtukufu aliandaa jeshi kubwa Ia kupigana na Warumi mkiwemo ndani mwake masahaba wakubwa na wazee wa Kiislamu. Uongozi wa jeshi hilo katika vita hivyo alipewa Usama bin Zaid ambaye alikuwa ni kijana asiyefikia hata umri wa miaka ishirini. Na wengine waliokuwemo katika jeshi hilo lenye kunyenyekea uongozi na amri za Usama walikuwa ni Abubakr, Umar na Abu Ubaida ibn Jarraah, Abdul Rahman bin Auf, Talha, Zubair, n.k. Baadhi ya masahaba waliudhika kutokana na uamuzi huo wa Mtume Mtukufu wa kumtanguliza Usama bin Zaid juu yao kutokana na umri wake mdogo, habari hiyo ikamfikia Mtume Mtukufu, naye akaghadhibishwa sana na kitendo hicho cha kumthamini mtu kulingana na kipimo cha umri ambacho kilikuwa kikitumiwa wakati wa Ujahilia. Kitendo hicho kilimfanya Mtume Mtukufu kutoka na kwenda msikitini kuwahutubia watu, juu ya kuwa na shida ya maradhi aliyokuwa nayo na kuumwa kwake. Miongoni mwa yale aliyoyasema katika hotuba yake siku hiyo ni: "Enyi watu! Ni nini haya maneno yaliyonifikia yaliyosemwa na baadhi yenu kwa sababu ya kumtanguliza kwangu Usama? Ikiwa mwapinga kumtanguliza kwangu Usama, hakika mlitangulia kuupinga (uamuzi wangu wa) kumtanguliza baba yake hapo mbeleni. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba baba yake alikuwa anastahiki uongozi, na hakika mwanawe baada yake naye anastahiki uongozi pia." (an-Nass wal ljtihad, uk. 9).

Naye Imam Jaafar Sadiq(a.s) alimkuta kijana Hisham bin Hakam kuwa na vipawa vikubwa na akawa akimdhihirishia mapenzi na heshima yake juu yake kwa kiasi kikubwa mpaka wazee wakaingiwa na wivu mioyoni mwao. Katika kitabu cha Safinatul Bihar imeelezwa kwamba heshima na cheo cha Hisham bin Hakam vimefikilia daraja Ia juu kabisa mbele ya Abu Abdillah Jaafar bin Muhammad Sadiq AS na kwamba Hisham alifika kwa Imam katika Mina, wakati alipokuwa anaanza kubalehe. Katika kikao hicho cha Imam walikuwepo baadhi ya masahaba zake wazee kama Hamraan bin Aayun, Qais al-Maasir, Yunus bin Ya'kub, Abi Jaafar al-Ahwal na wengineo, na Imam akampa Hisham heshima kubwa kushinda wazee wote waliokuwepo hapo. Abu Abdillah alipoona kwamba kitendo hicho kilikuwa kikubwa mbele ya masahaba wake, alisema: "Kijana huyu ametunusuru kwa ulimi wake, moyo wake na mikono yake." (jz. 2, uk. 719) Kauli ya mwisho juu ya maelezo haya yatakikana ifahamike kwamba haiwezikani kabisa kumwacha au kumtenga barobaro huku tukivipuuza vipawa vyake. Haimkiniki kumtupa na kumwacha abakie akiwa hana thamani yoyote au atenganishwe na maisha ya umma. Hakika yatakikana athaminiwe na aheshimiwe na apewe wajibu muhimu azitekeleze na vilevile aongozwe iIi aujenge utu wake. Bila shaka, ikiwa sisi tutamshajiisha na kumpa miongozo yenye kufaa, tutafaidika naye; na hayo yatakuwa ni matayarisho muhimu ambayo yatamjenga na kumfanya awe chimbuko jema lililo muhimu katika siku zijazo. Na ikiwa tutampuuza na kudharau rai zake na uwezo Wake na hatutompa nafasi ya kushughulika na jambo lolote au kumshajiisha na kumtia nishati na kumwongoza katika njia sahihi, tujuwe wazi kwamba atatekwa na wengine na kufaidiwa na wengine, na watamtayarisha kulingana na taratibu zao na miongozi yao miovu yenye kupoteza na kupotosha.

Majaribio mengi yamethibitisha kwamba kijana anapopewa nyadhifa au shughuli za kijamii kuziendesha au kusimamia wajibu wa kidini, huwa yuko tayari kutoa juhudi zake zote kuushughulikia umma wake, tena hushikamana zaidi na kulazimiana zaidi na dini. Ama kule kuwahimiza vijana kusali na kufunga na kuwahimiza kusikiliza hotuba na mihadhara pekee hakutoshelezi hata kidogo kudhamini utengevu wa vijana hao wala uongofu wao, wala hakutoshelezi kuyalelea maadili yao na vipawa vyao. Ni wajibu ulioko juu yetu kuwapa nidhamu na mipango yenye kuwataharakisha na kuwapa nishati. Nidhamu hizo ziwe nzuri ili ziweze kuwatambulisha umuhimu wao katika jamii. Miongoni mwa mambo yanayotia uchungu moyoni ni upinzani unaotoka kwa jamii kuwapinga vijana waumini, au kikundi chema kilichojitolea kusimamia na kutekeleza nishati muhimu za kijamii au za kidini.

Umma huwawekea tuhuma na shaka na huwapinga. Mara ngapi tunayashuhudia makundi ya vijana wema wenye nia safi kwa umma wao, vijana walio na hamasa kwa ddini yao, wanaotaka kusimamia jambo la kidini au la kijamii, au kuunda kamati za maendeleo ya kidini na kijamii, lakini kwa masikitiko utaona jamii hufanya ubahili katika kuwashajiisha na kuwatia moyo. Utaona hawawashajiishi hata kidogo, bali huzuia misaada yao katika pande zote na mara nyingine huwapinga na huwawekea vikwazo. Kwa nini? Je, ni kwa kuwa baba zetu na viongozi wa jamii hawajui tabia ya kipindi hiki cha ujana, wala hawajatambua hatari yake? Au ni kwa kuwa hao wazazi na viongozi hawataki kuwaruhusu vijana washirikiane nao katika kuyaongoza mambo ya kijamii kwa lengo la kuiendeleza hadhi yake? Basi ni kwa sababu gani? Hakika kufanya hivyo ni hiana na makosa makubwa.

2

WAJIBU WA VIJANA

MAPAMBANO DHIDI YA UJINGA NA UPOTEVU

Ili kupambana na hali hii mbaya yenye kusikitisha unaoishi umma wetu wa Kiislamu, panahitajika sana kuwepo moyo wa kimapinduzi na moyo wa kutaka kuleta mabadiliko na kuwa na msimamo wa kukataa na kupinga utaghuti (udhalimu). Serikali za kidikteta na za kidhalimu zinaendelea kuzitwisha tawala zao kwa mataifa yetu manyonge na zinayatawala kwa siasa yao ya kikoloni na kwa kutumia njama za mataifa makubwa. Vilevile fikra za zamani zilizoyaweka nyuma mataifa bado zingalimo ndani mwa akili za viongozi wetu na wakuu wetu wa kidini na kijamii, na wakiwa katika wao wako katika hali kama hi wanauongoza umma wetu.

Nazo ada mbaya pamoja na mienendo iliyo chakaa ingali inazidi kuleta matatizo na vikwazo katika umma wetu. Kubakia nyuma katika maendeleo kunazidi, na udikteta unaotawala umetia fora. Haya ndiyo maisha tunayoishi kila siku na ndiyo hali iliyoenea katika umma wetu. Sasa imebakia tujiulize: Ni nini msimamo wa umma wetu juu ya kuishi katika hali kama hii na maisha kama haya? Hali ambayo inachoma mioyo yetu na kutuudhi? Hakika ile roho ya kimapinduzi ya kutaka mabadiliko na kukataa kudhalilishwa iliyokuwemo ndani mwa nafsi za umma wetu imeyeyuka kabisa. Msimamo wa kupinga ufisadi pia umetoweka. Nafsi zilizothubutu kupinga zimekosekana. Mioyo yenye ghera na kaa lenye kuwasha utambi wa upinzani limezimika. Kila mmoja wetu amekuwa akipuuza kila jambo isipokuwa yale mambo yanayohusiana na maisha yake tu. Hafikiri kitu isipokuwa mambo yanayohusiana na maslahi yake ya kibinafsi. Ama kufikiria hali ya umma au hali ya muundo wake wa kisiasa na kiuchumi, hayo yote ni mambo ambayo fikra yake haimpi nafasi kuya fikiria, wala hamu yake haiyapi umuhimu wowote.

Hadi hivi sasa tungali tumebakia twaishi katika hali hi ya kupooza na kukosa thamani. Yawezekana watu wabadilike na mambo pia kubadilika na yakawa mengine, lakini hali yetu itabakia kuwa ni ileile ya ujinga, upotevu, kubakia nyuma katika elimu na uchumi na kutengwa kwenye uongozi wa nchi yetu. Tutabakia katika hali ileile ya kupomoka na kuwa katika dhiki na mateso. Tutabakia katika maisha haya na hali hii hadi pale roho ya kutaka mapinduzi na mabadiliko itakapozaliwa upya ndani mwa nafsi zetu na mioyo yetu, na pale hisia za upinzani zitakapojumuika kwa wingi na tushughulike na misimamo ya kupinga na kukataa hii hali yetu ya kubakia nyuma katika maendeleo yanayoenea. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ ﴿١١﴾

"Hakika Mwenyezi Mungu h a yabadili yale yalioko kwo kaumu (watu) hadi (wao) wabadili yale yaliyomo nafsini mwao." (13:11).

Ikiwa tunaitamani roho hii ya kimapinduzi na tunataka kumiliki mioyo yenye kukataa na kupinga, basi katika kipindi cha ubarobaro ziko mbegu zilizo hai kabisa, na iko hali ya kimaumbile kabisa inayokubaliana kutekeleza matakwa haya. Na huu ndio wakati unaotakikana kwenda mbio kuitafuta roho kama hii.

Na hii ni kutokana na sababu zifuatazo:

Kwanza : Kijana huhisi kuwa na nguvu nafsini na viungoni mwake baada ya kuwa alikuwa akiishi katika hali ya udhaifu alipokuwa mdogo. Kutokana na sababu hii hujiona ana jukumu Ia kupinga na kukataa.

Pili : Tukimzingatia kwa makini tutamkuta kwamba kijana huanza maisha yake yungali hajavaana nayo bado wala hana pupa nayo kama wanavyoyapupia watu wakubwa, bali inakuwa kinyume chake, yeye hupendelea kujitosa kwenye ukinzani na kukabiliana na hatari. Haya ndiyo yanayostahiki kuigwa na nafsi inayotaka kumiliki roho ya kutaka mapinduzi na kukataa.

Tatu : Kijana hana fungamano na maisha haya ya dunia wala hajaonja ladha zake zenye kumfanya aipondokee. Na hii ni kutokana na muda mfupi aliyoishi hapa duniani na kwa sababu ya kutokuwepo maslahi mengi yenye kumvuta zaidi kuyapenda maisha haya. Ni tabia ya binadamu kwamba anapoishi katika hali maalum kwa muda mrefu na maslahi yake yakawa mengi katika hali kama hiyo, huwa inakuwa vigumu kwake kufikiria kuibadili hali kama hiyo au maisha kama hayo, bali mara nyingine hupatwa na babaiko pakiwepo matara jio ya kupatikana mabadiliko. (Kwa mfano, Jean Jacques Rousseau alikuwa akiona hali kama hiyo kwa ufalme wa Kifaransa. Yasemekana alikuwa akisema kwamba alikuwa akipatwa na babaiko kutokana na kuisawiri Ufaransa ikijiendeleza bila ya kuwa na mfalme, juu ya kuwa alikuwa ni miongoni mwa wanafikra na wanafalsafa wakubwa waliowaita watu katika kuendeleza hali ya kisiasa wakati ule. Hii ni kwa sababu Rousseau alikulia katika chombo cha utawala wa kifalme na kuvuta hewa yake kwa muda wote wa maisha yake).

Vivi hivi utaona kwamba kundi Ia vijana ndilo kundi ambalo linaelekea zaidi kuwa na roho ya kutaka mapinduzi na kuleta mabadiliko, na wao ndio watu ambao wako tayari kabisa kuleta upinzani na kukataa ufisadi na dhuluma. Ushahidi mkubwa ni hizi hoja zifuatazo: Tume zote zilizotoka mbinguni, mapinduzi yote ya kijamii yaliyofanyika yamefaidika na vijana. Vijana walitegemewa kama viongozi wa kuleta mabadiliko na kuwa kama nguzo ya kuyaendeleza mapinduzi. Ama katika jamii zetu za Kiislamu kuna kosa kubwa linalotendeka katika kuamiliana na vijana wetu wanaokulia. Badala ya wao kuzikuza na kuziogoza roho zao ya kutaka mapinduzi na mabadiliko waliyonayo, vilevile badala ya kuiongoza roho ya kupondokea kwao katika upinzani, kuupinga ujinga ulioenea na upotevu uliotawala, sisi hufanya kila juhudi kuiua roho hii ya kimapinduzi iliyomo ndani mwa nafsi za vijana wetu. Pia huziua hamasa zao zilizowaka moyoni mwao ambazo ziko tayari kupambana na hali kama hizi. Mara nyingine utaona tunashughulika zaidi katika kutafuta njia za kuwakinaisha na kuwafanya wasalimu amri na kutii hii miweko ya ufisadi na kukubali kufuata hii miongozo michafu kwa njia za kuwavunja mioyo na kuzirudisha nyuma azima walizonazo na kuwakatisha tamaa nafsini mwao. Wakati huu tunapotumia hila za kuwakinaisha mabarobaro, huwa tunatumia kila mbinu na kila njia hata ikiwa ni kwa kuyapotoa baadhi ya mafunzo ya Kiislamu ili tu tuwakinaishe vijana wetu wasiweze kupinga au kukataa lolote analoambiwa.

Miongoni mwa tashwishi za kuvunja moyo ni ile itikadi ya taqiya (ufichaji wa imani), eti taqiya ni wajibu wa kisheria inayomruhusu mtu amnyamazie au amnyenyekee dhalimu yeyote anayetawala umma kwa dhuluma na maonevu!! Eti kupambana ni kuiingiza nafsi kwenye maangamivu, na kufanya huko ni haramu katika sheria yetu ya Kiislamu!! Eti kufanya mapinduzi au kuleta aina yoyote ya mabadiliko kunahitaji fatwa ya mujtahidi (mufti) ambaye haoni kuwepo maslahi kwa dini kwa hivi sasa kutoa fatwa!! Eti fursa ya kufanya mapinduzi imepita kitambo, na ni wajibu kwa waumini kwa hivi sasa kungojea kudhihiri kwa Imam Mahdi!! Hebu tafakari kidogo. Je, haya mafundisho na fikra hizi zisizo nyofu na zenye kupinga mapinduzi zinakubaliwa na vijana wetu wote? Vijana wanaotaka kuleta mabadiliko, waliojaa hamasa, walio na matumaini ya kuasi udhalimu na walio na lengo Ia kuhakikisha kupatikana mapinduzi watakubali fikra hizo?

La hasha!! Umma wetu na watu wetu wana akili imara zilizo madhubuti ambazo hufikiria na kuyapima mambo yanayotolewa na fikra hizi na mafunzo haya. Ndiyo, yawezekana wapatikane baadhi ya vijana ambao watahadaika na kukubaliana na hali hii ya ufisadi. Kisha wajiondoe kwenye mkondo wa kutaka mapinduzi ambapo utawakuta wengine wanaitafuta njia ya mapinduzi popote ilipo ili waiandame hadi wahakikishe kwamba lengo lao Ia kuleta mabadiliko limepatikana. Hii ndiyo fursa wanayoipatiliza makundi ya upinzani na ndiyo nafasi inayopatilizwa na watu wenye hila za kikoloni ili wawawinde vijana wetu kwa jina Ia kuleta mabadiliko na maendeleo chini ya wito wa kupinga na kukataa. Wakati ambapo kijana anapoona njia mbili mbele yake: njia inayomwamuru kutii na kunyenyekea upotevu na utaghuti (udhalimu) (kama wanavyoiona baadhi ya wapingamaendeleo), na njia inayomshajiisha kufanya mapinduzi na kumtia moyo wa kuleta maendeleo na mabadiliko - ni dhahiri na ni kawaida kwamba vijana wengi watafuata njia ya pili, kwa sababu njia hiyo inakubaliana zaidi na tabia yao na maumbile yao ya kutaka mabadiliko. Vilevile njia hi inachukuana na maumbile yao ya kutaka mabadiliko na inaafikiana na maumbile ya mwanadamu ya kutokata tamaa na kuwa na moyo wa matumaini usiokuwa na kifani.

Kwa hakika, tukizingatia, tutaona kwamba dhati au umbile Ia Uislamu ni mapinduzi, linapinga kubakia nyuma na linakataa dhuluma na upotevu. Tamko Ia KiisIamu Ia Laa ilaaha illa-Ilah (Hapana mungu mwingine anayeabudiwa ila Allah tu) linamaanisha kuwakufuru na kuwakataa waungu wote wa udikteta na upotevu. Mafunzo ya Kiislamu yamemfaradhia kila binadamu aliyeukubali Uislamu kupambana na dhuluma, kukomesha ufisadi na ubatilifu, kukataa ujeuri na upotovu, na kuukomesha kabisa. Lau sisi twasimama kwa nia safi na kufundisha Uislamu halisi kwa vijana wetu pamoja na kuyaejezea mafunzo yake ya kimapinduzi na misingi yake ya kuleta mabadiliko, basi vijana wetu wangekuwa walinganifu, wenye nia safi ya kuuhudumia Uislamu, na wangekuwa wanamapinduzi wenye kupambana kwa ajili ya kuuhuisha Uislamu na kuujenga umma wenye imani na wenye kuiongoza dunia.

Barobaro na Kujitolea katika Njia ya Mwenyezi Mungu Njia ya Mwenyezi Mungu ni njia ya haki, uadilifu na uhuru. Kuitumikia njia ya Mwenyezi Mungu ni kushughulika katika kuitekeleza haki, kuiandama na kuhakikisha kwamba uadilifu uko juu na uhuru uko kwa wote. Matukio ya tarekhe (historia) na mazingira ya maisha yametufundisha na kututhibitishia kwamba haki, uadilifu na uhuru haviwezi kupatikana ila kwa njia ya kupambana na kujitoa mhanga. Umma ule unaomiliki roho yakujitolea, kujitoa mhanga na njia ya mapambano na mapigano unastahiki kupata uadilifu na uhuru ili ufikie anga Ia kuvuta hewa iliyojaa haki na usawa. Ama umma ulio bahili na mwoga, jazaa yake ni kutawaliwa na tawala za kibatili, kidikteta, na kidhalimu ambazo zakandamiza umma na kuutia utumwani. Na wale wanaongojea uadilifu na uhuru usimame na kuenea kila pahali kwa kuomba dua misikitini, kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, kutamani au kutumaini tu bila ya kusimama na kuyahakikisha hayo kwa vitendo, hao ni juu yao kuzidi kungojea dhuluma, maonevu, madharau, vitisho, n.k.

Uadilifu ni njia ambayo haimkiniki kuifikia ila kwa kulendea; uhuru wenye thamani haumkiniki kupata ila kwa kuilipia. Njia ya kupata haki na uadilifu ni mapambano tu. Thamani ya kupata uhuru ni kujitoa mhanga, kujitetea na kuinyakua haki hiyo kwa nguvu. Mtume Mtukufu amesema: "Kheri yote iko upangani. Hakuna kinachowanyorosha watu isipokuwa upanga, na upanga ndio vishikilio vya Pepo." Naye Amirul Mu'miniyn Ali bin Abu Talib akiwatahadharisha wale wanaopenda kujiweka nyuma kuuacha mkondo wa kujitoa mhanga na kujitolea kusaidia na wanaojitenga na kuiacha njia ya mapambano na kujikomboa, alisema: "Jihadi ni mlango miongoni mwa milango ya Peponi. Mwenyezi Mungu ameifungua kwa wale mawalli Wake mahususi. Ni nguo ya uchaji Mungu, deraya ya Mwenyezi Mungu iliyo na hifadhi, na ni Pepo Yake iliyoimarishwa na inayotegemewa. Mwenye kuiacha (jihadi) kwa ajili ya kuichukia, Mwenyezi Mungu atamvika nguo ya udhalilifu na balaa itamwenea, na atadhalilika kwa madogo na matwevu. "

Vijana wa umma ndlo walio na uwezo zaidi wa kupambana na kujitoa mhanga. Umbile lao na tabia yao wanayokuwa nayo katika kipindi hiki cha ujana huwavuta zaidi na kuwapambia kujiingiza kwenye mambo ya hatari bila ya kuyajali maisha, kwa sababu za kinafsi tulizotangulia kuzielezea katika faslu zilizotangulia. Kwa hivyo, ni juu yetu kuihifadhi hii tabia iliyoko kwa wingi nafsini mwa vijana wetu. Tujibidiishe kuwaongoza kwenye njia ya kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yaani katika njia ya kuhakikisha kuisimamisha haki, kuusimamisha uadilifu na kuulinda uhuru. La sivyo, umbile hili laweza kuelekezwa katika upande uliopotoka, na wakati huo kutapatikana vikundi vya vitisho na mapote yenye kuleta uharibifu na upotevu. Vipote hivyo vitakuwa na tabia ya kuilingiza kwenye ufisadi bila ya kujali, au vijana wetu watalelewa na makundi mengine maovu yaliyo kinyume chetu na kuwafanya wawe ndizo kuni za kuidumisha mipango yao ya uadui, au madaraja yao ya kuwavusha na kuwafikisha kwenye matakwa yao ya kikoloni.

Mafunzo ya Kiislamu Yazinduayo Ndiyo Yanayotakikana Zaidi Fikra huzinduka na kuamka. Bongo hufunguka na alama za kuuliza huanza kuambata fikrani mwa vijana chipukizi. Maswali mengi humjia akilini mwake. Mimi ni nani? Kwa nini nimekuja ulimwenguni? Ni nani aliyeniumba na kunipa uhai? Ni mwisho gani unaonisubiri ambao utakomesha maisha yangu? Ni nini msimamo wangu katika jamii ninayoishi nayo? Maswali kama haya na makumi mfano wake huchoreka ndani mwa akili ya kijana chipukizi na hubakia katika hali hii yakitafuta majibu ya maswali hayo ambayo yatapoza na kukinaisha moyo wake. Hi ni kwa sababu kijana huishi katika hali ya upungufu wa fikra na ni punde tu ambapo bongo lake hufunguka na kuanza kuyafikiria mambo haya kwa makini. Hi ndiyo fursa inayopatilizwa na makundi yaliyopotoka, yanayoingilia wakati kama huu ili kusimamia uandalizi wa fikra ya kijana kwa miongozo iliyopotoka ambayo hutayarishwa kwa ustadi na kwa lengo Ia kutupiga sisi wenyewe. Makundi haya huijaza fikra ya kijana kwa kumpa jawabu zenye upotevu ambazo si za haki katika kuyajibu maswali yake yaliyomo akilini na mawazoni mwake. Kutokana na sababu kama hizi ndiyo utaona kwamba mafunzo ya viongozi wa kidini yanatilia mkazo na kututanabahisha juu ya hatari ya kipindi hiki cha ujana kwa upande huu. Mafunzo hayo na riwaya hizo zinawakumbusha wazazi, viongozi na wanavyuoni wa jamii yetu umuhimu wa kufanya haraka kupatiliza kuwaelimisha watoto na vijana na kuijaza faragha ya kifikra kwa itikadi sahihi za Kiislamu na kwa mafunzo yake yaliyo salama.

Uislamu unazingatia kwamba kumwelimisha mtoto ni haki mojawapo miongoni mwa haki za mzazi kwa mwanawe. Baba wa mtoto akiacha kutoa haki hiyo, basi Mwenyezi Mungu atamhoji na kumwuliza, na ikiwa atapatikana na makosa basi Mwenyezi Mungu hatasita kumtesa siku hiyo ya Kiyama. Imam Ali bin Husayn Zaynul Abidiyn AS amesema: "Ama haki ya mwanao, ujue kwamba yeye atokana nawe, na Akhera atawekwa nawe pamoja na kheri na shari zake. Nawe utaulizwa juu ya yote uliyomfunza katika adabu nzuri na katika kumthibitishia (Uungu wa) Mola wake Mwenyezi na Mtukufu na kumsaidia katika kumtii Mwenyezi Mungu. Basi mfanyie mwanao matendo mazuri na jueni kwamba mtalipwa thawabu kwa kumfanyia vizuri na mtateswa kwa kumfanyia maovu." Ali bin Abu Talib AS ameitaja hali ya faragha ambayo kijana anayekulia huishi nayo. Ameitaja kwa kuashiria kwamba ni miongoni mwa sababu zinazomwandaa kukubali fikra yoyote anayoelezwa. Akasema: "Hakika moyo wa kijana ni kama ardhi isiyokuwa na kitu (isiyolimwa), chochote kinachoingizwa (kinachopandwa) hukikubali."

Imam Ja'far Sadiq(a.s) anasisitiza kuharakisha kuelimishwa vijana wanaokulia ili kuwafutisha fursa mirengo iliyopotoka na kuwakinga kutokana na misingi inayobomoa. Alisema: "Wapatilizeni watoto wenu wadogo kwa kuwafunza Qur'ani na Hadithi kabla hamjatanguliwa na wapingamaendeleo. " Wapingamaendeleo (marjaiyyah) ni kundi lililokuwa na fikra zilizopotoka katika jamii ya Kiislamu katika zama hizo. Leo katika zama zetu hizi tunaposhuhudia jinsi mawimbi ya upotevu yanavyoleta uharibifu na yanavyouweka Uislamu mbali na wengi wa vijana na mabarobaro wetu, na jinsi yanavyowavuta na kuwakumba vijana wetu waliozama katika malezi ya Mashariki na Magharibi, huwa hatuna budi ili kufikiria kwa makini misingi ya matatizo hayo na chanzo chake ili tuweze kupambana na haya mawimbi ya upotofu ambayo yanahatarisha kwa kiwango kikubwa hali ya usoni ya umma wetu na ujumbe wa Kiislamu.

Si sahihi wala si kweli kwamba yote haya waliyonayo vijana wetu yanasababishwa na ubaya na uovu ambao uko ndani mwa nafsi zao. Vivyo hivyo, haifai kuzikubali fikra zilizochakaa za hao viongozi wapingamaendeleo ambao wanayafasiri haya yote yanayotokea na kutendeka kwamba hayana bud yatokee. Wana dalili kwamba ni lazima ufisadi udhihiri katika bara na bahari na ujeuri na dhuluma uenee ulimwenguni kote. Vivyo hivyo, wanasema kwamba haimkiniki kuyazuia yale yaliyokadiriwa na yaliyojaaliwa na historia. Kwa jumla, udhaifu wa vijana wetu wa kutopendelea dini na kutoshikamana na mafunzo yake na badala yake kushikamana na mafunzo maharibifu yaliyoingizwa kutoka nje, unatokana na sababu maalum zinazotokana na hali yetu ya kubakia nyuma katika maendeleo ya kila aina. Sisi tuna jukumu mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya historia katika suala Ia kupotea umma wetu ujao. Kwa sababu sisi ndio chanzo cha kupotea kwao na kwenda kombo. Kutokana na hali ya kujibakiza kwetu nyuma, kuacha kuwaongoza na kutojali kuwaelimisha hadi kufikia kiwango sahihi kinachostahili na kinachotakikana.

Uislamu Uliopotoshwa Miongoni mwa misingi muhimu na sababu zilizowasababisha vijana wetu kuyatoroka mafunzo ya dini yao ni hii hali ya Uislamu uliopotoshwa katika umma wetu wa kila mahali. Kijana anapofumbua macho yake na kuiona jamii yake jinsi iliyotanikatanika katika mila, desturi na tabia, ilivyorudi nyuma katika elimu na maendeleo kadha wa kadha, ilivyotawaliwa na ubinafsi na ukabaiIa na badala yake kuthamini utabaka na dhuluma, au atakapoiona jamii hiyo ikiwa na fikra finyu na huko hayo yote hutendwa kwa jina Ia Uislamu na katika vazi Ia kidini, basi huchukulia kwamba yule mtawala au kiongozi hutawala kwa jina Ia Uislamu. Vilevile hudhania kwamba kilichosababisha watu kubakia nyuma ni mfumo wa Kiislamu. Kwa kawaida, zile fikra za wale viongozi wapingamaendeleo zilizoganda hushikilia nafasi ya fikra za wanavyuoni halisi wa Kiislamu. Zile fikra ambazo hazikushikamana na mafunzo halisi ya KiisIamu na zilizojaa mafunzo ya woga na kupokonya moyo wa ushujaa, ndizo ambazo zinatangulizwa mbele ya watu ili zionyeshwe kama mafunzo sahihi ya Kiislamu.

Maadamu Uislamu unaonyeshwa na kufundishwa kwa mabarobaro wetu kwa sura kama hii iIiyochushwa ambayo inaonyesha kwamba ndilo chimbuko halisi lililosababisha umma kubakia nyuma, basi utakuwaje msimamo wa hao vijana wetu kuihusu dini hii? Hapana shaka kwamba watautoroka Uislamu huu na kuyakataa mafunzo yake, na badala yake watatafuta njia nyingine waifuate ili waweze kuleta mabadiliko ndani ya umma, mabadiliko ambayo watayatarajia kulendeleza jamii yao. Maisha haya ya kubaki nyuma, kuishi kwa jina na vazi Ia Kiislamu na kushikilia fikra hizo za kutotaka kuleta mabadiliko ambayo yanatoa picha iliyochafuliwa ya maendeleo ya Kiislamu, ndiyo sababu muhimu iliyowafanya vijana hao wanaokulia kuacha kushikamana na dini yao ya Kiislamu.

Wanajua Nini katika Dini ya Kiislamu? Kabla hatujatoa mawaidha ya kuwashambulia, kuwakufurisha na kuwafanya mafasiki vijana wetu, ni wajibu juu yetu kujiuliza wenyewe: Je, tumejaribu kuueleza Uislamu na kuwafunza kisha wao wakaukataa? Jawabu ni la. Aghlabu ya vijana hawajui chochote katika mafunzo ya mfumo na misingi ya Kiislamu.Taaluma zote zilizokuwa zikifunzwa katika jamii zetu za Kiislamu, hazikukeuka hukumu za shaka katika masiala ya hedhi, nifasi, n.k. ambayo ni miongoni mwa mafunzo ya kifiqihi na kiibada. Ama kwa upande wa fikra, uchumi, siasa au elimujamii ya Kiislamu, mafunzo haya muhimu hayakupatikana ila kwa uchache. Vijana wetu hawakuweza kuyapata mafunzo namna hii kwa urahisi. Je, haya yote si kweli? Katika hali kama hii ambapo kumeenezwa kasumba ya kila aina ya kupotosha na propaganda zinazotangazwa na mashirika pamoja na makundi mbalimbali potofu, tunataraji nini kwao? Wengi wa vijana walioyaepuka mafunzo ya dini na kuacha kushikamana na sheria zake walifanya hivyo kutokana na kutoujua kwao Uislamu, kutojua umbile lake tukufu na umuhimu wake. Nasi tujue kwamba Mwenyezi Mungu atatuuliza kuhusu huu upungufu tulioufanya wa kutowafunza vijana wetu Uislamu halisi na kuwapa misingi ya mafunzo yake bora.

Vipi Tuifundishe Dini? Mfalme aliota ndoto iliyomfadhaisha sana. Akaamka akiwa na fadhaa na hali ya kuingiwa na hofu. Akamwita mfasiri ndoto na kumwelezea yote aliyoyaona ndotoni. Akasema: "Nimeona meno yangu yakidondoka moja baada ya jingine. Hebu niambie maana yake ni nini?" Mfasiri ndoto akainamisha kichwa kwa muda mfupi huku akifikiria, kisha akainua kichwa chake na kusema kwamba aliyoyaona yatakuwa kweli, na maana yake ni kuwa watu wote wa familia yake (mfalme) watakufa katika wakati wa uhai wake.

Tafsiri hi kavu yenye kisirani na fali mbaya ilimkasirisha mfalme na kumtia hofu. Kwa hivyo, akaamuru mtaalamu huyo auawe mara moja. Kisha akaamuru aletwe mfasiri ndoto mwingine; na akaletwa haraka mbele yake. Mfalme akamwelezea ndoto ileile; naye mfasiri ndoto akamjibu jawabu kama ile iliyotolewa na mfasiri ndoto wa kwanza, kwamba watu wa nyumbani kwake watakufa katika wakati wa uhai wake. Jawabu hii pia haikumridhisha, na akaamrisha tena auawe. Wakamletea mfasiri ndoto wa tatu. Tena mfalme akamwelezea ile ndoto kwamba ameyaona meno yake yaking'oka moja likifuatiwa na jingine. Mfasiri ndoto huyo akamsikiliza kwa makini kisha akainamisha kichwa kufikiri; na baada ya muda kupita katika kuwaza na kuzingatia, akasema: "Ikiwa yale uliyoyaona ni kweli, basi wewe utakuwa mtu mwenye umri mrefu zaidi katika familia yako, inshaallah." Jawabu hii iliufanya moyo wa mfalme kukunjuka na uso wake ukaonyesha furaha na kuondokewa na dhiki kutokana na tafsiri hiyo nzuri. Hivyo, akaamuru mfasiri ndoto apewe zawadi yenye thamani.

Msomaji mtukufu hebu zingatia kisa hiki. Je, unaona tofauti yoyote katika maana baina ya tafsiri hizo mbili? Ukweli ni kwamba hapana hitilafu. Zote mbili zinathibitisha hakika moja tu, nayo ni kuwa mfalme atabakia baada ya kuwakosa (kufa) watu wake wote. Basi kwa nini msimamo wa mfalme ulitofautiana mbele ya wafasiri ndoto hadi akaamuru wale wawili wa awali wauawe, na wa mwisho apewe zawadi? Ukizingatia utaona kwamba siri kubwa mefichika katika nija iliyotumika kueleza, kwani hakika ni ileile moja haikubadilika, lakini mara ya kwanza ilielezwa kwa njia inayoleta kisirani na kutisha, na mara ya pili ilielezwa kwa njia iliyojaa bishara, fali njema na furaha. Mbinu ya Kuelezea ni Muhimu Sana Katika kisa hicho imetudhihirikia wazi umuhimu wa mbinu ya kulielezea jambo lolote lile na umuhimu wake katika kuhadidisha msimamo wa watu kutokana na jambo lililoelezwa. Hata ikiwa jambo moja ni la kweli lakini ikawa halikuelezwa kwa mbinu nzuri, basi hakuna dhamana kwamba watu watalikubali jambo hilo. Vivyo hivyo, ikiwa jambo jingine ni la batili lakini kukatumika mbinu nzuri katika kulielezea, basi huenda watu wengi wakahadaika na kulifuata. Hivi sasa tunashuhudia vile hali ya watu kuelekea katika dini na kule kupungua katika kushikamana nayo. Tutaweza vipi kuwavuta na kuwaelekeza kwenye dini yao na kuwaelimisha ujumbe wao mtakatifu?

Ninaitakidi kwamba ni dharura mno kufikiria njia na mbinu nzuri ya kulelezea dini kwa watu. Wabalighi (wanatablighi) wengi na wanavyuoni hawajafaulu katika kuchagua ile mbinu nzuri, na kutokana na sababu hi hawakuafikiwa kufaulu katika shughuli zao, bali mara nyingine matokeo yake huwa kinyume chake na mara nyingine hutokea kwa baadhi yao upinzani na chuki ambavyo husababisha kuitoroka dini. Qur'ani Tukufu inatuzindua juu ya umuhimu wa jambo hili katika kulingania Uislamu. Inasisitiza juu ya kutumia mbinu nzuri katika tablighi. Inasema:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ﴿١٢٥﴾

"Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa lile ambalo ni zuri." (16:125).

Pia Qur'ani yatuzungumzia kuhusu maadili (akhlaki) ya Mtume Mtukufu na taathira yake katika kuwavuta watu katika dini. Inasema:

وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ﴿١٥٩﴾

"Na lau ungekuwa mkali na mwenye moyo mgumu wangetawanyikatawanyika pembezoni mwako." (3:159).


3