UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI8%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 53073 / Pakua: 6142
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KIMEANDIKWA NA SHEIKH JA'FAR SUBHANI

KIMETAFSIRIWA NA MUSABBAH SHAABANI MAPINDA

KIMETOLEWA NA AHLUL BAYT ASSEMBLY OF TANZANIA

Dar es Salaam - Tanzania

MUHTASARI

Afrika ya Mashariki imefaidi mazingira ya amani sana kiasi cha karne mbili zilizopita. Watu wa imani na itikadi zote waliishi pamoja kwa upendo na mapenzi. Kila mmoja akishiriki kwenye shughuli za mwenzake za kijamii na za Kidini. Ukiangalia kwenye Jumuiya za Kiislamu, wote wakihudhuria kwenye Misikiti ya kila mmoja, waliungana pamoja katika Maulidi na hafla za Muharram, na kupanua ushirikiano wao katika miradi ya kila mmoja. Kama Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi alivyosema katika hotuba moja ya hadhara; "Misikiti mingi ya Waislamu wa (Madhehebu ya) Shafi'i iliyoko Zanzibar na Pemba ilijengwa na kutolewa na Shia Ithna-ashariyya" Hatimaye Wahhabi walianza Tabligh (Mahubiri) yao hapa. Badala ya kujaribu kuwaleta mapagani au wasio waislamu kwenye boma ya Uislamu, nia yao kabisa ilikuwa na bado inakaziwa katika kuwabadilisha Mashafii wawe Mawahabi. Kwa lengo hili, hujifanya kama wao ni Masunni, na kuchanganyika pamoja na Masunni. Mawahabi hao wamepanda mbegu ya fitina na chuki kati ya Madhehebu mbali mbali za Kiislamu, na hususan kati ya Sunni na Shia. Wanazungumza dhidi ya Shia, na kusambaza vitabu na vijitabu (vya mambo ya dini) dhidi ya itikadi ya Shia ambavyo vimejaa mambo ya uwongo na uzushi. Kishawishi chao kiko wazi, kwa kuwatenganisha Masunni na Mashia, wakitumaini kupata urahisi wa kuingia katika jamii ya Sunni na Misikiti yao, ingawaje tumaini hili lingali bado kukamilishwa katika Tanzania.

Hebu tuangalie katika mzizi wa uovu wa kampeni hii. Huenda hapo nyuma katika mwaka 1979, ambapo Mapinduzi ya Ki-Islamu yalipotokea katika nchi ya Iran, na watawala wa Kiwahaabi wa Saudia walihadharishwa vikali mno, hata kabla ya tukio la Mapinduzi ya Kiislamu, wakati Ayatullah al-'uzma al-Khomeini (r.a.) akiwa bado Najaf (Iraq). Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia, akizungumza katika hadhara moja ya Waarabu, aliuonya ulimwengu wa Waarabu kwamba kama Khomeini ataruhusiwa kuendeleza harakati zake kutoka Iraq kama hapo nyuma, sio tu kwamba utawala wa Shaha utaangushwa, lakini, hali katika eneo lote vile vile itakuwa imetibuliwa. Hivyo wakaishinikiza Iraq kuweka vikwazo juu ya Khomeini kwa hofu ya kwamba, kama juhudi zake zitafanikiwa katika Iran, zitatingisha tawala zao wenyewe zisizo imara. Haikushangaza kwamba mara tu Mapinduzi ya Kiislamu yalipoimarika nchini Iran, hawa Wahhabi wakuanza propoganda kali yenye chuki dhidi ya Khomeini, dhidi ya Iran na dhidi ya Ushia. Kalamu za kukodisha zikuanza mchakato kutoa vitabu, makala na vijitabu (vya mambo ya dini) dhidi ya Shia. Shia waliitwa Makafiri, na pengine mtu angeuliza: Kama ni Makafiri, basi kwa nini wanapewa viza kwa ajili ya Hija na Umra? Wairani waliitwa Majus (Waabudu Moto) kwa nini? Kwa sababu kabla ya kuja kwa Uislamu waliabudu moto. Kwa hoja hii nasi hatuna haki ya kuwaita Wahhabi Mushrikuna? Kwa sababu kabla ya kuja kwa Uislamu wata wa Najd walikuwa wakiabudu Masanamu.

Baadhi ya waajiriwa wao wa ngazi za juu walikuwa ni (marehemu) Ihsan Ilahi Zaheer wa Pakistan, na Manzoor Ahmad Nu'mani na Abul Hasan Ali Nadwi wa India. Sauti itokayo kwenye vinywa vyao ni katika watakiwayo na mabwana zao kuyasema, na jambia la uzayuni lilichovywa kwenye damu ya waislamu linatumika kama kalamu yao. Kitabu kinachoandikwa dhidi ya Shia na watumwa hawa, kwa miezi michache tu kinatarujumiwa katika lugha zote kubwa za ulimwengu wa Kiislamu; na hufanywa kipatikane kila mahali, kadhalika husambazwa bure miongoni mwa Mahujaji: Nimeandika majibu kwa kitabu kimoja kama hicho, ambacho kilichapishwa katika mwaka 1994 nchini Tanzania na Marekani kwa jina la "Wahhabi's Fitna Exposed". Kimevunja habari za uwongo wao wote na masingizio yasiyo na msingi dhidi ya Shia. Tarjuma yake ya Kiswahili (Fitina za Wahhabi Zafichuliwa) imechapishwa na Bilal Muslim Mission of Tanzania, Dar es Salaam.

Bado inahisiwa haja ya kuweko kitabu katika sehemu hizi za ulimwengu ambacho kitaangalia katika mawazo yote na mafundisho ya Uwahhabi na kushughulika nayo katika mwanga wa Qur'an na Hadithi, ili kufichua uwongo na itikadi yao na mtizamo wao juu ya vita vitakatifu vya Kiislamu. Ahlul-Bayt(a.s) Assembly of Tanzania, ina furaha kutoa kitabu kama hiki kwa wata wazungumzao Kiswahili. Nimechagua kwa ajili ya madhumuni haya kitabu (kitwacho) "Al-Wahhabiyah Fil-Mizan" kilichoandikwa na Mwanachuoni mashuhuri wa dini na mtunzi, aitwaye Shaykh Ja'far Subhani, Profesa wa Chuo cha dini Qum (Iran). Kitabu hiki kwa hakika (bila kupendelea) kinaangalia katika hoja zote zilizotolewa na Wahhabi na kutahini kusihi kwake kutoka kwenye Qur'an na Sunnah.

Shaykh Musabbah Shaabani Mapinda, wa Dar-es-Salaam kwa ushauri wangu amefanya tarjuma ya kitabu hiki kutoka Kiarabu kwenda kwenye Kiswahili, kinachoitwa "Uchunguzi juu ya Uwahhabi". Nimekikagua kwa utaratibu ili kuhakikisha kwamba mafuhumu ya Kiarabu kwa uaminifu na ukweli yametolewa kwenda kwenye Kiswahili. Hiki ni kitabu cha kwanza cha "Ahlul-Bayt(a.s) Assembly of Tanzania", na nina fahari kwa kushirikishwa katika kila hatua. Namuomba Allah Subhanahu Wa Ta'ala atoe malipo yake kwa Mtunzi, mtarjumi na wale wote ambao wamesaidia katika kuchapishwa kwake kwa njia yoyote ile. Wa Ma Tawfeeq Illa Billah

Syed Saeed Akhtar Rizvi

Mwenyekiti,

Ahlul-Bayt (A.S.) Assembly

P.O. Box 75215,

Dar- es- Salaam, Tanzania

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UTANGULIZI WA CHAPA YA KWANZA

KUHUSU MAWAHABI NA ITIKADI ZAO

Shukurani zote Anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye ni Mtangu na hapana kitu kilichokuwepo kabla yake, naye ndiye wa mwisho hapana baada yake chochote. Na yeye ni dhahiri hapana kilicho dhahiri kuliko yeye, naye ni batin hapana kilicho Batin kuliko yeye. Na Sala na Salamu zimshukie Mtume wake na mbora wa viumbe wake ambaye alimtuma katika kipindi ambacho watu walikuwa ndani ya upotevu wakihangaika na wamezama ndani ya Fitna, na wametekwa na matamanio yao na wamepotoshwa na ujeuri na akili zao zimepotoshwa na Ujahili uliopita kiasi, wakihangaika katika mambo yaliyovurugika na balaa linalotokana na ujinga, basi Mtume[s .a.w.w ] akatoa nasaha kwa upeo, akaitengeneza njia na akalingania kwa hekima na mawaidha mazuri.

Mwenyezi Mungu alimtuma kuitimiza ahadi yake na kukamilisha Utume wake. Alichukua ahadi yake toka kwa Manabii na alama zilikuwa Mashuhuri na mazazi yake yalikuwa matukufu hali ya kuwa walimwengu katika zama hizo wakiwa na mila tofauti tofauti, na fikra mbali mbali na ni vikundi vingi wakiwemo wanaomshabihisha Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake au walikuwa wakifanya kufuru na shiriki katika jina lake au wakimuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akawaongoa kupitia kwa Mtume[s.a.w.w] kutoka kwenye upotovu na akawaokoa kutokana na ujinga kwa njia yake na ni nguzo ya dini yake. Na Rehma za (Mwenyezi Mungu) zimshukie Mtume na kizazi chake (watu) ambao ndiyo wa ndani wake na ni tegemeo la dini yake na ni chombo cha elimu yake, na ni rejea ya hekima zake na ni hazina ya vitabu vyake.

Kwao wao Mwenyezi Mungu aliimarisha dini yake, na ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewaondoshea uchafu na kuwatakasa mno. Na (Pia) ziwashukie Masahaba wake ambao waliisoma Qur'an na wakazitumia hukmu zake na wakazizingatia faradhi kisha wakazisimamisha. Waliihuyisha Sunna na kuuwa Bid'a, walilinganiwa kwenye jihadi wakaitika, na walimuamini kiongozi wao (ambaye ni Mtume[s.a.w.w] , kisha wakamfuata. Wamekutana na Mwenyezi Mungu na akawalipa ujira wao, na amewapa makazi ya amani baada ya khofu waliyokuwa nayo, waliendelea katika njia ya Dini na wakaifuata haki, Rehma ziwashukie daima milele muda wote wa kudumu mbingu na ardhi. Amma baad, bila shaka umma wa Kiislamu tangu mwanzoni umeshikamana juu ya Tauhudi katika nyanja zake mbali mbali, ukaafikiana juu ya kuipwekesha dhati ya Mwenyezi Mungu na kwamba, yeye ni mmoja hana mshirika wake na ni mpweke hana mfano. Kama ambavyo umeafikiana ya kwamba, yeye ni uumba na hapana muumba asiyekuwa yeye. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, kuna muumba asiyekuwa Mwenyezi Mungu " Qur'an, 35:3.

Na Amesema tena: "Waambie, Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu " Qur'an, 13:16.

Vile vile umekubaliana juu ya Tauhidi yake katika Rububiya yake na kwamba hapana Mola wala mwenye kusimamiya (mambo yao) asiyekuwa yeye. Amesema Mwenyezi Mungu: Yeye ndiye anayesimamia mambo yote hakuna muombezi ila baada ya idnini yake, huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu basi muabuduni yeye, Je, hamna kumbukumbu? Pia wamekubaliana kempwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada na kwamba, yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola ambaye anastahiki kuabudiwa na hukuna wa kuabudiwa asiyekuwa Yeye. Mwenyezi Mungu Amesema:

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

"Waambie, Enyi mliopewa Kitabu, njooni kwenye neno lililo sawa kati yetu na ninyi ya kwamba, tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, na wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yeta tusiwafanye kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu". Qur 'an, 3:64.

Bali hizi ndizo nukta ambazo zenye kuafikiana baina ya sheria zote za mbinguni, na yote haya yanaonekana kuwa ni miongoni mwa mambo ya kipekee kwa baadhi ya wafuasi wa sheria zilizopita. Basi mtazamo uliyo kinyume na misingi hii ni miongoni mwa vitendo vya uchafuzi na kupotosha vinavyotokana na wanachuoni, Watawa na Makasisi (wao).

MAWAHABI NA MSIMAMO WAO KWA UNDANI KATIKA QADHIYYAH ZA TAUHID

Cha ajabu, (na midhali uhai utona maajabu zaidi) in kwamba, Uwahabi unatokana na fikia ya Sheikh mpotofu aitwaye Ibn Taimiyyah ambaye ametuarifisha maana ya Tauhidi katika kitabu chake aliposema: "Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu ya mbingu yake kwenye arshi yake, yuko juu ya viumbe wake".[1] Na amesema tena: "Mola wete hushuka mpaka kwenye mbingu ya dunia kila siku inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku kisha husema; Nani ataniomba (saa hizi) nami nitamkubalia (maombi yake) nani ataniomba nami nitampa, ni nani atanitaka msamaha nami nitamsamehe".[2] Haya ndiyo maarifa ya mtu huyo (Ibn Taimiyyah) na huku ndiko kumtakasa kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na (yote haya aliyoyasema) inajulisha wazi kabisa kuwa yeye anaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu anao mwili na anapatikana upande fulani. Na (huyu Ibn Taimiyyah) amesema hayo kutokana na kung'ang'ania kwake dhahiri ya aya na hadithi za Mtume bila ya kuzitafiti kwa undani aya zilizokuja kuhusu maudhui hiyo, na bila ya kufanya uhakiki katika isnadi za hadithi na madhumuni yake.

Basi iwapo haya ndiyo maoni ya mwalimu (wa Mawahabi) basi itakuwaje hali ya watu wanaoramba vikombe vyake na wanakaa katika meza zake kama kina Ibn Al-Qayyim na Muhammad bin Abdul-Wahhab. Na cha ajabu ni kwamba, hawa nao wanataka wawe ni waalimu wa Tauhidi na walinganiaji wa Tauhid. Na Mwenyezi Mungu amrehemu mshairi aliyesema: "Katika maajabu ya duniani ni kwamba, mwenye ugonjwa wa manjano anadai kuwa ni mganga na mwenye macho mabovu awe mwenye kutengeneza dawa ya macho na kipofu awe mnajimu, na msomaji wetu wa Qur'an awe Mturuki na Khatibu wetu awe Muhindi, basi njooni tulie na tupige vifuajuu ya Uislamu, (Tuulilie kwa msiba uliyoufika). Hii ndiyo itikadi ya jamaa hawa kuhusu Mwenyezi Mungu, basi iwapo tutataka kuzipima fikra hizi, basi tunawajibika kulinganisha kati ya maelezo hayo na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume[s.a.w.w] kuhusu makusudio hayo (ya Tauhid), kisha tuone ni lipi kati ya makundi haya mawili lenye haki ya kufuatwa.

Je, ni yule amsifuye Mwenyezi Mungu kwamba, yeye ana mwili na anakaa upande fulani na kuteremka mpaka mbingu ya dunia, (ndiye wa kufuatwa) au yule amsifuye Mwenyezi Mungu kwa kusema: "Shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye hawafikii kikamilifu sifa zake wenye kuzisema, wala hawazidhibiti neema zake wenye kuhesabu, na wala hawatekelezi ipasavyo haki yake wenye kujitahidi, Mwenyezi Mungu ambaye fikra hazimfikii hate ziende umbali kiasi gani, wala akili hazimfikii japo ziende ndani kiasi gani, ambaye sifa zake hazina mpaka, wala hakuna maneno yatakayoeleza sifa zake kikamilifu. Na yeye hana wakati uliohesabiwa wala muda uliopangwa, mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa fikra zake atakuwa kamfanyia mwenza, na mwenye kumfanyia mwenza atakuwa kanifanya wawili na mwenye kumfanya wawili basi atakuwa kamgawa. Na mwenye kumgawa hakumjua, na asiyemjua atamuashiria na mwenye kumuashiria atakuwa kamuwekea mipaka, na mwenye kumuwekea mipaka atakuwa kamfanya kuwa zaidi ya mmoja, na atakayeuliza yuko katika kitu gani, basi yeye atakuwa kamuweka ndani ya kitu, na atakayemuuliza kuwa yuko juu ya kitu gani, basi yeye atapafanya mahala pengine pote kuwa Mwenyezi Mungu hayupo. Yeye yupo lakini si kwamba hapo kabla hakuwepo. Yupo pamoja na kila kitu, lakini si kwa kuambatana naye yu mbali na kila kitu lakini si kwa kuondoka.[3]

(Ndugu msomaji), utakapolinganisha yale yaliyonakiliwa kutoka kwa As-Habul-Hadithi kuhusu Tauhidi ya Mwenyezi Mungu na kumtakasa kwake utastaajabu, kwani Imam Al-Ash-Ari amenakili toka kwao kwamba, maana ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika kuomba ni kuwa: Maovu ya waja anayaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa matendo ya waja anayeyaumba ni Mwenyezi Mungu na waja hawawezi kufanya chochote.[4] Bila shaka ibn Taimiyyah na wale walioko kama yeye wanajisifu wenyewe kuwa ni Ahlul-hadithi na wanaitafsiri Tauhidi inayohusu kuumba kwa maana hii. Basi Je, baada ya hali hii itawezekanaje kwao (kina ibn Taimiyyah) kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na dhulma na ujeuri na kuvuka mipaka. Basi iwapo Mwenyezi Mungu ndiye anayeumba maovu ya waja, na waja hao wakawa hawana walichokifanya katika maovu hayo, si kwa uwezo wao wala kwa kuiga basi ni kwa nini Mwenyezi Mungu awaadhibu? Je, hali hii siyo miongoni mwa kauli za msemaji fulani aliposema: "Amefanya makosa mwingine nami ninaadhbiwa."

Nawe unatambua kwamba Tauhid inayohusu kuumba haimaanishi kama walivyoileza Ahlul-Hadithi, na kabla na baada yao (waliyasema kama hayo) Jabriyyah na ibn Taimiyyah na wafuasi wake. Bali maana yake ni kwamba: Muumba mwenye kujitosheleza na mtendaji asiyehitaji kitu chochote ni yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu. Lakini wako watendaji wanaotenda kwa idhini yake na wanaumba kwa amri yake na husimama na kukaa kwa uwezo wake na nguvu zake, hivyo basi mtu analo jukumu lake kutokana na matendo yake na kazi zake: "Kila nafsi itafungika kwa yale iliyoyatenda ". Qur'an, 74:38.

WANACHUONI WA KIWAHABI WANAJIPENDEKEZA KWA WATAWALA

Tunaona kwamba wanachuoni wa Kiwahabi nchini Saudia na sehemu zingine wanajipendekeza kwa watawala na Makhalifa wajeuri, wanajaribu kuyatakasa matendo ya dhulma ya watawala hao na msimamo wao wakijeuri, na wanajitahidi kutoa kibali cha kisheria kwa kila kinachotokana na watawala wao na wenye mamlaka juu yao (mtawala huyo) awe mwema au muovu. Na hilo siyo jambo la ajabu (kwao) kwani wao (Mawahabi) ndiyo wanaoona kuwa kusali nyuma ya kila Imam mwema au muovu sala inasihi, na kuwaombea wema viongozi wa Waislamu ni faradhi, na kuwapinga wanapopotoka ni haramu.[5] Wanaichukuliaje kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu [s.w.t] kama alivyoinakili toka kwake mjukuu wake Husein bin Ali[a.s] "Abu-Shuhadaa" pale aliposema: "Enyi watu, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu [s.w.t] amesema; mtu yeyote atakayemuona mtawala muovu anayehalalisha haramu ya Mwenyezi Mungu, mwenye kutengua ahadi ya Mwenyezi Mungu, mwenye kwenda kinyume cha Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, anawatendea uovu na uadui waja wa Mwenyezi Mungu, kisha mtu huyo akaacha kumkataza kwa kitendo au kauli, basi Mwenyezi Mungu atakuwa na haki ya kumuingiza motoni mtu huyo." [6] [6] Hebu niambie kweli, ni ipi baina ya kauli mbili na ni ipi baina ya njia mbili inayotokana na Uislamu halisi na inaonyesha picha ya nadharia ya Uislamu halisi?

Mwenyezi Mungu amesema: "Wala msiwategemee (mkawa pamoja nao) wale wanaodhulumu usije kukupateni moto ." Qur'an, 11:113.

MAPINDUZI YA KIISLAMU NA HUJUMA ZA KIWAHABI

Kwa hakika Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yameleta mshituko mkubwa katika ghuba, na kuzisononesha tawala zote zilizoko sehemu hiyo na hasa hasa zile zinazohusiana na mataifa makubwa na kuyategemea kwa kila hali, na kwa upande mwingine madola hayo ya kikoloni yanazitegemea nchi hizo na miongoni mwa tawala hizi ni ule utawala wa Kiwahabi unaotawala nchi kubwa miongoni mwa nchi za Kiislamu, nchi ambayo inasifika kwa utajiri mkubwa wa asili na inufaika kwa hali maalum ya kijiografia. Basi ukoloni mbaya na vibaraka wake na watendaji wake wakiongozwa na waliaganiaji wa Kiwahabi wamekusudia kupinga mapinduzi ya Kiislamu na kimbunga chake kwa njia mbali mbali, miongoni mwa upinzani huo ni kuzusha wasi wasi ndani yake na kuwasha mioto ya vita dhidi yake na kulazimisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya mapinduzi hayo. Na njama zote hizi za upinzani dhidi ya mapinduzi ziliposhindwa, wakakusudia kuleta picha mbaya ya utamaduni wa mapinduzi an kuondosha Mafhumu yake na kuuzushia uongo na kuupakazia uzushi ili kuwazuia watu kufuata muongozo wake na kumfuata kiongozi wa mapinduzi hayo. Kwa hakika njama hii ya kiadui dhidi ya utamaduni wa mapinduzi ya Kiislamu, inabainika katika mambo yafuatayo:

1. Kueneza matangazo na magazeti aina nyingi katika nchi mbali mbali za ulimwengu ili kuzungumzia dhidi ya mapinduzi na kufanya ushawishi dhidi yake na kuonyesha sura mbaya ya utamaduni wake halisi.

2. Kuchapisha vijitabu na vitabu vingi mno kuhusu utamaduni huo kwa kupitia mikono ya watu na waandishi ambao wameuza nafsi zao na hawajali isipokuwa mlo wao na pengine vyeo vyao vya kidunia, wakiongozwa na yule muongo mkubwa ih-Sa'an ilahi dhahiri[7] ambaye ni miongoni mwa watu wanaopata mali nyingi kutoka Saudia. Mtu huyu amesimama kidete kwa nguvu zake zote na kwa kila kile ambacho Suudia inakitoa ili kutoa picha mbaya ya taaluma ya mapinduzi miongoni mwa Waislamu.

Na huyu Bwana ni masikini kwa kila kitu hata katika madai yake kuwa anayafahamu madhhebu ya Shia Imamiyyah, basi anachanganya na kuvuruga na wala hapambanui baina ya Asili na Far-i. Wala baina ya Aqida na Riwaya, na anatoa ushahidi kwa kutumia riwaya kuwa eti ndiyo madhhebu ya Shia (yalivyo). Yapo mengi zaidi ya hayo, katika uongo wake na uzushi wake na natija mbovu atoazo, hivyo basi sisi tutahusika naye mahala pengine ndani ya kitabu pekee.

3. Kuyaeneza Madhhebu ya Kiwahabi miongoni mwa vijana katika Eneo hilo kwa njia mbali mbali huku wakibainisha wazi kuwa Mawahabi ndiyo Waislamu na kwamba wao ndiyo wanaompwekesha Mwenyezi Mungu na ndiyo wanaoitumia Qur'an na sunna kwa usahihi, na wasiyokuwa wao wako mbali mno na hayo. Basi kwa ajili hiyo tumeweka risala hiyo kuyabainisha madhhebu ya Kiwahabi, na kuweka bayana ndani yake upeo wa yale wayasemayo Mawahabi na upeo wa kuwa kwao mbali na Qur'an na Sunna na sera ya Waislamu.

Mwisho, tunatoa ushauri kwa wanachuoni wa Kiislamu walioko ulimwenguni kwanza, na pili kwa waandishi wa Kiwahabi, wasimamie kuitisha mkutano wa Ulimwengu wa Kiislamu, mkutano ambao utawakusanya wanachuoni wa Kiislamu kutoka vikundi vyote vya Kiislamu ili kuyachambua Mas-ala haya kwa mujibu wa Qur'an na Sunna na kuyasambaza matokeo ya mkutano huo kwa Waislamu wote ili haki iwabainikie kwa uwazi na ifuatwe, na iliyo haki ndiyo yenye haki mno kufuatwa, na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwafikisha na ndiye msaidizi. Jaafar Subhani

Qum Takatifu

1/Mfunguo Tano/1405

1

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UTANGULIZI WA CHAPA YA PILl

HAJA YA KUWEKO MKUTANO WA KIISLAMU WA ULIMWENGU ILI KUIDURUSU TAUHIDI NA SHIRKI

Bila shaka Al-Kaaba ndiyo nyumba ya mwanzo iliyojengwa kwa ajili ya ibada ya Mwenyezi Mungu na humo apwekeshwe yeye Mwenyezi Mungu, na kwa hakika misingi yake ilidhoofika kabla ya zama za Nabii Nuh[a.s] , na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu inatueleza juu ya jambo hilo.

إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾

"Kwa yakini nyumba ya mwanzo iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya Ibada) ni ile iliyoko katika jangwa takatifu (Makka) lenye kubarikiwa na muna uongofu kwa walimwengu." Qur'an, 3:96.

Na kwa kweli Al-Kaaba (baada ya kujengwa) ilichakaa kwa sababu ya tufani (zilizokuwa zikitokea), jambo ambalo lilipelekea kubomoka jengo lake na kuvunjika kuta zake, na alipokuja Nabii Ibrahim[a.s] akalijenga jengo lake kama anavyotufahamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema:

وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٢٧﴾

Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi." Qur'an, 2:127.

Na baada ya Ibrahim[a.s] kuisimamisha misingi yake na kuijenga AI-Kaaba alielekeza mwito maalum kwa amri ya Mwenyezi Mungu na Wahyi wake kwa kila mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu ili aizuru nyumba hii na akahiji. Mwenvezi Mungu anasema: "Watangazie watu habari ya Hijja ". Qur'an, 22:27.

Na Mwenyezi Mungu ameifanya nyumba yake hiyo tukufu, kuwa ni kituo cha mkusanyiko wa waumini na ni nyumba ya amani kwa wenye kumpwekesha, basi inapasa mtu yeyote asihisi hofu awapo hapo wala asiogope hatari yoyote wala dhulma, kama kauli ya Mwenyezi Mungu inavyojulisha.

وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا ﴿١٢٥﴾

"Na kumbukeni tulipoifanya nyumba (AI-Kaaba) pawe ni mahala panapoendewa na watu na pawe pa amani". Qur 'an, 2:125. Pia 28:57.

Hiyo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameifanya ziyara ya kuzuru nyumba yake iwe ni dhamana ya kuendelea kwa maisha ya waumini, na imekuwa kusimamisha maadhimisho ya Hijja ni jambo linaloleta amani kwa maisha ya mtu mmoja mmoja na jamii, pia kwa maisha ya kimaada na ya kiroho kwa waumini. Mwenyezi Mungu ameifanya Al-Kaaba (ambayo ni) nyumba takatifu kuwa tengenezo la (maisha ya) watu. Qur'an, 5:97.

Kwa majibu wa aya hii Tukufu Imam As-Sadiq[a.s] anasema: "Dini itaendelea kuwa imara muda wote Al-Kaaba itapokuwa imesimama."[8] Kwa hakika ubora wa kuizuru nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu ni mwingi mno kuliko tunavyoweza kuuzungumzia ndani ya utangulizi huu, lakini kitu tunachopenda kukiashiria ni yale mazingira iliyonayo Al-Kaaba leo hii, mazingira ambayo yameifanya iwe mikononi mwa watu ambao wao wanajiona kuwa ni watumishi wa miji miwili mitakatifu, na wanajifakharisha kwa jambo hilo. Nasi kufuatana na ubora ambao Mwenyezi Mungu ameihusisha nao Al-Kaaba, tunajiuliza mambo mawili muhimu.

Kwanza: Je, hivi leo hii maadhimisho ya hija yanazingatiwa kuwa ni tengenezo (litakalowarekebisha) watu sasa hivi? Je, kuizuru Al-Kaaba na kukusanyika pembezoni mwake Waislamu zaidi ya milioni mbili kumeleta amani kwenye maisha ya kimaada na ya kiroho kwa Waislamu na kuwadhaminia kuendelea kwa amani hiyo maishani mwao? Kama kweli ndivyo, basi hebu tuulizaneni, ni msimu upi miongoni mwa misimu ya hija za kila mwaka Makhatibu wa Makka na Madina walipata kuzungumzia masuala ya maisha ya Waislamu?

Na je, mambo ya Waislamu na matatizo yao yalipata kuwasilishwa katika uwanja wa majadiliano na kuyatafutia ufumbuzi katika mikusanyiko hii mikubwa? Basi ni lini watumishi hao wa Haramain (Makka na Madina) na Makhatibu wao walipata kuyasuluhisha mambo ya Waislama na matatizo yao? Na ili iwe kama mfano kuhusu mazingira ya kuhuzunisha ambayo Al-Kaaba inakabiliana nayo, ninaeleza kisa kifuatacho. Mwaka 1396 A.H. nilibahatika kuizuru nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na nikafanya umra pamoja na kundi la watu waliohifadhi Qur'an, ili kushiriki mashindano ya kuhifadhi Qur'an. Na katika siko hizo (Tulipokuwa Makka) idhaa mbali mbali na vyombo vya habari vilikuwa vikitangaza uvamizi wa Israel huko kusini mwa Lebanon na vitendo vyake vya kishenzi ilivyokuwa ikivifanya dhidi ya Wapalestina na wengineo.

Na katika siku ya Ijumaa tulifika kwenye kituo cha kuhifadhisha Qur'an kilichopo ubavuni mwa msikiti mtukufu wa Makka, na baada ya kumalizika kikao cha mashindano ya Qur'an paliadhiniwa na hivyo wakati wa Sala ukawa umeingia, na Khatibu akapanda kwenye mimbari ili kutoa khutba. Mimi nilikuwa nikidhnai kwamba, Khutibu huyu huenda atahutubia kuhusu tukio lililotawala katika kipindi hicho (nalo ni lile la uvamizi kusini mwa Lebanon na wajibu wa Waislamu kusimama dhidi ya vita hivi vya Kizayoni vya kupanua mipaka yake) lakini mara dhana yangu nzuri ilibadilika na kuwa yakini mbaya, kwani Khatibu huyu alianza kuzungumzia unadhifu na namna ulivyosisitizwa na athari zake nzuri na (alizungumzia) adabu zinazohusu msikiti na Sala ya Ijumaa na mengine kama hayo na wala hakutamka japokuwa neno moja kuhusu tukio lilokuwepo katika kipindi hicho.

Kuna mtu fulani alikuwa amekaa pembeni yangu ambaye alikuwa Mmisri miongoni mwa "Ikh-Wanil-Muslimina" waliokimbia kutoka Misri na kwenda Hijaz, basi mimi nikamwambia, hivi kweli khutba hii ilikuwa inaafikiana na mazingira wanayoishi Waislamu leo hii? Na kwa kuwa mtu huyu alikuwa mtu wa haki alishirikiana nami katika masikitiko na huzuni.

Inaonyesha wazi kwamba khutba za sala ya Ijumaa zote huwa zinafanyiwa sensa na uchunguzi kabla ya kusomwa, na serikali ya Saudia ndiyo inayowaelekeza Makhatibu kile watakiwacho kukisema ili wasije wakayavuka maelekezo hayo. Basi hakuti katika khutba hizo maelezo yoyote juu ya ukoloni na vitimbi vyake dhidi ya Uislamu wala maneno yanayohusu maadui wa Uislamu na hali za Waislamu.... Amma kuwazungumzia Mashia na "Majusi" hilo linazungumzwa kwa mapana yote kwa kiwango cha kumridhisha shetani. Na kwa hakika baada ya mapinduzi (ya Kiislamu) nchini Iran, kilitolewa Kitabu kiitwacho, "Wajaa Daurul-Majus" yaani umefika wakati wa majusi.[9]

Baada ya maelezo yaliyotangulia, Je, inafaa kusemwa kwamba, watawala wa Najdi na Hijazi ni wattumishi wa Haram ya Mwenyezi Mungu na walinzi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu?!

Na je, Hivi katika zamn zao (Watawala hawa) Al-Kaaba imekuwa ni tengenezo kwa ulimwengu wa Kiislamu? Ya Pili: Je, Haram ya Mwenyezi Mungu ni nyumba ya utuliva na amani siku hizi? Kwa hakika Qur'an Tukufu inaizingatia Al-Kaaba na viunga vyake kuwa ni Haram ambavyo ni mahala pa Mwenyezi Mungu penye amani. Mwenyezi Mungu Anasema: "Na yeyote atakayeingia Makka atakuwa katika amani. " Qur'an, 3:97.

Bila shaka Nabii Ibrahim ambaye ndiye baba wa Waislamu wote, alimuomba Mola wake aifanye Haram (ya Makka) kuwa hi mahali pa salama na amani. Mwenyezi Mungu amesema Akimnukuu Ibrahim: "Ewe Mola wangu ufanye mji huu kuwa mahali pa amani " Qur'an, 14:35.

Na sasa hebu tujiulize: Je, Watumishi hao wa Haramaini hivi wao kweli ndiyo walinzi wa sheria hii ya Mwenyezi Mungu? Je, Waislamu pamoja na Khitilafu zao za Madh-hebu wanao uhuru wa kutatua mambo yao ya kisiasa na kubadilishana mitazamo yao hapo kivenye Al-Kaaba Tukufu? Hivi Waislamu waliokusanyika kwenye Al-Kaaba wanaweza kutangaza matatizo yao na kujulishana wao kwa wao hali zao na mambo yanayowakabili? Je, Mambo ndivyo yalivyo, au ni kwamba uhuru wa kusema na kutoa maoni unatolewa kwa madh-hebu ya Hanbal peke yake tu miongoni mwa Madhehebu ya Kiislamu?! Na wala hakuna ruhusa ya kutoa fikara na maarifa ya juu katika Uislamu isipokuwa zile fikra dhaifu za Ibn Taymiyah na Ibn AI-Qayyim na zaidi ya hapo ni fikra za Muhammad Ibn Abdil-Wahab!! Na wala hakuna kizungumzwacho katika khutba za Ijumaa na nyinginezo kuhusu maudhui yoyote ya Uislamu isipokuwa ni kuzuru makaburi na kuharamisha hafla za maulidi ya Mtume[s.a.w.w] na kuharamisha kuwaheshimu Mawalii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, eti kama kwamba Uislamu umedhibitiwa katika maudhui hizi peke vake!!

Na yeyote mwenye kuzikhalifu fikra zao hizo batili, basi malipo yake ni kumhukumu kuwa ni kafiri na ni mshirikina, na kwamba inajuzu kumshutumu na kumpiga na kumlaani, hivyo basi ni kafiri tena mshirikina na mengineyo. Je, hii ndiyo maana ya "Haraman Aminan" (Yaani Nyumba Tukufu ya Amani) na je, hivi tutakuwa tuko kinyume cha ukweli ulivyo iwapo tutasema kwamba leo hii Al-Kaaba inakanyagwa na nyayo za Mawahabi? Bila shake fikra Kiwahabi imesimama juu ya msingi wa kuyakufurisha Madh-hebu na vikundi vya Kiislamu na kupanda mbegu ya utengano miongoni mwa Waislamu, na kuharibu heshima ya Uislamu na mafunzo yake bora na kuondosha athari za Utume, na (pia Uwahabi umesimama juu ya msingi wa) kufanya mapatano na kujipendekeza kwa kila waovu na watawala wachafu na waovu mpaka hata (wanajipendekeza) kwa Yazid bin Muawiyah!! Nao Makhatibu na waandishi ambao wanatumiwa na Masultani wa Kiwahabi, hao siyo Makhatibu (Safi) isipokuwa ni waajiriwa wa Pilato na wawaidhi wa Masultani, hawasemi wala hawaandiki ila kile wanachokitamani mabwana zao wa Kiwahabi wasiyoijuwa Dini. Ewe msomaji Mtukufu, huenda ukatuona sisi labda tumezidi mao katika kuwalezea (Mawahabi) na tumejitenga mbali na ukweli na uadilifu katika maelezo tuliyoyaeleza juu ya kundi hili.

Lakini ili usiendelee kuwa na mashaka na wala usitutuhumu kuvuka mipaka katika maelezo, basi sisi tunaweka mbele ya macho yako picha ya Jalada la kimoja kati ya vitabu ambavyo vimechapishwa na Serikali ya Saudia na kuvigawa kwa wingi, na kitabu hiki kinahusu kumtukuza na kumheshimu mtu ambaye jeshi Iake liliipiga Al-Kaaba kwa mizinga, na kuhalalisha kila kilicho haramu katika mji wa Mtume wa Mwenyezi Mungu [s.w.t] kwa jeshi lake kuukalia siko tatu kamili likipora mali na kuwavunjia watu heshima zao na kuwauwa! Na utaona kwa macho yako pameandikwa juu ya jalada kwamba Wizara ya Elimu katika Serikali ya Kiwahabi ndiyo iliyobeba jukumu la kuchapa na kusambaza kitabu hiki kilichobatili. Baada ya maelezo hayo.... tunsema kwamba: Katika nchi ya Hijazi kuna uhuru usiyo na mpaka na wakati huo huo kuna ukandamizaji usiyo na mpaka.

Ama uhuru usiyo na mpaka ni ule walionao Mawahabi na washirika wao miongoni mwa wanaokula fadhila zao, kwani vitabu na vijitabu vilivyojazwa maandiko yanayowasifia madhalimu na kuwatukuza mafasiki wa Kibanu Umayyah na Bani Abbasi vinachapishwa na kusambazwa bila kikwazo cho chote au Sharti yoyote, bali serikali inachangia kuvichapisha kuvisambaza. Ama shinikizo na ugandamizaji na unyanyasaji na vizuwizi na kupiga marufuku kuko kwenye vitabu vinavyozungumzia Uislamu kama ulivyo shuka toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na vinavyozungumzia Ah-lul-Bait ambao Mwenyezi Mungu amewalinganisha na Qur'an na akaiteremsha Qur'an ndani ya nyumba zao na akawatakasa mno kutokana na uchafu.

Naam... bila shaka kila kitabu kianchoingia Hijazi (Saudi Arabia) ni lazima kichunguzwe na kufanyiwa utafiti na wala hakiruhusiwi kuingia nchini humo mpaka kwanza Wizara ya habari itoe ruhusa!! Kwa hakika mwaka uliopita, ambao ni mwaka wa 1404 A.H. mimi nilikwenda hija na kuyazuru maziyara matukufu likiwemo la Mtume[s.a.w.w] na kizazi chake kitukufu[a.s] huko Madina. Basi katika uwanja wa ndege wa Madina nilikuwa na nakala kumi za kitabu kiitwacho "Mas-dar Al-Wujud". Ambacho kinachambua dalili za kimaumbile na za kiakili juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na lengo la kuzichukua nakala hizo katika nchi hiyo ilikuwa ni kushirikiana kueneza Tauhid na kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba, mtu anayehusika na mambo ya vitabu katika uwanja wa ndenge aliamuru nakala hizo zizuwiwe na zisisambazwe mpaka hapo itakapotolewa hukumu nyingine. Na baada ya yeye kukipitia kitabu hiki kwa haraka haraka aliniambia: "Japokuwa kitabu hiki ni chenye faida na ni kizuri lakini ni lazima kukipeleka kwenye wizara ya habari nawe utakichukua kutoka kwao. Naama hii ndiyo maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Nchi yenye Amani"!!!?

NENO "SHIRKI" LITAKUKUTA KILA UPANDE

Bila shaka kabisa miongoni mwa maneno ambayo ni rahisi na yanatumika katika nchi ya Saudia ni neno "Shirki", na tuhuma hii huelekezwa kwa wanachuoni wengi na watu wenye heshima katika Uislamu! Utakapokutana na watu idara ya "Al-Amri Bil Maaruf Wannahyi Anil Munkar neno utakalolisikia kila wakati ni hili neno baya na mfano wa hili, kama kwamba ndani ya kamusi zao hakuna maneno mengine isipokuwa maneno haya mabaya yenye kuchukiza tena machafu na ni kana kwamba hawana jingine la maana isipokuwa kuelekeza tuhuma hii ya shirki kwa kuwatuhumu (vibaya) wageni wa Mwenyezi Mungu na mahujaji wa nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu!! Wakati nikiandika utangulizi huu kimenifikia kitabu kiitwacho, "As-hiatu-wa At-Tashayuu" kilichotungwa na Mpakistani mwenye chuki ambaye ni miongoni mwa wanaofadhiliwa na Mawahabi, jina lake ni Ihsan Ilahi Dharir, na kimechapishwa Saudia. Na ndani yake anazitupa tuhuma na uzushi dhidi ya Ushia, na anadai kwamba yeye anaeleza kutokana na vitabu vyao na rejea zao.

Kwa mfano, utaona katika ukurasa wa ishirini wa kitabu hicho, anataja neno la Al-Marhum Al-Ustadh Mheshimiwa Sheikh Muhammad Husein Al-Mudhaffar, kisha analisherehesha kufuatana na vile apendavyo na namna inavyompelekea nafsi yake inayoamrisha uovu. Katika maelezo yafuatayo tunaweka mbele yako Ewe msomaji Mutukufu neno hilo pamoja na sherehe ya Wahabi huyu ili uone mwenyewe ni vipi Mawahabi waliofilisika kwa dalili wanavyotegemea maneno ya tuhuma na uzushi na uongo dhidi ya Shia. Marhum Al-Mudhaffar anasema: "Fakanatid-Daawatu Littashayui Liabil-Hasan Alayhis Salaam Min Sahibir-Risalat Salallahu Alayhi Waalihi Wasallama Tamshi Minhu Janban Lijanbin Maad-dawat Lish-Shahadatayn." Tafsiri Yake: Mwito kutoka kwa Mtume[s.a.w.w] kumfuata Abul-Hasan Ali[a.s] ulikuwa ukienda sambamba na mwito wa Shahada mbili. Na maana ya maneno yake haya ni kwamba: Ushia haukuzalikana kutokana na hali ya kimazingira wala siyo Madh-hebu yaliyoanzishwa baadaye, bali ni Mah-hebu ya asili ambayo chanzo chake kinaanzia kwa Mwenyewe Mtume Muhammad[s.a.w.w] , kwani Mtume alikuwa akilingania wau juu ya Uimamu wa Amirul-Muuminina Ali[a.s] sambamba na wito Wa Shahada mbili.

Kisha Wahabi huyu muovu anayawekea Taaliq maneno ya Sheikh Mudhaffar na anasema: Hakika Mtume (kwa mujibu wa madai ya Mudhaffar) alikuwa akimfanya Ali kuwa ni mshirika wake katika Unabii wake na ujumbe wake"!! Iwapo Mwandishi huyu siyo mtumwa wa matamanio yake na chuki na mwenye kufadhiliwa na Mawahabi, na iwapo ni mchunguzi wa misingi ya itikadi za Kiislamu za Kishia na misingi Tabari, nasi kwa sasa hivi hatuna lengo la kufanya ufafanuzi katika maudhui hii, lakini tunataja mfano wa jambo hilo: Ndani ya Kitabu "As-hiatu-wa At-Tashayuu" uk. 49 mtungaji anatuhumu Ushia kwamba umepokea fikra zake kutoka kwa Abdallah bin Sabaa aliyezalikana kutoka kwa Myahudi wa Yemen, na anavyoitakidi Tabari kwamba (Abdallah bin Sabaa) alidhihirisha Uislamu na kuficha Uyahudi na mapenzi yake kwa Imam Ali aliyafanya kuwa ni kifuniko cha kueneza fikra zake.

Jambo hili hatutalitafiti kwa wakati huu. Basi utamona mwandishi huyu wa Kiwahabi anategemea mambo aliyoyapokea Tabari kuhusu uzushi huu, Amma Sanad za riwaya ambayo Tabari anaieleza ni kama ifutavyo neon kwa neon:"Aliniandikia As-Sariyyu kutoka kwa Shuaib, kutoka kwa Seif, kutoka Atiyyah naye toka kwa Yazid Al-Faq-Asi: Abdullah bin Sabaa alikuwa Myahudi katika watu wa Sanaa...." (Vile vile ameipokea riwaya hii Ibn Khaladun Al-Magharibi na Ibn Kathir Ash-Shami na walio mfano wa Tabari miongoni mwa maadui wa Ahlul-Bait. Sasa hivi tunaiweka riwaya hii kwenye meza ya uchunguzi wa uhakiki ili tuone, je, inajuzu kuitegemea riwaya ya wapokezi hawa amboa majina yao yametajwa hapa au haifi? Kwa mtazamo wa haraka ndani ya vitabu vya elimu ya rijali (ambavyo vimeandikwa na wanachuoni wa Kisunni) vitatutosheleza kufahamu hali zaa wapokezi hawa.

Hebu Tazama uhakika wenyewe:

1. As-Sari sawa sawa akiwa ni As-Sari ibn Ismail Al-Kufi au As-Sari lbn A'sim aliyekufa mwaka 258 kila mmoja wao ni miongoni mwa waongo na wazushi.[10]

2. Shuaib ibn Ibrahim Al-Kufi: Maj-hul (Hatambulikani hali yake).[11]

"Hakika huyu ni ndugu yangu na ni wasii wangu na ni khalifa wangu kwenu, basi msikilizeni na mumtii.[12]

Kutokana na ukweli huu wa kihistoria Mashia wanasema kwamba, tangu siku hiyo aliyoamrishwa Mtume[s.a.w.w] kulingania Tauhidi na Utume, aliamuriwa pia katika siku hiyo kulingania Uimamu wa Ali[a.s] na ukhalifa wake baada yake, basi mwito wa imani na Utume umeambatanishwa na mwito na kuamini Uimamu. Je, inasihi kusemwa kwamba Mashia wanaitakidi kuwa Ali[a .s ] alikuwa mshirika wa Mtume katika Utume?" Na Je, mwito wa Ukhalifa wa Imam Ali[a.s] baada ya Mtume[s.a.w.w] kufariki maana yake ni mwito wa Unabii?

MAKOSA KATIKA VITABU VYA MASUNNI

Naam bila shaka upungufu na kosa lililoko katika vitabu vya Masunni na hasa Mawahabi linarudi kwenye mambo mawili:

Jambo la Kwanza: Ni kukosa kwao maarifa mengi ya kutosha kuhusu madhehebu ya haki, na upungufu huu walionao hauhusu zama zetu hizi tu, bali unarudi hadi kwenye karne zilizopita katika historia, na huenda sababu ya jambo hilo ni ile hali iliyokuwa ikitendwa na serikali za watu wa Jahannam yaani Banu Umayyah na wengineo katika kuwakandamiza na kuwanyima uhuru Mashia na kutokuwapa nafasi ya kubainisha itikadi zao za haki katika Mahfali na mikusanyiko ya Kielimu, ili watu waufahamu Ushia kutoka katika vinywa vya viongozi wake wasipotoshwe na uzushi wa maadui zake. Kwa hakika historia inatuthibitishia kwamba, Madh-hebu yote yalikuwa yanauhuru wa kutoa maoni na kubainisha itikadi (zao) isipokuwa haya Madh-hebu ya haki yalikuwa yamezuwiliwa kufanya hivyo.. Naam, upepo wa uhuru kwa Mashia ulivuma katika baadhi ya nyakati ambazo hazikutosheleza kulithibitisha lengo hili.

Na kwa hali yoyote ile, kutokuyafahamu Madh-hebu ya Ushia (na wakati mwingine chuki) imekuwa ndiyo sababu ya kutengenezwa uongo na uzushi huu na kuvijaza vitabu uzushi na kuichafua shabaha ya Madh-hebu haya ya haki. Na kwa hakika Ahmad Amin wa Misri, mwandishi wa kitabu kiitwacho "Fajrul-Islam" amekiri jambo hili baada ya kutawanya kitabu chake hicho kilichojaa uongo na uzushi dhidi ya Shia, kisha akauzuru mji wa Najaf baadhi ya wanachuoni wakamlaumu kuhusiana na kupotosha kwake na uzushi wake dhidi ya Shia, na udhuru wake mkubwa aliokuwa nao ilikuwa ni kutokuujua Ushia na uchache wa rejea. Jambo La Pili: Ni kuharibika kwa utaratibu wa masomo katika vyuo vya Kisunni na kubadilishwa kwa vitabu vyenye maarifa kwa undani kama vile "Kitabul-Mawaqifi na Sharhul Maqasid" (Na badala yake vikawekwa) vitabu vya kiwango cha chini visivyokuwa na uchunguzi wa kina, na jambo hilo limepelekea kushuka kwa kiwango chakufikiri na utunzi na kutoweka fikra za uchunguzi wa kina kiasi kwamba hakuna katika nchi nyingi za Kiislamu anayeweza kuvisomesha vyema vitabu hivi viwili ambavyo vimeandikwa katika karne ya nane Hijiriyyah.

Kwa sababu hii basi, siyo jambo la ajabu kumuona "Ihsan Ilahi Dhahir" kwa mfano anatangatanga hajui anachokifanya kwani hatenganishi baina ya mwito wa Uimamu na mwito wa Utume, na anaandika kitabu juu ya madh-hebu katika historia na kuvitawanya kwa kusaidiwa na mali zinazotokana na petroli ambaye inaporwa na serikali ya uvamizi ya Kiwahabi ndani ya Hijazi, na hili linafanyika hali ya kuwa inafahamika kwamba mwandishi huyu hafahamu misingi ya itikadi ya Kishia.

UCHACHE WA KUFIKIRI KWA UNDANI

Tangu zaidi ya miaka mia moja iliyopita, vita ya kifikra dhidi ya Uislamu ikiwa inawasha moto wake, na mataifa ya magharibi na mashariki yakisaidiana na vibaraka wao walioko katika nchi za Kiislamu yanafanya juhudi zao za upeo mkubwa ili kuinagamiza dini hii tukufu na kuchafua shabaha yake, haipiti wiki au mwezi isipokuwa hutolewa kitabu dhidi ya dini tukufu ya KiisIamu. Katika hali hii yenye majonzi, hivi kweli inafaa kwa Saudia kukusanya nguvu zake na uwezo wake na matoleo yake yote ili kuupiga vita Ushia peke yake tu?!! Na kana kwamba katika ulimwengu wa Kiislamu hakuna tatizo jingine isipokuwa Ushia?!! Hata hivyo, lau vijitabu hivyo vingekuwa vinazungumza juu ya msingi wa mantiq na dalili tusingevipinga kwani mantiq inakubalika kwa wanachuoni wa Kishia, kwani wao huikubali au kuipinga kwa mantiq na hoja, lakini kwa bahati mbaya sana vijitabu vyao vingi utaviona vimejaa uongo, uzushi, makosa na uzandiki dhidi ya Mashia na dhidi ya wanachuoni wao wema (r.a).

Bali utaona katika baadhi ya vitaba hivyo kuwa, havikuepukana na kumtweza na kumkosea Adabu Imamul-Muta-Qina na Amirul-Muuminina Bwana wetu na kiongozi wetu Ali[a.s] . Hebu chukua mfano wa hilo katika kitabu, "Ashiatu WatTashayyuu" tulichokiashiria hapo kabla, hicho ni mfano ulio wazi miongoni mwa vijitabu vyenye kupotoka, kwani utamuona mtunzi (Akinakili kutoka kwa Tabari, Ibn Kathir, Ibn Khaladun na wengineo miongoni mwa maadui wa haki) anauona Ushia kuwa ni (Dhehebu) lililozalikana kutokana na fikra ya Abdallah Bin Sabaa ambaye ni Myahudi, kisha anatolea Ushahidi aliouandika Ahmad Amin wa Misri (ndani ya kitaba kiitwacho Fajrul-Islam) dhidi ya Shia, kisha anakamilisha safari yake kutolea ushahidi makala za mustashriqin Mayahudi na Wakristo "Dauzi" na "Mul-Aer" na "Wilhazen".

Lakini hataji chochote kutoka katika vitaba vya Mashia, basi je, hii ndiyo Insaaf (Usawa)!? Hakika wanachuoni wa Kishia wa hapo mwanzo kama vile Sheikh Saduq aliyefariki mwaka 381 A.H. na Sheikh Mufid aliyefariki mwaka 413 A.H. na wengineo, bila shaka waliziandika Aqida (Itikadi) za Kishia na kuzitawanya kwa watu nazo ni nyingi mno ndani ya maktaba na zinatoa picha ya asili ya Aqida za Kishia, basi ni vipi hazitegemei katika kuzinakili? Je, Siyo kwamba "'Wenye nyumba ndiyo wajuao zaidi kilichomo ndani yake"?! Je, Ahmad Amin wa Misri ambaye haujui Ushia na hautambui kama alivyokiri yeye mwenyewe ndiye ayajuaye madhehebu ya haki kuliko wanachuoni wake wema? Na utamuona mwandishi huyu muovu wa Kiwahabi anajaribu kujitakasa makosa aliyoyafanya dhidi ya Mashia kwa kutegemea vitabu vya maadui zao anasema: "Kwa hakika vitabu hivi (yaani vitabu vya itikadi za Kishia) ni vitabu vya propaganda za Kishia ama kwa itikadi yao halisi haikutajwa ndani ya vitabu hivi!!!

Na baya zaidi kuliko hilo ni kwamba, yeye anaileta hadithi iliyoko ndani ya 'Biharul-Anwaar" na Al-n-Waarun-Nu'maniyyah na kuizingatia kuwa ni dalili ya itiqadi ya Mashia, huku akijua kwamba hapana shaka kuwa kuna hadithi dhaifu ndani ya vitabu vya Kisunni na Kishia, hili sote tunalijua, na kutaja hadithi moja haiwi ndiyo dalili juu ya itikadi ya watu fulani (kwa namna yoyote ile) kwani wako wapokezi wengine ni dhaifu na waongo na ni Majhul hawatambulikani hali zao". Basi haiwezekani kuitegemea hadithi ila baada ya kuihakiki katika sanadi yake na wapokezi wake. Sisi tunamuuliza Wahabi huyu mwenye kuajiriwa na wengineo mfano wake miongoni mwa wanaofadhiliwa: Je, hivi kila kilichokuja katika Tarikhut-Tabari kinazingatiwa kuwa ni sahihi bila ya shaka au ni kwamba kuyategemea hayo aliyoyaleta kunategemea uhakiki katika Isnadi yake?! Hakika katika mambo yasiyokuwa na shaka ndani yake, ni kuwemo kwa wapokezi waongo wa wazushi ndani ya riwaya za yake, basi Taaliq hiyo mbovu isingetoka kwake na wala asingemkosoa Sheikh Mudhafar ambaye ni mwanachuoni mkubwa. Kishia sisi tunasema, ikiwa mwito wa Uimamu wa Ali[a.s] unazingatiwa kuwa ni shirki au ni kuushirikisha na utume, basi Qur'an imetangulia kulisema hilo, kwani imetoa mwito kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Ulul-Amri katika Siyaqi moja. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu "Mtiini Mwenyezi Mungu na mumtii Mtume na Ulul-Amri miongoni mwenu. " Qur'an, 4:5.

Basi kwa mujibu wa maoni ya mwandishi huyu wa Kiwahabi, ni kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu [s.w.t] badala ya kulingania Tauhidi alilingania shirki na Aqida ya miungu wawili kwani aliambatanisha baina ya kuwatii Ulul Amri na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani neno Ulul Amri kwa namna yoyote ile tutakayolifasiri bila shaka litamuingiza Imam Ali[a.s] (Katika maana hiyo), bali yeye anastahiki zaidi kuliko wengine. Wanahistoria na wanachuoni wa Tafsiri na hadithi wameeleza kwamba iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Na Uwaone Jamaa zako wa karibu " Qur'an 26:214.

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu [s.w.t] aliwaita jamaa zake wa karibu (nduguze, na wazee wake) kwenye karamu ya chakula nyumbani kwake, kasha akawatangazia habari ya Unabii wake na Utume wake na baada ya hapo akasema: "Ni nani kati yenu atakayenisaidia juu ya jambo hili kwa sharti awe ndugu yangu na wasii wangu na Khalifa wangu kwenu"? Basi hapana yeyote aliyesimama isipokua Imam Ali[a.s] akasema, "Mimi Ewe Mjumbe wa Mwenezi Mungu." Mtume[s.a.w.w] alikariri maneno yake hayo mara ya pili na ya tatu ili awape fursa ya kuchukua uthibitisho..... Na hakuna yeyote aliyejibu isipokuwa Amir-ul-Muuminina Ali[a.s] basi Mtume akasema:

3. Seif Ibn Umar: Anasimulia hadithi za uongo na kuzinasibisha kwa wapokezi waaminifu.[13]

4. Yazid Al-Faq-Asii: Maj-hul kabisa (Hatambulikani hali yake kabisa) jina lake halikutajwa popote ndani ya vitabu vya "Rijal" (yaani vitabu vinavyochunguza hali za wapokezi wa hadithi).

Na inafaa kusema kwamba, Tabari anasimulia ndani ya juzuu Ia tatu, la nne na la tano katika Tarikh yake tokea mwaka wa kumi na moja A.H. mpaka mwaka wa thelathini na saba A.H. na miaka hii ni kipindi cha utawala wa Abubakr na Umar na Uthman na riwaya zote hizo zimepokelewa kutoka kwa watu hawa watano tu!! Na matokeo yake Tabari amezua matukio mengi miongoni mwa hayo na akayaeleza kama vile ipendavyo nafsi yake!! Basi Je, hii inasihi na Je, inajuzu kuzitegemea riwaya kama hizi?! Na kinacholeta mshangao zaidi ni kwamba, riwaya za watu hawa watano ziko katika juzuu ya tatu na ya nne na ya tano tu ndani ya Tarikh Tabari, amma majuzuu mengine huwezi kuona majina yao yanatajwa wala riwaya itokayo kwao isipokuwa riwaya moja tu ndani ya juzuu ya kumi!! Basi Je, Ujuzi wa Tarikh (Historia) alionao "Sari" na "Seif bin Umar" ulikuwa umedhibitiwa katika kipindi hiki peke yake tu, na ulikuwa unahusika na mambo ya Madh-heb peke yake?!!

Naam, yeyote mwenye kuzichunguza kwa undani riwaya za watu hawa watano atafahamu wazi kwamba riwaya hizo ni uzushi wa mtu mmoja, na kwamba ndani yake kulikuwa na lengo makhsusi. Ni mushkeli kufikiria kuwa Tabari hakufahamu jambo hili, basi ni kwa nini Tabari ametaja yote haya? Jawabu lake ni kwamba: Bila shaka hiyo ni hali ya kupenda na chuki vitu ambavyo humpofua mtu na kumfanya awe kiziwi! Na kinachohuzunisha zaidi ni kwamba kundi la wanahistoria waliokuja baada ya Tabari wakanakili toka kwake na wakafuata nyayo zake na wakazileta riwaya hizi za uzushi na uongo ndani ya vitabu vyao vya historia bila ya uchunguzi wowote juu ya kusihi kwake na watu waliozisimulia na sanadi zake, wakidhani kwamba kila anachokisimulia Tabari ndiyo hasa tukio halisi na ndiyo ukweli ulivyo. Iangalie Tarikh ya Ibn Asakir na Al-kamil ya Ibn Al-Athir, na Al-Bidayatu Wan-Nihayah ya Ibn Kathir na Tarikh ya Ibn Khaladun na nyinginezo utaona usahihi wa maneno yetu.

Hali ni hiyo hiyo kwani vitabu vya Tarikh vya sasa hivi havikusalimika na uzushi huu mbaya na Ikhtilafu inayochukiza. Lakini kwa bahati nzuri watu wa Sanadi ndani ya riwaya zilizomo katika Tarikh ya Tabari wametajwa, na hilo ni miongoni mwa mambo ambayo yanatoa nafasi ya kufahamu riwaya sahihi na kuilinganisha na riwaya dhaifu au iliyozushwa kama tulivyokuletea mfano mmoja unaoeleza jambo hilo. Na sasa tunarudia mazungumzo juu ya Kitabu "As-Shiatu Wa At-Tashayyuu" na tunasema: "Kwa hakika kitabu kinachotegemea rejea ambazo riwaya zake ni za uzushi na wapokezi wa riwaya hizo ni waongo tena wazushi, basi kitabu hiki kitakuwa hakimiliki japo thamani ndogo, nasi sasa hivi tuko katika zama za usomi na uchunguzi.

Basi Je, hivi itasihi kwa kundi kubwa la Kiislamu Ienye hadhi kubwa katika elimu za Kiislamu na kuhuisha Sunna Tukufu ya Mtume[s.a.w.w] ambalo liko mstari wa mbele kuwapiga wavamizi wa Ki'Israeli, hivi kweli ni sahihi kundi hilo linasibishwe kwa Myahudi asiyejulikana kwa kutegemea Tarikh potofu ambazo umekwisha thibiti uongo wa wapokezi wake?


3

4

5

6

7

8

9

10

11

12

13

14

15

16

17

18

19

20

21

22

23