UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 50942
Pakua: 5274

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 50942 / Pakua: 5274
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

11

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KUTABARUKU KWA ATHARI ZA MAWALLI WA MWENYEZI MUNGU NA KUOMBA UPONYO

Mawahabi wanaitikadi kwamba kutaka baraka kwenye Athari za Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Mawahabi pia wanamuona kuwa ni mshirkina mtu ambaye ataibusu mihrabu ya Mtume[s.a.w.w] na mimbari yake, japo hatafanya hivyo kwa nia ya ibada, isipokuwa ni kwa ajili tu ya mapenzi yake kwa Mtume[s.a.w.w] ndiyo maana katabaruku na kutaka uponyo kwenye Athari zake. Kukataza kutabaruku kwa athari za Mtume[s.a.w.w] na kulibusu kaburi lake na mimbari yake tukufu ni katika mambo ambayo Mawahabi wametilia nguvu kuyapinga dhidi ya Waislamu, na wamekuwa wakitumia makundi ya askari wa kigaidi waliopewa jina la waamrishaji mema na kukataza maovu, na wamewasambaza (askari) hao katika Msikiti wa Mtume[s.a.w.w] ili wazuwiye kulibusu kaburi lake tukufu na mimbari yake tukufu, pamoja na mihrab ya Msikiti wa Mtume[s.a.w.w] . Mawahabi hawa wanawahujumu mahujaji hapo Madina kwa kila aina ya mateso na kuwazuwiya kutabaruku na kulibusu kaburi la Mtume[s.a.w.w] na utawaona kila mara wameshika fimbo, na mikononi mwao mna nyaya ngumu tayari kumshambulia kila Hujaj atakayethubutu kutabaruku au kulibusu kaburi la Mtume[s.a.w.w] . Na kutokana na hali hii basi, mara kwa mara wamekuwa wakimwaga damu za mahujaji wasio na makosa na kuudhalilisha utu wao katika Msikiti wa Mtume[s.a.w.w] , kwa madai kwamba kutabaruku na kulibusu kaburi ni kumuabudu huyo aliyezikwa hapo.

Kwa hakika watu hawa hawaujuwi Uislamu, na wamekosea kufahamu maana ya Ibada na Maf-humu yake, na kwa sababu hii basi wamepotea njia na wanatangatanga ndani ya upotevu. Wamekuwa wanaona eti kila anapoheshimiwa mtu aliyekwisha kufa ni kumuabudu mtu huyo, pamoja na kufahamu kwamba kubusu kaburi tukufu na kutabaruku kwa athari za Utume siyo kwa ajili nyingine isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Waislami hawamtukuzi Mtume Mtukufu wala hawatabaruku kwa athari zake ila ni kwa kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni Nabii wake mteule ambaye Mwenyezi Mungu amemtukuza kuliko Manabii wote na viumbe wote. Basi na ifahamike kwamba kila wanapoheshimiwa na kutukuzwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu tendo hilo (kwa asili) ni kumtukuza Mwenyezi Mungu. Na hauthibitiki ukweli wa Tauhidi ila pale kila kitu kitakapotendwa kiwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na katika njia yake, na hapo ndipo itakapokuwa kila kitu kinaanzia kwa Mwenyezi Mungu na kila kitu kinaishia kwake.

Tutazungumzia maana ya Ibada katika sehemu ifuatayo kwa undani, ama sasa hivi utafiti wetu utahusu kutabaruku kwa athari za Mawalii, na utafiti huu tutalazimika kuulekeza kwenye kipimo cha Qur'an na Sunna ya Mtume[s.a.w.w] ili haki iweze kubainika.

MTAZAMO WA QUR'AN JUU YA KUTABARUKU

Katika Qur'an tunatosheka na aya moja tu, nayo ni ile inayomnukuu Nabii Yusuf[a.s] akisema: "Nendeni na kanzu yangu hii mukaiweke usoni kwa baba yangu (macho yake yatarudi) ataona". Qur'an, 12.93. Nabii Yusuf aliituma kanzu yake kwenda kwa baba yake na akawaambia ndugu zake "Nendeni na kanzu yangu hii na muiweke usoni kwa baba yangu ili macho yake yarudi apate kuona. Mwenyezi Mungu anasema: "Na alipokuja mtoaji habari njema, aliiweka kanzu ile usoni kwake na macho yalirudi akaona". Qur'an, 12:96. Aya hii iko wazi kutoa ruhusa ya kutabaruku kwa athari za Manabii na Mawalii kiasi kwamba hata Nabii anatabaruku kwa Nabii mwenziwe kama hivi Nabii Yaqub[a.s] anatabaruku kwa kanzu ya Nabii Yusuf[a.s] .

Na ni wazi kabisa kwamba kuponya kunatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na yeye ndiye mtendaji halisi, isipokuwa kutabaruku kwa kanzu ya Nabii kumekuwa ni wasila wa kuponya kama tunavyotumia dawa kuwa ni wasila wa kupona kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ewe msomaji ingekuwaje kama kutabaruku kwa Nabii Yaqub kwa kanzu ya mwanawe Yusuf kungelitokea mbele ya watu wa Najdi na wafuasi wa Muhammad Ibn Abdul-Wahab, wangelihukumu namna gani jambo hili? Je, wangehukumu kuwa ni kafiri au mshirikina au mwenye dhambi? Wakati yeye ni Nabii na ni maasum? Kutabaruku kwa Waislamu kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] na makaburi ya watu wa nyumba yake na pia athari zao hakuna tofauti na kutabaruku alikotabaruku Nabii Yaqub[a.s] kwa kanzu ya mwanawe Yusuf[a.s] .

KUTABARUKU NA SERA YA WAISLAMU

Mtazamo wa haraka katika sera ya Waislamu kuanzia kwa Masahaba mpaka leo, unatuonyesha wazi sunna inayofuatwa kuhusu kutabaruku kwa Mtume[s.a.w.w] yeye mwenyewe na athari zake tukufu katika kpindi chote cha historia ya Uislamu. Na katika maelezo yafuatayo tutaeleza mifano michache inayohusu kutabaruku:

1. Bibi Fatma Az-Zahra ambaye ndiye mwanamke bora ulimwenguni na ni binti ya Mtume[s.a.w.w] , alifika kwenye kaburi la baba yake na akachukua gao Ia udongo wa kaburi akawa anaunusa na kulia huku akisema: "Mtu aliyenusa udongo wa kaburi la Ahmad, halaumiwi iwapo hatanusa mafuta mazuri ya ghaliya." Yamenipata milele masaibu ambayo lau yangeliupata mchana ungegeuka na kuwa usiku. Wameitaja Qadhiya hii wanahistoria wengi miongoni mwao ni As-Samhudi.[151] Kwa hakika kitendo hiki cha Bibi Fatma Az-Zahra ambaye ni maasum kinajulisha kwamba kutabaruku kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] ni jambo linalofaa na pia kutabaruku kwa udongo wa kaburi lake.

2. Bilal ambaye alikuwa ni muadhini wa Mtume[s.a.w.w] alipata kuishi Shamu katika kipindi cha utawala wa Omar Ibn Khattab. Siku moja alimuona Mtume[s.a.w.w] katika ndoto anamwambia:

"Ewe Bilal mbona umenitupa kiasi hiki, je haujakufikia wakati wa kunizuru ewe Bilal?" Basi Bilal alizindukana usingizini akiwa na huzuni na khofu nyingi na alipanda kipando chake kuelekea Madina na akafika kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] akawa analia pale kaburini huku anausugua uso wake kwenye kaburi, mara Hasan[a.s] na Husein[a.s] wakafika, Bilal akawakumbatia na kuwabusu....[152]

3. Ibn Hajar anasema: "Kila mtoto aliyezaliwa katika zama za uhai wa Mtume[s.a.w.w] huhukumiwa kwamba alimuona Mtume[s.a.w.w] , na hii ni kwa sababu Ansar wote walikuwa wakiwaleta watoto wao kwa Mtume[s.a.w.w] kwa ajili ya Tahnik [153] na kupata baraka kiasi kwamba imesemwa kuwa: Wakati Makka ilipotekwa na (Waislamu), watu wa Makka wakawa wanakuja kwa Mtume[s.a.w.w] wakiwa na watoto wao ili awaguse vichwa vyao na awaombee baraka".[154] Na kuhusu jambo la kutabaruku, mwandishi wa kitabu kiitwacho, "Tabar-rukus Sahabah" amesema: "Hapana shaka kwamba athari za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ambaye ni) mbora kuliko viumbe wote na mbora kuliko mitume wote, kuwepo kwake ni jambo lenye kuthibiti na ni mashuhuri mno. Basi kwa hiyo athari hizo ndiyo bora kutabaruku kwazo, na idadi kubwa ya Masahaba wameziona na wakaafikiana kutabaruku kwazo na kuzipa umuhimu wa kuzikusanya nao Masahaba ndiyo watu waongofu na ni kiigizo kizuri, kwani walitabaruku kwa nywele zake na maji aliyotawadhia na jasho lake na nguo zake na pia kuugusa mwili wake na mengineyo yanayofahamika katika athari zake tukufu ambazo zimesihi khabari zake toka kwa watu wema.[155] Yanatosheleza maelezo aliyoyataja Muslim katika Sahih yake kuhusu kutabaruku aliposema: "Hakika Mtume[s.a.w.w] alikuwa akiletewa watoto naye huwafanyia tahnik.[156]

4. Masahaba walikuwa wakitabaruku kwa maji ya udhu aliyotawadha na aliyokoga Mtume[s.a.w.w] : Bukhari amopokea hadithi isemayo: "Mtume[s.a.w.w] alitutokea katika kipindi cha jua kali, akaletewa maji ya kutawadha na akatawadha, basi watu wakawa wanachukua maji ya udhu atawadhayo Mtume[s.a.w.w] wanajipangusia". [157] Kuhusu jambo hilo kuna riwaya nyingi zilizojaa katika vitabu vya hadithi.

5. Masahaba walikuwa wakitabaruku kwa nywele za Mtume[s.a.w.w] kama alivyopokea Anas kwamba: "Mtume[s.a.w.w] aliponyoa kichwa chake, Abu Tal-ha alikuwa ni mtu wa kwanza kuchukuwa nywele za Mtume[s.a.w.w] . [158] Anas anaposema "Abu Tal-ha ndiyo mtu wa kwanza kuchukua nywele za Mtume[s.a.w.w] " inaonyesha wazi kuwa Masahaba walishindana katika kutabaruku kwa nywele za Mtume[s.a.w.w] lakini Abu Tal-ha alikuwa wa kwanza kuzichukua. Na imepokewa tena kwamba: "Mtume[s.a.w.w] alifika Mina akaenda kwenye Jamrah akalipiga, kisha akaenda kwenye makazi yake hapo Mina, kisha akamwambia kinyozi, "ninyowe," na akaashiria upande wa kulia kisha kushoto kisha akaendelea kuwapa watu (nywele zake)". [159]

6. Masahaba vile vile walikuwa wakitabaruku kwa chombo alichokuwa amenyewea Mtume[s.a.w.w] : Abu Bar-da amesema: "Abdullah bin Salaam aliniambia, "Je, nisikunyweshe kwenye chombo alichonywea Mtume?"[160] Riwaya hii inaonyesha kwamba, Abdallah bin Salaam alikuwa amekihifadhi chombo hicho kwa kuwa kilikuwa kimepata baraka kwa sababu mjumbe wa Mwenyezi Mungu alinywea chombo hicho.

7. Pia Masahaba walikuwa wakitabaruku kwa mikono yake Mitukufu: "Imepokewa toka kwa Abu Juhaifah amesema, "Mtume alitoka katika siku yenye joto kali akaenda mpaka Bat-haa akatawadha kisha akaswali Adhuhuri rakaa mbili na Al-asr rakaa mbili.... watu wakasimama wakaishika mikono yake wakawa wanajipangusia nyuso zao. Anasema Abu Juhaifah, "Nikauchukua mkono wake nikauweka usoni kwangu, basi niliuona ubaridi mno kuliko theluji na una harufu nzuri kuliko miski".[161]

8. Pia wakitabaruku kwenye mimbari yake tukufu:

Imepokewa toka kwa Ibrahim bin Abdur-Rahman bin Abdil-Qari kwamba yeye alimuona Ibn Omar ameweka mkono wake kwenye Mimbar mahala ambapo Mtume[s.a.w.w] alikuwa akikaa, kisha akauweka nikono wake usoni kwake.[162]

9. Vile vile walikuwa wakitaka uponyo kwenye kaburi lake tukufu: Imepokewa toka kwa Imam Ali[a.s] kwamba yeye amesema, "Kuna bedui alikuja kwetu baada ya kuwa tumemzika Mtume[s.a.w.w] kiasi cha siku tatu zimepita, akajitupa kwenye kaburi Ia Mtume[s.a.w.w] , akajipaka kichwani udongo wa kaburi Ia Mtume[s.a.w.w] na akasema, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulisema tukasikia usemi wako na uliyapokea toka kwa Mwenyezi Mungu, nasi tulipokea toka kwako na miongoni mwa yale ulioteremshiwa na Mwenyezi Mungu ilikuwa, lau wao watazidhulumu nafsi zao wangekujia... nami nimedhulumu (nafsi yangu) na nimekujia unitakie msamaha". Basi palisemwa kutoka kaburini "Hakika umesamehewa." [163] Kwa kifupi, iwapo mtu atavirjea vitabu vya historia (As-sihah na As-Sunan na Masanid) ataona ni jinsi gani Masahaba na Tabiina walivyokuwa wakitabaruku kwa kila kitu ambacho kinamafungamano na Mtume[s.a.w.w] , na walikuwa wakitaka kuponywa kwenye kaburi lake kwa kuweka mashavu yao juu ya kaburi na kuunusa udongo wa mahali hapo na kulia kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] .

Zaidi ya hapo, walikuwa pia wakitabaruku kwa fimbo ya Mtume[s.a.w.w] na mavazi yake na kuswali sehemu alizokuwa akiswali au alimopita. Na masimulizi yanayozungumzia jambo la kutabaruku ni mengi mno na haiwezekani kwa mtu mwenye akili kusema eti masimulizi haya ni ya kutungwa tu. Basi yatakuwaje ni ya kutunga wakati Bukhari na Muslim pamoja na wanachuoni wengine wa hadithi wameyapokea? Isitoshe hali hii, bali wanachuoni wawili wakubwa wamesimamia ukusanyaji wa riwaya hizi na kuzifafanua pamoja na kutaja rejea zake. Wa kwanza ni, Al-Ustadh Sheikh Muhammad Tahir Makki katika kitabu chake kiitwacho "Tabar-rukus-Sahabah Bia'thari Rasulillah". Wa pili ni, Al-Ustadh Sheikh Ali Ahmadi katika kitabu chake madhubuti kiitwacho "At-Tabar-ruk". Yeye amefafanua kwa undani habari zote zilizokuja kuhusu Tabar-ruk; na kitabu hiki kinahesabiwa kuwa bora cha zama hizi. Basi watasemaje Mawahabi juu ya hadithi hizi ambazo ni mutawatiri kimatamko na kimaana? Na ni upi msimamo wao kutokana na ukweli huu ulio wazi?

Basi ni za nini kelele hizi wazipigazo dhidi ya kutabaruku kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] jambo ambalo Masahaba na Tabiina wamekuwa wakilifanya bila ubaya wowote wala kulipinga au kuliharamisha, wakati hatuoni popote kwamba Mtume au Masahaba wake waliharamisha jambo hili. Na ni kwa nini Mawahabi hawawaachi Waislamu walibusu kaburi la Mtume[s.a.w.w] na wapate baraka zake na waonyeshe hisiya zao na mapenzi yao kwa Mtume[s.a.w.w] ? Je, Mawahabi hawajuwi kuwa, kukataza kutabaruku kwenye kaburi la Mtume na athari zake ilikuwa tabia na kazi ya Bani Ummayya hasa Mar-wani aliyelaaniwa na Mtume[s.a.w.w] ? Hebu soma mapokezi aliyoyapokea Al-Hakim ndani ya Mustad-rak yake kutoka kwa Dawuud bin Salih amesema: "Sika moja Mar-wan alikuja akamkuta mtu ameweka uso wake juu ya kaburi (la Mtume[s.a.w.w] ) akamshika shingoni kisha akamwambia, "Je unafahamu unachokifanya"? Kumbe mtu yule alikuwa Abu Ayyubul-Ansari, akamjibu, "Ndiyo mimi sikulijia jiwe hapa nimemjia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu". Nimemsikia mjumbe wa Mwenyezi[s.a.w.w] akisema: "Msiililie dini (msiihuzunikie) kama watawala wake ni watu wanaostahiki lakini ililieni dini watakapoitawalia wasiostahiki". [164] Mar-hum Sheikh Al-Amini amesema:

"Hadithi hii inatufahamisha kwamba kuzuwiya kutawas-sal kwenye makaburi matakatifu ni miongoni mwa Bid'a za Banu Ummayya na upotevu wao tangu zama za Masahaba na hakuna hata sikio moja kabisa lililopata kumsikia Sahaba akipinga tawas-sul hiyo isipokuwa Mar-wan mdhalimu aliyetokana na kizazi cha Umayya". Ni kweli "Ng'ombe huilinda pua yake kwa pembe zake". Ni kweli pia kwamba "Kwa kisingizio cha kumtafuta njiwa, muwindaji hula tende (za shamba la mitende aliloingia). Ukweli ulivyo ni kwamba Banu Ummayya na hasa Mar-wan, wanayo chuki dhidi ya Mtume[s.a.w.w] tangu siku ile Mtume[s.a.w.w] alipokuwa hakubakisha heshima yoyote ya Banu Ummayya, ila aliivunja wala cheo chochote ila alikiharibu na wala nguzo yao yoyote isipokuwa aliivunja na hayo yametokea kutokana na maneno makali ya Mtume[s.a.w.w] kuhusu Bani Ummayya ile siku ya Badri alipowapiga. Mtume[s.a.w.w] hasemi lolote kwa matamanio ya nafsi yake ila ni wahyi aliyopewa (aliyemfundisha Bwana Mtume ndiye mwenye nguvu zote) kwani imepokewa hadithi sahihi kuwa Mtume[s.a.w.w] amesema, "Itakapofika idadi ya Banu Ummayya watu arobaini watawafanya waja wa Mwenyezi Mungu kuwa ni watumwa, na mali ya Mwenyezi Mungu wataipora na kuifanya knwa ni mali yao na watakitumia vibaya kitabu cha Mwenyezi Mungu". [165]

Umeona jibu la Abu Ayyubul-Ansari kwa Mar-wan pale alipomuuliza unafanya nini? Akawa amejibu, sikujia jiwe bali nimemjia mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Hapa tunamuona Abu Ayyubul-Ansari anaeleza kwamba: "Makusudio ya kutawas-sal na kutabaruku ni kwa Mtume[s.a.w.w] ambaye tunaitakidi kuwa hapana tofauti baina ya kuwa yu hai au amekufa katika suala hili, lakini udongo na jiwe havina umuhimu wowote, isipokuwa udongo na jiwe vilivyopo kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] vimepata heshima na utukufu kwa sababu ya Mtume[s.a.w.w] . Ewe msomaji mpendwa, Bukhari ambaye kitabu chake kinazingatiwa na Masunni kuwa ndiyo kitabu sahihi mno kuliko vingine, yeye ameweka mlango aliouita "Babu Ma-dhukira Min Dir-in-nabi wa asahu wa Saifahu wa qadahahu wa khatamahu wa mas-ta-amalal-khulafan baadahu. Yaani mlango unaozungumzia habari za deraya ya Mtume, panga lake na fimbo yake, kikombe chake, pete yake na vitu walivyovitumia makhalifa waliokuja baada yake katika vitu ambavyo havikugawanywa na nywele zake, na viatu vyake na vyombo vyake ambavyo Masahaba wa Mtume na wengineo walikuwa wakitabaruku kwa vitu hivyo baada ya kufa Mtume[s.a.w.w] . [166]

Kama Mawahabi watazifuatilia hadithi hizi nyingi zaidi ya mia hawatakuwa na njia isipokuwa kukubali ukweli na kukiri iwapo tu watakuwa miongoni mwa wale wanaosikiliza maneno na kufuata yaliyo bora, vinginevyo: "Siku ya Hukumu imewekewa wakati maalum".

TAUHIDI KATIKA IBADA

Msingi wa wito wa Manabii[a.s] siku zote umekuwa ni kulingania kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na siyo kumuabudu mwingine peke yake, au kumshirikisha na Mwenyezi Mungu. Na msingi wa hukmu za mbinguni tangu mwanzo wa kutumwa ujumbe wa Manabii ilikuwa ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kukata mizizi ya shirki. Ukweli halisi ulivyo ni kwamba, lengo la kutumwa kwa Manabii ni kulingania (watu) kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu peke yake, na kupiga vita ushirikina wa aina zote na khususan kupinga shirki katika ibada. Qur'an Tukufu inaashiria ukweli huu wazi wazi na inasema:

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ﴿٣٦﴾

"Na bila shaka tulimpeleka Mjumbe kwa kila umma (akawambie umma wake) muabuduni Mwenyezi Mungu na muyaepuke masanamu. (Qur'an, 16:36)

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾

Na hatukumtuma kabla yako Mjumbe yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hakuna apasiwaye kuabudiwa ila mimi, basi niabuduni." (Qur'an, 21:25) Qur'an imeizingatia ibada ya Mwenyezi Mungu kuwa ni jambo linalokusanya na kushirikisha sheria zote za mbinguni na inasema:

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا ﴿٦٤﴾

"Waambie, Enyi mliopewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu na wala tusimshirikishe na chochote." (Qur 'an, 3:64)

Tauhidi katika ibada ni msingi imara kwa Waislamu wote, na hapana yeyote aipingaye Tauhidi au kuwa na tofauti ndani yake miongoni mwa vikundi vyote vya Kiislamu, ijapokuwa Mutazilah mtazamo wao juu ya Tauhid ya matendo ya Mwenyezi Mungu unatofauti, na vile vile Ashaira nao wanayo tofauti juu ya Tauhid katika sifa za Mwenyezi Mungu, lakini madhehebu zote za Kiislamu zinaafikiana kuhusu Tauhid ndani ya ibada na hakuna nafasi ya kupinga hilo. Kama kutakuwa na khitilafu, basi ikhtilafu hiyo haiko katika msingi wa Tauhidi ya ibada bali iko katika Misdaaq za Tauhidi ya Ibada. Hii inamaanisha kwamba, baadhi ya Waislamu wanaona kuwa baadhi ya matendo ni ibada na Waislamu wengine wanaona kuwa (matendo hayo) ni Takrima na Taadhima tu na siyo ibada. Na kwa mujibu wa Istilahi ya Elimu ya "Mantik" Tofauti kama hii iko ndani ya 'As-Sughraa" ambayo ni Je, kitendo hiki ni ibada au hapana? Wakati ambapo hakuna tofauti katika 'Al-Kubraa" ambayo ni je, inafaa kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu au hapana? Na hii wameafikiana (Waislamu wote) kwamba haijuzu kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Kwa maneno mengine (Tunaweza kusema) tofauti iliyopo inatokana na Mawahabi kuyazingatia matendo fulani kuwa ni ibada wakati ambapo wasiokuwa wao miongoni mwa Waislamu ulimwenguni kote hawayazingatii kamwe matendo hayo kuwa ni ibada. Hapana budi tuifafanue maana ya "Ibada" kwa mujibu wa lugha na vile vile kwa mjibu wa Qur'an, na hapo ndipo yatakapofahamika matawi ambayo ndani yake imekuja tofauti kuyahusu mwenyewe kwa dhati yake, na ndipo utakapotudhihirikia uhakika na ukweli wa ibada.

TAARIFU KAMILI YA MAANA YA IBADA

Bila shaka maana na Maf-humu ya Ibada iko wazi katika lugha ya Kiarabu, na lau tutakwa hatuwezi kuiarifisha "Ibada" kwa Taarifu ya kimantik kwa kutumia neon moja, basi ni kama mbingu na ardhi ambazo zina maana mbili zilizowazi, wakati ambapo wengi katika sisi hawawezi kutoa taarifu kamili kwa kutumia neon moja lakini hali hii haizuwii kujengeka maana ya ardhi na mbingu katika akili zetu tunapoyasikia matamko hayo. Bila shaka basi, maana ya Ibada ni kama maana ya ardhi na mbingu ambayo inafahamika kwetu sote, pamoja na kutokuweza kuziarifisha mbingu na ardhi kwa taarifu ya kimantiki: Kwa hiyo basi "Ibada" na "Kutukuza" na "Kuheshimu" na "Kukirimu" ni matamko mbali mbali yenye matawi yanayofahamika, na kuyachambua ni jambo rahisi tena jepesi.

Kwa hakika mtu ambaye anampenda yeyote yule kwa mapenzi ya kweli kabisa, utamuona akibusu kutaza nyumba ya mpenzi wake na kunusa mavazi yake na kuyakumbatia kifuani, na atapokufa (mpenzi wake huyu) atalibusu kaburi lake na udongo wa kaburi hilo.... Pamoja na matendo yote haya, hapana yeyote atakayeona kuwa matendo yake huyu mwenye kupenda ni ibada amfanyiayo yule mpenzi wake. Hali hii ni kama ile ya watu kukimbilia kwena kuona miili ya viongozi iliyomo ndani ya majeneza, au kuona kumbukumbu zao na majumba walioyokuwa wakiishi na kusimama dakika chache kuonyesha huzuni kwa ajili ya rohozao yote haya hayazingatiwi kuwa ni ibada katika Taifa lolote miongoni mwa mataifa ulimwenguni, japokuwa mapenzi yao na unyenyekevu wao kwa wato hao uko katika kiwango cha unyenyekevu wa waumini kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hivyo basi, watu wenye maarifa na wachambuzi wa mambo ndiyo ambao wanaweza kupambanua baina ya kuheshimu na ibada. Ewe msomaji mtukufu iwapo tutataka kutoa taarifu ya ibada kimantik, basi ibada itakuwa na taarifu za aina tatu na zote hizi zitalenga maana moja. Ama Mawahabi wao wamechagua Taarifu mbili nyingine na wakazitegemea, lakini zinaupungufu hazikukamilika. Katika maelezo yafuatayo tunazileta hizo Taarifu zao ili tuzijadili.

TAARIFU MBILI PUNGUFU KUHUSU IBADA

Ibada ni kunyenyekea na kudhalilika. Ndani ya vitabu vya lugha Taarifu ya ibada imekuja kwa maana ya kunyenyekea na kudhalilika. Na maana hii imekuja katika Qur'an tukufu lakini Taarifu hii ya Ibada haitoi maana ya ibada kwa undani, na hiyo ni kwa sababu zifuatazo: Ikiwa ibada inakubaliana katika maana na kuwa ni kunyenyekea na kudhalilika, basi haitawezekana kwa mtu yeyote kumzingatia kuwa anampwekesha Mwenyezi Mungu, kwani mtu kwa maumbile yake humnyenyekea Mwalimu wake na mtoto naye huwanyenyekea wazazi wake wawili na kila mpenzi kwa ampendaye. Bila shaka Qur'an Takufu inamuamuru mtu adhalilike kwa wazazi wawili inasema:

وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

"Na wainamishie Bawa Ia udhalili kwa kuwaonea huruma na useme, Mola wangu wahurumie (wazazi) wangu kama walivyonihurumia mimi nilipokuwa mdogo". (Qur'an, 17:24)

Basi iwapo unyenyekevu na udhalili maana yake ni kumfanyia ibada uliyemdhalilikia, basi italazimu kumhukumu ukafiri yeyote anayelea wazazi wake wawili na kinyume chake itakuwa ni lazima kumhukumu kuwa ni mtu wa Tauhidi yule anayewatelekeza wazazi wake na kutowafanyia wema. B: Ibada ni ukomo wa kunyenyekea. Baadhi ya wafasiri walijaribu kuitengeneza na kuirekesbisha Taarifu ya ibada ya kilugha pale walipogundua kuwa inaupungufu wakasema:

"Ibada ni ukomo wa kunyenyekea kwa yule ambaye utukufu wake na ukamilifu wake unafahamika." Taarifu hii inashirikiana na ile ya kwanza katika upungufu na utata. Mwenyezi Mungu anawaamuru Malaika wamsujudie Adam anasema:

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾

"Na kumbuka tulipowaambia Malaika, msujudieni Adam, wakasujudu wote isipokuwa Iblisi". Qur'an, 2:34

Bila shaka kusujudu ndiyo ukomo wa kadhalilika na kunyenyekea kwa yule unayemsujudia, basi ikiwa maana ya ibada ni ukomo wa kunyenyekea italazimu kuwakufurisha Malaika waliotekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na Iblisi kwa kupinga kwake amri ya Mwenyezi Mungu atakuwa ndiyo mwenye imani. Hakika ndugu wa Nabii Yusuf na wazazi wake Nabii Yusuf wote walimsujudia Yusuf kama asemavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى الْعَرْشِ وَخَرُّوا لَهُ سُجَّدًا وَقَالَ يَا أَبَتِ هَـٰذَا تَأْوِيلُ رُؤْيَايَ مِن قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّي حَقًّا ﴿١٠٠﴾

"Na waliporomoka wote kumsujudia, (Naye Yusuf) akasema: Ewe Baba yangu hii ndiyo Tafsiri ya ndoto yangu ya zamani bila shaka Mwenyezi Mungu ameithibitisha". Qur'an, 12:100

Ndoto aliyoiashiria Nabii Yusuf katika Aya hii, hi ile iliyoko katika kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ ﴿٤﴾

"(Kumbuka) Yusuf aliopomwambia Baba yake, Ewe baba yangu hakika nimeona (ndotoni) nyota kumi na moja na jua na mwezi vinanisujudia" (Qur'an, 12:4)

Ni hakika (isiyopingika) kwamba Waislamu wote kwa kufuata mwendo wa Mtume[s.a.w.w] huwa wanalibusu "Hajarul-As-wad". Jiwe jensi lililoko kwenye kona ya Kaaba Tukufu na pia hutaka baraka kwenye jiwe hilo. Kitendo kile kile hufanywa na waabuduo sanamu kwenye masanamu yao jambo ambalo moja kwa moja ni shirki, lakini tendo la Waislamu kwenye Hajarul-As-wad ni tendo la Tauhidi bila shaka yoyote. Kwa hiyo, maana ya ibada siyo ukomo wa kunyenyekea na kudhalilika ingawaje (kunyenyekea na kudhalilika) hakika ni miongoni mwa nguzo za Ibada lakini siyo kwamba hizo ndiyo nguzo pekee za ibada. Hivyo basi, hapana budi pasemwe kuwa, Ibada maana yake ni kunyenyekea na kudhalilika kunakoambatanishwa na itikadi maalum, kitu ambacho kitaifanya ibada iwe imeundika katika misingi miwili.

1. Kunyenyekea na kudhalilika.

2. Itikadi maalum.

Na hii itikadi maalum ndiyo ambayo inaweka msimamo wa kufafanua Qadhiya ya ibada, kwani kunyenyekea japo si sana, ikiwa kutaambatanishwa na itikadi maalum, basi itakuwa ibada. Kwa hakika "Itikadi Maalum" ndiyo inayokivalisha kitendo vazi Ia Ibada, na bila itikadi hiyo maalum ibada haithibitiki japo itadhihirika katika hali ya Ibada.

Na sasa baada ya kuwa tumethibitisha ubatili wa Taarifu mbili ambazo Mawahabi wamezitegemea, na umedhihiri upungufu wake na udhaifu wake, umefika wakati wa kuzungumzia zile Taarifu tatu. Sasa suali ni je, ni nini hiyo "Itikadi maalum" ambayo inaitenganisha ibada na visivyokuwa ibada? Jawabu lake: Kwa hakika ukweli na usahihi, hapa ndipo mahali pa uchambuzi na uhakiki, na jawabu lake litaonekana ndani ya Taarifu tatu zifuatazo:

Taarifu ya Kwanza: Ibada ni kunyenyekea kimatendo au kimatamko, ambako kunatoka ndani ya itikadi ya mtu kwa ajili ya Uluhiyyah (Uungu). Nini maana ya Uluhiyyah nukta hii ni muhimu sana kwa hiyo ni lazima kuieleza.

Jibu: "Uluhiyyah" ni tamko litakanalo na neno "Al-Ilahu" na hilo neno "Al-Ilahu" ndiyo Allah kwa tamko la nakira, (naye ndiyo muumba mtukufu). Na ilivyokuwa neno "Al-llahu" hupata likafasiriwa kwa maana ya mwenye kuabudiwa, basi tafsiri hiyo hiyo ni tafsiri ya kulazimiana, yaani Uluhiyyah unalazimu kuabudiwa siyo kwamba Ilahu maana yake ni mwenye kuabudiwa.

Bila shaka watu wanaoitakidi Ilahu vile vile wanaitakidi kuwepo ulazima wa kumuabudia, sawa sawa ikiwa ni Ilahu wa haki kama alivyo Mwenyezi Mungu au akawa siyo wa haki kama illvyo miungu isiyokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo neno Al-Ilahu hufasiriwa kwa maana ya chenye kuabudiwa kutokana na hali hii tu basi. Dalili iliyowazi kuhusu taarifu hii ni Aya za Qur'an zilizokuja kuzungumzia nyanja hii. Katika mazingatio ndani ya aya hizo inatudhihirikia kwamba "Ibada" na matendo na maneno yanayotokana na Itikadi za Uungu, na kwamba Itikadi hii inapokosekana, basi maana ya Ibada haithibitiki, na ndiyo maana utaiona Qur'an wakati inapoamuru ibada ya Mwenyezi Mungu, basi haraka sana hutoa maelekezo kwamba, hapana mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kwa mfano isema:

"Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu ninyi hamna Mungu ila yeye." Madhumuni ya aya hii yamekuja katika sehemu tisa ndani ya Qur'an au zaidi, nawe msomaji mpendwa unaweza kuzirjea aya hizi katika Surat A'araf aya ya 65, 73 na 58. Pia Surat Huud aya ya 5, 61 na 84, vile vile Surat Anbiyyah aya ya 25, kadhalika Surat Muuminnuna aya ya 23 na 32 na Surat Taha aya ya 14. Ibada zote hizi zinajulisha kwamba, ibada ni kule kunyenyekea na kudhalilika kunakotokana na itikadi ya kuitakidi Uluhiyyah na bila itikadi hii tendo hilo halitaitwa Ibada. Hebu angalia aya zaidi zinazojulisha makusudio hayo. Anasema Mwenyezi Mungu:

إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾

"Hakika wao walipokuwa wakiambiwa, hapana Mungu (Mwingine) ila Mwenyezi Mungu wao Hupinga." Qur'an, 37:35

Ni kwa nini walikuwa wakipinga? Ni kwa sababu wanaitakidi waungu wasio Mwenyezi Mungu na wanawaabudu. Na anasema Mwenyezi Mungu:

أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٣﴾

"Au wanaye Mungu mwingine asiye Mwenyezi Mungu, ametakasika Mwenyezi Mungu kutokana na hao washirikina hao wanaowashirikisha." Qur'an, 52:43.

Qur'an inawazingatia watu hawa kuwa ni washirikina kwa kuwa wanaitakidi uungu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anasema tena Mwenyezi Mungu:

الَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿٩٦﴾

"Wale ambao wanafanya pamoja na Mwenyezi Mungu; Mungu Mwingine basi hivi karibuni watajua." Qur'an , 15:96

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ﴿٦٨﴾

"Na wale ambao hawamuombi mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu..... (Qur'an, 25:68).

Na miongoni mwa aya zinazojulisha kwamba maombi ya Washirikina yalikuwa yakiambatana na itikadi ya uungu kwa masanamu yao ni hizi zifuatazo:

وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لِّيَكُونُوا لَهُمْ عِزًّا ﴿٨١﴾

"Waliwafanya waungu wengine badala ya Mwenyezi Mungu ili wawe wenye nguvu." Qur'an, 19:81.

"Je, ninyi mnashuhudia kwamba kuna waungu wengine pamoja na Mwenyezi Mungu." Qur'an, 6:19

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٧٤﴾

"Na (kumbukeni) Ibrahimu alipomwambia Baba yake Azar. 'Unawafanya Masanamu kuwa ni waungu.'" Qur'an, 6:74

Mazingatio katika aya zinazozungumzia shirki yawatu wanaoabudu sanamu yatatudhihirishia ukweli huu, nao ni kuwa ushirikina wa watu hawa umekuja kwa sababu ya kuitakidi kwao uungu wa masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu, na kwamba masanamu hayo ni miungu wadogo ambao Mungu mkubwa amewapa baadhi ya mambo yanayomstahiki, basi (masanamu hayo) yameumbwa na wakati huo huo yanaabudiwa. Na kwa ajili hii basi walikuwa wakiikataa Tauhidi. Qur'an inasema:

ذَٰلِكُم بِأَنَّهُ إِذَا دُعِيَ اللَّـهُ وَحْدَهُ كَفَرْتُمْ وَإِن يُشْرَكْ بِهِ تُؤْمِنُوا فَالْحُكْمُ لِلَّـهِ الْعَلِيِّ الْكَبِيرِ ﴿١٢﴾

"Hii ni kwa sababu mlikuwa akitajwa Mwenyezi Mungu peke yake mnakanusha, na akishirikishwa mnaamini, basi (leo) hukumu ni yake Mwenyezi Mungu Mtukufu aliye mkuu." Qur'an, 40:12

Na kwa ajili hii mfasiri mkubwa mar-hum Ayatullah Sheikh Muhammad Jawad Al-Balaghi ametoa Taarifu nzuri ya "Ibada" katika tafsiri yake madhubuti iitwayo Aalaur-Rahman anasema: "Ibada: Ni hisia ya unyenyekevu wanayoifanya kwa ajili ya yule wanayemfikiria kuwa ni Mungu wake ili atimize haki yake makususi ya uungu.[167]

Bila shaka marehemu Al-Balaghi ametoa mtazamo wake wa kielimu kutokana na ufahamu wa kimaumbile juu ya neno "Ibada" katika msingi wa tamko, ndipo ilipokuja Taarifu hii inayokubaliana na aya za Qur'an. Taarifu ya Pili ya Ibada: Hakika Ibada ni kunyenyekea mbele ya yule ambaye (Mwenye kunyenyekea) humzingatia kuwa ndiyo Rabbi (Mola). Na tunaweza kuiarifisha ibada kama ifuatavyo; Ibada ni kunyenyekea kimatendo au kimaneno kwa yule anayeitakidiwa kuwa Mola basi kuabudiwa kunalazimiana na kuwa Mola na ikiwa mtu atajiona yeye mwenyewe kuwa ni mja kwa yule anayemuitakidi kuwa ni Mola wake kwa kuumba; sawa sawa Mola huyo akiwa ni kwa hakika au hapana, na akamnyenyekea pamoja na itikadi hii basi atakuwa amemuabudia. Na katika Qur'an Tukufu kuna aya zinazofahamisha kuwa ibada ni miongoni mwa mambo ya umola yaani "Ar-rububiyyah". Hebu ziangalie baadhi ya hizo aya:

وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ﴿٧٢﴾

"Naye Masihi alisema, Enyi wana wa Israeli, mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu". Qur'an, 5:72

إِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٥١﴾

"Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na ni Mola wenu. Basi muabuduni hii ndiyo njia iliyonyooka" Qur'an 3.51

Na aya nyinginezo zaidi ya hizi. Na kuna aya nyingine zinazoizingatia Ibada kuwa ni miongoni mwa mambo ya muumba kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema:

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ﴿١٠٢﴾

"Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu, hakuna anayeabudiwa kwa haki ila yeye muumba wa kila kitu, basi muabuduni." Qur'an 6:102

Ni maana ya neno (Ar-Rabbu)? Neno Rabbu hutumika katika lugha ya Kiarabu kwa yule aliyetegemezewa uangalizi wa kitu fulani na yakaachwa mikononi mwake matokeo au ukomo wa kitu hicho. Basi iwapo neno hili litatumika kwa mtu anayemiliki nyumba na au anayemiliki ngamia au mlezi wa mtoto na mkulima na wengineo, basi hiyo ni kwa sababu wanamiliki kuendesha kitu hicho na kusimamia majukumu yake. Nasi tunapomzingatia Mwenyezi Mungu kuwa ni "Ar- Rabbu" ni kwa sababu mambo yetu na mwisho wetu kama vile mauti, uhai, rizki, afya na uwekaji wa sheria pia msamaha na mambo mengineyo, yote yako mikononi mwake Mwenyezi Mungu Mtukufu. Sasa basi Iau kuna mtu ataitakidi kwamba, moja katika mambo haya au yote, Mwenyezi Mungu amempa mtu fulani (Ayasimamie), basi maana ya itikadi hii ni kwamba kumzingatia huyo mtu kuwa ni "Rabbu" na kumuamini Rabbi huyu na kumnyenyekea itakuwa ni kumuabudia. Kwa maneno mengine tunasema, "Bila shaka ibada inatokana na hisiya za mtu kujiona kuwa yeye ni mja (mtumwa) na hii ndiyo hakika ya ubudiyah, ni ni mtu kuizingatia nafsi yake kuwa amemilikiwa na yuko juu yake aliyemmiliki, kuwepo kwake na kifo chake na uhai na rizki yake na mengineyo. Au kwa uchache akamfanya huyo aliye juu yake kuwa ni mwenye kumiliki uwezo wa kusamehe:

(1) Mwenyezi Mungu Anasema:Nani anayesamehe madhambi isipokuwa ni Mwenyezi Mungu ; 3:135

(2) Mwenyezi Mungu Anasema:Waambie Shafaa ni ya Mwenyezi Mungu ; Az-zumar: 44

(3) Mwenyezi Mungu Anasema:Waliwafanya Makasisi wao na watawa wao kuwa ni Mola badala ya Mwenyezi Mungu, 9:31 Na Shafaa, na kumuwekea Kanuni (za maisha yake) na wajibu mwingineo, basi kwa ajili hiyo atakuwa amemfanya kuwa ni "RABBU" mlezi wake. Kwa hiyo yeyote ambaye atakayeamini na kuitakidi katika nafsi yake (kama tulivyoeleza hapo kabla) na akaifasiri itikadi hiyo kwa maneno na matendo, basi hapana shaka kwamba anamuabudu huyo aliyemzingatia kuwa ni "Rabbu".

TAARIFU YA TATU YA IBADA

Hapa tunaweza kutoa Taarifu hii ya tatu ya ibada inayopatikana kutokana na maumbile na nguvu ya nafsi. Tunasema: "Ibada ni kumnyenyekea yule ambaye tunamzingatia kuwa Mungu na ndiyo asili ya matendo ya kiungu". Hapana shaka kwamba matendo ambayo yanahusiana na ulimwengu, kama vile kusimamia uendeshaji wa ulimwengu na kuhuisha na kufisha na kugawa rizki baina ya viumbe na kusamehe madhambi yote haya yanamuhusu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nawe (msomaji) lau utazizingatia vyema aya za Qur'an zinazozungumzia maelezo tuliyotangulia kuyataja, katika Aya ya 35 Surat Al- Qasa, Aya ya 60 mpaka Aya ya 64 Surat An-Namli Aya ya 5 na ya 6 Sura Az-Zummar. Utaona kwamba Qur'an inasisitiza kwa nguvu sana kuwa matendo haya yanamuhusu Mwenyezi Mungu tu na wala hayamuhusu mwingine asiyekuwa yeye. Hii ni kwa upande mmoja, ama kwa upande wa pili: Sote tunafahamu kwamba ulimwengu wa viumbe ni ulimwengu uliopangwa vyema kabisa, na hakiwezi kutokea kitu isipokuwa sababu ya kutokea kwake itarejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Qur'an Tukufu inaonyesha (ukweli) wa jambo hili. Mwenyezi Mungu anasema:

وَهُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ وَلَهُ اخْتِلَافُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٨٠﴾

"Na ni yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye anayehuisha na kufisha, na mabadiliko ya usiku na mchana yamo katika milki yake." Qur'an, 23:80.

Katika mahala pengine Mwenyezi Mungu anasema kwamba miongoni mwa Malaika wapo wanaosimamia utoaji wa Roho. Nayo ni kauli yake isemayo:

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ ﴿٦١﴾

"Hata pale mmoja wenu anapofikiwa na mauti wajumbe wetu humfisha." Qur'an, 6:61

Kwa kuijengea hali hii, inawezekana kuzikusanya aya hizi mbili na tukasema kama ifuatavyo: "Bila shaka hizi sababu zinazosababisha pia matendo ya ulimwenguni, kama yatakuwa ni ya kimaumbile ya kawaida au kimaana kama vile Malaika, basi iwe iwavyo yanathibitika kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu naye ndiye mtendaji halisi." Kwa maneno mengine ni kwamba, kitendo cha watendaji hawa wawili (Mwenyezi Mungu na Malaika) ni kitendo kimoja tu na si vitendo viwili lakini mtendaji wa kwanza anafanya kwa uwe wake na yule wa pili anamfuatia yule wa kwanza (kutekeleza maamrisho yake).

Maana hii ni miongoni mwa maarifa ya juu katika Qur'an ambayo hufahamika kwa kuzirejea aya za Qur'an zinazozungumzia matendo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Sasa basi ikiwa mtu ataitakidi kwamba Mwenyezi Mungu amewapa baadhi ya viumbe wake kama vile, Malaika na Mawalii matendo yake ya kuruzuku, na kuhuisha na yasiyokuwa hayo, na akaammi pia kuwa viumbe hao ndiyo wanaoendesha mambo ya ulimwengu na kuyasimamia mambo yake na akaona kuwa Mwenyezi Mungu hahusiki tena kwenye matendo hayo kiasi kwamba itikadi hiyo ikampelekea kuwanyenyekea viumbe hawa, basi hapana shaka yoyote kwamba unyenyekevu wake huu ni ibada na tendo hili ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa maneno mengine tunasema: "Lau mtu ataitakidi kwamba Mwenyezi Mungu ameukabidhi ustahiki wa kutekeleza matendo kwa Malaika na Mawalii, na Mwenyezi Mungu akawa amebaki hana ustahiki wote wote (katika matendo hayo) na hao Malaika na Mawalii wanayafanya matendo hayo bila kumtegemea Mwenyezi Mungu na bila idhini yake, basi mtu huyu aliyeitakidi itikadi hii, hakika amemfanyia Mwenyezi Mungu mshirika na amemfananisha (Na viumbe vyake). Hapana shaka kwamba itikadi kama hii ndiyo kuishirikisha dhati ya Mwenyezi Mungu na kutawas-sal na kunyenyekea kunakotokana na itikadi hii ni ibada kama ilivyokuja katika Qur'an Tukufu.

Anasema Mwenyezi Mungu:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ﴿١٦٥﴾

"Na miongoni mwa watu wako wanaofanya waungu badala ya Mwenyezi Mungu, na wanawapenda kama (anavyostahiki) kupendwa Mwenyezi Mungu". Qur'an, 2:165

Kwa hakika chochote chenye kuwa na kuwepo hakiwezi kuwa mfano wa Mwenyezi Mungu au mshiriki isipokuwa kitakapokuwa na uwezo wa kuuendesha ulimwengu kwa matakwa yake binafsi bila ya matakwa ya Mwenyezi Mungu lakini hakuna yeyote mwenye uweza huo. Bali kila kilichopo ni chenye kunyenyekea mbele ya matakwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kitake au kisitake basi kwa hiyo hakiwezi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu bali kitakuwa kitiifu kwake kutenda kama atakavyo yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ukweli halisi in kuwa, washirikina walikuwa wakiitakidi kwamba, masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu yanajitegemea katika kunendesha ulimwengu huu na pia katika mambo ya uungu.

Na katika zama za Jahiliya (kabla kuja Uislamu) kulikuwa na ushirikina wa namna mbali mbali na ushirikina wa daraja ya chini kabisa ilikuwa ni itikadi ya Mayahudi na Wakristo kwamba mapadri na Makasisi wao wanayo madaraka ya uwekaji wa kanuni na sheria kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾

"Waliwafanya wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni waungu wao kinyume cha Mwenyezi Mungu". Qur 'an, 2:31

Kadhalika washirikina walikuwa wakiitakidi kwamba, ustahiki wa Shafaa na Maghfira (mambo ambayo yanamstahiki Mwenyezi Mungu tu) vimekabidhiwa kwa Masanamu yao wanayoyaabudu, na masanamu hayo yanafanya mambo hayo yenyewe kikamilifu kwa kujitegemea katika ustahiki huo. Na kwa ajili hii utaona aya nyingi za Qur'an zinazozungumzia Shafaa zinasisitiza kwamba Shafaa haithibitiki ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu asemavyo ndani ya Qur'an:

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ﴿٢٥٥﴾

"Na ni nani huyo awezaye kushufaiya (kuombea) mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini yake." Qur 'an, 2:255

Na lau washirikina wangekuwa wanaitakidi kwamba, masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu yanauwezo wa kushufaiya kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, basi usingeona Qur'an inakanusha moja kwa moja Shafaa bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya wanafalsafa wa Kiyunani walikuwa wamejenga ndani ya fikra zao Miungu wengi kwa kila jambo miongoni mwa mambo ya ulimwenguni. (Kwa mfano) mvua ina Mungu wake, mimea ina mungu wake, mtu ana Mungu wake na mambo mengine (kila moja lina mungu wake). Na walikuwa wakidai kwamba utendaji wa kuendesha mambo ya ulimwengu ambao unamuhusu Mwenyezi Mungu peke yake, umekabidhiwa kwa miungu hawa. Na katika zama za Jahiliya, baadhi ya Waarabu walikuwa wakiabudu Malaika na nyota zitembeazo na zile zisizotembea hali ya kuwa wakidhani kwamba usimamizi wa mambo ya ulimwengu na watu umekabidhiwa kwa vitu hivyo, navyo ndivyo vinavyotenda kikamilifu kwa kujitegemea na hiyari kamili, na kuwa Mwenyezi Mungu ameuzuliwa na hana uwezo wowote juu ya mambo haya kabisa (ametakasika Mwenyezi Mungu na fikra hizi sana sana).[168]

Na kwa hiyo basi kila aina ya unyenyekevu utaofanywa kwa Malaika na nyota utazingatiwa kuwa ni ibada kwa kuwa unatokana na itikadi hii yenye makosa. Kuna baadhi ya Waarabu wengine wa zama za Jahiliyyah, hawakuyaitakidi masanamu yaliyochongwa kwa miti na madini kuwa ni Miungu na kwamba ndiyo yaliyowaumba wala kusimamia mambo ya ulimwengu na watu, bali wao walikuwa wakiyaamini kuwa yanao uwezo wa kuwaombea na walikuwa wakisema: "Masanamu haya ni waombezi wetu mbele ya Mwenyezi Mungu".[169] Na kwa msingi wa mtazamo huu batili, walikuwa wakiyaabudu Masanamu haya kwa lengo la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na walikuwa wakisema wamasema:

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ ﴿٣﴾

"Sisi hatuyaabudu (Masanamu) isipokuwa kwa ajili ya kutukurubisha kwa Mwenyezi Mungu." Qur 'an, 39:3

Kwa kifupi tunasema: "Bila shaka tendo lolote litokanalo na itikadi hii na likajulisha kufuata na kunyenyekea basi ni ibada, na kinyume chake ni kuwa tendo lolote ambalo halikutegemezewa itikadi kama hii haliwezi kuzingatiwa kuwa ni ibada wala shirki."

Lau mtu atanyenyekea mbele ya mtu na akamuheshimu na kumtukuza bila ya kuamini itikadi kama hii, basi tendo hili halitachukuliwa kuwa ni shirki wala ibada hata kama tendo hilo litakakadiriwa kuwa ni haramu.

Kwa mfano: Haitazingatiwa kuwa ni ibada sijda ya mpenzi kwa mpenzi wake, wala mwenye kuamriwa kumsujudia aliyemuamuru na mke kumsujudia mume pamoja na kwamba Sijda kumsujudia asiye Mwenyezi Mungu ni haramu kisheria, kwani Sijda ni Makhsusi kwa Mwenyezi Mungu peke yake wala hairuhisiwi kwa yeyote yule kafanyiwa japo itakuwa ni kwa sura ya dhahiri isiyokuwa na itikaadi isipokuwa kama Mwenyezi Mungu ataamuru kufanywa kwa sijida hiyo (kwa asiye Mwenyezi Mungu).