UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 50939
Pakua: 5274

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 50939 / Pakua: 5274
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

18

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KUWAOMBA MSAADA MAWALII WA MWENYEZI MUNGU

Je, inafaa kuwaita Mawalii wa Mwenyezi Mungu kuwaomba msaada wakati wa shida na matatizo? Mas-ala haya ni miongoni mwa Mas-ala ambayo kuna tofauti ndani yake baina ya Waislamu na Mawahabi. Kuwaomba msaada Manabii na Mawalii wa Mwenyezi Mungu, na pia kuwaita kwa majina yao wakati wa shida, matatizo na mambo ya hatari ni sunna iliyojengeka miongoni mwa Waislamu. Basi, ni sawa sawa kuwaomba msaada huo kwenye makaburi yao matukufu au sehemu nyingine yoyote ile na wala hawaoni ubaya wowote katika kuomba msaada wa aina hii wala siyo shirki na wala si kinyume cha dini. Wakati Mawahabi wanalipinga jambo hili kwa bidii zote, Waislamu hawaoni ubaya wa kulitenda wala siyo shirki ndani ya uombaji huu wala siyo kinyume cha dini. Mawahabi hawa kila wafanyapo upinzani wao dhidi ya mas-ala haya wanatumia baadhi ya aya za Qur'an ambazo kamwe hazina uhusiano wowote na mas-ala haya, isipokuwa lengo lao ni kuuchanganya uovu wao huo na haki. Aya wazitumiazo ni kama hii ifuatayo: Mwenyezi Mungu amesema:

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا ﴿١٨﴾

"Na kwa hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu". Qur'an, 72:18.

Ewe msomaji mpendwa, ili uweze kuzifahamu aya za Qur'an ambazo Mawahabi wanazitolea ushahidi kutilia nguvu maoni yao ya kipekee, tunazileta hapa aya hizo kwa ajili ya kufanya utafiti na uchunguzi ili uweze kufahamu tafsiri yake sahihi "Insha-Allah". Na kwa hiyo basi sisi tunawajibu kwa Qur'an hii hii ambayo wao wanadai kuwa ndiyo wanayoitolea ushahidi kabla ya kitu kingine chochote. Baadhi ya aya hizo tunazitaja kama ifuatavyo:

لَهُ دَعْوَةُ الْحَقِّ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيْءٍ ﴿١٤﴾

"Kwake ndiko yaliko (maitikio ya) maombi ya haki, na wale wawaombao asiyekuwa yeye hawatawaitikia kwa chochote". Qur'an, 13:14.

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ ﴿١٩٧﴾

"Na wale mnaowaita badala yake, hawawezi kukusaidieni wala hawawezi kujisaidia nafsi zao". Qur'an, 7:197

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾

"Na wale mnaowaita kinyume chake, hawamiliki japo utando wa kokwa ya tende." Qur'an, 35:13

إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ﴿١٩٤﴾

"Na wale mnaowaita kinyume cha Mwenyezi Mungu (wao) ni waja kama ninyi". Qur'an, 7:194.

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾

"Waambie, waiteni wale mnaodai (kuwa ni Miungu) kinyume chake (Mwenyezi Mungu) hawawezi kukuondoleeni matatizo wala kubadilisha (chochote). Qur'an, 17:56

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ ﴿٥٧﴾

"Hao wanaowaita wao (wenyewe) wanatafuta (njia) ya ukaribiano na Mola wao". Qur'an, 17:57

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ﴿١٠٦﴾

"Wala usikiite (chochote) kinyume cha Mwenyezi Mungu, ambacho hakikunufaishi wala kukudhuru". Qur'an, 10:106

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ ﴿١٤﴾

"Kama mkiwaomba (masanamu hao) hawasikii wito wenu: Qur'an, 35:14

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ﴿٥﴾

"Ni nani mpotevu mkubwa kuliko yule anayemuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye hatamjibu mpaka siku ya Qiyama?" Qur'an, 46:5

Kwa kutumia aya hizi, Mawahabi wanazitolea ushahidi kuharamisha kuomba msaada kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na pia kuwaita baada ya kufa kwao, na (wanasema) kwamba, kufanya hivyo ni kuwaabudia Mawalii hao na ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Wanasema Mawahabi, "Kama mtu atasema kwenye kaburi la Mtume[s.a.w.w] au akawa sehemu nyingine akasema, "Ewe Muhammad". Basi atakuwa amemuabudu (Mtume) kwa wito huu alio mwita na dua hii. Wahabi aitwaye As-San-Ani anasema: "Bila shaka Mwenyezi Mungu ameiita dua kuwa ni ibada pale aliposema, "Niombeni nitakuitikieni, kwa hakika wale wanaopinga ibada yangu...." Basi yeyote atakayeliita jina la Mtume fulani au Mcha mungu fulani kwa kutaka kitu fulani (kwa Nabii au Mchamungu huyo) au akasema (Ewe Nabii) niombee kwa Mwenyezi Mungu katika shida yangu au akasema, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu katika shida yangu, au akasema, (Ewe Nabii) nilipie deni langu, niponye ugonjwa wangu na mengineyo mfano wa haya, basi atakuwa amemuomba Nabii huyo au Mchamungu huyo wakati dua ni Ibada, na zaidi ya hapo (dua) ndiyo roho ya ibada, hivyo amemuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu na amekuwa mshirikina, kwani tauhidi haitimii isipokuwa kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uungu kwa kuitakidi kuwa hakuna muumba wala mwenye kutoa riziki isipokuwa yeye, na pia kumpwekesha katika ibada kwa kutokumuabudu asiyekuwa yeye japo kwa baadhi ya ibada, na wale waabuduo sanamu walikuwa washirikina kwa kutompwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada."[230]

Jibu Lake: Miongoni mwa mambo yasiyokuwa na shaka ndani yake ni kwamba, tamko "Dua" katika lugha ya Kiarabu maana yake ni wito, na huenda pia likatumika kwa maana ya ibada, isipokuwa tu haiwezekani kwa namna yoyote ile matamko ya dua na ibada kuwa na maana moja. Haiwezekani kusema kuwa "Kila dua ni Ibada" kutokana na sababu zifuatazo:

1. Bila shaka Qur'an imelitumia tamko la dua mahala pengi na haiwekani kusema kuwa makusudio yake yalikuwa ni ibada, kwa mfano: Mwenyezi Mungu anasema:

قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا ﴿٥﴾

"(Nuhu) akasema, Ee Mola wangu hakika nimewalingania (yaani Daawtu) watu wangu usiku na mchana". Qur'an: Nuh: Aya ya 5

Hivi kweli inakubalika kusema kwamba Nabii Nuh[a.s] kwa maneno yake hayo alikusudia kwamba yeye amewaabudu watu wake usika na mchana? Hebu soma kauli ya Mwenyezi Mungu akimnukuu Ibilisi atapokuwa akiwaambia wenye dhambi siku ya Qiyama:

وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ﴿٢٢﴾

"Wala sikuwa na mamlaka juu yenu (ya kukulazimisheni mnifuate) isipokuwa nilikwiteni (yaani Daawtukum) nanyi mkaniitikia". Qur'an, 14:22 Je, kuna yeyote atakayepelekea (mawazo yake) kwamba, maana ya wito (yaani dua) wa shetani kwa watu wenye dhambi unamaanisha kuwa shetani aliwaabudu wata hao? Pamoja na hali hii tunafahamu kwamba, kama ibada ikithibitika basi ibada hiyo itatoka kwa watu hao wenye madhambi kumuabudia shetani na siyo shetani kuwaabudia wao. Ndani ya aya hizi mbili na zingine zinazofanana na hizi, tamko "Aad-Daawah" limekuja siyo kwa maana ya ibada, kwa ajili hiyo basi haiwezekani kusema kuwa dua na ibada ni matamko mawili yenye maana moja, wala haiwezekani kusema kwamba yeyote mwenye kumuita mmoja wa Manabii au Mawalii basi atakuwa kamuabudia na amemshirikisha Mwenyezi Mungu hapana sivyo kabisa, kwani mwito na dua yana maana pana zaidi kuliko ibada na mengineyo.

2. Maana ya dua katika aya walizotolea ushahidi Mawahabi haina mama ya wito tu, bali ni wito ambao uko katika maana ya ibada, kwa kuwa aya zote hizi zilishuka kuwahusu wafanyao ibada ya masanamu, ambao walikuwa wakiyaitakidi masanamu yao kuwa ni mungu wadogo waliopewa jukumu Ia (kusimamia) baadhi ya mambo ya ulimwengu, na miungu hao wanaouwezo wa kuendesha (mambo ya ulimwengu).

Zaidi ya hapo ni kwamba, dua na mwito kwa masanamu haya sawa sawa kama yatakuwa ni miungu wakubwa au wadogo, kuitakidi kuwa yanamiliki uwezo wa kushufaiya na maghfira ni kuyaabudu na ni shirki. Dalili iliyo wazi mno juu ya kwamba waabudu sanamu walikuwa wakiyaita masanamu yao kwa kuitakidi kuwa hayo ni miungu ni hii kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

فَمَا أَغْنَتْ عَنْهُمْ آلِهَتُهُمُ الَّتِي يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ﴿١٠١﴾

"Haikuwafaa kitu miungu waliyokuwa wakiita kinyume cha Mwenyezi Mungu". Qur'an, 11:101.

Kwa hiyo basi aya zilizotajwa (Na Mawahabi) hazina kabisa uhusiano kati yake na mas-ala haya, kwa kuwa mas-ala haya yanachunguza juu ya uwezekano wa mtu kumuomba msaada mtu mwingine bila ya kumuitakidi kuwa ni mungu wala kumuitakidi kuwa na uwezo wa kujitegemea na kumiliki uendeshaji wa mambo ya ulimwengu wala dunia wala akhera isipokuwa (anaombwa msaada huo hali ya) kuzingatiwa kuwa ni mja mwema mwenye cheo mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Utume au Uimamu, na Mwenyezi Mungu ameahidi kukubali maombi ya mja huyu mwema kwa amuombeaye kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿٦٤﴾

"Lau wao waliopojidhulumu nafsi zao wangekujia na wakamuomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mtume naye akawaombea msamaha, wangemkuta Mwenyezi Mungu ni mwenye kukubali toba Mwenye huruma". Qur'an, 4:64.

3. Bila shaka aya zilizotolewa na Mawahabi kama ushahidi zinaonyesha kuwa Makusudio ya neno "Dua" yanamaanisha maana ya "Ibada" nasiyo kinyume cha hivyo. Hebu fanya mazingatio ya kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ ﴿٦٠﴾

"Na Mola wenu anasema, niombeni nitakujibuni, kwa hakika wale wanaojivuna kufanya ibada yangu, bila shaka wataingia motoni wadhalilike." Qur'an, 40:60.

Bila shaka Mwenyezi Mungu amelitaja jambo la "Ud-uuni" kisha akalifuatisha tamko la Ibada yangu, "ibaadati" jambo ambalo linajulisha wazi kwamba, makusudio ya "Niombeni (Ud-uuni)" katika aya hii ni ibada ya Mwenyezi Mungu na (kunatakiwa) kuacha ibada isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, na hii inaonyesha kuwa washirikina walikuwa wakijivuna kufanya dua na ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu." Mjukuu wa Mtume[s.a.w.w] , al-Imam Zainul-Abidin[a.s] anasema katika moja ya dua zake: "Dua ya (kukuomba) wewe umeiita kuwa ni ibada, na kuiacha umekuita ni kujivuna na umeonya kwa kuiacha (kutasababisha) kuingia motoni katika hali ya kudhalilika. " [231] [233] Katika Qur'an kuna aya mbili zilizokuja zikiwa na maana moja, mojawapo limetumika tamko 'Al-Ibadah" na ya pili limetumika tamko 'Ad-Daawa". Aya ya kwanza Mwenyezi Mungu Anasema:

قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا﴿٧٦﴾

"Waambie, Mnawabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu ambao hawamiliki dhara wala manufaa"? Qur'an, 5:76

Ya pili kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

قُلْ أَنَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا ﴿٧١﴾

"Waambie, Je, tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye hatatunufaisha wala kutudhuru"? Qur'an, 6:71. Pia Mwenyezi Mungu Anasema:

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾

"Na wale muwaombao hawamilki japo utando wa kokwa ya tende". Qur'an, 35:13

Ndani ya aya hii imekuja kwa tamko "Mnaomba," yaani "Tad 'uuna" na humo mna dalili iliyo wazi kabisa kwamba, ombi hili 'Ad Daawah" ni la kuwaomba masanamu, na hiyo ndiyo iliyokuwa itikadi ya washirikina, wakiitakidi kuwa masanamu ni Miungu inayodhuru na kunufaisha kinyume cha Mwenyezi Mungu na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawakosoa kwa kuwaambia kuwa (Masanamu) hayo "Hayamiliki japo utando wa kokwa ya tende." Maana kama hii imekuja katika aya inayofanana kwa tamko la "Ta'abuduna" kama ilivyo kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا ﴿١٧﴾

"Bila shaka hao mnaowaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu hawana mamlaka ya riziki zenu". Qur'an, 29:17.

Na ndani ya aya nyingine yamekuja maneno mawili yenye kulingana kwa maana moja. Mwenyezi Mungu anasema:

قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ﴿٥٦﴾

"Waambie, Mimi nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaita kinyume cha Mwenyezi Mungu". Qur'an, 6:56.

Na karibu na maana ya aya hii ni aya ya 66 Sura ya 40.

Ewe msomaji mpendwa nakutarajia kuwa utairejea al-Mujamul-Mufahras Li alfaadhil-Qur'an il-Karim katika madda ya "Abada, ameabudu" na "Daa, ameomba" ili upate kuona kwa macho yako ni namna gani tamko la ibada lilivyokuja katika aya fulani na pia tamko la "Ad daawat" na "Ad duaa" yalivyokuja katika aya nyingine. Utaona kuwa matamko hayo katika namna hizo mbili yamekuja kwa maana na madhumuni ya namna moja yaani ibada, jambo ambalo ni dalili iliyo wazi kuonyesha kuwa makusudio ya "Ad Daawat" na "Ad Duaa" katika aya hizi ni ibada na kwamba aya hizi hazihusiki na mwito peke yake. Basi utakapozifanyia mazingatio aya ambazo zimeambatana na tamko "Ad Duaa" na "Ad Daawat" kwa maana ya ibada, utaona kuwa aya hizo zinazungumzia mapambano kati ya imani na kufru, na pia baina ya ibada ya Mwenyezi Mungu, Tauhidi, imani ya uungu wake dhidi ya ibada ya masanamu na itikadi za (kuyapa) uwezo wa kumiliki riziki, maghfira, shafaa, kunufaisha na kudhuru.

Hivyo basi, Mawahabi kutoa ushahidi kwa aya hizi ili kuharamisha kuwaita Manabii na Mawalii na kutaka kwao msaada, ni jambo linalopelekea kushangaza na kustaajabisha hasa inapoonekana kuwa aya walizotolea ushahidi hazina uhusiano wowote na mas-ala haya. Kifupi tu, kwa yale yaliyothibiti ndani ya utafiti huu ni kuwa: Kauli yako utaposema, "Yaa Ali" hali ya kuwa unakusudia kumsemesha Khalifa wa Mtume [s] au ukasema, "Ya Husain" au "Ya Zahraa" au ukataja jina jingine la mmoja miongoni mwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu waliotakasika hakuna tatizo kabisa kwa kusema hivyo, bali ni namna ya kuomba msaada kwao, Mwenyezi Mungu awateremshie Rehma wote. Basi jambo hili ni zuri linalofaa kufanywa, na humsaidia mtu kujinasua toka kwenye matatizo na shida na kumuokoa kutokana na maangamizi na kisha kumpa faraja.

HIJJA - MSIMU WA IBADA NA NI MKUTANO WA KISIASA

Mwenyezi Mungu ameifanya al-Kaaba kuwa ni nyumba tukufu na ni wasila wa kusimamisha amani miongoni mwa watu, na akaifanya Hijja kuwa ni msimu wa ibada na ni fursa ya Waislamu kutoka kila upande kukutana na kufahamiana, na pia wafahamishane mambo muhimu ya Dini yao na kuzichunguza hali zao. Basi mambo haya baada ya Ibada ni miongoni mwa uthibitisho dhahiri wa kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

"Na ili washuhudie manufaa yao " Qur'an, 22:28. Basi ni manufaa yepi makubwa baada ya ibada kuliko Waislamu kukutana mahala pamoja ambapo wameacha kila hisia ya dhati na jamii na mipaka ya kitaifa na kimataifa na rangi, bali Waislamu wote hufunikwa na kivuli cha Dini na kupambwa na hisiya za upendo pia moyo wa udugu wa kweli? Na ni mas-ala gani muhimu kuliko Waislamu kufahamishana hatari na matatizo yaliyowazunguka, na wakaeleweshana namna ya kuyatatua kwa pamoja na kwa nguvu moja na azma ya pamoja ili kuyaondoa au kupunguza uzito wake?

Na Je, Ni tatizo gani kubwa zaidi linalowakandamiza Waislamu leo hii kuliko tatizo la ukoloni wenye aina tofauti ambao umezikalia nchi za Waislamu kijeshi, au kuzitawala kisiasa au kizipiga vita kitaaluma na kisha kuupora uchumi wa Waislamu na kueneza fitna miongoni mwao na kuwauwa watoto wao na kuwaharibu (kitabia) vijana wa Kiislamu, na, na, na, na......!!! Je, siyo kwamba Hijja ndiyo mahali bora pa kutangazia uchungu wa Waislamu wote dhidi ya ukoloni huu mbaya unaongozwa na Amerika na Urusi? Na kama Waislamu wenye kudhulumiwa na kutawaliwa katika nchi zao hawawezi kutangaza uchungu wao na chuki yao dhidi ya wakoloni wakiwa ndani ya kitovu cha nchi zao kwa kuwa tu kuna serikali zinazotumiwa kuwaziba vinywa na kunyamazisha sauti zao, basi Hijja haiwi ndiyo fursa inayofaa mno kutangaza uchungu wao na chuki zao bega kwa bega, Waislamu wote wakiwa katika ibada unyenyekevu na kutubia (kwa Mwenyezi Mungu)? Je, kuwapinga mabeberu ambao kuwatii hukmu zao na kukubaliana nao na pia kuwategemea ni miongoni mwa shirki katika twa'a ya Mwenyezi Mungu? Je, kuwapinga mabeberu siyo miongoni mwa aina dhahiri mno za tauhidi ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya Hijja iwe ndiyo kielelezo chake na uthibitisho wa ukweli wake?

Na kwa hakika leo hii Waislamu wameutambua ukweli huu pamoja na kukua kwa harakati za Kiislamu na kuongezeka kwa jamii ya Kiislamu. Waislamu wamekwisha tambua kwamba Hijja ndipo mahali panapofaa na ni fursa inayofaa kuwaunganisha Waislamu na kuwazindua, kisha kawatambulisha ukweli wa matukio ya kusikitisha ambayo yanatendwa na maadui wa Uislamu, (ambao ni) Amerika, Urusi, Ufaransa, Uingereza na wengineo miongoni mwa tawala za kikoloni na kibeberu. Kwa hakika Waislamu wamekwisha fahamu kwamba, Hijja ndiyo fursa nzuri ya kutangaza uchungu wa Waislamu bega kwa bega kutokana na ukoloni muovu pamoja na kufanya ibada na kutubu kwa kufuata kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

"Ili washuhudie manufaa yao na wamtaje Mwenyezi Mungu ". Qur'an, 22:28 Kauli hii (ya Mwenyezi Mungu) inaashiria falsafa ya Hijja inayochanganya ibada na siyasa na malengo yake ya kidunia na akhera. Na kwa ajili hii ndiyo maana kumekuweko mshikamano mkubwa wa kisiasa ambao Waislamu wameuanzisha katika siku za Hijja kwa miaka kadhaa wakiongozwa na Waislamu wa Iran.

Lakini kwa huzuni kubwa tunakuta baadhi ya watu wanaodai kuwa na elimu na wanakalia vyeo vya uenezaji wa Uislamu, wanapinga kwa nguvu harakati hizi tukufu, na wanapinga hatua hizi zenye athari (nzuri) ambazo hazilengi ila kuwakomboa wenye kunyimwa na kudhulumiwa (haki zao) (pia harakati hizi zinalenga) kuutokomeza ukoloni na utumwa. (Watu hao wapingao wanapinga) hali ya kuwa kila sika wanasikia habari za mauaji na uchinjaji wa mamilioni ya vijana wa umma wa Kiislamu huko India, Palestina, Lebanon na Afghanistan, Eritrea na katika mipaka ya Iraq na Iran na kwingineko. Na mauaji hayo moja kwa moja yanatokana na sababu zinazosababishwa na ukoloni. Watu hawa badala ya kuunganisha sauti zao na sauti za Waislamu wengine wanaopinga matendo ya ukoloni ambao kwa uovu wake unapokonya haki za Uislamu na Waislamu, tunawakuta wananyanyua sauti zao upande wa ukoloni dhidi ya Waislamu, na wanapinga chuki na hasira za Waislamu dhidi ya ukoloni mamboleo wa Kimarekani, Urusi, Uingereza na Ufaransa ambao mikono yao imelowana kwa damu ya Waislamu na majumba yao yamejengwa kwa mafuvu ya watoto wa Kiislamu. Cha ajabu zaidi kuliko hili, ni kule kushikilia kwao kuharamisha hatua hizi tukufu (za kupinga wakokoni kwenye Hijja) kwa kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema;

"Hapana kusema maneno machafu wala kufanya vitendo vichafu wala asibishane katika Hijja. " Qur'an, 2:197

Huyo ni Sheikh Abdallah al-Khayyat ambaye ni Imam na ni Khatibu wa msikiti Mtukufu wa Maka. Yeye ameona kuwa, kuyaeleza matatizo ya kisiasa ya Waislamu katika msimu wa Hijja ni kutoka nje ya lengo la Hijja, na akatoa dalili ya madai yake kwa kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema:

فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ﴿١٩٧﴾

"Basi yeyote aliyekusudia kufanya Hijja, asiseme maneno machafu wala kufanya vitendo vichafu, wala asibishane katika hiyo Hijja." Qur'an, 2:197.

Na akasema tena Sheikh Khayyat, "Na kama alivyoikusudia Mtume[s.a.w.w] Ibada ya Hijja pale aliposema, "Yeyote mwenye kuhiji na akawa hakusema maneno machafu wala hakutenda matendo machafu hurejea kama siku aliyozaliwa na mama yake". Anaendelea kusema Sheikh Abdallah al-Khayyat, "Ama wito wa Iran ya Khomein ambao anataka kuigeuza Hijja kuwa ni matangazo ya kisiasa na maandamano ya kudai (haki) na kupinga Serikali, mambo hayo hayakubaliki namna yafanyikavyo na pia madhumuni yake, kwani yanapingana na mafunzo ya Dini yetu tukufu na yanatoka nje ya maana yake na misingi yake bora, kwa kuwa yanavunja moja ya nguzo miongoni mwa nguzo (za Dini)."

"Ndani yake mna uvunjaji wa heshima ya vitu vitukufu vya Mwenyezi Mungu na kuna kiburi dhidi ya mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu na pia kwenda kinyume cha mwelekeo alioelekeza Mwenyezi Mungu." "Anaendelea kusema: "Bila shaka mwito wa Iran ya Khomein unaeneza fitna na kubomoa umoja na kubadilisha upendo kuwa chuki na kuzigeuza sehemu takatifu kuwa nyanja za kutangaza mambo ya siasa na kueneza miito isiyokuwa na maana. Hapana Muislamu yeyote ulimwenguni isipokuwa anapinga wito huu, kwani ndani yake kuna mambo yanayopinga Uislamu na kuvunja heshima ya alama za Kiislamu. Na Hijja haiwezekani kuwa isipokuwa ni mkutano wa kiroho na ni mkusanyiko wa kila mwaka ambao Waislamu toka kila shemu za mbali hukusanyika".[232] Bila shaka yaliyomo ndani ya khutba hii (iliyotangulia) ndiyo maneno ambayo tunayasikia (kila mara) kutoka kwa watu wanaoajiriwa na Suudiya, kila mwaka tunayasikia, na katika kila hotuba na kila muhutubiaji (anayasema), basi wao hawakiuki zaidi ya kusoma aya hiyohiyo na kufuata vile alivyosoma khatibu huyo maneno ambayo ni matupu.

Na sisi hapa hatutamkabili Sheikh isipokuwa kwa njia aliyotuamuru Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema, "Jadiliana nao kwa njia iliyo njema", hivyo basi tunaifafanua maana ya aya hiyo na kuiweka wazi ili makusudio yake yaeleweke na watu wote wajue kwamba maandamano ya kisiasa na kutangaza kujitenga na makafiri na kuyatokomeza matendo yao yanayoupinga Uislamu na Waislamu, na kuwaita Waislamu kwenye umoja ambao ndiyo nguzo ya maandamano aliyoyaamrisha Imam Khomeini siyo uthibitisho wa mabishano yaliyotajwa katika aya hiyo. Hebu iangalie tafsiri ya aya hiyo na ufafanuzi wa makusudio yaliyomo. Amesema Mwenyezi Mungu,

لْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ﴿١٩٧﴾

"Hijja ni miezi maalum, basi yeyote anayekusudia kufanya Hijja katika miezi hiyo, asiseme maneno machafu wala asifanye matendo machafu na wala asibishane katika Hijja". Qur'an, 2:197.

1. Bila shaka kukaririka kwa tamko la "Hijja" mara tatu katika aya hii, imeweka neno dhahiri badala ya dhamiri, hata hivyo hapa ni ufupisho kwani makusudio ya Hijja ya kwanza ni kutaja "wakati wa kufanya Hijja" na ile ya pili ina maana ya "tendo lenyewe la Hijja" na ile ya tatu inakusudia wakati na mahala pa kufanyia Hijja", na Iau siyo kudhihirisha (tamko la) Hijja ingekuwa hapana budi kuleta "It-Nab Ghair lazim" (Ufafanuzi usiyo wa lazima). Amesema ndani ya tafsiri aI-Manar ya Rashid Ridhaa: "Bila shaka miongoni mwa "Balaghatul-Iijaz" katika aya hii ni kule kuweka dhahiri mahala pa kuweka dhamiri kwa kuitaja Hijja mara tutu, ya kwanza ikiwa na maana ya kipindi cha Hijja kama wasemavyo "Baridi ni miezi miwili", na ya pili maana yake ni ile Hijja yenyewe ambayo ni Ibada, na ya tutu makusanya kipindi cha kutekeleza na mahala pake ambapo ni ardhi tukufu ya msikiti wa Maka nasehemu zinazofuatia kama vile Arafa".[233]

2. Makusudio ya kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema: "Yeyote anayekusudia kufanya Hijja katika miezi hiyo" Yami ameilazimisha nafsi yake kuanza Hijja kwa nia ya makusuduio ya ndani (ya moyo) na kuhirimia kwa kutenda dhahiri na kuitikia kwa kutamka labbaika.[234]

3. Iliyo Mash-huri ni kwamba maana ya neno "Ar-Rafathu" ni "kuingilia", imepokewa kwa Abdallah bin Omar na Tauus na Atwa'a na wengineo kuwa, "Ar-Rafathu" ni kutusemesha mwanamke kwa maneno machafu au uchafu kwa jumla, na imesemwa vinginevyo pia.[235]

4. Na wamelifasiri neno "Fusuuq" kuwa ni maasi yote, amesema Ibn Zaidi na Malik "Al-Fusuuq" ni kuchinja kwa ajili ya masanamu, na Adhahak amesema "Al-Fusuuq" ni kuitana (kuaibishana) kwa majina mabaya, na amesema Ibn Omar, "Al-Fusuuq" ni "Kutukana". Na kauli ya mwanzo ndiyo sahihi zaidi kwani inakusanya kauli zote. Na imepokewa kwa Mtume[s.a.w.w] kwamba amesema, "Atakayehiji ikawa hakusema maneno machafu wala kufanya matendo mabaya hurejea kama siku aliyozaliwa na mama yake". "Na Hijja iliyotekelezwa vyema haina malipo isipokuwa pepo". Amepokea hadithi hizi Muslim na wengineo.

5. "Jidala" katika maana ya kilugha ni mabishano, uhasama na ugomvi. Na uhasama umeitwa kuwa ni mjadala kwa kuwa kila mmoja hutaka kumgeuza mwenziwe kutoka kwenye rai yake. La muhimu mahala hapa ni kuifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo kuwa, "Na asibishane katika Hijja" na pia kubainisha makusudio yake. (Kauli hii ya Mwenyezi Mungu) kwa watu wanaoajiriwa na Suudiya wanaifanya kuwa ndiyo dalili ya kuharamisha maandamano na utoaji wa hotuba za kisiasa na miito ya umoja na kudhihirisha kujitenga na makafiri na wanafiki.

Wala hakiwezi kubainika kiwango cha dalili ya aya hii kama waionavyo watu hawa, isipokuwa ni kunakili maoni ya uwezekano wa namna ya kuifasiri aya hii kama yalivyotajwa na wafasiri wakubwa kama ifuatavyo:

A. Maoni aliyoyataja Qadhi al-Baidhawi na ar-Razi naye ameegama kwa Baidhawi, kwa kuichukulia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "La Rafatha Wala Fusuqa Fil-Hajji Wala Jidalafil Haji" kuwa ni "Khabar" maelezo ambayo maana yake ni kwamba, "Hijja haiwezi kuthibiti (ikitendwa) pamoja na mojawapo ya mipaka hii, bali itaharibika kwa kuwa ni kama kufanya kinyume chake, na mambo hayo yanazuwia kusihi kwa Hijja. Kwa hiyo basi matamko hayo matatu ni lazima yachukulike kuwa ni yenye kuharibu Hijja na muradi wake ni vitendo vinavyoharibu Hijja na yanawajibisha kulipa Qadha mwakani iwapo Hijja hii ilikuwa ni wajibu.

Basi "Ar-Rafathu" hufasirika kwa maana ya "Kuingilia" na "Al-Fusuqu" kwa maana ya "Kuzini" kwa sababu vitendo hivi vinaharibu Hijja, na jidala huchukuliwa kwa maana ya kuitilia Hijja juu ya kuwa kwake ni wajibu na kusihi kwake kisheria na kuwa kwake ni tendo linalokubaliana na akili.[236] Kwa kifupi, bila shaka kilicho dhahiri ni kule kuwepo kinyume kati ya mambo haya na Hijja ambayo Mwenyezi Mungu ameamuru mwanzoni na kwa msingi huo basi, kama ambavyo haiwezekani kuchukulia neno "Fusuqu" katika maana ya lugha kwani siyo kila "Fusuqu" huharibu Hijja kama vile uongo na kuteta, vile vile haiwezekani kuchukulia neno "Jidala" katika maana ya kila ubishi kwani siyo kila ubishi unaharibu Hijja, bali muradi wake ni mabishano maalum ambayo hayawezi kukusanyika pamoja na Hijja kama vile kutia shaka uwajibu wa Hijja na kusihi kwake kisheria na kuona kuwa ni upuuzi kule kutufu jiwe, udongo na ubao - al-Kaaba.

Maana hii ndiyo aliyoichagua Qadhi (al-Baidhawi) na akaiunga mkono Ar-Razi katika tafsiri yake, na (maana hii) ndiyo chaguo la wanachuoni wengi ndani ya sentensi nyingi (zilizokuja namna hii) kama vile: "La Salata ila Bifatihatil-Kitabi" Yaani, hakuna Sala ila kwa (kusoma) "Suratil-Fatiha". Au "La Salata ila Bitahurin" Yaani, hakuna Sala ila kwa Tahara." Na makusudio yake ni kukanusha kusihi (kwa Sala) bila ya vitu hivyo viwili, na kwamba kuthibiti kwa Sala kumetegemea vitu hivyo, kama ambavyo makusudio ya aya ile vile vile ni kukanusha kusihi kwa Hijja (ikitendwa) pamoja na mambo hayo matatu. Basi iwapo uwezekano huo utasihi, haitafaa kuitolea dalili kwa namna waionayo hawa (wanaofadhiliwa na Suudiya) kwa kuharamisha kila majadiliano ikiwa ni pamoja na maandamano, kwani makusudio ya aya ni kubainisha uharamu wa majadiliano ambayo hayaafikiani na kusihi kwa Hijja, na makusidio (ya aya) siyokubainisha uharamu wa kila mjadala japokuwa unaafikiana na usahihi wa Hijja. Hata kama tukikubali kwamba Jidala na maandamano juu ya kuyakadiria ni haramu lakini haiharibu Hijja.

B. Kutenganisha kati ya mambo haya matatu kwa kuyachukulia yale mawili ya mwanzo kuwa ni katazo, japokuwa itakuwa ni kwa kulihalifu dhahiri ya tamko yaani "La Tar-Fathuu Wala Tufsiquu" (msitoe maneno machafu wala vitendo vichafu) na kulichukulia lile jambo la tatu kuwa ni "Khabari" yaani, hapana mjadala wala kwenda kinyume ndani ya wakati wa Hija na sehemu ya (kufanyikia) Hijja, kwa msingi huu basi, makusudio itakuwa, "Hapana mjadala wala kwenda kinyume ndani ya kipindi cha Hijja na mahali panapofanyikia Hijja, na maana hii ndiyo ambayo ameishikilia Ibn Jariri at-Tabari ndani ya Tafsiri yake.[237] Na ameitaja pia Az-Zamakh-Shari:[238] Na wote wawili wametoa ushahidi kwa namna mbili: Ya Kwanza: Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] amesema: "Yeyote atakaye Hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu akawa hakusema maneno machafu wala kufanya matendo mabaya hurejea katika hali yake kama siku aliyozaliwa na mama yake". Na wala (Mtume) hakusema "Wala hakufanya mjadala". Kwa msingi huu kuna dalili kwamba yale mambo mawili ya mwanzo yana maana ya makatazo ya kusema machafu na kutenda mabaya, wala hakuna katazo kwa lile la tatu, vinginevyo lingefuatishwa kwa hayo mawili kwa namna ya katazo, isipokuwa (hili la tutu) lina maana ya kutoa khabari na kukanusha kuwepo mjadala na kubishana katika kipindi cha Hijja na mahali pa Hijja.

Kwa hiyo kutokana na pande hizi mbili (yaani mahala na wakati) inajulikana wazi kuwa hapastahiki kutiliwa mashaka wala wasi wasi. Ya Pili: Hakika Maquraishi walikuwa wakiwakhalifu Waarabu wengine, wao husimama Mash-Aril-Haram na Waarabu wengine husimama Arafah, na walikuwa mwaka mwingine wakiiwahisha Hijja na mwaka mwingine wakiichelewsha na hiyo ndiyo "An-Nasii". Basi Hijja ikarejeshwa kwenye wakati mmoja na Wuquuf ikarudishwa Arafah, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza kwamba "Hakika tofauti imeondoka katika Hijja" na Mwenyezi Mungu akaieleza "An-Nasii" kuwa ni kuzidi katika kufru, inawapotosha waliokufuru wanahalalisha mwaka fulani na wanaiharamisha mwaka mwingine. Naam, Hijja ilirejea kwenye wakati wake na mahala pake katika Hijja ya kuaga, Mtume[s.a.w.w] alisema, "Bila shaka wakati umerejea kama ulivyokuwa siku iliyoumbwa mbingu na ardhi". Naye Qur-tubi amesema maana yake ni kuwa, "Suala Ia Hijja limerejea kama lilivyokuwa, yaani limerejea kwenye siku yake na wakati wake".

Na amesema Mtume[s.a.w.w] alipohiji yakuwa "Chukueni Ibada zenu kutoka kwangu " akabainisha visimamo vya Hijja na mahala pake. [239] Basi kama tukikubali maana hii kauli ya Mwenyezi Mungu haitakuwa na mafungamano yoyote na maoni ya huyu khatibu al-Khayyat, kwani kauli hiyo haina maana ya katazo ili iwe Taklifu II-zami inayokusanya aina yoyote ya mjadala, isipokuwa hiyo ni jumla Khabariyah na hii khabari inaeleza mambo ya kimaumbile. Kwa hakika baada ya matendo ya Mtume[s.a.w.w] na kuweka kwake mipaka ya visimamo na Mash-Ari na kuithibitisha katika mwezi maalum, Hijja imekuwa kama jua la mchana, basi haiwezi kukurubiwa na shaka kuhusu wakati wake na mahali pake, basi maneno haya yana uhusiano gani wa kuharamisha mjadala na kuharamisha maandamano ya kisiasa hata kama tutasema kwamba maandamano ya kisiasa yanaingia katika maana ya mjadala. Amesema Ibn Jariri: Kauli zinazostaajabisha mno kwangu mimi kuhusu jambo hilo, iwapo litakuwa kama nilivyoeleza kwamba, kisomo cha atakayesoma, "Falaa Rafathun Wala Fusuqun Wala Jidala FilHaj" kwa kuitia Raf-u Rafathu na Fusuqu na kuzitia Tan-win zote hizo mbili, na kuitia Fataha jidala bila ya Tan-wini, kisomo ambacho ni cha watu wa Basra na watu wengi wa Maka akiwemo Abdallah bin Kathiri, na Ibn Amri bin Al-Ula.[240] Na bila shaka yamerufaishwa matamko mawili ya mwanzo na likanasibishwa la tatu kwa kuyachukulia yale matamko mawili ya mwanzo kwa maana ya makatazo, na ikawa kama kwamba pamesemwa kwa mkazo pasiwepo maneno machafu na wala matendo mabaya, na la tatu kwa maana ya kueleza kukanushwa kwa mjadala ikawa kama kwamba pamesemwa, hapana shaka wala kutofautiana katika Hijja, yaani ndani ya kipindi chake na mahali pake. Ya Tatu: Ni kauli iliyoteuliwa na wafasiri wengi, nayo ni kuichukua nafyi (kanusho) na kulipeleka kwenye makatazo, na lengo liwe ni kukataza mambo yote matatu, na katika kipindi hiki (ifanywapo namna hii) ndipo anapokanganyika mtoaji wa dalili, kwa kuwa dhahiri ya aya inakataza mjadala wowote ule ikiwa ni pamoja na maandamano ya kisiasa.

Lakini ni lazima kwa mtu anayetaka kupata ukweli atulizane kidogo ili yambainike mambo mawili:

1. Jidala, inagawika kwenye haramu, mubaha na mustahabbu sasa basi kilichokatazwa ni jidala (mjadala) wa aina yeyote au ni ule unaohusu sehemu ya kwanza (yaani mjadala ulio haramu) na kama mjadala huo utakuwa haramu katika nyakati zingine basi haipingiki kuwa ni haramu katika Hijja vile vile na inakuwa mkazo zaidi uharamu wake katika Hijja.

2. Bila shaka maandamano ya kisiasa na kutoa hotuba na kuwazindua Waislamu kutokana na kujisahau kwao, na kudhihirisha kujitenga na maadui zao wa mashariki na magharibi, Je, hayo ni katika aina za "Jidala" na ndiyo milango yake au hayana kabisa mahusiano nayo? Hebu angalia ufafanuzi wa mambo mawili: Bila shaka makusudio ya "Jidala" Ni kubishana ambako ni lazima kuepukwa katika Hijja na kwingineko, lakini katika Hijja ndiyo muhimu zaidi kuepuka. Amesema Zamakhshari: "Wala Jidala, Yaani hapana mabishano na marafiki na watumishi wa wenye kuajiriwa, na imeamuriwa kujiepusha na ubishani na ni wajibu kujiepusha nao kwa hali yoyote ile, kwani katika Hijja ni kubaya nino (kubishana) kama vile kuvaa nguo ya hariri katika Sala na kujitingisha tingisha wakati wa kusoma Qur'an."[241] .

Na amesema ndani ya Tafsir Al-Manaar kwamba, "Al-Jidalu, ni kubishana na kukhasimiana (kugombana) basi yote haya yaliyokatazwa yanakuwa ni mafunzo ya ulimi (namna ya kuzungumza) na ni wajibu kwa mtu anapokuwa katika ibada na mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, awe mwenye ukamilifu wa adabu na mazingira bora".[242] Al-Jas-Sas amesema: Al-Jidal ni Mabishano, na Ibn Abbas amesema, Al-Jidal ni kumjadili mwenzio mpaka ukamkasirisha, kisha akasema, hakika aliyehirimia amekatazwa kutukana na kubishana katika miezi ya Hijja na katika miezi mingine, na amekatazwa matendo mabaya japokuwa matendo hayo ni haramu hata kabla ya kuhirimia, basi Mwenyezi Mungu ameyataja uharamu wake wakati wa kuhirimia ili kuonyesha ubaya zaidi kutokana na utukufu wa Ih-ram, na hasa kwa kuwa kufanya maasi katika hali ya kuwa ndani ya Ih-ram kuna adhabu kubwa zaidi kuliko katika wakati mwingine.[243] Na kinachoweka bayana zaidi ni kule kuikutanisha "Jidala" na "Fusuqu" kwani kunaonyesha kuwa, mambo haya mawili yanatokana na asili moja ya jinsi moja, basi haifai kukusanya jidala kwa ujumla, (yaani) Jidala Mubaha au Mustahabu katika sheria. Na ndani ya sheria ya Kiislamu kuna aina za majadiliano mbayo ni Mubaha na zaidi ya hapo kuna ambayo ni mustahabbu na aya ile haihusiki nayo. Ama Jidala (majadiliano) ambayo ni Mubah miongoni mwake ni yale yaliyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿١﴾

"Bila shaka Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya mwanamke ambaye anajadiliana nawe kuhusu mumewe, na anashitakia mbele ya Mwenyezi Mungu" Qur'an, 58:1.

Lau litawafika jambo kama hili katika Hijja haliwezi kuwa haramu si kwa msemaji wala kwa msikilizaji. Kinachojulisha hapa ni kwamba, makusudio ya Jidala ni majadiliano na mabishano yaliyokatazwa ambayo ni lazima kujiepusha nayo, nao wameyafasiri majadiliano ndani ya aya hiyo kuwa ni mambo yote yasiyotokana na mjadala na ubishi uliokatazwa. Amesema Ar-Razi: "Wafasiri wametaja namna nyingi kuhusu mahali hapa:

1. Mjadala unaohofiwa kuleta matusi na kukadhibishana na kupeana sifa ya ujinga.

2. Amesema Muhammad bin Kaab Al-Quradhi, "Hakika Maquraish walikuwa wakikusanyika Mina na kuambizana, "Hijja yetu imetimia" Na wengine husema, "Sisi yetu ndiyo iliyotimia", Basi Mwenyezi Mungu akawakataza kufanya hivyo".

3. Malik amesema katika Muwatta, "Jidala katika Hijja, (maana yake) ni kwamba Maquraishi walikuwa wakifanya wuqufu kwenye Mash-Aril-Haram katika Muzd-alifa Mahala paitwapo Qaza na wengine hufanya wuquf Arafa, na walikuwa wakibishana hawa husema "Sisi ni sahihi zaidi" Na hawa nao husema "Sisi ndiyo sahihi zaidi", Mwenyezi Mungu akasema:

لِّكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا هُمْ نَاسِكُوهُ فَلَا يُنَازِعُنَّكَ فِي الْأَمْرِ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ إِنَّكَ لَعَلَىٰ هُدًى مُّسْتَقِيمٍ ﴿٦٧﴾ وَإِن جَادَلُوكَ فَقُلِ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٦٨﴾

"Kila umma tumeujalia ibada wanayoishika, basi wasishindane nawe katika jambo hili, walinganie watu kwa Mola wako, bila shaka wewe uko katika uongofu ulio sawa kabisa, na kama wakiendelea kukujadili basi waambie Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayoyatenda". Qur'an, 22:67-68

Malik amesema haya ndiyo majadiliano (yaliyoharamishwa katika aya hii).

4. Amesema Qasim bin Muhammad "Majadiliano katika Hijja ni wengine kusema, "Hijja nileo" na wengine weseme, "Hijja ni kesho" na hiyo ni kwa kuwa walikuwa wameamrishwa kuweka hesabu ya miezi kwa kuonekana mwezi.

5. Amesema Al-Qaffaal: "Katazo linaingia kutokana na mambo ambayo walimjadili Mtume[s.a.w.w] alipowaamuru kubadilisha Hijja na kufanya Umra tamatui wakaona vibaya kufanya hivyo, na wakasema, Je, tutakwenda Mina hali yakuwa tupu zetu zinadondosha manii? Mtume[s.a.w.w] akasema, kama ningelijuwa mwanzoni kitu nilichoamuriwa sasa hivi nisingeleta pamoja nami wanyama wa kuchinja, na ningelifanya umra tamatui, basi baada yake wakuacha mjadala.

6. Amesema Abdur-Rahman bin Zaid: "Mabishano yao katika Hijja ni kwa sababu ya kuhitilafiana kwao kuhusu nani kati yao ambaye Hijja inafanana nmo na Hijja ya Nabii Ibrahim[a.s] ?

7. Wao walikuwa wakitofautiana katika miaka, wakaambiwa hapana kujadiliana kuhusu wakati wa Hijja kwani nyakati zimerejea kama ilivyokuwa wakati wa Ibrahim[a.s] . Basi huu ni mkusanyiko wa yale waliyoyasema wafasiri katika mlango huu.[244] Mifano hii inajulisha kuwa makusidio ya majadiliano ndani ya aya hiyo, ni majadiliano yaliyokatazwa sawa yakiwa yamekatazwa katazo Ia kuharamisha au katazo la karaha. Na imekuja katika kitabu kiitwacho Al-Fiqhi Alal Madhahibil-Arbaa, kwamba "Ni haramu kutoka katika taa (kumtii) Mwenyezi Mungu tendo lolote la haramu japo litakuwa tendo hilo limeharamishwa mahala pasipokuwa pa Hijja, isipokuwa kunatiwa mkazo zaidi katika tendo hilo wakati wa Hijja, na ni haramu kugombana na marafiki na watumishi na mfano wa hao kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema, "Yeyote atakayekusudia Hijja, basi asiseme maneno machafu, wala asitende matendo mabaya wala asijadiliane katika Hijja", na Jidala (maana yake) ni kukhasimiana.[245]

Na kwa msingi huu basi, majadiliano ambayo ni Mubah na kupingana bila ya kuzusha ghadhabu kwa mwingine ni kama majadiliano yaliyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema, "Bila shaka Mwenyezi Mungu ameisikia kauli ya mwanamke anayejadiliana nawe kuhusu mumewe na anashitakia kwa Mwenyezi Mungu". Majadiliano hayo yako nje ya mtiririko wa aya hiyo, na lau yule mwanamke anayeshitakia angekuwa katika hali ya Ihram na angelipeleka mashitaka yake kwa Mtume[s.a.w.w] na kutaka haki yake toka kwa mumewe, hiyo isingehesabiwa kuwa ni majadiliano haramu na kugombana kuliko kuchukiwa bali itahesabiwa kuwa huyu anafuta haki kwa njia iliyo sahihi.

Wafasiri wamesimulia kwamba, kuna mwanamke wa Kiansari ambaye baada ya mumewe kumfanyia dhihari alikwenda kwa Mtume[s.a.w.w] akasema, "Hakika mume wangu aliniowa nikiwa bado kijana tena najitosha kwa mali na jamaa, alipokwisha kula mali yangu na kuumaliza ujana wangu na jamaa zangu kutawanyika na umri wangu kuwa mkubwa amenifanyia dhihari...." Na mengine aliyoyataja. Ikiwa Jidala iliyo Mubaha iko nje ya aya hiyo basi mjadala ambao ni mustahabbu unayo haki zaidi kutoka kuliko hii, na kwa nini isiwe hivyo wakati Mwenyezi Mungu amemuamuru Mtume wake katika kitabu chake kufanya mjadala uliyo Mandub. Lau wakati wa Hijja yatatolewa Mas-ala ya Kifiq-hi au Akida au Tafsiri na kila mmoja akatowa Maoni yake na mwingine akamjadili kwa njia nzuri, basi haitakuwa haramu jambo hilo, bali litakuwa ni kutekeleza kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ﴿١٢٥﴾

"Waite watu katika njia ya Mola wako kwa hekima na Mawaidha mema na ujadiliane nao kwa namna iliyo nzuri". Qur'an, 16:125

Na lau utatokea uchambuzi katika mahema ya Arafah kuhusu Mas-ala ya Kifiqhi au Akida kisha mmoja wa Waislamu akashika msimamo wake maalum na kutetea itikadi yake kwa dalili na hoja, bila ya kuonyesha uhasama au ubishi au jeuri, hapana shaka kwamba jambo hilo linafaa, na wala halitahesabiwa kuwa ni kuingia kwenye mjadala uliokatazwa na aya hiyo. Maelezo yote yaliyotangulia ndiyo msimamo ulivyo kwa Ahli-Sunna, ama kwa upande wa msimamo wa watu wa nyumba ya Mtume[s.a.w.w] ambao wako sambamba na Qur'an na ni wenza wa Qur'an kwa mujibu wa kauli ya Mtume[s.a.w.w] , wao wanafasiri "Jidala" iliyotajwa katika aya kuwa ni kauli ya mtu atakaposema La Wallah, Wallah (Nime....) Na (akasema) Balaa Wallah..... Ikiwa ataapa viapo vitatu vya kweli mfululizo basi huyo amefanya "Jidala" na anawajibika achinje, na akiapa kiapo kimoja cha uongo (Pia) atakuwa kafanya "Jidala" na anawajibika kuchinja. [246]

Basi uko wapi uharamu wa kuharamisha kila aina ya "Jidala" wanaoudai watu hawa? Na kilicho haramu kwa mujibu wa riwaya zao ni mabishano "Jidala" Maalum kama ulivyokwisha fahamu (hapo kabla). Hebu tukadirie kwamba aya inakusanya majadiliano ya aina zote, yale yaliyo haramishwa katika wakati usio wa Hijja na yale ya Mubaha na Mandubu yote hata kama tutakubali hivyo basi makusudio ni mjadala baina ya Haji na Haji mwingine. Ama mjadala wa Haji na watu walioko katika haram (ya Maka), na ama yale maandamano yanayofanywa na Mahuhjaji wa Kiislamu na kutangaza kujitenga kwao na makafiri na kukemea matendo yao ya uadui kwa Waislamu na Uislamu, na (ama) kuwaita Waislamu kwenye umoja miongoni mwao ili kuzikabili hatari na ushindani, yote hayo asilani hakuna cho chote cha mabishano. Hapana chochote katika mkusanyiko huo isipokuwa ni (kuonyesha) umoja wa Waislamu na hapana yeyote miongoni mwa makafiri na wanafiki anayekabiliana nao (wakati huo kwenye Hijja) mpaka (Eti) isababishe kuzuka kwa majadiliano kati ya pande mbili hizo.

Hebu angalia, hivi je, inahesabiwa kuwa kitendo alichokifanya Imam Ali[a.s] alipowasomea makafiri aya zilizoko katika Surat Al-Baraat katika msimu wa Hijja kwa amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (kitendo hicho kinaitwa) kuwa ni majadiliano? "Jidala Fil-Hajj"? Au ni tangazo la Mwenyezi Mungu na Mtume wake kujitenga na makafiri na washirikina? Na iko wapi basi tofauti kati ya misimamo hii miwili? Bila shaka maandamano wanayoyafanya Waislamu wanaokwenda Kuhiji wakati wa Hijja kwa amri ya Imam Khomeni "Mwenyezi Mungu amrehemu" si kwa maana nyingine ila ni kutekeleza kwa vitendo na kuyathibitisha maelekezo yaliyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema:

أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ﴿٢٩﴾

"(Waislamu) ni wakakamavu dhidi ya makafiri na ni wenye kuhurumiana wao kwa wao". Qur'an, 48:29

Naam, bila shaka watawala wa Suudiya ndiyo wanaoleta mazingira ya Jidala iliyokatazwa kwa kuwa wao ndiyo wanaowazuwiya Waislamu kutangaza chuki zao dhidi ya makafiri, na kuonyesha chuki zao kwa matendo yao maovu. Kuwa wanawazuia Waislamu wasitekeleze wajibu wao wa Kiislamu, na wanawalazimisha Waislamu wasiwahoji (watawala hao) na kuwajadili, basi watawala wa Suudiya ndiyo mjadala na ndiyo sababu ya jidala (mabishano). Basi Iau ingetolewa fursa ya Mahujaji wote wakaafikiana juu ya umuhimu wa kushirikiana katika maandamano haya yanayopinga matendo ya makafiri na uovu wa Walahidi, haitakuwepo tofauti miongoni mwa Mahujaji (kuhusu jambo hili) isipokuwa kile wanachokichochea watawala wa kizazi cha Suud. Mwisho tunamuuliza Khayyaat: Yeye anasema katika Khutba yake kuwa "Hijja ni mkutano wa kila mwaka ambao Waislamu hukusanyika kutoka sehemu mbali mbali". Basi ikiwa Hijja ni kama adaivyo yeye, Je, ni Mas-ala gani miongoni mwa Mas-ala yanayopasa kutolewa katika mkutano huu?

Je, inapasa kuzungumza maneno madogo madogo kama vile ukaraha wa kula kitunguu maji na kitunguu thaum kwa mtu atakaye kuingia msikitini au kuzungumzia kukosha nyayo na viatu kutokana na udongo na jasho kama ambavyo tumekuwa tukisikia mara nyingi (maneno hayo) toka kwa Makhatibu wa msikiti mtukufu wa Makka katika siku za Hijja na katika Sala za Jamaa, kama kwamba hakuna mambo mengine ya Kiislamu (yanayopaswa kuzungumzwa) isipokuwa haya. Utakapo kubainikia ewe msomaji ubatili wa yale aliyoyasema Khayyat, na pia ubatili wa ushahidi wake, bali kutokuwepo kwa maungamano ya aya (aliyoitowa) na Qadhiya hii (ya maandamano kwenye Hijja) basi inapasa tuwe na msimamo wa pamoja juu ya (kuifahamu) falsafa (Hekima) ya Hijja ya kweli kwa namna ya uchambuzi kwa mujibu wa aya za Qur'an na hadithi tukufu na pia matukio ya kihistoria na sera za waliotangulia. Na sasa hebu tazama maelezo haya yafuatayo kwa ujumla.