UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI13%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 52158 / Pakua: 5895
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

IBNU TAYMIYYAH NI NANI?

Bwana huyu alikuwa hi miongoni mwa wanachuoni wa Kihanbal, na alifariki mwaka 728 A.H. Jina lake ni Abu'l-'Abbas Ahmad bin 'Abdul-Halim, anayejulikana sana kwa jina la Ibnu Taymiyyah. Kutokana na rai zake mbovu, na fikra zake zilizo kinyume na itikadi za Waislamu (pamoja na kuwepo tofauti ya kimadhehebu baina yao) Wanachuohi wa zama zake walikuwa wakimpinga na kutangaza vita dhidi yake, isitoshe walimhukumu kuwa hi fasiki (mharibifu wa Dini) na hasa pale alipoandika vitabu vinavyoeleza itikadi zake na akavisambaza miongonini mwa watu. Vita vya kidini dhidi ya Ibnu Taymiyyah vilikuwa katika pande mbili muhimu: Kwanza: Utunzi wa vitabu kupinga fikra zake potofu na kuzitengua kwa mujibu wa Qur'an na Sunna Tukufu ya Mtume[s.a.w.w] . Kwa mfano, tunataja baadhi ya vitabu vilivyotungwa na kutolewa dhidi ya Ibnu Taimiyyah:

1). Shifa's-Saqam Fi Ziyarati Qabril-Imam: kimeandikwa na Taqiyu'd Din Subaki.

2). Ad-Durrah Al-Mudiyyah Fi 'r-Raddi Ala Ibni Taimiyyah: kimeandikwa na mtunzi wa kile cha kwanza.

3). Al-Maqalatu'l-Mardiyyah: kimetungwa na Qadi'l-Qudat Al-Malikiyyah Taqiyu'd-Din Abi 'Abdillah Al-Akhnai.

4) Najmu'l-Muhtadi wa Rajmul-Muqtadi, kilichoandikwa na Fakhr bin Muhammad Al-Qurashi.

5). Daf'us'h-Shubhah, kimeandikwa na Taqiyu'd-Din Al-Hisni.

6). At-Tuhfatu'l-Mukhtarah Fi'r Raddi Ala Munkiri'z-Ziyarah, kimeandikwa na Taju'd-Din.

Hivi ni baadhi ya vitabu vilivyoandikwa dhidi ya itikadi na rai mbovu za lbn Taimiyyah, na vilidhihirisha ubovu wa itikadi hizo pamoja na ubaya wake.

Upande wa pili kuhusu vita dhidi ya Ibn Taimiyyah, ni hujuma dhidi yake zilizokuwa zikifanywa na wanachuoni wa zama zake, ikiwa na pamoja na kutoa Fatwa kuwa yeye Ibn Taimiyyah hi fasiki, na wakati mwingine walimhukumu kuwa ni kafiri, pia wakiwatahadharisha watu juu ya uzushi aliouzusha katika dini tukufu ya Kiislamu. Miongoni mwa Wanachuoni hao ni Qadi 'l-Qudat Al-Badru ibn Jama'ah wa Misri, yeye aliandikiwa suala kuhusu rai ya Ibn Taimiyyah juu ya kufanya ziyara ya kumzuru Mtume[s.a.w.w] kuwa haifai. Qadi huyu aliandika jawabu lifuatalo: "Kwa hakika kumzuru Mtume[s.a.w.w] ni jambo la Sunna iliyosisitizwa, na wanachuoni wameafikiana katika jambo hili; na yeyote anayeona kuwa kumzuru Mtume ni haramu, ni wajibu juu ya Wanachuoni kumkemea na kumkataza aondokane na mawazo ya aina hii; na iwapo hataachana na mawazo hayo, basi itakuwa ni lazima kumfunga na kumfedhehesha mbele za watu ili wasimfuate".

Qadi huyu wa Kishafi'i wa Misri siyo yeye peke yake aliyetoa Fatwa ya aina hii, bali Maqadhi wa Madhehebu ya Maliki na Hanbal nao walitoa Fatwa zinazofanana katika kuonyesha uovu wa Ibn Taimiyyah na wakahukumu kuwa yeye ni mpotevu. Katika kutilia nguvu maelezo yaliyotangulia hivi punde, mwanachuoni aitwaye Adh-Dhahabi ambaye anazingatiwa kuwa miongoni mwa wanachuoni wakubwa katika Karne ya Nane Hijiriyya (alitunga vitabu vingi vya maana mno katika hadithi na wapokezi wa hadithi, na aliishi katika zama zile zile za Ibn Taimiyyah) alimuandikia Ibn Taimiyyah barua ya nasaha, akamkataza mambo yake hayo mabaya na alimfananisha (kutokana na uovu wake huo) kwa Al-Hajjaj Ath-Thaqafi katika uovu na upotevu wake.[27]

U'ipofikamwaka 728 Hijiriyya Ibn Taimiyyah alifariki katika gereza Ia Shamu, na mwanafunzi wake aitwaye Ibn Al-Qayyim akajaribu kuendeleza mwenendo wa mwalimu wake lakini hakufaulu. Jambo la kuhuzunisha sana ni kwamba, shetani aliutega mtego wake kwa mara nyingine alipokuja Muhammad ibn AbdulWahab, hali ya kuwa amezibeba fikra za Ibn Taimiyyah zilizokuwa zimetoweka, akaafikiana yeye na kizazi cha Wasaudi kwamba, kila mmoja amsaidie mwenziwe, mmoja ashike mambo ya utawala na mwingine ashike mambo ya dini. Basi kipindi hiki upotovu ukawa umerudi na kueneza mizizi yake katika nchi ya Najdi, hivyo basi Uwahabi ukaenea katika nchi hiyo mfano wa maradhi mabaya ya Kansa katika mwili.

Watu wengi walihadaika na wakuanzisha kundi lao; inasikitisha sana kusema kwamba walitumia nembo ya Tauhidi ili kuwaua watu wa Tauhidi, na walimwaga damu za Waislamu kwa madai ya kuwapiga vita washirikina. Maelfu ya watu, wanaume na wanawake, wakubwa kwa wadogo, walijitolea muhanga dhidi ya uzushi huu. Kwa hiyo mfarakano baina ya Waislamu ulipanuka; na likaongezeka dhehebu jipya kwenye madhehebu mengi ya Kiislamu yaliyokuwepo hapo kabla. Na msiba huu mkubwa ulifikia kilele chake wakati miji miwili mitukufu ya Makka na Madina ilipoangukia mikononi mwa kundi hili ovu Ia Kiwahabi. Hivyo basi, Mawahabi kutoka Najdi walijiimarisha kwa kupewa msaada na Serikali ya Uingereza ambayo kwa chuki yake dhidi ya Uislamu, sika zote ilikuwa ikikusudia kuigawa dola ya Kiislamu (iliyokuwa chini ya ukhalifa wa Kiturki), na kuifanya kuwa vijidola vidogo vidogo ambavyo vitatenganishwa na mipaka ya kijiografia. Mawahabi walikusudia kuondoa kumbukumbu zote za Kiislamu zilizokuwepo Makka na Madina, na kuyabomoa makaburi ya Mawalli wa Mwenyezi Mungu na kukiondolea heshima kizazi cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, pamoja na mambo mengine maovu na machafu (waliyoyatenda Mawahabi) ambayo hutetemesha nafsi ya Muislamu.

Baadhi ya wanahistoria wanasema: "Jambo la kwanza walilolifanya Mawahabi haraka haraka baada ya kuiteka Makka ni kuchukua na shoka na kuibomoa Mualla (makaburi ya Maqureish) ambapo palikuwa na qubba nyingi za watukufa wa Kiislamu. Miongoni mwa Maqubba hayo lilikuwa ni qubba la Sayyidina Abdul-Mutalib ambaye ni babu yake Mtume[s.a.w.w] , na qubba Ia Sayyidina Abu Talib (r.a.) ami yake Mtume, pia qubba la Bibi Khadija (r.a) mkewe Mtume[s.a.w.w] . Vile vile walibomoa jengo alimozaliwa Mtume[s.a.w.w] , na lile la Abubakr na mahala alipozaliwa Imam Ali [a.s] , na wakabomoa Qubba la Zam-zam lililokuwa pembeni ya Al-Ka'bah; pia walifuatilia kila mahali zilipo kumbukumbu za watu wema wakazibomoa". "Wakati wakibomoa walikuwa wakiimba na kupiga ngoma na kuyashutumu makaburi... kiasi yasemekana kwamba baadhi yao walilikojolea kaburi la Bwana Mpendwa.....!![28]

Amesema mwanachuoni mkubwa aitwaye As-Sayyid Sadru'd-Din As-Sadr (Mwenyezi Mungu amrehemu) kwamba: "Naapa kwa 'umri wangu kwa hakika tukio la (kubomolewa makaburi ya) Baqii' huzifanya kuwa kongwe nyoyo za watoto wachanga." "Huenda (tukio hili) likawa ndiyo mwanzo wa kufikwa na misiba (mfululizo) ikiwa (waislamu) hawatazinduliwa kutoka katika usingizi (walionao)". "Je, hayuko Muislamu awezaye kuzichunga haki za Mtume, aliye kiongozi na muombezi wetu (kwa ajili ya Mwenyezi Mungu)?" Amesema msha'iri mwingine: "Wameangamia wajukuu wa Mayahudi (yaani kizazi cha Saudi) kwa matendo waliyoyatenda, hawakupata isipokuwa fedheha. Wameitweza heshima ya Mtume Muhammad kuhusu kizazi chake. Ole wao, watapata adhabu kali kwa kumuasi Mwenyezi Mungu mwenye nguvu. Wameyabomoa makaburi ya watu wema kutokana na chuki walizo nazo, kwa hakika wameangamia na wamemchukiza Mtume[s.a.w.w] ." Kufuatia kauli yake Mtume[s.a.w.w] kwamba:

"Pindi bid'ah itakapodhihiri, basi ni wajibu kwa Mwanachuoni kudhihirisha elimu yake (kupingana kukemea bid'ah hizo) na iwapo hatafanya hivyo, basi laana ya Mwenyezi Mungu imshukie mwanachuoni huyo". Kwa hiyo basi wanachuoni wengi wa Kishia na wale wa Kisunni walijitokeza (kupinga na kukemea uzushi wa Kiwahabi), kama tulivyokwisha taja hapo kabla, waliandika vitabu na kuvitawanya ili kumfedhehesha mtu huyu (Muhammad ibn Abdul Wahabi) ambaye alikuja kutekeleza malengo ya Waingereza, akiwa amevaa ngozi ya kondoo; na walizifichua siri zake kwa kuidhihirisha asili yake pia walizipinga na kuzikemea fikra zake mbaya. Kitabu cha kwanza kutolewa dhidi ya Muhammad ibn Abdul Wahab ni "As-Sawa'iqul Ilahiyyah fi'r Raddi 'Al Wahabiyyah", kilichoandikwa na Sheikh Suleiman ambaye ni ndugu wa Muhammad Abdul Wahabi.

Kadhalika kwa upande wa Kishia, kitabu cha kwanza kutolewa dhidi ya Muhammad ibn Abdul-Wahabi ni "Man-haju 'r-Rashad" kilichoandikwa na mwanachuoni mkubwa aitwaye Sheikh Ja'far Kashif Al-Ghita' aliyefariki mwaka 1228 A.H. Sheikh Kashif Al-Ghita' alikiandika kitabu hiki kuwa ni jawabu la barua iliyotumwa kwake na mmoja wa Maamiri wa Kisuud katika wakati huo aliyekuwa akiitwa Abdul-'Aziz ibn Su'ud. Ndani ya kitabu hicho Sheikh Kashif Al-Ghita' ameudhihirisha wazi uwongo wa fikra za Muhammad ibn Abdul-Wahab, na amethibitisha ubatili (ubovu) wa fikra hizo kwa mujibu wa Qur'an na Sunna.

Kitabu hicho kilichapishwa katika mji mtukufu wa Najaf (Iraq) mwaka 1343. Baadaye ulifuatia ukosoaji na kukemea itikadi za Kiwahabi katika nyakati mbali mbali, na vikatolewa vitabu mfululizo kimoja baada ya kingine mpaka katika zama zetu hizi. Na wakati huu Mawahabi wamezielekeza hujuma zao zenye hatari kubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kutumia mali zao nyingi ambazo kizazi cha Wasuud kinazipata kutokana na mauzo ya mafuta ambayo faida yake yote hurejea kwenye kizazi hiki cha Wasuud peke yao. Watawala wavamizi wa Kisuud wametenga fungu kubwa Ia pesa zinazotokana na mauzo ya petroli kwa ajili ya kuyaeneza Madhehebu yao yaliyotoka Uingereza miongoni mwa Waislamu, na pia kuyaimarisha na kuyalinda madhehebu hayo. Lau isingekuwa mali hizi nyingi, madhehebu haya duni yaisingeweza kabisa kudumu mpaka wakati huu. Kwa hakika wakoloni ndani ya madhehebu haya wamekipata walichokuwa wanakitafuta, nao wameyatumia kuwa ndiyo njia bora ya kuleta mgawanyiko baina ya Waislamu na kuvunja umoja wao na kuwafanya wapigane wao kwa wao.

Na Madhehebu haya yametekeleza na kutimiza malengo ya wakoloni waovu wa Kiingereza, kwani utaona kuwa yamezusha ugomvi kati ya Waislamu; imekuwa Mwislamu huyu humuona Mwislamu yule kuwa ni fasiki na mwingine naye humkufurisha. La hawla wala Quwwata Illa Billahil 'Aliyyil 'Azim. Ewe msomaji mtukufu, kwa kweli tumekusudia katika kitabu hiki kuzichambua kwa utafiti wa kina itikadi za Kiwahabi, na tutafichua kiini chake mpaka ikudhihirikie kwamba itikadi za Waislamu zimetegemea Qur'an na Sunna tukufu, na kwamba itikadi za Kiwahabi zinakwenda kinyume cha Qur'an na Sunna ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] , nasi tumetumia njia ya kufupisha maelezo lakini yanayoeleweka.

MAWAHABI NA QADHIA YA KUJENGEA MAKABURI YA MAWALII

Kwa mujibu wa fikra ya Mawahabi, kujengea na kuimarisha majengo juu ya makaburi ya Manabii, Mawalii na Wachamungu ni miongoni mwa mambo yasiyoweza kuvumiliwa. Ibn Taimiyya na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim, ni watu wa kwanza kutoa fatwa ya kuharamisha ujenzi huu na kwamba ni wajibu kuyabomoa majengo hayo. Ibn Al-Qayyim anasema: "Ni wajibu kuyabomoa majengo ambayo yamejengwa kwenye makaburi, na wala haifai kabisa kuyaacha japo siku moja kila itakapowezekana kuyabomoa na kuyaondoa."[29] Katika mwaka wa 1344 A.H., baada ya watawala wa kizazi Ili kufanikisha azma yao, watawala hawa waliwauliza maswali wanachuoni wa Madina kwa kuwataka wanachuoni hao watoc fatwa inayoharamisha kujengca makaburi, na pia kufanya kila mbinu kuutakasa msimamo wa watawala wa Kisuud mbele ya mtazamo wa Waislamu wengine, na hasa katika nchi ya Hijazi. Na hii ilitokana na ukweli kwamba, Waislamu wa Hijazi (nchi ambazo zimo Makka na Madina) walikuwa na msimamo kama Waislamu wengine ulimwenguni kuhusu jambo hili, na walikuwa wakiitakidi utukufu wa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuwaheshumi, pia walikuwa wakikubali kuyajengea makaburi yao. Kwa hiyo 'Mawahabi wakajaribu kuingiza maovu yao kwa kulitumia vazi la Uislamu, ili wazuie shutma na lawama kutoka kwa Waislamu!!! Subhanallah!!!

Watawala wa Kisaud walimtuma Qadhi Mkuu wa Najdi Suleiman ibn Balhiid aende Madina ili akatake fatwa kwa wanachuoni wa Madina juu ya kujengea makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Lakini ni lazima kueleza kwamba, maswali aliyoyauliza ibn Balhiid yalikuwa yanayo majibu ndani yake ambayo yanaafikiana na mtazamo halisi wa Kiwahabi. Hivyo basi wanachuoni hao hawakuwa na la kufanya ila kujibu kama maswali yenyewe yalivyo. Na wanachuoni hao wa Madina hawakuwa na ushujaa au ujasiri wa kuweza kuitangaza haki kwa kutoa fatwa iliyo sahihi, hasa kwa sababu ya wao kuwa ni watu ambao riziki zao walikuwa wakizipata kupitia milango ya watawala siku zote, na walikuwa wakifahamu tangu mwanzo kwamba, kutoa fatwa kinyume cha mtazamo wa watawala kutawasababishia kutuhumiwa kuwa ni makafiri na ni washirikina, na watahukumiwa kuuawa iwapo watakataa kutubia. Katika Mwezi wa Mfunguo Mosi Mwaka 1344 A.H., jarida liitwalo "Ummul Quraa" linalotolewa huko Makka, lilichapisha maswali na majibu kati ya Qadhi Ibn Balhiid na wanachuoni wa Madina.

Kwa hakika kuchapishwa kwa maswali hayo kulizusha zogo na kelele nyingi miongoni mwa Waislamu, Mashia na Masunni wote; kwani walikuwa wakifahamu wazi kwamba matokeo ya fatwa hii ambayo imetolewa chini ya maafikiano yenye vitisho, yatakuwa ni kubomoa Maquba na majengo yaliyojengwa kwenye makaburi ya viongozi wa Uislamu na watu watukufu katika Uislamu. Na hayo ndiyo yaliyotokea. Na baada tu ya fatwa hii kutolewa na hao wanachuoni wa Madina wapatao kumi na tano, na ikaenea fatwa hiyo katika nchi ya Hijazi, utawala wa Kiwahabi ulianza kuyabomoa makaburi ya kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] , mnamo tarehe nane ya mfunguo mosi mwaka ule ule, na uliondosha kumbukumbu za kizazi cha nyumba ya Mtume[s.a.w.w] na Masahaba, pia walipora kila kilichokuwemo katika haram hivo tukufu yakiwemo mazulia ya thamani na vitu vingine vya thamani.

Kikundi hiki cha wakorofi kikaugeuza uwanja mtukufu wa Baqi' kuwa ardhi tupu yenye kuhuzunisha. Katika maelezo yafuatayo tutataja sehemu ya namna maswali yalivyoulizwa na lbn Balhiid; ili ufahamu ni namna gani muulizaji alivyoyatayarisha majibu katika masuali yake na utafahamu pia kwamba lengo halikuwa kuuliza na kutaka fatwa, bali ilikuwa ni kutaka kupatikane kuungwa mkono na kuupotosha mtazamo wa Waislamu wote, na pia kuziangamiza kumbukumbu za Unabii na Utume. Lau lengo lingekuwa ni kutaka fatwa ya kweli na kufahamu mtazamo wa uislamu, basi nini maana ya kuingiza majibu ndani ya maswali wakati wa kutaka fatwa hivo? Bali sisi tunadhani kwamba maswali na majibu yote yalikuwa yameandaliwa tangu hapo mwanzo katika karatasi maalum, kisha karatasi hiyo ilitumwa kwa hao wanachuoni wa Madina ili kutia saini tu.

Vinginevyo haiingii akilini kuwa, eti wanachuoni wa Madina kubadilisha muelekeo wa mtazamo wao ghafla na wakatoa fatwa kuharamisha kujengea kwenye makaburi na kuwa eti ni wajibu kuyabomoa, hali ya kuwa wakifahamu kwamba, wao na wazee wao waliyokwisha pita walikuwa wakilingania kuzihifadhi kumbukumbu za Mtume, na pia wakiyazuru majengo hayo matakatifu. Ibn Balhiid anasema katika maswali yake hayo: "Ni ipi kauli ya wanachuoni wa Madina (Mwenyezi Mungu na awazidishie fahamu na elimu) juu ya (uhalali) wa kujenga kwenye makaburi na kisha kuyafanya majengo hayo kuwa ni Misikiti, je jambo hili linafaa au hapana?" "Na iwapo haifai bali ni jambo linalokatazwa sana sana, basi je, ni wajibu kuyabomoa na kuzuia watu wasisalie mahala hapo au hapana?"

"Na kama jengo litakuwa kwenye ardhi iliyowekwa wakfu kama vile "Baqi", hali ya kuwa linazuia kuzika maiti mwingine katika nafasi iliyochukuliwa na jengo hilo, basi je kufanya hivyo itakuwa ni kupora sehemu hiyo, jambo ambalo ni wajibu kuliondosha kutokana na kuwa ni miongoni mwa dhulma dhidi ya wanaostahiki na kwamba itakuwa ni kuzuia haki yao au hapana?" Kwa kuwa maswali haya yaliulizwa hali ya kuwa wanachuoni hao wa Madina walikuwa chini ya vitisho, basi majibu yao kwa Sheikh Ibn Balhiid yakawa kama ituatavyo:

"Ama kujenga juu ya makaburi ni jambo ambalo limekatazwa kwa ijmai' kutokana na hadithi sahihi zilizokuja kukataza jambo hilo; na kwa hiyo basi wanachuoni wengi wametoa fatwa kuwa ni wajibu kuyabomoa majengo hayo wakitegemea hadithi ya Ali (r.a.) kwamba yeye alimwambia Abul-Hayyaaji, "Nakutuma kwa jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu alinituma mimi nikalifanye, nalo ni kwamba usiliache sanamu lolote ila ulivunje, na wala usiache kaburi lolote lililonyanyuliwa ila ulisawazishe." Sheikh An-Najdi anasema katika makala iliyochapishwa na jarida la "Ummu'l-Quraa" katika toleo lake Ia Mwezi wa Mfunguo tisa Mwaka 1345 A.H. kwamba: "Hakika ku jenga maquba juu ya makaburi ya Mawalii ni jambo ambalo limekuwa likiendelea kuwepo tangu karne ya tano Hijiriyya." Naam: Hii ni baadhi ya mifano ya maneno ya Mawahabi kuhusu suala la kujenga juu ya makaburi. Na utaona kwamba mategemeo ya ushahidi wao katika kuharamisha kujengea makaburi ndani ya vitabu vyao na maandiko yao yako kwenye hoja mbili:

1. Wanadai kuna ijma'i ya wanachuoni wa Kiislamu juu ya kuharamisha jambo hilo.

2. Hadithi ya Abul-Hayyaaj aliyoipokea kwa Imam Ali[a.s] , na zingine zinazofanana na hadithi hiyo.

Sasa hivi sisi tutazungumzia juu ya kujenga juu ya makaburi na kuyawekea paa na kusimamisha majengo kwenye makaburi hayo. Ama kuhusu suala la kuyazuru makaburi tutalizungumzia katika sehemu yake maalum "Mwenyezi Mungu apendapo". Kwa munasaba wa lile suala la kwanza (kuwa kuna ijma'i ya wanachuoni wa Kiislamu kuharamisha kujengea makaburi) tutalizungumzia katika vipengele vitatui:

1. Je, nini mtazamo wa Qur'an katika kujenga juu ya makaburi, naje, katika Qur'an jambo hili limebainishwa wazi?

2. Je, ni kweli kwamba umma wa Kiislamu umeafikiana juu ya uharamu wa kujenga juu ya makaburi? Au kujenga huku kumekuwa kukiendelea kuwepo katika

zama zote za Uislamu kuanzia wakati wa Mtume[s.a.w.w] na Masahaba?

3. Hadithi ya Abul-Hayyaaj inakusudia nini? Pia hadithi aliyopokea Jabir na Ummu Salamah na Na'im? Hadithi hizi ambazo Mawahabi wanatolea kama ushahidi wa mambo yao maovu.

A: MTAZAMO WA QUR'AN KATIKA KUJENGA JUU YA MAKABURI

Qur'an haikuweka wazi hukumu ya kujenga juu ya makaburi; isipokuwa inawezekana kuifahamu hukumu yake kwa kupitia baadhi ya aya tukufu ambazo zimelizungumzia jambo hili kiujumla. Hebu fuatilia ufafanuzi ufuatao:

1). KUJENGA JUU YA MAKABURI YA MAWALII NA KUVIHESHIMU VITU VITUKUFU VYA MWENYEZI MUNGU

Hakika Qur'an Tukufu inakichukulia kitendo cha kuheshimu mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu kuwa ni dalili ya ucha Mungu (Utawa). Mwenyezi Mungu anasema:

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾

"Na ye yote anayeziheshimu alama za Mwenyezi Mungu, basi kufanya hivyo ni miongoni mwa uchaji wa moyo." (Qur'an, 22:32).

Sasa tunajiuliza: Nini maana ya "taadhim sha'airillah?" Jawabu: "Sha'air" ni tamko la uwingi na umoja wake ni "Sha'irah", nalo lina maana ya dalili na alama, na wala haikuwa makusudio ya "Sha'air" katika aya hii kuwa ni alama zinazothibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, kwani ulimwengu wote ni dalili ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Mshairi mmoja anasema: "Katika kila kita kuna dalili inayojulisha kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja."

Kama ambavyo ni vema ifahamike kwamba hakuna ye yote anayesema kuwa, "kukiheshimu kila kita kilichoko ulimwenguni ni dalili ya ucha Mungu"; bali makusudio ni kuziheshimu dalili (alama) za dini ya Mwenyezi Mungu. Na maana hii ndiyo ambayo waisemayo wafasiri wa Qur'an katika aya hii kwamba, neno "Sha'airullah", maana yake ni vitambulisho vya dini ya Mwenyezi Mungu. Na iwapo "safa" na "Marwah" na pia ngamia anayepelekwa Mina kwa ajili ya kuchinjwa ni miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu, basi siyo kwa sababu nyingine bali ni kwa kuwa ni vitambulisho vya dini tukufu na mpenzi wa Mwenyezi Mungu Nabii Ibrahim[a.s] . Na iwapo Muzdalifah huitwa "Mash'ar" hiyo ni kwa sababu ipo miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; na kwamba kusimama katika Mashar hiyo ni dalili za kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Vile vile Ibada za Hija zinapoitwa kuwa ni Sha'air; basi siyo kwa sababu nyingine isipokuwa ni kwa kuwa ni alama za tauhidi na za dini tukufu. Kwa kifupi ni kwamba, kila kile ambacho ni kitambulisho cha dini ya Mwenyezi Mungu, kukiheshimu ni katika mambo yanayomsogeza mtu katika ucha Mungu. Hivyo basi hakuna shaka kwamba Manabii na Mawalii wa Mwenyezi Mungu, wao ndiyo alama kubwa zaidi miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu, kwani wao walikuwa ndiyo njia bora ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuueneza miongoni mwa watu.

Hakika miongoni mwa mambo yenye kuthibiti kwa kila mtu aliyemuadilifu ni kwamba, kuwepo kwa Mtume[s.a.w.w] na Maimamu watukufa[a.s] ni katika alama na vitambulisho vya dini hii tukufu, kwa hiyo kuwaheshimu wao ni kumtukuza Mwenyezi Mungu, na ndiyo alama ya ucha Mungu. Na hapana shaka kwamba, kuhifadhi kumbukumbu zao na kuyahifadhi makaburi yao yasiondolewe, ni moja katika aina ya kuviheshimu vitambulisho vya dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kwa maneno mengine, tunaweza kufahamu umihimu wa kuheshimu makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu kwa kupitia nukta mbili zifuatazo:

Kwanza : Mawalii wa Mwenyezi Mungu hasa wale ambao waliuawa kwa ajili ya kueneza dini, wao ni vitambulisho vya Mwenyezi Mungu na ni alama za dini yake.

Pili : Kujenga juu ya makaburi yao ili kudumisha utajo wao na kuishi kwa kufuata mwenendo wao wa haki ni aina ya kuonyesha kuwaheshimu na kuwatukuza. Kwa msingi huu basi, ndiyo maana tunaona mataifa yote ulimwenguni yanatenga maeneo maalum kwa ajili ya makaburi ya watu wao mashuhuri wa kidini na kisiasa, ili kuzibakisha kumbukumbu zao zidumu kwa ajili ya wafuasi wao milele. Kwa hiyo inakuwa kana kwamba kuyahifadhi makaburi yao yasitoweke na kuharibiwa ni katika jumla ya kudumisha kumbukumbu zao na kuendelea kuwepo kwa fikra zao na miongozo yao. Ili kuufahamu vyema ukweli huu, hapana budi tuifanyie mazingatio aya ya 36 katika Surah Al-Haj: "Na ngamia, ngombe, mbuzi na kondoo (muwachinjao) tumekufanyieni kuwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu".

Baadhi ya Mahujaji wa Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu walikuwa wakienda hija pamoja na ngamia wao kutoka katika miji yao ili wanyama hao wapelekwe iliko Al-Kaaba - kwa madhumuni ya kuwachinja karibu na nyumba ya Mwenyezi Mungu, pia walikuwa wakiwavalisha makoja shingoni mwao ikiwa ni alama ya kutambulisha kwamba, mnyama huyo atapelekwa Makka kwa ajili ya kuchinjwa. Basi mnyama huyo huwa amewekwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hawezi kuuzwa wala kununuliwa; na kitambulisho chake katika kundi la ngamia wengine hi huko kuvalishwa hilo koja. Kwa sababu hii basi, Mwenyezi Mungu amemzingatia mnyama wa aina hii kuwa ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu. Na kwa ajili hii, Uislamu umetoa hukumu ya kumheshimu mnyama huyu; hivyo basi haifai kumpanda; na ni wajibu kumkamilishia mahitaji ya chakula na kinywaji mpaka wakati wa kuchinjwa hapo karibu na Al-Kaaba.

Sasa basi, ikiwa ngamia huyu anapata heshima hii na utukufu huu kwa sababu tu amekuwa miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi utasemaje juu ya Manabii na Maimamu watukufu? Je, Manabii na Maimamu watukufu[a.s] pamoja na wanachuoni na mashahidi ambao walivaa makoja ya utuinwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tangu hapo mwanzo, na walijitoa muhanga nafsi zao kuitumikia dini ya Mwenyezi Mungu, pia wakawa ni wawakilishi wa Mwenyezi Mungu katika kuwaongoza na kuwaongoza viumbe wake; basi kwa yote haya hawatazingatiwa kuwa ni miongoni mwa vitambulishovya dini ya Mwenyezi Mungu?

Je, hivi siyo jambo la wajibu kuwatukuza na kuwapa heshima inayowastahiki wakiwa hai na baada ya kufa kwao? Ikiwa Al-Kaaba, Safa na Marwah, Mina na Arafat (vitu ambavyo havina uhai, na ni mchanganyiko wa udongo na mawe tu vinazingatiwa kuwa ni alama za Mwenyezi Mungu, na vinastahiki heshima na utukufu unaonasibiana navyo kwa sababu tu ya kuwepo mafungamano ya vitu hivyo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi kwa nini Mawalii wa Mwenyezi Mungu ambao wao ndiyo watetezi wa dini ya Mwenyezi Mungu na walizieneza shari'ah zake wasiwe ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu? Basi sisi tunawataka Mawahabi waamue wenyewe kuhusu jambo hili, na tunawauliza maswali yafuatyo: Je, mnayo mashaka yoyote au wasiwasi wowote kwamba Manabii na Mtume ni miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu? Je, nafsi zenu hazioni umuhimu na kuwatukuza na kudumisha utajo wao na kushikamana na mafundisho yao? Se, kujenga juu ya makaburi yao na kuvisafisha viwanja yalipo makaburi yao ni kuwatukuza na kuwaheshimu? Au kuyabomoa makaburi yao na kuvipuuza bila kuvisafisha viwanja walipozikwa na kuvitelekeza ndiyo kuwatukuza?!

2. KUWAPENDA AL-QURBAA

Kwa hakika Qur'an inatuamuru wazi wazi kuwapenda jamaa wa Mtume[s.a.w.w] na kushirikiana nao vizuri, na inasema:

قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ ﴿٢٣﴾

"Waambie (ewe Mtume Wetu) sikuombeni malipo yoyote (katika kazi hii) isipokuwa muwapende jamaa (zangu), (42:23).

Kitu kinachoonekana wazi kwa ye yote yule ambaye Mwenyezi Mungu amemsemesha kwa usemi uliyomo katika aya hii ni kwamba, kujenga juu ya makaburi ya watu wa nyumba ya Mtume[s.a.w.w] ni moja katika aina za kuonyesha upendo kwao. Desturi hii (ya kujenga juu ya makaburi ya viongozi) ni yenye kufuatwa na mataifa yote katika ulimwengu, na wote wanaizingatia hali hii kuwa ni namna mojawapo ya upendo kwa huyo aliyezikwa kwenye kaburi hilo; na ndiyo maana utaona wanawazika viongozi wao wakubwa wa kisiasa na utaalamu mbali mbali katika makanisa na sehemu mashuhuri za kuzikia, na kisha wakapanda pembeni ya makaburi hayo aina tofauti za maua na miti.

3. KUJENGEA MAKABURI KATIKA NYUMATI LILIZOPITA

Baadhi ya aya tukufa za Qur'an zinatufahamisha kwamba, kuyaheshimu makaburi ya waumini ni jambo ambalo lilikuwa limeenea miongoni mwa nyumati zilizotangulia kabla Uislamu haujadhihiri. Kwa mfano, zilipokuwa zimeenea habari za As-habul kahfi (Watu wa Pangoni) miongoni mwa watu, na watu hao wakaenda kwenye hilo pango ili wakawaone hao As-habul Kahfi wenyewe, ilitokea tofauti na mabishano juu ya mahala pa maziko yao hao As-habul-Kahfi, na watu wakagawanyika makundi mawili. Kundi moja likasema: Jengeni jengo juu yao". Na kundi la pili likasema: "Bila shaka tutajenga Msikiti juu yao" Hapa utaona kwamba Qur'an Tukufu inatutajia rai hizi mbili bila ya kuzikosoa; kwa hali hiyo basi inawezekana kusema kwamba lau rai hizi mbili zingekuwa hazifai, bila shaka Qur'an ingezikosoa au ingesimulia kisa cha semi mbili hizi kwa kuzipinga na kuzikemea. Wafasiri wa Qur'an wanasema: "Mzozo kuhusu mahali walipozikwa As-habul-Kahfi, ulitokea baina ya waumini na makafiri ama makafiri wao walisema: "Jengeni jengo juu yao", na waumini nao walisema: "Tutajenga msikiti juu yao."

Ushindi waliupata waumini, kwani Mwenyezi Mungu anasema:

قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِم مَّسْجِدًا ﴿٢١﴾

"Wakasema wale walioshinda katika shauri lao, bila shaka tutajenga msikiti juu yao". (Qur'an, 18:21).

Msikiti ulijengwa na makaburi ya As-habul-Kahfi yakawa ni mahali panapotukuzwa na kuheshimiwa. Hali hii inatuonyesha kwamba lengo Ia kujenga juu ya makaburi ya hao As-habul-Kahfi halikuwa jingine isipokuwa ni kuonyesha namna ya kuwatukuza Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Ewe msomaji mpendwa, baada ya aya tatu za Qur'an zilizotangulia hapo kabla, ni dhahiri haiwezekani kuharamisha kujengea juu ya makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu, wala hakuna karaha ya kutenda hilo kwa namna ye yote ile, isipokuwa kinachowezekana ni kulizingatia tendo la kujengea juu ya makaburi kuwa ni katika namna ya kuviheshimu vitambulisho vya dini ya Mwenyezi Mungu, na kwa kufanya hivyo ni katika kuonyesha wazi upendo wa jamaa ya Mtume[s.a.w.w] .

4. RUHUSA YA NYUMBA MAALUM

Bila shaka Mwenyezi Mungu ametoa ruhusa ya nyumba ambazo ndani yake litatajwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mwenyezi Mungu akasema:

فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّـهُ أَن تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ ﴿٣٦﴾ رِجَالٌ لَّا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ ﴿٣٧﴾

"Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha litajwe humo jina lake, humtukuza humo asubuhi na jioni. Watu ambao hawashughulishwi na biashara ya kuuza na kununua (wakasahau) kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. (Qur'an, 24:36-37).

Katika aya hizi, ushahidi wa kufaa kujenga juu ya makaburi utakamilika kwa kubainisha mambo mawili: La kwanza: Nini makusudio ya neno Al-Buyut (nyumba) lililomo katika aya? La pili: Nini makusudio ya neno Ar-Raf'u pia lililoko katika aya? Kuhusu lile neno la kwanza, kinachokusudiwa katika neno "Al-Buyut" siyo Misikiti peke yake, isipokuwa muradi wake ni misikiti na sehemu ambazo hutajwa katika sehemu hizo jina Ia Mwenyezi Mungu, sawa sawa ikiwa ni misikiti au isiwe misikiti, kama vile nyumba za Manabii na Maimamu[a.s] na wacha Mungu ambao haiwashughulishi biashara ya kuuza na kununua kiasi cha kuwasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu.

Basi nyumba hizi zitazingatiwa kuwa ni miongoni mwa makusudio yanayojitokeza katika aya hiyo tukufu. Bali inawezekana kabisa kusema kwamba makusudio ya "Al-Buyuut" siyo Misikiti, kwa sababu "Al-Bait" kwa maana ya nyumba, ni jengo ambalo Iimejengwa kwa kuta nne na juu yake kuna paa. Sasa basi ikiwa Al-Kaaba inaitwa kuwa ni nyumba ya Mwenyezi Mungu (Baitullahi), hakuna kinachosababisha iitwe hivyo ila ni kwa kuwa inalo paa. Qur'an kwa upande wake, inazingatia neno "Al-Bait" kwa maana ya nyumba yenye paa. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

"Na isingekuwa watu watakuwa kundi moja, bila shaka tungeliwafanyia wanaomkufuru (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa Rehema, majumba yao kuwa ni yenye mapaa ya fedha "..... (Qur'an, 43:44).

Kinachofahamika katika aya hii ni kwamba nyumba "Al-Bait" huwa haiepukani na paa. Na kwa kisheria inapendekezwa Misikiti isiwe na paa na ndiyo maana unanona msikiti Mtukufu wa Makka kwa juu uko wazi haukufunikwa na paa. Na kwa hali yoyote ile, makusudio ya "Al-Buyuut" ima yatakuwa na maana zaidi ya ile manna ya misikiti au manna yake isikusudie misikiti. Maelezo yaliyotangulia hivi punde yamelihusu lile jambo la kwanza yaani nini makusudio ya neno "Al-Buyuut". Na ama lile la pili ambalo ni maana ya (Ar-Raf'u), hili linawezekana kuwa na manna mbili. Maana ya kwanza: Ni kuwa makusudio ya neno "Ar-Raf'u" (kuinua) ni kwa ile maana ya kimaada inayoonekana wazi wazi, maana ambayo huthibitika kwa kuweka msingi (wa jengo) na kusimamisha kuta na hatimaye jengo lenyewe kusimama kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ ﴿١٢٧﴾

Na (kumbukeni pale) Ibrahimu alipoziinua kuta za nyumba na Isma'il. (Qur'an, 2:127).

Maana ya pili: Ni kuwa makusudio ya neno "Ar-Raf'u" ni kimaana (na wala siyo ya kimaada) kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na tulimuinua daraja ya juu kabisa, maana yake ni kuwa "Tulimpa daraja ya juu kabisa". Iwapo makusudio ya Ar-Raf'u yatakuwa ni kwa ile maana ya kwanza, basi itakuwa inajulisha wazi kabisa kwamba inafaa kuyajenga na kuyaimarisha majumba ya Manabii na Mawalii wa Mwenyezi Mungu, katika zama za uhai wao na baada ya kufa kwao. Na ni jambo linaloeleweka kwamba mahali alipozikwa Mtume[s.a.w.w] na mahali walimozikwa wengi wa Maimamu watukufu na Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni katika majumba yao.

Hivyo basi, kuyajenga majumba haya na kuyahifadhi yasiharibiwe na kuondoka alama zake ni tendo linalofaa kwa mujibu wa nassi ya aya tukufu ya Qur'an; na zaidi ya hapo ni jambo lililopendekezwa litendwe. Na kama muradi wake neno Ar-Raf'u itakuwa ni ile ya kimaana tu yaani kutukuza (kuinua daraja, cheo) matokeo yake yatakuwa ni kupatikana ruhusa ya kuyaheshimu na kuyatakuza majumba hayo na kuyahifadhi na kuyaepusha kutokana na kila kile ambacho hakistahiki heshima yake. Na kwa hali yoyote, ile ruhusa iliyopo katika maana ya neno Ar-Raf'u, sawasawa kama itakuwa ni ile ya kimaada au ni ile ya kimaana tu, basi itakuwa haikupatikana ila kwa sababu ya kuwepo katika mahali hapo watu wema, ambao humtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu asubuhi na jioni. Baada ya kuitaja aya hii na aya nyingine zinazofanana na hii, basi itakuwaje Mawahabi waone kuwa inafaa kuyabomoa majumba waliyokuwamo kizazi cha Mtume[s.a.w.w] , majumba ambayo yalikuwa ni mahala ambapo Malaika wa Mwenyezi Mungu walikuwa wakishuka na pia yalikuwa ni vituo vya kumtaja Mwenyezi Mungu na kueneza dini yake na hukumu zake?

Vipi itakuwa inafaa kwa Mawahabi kubomoa makaburi matukufu ambayo ndiyo mahala pa (kuonyesha) upendo wa nyoyo za mamilioni ya waumini ambao walikuwa wakiyazuru - wake kwa waume, asubuhi na jioni, na walikuwa wakimtaja Mwenyezi Mungu katika majumba hayo, kwa kuswali, kuomba na kumtakasa? Kwa nini basi Mawahabi wamefanya jeuri kwa kuyadharau majumba haya na kuyadhalilisha na kuyapuuza? Kwa nini wameyageuza yakawa hi mahala palipotengwa na kubaki pweke. Nyoyo za waumini wote huomboleza na kuhuzunika kutokana na kuyadharau na kuyadhalilisha majumba haya. Kwa nini? Tena kwa nini? Amepokea Al-Hafiz As-Suyuti kutoka kwa Anas ibn Malik na Buraidah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu[s.a.w.w] aliisoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu (isemayo) "Katika majumba ambayo Mwenyezi Mungu ameamrisha zijengwe....." Basi alisimama mtu fulani akasema: "Ni nyumba gani hizi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?"

Mtume[s.a.w.w] akasema: "Ni nyumba za Mitume." Basi Abubakar akasimama na akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na nyumba hii ni miongoni mwa hizo?" Na aliashiria nyumba ya Ali na Fatma[a.s] . Mtume[s.a.w.w] akasema: "Ndiyo; nayo ni bora mno kuliko zingine".

B: UMMA WA KIISLAMU NA KUJENGA JUU YA MAKABURI

Uislamu ulipokuwa umeenea katika bara Arabu, na nuru yake ikaenea katika sehemu kubwa ya mashariki ya kati, makaburi ya Manabii yaliyokuwa yakifahamika yalikuwa yamejengewa na kuwekwa mapaa yaliyoyafunika. Baadhi ya makaburi hayo yalikuwa yana Maquba imara na kuna madharih mazuri, na baadhi yake yapo mpaka leo. Katika mji wa Makka yenyewe utaliona kaburi la Nabii Isma'il na mama yake, Hajirah, yapo katika mahala panapojulikana kama "Hijri Isma'il". Na kadhalika Kaburi Ia Nabii Daniel liko katika mji wa Shush nchini Iran. Na makaburi ya Manabii Hud, Saleh, Yunus, Dhulkifl[a.s] yako nchini Iraq. Vile vile kaburi la Nabii Ibrahim na makaburi ya wanawe kina Ishaq; Ya'qub na Yusuf[a.s] yako huko Baitul-Muqaddas (Jerusalem).

Na hapo kabla makaburi haya ya wana wa Ibrahim[a.s] yalikuwa Misri, na baadaye Nabii Musa[a.s] akaihamishia miili yao mitukufu huko Quds kwa amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mpaka leo makaburi hayo bado yapo, na kila kaburi limejengwa imara na linajulikana wazi. Na kaburi la mama Hawa (mama wa wanaadamu) liko katika mji wa Jeddah ndani ya nchi ya Hijazi, kwa mujibu wa kauli iliyo mashuhuri; na umeitwa hivyo mji huu kutokana na kuwepo kwa kaburi la mama Hawa katika sehemu hiyo. Kaburi hili Ia mama Hawa hapo mwanzo alama zake zilikuwa zikionekana, lakini Mawahabi walipokwisha kuikalia nchi ya Hijazi waliziondosha alama zake na kufuta kabisa athari zake.

Makaburi yote haya tuliyoyataja yaliendelea kuwepo hata baada ya Waislamu kuiteka miji hiyo na waliyaona, lakini pamoja na hali hiyo hawakutenda tendo lolote la kupinga kuwepo kwa makaburi hayo na wala hawakuamrisha yabomolewe au kuharibiwa. Basi lau ingekuwa kujenga juu ya makaburi na kuwazika wafu katika makaburi yaliyojengwa na kuwekewa mapaa ni jambo lililoharamishwa katika Uislamu, lingekuwa ni jambo la lazima kwa Waislamu hao kabla ya kufanya chochote wayabomoe makaburi hayo ambayo yapo mpaka leo katika sehemu mbali mbali nchini Iraq, Jordan na Palestina.

Pia Waislamu hao wangezuia kujengwa upya makaburi hayo kila yanapoharibika muda wote. Lakini tunachokiona ni kuwa, Waislamu hao hawakuamuru yabomolewe, bali waliendelea kuyaimarisha na kuyahifadhi muda wote wa kipindi cha karne kumi na nne. Kwa hakika walikuwa wakifahamu kwa kupitia ufunuo wa kiakili kwamba, kuzilinda kumbukumbu za Manabii na kuzihifadhi ni miongoni mwa kuwaheshimu Manabii hao, na kwamba jambo hilo huwakuru - bisha kwa Mwenyezi Mungu na linawapatia malipo mema.

Ibn Taimiyya anasema ndani ya kitabu chake kiitwacho, As-siratul-Mustaqiim: "Quds ilipokuwa imeingia mikononi mwa Waislamu, makaburi ya Manabii yalikuwa yamo ndani ya majengo, lakini milango ya majengo hayo ilikuwa imefungwa mpaka katika karne ya nne Hijriyya."[30] Kwa hiyo basi, lau kujengea makaburi ingekuwa ni haramu, pasingekuwa na sababu yoyote ya kuyaacha makaburi hayo kama yalivyokuwa na huku milango yake imefungwa; isipokuwa ingekuwa ni jambo la wajibu kuyabomoa mara moja, (Hata kama tukichukuwa usemi wa Ibn Taimiyya kwamba milango yake ilikuwa imefungwa mpaka karne ya nne, lakini kauli hii haina uthibitisho.) Kwa kifupi kuyabakisha majengo hayo na Maquba yaliyojengewa kwenye makaburi muda wote huu mbele ya macho ya wanachuoni na mafaqihi wa Kiislamu, ni dalili iliyo wazi ya ruhusa ya kuyajengea makaburi katika dini ya Kiislamu.

10

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU

MAISHA YA MOTONI

Moto umetumiwa katika Qur'an na Hadithi kuonyesha makazi mabaya watakaposhukia waovu, walioamua kumpinga Allah (s.w.) na kuendesha maisha yao ya hapa duniani kinyume na kanuni na taratibu alizoziweka Allah (s.w.). Maisha ya motoni ni kinyume na maisha ya peponi ambayo picha yake tumeshaiona. Hebu tuelekeze kamera yetu motoni na kupiga picha ya maisha ya huko. Kwanza kabisa tunafahamishwa na Qur'an kuwa motoni kuna daraja au milango saba.

﴿ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٤٣﴾ لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ ﴾

"Na bila shaka Jahannam ndipo mahali pao walipoahidiwa Ina milango saba, na kwa kila mlango iko sehemu yao iliyogawanywa" [15:43-44]

Daraja hizi za moto zimepewa majina kama tusomavyo katika Qur'an: Jahannam: Jina hili limetumiwa katika aya nyingi za Qur'an kama jina la ujumla la maisha ya motoni. Hutwamah:

﴿كَلَّا لَيُنبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ ﴾

"Moto wa kuvunja vunja - moto uliowashwa kwa ukali barabara". [104:4]

Moto mkali wa kuunguza [4:55]

Moto unaobabua. [74:26]

Moto mkali. Qur'an (26:9 na 102:6]

Moto uwakao kwa ukali. Qur'an (101:9]

Mioto hii itawaunguza wakosaji kulingana na makosa yao.

Kwa ujumla aina yoyote ya moto ulioandaliwa makafiri hata ukiwa na daraja ya chini namna gani, utakuwa ni mkali usiokifani na usiovumilika hata kwa muda mfupi sana kama Allah anavyotufahamisha:

﴿إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴾

"Hakika hiyo (Jahannam) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa (hata kwa muda mfupi) " [25:66]

Hebu tuone pia anavyotufahamisha Mtume(s.a.w.w) juu ya kiwango cha ukali wa adhabu ya motoni: Nuuman bin Bashir amesimulia kuwa, Mtume(s.a.w.w) amesema:Hakika atakayekuwa na adhabu nyepesi kabisa katika wakazi wa motoni atakuwa yule atakayekuwa na viatu vya moto. Kwa moto huu (wa nyayoni) utachemsha ubongo wake kama maji yachemkayo kwenye birika. Haitaonekana kuna mwenye adhabu kali kuliko hii, lakini hiki ndio kiwango cha chini kabisa cha adhabu .[Bukhari na Muslim]

Kwa ujumla moto wa adhabu aliouandaa Allah (s.w.) kwa watu waovu ni mkali sana wenye miale yenye kupanda juu kwa hasira. Moto huu umeunguzwa kwa ukali kwa muda wa miaka elfu moja mpaka ukabadilika kuwa mwekundu. Uliunguzwa tena kwa muda wa miaka mingine elfu moja mpaka ukabadilika kuwa mweupe. Kisha uliunguzwa tena kwa miaka mingine elfu moja mpaka ukabadilika kuwa mweusi. Hivi ndivyo tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:Abu Hurairah amesimulia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ambaye amesema: Moto uliunguzwa kwa muda wa miaka elfu moja mpaka ukawa mwekundu. Kisha uliunguzwa kwa muda mwingine wa miaka elfu moja mpaka ukawa mweupe. Tena uliunguzwa kwa mara nyingine kwa muda wa miaka elfu moja mpaka ukawa mweusi. Sasa ni mweusi tii. [Tirmidh]

Pia tunafahamishwa kuwa Jahannam kutakuwa shimoni kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo: Uthman bin Ghazwaan amesimulia: Imesimuliwa kwetu na Mtume(s.a.w.w) kuwa jiwe litatupwa kutoka ukingoni mwa moto. Litaendelea kuanguka kwa miaka sabini bila kufika chini. Naapa kwa jina la Allah kuwa itajazwa. Na tulifamishwa kuwa umbali katika kati ya milango miwili ya moto na mwendo wa siku arubaini na patakuja siku ambapo itajaa watu. [Muslim]

Humo ndani ya shimo la moto wa Jahannam patakuwa na mashimo (mabonde) na shimo baya kabisa kuliko yote ni "Jabal- Huzn", ambapo Jahannam yenyewe inaomba kukingwa na moto huo wa "Jabal-Huzn" mara sabiini kwa siku. Ndani ya mazingira ya motoni pia patakuwa na miti michungu, na miti maarufu kwa uchungu wake hujulikana kwa jina la "Zaquum". Tumefahamishwa katika Hadith kuwa: Ibn Abbas amesimulia kuwa Mtume (s.a.w.w) alisoma aya hii:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴾

"Enyi mlioamini muogopeni Allah kama ipasavyo kumuogopa,wala msife isipokuwa mmeshakuwa Waislamu kamili". (3:102).

Mtume(s.a.w.w) alisema:Kama tone la Zaquum lingeanguka kwenye nyumba ya dunia hii, lingelitosha kuharibu vitu vyote wanavyovitumia wakazi wa dunia. Sasa itakuwaje kwa yule ambaye hicho kitakuwa ndio chakula chake? [Tirmidh]

Tunapata maelezo kamili ya mti wa Zaquum. Ambao umemea katikati ya Jahannam na watakaostahiki kuula katika aya zifuatazo:

﴿ أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ ﴿٦٢﴾ إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِّلظَّالِمِينَ ﴿٦٣﴾ إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ ﴿٦٤﴾ طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ ﴿٦٥﴾ فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٦٦﴾ ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ ﴾

"Je, karibisho la namna hii silo bora au kupata mti wa Zuqquum? (Mti mchungu kabisa watakaolishwa watu wa motoni). Kwa yakini sisi tumeufanya ni adhabu ya (hao) madhalimu (wa nafsi zao). Hakika huo ni mti unaotoka (unaoota) katikati ya Jahannam. (Panda za) matunda yake (zinatisha) kama kwamba ni vichwa vya mashetani. Bila shaka wao watakula katika (mti) huo, na kwa huo wajaze matumbo (yao). Kisha bila shaka utawathubutikia, juu ya uchungu wa mti huo, mchanganyiko wa maji ya moto". [37:62-67]

Pia katika mazingira ya motoni patakuwa na nyoka na nge wakubwa wenye sumu kali ambao watakuwa wanauma wakazi wa humo kama sehemu ya adhabu yao kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo:

Abdullah bin Harith bin Jazin amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:"Kuna nyoka huko motoni wakubwa kama ngamia. Mmoja wao akikuuma mara moja, uchungu wake hubaki kwa miaka arobaini. Kuna nge huko motoni wakubwa kama nyumba. Mmoja wao atamuuma mtu na uchungu wake utabakia kwa muda wa miaka arobaini . [Ahmad]

Kwa vyovyote itakavyokuwa maisha ya motoni yatakuwa magumu sana kwa wakazi wake. Chakula chao kitakuwa cha moto wa kuunguza kila kitu tumboni, mavazi yao yatakuwa ya moto, kinywaji chao cha moto kitakachochemsha matumbo yao. Picha halisi ya mazingira ya motoni, maisha ya wakazi wake na sifa zitakazowafanya wastahiki kuingia humo, aya zifuatazo zinafafanua zaidi:

﴿وَقَالُوا أَإِذَا ضَلَلْنَا فِي الْأَرْضِ أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ بَلْ هُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ كَافِرُونَ ﴿١٠﴾ قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الْمُجْرِمُونَ نَاكِسُو رُءُوسِهِمْ عِندَ رَبِّهِمْ رَبَّنَا أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَارْجِعْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ ﴿١٢﴾ وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٣﴾ فَذُوقُوا بِمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا إِنَّا نَسِينَاكُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴾

"Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?" (Ndio) Bali wao hawakiri kwamba watakutana na Mola wao. Sema: "Atakufisheni malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu; kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu".Na ungaliwaona waovu wakiinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao, (na kusema): "Mola wetu! Tumekwishakuona na tumekwisha kusikia, basi turudishe tutafanya vitendo vizuri, hakika (sasa) tumeyakinisha.Na tungalitaka tungempa kila mtu uwongofu wake (kwa lazima kama tulivyowapa malaika, lakini binadamu amepewa nguvu ya kufanya alitakalo lililo jema na baya), lakini imehakikika kauli iliyotoka Kwangu: Kwa yakini nitaijaza Jahannam kwa wote hawa; majini na watu (ambao ni wabaya). "Basi ionjeni (adhabu) kwa sababu ya kusahau makutano ya siku yenu hii, na sisi tutakusahauni (humo motoni) na onjeni adhabu idumuyo kwa yale mliyokuwa mkiyatenda". [32:10-14]

﴿ إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾ لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾ لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ﴿٢٣﴾ لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ﴿٢٤﴾ إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ﴿٢٥﴾ جَزَاءً وِفَاقًا ﴿٢٦﴾ إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ﴿٢٧﴾ وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ﴿٢٨﴾ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ﴿٢٩﴾ فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ﴾

"Kwa hakika Jahannam inawangoja wabaya.Ni makazi ya maasi.Wakae humo dahari nyingi (karne baada ya karne) Hawataonja humo baridi (wala usingizi) wala kinywaji.Ila maji yachemkayo sana na usaha (wanalipwa) malipo yaliyo sawa (na amali zao).Hakika wao hawakuwa wakiogopa hisabu (ya Mwenyezi Mungu).Na wakikadhibisha aya zetu kukadhibisha (kukubwa kabisa). Na (hali ya kuwa) kila kitu tumekidhibiti kwa kukiandika. Basi onjeni (leo adhabu yangu). Nasi Hatutakuzidishieni (kitu) ila adhabu (juu ya adhabu) ". [78:21-30]

﴿وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي ﴿٢٤﴾ فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ ﴿٢٥﴾ وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ ﴾

"Basi siku hiyo italetwa Jahannam.Siku hiyo mwanadamu atakumbuka,lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? Atasema:"Laiti ningalitanguliza (wema) kwa ajili ya uhai wangu (huu wa leo)".Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu Kwake (Mwenyezi Mungu). Wala hatafunga yeyote jinsi ya kufunga Kwake (Mwenyezi Mungu) " [89:23-26]

Aya hizi kwa ujumla zimesisitiza kuwa, watakaostahiki adhabu ya motoni ni wanadamu na majini waovu ambao waliendesha maisha yao ya hapa duniani kwa kibri na kinyume na utaratibu aliouweka na kuuridhia Allah (s.w.). Kuhusu adhabu yenyewe itakavyokuwa tunafahamishwa katika aya zifuatazo:

﴿إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴾

"Hakika wale waliozikataa Aya zetu, tutawaingiza katika moto. Kila ngozi zao itakapowiva, tutawabadilishia ngozi nyingine badala ya zile, ili wawe wanaonja (uchungu wa) adhabu (maisha). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na Mwenye Hikima) " [4:56]

Hawa mahasimu wawili waliohasimiana kwa ajili ya Mola wao. Basi wale waliokufuru watakatiwa nguo za moto na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yachemkayo.

﴿هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ فَالَّذِينَ كَفَرُوا قُطِّعَتْ لَهُمْ ثِيَابٌ مِّن نَّارٍ يُصَبُّ مِن فَوْقِ رُءُوسِهِمُ الْحَمِيمُ ﴿١٩﴾ يُصْهَرُ بِهِ مَا فِي بُطُونِهِمْ وَالْجُلُودُ ﴿٢٠﴾ وَلَهُم مَّقَامِعُ مِنْ حَدِيدٍ ﴿٢١﴾ كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا فِيهَا وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴾

"Kwa (maji) hayo vitayayushwa vilivyomo matumboni mwao na ngozi zao (pia). Na kwa ajili yao (yatakuwapo) marungu ya chuma. Kila mara watakapotaka kutoka humo (adhabuni) kwa sababu ya uchungu watarudishwa humo na (kuambiwa): "Ionjeni adhabu ya kuungua".[22:19-22]

﴿وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿١٠٣﴾ تَلْفَحُ وُجُوهَهُمُ النَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَالِحُونَ ﴿١٠٤﴾أَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿١٠٥﴾ قَالُوا رَبَّنَا غَلَبَتْ عَلَيْنَا شِقْوَتُنَا وَكُنَّا قَوْمًا ضَالِّينَ ﴿١٠٦﴾ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْهَا فَإِنْ عُدْنَا فَإِنَّا ظَالِمُونَ ﴿١٠٧﴾ قَالَ اخْسَئُوا فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ ﴾

"Na wale ambao mizani yao itakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao, na katika Jahannam watakaa muda mrefu. Moto utababua (utaziunguza) nyuzo zao, nao watakuwa humo wenye kukenya (meno yao kwa adhabu).(Waambie): Je! Hazikuwa aya zangu mkisomewa na nyinyi mkizikadhibisha? Watasema:"Mola wetu: Tulizidiwa na ubaya wetu na tukawa watu wenye kutopea. Mola wetu! Tutoe humu (motoni, uturejeshe ulimwenguni, tukafanye amali nzuri), na tufanyapo tena bila shaka tutakuwa madhalimu (wa nafsi zetu kweli kweli). Atasema (Mwenyezi Mungu):"Hizikeni humo wala msinisemeshe (msiseme nami) ". [23:103-108]

﴿إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ ﴿٤٣﴾ طَعَامُ الْأَثِيمِ ﴿٤٤﴾ كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ ﴿٤٥﴾ كَغَلْيِ الْحَمِيمِ ﴿٤٦﴾ خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ ﴿٤٧﴾ ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ ﴿٤٨﴾ ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ ﴿٤٩﴾ إِنَّ هَـٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ ﴾

"Bila shaka mti wa Zaqquum, ni chakula cha (kuliwa na) maasi,(kwa umoto wake ni) kama shaba iliyoyayushwa; huchemka matumboni kama chemko la maji ya moto kabisa. (Kuambiwe):"Mkamateni (huyo asi) na mumtupie katikati ya Jahannam.Kisha mwagieni juu ya kichwa chake (aonje) adhabu ya maji ya moto. (Aambiwe): Onja! Ulikuwa (ukijidai kuwa) wewe ni mwenye nguvu, mhishimiwa, (onyesha leo nguvu zako).Hakika hii ndiyo ile (adhabu) mliyokuwa mkibishana (mkiitilia shaka) ". [44:43-50]

﴿ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ ﴿٥١﴾ لَآكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ ﴿٥٢﴾ فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٥٣﴾ فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ ﴿٥٤﴾ فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ ﴿٥٥﴾ هَـٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ ﴾

"Kisha nyinyi, mliopotea (na kukadhibisha) kwa yakini mtakula mti wa Mzaqquum, na kwa huo mtajaza matumbo (yenu).Na juu yake mtakunywa maji ya moto yanayochemka. Tena mtakunywa kama wanywavyo ngamia wenye kiu sana.(Na kila wakinywa kiu haiweshi). Hiyo ni karamu yao siku ya malipo". [56:51-56]

﴿هَـٰذَا وَإِنَّ لِلطَّاغِينَ لَشَرَّ مَآبٍ ﴿٥٥﴾ جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٥٦﴾ هَـٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ ﴿٥٧﴾ وَآخَرُ مِن شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ ﴾

"Hivyo (ndivyo itakakavyokuwa).Na kwa hakika wale warukao mipaka, pa kurudia pao patakuwa pabaya: Jahannam - wataingia. Nayo ni matengenezeo mabaya kabisa.(Ndivyo hivyo itakavyokuwa). Basi waonje (wanywe) maji ya moto na usaha. Na (adhabu) nyingine za namna hii nyingi.(Kila likitiwa jeshi jingine huko motoni waambiwe wale waliotangulia". [38:55-58]

﴿وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٦﴾ إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُورُ ﴿٧﴾ تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ كُلَّمَا أُلْقِيَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ ﴿٨﴾ قَالُوا بَلَىٰ قَدْ جَاءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ كَبِيرٍ ﴿٩﴾ وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿١٠﴾ فَاعْتَرَفُوا بِذَنبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴾

"Na kwa waliomkufuru Mola wao iko adhabu ya Jahannam (inawaongojea). Na ni marejeo mabaya yaliyoje: Watakapotupwa humo watasikia rindimo (mngurumo) lake, na hali ya kuwa inafoka. Unakaribia kupasuka kwa hasira (yake juu ya wabaya).Kila mara litakapotupwa humo kundi (la wabaya) walinzi wake watawauliza: Je! Hakukufikieni mwonyaji? Watasema: Kwanini? Alitujia muonyaji, lakini tulikadhibisha na tulisema: Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote, nyinyi hamumo ila katika upotofu (upotevu) mkubwa. Na watasema: Kama tungalikuwa tunasikia au tungalikuwa na akili tusingalikuwa katika watu wa motoni (leo). Watakiri dhambi zao; (lakini hapana faida).Basi kuangamia kumewastahikia watu wa motoni". [67:6-11]

﴿إِنَّهُ مَن يَأْتِ رَبَّهُ مُجْرِمًا فَإِنَّ لَهُ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ﴾

Hakika atakayekuja kwa Mola wake, hali ya kuwa mkosa, basi kwa yakini atapata moto wa Jahannam, hatakufa humo wala hataishi (maisha mazuri). [20:74]

﴿فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ﴾

Basi siku hiyo hataadhibu yoyote namna ya kuadhibu Kwake(Mwenyezi Mungu). [89:25]

Aya hizi chache zimetupa picha ya kutisha ya maisha ya Motoni ambapo wakazi wake hawatakuwa na hata chembe ya furaha na hawatakufa japo watatamani wafe. Na hasara kubwa zaidi watakayoipata ni kutomuona Allah (s.w.). Kwani kumuona Allah (s.w.) ni kilele cha furaha na ilihali watu wa motoni wameharamishwa hata chembe ya furaha. Kwa ujumla marejeo ya motoni ni marejeo mabaya kabisa na kila mja mwema hana budi daima aombe:

﴿وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾ إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا﴾

"Mola wetu: Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea. Hakika hiyo (Jahannam) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa (muda mfupi au mrefu). [25:65-66]

11

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU

MAANANA YA KUAMINI SIKU YA MALIPO KATIKA MAISHA YA KILA SIKU

Muumini wa kweli wa Siku ya Mwisho ni yule atakaye jitahidi kwa jitihada zake zote kufanya yafuatayo:

1. Kufanya wema kwa kadiri ya uwezo wake ili apate radhi za Allah (s.w) ili astahiki kupata makazi mema katika maisha ya akhera.

Huingia katika biashara na Allah (s.w):

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿١٠﴾ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١١﴾ يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾ وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴾

Enyi mlioamini! Je! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo? (Basi biashara yenyewe ni hii):- Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu; ikiwa mnajua (kuwa ni bora, basi fanyeni).(Mkifanya haya) Atakusameheni dhambi zenu na atakuingizeni katika Mabustani yapitayo mito mbele yake na (atakupeni) maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele: huku ndiko kufuzu kukubwa. Na (atakupeni) kingine mnachokipenda: Nayo ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi ulio karibu! Na wapashe habari njema waumini (61:10 -13)

﴿إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴾

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani.Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa, (9: 111)

2. Kujiepusha na maovu kwa kadiri ya uwezo wake na kila mara kuleta Istighfar na dua, kumuomba Mola wake amuepushe na adhabu ya akhera. Katika Qur-an tunafahamishwa waja wa Rahman (Waumini wa kweli) ni wale waombao:

"Mola wetu tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea. Hakika hiyo (Jahannam) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa" (25:65-66)

3. Kuleta toba ya kweli atakapoteleza kwa kufanya jambo lolote lile kinyume na radhi ya Allah (s.w). Mwenyewe Allah (s.w) anatuamrisha:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ﴾

"Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allah toba ya kweli, huenda Mola wenu Atakufutieni maovu yenu na kukuingizeni katika pepo zipitazo mito mbele yake,.." (66:8)

﴿وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴾

"Na ombeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa Kurehemu." (73:20)

﴿إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾ وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا﴾

Allah (s.w) ameahidi kuwasamehe wale watakao leta toba ya kweli kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo: Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri; basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu. Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu.(25:70-71)

﴿ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾

Kisha hakika Mola wako kwa wale waliofanya ubaya kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mema; bila shaka Mola wako baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu (16:119)

﴿وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾

Na (wewe Mtume) wanapofika wale wanaoamini Aya zetu(na hali wamekosa kidogo; wanakuja kutubia) waambie "Amani iwe juu yenu, Mola wenu amejilazimisha rehema, kwamba atakayefanya miongoni mwenu uovu kwa ujinga, Mwenyezi Mungu atamghufiria kwani yeye ni Mwingi wa Rehema. (6:54)

﴿قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴾

Sema,"Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu; bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote; hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu." (39:53)

Kutokana na aya hizi, tunajifunza kuwa toba ya kweli itapatikana kwa kuzingatia masharti yafuatayo:

1. Mwenye kuleta toba awe amefanya kosa kwa ujinga au kwa kutelezeshwa na vishawishi vya mazingira ya kishetani bila ya kudhamiria.

2. Baada ya kutanabahi kuwa amemuasi Mola wake, Muumini wa kweli atajuta na kuilaumu nafsi yake, na kulalama kwa Mola wake, kama walivyolalama wazazi wetu, Adam(a.s) na Hawwa (r.a):

﴿قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴾

"Mola wetu!Tumedhulumu nafsi zetu, na kama hutatusamehe na kuturehemu,bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye khasara." (7:23)

Pia katika Hadithi iliyosimuliwa na Abubakar Swidiq (r.a) na kukubaliwa na Maimamu wote wa hadith, Mtume (s.a.w) ametufundisha kuleta majuto moyoni mwetu kwa kuomba: "Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika nimedhulumu nafsi yangu dhulma kubwa.Hapana yeyote mwenye kusamehe dhambi isipokuwa wewe tu.Basi nakuomba unipatie msamaha utukao kwako na unihurumie.Hakika wewe ni Msamehevu, Mrehemevu."

3. Kuazimia moyoni kuacha maovu.

4. Iwapo makosa yake yamehusiana na kudhulumu haki za watu, itabidi awatake radhi wale aliowakosea na kuwarejeshea haki zao zile zinazorejesheka.

5. Kuzidisha kufanya amali njema kwa kuzidisha kutoa sadaqa, kuzidisha kuleta swala na funga za sunnah, na kuzidisha juhudi ya kupigania dini ya Allah kwa mali na nafsi. Rejea Qur-an (61:10-13) na (9:111).

Shufaa Ni muhimu baada ya mada hii ya "maana ya kuamini siku ya mwisho", tuiangalie shufaa kwa mtazamo wa Kiislamu. Ni muhimu kwa sababu imetokea kwa baadhi ya watu wanaoitakidi kuwa ni waumini, kwa kupenda kwao njia ya mkato, wanaacha kutekeleza wajibu wao wa kuishi kama anavyotakiwa kuishi muumini wa kweli na badala yake wanaendesha maisha yao ya kila siku kama wafanyavyo makafiri na wakati huo huo wanamatumaini makubwa ya kupata neema za peponi kwa njia ya shufaa.

Maana ya Shufaa: Kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah shufaa ni uombezi wa watu wema kuwaombea msamaha watu watakaokuwa katika hali ya udhalili katika maisha ya akhera ili Allah (s.w) awatoe katika hali hiyo ya udhalili na kuwapeleka katika hali bora. Patakuwa na shufaa ya:

(i) Kuwaombea watu hisabu nyepesi na wachukue muda mfupi katika hisabu.

(ii) Kuwaombea waja wema waingie peponi moja kwa moja bila ya hisabu ili kuepukana na mazito ya siku ya Hisabu.

(iii) Kuwaombea waingizwe peponi wale ambao mizani ya mema na mabaya yao imekuwa sawa sawa.

(iv) Kuwaombea watu watolewe kutoka motoni na waingizwe peponi.

(v) Kuwaombea watu wema wapandishwe daraja katika Pepo; watolewe katika pepo ya daraja ya chini na kupandishwa katika pepo ya dara ya juu.

Masharti ya Shufaa: Pamoja na shufaa kuwepo katika siku hiyo ya malipo, Uislamu hauichukulii shufaa kwa mtazamo wa kikristo au mtazamo wa dini nyingine, ambapo hao watakaoshufaia wameitakidiwa kuwa watakuwa na uwezo wa kuwaokoa watu na adhabu ya Allah (s.w) na kuwaingiza Peponi. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Shufaa haitafanyika ila kwa idhini ya Allah (s.w). Ni lazima kwanza Allah (s.w) aridhike kuwa mkosaji anastahiki ndio atoe ruhusa ya shufaa kwa yule aliyemridhia na kisha baada ya msamaha huo kuombwa ni khiari yake Allah (s.w) kusamehe au kutosamehe. Msimamo huu juu ya shufaa umewekwa bayana katika Qur-an:

﴿مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ﴾

" Nani huyo awezaye kushufaia mbele yake (Allah) bila ya idhini yake?" (2:255)

"Na wako Malaika wangapi mbingu ni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia." (53:26). Pia rejea Qu r-an (6:51, 10:3, 19:87, 39:44, 43:86 na 74:48).

Kwa ujumla shufaa ni rehema ya Allah (s.w) atakayo ikunjua kwa wale watakaostahiki kuipata kutokana na jitihada zao za kutenda mema hapa duniani kwa ajili ya Allah (s.w) japo wakati mwingine wanaweza kutekeleza na kumuasi. Muumini wa kweli wa siku ya malipo atajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kutenda mema kwa ajili ya Allah (s.w), kujiepusha na maovu kwa kuchelea ghadhabu za Allah (s.w) na kuomba maghfira kwa haraka haraka kila atakapomkosea Allah (s.w) au kumkosea mwanaadamu mwenziwe. Udhaifu utakaompitia muumini huyu, Allah (s.w) atamsamehe kwa njia mbali mbali na hii ya kuombewa shufaa ikiwa ni mojawapo.

Nani watakao shufaia? Watakaoombea waumini shufaa kama tulivyoona katika aya zilizotangulia ni pamoja na Malaika, Mitume, watu wema ikiwa ni pamoja na watoto wachanga na amali njema kama Swala, Swaumu, Qur-an, n.k. Wa kwanza kushufai katika siku ya kutisha, siku ya Kiyama atakuwa ni Mtume(s.a.w.w) kama tunavyofahamishwa katika hadith nyingi. Baada ya Hukumu kupita,Mitume watawaombea shufaa miongoni mwa wafuasi wao ambao watakuwa wamehukumiwa kuingia motoni. Pia waumini watakoingia Peponi watapewa fursa ya kuwaombea shufaa waumini wenzao ambao kwa njia moja au nyingine walifeli mtihani na ikabidi waingie motoni.

Hebu tuzingatie hadith zifuatazo: Uthman bin Affan amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) kasema: "Watatu watashufaia katika siku ya Kiyama: Mitume, kisha wanachuoni, kisha waliokufa mashahidi". (Ibn Majah). Abu Sayyid amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:Kati ya Umma wangu patakuwa na watakaoshufaia makundi mengi ya watu kati yao kuna watakaoomba shufaa kwa kabila (moja) na kati yao kuna wakaoomba shufaa ya mtu mmoja, mpaka wangie Peponi." (Tirmidh)

Anas kasema: Wakazi wa motoni watapangwa katika mistari, kisha mmoja wa wakazi wa Peponi atawapitia. Mmoja katika wao atasema: Ewe Fulani, hunitambui?Nilikuwa yule niliyekupa maji. Na wengine watasema: Tulikuwa ni wale tuliyekupa maji ya kutawadhia. Hivyo atamuombea (kila mmoja) kwa Allah (s.w) na kumwingiza peponi. (Ibn Majah). Abu Sayyed al-Khudry amesimulia kuwa Mtume(s.a.w.w) amesema:"Kila mwenye imani uzito wa hardali (atom weight) atatolewa motoni". (Tirmidh).

Jambo la kuzingatia na kusisitiza sana hapa ni kwamba shufaa haitaombwa kwa misingi ya udugu, ukoo, utaifa au kwa misingi ya upendeleo wa aina yeyote, bali itajuzu tu kwa wale Allah (s.w) atakaoridhia waombewe na akatoa idhini juu ya kuombewa kwao. Kwa maana nyingine shufaa itategemeana na matendo mema ya mtu aliyoyatanguliza. Mitume watashufaia wafuasi wao waliowafuata kwa uadilifu, watu wema watawashufaia jamaa zao, jirani zao, rafiki zao, wananchi wenzao, waliowatendea wema kwa ajili ya wema wao, watoto wadogo wawashufaia wazazi wao waliokuwa wema kwao, n.k. Shufaa hizi zitapata ruhusa na kukubaliwa tu iwapo wale wanaoombewa walikuwa waumini ambao kwa njia moja au nyingine waliteleza na kumuasi Allah na wakastahiki kuwa katika hali hiyo ya dhiki. Kwa kafiri au mushriki shufaa ya aina yeyote haitakubaliwa hata kama shufaa hiyo itaombwa na Mitume au vipenzi vya Allah (s.w). katika Qu-an tumeona kukataliwa kwa maombi ya Nabii Muhu juu ya mwanawe aliyestahiki kuangamizwa pamoja na walioangamizwa kwa ukafiri wao:

"Ikiwa hiyo (jahazi) inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe aliyekuwa mbali (kakataa kuingia jahazini): "Ewe mwanangu!Panda pamoja nasi wala usiwe pamoja na makafiri". Akasema (huyo mtoto): "Nitaukimbilia mlima utakaonilinda na maji". Akasema (Nuhu): "Hakuna leo kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule atakayemrehemu (Mwenyezi Mungu)". Mara mawimbi yakaingia baina yao na akawa miongoni mwa waliogharikishwa. Na (baada ya kuangamizwa wote na vyote alivyotaka Mwenyezi Mungu viangamie) ikasemwa:P "Ewe ardhi: Meza maji yako. Na ewe Mingu jizuie (na kuteremsha mvua). Basi maji yakadidimia chini na amri ikapitishwa (ya kuangamizwa makafiri), na (jahazi) likasimama juu ya (jabali linaloitwa) Judi.Na ikasemwa likasimama juu ya (jabali linaloitwa) Judi. Na ikasemwa "Wameangamiliziwa mbali madhalimu"

Na Nuhu alimwomba Mola wake (alipomwona mwanawe anaangamia) akasema:

﴿ وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ ﴿٤٥﴾قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ﴾

"Ewe Mola wangu! Mwanangu ni katika watu wa nyumbani kwangu (mbona anaangamia)? Na hakika ahadi yako ni haki; nawe ni Mwenye haki kuliko mahakimu (wote): Akasema (Mwenyezi Mungu): Ewe Nuhu! Huyu si miongoni mwa watu wako. Yeye ni (mwenye) mwendo usiokuwa mzuri. Basi usiniombe ambayo huyajui Mimi nakunasihi usiwe miongoni mwa wajinga" (11:45-46)

Pia tunafahamishwa katika Hadith jinsi Nabii Ibrahim (a.s) atakavyokataliwa maombi yake kwa Allah (s.w) kumuombea baba yake Azar aepushwe na adhabu kali waliyoandaliwa washirikina: Abu Hurairah amesimulia kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) aliyesema: Ibrahim atakutana na baba yake. Azar katika siku ya Kiyama. Uso wa Azar utakuwa umefunikwa na lami na mavumbi.

Ibrahimu atamsemesha: "Sikukuambia kuwa usiache kunitii (usinikadhibishe)?" Baba yake atamjibu: "Leo sitaaacha kukutii". Ibrahim ataomba: Ewe Mola! Hakika umeniahidi kuwa hutanifedhehesha siku watakapofufuliwa watu.Sasa ni fedheha gani zaidi kuliko kuwekwa mbali na baba yangu? Allah (s.w) atasema: Hakika Nimeiharamisha Pepo kwa Washirikina. Kisha itasemwa kwa Ibrahimu: Angalia ni kitu gani kilichoko miguuni mwako. Ataangalia, hamaki: shingo kubwa itatokeza. Ataburuzwa (Azar) kwa miguu yake na kutupiwa motoni. (Bukhari)

Vile vile tukirejea tena Qur-an tunaona jinsi Mtume(s.a.w.w) alivyokataliwa maombi yake alipowaombea wanafiki:

﴿اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴾

Waombee msamaha au usiwaombee.Hata ukiwaombea msamaha mara sabiini,Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotofu.(9:80)

Hivyo kutokana na maelezo haya, tumeona kuwa shufaa itakuwepo, lakini itawanufaisha tu walioamini na sio makafiri, washirikina na wanafiki. Jambo muhimu kwa Muislamu ni kujitakasa kwa kutenda mema na kuacha maovu na kuwa mwepesi na kurejea kwa Allah (s.w) kwa toba baada ya Kumkosea au kuhisi Kumkosea. Si vyema kwa Muislamu kuzembea katika kufanya mema na kuendelea kufanya maovu kwa matarajio ya kupata shufaa ya Mtume(s.a.w.w) au ya yeyote yule amtegemeaye kuwa atamshufaia. Kuna mambo mawili muhimu ya kuzingatia kwa wale wanaoacha kujitahidi kutekeleza wajibu wao kama anavyoridhia Allah (s.w) na badala yake wakaishi watakavyo kwa tegemeo la kupata uokovu kutokana na shufaa:

Kwanza kutegemea shufaa ni jambo la kubahatisha mno, kwani si jambo lililoko kwenye mamlaka ya yeyote isipokuwa Allah (s.w) pekee. Pili, shufaa nyingine itakuja baada ya mja kuadhibiwa kwanza, adhabu ambayo ni kali mno, inayodhalilisha au kuhilikisha hata kama mja atakaa humo muda mfupi sana. Ni vyema tuzingatie sana aya ifuatayo:

Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu Kwake (Allah) (89:25)

Hivyo, jambo la busara ni Muislamu kujitahidi kuepukana na adhabu kali ya Allah (s.w) aliyowaandalia watu maasi na badala yake ayaendee kwa juhudi kubwa iliyoambatana na subira na yale yatakayompelekea kustahiki kuingizwa peponi moja kwa moja.

6

7

8

9

10

11

12

13

14

15

16

17

18

19

20

21

22

23