UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI0%

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI Mwandishi:
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi: Vitabu mbali mbali

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi: SHEIKH JA'AFAR SUBHANY
: SHEIKH MUSABBAH SHA'ABANI
Kundi:

Matembeleo: 50929
Pakua: 5274

Maelezo zaidi:

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 24 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 50929 / Pakua: 5274
Kiwango Kiwango Kiwango
UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

Mwandishi:
Swahili

6

UCHUNGUZI JUU YA UWAHABI

KUZURU MAKABURI KWA MUJIBU WA QUR'AN NA SUNNA

Wanachuoni wa Kiislamu na wataalamu wa sheria ya Kiislamu wametoa fatwa inayoruhusu kuzuru makaburi, hasa yale ya Manabii na watu wema. Fatwa hii wameitoa hali ya kuwa wanategemea aya nyingi za Qur'an na hadithi za Mtume [s] zinazohusu jambo hiti. Zaidi ya Fatwa inayoruhusu jambo hili, wanachuoni hao wametoa Fatwa kusisitiza kufanywa ziyara kuwa ni jambo bora na pia ni mustahab. Ama Mawahabi, kama inavyodhihiri ni kwamba hawaharamishi asili ya kuyazuru, bali wanaharamisha kukusudia safari ya kuzuru makaburi ya watu wema. Kwa hiyo basi utafiti wetu juu ya jambo la kuzuru makaburi utakuwa katika sehemu mbili.

1. Ziyara.

2. Safari kwa ajili ya ziyara.

KUZURU MAKABURI

Katika mambo yasiyo na shaka ndani yake ni kuwa, kuzuru makaburi huwa kuna jumuisha kupatikana athari muhimu za tabia njema na mafunzo mengine mema. Tunaonyesha kwa ufupi kama ifuatavyo: Kushuhudia uwanja uliotulizana kimya, ambao chini yake kuna idadi kubwa ya watu waliopata kuishi katika dunia hii kisha wakafariki, wakiwemo masikini na matajiri, wanyonge na wenye nguvu, kipindi hicho wakiwa hawana wanachokimiliki isipokuwa sanda, hali hii huutingisha moyo na roho ya mtu na kumpunguzia furaha na tamaa ya dunia na starehe zake. Lau mtu atauangalia uwanja huu wa makaburi kwa jicho Ia mazingatio, hakika atabadili mwenendo wake katika hii dunia na kuweka mazingatio yake akhera, na atakuwa akijiwaidhi mwenyewe kwa kusema: "Hakika maisha ya dunia ni ya muda na yatatoweka tu, na kwamba kipindi cha maisha ninayoishi kina mwisho na matokeo yake nitazikwa kaburini na kukandamizwa na rundo la udongo, na huko akhera kuna malipo ima mema au mabaya.

Kwa hiyo ataona kuwa maisha haya ya dunia haifai kwa mtu kusumbuka kutafuta mali na heshima na cheo kwa kumdhulumu huyu au yule, kitu ambacho kitamfanya achume dhambi na mambo maovu. Mtazamo wa makini kwenye uwanja hun uliotulia kimya, hulainisha moyo hata kama ulikuwa mgumu, na humfanya mtu asikie hata kama alikuwa kiziwi, na kuyafungua macho hata kama yalikuwa hayaoni, na zaidi ya hapo humfanya mtu asahihishe tabia yake na maisha yake na ajihisi kuwa analo jukumu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mutukufu na watu.

1. Mtukufu Mtume[s.a.w.w] anasema: "Zuruni makaburi kwani yanakukumbusheni akhera".[73] Pamoja na ukweli kwamba Masala ya kuzuru makaburi hayahitaji kutolewa dalili na hoja juu yakusihi kwake na umuhimu wake, sisi tunalazimika kuyazungumzia kwa wale wenye shaka (ili tuwaondolee shaka yao).

QUR'AN NA KUZURU MAKABURI

Mwenyezi Mungu anamkataza Mtume[s.a.w.w] kuswalia jeneza Ia mnafiki na kusimama kwenye kaburi lake anasema: "Wala usinisalie kamwe mmoja wao yeyote yule akifa, wala usisimame kaburini kwake hakika hao wamemkufuru Mwenyezi Mungu na mjumbe wake na wakafa hali ni mafasiki. Qur'an, 9:84. Aya hii tukufu inalenga kuvunja heshima (dhati) ya mnafiki na inatoa onyo mbele ya wanafiki wenziwe na wenye mfano kama huo. Kukatazwa kwa mambo mawili haya (kumsalia mnafiki na kusimama kaburini kwake) maana yake na maf-humu yake ni kwamba asiye mnafiki anastahiki kufanyiwa mambo haya mawili. Sasa tunalazimika tuangalie nini maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema: "Wala Taqum Ala Qabrih", (yaani wala usisimame kaburini kwake). Je, maana yake ni kuwa, kule kusimama kwenye kaburi ambako haifai kwa mnafiki, na kwa muumini inafaa, ni katika kipindi kile cha mazishi tu au maana yake inaenea tangu wakati wa kuzika na hata baada ya wakati huo? Jawabu ni kwamba: Baadhi ya wafasiri wameichunguza aya hii kwa uchunguzi au mtazamo finyu na wakatumia ile kauli ya kwanza, yaani ni ule tu wakati wa kuzika.

Lakini wengine kama vile Al-Baidhawi na wengineo wanaitazama kwa mtazamo mpana na wakasema: "Hakika katazo lililoko katika "Usisimame kaburini kwake", linaanzia tangu kuzika mpaka kumfanyia ziyara". Mtazamo wenye mazingatio unatupeleka kwenye maana hii tulioyoitaja hivi punde, maana ambayo ni pana. Hali hii inakuja kutokana na aya yenyewe kushikamana na sentensi mbili: Ya Kwanza: "La Tusali Ala Ahadinmin-hum Mata Abadan, Usimsalie kamwe mmoja wao yeyote yule akifa." Hakika tamko 'Ahadan" kwa sababu limefuata nafyi hufidisha umumu na Istighraqi kwa afradi zote na kadhalika. Tamko 'Abadan" linapokuja katika mtiririko wa kukanusha huwa linafidisha "Al-umumu Wal-istighraq Lijamiil-afrad" na tamko "Ahadan" huwa linafidisha "Al-istighraquz-zamani", yaani linaenea wakati wote.) Kwa hiyo maana ya aya itakuwa, "Usimsalie kamwe mmoja wao ye yote miongoni mwa wanafiki wakati wowote ule".

Baada ya kufahamu matamko mawili haya pia tunafahamu wazi kabisa kwamba, lengo la kukatazwa kumsalia maiti mnafiki halihusu sala ya maiti wakati wa mazishi tu, kwa sababu sala ya maiti haisaliwi mara kwa mara siku baada ya siku, bali maana ya sala katika aya hii kinachokusudiwa ni dua yoyote na kumuombea rehma, iwe ni wakati wa kuzika au baadaye. Lau ingekuwa imekusudiwa wakati wa mazishi tu, basi palikuwa hakuna haja ya kuwepo tamko "Abadan". Iwapo kuna mtu atasema: Tamko abadan ni kwa ajili ya kusisitiza kuenea afradi zote "Taukidil-istighraqil-afradi na siyo kwa ajili ya kusisitiza wakati. Jawabu lake ni hili ifuatalo:

1. Tamko "Ahadin" (yeyote) lilifidisha kuwakusanya na kuwaenea wanafiki wote (Basi hapakuwa na haja ya kuongeza Abadan).

2. Tamko "Abadan" katika lugha ya Kiarabu hutumiwa ili kuenea nyakati zote kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

"Wala tankihuu Az-wajahu Min Baadihi Abadan", yaani: Wala musiwaoe wake zake baada yake kamwe ". Qur an, 33:53.

Kwa hiyo basi matokeo yanakuwa kwamba, kilichokusudiwa ni kukataza kumrehemu mnafiki na kumuombea msamaha, sawa sawa kwa kumsalia au kwa jingine. Ya Pili: "La Taqum Ala Qabrih" - (usisimame kaburini kwake). Maf-humu ya jumla hii itakuwa, "Wala Taqum Ala Qabrihi Abadan" yaani, kamwe usisimame kaburini kwake". Na hii ni kwa kuwa jumla hii inaat-fia (inafuatia) ile jumla iliyotangulia "La Tusali Ala Ahadinmin-hum Mata Abadan." Kwa hiyo kila kilichothibiti kwenye kile kinachofuatwa yaani "Abadan" ambayo ni "Qayd" basi pia kitathibiti kwa hiki kinachofuata vile vile. Katika hali hii basi, haiwezekani kusema kwamba: "Makusudio ya kusimama kwenye kaburi ni wakati wa kuzika tu kwa sababu ya kutowezekana kukaririka kisimamo cha kuzika, kama tulivyoeleza kuhusu swala ya maiti. Na tamko Abadan lililokadiriwa kwenye hii jumla ya pili linafidisha uwezekano wa kukaririka tendo hili la kusimama kwenye kaburi. Hivyo basi inajulisha kwamba kusimama kwenye kaburi la mnafiki hakuhusu wakati wa mazishi tu bali wakati wote.

Na kama kuna msemaji atasema kuwa tamko "Abadan" lililokadiriwa katika jumia ya pili maana yake hi kuenea afradi zote. Sisi tutasema: "Maelezo ya hilo yamekwisha tangulia, na kwamba tamko "Ahadin" ndilo linalohusu istighraqi ya afradi zote wala siyo tamko "Abadan" ambalo ni istighraqi ya nyakati zote. Kwa hiyo maana ya aya tukufu itakuwa ni kwamba, Mwenyezi Mungu anamkataza Mtume[s.a.w.w] kumtakia Magh-fira na kumrehemu mnafiki, sawa sawa kwa kumswalia au kumuombea dua, na pia anamkataza kusimama kwenye kaburi la mnafiki, uwe ni wakati wa mazishi au wakati mwingine. Na Maf-humu yake ni kwamba, mambo haya mawili yanajuzu kufanyiwa "Muumini". Na kwa maelezo haya inathibiti kuwa inajuzu kuzuru kaburi la Muumini na inajuzu kuisomea Qur'an roho yake hata kama ni baada ya mamia ya miaka.

Kwa hiyo maelezo haya ni kwa munasaba wa Mar-hala ya kwanza nayo ni asili ya kuzuru makaburi kwa upande wa Qur'an inavyosema. Ama kwa munasaba huu wa ziyara kwa upande wa hadithi za Mtume[s.a.w.w] hebu tazama ufafanuzi wake kama ifuatavyo:

HADITHI TUKUFU ZA MTUME [s.a.w.w] NA KUZURU MAKABURI

Kinachoeleweka katika hadithi tukufu za Mtume[s.a.w.w] ambazo wamezipokea hao wenye sihah na sunan ni kwamba: Mtume[s.a.w.w] alikataza kuyazuru makaburi kwa muda fulani na kwa sababu maalum, kisha baadaye aliondoa katazo hilo na akasisistiza kuyazuru: Na huenda sababu ya kukataza kwa muda ilikuwa ni kwamba, maiti hao walikuwa ni washirikina na waabudu sanamu, wakati ambapo Uislamu ulikuwa umekata kila aina ya mahusiano na shirki pamoja na washirikina, ndipo Mtume[s.a.w.w] akakataza kuwazuru wafu (kwenye makaburi yao). Na inatiwa nguvu fikra hii na kauli ya Mtume[s.a.w.w] wakati alipokuwa anazuru makaburi husema, "nyumba ya watu walioamini" kama tutakavyoeleza baadaye. Pia huenda sababu ya kukataza ikawa ni jambo jingine, nalo ni kwamba, Waislamu walikuwa bado ni wageni katika Uislamu, kwa hiyo walikuwa wakiomboleza wafu wao kwa maombolezo batili yanayoweza kuwatoa katika sehemu fulani ya sheria.

Na pale Uislamu ulipokuwa umeimarika katika mioyo ya Waislamu na kuzizoweya sheria na hukmu za Uislamu, hapo ndipo Mtume[s.a.w.w] kwa amri ya Mwenyezi Mungu akalibatilisha lile katazo la kuzuru makaburi kwa kuwa kuzuru makaburi kuna kumbukumbu na matokeo mema, na ndiyo maana wamepokea wenye sihah na sunan kwamba, Mtume[s.a.w.w] amesema: "Nilikuwa nimekukatazeni kuyazuru makaburi, basi sasa yazuruni kwani yanafanya musiipende (sana) dunia na yanakumbusha akhera". [74] Na kwamba msingi huu basi Mtume[s.a.w.w] mwenyewe alikuwa akilizuru kaburi la mama yake Bibi Amina binti Wahabi [r.a] na akiwaamuru watu kuyazuru makaburi kwani kuyazuru kunamkumbusha mtu akhera. Naye Muslim amepokea katika Sahih yake:

3. Mtume[s.a.w.w] alilizuru kaburi la mama yake, kisha akalia na waliokuwa karibu yake nao wakalia, kisha akasema;Nimemuomba Mola wangu ruhusa ya kuzuru kaburi lake (Bibi Amina binti Wahabi) na ameniruhusu, basi nanyi yazuruni makaburi kwani yatakukumbusheni kifo .[75] Naye Bibi Aisha amesema:

4. "Hakika mjumbe wa Mwenyezi Mungu ameruhusu kuyazuru makaburi ".[76]

5. Na amesema tena Bibi Aisha kwamba, Mtume[s.a.w.w] amesema: "Ameniamuru Mola wangu niende Baqii nikawaombee msamaha." Mimi nikasema, "Basi nitasemaje ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu"? Mtume akasema; "Sema, As-salaamu Ala Ah-lid-diyari Minal-Muuminina Wal-Muslimina Yar-hamullahu Al-Mustaqdimina Minna WaI-Mustaakhirina, Wainna Insha-alIahu Bikumu Lahiquuna". Maana Yake: Amani iwafikie watu wa makazi haya miongoni mwa Waumini na Waislamu, Mwenyezi Mungu awarehemu waliokwisha tangulia miongoni mwetu na hao watakaokuja baadaye, nasi apendapo Mwenyezi Mungu tutakutana nanyi.[77] Na imekuja katika hadithi zingine zilizotaja maneno ambayo Mtume[s.a.w.w] alikuwa akiyasema wakati anapozuru makaburi. Maneno inengine ni haya:

6. As-salaam-Alaikum Dara Qaumimuuminina Wainnaa wa Iyyakum Mutawaaiduna Ghadan Wamuwakiluna, Wainna lnsha-allahu Bikum Laahiquuna Allahummagh-fir Li-ahlil-baqiil-gharqad.[78] Maana Yake: Amani ikufikieni enyi watu wa makazi haya ya waumini, sisi na ninyi tutakutana kesho na tutapata riziki pamoja toka kwa Mwenyezi Mungu nasi kwenu tutafika, Ewe Mwenyezi Mungu wasamehe watu wa Baqiiul-gharqad. Na imekuja katika hadithi nyingine iliyotaja maneno hayo kama ifuatavyo: "As-salaam Alaikum Ah-lad-diyari Minal-Muumina WalMuslimina, Wainna Insha-allahu Bikum Lahiquna, Antum Lana Far-tun Wanahnu Lakum Tabaun As-Alullahal-afiyata Lana Walakum."[79] Maana Yake: Amani ikufikieni enyi wenye makazi haya mkiwa ni miongoni mwa Waumini na Waislamu nasi apendapo Mwenyezi Mungu tutafika huko mliko ninyi, ninyi mmetutangulia nasi tutakukuteni, namuomba Mwenyezi Mungu atupe afya nanyi pia akupeni afya. Na katika hadithi nyingine ya tatu:

As-salaamu Alaykum Dara Qaumi Muuminina Wainnaa Insha-allahu Bikum Lahiquna.[80] Maana Yake: Amani ikufildeni enyi wenye makazi nikiwa miongoni niwa waumini nasi apendapo Mwenyezi Mungu tutafika huko niliko. Na kutokana na hadithi ya Bibi Aisha inafidisha kwamba Mtume[s.a.w.w] alikuwa akitoka kila sika mwishoni mwa usiku na kwenda Baqii kisha husema: "As-salaamu Alaikum Dara Qaumimuuminina Waatakum Matuuaduna Waghadan Muwajaluna, Wainna Insha-allahu Bikum Lahiquna, Allahummaghfir Liah-li Baqiil-gharqad."[81] Maana Yake: Amani ikufikieni enyi wenye makazi mukiwa miongoni mwa waumini na akupeni Mwenyezi Mungu uliyokuahidini na kesho akupeni ahyokuwekeeni nasi apendapo Mwenyezi Mungu takukutana nanyi. Na katika hadithi nyingine inafidisha kwamba Mtume[s.a.w.w] alikuwa akizuru makaburi yeye pamoja na kundi miongoni mwa Masahaba wake, na akiwafundisha namna ya kuzuru makaburi.

Mtume alikuwa akiwafundisha Masahaba wake wanapotoka kwenda makaburini, basi msemaji wao alikuwa akisema: "As-salaamu Alaa Ah-lid-diyar, au husema: As-salamu alaikum Ah-lad-diyar Minal-Muumina Wal-muslimina wainnaa Insha-allahu Lahiquna, As-alullaha Lana Walakumul-afiyah." Maana Yake: Amani iwe kwenu watu wa makazi haya au Amani iwe kwenu enyi watu wa makazi miongoni mwa waumini na Waislamu, namuomba Mwenyezi Mungu atupe afya nanyi akupeni afya.[82]

WANAWAKE NA KUZURU MAKABURI

Jambo la mwisho ambalo inapasa tulizungumzie, ni la wanawake kuzuru makaburi. Kuna mapokezi katika baadhi ya hadithi kwamba Mtume[s.a.w.w] amewakataza wanawake kuzuru makaburi: "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amewalaani wanawake wanaozuru makaburi".[83] Pamoja na kuwepo hadithi hii kuna haja ya kufahamu kwamba, kuharamishwa wanawake kuzuni makaburi kwa hoja ya hadithi hii siyo sahihi kutokana na sababu nyingi tu.

Ya Kwanza : Wanachuoni wengi wanazingatia kuwa, kukatazwa huku ni (kwa karaha siyo kwa kuharamisha) na karaha kwenye jambo hili limekuja kutokana na sababu maalum zinazohusika na wakati ule. Mwandishi wa kitabu kiitwacho "Mif-tahul-hajat Fii Shar-hi Sahihi Ibn Majah" anaashiria sababu hizo na anasema: "Wametofautiana (wanachuoni) katika karaha (ya kuzuru makaburi) je ni karaha Tahriim au ni karaha Tanzih? Wengi wao wameruhusu (wanawake wazuru makaburi) kama hakutakuwa na fitna.[84]

Ya Pili : Hapo kabla imetangulia hadithi ya Bibi Aisha kwamba, Mtume[s.a.w.w] ameruhusu kuzuru makaburi. Rejea hadithi namba 4. Lau ruhusa hii ingewahusu wanaume peke yao, basi ingekuwa lazima kwa Bibi Aisha kulitaja jambo hilo hasa kwa kuwa yeye mwenyewe ni mwanamke, na pia lilikuwa ni jambo Ia kawaida kwa wanawake kuwepo katika msikiti wa Mtume[s.a.w.w] na kila aliyekuwa akisikia hotuba ya Mtume, alikuwa akifahamu kuwa kila hukmu (inayotolewa na Mtume) inamuhusu isipokuwa kama Mtume atabainisha wazi kutowahusisha wengine.

Ya Tatu : Pia imetangulia hadithi hapo kabla ya kuwa, Mtume[s.a.w.w] alimfundisha Bibi Aisha maneno yanayopaswa kusemwa wakati wa kuzuru makaburi, naye Bibi Aisha alikuwa akiyazuru makaburi baada ya Mtume[s.a.w.w] kufariki. Rejea hadithi namba 5.

Ya Nne : At-Tirmidhi anapokea hadithi kuwa; Abdur-Rahman bin Abubakr (nduguye Bibi Aisha) alipokufa huko Al-junta, waliubeba mwili wake hadi Makka na wakamzika hapo hapo, Bibi Aisha alipokuja Makka kutoka Madina alitoka kwenda kuzuru kaburi la nduguye na akasoma beti mbili za mashairi kuomboleza kifo cha nduguye.[85]

Aliyesherehesha Sahih At-Tirmidhi Al-Hafidh Ibnul-Arabi aliyezaliwa mwaka 435 Hijiriya na kufariki mwaka 543 anasema: "Iliyo sahihi ni kwamba, Mtume[s.a.w.w] aliwaruhusu wanaume na wanawake wayazuru makaburi, na yule asemaye kuwa ni karaha (wanawake kuzuru makaburi) hiyo ni kwa sababu ya woga walionao na uchache wao katika kusubiri au ni kwa kukosa kwao wanawake kuvaa hijabu."

Ya Tano : Bukhari anapokea kutoka kwa Anas kwamba yeye Anas amesema: "Siku moja Mtume[s.a.w.w] alipita akamkuta mwanamke analia kwenye kaburi, Mtume akamwambia mche Mungu na uwe na subira. Yule mwanamke akasema niondokee hapa hakika wewe hukufikiwa na msiba wangu, (na wala mwanamke huyu hakumtambua Mtume[s.a.w.w] . Baadaye yule mama akaambiwa, "Huyo ndiye Nabii", basi akaja nyumbani kwa Mtume akasema; "Nilikuwa sikukufahamu". Mtume akasema; "Hakika subira iliyotimia iko mwanzoni wa msiba unapokupata ". [86] Kama kuzuru makaburi itakuwa ni haramu, Mtume angemkataza mwanamke yule kuzuru makaburi, lakini utaona kwamba Mtume anamuusia mwanamke yule kumcha Mungu na kusubiri wakati wa msiba, wala hamkatazi kuzuru makaburi.

Ya Sita : Bibi Fatma az-Zahraa ambaye ni Binti ya Mtume[s.a.w.w] alikuwa akitoka kila wiki mara moja au zaidi kwenda kulizuru kaburi la Bwana Hamza ambaye ni Ami yake Mtume[s.a.w.w] , na akiswali kaburini hapo na kulia. [87]

Ya Saba : Al-Qurtubi anasema: "Mtume[s.a.w.w] hakumlaani kila mwanamke anayezuru makaburi, bali amemlaani mwanamke ambaye anazuru makaburi mara kwa mara mfululizo, na dalili ya kuthibitisha hilo ni kauli ya Mtume aliyoitumia "Zuwwaratul-Quburi" na tamko Zuwwaaru ni tamko Ia Mubalagha na linajulisha kukaririka mara kwa mara". Na huenda sababu ya kulaaniwa wanawake wanaozuru makaburi mara kwa mara mfululizo ni kwamba, wingi huo wa ziyara unapelekea kupoteza haki ya mume na pia kumsababishia mwanamke huyo kuwa ni mwenye kudhihirisha mapambo yake jambo ambalo limekatazwa, na atakuwa (pengine) ni mwenye kulia kwa sauti ya juu. Lakini iwapo ziyara ya wanawake makaburini itakuwa haina mambo yaliyoharamishwa hakuna ubaya ndani yake kabisa, kwani kukumbuka mauti na akhera ni katika mambo ambayo wanaume na wanawake wanayahitajia wote sawa kwa sawa.

Ya Nane : Kuzuru makaburi licha ya kupelekea (kumfanya mtu) kiipa nyongo dunia na starehe zake, pia kunamnufaisha maiti aliyelala chini ya rundo la udongo, kwani kwa kawaida ziyara makaburini inaambatana na kusomwa Suratul-Fatiha na kuizawaidia roho ya maiti (aliyekusudiwa). Na zawadi hii ndiyo zawadi bora aitoayo mtu aliye hai kuipa roho ya marehemu. Anasimulia Ibn Majah kwamba imepokewa kwa Mtume[s.a.w.w] amesema: "Wasomeeni Surat Ya'asini maiti wenu ". [88] Basi iko wapi tofuati kati ya mwanamume na mwanamke katika jambo hili ili ziyara ya mmoja wao iwe inafaa na ya mwingine ni haramu, kama visingekuwepo vitu maalum vilivyoharamishwa ambavyo vimetajwa hapo juu? Na sasa baada ya kuthibitisha kwamba inajuzu kuzuru makaburi, umefika wakati wa kuzungumzia athari nzuri na matokeo mazuri ya kuzuru malazi (makaburi) ya mawalii wa Mwenyezi Mungu. Hayo tutayaleta katika sehemu inayofuata.

lliyochapishwa pamoja na sherehe ya Ibn Al Arabi Al Maliki. Tirmidhi anasema baada ya kuinakili hadithi hii kutoka kwa Buraidah "Hadithiya Buraidah ni Sahihi na inatumika kwa wanachuoni, na wala hawaoni ubaya wowote kuyazuru makaburi, na hiyo ndiyo kauli ya Ibn Al-Mubarak na Shafii na Ishaq." Na kuhusiana na sehemu hii ni bora kuzirejea zifuatazo:

(1.) Sahih Muslim, Juz 3, Babu is-Tiidhanin-Nabi Rabbahu azza wajalla Fi Ziyarat Qabri ummih, uk. 65.

(2.)Sahih Abu Dawood. Juz. 2, Kitabul-Janaiz Babu Ziyaratil-Qubur uk. 195.

(3.) Sahih Muslim, juz. 4, Kitabul-Janaiz Babu Ziyaratil-Qubur, uk. 73.

Nasema kwamba, sababu wanayoitaja kwa Mtume[s.a.w.w] kuomba ruhusa ya yeye kuzuru kaburi la mama yake ni (kama wanavyodai) kwamba, mama yake Mtume alikuwa mushriki lakini ukweli usio na shaka ni kwamba mama yake Mtume[s.a.w.w] alikuwa kama walivyokuwa babuzake Mtume[s.a.w.w] yaani alikuwa miongoni mwa watu wa Tauhid na Imani, kwa ajili hii mtazamo huu na tafsiri hii inakhalifu kabisa misingi ya aqida ya Kiislamu na inawezekana ikawa na tafsiri nyingine.