• Anza
  • Iliyopita
  • 4 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 4075 / Pakua: 3010
Kiwango Kiwango Kiwango
BIBLIA NENO LA MUNGU

BIBLIA NENO LA MUNGU

Mwandishi:
Swahili

BIBLIA NENO LA MUNGU

KIMETUNGWA NA: SEYYID MUHAMMAD MAHDI HUSAINI SHIRAZI

KIMEFASIRIWA NA: SEYYID MUHAMMAD MAHDI MUSAWY SHUSHTANI

KIMETOLEWA NA: BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

P.O. BOX 20033

DAR ES SALAAM

Tanzania

DIBAJI

Hii ni tafsiri ya Kijitabu Kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, Kilichoandikwa na Ayaatullah Seeyyid Muhammed Mahdi Shirazi wa Karbala. Tafsiri yenyewe ilifanywa na Seyyid Muhammed Mahdi Shushtari wa Unguja. Sura nyingi Zilichapishwa kwa mfulizo katika gazeti letu. Sauti ya Bilal na zilipendeza sana. Sasa kijitabu hiki kimechapishwa ili Kuwarithisha zaidi wasomaji wetu. Hatuna budi kutamka hapa kuwa mujibu wa imani yetu, Mitume wote waalikuwa wametumwa na Mwenyezi Mungu Kuwaongiza watu katika njia iliyo sawa. Waalifanya hivyo kwa kuhubiri wema wao mkuu na kwa matendo yao maadilifu.

Kufanya hivyo iliwapasa wawe waongofu zaidi, waadilifu na kuwa wakamilifu katika uchaji wao kwa Mwenyezi Mungu. Wasingeweza kusema uwongo iwapo wao walifundisha watu kusema kweli.Wasingeweza kumwomba Miungu, iwapo wao waliwataka watu kumwomba Mungu Aliye Mmoja tu, na kadhalika. Hata hivyo, Biblia inasingizia zote za maovu na madhambi kwa Mitume hao. Ama viongozi wa Kiyahudi na Wakristo walikuwa na madhambi makubwa kabisa, la sivyo, basi ni makosa ya Biblia yenyewe (inayoaminiwa kuwa si maandishi ya Musa wala Isa a.s) Kwa hiyo, ni juu ya msomaji mwenyewe kuteua yapi yanayomfaa na yapi yasiyomfaa.

Syed saeed Akhtar Rizvi

MUNGU WA BIBLIA

Je, wewe unaona huyu Mungu wa Biblia ni wa namna gani? Kama Mungu nao mwili, nywele na vazi, anaishi katika mahala, hajui kitu kilichofichika nyuma ya mti, anadanganya watu, huvunja ahadi yake, je binadamu yukoje?

Swali : Ati Mwenyezi Mungu ana sura ya binadamu?

Jibu : Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha kwanza kiitwacho Mwanzo, Sura ya 1, aya ya 26 na 27, Imeandikwa hivi: "Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, Kwa sura yetu, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, Kwa mfano wa Mungu na Mungu alimwumba, Mwanamume na Mwanamke aliwaumba. "

Swali : Ati Mwenyezi Mungu anazo nywele? Anacho kivazi?

Jibu : Sivyo kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha Danieli, Sura ya 7, Aya ya 9, imeandikwa hivi:

"Ni katazama hata viti vya enzi vikawekwa, na Mmoja aliye mzee wa siku (Mwenyezi Mungu) ameketi, Mavazi yake yalikuwa meupe kama theeluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi .

Swali : Ati Mwenyezi Mungu anayo miguu miwili?

Jibu : Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha kutoka sura ya 24, aya ya 10, Imeandikwa hivi:

"Wakamwona Mungu wa Israeli: chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi Nao wakamwona Mungu, Wakala na kunywa. "

Swali : Ati Mwenyezi Mungu ana pahala ambapo anaonekana?

Jibu : Sivyo kamwe. Lakini Biblia katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Sura ya 4, aya ya 2, Imeandikwa hivi:

"Na mara nalikuwa katika Roho: na tazama, Kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kiti: na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe laq yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi. "

Swali : Ati Mwenyezi Mungu hutembea?

Jibu : Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia kitabu cha kwanza kiitwacho Mwanzo, sura ya 2,aya ya 8, imeandikwa hivi:

"Kisha wakasikia (Adamu na mkewe) sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga: Adam na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. "

Swali : Ati Mwenyezi Mungu hutembea?

Jibu : Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha Pili kiitwacho kutoka, sura ya 19, aya ya 20, imeandikwa hivi:

"Bwana akaushukia mlima, Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima: Musa akapanda juu. "

Swali : Ati Mwenyezi Mungu huteremka juu ya wingu na anakwenda mbele ya mtu?

Jibu : Sivyo kabisa Biblia kitabu cha pili kiitwacho "KUTOKA" katika sura ya 34 aya ya 5 na 6, imeaandikwa hivi:

"B wana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitantaza jina la Bwana. Bwana akapita mbele yake. "

Swali : Ati Mwenyezi Mungu huchagua mahala pa kukaa yeye?

Jibu : Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia kitabu cha Zaburi ya 132, aya 13, imeandikwa hivi:

"kwa kuwa Bwana ameitamani akae ndani yake."

Swali : Ati Mwenyezi Mungu mjinga? Hapambanui kati ya milango ya wenyekuamini na makafiri ila kwa alama?

Jibu : Sivyo Kabisa. Lakini Biblia kitabu cha pili, Kiitwacho, KUTOKA, sura ya 12. aya ya 12 na 13, meandikwa hivi:

"Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wamwanadamu na wanyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri."

Swali : Ati Mwenyezi Mungu hawezi kujua kwamba mtu amejificha katika mti? Vile vile hajui nani amemfundisha binadamu?

Jibu : Sivyo kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo sura ya 3, aya 9-11, imeandikwa hivi:

"Bwana na Mungu akamwita Adamu, akamwambia uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi :nikajifificha." Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa uchi?

Swali : Ati Mwenyezi Mungu anavunja ahadi zake?

Jibu : Sivyo kabisa. Kuvunja ahadi ni aibu kubwa. Lakini Biblia katika kitabu cha kwanza cha cha Samweli, Sura ya 2, aya ya 30 na 31, imeandikwa hivi:

"Kwa sababu hiyo,Bwana, Mungu wa Israel, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele:lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbalinami Angalia, Siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbali ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwa mzee ."

Mungu yu mbali na uzushi huu juu yake. Kama vile, a ti aliwahidi Eli kwamba ukuhani wake ulikuwa wa maisha juu yake na wanawe, lakini baadaye hayo hayakutekelezwa.

Na vilevile katika sura ya 13,aya 13 imeandikwa hivi:

"Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele. Lakini sasa ufalme wako hautadumu."

Mungu yu mbali na uzushi huu juu yake kama vile, Ati alimwahidi Sauli Ufalme wake kuwa imara milele, na baadaye akavunja ahadi na akampa ufalme mtu mwingine:

Swali : Ati upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu?

Jibu : Sivyo Kabisa. Mwenyezi Mungu si mpumbavu kamwe, basi vipi itakuwa upumbavu wake una hekima zaidi ya wanadamu: Lakini Biblia katika waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho, sura ya kwanza, aya ya 25, imeandikwa hivi:

"Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu. "

Swali : Mwenyezi Mungu hujuta akisha tenda jambo?

Jibu : Sivyo Kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha kwanza cha Samweli, Sura ya 15, aya ya 10 na 11, Imeandikwa hivi:Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, Kusema, "najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe Mfalme.

Swali : Ati Mwenyezi Mungu husikitika na kuwa na majonzi kwa kitendo alichofanya?

Jibu : Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia kitabu cha Mwanzo, Sura ya 6, aya ya 6 na 7, imeandikwa hivi:

Bwana akaghairi kwa kuwa amefanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. Bwana akasema, Nitamfuatilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi.

Swali : Ati Mwenyezi Mungu hushinda mweleka na mtu?

Jibu : Sivyo kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo, sura ya 32, aya ya 24 na 28, imeandikwa hivi:

Yakobo akakaa peke: na mtu mmoja akaashindana naye mweleka hata alfajiri.. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, Ila Israeli, Maana unashindana na Mungu.

Swali : Ati Mwenyezi Mungu husema uwongo halinyoka husema kweli?

Jibu : Sivyo Kabisa. Lakini Biblia Katika kitabu cha Mwanzo, sura ya 3, aya ya 3 hadi ya 6 , imeandikwa hivi:

Lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema , msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na baya.

Baadaye imeelezwa kwamba Adamu na Hawa baada ya kula matunda ya mti huo, wakawa huko yameelezwa mambo ambayo si shani ya Mwenyezi Mungu kuambiwa hi vyo.

Swali : Ati Mwenyezi Mungu hushuka kutoka mbinguni ili kuchafua umoja wa watu ili wasisikilizane kwani anaogopa umoja wao?

Jibu : Sivyo, sivyo kabisa mara elfu. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanza, Sura ya 11, aya ya kwanza hadi 9, imeandikwa hivi:

Nchi yote ilikuwa na na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambalale katika nchi ya Shinari: waakakaa huko. Waliambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni tujifanye jinaa: ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha moja : na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno Wanalokusudia kulifanya, Haya, na tushuke huko huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno yao. Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni paa nchi yote: wakaacha kujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Baabeli.

Swali : Ati Mwenyezi Mungu husema kitu baadaye akafanya mengine?

Jibu : Sivyo Kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo, Sura ya 6, aya ya 3, inasemaa hivi:

Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na wanadamu milele kwa kuwa yeye naye ni nyama: basi siku zake zitakuwa miakaa mia na ishirini.

Hayo yalikuwa mwanza wa kuumba Binadamu, hebu tutazame, Mungu alifuata ahadi yake? Biblia inasema Mungu aligeuza maneno yake, Kwa hivyo watu wengi waliishi juu ya umri alioahidi Mungu. Kwa mfano, imeandikwa katika Mwanzo, Sura ya tisa, aya ya ishirini nia nne (mwa 9:28), kwamba:

Na Nuhu akaishi baada ya ile ghaarika miaka mia tatu na hamsini. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafaa.

MITUME WA BIBLIA NABII ISA

Mitume waalitumwa kufundisha watu wema na ukweli. Mitume wa Biblia wanasema uwongo.

Swali : Ati Yesu (Isa a.s) husema uwongo?

Jibu : Sivyo, Kamwe: Lakini katika Biblia, Injil ya Yohana Mtakatifu, Sura ya 7, aya ya 2-3, Inasema hivi:

Na sikukuu ya Waayahudi, Sikukuu ya vibanda ili kuwaa karibu. Basi ndugu zake wakamwambia, ondoka hapa, uende hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaaye nena kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhi hirishe kwa ulimwengu. Maana ana hata nduguze hawakumwamini. Basi Yesu akamwambia, Haujaafika bado wakati wenu siku zote upo. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi: kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. Kweni ninyi kwenda kula sikukuu: Mimi si kweli bado kwenda kula sikukuu hii: kwa kuwaa haujatimia wakati wangu. Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vibi hivi huko Galiliya. Hata ndugu zake walipokwisha kuwa kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.

Swali : Ati Yesu (Isa a.s.) hutengeneza mvinyo, na anaweza kuwanywesha Masahaba wake?

Jibu : Sivyo, sivyo kabisa. Lakini katika Biblia inasema hivyo, na isitoshe hayo inasema kuwa ndio ufunguo wa Utume wake, na ndicho kitu alichotumia hadi akaaga dunia: Usiseme, hivyo huenda ikawa katika madhehebu ya Yesu (Isa a.s) pombe kuwa halali. Naogopa Mungu kwa masingizio hayo, kwani Agano jipya zinabainisha uharamu wa mvinyo. Basi kwanza tueleze wazi amri ya uharamu wa mvinyo katika Biblia na baadaye tueleza masingizio juu ya Yesu (Isa a.s) Katika Biblia kitabu cha Hosea, Sura ya nne, aya 10 na 11 imeandikwa hivi:

Nao watakula, lakini hawatashiba: watafanya zinaa, lakini hawataongezeka:kwa sababu wameacha kumwangalia Bwana. Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.

Vile vile katika Isaya sura ya 5 , aya 11 na 12 na 13 li Nasema hivi:ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo, wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo umewaka kama moto ndani yao:

Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo zote ziko katika karamu zao: Lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa.

Katika kitabu cha kumbukumbu la Torati, sura 21, aya ya 18-21, inasema hivi:

Mtu akiwa na mwana Mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikilizi, ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake: wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu hasikizi sauti yetu: Ni mwasherati, na tena ni Mlevi Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe: ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako : na Israeli wate watasikia na kuogopa.

Katika kitabu cha luka, sura ya 7, aya ya 33 na 34, Inasema hivi:

Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. Mwana wa Adamu amekuja, ana kula na kunywa: nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.

Katika kitabu cha Yohana Mtakatifu, sura ya pili, aya ya 1-11, inasema hivi:

Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko kana, mji wa Galilaya: naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pomoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni.

Basi kulikuwapo huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, Sasa tokeni mkampeleka. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale mali yaliyopata kuwa divai , (wala asijue ilikotoka, Lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu za meza alimwiita bwana arusi akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema: hata sasa.

Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. Jambo hili linadhihirisha kwamba kunywa mvinyo haikuwa inafikiriwa kuwa mwiko katika dini kwa mujibu wa Agano jipya. Angalia jinsi Isa (Yesu) alivyotengeneza mvinyo akiwaambia wengine wainywe. Tukio lingine:

Katika kitabu cha Luka Mtakatifu, Sura 22, aya 14-18 inasema hivi:

Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale miyume (kumi na wawili) pamoja naye. Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu: kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimiwa katika ufalme wa Mungu. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki mgawanye ninyi kwa ninyi: Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja.