5
MAISHA YA BIBI KHADIJA
SURA YA SABA
WAPAGANI WALIWATESA WAISLAMU
Ingawa Abu Lahab mara kwa mara alifaulu kuwasambaza watu waliokusanyika kusikiliza ujumbe wa Uislamu, taarifa hiyo ilienea Makka. Watu walizungumza habari za ujumbe wa Uislamu. Wenye mawazo mazuri miongoni mwao waliuliza: "Hii ni dini gani ambayo Muhammad anatuita tuingie?" Swali hili lilionyesha udadisi na baadhi yao walitaka kujua zaidi kuhusu Uislamu.
Katika siku zilizofuata, Muhammad, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alijaribu mara nyingi kuhubiri kwa wakazi wa Makka. Abu Lahab na mwenzake Abu Jahl, walifanya kila walivyoweza kuhujumu kazi yake lakini hawakuweza kumpoteza kutoka kwenye lengo lake.
Huu ulikuwa ujumbe mpya ambao Muhammad aliuleta kwa Waarabu, na ulikuwa wa pekee. Hakuna mtu yeyote ambaye alipata kusikia mfano wake kabla ya hapo. Kama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Muhammad aliwaambia wasiabudu vitu visivyo kuwa na uhai ambavyo wao wenyewe walivichonga, na ambavyo havikuwa na uwezo wa kuwapa wao kitu chochote au kuwaondolea kitu chochote, na ambavyo wao walivipa hadhi ya miungu wa kiume na wa kike. Aliwaambia badala yake waelekeze mapenzi na utii wao kwa Mwenyezi Mungu, Mola Aliye Pekee wa ulimwengu wote. Pia aliwaambia kwamba mbele ya Yeye-Muumba - wote walikuwa sawa, na kama wote wangekubali kuwa Waislamu, wote wangekuwa ndugu wa kila mmoja wao. Lakini ibada ya masanamu ilikuwa ni "tamaa kuu" ya zamani kwa Waarabu na hawakuwa tayari kuyatupa masanamu yao. Hawakupenda karipio la Muhammad dhidi ya masanamu, na walimwonyesha hasira zao waziwazi.
Pia Muhammad aliwaambia Waarabu matajiri kugawana utajiri wao na mafukara na wasiojiweza. Alisema, masikini walikuwa na haki ya kugawiwa mafungu wanayostahiki kutoka kwa matajiri. Aliendelea kusema kwamba mgao huo, ungekuwa dhamana ya kila mtu kupata mgao sawa katika jamii. Waarabu wengi wa Makka walikuwa wakopeshaji wa pesa. Walitajirika kwa sababu ya kukopesha masikini kwa kuwatoza riba ya juu sana. Masikini hawakuweza kulipa madeni yao kwa hiyo walikuwa watumwa wa kudumu wa kiuchumi. wakopeshaji hawa walineemeka kwa riba kama wanyonya damu wanavyoneemeka kwa damu. Kugawana utajiri uliopatikana kwa njia haramu na watu hao hao waliowanyonya, kwao ilikuwa "kufuru." Kwa kuwashauri kwamba wagawane utajiri wao na masikini, Muhammad amewachokoza maadui.
Pia Muhammad alitaka kuiweka jamii ya Kiarabu kwenye mpangilio mwingine. Imani mpya ambayo aliifundisha kwa madhumuni hayo, ili-fanya Imani badala ya damu, kuwa "kiungo muhimu" kwa jamii. Lakini Waarabu walilelewa kwenye desturi na mila za kipagani; waliamini katika misingi ya kikabila na mpangilio wa undugu. Kwao "Damu" uny-onyaji ulikuwa ndio njia pekee inayofaa kuwa msingi wa kupangilia jamii. Kwa utambuzi wao, kama Imani iliruhusiwa kushika nafasi ya Damu katika mfanano huu, ingeharibu mpangilio mzima wa jamii yote ya Kiarabu.
Lakini Muhammad alikuwa hapendelei sana katika mfumo wa "jamii ya Kiarabu". Lengo lake ilikuwa kuanzisha na kuimarisha "jamii ya Kiislamu", ambayo kiungo chake ni Imani si Damu. Kwa hiyo, kwa uan-galifu aliendeleza na kupanga ukombozi, uwezo wa miujiza ya Imani. Philip K. Hitti Kwa kuifanya dini iwe ndiyo mbadala kwa muunganisho wa damu wa karne nyingi, kama msingi wa mshikamano wa jamii, kwa kweli ulikuwa ni ujasiri wa ukamilishaji wa kwanza wa Mtume nchini Arabuni.
(Islam, A way of Life). Kwa Waarabu, mawazo hay a yote yalikuwa mapya na yasiyojulikana; hakika yalikuwa ya kimapinduzi. Kwa kuhubiri fikira za kimapinduzi kama hizi, Muhammad aliikasirisha serikali ya zamani. waliokasirika sana, na imara sana katika serikali hiyo ya zamani, ni ukoo wa Banu Umayya wa Quraysh. Wajumbe wake (wa serikali hiyo) walikuwa wanaongoza katika ualaji riba na Mabepari wakubwa wa Makka, na hao walikuwa makuhani wakuu wa mahekalu ya kipagani. Walimwona Muhammad na ujumbe wa Uislamu kama tishio kwa mfumo wao wa kijamii ambao uliendeshwa katika misingi ya upendeleo, kitabaka na mabavu. Kwa hiyo, fikira zake zilichukiwa sana na wao, na waliamua kumzuia asibadili hali kama hiyo. Phili K. Hitti.
"Quraysh hususani ukoo wake wa Umayya, ambao ndio waliokuwa waangalizi wa Kaaba na kisima cha Zamzam, wamiliki wa misafara ya biashara na mabwana wa serikali ya wachache ya jiji la Makka, walikuwa na sababu maalum kumkabili Muhammad. Mahubiri mapya labda yangeharibu hija kwenye Al- Kaaba, ambayo ilikuwa chanzo chao cha mapato baada ya biashara. Aidha, (Muhammad) aliyewahi kuwa yatima anaanzisha itikadi hizi hatari za kiuchumi kama haki ya madai ya ombaomba na fukara kwenye mgao wa utajiri wa matajiri. Kwa nyongeza, Muhammad alitetea itikadi ya hatari, ambayo itakuwa mbadala wa imani kwa damu kama mfungamano wa kijamii wa uhai wa jumuiya. Kama 'Kwa hakika waumini wote ni ndugu" ...' (Q. 49:10)
ilikuwa inaathiri juu yao, familia yote, ukoo, na umoja wa kika- bila ungedharauliwa na mahala pake kuwekwa umoja wa kidini..." (Islam - A Way of Life).
"Uadui wa Banu Umayya kwa Muhammad na Uislamu ilionyeshwa kwa ukali usio na simile, kwa upande mwingine, kwa sababu ni kitu kili-choibuka, ambacho hakikuzoewa na vizazi vingi vilivyopita. mabadiliko hayo hayakutokea kwa vizazi vingi. Fikira zao ziliishia kwenye vizazi vya upagani. walionyesha upinzani mkubwa kwa Muhammad alipokuwa Makka, na walianzisha vita isiyo suluhishika dhidi ya Uislamu alipohamia Madina." Philip K. Hitti "...kiini cha upinzani, Banu Umayya, waliendelea kuwa wakaidi kwa Muhammad..." (Islam, A Way of Life).
Lakini pia walikuwepo watu wachache ambao waliona mvuto imara kwenye mawazo mapya ambayo Muhammad alikuwa anauanzisha, kwa pamoja unaoitwa Uislamu. Kwa hakika waliyaona mawazo haya kuwa ya kuvutia sana, hivyo wakayaamini. Waliacha masanamu yao na walianza kumwabudu Mwenyezi Mungu - Muumba. Uislamu ulishikilia mwito maalum kwa ajili ya tabaka za chini mjini Makka; kwa ajili ya wale waliokuwa "masikini na dhaifu." Watu wa tabaka hizi walipoanza kuingia kwenye Uislamu, pia walitambua kwamba walipokuwa Wapagani walidharauliwa na kukataliwa na tabaka za juu za Makka, lakini Uislamu uliwapa heshima mpya. Kwenye Uislamu waliona fahari mpya nafsini mwao.
Watu wengi waliosilimu mwanzoni walikuwa "masikini na wanyonge." Lakini walikuwepo pia Waislamu wachache ambao walikuwa matajiri kama Hudhayfa bin Utba na Arqam bin Abil-Arqam. Na watu wote wale ambao Abu Bakr aliwaleta kwenye Uislamu, kama vile Uthman, Talha, Zubayr Abdur Rahman bin Auf, Sa'ad bin Abi Waqqas na Abu Ubaidah Aamir bin al-Jarrah, pia walikuwa matajiri. Walikuwa katika koo mbalimbali za Quraysh.
Tunaweza kufikiria kwamba, mwanzoni, wapagani makabaila wa Makka walishuhudia juhudi za Uislamu ulivyokuwa unatambuliwa, kwa shangwe zaidi na si kwa maudhi, bila kutaja chuki na jazba iliyowaingia baada ya muda mfupi. Lakini; jinsi harakati ilivyozidi kupataa kasi, walihisi kwamba fikira ambazo Muhammad alikuwa anazitangaza kwa hakika zilikuwa za "hatari" na kwamba sio mchezo. Walihoji kwamba babu zao waliabudu masanamu, vizazi na vizazi, kwa hiyo ibada ya masanamu ilikuwa sahihi, na walikataa kuiacha kwa sababu Muhammad aliishutumu. Lakini Muhammad hakutosheka na kushutu-mu tu ibada yao hiyo, bali jambo la hatari na kuogofya kwa ukoo wa Umayya, ilikuwa zile fikira zake za kiuchumi na haki sawa kwa jamii ambazo ndizo zilizotishia kuvunja ngome ya wao kujipendelea; na kuvunjika kwa mfumo wao wa utendaji dhambi wa ukiritimba, kubo-moa muundo wa zamani wa mamlaka na utawala msonge; na kuvunjilia mbali taasisi zote za zamani. Kwa hiyo, waliweka wazi kwamba fursa ya upendeleo ni kitu ambacho kamwe hawatakiacha - iwe vyovyote iwavyo.
Lakini wazo moja ambalo mamwinyi waliojitawalisha wenyewe wa kabila la Quraysh waliloliona la kuchukiza mno ilikuwa ni ile "dhana" iliyoendelezwa na Muhammad; kwamba watu wanaokandamizwa, kud-harauliwa, walikuwa sawa nao - usawa wa hali ya juu na ukubwa wa Maquraysh! Na lilo la kuchukiza zaidi kwao ni wazo la kwamba, mtumwa anapokubali Usilamu, kwa hakika anakuwa bora zaidi kuliko wakuu wote na mamwinyi wa Quraysh. Kawaida ya maisha yao ilikuwa ni kiburi na fahari; na usawa na watumwa wao wenyewe, waliokuwa watumwa na wateja, ni jambo ambalo halifikiriki kwao. Walijazwa na wenda wazimu wa utukufu wao wenyewe na "ubora" kuliko wanadamu wote. Usawa na udugu wa watu, kwao ilikuwa fikira ngeni na ya kuchukiza kwao. Kwa kutangaza itikadi ya usawa; imani yenye kufuatwa tofauti na wingi wa watu - usawa wa mtumwa na bwana wake, masikini na tajiri, na Waarabu na wasio Waarabu na kukataa madai ya ubora wa undugu wa damu. Muhammad ametenda uhaini dhidi ya Maquraysh! Maquraysh waliabudu masanamu mengi sana na utaifa ilikuwa mojawapo.
Lakini, ufahari wa kitaifa haukubaliwi na Qur'ani Tukufu ambayo inatamka kwamba mwanadamu alitokana na Adamu na Adamu alikuwa konzi mmoja tu ya vumbi. Ibilisi (Shetani) amekuwa mlaaniwa kwa usahihi kwa sababu alihoji kuhusu ukuu wa kuumbwa kwake kinyume na alivyo fikiri kwamba chanzo cha kuumbwa Adamu ni cha daraja la chini. Alisema: "Mtu aliumbwa kutokana na udongo ambapo mimi nil-iumbwa kutokana na moto." Tabia hiyo yakibaguzi ambayo pia ime-wakumba binadamu kwa sababu ya utashi wa kudai ubora wa damu, umekataliwa na Uislamu.
قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ ﴿٧٦﴾ قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ ﴿٧٧﴾ وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِي إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٧٨﴾
"Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika. Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo. " (Qur'an 38:76-78).
Uislamu umeivunja hoja ya umuhimu wa rangi ya ngozi, utaifa na upen-deleo, na unawakataza Waislamu kuwagawa watu kwenye makundi katika misingi ya damu, na au ujirani wa kijiografia au upendeleo fulani ambao wanaweza kudai. Qur'ani imemsifu mtu ambaye ni Muttaqi - yaani mja anayempenda na kumtii sana Mwenyezi Mungu. Katika Uislamu, mtihani pekee wa ubora wa mtu, ni mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu. Mitego mingine yote ya maisha ya mtu binafsi haina maana yoyote.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿١٣﴾
"Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye Mcha Mungu zaidi katika ninyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari." (Qur'an 49:13).
Lakini kama ilivyoonyeshwa hapo juu, Maquraysh wa Makka hawakuwa katika hali ya kuzipokea fikira kama hizo. Labda hawakuwa na uwezo wa kiakili kuweza kuzielewa. Walizifikiria kama maneno ya kukufuru. Ndipo walipoamua kumpinga Muhammad, Mtume wa Uislamu(s.a.w.w)
na kuangamiza "uasi" ulioitwa Uislamu, kabla ya kuimarika na kuwa na nguvu. Uamuzi wao haukueleweka vizuri kwa ukaidi, tamaa ya mali, wazimu wa kujiona wanaonewa kila wakati, na utambuzi wa upofu. Walisukumwa na majivuno yao - fahari ambayo yenyewe hushinikiza nje ya mipaka ya vipimo vya ubinadamu na kwa kupenda kwao sana mali kuweza kufikia uamuzi wa namna hiyo dhidi ya Muhammad na Uislamu.
Baada ya kufanya uamuzi huu, Maquraysh walitangaza nia yao ya kupi-gana kwa lengo la kutetea masanamu na miungu ya uongo, mpangilio wao wa kiuchumi na kijamii ambao ulikuwa unawahikikishia hali ya wao kuendelea kupendelewa. Makka ilikuwa katika hali ya vita!
Maquraysh walianza kampeni dhidi ya Uislamu kwa kuwanyanyasa na kuwatesa Waislamu. Mwanzoni mateso dhidi ya Waislamu yalikuwa matusi, kuzomewa na dhihaka, lakini baada ya kupita muda, Maquraysh waliacha kuwatesa Waislamu kwa maneno - walianza mateso ya viten-do. Walidhani kwamba kutumia nguvu wangeangamiza au angalau wangeidhoofisha imani ya Waislamu. Hawakutaka kumjeruhi Muhammad binafsi kwa kuogopa kisasi cha Waislamu lakini hawakuwa na vipingamizi katika kudhuru safu ya Waislamu. Kwa kipindi kirefu, walikuwa ni Waislamu ambao walichoshwa na nguvu kuu ya chuki kubwa na hasira kubwa ya Maquraysh. Muhammad bin Ishaq.
"Halafu Maquraysh waliwachochea watu wawatese Masahaba wa Mtume ambao walisilimu. Kila kabila liliwapiga Waislamu na kuwashawishi warudi kwenye upagani. Mungu alimpa ulinzi Mtume Wake kwa kumtumia (Abu Talib), ambaye baada ya kuona vurugu za Maquraysh aliwaita Bani Hashim na Bani Al-Muttalib kusaidiana naye katika kumlinda Mtume. Walikubali isipokuwa Abu Lahab." (Life of the Messenger of God). Miongoni mwa waathirika wa mateso walikuwa: ? Bilal, Muethiopia (Mhabeshi) aliyekuwa mtumwa wa Umayya bin Khalaf. Mtu huyu aliteswa hadharani na Bwana wake akiwa na waabudu masanamu wenzake, walimtesa kuzidi kiwango cha kuvumiliwa na binadamu. Lakini alitiwa nguvu na imani na hakutetereka.
Kwa sababu ya kumpenda Mwenyezi Mungu na mjumbe Wake, Bilal alivumilia maumivu ya mateso kwa matumaini. Abu Bakr alimnunua Bilal na akamwacha huru. Wakati Mtume wa Mungu na wafuasi wake walipohamia Madina, alimteua Bilal kuwa muadhini wa kwanza katika Uislamu. Sauti yake nzito na nyenye nguvu ilivu-ma kwenye anga ya Madina iliyosema: Allahu-Akbar (Mungu Mkubwa). Baada ya ushindi wa rasi (ya Arabuni) kukamilika, Mtume alimteua Bilal kama katibu wake wa hazina. ? Khabab bin el-Arat Alikuwa kijana wa miaka 20 aliposilimu.
Alikuwa mmoja wapo wa ukoo wa Bani Zuhra. Maquraysh wal-imtesa mara nyingi hadi alipoamua kuhamia Madina pamoja na Mtume wa Uislamu? Suhaib bin Sinan. Suhaib alikuja Makka kama mtumwa. Aliposilimu, Bwana wake alimpiga sana lakini hakuivunja imani yake? Abu Fukaiha, aliyekuwa mtumwa wa Safwan bin Umayya. Alisilimu pamoja na Bilal. Kama alivyo fanyiwa Bilal yeye pia alifungwa kamba miguuni mwake na kuvutwa kwenye mchanga wenye joto. Abu Bakr alimnunua na kumpa uhuru. Alihamia Madina lakini ali-fariki dunia kabla ya vita ya Badr.
Lubina alikuwa mtumwa mwanamke wa Bani Mumil bin Habib. Amin Dawidar anaandika katika kitabu chake: "Pictures from the life of the Prophet" (Cairo, 1968,) kwamba Umar bin Khattab, aliyekuja kuwa Khalifa wa Waislamu, alimtesa, kila alipopumzika, alisema: "Nimeacha kukupiga si kwa sababu ya kukuhurumia, isipokuwa ninapumzika." Alipotosheka kupumzika aliendelea kumpiga tena. Abu Bakr alimnunua na alimuacha huru.
Zunayra alikuwa mtumwa mwingine wa kike. Alipotangaza kwamba amesilimu, Umar bin al-Khattab na Abu Jahl walimtesa kwa zamu. Waliendelea kumtesa hadi akawa kipofu. Amin Dawidar anasema kwamba miaka michache baadae alianza kuona tena, na Maquraysh walilihusisha tukio hili na "uchawi" wa Muhammad. Abu Bakr alimnunua na alimuacha huru.
Nahdiyya na Umm Unays walikuwa watumwa wengine wa kike ambao waliteswa na mabwana zao kwa sababu ya kusilimu. Yasemekana Abu Bakr aliwanunua na kuwaacha huru. Muhammad Husayn Haykal Abu Bakr aliwanunua watumwa na wateja wengi ambao walikuwa wanateswa na makafiri. Miongoni mwao, Abu Bakr alimnunua mtumwa mwanamke kutoka kwa Umar bin Khattab kabla hata haja sil-imu. Mwanamke mmoja aliteswa hadi kufa kwa sababu ya kusilimu. (The Life of Muhammed, Cairo 1935) Walikuwepo Waislamu wengine ambao ingawa hawakuwa watumwa lakini walikuwa "masikini na wanyonge" na kwa hiyo, walikutana na mateso ya Maquraysh waovu. Mmojawapo alikuwa Abdallah bin Masud. Alikuwa mashuhuri miongoni mwa Masahaba wa Mtume.
kwa sababu alikuwa na ujuzi wa mambo mengi. Inawezekana alikuwa na uzoefu mkubwa wa maadili ya Kiislamu na sheria za Kiislamu kuliko sahaba wengine wengi. Abdullah bin Masud alikuwa miongoni mwa watu waliohifadhi Qur'ani katika Uislamu. Kila ilipoteremshwa Aya, yeye aliihifadhi na kuten-geneza nakala yake ya Qur'an. Nakala hii ilichukuliwa kwa nguvu na kuchomwa na Uthmani bin Affan, khalifa wa tatu, wakati wa utawala wake.
Inasemekana kwamba ilipoteremshwa Sura ya 55 (Sura ya Rahman), Mtume wa Mungu aliwauliza sahaba wake kama nani miongoni mwao ambaye angekwenda Ka'aba na awasomee makafiri. Masahaba wengine waliduwaa lakini Abdullah bin Masud alijitolea. Alikwenda ndani ya Al-Ka'aba na akaisoma sura hiyo mpya kwa sauti. Akifuatiwa na Muhammad Mustafa, Abdullah bin Masud, alikuwa mtu wa kwanza kusoma Qur'ani ndani ya Al-Ka'aba mbele ya kundi la waabudu masana-mu waliokuwa wamechukia. Walimuumiza mara kadhaa lakini hawakuweza kumnyamazisha kwa kutumia vitisho. Muhammad bin Ishaq.
Yahya bin Urwa bin al-Zubayr aliniambia kuwa na yeye alihadithiwa na baba yake kwamba mtu wa kwanza kusoma Qur'ani kwa sauti kubwa Makka baada ya Mtume alikuwa Abdullah bin Masood. (The Life of Messenger of God) "M. Shibli mwanahistoria kutoka India, anasema kwenye kitabu chake "Seera" kwamba Abu Bakr alikuwa sawa na wakuu wengine wa Maquraysh kwa hadhi na utajiri, lakini hakuweza kusoma Qur'ani kwa sauti ndani ya Al-Ka'aba.
Miongoni mwa Masahaba wa mwanzo kabisa wa Muhammad Mustafa alikuwa Abu Dharr al-Ghaffari. Alitokea kwenye kabila la Ghaffar ambalo lilijitafutia riziki yake kwa unyang'anyi. Alisikia kutoka kwa wasafiri kwamba ametokeza Mtume Makka ambaye alihubiri imani mpya iitwayo Uislamu na aliwashawishi watu kuacha kuabudu masanamu na kuanza kumcha Mungu Mmoja tu, kuwapa chakula wenye njaa, kutowakashfu wanawake, na kuacha kuwazika watoto wao wa kike wakiwa hai. Abu Dharr alikwisha tengwa na waabudu masanamu hata kabla hajasikia ujumbe wa Uislamu na kazi ya Muhammad. Kwa hakika aliishi kama mtu anayejinyima anasa, na hakushiriki kwenye vitendo vya uvamizi wa misafara ya biashara na ya mahujaji vilivyofanywa na watu wa kabila lake. Aliishi kama mchunga kondoo.
Abu Dharr alimtuma kaka yake kwenda Makka ili athibitishe taarifa ali-zozisikia kuhusu Muhammad. Kaka yake alikwenda Makka, akakutana na Muhammad akazungumza naye na akamuuliza maswali mengi, alim-sikiliza anasoma Qur'an, alirudi kwao na kumtaarifu Abu Dharr yale aliyoyaona na kusikia. Alimwambia Abu Dharr: "Tayari unafanya mambo mengi ambayo Muhammad anafanya kwa vitendo na kuhubiri." Kama vile nondo anavyovutiwa na mwanga wa taa ndivyo Abu Dharr alivyo vutiwa na nuru ya Imani iliyokuwa inawaka Makka. Alipata shauku ya kumuona Mtume kwa macho yake na kuisikia Qur'an iki-somwa naye aliamua kwenda Makka.
Abu Dharr alikuwa mgeni. Kaka yake alikwisha mwambia kwamba Makka ilijaa chuki dhidi ya Mtume mpya. Kwa hiyo, bila kujua nani rafiki ya Mtume na nani adui ya Mtume, hakutaka kumuuliza mtu yeyote kuhusu yeye. Kwa muda wa siku nzima alikaa kwenye kivuli cha Ka'aba akiwatazama wapita njia. Wakati wa jioni, Ali Abi Talib alipita sehemu hiyo, aligundua kwamba alikuwa mgeni hapo, alimkaribisha aende naye nyumbani kwake wale chakula cha jioni. Abu Dharr alikubali mwaliko huo na baadaye alimfahamisha Ali madhumuni yake ya kutembelea Makka, kwamba alikuwa na nia ya kumuona Mtume wa Uislamu. Kama iliyvo kawaida yake, Ali alifurahi sana kumpeleka rafiki mpya kwa Bwana wake, Muhammad Mustafa.
Abu Dharr alisalimiana na Mtume. Baada ya muda mfupi, Abu Dharr alikubali kwamba mtu huyo alikuwa mjumbe wa kweli wa Mungu. Alisikia ujumbe wa Mungu, Qur'an, kutoka kwa mjumbe wa Mungu na alifundishwa maana ya Uislamu. Aliona kwamba, mjumbe na ujumbe ni vitu visivyopingika. Alipendezwa sana na mvuto wa Uislamu. Hakika, alishangaa, angeishije bila Uislamu. Alisahau maisha yake ya zamani aliyoishi bila Uislamu. Baada ya kusilimu, jambo la kwanza alilofanya Abu Dharr, alionyesha ujasiri waziwazi dhidi ya makafiri wa Makka. Aliingia ndani ya Al-Ka'aba na kusema kwa sauti kubwa: "Hapana Mungu ila Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni Mjumbe wake."
Kama ilivyotazamiwa, makafiri hawakukawia kumwandama, walianza kumpiga. Abbas bin Abdul Muttalib ami yake Mtume, ndiye aliyem-nusuru Abu Dharr kwenye ghasia hii. Aliwaambia Maquraysh kwamba Abu Dharr ni wa ukoo wa Ghiffar ambao makazi yao yapo sambamba na njia ya misafara upande wa kaskazini na kama wangemuumiza, watu wa kabila lake wangefunga njia inayokatiza nchini mwao kwenda Syria. Abu Dharr el-Ghiffari ni mtu anaye sifika sana katika historia ya Uislamu. Alionesha waziwazi kuchukizwa kwake kwa Maquraysh na kiburi chao cha madaraka. sio tu Makka walipokuwa wanaabudu masanamu, lakini pia hata kule Madina baada ya kuukubali Uislamu, lakini walirejesha tena mfumo wa ubepari wa kabla ya Uislamu. Alikuwa mzungumzaji sana asiye na woga miongoni mwa Masahaba wote wa Muhammad Mustafa ambaye aliwahi kusema: "Wingu halita-mfunika mtu yeyote atakaye kuwa mkweli zaidi ya Abu Dharr."
Abu Dharr alikuwa kama nguvu ya asili iliyokuwa inatafuta lengo kati-ka maisha na ililipata ndani ya Uislamu. Alikuwa sauti ya Dhamira ya Uislamu. Hofu ya ghasia za Maquraysh hazikuzuia hizi roho jasiri na adilifu kuukubali Uislamu, na kila moja iliacha alama za kujitolea kwake mhanga. Vilevile mwingine aliyejulikana sana miongoni mwa Waislamu wa mwanzo alikuwa Mas'ab bin Umayr, binamu ya baba yake Muhammad Mustafa. Miaka mingi baadaye katika Kiapo cha kwanza cha Aqaba, raia wa Madina walimwomba Mtume kuwapelekea mwalimu wa Qur'an na uteuzi ulimwangukia yeye. Hii ilimfanya yeye kuwa ofisa wa kwanza katika Uislamu. Pia alikuwa mbeba bendera wa jeshi la Uislamu kwenye vita ya Uhud lakini aliuawa katika mapigano.
Kama mtu wa familia ya kipagani alisilimu, alitengwa moja kwa moja, bila matumaini ya kurejesha uhusiano tena. Wakazi wengi wa Makka waliuona Uislamu kama "jambo linalowagawa watu" ambalo lilikuwa linavunja familia zao, na baadhi miongoni mwao walifikiria kuikome-sha hali hiyo ya "kugawika" isiendelee kuenea.
Lakini, zaidi ya tishio la kutumia nguvu kwa lengo la kuusambaratisha Uislamu, hawakuweza kufikiria njia nyingine ambayo ingefaa zaidi kuzuia usiendelee. Pia walifikiri kwamba kama hawakuchukua hatua zozote haraka na zilizo thabiti, dalili zilikuwa zinaonyesha kwamba kila nyumba huko Makka ingegeuka kuwa uwanja wa vita ambapo viongozi wa imani za zamani na mpya wangeingia kwenye umwagaji wa damu kwa kushambuliana wao kwa wao. Wapo watu wengine walidhani kwamba Muhammad ali-chochewa na tamaa ya kukanusha na kushutumu ibada za wahenga wao na masanamu yao. Wote kwa pamoja walijaribu kutafakari na kupata jibu kwa kutumia njia isiyo ya kawaida. Baada ya mazungumzo marefu, waliamua kumtuma Utba, mmoja wapo wa wakuu wa Maquraysh, kumuona Muhammad, kujaribu kumsihi aache mpango wa ujumbe wake.
Utba alikuwa anajulikana kwa uwezo wake wa kushawishi. Utba alikwenda kwa Muhammad Mustafa na kumwambia: "Ewe Muhammad! usilete mfarakano na kutokuelewana miongoni mwa Waarabu, na usilaani miungu ya kiume na kike ambayo wahenga wetu wamekuwa wanaiabudu kwa karne nyingi na tunaiabudu leo hii. Kama lengo lako kufanya hivyo unataka kuwa kiongozi wa kisiasa, tupo tayari kukutambua wewe kuwa mtawala wa Makka. Ukitaka utajiri, wewe sema tu na tutakupa kila kitu tuwezacho. Na endapo unataka kuoa mke mzuri sana kutoka kwenye familia mashuhuri, wewe sema, sisi tutafanya mpango."
Utba alimaliza hotuba yake kwa matumaini kwamba angepata jibu la kupendeza. Alistaajabu alipoona Muhammad haonyeshi dalili ya kutaka ukubwa au utajrii au uzuri wa mwanamke. Badala yake alimsomea Sura Sajda (Sura 32 ya Qur'ani) ambayo katika siku hizo hizo ndio ilikuwa imeteremshwa kutoka mbinguni. Muhammad kamwe hakuruhusu makubaliano yenye msingi wa kudhoofisha mamlaka yake ya kiroho.
Utba alisikia, hakusema kitu, na alirudi kwa Maquraysh na kutoa taari-fa kuhusu kazi aliyotumwa. Aliwashauri Maquraysh wamwache Muhammad aendelee na mambo yake bila kubughudhiwa. Pia inasemekana kwamba aliwaambia Maquraysh kwamba kama Muhammad akishindwa kwenye ujumbe wake, wao hawatapata hasara, lakini kama angefaulu, wangegawana utukufu na mamlaka na yeye.
Lakini Maquraysh hawakukubali ushauri wa Utba kwa kujizuia na kupunguza makali dhidi ya Muhammad na wafuasi wake. Maquraysh waliendelea kumnyanyasa Mtume na kuwatesa Waislamu. Lakini pia waliendelea kujaribu kubuni vigingi vipya katika kampeni dhidi ya Uislamu ambavyo vingeweza kuleta matokeo mazuri zaidi kuliko yaliyofanywa na vurugu zao hadi hapo.
Muhammad Mustafa alipewa ulinzi na ami yake na mlezi wake, Abu Talib. Wapagani hawakuweza, kumuonea mpwa wa Abu Talib wakati wa uhai wake. Baadhi yao walileta fikira mpya kwamba labda wange-lazimika kujaribu kumshawishi Abu Talib mwenyewe aache kumpa ulinzi Muhammad kwa jina la umoja wa kikabila. Umoja wa kikabila ni msingi wa kuendeleza maisha jangwani. Wazo hili lilionekana zuri sana na liliwapendeza viongozi wote wa kikabila. Kwa vyovyote vile, umoja wa kikabila ulikuwa jambo la muhimu sana hivyo kwamba haungestahili kufanyiwa masihara hata na Abu Talib, bila kujali mapen-zi ya mpwa wake.
Maquraysh waliamua kutuma ujumbe kwa Abu Talib. Waliteuwa watu wa ujumbe huo kwa uangalifu sana na walimuona na wakamwomba kwa ajili ya kudumisha umoja wa kikabila asitishe ulinzi wake kwa Muhammad ambaye alikuwa "anauharibu" umoja huo. Hata hivyo, Abu Talib hakuwa na nia ya kusitisha ulinzi wake au kuacha kumuunga mkono Muhammad. Lakini aliwaridhisha wajumbe wa Maquraysh kwa maelezo ya uchaji Mungu na kutuliza na akawaambia warudi.
Wajumbe hao pia walitambua kwamba walirudi nyumbani kutoka kwenye kazi ya "kufukuza zimwi" kazi ngumu isiyo tekelezeka. Lakini hawakushtushwa na kushindwa kwao na baada ya muda kidogo, wali-fanya jaribio lingine lakumlaghai Abi Talib amkimbie Muhammad. Ujumbe mwingine tofauti na ule wa kwanza ulikwenda kumuona na safari hii walimpelekea kijana wa kiume mwenye sura nzuri jina lake Ammara bin Waleed, ambaye walimpa Abi Talib awe mtoto wake wa kufikia kama angekubali kumsalimisha Muhammad kwao.
Abi Talib aliwacheka makafiri kwa ujinga wao. Hivi waliamini kabisa kwamba angewapa mtoto wake wamuue, na angemlea mtoto wao kama mwanae? Wazo hili lilikuwa la kipuuzi sana lakini kwa mara nyingine Abu Talib alitumia busara kubwa kulitatua tatizo hili kwa kutumia werevu wake, wakaondoka kwenda zao.
Jaribio la pili la viongozi wa Quraysh kumshawishi Abu Talib aachane na Muhammad halikufaulu. Maana ya kushindwa jaribio lao la pili ilipo-tua akilini mwao, walihoji kwamba njia zote za amani zimeshindikana, na sasa kwa kweli lazima wajaribu kuchukua hatua kali. Katika hali ya ghadhabu na kukata tamaa, Maquraysh wenye madaraka ya kutengeneza sera, waliamua kuchukua "hatua kali" na waliutuma ujumbe wa tatu na wa mwisho kumuona Abu Talib. Lengo la ujumbe ilikuwa kumlazimisha awaruhusu wamchukue Muhammad. Viongozi wa ujumbe huo walimkabidhi Abi Talib sharti la mwisho; ama awaruhusu wamchukue Muhammad au mambo yange mgeukia yeye mwenyewe.
Abu Talib alikuwa na tabia ya uchangamfu na siku hiyo jua liliwaka lakini ilikuwa majonzi kwake. Maquraysh wale aliokuwa anawajua, hawakuwa na masihara, kwa hiyo alimuita Muhammad, akamwelezea kuhusu azma ya Maquraysh na kuongezea: "Lo! Maisha ya ami yako! Usinibebeshe mzigo ambao utanishinda kuubeba." Muhammad alijibu: "Ewe ami yangu! kama Maquraysh watanipa jua nilibebe kwa mkono wangu wa kulia na mwezi mkono wa kushoto, sitaacha kutangaza Upweke wa Mungu. Katika kutekeleza kazi hii, ama nitafaulu na Uislamu utaenea, au, kama nikishindwa, nitaangamia nikiwa ninajaribu kuifanya kazi hiyo." Abu Talib hakuwa na nia ya kumwambia mpwawe aache kuhubiri Uislasmu. Alikuwa anajaribu kuona uamuzi wake ulikuwa thabiti kiasi gani. Baada ya kusikia jibu la Muhammad alikubali na kutosheka kwamba mpwawe hangetetereka, akamwambia: "Mwanangu nenda, na ufanye uonavyo sawa. Hakuna mtu atakayethubutu kukuumiza wewe."
Sir William Muir "Lakini fikira ya kukimbiwa na mlinzi wake mwema (Abu Talib) ilimuelemea Muhammad. Alilia sana na alirudi na kuondoka. Halafu Abu Talib alimuita kwa sauti kubwa: 'Mtoto wa kaka yangu! Rudi! Alirudi. Na Abu Talib akasema: "Ondoka nenda kwa amani, mpwa wangu, na useme chochote kinachokupendeza. Kwa Jina la Mola wangu, kwa vyovyote vile, sitakutoa kwamwe kwa watu hao." (The Life of Muhammed, London, 1877). Muhammad Husayn Haykal.
Abu Talib akasema: 'Nenda haraka mpwa wangu, na sema lolote unaloweza kwa Jina la Mungu yule yule ninaapa sitakusaliti wewe kwa maadui zako.' "Abu Talib aliwasilisha uamuzi kwa Bani Hashim na Bani al-Muttalib na alizungumza nao kuhusu mpwawe kwa kumsifu sana na kupendeze-wa sana kuhusu utukufu wa daraja la Muhammad. Aliwaomba wote wamlinde Muhammad asishambuliwe na Maquraysh. Wote walikubali isipokuwa Abu Lahab ambaye alitangaza waziwazi uadui wake kwa Muhammad na akajitoa na kuingia kwenye kambi ya upinzani. "Maquraysh waliwafanyia Masahaba Muhammad kila aina ya maumivu ambayo aliokolewa tu kwayo kwa ulinzi wa Abu Talib, Banu Hashim na Bani al-Muttalib." (The Life of Muhammed, Cairo, 1935).
Abu Talib alijitahidi kuwazuia mara nyingi Maquraysh wasiwatese sahaba wa Muhammad, uvumilivu wa wapagani ulifika mwisho. Ukali wao ulijilimbikiza kwa miaka mingi. Baada ya jaribio lao la tatu kushindwa, walianza kukata tamaa na wasiojali, na wakaanza kuwa fed-huli na tishio kwa Waislamu. Waliamua kuwaangushia Waislamu ambao hawakuwa na ulinzi hasira zao zote, na kuiangamiza imani mpya kwa vitisho na ukatili. Ilionekana kama vile Maquraysh walipagawa!
Wahanga wa kwanza kutokana na msuguano na uvamizi wa wapagani walikuwa Waislamu wote ambao hawakuwa na uhusiano wowote na makabila ya Makka. Yasar na mkewe, Sumayya na mtoto wao wa kiume, Ammar hawakuwa na uhusiano wa kikabila kwa hiyo, walikuwa "wageni" hapo Makka, na hapakuwa na mtu wa kuwalinda. Wote watatu waliteswa na Abu Jahl akisaidiwa na wapagani wengine. Sumayya, mke wa Yasar alikufa alipokuwa anateswa. Kwa hiyo mke wa Yasar akawa shahidi wa kwanza wa Uislamu. Baada ya muda si mrefu, mumewe, Yasar naye aliuawa wakati anateswa, naye akawa shahidi wa pili wa Uislamu. Katika hali hii mke na mume walifanya uchaguzi wa mgongano usioisha baina ya nuru na giza, wema na uovu, ukweli na uongo, haki na batili na Uislamu na upagani. Uchaguzi huo ulikuwa mgumu lakini hawakuwa na jinsi nyingine kuhusu jambo hilo, na kwa furaha walitoa maisha yao kwa ajili hiyo! Waliyafanya maisha yao kuwa kafara kwa Uislamu.
Maquraysh walichafua mikono yao kwa damu isiyokuwa na hatia! Katika orodha tukufu ya mashahidi, Sumayya na mumewe, Yasar wana daraja miongoni mwa walio juu. Waliuawa si kwa sababu nyingine isipokuwa kwa kujitolea kwa Mwenyezi Mungu na kuupenda Uislamu na Muhammad Mustafa. Waislamu wale waliouawa kwenye vita vya Badr na Uhud walikuwa na jeshi la kuwalinda na kuwakinga mkono wao. Lakini, Sumayya na mumewe Yasar, hawakuwa na ulinzi wowote.
Hawakuwa na silaha, na walikuwa Mashahidi ambao hawakuwa na ulinzi kabisa, katika historia ya Uislamu. Kwa kujitoa mhanga, wali-sisitizia ukweli wa Uislamu na waliimarisha muundo wake. Kujitolea kwao muhanga ilikuwa ni ushindi wa imani dhidi ya mali. Marafiki na maadui zao walishangaa kuwaona hawajali kifo. Kujitolea na kuwa muhanga wa Uislamu ilifanywa kuwa desturi na kitengo cha muhimu katika maadili ya Uislamu.
مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا ﴿٢٣﴾
"Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo."(Qur'an 33:23).
Maelezo ya Mutarjumi.
"Katika kupigana kwa kweli, wengi walijitoa mhanga na wanaendelea kufanya hivyo kwa kutumia mali zao, ujuzi wao, maongezi yao, uhai wa maisha katika njia ya Mwenyezi Mungu na hawakutetereka wakati huo hadi sasa. Kama walishinda taji la kujitolea muhanga walineemeka." (A. Yusuf Ali) Mapema kabisa, Sumayya, Yasar na Ammar walipata ushindi wa heshima ya kuwa Familia ya kwanza ya Kiislamu.
Sasa wamepata ushindi wa heshima nyingine. Sumayya na Yasar walikuwa Mashahidi wawili wa kwanza wa Uislamu. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye alifahamu vipi na kwa nini walikuwa wanateswa, aliwaliwaza; aliwashauri wawe na subira ya muumini wa kweli, na aliwaambia kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha wajengea Ikulu huko Peponi. Mtoto wao Ammar taji la ushahidi lilikuwa linamngojea ingawa itakuwa hapo baadaye. Kama familia ya Yasar walikuwa Familia ya kwanza ya kiislamu, vile viles walikuwa Familia ya kwanza ya Mashahidi. Kila mmoja wa famil-ia hii iliyo barikiwa alikufa kwa ajili ya kuthibitisha misingi ya haki na kweli iliyomo kwenye Uislamu. Mungu alifurahishwa kwa kuwapa hes-hima mbili kuu, ubora katika imani na ubora katika ushahidi.
Kama ilivyoonyeshwa kwenye kurasa za nyuma, Bilal, Khatab bin el-Arat, Suhaib Rumi na Waislamu wengine masikini na ambao hawakuwa na ulinzi, walilazimishwa kusimama kwenye mchanga wenye joto kali na walichapwa viboko na wapagani. Walinyimwa chakula na maji kwa matumaini yasiyokuwa na matokeo ya kuwafurahisha wao kwamba njaa na kiu ingewalazimisha wao kutengana na Muhammad na Uislamu. Katika kuwatesa Waislamu, wapagani walikuwa na msimamo, nia ya kuendeleza mpango huo na kuvumbua njia za kuendeleza mpango huo.
Kama Maquraysh walimkuta Muhammad yuko peke yake, walipata fursa ya kumsumbua. Kwa vyovyote vile walitamani lakini ilibidi waizuie tamaa hiyo. Kama wangemuua, wangekuwa wameanzisha kulipizana visasi au hata kuanzisha vita vya kikabila. Mnamo mchana wa siku moja Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alikwenda kwenye Al-Ka'aba kusoma Qur'an. Wakati anaendelea kusoma Qur'an ghafla alijikuta amezuungukwa na waabudu masanamu. Walimfanyia ghasia, na inawezekana wangemuumiza vibaya lakini aliingilia kati Harith bin Abi Hala mpwa na mtoto wa kufikia wa Khadija, ambaye alibahatika kufika hapo. Harith aliingia kwenye vurumai hiyo na akafanikiwa kumpa ulinzi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye alinusurika kutoka kwenye vurugu za waabudu masanamu na wapagani wa Makka.
Harith bin Abi Hala aliwapiga ngumi wapagani. Inawezekana sana kwamba Harith alikuwa na upanga au jambia lakini hakutaka kuutumia kwa kuwa hakutaka damu imwagike ndani ya Al-Ka'aba. Lakini wakati tafrani hiyo inaendelea, mmojawapo wa waabudu masanamu alitoa jam- bia na kumchoma Harith mara kadhaa. Alianguka kwenye dimbwi la damu yake, na akafariki kutokana na majeraha makubwa kifuani mwake, kwenye bega na uso. Alikuwa Mwislamu wa kwanza kuuawa kwenye eneo la Al- Ka'aba.
Harith alikuwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na saba, na aliyatoa maisha yake kwa sababu ya kuokoa maisha ya Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Kwa kufanya hivyo alijinyakulia ushin-di wa taji la Ushahidi. Alikuwa Shahidi wa Tatu. Kifo chake ambacho kilimjia mapema sana katika maisha yake, kilimsikitisha sana Mtume. Kwa Khadija, kifo cha Harith kilikuwa hasara yake binafsi. Alimlea Harith kama mwanae wa kumzaa. Lakini Khadija alisahau huzuni yake ili aweze kumliwaza mume wake katika huzuni hiyo.
Ingawa wanahistoria wa Kiarabu hawasemi lolote kuhusu jambo hili, lazima palifanyika mapigano makali sana Makka baina ya Waislamu na Wapagani kabla Mtume wa Uislamu hajahamia Madina. Abu Talib, alimlinda mpwa wake kipindi chote cha uhai wake, na baada ya kifo chake, mwanawe Ali, aliendelea kumlinda Mtume.
Alikuwa bado hajafika miaka ishirini alipojiteua mwenyewe kuwa mlinzi wa Muhammad Mustafa. Baada ya mauaji ya Harith bin Abi Hala, ndani ya Ka'aba yaliyofanywa na wapagani, Ali alianzisha mpan-go wa kufuatana na Mtume wakati wowote alipotoka ndani ya nyumba yake na popote alipokwenda na alikuwa anasimama katikati yake na maadui zake. Kama mhuni alimwendea Muhammad kwa lengo la kumtishia, haraka Ali alimkabili mtu huyo, na alipambana naye. Akiandika kuhusu kipindi hiki cha historia ya Uislamu, mwanahistoria Muingereza, D.S. Margoliouth, anasema: "Watu ambao kuingia kwao kwenye Uislamu kulifurahiwa sana walikuwa ni watu wenye nguvu za kimwili, na mapigano mengi hasa lazima yatakuwa yametokea huko Makka kabla ya kukimbia,; vinginevyo utayari ambao kwamba ungetolewa na Waislamu baada ya kukimbia (kutoka Makka) kutokana na idadi ya mabingwa wao wakutegemewa isingeelezeka. Mabingwa wa kutegemewa lazima wangejaribiwa mahali fulani; na hakuna mapigano ya nje yaliyotaarifi-wa au hata suala la dokezo kwa kipindi hiki." (Muhammed and the Rise of Islam, London, 1931).
Hapakuwepo na mapigano ya nje hapo Makka kabla ya Hijira (kuhama kwa Mtume kutoka Makka kwenda Madina); lakini yalikuwepo mengi mitaani na sehemu za wazi ndani ya jiji la Makka. Vijana wahuni wa Makka walimtupia Mtume mawe au tende kavu alipokuwa katika shughuli zake, na Ali aliziumiza pua zao, alingoa meno yao na alivunja miguu yao. Ilikuwa kwenye 'viwanja hivi vya mapigano" ambamo ndimo Ali, mpiganaji jasiri kijana alipata ustadi wa kivita. "Vita" hivi hapo Makka vilikuwa "mazoezi" ya kazi aliyotakiwa kuifanya miaka michache baadaye huko Madina kwenye mapambano ya Uislamu na upagani. Pia ilikuwa ni wakati huu wa mwanzo, kabla ya Hijira ndipo Ali alipata kuwa "msitari wa mbele wa kutetea Uislamu." Kwa hakika wakati huo huo, pia alikuwa msitari wa pili na wa mwisho wa kutetea Uislamu. Yeye alishika nafasi hizo peke yake, aliendelea hivyo hadi mwisho wa uhai wake.
Maquraysh waliitesa miili ya Waislamu ambao hawakuwa na ulinzi jiji-ni Makka kwa matumaini kwamba wangewalazimisha kuukana Uislamu lakini walishindwa. Hakuna yeyote miongoni mwa hawa Waislamu "fukara na wanyonge" aliye ukana Uislamu kamwe. Hali mbaya inaweza kukatisha tamaa hata watu madhubuti, na kwa Waislamu, hali haingekuwa na nafuu yoyote. Lakini, kwa vyovyote hali ilivyokuwa haikuweza kuwavunja moyo. Uislamu uliwaunganisha pamoja. Kwa hawa Waislamu "fukara na wanyonge," Uislamu ulikuwa umewakolea kiasi cha kulewa. Uislamu uliwaunganishia maisha yao, uliwa-pa maana ya maisha; ukiwafanya watambue makusudio yao katika maisha na uliweza kuwafanya wajue upeo wa fikira zao.
Kwa hiyo, walidharau usalama, starehe na raha za maisha; na baadhi yao kama Sumayya na mumewe Yasar, walidharau uhai wao; lakini walishikilia imani. Walikufa baada ya kuteswa sana na maadui wa Uislamu lakini hawakukubali uwongo. Mwenyezi Mungu na aziridhie roho hizi jasiri na adilifu na Azineemeshe. Imani zao na mioyo yao ilikuwa, kama Maquraishi walivyogundua, haishindiki.. kama ilivyokuwa imani na moyo wa Bwana na kiongozi wao, Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Hawa walikuwa almasi ambazo zilipatikana kutoka kwenye majabali ya dunia. Kwa idadi walikuwa wachache lakini thamani yao haina kiwango, ambayo ingeweza kuelezewa si kwa uwingi ila kwa ubora tu; na ubora huo ulikuwa wa hali ya juu sana.