MAISHA YA BIBI KHADIJA

MAISHA YA BIBI KHADIJA0%

MAISHA YA BIBI KHADIJA Mwandishi:
Kundi: Waheshimiwa wa Kidini

MAISHA YA BIBI KHADIJA

Mwandishi: Syed A .A .Razwy
Kundi:

Matembeleo: 24563
Pakua: 4180

Maelezo zaidi:

MAISHA YA BIBI KHADIJA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 16 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 24563 / Pakua: 4180
Kiwango Kiwango Kiwango
MAISHA YA BIBI KHADIJA

MAISHA YA BIBI KHADIJA

Mwandishi:
Swahili

6

MAISHA YA BIBI KHADIJA

SURA YA NANE

KUHAMA MARA MBILI KWA WAISLAMU KWENDA ETHIOPIA (615 - 616)

Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alishiriki katika huzuni zote na huzuni na maumivu ya mateso ya wafuasi wake ambao walikuwa wakiteswa kwa sababu ya kuamini Tauheed (Upweke wa Mungu) lakini hakuwa na namna ya kuwalinda. Ilipoonekana kwamba vurugu na mateso hayangepungua dhidi ya Waislamu toka kwa wapa-gani, aliwashauri waondoke Makka, wakimbilie Abyssinia nchi iliyokuwa inatawaliwa na mfalme Mkristo, aliyejulikana sana kama mtu muadilifu na mchamungu.

Baada ya ushauri huu, kundi la Waislamu; wanaume kumi na moja na wanawake wanne, waliondoka Makka na wakaenda Abyssinia. Kundi hili lilijumuisha watu kama Uthman bin Affan (Baadaye akawa Khalifa wa Waislamu) na Zubyr bin al-Awwan, binamu ya Mtume. Mtume alimteua mmoja wa Masahaba wake wakuu, Uthmani bin Mazoon, kama kiongozi wa kundi hili. Muhammad bin Ishaq. Mtume alipoona mateso ya Masahaba wake na kwamba ingawa yeye aliyakwepa kwa sababu ya msimamo wake kwa Mwenyezi Mungu na ulinzi wa ami wake, Abu Talib, hakuweza kuwapa ulinzi, aliwaambia: "kama mngeondoka kwenda Abyssinia (ni bora zaidi kwenu), kwa sababu mfalme (wa kule) hatavumilia uonevu, na nchi hiyo ni rafiki, hadi hapo Mwenyezi Mungu atakapo waondolea dhiki."

Bila kukawia Masahaba wake walikwenda Abyssinia, wakiogopa wasije wakamkana na kumkimbia Mungu na dini yao. Hii ilikuwa hijira ya kwanza katika Uislamu. (The Life of the Messenger of God). Hijra ya kwanza ilikuwa mnamo mwaka wa tano wa Wito (Kutangazwa Uislamu) yaani, 615 A.D.

Mfalme wa Abyssinia aliwakaribisha wakimbizi Waislaamu kutoka Makka kwenye himaya yake. Aliwapa hifadhi, na wakapata amani na salama, na walifurahia uhuru wa kuabudu. Inasemekana kwamba baada ya kama mwaka mmoja, Waislamu wakimbizi waliokuwa Abyssinia walisikia tetesi kwamba Maquraysh wa Makka waliukubali Uislamu. Kama ilikuwa hivyo, basi hapakuwepo na sababu ya wao kuendelea kuishi uhamishoni, na wakatamani sana kwenda kwao. Kwa hiyo, walirudi Makka. Lakini walipokuwa Makka waligundua kwamba si tu kwamba taarifa za kusilimu Maquraysh zilikuwa za uongo bali waliongeza kasi ya kutesa Waislamu. Kwa hiyo, kwa mara nyingine waliondoka Makka lakini si wao tu.

Safari hii Waislamu wengine wengi walikwenda nao Abyssinia. Kundi hili jipya lilikuwa na jumla ya watu themanini na tatu (wanaume) na wanawake kumi na nane, wakiwemo wakimbizi wa zamani na wapya; miongoni mwao akiwemo Abdur Rahman bin Auf, Abu Salma Makhzumi na Abdullah bin Masud. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimteua Binamu yake Jaafar bin Abu Talib, kaka mkubwa wa Ali, kuwa kiongozi wa kundi hili.

Hijira ya pili ya Waislamu kwenda Abyssinia ilikuwa mnamo mwaka wa sita baada ya Wito (Kutangazwa kwa Uislamu). Yaani, 616 A.D. Kuhama kwa Waislamu na kupokewa kwao Abyssinia, kuliwashtua Maquraysh. Walihofia kwamba Waislamu huko Abyssinia labda wangekusanya nguvu ya kupigana au wangepata washirika wapya, na halafu, wangerudi Makka na kuwakabili. Kwa hiyo, ili kuzuia tishio hili lenye nguvu, kama ambavyo waliona, waliamua kutuma ujumbe kwenye baraza la mfalme wa Abyssinia kumuomba awarudishe Waislamu Makka.

Wakimbizi wa kiislamu ambao walitegemea wangeachwa katika hali ya amani, walishangaa na kukasirika kuona ujumbe kutoka Makka unafika Abyssinia ambao uliongozwa na Amr bin Ass. Amr alimletea mfalme na watumishi wake zawadi za thamani ili ajipendekeze nazo kwao.

Mfalme alipowapa nafasi ya kuongea, kiongozi wa ujumbe wa Maquraysh alisema kwamba, Waislamu waliopo Abyssinia hawakuwa wakimbizi waliokimbia mateso lakini walikuwa watoro waliotoroka haki na sheria; na alimuomba awarudishe Makka. Hata hivyo, mfalme, alitaka kusikiliza maelezo kutoka upande wa pili kabla ya kutoa uamuzi, na alimwita Jaafar bin Abi Talib, kiongozi wa wakimbizi, kujibu mashitaka dhidi ya Waislamu. Jaafar alitoa utetezi usio sahaulika. Ifuatayo ni hotuba yake ikijibu maswali yaliyo ulizwa na mfalme Mkristo wa Abyssinia. "Ewe mfalme! Tulikuwa watu wajinga na tuliishi kama hayawani wa msituni.

Wenye uwezo miongoni mwetu waliwanyonya wanyonge. Hatukutii sheria yoyote na hatukutambua mamlaka yoyote isipokuwa ile yakutumia nguvu. Tuliabudu masanamu ya mawe na miti iliyochongwa, na hatukujua lolote kuhusu hadhi ya binadamu. Halafu Mwenyezi Mungu kwa huruma zake alituletea mjumbe wake ambaye alikuwa mmoja wetu. Tulikuwa tunafahamu kuhusu ukweli wake na hadhi yake. Tabia yake ilikuwa mfano wa kuigwa, na alikuwa mzawa aliye bora wa Waarabu. Alitukataza kuabudu masanamu na alituita na kutuambia tumwabudu Mungu Mmoja. Alitushauri kusema kweli, na kuwapa ulinzi wanyonge, fukara, wanyenyekevu, wajane na yatima.

Alituamuru kuonyesha heshima kwa wanawake, na kamwe tusiwasengenye. Tulimtii na tulifuata mafundisho yake. Nchini mwetu, wapagani bado wapo wengi sana na walitukataza tusisilimu na kufuata imani mpya. Walianza kututesa, na ilikuwa kwa sababu ya kukwepa mateso kutoka kwao, hivyo kwamba tukatafuta na kupata hifadhi hapa kwenye himaya yako." Jaafar alipomaliza kuhutubia, mfalme alitangaza kwamba aliridhika na ukweli wake, na aliongeza kusema kwamba Waislamu waliruhusiwa kuishi bila woga wowote. Usemi ambao ulimkasirisha sana Amr bin Al- As. Lakini Amr bin Ass alipata fikira nyingine, ambayo alikuwa na uhakika ingemridhisha mfalme ambaye alikuwa Mkristo. Kama ingekubalika, alikuwa na uhakika kwamba ingebadilisha hali dhidi ya Waislamu, na wangerudishwa Makka.

Kwa hiyo siku iliyofuata, alirudi barazani na akamwambia mfalme kwamba lazima asitishe ulinzi kwa Waislamu kwa sababu walikana uungu wa Yesu (Isa) na walidai kwamba yeye ni binadamu kama wengine. Mfalme alipomuuliza Jaafar kuhusu jambo hili, alisema: "Uamuzi wetu kuhusu Yesu (Isa) ni kama alivyo funuliwa Mtume wetu, kwamba Yesu (Isa) ni mtumishi wa Mungu na Mtume wake, Roho Yake na Amri yake iliyotolewa kwa Mariam, bikira mtakatifu."

Mfalme alimwambia Jaafar: "Yesu (Isa) yu vilevile ambavyo umesema na hakuna zaidi ya hapo." Halafu akawageukia Waislamu na kusema: "Nendeni nyumbani kwenu na muishi kwa amani. Kamwe sitawaruhusu maadui zenu wawakamate."Alikataa kuwarudisha Waislamu Makka, alimrudishia Amr bin Al-As zawadi alizokwisha mpa na kuwaambia warudi walikotoka. Washigton Irving.

"Miongoni mwa wakimbizi waliokwenda Abyssinia, alikuwepo Jaafar, mtoto wa Abu Talib na kaka wa Ali, binamu wa Muhammed. Alikuwa mtu mwenye uwezo wa kujieleza na umbo la kupendeza sana. Alisimama mbele ya mfalme wa Abyssinia, na akamweleza imani ya Uislamu kwa hamasa na nguvu. Mfalme ambaye alikuwa Mkristo wa dhehebu la Nestorian, aliona imani hizi zinafanana sana katika mambo mengi na kwa hiyo alikataa kabisa imani ya kuabudu masanamu iliyokuwa inakumbatiwa na Maquraysh hivyo kwamba, hadi hapo, badala ya kuwafukuza watoro, aliwakubali zaidi na kuwapa upendeleo na ulinzi maalum na akimrudishia zawadi alizokwisha mpa Amr bin Al-Ass na Abdullah na kuwafukuza hapo mahakamani." (The Life of Muhammed).

Waislamu waliishi miaka mingi Abyssinia. Baada ya miaka kumi na tatu, walirudi Madina, si Makka - mnamo mwaka wa saba Hijiria (A.H.) (628 A.D).- miaka saba baada ya Mtume wa Mungu kutoka Makka kwenda Madina. Kufika kwao Madina iligongana na ushindi wa Waislamu huko Khybar. Jaafar bin Abi Talib alikuwa kiongozi wa Waislamu wote waliokwenda Abyssinia mwaka wa 615 na 616 A.D. inaonyesha kama vile alikuwa peke yake kutoka ukoo wa Bani Hashim aliyeondoka Makka kwenda Abyssinia na wakimbizi wengine. Watu wengine wote wa ukoo wa Bani Hashim walibaki Makka.

SURA YA TISA

HAMZA AUKUBALI UISLAMU - 615 A.D.

Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) , ingawa alikuwa salama kutokana na ulinzi wa ami wake Abu Talib, si kwamba yeye hakufanyiwa fujo na makafiri. Kila walipopata fursa ya kumnasa, hawakumkosa. Ilitokea wakati fulani, Abu Jahl alimkuta akiwa peke yake na alitumia lugha ya matusi machafu kumtukana Mtume. Jioni hiyo hiyo, ami wake, Hamza bin Abdul Muttalib alirudi nyumbani kuto-ka safari ya kuwinda, mtumwa wake wa kike alimweleza kuhusu tukio la Abu Jahl kumtukana Muhmammad, na jinsi Mtume alivyo vumilia na kwamba yeye alishuhudia hayo kwa macho yake.

Hamza alikuwa shujaa, mwindaji na mwana michezo, na hakuwa anapendelea kujua yanayo tokea mjini Makka kila siku. Lakini, tabia ya Abu Jahl kwa mpwa wake ilimkasirisha mno hivyo kwamba alichukua upinde wake na kwenda kwenye mkusanyiko wa Maquraysh ambapo Abu Jahl alikuwa anatoa maelezo kuhusu matukio ya siku hiyo kwa wenzake, alimpiga kichwani kwa upinde na kuanza kutoka damu na akasema kwa sauti ya juu sana "Mimi pia nimesilimu na kuukubali Uislamu."

Hii ilikuwa changamoto kwa Abu Jahl lakini aliona kwamba ukimya ulikuwa sehemu muhimu sana ya ushujaa, na hakugombana (hakupambana) na Hamza, pia akawazuia marafiki zake ambao walitaka kuamka kwa ajili ya utetezi wake. Hamza akawa Mwislamu wa dhati na shujaa wa Uislamu. Akawa rafiki mkubwa wa mpwa wake mwengine Ali bin Abi Talib, na ilikuwa ni wao wawili walioua wapiganaji wa jeshi la Makka kwenye vita ya Badr - vita ya kwanza ya Uislamu ambayo ilipiganwa miaka michache baada ya Hamza kuwa Mwislamu.

Vita ya Uhud ilikuwa vita ya pili ya Uislamu. Kwenye vita hiyo, Hamza alimuua mbeba bendera mmoja wa jeshi la wapagani wa Makka. Walipo shambulia safu ya Waislamu, Hamza aliingia kati yao. Alikuwa anawakatakata miongoni mwao, huku akisonga mbele ambapo Wahshi mtumwa kutoka Abyssinia alitupa mkuki na kumchoma Hamza tum-boni, alianguka na kufa hapohapo. Wahshi aliajiriwa na Hinda, mke wa Abu Sufyan na mama wa Muawiya kwa lengo la kumuua Hamza. Kwenye vita ya Uhudi Waislamu walishindwa. Baada ya ushindi wao Hind, na wakatili wengine aliokuja nao kutoka Makka, waliikatakata miili ya Waislamu waliouawa. Hind alipasua tumbo la Hamza, akachukua ini na kulitafuna. Muhammad bin Umar Waqidi, mwanahis-toria, anasema kwamba, Hind alikoka moto kwenye uwanja wa vita, na akachoma moyo na ini la Hamza akala. Hakutosheka na hilo, alikata miguu, masikio na pua ya Hamza akavitunga kwenye kidani chake na akaingia Makka akiwa amevaa kama alama ya ushindi.

Hamza alimuua Utba, baba ya Hind, kwenye vita ya Badr. Kwenye vita ya Uhud alikuwa na hamu ya kulipiza kisasi jambo ambalo lilikuwa linamnyima raha tangu vita ya Badr. Muhammad Mustafa, Mtume wa Mungu, alisikitishwa sana na kifo na kukatwakatwa vipande mwili wa mkereketwa wa Uislamu kama Hamza. Alimpa vyeo vya "Simba wa Mungu" na "Mkuu wa Mashahidi." Hamza alisilimu mnamo mwaka wa tano baada ya kutangazwa kwa Uislamu. Mwenyezi Mungu na Amridhie na Amneemeshe.

SURA YA KUMI

UMAR KUSILIMU KWAKE KUWA MUISLAMU 616 A.D

Tukio lililokuwa kubwa mnamo mwaka wa sita baada ya Wito (Tangazo la Uislamu) ilikuwa kusilimu kwa Umar bin al-Khattab, Khalifa wa baa-daye wa Waislamu. Huyu alikuwa adui mkubwa wa Uislamu, na Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na alikuwa mte-saji mkubwa wa Waislamu. Mwanahistoria wa zama za sasa, Amin Dawidar, anasema kwenye kitabu chake. Pictures from the Life of the Prophet, kwamba chuki ya Umar kwa Uislamu, na uadui wake kwa Muhammad Mustafa, ililinganishwa tu na chuki na uadui kwao na ule wa mjomba wake, Abu Jahl. Inasemekana kwamba siku moja Umar aliamua, kwa ghadhabu kali, kumuua Muhammad Mustafa, na kuzima kabisa mwale wa Uislamu. Aliondoka nyumbani kwake akiwa na nia hiyo.

Kama ilivyoonyeshwa huko nyuma, Waislamu wakati huu (mwishoni mwa mwaka wa sita) bado walikuwa ndani ya nyumba ya Arqam bin Abil Arqam wakisali sala ya jamaa. Ndio kwanza walianza kukusanyika wakati mmoja wao alichungulia dirishani, alimuona Umar anakuja akiwa ametoa upanga wake kwenye ala. Katika hali ya mshangao, ali-waambia wenzake alichokiona. Bila shaka, na wao pia walishtuka. Lakini Hamza ambaye naye alikuwepo ndani humo, aliwahakikishia, na akasema kwamba kama Umar alikua anakuja kwa nia njema, basi haku-na tatizo, vinginevyo, yeye (Hamza) angemuua kwa upanga wake mwenyewe. Lakini, ilitokea kwamba Umar alikuja kwa lengo la kusilimu, na alifanya hivyo.

Hadithi inasimuliwa kwamba Umar alikuwa anakwenda Darul-Arqam kwa lengo la kumuua Mtume ambapo mpita njia alimsimamisha, na akamtaarifu kwamba dada yake mwenyewe na mume wake walisilimu, na alimshauri ajisafishe yeye mwenyewe kwanza nyumbani mwake kabla ya kufanya jambo lolote litokanalo na dhana. Muhammad Husayn Haykal.

"Umar alikwenda Dar-ul-Arqam mwenye nia ya kumuua Muhammad na kuwapunguzia Maquraysh mzigo, kurejesha mshikamano wao ulioteketezwa, na kuanzisha tena heshima ya miungu ambayo Muhammad aliikemea vikali. Alipokuwa njiani alikutana na Nuaym bin Abdullah. Baada ya kufahamu madhumuni ya Umar, Nuaym alisema, "Kwa Jina la Mungu, umejidanganya mwenyewe, Ewe Umar! Unadhani kwamba Bani Abd Manaf watakuruhusu uwe hai mara baada ya kumuua Muhammad. Dada yako ni Mwislamu sasa. Kwa nini usirudi nyumbani kwako na kuiweka sawa?" (The Life of Muhammed, Cairo, 1935) "Umar alikasirika aliposikia hivyo. Haraka sana alibadili njia na kuelekea nyumbani kwa dada yake ili apeleleze kama madai hayo ni ya kweli. Katika kumjibu, dada yake alimpa jibu la moja kwa moja lakini la werevu."

Muhammad bin Ishaq Umar alikwenda kwenye mlango (wa nyumba ya dada yake) na wakati huo huo Khabbab (sahaba wa Mtume) alikuwa anasoma Sura: Taha na pale jua litakapopinduliwa. Wapagani walikuwa na desturi ya kuyaita maandishi haya "uchafu." Umar alipoingia ndani, dada yake aling'amua kwamba alitaka kufanya madhara na walificha maandishi hayo waliyokuwa wanayasoma. Khabbab aliingia ndani haraka. Umar ali-uliza maneno gani ya kipuuzi aliyosikia wanasema? Dada yake alijibu kwamba hayo yalikuwa mazungumzo ya kawaida tu kati yao.." (The life of the Messenger of God).

Umar alipandwa na hasira kwa kile alichodhani ni uwongo, na alimpiga dada yake usoni. Pigo hilo lilisababisha damu kutoka mdomoni mwa dada yake. Umar alitaka kumpiga tena lakini alipoona damu aliacha. Mara alionekana hana hasira, na halafu kwa sauti tofauti kabisa alim-womba dada yake amwonyeshe kile alichokuwa anasoma. Dada yake aliona mabadiliko kwa kaka yake lakini alisema: "Wewe ni mwabudu masanamu mchafu, na siwezi kukuruhusu wewe kushika neno la Mwenyezi Mungu."

Haraka Umar alikwenda nyumbani kwake, akaoga, akarudi nyumbani kwa dada yake, akasoma maandishi ya Qur'an na halafu akaenda nyumbani kwa Arqam ambako alishahadia Upweke wa Muumba na Utume wa Muhammad. Sir William Muir anasema kwamba Umar alisilimu mwishoni mwa mwaka wa sita baada ya kutangazwa kwa Uislamu. Sir William Muir

Umar alisilimu wakati wa Dhul Hijja, mwezi wa mwisho wa mwaka. Inasemekana wakati huo waumini walifikia wanaume 40 na wanawake 10, au kwa hesabu nyingine; wanaume 45 na wanawake kumi na mmoja. (The Life of Mohammed, London, 1877) Umar alikuwa na miaka zaidi ya thelathini aliposilimu. Muhammad Husayn Haykal "Wakati huo, Umar bin al-Khattab alikuwa mtu mzima mwenye umri wa miaka kati ya thelathini na thelathini na tano." (The Life of Muhammad, Cairo, 1935).