9
MAISHA YA BIBI KHADIJA
SURA YA KUMI NA TATU
KHADIJA MAMA WA WAUMINI KABLA YA UISLAMU
Khadija alikuwa Malkia wa Makka. Wakati jua la Uislamu lilipochomoza juu ya upeo wa macho, Mwenyezi Mungu ali-furahi kumfanya pia Malikia wa Uislamu. Mwenyezi Mungu pia alifu-rahishwa kumfanya yeye Mama wa Waumini, kama Asemavyo kwenye Kitabu chake.
النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ ﴿٦﴾
"Nabii yu karibu zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao wenyewe, na wakeze ni mama zao. (33:6).
Maelezo ya mfasiri "Sura hii ya (33) inathibitisha hadhi na nafasi ya wakeze Mtukufu Mtume, ambao walikuwa na ujumbe maalum na wajibu kama Mama wa Waumuini. Hawakutakiwa kuwa kama wanawake wa kawaida: wali-takiwa kuwaelekeza wanawake katika mambo ya kiroho, kuwatembelea na kuwasaidia wagonjwa au wenye dhiki, na kufanya mambo mengine mema katika kusaidia ujumbe wa Mtume." (A.Yusuf Ali) Cheo cha Mama wa Waumini kinaonyesha kutayarishwa hususani kwa ajili ya Khadija. Bila Khadija, cheo hiki hakina maana. Yeye na yeye peke yake alionyesha mapenzi ya dhati ambayo yanatolewa na mama tu kwa waumini. Mama anaweza kuwa anahisi njaa lakini kama watoto wake wana njaa, atawapa chakula watoto wake kwanza. Kwa hakika, kama ni muhimu katika hali ya dharura atawalea na njaa huku akifurahi. Hali hii imetokea mara nyingi katika historia, hasa zaidi wakati wa vita na njaa. Ni jambo la uhakika kwamba watoto walioshiba na kutosheka, inatosha kumfanya mama afurahi na kutosheka, inatosha kumfanya yeye (mama) asahau njaa na kiu yake. Mapenzi ya mama hayana shar-ti; yanalenga hali zote na kujumuisha wote.
Waislamu walio wengi Makka walikuwa masikini. Hawakuwa na vyan-zo vya mapato, na walikuwa hawana namna ya kuwawezesha kujipatia riziki kwenye jiji ambalo uchumi wake ulikuwa mikononi mwa makun-di ya siri ya waubudu masanamu. Wanachama wa makundi ya siri wal-itoa agizo kwamba Mwislamu asilipwe ujira wowote kwa kazi yoyote atakayofanya na ni marufuku kununua kitu chochote kutoka kwake. Walitambua kwamba ufukara wa mali uliathiri vibaya mwili na roho na walidhani kwamba wakati upinzani wa Waislamu utakaposhindwa, kutokana na kudhoofika kiuchumi, wangeukana Uislamu, na wangemkataa Muhammad. Lengo la sera hii ilikuwa ni kuwanyima chakula Waislamu. Lakini Khadija aliwalisha Waislamu masikini kila siku, hivyo kwamba hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyedhikika kwa njaa, na aliwapa mahali pa kukaa. Kwake yeye, utoaji wa sadaka halikuwa jambo jipya lakini kipimo na uwezo wa msimamo ilikuwa kama ifuatavyo: alitumia fedha nyingi mno kwa ajili ya masikini na Waislamu wa Makka wasiokuwa na nyumba, hivyo alikwamisha mpango wa matajiri wa Makka waabuduo masanamu.
Msaada ambao Khadija aliutoa kwa jamii ya Waislamu wa Makka, ulikuwa muhimu kwa uhai wa Uislamu. Msaada wake kwa jamii ya Waislamu ulihakikishia uhai wa Uislamu wakati ulipokuwa katika hali ya mkwamo. Katika hali hii, alikuwa mtengenezaji wa historia - histo-ria ya Uislamu. Wake zake Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wote ni kina Mama wa Waumini; lakini kuna tofauti kubwa kati yao na Khadija. Wanawake wote walioolewa na Mtume Muhammad huko Madina walipokea ujira kutoka Hazina ya Umma. Baadhi yao walidai haki maalumu na marupurupu kutoka kwake. Walisema kwamba haki maalum zilizolipwa zilikuwa hazitoshi kwa mahitaji yao. Kwa upande mwengine, Khadija kamwe hakuomba kitu chochote kuto- ka kwa mume wake. Khadija aliamua mali yake iwe Hazina ya Umma kwa ajili ya Waislamu. Hapo Makka hapakuwepo Hazina ya Umma, ilikuwa ukarimu usio na mpaka na utajiri mwingi wa Khadija ambao ndio uliiokoa Jamii ya Waumini. Alikuwa anajihusisha sana na ustawi wa wafuasi wa mume wake, hivyo kwamba aliridhika kutumia fedha zake zote kwa madhumuni haya.
Mwenyezi Mungu ambariki mtumishi Wake, Khadija, Mama wa Waumini zaidi na zaidi. Khadija kama Mama. Dk. Sir Muhammed Iqbal (d. 1938) alikuwa Mshairi Mwana falsafa wa Indo Paksitan. Pia alikuwa kichocheo cha mwamko wa Waislamu karne ya 20. Anasema kwamba, mama anashika nafasi ya pili baada ya Mungu Mwenyewe.
Mama analeta maisha mapya hapa duniani, yaani anaumba; na tendo hilo tendo la kuleta maisha mapya hapa duniani au tendo la kuumba, linamtaka mtu ajitolee muhanga. Katika kuleta maisha mapya hapa duniani, mama huyaweka maisha yake hatarini. Kwa hiyo, mama anastahili hadhi na heshima kubwa sana. Kinachomfanya mama ayatoe muhanga maisha yake ni mapenzi-mapenzi kwa mwanawe.
Mapenzi kwa mwanawe ni mapenzi yaliyotakasika. Kwenye utakatifu, mapenzi ya mama kwa mwanae yanashika nafasi ya pili baada ya mapenzi ya Mungu Mwenyewe. Khadija alikuwa mama aliyejivunia watoto watatu - watoto wanaume wawili na mwanamke mmoja, kama ilivyokwisha onyeshwa huko nyuma. Watoto wawili wa kiume - Qasim na Abdullah walifariki dunia wakiwa wachanga. Mtoto wake wa mwisho na ndiye tu aliyebaki katika kuishi alikuwa Fatima Zahra. Kama Khadija alikuwa mama bora, Fatima Zahra alikuwa binti bora. Fatima Zahra, binti bora wa Muhammad Mustafa na Khadija, naye pia alipata kuwa mama bora. Alikuwa mama wa watoto wa kiume wawili -Hasan na Husain - na mabinti wawili- Zainabu na Umm Kulthum.
Khadija na Fatima Zahra - mama na bintiye - walikuwa wawili miongo-ni mwa wanawake wanne walio bora hapa duniani. Wote wawili wali-fanya umama utakasike. Waliufanya umama utukuke na kuheshimiwa. Kama ambavyo imesemwa huko nyuma, katika kitabu hiki wanawake hawakuwa na hadhi kabla ya Uislamu huko Arabuni. Kwenye jamii iliy-otawaliwa na mfumo dume walikuwa wana dhulumiwa kikatili na wal-ifanyiwa mambo kama wanyama. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alikomesha dhuluma ya wanaume kwa wanawake, na aliwapa hadhi ambayo wanawake walikuwa hawajapewa katika nchi yoyote na wakati wowote. Kuhusu wakina mama alisema: "Pepo ya mtu ipo chini ya miguu ya mama
."
Maana yake ni kwamba hakuna mtu anayeweza kuwa na matumaini ya kupata pepo kama amemkasirisha mama yake. Mtu kuipata pepo lazi-ma awe na uwezo wa kufuzu kuupata wokovu, na hakuna mtu ambaye amemkasirisha mama yake akaupata wokovu. Hivyo Mtume wa Uislamu amefanya mtu kufuzu kupata radhi ya mama - mwanamke - sharti linalo tanguliwa kabla mtu hajapata wokovu na kuingia peponi.
SURA YA KUMI NA NNE
KHADIJA, MWANAMKE MKAMILIFU
Kumekuwepo na wanawake wengi katika historia ya ulimwengu huu ambao walipata kuwa wakubwa na maarufu kwa sababu ya matendo yao makubwa. Jamii ya kibinaadamu inaweza kujivunia kwa haki kabisa kutokana na (wanawake) hawa.
Lakini katika historia ya ulimwenguni wote, wako wanawake wanne tu ambao wangeweza kufikia vipimo vya daraja ya juu vya ukubwa wa kweli na ukamilifu uliowekwa na Uislamu. Walifikia kwenye vipimo hivi kutokana na huduma zao kubwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Muhammad Mustafa, Mtume wa Uislamu, Mpokeaji wa Ufunuo (Wahyi) kutoka mbinguni, na Mfasiri wake, aliwatambua. Nao ni:
1.
Asiya, mke wa Firauni,
2.
Maryam, mama wa Isa, (Yesu)
3.
Khadija, binti wa Kuwaylid na
4.
Fatima Zahra, binti ya Muhammad Mustafa(s.a.w.w)
Muhammad Mustafa aliwaona wanawake wanne tu walio bora katika jamii ya dunia nzima. Baina ya hao wanne, wawili wa mwisho wanato-ka nyumba moja; wao ni Khadija, mama wa Fatima, na binti yake, Fatima. Khadija alikuwa mfano kwa roho iliyo bora na iliyokamilika.
Katika jamii iliyosalia hapa duniani, wanawake wengine tu ambao wanaweza kufuzu kuwa wanawake wenye sifa ya ubora, wangekuwa ni wake zake wengine wa Muhammad Mustafa. Lakini yeye mwenyewe alitoa hukumu kuhusu jambo hili, na hukumu yake haifutiki haibadili-ki. Alimtaja Khadija tu miongoni mwa wake zake kwamba ni mwanamke bora, na kwa hiyo aliwatenganisha - kwa amri wake zake wengine kutoka kwenye kundi la wanawake bora. Khadija alikusanya katika utu wake sifa zote hizo zinazo mfanya mtu kuwa bora. kama angepungukiwa na yoyote katika sifa hizo, mume wake hangemweka kwenye kundi la walio bora. Na hakuna ushahidi wowote kwamba alikuwa na kasoro hizo, ambazo zinasemekana kwa kanuni kuwa ni tabia za kimaisha ya wanawake. Tabia mojawapo ya udhaifu wa wanawake ni wivu. Khadija hakuwa na wivu wa aina yoyote. Alikuwa mwanamke aliyeona ukamilifu, furaha na kutosheka katika kutoa msaada. Alikuwa mlezi karimu wa masikini. Alikuwa anajisikia mwenye raha wakati anawapa chakula wenye njaa na huzuni. Matendo ya kuwalisha na kuwaliwaza wenye njaa na huzuni haikulazimu juhudi ya dhamira kwa upande wake; kwake matendo hayo yalikuwa kawaida yake.
Kama vile ambavyo Khadija alivyokuwa hana wivu, pia alikuwa habezi. Kitu kimoja ambacho kamwe hakukifanya, ni kuumiza hisia za mtu. Hakumtania mwanamke yeyote, hakujaribu kumdhalilisha mtu yeyote; kamwe hakumdharau mtu yeyote; kamwe hakukasirika na kuchukia na hakujiingiza katika kutoa maamuzi. Hakutamka neno baya au neno la kashfa dhidi ya mtu yeyote. Alikuwa na moyo wa kuelewa, alikuwa mtu wa kujihusisha sana na hisia za wanawake wanyenyekevu na masikini sana, na alidhikika kwa sababu ya dhiki ya wengine.
Kuna wakati ambapo Khadija aliitwa Binti wa Wafanyabiashara na Binti wa Makka. Halafu kuna wakati ambapo aliamua mali yake nyingi imi-likiwe na Uislamu. Alikuwa tajiri sana lakini baadaye akawa masikini kwani hakuwa na kitu. Alibadilisha mfumo wa maisha ya starehe na kuendesha maisha ya dhiki. Lakini hakuna kilichobadilika katika tabia yake. Alikuwa mwenye furaha, karimu, mkamilifu kama mwanzo. Alitumia muda mwingi sana kujitolea kumtumikia Mwenyezi Mungu, na Mjumbe Wake, na kama ilivyo kawaida, kamwe hakusahau ustawi wa umma wa Waumini. Aya ifuatayo inatoa maelezo kuhusu alivyo:
وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ ﴿٣٢﴾
"Na wako wanaokwenda mbele kabisa katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kubwa."Qur'an 35:32
Khadija, aliyemkamilifu, alikuwa mstari wa mbele kufanya "Matendo mema." Alikuwa na hali ya msukumo wa utakatifu ndani mwake. Kupitia "matendo yake mema" akawa mpokeaji wa neema za hali ya juu kutoka Mbinguni. Khadija alikuwa mwanamke aliyekamilika, mke aliyekamilika wa Muhammad Mustafa, Mama aliyekamilika wa watoto wao, na Mama aliyekamilika wa Waumini. Imani kwamba Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma ilikuwa kama springi ambapo ndipo Khadija alipata majibu ya mafanikio ya maisha yake. Yeye aliyepewa kile Quran inachokiita Qalb Salyim (moyo mtulivu) aya ya 89 kwenye Sura ya 26. Qalb Salyim au moyo mtulivu, A. Yusuf Ali mfasiri na mfafanuzi wa Quran Majid ametoa maana ifu-atayo: "Moyo uliotakasika, na usio athiriwa na maovu yanayotesa wengine. Kwa sababu kwa lugha ya Kiarabu moyo unaeleweka kama kiini cha hisia maono na akili, na matokeo ya tendo, ina jumuisha tabia yote."
Ulinganifu wa tabia ya Khadija ilikuwa ishara ya Qalb Salyim yake. Khadija alizaliwa na "Qalb Salyim" (moyo mtulivu) kama vile tu wale wateule wa Mwenyezi Mungu wanavyo zaliwa nayo. Ni moyo uliokuwa unabubujika imani, kuutumikia Uislamu. Mapenzi na shukurani kwa Mwenyezi Mungu.
SURA YA KUMI NA NA TANO
UKARIMU WA KHADIJA
Khadija Bint wa Arabuni, na Muhammad Mustafa, walioana mwaka wa A.D. 595. Miaka kumi na tano baadaye, Muhammad aliteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Mjumbe Wake. Kama Mjumbe wa Mungu, kazi yake ilikuwa kutangaza Uislamu hapa duniani. Kuanzia hapo, kila kitu kilibadilika kwa Khadija. Alitoa wakfu utajiri wake wote kwa ajili ya Uislamu. Wakfu huo ulipatikana katika kipindi mwafaka kwa Uislamu. Khadija alimwambia mumewe kwamba utajiri wake wote umekuwa mali yake, na atumie utajiri huo kwa jinsi apendavyo.
Ukarimu wa Khadija ulikuwa mng'aro wa kiwenyewe. Muhammad Mustafa "aliwekeza" utajiri wa Khadija kwenye Uislamu. Hapajafanyika "uwekezaji" mzuri kama huo katika historia ya binadamu. "Uwekezaji" huu ulikuwa hakikisho kwamba mwendo wa Uislamu hautsimamishwa au hata kudumazwa kwa sababu ya kusefu wa matumizi muhimu na msaada. Ulikuwa ni uwekezaji ambao, mpaka hii leo, unalipa "migawanyo" mingi na utalipa "migawanyo" kwa kila kizazi cha Waislamu, mpaka mwisho wa muda.
Lakini nyenzo ya utajiri haikuwa ya uwekezaji pekee ambao Khadija alifanya kwa ajili ya Uislamu. Vilevile aliwekeza muda wake, kipaji, nguvu na juhudi na moyo katika Uislamu, uwekezaji unaojulikana vinginevyo kama msimamo wa kujituma. Alitambua ndoto na matu-maini ya mume wake na alishiriki yote pamoja naye. Nia ya Khadija kusaidia Uislamu ilikuwa dhahiri mno hivyo kwamba Mwenyezi Mungu(s.w.t)
alifurahi na kuuita utajiri huo wa Kwake Mwenyewe katika ay a ifuatayo:
"Na akakukuta fakiri akakutajirisha" Qur'an 93:8
Maelezo ya mfasiri: "Mtukufu Mtume hakurithi utajiri wowote na alikuwa masikini. Mapenzi ya kweli, safi, na ya dhati ya Khadija si tu kwamba yalimwon- dosha na kumweka juu ya tamaa ya kupata, bali yalimfanya ajitegemee kwa mahitaji ya kidunia, mnamo siku za usoni za maisha yake, yal-imwezesha yeye kutumia muda wake wote kumtumikia Mwenyezi Mungu." (A.Yusuf Ali).
Mwenyezi Mungu alimtajirisha mtumishi wake, Muhammad, kwa mali ya Khadija. Khadija na makundi mawili ya Wahamiaji Waislamu kwenda Abyssinia (Uhabeshi) Makundi mawili ya Waislamu yaliondoka Makka mwaka wa 615 na 616 kuepuka mateso ya Maquraysh na walitafuta hifadhi Abyssinia. Jumla ya idadi ya wanaume na wanawake katika makundi yote mawili ilikuwa takriban mia moja. Wakitolewa wachache katika kundi kama Uthmani na Zubayr, wakim-bizi wengine wote walikuwa masikini mno kiasi cha kushindwa kumudu gharama za usafiri kwenda Abyssinia. Nani aliyefanya mipango yote ya misafara kuipatia vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na chakula na maji na gharama nyengine zote za kuwezesha kusafiri? Wataalamu wa historia hawajatoa jibu la swali hili. Lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba Khadija aliipatia misafara vifaa na kulipa gharama za usafiri, na Waislamu wakawa na uwezo wa kukimbilia Abyssinia. Hapa Makka ni Khadija peke yake ndiye aliyekuwa na uwezo wa kudhamini uhamaji wa Waislamu wa kiwango hicho.
SURA YA KUMI NA SITA
KHADIJA NA MUHAMMAD MUSTAFA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA KUMI NA TANO YA MWANZO WA NDOA YAKE
kazi za Khadija zilikuwa zile hasa za mke na mama wa nyumbani. Mwaka wa A.D. 610 Mwenyezi Mungu (S.w.t) alimteua Muhammad kuwa Mjumbe Wake, na tangu hapo kazi za Khadija ziliongezeka. Zaidi ya kuwa mume wake, Muhammad alikuwa kiongozi na mlezi wake katika malimwengu yote mawili hapa duniani na Akhera. Khadija alikuwa makini sana katika utendaji wa kazi zake kama mke na mama; na pia, sasa akajitambua katika kazi zake kama Mwislamu na Muumini wa kweli. Alifurahi kwamba Mwenyezi Mungu alimteua mume wake kuto-ka miongoni mwa viumbe wote kuchukua ujumbe wa Uislamu kuufik-isha duniani, na yeye alijitolea nafsi yake, kwa moyo, akili na roho, kuhakisha kwamba kazi hiyo inatekelezeka ipasavyo na kuleta mafanikio Wazazi wa Khadija, kama wale wa Muhammad Mustafa, walifariki akiwa bado mdogo sana. Kwa hiyo hakuwa nayo mapenzi ya huruma na upole wa wazazi kama ilivyokuwa kwa Muhammad. Khadija na mume wake walikuwa mayatima lakini hatimaye wote wawili wangekuwa watu wa kuwapa mapenzi na huruma mayatima wa dunia yote. Kile walichopoteza kutoka kwenye mapenzi na huruma ya wazazi wao, walifanikiwa kupata mapenzi na huruma kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe (s.w.t) za milele na milele.
Khadija alipoingia nyumba ya Muhammad baada ya kuolewa, hakuonyesha kupenda kujikwatua kwa kutumia vipodozi, kuvaa mapambo ya gharama kubwa yaliyoingizwa kutoka nchi za nje na kad-halika. Baada ya ndoa yake, alikuwa na mapenzi ya kufanya kitu kimo- ja tu, nacho ni kumpa mume wake starehe na furaha. Aliweza kufanik-isha hayo kwa kutumia nguvu zake zote kwa uthabiti. Alistarehe pale ambapo mume wake alikuwa na starehe na alifurahi tu ikiwa mume wake alikuwa na furaha. Furaha ya mume wake ilikuwa furaha yake. Alipewa kipaji hicho adimu na ule mkono stadi uliofanya nyumba ya mume wake kufana kama Pepo hapa duniani.
Wajibu aliofanya Khadija baada ya mume wake kutangaza ujumbe wake kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikuwa muhimu sana katika his-toria ya Uislamu. Mara alipotoka nyumbani mwake, alipambana na matatizo. Wapagani walimtesa kwa matusi na walimuumiza kwa mikono yao. Kazi yake ilijaa matatizo, ugomvi na jirani wasio na adabu waliifanya kuwa ngumu zaidi. Lakini mara alipoingia nyumbani mwake, Khadija alimsalimia kwa tabasamu iliyomfanya afurahi. Alisema maneno ya kuchangamsha yenye matumaini na starehe na wasiwasi na woga wake wote ulitoweka.
Tabasamu na maneno ya Khadija yalikuwa kama kitulizo cha mateso aliyofanyiwa Muhammad na waabudu masanamu kila siku. Na kila siku Khadija alimtia moyo na kurejesha ari yake. Uchangamfu wake ulipun-guza shinikizo baya lililosababishwa na matukio wakati wa shughuli zake, na aliweza kupambana na maadui zake tena akiwa mwenye kuji-amini. Khadija alikuwa ndio chanzo pekee cha furaha yake wakati wa vitisho na hofu. Huzuni na majonzi yalikuja kwa mfululizo kama maw-imbi, yakimtishia kumshinda, lakini mke wake alikuwepo wakati wote na kumwezesha apate ujasiri na ushupavu zaidi kuendelea na kazi yake. Kwake yeye mke wake alikuwa ngao ya kisaikolojia dhidi ya vurugu za Maquraysh zilizokuwa zinaongezeka mara kwa mara.
Khadija alikuwa na uelewa sawa ujumbe huu kama Muhammad alivy-ouelewa, na yeye alikuwa na shauku ileile aliyokuwa nayo mume wake kuona Uislamu unashinda upagani. Zaidi ya kuwa na shauku ya kuona Uislamu unashinda, yeye aliongeza msimamo na uwezo. Alifanya hivyo kwa kuhakikisha mume wake anafanya kazi ya kutangaza Uislamu tu, na kazi ya kutafuta riziki alifanya yeye. Kwa hiyo Khadija alimwezesha mume wake kuelekeza uangalifu wake wote, nguvu zake zote na muda wake wote katika kuendeleza Uislamu. Huu ni mchango wake muhimu alioufanya katika kazi ya mume wake kama mjumbe wa Mungu. Khadija alikuwa tegemeo ambalo alihitaji, kwa maneno yake A. Yusuf Ali, "miaka yote ya matayarisho yake." Miaka ile kabla ya kutangazwa Uislamu, ilikuwa "miaka ya matayarisho" kwa utume wake. A.Yusuf Ali.
Mchana na usiku Muhammad alikuwa ndani ya pango la Hira na Mola wake Mlezi. Matatizo magumu aliyoyatafakari akilini mwake, magumu zaidi kuliko jiwe la kito jekundu litokanalo kwenye jabali lililomzungu-ka, matatizo ambayo si yake, lakini matatizo ya watu wake, ndio, na ya hatima ya mwanadamu, ya huruma ya Mungu na mgongano wa miaka mingi ya uovu na wema, dhambi na Rehema nyingi. (The Holy Qur'an Introduction) Inawezekana sana kwamba Muhammad, Mtume - Mteule, aliupangilia na kuuwekea msimamo Uislamu ndani ya pango la Hira. Sura ya Uislamu ilikuwa dhahiri na kuonekana wazi ndani ya maisha yake binafsi muda mrefu kabla hajatangaza kwamba alikuwa mjumbe wa Mungu. Hatujui kwa ufasaha "miaka ya matayarisho" ilidumu kwa muda gani hadi hapo alipofikisha umri wa miaka 40, msingi wa Uislamu ulikuwa akilini mwake.
Muda ulikuwa jambo la msingi katika mpangilio wa Uislamu, na Khadija alijua umuhimu wake kwa mume wake katika kazi yake kwa hiyo Khadija alitengeneza mazingira bora ambamo mume wake angepata mafaniko ya muda, na kusababisha matokeo mazuri. Khadija alikuwa na kipaji cha kusoma hisia za mtu mwengine. Alikuwa anategemea matamshi yasiyotamkwa kutoka kwa mume wake na aliendelea kufanya kile alichotaka kufanya. Miaka ishirini na tano ya maisha ya ndoa, aliyafanya mawasiliano sahihi kabisa na ya karibu sana baina yake na mume wake.
Mnamo mwaka wa 10 baada ya Tangazo la Uislamu, Khadija alifariki dunia. Kifo cha mpendwa huonyesha jinsi mapenzi ya binadamu yanavyoathiriwa na tukio hilo lakini mapenzi ya Muhammad na Khadija hayakuwa ya kusitishwa na kifo; yalikuwa mapenzi ya milele daima. Khadija alipofariki, mapenzi ya Muhammad kwake hayakukatika. Kwa hakika, mapenzi yake kwa Khadija yaliendelea kuongezeka hata baada ya kutoweka duniani. Hata kuwapo kwa wake zake tisa haikuwa sababu ya kuzuia ongezeko la mapenzi kwa Khadija, na mapenzi yake kwa marehemu, wakati wote yalikuwa yanatafuta namna ya kujionyesha. Kama Khadija alimfanyia wema mtu wakati fulani na hata kama ali-fanya hivyo mara moja tu, Muhammad Mustafa alikumbuka na aliji-tahidi kuonyesha wema wa aina ileile kwa mtu huyo hata baada ya kifo chake, na alifanya hivyo mara nyingi iwezekanavyo.
Huko Madina, ilitokea Bibi kizee alikuja kumuona Muhammad Mustafa na akampa maombi fulani. Alimsalimia kwa upole, na alionyesha kuhusika sana na tatizo lake, na alimtimizia ombi lake hapohapo. Alipoondoka Bibi kizee huyo, Aisha ambaye alikuwa mmojawapo wa wake zake, alitaka kujua mtu huyo ni nani. Alisema: "Wakati Khadija na mimi tulipokuwa Makka, mwanamke huyu alikuwa na mazoea ya kuja kumuona mara kwa mara." Wakati wa uhai wake, Khadija alionyesha ukarimu na wema kwa watu wengi sana. Baada ya kifo chake, Muhammad Mustafa hakuwasahau watu hao waliokuwa wanapokea ukarimu na wema kutoka kwa Khadija, baada ya kifo chake, waliendelea kufanyiwa hayo na mume wake.
Kuhusu haya Aisha alisema: "Wakati alipochinjwa mbuzi au kondoo (nyumbani kwa Mtume), mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliamuru nyama ipelekwe kwa wanawake ambao walikuwa marafiki zake Khadija. Siku moja nil-imuuliza kwa nini alifanya hivyo na alisema: Nawapenda watu wote ambao walimpenda Khadija."(Isaba, Vol. 4, P. 283) Mwenyezi Mungu (s.w.t) Alimpa heshima mtumishi wake ampendaye, Khadija, kwa kutokuchangia mapenzi ya mume wake na wake wengine. Kipindi chote cha robo karne cha maisha ya ndoa, ni Khadija pekee ndiye alikuwa sahaba na rafiki wa mume wake, Muhammad Mustafa. Kila mmoja aliishi kwa ajili ya mwenzake na walipata machungu na matamu ya maisha wote pamoja.
Mwenyezi Mungu alimpa mtumishi Wake Khadija nafsi na tabia yenye sifa nyingi. Kama alivyoneemeshwa kwa wingi mno kupewa sifa hizo, yeye aliziimarisha kwa kuutendea wema Uislamu. Khadija alizipamba sifa hizo kwa kumpenda Mwenyezi Mungu kwa kumtii mume wake na kuutumikia Uislamu. Upendo na kutumika kwake ni sifa zilizo mnyanyua Khadija na kumweka kwenye nafasi ambayo hakuna mke mwingine wa Muhammad Mustafa aliyeweza kuifikia. Khadija peke yake, kwa kemikali ya tabia yake aliifanya nyumba ya Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kuwa kama kisi-wa cha amani, kutosheka na furaha katika bahari ya mapambano na ugomvi.
Iliamriwa huko Mbinguni kwamba Muhammad Mustafa lazima aoe mwanamke mwenye malezi mazuri na mwenye kuelewa sana katika Arabu yote. Hapakuwepo mwanamke wa aina hiyo isipokuwa Khadija. Mwenyezi Mungu alikuwa na madhumuni ya pekee ambayo yange-timizwa na Khadija. Kwa hiyo, ndoa yao ilitengenezwa Mbinguni. Abbas, Mahmud al-Akkad wa Misri anasema kwenye kitabu chake, "Aisha": "Ilikuwa amri maalumu ya Mwenyezi Mungu kwamba mke wa mjumbe wake anatakiwa awe mwanamke mpole sana, mwema na aliyetakasika kama Khadija."
Khadija alikuwa mfano halisi wa uchaji Mungu, utakatifu na alikuwa mlezi wa ukamilifu wa kiwango cha juu na maadili ya juu sana. Inaelekea kwamba kama Muhammad Mustafa hakutokea, Khadija angeishi maisha ya pekee bila mume. Muhammad Mustafa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wakati fulani alisema kuhusu binti yake Fatima Zahra, kwamba hakuna mtu mwengine ambaye angemuoa isipokuwa Ali bin Abi Talib: Ingekuwa kweli kabisa kusema kwamba hapana mtu mwengine ambaye angestahili kumuoa Khadija isipokuwa Muhammad.
Kuhusu suala hili, A. Yusuf Ali, mfasiri na mfafanuzi wa Qur'an Majid anasema: Ilikuwa baina yake na Hadhrat Khadija, mwanamke na mke bora kuliko wote. Alimuoa miaka kumi na tano kabla ya kupewa Utume; maisha yao ya ndoa yalidumu miaka ishirini na tano, na mapen-zi yao yalikuwa ya kiwango cha juu sana, yakilinganishwa katika kipi-mo cha kiroho na kijamii. Wakati wa uhai wa Khadija mume wake hakuoa mke mwingine, jambo ambalo si la kawaida kwa mtu mwenye hadhi kama yake miongoni mwa jamii yake. Mkewe alipokufa, yeye alikuwa na umri wa miaka hamsini (50), na kwa sababu mbili tu, inaelekea kamwe hangeoa tena, kwa kuwa alikuwa anajiepusha sana katika maisha ya kidunia.
Mambo mawili yaliyotawala ndoa zake zilizofuata ni:
1.
Aliwaonea huruma na kuwaonyesha upole wajane walio na dhiki na hawangesaidiwa kwa namna nyingine yoyote katika hali ya jamii ile, baadhi yao, kama Sauda, walikuwa na watoto katika ndoa zao za zamani, hivyo walihitaji ulinzi;
2.
Msaada katika kazi yake ya uongozi, kutoka kwa wanawake ambao walipewa maelekezo na kuwekwa pamoja katika familia kubwa ya Waislamu, ambapo wanawake na wanaume walikuwa na haki sawa za kijamii. Muhammad Mustafa, Mtume wa Mwenyezi Mungu, alitumia fursa zote kuonyesha kuvutiwa kwake na mapenzi kwa Khadija na kutambua ukubwa wa kiwango alicho utumikia Uislamu. Alifanya hivyo, kwanza kabisa kutii amri ya Mwenyezi Mungu kama Kitabu chake kinavyose-ma kwenye Ay a zifuatazo:
1 "... Na kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu...." (Sura Al-Baqara 2:231)
2. " ...Na neema za Mola wake Mlezi zisimulie..." (Sura 93:11 ).
Muhammad Mustafa mtumishi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alipokea upendeleo na ukarimu mwingi kutoka Kwake kupitia kwa Khadija - alizikariri na kuzitangaza. Halafu, pili, Muhammad Mustafa alipenda kutaja matendo mema, makubwa ya Khadija aliyoyafanya katika kumtumikia Mwenyezi Mungu na Uislamu, kwa sababu ya kuonyesha mapenzi kwake (Khadija). Hii ilikuwa njia mojawapo ya kuonyesha mapenzi. Ilikuwa pia namna nyingine ya kujikumbusha muda waliyotumia yeye na Khadija wakiwa pamoja Makka. Mtu anaweza akaona waziwazi kwam-ba katika kumbukumbu zake, fikra zake zilikuwa zinayatembelea maisha yake ya zamani; na pia mtu anaweza kugundua humo dalili za mambo aliyozoea zamani. Palikuwepo na muda katika maisha ya kila mtu ambapo alizidiwa na kumbukumbu ya mambo aliyoyazoea.
Waandishi wa vitabu viwili mashuhuri, Isaba na Istiab, wamemnukuu Bi Aisha akisema: "Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu akiondoka kwenda popote, alimkumbuka, alimsifu na kumrehemu Khadija." Jinsi muda wa maisha ya ndoa ulivyopita, mapenzi ya Muhammad na Khadija yalizidi kupenya kwenye mioyo yao kwa nguvu zaidi. Kwa mapenzi yake, aliondoa wasiwasi wake wote, woga na huzuni kama ilivyoelezwa hapo kabla. Kwa kutumia istiari ya mashariki: Khadija aling'oa miba yote katika maisha ya Muhammad Mustafa, badala yake, alipanda maua ya waridi ya mapenzi.
Maua hayo kamwe hayakunyau-ka; rangi, harufu na ubichi wao ulikuwa wa daima milele. Kama palikuwepo na ndoa iliyopendeza wakati wote, ndoa hiyo ilikuwa ni ile ya Muhammad na Khadija; ndoa hiyo ilikuwa mpya siku ya mwisho wake kama ilivyokuwa siku ilipoanza. Khadija alikuwa hai moyoni mwake daima milele. Jina la Khadija lilikuwa mdomoni mwake wakati wote, na mapenzi ya Khadija yalijaa moyoni mwake. Hata kuzungumza juu yake na kumsifu kulimfanya Mtume afurahi.
Kila neno na tendo la Khadija lilidhihirisha busara zake. Katika kuch-agua mume wake, alionyesha uwezo wa kushangaza na wepesi wa kuelewa wa hali ya juu. Lakini uwezo na wepesi wa kuelewa ni vipaji ambavyo wanawake wengine vile vile wanaweza kuwa navyo, na Khadija hakuwa mwanamke pekee aliyepewa vipaji hivi. Maelezo kuhusu uamuzi wenye msukumo wa kimungu uliofanywa na Khadija kukubali kuolewa na Muhammad Mustafa ni kwamba kulifanywa chini ya mwongozo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) Mwenyewe. Kwa hiyo, hangeamua vibaya. Alipokutana na Muhammad, Mtume mteule, Khadija aliona Utukufu kwa mbali sana ndani yake, na alikabidhi hati-ma yake kwenye mikono yake iliyobarikiwa. Mikono hiyo ilinyanyua hatima yake, na kuifanya tukufu.