3
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
SURA 3
UTEUZI WA MAIMAMU, SIFA ZAO NA WAAJIBU WA VEEO VYAO
Imam ni neno la kiarabu linalomaanisha, "mkuu", "kiongozi", na "mwongozi."
Uteuzi wa imam hufanywa na mungu na kumjulisha mtume wake, ambaye hutangaza uteuzi wa imam huyo kwa wafuasi wake. mwenyezi mungu amesema katika qur'an "na bwana wenu anayeumba na kumchagua anayempenda, na siyo hiari yao, na kutukuzwa ni yeye ambaye ni juu ya vyote anavyo shirikishwa nae" kuna aya nyingi katika qur'an zinazoeleza kwamba uteuzi wa imam ni wa mungu na hufanywa na mungu mwenyewe. kwa mfano kuhusu nabii adam:
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ﴿٣٠﴾
Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa ...(2:30).
Kuhusu Nabii Daudi, Mungu amesema katika Qur'an:
يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ فَاحْكُم بَيْنَ النَّاسِ بِالْحَقِّ ﴿٢٦﴾
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki... (38:26).
Kuhusu Nabii Ibrahim, Qur'an imeleza:
وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾
Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu." (2:124).
Kutokana na aya hizo imedhihirika kwamba mtume(s.a.w.w)
humteua (tangaza) imam kutokana na amri ya mungu tu. La sivyo, yeye hana uwezo wa kumteua imam kwa sababu imam lazima awe mwenye hekima yote na. awe maasum (asiyekosa, asiye na dhambi na kuwa taahir).
Qur'an inazungumzia maimam aina nyingi, k.m.
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾
"Na sisi tumewafanya kuwa maimam wanao ongoza watu kwa amri yetu na tumewaamrisha kutenda wema, kuimarisha swala na kutoa zaka na sisi peke yetu tu wao hututumikia." (21:73).
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾
"Na sisi tumewafanya maimam ambao huwaongoza watu kwenda motoni, na siku ya hukumu hao hawatasaidiwa." (28:41).
Yafuatayo ni madondoo machache ya wanazuoni mashuhuri wa kisunni kuhusu imam na sifa zake. aalim mashuhuri wa kihindi katika kitabu chake madhahibul islam katika ukurasa 106 aandika:
Imam ni mwakilishi wa mtume(s.a.nv.w)
na kwa niaba yake ni mtawala na mhifadhi wa mambo yao duniani na mtoaji mwongozo kuhusu mambo ya kidini, kudumisha elimu ya dini, kutekeleza maagizo ya kiislam, kuamrisha watu kutenda mema, na kuwakataza watu waache maasi, kupingana na makafiri na kuwapa adhabu wahalifu kufuatana na mwongozo wa dini."
licha ya hayo, katika madhehebu ya sunni neno la "imam" hutumika katika maana ya kawaida tu. Mtu yeyote ambaye ni mtaalamu katika hadithi na sheria ya kiislam vile vile huweza kuitwa imam. k.m.
Imam ghazali, imam shafi, imam abu hanifa. lakini hata hivyo wanaamini kwamba kuwa mrithi (mwakilishi) wa mtume(s.a.w.w)
na faradhi za mtume(s.a.w.w)
imam lazima awe na masharti yafuatayo.
Imam lazima awe:
1)
Mwislam.
2)
Mwanamume.
3)
Mtu huru (asiwe mtumwa)
4)
Awe na akili timamu.
5)
Awe amebaleheghe (siyo mtoto mdogo)
6)
Awe mcha mungu (asiwe mtenda maasi)
7)
Awe anatokana na kabila la quraishi.
8)
Asiwe na kilema cha aina yoyote; kiziwi, bubu au kipofu.
9)
Awe mtaalam katika sheria ya kiislam.
Imam wa 32 wa ismaili (wafuasi wa aga khan) shah mustansir billah, ameandika sifa za watakatifu katika kitabu chake kiitwacho "fidi aad jawan mardi".
Kitabu hiki kinahesabika kuwa ni cha uhakika wa hali ya juu kwa waismailia na vile vile kuna makala ya watakatifu. toleo moja la kitabu hiki kilichapishwa katika mwaka wa hindoo 1961 na laljibhai devraj katika lugha ya kiajemi (persian) lakini katika hija ya kihindi. katika ukurasa wa 94 sifa za watakatifu zimeelezwa "eh waumini, jueni kwamba "peer" (mtakatifu) huwa mtu thabiti, pili humkumbuka na kuamini mungu, na wajibu wake ni kutafakari, kuhubiri na kuhutubia juu ya ukweli.
Yeye lazima kwanza hujitaradhia nafsi yake kabla ya kuwasihi wengine." "tena katika kurasa 94-96 anaendelea: "mtakatifu wa haki ni yule ambaye ni mwenye matamanio katika makuu ya dunia, huepuka kwenda pahala pasipo pazuri na vitendo vya fuska, mwenye subira, makini, mkweli na mcha mungu". mwishowe tunasimulia hadithi moja kuhusu sifa za imam, kutoka kitabu cha shia ithnaasheri. hassan bin fadhal asimulia kutoka kwa baba yake kwamba Imam Ali-ridha
, imam wa nane, ameeleza sifa 30 zinazo mhusu imam, nazo ni:
1.
Imam lazima awe na elimu zaidi kuliko watu wote wa wakati huo.
2.
Awe kiongozi na mwamuzi wa watu wote.
3.
Awe ni mtu mwenye subira zaidi kuliko wote katika karne
anayoishi.
4.
Awe mcha mungu zaidi kuliko watu wote wa wakati wake.
5.
Awe shujaa kuliko wote.
6.
Awe mtu mwenye dini na mwabudu mungu zaidi kuliko wote.
7.
Awe mkarimu kuliko wote.
8.
Awe amezaliwa akiwa ametahiriwa.
9.
Huzaliwa msafi na huwa mcha mungu.
10.
Huweza kuona nyuma yake kama anavyoona mbele bila kugeuka nyuma.
11.
Hawi na kivuli cha mwili wake.
12.
Anapozaliwa papo hapo huweka viganja vyake juu ya ardhi
(Sakafu).
13.
Hutoa shahada juu ya upekee wa mungu na utume (unabii) wa
Mtume muhammad(s.a.w.w)
14.
Hapati ndoto za unyevunyevu.
15.
Hata akiwa amelala huwa macho kifahamu.
16.
Malaika huja kumwamkia na kuzungumza naye.
17.
Deraya ya mtume(s.a.w.w)
humtosha barabara.
18.
mkojo au kinyesi chake hakionekani na mtu yeyote. hunyonywa
(mezwa) na ardhi, haiwi na harufu mbaya lakini hutoa harufu ya
ambari na miski."
19.
Hudhibiti maisha ya watu.
20.
Huwa na huruma zaidi juu ya watu kuliko wazazi wao.
21.
Huwa mnyenyekevu mno katika swala zake na ibada ya mungu.
22.
huwa wa kwanza katika kutekeleza amri za mungu.
23.
Hujizui kwa dhati na juhudi kuepuka na maasi.
24.
Dua zake zote hutakabaliwa na allah na hakuna kitu anachomwomba mola hukataliwa na mungu, akimwomba mungu jiwe gumu lipasuke hupasuka.
25.
Huwa anamiliki deraya ya mtume(s.a.w.w)
pamoja na upanga wake dhulfikar.
26.
Huwa na daftari lenye orodha ya wafuasi wake wote pamoja na
wale ambao watakao zaliwa mpaka siku ya hukumu.
27.
Huwa na kitabu chenye orodha ya maadui wake wote.
28.
Huwa na jaamiah yenye urefu wa yadi 70 ambamo kuna maelezo kamilifu kuhusu mambo ya dunia.
29.
Huwa na nyaraka kubwa iliyo tengenezwa kwa ngozi ya mbuzi na nyingine ndogo iliyotengenezwa kwa ngozi ya kondoo ambazo huitwa jafar kuu na jafar ndogo ambazo zinaeleza kanuni zote za kidini hata kuhusu mambo madogo kama vile sheria inayomhusu mtu akimcho mamwezie kwa ukucha.
30.
Huwa na kitabu alicho rithishwa kutoka mwana fatima
binti muhammad(s.a.w.w)
.
Ikiwa mtu hana hizo sifa 30, basi kwa mujibu wa itikadi ya shia ithnaashery hawezi kamwe kukubaliwa kuwa imam.
Kwa hakika ni wajibu wa mtume(s.a.w.w)
na warithi wake kumi na wawili kuishi maisha kwa mujibu wa amri za mola na kanuni zilizoandikwa katika qur'an tukufu na kuongoza waislamu ili kuishi maisha ya kidini bila kuleta mabadiliko ya aina yoyote katika amri takatifu. kuhusu jambo hilo tunakumbusha aya chache zinazohusika za qur'an:
وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾
Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa (53:3- 4).
وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾
"Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri." (5:44).
وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾
"Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu." (5:45).
ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨﴾
"Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu". (45: 18)
وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ ﴿٤٤﴾ لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ ﴿٤٥﴾ ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ ﴿٤٦﴾ فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ ﴿٤٧﴾
Na angalikuwa amezua chochote kinyume cha amri zetu, kwa hakika tungelimtwaa upande mkono wa kuume na baadaye tungelikata mishipa yake ya damu upande wa kushoto wa moyo. Na hakuna hata mmoja katika nyinyi angeweza kumkinga." (69:44-47).
Wakati hata mtume mtukufu(s.a.w.w)
hana madaraka ya kuongeza au kupungu za, kubadilisha au kugeuza yaliyoteremshwa (wahyi) na allah kama ilivyoelezwa katika qur'an tukufu. Basi kwa hakika imam
pia hana uwezo wa namna hiyo. Maimam wote
ni viongozi wa wafuasi, huwafunza amri za mungu kama alivyofunza mtume(s.a.w.w)
.
Kwa hiyo ni jambo la lazima kuwa elimu ya maimam
kuhusu qur'an tukufu na hadithi iwe bora kuliko ya waislam wote.