7
ASIYEMTAMBUA IMAMU WA ZAMA ZAKE
SURA 7
KUTAJWA KWA HADHRAT MAHDI (AS.) KATIKA GINAN ZA PEER (VIONGOZI) (NYIMBO ZA DINI ZA WATAKATIFU WA KIISMAILI)
Katika kitabu cha Sala ya waismailia, wafuasi wa Aga Khan, kiitwacho so ginan, sehemu ya kwanza ukurasa 70, katika sala ya nne ya peer shams imeandikwa kwamba huyo mehdi aliyetakasika atakuja amepanda farasi duldul.
Katika kitabu hicho hicho, sehemu 2, ukurasa wa 3, katika sala ya peer ismaili shah yafuatayo yameandikwa: "yeyote asiyemtambua mehdi shah atahesabika hakuelimika (mjinga) na atakabiliwa na hasara duniani na akhera na hataokoka. mehdi ataua makafiri wote na atafundisha qur'an na kufuta ujinga."
Katika kitabu hicho hicho sehemu ya 6, kuna sala za peer hassan kabirdin ambaye amearidhia "imam wa mwisho imam Mahdi
atakuja. Yeye (Mahdi) ni mtakatifu mno na watakaomfuata watakuwa wamebahatika. Wa kwanza ni ali
, mwisho ni mehdi
ambaye ni imam mtukufu. Yeyote atayemkataa na kutomfuata yeye (Mahdi) aamali (sala zake) hazitakubaliwa."
Sala nyingine ya peer Hassan Kairdin, katika kitabu hicho hicho inasema: "Mahdi aliye shujaa atafundisha kiarabu na jina lake litakuwa Mahdi Shaah. yeye atawaua iblis na Dajjal na kutawala bara zote duniani."
Tanbihi: wadanganyifu wote waliodai kuwa wao ni mehdi hawakuweza kutawala hata kijiji kidogo licha bara zote duniani. Kutokana na hizo sala zote nne zilizotajwa uhai wa hadhrat mehdi
umethibitika na kuja kwake kutawala ulimwengu na kuleta usawa na amani vile vile kumebitika.
SURA 8
KUZALIWA KWA HADHRAT MEHDI (A.S)
Mwenyezi Mungu amesema katika qur'an:
يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّـهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٣٢﴾
" Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia."(9:32).
Maadui wa allah hawakuacha jambo lolote katika jitihada zao za kumwumbua mtume mtukufu(s.a.w.w)
na ahlul-bait wake
. wamewaua kwa kuwachinja au kwa kuwapa sumu dhuria ya mtume(s.a.w.w)
moja baada ya mmoja, iakini "nuru" imeendelea kuangaza na itaangaza hadi siku ya kiyama. khalifa mo'tamid aliyekuwa katika makhalifa wa bani abbas alimweka kizuizini imam wa kumi na moja, hadhrat imam hassan askari
, miaka mingi gerezani. alikuwa ana habari kamili juu ya hadithi ya mtume muhammad(s.a.w.w)
kwamba imam hassan .askari atapata mwana hadhrat mehdi
na huyo ataanzisha na kustawisha utawala wa dhuria ya mtume(s.a.w.w)
ulimwenguni na kuangamiza maadui wa Ahlul-Bait na wa mtume(s.a.w.w)
. kwa hivyo alimweka imam hassan askari
gerezani kwa muda mrefu sana ili kuzuia bishara ya mtume(s.a.w.w)
.
Firaun alidai kwamba yeye mungu. wanajumi walimshauri kwamba kutokana na kizazi cha bani israel atazaliwa mtoto ataye angamiza ufalme wake, kumwua yeye (firaun), wafuasi na masahaba wake. kwa hiyo firaun aliweka ulinzi mkali juu ya wanawake wa bani israel. kila mtoto akizaliwa akiuliwa ili kuzuia kuzaiiwa kwa nabii musa. Hata hivyo, alivyotaka mungu ikawa. nabii musa alizaliwa katika nyumba hiyo hiyo ya firaun. Licha ya kuzaliwa tu, hata kalelewa nyumbani mwa firaun. kama vile alivyo firaun, mo'tamad alitaka hadhrat mehdi
asizaliwe. Lakini hakuna mtu anayeweza kufaulu kuzuia amri ya mungu.
Katika kipindi imam hassan askari
alipokuwa kizuizini kulitokea ukame mkali sana samarra. kwa muda mrefu hapakunyesha hata tone moja la mvua. waislamu waliswali swala maalum ya kuomba mvua inyeshe lakini hawakufanikiwa.
Wakati waislamu wote walipokusanyika nje ya jiji la samarra, padri mmoja wa kikristo akanyanyua mikono yake kuomba mungu na papo hapo mawingu yakakusanyika na myua ikanyesha kidogo. Kuona hivyo waislamu wote walibabaika. Wakaanza kupatwa na wasiwasi kwamba labda ukristo ni dini ya kweli. Khalifa papo hapo akaitisha baraza lake na kuchukua ushauri wa wanavyuo, mawaziri na maofisa wake. Wote walipigwa butaa. Mmoja wa washauri wake akatoa wazo kwamba yuko mwokozi mmoja tu ambaye anaweza kuwaokoa, naye ni imam hassan askari
ambaye alifungwa gerezani. khalifa alikuwa na hakika (yakini) juu ya elimu, ukweli na uimam wa imam hassan askari
na haki yake ya utawala (ukhalifa). akamwita imam hassan askari katika baraza la kifalme.
Hadhrat imam hassan askari
alipofika kasri, khalifa akasimama kwa taadhima, akamkaribisha, na akamkalisha karibu na kiti cha kifalme na kumweleza mambo yote. Imam akasema "usiwe na wasiwasi. Hilo si jambo kubwa. Waamrishe waislamu wote wakusanyike nje ya jiji kesno ili waswali na kuomba mvua inyeshe. Na wakati huo huo mwamrishe huyo padri wa kikristo alike". Kesho yake waislamu wote pamoja na yule mkristo walikusanyika huko. Imam akamwambia huyo padri aombe mungu na papo hapo mawingu yakakusanyika. Irnam akamwomba khalifa kumtuma mtu akalete kile kitu padri huyo alichoficha katikati ya vidole vyake. Khalifa aliamrisha afisa wake akamnyang'anye mfupa uliofichwa katikati ya vidole vya padri, na akamkabidhi imam hassan askari
. imam Hassan Askari
akaufunika huo mfupa katika leso na kuiweka hiyo leso mfukoni mwake. papo hapo mawingu yaliyokusanyika yakatawanyika. Hapo hadhrat akamwambia huyo padri amwombe mungu ili inyeshe mvua. Padri huyo alijitahidi sana kumwomba mungu lakini hakufanikiwa hapo imam akamjulisha khalifa kwamba ule mfupa ulikuwa wa nabii mmojawapo na wakati wowote unapowekwa chini ya mbingu basi mawingu hukusanyika imam akiwaongoza waislamu katika swala akanyanyua mikono yake mitakatifu. Papo hapo mawingu yakakusanyika pande zote. Imam akawaamuru watu waende makwao na baadaye mvua kubwa ikanyesha. imam na khalifa walirudi kitaluni na hilo lilikuwa jambo pekee likizungumzwa na kila mtu. Khalifa alifurahi mno kwa sababu uislam ulinusurika.
Khalifa na watu wote waliamini mafaa ya swala, ukweli na utawala wa imam. Baada ya muda imam
akaondoka. Khalifa alipomwuliza alikokuwa anaelekea imam akamjibu kuwa alikuwa anarudi kifungoni alimo wekwa na khalifa. Kusikia hayo, khalifa aliona haya sana na akasema, "eh mjukuu wa mtume, tafadhali rudi nyumbani kwako". Hapo imam alirudi nyumbani kwake. Katika muda huo narjis-khatun (mama yake imam wa kumi na mbili akawa mja mzito).
يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٨﴾
"Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia." (61:8).
Jina la mama yake hadhrat mehdi
hasa lilikuwa narjis khatun. majina yake mengine yalikuwa malika, sausan na 'rayhana. Yeye ni mjukuu wa mfalme wa utawala wa uturuki. Historia ya kuvutia ya narjis khatun kufika samarra ni kama ifuatavyo: imesimuliwa na bashir bin suleiman kuwa: "niliitwa na imam ali naqi (baba yake imam hassan askari
, imam wa kumi na kuambiwa: 'wewe ni katika kizazi cha wasaidizi wetu na marafiki zetu. Nitakupa shughuli muhimu kwa sababu mimi nina imani na wewe: mimi nilimwomba aniamrishe tu kwa sababu nilijiandaa kutimiza anachotaka. ameniambia kwamba anahitaji kumnunua kijakazi.
Akaniamrisha niende baghdad kwa ajili ya shughuli hiyo, na nitapofika huko niende kwenye ukingo wa mto. Huko mimi nitaona majahazi mengi na mateka wa kike wakiuzwa. Mimi niende kwa mtu mmoja aitwaye omar bin yazid ambaye atakuwa na mtekwa wa kike aliyevaa nguo mbili za hariri. yeye (huyo mtekwa wa kike) atakataa kuuzwa kwa mnunuzi yeyote na atakuwa anazungumza lugha ya kituruki. Imam ali naqi akanipa dinar 120 akaniambia kwamba mwuzaji atakubali kumwuza huyo mtekwa kwa hiyo bei. Vile vile alinipa barua ya kumpa huyo mtekwa wa kike.
Mimi nilikwenda baghdad kama nilivyoagizwa na kwa alama nilizo elezwa na imam ali naqi, nilimtambua huyo mtekwa na nikampa barua. kusoma barua hiyo tu huyo bibi machozi yalimjaa machoni mwake na akamwambia maliki wake kwamba hatakubali kununuliwa na mtu yeyote ila miye (bashir bin suleiman). Kwa hivyo nilirudi nyumbani (huko baghdad) na huyo mtekwa ambaye aliweka barua hiyo juu ya macho yake na kulia sana. Nilimwuliza kwa nini anabusu hiyo barua na kulia wakati yeye ni mgeni kutoka uturuki na hamjui mwandishi wa barua hiyo. Yeye akasema: "Sikiliza, mimi ni mjukuu wa kaisar, mfalme wa uturuki na jina langu ni malika.
Jina la baba yangu ni yashua na jina la mama yangu ni shamunusafaa. baba yangu aliandaa mipango niolewe na mpwa wake. Siku moja aliwaita mapadri wote, mawaziri, viongozi na wafuasi wake, na kumkalisha mpwa wake juu ya kiti cha enzi ambacho kilipambwa na almasi na kumwomba padri afunge ndoa yetu. Padri alipoanza kufungua kitabu kutaka kufunga ndoa masanamu waliotundikwa ukutani waliporomoka na mwana mfalme (mpwa wa babu yangu) akazirai na kuanguka na kiti cha enzi kilivunjika vipande vipande. mapadri walitetemeka na kumwomba msamaha baba yangu mfalme, kwa sababu hawakutarajia kutatokea balaa hiyo.
Mfalme alihuzunika sana. Akaona ndoa hiyo ilikuwa na nuksi na kwa hivyo aliagiza kiti kingine cha enzi na kutundika masanamu tena ukutani. padri tena akaanza kufunga ndoa na tukio hilo hilo likatokea tena. waliohudhuria wote walishtuka sana na wakaondoka papo hapo. baba yangu alifedheheshwa sana na siku nyingi alikuwa hakutoka nje ya kasri.
Usiku huo huo nilimwona nabii issa katika ndoto. Yeye alikuwa pamoja na masahaba wake waliokuwa wamehudhuria sherehe ya ndoa yangu. kiti kirefu cha enzi kiliwekwa pahali palipo wekwa kiti cha mwana wa mfalme (aliyetaka kunioa) na kilikaliwa na mtu mkubwa mwenye uso uliojaa nuru. Baada ya muda mfupi tu niliwaona watu wenye nyuso za nuru na hapo nabii issa alisimama kuwakaribisha na kuwapa nafasi karibu yake. Nilimwuliza mtu mmoja anijulishe hao waliokuja walikuwa nani? nikaarifiwa kwamba hao ni mtume wa uislam pamoja na mrithi wake na maimam kumi na moja wanaotokana na dhuria yake.
Mtume mtukufu hapo akamwomba nabii issa kumcchumbia malika binti wa shamunusaafa mjukuu wake imam H assan askari ambaye uso wake uking'aa kwa nuru (ombi hilo lilifanywa kwa nabii issa kwa sababu malika alitokana na kizazi cha hadhrat shamoon mrithi wa nabii issa). Nabii issa akamwomba hadhrat shamoon atoe kibali chake na papo hapo hadhrat shamoon akakubali kwa kuona hiyo ni heshima kuu. Kwa hiyo ndoa yangu ikafungwa na imam hassan askari
. macho yangu yakafunguka ghafla na mimi nilijawa na furaha. Nilikumbuka hiyo ndoto. Hata hivyo niliogopa sana na sikumhadithia ndoto hiyo mtu yeyote. Hapo baadaye mimi nikaanza kuwa mgonjwa ona kumkumbuka imam hassan askari na hali yangu ikaanza kudhoofu. Safari moja nilimwona binti wa Mtume(s.a.w.w)
mwana Fatima
na katika ndoto mimi nilisimama kwa taadhima na nikamweleza hali yangu na kutomwona imam hassan askari
. aliniamrisha nisome "shahada", nikawa mwislamu na baadaye kila usiku nilimwona imam hassan askari katika ndoto akinituliza. Mara moja imam hassan askari aliniambia kwamba babu yangu atatuma jeshi kuivamia nchi ya waislamu na mimi nibadilishe mavazi yangu niungane na jeshi kama mtumishi mmojawapo. Waislamu watashinda vita hivyo, na mimi nitatekwa na kwa hivyo niungane na mateka wengine, mpaka baghdad."
Mimi (bashir bin suleiman) niliposikia hayo nilijawa na furaha na nilimleta bibi narjis khatun samarra kwa imam ali naqi
. imam Ali naqi
alimkaribisha pia akamkabidhi kwa dada yake Halima Khatun. Baadaye imam ali naqi
alimwozesha bibi narjis khatun na mwanawe imam Hassan Askari
akawabashiria kwamba watampata mwana ambaye atakuwa hujjat (dalili) duniani wa kuthibitisha kuwepo kwa mungu. Wakati dunia itapokuwa imeghariki katika ukandamizi, uovu na ulaghai yeye atakuja kutawala na kuleta insafu na usawa. Imam Mahdi
alizaliwa samarra iraq alfajiri siku ya ljumaa tarehe 15 shaaban 255 a.h. nyumbani kwa baba yake mtukufu. Alizaliwa tohara na amekwishatahiriwa na uso wake ulivyojaa na nuru ambayo ilipenya paa na kuelekea mbinguni. Alipozaliwa tu, kwanza alisujudu na huku akiwa amenyosha kidole chake cha shahada kuelekea samawati na kuthibitisha upweke wa mungu na unabii wa mtume muhammad(s.a.w.w)
na uimamu wa Ali
pamoja na warithi wake kumi kuwa ni maimam wa kweli. Hapo baadaye akamwomba mungu atimize ahadi yake.
Halima khatun, binti wa imam wa tisa, hadhrat imam mohammed taqi
, shangazi yake imam hassan askari
, akamnyanyua mtoto aliyezaliwa na kumpa baba yake ambaye alimpakata. Imam Mahdi
papo hapo akamwamkia baba yake ambaye alimjibu na akamwambia aendelee kusema kwa amri ya mungu. hapo tena hadhrat mehdi
akarudia kuthibitisha upweke wa mungu, utume wa Mtume Muhammad(s.a.w.w)
urithi wa maimam kumi na moja na kusoma aya ya qur'ani "tumekusudia kuwajalia jamala yetu wale ambao waliofikiriwa ni wanyonge duniani na kuwateua maimam na kuwafanya warithi duniani" (28:5). Hapo baadaye imam Hassan askari
akamrudisha huyo mwana kwa bibi Halima Khatun na Halima Khatun akamrudisha mtoto kwa mama yake. Mwana huyo alimwamkia mama yake vile vile. Katika Sherehe ya akika imam Hassan Askari
alimwamrisha wakili wake Othman Saidi Omari kuwagawia maskini nyama ya mbuzi 10,000 na mikate 10,000.
Kuna marejeieo mengi katika vitabu vya kisunni kuhusu kuzaliwa kwa hadhrat mehdi
. tuna nakili madondoo machache pamoja na ushahidi. mwanazuoni wa kisunni, ubeidullah amrat-sari katika kitabu chake sawanahe umry hadhrat Ali
ukurasa 433, kuhusu imam hassan askari
. ameandika, "hakuna mwana yeyote aliyeishi baada yake ila mwanawe aabdal qassim mohammad al-hujjat tu" zanabl katika kitabu chake tarikhul islam ameandika kwamba imam wa kumi na mbili amezaliwa katika mwaka 256 a.h.
Sheikhul Sislam wa istanbul, sheikh suleiman balkhi kanduzi, katika kitabu chake yanabiul mawaddah ameeleza bayana kuhusu kuzaliwa kwa hadhrat mehdi
kama vile maelezo yaliyomo katika vitabu vya ithnaasheri. Yeye ameandika kuwa hadhrat mehdi
alizaliwa mwaka 250 a.h. ambayo nitofauti kidogo na hiyo ilisababishwa na kosa la uchapishaji. katika kitabu maarufu sana cha kisunni tarikh ibnul khaladun juzuu la pili, ukurasa 24, mwandishi anaeleza "Mahdi
anaye subiriwa alizaliwa siku ya ijumaa tarehe 15 shaaban 255 a.h. na baba yake ni imam hassan askari (a.s.). 5) mulla abdur-rahman jami katika shawahidu Nubakhat, ukurasa 247, ameandika kuwa "mwana wa imam ridha ni muhammad, na mwanawe ni ali na mwanawe hassan na mwanawe ni muhammad mehdi
, huyu wa mwisho alizaliwa samarra 255 a.h.